MASWALI YA KUJADILI: WAKOLOSAI 1:1-29
- Mungu anakuwaje Baba yake Yesu Kristo? Tumaini walilowekewa akiba mbinguni watakatifu wa Kolosai ni lipi? Je Injili inazungumza chochote kuhusu tumaini hilo? Kwa nini waumini wa Kolosai wanaitwa watakatifu waaminifu? Dalili inayotambulidha kuwa Injili imewafikia watu na inazaa matunda ni nini? Je, kujazwa na maarifa ya mapenzi ya Mungu katika hekima yote na ufahamu wa rohoni ni kwa umuhimu kwa ukuaji wa kiroho?
- Kwa nini Wakolosai walioitwa watakatifu waaminifu wanahimizwa kuwa na mwenendo unaompendeza Mungu huku wakizaa matunda mema? Je,mtu aweza kuitwa mtakatifu na bado akawa na mapungufu ya kiroho? Je watakatifu wanahitaji kuwezeshwa na Mungu ili wakamilike au wana uwezo wa kujisimamia wenyewe? Urithi wa watakatifu ambao Mungu Baba ametustahilisha kuupokea ni upi? Mungu Baba alituokoaje na alituokoa lini kutoka nguvu za giza na kutuhamishia katika ufalme wa Mwana wa pendo lake?
- Ukombozi una uhusiano gani na msamaha wa dhambi? Je, ukombozi ni jambo lenye uhakika lisilo na shaka au lintegemea majaaliwa ya Mungu au juhudi zetu wenyewe? Yesu anakuwaje mfano wa Mungu asiyeonekana na hapo hapo mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote? Kufanywa kwake mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote kunalenga kutupatia nini sisi wanadamu? Kwa nini vitu vyote viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake? Uthibitisho wa jambo hilo ukoje? Utimilifu ulio ndani ya Yesu ni utimilifu wa nini? Yesu anakuwaje mzaliwa wa kwanza katika wafu?
- Damu ya Yesu ilivipatanishaje vitu vyote vya vilivyo juu ya nchi na vilivyo mbinguni? Kazi ya kutufanya watakatifu wasio na mawaa wala lawama inafanywa na sisi wenyewe au inafanywa na Yesu? Injili ilihubiriwaje kwa viumbe vyote chini ya mbingu? Siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote ni ipi? Maonyo yanamfanyaje mtu kuwa mkamilifu katika Kristo? Huyo atendaye kazi ndani yetu kwa nguvu ni nani? Kuna uthibitisho gani juu ya hilo?
MASWALI YA KUJADILI: WAKOLOSAI 2:1-23
- Kwa nini Kristo ni siri ya Mungu? Kwa nini inasemwa kuwa hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika ndani ya Yesu Kristo? Je, inawezekana kudanganya bila kutumia maneno ya kushawishi? (Methali 1:10). Je kushawishi ni sawa na kubembeleza? (Methali 7:6-21). Mafundisho ya awali ya ulimwengu anayoyazungumzia Paulo ni yapi? Utajijuaje kama wewe ni mwenye shina na mwenye kujengwa katika Kristo? Je jambo hilo ni muhimu?
- Utimilifu wote wa Mungu kwa jinsi ya mwili ni kitu cha namna gani? Jambo hilo lina umuhimu gani kwa mwanadamu? Kuna uthibitisho gani kwamba jambo hilo lilikuwemo ndani ya Kristo? Wanadamu wanatimilikaje katika Kristo? Kuna uthibitisho gani kuwa Kristo ndiye kichwa cha enzi yote na mamlaka? Tohara ya Kristo inafanyikaje? Kwa nini kuuvua mwili wa nyama kunafananishwa na tohara? Mwili wa nyama unavuliwa wakati gani
- Kwa nini tohara iliyofanywa kwa mikono ina hadhi ndogo kuliko ile isiyofanywa kwa mikono wakati iliyofanywa kwa mikono iliagizwa naMungu? Tulizikwaje na kufufuliwaje pamoja na Kristo katika ubatizo? Kristo alitufanya hai pamoja naye akiisha kutusamehe makosa yote. Je tunaokolewa baada. ya kusamehewa au tunasamehewa baada ya kuokolewa? Hati iliyoandikwa ya kutushitaki ilikuwa na madai gani? Nani aliandika hati hiyo na alikuwa anamwandikia. nani?
- Nani aliifuta hati iliyokuwa inatushitaki na alifanya hivyo kwa mamlaka gani? Hati hiyo iligongomelewaje msalabani? Je enzi na mamlaka alizozivua alipokuwa anaigongomelea hati iliyotushitaki msalabani vilikuwa vya nani? Kwa nini kuzivua hizo enzi na mamlaka kulileta shangwe? Vyakula, vinywaji, sikukuu, na sabato ambazo hapaswi mtukutuhukumu navyo ni zipi? Je, kwa agizo hili alikuwa anaondoa ulazima wa kutunza siku ya saba ya juma kama siku ya kumwabudu Mungu?
- Unatambuaje na kutofautishaje sabato iliyokuwa kivuli cha mambo yajayo na ile ambayo haikuwa kivuli? Mtu anayetumia akili zake za kimwili akijitia kwenye maono yake mwenyewe utamtambuaje? Ni amri zipi anazozungumzia Paulo ambazo waliokufa na Kristo na kuacha mafundisho ya awali ya uliwengu hawapaswi kujitia chini yake? Mambo ambayo hayafai katika kuzizuia tamaa za mwili na ambayo huonekana kama yana hekima katika kutawala mwili kwa ukali ni yapi?
MASWALI YA KUJADILI: WAKOLOSAI 3:1-25
- Ni lini tulipofufuliwa pamoja na Kristo? Je, kufufuliwa pamoja na Kristo hutokea wakati wa ubatizo au wakati tunapokuwa tumemwamini Kristo? Ni lini tulipokuwa tumekufa pamoja na Kristo na uhai wetu kufichwa pamoja na Kristo? Kwa nini kufikiria yaliyo juu kunakuwa kugumu kwa wengi kuliko kufikiria yaliyo chini? Tutafunuliwa pamoja na Kristo katika utukufu. Jambo hilo litakuwaje? Huo utukufu utakuwa wa aina gani?
- Ni mambo gani yanayochochea ghadhabu ya Mungu na kwa nini? Mtu anavifishaje viungo vilivyo katika nchi? Kwa nini vinaitwa viungo vilivyo katika nchi? Kwa nini utu wa kale unavuliwa kana kwamba ni vazi? Je, mtu aweza kuuvaa utu wa kale baada ya kuuvua? Je mtu aweza kukirudia kitu alichokiweka mbali hapo awali? Matendo ya utu wa kale ni yapi? Je, wanaoambiana uwongo huwa ni wanafiki pia? Unadhani unafiki nimojawapo ya matendo ya utu wa kale? Je, Mungu anaposema msiambiane uwongo amesema pia msiwe wanafiki?
- Utajuaje kama utu mpya uliouvaa unafanana na ufahamu wa yule aliyeuumba? Je kuna uwezekano wa kuwa na utu mpya usio na ufahamu unaofanana na ule aaliouumba? Kwa nini wafuasi wa Kristo wanaitwa wateule wa Mungu watakatifu wapendwao? Utajuaje kama Neno la Kristo limekaa kwa wingi mioyoni mwetu? Kipimo cha kujua utii huu kwa mume unampendeza Bwana ni kipi? Uchungu ambao waume hawatakiwi kuwa nao kwa wake zao ni upi? Kama mke anakukera unatakiwa ufanyeje?
- Wazazi huwachokoza watoto wakati wanapofanyaje? Kwa nini watoto wanapochokozwa na wakina baba hukata tamaa? Je wenye mazoea ya kuchokoza watoto huwa ni wa baba zaidi kuliko wa mama? Je ni halali kwa mtumwa anayetumikishwa bila malipo kumtii Bwana wake kwa moyo? Je hapa Ukristo hauwezi kutumika kuhalalisha ukandamizajiJe urithi waweza kuwa ujira? Huo urithi ni wa kitu gani?
MASWALI YA KUJADILI: WAKOLOSAI 4:1-18
- Kila aliye mkubwa angejua ana mkubwa wake huko mbinguni ingepunguza unyanyasaji? Je ipo haja ya kuomba ili milango ifunguliwe na neno lihubiriwe? Kwa nini kunahitajika kwenda kwa hekima kwa wale walio nje? Je kujibu kunahitaji hekima? Jibu linalofaa linapimwa kwa vigezo gani? Mameno yaliyokolea munyu yapoje? Unatakiwa kufanya nini ili ujue namna ikupasayo kuwajibu watu?