Seventh-day Adventist® Church

PASTOR LETTA'S OFFICIAL WEBSITE

Menu

MISHAEL CHIGULA MUTAKI


WASIFU WA MCHUNGAJI MISHAEL CHIGULA MUTAKI

KUZALIWA:

Marehemu Mchungaji Mishael Chigula Mutaki alizaliwa tarehe 04 Aprili, 1949, katika kijiji cha Mchilongo, Tarafa ya Nyanja, Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara.

ELIMU:

Marehemu Mchungaji Mishael Chigula Mutaki alianza elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Murangi mwaka 1958 hadi 1961. Alijiunga na Shule ya Kati (Middle School) ya Bumangi kuanzia mwaka 1962 hadi mwaka 1965.

Kwa upande wa elimu ya sekondari, marehemu Mchungaji Mishael Chigula Mutaki alisoma katika Sekondari ya Musoma Alliance School kuanzia mwaka 1966 hadi mwaka 1969 na shule ya Shinyanga Commercial Institute (SHYCOM) mwaka 1970 hadi 1972.

Mwaka 1977 hadi mwaka 1978, marehemu Mchungaji Mutaki alisomea na kupata stashahada (Diploma) ya masuala ya Theolojia na Afya katika Tanzania Adventist Seminary - TASC, Arusha.

Mwaka 1988 hadi 1990 alipata tena, “Diploma”, ya masuala ya Theolojia katika Tanzania Adventist College (TAC).

Mwaka 1991 hadi 1993, marehemu Mchungaji Mutaki alisoma na kupata Shahada ya Kwanza ya masuala ya Theolojia na Kiingereza katika Chuo cha Solusi, Zimbabwe.

Mwaka 1993-1996, marehemu Mchungaji Mutaki alitunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Masuala ya Uchungaji yaani, MA. In Pastoral Ministry, katika Chuo cha Andrews University (Campus ya Newbold College, Uingereza).

 

UCHUNGAJI, UHADHIRI NA AJIRA KWA UJUMLA:

Kuanzia mwaka 1972 hadi 1976, marehemu aliajiriwa na kufanya kazi katika Wizara ya Fedha, Dar es Salaam kama Mhasibu.

Mwaka 1979 hadi 1982 alijiunga na uchungaji akawa mchungaji wa Mtaa wa Morogoro, na hatimaye Tukuyu.

Mwaka 1982 hadi 1986, alifanya kazi kama Mfasiri wa Lessoni (Translator) katika Unioni ya Tanzania.

Mwaka 1987 hadi 1988 aliwekewa mikono na kuwa mchungaji wa Mtaa wa Mbeya.

Mwaka 1997 hadi 2001, alikuwa Mchungaji wa Chuo, Tanzania Adventist College, Arusha.

Mwaka 2001 hadi 2005, alikuwa Mkuu wa Kitivo cha Theolojia na Dini, Tanzania Adventist College/University of Arusha.

Mwaka 2005 hadi kustaafu 2015, amekuwa Mhadhiri katika University of Arusha (Miaka 36 ya utumishi uliotukuka).


Kwa wadhifa wake aliokuwa nao ulimfanya pia awe; pamoja na nyadhifa nyingine: Mwenyekiti wa UoA SACCOS, 2011 hadi Umauti, Mjumbe wa Kuhakiki Mwongozo wa Wafanyakazi, UoA, 2010, Mjumbe wa Kuhakiki Charter ya UoA, 2010, 2011, Mwenyekiti, Kamati ya Nidhamu ya Chuo, 2012, Mwenyekiti wa ATAPE, UoA, 2021.

KUUGUA NA KUFARIKI:

Marehemu Mchungaji Mutaki alianza kuugua na kupelekwa Hospitali ya St. Elizaberth (Arusha), siku ya tarehe 6, May 2021, ambako alilazwa kwa muda wa siku sita. Kabla ya hapo alishawahi kutibiwa KCMC na Muhimbili. Katika yote ilibainika kuwa alikuwa akisumbuliwa na tatizo la mgongo.

Aliruhusiwa kurudi nyumbani kwa uangalizi zaidi hadi tarehe ya kulala ilipofika siku ya tarehe 04 Juni 2021, majira ya saa 3 asubuhi nyumbani kwake mbele ya Mke wake na Mchungaji Lameck Mwamkonda. Tunawashukuru madaktari na ndugu wote waliohusika katika kumuuguza marehemu.


HITIMISHO:

Marehemu Mchungaji Mutaki ameacha Mjane Bi. Miriam na watoto watatu (3) ambao ni ASIFIWE, SHUKRANI, na BITURO. Pia ameacha wajukuu sita (6), NEEMA, NATANIA, TROPHIMO,TRIFINA, TRUST NA ELSA.

“Yeye aliye Mungu wa pekee, Mwokozi Wetu kwa Yesu Kristo, Bwana wetu, Utukufu una Yeye, na Ukuu, Uwezo, na Nguvu, tangu milele na sasa na hata milele”

(Yuda 1:25)