Seventh-day Adventist® Church

PASTOR LETTA'S OFFICIAL WEBSITE

Menu

AYUBU

NILIYOGUNDUA NA KUJIFUNZA: AYUBU 1:1-22

  1. Ayubu alikuwa mcha Mungu mwenye mafanikio makubwa ya kiuchumi. Hakuna mgongano wowote kati ya mafanikio ya kiuchumi na hali bora ya kiroho. Wale ambao mali na utajiri vimewafanya wamsahau Mungu aliyewapa wanatoa taswira isiyo sahihi juu ya kumiliki mali. Ayubu alimiliki wanyama na alimiliki eneo kwa ajili ya malisho na uzalishaji. Uchumi huenda sambamba na kumiliki ardhi. Maadamu ardhi ingalipo tuwe na juhudi ya kumiliki maana ni halali yetu (Joshua 1:3).
  2. Malezi bora ya watoto huandamana na kuwafanyia sherehe katika matukio yao muhimu na kuwatunuku wale waliofanya vyema. Ayubu aliwafanyia hivyo wanawe na binti zake. Hakuwabagua watoto wa kike aliwaona ni sehemu ya familia. Tena aliwaombea kila siku asubuhi ili Mungu awakinge na majaribu ya yule mwovu. Watoto wa wacha Mungu wanahitaji kuombewa sana maana Shetani ana vita nao. Kumbe mzazi anaweza kumuombea mwanae msamaha kwa Mungu ili ikiwa kuna dhambi aliyotenda asamehewe (Yakobo 5:15).
  3. Shetani ana wivu mchungu na wacha Mungu waliofanikiwa kiuchumi na wanaomtii Mungu kikamilifu naye hutumia fursa za kuongea na Mungu kuwachonganisha na Mungu wao (1Petro 5:8; Ufunuo 12:10). Ingawa kuna msemo umuogope yule anayeingia vikao usivyoweza kuingia lakini kamwe usiogope vikao vya Mungu na Shetani. Katika vikao hivyo Mungu husimama kututetea kwa mambo Shetani anayotuchongea. Mungu hadanganyiki na mambo unayosingiziwa na Shetani au na wanadamu wenzako.
  4. Katika pambano kuu lililoanzia mbinguni na linaloendelea sasa duniani Shetani hutumia silaha ya kudanganya na akishindwa huingilia kuudhuru mwili wa mhusika (Ufunuo 12:12; 2 Timotheo 3:12). Si kila anayepitia mfululizo wa mikasa maishani anakuwa anaadhibiwa kwa dhambi zake au Mungu amemuacha. Wakati mwingine Mungu ameruhusu ajaribiwe ili kumuimarisha au kuwaimarisha wengine au kuthibitisha madai ya Shetani si ya kweli.
  5. Usimwazie Mungu kwa upumbavu unapopitia majaribu ambayo huelewi sababu yake. Amini kuwa ana sababu kwa nini ameruhusu jaribu hilo na anajua wakati gani atafungua mlango wa kutokea (1 Wakorintho 10:13). Usinung'unike. Mshumaa unapoangazia chumba huwa unateketea. Kuna wakati Mungu anaweza kukuchagua uwe mshumaa wa kuangazia wengine.

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 2:1-13

  1. Utaratibu wa kuwa na vikao na Mungu ambapo wana wote wa Mungu walihudhuria ulikuwa na makusudi gani? Kama waliotakiwa kuhudhuria ni wana wa Mungu kwa nini Shetani alihudhuria na wala hakutimuliwa kikaoni? Je alipokea mwaliko? Utaratibu huo wa Shetani kuhudhuria vikao vya mbinguni ulikoma lini na kwa nini? Je kuna uwezekano wa vikao vya kiroho vya makanisani Shetani kuhudhuria? Je dalili za kujua kuwa Shetani kahudhuria ni zipi?
  2. Mungu ana urafiki na Shetani? Kwa nini anaongea naye? Ungepata nafasi ya kukutana na Shetani ungemuuliza nini? Ungekutana na Shetani ameumia anahitaji msaada wako ungemhurumia na kumsaidia? Unadhani Shetani alikuwa anazunguka huko na huko kutafuta nini? (1 Petro 5:8).
  3. Je kuna wakati Shetani humchochea Mungu atuangamize bila sababu? Shetani anafurahia nini wanadamu wakiangamizwa? Je kama angetaka kukushitaki wewe leo kwa Mungu angekosa sababu? Unadhani ni kwa nini hata kunapokuwepo sababu ya kutuangamiza huwa hatuangamii? Unadhani utetezi wa Yesu umekuwa ukitusaidia? (Zekaria 3:1-5; Yuda 1:9).
  4. Unadhani Mungu anajivunia nini kwako? Je, kulikuwa na haja yoyote kwa Mungu kwenda kumtambishia Shetani juu ya Ayubu? Je tabia njema kwa mzazi kuwa unamsifia mwanao mwadilifu mbele ya watu? Je kuna uwezekano wa kumkufuru Mungu wakati unapopitia mateso? Kwa nini Mungu hubebeshwa lawama kwa shida tunazopitia? Unadhani anastahili lawama?
  5. Je kuna magonjwa yanayowatokea watu kwa kuwa kuna vita inayoendelea kwenye ulimwengu wa roho? (Waefeso 6:12; Yohana 11:3-4). Je, yapo magonjwa wanayougua watu yanayohitaji kufunguliwa na wala si vidonda wala sindano? Kama ungekuwa unafahamu kinachoendelea nyuma ya pazia kuhusu ugonjwa wake ungemsaidiaje?
  6. Je mke wa Ayubu anawakilisha ufinyu wa akili ya wanawake katika kushauri waume zao? Mke wa Ayubu alikosea wapi katika ushauri wake? Je unadhani haikeri kumuuguza mtu anayejinasibu ni rafiki mkuu wa Mungu wakati huyo Mungu wake hamsaidii kupona? Je kuna wakati wauguzao mgonjwa huchoka kuuguza? Je wauguzaji wanahitaji kuhurumiwa na kuombewa sawa na wagonjwq wanaowauguza?
  7. Je lugha aliyotumia Ayubu kumkemea mkewe ilistahili au ilivuka mipaka? Je Ayubu hakufanya dhambi hata pale alivyomwita mkewe kuwa anafanana na mmojawapo wa wanawake wapumbavu? Ni nani walio mahodari kuwashawishi wenzi wao kumwacha Mungu pale mambo yanapowaendea kombo maishani kati ya mume na mke? Unadhani wauguzi wakionesha hali ya kukata tamaa hali hiyo yaweza kuifanya hali ya ugonjwa kuongezeka? Je ni vibaya kulia kwa kumsikitikia mgonjwa kutokana na hali mbaya aliyonayo?
  8. Je ungependa mtu anayekuja kukuona ukiwa mgonjwa awe anauliza maswali ya kwa nini ugonjwa huo umekupata na kujaribu kuuhusianisha na mahusiano yasiyo mazuri na Mungu wako au akae kimya akisubiri kukusaidia unapohitaji msaada?

BIBLE DISCUSSIONS: JOB 3:1-26

  1. What was the purpose of having meetings with God where all the sons of God attended? If those who were required to attend are the sons of God, why did Satan attend and was not expelled from the meeting? Did he receive an invitation? When did the process of Satan attending heavenly meetings stop and why? Is it possible for Satan to attend spiritual meetings of your churches? What are the signs of knowing that Satan is present?0
  2. Is God friendly with Satan? Why is he talking to him in that friendly manner? If you had the chance to meet Satan, what would you ask him? If you find Satan hurt or in pain, and that he needs your help, would you sympathize with him and help him? What do you think Satan was looking for during rooming activities in the world? (1 Peter 5:8).
  3. Is there a time when Satan provokes God to destroy us for no reason? What does Satan enjoy when humans are destroyed? If he wanted to sue you today, would he lack a reason? What do you think is the reason why we are not destroyed even when there is evidence of our wrong behaviour and mistakes? Do you think the advocacy ministry of Jesus has been protecting us from our right punishment? (Zechariah 3:1-5; Jude 1:9).
  4. What do you think God is proud of you for? Was there any need for God to go and tell Satan about Job? Is it good behavior for a parent to praise your righteous son in front of people? Is it possible to blaspheme God when you are going through suffering? Why is God blamed for the problems we experience? Do you think he deserves the blame?
  5. Are there diseases that occur to people because there is a war going on in the spirit world? (Ephesians 6:12; John 11:3-4). Are there diseases that people suffer from that need to be healed spiritually and which does not need pills? If you knew what was going on behind the scenes about his illness, how would you help Job?
  6. Does Job's wife represent the narrow mind of women in advising their husbands? Where did Job's wife go wrong in her advice? Do you think it is offensive to nurse a person who happens to be God's best friend when his God is not helping him to recover? Is there a time when nurses get tired of nursing? Do nurses need to be pitied and prayed for the same as the patients they nurse?
  7. Was the language used by Job to rebuke his wife appropriate or did it cross the line? Didn't Job sin even when he called his wife that she looked like one of the foolish women? Who are able to convince their spouses to leave God when things go wrong in life between husbands and wives? Do you think that if nurses show a sense of desperation, that situation can make the condition of the disease increase? Is it wrong to cry out of pity for the patient due to his bad situation?
  8. Would you like the person who comes to see you when you are sick to ask questions about why the illness has struck you and try to relate it to bad relationships with your God or to sit quietly waiting to help you when you need help?
  9. Do you find any chaplaincy ministry exercised in Job's fiends? Is keeping quite useful when attending the suffering one? Was Job's wife practicing chaplaincy when she provoked Job to curse God for not helping him? By so doing was she practicing sympathy or empathy to Job or both? Job's sickness needed the medical treatment of doctors and nurses of spiritual care giver only?

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 3:1-26

  1. Mke wa Ayubu alimtaka mumewe amlaani Mungu kwa kushindwa kumponya. Mara hii Ayubu yeye mwenyewe analaani siku aliyozaliwa akitamani asingezaliwa na kukutana na ugonjwa anaoupitia. Je kulaani siku uliyozaliwa ni sawa na kumlaani Mungu? Unadhani ni kweli Ayubu alikuwa na mawazo ya kutaka kujiua? Je mtu aliyekamilika na mwenye kuepukana na uovu anaweza kuwaza kufa au kujiua? Je Mungu anamchukuliaje mtu anayelalamika kwa nini alizaliwa? Je mtu anayekufa kwa kujiua atakwenda mbinguni? Katika kuzikwa azikwe kama mpagani?
  2. Mtu anayetaka kujiua anahisi maisha yake baada ya kufa yatakuwa bora kuliko yalivyo katika uhai. Je, mtu anayewaza hivyo anasukumwa na nguvu za giza au matatizo ya afya ya akili? Unadhani Ayubu alikuwa na matatizo ya afya ya akili? Je ukiwa na matatizo ya afya ya akili unaweza kujitambua?
  3. Je kuwa na hofu isiyo ya kawaida ni dalili ya kuwa na mgogoro kwenye afya ya akili? Kwa nini ukijiwa na hisia za kutokewa na jambo baya hutokea? Je hofu ina uwezo wa kutengeneza tatizo la kiafya? Kwa nini mwenye hofu moyo humwenda mbio? Mwenye kutaka kujiua huona mbele yake giza nene lenye tundu dogo liingizalo mwanga? Je kwa mujibu wa Ayubu 3:20 Ayubu aliifikia hali hiyo? Je kuzingirwa na mawazo ya uwepo wa Mungu kwaweza kumpa tumaini anayekabiliwa na kujiua?
  4. Je unadhani Mungu alikosea kukuumba? Umewahi kumshukuru Mungu kukuumba hivyo ulivyo? Ili kushinda changamoto za maisha unahitaji mfumo unaokutegemeza na kukusaidia na majanga. Unadhani Ayubu alikuwa na mfumo tegemezi ulio imara? Kama alikuwa nao kwa nini alianza kukata tamaa?

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 4:1-21

  1. Elifazi Mtemani baada ya ukimya wa muda mrefu alimhoji Ayubu ili kujiridhisha juu ya uadilifu wake. Elifazi alikosea kuamini kuwa matatizo hayawezi kumpata aliye muadilifu. Je ni sahihi kudadisi sababu za ugonjwa kwa lengo la kujiridhisha kama mgonjwa hahusiki na kuwepo kwa ugonjwa?
  2. Unadhani mgonjwa anahitaji nini zaidi kwa wale wanaomtembelea akiwa anaumwa? Je kusutwa na maswali magumu ni sehemu ya hitaji la mgonjwa? Maswali aliyoulizwa Ayubu yalikuwa ya lazima katika mazingira yale ya ugonjwa? Je, Elifazi alimuuliza maswali hayo akiwa na nia ya kutaka kumsaidia au katika namna ya kumtuhumu? Ukikutana na rafiki yako aliyekonda sana tofauti na ulivyozoea kumuona huko nyuma utamshangaa, na kumhoji nini kimemsibu au utanyamaza na kujifanya hujamuona ili usimkatishe tamaa?
  3. Je ukiwa kiongozi ni salama kutoa kauli za kumlaumu Mungu au Kanisa lake mbele ya waumini wachanga? Kufanya hivyo kwaweza kuathiri vipi imani yao kwa Mungu wao na kwako pia? Ukiona kiongozi wako wa kiroho akiongelea mambo yenye uwezekano wa kuhafifisha imani za watu utachukua hatua gani? Kama ulikuwa ukiwahubiria watu kuwa kumtumikia Mungu kunaepusha mabaya na mara ukapatwa na hayo mabaya utamuona Mungu kuwa amekuangusha na kukuumbua? Je kwa kuwa mabaya yamekukuta hiyo inamaanisha kuwa umetenda dhambi?
  4. Je, unadhani Ayubu alijihisi kuwa mtu mkamilifu mwenye kutumainiwa sana na Mungu ndiyo maana alilalamika alipoteswa? Je kitendo cha Ayubu kuteswa wakati akiwa hana hatia kilikuwa kitendo cha haki? Je Mungu huwa anakosea? Je kuna nyakati Mungu huwaonea wanadamu akishirikiana na Shetani? Je, ni rahisi kuendelea kumsifu Mungu pale anaporusu mabaya yatupate? Je ni sahihi kumkasirikia Mungu?

DISCUSSION QUESTIONS: JOB 4:1-21

  1. Eliphaz the Temanite after a long silence questioned Job to satisfy himself about Job's integrity. Eliphaz was wrong to believe that problems cannot befall the righteous. Is it correct to inquire about the causes of the disease in order to prove whether the patient caused the sickness.
  2. What do you think the patient needs most from those who visit him when he is sick? Is being confronted with difficult questions? Were the questions asked to Job necessary in the circumstances of such a disease? Did Eliphaz ask him those questions with the intention of wanting to help him or in a way to accuse him? If you meet your friend who is very thin, unlike what you used to see in the past, will you be surprised, and ask him what has happened to him or will you keep quiet and pretend you have not seen him so as not to disappoint him?
  3. As a leader, is it safe to make statements blaming God or his Church in front of young believers? How can doing so affect their faith in their God and in you too? If you see your spiritual leader talking about matters that are likely to weaken people's beliefs, what action will you take? If you were preaching to people who believe that serving God keeps someone very far from evil? What comes in your mind when God allows calamities to befall you? Will you feel like God has dissapointed you? Does the fact that evil has befallen you mean that you have sinned?
  4. Do you think that Job felt himself to be a perfect person who was trusted by God and that is why he complained when he was persecuted? Was Job's act of being tortured when he was innocent an act of justice? Does God sometimes make mistakes? Are there times when God oppresses humans in collaboration with Satan? Is it easy to continue to praise God when he allows bad things to happen to us? Is it right to be angry with God?

MAMBO NILIYOGUNDUA NA KUJIFUNZA:

  1. Taabu haisababishwi na kile mtu afanyacho bali hutokana pia na ukweli kuwa wanadamu wamebeba kiini cha matatizo. Hali hiyo haibagui mwenye haki na asiye na haki. Taabu humkuta yeyote. Huu ndiyo ukweli unaopaswa kuzingatiwa na wanaopitia mateso, waombolezaji na wafariji. Ufumbuzi wa mateso na maumivu tunayopitia upo kwa Mungu pekee. Yeye ndiye anayepaswa kukimbiliwa wakati wa taabu. (1 Petro 5:6-7).

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 5:1-27

 

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 6:1-30

 

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 7:1-21

 

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 8:1-22


MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 9:1-35

  1. Mungu ndiye kipimo cha haki kuwa hajawahi kuishi kinyume cha haki. Kuwa mwenye haki ni kuwa kwenye kiwango alichonacho Mungu? Je ni vibaya kujitambulisha kama ni mwenye haki? Katika Mwanzo 7:1 Mungu anamtambulisha Nuhu kama mwenye haki. Je unamuona Nuhu kustahili hadhi hiyo hasa ukizingatia aliyoyafanya baada kutoka kqenye Safina? Unadhani Akida aliona nini kwa Yesu hata akamtangaza kuwa alikuwa mwenye haki? (Luka 23:47). Yesu aliwatahadhari watu wasiridhike na haki ya Mafarisayo. Kwani Mafarisayo walikuwa na haki gani? (Mathayo 5:20).
  2. Kwa nini wanadamu hushindwa kuyaishi yale Mungu anayowaagiza kuyatenda lakini Mungu mwenyewe hapati ugumu kuyatenda? Kuna haja gani ya kuwaagiza wanadamu kufanya yale unayojua hawawezi kufanya? Je ukijitahidi kufanya yale Mungu anayojua huwezi kuyafanya unakuwa unamchukiza au unamfurahisha? Mungu anajisikiaje watoto wake wanapojaribu tena na tena kufanya mapenzi yake na kuishia kushindwa? Anawacheka au anawahurumia?
  3. Je ni jambo lenye tija kutaka kulumbana na Mungu kwa namna unayoona kuwa hakutendei haki? Je Mungu anapenda kuhojiwa? Anaweza kuvumilia kulaumiwa? Je hawezi kutumia uwezo wake wa nguvu kuwanyamazisha wanaomlaumu? Je ukipata nafasi ya kumshauri Mungu ungemshauri nini? Je kuna wakati wowote Mungu amewahi kupokea ushauri kutoka kwa binadamu? (Mwanzo 18:20-33; Mwanzo 19:17-22).
  4. Unadhani Mungu aliyeuumba ulimwengu kwa uwezo wa kushangaza ana jambo linaloweza kumshinda kulitatua? (Luka 1:37). Unachukuliaje pale ambapo umemuomba na kusubiri sana ahadi yake bila mafanikio? Kwa nini alipojulishwa kuwa rafiki yake Lazaro ni mgonjwa alikawiakawia hadi mgonjwa akafariki? (Yohana 11:1-6). Unadhani Lazaro alijisikiaje alipoona anakaribia kufa na rafiki yake hajaja kumponya?
  5. Je Mungu angekuwa hawapendi wanadamu kwa nini hakuwaangamiza pale walipokataa kumtii na kumsikiliza kiumbe ambaye naye ameumbwa na Mungu? Unadhani jambo hilo la kukosa shukrani kwa Muumba wao lilimhuzunisha au lilimkasirisha? Kwa nini Mungu asitumie uwezo wake kututimizia yale tunayomuomba? Sababu ya kutofanya hivyo ni kwa kuwa anatuchukia?(Yeremia 31:3; Isaya 49:16; Yohana 13:1).
  6. Je kutambua kwamba Mungu anakujali kwaweza kukupunguzia maumivu na kukuongezea matumaini unapopitia vipindi vigumu vya changamoto za maisha? Hata kama uliloomba halijatimizwa kwa wakati uliohitaji unaamini kuwa Mungu hatakuacha? (Waebrania 13:5).

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 10:1-22 

  1. Je kuna mazingira ambayo mtu anaweza kuchoka na maisha? Unadhani mtu aliyechoka na maisha anatamani kuishi au anatamani kufa? Je mtu mwenye saratani yenye maumivu inayotoa harufu kali na inayoendelea kukua anaweza kufikia hatua ya kuchoka na maisha? Ili kumsaidia mtu kama huyu unafanyaje? Mungu katika nyakati kama hizo huwa wapi? Bado unaweza kusema Mungu ni upendo unapokuwa unapitia nyakati kama hizo?
  2. Je kuna nyakati Mungu anaonea watu wake au ni hisia tu zinazotokana na maumivu? Ukizingatia kuwa Mungu ndiye aliyeuumba mwili wa binadamu inatokeaje anaruhusu ushambuliwe na maradhi na kuharibiwa? Je mwanadamu wakati fulani ana mchango katika kuharibu afya ya mwili wake? Je kujua sababu ya maradhi aliyonayo mgonjwa kwaweza kuleta unafuu kwa mgonjwa huyo? Hisia kwamba ugonjwa ulio nao umetokana na kulogwa kwaweza kuwa sahihi? Je inafaa kuyashikilia mawazo hayo au kuyatupilia mbali? Je kuna wakati waweza kushughulika sana na kuagua kwa waganga wa kienyeji na kujenga uhasama na watu wakati ulikuwa ugonjwa uliotokana na kuvunja kanuni za afya na unaotibika hospitalini?
  3. Ikiwa Mungu ndiye aliyetuvika ngozi na nyama na kutuunga pamoja kwa mifupa na mishipa yawezeka akawa ndiye daktari bingwa wa miili ya wanadamu kuliko hawa madaktari bingwa tulionao? Kwa nini mara nyingi tunaweka tumaini zaidi kwa wataalamu wa tiba kuliko kwa Mungu? Je kuna wakati Mungu hutumia ugonjwa kurekebisha hali yetu ya kiroho?
  4. Je maisha ya mtu anayeteseka kwa ugonjwa wakati wote yana faida kwa nani? Mungu aliruhusuje mtu huyo aje duniani? Je kama mimba ya mtu huyo ingeharibika tumboni kwa mamaye ingekuwa na nafuu? Ikiwa maisha ya mtu huyo yatajaa mateso na baada ya kufa akutane na adhabu ya moto wa milele kulikuwa na sababu ya yeye kuzaliwa?

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 11:1-20 

  1. Unapokwenda kumuangalia mgonjwa au mhanga unapaswa kuthamini hisia zake hata kama zimepotoka au kuthamini hisia zako wewe uliye mzima? Je katika kujieleza kwa mgonjwa unaweza kugundua tatizo linalotokana na hisia za kishirikina au kuvurugika kwa mahusiano vinavyochangia kuwepo au kuongezeka kwa ugonjwa? Wale wanaobainika kwamba hawana ugonjwa baada ya uchunguzi wa maabara wanaweza kuwa na ugonjwa unaotambulika kupitia mahojiano na mgonjwa tu?
  2. Unadhani mahojiano anayofanya Sofari yanalenga kugundua kama Ayubu ana tatizo katika mahusiano yake na Mungu ili amsaidie ama wanapimana misuli ili ijulikane nani mbabe katika kujenga hoja? Je kuna hatari gani mtu anapodhani anamuelewa Mungu zaidi ya wengine? Je kumwelewa Mungu kunatokana na akili au mafunuo? Je ni sahihi dhana isemayo siku tutakayomuelewa Mungu kikamilifu bila kusaza siku hiyo Mungu atakoma kuwa Mungu?
  3. Unadhani Sofari anayemtahadharisha Ayubu kutokuwa na majivuno kwa kauli zake haonyeshi majivuno? Kwa nini wenye majivuno hukerwa sana na majivuno ya wengine? Je inawezekana Ayubu alikuwa mcha Mungu mwenye majivuno? Mtu anayekataa kutambua uwepo wa tabia zisizoridhisha kwa upande wake huwa anasumbuliwa na nini? Ni kweli kuwa hana mapungufu yoyote au ana tabia ya kujihesabia haki? Dawa ya watu kama hao ni nini?
  4. Kwa nini Sofari anasema mwanadamu huzaliwa kama mtoto wa punda-mwitu? Je sehemu kubwa ya tabia mbaya tulizonazo tulijifunza utotoni au tulizaliwa nazo? Je kujisalimisha kwa Yesu laweza kuwa jambo pekee litakalotusaidia kurekebisha tabia hizo?

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 12:1-25

  1. Kama Ayubu anatambua kuwa ana fahamu kama za washindani wake kwa nini aseme watakapokufa ndipo na hekima itakoma? Alikuwa anawakejeli? Je unamsaidiaje anayejiona anajua zaidi yako? Unampuuza au unamuonesha mapungufu yake? Unapoona Mungu akitafsiriwa vibaya unao wajibu wa kumtetea? Unadhani kati ya Ayubu na washindani wake ni nani alikuwa na haki ya kumjua Mungu zaidi? Kama Ayubu anashuhudia alikuwa na uzoefu wa kumwita Mungu na kumjibu kwa nini mara hii sikio lake limekuwa zito hata hataki kusikia?
  2. Je kuchekwa na jirani unapokuwa umekumbwa na tatizo ambalo Mungu alikuwa na uwezo wa kuliondoa kunaongeza hasira na maumivu? Unadhani unaweza kuwaaminisha watu wanaokucheka kutokana na hali yako ngumu kuwa wewe una Mungu? Ayubu analaumu kitendo cha Mungu kuwapatia vitu vingi wale aliowaita wapokonyi. Je hapa Ayubu hakumwazia Mungu kwa upumbavu? (Ayubu 1:22). Au ni kwa sababu huko mbele alitubu? Mungu anapowagawia afya njema na utajiri wasio na shukrani kwake anawakatisha tamaa wale waaminifu aliowanyima?
  3. Je viumbe wengine kando ya wanadamu wana uwezo wa kutambua kuwa kuna Mungu aliyewaumba? Wanyama wanaosafiri kutoka mbuga za nchi jirani na kuja Tanzania kila msimu fulani unapofika huwa wanaongozwa na Mungu? Wanyama, ndege, na vitambaavyo viliwezaje kutii sauti ya Mungu na wanadamu walioumbwa kwa mfano wa Mungu wasiweze?
  4. Je hekima ni majaliwa ya Mungu au hutokana na kuishi siku nyingi? Kama mdanganyaji na adanganywaye wote ni wa Mungu je kosa la anayedanganya pia ni la Mungu? Kwa nini ufahamu na hekima vyaweza kukosekana kwa wazee wakati vitu hivyo hupatikana kwa kuishi siku nyingi? Je unaiona hali ya wakuu wa watu wa nchi wakipotezwa nyikani pasipokuwa na njia na mwanga kwa kushadadia ushoga?

DISCUSSION QUESTIONS: JOB 12:1-25

  1. If Job realizes that he has the same consciousness as his competitors, why should he say that when they die, wisdom will cease? Was he mocking them? How do you help someone who thinks he knows more than you? Do you ignore him or show him his shortcomings? When you see God being misinterpreted, do you have a duty to defend him? Who do you think between Job and his competitors had the right to know God more? If Job testifies that he had the experience of calling God and answering him, why this time his ear [God] has become so heavy that he does not want to hear?
  2. Does being laughed at by a neighbor when you are faced with a problem that God had the power to remove increase anger and pain? Do you think you can convince people who laugh at you because of your difficult situation that you have God? Job blames God's act of giving many things to those he called reapers. In this very action, did Job not evaluate God foolishly? (Job 1:22). Or is it because he repented later? When God gives good health and wealth to those who are not grateful to him, does this action disappoint the faithful ones whom he denied?
  3. Do other creatures besides humans have the ability to recognize that there is a God who created them? Are the animals that travel from the parks of neighboring countries and come to Tanzania when a certain season arrives are they guided by God? How could animals, birds, and creeping things obey God's voice during Noah time and humans created in God's image could not?
  4. Is wisdom a gift from God or does it come from living many days? If both the deceiver and the deceived belong to God, is the fault of the deceiver also accounted to God? Why can understanding and wisdom be lacking in the elderly when those things are obtained by living for many days? Do you see the state of the heads of the people of the country being lost in the wilderness without a way and light for promoting homosexuality?

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 13:1-28

  1. Marafiki wa Ayubu walikuwa wanatafuta chanzo cha ugonjwa wa Ayubu ili waone namna ya kumsaidia. Kwa nini Ayubu anawaita matabibu wasiofaa? Hawafai kwa sababu hawakupata chanzo halisi cha ugonjwa wake au kwa sababu waliendeleza malumbano badala ya kumpa faraja? Je kuna wakati wataalamu wa tiba za asili au madaktari wa tiba za kisasa wa mikoani wanakuwa na msaada mkubwa zaidi kuliko madaktari bingwa wa hospitali za rufaa? Hali hiyo husababishwa na nini?
  2. Je kunyamaza kabisa kunamsaidiaje mgonjwa aliyezidiwa au aliyefikwa na majanga kukilinganishwa na maneno ya kukatisha tamaa? Je ni sahihi kumyamazisha anayelia msibani kutokana na kuondojewa na mpendwa wake. Maneno yanayotumika kufariji waliofiwa kwamba Mungu amempenda zaidi marehemu yana umuhimu wowote. Je maneno hayo yanaongeza faraja au yanaongeza uchungu?
  3. Je kuna wakati ambao hupaswi kumtetea Mungu bali Yeye mwenyewe asimame na kujitetea? Je kuna hatari gani ya kumtetea Mungu katika kila hoja? Katika kumtetea Mungu kuna uwezekano wa kuishia kuwa mdanganyaji? Je kuna uwezekano wa kuendelea kumtumainia Mungu hata kama unahisi amekutelekeza? Je mtu aweza kujiridhisha kuwa yu mwenye haki? Je ni sahihi kuwatambua kama watakatifu watu wanaomwamini Kristo Yesu? (Wafilipi 1:1) Je utakatifu wao unatokana na vile walivyo kwa sasa au vile Mungu anavyowatarajia kuwa?
  4. Je waliokombolewa na Yesu wana uhalali wa kumhoji Mungu kile anachokusudia kutokana na mambo ya utata anayoruhusu kutokea? (Isaya 41:21). Kwa nini watu wengine hujisikia hatia linapokuja swala la kumuuliza Mungu maswali magumu? Je kumwomba Mungu akuonyeshe dhambi yako ni dhambi? Unadhani Ayubu angejulishwa kuwa hana dhambi isipokuwa shida anayoipitia imetokana na tuhuma za Shetani kuwa yeye Ayubu akipitishwa kwenye mateso anaweza kumkana Mungu angejisikaje? Je hiyo ingempa unafuu kwenye maumivu yake?

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 14:1-22

  1. Kwa nini siku za kuishi za mwanadamu si nyingi nazo zimejaa taabu? Siku za kuishi zingetakiwa ziwe ngapi ili ziwe za kutosha? Je maisha yaliyojaa taabu yanamfanya mtu kutamani kuishi? Shetani ndiye aliyeishi maisha marefu kuliko kiumbe yeyote hapa duniani. Je maisha yake yana mbaraka wowote kwa dunia? Je chenye umuhimu ni urefu wa maisha uliyoishi au thamani ya maisha uliyoishi?
  2. Je kuna chochote cha kujivunia hapa duniani ikiwa sote tutakufa katika siku tusiyoijua na hatutaondoka na chochote cha maana? Je Mungu anatawaliwa na wakati? Je Mungu anaweza kuchelewa au kuwahi? Je kuna mtu anayekufa kabla hajatimiza miaka yake ya kuishi? Je inawezekana kuishi zaidi ya siku ambazo Mungu amekusudia utaishi? Je mwanadamu ana mchango wake kuhusu maisha yake yatakavyokuwa au yote hupangwa na Mungu na hakuna anachoweza kubadili?
  3. Je inawezekana kutoa kitu kisafi kutoka katika kitu kichafu? Je inawezekana mwanadamu akaishi bila kutenda dhambi? (Mhubiri 7:20; Yeremia 13:23; 1 Yohana 1:8; 1 Yohana 3:9; Waebrania 4:15). Je iliwezekanaje Rahabu kahaba awemo katika orodha ya bibi zake Yesu? Je Yesu aliyetokana na ukoo wa watu wenye sifa mbaya aliwezaje kuwa asiye na waa hata kidogo? (1 Petro 2:22).
  4. Mti ukikatwa unatumainia kuwa utachipuka tena wala machipukizi yake hayatakoma. Kwa nini wanadamu wakikatwa wanapoteza matumaini ya kuishi? Mwanadamu anapokufa hutoa roho. Je roho inayomtoka mwanadamu wakati wa kufa ni nafsi inayoweza kuishi bila mwili? Baada ya kufa mwanadamu hula chinii akisubiri siku ya mbingu kutokuwepo tena. Siku hiyo ya mbingu kutokuwepo tena ni ipi? (Ufunuo 6:14-17). Je dhana ya kuwa wanaokufa wanaenda mbinguni au motoni imetoka wapi? Je waliokufa wana uwezekano wa kuona na kushiriki mambo ya ndugu zake yanayotendeka duniani au mawasiliano hayo hayawezekani tena?

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 14:1-22

  1. Kwa nini siku za kuishi za mwanadamu si nyingi nazo zimejaa taabu? Siku za kuishi zingetakiwa ziwe ngapi ili ziwe za kutosha? Je maisha yaliyojaa taabu yanamfanya mtu kutamani kuishi? Shetani ndiye aliyeishi maisha marefu kuliko kiumbe yeyote hapa duniani. Je maisha yake yana mbaraka wowote kwa dunia? Je chenye umuhimu ni urefu wa maisha uliyoishi au thamani ya maisha uliyoishi?
  2. Je kuna chochote cha kujivunia hapa duniani ikiwa sote tutakufa katika siku tusiyoijua na hatutaondoka na chochote cha maana? Je Mungu anatawaliwa na wakati? Je Mungu anaweza kuchelewa au kuwahi? Je kuna mtu anayekufa kabla hajatimiza miaka yake ya kuishi? Je inawezekana kuishi zaidi ya siku ambazo Mungu amekusudia utaishi? Je mwanadamu ana mchango wake kuhusu maisha yake yatakavyokuwa au yote hupangwa na Mungu na hakuna anachoweza kubadili?
  3. Je inawezekana kutoa kitu kisafi kutoka katika kitu kichafu? Je inawezekana mwanadamu akaishi bila kutenda dhambi? (Mhubiri 7:20; Yeremia 13:23; 1 Yohana 1:8; 1 Yohana 3:9; Waebrania 4:15). Je iliwezekanaje Rahabu kahaba awemo katika orodha ya bibi zake Yesu? Je Yesu aliyetokana na ukoo wa watu wenye sifa mbaya aliwezaje kuwa asiye na waa hata kidogo? (1 Petro 2:22).
  4. Mti ukikatwa unatumainia kuwa utachipuka tena wala machipukizi yake hayatakoma. Kwa nini wanadamu wakikatwa wanapoteza matumaini ya kuishi? Mwanadamu anapokufa hutoa roho. Je roho inayomtoka mwanadamu wakati wa kufa ni nafsi inayoweza kuishi bila mwili? Baada ya kufa mwanadamu hula chinii akisubiri siku ya mbingu kutokuwepo tena. Siku hiyo ya mbingu kutokuwepo tena ni ipi? (Ufunuo 6:14-17). Je dhana ya kuwa wanaokufa wanaenda mbinguni au motoni imetoka wapi? Je waliokufa wana uwezekano wa kuona na kushiriki mambo ya ndugu zake yanayotendeka duniani au mawasiliano hayo hayawezekani tena?

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 15:1-35 

  1. Je mtu mwenye hekima hutambulika kwa namna anavyojibu maswali? Majibu ya uvuvio ya mtu mwenye hekima yakoje? Je mtu mwenye hekima aweza kujibu hata mazungumzo yasiyo na faida? Mazungumzo yasiyo na faida yanatambulikaje? Mazungumzo yanayoondoa kicho kwa anayestahili kicho ni sehemu ya mazungumzo yasiyo na faida? Je kuna uhusiano wowote kati ya mazungumzo yanayomuondolea kicho anayestahili kicho na uovu ulio ndani ya mnenaji? Je kunahitajika umakini katika kutoa matamko kuepuka midomo yako mwenyewe kukuhukumia makosa?
  2. Mtu anayejidhania kuwa yeye peke yake ndiye mwenye hekima anasaidiwaje? Mtu akidhania kuwa ana hekima iliyo bora zaidi ya kuliongoza kanisa la Mungu anaonesha dharau kwa Mungu? Je mtu akionesha dharau kwa wazee wenye rika moja na baba yake anaonesha dharau kwa baba yake pia? Je asiye na kawaida ya upole anaashiria kutokuwepo utulivu au amani moyoni mwake?
  3. Kwa nini mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke hawezi kuwa safi na hawezi kuwa mwenye haki? Inakuwaje hata mbingu nazo zisiwe safi machoni pa Mungu? Kwa nini Mungu hawategemei watakatifu wake? Mungu anamchukuliaje mwanadamu anywaye uovu kama anywavyo maji?
  4. Wale wanaonyosha mkono juu ya Mungu na kuendelea kuwa na kiburi kinyume cha Mwenyezi Mungu atawafanya nini? Je Mungu aweza kupukutisha mafanikio ya watu kama hao yanayowafanya kuwa na kiburi? Kutunga mimba za madhara zinazozaa uovu ni kitu cha namna gani?

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 16:1-22

  1. Unadhani rafiki wa Ayubu walistahili kuitwa wafariji wataabishaji? Utaabishaji wao ulikuwa katika kufanya nini? Wanawezaje kuwa wafariji wakati huo huo wakiwa wataabishaji?

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 17:1-16 

  1. Ukitambua kuwa siku zako za kuishi zimebaki kidogo kutokana na taarifa ya daktari utachukua hatua gani? Je maombi katika hatua kama hiyo ni ya muhimu? Je ikiwa taarifa hizo wamepewa ndugu wanaomuuguza mgonjwa wana haja ya kumjulisha mgonjwa mwenyewe? Je huduma ya kumpaka mafuta mgonjwa hufanyika kwa lengo gani? Je, ni kwa kusudi la kuzuia asifariki? Ikiwa baada ya huduma hiyo mgonjwa atafariki nani anastahili lawama?
  2. Je mgonjwa anayejua atakufa anatakiwa kupinga au kutoukubali ukweli huo? Je, anahitaji kupatana na Mungu wake kwanza? Je anapaswa kujifikiria yeye zaidi au kuwafikiria zaidi wanaobaki na kuweka sawa mambo yao? Katika kutafuta maridhiano na Mungu anaweza kuomba kuongezewa siku za kuishi ili aweke sawa mambo yake na ya wale wanaobaki?
  3. Hisia za kusamehewa na kupatana na mliotofautiana katika kipindi cha uhai vyaweza kumfanya mgonjwa aliye katika hali ya kufa kukikabili kifo kwa ujasiri na kupumzika kwa amani? Katika hatua ambayo mgonjwa amehakikishiwa kuwa hatapona lawama kwa Mungu, kwa madaktari, na ndugu huwa zinaepukika? Ni kweli kuwa madaktari na hata ndugu wanaweza kusababisha kifo cha mgonjwa?
  4. Je kukubali kuwa unaelekea kufa baada ya kuhakikishiwa hivyo ni jambo jema? Ni nini ungependa kuongea au kufanya katika hatua kama hiyo? Je wanao, wazazi wako, au mwenzi wako wa maisha angependa kusikia nini kutoka kwako kitakachobaki katika kumbukumbu zake?

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 18:1-21 


MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 19:1-29 

  1. Je maneno yana uwezo wa kumvunja vunja mtu? Je kuna haja ya kupima kama maneno yetu yanaweza kuwadhuru wengine? Kama Mungu amekupa uwezo wa kustahimili maneno yanayoumiza kuna haja ya kuwaomba wanaoyatoa kuacha kufanya hivyo? Je kuna ukweli kwamba wapo watu waliojaaliwa na Mungu kutoa maneno yanayoumiza?
  2. Je ni kweli kuwa hata watu au wanyama wanaodhaniwa ni wakatili hufika wakati wakahotaji huruma za Mungu au za wanadamu? Haja ya kutaka kuhurumiwa inakujaje wakati wao wenzao walipolia hawakuwahurumia? Je, maumivu ni kitu cha muhimu na chenye faida maishani mwetu? Je, Mungu anajua maumivu wanayopitia watu wake? (Kutoka 3:7)
  3. Je, ni sahihi kwa Ayubu kusema Mungu amempotosha? Je katika maisha haya kuna wakati wa mwanadamu kuvuliwa utukufu wake? Uzoefu huo huwa ni mchungu kiasi gani? Je uzoefu huo una umuhimu wowote katika kuimarisha tabia za mtu? Je umewahi kutengwa na watu uliowahi kuwasaidia? Je ulijilaumu kwa nini uliwasaidia? Je uliwakumbusha kuwa uliwahi kuwasaidia? Unadhani ni watu wote wanaostahili kusaidiwa?
  4. Kutambua kuwa unaye mtetezi asimamaye kando yako daima ili kukupigania kunaweza kupunguza msongo wa mawazo? Je Mungu ana mpango wa kuwarejeshea viungo afya yao wale ambao wamepoteza vitu hivyo? Kwa nini Ayubu anasema atamwona Mungu pasipo mwili wake? Je Yesu atakaporudi watu wangapi watamwona? (Ufunuo 1:7; Matendo 1:10-11).

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 20:1-29  

  1. Je, kuna ushahidi unaothibitisha kuwa shangwe ya waovu ni kwa muda kidogo na furaha ya wapotovu ni ya dakika moja? Kwa nini shangwe na furaha yao huwa haidumu? Kwa nini watu huikimbilia furaha hiyo na hali ni furaha isiyodumu? Furaha idumuyo inapatikanaje? Wanaolazimisha kujipatia mali na vyeo isivyo halali hufanikiwa kupata furaha?
  2. Je kudhulumu haki za watu kwaweza kukufanya upoteze heshima yako katika jamii? Je mwanadamu anaweza kushuka thamani hadi afanane na mavi yake mwenyewe? Je kushuka chini kiuchumi na kiroho baada ya kutumia vibaya fursa zilizokuwepo kunatoa nafasi ya mtu kama huyo kupanda tena?
  3. Je ni kweli kuwa uovu una utamu kinywani mwa anayeutenda? Kinachofanya watu waing'ang'anie dhambi ni kwa sababu wanaihurumia? Kwa nini dhambi zingine huwa na matokeo machungu tofauti na zinavyokuwa wakati unapozifanya? (Methali 23:29-32; Methali 6:32-33).
  4. Je, aliyepata mali kwa dhuluma huwa hana furaha nayo na kwamba haokoi chochote katika hiyo mali? Je ni kweli kuwa mkono wa kila anayesumbuliwa utamjia na mali zake hazitadumu? Je ni sababu gani inayowafanya watu kutafuta utajiri hata kwa njia ya kudhuru au kudhulumu wengine ikiwa hawataweza kuzifurahia hizo mali? Je kungojea mibaraka kutoka kwa Mungu badala ya kujipatia utajiri kwa hila kunalipa?

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 21:1-34

  1. Je, nikibaini kuwa mwenye jawabu na tatizo ninalolipitia ni Mungu napaswa kusubiri? Je waovu wananeemeshwa na nani? Je kuna wakati Mungu anawaneemesha waovu na kuwasahau watu wake? Kwa nini waovu wasipatwe na mambo mazito ili kuwafanya waache kufanya uovu? Je kuna wakati sababu ya kukata tamaa mtu anaweza kuacha kumuomba Mungu?
  2. Je mtu awaye yote aweza kumfundisha Mungu maarifa? Je waliokufa hulala makaburi na kuliwa na mafunza au huenda mbinguni na motoni?

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 22:1-30 

  1. Je Mungu hufurahia mwanadamu anapokuwa mwenye haki? (Mwanzo 7:1; Warumi 1:17; Warumi 3:10). Je mwanadamu anapofanya juhudi zake mwenyewe ili awe mtimilifu Mungu hupata faida yoyote? Je Mungu aweza kumkemea au kumwadhibu mtu anayemcha? Je kila maumivu wayapatayo wanadamu yanatokana na uovu wao? Kumpa maji ya kunywa aliyechoka katika mazingira yako unakufananisha na nini? Umeshafikiria wenye njaa ambao uliwajibika kuwalisha na hukufanya hivyo? Kushindwa kuwahudumia wahitaji kwaweza kutuzuia kutorithi ufalme wa Mungu? (Mathayo 25:41-42).
  2. Je kanisa lako na wewe binafsi una mkakati wa kuwasaidia wajane na wagane? Je unadhani ni wajibu wako kuwasaidia watu hao hata kama si ndugu zako? Je kumjua Mungu kwaweza kumfanya mtu kuwa na amani? Je kumjua Mungu kwaweza kufanya mema yakujie? Je yaliyomkuta Ayubu yalitokana na kutomjua Mungu? Kwa nini watu wengine huwa wepesi kuinuka wanapoanguka na wengine huwa ni vigumu?

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 23:1-17 

  1. Pigo gani lililowahi kukupata maishani ambalo bado unalikumbuka ingawa lilitokea zamani sana? Kwa nini inakuwa vigumu kulisahau pigo hilo? Je, unadhani Mungu anastahili lawama kwa kushindwa kuzuia pigo hilo? Je kuna faida yoyote katika kumfahamu mbaya wako na njama anazokufanyia? Unadhani kumfahamu kutakupatia amani au unafuu wowote?
  2. Je umewahi kufikia hatua ambayo huoni nuru katika maisha yako yajayo ila giza na hali ya kukata tamaa ambapo Mungu anaonekana kuwa mbali nawe? Je, pale ambapo huwa hatujui kesho yetu itakuwaje Mungu huwa anajua? Je, katika mazingira kama hayo inaweza kuwa salama kumtegemea Mungu ili akuvushe? Je mapito kama hayo yanakusudia kutuharibu au kutufanya kuwa bora zaidi? Unadhani matatizo huwafanya watu kumsogelea zaidi Mungu au kumkimbia?
  3. Je Mungu anatushirikisha anapopanga kuruhusu pigo litokee maishani mwetu? Angekuwa anatushirikisha kutoa maoni yetu unadhani tungeridhia kila Mungu anachokusudia kufanya kwa ajili yetu? Ni mawazo gani yangekuwa bora zaidi kati ya yale ya kwake na yale ya kwetu?

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 24:1-25

  1. Je kuna wakati dhuluma hufanyika kwa kuondoa alama za mipaka? Wajibu wa mamlaka za kisheria katika jamii ni upi wakati migogoro ya mipaka inapotokea? Na kama migogoro ya mipaka inasababishwa na mamlaka zinazosimamia alama za mipaka ufumbuzi wake huwa nini? Nini kinatakiwa kufanyika ili kuepuka migogoro ya mipaka? Ili mali unayoimiliki itambuliwe kuwa ya kwako unatakiwa kufanya nini? Je kwa kutumia vifungu vya sheria mtu aweza kunyang'anywa mali iliyo yake?
  2. Je juhudi za mtu anayetafuta kujikwamua kwenye umaskini wa kipato zawezaje kukwamishwa na watu wenye fedha? Je unyonge wa maskini una uhusiano wowote na utajiri wa maskini? Je, ni nani anayemhitaji mwenzake zaidi kati ya tajiri na maskini? Je hali ya mazingira ya mahali husika yaweza kuwa kikwazo cha mtu kujipatia mahitaji muhimu? Je jangwa laweza kutoa chakula kwa ajili ya watoto wako?
  3. Ni kwa namna gani wanaofanya dhuluma kwa watu wanakuwa wameuasi mwanga? Kwa nini dhambi nyingi hufanyika gizani? Muuaji anayewaua waskini na wahitaji ana tofauti gani na anauewaua matajiri? Vita ya maskini na tajiri ni nani mwenye uwezekano wa kuibuks mshindi? Maskini wasipoungana na kumtegemea Mungu zaidi wana uwezekano wa kushinda vita yao dhidi ya matajiri?
  4. Mungu ameahidi kushughulika vipi na wanaodhulumu maskini? (Yakobo 5:1-5). Mungu anaahidi nini kwa wanaodhulumiwa na wasio na matumaini ya kuishi? (Ayubu 24:22-23). Je, unadhani kuna tumaini la kupata haki wakati mifumo ya utoaji haki inapokuwa imeharibika? Je unaamini kuwa utulivu na amani ni zao la haki? Je wanyonge wanaonyimwa haki zao wana uwezo wa kuifanya jamii isiwe na utulivu?

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 25:1-6 


MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 27:1-23

  1. Ayubu anamaanisha nini anaposema roho ya Mungu i katika pua yake? Je pumzi tuivutayo kupitia puani hutambuliwa kama roho ya Mungu? Je kwa tafsiri hiyo kuna uwezekano ile roho inayomrudia Mungu siku mwanadamu anapofariki ikawa ni pumzi ya uhai? (Mhubiri 12:7). Kama roho ni pumzi ya uhai kuna mantiki yoyote ya kusema Mungu aiweke roho ya marehemu peponi?

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 28:1-28

  1. Je ardhi ndiyo chimbuko la utajiri wa dunia? Je Mungu aliweka uwiano sawa katika kuweka madini na mali nyingine ardhini au yapo maeneo yaliyopendelewa zaidi? Kwa nini katika maeneo yanayodhaniwa kupendelewa zaidi kama Afrika maendeleo yake hayalingani na utajiri ambao Mungu aliwekeza katika ardhi yake?
  2. Kwa nini kazi ya kwanza ya binadamu ilikuwa kuilima ardhi na kuitunza? Kwa nini kuna njaa wakati ardhi itoayo chakula ipo? Ukusanyaji wa maji na uchimbaji wa visima ni wa muhimu ili kujihakikishia kuwepo kwa chakula? Kwa nini shughuli ya kilimo haionekani kama ajira ya maana leo? Unadhani utaalamu wa kutambua madini ardhini unahitajika zaidi leo ili kunufaika na utajiri huo ulio ardhini?
  3. Je kutambua thamani yako ndiyo mwanzo wa mabadiliko yako makubwa ya kiuchumi? Mtu huitambuaje thamani yake? Mungu alimpa mwanadamu uwezo gani wa kutawala mazingira yake na kuyabadilisha kuwa utajiri? Kwa nini wanadamu wengine wameruhusu kutumika kuwatajirisha wengine huku wenyewe wakibakia maskini?
  4. Je kumfahamu Mungu na kumruhusu kuyaongoza maisha kwaweza kuwa chanzo cha mafanikio ya kiuchumi? (Zaburi 37:25) Je, ni kweli kuwa koo na maeneo yaliyowapokea wamishionari wa Kikristo katika Afrika zilipiga hatua kubwa ya maendeleo ukilinganisha na zile ambazo hazikuwapokea? (Methali 1:7)

MASWALI KUJADILI: AYUBU 29:1-25 

  1. Je kuna wakati umetamani maisha uliyoishi zamani? Je unahisi nini kilitokea kilichobadilisha mahusiano yako na Mungu na watu wako wa karibu? Unadhani upo uwezekano wa kuyarejea maisha hayo ya awali? Je umeshawahi kujihukumu kwa mambo ambayo unadhani ulichangia hadi kuwepo kwa hali hiyo? Unadhani kuna mambo ambayo huwezi kamwe kuyatolea maelezo ni kwa nini yalitokea?
  2. Kuna wakati katika maisha ambapo watoto waliokuwa wakiizunguka meza ya chakula hawaendelei kuishi na wazazi tena. Je maisha hayo yanaweza kuvuta hisia za huzuni na upweke? Watoto wanapaswa kufanya nini katika mazingira hayo? Je hiyo inaweza kuharakisha kifo Cha wazazi hao?
  3. Je maisha yaliyotumika kubariki watu katika kipindi cha ujana na utu uzima huvuta mibaraka wakati wa uzee wa mtu? Je hekima ya mtu ina kawaida ya kupungua au kuongezeka kadri umri unavyoendelea? Je umekuwa mshauri wa watu usiowajua na mguu kwa anayechechemea? Unajisikiaje baada ya kuwatia moyo waliokata tamaa?

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 30:1-31

  1. Kwa nini watu wazima hawapendi kufanyiwa dhihaka na watu walio wadogo kwao au ambao baba zao hawakuwahi kuwafanyia dhihaka? Je kuna haja ya kuthibitisha kuwa unao uwezo kwa mtu unayejua umemzidi uwezo kwa mbali sana? Je watoto wanapofanyia dhihaka wakubwa watoto hao wanastahili kufanywa nini? Je watoto waliomdhihaki Nabii Elisha walistahili kupewa adhabu waliyopewa? (2 Wafalme 2:23-24). Kwa nini Elisha hakuwasamehe kama Yesu alivyowasamehe waliomkosea? (Luka 23:34).
  2. Je wanadamu waliomtemea mate Yesu wangejua ndiye aliyewaumba wangethubutu kufanya hivyo? Kwa nini Yesu hakuwatambulisha kuwa Yeye ndiye aliyewaumba ili wasiendelee kumtemea mate? Unadhani hatua hiyo ingeweza kusaidia kukomesha dharau na dhihaka alizokuwa anatendewa? Kuna wakati watu wanaweza kukutendea dhihaka na dharau kwa kuwa umekuwa na mahusiano mazuri na Mungu wako? Je kunenewa mabaya ambayo hujayafanya kwaweza kukushushia heshima na hadhi yako katika jamii?
  3. Ugonjwa wa Ayubu uliwezaje kuharibu mavazi yake? Kwa nini Ayubu anamlaumu Mungu kutokana na maradhi yake? Unapomuuguza mgonjwa aliyeugua kwa muda mrefu na aliye mwaminifu kwa Mungu wake kwa nini Mungu hamponyi utamjibuje? Je ni halali kwa mgonjwa kulilia msaada katika ugonjwa wake? Nyumba waliyoandikiwa wenye uhai wote ni ipi? Je unapolipwa mabaya kwa mema uliyotenda inakufanya usiendelee kutenda mema?

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 31:1-40

  1. Je kuna ubaya gani katika kumwangalia msichana? Je kumwangalia msichana kwa kumtamani kuna uzito zawa na kuzini? (Matayo 5:28). Binti anayevaa katika namna ya kutamanisha wanaume ana hatia yeyote? (Ezekieli 13:18-20).
  2. Kwa nini wanawake wanashauriwa kuvaa nguo za adabu na zenye kujisetiri? (1 Timotheo 2:9). Je ni kweli kuwa uzinzi unasababishwa na wanawake wasiosetiri miili yao? Kwa nini nyakati walizoisho watu wa kale waliokuwa wanajifunika magome hazikuwa na matukio ya ubakaji na zinaa wakati wanawake walikuwa kwa sehemu kubwa wanatembea uchi?
  3. Ayubu anapojiapiza kuwa kama alishawahi kushawishika na mwanamke mke wake asage kwa mwingine na wengine wainame juu yake ana maana gani? Je uzinzi unafukuza baraka? Ayubu anashuhudia kwamba alikuwa mtoaji wa msaada kwa maskini, wajane na yatima. Aliwezaje kuwa tajiri mkuu upande wa Mashariki? Je usemi kuwa amsaidiaye maskini humkopesha Bwana ina ukweli gani?
  4. Matajiri wa leo wangeweka kipaumbele cha kuwasaidia wahitaji dunia yetu ingekuwaje? Je matajiri wangekuwa matajiri zaidi na maskini wangekosekana? (Kumb. 15:4). Je kufurahi kwa sababu mali zako zimekuwa nyingi ni dhambi? Kwa nini Ayubu anatamba kuwa hakuwahi kufurahi kwa sababu ya mali yake kuwa nyingi? Je inawezekana kuwa tajiri lakini usiitumainie mali yako?

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 32:1-22

  1. Kutotambua kuwa una mapungufu ni kujihesabia haki na ni kujitwalia haki ambayo Mungu pekee ndiyo anayo. (1 Yoh. 1:10). Je unaiona hali hiyo kwa Ayubu? Je Mungu hakuwa ametangulia hapo mapema kumtambulisha Ayubu kama mtu mkamilifu? Kulikuwa na ubaya gani basi kwa yeye Ayubu kujitambulisha kama asiye na mapungufu? Je wakati wazee wanatoa hoja ni sahihi kwa kijana kuingilia kati na kuwasahihisha? Elihu aliposema yafaa siku ziseme na wingi wa miaka ifundishe hekima alimaanisha nini? Je umri una mchango gani katika kumuongezea mtu hekima?
  2. Ni nini kinachohitajika ili mtu aweze kujibu maswali kwa usahihi? Kipi muhimu kati ya kujibu swali na kulielewa swali? Watu wengi wanaoshindwa kujibu swali ni kwa kuwa hawakulielewa swali? Kwa nini watu wenye kiherehere hukosea sana katika kuelewa hoja na kujibu maswali? Unapoona hoja inapotoshwa waweza kuendelea kukaa kimya hata kama hoja haikuhusu?
  3. Je kujipendekeza kunaweza kusababisha watu kutosema ukweli? Nini humsukuma mtu kutaka kujipendekeza kwa wengine? Unapaswa kufanya nini kwa mtu anayejipendekeza kwako? Kupendelea kwaweza kusababisha kazi kuharibika? Nini husababisha kupendelea watu wasio na sifa? Je Mungu ana upendeleo? (Matendo 10:34). Kama hana upendeleo kwa nini koo au mataifa fulani huonekana kustawi zaidi kuliko mengine?

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 33:1-33 

  1. Ayubu anaposema Roho ya Mungu imeniumba (fng 3) anamaanisha nini? Je Roho mwenye uwezo wa kuumba ana hadhi ya kuwa Mungu? Kama Roho alihusika katika kumuumba mwanadamu Baba na Mwana (nafsi) walihusika katika nini? Je walishirikiana? (Mwanzo 1:26). Kama Roho alihusika kuumba dhana kuwa hadhi yake ni ya chini kuliko ya Baba inatokana na nini?
  2. Elihu anaposema alifinyangwa katika udongo anamaanisha nini? Je anaelezea asili ya mwanadamu kwamba ilitokana na kufinyangwa kwenye udongo? (Mwanzo 2:7). Kwa nini dhana ya kuwa mwanadamu alitokana na nyani imeshamiri sana licha ya kuweko ushahidi wa Maandiko kwamba alitokana na udongo?
  3. Je ni sahihi mtu kujidhania kuwa hana makosa, hana hatia, na hana uovu ndani yake? (Warumi 3:12; 1 Petro 2:22; Mathayo 27:3). Je Mungu analazimika kutoa maelekezo juu ya maumivu anayoruhusu kutokea kwa wanadamu? Je inatosha kuamini kuwa kazi ya Mungu haina makosa? Je maumivu ambayo Mungu huyaruhusu kwa wanadamu yaweza kuwa na lengo la kuwaepusha na madhara makubwa zaidi? Je ukomo wa maumivu ambayo Mungu huyaruhusu kwa wanadamu?
  4. Je kutoa ushuhuda juu ya uponyaji wa Mungu ni kwa muhimu kwa mtu aliyeponywa kutoka kwenye mapito magumu ya maisha? Ni faida gani inayopatikana kwa Mungu, kwa mtu husika, na kwa wanaosikiliza shuhuda? Je kuna nyakati ambazo Mungu aliokoa nafsi yako isiende shimoni? Unadhani ni kipi ulistahili kati ya nafsi yako kuokolewa na kwenda shimoni? Je kujua kuwa mema unayotendewa na Mungu hukustahili kwaweza kupunguza manung'uniko?

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 34:1-37

 


 MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 35:1-16 


MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 36:1-33 

  1. Mungu hamdharau mtu yeyote. Je mtu anayemuwakilisha Mungu au anayejinasibu kuwa ni mtu wa Mungu aweza kuonesha dharau kwa watu? Kumdharau mtu kuna madhara gani? Je unayemdharau unaweza kumpenda? Je mtu anayemuaibisha Mungu anastahili kudharauliwa? Je unapomdharau mtu unamkosea Mungu? Kwa nini Mungu huwa hadharau watu? Je, anayedharau watu anaonyesha uhodari au anaonyesha woga?
  2. Je kuna namna majivuno huchangia mateso wayapatayo wenye haki? Je Mungu anao mpango wa kuwafanya wenye haki kuwa watawala na kuwaketisha kwenye viti vya enzi milele? Je mateso wanayoyapitia ni sehemu ya maandalizi ya mpango huo? Je, kusikia sauti ya Mungu na kuitii kunaleta mafanikio gani maishani? Je Mungu anao mpango wa kuwaponya wanaotaabika? Ni nini kinachomzuia Mungu kufanya hivyo? Mungu anatoa ushauri gani kwa watu kama hao?
  3. Je, ni kweli kuwa Mungu ni mkuu kiasi ambacho sisi hatumjui? Ni nini kinachotuzuia tusimjue Mungu? Nini kingetokea kama tungemjua Mungu vizuri? Kwa nini hesabu ya miaka ya Mungu haitafutiki? Kwa nini Mungu hana mwanzo na wala hana mwisho? Je, kuutazama uovu kuna madhara yoyote? Utajiepushaje kuutazama uovu ikiwa unaishi katikati yake? Je kwenda kuishi nje ya miji yenye uovu ni suluhisho la uovu?
  4. Mvua hutengenezwa na mvuke utokao baharini unaojikusanya kwenye mawingu. Je Mungu ana sehemu gani kwenye mchakato huo wa kisayansi? Je mvua inapoadimika ni sahihi kumuomba Mungu alete mvua? Nani aliye juu ya mwingine kati ya wanasayansi na Mungu? Je wanasayansi wanajua kila kitu au kuna mambo mengi wasiyoyajua kwenye elimu ya sayansi wanayopaswa kujifunza kutoka kwa Mungu? Je ukisikia mwanasayansi anadai hakuna Mungu unahisi nini kichwani mwako?

 MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 37:1-24 

 


MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 38:1-41

 


MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 39:1-30 


MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 40:1-24 

  1. Je inawezekana kushindana na Mungu kwa hoja? Je unadhani kuna swali gumu ambalo Mungu hawezi kulitolea ufafanuzi? Je kama ana upendo na anaacha watu wakionewa na wenye nguvu upendo wake Mungu huyo uko wapi? Wakati Waafrika walipovamiwa na wageni na kuuzwa utumwani na kutawaliwa na wakoloni upendo wake ulienda wapi? Akitokea mtu akasema Mungu alikuwa amezidiwa nguvu au alikosa upendo atakuwa yupo sahihi?
  2. Je kuna wakati unaona Mungu au mkubwa wako anastahili kubebeshwa lawama lakini unasita kutoa lawama hizo? Je ni sahihi kuamini kuwa Mungu au mkuu wako hata akikosea huwa ana nia njema? Je kulalamika mbele ya watu juu ya kiongozi wako ni sahihi? Wale wanaojaribu kumsahihisha Mungu wanalenga kuwaaminisha watu kuwa wana uwezo zaidi kuliko Mungu?
  3. Kwa nini Mungu ameweza kuumba viumbe aliowajalia uwezo mkubwa lakini akashindwa kuumba viumbe wenye uwezo wa kushinda dhambi kama malaika na wanadamu? Je Mungu alikuwa na uhalali wowote wa kuwatoa Wakaanani kutoka nchi yao na kuwapatia Waisraeli? (Walawi 18:24-25). Je, Mungu anayewatunza wanyama wa mwitu aweza kuwasahau 7wanadamu walioumbwa kwa mfano na sura yake? (Mathayo 6:25-34)

MASWALI YA KUJADILI: AYUBU 42:1-17