Seventh-day Adventist® Church

PASTOR LETTA'S OFFICIAL WEBSITE

Menu

KIHONDA NET EVENT

MFULULIZO WA HOTUBA ZA ATAPE KIHONDA NET EVENT

ATAPE KIHONDA NET EVENT: NYAYO ZA MATUMAINI:

SIKU YA 01/21

HUDUMA KUU:

TAREHE: 13/05/2023

MHUDUMU, MCH. PAUL SEMBA

SOMO: NYAYO ZA MATUMAINI:

Tunaishi katika dunia ambayo haina matumaini kwa sababu kadha wa kadha lakini katika masomo haya tutaona mambo mbalimbali ambayo yanaifanya dunia kukosa matumaini, miongoni mwa mambo hayo ni kama vile: VITA. Kila sehemu kuna vita, wakimbizi kila mahali ambapo hupelekea njaa, majonzi, vifo na magonjwa yanayotokana na njaa. Habari gani matetemeko ya ardhi kila mahali hakuna matumaini, ulimwengu hauna amani. Habari gani Uviko 19, ilivyoua watu na kupoteza matumaini kwa watu.

Neno la Mungu linasema;

“Kisha nikaisifu furaha, kwa sababu mwanadamu hana neno lo lote lililo jema chini ya jua, kuliko kula, na kunywa, na kucheka; na yakuwa hilo likae naye katika amali yake, siku zote za maisha yake alizompa Mungu chini ya jua.” (Mhubiri 8:15)

Yesu alisema haya pia katika matukio mawili wakati wa Nuhu na wakati wa Lutu;

“Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu.” (Luka 17:26)

“Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote.” (Luka 17:27)

“Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga.” (Luka 17:28)

“Lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote.” (Luka 17:29)

“Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu.” (Luka 17:30)

Dunia kwa sasa haina amani kabisa kwa sababu ya kukosa amani, utulivu na Matumaini.

Gharika ilikuja kwa Sababu watu hawakuzingatia utaratibu wa Ndoa.

“Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.” (Mwanzo 6:1-2)

Hawakuzingatia utaratibu wa kijamii.

“Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wa wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? Uwatoe kwetu, tupate kuwajua.” 

Mwanzo 19:5

“Lutu akawatokea mlangoni, akafunga mlango nyuma yake.” 

Mwanzo 19:6

“Akasema, Basi, nawasihi, ndugu zangu, msitende vibaya hivi.” 

Mwanzo 19:7

Tazama, ninao binti wawili ambao hawajajua mtu mume, nawasihi nitawatolea kwenu mkawafanyie vilivyo vyema machoni penu, ila watu hawa msiwatende neno, kwa kuwa wamekuja chini ya dari yangu. 

Mwanzo 19:8

Wakasema Ondoka hapa! Kisha wakanena, Mtu huyu mmoja amekuja kwetu kuketi hali ya ugeni; naye kumbe, anataka kuhukumu! Basi tutakutenda wewe vibaya kuliko hawa. Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu, wakakaribia wauvunje mlango. 

Mwanzo 19:9

Lakini wale watu wakanyosha mikono yao, wakamwingiza Lutu kwao nyumbani, wakaufunga mlango. 

Mwanzo 19:10

Mambo ya ngono na ushoga.

Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; 

Warumi 1:26

wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao. 

Warumi 1:27

Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. 

Warumi 1:28

Mwanzo 6:9-13.

Dunia ilikuwa imejaa dhuluma, jamii haijifunzi tusomapo katika nyakati za Lutu na Nuhu.

Kuna ubatili unaofanyika juu ya nchi, kwamba wako wenye haki nao wapatilizwa kama kwa kazi yao waovu; tena wako waovu, nao wapatilizwa kama kwa kazi yao wenye haki. Nami nikasema ya kuwa hayo nayo ni ubatili. 

Mhubiri 8:14

Hata katika kisiasa hatujifunzi, vita baina ya mataifa na mataifa mengine kama vile Urusi na Ukraine. Habari gani vita ya mwaka 1919, na vita kuu ya pili ya mwaka 1939. Je, ni wapi wanadamu wanajifunza katika hili? Kizazi baada ya Kizazi huingia katika vita yaani ni vita kwa vita hivyo kwa haya yote jamii haijifunzi kabisa. 

Mwisho mwanadamu anafikia kusema hakuna maisha kwani kuna magumu, kuna ukatili na jambo lingine ni kwamba maisha hayana maana, mwanadamu anakata tamaa kisha anajiua kwa sumu, kwa vidonge, na kujinyonga. Kwa bahati mbaya watu wote matajiri au masikini, wenye ndoa na wasio na ndoa kila mahali watu wasomi na wasio wasomi wanajiua kwa kuona maisha hayana maana kabisa. Habari gani Kifo kinapoondosha ndugu zetu watu hujiuliza kwanini haya? 

Je, Tumaini liko wapi sasa? Tumaini liko kwa Yesu pekee. Hakuna maisha yenye matumani sahihi kwenye dunia hii au kwenye vyeo ni kwa Yesu pekee.

Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini.

Warumi 15:4

Neno la Mungu peke yake ndilo lenye tumaini katika dunia isiyo na Matumaini. Kwani neno linasema;

Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. 

Yeremia 29:11

Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. 

Waebrania 4:12

Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako. 

Zaburi 119:9

Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. 

Zaburi 119:11

Ni neno peke yake linaweza kuleta amani, neno linatakasa na kuleta amani Moyoni mwa kila aaminie maneno ya Mungu.

Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. 

Yohana 17:17

Neno linaendelea kusema;

Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; 

2 Timotheo 3:16

ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema. 

2 Timotheo 3:17

Ni katika neno tunapata faraja, amani, uvumilivu na utulivu katika Bwana.

Bwana asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani? 

Isaya 66:1

Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema Bwana; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu. 

Isaya 66:2

Neno la Bwana ni taa na Mwangaza katika magumu yote. Kama neno lisemavyo kwamba,

Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu. 

Zaburi 119:105

TUMAINI PEKEE LA MAISHA YA KWELI KWA MWANADAMU, LINAJENGWA KATIKA NENO LA BWANA PEKEE, UKILIAMINI LITAKUONGOZA VYEMA. MUNGU AKUBARIKI UNAPOTAFAKARI NENO YAKE




ATAPE KIHONDA NET EVENT: NYAYO ZA MATUMAINI:

SIKU YA 02/21

HUDUMA KUU

TAREHE: 14/05/2023

MHUDUMU: MCHUNGAJI PAUL SEMBA

SOMO: NYAYO KATIKA MAPAMBANO

Ulimwengu unajiuliza nini chanzo cha mambo haya duniani? Magonjwa, Vifo na mchungu yote nk..

Historia inatuonyesha kwamba ulimwengu ulikuwa mkamilifu pasipo dhambi, katika Mwanzo 1;2. Lakini ulimwengu unaanguka katika anguko la Dhambi, tunaona Pambano likianza katika Mwanzo sura ya Tatu (3), Pambano kati ya Wema na Uovu yaani Mungu na Shetani, ambapo ndiyo mwanzo wa Uchungu na Machungu yote tunayopitia wanadamu leo. Kupitia udanganyifu wa Shetani pale Edeni, ilipelekea mwanadamu kuanguka dhambini. Lakini tumaini la pekee ni Nyayo za Mungu za Matumaini zinazotembea Bustanini zikiuliza Adamu uko wapi?

Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? 

Mwanzo 3:1

Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; 

Mwanzo 3:2

lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. 

Mwanzo 3:3

Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, 

Mwanzo 3:4

kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. 

Mwanzo 3:5

Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala. 

Mwanzo 3:6

Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo. 

Mwanzo 3:7

Shetani amekuwa akibadili Neno la Mungu ili kujinufaisha mwenyewe, ndiyo maana Mungu wetu kila wakati hajwahi kukosea maelekezo yake.

nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino. 

Mwanzo 3:15

Pambano tunalojifunza katika Sura hii ni Pambano kati ya Mungu na Nyoka.

Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. 

Mwanzo 3:16

Mungu alisema ataweka nyayo juu kichwa cha Nyoka na siyo Adamu(Mwanadamu).

Mungu hafanyi mapambano na Mwanadamu bali na Joka.

Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika. 

Mwanzo 3:21

kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa. 

Mwanzo 3:23

Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima. 

Mwanzo 3:24

Kwa sababu walipoteza utukufu wa kwanza, Mungu aliwatoa katika Bustani ili wasije kula matunda wakaishi tena. Hii ilikuwa kumsaidia mwanadamu badaye aje aishi pasipo machungu.

Swali la msingi,

Uko wapi Adamu? Ni swali linaloendelea kuulizwa kwetu leo. Ni kweli tunapitia machungu mengi, vifo, magonjwa nk lakini Mungu hayo yote anayajua na si kwamba haoni kwani saa inakuja Tumaini lake litatufariji na kurejesha upya hali ya utakatifu wa kwanza. Hivyo hadi siku ile atakapoondoa pambano ndipo ushindi wa Mugumu yote utapatikana milele zote.

Mungu hana vita na Mwanadamu bali na Joka. Maneno haya yanapaswa kutupatia matumaini tunapoendelea kumngoja Bwana akirudi hivi karibuni.

Hata kama tutalala leo bado Mungu yuko tayari kutupatia Matumaini, usiogope.

Neno la Mungulinaendelea kusema;

Irudieni ngome, enyi wafungwa wa tumaini; hata hivi leo nasema ya kwamba nitakurudishia maradufu. 

Zekaria 9:12

Jina la Bwana ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.

Mithali 18:10

Usiogope saa inakuja Bwana atarejesha yaliyoharibika yote tangu Mwanzo. Ajenda ni Hii Tuirudie Ngome ya Bwana na Yeye atatuokoa na taabu zote nasi tutakuwa salama. 


 

 

ATAPE KIHONDA NET EVENT: NYAYO ZA MATUMAINI

SIKU YA 03/21

HUDUMA KUU

TAREHE: 15/05/2023

MHUDUMU: MCHUNGAJI PAUL SEMBA

SOMO: NYAYO KATIKA MAPAMBANO 2

Jana tuliangalia chanzo cha Mapambano sehemu ya kwanza na kuona mwanzilishi wa Pambano ya kuwa ni Shetani na kwamba Mungu hana Mapambano na Mwanadamu bali ana mapambano na Joka(Shetani)na tukaona kwamba wale wanaokimbilia katika Ngome ya Kristo watashinda, leo ni sehemu ya pili ya Somo.

Tuliona jukwaa la Mapambano katika Mwanzo sura ya kwanza kila kitu kikiwa chema na sura ya pili Mungu akatoa maelekezo, lakini katika sura ya Tatu Pambano linaanza.

Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita. 

Mwanzo 1:31

walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika. 

Mwanzo 2:17

Mungu akingia Busitanini na ndipo akasema maneno haya;

Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; 

Mwanzo 3:14

nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino. 

Mwanzo 3:15

Mungu anaweka uadui kati ya Nyoka na Mwanamke, Na uadui wa uzao wa nyoka na Mwanamke. Nini maana yake? Ni kinyume na upendo na urafiki. Mbingu zimeweka uadui na Shetani na tunapaswa kuelewa hivyo kwamba mwanadamu lazima achukie uadui kati yake na Nyoka. Tunapaswa kupambana na Shetani na siyo sisi kwa sisi kati maisha ya Ukristo.

Jambo lingine Mungu anasema "huo utakuponda kichwa" huo uzao ni nini? Ni Uzao wa mwanaume kwa yule mwanamke. Ushahidi wa haya tunayapata katika Neno la Mungu;

Basi ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa wazao, kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani, Kristo. 

Wagalatia 3:16

na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu. 

Mwanzo 22:18

Kinachozungumzwa hapo ni habari ya Yesu Kristo mwenyewe.

Na jukwaa la vita tunaona likifanywa nje ya Bustani ya Edeni.

Utabiri wa kuzaliwa kwa Yesu ulikuwa hivi;

Mwanzo 15:13-15.

Hesabu 18:17.

Mathayo 2:1-2.

Mwanzo 49:10.

Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii. 

Mwanzo 49:10.

Isaya 7:14.

Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli. Isaya 7:14.

Isaya 9:6.

Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. 

Isaya 9:6

Mungu pamoja nasi. Mathayo 1:23.

Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi. 

Mathayo 1:23

Luka 1:23-35.

Huu ndio Utendaji wa Mungu peke yake mtu kuzaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ambao hauwezi kufanywa na mwanadamu awaye yote.

Zaburi 95:1.

Yesu ndiye Mwamba aliyetabiriwa kuja kupambana na Shetani.

Alizaliwa Bethelehemu. Mika 5:2.

Yohana 1:45.

Alizaliwa katika Holi la Ng'ombe.

Wagalatia 4:4-5.

Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, 

Wagalatia 4:4

kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana. 

Wagalatia 4:5

Yesu alikuja duniani wakati dunia ikiwa imeungana chini ya Taifa moja, dini moja, na lugha moja ya Kiyunani, katika taifa la Kirumi, ambapo ndipo ulikuwa kipindi cha Utimilifu wa Wakati.

Leo dhambi imefunikwa na Mwamvuli wa Sayansi, iko taabani haijui iendako lakini Mungu ni mkuu kupitia

Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! 

Yohana 1:29

Yesu alikuja Kutuokoa sote, Yeye aliye Mwamba wa wote.

Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, 

Waebrania 2:14

awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa. 

Waebrania 2:15

atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. 

1 Yohana 3:8

kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake. 

Waebrania 9:26

Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo; sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje. 

Yohana 12:31

Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu. 

Yohana 12:32

Aliyanena hayo akionyesha ni mauti gani atakayokufa. 

Yohana 12:33

YESU ALIYE MWAMBA WA WOKOVU WETU YUKO PAMOJA NASI USIOGOPE.


 

ATAPE KIHONDA NET EVENT: NYAYO ZA MATUMAINI

SIKU YA 04/21

HUDUMA KUU

TAREHE: 16/05/2023

MHUDUMU: MCHUNGAJI PAUL SEMBA

SOMO: NYAYO ZENYE NYAYA 1

Hizi ni nyaya zenye cheche, yaani nyaya zenye moto au nyaya zenye uhai. Hivyo nyayo za matumaini ni nyaya zinazowaka moto zikimwakilisha Yesu Mwenyewe.

Yesu alifia Dhambi ya Adamu.

Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! 

Yohana 1:29

Yesu hakuja kubeba dhambi ya kutenda au kutokutenda. 1Yohana 3:4, Yakobo 4:17.

Dhambi inayo zungumziwa ni Dhambi ya Adamu.

Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi; 

Warumi 5:12

walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja. 

Warumi 5:14

Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo. 

Warumi 5:17

Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima. 

Warumi 5:18

Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.

Warumi 5:19

Kwa Sababu ya Dhambi ya kutomwamini Mungu Adamu aliingia katika Dhambi ya kutokutii.

Kifo alichoambiwa Adamu na Hawa kilikuwa ni kifo cha kutengwa kutoka kwa aliye chimbuko la Uhai yaani Mungu.

Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. 

Isaya 53:3

Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. 

Isaya 53:4

Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. 

Isaya 53:5

Hizo ndizo nyaya zenye moto kwakuwa YESU alikuja kubeba dhambi ya Adamu.

Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, 

Waebrania 2:14

awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa. 

Waebrania 2:15

Kupitia kifo cha Yesu mfumo wa Shetani wote ulibadilishwa.

Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo. 

Yohana 8:44

Yeye aliyeukubali ushuhuda wake ametia muhuri ya kwamba Mungu ni kweli. 

Yohana 3:33

Mungu ni Upendo.

Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake. 

1 Yohana 4:16

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 

Yohana 3:16

Yesu ni waya ambao ukiguswa na Shetani anasambalatika.

Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. 

Ufunuo wa Yohana 3:21

Hata itakuwa yeye atakayejibariki duniani, atajibariki kwa Mungu wa kweli; naye atakayeapa duniani, ataapa kwa Mungu wa kweli. Kwa kuwa taabu za kwanza zimesahauliwa, na kwa kuwa zimefichwa machoni pangu. 

Isaya 65:16

Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu. 

Yohana 18:37

Yesu alikuja ili aishuhudie kweli. 

Msalaba ni onyesho la Upendo wa Mungu.

Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. 

Warumi 5:8

Tulikombolewa kwa Damu ya Mwanakondoo peke yake na siyo vinginevyo.

Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; 

1 Petro 1:18

bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo. 

1 Petro 1:19

Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu; 

1 Petro 1:20

Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe. 

Matendo ya Mitume 20:28

Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua. 

Yohana 1:18

Yohana 12:31-33.

2Wakorintho 4:14.

Yohana 10:15, 17, 18, 28.

Neno linaendelea kusema juu ya Nyayo zenye Nyaya(YESU);

Na pale pale aliposulibiwa palikuwa na bustani; na ndani ya bustani mna kaburi jipya, ambalo hajatiwa bado mtu ye yote ndani yake.

Yohana 19:41

KWA MTU MMOJA (ADAMU) ULIMWENGU ULIINGIA KATIKA DHAMBI, NA KUPITIA KWA YESU TUMEKOMBOLEWA, HAKIKA MUNGU NI MWAMINIFU UKIMWAMINI LEO AHADI YA UZIMA WA MILELE IKO KWA AJILI YAKO NA KWA AJILI YANGU.


 


ATAPE KIHONDA NET EVENT: NYAYO ZA MATUMAINI

SIKU YA 05/21

HUDUMA KUU

TAREHE: 17/05/2023

MHUDUMU: MCHUNGAJI PAUL SEMBA

SOMO: NYAYO ZENYE NYAYA II.

Jana tuliangalia katika somo la Nyayo zenye Nyaya sehemu ya Kwanza na kuona kwamba Yesu ndiye mwenye nyayo zenye nyaya ambapo Shetani akigusa anasambalatika. Leo ni sehemu ya pili ya somo letu.

Neno la Mungu linasema hivi;

Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake. 

Yohana 19:30

Yesu aliishi hapa duniani ili kutenda na kutimiza mapenzi ya Baba yake wa Mbinguni.

Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile. 

Yohana 5:19

Lakini Yesu alikuja kutimiza yote yaliyoandikwa katika Manabii, Zaburi, na Torati yote.

Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi. 

Luka 24:44

Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyachungulia. 

1 Petro 1:12

Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. 

Yohana 5:39

Yesu alitoa uhai wake kwa hiari yake mwenyewe na si kwa Kushurutishwa si dola ya Kirumi wala Wayahudi waliomwua.

Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena.

Yohana 10:17

Basi alipowaambia, Ni mimi, walirudi nyuma, wakaanguka chini.

Yohana 18:6

Walianguka kwa sababu walikutana na nguvu halisi yaani nyayo zenye nyaya ambaye ni Yesu zikawangusha chini.

Hivyo Yesu anaposema Imekwisha alikuwa akitimiza Mapenzi ya Baba yake kwa Kuutoa uhaiwake mwenyewe.

Marko 10:45.

Warumi 6:3

Yohana 12:31-33.

Yohana 16:7-11.

Kifo cha Yesu kilikuwa ni hukumu inayokamilika dhidi ya Shetani pale aliposema "IMEKWISHA".

Yesu amelipa Deni lote kupitia pale Msalabani, kwamba nimekwisha kutoa hukumu yote kwa yule Shetani.

Imekwisha, Yesu alikuwa anazungumza kwa Baba yake.

Yohana 18:13-14,19-24.

Marko 14:55-59.

Mathayo 26:63-66.

Yohana 10:30-33.

Dini ya Kweli ni ile ya Mungu kuwafikia wanadamu wake kwani hatuwezi Kumtafuta Mungu bali Yeye ndiye anayetutafuta sisi, nje ya hapo ni Dini iloyokufa yaani dini ya Mafarisayo, Kayafa, Pilato walipodhania kwamba wanaweza kumfikia Mungu.

Yohana 18:37-38.

Luka 23:8-12.

Siku zote viongozi dhaifu hutafuta Sifa kwa kupigiwa makofi na matokeo yake ni utendaji mbaya wa madaraka dhidi ya wanaowaongoza, lakini Yesu hakuwa hivyo.

Imekwisha, ilibadili maisha ya watu. Neno linasema;

Luka 23:47.

Mathayo 27:54.

Luka 23:48.

Wale wasioamini Yesu aliwakagua, dini ya kweli ni ipi? Inayosema Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu ambaye anatia uhai, anayebadilisha maisha ya watu, anayetoa uhai na kuutwaa tena, Ambaye amekwisha mhukumu Shetani kwa kulipa deni pale Msalabani kwa kutimia neno "IMEKWISHA".

LEO TEMBEA UKIWA NA MATUMAINI YA USHINDI KWA KUWA "IMEKWISHA" YESU ALILIPA YOTE PALE MSALABANI, USIOGOPE.




ATAPE KIHONDA NET EVENT: NYAYO ZA MATUMAINI

SIKU YA 06/21

HUDUMA KUU

TAREHE: 18/05/2023

MHUDUMU: MCHUNGAJI PAUL SEMBA

SOMO: NYAYO KATIKA MIZANI 1

Leo tunazungumzia Nyao katika Mzani. Ni Mzani upi huu? Kama ujuavyo kwamba Mzani ni kipimo kinachopima vitu ili kupata utimilifu na kupata ulinganifu kamili aidha katika kununua au kuuza. Mzani unakuonyesha uzito fulani mfano magari yanapopimwa uzito Barabarani ili kuona kama uzito wa gari na kile kilichobebwa ikiwa viko sawa.

Somo la leo linaturejesha tena katika Bustani ya Edeni, kama tulivyoona katika Mwanzo Moja dunia inaumbwa kwa ukamilifu, sura ya pili na ya tatu Pambano linaanza na Sura ya Nne tunaona kifo kinaanza katika mgogoro wa Kaini na Habili lakini sura ya Tano hadi ya Nane tunaona habari ya Gharika na mengine mengi. Neno linasema;

Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? 

Mwanzo 3:9

Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha. 

Mwanzo 3:10

Adamu aliposikia sauti alisema aliogopa, yuko uchi, akajificha, Hapa tayari mambo yalikwisha haribika maana yake ni kwamba Mungu kwake siyo mwema kama ilivyokuwa mwanzo kabla ya Dhambi.

Siku zote Tabia ya Mungu ni ya wema. Na ndiyo maana tunamwona Mungu akimtafuta Adamu Bustanini.

Akasema, Nakusihi unionyeshe utukufu wako. 

Kutoka 33:18

Akasema, Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la Bwana mbele yako; nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu. 

Kutoka 33:19

Utukufu wa Bwana ni Wema wake pamoja na Jina Lake.

Bwana akashuka ndani ya lile wingu, akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina la Bwana. 

Kutoka 34:5

Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; 

Kutoka 34:6

mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne. 

Kutoka 34:7

Musa akafanya haraka, akainamisha kichwa chake hata nchi, akasujudu. 

Kutoka 34:8

Kumbe Utukufu wa Mungu ni wema wake, Jina Lake ambayo ndiyo Tabia yake.

kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; 

Warumi 3:23

Utukufu uliopungua ni Wema wa Mungu kwa wanadamu. Mungu ni mwema kwa asili yake kwani hakuanza kuwa Mungu ndiyo akawa Mwema na wala hapokei wema kutoka kwa vitu vyake bali Yeye ni MWEMA.

Bwana ni mwema kwa watu wote, Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote.

Zaburi 145:9

Ibada inajengwa tu pale unapofahamu utukufu na Wema wa Mungu.

Mungu ni mwema hata kama hutatenda jema wewe Yeye atadumu kuwa mwema.

Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka.

Yakobo 1:17

Waebrania 13:8.

Mathayo 5:45.

Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. 

Maombolezo 3:22

Mungu anapomsamehe anayetubu ni REHEMA yake.

Mungu anapomsaidia mwenye dhiki ni HURUMA yake.

Mungu anapochukuliana na Waasi ni UVUMILIVU wake.

Mungu anapoitimiza ahadi yake ni KWELI.

Mungu anapomgawia Maskini FADHILI zake.

Mungu anapomwadhibu mwenye hatia ni HAKI yake.

Mungu anapokutana na asiyestahili ni NEEMA yake.

Ndiyo maana Adamu alitengenezewa Ngozi kama sehemu ya Neema ya Mungu ambapo kwa ujumla ndiyo wema wa Mungu.

WEMA-NEEMA-IMANI.

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 

Yohana 3:16

Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; 

Waefeso 2:8

wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. 

Waefeso 2:9

Neema ndiyo ilitufikia sisi tusiostahili bali ni kwa NEEMA tu.

Neema ni utendaji wa Mungu kumfikia mwanadamu asiyestahili, na mwanadamu kazi yake ni moja tu anayotakiwa kufanya nayo ni kumwamini MUNGU pekee. Tumeokolewa kwa Neema kwa njia ya Imani.

Mtu atapotea si kwa kile alichotenda Adamu la! Bali kwa Kutomwamini Mungu kwa mtu mmojammoja.

Imani hupokea Neema ya Bwana. Na chanzo cha Imani ni kusikia Neno la Kristo.

Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. 

Warumi 10:17

Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. 

Waebrania 11:6

Je, Imani ni nini? Imani ni KUAMINI KWAMBA MUNGU YUPO NA ANAISHI.

Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO na AMBAYE NIKO;akasema,Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli;MIMI NIKO amenituma kwenu.

Kutoka 3:14

Anayekataa kuwa Mungu hayupo ni sawa na Mpumbavu.

Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema. 

Zaburi 14:1

Warumi 1:21-22.

Wanaoamini kuwa Mungu yupo wanaishi na kuenenda sawasawa na Mapenzi Yake.

Kinachotuunganisha na Mungu pamoja na Tabia ya wema wake ni kwa kuamini pekee yaani IMANI YAKE.

Kuamini huenda zaidi ya kuona na kusikia.

Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. 

Waebrania 11:1

Imani inavuka kuona au kufikiri.

Mathayo 14:26-29.

Imani inavuka uelewa. Hakuna kinachofanikiwa pasipo Imani, chochote anachofanya mwanadamu ni lazima anaamini matokeo fulani yatatokea. Hivyo kwa Imani hiyohiyo tunapaswa kumwamini Mungu na kumpokea katika mioyo yetu atatupigania daima.


 

ATAPE KIHONDA NET EVENT: NYAYO ZA MATUMAINI

SIKU YA 07/21

HUDUMA KUU

TAREHE: 19/05/2023

MHUDUMU: MCHUNGAJI PAUL SEMBA

SOMO: NYAYO KATIKA MIZANI 2

Kama jana tulivyoona katika somo la Nyao katika Mzani kwamba wema wa Mungu ni mkuu na kwamba hata kama sisi hatutakuwa tayari kutenda yaliyo mema ila Mungu atabaki kuwa Mwema tu. Leo ni Nyayo katika Mzani sehemu ya Pili.

Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; 

Yohana 8:31

tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru. 

Yohana 8:32

Wakamjibu, Sisi tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru? 

Yohana 8:33

Yeye anichukiaye mimi humchukia na Baba yangu. 

Yohana 15:23

Yesu anatuita ili kutuweka huru kwelikweli. Wale wanaomchukia Yesu humchukia Mungu.

Kila amkanaye Mwana, hanaye Baba; amkiriye Mwana anaye Baba pia. 

1 Yohana 2:23

Ukimkubali Yesu umemkubali Baba, ukimkataa Yesu umemkataa Mungu.

Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. 

Matendo ya Mitume 4:12

Ukristo ni Dini usiyopaswa kuutetemekea kwani Yesu wetu ni Mweza wa Yote. Hakuna cha kushindwa kwa lolote ukiwa na Yesu unashinda na utashinda hakika.

Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; 

Yohana 1:12

waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu. 

Yohana 1:13

Ni kwa uwezo wa Mungu pekee tunaliamini jina la Yesu.

Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. 

Marko 16:15

Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. 

Marko 16:16

Kuamini huenda sambamba na kutenda na ni katika kukiri imani kwa njia ya Ubatizo wa maji mengi. Ikiwa unasema unaamini na hujabatizwa bado hujaamini.

Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. 

Mathayo 3:13

Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? 

Mathayo 3:14

Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali. 

Mathayo 3:15

Kwanini Yohana alikuwa anakataa Yesu asibatizwe? 

Ni kwa sababu alijua Yesu hana dhambi.

Yohana alibatiza kwa maji, Yesu kwa Roho.

Mathayo 3:2.

Luka 3:3.

Yohana 1:29; Yohana 8:46; Luka 23:14-15; 1 Petro 2:22; Waebrania 4:15; Mathayo 3:11.

Kwanini Yesu ni Mwana wa Adamu? Kwa sababu anashiriki ubinadamu, na wala haijapunguza Uungu na Ukuu wake wa Utendaji. 

Yohana 12:34.

Marko 13:26.

Luka 22:66

Yesu kuwa mwana wa Adamu haimanishi si Mungu bali ni Mungu.

Yohana 1:1,4.

Yohana 6:46.

Yohana 1:18.

Mathayo 1:23.

1Yohana 4:12.

Yohana 5:18,24; 10:30-33; 19:7.

Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; 

Mathayo 3:16

Naye aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti, alianza kupaza sauti yake, na kusema, Mwana wa Daudi, Yesu, unirehemu. 

Marko 10:47

Ubatizo ni nini? Maana ya Ubatizo ni kuungana na Kristo katika mauti yake.

Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? 

Warumi 6:3

Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. 

Warumi 6:4

Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake; 

Warumi 6:5

mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena; 

Warumi 6:6

Unapobatizwa unatangaza kwamba Yesu anaokoa, Yesu anaponya, Yesu ni Mweza wa yote.

Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu. 

Wakolosai 2:12.

Hivyo ubatizo ni Ishara ya Nje ya kuonyesha Ukristo na Imani yako kwa Mungu.

Baada ya Yesu kubatizwa ni nini kilitokea?

na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye. 

Mathayo 3:17

1Wakorintho 10:1-2.

Mungu aliweka Ubatizo katikati ya WOKOVU na DHAMBI. Ubatizo ni uhusiano pamoja na Kristo. Tunaweza kusulubisha utu wetu wa kale pamoja na Kristo kwa njia ya Ubatizo.

Ubatizo ni ushaidi wa Nje au ishara ya nje ya kumkubali Kristo maishani mwetu.

IKIWA UNAHITAJI KUKOMBOLEWA KATIKA KRISTO, KUBALI KUBATIZWA PAMOJA NA KRISTO NA HAPO UTAKUWA UMEITIMIZA HAKI YOTE.


 


ATAPE KIHONDA NET EVENT: NYAYO ZA MATUMAINI

SIKU YA 08/21

HUDUMA KUU

TAREHE: 20/05/2023

MHUDUMU: MCHUNGAJI PAUL SEMBA

SOMO: NYAYO ZISIZOFUNIKWA

Leo tunaangalia somo lingine la pekee tena lisemalo Nyayo zisizofukiwa je ni nyayo gani hizi zisizofukiwa?

Katika dunia hii watu wamefukia vitu vingi sana na wengine wakidhani kuwa wamefanikiwa lakini si kweli, ukweli ni kwamba ziko nyayo zisizofukiwa.

Katika somo liliopitq tulijifunza habari ya Ubatizo Yesu akimwambia Yohana Mbatizaji kwamba Kubali hivi leo. Inamaanisha nini kusema Nyayo zisizofukiwa? 

Mungu aliweka Kalenda ya Matukio ambapo Yeye ndiye Atayatimiza.

Bwana akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, akawaambia, 

Kutoka 12:1

Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu. 

Kutoka 12:2

Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana. 

Kutoka 12:12

Kwa kuwa Bwana atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, Bwana atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi. 

Kutoka 12:23

Kwa nini Mwezi wa kwanza?

Utunze mwezi wa Abibu, ukamfanyie pasaka Bwana, Mungu wako, kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku Bwana; Mungu wako. 

Kumbukumbu la Torati 16:1

Leo Mwezi wa Abibu ni mwezi kati ya Watatu au Wanne leo. Ambao ndio utakuwa mwanzo wa Mwenzi katika Kalenda ya Kiebrania ambapo kwao ndio mwezi wa kwanza, sisi katika Kalenda ya Gregory ni mwezi watatu au wanne. Kuanza kwa taifa la Israeli ni kuumba upya, ni ukombozi.

Kwa nini watu husherehekea Pasaka leo? Ni kwa sababu hawajui kwamba tayari Yesu alikwishafanyika Pasaka. Hata hivyo Pasaka inayoadhimishwa leo siyo ile Yesu aliyosema kwani Yesu alisema Mkate na Divai ndiyo alisema tufanye kwa ukumbusho wake.

Walawi 23:4-5

1Wakorintho 5:7.

Zaburi 118:25.

Yohana 1:29.

Mikate iliyoagizwa ilitakiwa isiwe na Chachu yoyote. Kwani Yesu alitolewa kikamilifu pasipo waa lolote wala dhambi yoyote. Ukiosoma katika; Kutoka 12:15.

Mtu anayesema ameokolewa kwa Neema na anaenda kinyume ni sawa na kazi bure tu kwani Neema haimsaidii chochote.

Ilikuwepo pia sadaka ya Malimbuko au Sadaka ya Kutikisa Mganda. 

Walawi 23:10-11

Nini maana ya kutikisa Mganda?

1Wakorintho 15:12-15, 16-20.

Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu? 

1 Wakorintho 15:12

Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka; 

1 Wakorintho 15:13

tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure. 

1 Wakorintho 15:14

Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi. 

1 Wakorintho 15:15

Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka. 

1 Wakorintho 15:16

Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu. 

1 Wakorintho 15:17

Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea. 

1 Wakorintho 15:18

Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote. 

1 Wakorintho 15:19

Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. 

1 Wakorintho 15:20

Yesu alikufa Mwezi wa Abibu siku ya Ijumaa kesho yake Sabato na badala yake siku iliyofuata ilikuwa siku ya Ufufuo wake yani siku ya Jumapili.

Paulo alisema kama Yesu hakufufuka basi Imani yetu ni bure.

Yesu ni Nyao zisizofukiwa kwa sababu baada ya Kifo chake katika siku ya Tatu alifufuka.

Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala.

1 Wakorintho 15:20

Ikiwa unaamini katika Dini ya viongozi waliokufa nje ya Yesu Imani hiyo ni bure, ni bure kabisa. Yesu peke yake ndiye alikufa akafufuka na hayumo Kaburini hadi leo.

Yesu anaporejea waliokufa katika Bwana watafufuliwa na kumlaki Bwana mawinguni.

Walio hai na walio kufa wakati wa kuja kwake watamlaki Bwana hewani. Hivyo mtu asikudanganye kuwa watu wakifa wanaenda Mbinguni.

Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. 

Yohana 5:28

Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu. 

Yohana 5:29

Mtu anapokufa haendi Mbinguni ni Uongo wa Shetani, WAFU WOTE WANAPOKUFA WANAENDA KABURINI.

Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.

Mhubiri 9:10

Mhuburi 3:18-20

Wafu wote wako Makaburini usidanganyike kwamba wafu wanakwenda mbinguni hakuna.

Neno linasema hivi;

Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. 

1 Wathesalonike 4:14

Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. 

1 Wathesalonike 4:15

Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. 

1 Wathesalonike 4:16

Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. 

1 Wathesalonike 4:17

Basi, farijianeni kwa maneno hayo. 

1 Wathesalonike 4:18

Ziko kauli za kipagani kwamba MTUT ANAPOKUFA WATU WANASEMA, SISI TULIMPENDA ILA MUNGU AMEMPENDA ZAIDI, JE, NI NANI YUKO TAYARI KUFA ILI MUNGU AMPENDE ZAIDI?

Neno linasema;

Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, 

1 Wakorintho 15:51

kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. 

1 Wakorintho 15:52

Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. 

1 Wakorintho 15:53

Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda. 

1 Wakorintho 15:54

Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako? 

1 Wakorintho 15:55

HATUTALALA SOTE BALI WOTE TUTABADILISHWA KUFANANA NA KRISTO MWENYEWE IKIWA TUTAISHI TUKITENDA MAPENZI YAKE.

Wengine husema Yesu alipaa kwenda Mbinguni na Mwivi Msalabani si kweli kwani Neno linasema;

Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu NIwenu. 

Yohana 20:17

Luka 24:39-42.

YESU ANAKUJA WALA HAKUNA UNYAKUO WA SIRI UTAKAOFANYIKA NA KILA JICHO LITAMWONA MWANA WA ADAMU ANAPOKUJA, BASI FARIJIANENI NA KWA MANENO HAYO.


 

ATAPE KIHONDA NET EVENT: NYAYO ZA MATUMAINI

SIKU YA 09/21

HUDUMA KUU

TAREHE: 21/05/2023

MHUDUMU: MCHUNGAJI PAUL SEMBA

SOMO: NYAYO KATIKA JUKWAA 1

Leo tunalo somo la pekee lingine lisemalo Nyayo katika Jukwaa, je ni Jukwaa gani hili?

Jukwaa ni Eneo lililoinuka juu. Lakini kwa mujibu wa somo la leo Jukwaa ni eneo lenye shughuli maalum inapotendekea, ni sehemu rasmi, hili ni jukwaa la pekee katika somo la leo tunapoalikwa kukwea katika Jukwaa hili. Neno la Mungu linasema;

Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu. 

1 Timotheo 3:16

Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua. 

Yohana 1:18

Siri ya utauwa ni ipi? Ni Kwamba Mungu alidhihirishwa katika Mwili.

Wale wanaosema Yesu siyo Mungu POLE!! Yesu ni Mungu aliyedhihirishwa katika Mwili. Hii ni habari njema sana. Yesu anaaminiwa katika Ulimwengu wote na tunamwamini kama Mungu Pamoja Nasi. Yesu alipaa na kwenda juu Mbinguni. Hii ndiyo maana ya somo la leo kwamba Nyayo katika Jukwaa.

Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. 

Matendo ya Mitume 1:9

wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni. 

Matendo ya Mitume 1:11

Alipokuwa anakwea kwenda Mbinguni aliacha ahadi ya Nguvu ya Roho Mtakatifu katika siku ya Hamsini yaani (Pentekoste). Je, nini maana ya Pentekoste?

Nanyi mtajihesabia tangu siku ya pili baada ya Sabato, tangu siku hiyo mliyouleta mganda wa sadaka ya kutikiswa; zitatimia Sabato saba; 

Mambo ya Walawi 23:15

hata siku ya pili ya hiyo Sabato ya saba mtahesabu siku hamsini; nanyi mtamsongezea Bwana sadaka ya unga mpya. 

Mambo ya Walawi 23:16

Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. 

Matendo ya Mitume 2:1

Je, hiyo ni nini basi katika Pentekoste?

Ndiyo siku walijazwa na Roho Mtakatifu kisha wakaanza kunena kwa Lugha zao.

Matendo 2:1-12.

Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya? 

Matendo ya Mitume 2:12

Yoeli 2:28-32.

Basi yeye, akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia. 

Matendo ya Mitume 2:33

Yesu ameketi yuko kwenye Mkono wa Kuume wa Kiti cha Enzi cha Mungu.

Zaburi 110:1; 1Petro 3:22; Waefeso 1:20; Wakolosai 3:1; Waebrania 1:3.

Yesu ameketi kwenye Jukwaa Mbinguni na hii ni baada ya kuja kwa Roho Mtakatifu kwetu duniani.

Mkono wa Kuume maana Yake ni Uwezo, Mamlaka, Kutukuzwa, Ukuu na Kuheshimiwa.

Yesu ni Mfalme wa Wafalme, Yesu ni Kuhani Mkuu. Pasipo Yesu kwenda Mbinguni Roho Mtakatifu asingekuja ndiyo maana alisema hivi;

Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. 

Yohana 16:7

Anayepokea Nguvu ya Roho Mtakatifu lazima awe Shahidi Mwaminifu wa Yesu, nje ya hapo ni bure.

Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

Matendo ya Mitume 1:8

Roho wa Mungu anakuja kutufunulia yaliyo mapenzi yake ili tuyatende. Wale waongozao watu na kunena lugha zisizoeleweka wanamtukuza Ibilisi maana Roho wa Mungu anazungumza lugha inayojulikana.

Yesu anafanya kazi hizi akiwa ameketi kwenye kiti cha Enzi katika Jukwaa kuu Akitoa TOBA, na MSAMAHA WA DHAMBI.

Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi. 

Matendo ya Mitume 5:31

1Yohana 2:1-2

Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, 

1 Yohana 2:1

naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote. 

1 Yohana 2:2

Yupo mmoja tu anayetupatanisha na Mungu naye ni Yesu Kristo pekee.

Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; 

1 Timotheo 2:5

ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake. 

1 Timotheo 2:6

Yesu peke yake ndiye Mpatanishi wetu kati ya wanadamu na Mungu peke yake na ndiyo maana yuko kwenye Jukwaa ameketi na siyo mtu awaye yote.

IKIWA TUNAHITAJI KUOKOLEWA BASI TUPANDE KATIKA JUKWAA ALIPO BWANA WA MABWANA NA MFALME WA WAFALME YESU KARISTO, HUYO NDIYE ANASAMEHE DHAMBI, ANAOKOA NA KUTUPATIA TOBA YA KWELI MAISHANI MWETU NA KUTUFANYA UPYA KILA SIKU. MUNGU ATUBARIKI SOTE.


 

ATAPE KIHONDA NET EVENT: NYAYO ZA MATUMAINI

SIKU YA 10/21

HUDUMA KUU

TAREHE: 22/05/2023

MHUDUMU: MCHUNGAJI PAUL SEMBA

SOMO: NYAYO KATIKA JUKWAA 2

Katika Sehemu ya kwanza ya somo hili tulijifunza habari ya Kristo alifufuka, akapaa, kisha Roho Mtakatifu akashuka na sasa yuko Mbinguni akiwa ameketi katika jukwaa la Pekee mahali pa juu sana, mahali pa pekee na palipo rasmi ambapo kila mmoja anapaswa kutazama katika jukwaa hilo. Leo ni Nyayo katika Jukwaa sehemu ya Pili. Somo hili la leo linatupeleka katika kuelewa mambo makubwa mawili na kila mwanadamu atakayeelewa atapata Tumaini lisilotetereka. Mambo hayo ni kama ifuatavyo Neno la Mungu linasema;

Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni, 

Waebrania 8:1

mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu. 

Waebrania 8:2

Jambo la kwanza ni UPATANISHO. Siku ya Upatanisho kwa Kiebrania (Yom Kippur) habari hii utaikuta kuanzia agano la Kale kipindi cha huduma za Hekalu Makuhani walipokuwa wakifanya huduma za Hekalu katika kumpatisha mwanadamu na Mungu, na chumba kile cha huduma kilikuwa na vitu na vifaa mbalimbali ikiwemo Mikate ya wonyesho, Vinara saba vya taa, Mana chakula cha Kuhani, nk. Kulikuwa na Pazia likitenganisha Chumba cha kwanza na cha pili Ambapo kulikuwa na Sanduku la Agano ambapo ndipo ilikuwa Hema ya kukutania.

Nao na wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa kati yao.

Kutoka 25:8

Sawasawa na haya yote nikuonyeshayo, mfano wa maskani, na mfano wa vyombo vyake vyote, ndivyo mtakavyovifanya. 

Kutoka 25:9

Hema ilikuwa na huduma kuu mbili, Moja ya Kuhani wa zamu kwa kila mtu atendaye dhambi hivyo anakuja na kitu chenye uhai Njiwa, Kondoo, Mbuzi ili kuungama juu ya dhambi alizozitenda kisha mnyama alichinjwa. Na hii ilikuwa ni kivuli cha kile Yesu alichofanya kama Biblia inavyosema katika Yohana 1:29. Baada ya hapo Kuhani alichukua damu na kuleta katika kufukiza Uvumba katika Hema ya kukutania kisha anatoka na kuwabariki watu baada ya Kufukiza Uvumba na hii ilikuwa ni kwa kila Kuhani anayekuwa Zamu ndiye alifanya huduma hiyo.

Baada ya mambo hayo Biblia inaelezaje juu ya Sikukuu ya Upatanisho?

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 

Mambo ya Walawi 23:26

Lakini siku ya kumi ya mwezi huo wa saba ni siku ya upatanisho; itakuwa kusanyiko takatifu kwenu, nanyi mtazitesa nafsi zenu; nanyi mtasongeza sadaka kwa Bwana kwa njia ya moto. 

Mambo ya Walawi 23:27

Nanyi msifanye kazi yo yote siku hiyo; kwa kuwa ni siku ya upatanisho, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu mbele za Bwana, Mungu wenu. 

Mambo ya Walawi 23:28

Kwa kuwa mtu awaye yote asiyejitesa mwenyewe siku iyo hiyo, atakatiliwa mbali na watu wake. 

Mambo ya Walawi 23:29

Siku ya Upatanisho ni Siku ya Kuhukumu Dhambi. Na huduma hiyo ilikuwa inafanywa na Kuhani Mkuu. Walawi 16. Na alikuwa na Vazi Maalumu lenye kubeba vifaa mbalimbali ikiwemo Njuga, alichukua Nivera kifuani, leo tunao watu wanajiita WACHUNGAJI, MAASKOFU, MASHEKHE lakini wanafanya uzinzi na waumini wao badala ya kubeba Dhambi zao kifuani mwao ni UOVU tu, leo tunao watu wajiitao viongozi wa kidini lakini wanatetea Maovu, Ushoga, usagaji, wanatetea badala ya kusema ukweli na kuwa waaminifu ni UOVU, lakini pia kulikuwa na Madini 12. Alikuwa anachukua Ng'ombe Mume, na Kondoo kwa ajili ya familia yake kabla hujapatanisha wengine lazima upatabishe familia yako kwanza, kisha alikuwa Na mbuzi wawili. Mbuzi wa kwanza kwa ajili ya Bwana na mwingine kwa ajili ya Azazeli na yule wa kwanza ilikuwa ni kwaajili ya taifa la Israeli. Kiti maana yake ni Mamlaka, Hivyo kuna kiti cha Rehema, kiti cha Enzi na Kiti cha Hukumu hivi siyo viti vingi bali na kiti kimoja kilekile na huwakilisha uleule wema wa Mungu. Hivyo Damu ilinyunyizwa juu ya Kiti cha Rehema Mashariki na mbele ya kiti na kutia damu pembe za Madhabahu, kwa sababu ya Machafu na dhambi zote za Israeli.

Waliofaidika na huduma hii ni wale walioleta dhambi zao Hekaluni walisamehewa walipona na hii ni baada ya kuungama na kuamini huduma hiyo dhambi zao zilihamia kwa mwanakondoo kutoka kwa Mdhambi ikimwakilisha Yesu Mwenyewe. Na baada ya Kuhani kumaliza huduma hiyo ndipo alitoka sasa.

Baada ya hayo sasa;

Jambo la kwanza Msalaba wa Kalvari Yesu anavaa uhusika wa Mwanakondoo(Mnyama aliyechinjwa ili damu ipatikane)

Kisha atatwaa chetezo kilichojaa makaa ya moto yatokayo katika madhabahu iliyo mbele za Bwana, na konzi mbili za uvumba mzuri uliopondwa sana, mikononi mwake, naye atauleta ndani ya pazia. 

Mambo ya Walawi 16:12

Kisha atatia ule uvumba juu ya moto mbele za Bwana, ili moshi wa ule uvumba ukisitiri kiti cha rehema kilicho juu ya ushuhuda, asije akafa. 

Mambo ya Walawi 16:13

Katika Sikukuu ya Upatanisho; Yesu Kristo Kuhani Mkuu aliingia Mbinguni akiwa amezungukwa na Mawingu(Uvumba)

Wanafunzi walimwona juu ya Mawingu. Matendo 1:9.

Danieli alimwona Yesu akiingia Mbinguni. Danieli 7:13-14.

Yohana pia alimwona akija na Mawingu. Ufunuo 1:7.

Zekaria 3:16.

Yohana 20:27.

Yohana 1:29; Ufunuo 5:6.

Wakolosai 3:1-4.

Habari gani Stefani?

Lakini yeye akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa mkono wa kuume wa Mungu. 

Matendo ya Mitume 7:55

Akasema, Tazama! Naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu. 

Matendo ya Mitume 7:56

Wakapiga kelele kwa sauti kuu, wakaziba masikio yao, wakamrukia kwa nia moja, 

Matendo ya Mitume 7:57

wakamtoa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi wakaweka nguo zao miguuni pa kijana mmoja aliyeitwa Sauli. 

Matendo ya Mitume 7:58

Wakampiga kwa mawe Stefano, naye akiomba, akisema, Bwana Yesu, pokea roho yangu. 

Matendo ya Mitume 7:59

Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala. Na Sauli alikuwa akiona vema kwa kuuawa kwake. 

Matendo ya Mitume 7:60

Walio waaminifu kwa Mungu hata kama watakufa Uhai wao utakuwa umefichwa kwa Kuhani Mkuu Yesu Kristo atakuwa pamoja nao kama Stefano. Hebu na tusalimishe maisha yetu kwa Kuhani Mkuu naye atatupigania, Haijalishi wenzetu wametufanyia mabaya kiasi gani yupo Kuhani Mkuu Yesu Kristo anatupigania.

USIOGOPE UWE SHUJAA TU, UWE MWAMINIFU YESU YUPO KWENYE JUKWAA NA UHAI WAKO UMEFICHWA NDANI YAKE USIOGOPE UWE MWAMINIFU TU NA MUNGU ATATUPIGANIA TU.

MUNGU ATUBARIKI SOTE, YESU YUKO KWENYE JUKWAA YUKO HAI, ANATUOMBEA, ANATUPATANISHA NA MUNGU ANASAMEHE DHAMBI NA KUFUTA UOVU WETU TUKIMWAMINI.


 

 

ATAPE KIHONDA NET EVENT: NYAYO ZA MATUMAINI

SIKU YA 11/21

HUDUMA KUU

TAREHE: 23/05/2023

MHUDUMU: MCHUNGAJI PAUL SEMBA

SOMO: NYAYO ZINAPOKUTANA 1

Leo tunalo somo lingine tena Nyayo zinapokutana, je hii inamaanisha nini Nyayo zinapokutana? Fuatilia somo hili likiwa ni sehemu ya kwanza.

Je ni nyayo zipi hizi zinazokwenda kukutana? Maana kila zinapokutana zinaleta Matumaini.

Tuliona Yesu ndiye Kuhani Mkuu, na anaokoa na kuponya watu kupitia Yeye. Yohana 14:5-6. Yesu ndiye Kuhani Mkuu yuko katika Jukwaa Kuu akiendeleza Upatanisho kati ya Wanadamu na Mungu.

Kwa habari za Hekalu utazipata katika cha Kutoka Sura ya 25-40. Na mwanzo ilianza kama Hema na ndipo badaye Hekalu.

Kupitia Hema Mungu alikuwa anafundisha juu ya Usafi wa Tabia kwa maisha ya mwanadamu Mdhambi.

Kadiri mtu alivyolisogelea Hema ndivyo alizidi kuona uzuri wa vitu vilivyomo Hekaluni.

Kuhani ndiye alihudumu Hekaluni na hivyo basi leo hatuna Mahekalu ila tuna makanisa tu, kwani Hekalun lilihusisha Makuhani pekee siyo watu wote. Hivyo makanisani leo tuna wachungaji, Mapadri na siyo Makuhani.

Walawi sura ya 1-6 inzungumzia Mwisraeli mmojammoja namna ya kumkaribia Mungu katika namna tofautitofauti. 

Na huduma ilitaka kwanza kabisa kujitenga na Dhambi ndipo huduma ifanyike 

Hivyo usipoteze muda wako kwenda kwa Kiongozi wako wa kanisa kuomba msamaha bali ni kwa Yesu pekee usidanganyike. Omba kwake na Yeye atakujaza sirini tangu Pazia lilopopasuka kati maana yake ilikuwa kwamba mwanadamu amepata nafasi ya kumwona Mungu moja kwa moja na siyo vingenevyo, hivyo kwenda kwa wanadamu wenzako kwamba watakusamehe hizo ni Porojo tu. Mathayo 27:57. Hatuna Kuhani leo na Kuhani ni Yesu Peke yake.

Walawi 4:6-7,17-18.

Kwa viongozi kwa habari ya Hekalu walipotenda dhambi ziliingia chumba cha Kwanza. 

Kama tulivyosoma Walawi 16:16; Ebrania 16:16.

Walawi 16:17-20 Damu ilianzia kwenye kifuniko cha juu.

Hema ilipokea dhambi na kisha kwenda Patakatifu kwa Kuhani Mkuu na baada ya hapo ilikwenda na kutoka Nje. Hii maama yake ni kwamba Hema ya kwanza ilikuwa na kazi ya kuchuja Dhambi ndipo inaenda kwa Kuhani Mkuu na hatimaye nje.

hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki. 

Wagalatia 2:16

Katika Kuhesabiwa haki hii ni kauli ya Kisheria. Na ni pale mtu anapomkiri Yesu kwa kuamini kuwa wewe ni Mdhambi na umekosa na hivyo unamhitaji Yesu hivyo kwa Kuamini na kukubali na kukiri tunapata ondoleo la dhambi. Kama Marko 16:16 alivyosema.

Mchakato wa dhambi ulikuwa katika hatua mbili;

  1. Utakaso wa Mdhambi, msamaha wa dhambi nje ya Patakatifu, Walawi 4:20, 26, 31, 35.
  2. Utakaso wa Patakatifu kwa njia ya Kalenda.

Kwa maana siku hiyo upatanisho utafanywa kwa ajili yenu, ili kuwatakasa; nanyi mtatakaswa na dhambi zenu zote mbele za Bwana. 

Mambo ya Walawi 16:30

Upatanisho ulikuwa katika Matokeo ya awamu mbili;

  1. Msamaha סָלַח. Walawi 4:20, 26, 31. Walawi 5:13. Huu ni msamaha wa ondoleo la dhambi, na unatolewa na Mungu peke yake.
  2. Utakaso wa Maadili(טָהֵר). Walawi 16:30.

Kama ndivyo, je! Dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha kusafishwa mara moja, wasingejiona tena kuwa na dhambi? 

Waebrania 10:2

Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka. 

Waebrania 10:3

Yesu Kristo ndiye Kuhani wetu mkuu. Endapo kuna dini yoyote duniani inayomweka Yesu nje dini hiyo ni BURE.

Utakaso kwa maana ya jumla ni KUSAFISHA TABIA, yaani mdhambi anafanywa kuwa mpya.

Wako watu huomba maombi ya ajabu kwamba "MUNGU IKIWA TUMETENDA DHAMBI BASI UFUTE MAJINA YETU KWENYE KITABU CHA HUKUMU, UYAANDIKE KWENYE KITABU CHA UZIMA." HAKUNA MWANADAMU AWAYE YOTE WA KUWEZA KUOMBA MAOMBI YA HIVYO, KWANI HAKUNA WA KUMSHURUTISHA MUNGU KUFANYA KAZI HIYO NA HAIFANYWI NA MTU YEYOTE YULE DUNIANI. 

Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako. 

Isaya 43:25

Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako. 

Isaya 43:26

Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. 

Zaburi 51:1

Mungu pekee ndiye anayeweza kuyafuta Makosa yetu kwakuwa Yeye anayo majina yetu.

Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. 

Waebrania 4:14

Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. 

Waebrania 4:15

Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji. 

Waebrania 4:16

Siku zote Mungu halazimishi dhamiri ya Mtu imfuate wala haitaji utii wa juujuu bali utii kamili kutoka Moyoni mwa kila mwanadamu amwaminiye.

Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. 

Ufunuo wa Yohana 3:20


 

ATAPE KIHONDA NET EVENT: NYAYO ZA MATUMAINI

SIKU YA 12/21

HUDUMA KUU

TAREHE: 24/05/2023

MHUDUMU: MCHUNGAJI PAUL SEMBA

SOMO: NYAYO ZINAPOKUTANA 2

Leo tunaendelea na somo lisemalo Nyayo zinapokutana ambapo kila zinapokutana zinaleta Matumaini ya Kuendelea kumtumainia Mungu katika Ukuu wake. Leo ni Nyayo zinapokutana sehemu ya Pili. 

Wokovu wa Mwanadamu haukuishia Kalvari. Na ndiyo maana Walawi 1-6 inaelezea habari za Kafara iliyohusisha Damu katika Yohana 1:29. Ilikuwa sharti Damu imwagike na ndiyo maana Huduma za Hekalu zilikuwa zikifanyika kupitia Kuhani Mkuu na ndiyo Kazi anayofanya hata sasa hii ndiyo maana ya Nyayo zinapokutana.

Sehemu ya Pili ya somo hili limejaa Matumaini makubwa kutoka kwa Bwana Mwenyewe hivyo fuatana nami katika Somo la leo.

Kuhani mkuu alikuwa ananyunyiza Damu. Walawi 16:14-16. Na kunyunyiza damu Ilikuwa kwa ajili ya haya;

  1. Kwa ajili ya kukubali. Waebrania 10:19-20.
  2. Kwa ajili ya Usalama na Uhifadhi. Kutoka 12.
  3. Kuwekwa wakfu kwa Makuhani. Kutoka 29:20; Walawi 8:23. Ndiyo kama leo tunavyoweka Viongozi wakfu, ili kusalimisha kila kitu mikononi mwa Mungu.
  4. Kwa ajili ya Utakaso(Purification), kuondoa Unajisi. Walawi 14:7.
  5. Kuthibitisha Agano kati ya Mtu na Mungu. Kutoka 24.
  6. Upatanisho, Usafishaji upatikanao kwa njia ya Haki kwa imani yaani badiliko la Kitabia.
  7. Damu ilinyunyizwa juu ya kiti cha Rehema upande wa Mashariki(7x) na mbele ya kiti cha Rehema. Walawi 16:14-16.
  8. Namba 7, Ukamilifu(Perfection) wa Yesu na dhabihu yake. Kwamba Yesu alitolewa pasipo Waa lolote la dhambi.

Kwanini damu juu ya Kiti cha Rehema? Neno linasema;

Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. 

Kutoka 25:21

Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. 

Kutoka 25:22

Walawi 16:2.

Hivyo kupitia hayo yote hunyesha kwamba Mungu yuko juu ya Kiti cha Rehema. Na ni lazima damu ikutane na Sanduku la Agano, pamoja na Kiti cha Rehema. Hapo ndipo mahali ambapo utakutana na Mungu wako. Mungu yupo chumba cha Pili kwenye kiti cha Rehema alipoketi Mungu mwenyewe. 

Kwanini kiti cha Rehema kimeshikana na Sanduku la Agano na kiko juu ya Sanduku la Agano? Hesabu 7:89; 1Samweli 6:2.

Ilikuwa ni Ikulu(Patakatifu) ya utawala wa Mungu duniani. Maagizo yote ya Waisraeli yalitoka Hapo.

Msingi wa Utawala wa Haki na Hukumu. Zaburi 97:2.

AJ—x2 Waebrania 9:5; Warumi 3:25. Yesu ndiye Kuhani Mkuu, Dhabihu ya Upatanisho.

Yohana 17:21-23. Hapa yuko Baba ameketi katika kiti cha Enzi pamoja na Mwana. Ufunuo 3:21; Yohana 10:30; 2 Wakorintho 5:8-20.

Msingi wa kiti hicho hutoa haki na Hukumu ambapo Baba na Mwana wanakutana Pamoja.

Ndani ya Sanduku kulikuwa na Nini?

Kulikuwa na vitu vitatu.

Na nyuma ya pazia la pili, ile hema iitwayo Patakatifu pa patakatifu, Waebrania 9:3

yenye chetezo cha dhahabu, na sanduku la agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye ile mana, na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya agano; Waebrania 9:4.

na juu yake makerubi ya utukufu, yakikitia kivuli kiti cha rehema; basi hatuna nafasi sasa ya kueleza habari za vitu hivi kimoja kimoja. Waebrania 9:5

  1. Kopo la Dhahabu lenye Mana. Kutoka 16:32-33.
  2. Fimbo ya Haruni iliyochipuka. Hesabu 17:1-11.
  3. Mbao mbili za Agano. Kutoka 20; Kumbukumbu 4:13.

Vitu hivi Ishara za uasi wa Mwanadamu; Mana, kukataa utoaji wa Mungu. Fimbo, kukataa uongozi wa Mungu.

Mbao mbili za mawe kukataa Amri za Mungu. Hapo ndipo Sheria inapokutana na Neema. Nyayo zinapokutana.

Kidole cha Mungu na Kidole cha Yesu. Waebrania 9:3-5.

Kidole cha Mungu Kimoja kiliandika Sheria pale Sinai, Kumbukumbu 9:15, Kidole kingine kiliandika Neema pale Kalvari. Na hapa vinakutana pamoja.

Unapompokea Yesu, Mungu anaona Damu mateso na kifo Waebrania 8:12; 10:17. Na mwisho wa yote ni Upatanisho mahali ambapo dhambi inapozimwa Sheria na Neema vinapokutana, Walawi 16:30.

Hii maana yake ni nini?

Damu inatukuza Sheria. Damu ipo kukwambia Sheria ya Mungu inadumu milele.

Damu inashinda Dhambi na si SHERIA.

DAMU inaunganisha Kiti cha Hukumu na Kiti cha Rehema.

Damu inakutanisha HAKI, HUKUMU, FADHILI pamoja Na KWELI, Zaburi 89:14.

Damu imeshikanisha Haki na Amani. Zaburi 85:10.

Katika Kalvari Damu inamwagika na DHABIHU ilitolewa Patakatifu, Damu hunyunyizwa na dhabihu INATUMIKA.

HIYO NDIYO MAANA YA NYAYO ZINAPOKUTANA, YAANI SHERIA NA NEEMA ZINAPOKUTANA MWANADAMU ANAOKOLEWA, MUNGU ATUBARIKI TUNAPOKUTANISHWA NA NYAYO ZAKE ZINAPOKUTANA.


 

 

ATAPE KIHONDA NET EVENT: NYAYO ZA MATUMAINI

SIKU YA 13/21

HUDUMA KUU

TAREHE: 25/05/2023

SOMO: NYAYO KATIKA MAKABIDHIANO 1

Leo tunalo somo la Pekee lisemalo Nyayo Katika Makabidhiano likiwa ni sehemu ya Kwanza. Ofisi nyingi hufanya makabidhiano, au hata katika familia watu hukabidhiana vitu mbalimbali. Lakini katika somo la leo haya ni Makabidhiano yaliyotimia kabisa yaletwayi na Nyayo za Matumaini.

Naye akiisha kufanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, na hema ya kukutania, na madhabahu, atamleta yule mbuzi aliye hai. 

Mambo ya Walawi 16:20

Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari. 

Mambo ya Walawi 16:21

Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyo watu; naye atamwacha mbuzi jangwani. 

Mambo ya Walawi 16:22

Hii ni Nyayo katika Makabidhiano, Mungu alimwambia Harunina Makuhani watakaofuata kwamba baada ya kufanya upatanisho kwa ajili ya Dhambi za watu, kitakachofuata ni hiki akitoka katika lango chumba cha pili na chumba cha kwanza ndipo kulikuwa na yule Mbuzi aliyebaki aweke mikono yake miwili na Aungame uovu wote, na Makosa yote na dhambi zote za wana waisraeli. Hivyo ndivyo walifanya katika wakati huo wa maagizo ya Mungu aliyoyatoa.

Na ilikuwa katika mfumo huu;

Uovu. Danieli 9:5; 2Yohana 4:4.

Makosa. Zaburi 51:1. Waebrania 2:2.

Dhambi. 2Nyakati 6:36; 1Yohana 3:4.

Kwa sababu ya mambo hayo ndiyo maana Haruni anaambiwa aende aungame kwa dhambi ya Israeli.

Watu walitenda dhambi/Uovu kwa kutofuata sheria ya Mungu, walitenda dhambi kwa makusudi huku wakijua kuwa ni Uovu.

Haruni anaungama dhambi za watu kwa kujua au kutokujua.

Huduma ya Upatanisho ilikuwa inakabidhi yafuatayo:

Mwanadamu Kwa Mungu (2Wakorintho 5:16-20)

Mwanadamu kwa Sheria ya Mungu— UPATANISHO huwafanya kuwa Waaminifu kwa Mungu.

DHAMBI kwa KUHANI.

Kupitia Kuhani, inakabidhi DHAMBI kwa AZAZELI. Walawi 23:29.

Hii ilifanyika ili kuleta uhusiano mzuri kwa Sheria ya Mungu wao, hivyo walitakaswa kabisa yaani hawana shida tena kwakuwa sheria iko mioyoni mwao na Kristo ndani yao. Hapo ndipo Kuhani waacha kwa Mungu.

Unapomwamini Yesu kila Uovu unaondolewa, ukimwamini Yesu.

Hivyo Kuhani kupitia huduma yake watu walisafishwa na kubakia safi na huru pasipo makosa kupitia mbuzi wa Azazeli.

Hilo zoezi lilifanywa kwenye Walawi 1,2,3,4. Ndipo huduma zilifanyika ila kwa sasa anayefanya kazi hiyo ni Kuhani. Hivyo ndivyo mchakato wa upatanisho ulivyofanywa na baada ya hayo yote dhambi ilikabidhiwa kwa Umilele.

Kuhani alikabidhi Uovu, Dhambi na Makosa yote na mwisho ndipo wenye haki sasa wanaokolewa maana dhambi zote zimerudi kwa Azazeli(Shetani)

Hivyo Usiogope kujihesabia hatia Mungu ameondoa Dhambi na uko huru kwa kila anayetu na Kumwamini Yesu maishani mwake.

Israeli waliokolewa kwa Kafara(Pasaka) kupitia Neema ya Mungu, walipofika Mlima Horebu wakakabidhiwa Sheria , Kutoka 12, 20. Na ndiyo maana Mungu akasema mtakuwa wakamilifu kama mimi nilivyo mkamilifu. Walawi 19:1,2. Mungu aliwaokoa kwa Neema.

Katika Kalvari, Mungu alionesha UPENDO wake kwa ulimwengu— anamkumbatia Mdhambi.

Katika Patakatifu, Mungu huonesha UTAKATIFU—anashughulikia Dhambi(Zaburi 73)

Wadhambi wanaotubu wanakumbatiwa na kupewa Sheria na ndiyo maana Mungu anasema;

Mkinipenda, mtazishika amri zangu. Yohana 14:15. Wanaompenda Mungu sharti washike amri zake.

Asiyezishika amri za Mungu ni Mwongo;

Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. 

1 Yohana 2:3

Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. 1 Yohana 2:4

Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito. 1 Yohana 5:3

Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. 1 Yohana 5:4.

Watu hutafuta njia ya kukimbilia anasa za dunia:

  • Kujitia ganzi ya Morphine ya uwongo ili wasishike amri za Mungu.
  • Hudumaza hisia zao kwa Mvinyo, karamu, tafrija na kwa starehe.
  • Wahubiri wanapotosha Sheri—Dhambi inatamalaki.
  • Wanasiasa wanapuuzia Sheria—Dhuluma inajitukuza.

Katika hayo yote ndipo yanaibuka makundi mawili ya watu;

  • Wale wanaoruhusu mapenzi ya Mungu kutawala katika maisha yao.
  • Wale ambao Mungu anaruhusu mapenzi yao kutawala katika maisha yao.

Hivyo unapaswa kuchagua kuwa unasimamia upande gani katika hayo? CHAGUA.

Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Warumi 5:8.

Wale wote wanaotupa sheria za Mungu nje kuwa zimepitwa na Wakati ni WAONGO wala KWELI haimo ndani yao.

"Upatanisho unaofanywa na Kuhani Mkuu ni sawa na Gari ya wagonjwa (Ambulance) mgonjwa anapochukuliwa huingizwa ndani kama mdhambi anavyoingizwa katika Kristo(Neema) kisha haishii hapo bali anapelekwa Hospitali kwa ukarabati zaidi na ndivyo Yesu anavyofanya akiwa Kuhani Mku ambapo kupitia kwake Tunafanyiwa ukarabati na kuwa wapya katika Kristo."

Kubali hivi leo kukarabatiwa na Kuhani Mkuu Yesu Kristo naye akabidhi kwa Azazeli. Ukimkabidhi Yesu dhambi zako leo Yeye atazikabidhi kwa Shetani mwenyewe.

FANYA MAKABIDHIANO YAKO LEO NA YESU KWA KUMKUBALI NA KUFUATA SHERIA YAKE. MUNGU ATUBARIKI SOTE.




ATAPE KIHONDA NET EVENT: NYAYO ZA MATUMAINI

SIKU YA 14/21

HUDUMA KUU

TAREHE: 26/05/2023

MHUDUMU: MCHUNGAJI PAUL SEMBA

SOMO: NYAYO KATIKA MAKABIDHIANO 2

Leo tunaendelea na somo la pekee sana Nyayo katika Makabidhiano sehemu ya Pili kama tulivyoona katika somo lililopita na tukaona kwamba Yesu ni Kuhani Mkuu anachukua dhambi anaweka kwa Mbuzi wa Azazeli na mdhambi anakuwa huru. Neno linasema;

Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari. Mambo ya Walawi 16:21

Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyo watu; naye atamwacha mbuzi jangwani. Mambo ya Walawi 16:22

Yako majina ambayo yamekuwa yakitaja Mbuzi wa Azazeli mmoj alifungwa kwenye pembe, na mwingine ni Mbuzi wa Bwana yeye alifungwa kwenye Shingo.

Sasa leo tunaangalia huyu mbuzi wa Azazeli aliachwa wapi? 

Kafara ilishughulikia upatanisho wa dhambi aidha zilkkuwa zimefanywa kwa kujua au kutokujua.

Waebrania. 9:7.

Mbuzi yule wa Azazeli alipelekwa mbali kabisa na makazi ya watu ili afe huko. Kwanini hawakumuuwa wao? Badala yake walimtupa? Tutaangalia katika somo linalofuata.

Azazeli ni nini basi? Hili ni neno la Kiebrania likimaanisha "KUZIMA" Kwamba huko anakokwenda Atazima yaani Dhambi itayeyuka kwamba haitarejea tena, itateketezwa hiyo ndiyo Azazeli. Kwanini huyu Mbuzi ndiyo kituo cha Mwisho cha kuchukua dhambi?

Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; Ufunuo wa Yohana 12:7

nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Ufunuo wa Yohana 12:8

Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. Ufunuo wa Yohana 12:9

Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. Ufunuo wa Yohana 12:10

Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. Ufunuo wa Yohana 12:11

Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu. Ufunuo wa Yohana 12:12

Vita hii ni kati ya Mikaeli na Shetani na inaanzia juu Mbinguni, ni vita ambayo haijaanzia duniani bali mbinguni. Mikaeli huwakilisha Mungu, na Ibilisi maana yake SHITAKI KWA UWONGO(SHAMBULIA TABIA YAKE, MCHAFUA JINA, ANAYEHARIBU JINA LA MUNGU)

Neno Vita siyo vita ya Mshale, wala kwa damu na nyama. Siyo vita ya Kimwili bali ni Vita ya Kiroho na ndiyo maana ushindi wake unapatikana kwa Damu ya Mwanakondoo wa Mungu, pia wanashinda kwa Damu ya Yesu, wanashinda kwa Neno la Mungu(Biblia kauli ni Moja) ndiyo maana vita hii tunashinda kwa Neno. Hivyo Pambano Kuu kati ya Wema na Uovu tunashinda kwa Neno peke yake. Hii ilikuwa ni Vita kuhusu Neno la Mungu yaani alichosema Mungu. Mwanzo 4; inaelezea vizuri kabisa na kupitia Pambano hili pamoja na Shetani kushuka na Theluthi ya Malaika bado waliobaki walishinda kwa Neno.

Wewe ulikuwa Kerubi mwenye kutiwa mafuta *afunikaye;* nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto. Ezekieli 28:14

Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata *uovu* ulipoonekana ndani yako. Ezekieli 28:15

Nini maana ya Kerubi Afunikaye? Maana yake ni kulinda, zuia, kuweka uzio, Weka mipaka, Tunza ndani. 

Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. Kutoka 25:20

Kutoka 25:8-9. Mungu alisema Wanifanyie Patakatifu apate kukaa.

Uovu unaotajwa hapo maana yake ni kupinda, Mpotovu, mkaidi, amekanyaga sheria, kuasi Sheria. Dhambi ni uasi wa Sheria.

Kazi ya hao Malaika wanaolinda Sanduku la Agano ni kutunza Sheria ya Mungu ndiyo maana Makerubi wanalinda, kwani Shetani alishindwa kabla hajaasi alikuwa Lusifa Kerubi afunikaye. Kabla ya kuasi alijua utukufu wa Mbinguni kila kitu alikijua ila akaamua kuasi, aliacha kutunza Sheria ila Mwenzake alibakia ambaye ni Gabrieli akiendelea na Kazi ya ulinzi lakini Shetani alishindwa na kupitia kwake shida ikaingia ulimwenguni.

AZAZELI>>VITA>>UFALME.

Dhambi imekuja kwa sababu ya uasi wa sheria ya Mungu yaani Tabia ya Mungu.

Shetani ndiye atachukua Dhambi zote kwani Yeye ndiye Mwasi wa kwanza wa Pambano.

Kwenye Matendo 1:9. Yesu alikwenda na Mawingu.

Katika Danieli, Yesu anakuja na Mawingu, Danieli 7:13-14.

Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. Danieli 7:13

Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa. Danieli 7:14

Kwa nini Yesu anapambana? Anapambana ili kurejesha Ufalme wake ulioharibiwa na Mwovu. Na Neno linasema hivi katika ule mwisho wa Vita;

Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. 1 Wakorintho 15:24

Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. 1 Wakorintho 15:25.

Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti. 1 Wakorintho 15:26.

Huduma ya Yesu ni kurudisha Mamlaka ya Mungu na kazi hiyo hufanywa na Mikaeli. Shetani atatawanywa na kutoweka kabisa.

Na huyo wa saba akakimimina kitasa chake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu, katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa. Ufunuo wa Yohana 16:17.

Maana yake mamlaka zitakuwa zimerudi Yesu atakaposema IMEKWISHA.

Yesu akija atakuja akiwa Mshindi, Mfalme anakuja na kila Jicho la nwanadamu litamwona. Anakuja Shujaa wa Msalaba, Shujaa aliye wa vita anakuja.

Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu, Ufunuo wa Yohana 5:11

wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka. Ufunuo wa Yohana 5:12

Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele. Ufunuo wa Yohana 5:13

Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka, wakasujudu. Ufunuo wa Yohana 5:14

Kazi tuliyonayo ni Moja tu Kumsujudia Mungu pekee, Mungu wa Pekee wa Kweli. Hapo ndipo Yesu atakuwa amekabidhi Ufalme kwa Mungu na Shetani atakuwa ameshindwa Milele na Miele Amina.

BWANA ATUBARIKI TUNAPOENDELEA KUMNGOJA SHUJAA WETU AKIJA HIVI KARIBUNI.


 

 

ATAPE KIHONDA NET EVENT 2023: NYAYO ZA MATUMAINI

SIKU YA 15/21

HUDUMA KUU

TAREHE: 27/05/2023

MHUDUMU: MCHUNGAJI PAUL SEMBA

SOMO: NYAYO ZA UFALME 1

Leo tunalo somo lingine la pekee linalosema kwamba Nyayo za Ufalme likiwa ni Sehemu ya kwanza, je ni Nyayo katika Ufalme gani huu? Somo la leo linaweka bayana.

Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Mathayo 28:18.

Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; Mathayo 28:19.

na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. Mathayo 28:20.

Mambo ya msingi katika mafungu haya:

Jambo la Kwanza Yesu amepewa Mamlaka yote Mbinguni na Duniani. Yeye amepewa vyote.

Jambo la pili, Anawatuma watu kwenda ulimwenguni na kuwabatiza wote kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Nini maana yake? Anasema hamtaogopa, hamtatishwa kwakuwa Mamlaka yote iko kwake Yesu Kristo, Hivyo ni marufuku kuogopa lazima kila ukweli usemwe maana yupo mwenye Mamlaka mwenye Nguvu nyingi.

Jambo la tatu alilosema Yesu ni kwamba na tazama nipo nanyi hata ukamilifu wa dahari, hivyo hatuna haja ya Kuogopa maana ana mamlaka yote TUSIOGOPE.

Nini maana ya enendeni ulimwenguni? Maana yake panda milimani, mabondeni shuka chini kwa ajili ya Yesu. Biblia inasema;

Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema, Mathayo 3:1

Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Mathayo 3:2.

Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Mathayo 4:17.

hata siku ile alipochukuliwa juu, alipokuwa amekwisha kuwaagiza kwa Roho Mtakatifu wale mitume aliowachagua; Matendo ya Mitume 1:2

wale aliowadhihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu hai, akiwatokea muda wa siku arobaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu. Matendo ya Mitume 1:3

Yohana alihubiri habari za Toba na baada yake Yesu naye akaja kuhubiri habari ya Toba kwa maana ufalme wa Mungu unakuja. Kila kitu ni kuhusu ufalme wa Mungu.

Luka ameandika, Marko naye ameandika juu ya habari za Ufalme.

Watahubiriwa na Toba na ondoleo la Dhambi tena wakianzia Yerusalemu.

Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko. 

Luka 24:45

Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; Luka 24:46.

na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Luka 24:47

Nyayo za Utume zinalenga ufalme wa Mungu kwani TOBA NDIYO INAYOMKARIBISHA MTU KWENYE UFALME WA MBINGUNI, INJILI ISIYOHUSU TOBA HAINA CHOCHOTE, INJILI YA YESU IMEJENGWA KWENYE TOBA.

uwafumbue macho yao, na kuwageuza waiache giza na kuielekea nuru, waziache na nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu; kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi. Matendo ya Mitume 26:18

Kutoka katika Giza ni kutoka kwa Shetani, na kwenda nuruni ni kwenda kwa Yesu.

Maana ya TOBA, ni kugeuka, kwamba ulikuwa katika uovu na sasa unatoka katika uovu huo na kurudi kwa Mungu, ni kuchukia dhambi na kumpenda Mungu. Toba ndiyo inawaingiza watu kwenye Ufalme wa Mungu.

Injili ni kuhubiri watu waache Dhambi na siyo vinginevyo. Leo utasikia mahubiri ya utajirisho, vyeo na kadhalika hayo ni mahubiri mfu hakuna Yesu humo. Toba ni Kugeuka kutoka dhambini na siyo vinginevyo.

Basi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme? Matendo ya Mitume 1:6

Akawaambia, Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe. Matendo ya Mitume 1:7

Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. Matendo ya Mitume 1:8

Wanafunzi walipouliza habari ya Ufalme waliambiwa siyo kazi yao kujua, wala majira hakuna aliyejua bali ni Baba wa Mbinguni pekee, hivyo wanaotabiri mwaka, tarehe ya kuja kwa Yesu wanajilisha upepo tu kwani Mungu ndiye ajuaye yote kuhusu kuja kwake na si vinginevyo.

Walichoambiwa ni mambo mawili tu yaani "Roho Mtakatifu" na "Utume" basi hayo ndiyo walipaswa kujua pekee.

Katika Mathayo 24:4-5, 11, 23, 24. Huelezea dalili za Kuja kwa Yesu katika jambo la kwanza alisema UDANGANYIFU WA KIDINI, na huu ndiyo unaoendelea katika dunia hii watu kujiita Manabii na Mitume na wengi wamedanganyika kabisa katika dunia hii. Mathayo 24:4,6,7. Vita, Majanga, Magonjwa nayo yalisemwa kuwa ni dalili za nyakati za Kuja kwa Kristo. Mathayo 24:9,10, Maadili kuahribika, tabia zitaharibika, watu watateswa kwa sababu ya uaminifu wao kwa Yesu, na hatimaye kwa kuongezeka maasi Upendo wa wengi utapoa. Lakini Mwenye kuvumilia hata mwisho ndiye ATAKAYEOKOKA.

Mathayo 24:8, hayo ni mwanzo wa Utungu tu na ule mwisho bado.

Neno linaendelea kusema kwamba;

Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja. Mathayo 24:14.

Injili ni habari njema inayoleta badiliko, habari ya kuwatoa watu kwa Shetani na kuwaleta kwa Yesu kwa ajili ya habari ya Ufalme wa Mbinguni.

INJILI YA YESU NDIYO INALETA MWISHO, WALA MWISHO HAULETWI NA MAGONJWA WALA MATETEMEKO BALI NI HABARI NJEMA ZA YESU, HABARI ZA UFALME WA YESU NDIZO ZITAULETA MWISHO YAANI UFALME WA MUNGU.


 


ATAPE KIHONDA NET EVENT 2023: NYAYO ZA MATUMAINI.

SIKU YA 16/21

HUDUMA KUU

TAREHE: 28/05/2023

MHUDUMU: MCHUNGAJI PAUL SEMBA

SOMO: NYAYO ZA UFALME 2

Leo ni sehemu ya pili ya Somo lisemalo Nyayo za Ufalme na hivyo Mungu wetu ni mwema kwakuwa anakwenda kuzungumza nasi. Yesu anakuja na haji kwa sababu ya Matukio yaliyopo anakuja kwa sababu habari njema za Ufalme zinahubiriwa.

Yesu alihubiri Injili ya Toba ili watu waache dhambi wangeukie Mungu. Paulo pia alihubiri hivyohivyo watu watubu maana ufalme wa Mungu unakuja.

Yesu alisema mwenyewe kuwa ana Mamlaka yote na hivyo twapaswa kwenda kwakuwa atakuwa pamoja nasi, Mathayo 28:18-20.

Zaidi ya Hapo Yesu alisema juu ya kuja kwake katika Mathayo 24; ya kwamba Injili lazima iende kwa ulimwengu katika ujio wa Yesu katika Mathayo 24:14. Injili pekee ndiyo italeta ufumbuzi wa tabia za wanadamu leo, hivyo ni vyema Injili ihubiriwe kwa Ulimwengu.

Katika Mathayo 24:8, Biblia inasema hayo yote yanayotokea ni mwanzo wa Utungu tu hivyo mwisho ule bado hata hivyo hatupaswi kutishwa kwayo kwakuwa Bwana alikwishasema katika mambo yote atakuwa pamoja nasi.

Kuja kwa Yesu hakuletwi na hayo bali na Injili pekee.

Na sharti Injili ihubiriwe kwanza katika mataifa yote. 

Marko 13:10

Paulo naye anasema hivi;

Maana, ijapokuwa naihubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri Injili! 1 Wakorintho 9:16.

Siku ya Bwana inakuja Yoeli alisema;

Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; Yoeli 2:28.

tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu. Yoeli 2:29.

Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, na minara ya moshi. Yoeli 2:30.

Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo. Yoeli 2:31.

Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama Bwana alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao Bwana. Yoeli 2:32.

Siku ya Bwana inakuja, Atamimina Roho ya Bwana, Itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokoka, watakuwepo waliosalia pia kwa ajili ya Bwana.

Je, siku ya Bwana ni ipi? Biblia inasema;

Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea. 2 Petro 3:10.

Siku ya Bwana inakuja na itakuja na haya yafuatayo:

Siku ya Bwana, Itaathiri Dunia,

Siku ya Bwana, Itaathiri viumbe vyote vya asili vilivyomo.

Siku ya Bwana, Itaathiri kila kitu kilichomo ndani yake.

Mfalme atakapokuja kila jicho litamwona wala haji kwa Kificho kama watu wasemavyo, Siku ya Bwana inakuja hakika.

Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu. Matendo ya Mitume 2:14

Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana; Matendo ya Mitume 2:15

lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli, Matendo ya Mitume 2:16

Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto. Matendo ya Mitume 2:17

Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri. Matendo ya Mitume 2:18

Nami nitatoa ajabu katika mbingu juu, na ishara katika nchi chini, damu na moto, na mvuke wa moshi. Matendo ya Mitume 2:19

Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri. Matendo ya Mitume 2:20

Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa. Matendo ya Mitume 2:21

Jambo moja kutoka kwa Petro kipindi cha Mitume katika Matendo 2:17.

Roho Mtakatifu atamwagwa siku za Mwisho. Alikuwa anaunganisha ujumbe wa Yoeli na Ujumbe wa Roho Mtakatifu kama ambavyo tunajifunza katika habari za kile Yesu anafanya katika kiti cha Enzi katika huduma ya Upatanisho.

Wakati wa Mwisho utakuwa lini?

Lakini wewe, Ee Danielii, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka. Danieli 12:4

Na mmoja akamwuliza yule mtu aliyevikwa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto, Je! Itakuwa muda wa miaka mingapi hata mwisho wa mambo haya ya ajabu? Danieli 12:6

Nami nikamsikia yule mtu aliyevikwa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto, hapo alipoinua mkono wake wa kuume na mkono wake wa kushoto kuelekea mbinguni; akaapa kwa yeye aliye hai milele na milele, ya kwamba itakuwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati; tena watakapokuwa wamekwisha kuvunja nguvu za hao watu watakatifu, ndipo mambo hayo yote yatakapotimizwa. Danieli 12:7

Nami nikasikia, lakini sikuelewa; ndipo nikasema, Ee Bwana wangu, mwisho wa mambo haya utakuwaje? Danieli 12:8

Akasema, Enenda zako, Danielii; maana maneno haya yamefungwa, na kutiwa muhuri, hata wakati wa mwisho. Danieli 12:9

Wengi watajitakasa, na kujifanya weupe, na kusafika; bali wabaya watatenda mabaya; wala hataelewa mtu mbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa. Danieli 12:10

Maarifa yataongezeka.

Kuvunja nguvu za Utakatifu.

Siku ya Mwisho itaanza lini?

Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati. Danieli 7:25

Pembe ndogo— linganisha na Danieli 8:23-25.

Inanena kinyume chake Aliyejuu —Mungu.

Atawatesa Watakatifu wa Mungu.

Atashughulikia Majira na Sheria.

Kwa kipindi cha Wakati, Nyakati 2, ½Wakati.

Huyu si Mnyama kama mnyama bali ni Mamlaka, Ufalme ambao ndiyo unazungumziwa kupitia hiyo PEMBE kwakuwa ni Ufalme ndiyo maana watumishi waaminifu wanateswa na Mamlaka hiyo.

Leo kwanini mambo mengi yanafanyika siku ya Sabato mitihani vyuoni? Vikao mbalimbali maofisini na Semina mbalimbali kwanini yafanyike siku ya Sabato? Ni kwa sababu ya hii Pembe Ndogo(Mamlaka) inayofanya Makufuru haya ya kumchukiza Mungu wa Mbinguni.

Kwa kipindi cha Wakati, Nyakati 2, ½Wakati. Nini maana yake Maneno haya?

WAKATI, NYAKATI 2, na ½ WAKATI.

Ufunuo 14:12, Wakati, Nyakati 2, ½ Wakati.

Ufunuo 11:12; 13:5. "Miezi 42"

Ufunuo 11:3; 12:6. "Siku 1260"

SIKU 1=MWAKA 1, Hesabu 14:34; Ezekieli 4:6.

SIKU 1260= MIAKA 1260.

Mwanzo wake "naye atawashusha wafalme watatu" Danieli 7:24.

Pembe 10 = falme 10 (Danieli 7:24.)

Ujerumani, Ufaransa, Italia, Uingereza, Uhisipania, Ureno, Uswisi, (Heruli 493B.K, Vandals 534B.K, Ostrogoth -538B.K

Rejea: The Maxmillian Encyclopedia, Revised and Updated, uk. 658.

Sasa wakati wa Mwisho utaanza lini? Jibu ni hili;

"Wakati wa Mwisho" ni kipindi kinachoanzia mwaka 1798BK hadi kuja kwa Yesu mara ya pili.....

HIVYO NDIVYO MANENO YA MUNGU YANAVYOELEKEZWA KWETU SHARTI TUYAFUATE, MFALME ANAKUJA JIWEKE TAYARI.




ATAPE KIHONDA NET EVENT 2023: NYAYO ZA MATUMAINI

SIKU YA 17/21

HUDUMA KUU

TAREHE: 29/05/2023

MHUDUMU: MCHUNGAJI PAUL SEMBA

SOMO: NYAYO WAKATI WA MWISHO 1.

Baada ya somo lililopita la Nyayo za Ufalme na kuona kwamba wakati wa Mwisho ulianza mnamo mwaka 1798B.K hadi kuja kwa Yesu mara ya Pili. Sasa leo ni katika somo lingine lisemalo NYAYO WAKATI WA MWISHO likiwa ni sehemu ya Kwanza. Ni Wakati gani huu? Hebu fuatilia Neno hili la Bwana katika somo la leo.

Katika Kitabu cha Yoeli 2:28-32 tuliona Mambo matano katika wakati wa mwisho ambayo ni: ROHO WA BWANA, SIKU YA BWANA, ISHARA ANGANI, WAPO MABAKI, ITA UPONE.

Na tukaona wakati wa Mwisho ulianza mwaka 1798BK. Katika wakati huu wengi wataliitia jina la Bwana wataokoka, na waovu wataendelea katika Uovu na hawatajua Danieli 12:10.

Leo tupo wakati wa mwisho na ndiyo tunaishi hapo na kuendelea.

Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Warumi 13:1

Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. Warumi 13:2

Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake; Warumi 13:3

kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu. Warumi 13:4

Kwa hiyo ni lazima kutii, si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri. Warumi 13:5

Kwa sababu hiyo tena mwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo hiyo. Warumi 13:6

Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima. Warumi 13:7.

Maana ya Itiini Mamlaka, maana yake ni Kujitiisha, kujisalimisha kwa hiari kwa matakwa ya wengine, Mamlaka, au utawala.

Lilikuwa neno la Kijeshi. Katika matumizi yasiyo ya Kijeshi huelezea mtazamo wa hiari wa kujisalimisha.

  1. Mamlaka zote zimewekwa na Mungu. (Warumi 13:1.)

Kuasi ni kushindana na Mungu— hukumu. (Warumi 13:2.)

Ni watumishi wa Mungu kwa mema. (Warumi 13:3-4.)

Ni watumishi wa Mungu dhidi ya Mabaya. (Warumi 13:3-4.)

Lazima kutii: Kodi, ushuru, hofu, heshima. (Warumi 13:5-7.)

  1. Watawala wanapomkataa Mungu:

Wanasimamisha Sanamu. (Danieli 3.)

Wanapoteza Mamlaka. (Danieli 4:32; Danieli 5:22-32.)

Wanapoteza utii toka kwa Waaminifu. ( Matendo 5:29)

Mamlaka yoyote inaposhindwa kuwa na utii kwa Mungu watumishi wa Mungu hupoteza Uaminifu kwao. Hivyo ni heri kumtii Mungu kuliko wanadamu kama Petro alivyosema, Danieli alikataa pamoja na kutupwa katika tundu la Simba, Shadraka, Meshaki na Abedinego walikataa kuabudu miungu wakamwabudu Mungu, Waaminifu wa Bwana hawatamsaliti Mungu wao hata kama raia wote watafanya kinyume na Mungu bado Mungu atakuwa na watumishi waaminifu tu. Hata kama tutasimama mbele ya mtutu wa Bunduki bado tutadumu kuwa waaminifu tu wala hatutaogopa kwakuwa Mungu atakuwa pamoja nasi.

Baada ya Kuona Mungu na Falme sasa ni Shetani na Falme.

SHETANI NA FALME:

Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. Ufunuo wa Yohana 16:13

Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi. Ufunuo wa Yohana 16:14

Shetani atatumia Mamlaka kutekeleza Mpango wake kabla ya Wakati wa Mwisho, kuna Nguvu ya Joka itakayowaendea wafalme au viongozi kwani akiwapa viongozi atafanikisha mambo makubwa sana katika mustakabali wa Dunia.

Walengwa wakubwa katika mpango wa Shetani kuuharibu ulimwengu ni Mamlaka za Serikali, Bunge, Mahakama hivyo akishika mamlaka hizi anakuwa amemaliza kazi yake kabla ya Kuja kwa Yesu. 

Haya yanaelezwa katika Kitabu cha Danieli 2&7. Habari za Wanyama ambao walikuwa ni Falme au Mamlaka. Danieli alionyeshwa katika njozi kwenye Sanamu ikiwa na falme ambazo ni Babeli, Umedi na Uajemi, Uyunani, Rumi, Chuma na Udongo ambapo katika Chuma na Udongo kwenye hizi Falme Biblia inasema hawatashikamana kwani hakuna umoja kati ya Chuma na Udongo.

Kadiri tunavyosogea mwisho wa wakati watawala watakosa nguvu na Thamani yao kwa mujibu wa Danieli 2.

Kwa nini watawala watapoteza Thamani ya Utawala? Danieli sura ya 7 inaongeza ukatili wa Falme za dunia kupitia utawala wa SIMBA, DUBU, CHUI na MNYAMA WA KUTISHA.

Kama kuna amani duniani mbona Silaha zinazidi kutengenezwa kwa ajili ya Vita maana yake ni nini?

Pamoja na Falme hizo kuwepo bado Mungu anasema hivi ni Utwala wa Yesu peke yake ndio Utasimama, wakati Falme za dunia hii zitakapoendelea kupoteza Thamani ya Utawala wao, NI UTAWALA WA MUNGU PEKE YAKE UTASIMAMA DAIMA.

Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele. Danieli 2:44.

Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti. Danieli 2:45.

TUNAISHIJE KATIKA WAKATI HUU AMBAPO MNYAMA ANAENDELEA KUTIWA PUMZI ILI ANENE? KUMBUKA TUNAISHI KWENYE NYAYO ZA ULE UTAWALA NA NDIYO MAANA KRISTO NI MSHINDI TUSIOGOPE.




ATAPE KIHONDA NET EVENT 2023: NYAYO ZA MATUMAINI

SIKU YA 18/21

HUDUMA KUU

TAREHE: 30/05/2023

MHUDUMU: MCHUNGAJI PAUL SEMBA

SOMO: NYAYO WAKATI WA MWISHO 2

Leo tunaendelea na Somo letu ikiwa ni sehemu ya Pili, kwamba Mungu ameweka Mamlaka ili Zimwinue Mungu na siyo vinginevyo, lakini tukaona kwamba Shetani atawatumia viongozi kuharibu mpango wa Mungu.

Na leo ni sehemu ya Pili. Neno la Mungu linasema;

Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru. Ufunuo wa Yohana 13:1

Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi. Ufunuo wa Yohana 13:2

Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule. Ufunuo wa Yohana 13:3

Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? Ufunuo wa Yohana 13:4

Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili. Ufunuo wa Yohana 13:5

Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni. Ufunuo wa Yohana 13:6

Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa. Ufunuo wa Yohana 13:7

Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia. Ufunuo wa Yohana 13:8.

Ufunuoa Sura ya 13 ni maelezo yanayoendelea kutoka katika sura ya 12. Joka anakwenda kufanya vita juu ya Mchanga wa Bahari, akiwatafuta watu wa Mungu wazishikao amri za Mungu na wana Imani ya Yesu hao ndio Joka anafanya vita nao. Mnyama anatoka Baharini maana yake anatoka kwa makutano ya watu wengi Ufunuo 17:9:12. Hivyo Mnayama maana yake ni utawala au Taifa, ni Ufalme, ni Kiongozi akiwakilishwa na Mnyama. Na anapotokea huko ni mfano wa Chui, na mfano wa Simba na Dubu kama tulivyosoma katika Danieli sura ya 7, hivyo sifa za yule mnyama ndizo sifa za Huyuhuyu Mnyama au Utawala, sifa za wanyama wale wanne zinakuwa na sifa moja kwa mnyama mmoja ambayo ni sifa ya Ukatili, Mnyama huyu ana vichwa saba, na Pembe Kumi ambao ni Falme au Mamlaka za Dunia hivyo Joka anawatumia Mataifa mbalimbali kukamilisha ajenda yake ya Ukatili kwa waaminifu wa Mungu, Mnyama ana majina ya Makufuru maana yake Matukano dhidi ya Mungu, Mnyama huyu anafanya vita na watakatifu na ni katika Kipindi kilekile cha Wakati, Nyakati mbili na Nusu wakati.

Yesu aliposulubishwa Serikali iliungana na Dini kumsulibisha Yesu na ndiyo maana kulikuwa na Mafarisayo na Masudakayo, tawala za Kifalme chini ya uongozi wa Pilato na wengine wengi, hivyo ndivyo itakavyokuwa katika wakati wa mwisho kama ilivyokuwa kwa Yesu.

Watu wana Dini na Serikali haina dini lakini saa inakuja ambapo Dini inakwenda kusimama kwa ajili ya Kumwabudu Mnyama, hivyo Serikali zote za Dunia zitafanya hayo yote kwa Mamlaka ya Shetani, na Ibada inayokuja imelenga kumwabudu Mnyama.

Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia. Ufunuo wa Yohana 13:8.

Watakosujudu Mnyama, au Joka ni wale tu hawamo katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo. Tupo wakati wa kila mtu kujisajili kwa Yesu wakati ni sasa, waaminifu hawatashindwa kamwe, Wakati wa Kujisalimisha ni Sasa ili majina yabaki katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo kwani mpango wa Mungu ni kutuokoa wote walio waaminifu kwake. Wanaoandikwa katika Kitabu cha Uzima ni wale wanaokubali kukaa ndani ya Kristo pekee yani maana yake ni Watakatifu kwa Mungu.

Katika Imani tuna Biblia tu na si nje ya hapo na hata kama ni Kiongozi ni Mmoja tu Yesu Kristo.

Huyu Mnyama je, anafanyaje hadi ulimwengu wote umkubali?

na wakati wa mwisho mfalme wa kusini atashindana naye; na mfalme wa kaskazini atamshambulia kama upepo wa kisulisuli, pamoja na magari ya vita, na wapanda farasi, na merikebu nyingi; naye ataingia katika nchi hizo, na kufurika na kupita katikati. Danieli 11:40.

Mfalme wa Kusini ni nani huyo?

Wakati wa mwisho ulianza 1798BK.

Mfalme wa Kaskazini ni Seleucid Dynasty Rumi ya Kipagani kisha Rumi ya Kidini (Danieli 11)

Mfalme wa Kusini—Ptolemaic Dynasty(Upagani)


FARASI: Nembo ya Vita: (Ezekieli 38:4; Ufunuo 6:1-8; 9:16; 16:12)

  1. Shinikizo la Uchumi ndilo atakalotumia Mmyama(Shetani) kuumaliza ulimwengu. Neno linasema kwamba;

Tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. Ufunuo wa Yohana 13:17.

  1. Shinikizo la Kijeshi nalo litatumiwa na Ibilisi kuuteka Ulimwengu.

Merikebu Nembo ya Uchumi (Ufunuo 18:19; Mithali 31:14)

"Shinikizo la Kijeshi toka Marekani na Washirika wake wameuminya Ukomunisti" Reader's Digest, March 1990.

Kwa nini watu wanaukataa ukweli hata kama ni ukweli ni kwa sababu ya (Relativism) yani maana yake ni kwwmba mtu ndiye anachagua ukweli mwenyewe na hachaguliwi, hayo yote yalianza tangu karne ya 18 hadi leo yanaendelea. Habari za ushoga kwamba ni haki ya mtu ndiyo yanaendelea leo na kutetewa kuwa mtu aweza kuchagua lolote atakalo, wanawake kutafuta haki sawa kwamba "wakiwezeshwa wanaweza" "Hamsini kwa Hamsini" heshima ya Mume inapotea ya kuwa kiongozi wa familia kwamba kila mtu ana haki yake, hiyo ndiyo sera ya Adui inayoendelea, haya yote yako chini ya Mwamvuli kwamba ni Haki za Binadamu. Hivyo Upande wa Dini na Upande wa Serikali havitatuacha Salama kwa habari ya yale yanayoujia Ulimwengu kupitia kwa Mnyama. Lakini Neno linasema hivi wale watakaosalimisha maisha yao kwa Yesu na Kuandikwa katika Kitabu cha Mwana-Kondoo watabaki salama wala hawatatishwa kabisa na mambo haya yanayoujia Ulimwengu, Usiogope kabisa Bwana Yu Nasi siku zote.

Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia. Ufunuo wa Yohana 13:8.

KUBALI JINA LAKO NA LANGU LIDUMU KWENYE KITABU CHA MWANA-KONDOO KWA KUDUMU KUTENDA MAPENZI YAKE, USIOGOPE WALA KUTISHWA NA KAZI ZA YULE MNYAMA KWANI MWISHONI MUNGU NDIYE ATASHINDA DHIDI YAKE.


 


ATAPE KIHONDA NET EVENT 2023: NYAYO ZA MATUMAINI.

SIKU YA 19/21

HUDUMA KUU

TAREHE: 31/05/2023

MHUDUMU: MCHUNGAJI PAUL SEMBA

SOMO: NYAYO CHUMBANI 1

Baada ya kuona Nyayo wakati wa Mwisho katika sehemu ya Kwanza, tuliona kwamba wakati wa Mwisho ulianza mwaka 1798B.K hadi kuja kwa Yesu mara ya pili. Lakini katika sehemu ya pili tukaona kwamba Shetani atatumia Serikali na Dini kukamilisha ajenda yake ya Ukatili kwa ulimwengu huu, lakini Waaminifu ambao majina yao yamo katika kitabu cha Mwana-Kondoo watabaki salama. Leo tunalo somo lingine lisemalo Nyayo Chumbani sehemu ya kwanza je ni wapi hapo? Neno linakwenda kutueleza.

Katika Ufunuo 16:13-14. Tuliona Mnyama ndiye anambeba mwamamke wa Ufunuo 17, huyu ni m

Mnyama mwenye kupewa Mamlaka na Shetani, mwenye kunena Makufuru. Huo ni Ushirika wa Utatu Mchafu. Lakini tukaona katika Ufunuo 12, 13 kuna Wanyama ambao ni Ufalme na anatumia Farasi kama nembo ya Vita, Merikebu nembo ya Uchumi lakini mwisho tunaona kwamba Dini na Serikali vinatumiwa katika kutimiza ajenda ya Shetani. Nabii wa uongo anatumia mafundisho ya Uongo na Miujiza na Ishara peke yake ili kuwaaminisha watu, na udanganyifu mwingi ili kuudanganya ulimwengu na hatimaye kinachotokea ni Ibada ya Sanamu ya Mnyama kama matokeo ya kuungana kwa Dini na Serikali, hivyo ni kila mtu kuchagua kwamba atamchagua nani wa Kumtumikia.

Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? Ufunuo wa Yohana 13:4.

Joka anatumia tawala za Dunia na Dini ili asujudiwe.

Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu. Ufunuo wa Yohana 13:13.

Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi. Ufunuo wa Yohana 13:14

Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. Ufunuo wa Yohana 13:15.

Lengo la Serikali na Dini ni kumsujudia Joka hivyo wakazi wa dunia watashurutishwa kumtii Mnyama kupitia Serikali na Dini huo ndio mpango mzima wa Shetani kupeleka watu kwa Ibada ya Sanamu(Joka).

"Ukristo ukawa dini ya Kipagani" (Church History)

Katika jumbe za Makanisa Yohana akiwa kule Patmo ujumbe ulikwenda Efeso wakaambiwa wameupoteza upendo wa kwanza tangu mwaka wa 30-100. Baada ya Hapo kanisa la Smirna, hiki kilikuwa kipindi cha Mateso makali watu waliteswa ila Mungu aliwatia moyo kuwa waaminifu hadi mwisho, baada ya hapo likaja Kanisa la Pergamo hawa walifanya Maridhiano(Compromisation ) uovu au upagani ukaanza kuingia taratibu kwa uhakika kwa sababu ya kuweka maelewano ukristo ukalegea ibada ikatoka kwa Mungu na kuwa Ibada ya Jua, katika kipindi cha Mfalme Kostantino akiwa kiongozi na Mtawala wa kidini, hivyo upagani ulitapakaa sana. Baada ya hapo Likaja kanisa la Thiatira kanisa lililo kufa, linanuka, limeharibiwa na mafundisho wa uongo, ibada ya sanamu, ibada za kuabudu watu, na kuanza kuabudu Jumapili ndiyo maana Yohana anaambiwa apeleke ujumbe huko, hayo yote ni kwa sababu ya Ibada maana ndiyo kiini cha yote. Leo utasikia umoja wa Dini na umoja wa Madhehebu kiini chake ni kufikia Ibada ya Sanamu. Neno ndilo linaleta umoja nje ya hapo ni bure. Njooni Chumbani Yesu anaita huko ndiko aliko yaani Ikulu ya Mbinguni. Hicho ndicho kipindi cha Pergamo kilivyokuwa watu badala ya kuomba Msamaha kwa Mungu ila wakawa wanapewa vyeti na kadi za Msamaha, yaani lilikuwa ni kanisa lilio gizani haswa. Ukristo ulikuwa upagani uliobatizwa (Church History) 

Baada ya hapo utakuta Rumi, ilibadilika kati ya Rumi ya Mashariki na Rumi ya Magharibi ikisimamiwa na Orthodox. Lakini katika hayo yote Jumapili ndiyo ilikuwa siku ya Ibada. Wengine wakiita kuwa ni siku ya Kufufuka kwa Yesu na siku ya Pentekoste lakini kwa mujibu wa Walawi 23:16 sivyo kama walivyotafsiri wao. Hivyo Jumapili haikuwa siku ya Ibada mahala popote katika Biblia. 

Kila kitu kimeandikwa katika Maandiko Matakatifu. Baada ya hapo Ibada za Jumapili zikasimama, Maombezi ya wafu yakasimama, Mila na Destrui zikapata nafasi, habari za (Purgatory) zikasimama ni katika kipindi cha Kanisa la Pergamo katika haya yote kinachotafutwa ni IBADA.

Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. Ufunuo wa Yohana 12:9.

Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari. Ufunuo wa Yohana 12:17.

Lengo la Shetani ni kuondoa Ibada ya kweli kwa wakazi wa Dunia na kupewa Joka haya yote ndiko tunakoelekea. Na hii ni baada ya Shetani kuondoa Amri za Mungu ili apenyeze Ibada yake, ukweli ni huu pamoja na mengi kubadilishwa bado Ibada ya kweli itasimama kama neno lisemavyo;

Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Kutoka 20:8

Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; Kutoka 20:9.

lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Kutoka 20:10.

MNYAMA ANAPOENDELEA KUTIWA PUMZI ILI ANENE TUELEWA KWAMBA, MUNGU ANAHITAJI IBADA YA KWELI, NA SHETANI ANAHITAJI IBADA BANDIA NI NANI TUTASIMAMA KUMWABUDU? TUKUBALI KUMWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI NDIPO TUTAKUWA SALAMA.




ATAPE KIHONDA NET EVENT 2023: NYAYO ZA MATUMAINI

SIKU YA 20/21

HUDUMA KUU

TAREHE: 01/06/2023

MHUDUMU: MCHUNGAJI PAUL SEMBA

SOMO: NYAYO CHUMBANI 2

Leo tunalo somo lingine lisemalo Nyayo Chumbani sehemu ya Pili. Katika sehemu ya kwanza tuliona jinsi ambavyo Upagani uliingia na zaidi ya hapo tukaona chanzo cha Ibada za Sanamu dhidi ya Ibada ya Mungu. Pia tukazidi kuona kwamba kadiri tunavyousogelea wakati wa Mwisho Shetani ataendelea Kutumia Serikali n Dini kwa Nguvu ili kutimiza ajenda yake ya kuhalalisha ibada bandia yaani Ibada ya Sanamu ya Mnyama. Leo ni Nyayo Chumbani Sehemu ya Pili.

Mwendo wote wa Joka yaani nabii wa uongo ni kuelekea Chumbani, kuharibu amri za Mungu yaani Tabia ya Mungu lililo sanduku la Agano.

Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka. Ufunuo wa Yohana 13:11.

Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona. Ufunuo wa Yohana 13:12.

Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu. Ufunuo wa Yohana 13:13.

Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi. Ufunuo wa Yohana 13:14.

Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. Ufunuo wa Yohana 13:15.

Biblia inaeleza Mnyama anayetoka Nchi Kavu, lakini tukaona kwamba Joka anasimama kwa wakazi wa Dunia, lakini anafanya nini hapo? Ufunuo 13:1-5, tuliona kazi yake kwamba ni kwa ajili ya kuwakalia wakazi wa dunia. Kumbuka Ufunuo 12 inaendelea hadi sura ya 17, ikimwonyesha Joka namna anavyotawala. Katika Ufunuo 17:1,2,3, 12-14. Hivyo Mnyama anastajaabiwa na dunia nzima na hatimaye Joka anasujudiwa na mwisho katika Ufunuo 13 inamalizia kwamba dunia yote itamsujudia. Ufunuo 13:5, wakazi wote wa dunia wanatengeneza Sanamu kwa ajili ya Mnyama wa kwanza anayesujudiwa na Ulimwengu Mzima. Mnyama anayetoka Baharini huwezi kumwona ila akinena ni Joka Mwenyewe, na huyu Joka ameanzia katika Ufunuo 12:6, 9,10; na Ufunuo 11:3. Jeraha la Mnyama huyu lilipona je maana yake ni nini? Je ni Mnyama gani huyu aliyeinuka mwenye sifa za Mnyama wa kwanza?

Katika ule mwisho wa Mwaka 1798B.K, watu waliteswa na hasa wakristo waaminifu, lakini kama utakumbuka kule Amerika katika wakati wa mwaka 1776 Amerika ilipata uhuru na kujitoa katika utawala wa Kikoloni na Hatimaye Rais Washington akawa ni Rais wa Nchi. Utakumbuka kwanini Biashara ya Pembe tatu ya Utumwa(Triangular Slave Trade) ilianzishwa katika mabara matatu; Asia, Amerika na Afrika? Baada ya wahindi kushindwa kufanya kazi kwa sababu ya kuchoka na kufa ndipo watu weusi wakachukuliwa ili kufanya kazi huko Marekani kwakuwa walikuwa na uwezo kulingana na afya zao kuhimili mazingira hayo. Leo unasikia Serikali haina Dini ila watu ndio wana dini, hii kauli muda si mrefu itapotea, tumia muda ungalipo kumcha Mungu. Katika wakati huo kule Amerika ndipo vita dhidi ya ugaidi ilianzia. Amerika tangu imepanda haijawahi kushuka, maana hii ndiyo itakayosimamisha Ibada ya Sanamu, Sanamu itatiwa Pumzi na Marekani, kwa sasa dini na Serikali haziko pamoja ila saa inakuka zitakuwa pamoja. Nani asiyejua kuwa Amerika ni kiongozi wa Dunia? Kila mtu atajua tu na ndicho kinaendelea kwakuwa Amerika ina Nguvu Kiichumi na ina Nguvu Kisiasa.

Hivyo Amerika itazidi kuwa Juu tu. Mnyama mwenye pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo. Atafanya ishara kubwa Ufunuo 16:14; Ufunuo 13. 

Atafanya Ishara Kubwa:

Uprotestanti wa Marekani utamtambulisha Mnyama.

Ili Marekani iunde Sanamu ya Mnyama, nguvu ya Kidini lazima itawale Dunia.

Mamlaka ya Serikali itaajiriwa na Kanisa ili kukamilisha lengo lake.

Inaundwa na Uprotestanti wa Amerika kwa kushawishi serikali kutekeleza Amri zao.

Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye. 

Mathayo 24:4

Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi. Mathayo 24:5

Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi. Mathayo 24:11

Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. Mathayo 24:24

Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. Mathayo 24:25

Dini itatawala Serikali za Dunia. Lazima Sanamu iundwe na Uprotestanti wa Marekani. Mwamvuli unaotumika leo wa Umoja wa Makanisa na dini ni kwa sababu ajenda ni kusimamisha Sanamu ya Mnyama duniani.

Pamoja na hayo bado Kuna Masalio wa Mungu.

Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama Bwana alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao Bwana. Yoeli 2:32

Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari. Ufunuo wa Yohana 12:17

Pamoja na watu waaminifu kuteswa, bado Mungu atakuwa na watu WALIOSALIA wakiwa waaminifu kwa Mungu wao.

Wana Amri za Mungu na Ushuhuda wa Yesu hao ndio waliosalia kwa ajili ya Bwana. Kutoka 20:8-11. Waliosalia wana sifa za kutunza Amri za Mungu.

Biblia inaposema Joka akamkasirikia yule Mwanamke maana yake;

Mwanamke-Kanisa (Isaya 62:11; 2Wakorintho 11:2; 14:4)

Waliosalia—

Wametokea baada ya kipindi cha Wakati, Nyakati mbili na ½Wakati. Ufunuo 12:14,6.

Wametokea Nyikani—Palitengenezwa na Mungu.

Wametokea Nyikani–walipolishwa na Mungu.

Wana sifa bainishi–wanashika amri za Mungu na Imani ya Yesu. Ufunuo 12:17.

Kazi ya Joka anachukia Amri zile kumi za Mungu, Joka analekea chumbani kuona lile Sanduku la Agano yaani Tabia ya Mungu lakini hatashinda kamwe, Mungu atashinda daima.

TUNASIMAMAJE KATIKA KIPINDI HIKI AMBACHO HIVI KARIBUNI MNYAMA ANAKWENDA KUTIWA PUMZI ILI ANENE? USALAMA WETU NI KUSIMAMA KATIKA NENO LA MUNGU PEKEE, KWA MUJIBU WA YOHANA 17:17; 17 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.  




ATAPE KIHONDA NET EVENT 2023: NYAYO ZA MATUMAINI

SIKU YA 21/21

HUDUMA KUU

TAREHE: 02/06/2023

MHUDUMU: MCHUNGAJI PAUL SEMBA

SOMO: NYAYO KATIKA MAWINGU

Baada ya kuona katika somo la Nyayo Chumbani sehemu ya kwanza na ya pili leo tunalo somo lingine lisemalo Nyayo katika Mawingu, je ni nini maana yake?

tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; Tito 2:13.

Mungu ni mkuu na Mwokozi wetu.

Warumi 9:10.

Isaya 7:14. 9:6. Yesu ni Mungu.

Mathayo 1:23,24.

Yesu atakuja hakika.

Basi, ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake, 2 Wathesalonike 2:1

Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; 2 Wathesalonike 2:3

Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa. 2 Wathesalonike 2:7

Mwisho wa Dunia utaambatana na mambo yafuatayo kabla ya kuja kwa Yesu:

  1. Mwisho wa dunia huchochewa na Injili kuhubiriwa ulimwenguni kote.
  2. Mwisho wa dunia hudhihirishwa kwa kuja kwa Yesu mara ya pili.
  3. Kuja kwa Yesu hutanguliwa na Dhiki ya Dunia. Mathayo 24:29.

B'. Dhiki ya dunia hudhihirishwa na ushirika mchafu wa utatu mchafu: Joka, Mnyama na Nabii wa Uongo.

A'. Dhiki ya dunia huchochewa na Injili ya Milele.

Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, Ufunuo wa Yohana 14:6

akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji. Ufunuo wa Yohana 14:7

Huu ni ujumbe kwa ajili kwa Mataifa yote kumwabudu Mungu, ni ujumbe usiozuiliwa na chochote, ni ujumbe Maalumu ukiwa umebebwa na Wajumbe Watakatifu wakiruka katikati ya Mbingu. Kama tulivyoona katika habari ya Joka kwamba anahitaji kuabudiwa. Hivyo wito na mwaliko ni kumwabudu Mungu na siyo Joka.

Utajuaje kuwa ninamwabudu Mungu wa kweli au la?

Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. Mwanzo 2:1

Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mwanzo 2:2

Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya. Mwanzo 2:3

Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa. Siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi. Mwanzo 2:4

Mungu ndiye Muumbaji na ndiye anapaswa kuabudiwa.

Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Kutoka 20:8

Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; Kutoka 20:9

Lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Kutoka 20:10

Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa. 

Kutoka 20:11

Ezekieli 20:12.

Ezekieli 20:20.

Sabato ni Ishara kwamba Mungu ndiye Muumbaji na ndiye anayetutakasa.

Wanadamu wote wanaitwa kumwabudu Mungu vizazi na vizazi. Kwa mujibu wa kitabu cha Isaya 66:22-23.

Mungu anatafuta watu ambao watamwabudu katika Roho na Kweli, Yohana 4:23-24.

Yesu aliabudu siku ya Sabato. Luka 4:16.

Sabato ilifanyika kwa ajili ya Mwanadamu na siyo vinginevyo.

Marko 2:27-28.

Sabato itaendelea siku zote kwani Yesu aliithiibitisha mwenyewe.

Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato. Mathayo 24:20

Jumapili imezungumzwa mara saba kuhusiana na kufufuka kwa Yesu na siyo vinginevyo.

Mathayo 28:1; Marko 16:1; Luka 24:1; Yohana 20:1,19.

Na Paulo akazungumzia nje ya Kufufuka kwa Yesu. Akisema;

Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja; 1 Wakorintho 16:2.

Jumapili siyo siku ya Ibada bali siku ya Sabato.

Katika ujumbe wa Malaika wa wa kwanza watu wanaitwa kurudisha ibada kwa Mungu, japo Shetani anaitafuta na kuilenga hasa.

Injili ya Milele inataja kiini cha Pambano Kuu: Kwa Mungu Mwumbaji na siyo Shetani.

Ukweli utashinda siku zote, simama katika Kweli ya Mungu usidanganywe. Yohana 8:32; Yohana 17:17.

Kuanzia miaka ya 1800's:

Wawalidensia walimwinua Yesu kwa kuutetea Ukweli. Johna Huss, Luther, Calvin, Anabaptist, Wesley, Miller, hadi kwa wa Adventista.

Na katika Miaka ya 1400's: Biblia, Utii, Neema, Ukuaji, Ubatizo, Utakatifu, Marejeo, Sabato, Kifo Afya. Vyote viliinuliwa na waaminfu katika karne zote.

Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake. Ufunuo wa Yohana 14:8.

Babeli ya Nimrodi iliangushwa na Mungu. Mwanzo 11:9.

Danieli 4:30. 5:30,31. Iliangushwa na Umedi na Uajemi.

Babeli ni Mafundisho yote ya Uongo yaliyoletwa na Babeli, Babeli anasema kula kila kitu, abudu siku yoyote, mtu anaishi baada ya kufa, siku ya kwanza ya Juma ikaingizwa kuwa siku ya Ibada, maombi juu ya watu waliokufa, Ubatizo Bandia. Haya yote ni Mafundisho ya uongo ya Babeli.

Lakini habari zitokazo mashariki na kaskazini zitamfadhaisha; naye atatoka kwa ghadhabu nyingi, ili kuharibu, na kuwaondolea mbali watu wengi. Danieli 11:44

Kwa nini Mashariki?

Katika ulimwengu wa kale, Mashariki ndicho kilikuwa kitovu cha Dira—Ezekieli 43:2-5; Isaya 41:2,4; Uf. 7:2; 16:12; Math 24:27.

Huu ni ujumbe unaohusu kuja kwa Yesu mara ya pili.

Kaskazini – “Nitaleta mabaya toka Kaskazini" Yeremia 4:6; Yer. 1:4; 3:18; 23:8; Zekaria 2:6; Ezekieli 9:1-10.

Kaskazini ni upande ambao maadui wa watu wa Mungu walifanyia mashambulizi yao kama walivyotumiwa na Mungu kutoa hukumu dhidi ya Uasi wa Israeli.

Huu ni ujumbe wa Hukumu ya Mungu.

Habari: "Kaskazini na Mashariki zitamfadhaisha naye atatoka kwa ghadhabu nyingi, ili kuharibu na kuondolea mbali watu wengi." Danieli 11:44.

Serikali na Mahakama, Dini na Madhehebu watafanya Shauri pamoja(Luka 23:12; Mathayo 22:34)

"Niliona viongozi wakuu wa nchi wakishauriana pamoja, na Shetani na Malaika zake wakishughulika kuwazunguka. Nikaona maandishi ambayo nakala zake zilitawanywa katika sehemu mbalimbali za nchi zikitoa amri kwamba watakatifu wasipoiacha imani yao ya pekee, kuiacha Sabato, na kuitunza siku ya kwanza ya juma, basi watu watakuwa huru kuwaua baada ya muda fulani kupita."(The Story of Redemption. 406.)

Huu ndiyo ujumbe utakaotikisa jeshi La Joka na Washirika wake.

Bwana atadumu kuwa na watu wake waaminifu pamoja na Dhiki kuu watalindwa.

Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. Danieli 12:1

Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele. Danieli 12:2

Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele. Danieli 12:3

Yesu atakuja na Kila Jicho litamwona akija na Watakatifu watashangilia wakisema;

Katika siku hiyo watasema, Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye Bwana tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake. Isaya 25:9.

HILO NDILO TUMAINI LENYE BARAKA YANI KUJA KWA YESU MAWINGUNI AKIJA KUTUCHUKUA WASHINDI WA DHAMBI, MUNGU ATUBARIKI SOTE, TUKUTANE MBINGUNI