Seventh-day Adventist® Church

PASTOR LETTA'S OFFICIAL WEBSITE

Menu

WAEBRANIA HADI UFUNUO

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: 1 WATHESALONIKE 5:1-28

JUMATATU, 01/11/2021

1 Wathesalonike 5 1

Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.

1 Wathesalonike 5 2

Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.

1 Wathesalonike 5 3

Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.

1 Wathesalonike 5 4

Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.

1 Wathesalonike 5 5

Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.

1 Wathesalonike 5 6

Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.

1 Wathesalonike 5 7

Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku.

1 Wathesalonike 5 8

Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu.

1 Wathesalonike 5 9

Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo;

1 Wathesalonike 5 10

ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, kwamba twakesha au kwamba twalala.

1 Wathesalonike 5 11

Basi, farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake, vile vile kama mnavyofanya.

1 Wathesalonike 5 12

Lakini, ndugu, tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu, na kuwasimamia ninyi katika Bwana, na kuwaonyeni;

1 Wathesalonike 5 13

mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Iweni na amani ninyi kwa ninyi.

1 Wathesalonike 5 14

Ndugu, twawasihi, waonyeni wale wasiokaa kwa utaratibu; watieni moyo walio dhaifu; watieni nguvu wanyonge; vumilieni na watu wote.

1 Wathesalonike 5 15

Angalieni mtu awaye yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.

1 Wathesalonike 5 16

Furahini siku zote;

1 Wathesalonike 5 17

ombeni bila kukoma;

1 Wathesalonike 5 18

shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.

1 Wathesalonike 5 19

Msimzimishe Roho;

1 Wathesalonike 5 20

msitweze unabii;

1 Wathesalonike 5 21

jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema;

1 Wathesalonike 5 22

jitengeni na ubaya wa kila namna.

1 Wathesalonike 5 23

Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.

1 Wathesalonike 5 24

Yeye ni mwaminifu ambaye awaita, naye atafanya.

1 Wathesalonike 5 25

Ndugu, tuombeeni.

1 Wathesalonike 5 26

Wasalimuni ndugu wote kwa busu takatifu.

1 Wathesalonike 5 27

Nawaapisha kwa Bwana, ndugu wote wasomewe waraka huu.

1 Wathesalonike 5 28

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi.

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Je kule kusema 'siku ya Bwana yaja kama mwivi' ni kumaanisha Yesu anakuja kuwatwaa walio wake kimya kimya bila watu wengine kufahamu kama mwivi afanyavyo?
  2. Je kuja kwa Yesu kutatokea wakati dunia ikiwa kuna machafuko makubwa au ikiwa katika amani bandia? Hao watakaokuwa wakisema Amani! Amani! Ni watu gani?
  3. Maneno haya 'Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo' yanakupa faraja gani wewe uliyeweka tumaini lako kwa Kristo? Je unadhani Mungu ana hasira na wewe au anatamani kukuokoa?
  4. Je swala la kuwatambua wanaojitaabisha kwa ajili yenu wakiwasimamia na kuwaonyeni linawahusu viongozi wako wa kiroho kama Wachungaji? Kwa nini wengine hawaoni wachungaji kama wanaostahili kutambuliwa? Je hawa wanapingana na Maandiko?
  5. Je kufurahi siku zote na kuomba bila kukoma ni jambo linalowezekana katika maisha haya? Hiyo ni kumaanisha kuwa uonyeshe furaha hata unapokuwa umefiwa au umefikwa na matatizo?

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: 1TIMOTHEO 1:1-20

IJUMAA, 05/11/2021

1 Timotheo 1 1

Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na Kristo Yesu, taraja letu;

1 Timotheo 1 2

kwa Timotheo, mwanangu hasa katika imani. Neema na iwe kwako, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.

1 Timotheo 1 3

Kama vile nilivyokusihi ukae Efeso, nilipokuwa nikisafiri kwenda Makedonia, ili uwakataze wengine wasifundishe elimu nyingine;

1 Timotheo 1 4

wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na ukomo, ziletazo maswali wala si madaraka ya Mungu yaliyo katika imani; basi ufanye hivyo.

1 Timotheo 1 5

Walakini mwisho wa agizo hilo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki.

1 Timotheo 1 6

Wengine wakiyakosa hayo wamegeukia maneno ya ubatili;

1 Timotheo 1 7

wapenda kuwa waalimu wa sheria, ingawa hawayafahamu wasemayo wala mambo yale wayanenayo kwa uthabiti.

1 Timotheo 1 8

Lakini twajua ya kuwa sheria ni njema, kama mtu akiitumia kwa njia iliyo halali;

1 Timotheo 1 9

akilifahamu neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu wa haki, bali waasi, na wasio wataratibu, na makafiri, na wenye dhambi, na wanajisi, na wasiomcha Mungu, na wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na wauaji,

1 Timotheo 1 10

na wazinifu, na wafiraji, na waibao watu, na waongo, nao waapao kwa uongo; na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;

1 Timotheo 1 11

kama vile ilivyonenwa katika Habari Njema ya utukufu wa Mungu ahimidiwaye, niliyowekewa amana.

1 Timotheo 1 12

Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akaniweka katika utumishi wake;

1 Timotheo 1 13

ingawa hapo kwanza nalikuwa mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye jeuri, lakini nalipata rehema kwa kuwa nalitenda hivyo kwa ujinga, na kwa kutokuwa na imani.

1 Timotheo 1 14

Na neema ya Bwana wetu ilizidi sana, pamoja na imani na pendo lililo katika Kristo Yesu.

1 Timotheo 1 15

Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi.

1 Timotheo 1 16

Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika mimi wa kwanza, Yesu Kristo audhihirishe uvumilivu wake wote; niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini baadaye, wapate uzima wa milele.

1 Timotheo 1 17

Sasa kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina.

1 Timotheo 1 18

Mwanangu Timotheo, nakukabidhi agizo hilo liwe akiba, kwa ajili ya maneno ya unabii yaliyotangulia juu yako, ili katika hayo uvipige vile vita vizuri;

1 Timotheo 1 19

uwe mwenye imani na dhamiri njema, ambayo wengine wameisukumia mbali, wakaangamia kwa habari ya Imani.

1 Timotheo 1 20

Katika hao wamo Himenayo na Iskanda, ambao nimempa Shetani watu hao, ili wafundishwe wasimtukane Mungu.

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Kwa nini sheria haimhusu mtu wa haki? Kwa nini katika kuifafanua sheria kumekuwepo na upotoshaji mwingi? (fng7) Namna isiyo halali ya kutumia sheria ni ipi?
  2. Je kila atendaye dhambi au makosa hufanya hivyo kwa sababu ya ujinga na kwa kutokuwa na imani? (fng13) Je, unapoomba msamaha waweza kuzitaja sababu hizo kama hoja za kumshawishi Mungu akusamehe?
  3. Je Paulo alikuwa sahihi kusema Himenayo na Iskanda amempatia Shetani ili awafundishe wasimtukane Mungu (fng20)? Je kuna wakati watumishi wa Mungu wanaruhusiwa kutamka maneno kama haya kwa waumini wao?

JIBU KWELI AU SI KWELI:

  1. Timotheo alipoitwa kutumika kama mchungaji na msaidizi wa Paulo alikuwa hajaoa.
  2. Mtu anaweza kumtumikia Mungu katika nafasi yoyote kanisani hata kama hajaoa au hajaolewa?

 

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: 1TIMOTHEO 5:1-25

JUMANNE, 09/11/2021

1 Timotheo 5 1

Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na vijana kama ndugu;

1 Timotheo 5 2

wanawake wazee kama mama; wanawake vijana kama ndugu wa kike; katika usafi wote.

1 Timotheo 5 3

Uwaheshimu wajane walio wajane kweli kweli.

1 Timotheo 5 4

Lakini mjane akiwa ana watoto au wajukuu, na wajifunze kwanza kuyatenda yaliyo wajibu wao kwa jamaa zao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Kwa kuwa hili lakubalika mbele za Mungu.

1 Timotheo 5 5

Basi yeye aliye mjane kweli kweli, ameachwa peke yake, huyo amemwekea Mungu tumaini lake, naye hudumu katika maombi na sala mchana na usiku.

1 Timotheo 5 6

Bali, yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai.

1 Timotheo 5 7

Mambo hayo pia uyaagize, ili wasiwe na lawama.

1 Timotheo 5 8

Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.

1 Timotheo 5 9

Mjane asiandikwe isipokuwa umri wake amepata miaka sitini; naye amekuwa mke wa mume mmoja;

1 Timotheo 5 10

naye ameshuhudiwa kwa matendo mema; ikiwa amelea watoto, ikiwa amekaribisha wageni, ikiwa amewaosha watakatifu miguu, ikiwa amewasaidia wateswao, ikiwa amefuata kwa bidii kila tendo jema.

1 Timotheo 5 11

Bali wajane walio vijana ukatae kuwaandika hao, maana, wakizidiwa na tamaa kinyume cha Kristo, wataka kuolewa;

1 Timotheo 5 12

nao wana hukumu kwa kuwa wameiacha imani yao ya kwanza.

1 Timotheo 5 13

Tena, pamoja na hayo, hujifunza kuwa wavivu, wakizunguka-zunguka nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni wachongezi na wadadisi, wakinena maneno yasiyowapasa.

1 Timotheo 5 14

Basi napenda wajane, ambao si wazee, waolewe, wazae watoto, wawe na madaraka ya nyumbani; ili wasimpe adui nafasi ya kulaumu.

1 Timotheo 5 15

Kwa maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani.

1 Timotheo 5 16

Mwanamke aaminiye, akiwa ana wajane, na awasaidie mwenyewe, Kanisa lisilemewe; ili liwasaidie wale walio wajane kweli kweli.

1 Timotheo 5 17

Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha.

1 Timotheo 5 18

Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng’ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake.

1 Timotheo 5 19

Usikubali mashitaka juu ya mzee, ila kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu.

1 Timotheo 5 20

Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope.

1 Timotheo 5 21

Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, na mbele za malaika wateule, uyatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo.

1 Timotheo 5 22

Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe safi.

1 Timotheo 5 23

Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara.

1 Timotheo 5 24

Dhambi za watu wengine zi dhahiri, zatangulia kwenda hukumuni; wengine dhambi zao zawafuata.

1 Timotheo 5 25

Vivyo hivyo matendo yaliyo mazuri ya dhahiri; wala yale yasiyo dhahiri hayawezi kusitirika.

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Utaratibu wa kukemea kwa kuangalia rika shida aliyonayo mtu unafaa kuzingatiwa na wahubiri wa leo? Kwa nini kuna malalamiko mengi hasa kutoka kwa wainjilisti kuwa Wazee wa kanisa na wachungaji hawakemei dhambi? Kuna ukweli wowote juu ya madai hayo?
  2. Wajane walioachwa peke yao wanatakiwa kuweka tumaini lao kwa nani na kwa nini? Mpango wa maombi kwa wajane kama hao ukoje? Kwa nini kwa kawaida wajane huachwa peke yao.
  3. Kwa nini asiyejizuia nafsi yake huhesabiwa kama aliyekufa ingawa yu hai?
  4. Kwa nini kasi ya wajane wasio wazee kuolewa ni ndogo? Je mjane akiolewa ni lazima ayaache makazi aliyojenga na marehemu mumewe? Huenda hiki kikawa ni kikwazo kinachozuia wasiolewe?
  5. Kwa nini asiyewatunza wa nyumbani mwake ni mbaya kuliko asiyeamini?
  6. Kwa nini wazee watawalao vyema na hasa wale wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha wanastahili kupewa heshima maradufu?
  7. Kwa nini wale wadumuo kutenda dhambi wanatakiwa kukemewa tena mbele ya watu wote? Je huku si kudhalilisha watu?
  8. Kwa nini Timotheo aliambiwa atumie mvinyo kidogo badala ya kutumia maji peke yake? Je mvinyo una faida gani katika mwili wa mwanadamu? Je fungu hilo linahalalisha watu kunywa pombe?

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: 1TIMOTHEO 6:1-21

JUMATANO, 10/11/2021

1 Timotheo 6 1

Wo wote walio chini ya kongwa, hali ya utumwa, na wawahesabie bwana zao kuwa wamestahili heshima yote, jina la Mungu lisitukanwe wala mafundisho yetu.

1 Timotheo 6 2

Na wale walio na bwana waaminio wasiwadharau kwa kuwa ni ndugu; bali afadhali wawatumikie, kwa sababu hao waishirikio faida ya kazi yao wamekuwa wenye imani na kupendwa. Mambo hayo uyafundishe na kuonya.

1 Timotheo 6 3

Mtu awaye yote akifundisha elimu nyingine, wala hayakubali maneno yenye uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo, wala mafundisho yapatanayo na utauwa,

1 Timotheo 6 4

amejivuna; wala hafahamu neno lo lote; bali ana wazimu wa kuwazia habari za maswali, na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matukano, na shuku mbaya;

1 Timotheo 6 5

na majadiliano ya watu walioharibika akili zao, walioikosa kweli, huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida.

1 Timotheo 6 6

Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa.

1 Timotheo 6 7

Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu;

1 Timotheo 6 8

ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo.

1 Timotheo 6 9

Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu.

1 Timotheo 6 10

Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.

1 Timotheo 6 11

Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole.

1 Timotheo 6 12

Piga vita vile vizuri vya imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi.

1 Timotheo 6 13

Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato,

1 Timotheo 6 14

kwamba uilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo;

1 Timotheo 6 15

ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana;

1 Timotheo 6 16

ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina.

1 Timotheo 6 17

Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha.

1 Timotheo 6 18

Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo;

1 Timotheo 6 19

huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli.

1 Timotheo 6 20

Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na maneno yasiyo ya dini, yasiyo na maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa uongo;

1 Timotheo 6 21

ambayo wengine wakiikiri hiyo wameikosa Imani. Neema na iwe pamoja nanyi.

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Ilikuwa sahihi kwa Paulo kuwasihi watumwa Wakristo kuendelea kuwaheshimu mabwana zao waliowafanya watumwa? Je kwa mtumwa kutomheshimu bwana wake kunatukanishaje jina la Mungu na mafundisho ya Kikristo?
  2. Majadiliano ya watu walioharibika akili zao huwazia maswali na maneno ya mashindano ambayo huishia kwenye matusi na ugomvi na matusi. Je umeshawahi kukutana nao watu wa aina hiyo kanisani kwako. Njia ipi sahihi zaidi ya kukabiliana na watu hao?
  3. Kwa nini kupenda fedha kunaitwa shina la mabaya ya kila namna? Je fedha na mafanikio ya kiuchumi vyaweza kumfanya mtu kufarakana na imani? Je fungu hilo (6) linatuagiza tusitafute fedha au mali?

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: 2TIMOTHEO 2:1-26
IJUMAA, 12/11/2021

2 Timotheo 2 1

Basi wewe, mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu.

2 Timotheo 2 2

Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.

2 Timotheo 2 3

Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu.

2 Timotheo 2 4

Hakuna apigaye vita ajitiaye katika shughuli za dunia, ili ampendeze yeye aliyemwandika awe askari.

2 Timotheo 2 5

Hata mtu akishindana katika machezo hapewi taji, asiposhindana kwa halali.

2 Timotheo 2 6

Yampasa mkulima mwenye taabu ya kazi kuwa wa kwanza wa kupata fungu la matunda.

2 Timotheo 2 7

Yafahamu sana hayo nisemayo, kwa maana Bwana atakupa akili katika mambo yote.

2 Timotheo 2 8

Mkumbuke Yesu Kristo, aliyefufuka katika wafu, wa uzao wa Daudi kama inenavyo injili yangu.

2 Timotheo 2 9

Nami katika hiyo nimeteswa hata kufungwa kama mtenda mabaya; lakini neno la Mungu halifungwi.

2 Timotheo 2 10

Kwa ajili ya hilo nastahimili mambo yote, kwa ajili ya wateule, ili wao nao waupate wokovu ule ulio katika Kristo Yesu, pamoja na utukufu wa milele.

2 Timotheo 2 11

Ni neno la kuaminiwa. Kwa maana, Kama tukifa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia;

2 Timotheo 2 12

Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi;

2 Timotheo 2 13

Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.

2 Timotheo 2 14

Uwakumbushe mambo hayo, ukiwaonya machoni pa Mungu, wasiwe na mashindano ya maneno, ambayo hayana faida, bali huwaharibu wasikiao.

2 Timotheo 2 15

Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.

2 Timotheo 2 16

Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu,

2 Timotheo 2 17

na neno lao litaenea kama donda-ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto,

2 Timotheo 2 18

walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata kuipindua imani ya watu kadha wa kadha.

2 Timotheo 2 19

Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu.

2 Timotheo 2 20

Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina.

2 Timotheo 2 21

Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema.

2 Timotheo 2 22

Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.

2 Timotheo 2 23

Walakini uyakatae maswali ya upumbavu yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi.

2 Timotheo 2 24

Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu;

2 Timotheo 2 25

akiwaonya kwa upole wao washindanao naye, ili kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na kuijua kweli;

2 Timotheo 2 26

wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambao hao wametegwa naye, hata kuyafanya mapenzi yake.

 

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Moja ya wajibu wa kiongozi wa kiroho ni kuwakabidhi watu waaminifu walio chini yake mambo ambayo watayafundisha kwa waumini. Je katika mazingira ambayo kila mmoja anajiona anajua jambo hili linawezekana?
  2. Ikiwa Bwana awajua walio wake ni kusema pia kuwa anawajua watakaopotea? Kama Bwana anawajua watakaochagua kupotea hiyo ni kusema hao watu hawawezi kubadilisha mtazamo na kuchagua kuokolewa?
  3. Mtumishi wa Mungu ajuaye kufundisha ana uwezekano wa kiasi gani wa kupunguza magomvi kwa watu anaowaongoza?
  4. Hatua ya kwanza ya kuwasaidia wagombanao na viongozi wao wa kiroho ni kutuliza hasira yao ili wapate kurudiwa na fahamu zao na kutoka katika mtego wa Ibilisi. Je ni sahihi katika kutuliza hasira zao kuwaambia wanaongozwa na Ibilisi? Je ni muhimu wakajua kwamba wanaongozwa na Ibilisi?

 

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: 2TIMOTHEO 3:1-17
JUMAMOSI, 13/11/2021

2 Timotheo 3 1

Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.

2 Timotheo 3 2

Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,

2 Timotheo 3 3

wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,

2 Timotheo 3 4

wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;

2 Timotheo 3 5

wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.

2 Timotheo 3 6

Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi;

2 Timotheo 3 7

wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.

2 Timotheo 3 8

Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.

2 Timotheo 3 9

Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao ulivyokuwa dhahiri.

2 Timotheo 3 10

Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na uvumilivu,

2 Timotheo 3 11

na upendo, na saburi; tena na adha zangu na mateso, mambo yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Listra, kila namna ya adha niliyoistahimili, naye Bwana aliniokoa katika hayo yote.

2 Timotheo 3 12

Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.

2 Timotheo 3 13

lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.

2 Timotheo 3 14

Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao;

2 Timotheo 3 15

na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.

2 Timotheo 3 16

Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;

2 Timotheo 3 17

ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.

 

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Nyakati za hatari za siku za mwisho hazitokani na vita bali zitatokana na kukithiri kwa tabia za ubinafsi. Kwa nini unadhani tabia zina mchango mkubwa katika kuzifanya siku za mwisho kuwa za hatari?
  2. Kwa nini wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi wamekuwa wahanga wa mafundisho ya uongo yanayoahidi uponyaji wa kimwili? Inawezekanaje watu wawe wakijifunza siku zote lakini wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli?
  3. Kwa nini wanaopingana na ukweli hawataendelea sana? Kwa nini wanaitwa ni watu walioharibika akili zao na kukataliwa kwa mambo ya imani?
  4. Kwa nini wote wapendao kuishi maisha ya utawa katika Kristo wataudhiwa? Ahadi ya Mungu ya kuwa atawalinda watu wake iko wapi?
  5. Kwa nini wadanganyaji wana kawaida ya kudanganya wenzao na kujidanganya wenyewe? Je! Wanapojidanganya huwa wanajua kuwa wanajidanganya?
  6. Ili mtu wa Mungu akamilike anatakiwa atende kila tendo jema. Jambo hilo linawezekanaje kwa kuzingatia hoja ya Yeremia na Paulo? (Yeremia 13:23; Warumi 7:18)
  7. Je inatosha kufundisha, kuonya, na kuongoza watu kwa kutumia Maandiko peke yake bila kutumia Roho ya Unabii? Utajuaje kama vitabu vilivyo ndani ya Biblia vina pumzi ya Mungu?

 

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: 2TIMOTHEO 4:1-22
JUMAPILI, 14/11/2021

2 Timotheo 4 1

Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake;

2 Timotheo 4 2

lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.

2 Timotheo 4 3

Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;

2 Timotheo 4 4

nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.

2 Timotheo 4 5

Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako.

2 Timotheo 4 6

Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika.

2 Timotheo 4 7

Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;

2 Timotheo 4 8

baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.

2 Timotheo 4 9

Jitahidi kuja kwangu upesi.

2 Timotheo 4 10

Maana Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu huu wa sasa, akasafiri kwenda Thesalonike; Kreske amekwenda Galatia; Tito amekwenda Dalmatia.

2 Timotheo 4 11

Luka peke yake yupo hapa pamoja nami. Umtwae Marko, umlete pamoja nawe, maana anifaa kwa utumishi.

2 Timotheo 4 12

Lakini Tikiko nalimpeleka Efeso.

2 Timotheo 4 13

Lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa, ujapo ulilete, na vile vitabu, hasa vile vya ngozi.

2 Timotheo 4 14

Iskanda, mfua shaba, alionyesha ubaya mwingi kwangu; Bwana atamlipa sawasawa na matendo yake.

2 Timotheo 4 15

Nawe ujihadhari na huyo, kwa sababu aliyapinga sana maneno yetu.

2 Timotheo 4 16

Katika jawabu langu la kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo.

2 Timotheo 4 17

Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa katika kinywa cha simba.

2 Timotheo 4 18

Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina.

2 Timotheo 4 19

Nisalimie Priska na Akila, na wale wa nyumbani mwa Onesiforo.

2 Timotheo 4 20

Erasto alikaa Korintho. Trofimo nalimwacha huko Mileto, hawezi.

2 Timotheo 4 21

Jitahidi kuja kabla ya wakati wa baridi. Eubulo akusalimu, na Pude, na Lino, na Klaudia, na ndugu wote pia.

2 Timotheo 4 22

Bwana na awe pamoja na roho yako. Neema na iwe pamoja nanyi.

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Kuhubiri Neno ni lazima kuandamane na kukaripia, kukemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. Kwa nini uvumilivu unahitajika katika kazi hiyo? Je ni lazima kila mhubiri awe na vipengere vyote hivyo kwa viwango vinavyofanana?
  2. Unafanyaje ikiwa uliopewa kuwaongoza ni watu walioyakataa mafundisho ya uzima na wanaojiepusha wasisikie yaliyo kweli? Mtu anayechagua mtu wa kumhubiria anaonesha dalili ya kuwa mzima au bado hajapona?
  3. Dalili za kutambua kuwa umevipiga vita vilivyo vizuri na imani umeilinda ni nini? Je mtu aliyewahi kukutendea ubaya ukiwa kwenye kazi ya Mungu unatakiwa umuombee mabaya? Kwa nini Paulo alifanya hivyo?
  4. Unajifunza nini kwa Paulo ambaye hapo mwanzo alimkataa Marko lakini baada ya kusaidiwa na Barnaba akamwona anafaa kwenda naye kazini?

 

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: TITO 2:1-15

JUMANNE, 16/11/2021

Tito 2 1

Lakini wewe nena mambo yapasayo mafundisho yenye uzima;

Tito 2 2

ya kwamba wazee wawe wenye kiasi, wastahivu, wenye busara, wazima katika imani na katika upendo na katika saburi.

Tito 2 3

Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema;

Tito 2 4

ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao;

Tito 2 5

na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe.

Tito 2 6

Vivyo hivyo na vijana waume uwaonye kuwa na kiasi;

Tito 2 7

katika mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahivu,

Tito 2 8

na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.

Tito 2 9

Watumwa na wawatii bwana zao, wakiwapendeza katika mambo yote; wasiwe wenye kujibu,

Tito 2 10

wasiwe waibaji; bali wauonyeshe uaminifu mwema wote, ili wayapambe mafundisho ya Mwokozi wetu Mungu katika mambo yote.

Tito 2 11

Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;

Tito 2 12

nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;

Tito 2 13

tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;

Tito 2 14

ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.

Tito 2 15

Nena maneno hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote.

 

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Utatambuaje kama unayonena ni mambo yapasayo mafundisho ya uzima? Uangalifu katika kuongea kunawahusu viongozi wa kiroho au hata waumini wa kawaida?
  2. Miongoni mwa wajibu wa wazee wa kike ni kuwafundisha wanawake vijana na kuwatia akili wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao. Unaona jambo hilo likitendeka leo makanisani? Je kungekuwa na matokeo gani kwa ndoa changa kama hilo lingekuwa linatendeka?
  3. Neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote inatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia. Je neema yaweza kutumika kama kibali cha kutenda dhambi? Kauli kuwa "dhambi ilipozidi; neema ilikuwa nyingi zaidi" ina maana gani? (Warumi 5:20)
  4. Yesu anatambulika kama Mungu Mkuu na Mwokozi wetu. Unadhani kwa nini anaitwa Mungu Mkuu? Kwa nini kuja kwa Kristo kunatatambulika kama tumaini lenye baraka?
  5. Yesu alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kutusafisha tuwe milki yake. Akiwa anatufanyia yote hayo ikiwa ni pamoja na kutupatia juhudi ya kutenda je tuna jambo la kutilia shaka kuhusu wokovu wetu?

 

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: TITO 3:1-16

JUMATANO, 17/11/2021

Tito 3 1

Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema;

Tito 3 2

wasimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote.

Tito 3 3

Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.

Tito 3 4

Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa;

Tito 3 5

si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;

Tito 3 6

ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu;

Tito 3 7

ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.

Tito 3 8

Ni neno la kuaminiwa; na mambo hayo nataka uyanene kwa nguvu, ili wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Hayo ni mazuri, tena yana faida kwa wanadamu.

Tito 3 9

Lakini maswali ya upuzi ujiepushe nayo, na nasaba, na magomvi, na mashindano ya sheria. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana.

Tito 3 10

Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae;

Tito 3 11

ukijua ya kuwa mtu kama huyo amepotoka, tena atenda dhambi, maana amejihukumu hatia yeye mwenyewe.

Tito 3 12

Wakati nitakapomtuma Artema kwako au Tikiko, jitahidi kuja kwangu huku Nikopoli; kwa maana huku nimekusudia kukaa wakati wa baridi.

Tito 3 13

Zena, yule mwana-sheria, na Apolo, uwasafirishe kwa bidii, wasipungukiwe na cho chote.

Tito 3 14

Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema, kwa matumizi yaliyo lazima, ili wasiwe hawana matunda.

Tito 3 15

Watu wote walio pamoja nami wakusalimu. Tusalimie wale watupendao katika imani. Neema na iwe pamoja nanyi nyote.

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Mojawapo ya wajibu wa mfuasi wa Kristo ni kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka. Kama ushauri huu ungezingatiwa nafuu gani ingepatikana nyumbani, makanisani, na mahali pa kazi? Je kiongozi katili na asiyetenda haki anastahili pia kunyenyekewa?
  2. Wema na upendo wa Mwokozi wetu Mungu una uhusiano gani na wokovu wetu? Je kutafakari zaidi juu ya wema na upendo wa Mwokozi kwa wanadamu kunatusaidiaje kujiepusha na uasi na kutukamilisha kwa wokovu?
  3. Matendo ya haki yana mchango gani katika kutupatia wokovu? Je tunafanywa warithi wa uzima wa milele kutokana na juhudi zetu?
  4. Je waliomwamini Mungu wanapaswa kudumu katika matendo mema? Matendo mema baada ya kuokolewa yana umuhimu gani?
  5. Je sehemu kubwa ya maswali yaliyo kwenye majadiliano ya kidini yanahusu mada za wokovu? Kwa nini hali iko hivyo? Je maswali ya kizushi yanastahili kupewa nafasi ya kujadiliwa?

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: WAEBRANIA 8:1-13
IJUMAA, 26/11/2021

1 Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni,

2 mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu.

3 Maana kila kuhani mkuu huwekwa ili atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu naye awe na kitu cha kutoa.

4 Kama angekuwa juu ya nchi, asingekuwa kuhani; maana wako watoao sadaka kama iagizavyo sheria;

5 watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.

6 Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora.

7 Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili.

8 Maana, awalaumupo, asema Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya;

9 Halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao, Katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri. Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana.

10 Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu.

11 Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua, Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.

12 Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena.

13 Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka.

 


USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: WAEBRANIA 5:1-14  

JUMANNE, 23/11/2021

1 Maana kila kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wanadamu amewekwa kwa ajili ya wanadamu katika mambo yamhusuyo Mungu, ili atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi;

2 awezaye kuwachukulia kwa upole wao wasiojua na wenye kupotea, kwa kuwa yeye mwenyewe yu katika hali ya udhaifu;

3 na kwa sababu hiyo imempasa, kama kwa ajili ya watu, vivyo hivyo kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi.

4 Na hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni.

5 Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu, lakini yeye aliyemwambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.

6 kama asemavyo mahali pengine, Ndiwe kuhani wa milele Kwa mfano wa Melkizedeki.

7 Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;

8 na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata;

9 naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;

10 kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.

11 Ambaye tuna maneno mengi ya kunena katika habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia.

12 Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu.

13 Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga.

14 Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.

 

MASWALI YA KUJIHOJI:

  1. Moja ya majukumu ya Kuhani Mkuu ni kuwachukulia kwa upole wale wasiojua na wenye kupotea. Je unajihisi kuwa na karama hiyo? Kwa nini wasiojua na wenye kupotea wanahitaji kuchukuliwa kwa upole?
  2. Licha ya kutoa dhabihu kwa ajili ya watu makuhani walitakiwa kutoa dhabihu kwa ajili yao wao wenyewe pia. Je viongozi wa kiroho wanaojitambua kuwa ni wenye dhambi wanaohitaji neema ya Mungu wana uwezekano wa kuwa na ufanisi katika kazi zao? Je kujitambua kuwa una mapungufu kwaweza kuwa muarobaini wa kutojitukuza?
  3. Mungu Baba alimwambia Kristo kuwa "Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa." Je hiyo ni kumaanisha maisha ya Kristo yalianzia siku ile. Katika hali ya kawaida siku ya kuzaliwa Baba aweza kuongea na mwanaye?
  4. Je, mateso yanamsaidia mtu kuwa mtii? Je ilikuwa ni lazima Yesu ateswe? Yesu anakuwaje sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii?
  5. Unadhani muda unaotumika kuelezea ukuhani wa kifalme wa Yesu unatosha? Kuna siri gani katika Yesu kuwa Kuhani Mkuu kwa mfano wa Melkizedeki? Je ni kweli kuwa watu wamekuwa wavivu wa kusikia Neno la Mungu hasa mambo yahusuyo wokovu wao?
  6. Kwa nini watu wa Mungu hupenda maziwa (mafundisho laini yasiyo na tija kwa wokovu) badala ya kupenda chakula kigumu kinachohusu unabii na namna tunavyohesabiwa haki? Je utajitambuaje kuwa ni mtoto mchanga unayehitaji maziwa na wala si vyakula vigumu vinavyokusaidia kupambanua mema na mabaya.

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: WAEBRANIA 8:1-13

IJUMAA, 26/11/2021

1 Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni,

2 mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu.

3 Maana kila kuhani mkuu huwekwa ili atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu naye awe na kitu cha kutoa.

4 Kama angekuwa juu ya nchi, asingekuwa kuhani; maana wako watoao sadaka kama iagizavyo sheria;

5 watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.

6 Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora.

7 Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili.

8 Maana, awalaumupo, asema Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya;

9 Halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao, Katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri. Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana.

10 Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu.

11 Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua, Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.

12 Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena.

13 Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka.

 

MASWALI YA KUJIHOJI:

  1. Kwa nini ile hema ya mbinguni inaitwa hema ya kweli? Kama kila Kuhani Mkuu huwekwa ili atoe vipawa, Yesu alitoa vipawa gani? Kwa nini Yesu asingekuwa Kuhani kwa mujibu wa sheria kama angekuwa juu ya nchi (duniani)?
  2. Yesu ni mjumbe wa agano bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora. Hilo linaloitwa agano bora ni lipi? Linakuwa bora likilinganishwa na agano lipi? Ni ahadi gani bora zilizo kwenye agano bora ambazo hazikuwemo kwenye agano lililotangulia?
  3. Mapungufu ya Agano la kwanza yaliyosababisha kuwa naAgano la pili ni nini? Je mapungufu ya Agano la kwanza yanatokana na kuwapo kwa sheria na amri?
  4. Je sheria katika agano Jipya zinaondolewa au kurekebishwa? Kwa nini haziondolewi? Kwa nini badala ya kuandikwa kwenye mbao mbili za mawe kwenye Agano Jipya zinaandikwa mioyoni?
  5. Agano la kwanza lililo kuukuu na lililo karibu na kutoweka ni lipi? Hii inamaanisha vitabu vya agano la kale ni vikuukuu?

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: WAEBRANIA 11:1-40

JUMAPILI, 28/11/2021

1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

2 Maana kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa.

3 Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.

4 Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena.

5 Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu.

6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

7 Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Na hivyo akauhukumu makosa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.

8 Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.

9 Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.

10 Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.

11 Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu.

12 Na kwa ajili ya hayo wakazaliwa na mtu mmoja, naye alikuwa kama mfu, watu wengi kama nyota za mbinguni wingi wao, na kama mchanga ulio ufuoni, usioweza kuhesabika.

13 Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi.

14 Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe.

15 Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea.

16 Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji.

17 Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee;

18 naam, yeye aliyeambiwa, Katika Isaka uzao wako utaitwa,

19 akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano.

20 Kwa imani Isaka akawabariki Yakobo na Esau, hata katika habari ya mambo yatakayokuwa baadaye.

21 Kwa imani Yakobo, alipokuwa katika kufa, akambariki kila mmoja wa wana wa Yusufu, akaabudu akiegemea kichwa cha fimbo yake.

22 Kwa imani Yusufu, alipokuwa amekaribia mwisho wake, alitaja habari za kutoka kwao wana wa Israeli, akaagiza kwa habari ya mifupa yake.

23 Kwa imani Musa, alipozaliwa, akafichwa miezi mitatu na wazazi wake, kwa sababu waliona kwamba ni mtoto mzuri; wala hawakuiogopa amri ya mfalme.

24 Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao;

25 akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo;

26 akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo.

27 Kwa imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana.

28 Kwa imani akaifanya Pasaka, na kule kunyunyiza damu, ili yule mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao.

29 Kwa imani wakapita kati ya Bahari ya Shamu, kama katika nchi kavu; Wamisri walipojaribu kufanya vivyo wakatoswa.

30 Kwa imani kuta za Yeriko zikaanguka, zilipokwisha kuzungukwa siku saba.

31 Kwa imani Rahabu, yule kahaba, hakuangamia pamoja na hao walioasi; kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi kwa amani.

32 Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii;

33 ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba,

34 walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.

35 Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora;

36 wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani;

37 walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya;

38 (watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi.

39 Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi;

40 kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi.

 

MASWALI YA KUJIHOJI:

  1. Unapokuwa na hakika na mambo unayotarajia hiyo ndiyo imani. Je ni lazima uhakika huo uwe umetokana na Neno la Kristo? (Warumi 10:17)
  2. Vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri. Jambo hilo lina ukweli wa kiasi gani? Je vilifanywa kwa kutumia nini? Je imani ilihusika katika kuumba dunia yetu?

 

  1. Kama huna imani kuwa Mungu huwapa thawabu wale wamtafutao, je kuna upungufu wowote katika imani yako hiyo? Kung'ang'ania kuwa Mungu aweza kufanya kile ulichomwomba kwa muda mrefu bila kuona matokeo uliyotarajia ni kulazimisha mambo au ndiyo imani yenyewe? Je kule kusema mapenzi yake yatimizwe kunatoa nafasi ya kuendelea kuliombea lile ambalo halijatimizwa kama ulivyotarajia?
  2. Je kupokea uwezo wa kuwa na mimba kunahitaji imani? Inakuwaje wengine wana imani na wengine hawana? Je imani ni karama au ni kitu ambacho kila mmoja anapaswa kuwa nacho? Je kizazi cha mwisho kitakuwa na tatizo la kupungukiwa imani? (Luka 18:8)

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: WAEBRANIA 12:1-29

JUMANNE, 30/11/2021

1 Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,

2 tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.

3 Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.

4 Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi;

5 tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye;

6 Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye.

7 Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye?

8 Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali.

9 Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi?

10 Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.

11 Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.

12 Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza,

13 mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe.

14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;

15 mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.

16 Asiwepo mwasherati wala asiyemcha Mungu, kama Esau, aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula kimoja.

17 Maana mwajua ya kuwa hata alipotaka baadaye kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi.

18 Maana hamkufikilia mlima uwezao kuguswa, uliowaka moto, wala wingu jeusi, na giza, na tufani,

19 na mlio wa baragumu na sauti ya maneno; ambayo wale walioisikia walisihi wasiambiwe neno lo lote lingine;

20 maana hawakuweza kustahimili neno lile lililoamriwa, Hata mnyama akiugusa huo mlima atapigwa kwa mawe.

21 Na hayo yaliyoonekana jinsi yalivyokuwa ya kutisha, hata Musa akasema, Nimeshikwa na hofu na kutetemeka.

22 Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,

23 mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,

24 na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.

25 Angalieni msimkatae yeye anenaye. Maana ikiwa hawakuokoka wale waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya nchi, zaidi sana hatutaokoka sisi tukijiepusha na yeye atuonyaye kutoka mbinguni;

26 ambaye sauti yake iliitetemesha nchi wakati ule; lakini sasa ameahidi akisema, Mara moja tena nitatetemesha si nchi tu, bali na mbingu pia.

27 Lakini neno lile, Mara moja tena, ladhihirisha kuhamishwa vile viwezavyo kutetemeshwa, kama vitu vilivyoumbwa, vitu visivyoweza kutetemeshwa vikae.

28 Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho;

29 maana Mungu wetu ni moto ulao.

 

MASWALI YA KUJIHOJI:

  1. Kwa nini Yesu anatambulika kama mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu? Je hiyo ina maana pasipo Yesu sisi hatuwezi kuamini? Nini kilimwezesha Yesu kustahimili msalaba na kuidharau aibu?
  2. Ili tusichoke na kuzimia mioyoni mwetu tunashauriwa kufanya nini? Kwa nini kutafuta amani na watu wote kunapaswa kuwa kipaumbele chetu?
  3. Kwa nini kupungukiwa na neema ya Mungu huchipua shina la uchungu lenye kuwasumbua na kuwatia watu unajisi?
  4. Kwa nini mkutano mkuu wa kanisa litakalokusanyika mbinguni litakuwa la wazaliwa wa kwanza? Sifa ya uzaliwa wa kwanza inapatikanaje? Kazi ya wazaliwa wa kwanza itakuwa nini? (Zab 89:27), (Danieli 7:27).

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: WAEBRANIA 13:1-25

JUMATANO, 01/12/2021*

1 Upendano wa ndugu na udumu.

2 Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.

3 Wakumbukeni hao waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao; na hao wanaodhulumiwa, kwa vile ninyi nanyi mlivyo katika mwili.

4 Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.

5 Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.

6 Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?

7 Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao.

8 Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele.

9 Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo hawakupata faida.

10 Tuna madhabahu ambayo wale waihudumiao ile hema hawana ruhusa kula vitu vyake.

11 Maana wanyama wale ambao damu yao huletwa ndani ya patakatifu na kuhani mkuu kwa ajili ya dhambi, viwiliwili vyao huteketezwa nje ya kambi.

12 Kwa ajili hii Yesu naye, ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa nje ya lango.

13 Basi na tutoke tumwendee nje ya kambi, tukichukua shutumu lake.

14 Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao.

15 Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake.

16 Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.

17 Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.

18 Tuombeeni; maana tunaamini kwamba tuna dhamiri njema, tukitaka kuwa na mwenendo mwema katika mambo yote.

19 Nami nawasihi zaidi sana kufanya hayo ili nirudishwe kwenu upesi.

20 Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, yeye Bwana wetu Yesu,

21 awafanye ninyi kuwa wakamilifu katika kila tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, naye akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amina.

22 Lakini nawasihi, ndugu, mchukuliane na neno hili lenye maonyo maana nimewaandikia kwa maneno machache.

23 Jueni ya kuwa ndugu yetu Timotheo amekwisha kufunguliwa; ambaye, akija upesi, nitaonana nanyi pamoja naye.

24 Wasalimuni wote wenye kuwaongoza, na watakatifu wote; hao walio wa Italia wanawasalimu.

25 Neema na iwe nanyi nyote.

 

MASWALI YA KUJIHOJI:

  1. Namna bora ya kuwahurumia walio kwenye dhiki ni kuhisi dhiki wanazopitia. Unadhani hili ni jukumu la kila mtu au la viongozi na watu wenye karama hiyo. Je huduma ya kuwaona wafungwa inafanyika kama inavyohimizwa na Maandiko?
  2. Je heshima ya ndoa inapatikana kwa wanandoa kuwa waaminifu kwa ndoa yao? Tofauti ya wazinzi na waasherati ni nini? Hukumu ya wasioheshimu ndoa hutolewa lini? Kwa nini mzinzi anachukuliwa kuwa ni mtu asiye na akili kabisa? (Mithali 6:32-33)
  3. Je kupenda fedha ni kosa sawa na kutafuta fedha? Je, hofu kwamba siku moja Mungu ataniacha yaweza kuwa chachu ya kufanya waitafute sana fedha leo? Mhubiri alimaanisha nini aliposema "fedha huleta jawabu la mambo yote"? (Mhubiri 10:19)
  4. Kuwatii na kuwanyenyekea wanaotuongoza hata makanisani imekuwa changamoto kubwa katika kizazi hiki. Unadhani nini kinachangia hali hii?
  5. Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu hutufanya wakamilifu katika kila tendo jema akitufanya tuyatende mapenzi yake. Je ukweli huo unakusaidiaje kuwa na uhakika na wokovu wako?

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: YAKOBO 1:1-27

ALHAMISI, 02/12/2021

1 Yakobo, mtumwa wa Mungu, na wa Bwana Yesu Kristo, kwa kabila kumi na mbili waliotawanyika; salamu.

2 Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;

3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.

4 Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.

5 Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.

6 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.

7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.

8 Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.

9 Lakini ndugu asiye na cheo na afurahi kwa kuwa ametukuzwa;

10 bali tajiri kwa kuwa ameshushwa; kwa maana kama ua la majani atatoweka.

11 Maana jua huchomoza kwa hari, huyakausha majani; ua lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo naye tajiri atanyauka katika njia zake.

12 Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.

13 Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.

14 Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.

15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.

16 Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike.

17 Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka.

18 Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake.

19 Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;

20 kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu.

21 Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.

22 Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.

23 Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo.

24 Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo.

25 Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.

26 Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai.

27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.

 

MASWALI YA KUJIHOJI:

  1. Kwa nini tunashauriwa kuhesabu ni jambo la furaha tupu tunapoangukia katika majaribu mbalimbali yanayopima imani yetu? Uwezo wa kustahimili majaribu unapatikanaje?
  2. Kwa nini maombi ya mtu mwenye mashaka huwa hayajibiwi? Kama Mungu ndiye awapaye wote kwa ukarimu mbona watu wengine wanalalamika kutojibiwa maombi yao na Mungu. Je kuna watu wenye upendeleo wa kusikilizwa maombi yao kuliko wengine?
  3. Je, ni kweli kuwa Mungu hamjaribu Mwanadamu? Kwa nini kwenye sala ya Bwana tunamuomba Mungu asitutie majaribuni?
  4. Je kuwa wepesi wa kusikia na si wepesi wa kusema huweza kuzuia magomvi yanayotokea mara kwa mara katika mahusiano ya kibinadamu? Mtu anayependa kusema sana kuliko kusikia utamsaidiaje? Kwa nini mtu asiyeuzuia ulimi wake hata dini yake huonekana kuwa haifai?
  5. Je unayo ratiba ya kwenda kuwatazama yatima na wajane katika maisha yako. Kwa nini watu wasio na mazoea hayo wanahesabiwa kuwa hawana dini safi?

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: YAKOBO 2:1-26

JUMAMOSI, 04/12/2021

1 Ndugu zangu, imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa kupendelea watu.

2 Maana akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri; kisha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu;

3 nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri; na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu,

4 je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu?

5 Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?

6 Bali ninyi mmemvunjia heshima maskini. Je! Matajiri hawawaonei ninyi na kuwavuta mbele ya viti vya hukumu?

7 Hawalitukani jina lile zuri mliloitwa?

8 Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema.

9 Bali mkiwapendelea watu, mwafanya dhambi na kuhukumiwa na sheria kuwa wakosaji.

10 Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.

11 Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria.

12 Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru.

13 Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu.

14 Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa?

15 Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki,

16 na mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini?

17 Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake.

18 Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu.

19 Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.

20 Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai?

21 Je! Baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu?

22 Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale.

23 Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.

24 Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake.

25 Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine?

26 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.

 

MASWALI YA KUJIHOJI

  1. Inawezekanaje wale wanaomwamini Yesu Kristo wawe na tabia ya kupendelea watu? Kupendelea watu kunaonesha hali ya kujiamini au kutojiamini? Je kupendelea watu ni dhambi? Madhara ya kupendelea watu kwenye kanisa la Mungu ni nini?
  2. Kati ya maskini na tajiri ni nani anayempenda Mungu kwa dhati? Kwa nini watu humchagua Mungu zaidi wanapokuwa kwenye uhitaji?
  3. Kwa nini kutoshika sheria kadhaa kati ya zile 10 zilizoamriwa kunakufanya uchukuliwe kuwa hujashika zote? Je tunaokolewa kwa sheria au kwa imani? Kwa nini imani isipokuwa na matendo imekufa? Kama matendo hayatuokoi kwa nini yanapewa umuhimu?

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: YAKOBO 3:1-18

JUMAMOSI, 04/12/2021

1 Ndugu zangu, msiwe waalimu wengi, mkijua ya kuwa mtapata hukumu kubwa zaidi.

2 Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.

3 Angalieni, twatia lijamu katika vinywa vya farasi, ili wamtii, hivi twageuza mwili wao wote.

4 Tena angalieni merikebu; ingawa ni kubwa kama nini, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote anakoazimia kwenda nahodha.

5 Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.

 

6 Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum.

7 Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu.

8 Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.

9 Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.

10 Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.

11 Je! Chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu?

12 Ndugu zangu, Je! Mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Kadhalika chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na maji matamu.

13 N'nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.

14 Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli.

15 Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani.

16 Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.

17 Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.

18 Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: YAKOBO 5:1-20

JUMATATU, 06/12/2021

1 Haya basi, enyi matajiri! Lieni, mkapige yowe kwa sababu ya mashaka yenu yanayowajia.

2 Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo.

3 Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho.

4 Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi.

5 Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo.

6 Mmehukumu mwenye haki mkamwua; wala hashindani nanyi.

7 Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.

8 Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia.

9 Ndugu, msinung'unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.

10 Ndugu, watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu.

11 Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.

12 Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, wala kwa mbingu wala kwa nchi; wala kwa kiapo kinginecho chote; bali ndiyo yenu na iwe ndiyo, na siyo yenu iwe siyo, msije mkaangukia hukumu.

13 Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.

14 Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.

15 Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.

16 Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.

17 Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.

18 Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake.

19 Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli, na mtu mwingine akamrejeza;

20 jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi.

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Je unadhani matajiri wanatajirika kwa kudhulumu ujira wa wanaowafanyia kazi na kwa bei ndogo wanayotoa kwa mazao ya wakulima? Katika mfumo wa soko huru ambapo bei hupangwa kulingana na hitaji la bidhaa na huduma katika kipindi husika kuna uwezekano wa kulikwepa hilo? Ili tajiri asionekane anadhulumu watu afanye nini? (Luka 3:14). Njia bora ya kujiwekea akiba kwa matajiri ni ipi?
  2. Manabii kama Ayubu walistahimili majaribu kwa uvumilivu mwingi nao wametuachia mfano bora wa kuigwa. Inakuwaje Nabii kama Yona hakuwa na sifa kama hizo? Je subira na uvumilivu ni kigezo cha kuwatambua watakatifu wa Mungu?
  3. Eliya alionesha imani kubwa kwa kuomba hadi mvua ikanyesha. Kwa nini imani yake iliyumba alipoambiwa mwanamke Yezebeli anamtafuta ili amuue? Je imani ina tabia ya kupanda na kushuka?
  4. Kama Eliya mwenye tabia moja na sisi aliomba na mvua ikanyesha licha ya baadaye kumkimbia Yezebeli, inakuambia nini juu ya uwezekano wa maombi yako kujibiwa?
  5. Je kuomba kwa kumpaka mafuta mgonjwa ni sawa na mazoea ya sasa ya baadhi ya makanisa ya kukanyaga mafuta? Kumpaka mgonjwa mafuta kunafanyika ili asife au ili aweke sawa mambo yake na Mungu wake?

 

BIBLIA KWA MPANGO: 1 PETRO 1:1-25

JUMANNE, 12/12/2021

1 Petro, mtume wa Yesu Kristo, kwa wateule wa Utawanyiko, wakaao hali ya ugeni katika Ponto, na Galatia, na Kapadokia, na Asia, na Bithinia;

2 kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.

3 Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu;

4 tupate na urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu.

5 Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.

6 Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali;

7 ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.

8 Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu,

9 katika kuupokea mwisho wa imani yenu, yaani, wokovu wa roho zenu.

10 Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi.

11 Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo.

12 Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyachungulia.

13 Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo.

14 Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu;

15 bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;

16 kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.

17 Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.

18 Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;

19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.

20 Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu;

21 ambao kwa yeye mmekuwa wenye kumwamini Mungu, aliyemfufua katika wafu akampa utukufu; hata imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu.

22 Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo.

23 Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele.

24 Maana, Mwili wote ni kama majani, Na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka;

25 Bali Neno la Bwana hudumu hata milele. Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Baba, Mwana (Yesu Kristo), na Roho Mtakatifu wameshirikiana kwa karibu sana kuhakikisha ukombozi wa wanadamu unakamilika. Hii inakupa fundisho gani kuhusu thamani ya mwanadamu na gharama ya kumkomboa? Unazipokeaje taarifa kuwa wewe unalindwa na nguvu za Mungu hadi upokee wokovu ulio tayari kufunuliwa?
  2. Unadhani urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yako ni urithi wa namna gani? Unadhani baada ya kuupokea urithi huo kitu gani hakitakuwa tena sehemu ya maisha yako?
  3. Gharama ya wokovu wetu ina mchango gani katika kutuzuia tusiendelee kuishi maisha ya dhambi? Je kuzaliwa mara ya pili ni kwa lazima ili kuishi maisha yenye ushindi dhidi ya dhambi?

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: 1 PETRO 2:1-25

JUMATANO, 08/12/2021

1 Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.

2 Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;

3 ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili.

4 Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.

5 Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.

6 Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.

7 Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.

8 Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha, Kwa maana hujikwaza kwa neno lile, wasiliamini, nao waliwekwa kusudi wapate hayo.

9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;

10 ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.

11 Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.

12 Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.

13 Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa;

14 ikiwa ni wakubwa, kama wanaotumwa naye ili kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema.

15 Kwa sababu ndiyo mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu;

16 kama walio huru, ila wasioutumia uhuru huo kwa kusitiri ubaya, bali kama watumwa wa Mungu.

17 Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme.

18 Enyi watumishi, watiini bwana zenu kwa hofu nyingi, sio wao walio wema na wenye upole tu, bali nao walio wakali.

19 Maana huu ndio wema hasa, mtu akivumilia huzuni kwa kumkumbuka Mungu, pale ateswapo isivyo haki.

20 Kwa maana ni sifa gani kustahimili, mtendapo dhambi na kupigwa makofi? Lakini kustahimili, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema hasa mbele za Mungu.

21 Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.

22 Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake.

23 Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.

24 Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.

25 Kwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu.

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Kama Yesu alikuwa jiwe lililo hai, teule, na lenye heshima, kwa nini Wayahudi na wanadamu walimkataa? Kama wangemkubali wokovu wa wanadamu ungekuwaje?
  2. Maziwa yasiyoghoshiwa ambayo watoto wachanga wa kiroho wanashauriwa kuyatumia ni yapi?
  3. Hadhi ya watakaokombolewa inajumuisha cheo cha ukuhani na ufalme. Hii inaashiria kuwa ukuhani utaendelea mbinguni? Je ukuhani huo utawahusu wanawake pia?
  4. Je ufalme wa waliokombolewa utahusika kutawala hata viumbe wengine wasio binadamu?
  5. Yesu alizichukuaje dhambi zetu katika mwili wake? Iliwezekanaje kwa Yesu kutotenda dhambi wakati ambao yeye alikuwa na mwili unaojaribiwa kama sisi?

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: 2 PETRO 1:1-21

JUMAPILI 12/12/2021

1 Simoni Petro, mtumwa na mtume wa Yesu Kristo, kwa wale waliopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika hali ya Mungu wetu, na Mwokozi Yesu Kristo.

2 Neema na iwe kwenu na amani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu.

3 Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.

4 Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.

5 Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa,

6 na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa,

7 na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.

8 Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.

9 Maana yeye asiyekuwa na hayo ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, amesahau kule kutakaswa dhambi zake za zamani.

10 Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.

11 Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuingia katika ufalme wa milele wa Bwana wetu, Mwokozi wetu Yesu Kristo.

12 Kwa hiyo nitakuwa tayari kuwakumbusha hayo siku zote, ijapokuwa mnayajua na kuthibitishwa katika kweli mliyo nayo.

13 Nami naona ni haki, maadamu nipo mimi katika maskani hii, kuwaamsha kwa kuwakumbusha.

14 Nikijua kwamba kule kuwekea mbali maskani yangu kwaja upesi, kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyonionyesha.

15 Walakini nitajitahidi, kwamba kila wakati baada ya kufariki kwangu mpate kuyakumbuka mambo hayo.

16 Maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake.

17 Maana alipata kwa Mungu Baba heshima na utukufu, hapo alipoletewa sauti iliyotoka katika utukufu mkuu, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.

18 Na sauti hiyo sisi tuliisikia ikitoka mbinguni tulipokuwa pamoja naye katika mlima ule mtakatifu.

19 Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing'aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.

20 Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.

21 Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Tunakuwaje washirika wa tabia ya Uungu kupitia ahadi kubwa za Mungu? Ahadi hizo kubwa mno ni zipi? Ahadi hizo zinatusaidiaje kuokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.
  2. Kwa nini upendo umekuwa hatua ya mwisho katika kumjua Mungu na kuzaa matunda? Kwa nini upendo ukikosekana sifa nyingine zote za ukristo zinapoteza maana? (1Wakorintho 13:1-2).
  3. Jitihada zinazotakiwa ili kufanya uteule wetu na kuitwa kwetu imara ni zipi? Mbona mahali pengine jitihada kama hizo zinaonekana kutohitajika? (Zekaria 4:6; Waefeso 2:8-9)
  4. Yesu alipata heshima gani na utukufu alipoletewa sauti iliyotoka kwa Baba alipoambiwa huyu ni mwanangu mpendwa wangu, ninayependezwa naye? Kwani kuna heshima na utukufu ambao hakuwa nao mwanzo? Yesu aliambiwa maneno hayo akimwakilisha Mungu au akimwakilisha mwanadamu?
  5. Kwa neno la unabii halijifunui lote kwa wakati mmoja bali hatua kwa hatua hadi kufikia mchana mkamilifu? Kwa nini hata ule unabii uliofunuliwa hupokelewa kwa shida na walio wengi?(Luka 13:34).
  6. Je unabii waweza kuwa na tafsiri mbili tofauti? Je, lipo kanisa linaloaminika kuwa mstari wa mbele katika karama hiyo ya unabii kuliko mengine? Vigezo vya kulitambua kanisa hilo ni vipi?

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: 2 PETRO 3:1-18

JUMANNE, 14/12/2021

1 Wapenzi, waraka huu ndio wa pili niwaandikiao ninyi; katika zote mbili naziamsha nia zenu safi kwa kuwakumbusha,

2 mpate kuyakumbuka yale maneno yaliyonenwa zamani na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana na Mwokozi iliyoletwa na mitume wenu.

3 Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,

4 na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.

5 Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu;

6 kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.

7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.

8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.

9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.

10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.

11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,

12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?

13 Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.

14 Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake.

15 Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa;

16 vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe.

17 Basi, wapenzi mkitangulia kujua hayo, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuuacha uthibitifu wenu.

18 Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Tangu zamani za mababu zetu dunia imeendelea kubaki hali ile ile. Je huu ni ushahidi tosha kuwa yale yanayotabiriwa kuwa yataupata ulimwengu si ya kweli? Ukweli kuwa dunia ilifanyizwa kutoka ndani ya maji kunathibitishaje kuwa yaliyotabiriwa yatakuwa?
  2. Dhana kuwa dunia yote iliwahi kugharikishwa na maji inaungwaje mkono na somo la historia inakinzanaje jiografia? Je wanasayansi wanaelewa zaidi umri wa dunia kuliko wanazuoni wa Biblia? Miaka alfu moja inakuwaje sawa na siku moja?
  3. Mungu anaonekana kukawia kutimiza ahadi yake kwa kuwa hapendi mtu yeyote apotee. Ikiwa wanadamu wataendelea kuwa wagumu wa kutubu ataendelea kuwasubiri? Tunaihimiza siku ya Bwana kwa kufanya nini?
  4. Nyaraka za Paulo ni ngumu kueleweka kwa watu wenye tabia gani? Je kuyaelewa Maandiko kunahitaji elimu? Ni mambo gani muhimu kuyazingatia ili kuelewa andiko?

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: 1 YOHANA 1:1-10

JUMATANO, 15/12/2021

1 Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima;

2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);

3 hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.

4 Na haya twayaandika, ili furaha yetu itimizwe.

5 Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza lo lote hamna ndani yake.

6 Tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli;

7 bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.

8 Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.

9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.

10 Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu.

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Kwa nini kusema kwamba hatuna dhambi ni kujidanganya wenyewe? Je moyo unashiriki kwa kiasi gani katika udanganyifu huo? Neno la Mungu linatusaidiaje kujitambua kuwa tuna dhambi?

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: 1 YOHANA 2:1-29

ALHAMISI, 16/12/2021

1 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,

2 naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.

3 Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake.

4 Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake.

5 Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake.

6 Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.

7 Wapenzi, siwaandikii amri mpya, ila amri ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo. Na hiyo amri ya zamani ni neno lile mlilolisikia.

8 Tena nawaandikia amri mpya, neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu; kwa kuwa giza linapita na ile nuru ya kweli imekwisha kung'aa.

9 Yeye asemaye kwamba yumo nuruni, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa.

10 Yeye ampendaye ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo.

11 Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.

12 Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake.

13 Nawaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Nimewaandikia ninyi, watoto, kwa sababu mmemjua Baba.

14 Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.

15 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.

17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.

18 Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.

19 Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.

20 Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote.

21 Sikuwaandikia ninyi kwa sababu hamwijui iliyo kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba hapana uongo wo wote utokao katika hiyo kweli.

22 Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo, yeye amkanaye Baba na Mwana.

23 Kila amkanaye Mwana, hanaye Baba; amkiriye Mwana anaye Baba pia.

24 Ninyi basi, hilo mlilolisikia tangu mwanzo na likae ndani yenu. Ikiwa hilo mlilolisikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana, na ndani ya Baba.

25 Na hii ndiyo ahadi aliyotuahidia, yaani, uzima wa milele.

26 Nimewaandikia haya katika habari za watu wale wanaotaka kuwapoteza.

27 Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.

28 Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, ili kusudi, atakapofunuliwa, mwe na ujasiri, wala msiaibike mbele zake katika kuja kwake.

29 Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa kila atendaye haki amezaliwa na yeye.

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Kipi rahisi kati ya kutenda dhambi na kuomba msamaha? Je wanaojitanabaisha kuwa hawatendi dhambi huwa wepesi wa kukiri makosa na dhambi? Kwa nini inakuwa hivyo? Kwa nini Yesu Kristo pekee ndiye mwenye uhalali wa kutuombea?
  2. Kwa nini kushika amri ni dalili inayowatambulisha wale wanaomjua na wanaompenda Yesu? (Yoh. 14:15) Kwa nini kudai unamjua Yesu na huku huzishiki amri zake kunafaninishwa na kusema uongo?
  3. Kwa nini ni vigumu kumpenda Mungu na huku unaipenda dunia? Unaiona dalili za watu wa Mungu kuipenda dunia hasa katika siku hizi za mwisho? Nini kifanyike kuzuia hali hiyo isiendelee?

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: 1 YOHANA 3:1-24

IJUMAA, 17/12/2021

1 Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.

2 Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.

3 Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.

4 Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.

5 Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake.

6 Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua.

7 Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki;

8 atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.

9 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.

10 Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.

11 Maana, hii ndiyo habari mliyoisikia tangu mwanzo, kwamba tupendane sisi kwa sisi;

12 si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.

13 Ndugu zangu, msistaajabu, ulimwengu ukiwachukia.

14 Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. Yeye asiyependa, akaa katika mauti.

15 Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake.

16 Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu.

17 Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo?

18 Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli.

19 Katika hili tutafahamu ya kwamba tu wa kweli, nasi tutaituliza mioyo yetu mbele zake,

20 ikiwa mioyo yetu inatuhukumu; kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote.

21 Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu;

22 na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.

23 Na hii ndiyo amri yake, kwamba tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi, kama alivyotupa amri.

24 Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa.

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Kuitwa kwetu mwana wa Mungu kunaandamana na upendeleo upi ambao hapo awali hatukuwa nao? Je hadhi ya Yesu ya kuitwa Mwana wa Mungu inafanana na hadhi yetu ya kuitwa wana wa Mungu?
  2. Dhambi inatafsiriwa kama uasi au kama ilivyo katika lugha ya kiingereza "Lawlessness" ambayo kwa tafsiri rahisi ni hali ya kutokuwa na sheria. Je ni kweli kuwa dhambi haiwezi kuwepo kama hakuna sheria? (Warumi 7:7). Je Biblia inaposema hatupo chini ya sheria inamaanisha hatuwajibiki kutii sheria?
  3. "Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi." Unadhani shida ipo wapi kwa wale Wakristo wanaoendelea kutenda dhambi. Paulo alipokuwa anasema "ndani yangu halikai jambo jema" alikuwa anazungumzia uzoefu wa Mkristo au wa mtu ambaye hajamjua Kristo? (Warumi 7:18).
  4. Tunathibitisha upendo wetu kwa binadamu pale tunapoutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu. Neno "kuutoa uhai" hapo linawakilisha kitendo gani?

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Kuitwa kwetu mwana wa Mungu kunaandamana na upendeleo upi ambao hapo awali hatukuwa nao? Je hadhi ya Yesu ya kuitwa Mwana wa Mungu inafanana na hadhi yetu ya kuitwa wana wa Mungu?
  2. Dhambi inatafsiriwa kama uasi au kama ilivyo katika lugha ya kiingereza "Lawlessness" ambayo kwa tafsiri rahisi ni hali ya kutokuwa na sheria. Je ni kweli kuwa dhambi haiwezi kuwepo kama hakuna sheria? (Warumi 7:7). Je Biblia inaposema hatupo chini ya sheria inamaanisha hatuwajibiki kutii sheria?
  3. "Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi." Unadhani shida ipo wapi kwa wale Wakristo wanaoendelea kutenda dhambi. Paulo alipokuwa anasema "ndani yangu halikai jambo jema" alikuwa anazungumzia uzoefu wa Mkristo au wa mtu ambaye hajamjua Kristo? (Warumi 7:18).
  4. Tunathibitisha upendo wetu kwa binadamu pale tunapoutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu. Neno "kuutoa uhai" hapo linawakilisha kitendo gani?

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: 1YOHANA 5:1-21

JUMAPILI, 19/12/2021

1 Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye.

2 Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake.

3 Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.

4 Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.

5 Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?

6 Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu. Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli.

7 Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.

8 Kisha wako watatu washuhudiao duniani], Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja.

9 Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe.

10 Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe.

11 Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe.

12 Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.

13 Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu.

14 Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.

15 Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.

16 Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo.

17 Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.

18 Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi.

19 Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu.

20 Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.

21 Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu.

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Kwa mujibu wa 1Yohana 5:3, kumpenda Mungu ni lazima kuandamane na kuzishika amri zake. Amri hizo tunazoagizwa kuzishika ni zipi.
  2. Warumi 8:7 inakuambia ile nia ya mwili haiitii sheria ya Mungu wala haiwezi kuitii. Nini kimefanya sheria (amri) katika 1Yohana 5:3 iwe si nzito? Je wanaofundisha na kujizoeza kutii amri za Mungu ni adui wa Mungu? (Mathayo 5:19).
  3. Kwa mujibu wa 1Yohana 5:12 ni kuwa yeye amwaminiye Mwana yaani Yesu anao uzima wa milele. Je wale wasiomwamini Yesu hawawezi kuwa na uzima wa milele. Kama Yesu ametajwa kwenye Kuraani mara nyingi kuliko mtume Mohamadi (SAW) hiyo inaashiria Mungu alitaka Waislamu wamuamini Yesu ili waokolewe?
  4. Utajuaje kuwa unachoomba kipo kulingana na mapenzi ya Mungu? Je kuna wakati unaomba jambo na huamini kuwa utalipata? Utafanyaje kubadilisha hali hiyo?

 

USOMAJI WA BIBLIA KWA MPANGO

JUMATATU, 20/12/2021, 2 YOHANA 1:1-13

1 Mzee, kwa mama mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na wote waijuao ile kweli;

2 kwa ajili ya hiyo kweli ikaayo ndani yetu, nayo itakuwa pamoja nasi hata milele.

3 Neema, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo Mwana wa Baba, zitakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.

4 Nalifurahi mno kwa kuwa nimewaona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyopokea amri kwa Baba.

5 Na sasa mama, nakuomba, si kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo, kwamba tupendane.

6 Na huu ndio upendo: tuenende kwa kuzifuata amri zake. Hii ndiyo ile amri, kama mlivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo.

7 Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na mpinga Kristo.

8 Jiangalieni nafsi zenu msiyapoteze mliyoyatenda, bali mpokee thawabu timilifu.

9 Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba na Mwana pia.

10 Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu.

11 Maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu.

12 Kwa kuwa ninayo mambo mengi, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini nataraji kuja kwenu, na kusema nanyi uso kwa uso, ili furaha yetu iwe imetimizwa.

13 Watoto wa ndugu yako aliye mteule, wakusalimu.

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: 3 YOHANA 1:1-15

JUMANNE, 21/12/2021

1 Mzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli.

2 Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.

3 Maana nalifurahi mno walipokuja ndugu na kuishuhudia kweli yako, kama uendavyo katika kweli.

4 Sina furaha iliyo kuu kuliko hii, kusikia ya kwamba watoto wangu wanakwenda katika kweli.

5 Mpenzi, kazi ile ni ya uaminifu uwatendeayo hao ndugu na hao wageni nao,

6 waliokushuhudia upendo wako mbele ya kanisa; utafanya vizuri ukiwasafirisha kama ipasavyo kwa Mungu.

7 Kwa maana, kwa ajili ya Jina hilo, walitoka, wasipokee kitu kwa Mataifa.

8 Basi imetupasa sisi kuwakaribisha watu kama hao, ili tuwe watenda kazi pamoja na kweli.

9 Naliliandikia kanisa neno, lakini Diotrefe, apendaye kuwa wa kwanza kati yao, hatukubali.

10 Kwa hiyo, nikija, nitayakumbuka matendo yake atendayo, atoavyo upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, ila yeye mwenyewe hawakaribishi hao ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa.

11 Mpenzi, usiuige ubaya, bali uige wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu, bali yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu.

12 Demetrio ameshuhudiwa na watu wote, tena na ile kweli yenyewe. Nasi pia twashuhudia, nawe wajua ya kwamba ushuhuda wetu ni kweli.

13 Nalikuwa na mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kukuandikia kwa wino na kalamu.

14 Lakini nataraji kukuona karibu, nasi tutasema uso kwa uso.

15 Amani kwako. Rafiki zetu wakusalimu. Wasalimu hao rafiki zetu, kila mtu kwa jina lake.

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Je wakati unaposhindwa kufikia malengo ya maendeleo uliyojiwekea huwa unafahamu kuwa Mungu wako anataka ufanikiwe katika mambo yote? (1Wakorintho 9:8). Je una mpango gani kwa yale yaliyoshindwa kufanikiwa mwaka huu? Je wewe mwenyewe unadhani ulichangia kufanya yasifanikiwe?
  2. Je, watu wapendao kuwa wa kwanza wakitamani kuchaguliwa kwenye nafasi kubwa kubwa wamekuwa chanzo cha machafuko yanayotokea makanisani leo? Je watu hao huwa na ugomvi wa mara kwa mara na wachungaji? Nini kinatakiwa kufanyika juu yao ili kuepuka machafuko?
  3. Kati ya wema na ubaya ni kipi kilicho rahisi kuiga? Kwa nini tunashauriwa kuiga wema? Je wema unalipa?


USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: YUDA 1:1-25

JUMATANO, 22/12/2021

1 Yuda, mtumwa wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, kwa hao walioitwa, waliopendwa katika Mungu Baba, na kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo.

2 Mwongezewe rehema na amani na upendano.

3 Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu.

4 Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.

5 Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, aliwaangamiza baadaye wale wasioamini.

6 Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.

7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.

8 Kadhalika na hawa, katika kuota kwao, huutia mwili uchafu, hukataa kutawaliwa, na kuyatukana matukufu.

9 Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee.

10 Lakini watu hawa huyatukana mambo wasiyoyajua, na mambo wayatambuayo kwa asili wajiharibu kwayo kama wanyama wasio na akili.

11 Ole wao! Kwa sababu walikwenda katika njia ya Kaini, na kulifuata kosa la Balaamu pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wameangamia katika maasi ya Kora.

12 Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa mara mbili, na kung'olewa kabisa;

13 ni mawimbi ya bahari yasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; ni nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba yao waliowekewa milele.

14 Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu,

15 ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake.

16 Watu hawa ni wenye kunung'unika, wenye kulalamika, waendao kwa tamaa zao, na vinywa vyao vyanena maneno makuu mno ya kiburi, wakipendelea watu wenye cheo kwa ajili ya faida.

17 Bali ninyi, wapenzi, yakumbukeni maneno yaliyonenwa zamani na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo,

18 ya kwamba waliwaambia ya kuwa, Wakati wa mwisho watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe za upotevu.

19 Watu hao ndio waletao matengano, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho.

20 Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu,

21 jilindeni katika upendo wa Mungu, huku mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hata mpate uzima wa milele.

22 Wahurumieni wengine walio na shaka,

23 na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili.

24 Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu;

25 Yeye aliye Mungu pekee, Mwokozi wetu kwa Yesu Kristo Bwana wetu; utukufu una yeye, na ukuu, na uwezo, na nguvu, tangu milele, na sasa, na hata milele. Amina.

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Kama wokovu umetolewa kwa watu wote kwa nini kuna watu watakosa kuokolewa siku ya mwisho?
  2. Imani inashindaniwaje? Je Paulo aliyetaka kilishindania kania kwa nini hakufanikiwa? Watakatifu waliyokabidhiwa imani wanaotajwa katika Yuda 1:3 ni nani?
  3. Je ni rahisi kuwatambua watu waliojiingiza kwa siri kaniani? Kwa kawaida watu hao hulionea huruma kanisa? Je watu hao wana uwezekano wa kupata wafuasi kanisani?
  4. Unadhani Shetani na maika zake walikuwa na sababu ya maana kutoridhika na nafasi waliyopewa?
  5. Tabia ya kuridhika unapohisi umeonewa ni ya Mungu au ya kishetani au inatokana na uzembe? Utafanyaje ili kuishinda roho ya ulalamishi? Kwa nini Yesu hakushindana na Ibilisi badala yake alimwambia Bwana akukemee?

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: UFUNUO 1:1-20

ALHAMISI, 23/12/2021

1 Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana;

2 aliyelishuhudia Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Kristo, yaani, mambo yote aliyoyaona.

3 Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu.

4 Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja; na zitokazo kwa roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi;

5 tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake,

6 na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele. Amina.

7 Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.

8 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.

9 Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu.

10 Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,

11 ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.

12 Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu;

13 na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.

14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto;

15 na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.

16 Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake.

17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,

18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.

19 Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo.

20 Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Zinaahidiwa baraka kwa wale wasomao na kusikia unabii wa kitabu cha Ufunuo. Je unadhani kitabu cha Ufunuo ni miongoni mwa vitabu vilivyo rahisi kuvielewa? Kwa nini lugha yake imekuwa ya mafumbo zaidi?
  2. Kwa nini ujumbe wa Ufunuo unaelekezwa kwa makanisa saba? Je hayo makanisa saba yangalipo hadi sasa? Kwa nini ujumbe huo unaelekezwa zaidi kwa malaika wa makanisa hayo kuliko kwa waumini wake?
  3. Je Mungu anakusudia kutufanya ufalme na makuhani hapa duniani au kule mbinguni? Ukuhani huo utawahusu wanawake pia?
  4. Je Kristo atakaporudi duniani ni nani watakaojaliwa kumuona? Je wenye dhambi na waliokufa watapata upendeleo huo? Wazo kwamba Kristo atakuja kulinyakua kanisa lake kisirisiri lina uthibitisho wowote wa Maandiko?
  5. Siku ya Bwana ambayo Yohana alipokea maono katika kisiwa cha Patmo ni Jumamosi au Jumapili? Mtu aliye mfano wa mwanadamu ambaye Yohana alimuona kwenye maono ni nani? Kutokana na maelezo yaliyotolewa Mtu huyo alikuwa kwenye chumba gani cha hekalu la mbinguni?
  6. Kwa sasa Yesu anafanya kazi gani mbinguni? Nyota saba ambazo Yesu alizishikilia mkononi mwake na ule upanga mkali uliotoka kinywani mwake vinawakilisha nini?

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: UFUNUO 2:1-29

IJUMAA, 24/12/2021

1 Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu.

2 Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo;

3 tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka.

4 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza.

5 Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.

6 Lakini unalo neno hili, kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo na mimi nayachukia.

7 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.

8 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai.

9 Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani.

10 Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.

11 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.

12 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili.

13 Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.

14 Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.

15 Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile.

16 Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu.

17 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.

18 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana.

19 Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.

20 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.

21 Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake.

22 Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake;

23 nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.

24 Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wo wote wasio na mafundisho hayo, wasiozijua fumbo za Shetani, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine.

25 Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapokuja.

26 Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,

27 naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu.

28 Nami nitampa ile nyota ya asubuhi.

29 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Kama Mungu anajua mazuri na mabaya yako yote je kuna haja ya kumficha chochote unapomuungamia dhambi? Je ungekuwa na mtu unayejua mabaya yake yote anayokuwazia na kukutendea ungekuwa tayari kuendelea kumfanya rafiki? Kwa nini Mungu anaweza hilo?
  2. Mungu huku akijua una uvumilivu wa kutosha na unasimamia ukweli kikamilifu, anaweza kukuacha ukiteseka sambamba na wenye dhambi wasiomcha. Je unapata faraja kujua kuwa anatambua na kuthamini msimamo wako. Kwa nini haonekani kuingilia kati mara moja kwenye shida zako?
  3. Kwa nini kwa kawaida upendo wa siku za kwanza za wapendanao huwa juu zaidi kuliko wa siku zinazofuatia? Ili wanandoa muendelee kupendana kama wakati wa uchumba panatakiwa kufanyika nini? Je upendo wa kanisa la awali utarejea tena katika kanisa la Kikristo?
  4. Kanisa la Efeso na Kanisa la Smirna yalitokea katika kipindi gani cha historia ya kanisa? Kipindi cha dhiki ya siku kumi kilitokea katika kipindi gani na ni nani alikisababisha? Kwa nini watu wa Mungu huteswa?
  5. Kwa nini kanisa la Pergamo linatambulishwa kama likaalo penye kiti cha enzi cha Shetani? Shetani alihusikaje katika kulitesa na kuliteka kanisa la Mungu katika vipindi vyake saba?
  6. Mafundisho ya Baalamu ni nini? Yana tofauti gani na mafundisho ya Wanikolai? Je ni mafundisho gani leo yanawakosesha watu wa Mungu kama Balaamu alivyotaka kuwakosesha na kuwaletea laana Waisraeli?
  7. Kwa nini na kwa vipi matendo ya mwisho ya Thiatira yalizidi yale ya kwanza? Ni nani huyu Yezebeli aliyewafundisha watumishi wa kanisa la Thiatira uongo na kuwapoteza?
  8. Yesu ameahidi kuwapa washindi wa imani, matunda ya mti wa uzima, mana, kutokufa tena, na mamlaka juu ya mataifa. Ni zawadi ipi inayokuvutia katika hizo? Kwa nini Yesu anatoa makemeo katika ujumbe wake kwa makanisa? Hiyo inaonesha jinsi anavyoyachukia makanisa hayo au jinsi anavyoyapenda? Unapenda kipi kati ya kusifiwa na kuonywa?



USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: UFUNUO 3:1-22

JUMAMOSI, 25/12/2021

1 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.

2 Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.

3 Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako.

4 Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.

5 Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake.

6 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

7 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.

8 Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.

9 Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.

10 Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.

11 Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.

12 Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.

13 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

14 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.

15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.

22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Sifa ya watu wenye jina la kuwa hai lakini wamekufa ni nini? Unayajua mambo yaliyosalia yanayotaka kufa maishani mwako?
  2. Kundi la watu wanaolinganishwa na watu wasioyatia unajisi mavazi yao katika Sardi ni kundi la watu gani?
  3. Huyu anayetambukishwa kama Shahidi Mwaminifu ni nani? Kwa nini anatambulishwa pia kama mwanzo mwa kuumba kwa Mungu?
  4. Kwa nini hali ya kanisa la Laodikia inalinganishwa na uvuguvugu? Kwa nini hali ya joto au baridi vinapendekezwa kuwa bora zaidi kuliko uvuguvugu?
  5. Kwa nini Laodikia anajiona ni tajiri aliyejitajirisha asiye na haja ya kitu chochote? Kwa nini hali hiyo inamtia Yesu kichefuchefu kinachomfanya atamani kutapika?
  6. Je Laodikia anayejiona amejitosheleza anaweza kupokea ushauri wa kununua dhahabu iliyosafishswa, mavazi meupe, na dawa ya macho? Dhahabu, mavazi, na dawa za macho ni nini?
  7. Je baada ya kanisa la Laodikia Yesu ana mpango wa kuanzisha kanisa lingine? Wale watakaoshinda watapewa kuketi kwenye kiti cha enzi cha Yesu kwa muda gani? Je wanadamu wakati huo watakuwa raia au watawala wa mbinguni?

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: UFUNUO 4:1-11

JUMAPILI: 26/12/2021

1 Baada ya hayo naliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo.

2 Na mara nalikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu ya kile kiti

3 na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la yaspi na akiki, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi.

4 Na viti ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wanne, wameketi, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu.

5 Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti na ngurumo. Na taa saba za moto zilikiwaka mbele ya kile kiti cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu.

6 Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma.

7 Na huyo mwenye uhai wa kwanza alikuwa mfano wa simba; na mwenye uhai wa pili alikuwa mfano wa ndama; na mwenye uhai wa tatu alikuwa na uso kama uso wa mwanadamu; na mwenye uhai wa nne alikuwa mfano wa tai arukaye.

8 Na hawa wenye uhai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; na pande zote na ndani wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja.

9 Na hao wenye uhai wanapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi utukufu, na heshima, na shukrani, yeye aliye hai hata milele na milele,

10 ndipo hao wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, nao humsujudia yeye aliye hai hata milele na milele, nao huzitupa taji zao mbele ya kile kiti cha enzi, wakisema,

11 Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: UFUNUO 5:1-14

JUMATATU, 27/12/2021

1 Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba.

2 Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N'nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja muhuri zake?

3 Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.

4 Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.

5 Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.

6 Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.

7 Akaja, akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi.

8 Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.

9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,

10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.

11 Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,

12 wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.

13 Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele.

14 Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka, wakasujudu.

 

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma na kilichotiwa muhuri saba ni nini? Kwa nini hapakuwa na mtu aliyeweza kukifungua hicho kitabu wala kukitazama? Kwa nini kushindwa kupatikana kwa mtu huyo kulisababisha kilio kwa Yohana?
  2. Kwa nini Yesu anaitwa Simba wa kabila la Yuda? Yesu ana vigezo gani vya kukifungua hicho kitabu? Je Yesu anastahili kuabudiwa? Viumbe vilivyopo chini ya nchi vinavyomtukuza Kristo kwa sifa ni vipi?
  3. Je Yesu alikuwa anaabudiwa na kupokea sifa hizi kutoka kwa viumbe wote kabla hajakamilisha mpango wa wokovu wa wanadamu? Kwa nini ni kosa kwa mwanadamu kutaka kuabudiwa?

 

 

 

 

 

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: UFUNUO 6:1-17

JUMANNE, 28/12/2021

1 Kisha nikaona napo Mwana-Kondoo alipofungua moja ya zile muhuri saba, nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema, kama kwa sauti ya ngurumo, Njoo!

2 Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate kushinda.

3 Na alipoifungua muhuri ya pili, nikamsikia yule mwenye uhai wa pili akisema, Njoo!

4 Akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.

5 Na alipoifungua muhuri ya tatu, nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake.

6 Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, Kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia, wala usiyadhuru mafuta wala divai.

7 Na alipoifungua muhuri ya nne, nikasikia sauti ya yule mwenye uhai wa nne akisema, Njoo!

8 Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi.

9 Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.

10 Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?

11 Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao.

12 Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,

13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.

14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.

15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,

16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.

17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?

MASWALI YA KUJADILI:

  1. Kwa nini kila muhuri ulipofunguliwa na kila mwenye uhai aliposema Njoo! Farasi wa rangi fulani alitoka kwa ajili ya mapambano? Kila farasi anawakilisha kipindi fulani cha kanisa katika historia. Unaweza kuelezea rangi za farasi zinavohusiana na vipindi wanavyoviwakilisha?
  2. Kufunguliwa kwa muhuri wa sita kunaandamana na kuondolewa na kukunjwa kwa mbingu kama ukurasa. Je tukio hili limetokea au lipo mbele yetu?
  3. Hasira ya Mwanakondoo inayofanya majemedari wa vita waone ni heri kuangukiwa na milima ni ya namna gani hiyo?
  4. Kipi ni salama zaidi kuanguka juu ya Mwamba ambaye ni Kristo au kuangukiwa na miamba siku ya mwisho?

 

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: UFUNUO 8:1-13

ALHAMISI, 30/12/2021

1 Hata alipoifungua muhuri ya saba, kukawa kimya mbinguni kama muda wa nusu saa.

2 Nami nikawaona wale malaika saba wasimamao mbele za Mungu, nao wakapewa baragumu saba.

3 Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi.

4 Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika.

5 Na huyo malaika akakitwaa kile chetezo, akakijaza moto wa madhabahu, akautupa juu ya nchi, kukawa radi na sauti na umeme na tetemeko la nchi.

6 Na wale malaika saba wenye baragumu saba wakajifanya tayari ili wazipige.

7 Malaika wa kwanza akapiga baragumu, kukawa mvua ya mawe na moto vilivyotangamana na damu, vikatupwa juu ya nchi; theluthi ya nchi ikateketea, na theluthi ya miti ikateketea, na majani mabichi yote yakateketea.

8 Malaika wa pili akapiga baragumu, na kitu, mfano wa mlima mkubwa uwakao moto, kikatupwa katika bahari; theluthi ya bahari ikawa damu.

9 Wakafa theluthi ya viumbe vilivyomo baharini, vyenye uhai; theluthi ya merikebu zikaharibiwa.

10 Malaika wa tatu akapiga baragumu, nyota kubwa ikaanguka kutoka mbinguni, iliyokuwa ikiwaka kama taa, ikaanguka juu ya theluthi ya mito, na juu ya chemchemi za maji.

11 Na jina lake ile nyota yaitwa Pakanga; theluthi ya maji ikawa pakanga, na wanadamu wengi wakafa kwa maji hayo, kwa kuwa yalitiwa uchungu.

12 Malaika wa nne akapiga baragumu, theluthi ya jua ikapigwa, na theluthi ya mwezi, na theluthi ya nyota, ili kwamba ile theluthi itiwe giza, mchana usiangaze theluthi yake, wala usiku vivyo hivyo.

13 Kisha nikaona, nikasikia tai mmoja akiruka katikati ya mbingu, akisema kwa sauti kuu, Ole, ole, ole wao wakaao juu ya nchi! Kwa sababu ya sauti zisaliazo za baragumu za malaika watatu, walio tayari kupiga.