Seventh-day Adventist® Church

PASTOR LETTA'S OFFICIAL WEBSITE

Menu

KWAHERI TWAKANIKI

Tarehe 26/08/2020 itakumbukwa kama siku ya huzuni katika kanisa la Mivumoni mtaa wa Wazo jijini Dar es Salaam, wakati ibada ya faraja kwa ajili ya marehemu Michael Zechariah Twakaniki ilipofanyika. Ibada hiyo iliendeshwa na Mchungaji Mark Malekana - Kiongozi mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato  Jimbo la Kusini mwa Tanzania pamoja na viongozi wenzake waandamizi wa majimbo.

Mchungaji Twakaniki aliyezaliwa 05/01/1958 Kibigwa wilayani Kasulu alikuwa mchungaji wa Kanisa la Waadventista wa Sabato aliyehudumu katika mitaa ya Mlela/Nkungwe, Nguruka, Kasulu West, Kiomboi Singida, Biharamulo, Kinondoni, Ubungo, Dodoma, na Wazo. Mchungaji pia aliwahi kuwa Chaplain na mwalimu wa shule ya Parane, na mkurugenzi wa Idara ya Huduma Binafsi, na maeneo mapya ya lililokuwa jimbo la Mashariki mwa Tanzania. Mchungaji Michael Twakaniki alipata shinikizo la juu la damu lililopelekea kifo chake kwenye hospitali ya Rabininsia Tegeta jijini Dar es Salaam asubuhi ya tarehe 21/08/2020 na kuzikwa kwenye makaburi ya eneo la Mivumoni jijini Dar es Salaam 26/08/2020. 


Marehemu ameacha mjane na watoto watano ambao ni Rehema, Happy, Ellen, Loveness na Amantulia na wajukuu 7. Tutamkumbuka marehemu kwa ucheshi na tabasamu lake la bashasha na uwezo wake wa kushawishi katika yale yanayodhaniwa kwamba hayawezekani na moyo wake wa kiuinjilisti.  ". . . Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe." (Ayubu 1:21)