Seventh-day Adventist® Church

PASTOR LETTA'S OFFICIAL WEBSITE

Menu

MSAFIRI YOHANA MAKANTA

Makanta, Msafiri Yohana (1930–2018)

Msafiri Yohana Makanta alikuwa mchungaji wa Kiadventista, mwalimu, mlezi, na mwandishi wa Tanzania.

Maisha ya Awali

Msafiri Yohana Makanta alizaliwa na kukulia katika kijiji cha Malindi wilayani Lushoto katika mkoa wa Tanga nchini Tanzania mnamo Februari 1, 1930, ambapo baba yake alikuwa mchungaji. Alikuwa wa tatu kuzaliwa kati ya watoto wanne. Mama yake alikuwa Nakijwa Makinya. Makanta alibatizwa mwaka wa 1950 katika kanisa la Waadventista Wasabato Miamba.

Elimu na Ndoa (1944-1951)

Makanta alihudhuria Shule ya Msingi ya Suji. Alipata cheti cha darasa la nane. Kuanzia 1952 hadi 1953, alijiunga na chuo cha ualimu cha Ikizu (Mara). Makanta alijiunga na Chuo cha Bugema nchini Uganda ambako alisomea Diploma ya uchungaji mwaka 1956 na 1957. Mwaka 1966, alihitimu Diploma ya elimu ya afya kutoka Chuo Kikuu cha Loma Linda cha Afya ya Umma katika Hospitali ya Heri. Mnamo 1971, alipata cheti katika masomo ya kilimo, pia kutoka Chuo Kikuu cha Loma Linda. Julai 7, 1954 alifunga ndoa na Sifael Paul Mweta katika kanisa la Waadventista wa Sabato Mamba Miamba wilayani Same mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania. Makanta na mkewe walikuwa na watoto watano, John (Makanta), Upendo, Stephen, Julius, na Joyce.

Uchungaji

Kuanzia 1954 hadi 1955, Makanta alifanya kazi ya ualimu katika Shule ya Msingi ya Chome. Alikuwa mwalimu na kiongozi wa wilaya katika Kituo cha Misheni cha Mbeya kuanzia mwaka 1958 hadi 1963. Mwaka 1964, alipewa utume alipokuwa mkuu wa wilaya ya Tabora. Kuanzia mwaka 1964 hadi 1965, aliwahi kuwa mchungaji katika wilaya ya Tabora. Alihamishiwa wilaya ya Magomeni, Dar es Salaam kuanzia mwaka 1967 hadi 1969. Kuanzia mwaka 1969 hadi 1970, alikuwa Chaplain wa Shule ya Sekondari ya Heri na Hospitali ya Heri ya Kigoma. Mwaka 1971, Makanta aliwahi kuwa kiongozi wa mtaa wa Kigoma. Aliteuliwa kuwa mkuu wa idara ya uwakili na huduma binafsi kwenye General Field ya Tanzania huko Morogoro mwaka 1972, jukumu ambalo alilibeba hadi 1976. Mnamo 1977, alikua mkurugenzi wa maendeleo ya kanisa, uwakili na walei kwenye Fildi ya Kaskazini Mashariki mwa Tanzania. Mwaka wa 1984, aliteuliwa kuwa mkuu wa idara ya Shule ya Sabato katika Union ya Tanzania hadi 1989. Mwaka uliofuata, aliteuliwa kuhudumu kama Mwenyekiti wa kwanza wa Fildi ya Magharibi mwa Tanzania huko Kigoma, jukumu alilolitekeleza hadi 1996 alipoteuliwa kuwa mwenyekiti mstaafu.

Baada ya Makanta kustaafu, alirudi nyumbani kwake Miamba na kuendelea kuongoza katika huduma mbalimbali za kanisa kwenye mtaa. Wakati wa uhai wake, aliandika vitabu na machapisho kadhaa kama vile KIOO, LIHUBIRI NENO, n.k. Alifariki Juni 15, 2018, katika Kituo cha Afya cha Bwambo, wilayani Same mkoani Kilimanjaro, Tanzania.

Mchango

Makanta alitoa mchango mkubwa katika elimu ya Kanisa la Waadventista Wasabato, huduma, na uongozi kwa miaka arobaini na miwili. Machapisho yake bado yanachangia katika malezi na uendeshaji wa kanisa. Wakati wa miaka yake ya kustaafu, alikuwa mkulima wa mfano na mshauri kwa wakulima wengi katika kijiji chake.