Seventh-day Adventist® Church

PASTOR LETTA'S OFFICIAL WEBSITE

Menu

YEREMIA

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 1:1-19

 1. Kama Mungu anatujua kabla hatujazaliwa na ametupangia hata kazi tutakazofanya kuna uwezekano wa sisi wenyewe kubadilisha mpango huo? Je kwa maana hiyo kuna waliopangiwa kuwa vibaka au wasio na mafanikio? Je unaweza kutambua kitu alichokupangia Mungu maishani mwako? Kwa nini Mungu ampangie mtu atakavyokuwa badala ya kumuacha ajipangie mwenyewe?
 2. Je Mungu akikuchagua kufanya kazi yake unaruhusiwa kukataa? Je kuna sababu ya kukataa kazi ya Mungu utaayoitoa kwake na akaridhika nayo? Kukataa kazi ya Mungu kutokana na ukubwa wake ni kuonyesha unyenyekevu au kiburi kwa Mungu? Kwa nini kwenye kufanya kazi ya Mungu haitakiwi kutanguliza woga? Je watoto wadogo wanaweza kuifanya kazi ya Mungu kwa usahihi kama watu wazima?
 3. Je kuna wakati ambao ni vigumu kusema kila neno uliloamriwa na Mungu? Nini husababisha ujumbe wa Mungu kutopelekwa kwa namna aliyoamuru? Mungu anatiaje maneno yake kwenye kinywa cha mtu?Kwa nini Mungu anamwagiza Yeremia mtumishi wake kung'oa, kubomoa, kuharibu, kuangamiza, ili kujenga na kupanda? (Mathayo 15:13).
 4. Kwa nini kuziabudu kazi za mikono yetu (tulizofanya kwa juhudi zetu bila kutumia uwezo wake) ni machukizo kwa Mungu? Je kwa nini Mungu humwadhibu anayekataa kufanya kazi yake? Kwa nini wanaopigana na watumishi wa Mungu huwa hawafanikiwi?

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 5:1-31

 1. Kwa nini kuusamehe Yerusalemu kulihitaji upatikanaji wa mtu mmoja atendaye haki? Je katika kuiokoa dunia palihitajika mtu huyo mmoja mwenye haki? (Mathayo 27:24). Kwa nini Mungu anachukizwa mno na uovu unaotendwa na wale anaowaita watu wake? Kwa nini katika kuupatiliza Yerusalemu kwa maovu yake anaagiza wasiuharibu kabisa bali wayaondoe tu matawi yake?
 2. Kama Mungu hakuwa na kusudi la kulikomesha kabisa taifa la Israeli kwa nini aliruhusu washambuliwe na maadui? Kama Mungu ndiye aliyeweka mpaka wa bahari ili maji yake yasivuke ilikuwaje kwenye Sunami maji ya bahari yalivuka mipaka yake na kuleta madhara kwa wanadamu?
 3. Kama wajinga ni watu wasio na ufahamu je wapunbavu ni watu wa namna gani? Nani mwenye unafuu kati ya mjinga na mpumbavu? Unadhani Mungu anapewa heshima anayostahili kulingana na namna anavyowahudumia wanadamu? Manabii wanaotabiri wana mchango gani katika kuendeleza uovu unaoendelea na maafa yatokeayo?

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 8:1-22

 1. Kwa nini wanadamu wanapenda jua, na mwezi nakuvitumikia na kuviabudu? Hicho kinachoitwa jeshi lote la mbinguni kinachotumikiwa na kuabudiwa ni nini? Kwa nini Mungu anaruhusu mifupa ya wakuu, makuhani, na maabii ifukuliwe na kuwa samadi juu ya uso wa nchi? Mungu anapinaje kama yaliyosemwa si sawa? Kwa nini jambo hilo linamkasirisha sana? Kwa nini watu waliolikataa neno lake wanaonekana kutokuwa na akili ndani yao?
 2. Je kitendo cha Mungu kuruhusu wake za waasi wachukuliwe na watu wengine kilikuwa kina kusudi la kuwaumiza waasi au kuchochea uzinzi? Wajibu wa wakuu (watawala), manabii, na makuhani katika Agano la Kale ulikuwa ni nini? Leo hii wajibu huo unafanywa na nani? Kuiponya jeraha za binti za watu wa Mungu ni kufanyaje? Jeraha inawakilisha nini? Kuna ubaya gani kuwaambia watu kuna amani wakati hakuna amani? Mtu anayefanya hivyo anatafuta kufurahisha watu, kujipendekeza, au kuwapoteza watu?
 3. Mungu anasema atatuma nyoka wasioweza kutumbuizwa kwa uganga, je kuna uwezekano wa nyoka kutumbuizwa (kupunguzwa makalu) kwa uganga? Mungu mwenye upendo anawezaje kufanya kitendo cha ukatili kama hiki? Sanamu za kuchonga zinamkasirishaje Mungu kiasi hicho? Je wenye kuabudu sanamu wanajua ubaya wa kuabudu sanamu? Je watakaokosa kuokolewa siku ya mwisho watalaumu kwa kutookolewa kwao? Watatamani maonyo waliyoyapuuza yarudiwe tena?

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 9:1-26

 1. Mungu anatamani kuwaacha watu wake waliozama kwenye uovu lakini pia anatamani kuwalilia kwa maafa ya kujitakia watakayoyapata. Unadhani kipikitakuwa rahisi kwa Mungu kukifanya kwa watu wake? Ikiwa anawapenda kwa nini asiwaepushie mabaya yasiwapate? Kwa nini uongo hutumika sana na wale wanaomwasi Mungu? 
 2. Je uwongo unaweza kuwapoteza watu wema? Uongo umechukua nafasi gani katika uasi na uovu ambao Shetani ameuleta duniani? (Mwanzo 3:4; Ufunuo 12:9; Yohana 8:44; Ufunuo 13:14). Mungu anapata faida gani Yerusalemu au dunia hii ikiangamizwa kutokana na uovu wa wanadamu? Katika mazingira haya Shetani ana uwezo wa kufanikisha udanganyifu wake kama awali? 
 3. Je kuiacha sheria ya Bwana lazima kuandamane na ushupavu wa moyo? Kwa nini mwenye hekima hatakiwi kujisifu kwa sababu ya hekima yake mwenyewe? (1 Wakorintho 4:7). Kwa nini kupenda sifa ni ugonjwa mkubwa wa wabadamu? Waliotahiriwa katika hali ya kutokutahiriwa ni watu wa aina gani?

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 15:1-21

 1. Musa na Samweli wanawakilisha utumishi wa namna gani hadi watajwe katika uasi uliokuwa ukitokea katika taifa la Israeli? Je kuna viongozi ambao licha ya madhaifu yao lakini Mungu anaridhika na uongozi wao? Musa anatajwa kuwa mpole kuliko wanadamu wote wa nyakati zake (Hesabu 12:3).
 2. Je upole ni mojawapo ya sifa inayomtambulisha kiongozi bora? Je, aina ya kifo atakachokufa kila mmoja wetu kinafahmika kwa Mungu? Je kimeandikwa wapi? Je mtu amaweza kubadilisha kutoka aina moja ya kifo alichoandikiwa kwenda aina nyingine ya kifo? Je kuna kifo kilicho nafuu? Je ni sahihi taifa zima kuuawa kwa ajili ya dhambi au uzembe wa kiongozi? Manase alifanya kosa gani lililomkasirisha Mungu kiasi hicho?
 3. Je Mungu huwa anachoka? Je Mungu anapoadhibu kusudi lake ni kuangamiza au kuwafanya wanaoadhibiwa kurudi na kuziacha njia zao mbaya? Usemi kuwa 'jua limekuchwa ungali ni wakati wa mchana' unamaanisha nini? Je, ni muhimu kumuomba Mungu akulipie kisasi juu yao wanakuudhi? (Warumi 12:19). Je, mtu anakulaje maneno ya Mungu? Mungu anamjazaje ghadhabu mwanadamu?
 4. Kwa nini Mungu huwafanya watu wake kuwa ukuta wa boma ya shaba? Nao watapigana nawe lakini hawatakushinda. Je unadhani Mungu ameruhusu adui wapigane nawe kwa sababu anajua hawatakushinda? Unatambua nyakati ambazo Mungu amekuokoa na kukuponya? Je ahadi hii inakuongezea ujasiri wa kuzikabili changamoto za maisha?

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 16:1-21

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 17:1-27

 

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 18:1-23

 1. Kwa nini Mungu anajifananisha na mfinyanzi? Je, kuna wakati unahisi Mungu ameruhusu uteseke wakati kiuhalisia ni kwamba anarudia kukufinyanga? Je kufinyangwa kunaleta maumivu kwa anayefinyangwa au kwa anayefinyanga? Je, kuna ukomo wa kufinyangwa na Mungu?
 2. Mungu hutoa angaizo juu ya mambo ya kuzibgatia ili mhusika asije akaingia hatiani na kukabiliwa na adhabu. Je hii inaonyesha kuwa Mungu anafurahia kuadhibu au hafurahii? Je ni sahihi kumuadhibu mtu ambaye hujawahi kumpa maonyo? Je Mungu ana mpango wa kuliadhibu taifa lolote hapa duniani lisilofuata maagizo yake?
 3. Kwa nini Mungu anarejesha mahusiano na watu pale wanapojirudi na kuacha njia zao mbaya? Kwa nini mwanadamu hupuuzia mashauri ya Mungu na kuamini zaidi mawazo yake mwenyewe? Kwa nini wasiomsikiliza Mungu huwaacha washambuliwe na adui zao? Waliokataa maonyo ya Mungu walimpigaje Yeremia kwa ndimi zao?

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 19:1-15

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 21:1-14

 1. Kwa nini mfalme Sedekia hakumuuliza Mungu yeye mwenyewe juu ya hatima ya nchi yake na badala yake anamuuliza Yeremia? Kwa nini manabii walikuwa muhimu nyakati taifa lilipokuwa linakabiliwa na mkwamo lakini walipuuzwa nyakati za amani?
 2. Kuhani, Nabii, na Mfalme walikuwa wanashikilia ofisi zinazotegemeana. Unadhani ilikuwa sahihi kwa Kuhani kutumwa na mfalme kwenda kwa Nabii?

Kwa nini mfalme asingeagiza taifa zima kuomba na kufunga kama suuhisho la changamoto iliyokuwa inawakabili?

 1. Kwa nini Mungu anakusudia kuwanga mkono Wakaldayo kwenye vita yao dhidi ya taifa la Mungu? Mungu ananufaika nini kwa watu wake kushindwa vitani? Je, lilikuwa jambo rahisi kwa Yeremia kutoa jibu alilopewa na Mungu kwa watu waliotunwa na mfalme?
 2. Kuhukumu kwa haki kuna uhusiano gani na kuwaponya waliotekwa nyara? Je kutolitendea haki taifa au taasisi unayoiongoza kwaweza kuliangamiza taifa au taasisi hiyo? Mungu anawekaje mbele ya watu wake njia ya uzima na mauti? Kwa nini Mungu anaadhibu kulingana na matunda ya matendo yetu?

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 22:1-30

 1. Mungu anapendelea wajane na yatima watendewe inavyostahili. Je unaona juhudi zozote katika kanisa au jumuiya yako ya kidini ya kutafuta na kusimamia haki za hao watu? Je kuna sera yoyote ya kuhakikisha hakihizo zinatekelezwa? Je kama hakuna sera viongozi wanastahili lawama yotote? Wajane na yatima wana wajibu wa kuzidai haki hizo?
 2. Kwa nini haitakiwi kumlilia aliyekufa? Je aliyekufa aweza kurejea tena kwenye nchi aliyozaliwa? Je aliyefia dhambini ni sawa na aliyefia uhamishoni kwenye nchi ya utumwa? Aliyekufa anawezaje kuishi tena?
 3. Kama mafanikio ya mtawala hayapimwi kwa ujenzi wa miundombinu hupimwa kwa kigezo gani? Kipimo cha kumjua Mungu ni nini? Maziko ya punda ni maziko gani?

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 23:1-40

 1. Wachungaji wanaharibuje kondoo wa malisho ya Bwana na kuwatawanya? Mungu atatoa adhabu gani kwa wachungaji kama hao? Wachungaji wanaotajwa hapa ni viongozi wote wa kiroho au ni wale wenye madaraka ya uchungaji tu? Je kuwatawanya waumini ni kosa? Kwa nini Mungu anawakusanya tena wale aliowafukuza?
 2. Je wale ambao Mungu amewakusudia wazae na waongezeke wnahitajika kuwa na sifa maalumu? Je wale wachungaji ambao Mungu huwachagua kulisha kondoo wake huwa na sifa maalumu? Hilo chipukizi la haki ambalo Mungu atamchipushia Daudi katika siku zijazo ni lipi? Sababu mojawapo ya malisho ya nyikani kukauka ni nini? Ni wakati gani mtu hutumia nguvu isiyo ya haki katika kutekeleza majukumu yake?
 3. Je kuna wakati manabii hunena maono ya mioyo yao wenyewe? Je ni kawaida ya manabii wa Mungu kuwaambia waovu kuwa hamtapatwa na ubaya wowote? Je kujishughulisha na tafsiri za ndoto wakati wote kuna lengo la kuwasahaulisha watu wa Mungu juu ya jina lake? Kwa nini Neno la Mungu linalinganishwa na moto na nyundo?

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 24:1-10

 1. Vikapu viwili vya tini vilivyowekwa mbele ya hekalu la Bwana vinawakilisha nini? Kwa nini wanachi wa kawaida wasio watawala hawakuwekwa kwenye kapu la tini zisizofaa kuliwa? Unadhani ni kwa nini mafundi na wafua chuma waliingizwa kwenye kundi la wakuu wa Yuda? Kwa nini Mungu aliruhusu Yehoyakimu mfalme wa Yuda achukuliwe mateka Babeli? Kutekwa kwa wakuu wa Yuda kulikuwa aibu kwa wakuu hao tu au ni aibu pia kwa Mungu?
 2. Kuwepo kwa kapu la tini nzuri kulikuwa kunaashiria wokovu kwa watu wake? Kwa nini mabaki waliosalia katika Yuda wanaunganishwa na watawala wa Yuda watakaotupwa huko na huko katika falme za dunia? Je kwenda utumwani Babeli na kubaki katika nchi ya Yuda ni ipi iliyoonekana kuwa ni amri inayotoka kwa Mungu? Je kutii amri ya Mungu kunakuhitaji uielewe kwanza? Hii ndiyo maana ya wake kuwatii waume zao kwa kila jambo? (Waefeso 5:22, 24).

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 25:1-38

 1. Kiongozi wa taifa asiyekubali kupokea maonyo ya nabii kwa muda wa miaka 23 anafaa kuendelea kuliongoza taifa hilo? Watawala wana kitu gani kinachowafanya wawe wagumu wa kusikia? Kuna uhusiano gani kati ya kutosikia kwa mtawala na kutosikia kwa raia wake?
 2. Kwa nini Mungu anamuita Nebukadneza mtawala wa nchi ya kipagani na adui wa taifa la Mungu kuwa mtumishi wangu? Je Mungu ana watumishi wake kila mahali? Utawatambuaje watumishi hao? Kwa kuacha kuisikiliza sauti ya Mungu kwa miaka 23 taifa la Yuda lilipelekwa utumwani kwa miaka 70. Je inawezekana Yuda walidhani wao pekee ndiyo taifa pekee analolithamini hapa duniani?
 3. Kujiona bora kuliko wengine ndiyo chanzo cha anguko la baadhi ya watu? Nini ufanye usikutwe na anguko hilo? Kama Mungu aliruhusu Babeli waitawale Yuda kwa miaka 70 kwa nini anawaadhibu baada ya kutimia hiyo miaka 70? Je hii inaonesha kuwa Mungu hana upendeleo katika kuadhibu makosa?

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 27:1-22

 1. Je Mungu ndiye mtawala mkuu wa tawala za dunia? Ilikuwaje tawala zingine zilazimishwe kuwa chini ya Nebukadeza? Je ilikuwa rahisi kwa nabii wa Mungu Yeremia aliyekuwa akiipigia debe Yuda kama taifa la Mungu kuanza kupiga debe kuwa iende ikatawaliwe na Babeli taifa la kipagani? Je kuna wakati Mungu anaweza kuruhusu au kuamrisha watu wake wawe chini ya utawala wa kipagani?
 2. Mungu aliyeumba wanadamu na wanyama anauonaje utaratibu wa kujichagulia watawala au viongozi wetu kwa njia ya uchaguzi ulio huru na haki? Je taifa la Babeli lilikuwa bora kuliko mataifa yaliyoagizwa kwenda kuwa chini yake? Kwa nini agizo la Mungu kupitia Yeremia linaelekeza utakapowadia wakati mataifa mengi na wafalme wakuu watamtumikisha Nebukadnza?
 3. Je kulikuwa na ulazima wowote wa Mungu kumwagiza Yeremia ajifanyizie vifungo na nira na kujivika shingoni anapowapelekea ujumbe watawala waliotakiwa kuwa chini ya Nebukadneza? Kwa nini Mungu anakumbusha kuwa Yeye ndiye aliyeiumba dunia hii, wanadamu, na wanyama kwa uweza wake mkuu, na kwa mkono wake ulionyoshwa? Kwa nini wanadamu wanapata kigugumizi cha kumtambua Mungu kuwa ndiye aliyeumba na badala yake kukimbilia dhana za uibukaji zinazokumbatiwa sana?

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 28:1-7

 1. Nabii Yeremia alimwambia nabii wa uongo kuwa "BWANA hakukutuma; lakini unawatumainisha watu hawa maneno ya uongo." Mara ngapi umefanya kosa hilo la kuwatumainisha watu kwa maneno ya uongo?
 2. Mungu asipokutuma nawe ukawatumainisha watu kuwa umetumwa itabidi Mungu akutume kwa kuruhusu ulale mauti. Je watu wadanganyao kuwa wametumwa na Mungu wanahitaji adhabu aliyopewa Hanania?

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 29:1-32

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 30:1-24

 1. Je wakati wa taabu ya Yakobo umeshawadia? Yakobo alipata taabu gani hadi uzoefu wake ujirudie kwa watu wa Mungu? Uzoefu wa taabu ya Yakobo utawasaidiaje watu wa Mungu watakaoishi nyakati za mwisho? Ni nini kitakachowaokoa wale watakaookolewa kwenye taabu ya Yakobo?
 2. Kwa nini Mungu pamoja na kumpa ahadi za matumaini bado anaahidi kutomwacha Yakobo bila adhabu? Adhabu ina umuhimu gani kwa watu wa Mungu? Kwa nini jeraha za Yakobo haziponyeki? Je haziponyeki hata kwa Mungu?

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 31:1-40

 1. Mungu anawapenda wanadamu kwa upendo wa milele. Upendo huo ukoje? Tofauti ya upendo huo na ile wa mbinguni wanadamu ni upi? Kwa nini mwanadamu hana au anapata shida kuuishi upendo wa Mungu? Ni upendo gani unaofanyika kwa lengo la kujipatia faida?
 2. Kwa nini Israeli anapewa nafasi ya pili baada ya ile ya kwanza kuitumia vibaya? Kwa nini anayepewa nafasi ya pili anaitwa bikira? Hii ni kuonyesha Mungu akikusamehe anakuhesabia kama ambaye hujawahi kufanya makosa kabisa? Je watakaorejeshwa kundini baada ya kuwa nje ya zizi kwa muda mrefu watakuwa wengi au wachache?
 3. Sauti iliyosikika Rama Raheli akiwalilia watoto wake ni unabii wa kuuawa kwa watoto gani? Je kuna tumaini lolote juu ya wale walioliacha kanisa kuwa watarejea? Kwa nini moyo wa Mungu unataabika kwa ajili waliotanga mbali naye kama Efrahimu? Je una upendo wa jinsi hiyo kwa wanadamu wenzako wanapotanga mbali?
 4. Agano Jipya ambalo Mungu anafanya na nyumba ya Israeli litatofautianaje na lile la zamani? Kwa nini katika Agano Jipya anatia sheria yake ndani ya mioyo badala ya kuibandika kwenye vibao vya mawe? Kwa nini Mungu huwa haumbuki dhambi aliyoisamehe? Kwa nini kwa Israeli kuendelea kuwa taifa mbele za Mungu kunahitaji sheria zake zisiondoke? Kuna nini kwenye sheria za Mungu kinachofanya Mungu asitengane nazo?
 5. Mungu anaposema nimekupenda kwa upendo wa milele anamaanisha nini? Tofauti ya upendo wa milele na huo upendo mwingine ni nini? Kauli kuwa "aliyemtawanya Israeli atamkusanya na kumlinda" zinaashiria upendo wa milele wa Mungu kwa wanadamu? Je anayelia kwa ajili ya kufiwa hata asikubali kufarijiwa anafanya dhambi ya kuhuzunika kama watu wasio na matumaini? (1 Wathesalonike 413).
 6. Mwanamke anamlindaje mwanaume wakati Biblia inamtambua kama chombo kisicho na nguvu? (1Petro 3:7). Je Agano Jipya analolifanya Mungu na Waisraeli wa kimwili na wa kiroho linaondoa Amri Kumi? Tofauti ya Agano la Kwanza na la Pili ni ipi?

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 32:1-44

 1. Je ilikuwa sahihi kwa Sedekia mfalme wa Yuda kumfunga Yeremia nabii kwa kuwa alitabiri Yuda itaangamizwa na Sedekia hatapona?Unamsahihishaje mtu mkubwa katika namna ambayo huwezi kupatikana na madhara? Kwa nini katika kuthibitisha kuwa hakuna neno gumu linalomshinda Mungu hutolewa mfano wa kuumba mbingu na nchi kama uthibitisho wa uwezo wake? Je ni halali kuwapatiliza watoto kwa uovu uliotendwa na wazazi?
 2. Je unadhani kuna jambo lolote lililo gumu ambalo Mungu hawezi kulifanya? Je hakuna jambo ulilowahi kumuomba Mungu na ambalo bado hajalifanya hadi sasa? Kwa nini Mungu aliruhusu nyumba za Yuda ziteketezwe? Namna moja ya kumchokoza Mungu ni ipi? Kama kufundisha pekee hakumsaidii mtu kupata mafundisho ni nini kinachosaidia kupata mafundisho?
 3. Kama Mungu anaahidi kuwapatia Yuda moyo mmoja na njia moja kama suluhisho la kutangatanga kwao hii inaashiria ufumbuzi wa matatizo yetu anao Mungu mwenyewe? Mungu anaposema atawapanda Yuda kwelikweli kwa moyo na roho yake yote anamaanisha nini? Je kuna uhakika gani kama Mungu ataleta mema yote aliyowaahidia wanadamu?Kuna hatari gani ya kusema mambo ya kweli lakini yasiyowapendeza wakubwa?
 4. Je matatizo ya Yeremia yalikuwa ya kujitakia? Je unaamini kuwa hakuna Neno lolote gumu Mungu asiloliweza? Je mara ngapi umemfikishia shida zako ukiamini juu ya ukweli huo? Mungu ana uwezo wa kutia kicho chake mioyoni mwetu ili tusimuache. Unadhani kwa nini hakufanya hivyo hata taifa la Yuda likamuacha na kuchukuliwa utumwani? Katika kipindi ambacho taifa la Yuda linakabiliwa na uvamizi Mungu anamhimiza Yeremia kununua mashamba. Kuna fundisho gani Mungu alitaka kulifikisha kwetu?

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 33:1-26

 1. Kwa nini Mungu anaendelea kumpa majukumu ya kutekeleza mtumishi wake aliye katika hali ya kufungwa? Je kuna uwezekano wa kutumika na Mungu ukiwa umefungwa? Je, Mungu akiitwa huwa anaitikia? (Waebrania 11:6). Mambo makubwa na magumu ambayo Mungu anaahidi kuwaonyesha wanaomwita ni kama yapi?
 1. Je, umeshawahi kushuhudia Mungu akikutendea mambo makubwa na magumu ambayo hukutarajia kama jibu la maombi yako kwake? Je unadhani Mungu anaingoja kwa shauku siku atakayotimiza neno jema alilolinena kwa ajili yako? Kutokana na mambo machungu aliyoruhusu yakupate maishai unadhani ni kweli kuwa Mungu anakuwazia mema? (Yeremia 29:11).
 2. Kwa nini kuokolewa kwa Yuda kunafanya Mungu aitwe Bwana ni haki yetu? Je wokovu wa mwanadamu hautokani na haki yake mweyewe? Je swala la Mungu kuwaokoa wanadamu ni jambo la kubahatisha ama ni la uhakika kwa kuwa lipo kwenye agano lake? Je Mungu akikusudia kumuokoa mwanadamu lipo jambo linaloweza kuzuia mpango huo?

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 34:1-22

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 35:1-19

 1. Kwa nini utii wa sheria za wanadamu unaonekana kuwa rahisi kuliko utii wa sheria za Mungu? Kiongozi wa dini akikuambia kwenye pombe kidogo si dhambi atakuwa anasema ukweli? Siri ya wazazi wanaoweza kuwatiisha watoto wao ni nini?
 2. Biblia inapotoa maonyo juu ya mienendo yetu kwa nini kunakuwepo upuuziaji? Je kuna haki ya mtu kuchagua kile anachopenda kutii na kile asichopenda kutii kaika Biblia? Je anayeacha kusikiliza maonyo kutoka kwa Mungu anakuwa amechagua kuabudu miungu mingine?

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 36:1-32

 1. Kwa nini Mungu anatumia kauli ya huenda nyumba ya Yuda watasikia ina maana yeye Mungu hajui watakachoamua? Kama Israeli, Yuda, na mataifa mengine yaliyowazunguka yalikuwa yamezama kwenye uovu ni taifa gani lilikuwa kielelezo duniani wakati huo? Kwa nini Israeli na Yuda walishindwa kuwa taifa kielelezo? 
 2. Kwa nini Mungu hakuyafuta mataifa haya yote na kuanza upya? Kwa nini mfame alilikata gombo la Yeremia? Je maneno yalimuogopesha? Kwa nini watawala wanapoonywa hawapendi kusikia? Huwa wanajiona kama miungu? Je siku maangamizi yakija yatampata mtawala mkaidi peke yake au na raia wake?

 

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 37:1-21

 1. Je kuna wakati binadamu hupenda kuambiwa maneno yadanganyayo? Kama una wajibu wa kumshauri kiongozi na ukabaini hapendelei kuambiwa ukweli unaouma utafanyaje? Je yapo mazingira ambayo mtu aweza kujihatarisha kwa kuwa na misimamo yenye ushupavu isiyo ya lazima? Je Yeremia alikuwa hivyo wakati fulani?
 2. Mfalme Sedekia alimchukulia Nabii Yeremia kama mtu wa kawaida na adui wa taifa wakati ambapo alikuwa akijaribu kuliepusha taifa na anguko kubwa. Kwa nini watawala waliopoteza mwelekeo hushindwa kupokea ushauri kutoka wale wasiowasifia kwa kila kitu?

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 38:1-28

 1. Yeremia aliwatabiria Yuda mambo aliyoagizwa na Mungu ambayo kwao yalikuwa ya shari na si ya heri. Kuna nini unachokitegemea leo ambacho Mungu akikuambia usiendelee kukitegemea utaona ni ujumbe wa shari na si wa heri? Je ni kweli Yeremia alikuwa anaidhoofisha mikono ya watu wa vita? Mfalme alipoombwa na raia wake kuwa nabii Yeremia auawe alijitetea akisema mfalme hawezi kufanya neno lolote kinyume chao?
 2. Unamfananishaje mfalme huyu na Pilato? Ebedimeleki mkushi alitoa ushauri kwa mfalme ili kumuokoa Yeremia asife kwa njaa na kwa mazingira yaliyokuwemo shimoni alikotupiwa. Unafananishaje kisa hiki na kisa cha Simoni mkirene (ambaye pia ni mwenye asili ya Afrika) aliyemsaidia Yesu kubeba msalaba? (Mathayo 27:32).
 3. Kwa nini mfalme aliyeruhusu Yeremia akamatwe na kuadhibiwa aliruhusu atolewe shimoni baada ya kusikia mateso anayopitia? Yeremia alielekezwa na mfalme atakavyowajibu watakaomuuliza alichoongea na mfalme na Yeremia akatii na hivyo kuyaokoa maisha yake. Unadhani alikuwa sahihi kusema uongo ili kujiokoa? Kwa nini hakuogopa kusema ukweli kwa mfalme ila akaogopa kusema ukweli kwa raia?

 

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 39:1-18

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 40:1-16

 1. Wakaldayo wanaoabudu miungu ya kipagani wana uhalali gani wa kuwaambia watu wa Yuda (Wayahudi) kuwa wamemwasi Bwana (Yehova) ambaye wao hawamuabudu? Kuna wakati Mungu huwatumia wasio wake kuwaonya walio wake?
 2. Je kuna wakati katika maisha inakulazimu kuwatumikia kwa dhati ya moyo watawala usioafikiana nao kama Yeremia na baadhi ya watu wa Yuda walivyofanya?

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 41:1-18

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 42:1-22

 1. Je kuna wakati katika maisha yako ulipotamani Mungubakuonyeshe njia unayopaswa kuiendea na jambo likupasalo kutenda? Je ni nani kati yako na Mungu anayejua zaidi njia ikupasayo kuiendea na lile likupasalo kulitenda?
 2. Je kuna wakati unahitajika mtu wa kukuombea kwa Mungu kuliko kuomba wewe mwenyewe? Maombi gani huwa na nguvu zaidi kati ya yale ya kuombewa na kujiombea mwenyewe? Je kuna wakati Mungu hujutia makosa aliyowatendea wanadamu? Hali hiyo hutokana na nini?

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 43:1-13

 1. Kwa nini wenye kiburi ni wakaidi hata kwa mambo ya Mungu? Mara nyingi wenye kiburi huonekana kama wanamtetea Mungu na kumpinga Shetani wakati ni kinyume chake. Utawafahamuje watu hao? Kwa nini Yeremia alikubali kupelekwa Misri alikowazuia watu wasiende?
 2. Je Mungu aliruhusu nabii Yeremia aende kule alikowakataza watu wasiende ili aendelee kuwaonya? Je Mungu anawaandikia watu siku ya kufa kwao na namna watakavyokufa? Je kuna jambo unaloweza kubadilisha juu ya siku yako ya kufa na namna utakavyokufa? Je una sababu ya kuogopa kifo?
 3. Je kwa kuruhusu Yuda kuingia Misri alikowakataza wasiende aliazimia kuteketeza miungu ya Misri na kile ambacho Misri ilikuwa inakitegemea? Kwa nini kila wakati Mungu anaposhindana na miungu mingine huwa anashinda? Kwa nini hilo haliwapi fundisho wanadamu kuwa Mungu ni mkuu kuliko miungu yote? Kwa nini Mungu anatumia taifa la Babeli lenye miungu kuangamiza taifa la Misri lenye miungu?

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 44:1-30

 1. Mungu anasema alikuwa anaamka asubuhi ili awatume manabii. Je, Mungu huwa analala? Je Mungu anapoonya anataka anayeonywa achukue hatua za kujisahihisha? Kama hatua za kujisahihisha hazichukuliwi kwa nini anamwadhibu mtu huyo wakati ametumia uhuru wake kukataa maonyo?
 2. Kwa nini watu wa Yuda hawakuwa tayari kumsikiliza Yeremia? Je walimwona Yeremia kama anayejitungia maneno anayowaambia? Watu wanaofanyia dhihaka maneno ya Mungu wanaponzwa na sifa au kiburi? Mwisho wao huwa ni nini?
 3. Kawaida ya Mungu ya kuwabariki waovu hata pale wanapofanya uovu inachangia hali ya kutomjali Mungu anapowapa maonyo? Kwa nini Yeremia anawaambia watu wote wazitimize nadhiri zao za kutoa sadaka kwa miungu mingine? Je alikuwa amekasirika?

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 45:1-5

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 46:1-28

 1. Vikapu viwili vya tini vilivyowekwa mbele ya hekalu la Bwana vinawakilisha nini? Kwa nini wanachi wa kawaida wasio watawala hawakuwekwa kwenye kapu la tini zisizofaa kuliwa? Unadhani ni kwa nini mafundi na wafua chuma waliingizwa kwenye kundi la wakuu wa Yuda? Kwa nini Mungu aliruhusu Yehoyakimu mfalme wa Yuda achukuliwe mateka Babeli? Kutekwa kwa wakuu wa Yuda kulikuwa aibu kwa wakuu hao tu au ni aibu pia kwa Mungu?
 2. Kuwepo kwa kapu la tini nzuri kulikuwa kunaashiria wokovu kwa watu wake? Kwa nini mabaki waliosalia katika Yuda wanaunganishwa na watawala wa Yuda watakaotupwa huko na huko katika falme za dunia? Je kwenda utumwani Babeli na kubaki katika nchi ya Yuda ni ipi iliyoonekana kuwa ni amri inayotoka kwa Mungu? Je kutii amri ya Mungu kunakuhitaji uielewe kwanza? Hii ndiyo maana ya wake kuwatii waume zao kwa kila jambo? (Waefeso 5:22, 24).
 3. Unazungumziaje wazazi wale wanaoona aibu kuwaadhibu watoto wao kwa kuhofia wataonekana hawana upendo na huruma? Kwa kitendo cha Mungu kuwaadhibu taifa la Yuda alionesha upendo na huruma?Je ameonesha kuwa ni mzazi mwema?
 4. Unadhani Misri isingejiongiza kuwasaidia waliokataa ibada ya Mungu wangeangamia vitani? Unadhani kuitegemeza kazi ya shetani na kuwatia nguvu waliomkataa Mungu kwa jeuri na dhihaka kwaweza kukuweka kwenye mazingira magumu waliyojikuta nayo Wamisri? Je, kuna mtu aliyewahi kushindana na Mungu akamshinda?
 5. Kwa nini Mungu anaahidi kumpigai Yakobo? Je, dhambi ya Yakobo hailingani na dhambi ya Misri? Je, unaiona dalili kuwa siku yako ya kutulia na kustarehe isiyo na hofu yoyote ndani yake inakaribia? Je, wakati huo adui zako watakuwa wamekwenda wapi?

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 47:1-7

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 48:1-47

 1. Moabu inatabiriwa kuangamizwa kwa kuwa ilitumainia matendo yake. Je kuna ubaya gani kutumainia matendo yako? Mungu anayaonaje matendo yetu ya haki tutendayo kwa juhudi zetu za kibinadamu? (Isaya 64:6). Kuokoka kwetu kunategemea nini? Kwa nini Mungu anamtangazia laana mtu afanyaye kazi yake kwa ulegevu?
 2. Je wanaomtumikia Mungu wanatakiwa kumwaga damu? Wanamwagaje hiyo damu? Kwa nini watu huwa na bidii katika kufanya kazi zao binafsi kuliko katika kufanya kazi ya Mungu? Je kuna wakati mtu hukimbia hofu? Je kukimbia hofu kunatokana na nini? Kwa nini wakimbiao hofu hutumbukia shimoni? Kama unahisi hofu moyoni dawa yake ni kufanya nini?

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 49:1-39

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 50:1-46

 

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 51:1-64

 1. Mungu hakuwaacha Israeli na Yuda ingawa aliruhusu wapigwe na kupelekwa itumwani. Unajifinza nini juu ya tabia ya Mungu kwa wenye dhambi? (Waebrania 12:6). Kati ya dhambi na mwenye dhambi ni kipi Mungu hukichukia zaidi?
 2. Je Mungu hulipiza kisasi? Kama Mungu analipiza kisasi kwa nini anawakataza wanadamu wasilipize kisasi? (Warumi 12:19). Je Mungu hulipiza kisasi muda wote au ana wakati wake maalum wa kulipiza kisasi? Kwa nini Mungu hukawia kulipiza kisasi?(2 Petro 3:9)
 3. Kwa nini Mungu hapewi heshima anayostahili licha ya kuwa ndiye aliyefanya mambo makuu kuliko kiumbe mwingine yeyote? Je Mungu ana hazina anakohifadhi upepo? Kwa nini mtu hudiriki kuiabudu sanamu aliyoichonga mwenyewe? Je ni sahihi kuwa katika kufanya hivyo anajiabudu mwenyewe? Kwa nini Mungu alilichagua kabila la Israeli kuwa urithi wake? Mungu analitumiaje taifa la Israeli lisilomtii na lifanyalo uasi kuvunja-vunja mataifa mengine? (Kumb. 7:6-8). Je kuwafananisha askari wa Babeli na wanawake ni kuwadhalilisha wanawake au ni kuelezea uhalisia wa wanawake?
 4. Je Mungu alitarajia mfalme Nebukadneza wa Babeli aonyeshe heshima kwake kwa upendeleo wa kuishinda Yuda? Unadhani Nebukadneza alielewa kuwa ushindi wake ulitokana na Mungu wa mbinguni Unaliona kemeo lolote kwa mataifa yenye mafanikio makubwa ya nguvu za kijeshi na uchumi huku wakipuuza kumfanya Mungu kuwa kipaumbele chao?
 5. Unazungumziaje wazazi wale wanaoona aibu kuwaadhibu watoto wao kwa kuhofia wataonekana hawana upendo na huruma? Kwa kitendo cha Mungu kuwaadhibu taifa la Yuda alionesha upendo na huruma?Je ameonesha kuwa ni mzazi mwema?

MASWALI YA KUJADILI: YEREMIA 52:1-34