Seventh-day Adventist® Church

PASTOR LETTA'S OFFICIAL WEBSITE

Menu

PAMBANO KUU

Pambano Kuu

Kwa nini Huna Budi Ukisome Kitabu Hiki

Kwa mamilioni ya watu maisha kwao hayana maana yoyote na huonekana kama upuuzi. Elimu ya Sayansi na ya ufundi wote, Elimu ya Filosofia hata ya mambo ya dini imemdhihirisha binadamu kama kiumbe aliyetokea kwa bahati tu. Walakini, kwa kusudi watu wake wanaona kwamba ni vigumu kukubali kuishi maisha ya ubatili. Ujeuri, ukaidi na uasi, kujaribisha madawa haya yote, kwa ujumla huonyesha upumbavu wa watu wanaoshindana na hali ya kutisha ya upotevu. Sawa kama mtoto yatima wanalia katika hali ya kukata tamaa, wakisema Mimi ni nani? Wazazi wangu walikuwa akina nani? Nitawapateje? TU i.1

Wengi hugeukia Sayansi ili wapate jawabu; hugeukia kwamba huuliza, Je, kuna mtu yeyote huko anayenifahamu ambaye ananiangalia? Lakini Sayansi haina jawabu. Sayansi imewekwa kuuliza tu maswali, chembechembe hufanyikaje? Hutawanyikaje? Mawazo yetu hufanyaje kazi? Ulimwengu umefanyikaje? TU i.2

Sayansi haiwezi kutueleza sababu za kuwako chembe ndogo, au kwa nini biandamu anaishi, au kwa nini ulimwengu uliumbwa. Wala haiawezi kujibu maswali muhimu ya watu wenye hekima ya dunia. TU i.3

Kama kuna maana na haki ulimwenguni kwa nini mwenye haki hutaabika pamoja na mwovu? Je, kuna maisha baada ya kufa? Je, nafsi ya mtu huishi milele? Je, makanisa ya kikristo ya leo kwa kweli humtetea Mungu? Ukweli ni nini? TU i.4

Hali ya ulimwengu wa baadaye ni nini? Je ulimwengu utakwisha kwa hali ya kitoto kutaabika kupata hewa ya mwisho katika machafuko ya hewa au utamalizwa na kombora kubwa lililotupwa kutoka katika chombo? Au mwanadamu ambaye tangu mwanzo hakuweza kuonesha uwezo wowote wa kujitawala asiwe mtu wa kuacha ubinafsi ghafla atokee kukomesha maovu, vita umaskini na kifo? TU i.5

Kitabu hiki kinatoa majibu ya hakika. Maisha yanaumuhimu! Sisi sio peke yetu ulimwenguni. Yuko mtunzaji! Kwa kweli yuko anayejishughulisha na mambo ya binadamu, ambaye alijiunga na jamii yetu ili tuweze kupitia kwake na yeye kwetu. Yuko ambaye mkono wake hodari hutunza sayari yetu ambaye ataongoza na kufikisha mahali pa usalama tena karibuni. TU ii.1

Lakini zamani za miaka iliyopita adui mwenye kushawishi alikusudia kuinyakua dunia yetu na kuitawala na kuuharibu mpango bora wa Mungu wa amani na furaha kwa jamaa nzima ya binadamu. Maelezo ya hali ya ulimwengu yameitaja hatari hii isiyoonekana ya uwezo ulio tayari kuuharibu ulimwengu wetu. Katika onekano la kibinadamu ukafiri na hali ya makanisa vimeungana pamoja na kuwa katika hatia. TU ii.2

Kitabu hiki kitaweza kuchapishwa na kutawanywa tu pale palipo na uhuru wa dini, maana kinatoboa wazi makosa katika siku zetu. Kinaeleza sababu zilizofanya matengenezo ya kanisa yakahitajika na kwa nini yalisimamishwa. Kinatoa kisa cha kusikitisha cha makanisa yaliyoanguka, na muungano wa kikatili wenye kutesa watu na kuinua kwa ushirikiano wa kanisa na serikali ambao utafanya sehemu yake ya ukatili kabla ya kumalizika kwa mshindano makuu kati ya uovu na wema. Katika mapambano haya kila mwanadamu atahusika. TU ii.3

Mwandishi anaandika mambo ambayo hayajatukia wakati wa uhai wake, lakini hayana budu kutukia. Anasema kwa hakika mambo ya kustusha. Mambo ya mapambano haya ni mazito mno kiasi cha kutaka mtu ayatangaze ili kuonya watu. TU ii.4

Hakuna msomaji atakayesoma mambo haya bila kushanga na kutaka kuyachunguza zaidi, na kuwa ilikuwa zaidi bahati yake kuyapata. TU ii.5

Utangulizi

Kufunua Kifuniko Ili Kuona Mambo Yajayo*

Kabla dhambi haijaingia ulimwenguni Adamu alifurahia maongezi pamoja na Muumba wake; lakini tangu watu walipojitenga wenyewe na Mungu wao kwa ajili ya uasi wanadamu wamekatwa kabisa na uhusiano wao umevunjika. Walakini kwa njia ya mpango wa wokovu njia imefunguliwa tena ambayo itawarudisha wanadamu katika ushirikiano na mbingu. Mungu amewasiliana na wanadamu kawa njia ya Roho Wake, na nuru ya Mungu imetolewa ulimwenguni kwa ajili ya ufunuo kwa watumishi waliochaguliwa: “Watakatifu wa Mungu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu” 2Petro 1:21. TU iii.1

Katika muda wa miaka 2500 ya kwanza ya historia ya wanadamu hapakuwako na maandiko yo yote yaliyofunuliwa. Wale waliofundishwa na Mungu walipitisha elimu hiyo kwa wengine, na ikapitishwa vivyo hivyo toka kwa baba mpaka kwa mwana kufuatana na vizazi. Matayarisho ya kutumia maandiko yalianzia kwa wakati wa Musa. Maandiko matakatifu yaliunganishwa pamoja katika kitabu kitakatifu. Kazi hii iliendelea muda mrefu wa miaka 1600 — tangu Musa aliyeandika historia ya uumbaji na sheria, mpaka Yohana, mwandishi wa kweli tukufu za Injili. TU iii.2

Biblia inamtaja Mungu kuwa mwandishi wake, lakini iliandikwa kwa mikono ya wanadamu, na kwa namna mbalimbali katika vitabu vyake huonesha tabia ya waandishi. Ukweli ulioandikwa humo wote una “Pumzi ya Mungu” (2Tim. 3:16) Lakini ukweli wote unaelezwa katika lugha ya kibinadamu, yaani maneno ya watu. Mungu Mwenyenzi kwa njia ya roho Mtakatifu aliwavuvia watumishi wake katika mawazo yao na katika mioyo yao. Aliwapa ndoto na njozi, na mifano na tarakimu, na wote waliopewa mambo hayo waliyakusanya wakayandika kwa kutumia maneno ya lugha ya kibinadamu. TU iii.3

Vitabu vya Biblia vilivyoandikwa nyakati mbalimbali na watu tofauti tofauti hali zote, na kwa kazi mbalimbali, huleta haki pana sana na aina ya uandishi tofauti lakini ujumbe ule ule. Kwa mtu mzembe ambaye anasoma juu juu tu huonekana kwamba Biblia inajipinga yenyewe, lakini kwa msomaji makini ataona kuwa Biblia haipingani hata kidogo. TU iii.4

Kwa jinsi ilivyoandikwa na waandishi wetu mbalimbali kweli imeletwa kwa aina mbalimbali. Mwandishi mmoja anakazia hasa jambo fulani, hushikilia viini vinavyohusiana na uzoefu wake na mwingine anasisitizia jambo jingine, na kila mmoja kwa kuongozwa na roho mtakatifu ujumbe wao wauletao huwafaa watu wa hali zote. TU iii.5

Mungu anapenda kwamba ukweli wake utangazwe ulimwe-nguni kwa njia ya wanadamu, na yeye Mwenyewe amewawezesha kufanya kazi hii kwa Roho Wake Mtakatifu. Aliwaongoza mawazo yao yapi ya kusema na yapi ya kuandika. Ujumbe wa thamani umekabidhiwa kwa vyombo vya duniani, lakini ni ujumbe wa mbinguni, na kweli iliyofunuliwa huunganishwa na kukamilika ili kufaa mahitaji ya wanadamu katika hali zote za maisha yao. Maneno ya ushuhuda hutolewa katika hali zote za maisha yao. Maneno ya ushuhuda hutolea katika lugha hafifu ya binadamu, lakini ni ushuhuda wa Mungu na wenye kuuamini ataona uwezo wa Mungu ndani yake umejaa neema na kweli. Katika neno lake Mungu ametoa mambo yote ya lazima kwa wokovu wa wanadamu. Maandiko matakatifu budi yapokelewe kama mwongozo halisi wa ufunuo wa mapenzi ya Mungu. Maandiko Matakatifu ndiyo kipimo kamili cha tabia na mafundisho. TU iv.1

“Kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema” 2Tim. 3:16-17. TU iv.2

Lakini alipokuwa Mungu amemfunulia mwanadamu mapenzi yake kwa njia ya neno lake, si kwamba amekomaa kuwaongoza watu kwa Roho Wake Mtakatifu. Kinyume cha huyo Roho Mtakatifu aliahidiwa ili apate kulitafsiri neno la Mungu kwa watu, ili wapate kuelewa na kushika mafundisho yake. Kwa kuwa roho Mtakatifu ndiye aliyewaongoza waandishi wa Biblia, hivyo haiwezekani kwa Roho Mtakatifu kupingana na hilo Neno. TU iv.3

Roho hakutolewa ili kuchukua nafasi ya Biblia. Kwa maana Maandiko yanasema wazi kwamba, neno la Mungu ndilo kipimo cha kupimia mafundisho yote ya Imani zote. Mtume Yohana asema, “Msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho kwamba zimetokana na Mungu. Kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani”. 1Yohana 4:1 na Isaya naye anasema, “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawa sawa na neno hili, bila shaka kwa hao hamna asubuhi”. Isaya 8:20. TU iv.4

Shutumu kubwa limetupwa kwa kazi ya Roho Mtakatifu kwa njia ya au wanaotangatanga huku na huku wakidai kwamba wanaongozwa na Roho Mtakatifu, wakisema kwamba hakuna haja ya kuongozwa na neno la Mungu. Wanatawaliwa na hali ya kujisikia msisimko kwamba hiyo ndiyo sauti ya Roho katika mioyo yao. Lakini hali hiyo inayowatawala siyo Roho wa Mungu. Kule kujisikia msisimko kukifuatwa huishia katika machafuko, udanganyifu na uharibifu. Hali hiyo huendeleza tu kazi ya mwovu. Kwa kuwa kazi ya Roho Mtakatifu ni muhimu sana katika kanisa la Kristo, ni makusudi ya Shetani kubuni mbinu za uongo kwa njia ya wakorofi wanaotangatanga na kujipendekeza kwamba wanaongozwa na Roho ili kuchafua kazi ya Roho na kuwafanya watu wa Mungu wasijali maandiko ambayo ndiyo njia iliyowekwa na Bwana mwenyewe. TU v.1

Pamoja na neno la Mungu Roho Mtakatifu ataendelea na kazi yake katika muda wote wa ujumbe wa Injili. Wakati ule ambapo Maandiko ya Agano la kale na Agano Jipya yaliyotolewa, Roho Mtakatifu hakuacha kuwasiliana na watu na kuwavuvia, mbali na alivyowaongoza katika kazi ya kuunganisha maandiko matakatifu katika kitabu. Biblia yenyewe inasema, jinsi watu walivyopata maonyo, kemeo mashauri na maongozi katika kazi ya kuunga Biblia kwa njia ya Roho Mtakatifu. Hata manabii kadhaa wametajwa katika vizazi mbalimbali ambao maneno yao hayakuandikwa. Vivyo hivyo baada ya mkusanyo wa maandiko Matakatifu na kuungwa katika kitabu, Roho Mtakatifu aliendelea na kazi yake ya kuwaelimisha, kuwaonya na kuwafariji watoto wa Mungu. TU v.2

Yesu aliwaahidi wanafunzi wake. “Msaidizi huyu Roho Mtakatifu ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha, yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia” “….. na mambo yajayo atawapasha habari zake, atawaongoza katika kweli yote” Yoh. 14:26; 16:13. Maandiko Matakatifu yanaeleza wazi kwamba ahadi hizi ambazo hazikukomea katika siku za mitume tu, zinaendelea katika kanisa la Kristo katika siku za mitume tu, zinaendelea katika kanisa la Kristo katika vizazi vyote. Mwokozi anawahakikisha wafuasi wake. “Mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari” Mathayo 28:20. Na Paulo asema kwamba karama ya maono ya Roho Mtakatifu vitakuwamo kanisani. “Kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; Hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa Imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufikia kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo”. Waefeso 4:12-13. TU v.3

Kwa waumini wa Efeso Mtume aliomba, “Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa Utukufu, awape ninyi Roho ya Hekima na ya Ufunuo katika kumjua yeye; macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la wito wake…. Na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadri ya utendaji wa nguvu za uweza wake.” Waefeso 1:17-19. Huduma ya Roho Mtakatifu katika kuelimisha, na kuwajulisha watu mambo ya Mungu kwa njia ya neno lake ndiyo mibaraka ambayo Paulo aliwatakia waumini wa kanisa la Efeso. TU vi.1

Baada ya matokeo ya ajabu ya siku ya pentekoste, Petro aliwasihi watu watubu na kubatizwa kwa jina la Kristo, kwa ajili ya ondoleo la dhambi. “Nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtaktifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie” Matendo 2:38-39. TU vi.2

Katika kuunganisha na siku kuu ya Mungu, Bwana kwa njia ya nabii Yoeli aliahidi maonyesho ya Roho Mtakatifu. Yoel 2:28. Unabii huu ulitimia sehemu katika siku ya Pentekoste; lakini utatimia kikamilifu wakati wa neema kuu ya Mungu itakayoonekana wakati wa kufunga kazi ya injili. TU vi.3

Mapambano makali baina ya wema na uovu yataendelea na kuzidi mpaka mwisho kabisa. Katika vizazi vyote hasira ya Shetani imeonekana ikipinga Kanisa la Mungu, na Mungu amewapa watu wake neema ili waweze kupingana na maovu hayo. Wakati mitume wa Kristo walipopaswa kueneza ujumbe mahali mahali ulimwenguni Mungu aliwajalia uwezo kwa neema yake, walimwagiwa Roho Mtakatifu na uwezo mwingi. Lakini kadiri kanisa linapokaribia mwisho, ili liokolewe, shetani atajitahidi sana kwa nguvu kulipinga. Ameshuka chini mwenye ghadhabu kuu, kwa kuwa anajua kuwa ana muda mdogo sana. Ufunuo 12:12. Atafanya kazi akitumia ishara na ajabu za uongo. 2Thesalonike 2:9. Kwa muda wa miaka 6,000 ibilisi huyu ambaye hapo kwanza alikuwa malaika Mkuu wa Mungu, amejitahidi kudanyanya ulimwengu kwa kila njia ya kuuangamiza. Ujanja wake wote na udanganyifu wa kishetani na ukatili na kila hali vyote vitatumiwa kuwapinga watu wa Mungu katika shindano la mwisho, na wakati huu wa hatari kuu, watu wa Mungu watatoa maonyo ya mwisho katika ulimwengu, kuhusu kuja kwa Yesu mara ya pili. Watu lazima watayarishwe ili kusimama mbele ya Kristo pasipo “mawaa wala kunyanzi”. 2Petro 3:14. Wakati huu neema ya Mungu itakayohitajiwa haitapungua kwa ile iliyotolewa siku ya Pentekoste, siku za mitume. TU vi.4

Mwandishi wa kitabu hiki amefunuliwa mapambano haya baina ya wema na uovu na Roho Mtakatifu. Wakati kwa wakati ameruhusiwa kuona maendeleo ya shindano hili ambalo limeendelea kwa vizazi vyote. Kristo ambaye ni mkuu wa uzima ndiye mwanzilishi wa wokovu wetu. Shetani, ambaye ni mkuu wa giza ndiye mwanzilishi wa dhambi, na ndiye aliyekuwa muasi wa kwanza wa sheria ya Mungu Takatifu. Uadui wa Shetani juu ya Kristo umeonekana dhahiri kwa wafuasi wake. Uadui ule ule uliokuwa wa kupinga kanuni za Mungu, njia ile ile ya udanganyifu ambayo hufanya kosa lionekane kuwa ni kweli, na kufanya sheria za watu kuwa bora kuliko za Mungu, kwa njia hiyo watu wameongozwa kuabudu kiumbe badala ya Mwumbaji, hali hiyo ikifuatiliwa inakwenda katika Historia yetu iliyopita. Juhudi ya shetani ya kumsema Mungu vibaya na kuharibu tabia yake, ili watu wamwelewe Mungu vibaya, wamwone kuwa ni katili wala hana upendo wowote, huwafanya watu wamwogope na kujaribu kuepukana na matakwa yake kadiri iwezekanavyo. Hali hiyo shetani ameitumia katika vizazi vyote. Hali hiyo ilionekana siku za Wazee na Manabii, Mitume na Wafia dini na za Watengenezaji wa kanisa. TU vii.1

Katika pambano kuu la mwisho, shetani atatumia njia zile zile hali ile ile, na namna ile ile ilivyokuwa nyakati za nyuma. Jinsi ilivyokuwa, ndivyo itakavyokuwa, isipokuwa tu shindano la kutisha, ambalo ulimwengu haujaliona. Madanganyo ya shetani yatakuwa ya ujanja mno na werevu mwingi. Mashambulio yake yatakuwa makali sana. Kama ikiwezekana yawapoteze hata wateule. Marko 13:22. TU vii.2

Jinsi Roho wa Mungu alivyonifunulia ukweli mkuu wa neno lake, na mambo yaliyopita na yale yajayo, nimeagizwa kuwajulisha wengine mambo haya, yaliyofunuliwa kwangu, kufuatilia historia ya mapambano yaliyokuwa hapo katika vizazi vya nyumba na yalivyo sasa na jinsi yakatakvyokuwa wakati ujao. Katika kushughulika na jambo hili nimejitahidi kuchagua na kupanga pamoja matokeo mbalimbali katika historia ya kanisa, ili kuona jinsi ukweli ulivyofunuliwa katika nyakati tofauti, na kutangazwa ulimwenguni, na jinsi ukweli huo ulivyochochea ghadhabu ya Shetani na uadui wa kanisa liupendalo ulimwengu ambao umetangazwa na watu ambao “hawakuthamini maisha yao hata kufa” TU vii.3

Katika maandishi haya tutaona kivuli cha mapambano yanayotukabili. Kuhusu mambo haya, katika nuru ya Neno la Mungu na uvuvio wa Roho tutaona jinsi mbinu za mwovu zinavyopangwa, pamoja na hatari, ambazo lazima ziepukwe na wale ambao watakutwa “bila mawaa” wakati wa kurudi kwake Bwana. TU viii.1

Matokeo makuu yaliyokuwa wakati wa matengenezo yamekuwa historia tu iliyopita ambayo inajulikana sana na kukubaliwa na makanisa yote ya kiprotestanti. Kuna ukweli usioweza kukanushwa. Historia hii nimesimulia kifupi tu, katika kitabu ambacho kimefupishwa, ambacho ukweli umefupishwa kwa ufahamu wa matumizi yake. Mahali pengine mtunzi au mwandishi wa historia ametoa maelezo kamili au pengine inapolazimu maneno yake yamenakiliwa, pengine imeachwa tu kama ilivyosimuliwa. Katika kusimulia mambo ya hao watengenezaji wa kanisa katika siku zetu, matumizi yale yale kutoka katika maandiko yao yametajwa. TU viii.2

Siyo kusudi la kitabu hiki kuleta ukweli mpya kuhusu mapambano haya ya zamani, ila kuleta kanuni za kweli kuhusu matokeo yajayo. Lakini kukumbusha sehemu iliyopita huonekana kuna umuhimu, maana humulika hali ya siku za mbele, kwa wale watakaopambana na hali hiyo kama watengeneza dini walivyofanya, kushuhudia na kutetea neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo. TU viii.3

Kitabu hiki hasa kusudi lake ni kufunua pambano kali kati ya kweli na uongo, kuonesha hila za Shetani, na njia ya kufaulu kuzipinga, kuonesha njia ya kutatua tatizo la uovu, kufunua upendo wa Mungu na haki yake jinsi anavyochukuliana na viumbe vyake, na kuonesha sheria ya Mungu isiyobadilika. Ili kwa kukisoma watu waweze kuokolewa kutoka katika nguvu za giza ili washiriki urithi wa watakatifu. Sifa kwake yeye aliyejitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ndiyo sala ya dhati ya mwandishi. TU ix.1

 

Sura ya 1:
Utabiri wa Ajali ya Ulimwengu

Kutoka juu ya kilele cha mlima wa mizeituni, Yesu aliutazama mji wa Yerusalemu. Hekalu lile maarufu lilionekana wazi. Jua la jioni lilitupa miale yake myeupe ya kuta za mawe na marumaru ing'aayo tangu mnara wake wa dhahabu mpaka chini. Mwisraeli ye yote angewezaje kulitazama bila kusifu kwa jinsi iliyvokuwa maarufu! Lakini Yesu alikuwa na mawazo mengine “Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia” Luka 19:41. TU 1.1

Machozi ya Yesu hayakuwa kujililia mweneywe, ingawa mbele yake palikuwa na Getsemane, mahali pa mateso makali yaliomkabili, na Kalwari, mahali pa kusulubishwa pake. Walakini siyo TU 1.2

mambo hayo yaliyomtia huzuni kiasi cha kulia. Aliwalilia maelfu ambao watafikwa na ajali waliomo Yerusalemu. TU 1.3

Historia ya miaka elfu ya watu wa Mungu walio wateule, na jinsi Mungu alivyokuwa akiwaangalia kwa huruma nyingi, ilipita katika macho yake Yerusalemu, mji uliotukuzwa na Mungu kuliko yote duniani mwote. “Bwana ameichagua Sayuni …… akae ndani yake”. Zab. 132:13. Kwa muda wa vizazi vingi manabii watakatifu walikuwa wakitoa ujumbe wa maonyo. Damu za kondoo zilikuwa zikitolewa kila siku kafara zikielekeza kwa Mwanakondoo wa Mungu. TU 1.4

Kama Israeli angedumisha ushirika wake na mbingu, Yerusalemu ungedumu milele, maana ni mteule wa Mungu. Lakini historia nzima ya watu hawa walipendwa na Mungu imekuwa ya uasi tu. Mungu alikuwa amewahurumia watu wake zaidi ya upendo wa Baba kwa mtoto wake. “Kwa sababu aliwahurumia watu wake, na makao yake” 2Mambo ya Nyakati 36:15. Maonyo na kusihi kote viliposhindwa, aliwatumia kipaji maarufu kabisa cha mbinguni, mwana wa Mungu mwenyewe, ili kushughulikia mji muasi. Kwa muda wa miaka mitatu Bwana na Nuru na utukufu, amekuwa akienda huku na huko kati ya watu wake, “Akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi”. “Kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka uliokubaliwa”. “Vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wanahubiriwa habari njema” Matendo 10:38; Luka 4:18; Mathayo 11:5. TU 1.5

Aliishi kati yao bila kuwa na makao maalumu ili apate kuwasaidia katika hali zao za kuhurumiwa, akiwasihi ili wapate kukikubali kipawa cha mbinguni, ambacho ni cha uzima. Huruma zake nyingi zilikataliwa na waasi hawa kwa masikitiko makubwa. Lakini Israeli alimkataa rafiki yake mkuu na msaidizi wake wa pekee. Kusihi kwake kwa upendo mwingi kumedharauliwa na kukataliwa. TU 2.1

Muda wa rehema na msamaha ulikuwa unatoweka. Mkusanyo wa ghadabu kwa ajili ya uasi wao, ambao ni wa muda mrefu, ulikuwa umejaa karibu kupasuka juu yao. Yule ambaye ndiye angeweza kuwaokoa na ajali dhahiri iliyokuwa ikiwakabili, amedharauliwa, amekataliwa na karibu atasulubishwa. TU 2.2

Kristo alipoutazama Yerusalemu na ajali yake ikiukabili, pamoja na taifa zima, aliona maangamizo yake yote kwa ukamilifu. Alimwona Malaika mwenye upanga tayari kuharibu na kuangamiza mji ambao umekuwa makao ya Mungu kwa muda mrefu. Kutokea mahali pale pale alipokuwa akisimama mpaka sehemu yote ya mji ambao baadaye Titus jemadari alisimama pamoja na jeshi lake, alitazama ng'ambo pale hekalu takatifu liliposimama. Machozi yakilengalenga machoni mwake, akiona jinsi kuta za mji zitakavyozungukwa na majeshi ya wageni. Alisikia vishindo vya majeshi vikijipanga kwa vita. Alisikia sauti za akina mama na watoto wao wakililia chakula, wakati mji umezingirwa na majeshi ya adui. Aliona nyumba takatifu ya Mungu ikiteketea katika ndimi za moto, na maangamizo makuu. TU 2.3

Akitazama mbele katika vizazi vingi aliona watu wa agano na Mungu wakitawanyika katika nchi zote, kama “mavunjiko jangwani”. Huruma za Mungu, upendo usio kifani, unaonekana katika maneno ya maombolezo ya Yesu juu yao. “Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uuaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wake, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mbawa yake, lakini hamkutaka” Mathayo 23:37. TU 2.4

Kristo aliona katika Yerusalemu mfano wa ulimwengu ambao ni mgumu kwa kutokuamini na uasi, nao una haraka kuingia katika hukumu za Mungu. Roho yake ilijaa huzuni kwa ajili ya maangamizo ya nchi. Alitamani kuwaokoa wote. Alikuwa tayari kujitoa kabisa mpaka kifo ili kuwaletea watu wote wokovu. TU 2.5

Mtukufu wa mbinguni analia! Jambo hilo laonesha jinsi ilivyo kazi ngumu mno ya kumwokoa mkosaji na matokeo ya kuvunja sheria ya Mungu. Yesu aliuona ulimwengu umehusika katika uasi sawa na Yerusalemu ulivyoangamizwa kwa uasi ule ule. TU 2.6

Dhambi kuu ya Wayahudi ilikuwa ile ya kumkataa Kristo. Dhambi kuu ya ulimwengu ni ile ya kukataa sheria ya Mungu, ambayo ndio msingi wa utawala wake, mbinguni na duniani. Watu mamilioni waliomo dhambini ambao wataangamia, katika mauti ya pili watakataa kusikia ukweli katika wakati wao wa wokovu. TU 2.7

Hekalu Maarufu Kuangamia.

Siku mbili kabla ya Pasaka Kristo na wanafunzi wake walikwenda tena katika mlima wa mizeituni kuelekea mji. Mara nyingine tena aliliangalia hekalu likiwa katika uzuri wake na mng'ao wake. Sulemani Mfalme wa Israeli, mwenye hekima kuliko wote alijenga hekalu la kwanza. Lilikuwa maarufu kabisa, ambalo ulimwengu haujaona kama hilo. Baada ya kuharibiwa na Nebukadneza, lilijengwa upya miaka mia tano kabla ya kuzaliwa kwa Kristo. TU 3.1

Lakini hekalu hili la pili halikulingana na lile la kwanza kwa utukufu. Wingu la utukufu, halikutua juu yake, wala moto kutoka mbinguni haukuja juu ya madhabahu yake. Sanduku, kiti cha rehema, na meza za wonyesho havikuonekana ndani yake. Hakuna sauti kutoka mbinguni iliyosema na makuhani kuwajulisha mapenzi ya Mungu. Hekalu la pili halikujia na utukufu wa Mungu, ila mmoja ambaye ni Mungu halisi alikuwako, yaani Kristo. Mmoja anayetakiwa na mataifa yote, ndiye amekuja katika hekalu lake. Ndiye, ambaye ni mtu wa Nazareti aliyefundisha katika ukumbi wake, na kuponya wagonjwa. Lakini Israeli wametia unajisi karama ya mbinguni. Basi, pamoja na mwalimu huyu mnyenyekevu alipotoka mlangoni mwa hekalu, utukufu uliwaacha milele pamoja na hekalu lao. Maneno ya Mwokozi yalikuwa yametimia tayari. “Nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa” Mathayo 23:38 TU 3.2

Wanafunzi walishangaa sana maneno ya Kristo ya kulaani hekalu, nao walitamani sana kufahamu maana yake. Herode Mkuu alikuwa ametia humo hazina tele ya Warumi na ya Wayahudi. Mawe ya marmar yenye kung'aa yaliyotolewa kutoka Rumi yalijengwa katika hekalu hilo. Kwa hayo wanafunzi walitaka Kristo aangalie na kustaajabia uzuri wake. Walimwambia “Tazama, yalivyo mawe na majengo haya” Marko 13:1. TU 3.3

Yesu akajibu na kusema “Amini nawaambieni, Halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa” Mathayo 24:2. Bwana alikuwa amewaambia wanafunzi kuwa atakuja mara ya pili. Hivyo alipotaja hukumu juu ya Yerusalemu mawazo yao yalirudi habari za kuja kwake, kwa hiyo walisema, “Mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako na ya mwiso wa dunia?” Mathayo 24:3. Kristo aliwaeleza wanafunzi mambo ya matokeo makuu yatakayotokea kabla ya mwisho wa ulimwengu. Unabii aliotoa ulikuwa na maana mbili. Wakati ulihusu maangamizo ya Yerusalemu, pia ulihusu matisho ya siku kuu ijayo. TU 3.4

Hukumu zitawaangukia Waisraeli kwa ajili ya kumkataa na kumsulubisha Masihi. “Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu lile lililonenwa na Nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu) ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani” Mathayo 24:15-16 soma pia Luka 21:20-21. Wakati hali ya ukafiri wa Kirumi utakapokuwa ukifanyika katika mahali patakatifu penye kuta za mji mtakatifu, wafuasi wa Kristo itawapasa watafute mahali pengine pa usalama wakakae. Wale watakaookoka itawapasa waharakishe kutoka bila kuchelewa. Kwa ajili ya dhambi za Yerusalemu, zimesababisha hukumu yake. Ukaidi wake na uasi wake umesababisha ajali hiyo. Soma Mika 3:9. TU 4.1

Wenyeji wa Yerusalemu walimlaumu Kristo, kwamba ndiye aliyesababisha maovu yote yaliyowapata, ambayo ni dhambi zao wenyewe. Ingawa walimfahamu kuwa hana dhambi yo yote, walisema kuwa hana budi kufa ili taifa zima lisiangamie. Walikubaliana na uamuzi wa kuhani wao mkuu; kwamba, “inafaa mtu mmoja afe kuliko taifa zima kuangamia.” Yohana 11:47-53. TU 4.2

Wakati walimchinja Mwokozi wao kwa ajili ya kutaja dhambi zao, wao wenyewe walijidai kuwa wana wa Mungu wapendwa, na walitazamia kuwa Mungu angewaokoa kutoka kwa adui zao Warumi!

Uvumilivu Wa Mungu

Mungu alikawiza hukumu yake juu yao kwa muda wa miaka karibuni arobaini. Kulikuwa na Wayahudi wengi ambao hawakuelewa kazi ya Kristo. Tena watoto hawakupata nafasi kama ile ya wazazi wao. Kwa njia ya mahubiri ya mitume nuru ya Injili ingewafikia wote. Wangeona jinsi unabii ulivyotimia, sio kwa kuuliwa kwa Kristo tu, bali kwa kifo na kufufuka kwake pia. Watoto wasingepaswa kupata adhabu kwa ajili ya dhambi za wazazi wao. Lakini walipoikataa nuru iliyowafikia, ndipo wakashiriki dhambi za wazazi wao na kukijaza kikombe cha uovu wao. TU 4.4

Wayahudi kwa ajili ya ukaidi wao na uasi wao walikataa karama yao ya neema ya mwisho waliyopewa. Ndipo Mungu akawaondolea ulinzi wake. Taifa zima likaachwa liongozwe na kiongozi waliyemchagua. Shetani aliwaamshia hali fedhuli kabisa, nyonge na ya udhalimu. Watu walikuwa kama wanyama tu wakitangatanga kama vipofu, wakawa wakatili. Marafiki na watu wa jamaa moja moja walisalitiana tu wao kwa wao. Wazazi waliwaua watoto wao, na watoto wazazi wao. Watawala hawakuweza kujitawala wenyewe, ukali wao ukawafanya kuwa wajeuri sana. Wayahudi walikubali maneno ya ushahidi wa uongo juu ya Kristo hata wakamwua Yule mwenye haki, Mwana wa Mungu, asiye na hatia. Sasa mashitaka yao ya uongo yamefanya maisha yao kuwa ya ovyo. Hofu ya Mungu haikuwa ndani yao tena. Shetani ndiye alikuwa mtawala wao. Viongozi wa upinzani wakaangamizana wao na wapinzani wao bila huruma. Hata mambo matakatifu ya hekaluni hayakuweza kuheshimiwa. Hekalu lilitiwa unajisi kwa maiti zilizokuwa zikitupwa huko ovyo. Hata hivyo matendo ya kinyama ya jinsi hii waliyoyatenda walikuwa wakiona sawa tu na kusema kuwa waliyoyatenda walikuwa wakiona sawa tu na kusema kuwa Yerusalemu hautaharibiwa, maana ni mji wa Mungu! Hata wakati ule Warumi walipozunguka mji wafedhuli hawa walikuwa na tumaini kuwa Mungu angeingilia kati na kuwafukuza Warumi. Lakini Israeli alikuwa ameondolewa ulinzi wake, na sasa yuko wazi bila kinga yoyote. 

Ishara ya Maangamizo

Utabiri wowote Yesu aliotabiri kuhusu uangamizo wa Yerusalemu ulikuwa unatimia moja kwa moja. Ishara na vioja vilionekana. Kwa muda wa miaka saba mtu fulani alikuwa akitembeatembea katika barabara za Yerusalemu huku akitangaza ole utakaoujia mji. Mtu huyu ambaye hajulikani alikotoka aliteswa na kufunga na kutendwa mabaya lakini kwa dharau na jeuri yeye alijibu, “Ole Ole, wa Yerusalemu”. Baadaye aliuawa katika kuuzingira Yerusalemu. Katika maangamizo ya Yerusalemu hakuna hata mkristo mmoja aliyepotea. Baada ya majeshi ya Kirumi chini ya jemadari Cestius kuuzingira mji,ghafla waliondoka bila kutazamiwa, wakati kila jambo lilikuwa tayari kwa mashambulio. Jemadari wa Kirumi aliamuru majeshi yake yaondoke bila sababu maalum. Dalili iliyoahidiwa na Kristo kwa wafuasi wake imefika. Luka 21:20-21. TU 5.1

Mambo yalitayarishwa kabisa ili kuwezesha wakristo kukimbia, ambavyo hayakuwezekana kuzuilika. Wayahudi au Warumi hawakuweza kuyazuia. Wakati majeshi ya jemadari Cestius yalipoondika, Wayahudi nao walitoka kuwafukuza, na wakati walipokuwa katika kupambana, wakristo walipata nafasi ya kukimbilia mahali pa usalama. Walikimbilia mji wa Pella. TU 5.2

Majeshi ya Wayahudi yaliyowafuatia Warumi yalishambulia majeshi ya nyuma. Hivyo Warumi walifaulu kwa shida sana kuendelea. Wayahudi walirudi Yerusalemu wakifurahi, wakiwa na vitu walivyoteka. Ushindi mdogo huu uliwaletea maafa makubwa. Walizidi kuwa wakaidi zaidi wasitake kujisalimisha kwa Warumi, hivyo maafa makubwa yasiyoelezeka, bila kipimo yalifuata baadaye. TU 5.3

Mabaya ya kutisha yaliujiaYerusalemu wakati jemadari Titus aliporudi na kuuzingira mji mara ya pili. Mji ulizingirwa wakati wa Pasaka, wakati Wayahudi kwa mamilioni walikuwa wamekusanyika ndani yake. Maghala ya vyakula yalikuwa yameharibiwa na watu wenye fitina, na sasa hali ya njaa iliwaingilia. Watu walikula ngozi za mishipi yao na viatu vyao. Watu wengi sana walikuwa wakipenya usiku na kutoka nje ya mji kutafuta matunda mwitu. Wengi walikuwa wakikamatwa na kuuawa kikatili. Mara nyingi hata wale waliowahi kurudi salama, walinyanganywa na wenzao kile walichopata huko nje. Waume waliwanyang'anya wake zao chakula na wake vivyohivyo waliwanyanga'nya waume zao. Watoto walipokonya chakula kutoka vinywani mwa wazee wao. TU 6.1

Viongozi wa majeshi ya Kirumi walikusudia kutoa kipigo kizito kwa Wayahudi ambacho kingewafanya wasalimu amri mara moja. Mateka walipigwa, wakateswa sana na kutundikwa mitini, mbele ya kuta za mji. Kufuata bonde la Yeoshafati na kuendelea mpaka mlima wa Golgota, misalaba mingi sana, ambako watu walikuwa wametundikwa ilijazana tena. Hapakuwako na nafasi ya kupita kati yake. Kwa hiyo matamshi yaliyotamkwa mbele ya kiti cha hukumu cha Pilato kwamba: “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu” yalikuwa yanatimia. Mathayo 27:25. TU 6.2

Jemadari Titus alijawa na hofu ya mshangao wa kuchukiza alipoona maiti za Wayahudi zimejazana bondeni humo. Alilitazama Hekalu; akaamuru kuwa mtu asiliguse. Aliwasihi viongozi wa Wayahudi wasalimu amri, asije akalazimika kuwaharibu, na kupaharibu mahali patakatifu kwa kumwaga damu; yaani wasiingize vita hekaluni. Kama Wayahudi wangalipigania mahali pengine, hakuna Mrumi hata mmoja angelithubutu kuharibu hekalu takatifu! Josephus aliwasihi sana wasalimu amri ili wajiokoe, na kuokoa mji wao, pamoja na hekalu lao takatifu. Lakini alijibiwa kwa matusi mabaya na kushambuliwa kwa ghafla. Hivyo ndiyo ilikuwa nafasi yao ya mwisho na Josephus alikuwa mwombezi wao wa mwisho. Titus alijaribu kuliokoa hekalu, lakini ilikuwa kazi bure. Mkuu kuliko yeye alikuwa ametamka kuwa, halitasalia jiwe juu ya jiwe. TU 6.3

Baada ya kuliteketeza hekalu, mji wote ukaangukia mikononi mwa Warumi. Viongozi wa Wayahudi waliziacha ngome zao. Titus alisema kuwa Mungu ndiye amezitia katika mikono yake, maana hakuwa na uwezo wa aina yoyote ile ambao ungaliweza kuzibomoa ngome hizo. Mji na hekalu pia vilibomolewa mpaka na misingi yake yote; na mahali pale hekalu takatifu lilipojengwa palilimwa kwa jembe na kusawazishwa kama shamba. Yeremia 26:18. Watu zaidi ya milioni moja waliangamia, na waliobakia wengine walitekwa na kupelea utumwani; wengine waliuzwa kama watumwa wengine walitawanyika wakaishi mahali pengine katika hali ya ukimbizi na wengine walitupwa katika matundu ya simba na wanyama wakali wakawa sinema ya kutazamwa na watu wakiangamizwa. TU 6.4

Wayahudi walikuwa wamekijaza kikombe chao cha kulipizwa kisasi. Katika misiba iliyowafuata baadaye ilikuwa na mavuno ya mambo waliyoyapanda kwa mikono yao wenyewe. “Ee Israeli, umejiangamiza mwenyewe;…. Kwa maana umeanguka kwa sababu ya maovu yako”. Hosea13:9; 14:1. Taabu yao ilitajwa kila mara kama adhabu iliyoagizwa na Mungu. Kwa njia hii mdanganyaji mkuu hufunika kazi yake na kuitupa kwa Mungu. Wayahudi kwa ajili ya ukaidi wao wa kukataa rehema na upendo wa Mungu walijiondolea ulinzi wa Mungu wakabakia wazi. TU 7.1

Hatujui kiasi gani tunawiwa na Kristo kwa ajili ya amani na ulinzi tulivyo navyo. Mkono wa Mungu wa kuulinda humzuia Shetani asituharibu. Kutotii na kutoshukuru ni deni kubwa tulilo nalo kwa Mungu. Lakini mtu anapovuka mpaka wa Mungu ulinzi wake huondolewa. Mungu hamtetei mtu huyu kama mshitakiwa. Huwaacha hao wakaidi wavune kile walichopanda. Kila cheche ya nuru iliyokataliwa ni mbegu iliyopandwa, nayo italeta mavuno. Roho wa Mungu anayesihi akipingwa daima, mwisho ataondoka. Ndipo mtu atabaki bila uwezo wa kuzuia tama mbaya kwake, hakuna kinga kwa madanganyo ya mwovu Shetani. TU 7.2

Uharibifu wa Yerusalemu ni onyo kuu kwa watu wote wanaokataa rehema za Mungu. Unabii wa Mwokozi kuhusu hukumu ya Yerusalemu utatimia kwa njia nyingine. Katika ajali ya mji mteule, tunaona msiba utakaowapata walimwengu waliokataa rehema za Mungu na kukanyaga sheria yake takatifu. Huzuni kuu ambayo haijatokea ulimwenguni. Iliwapata watu wapotovu. Kukataa mamlaka ya mbinguni kumekuwa jambo la kutisha sana. Lakini wakati ujao utakuwa wa huzuni kuu zaidi. Wakati roho wa Mungu atakapoondolea kabisa ulimwenguni, hakuna kitu kitakachozuia hali ya kinyama, na hasira za kishetani na udanganyifu wake wa kikatili. TU 8.1

Katika siku hiyo, sawa na ulivyokuwa kwa Yerusalemu, watu wa Mungu wataokolewa. Soma Isaya 4:3; Mathayo 24:30-31. Kristo atakuja mara ya pili ili kuwakusanya watu wake. “Ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni, pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu” Mathayo 24:30-32. TU 8.2

Hebu watu na waangalie sana, wasije wakasahau maneno ya Kristo. Kama vile alivyowaonya wanafunzi wake kuhusu uharibifu wa Yerusalemu, juu ya kukimbia kwao, ndivyo pia ameonya ulimwengu kuhusu uharibifu wa mwisho. Wale wapendao wanaweza kukimbia ghadhabu ijayo. “Tena kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi na nyota; na katika nchi dhiki ya mataifa” Luka 21:25. Soma pia Mathayo 24:29; Marko 13:24-26; Ufunuo 6:12-17. Maneno ya Kristo ya maonyo ni kwamba, “Kesheni basi” Marko 13:35. Wale watakaojali maonyo hawataachwa wakae gizani. TU 8.3

Sasa ulimwengu hauko tayari kupokea maneno ya ujumbe wa Kristo kwa wakati huu, kuliko Wayahudi walivyopokea maonyo ya Kristo kuhusu uharibifu wa Yerusalemu. Njoo, maadamu ni leo. Siku ya Mungu itawaghafilisha wote, wasiomcha Mungu. Wakati maisha yatakapokuwa yanaendelea kama kawaida; wakati watu watakapozama kabisa katika anasa; katika shughuli, na katika uchumi; wakati waongozi wa dini watakaposifia maendeleo ya ulimwengu na watu wakijitumainisha kuwa na amani na usalama, ndipo, kama vile mwizi aibavyo usiku, ndivyo uharibifu utakavyowajia wote wasiomcha Mungu, “Wala hakika hawataokolewa”. 1Thes. 5:2-5.

 

Sura ya 2: Wakristo wa Kwanza Waaminifu wa Kweli

Yesu aliwafunulia wanafunzi wake hali ya watu wake jinsi itakavyokuwa tangu siku ile atakayoaacha kwenda zake mbinguni, hata siku atakaporudi mara ya pili kwa nguvu na utukufu mwingi. Alipenyeza macho yake akaona hali ya fujo na mateso itakayowapata wafuasi wake siku za usoni. Soma Mathayo 24:9,21-22. Wafuasi wa Kristo hawana budi kupitia njia ile ile ya dharau na dhihaka na masumbuko, kwa Mwokozi wa ulimwengu, utaonekana kwa wote watakaoliamini jina lake pia. TU 9.1

Umizimu uliona kuwa kama ukristo utafaulu utaondolea mbali mahekalu na madhehebu zote za giza kwa hiyo moto wa mateso ukachochewa. Wakristo walinyang'anywa mali zao, na kufukuziwa mbali kutoka katika miji yao. Watu wenye elimu na wasio na elimu, walichinjwa bila huruma. TU 9.2

Mateso yalianzia wakati wa mfalme Nero yakaendelea kwa karne nyingi. Wakristo walisingiziwa kuwa ndio wameleta njaa, tauni, na tetemeko la nchi. Walisaliti na wachochezi walikuwa tayari kusaliti na kuwasingizia wasio na hatia kwamba ni hatari kwa jamii. Wengi sana walitupwa katika matundu ya wanyama wakali au walichomwa moto; wengine walitundikwa mitini, wengine walivishwa ngozi za wanyama wakatupiwa mbwa na kurarulia nao. Katika mikutano ya hadhara, watu wengi walihudhuria ili kushangilia mateso yao na jinsi walivyokufa kikatili kabisa. TU 9.3

Wafuasi wa Kristo walilazimishwa kutafuta maficho mahali pa ukiwa nyikani. Chini ya milima iliyoko nje ya mji wa Rumi walichimba mifereji mirefu, wakafanya makao katika mapango hayo chini ya miamba. Humo ndimo walimozika wafu wao pia. Hayo yalikuwa makimbilio yao. Wengine walikumbuka maneno ya Bwana, kwa hiyo walipoudhiwa walifurahi tu. “Thawabu yao itakuwa kubwa sana mbinguni, maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yao” Mathayo 5:11-12. TU 9.4

Nyimbo za ushindi zilisikika kutoka katika miale ya moto wakiziimba kwa furaha. Kwa imani walimwona Kristo na malaika wakiwazunguka kwa kupendezwa sana kwa ajili ya ushujaa wao. Sauti ilisikika kutoka katika kiti cha enzi cha Mungu, ikisema: “Uwe mwaminifu mpaka kufa, nami nitakupa taji ya uzima”. Ufunuo 2:10. TU 10.1

Shetani alijitahidi kuliharibu kanisa la Kristo, kwa njia ya mateso, lakini ilikuwa kazi bure. Watendakazi wa Mungu walichinjwa, lakini Injili ilizidi kuenea, na wafuasi kuongezeka. Mkristo mmoja alisema, “Mnatukatakata kama majani, lakini tunazidi kuongezeka; damu ya wakristo ndiyo mbegu.” TU 10.2

Kwa hiyo shetani alipanga vita kwa njia nyingine ya kufaulu zaidi. Alisimamisha bendera yake katika kanisa la kikristo, ili kupata wakristo wadanganyifu, wenye hila, hivyo alifaulu kuliko alivyotumia mateso, akatumia vishawishi na heshima. Ibada ya Sanamu ilikubaliwa kuwa ni sehemu ya ukristo, na ukweli halisi akakataliwa. Walijidai kuwa watu wa Mungu lakini huku wakishikilia dhambi, bila kuwa na haja ya kuziungama na kuziacha. Hapakuwako badiliko lolote katika mioyo yao. Walikubaliana tu ya kuwa wote “waamini katika Kristo” TU 10.3

Sasa kanisa lilikuwa katika hatari kubwa. Magereza, mateso, kuchomwa moto na upanga, hayo yote yalikuwa nyeti kulinganisha na hali hii ya ukristo bandia. Baadhi ya wakristo walisimama imara. Wengine walipendelea kugeuza imani zao na kufuata ukristo huu bandia. Katika vazi hili jipya la ukristo wa kujifanya, shetani alijipenyeza kanisani na kuchafua imani yao. TU 10.4

Wakristo wengi baadaye walipotoka kabisa na kushusha hadhi yao. Mwisho mwungano wa ukristo na umizimu ulifanyika. Ingawa waabudu sanamu walijidai kuungana na kanisa, lakini walishikilia sanamu zao tu, ila walibadili sanamu zao ziwe mfano wa Yesu, na mfano wa Maria na watakatifu wengine. Wakaingiza mafundisho ya uongo mambo ya ushirikina na uchawi, na mambo ya ibada ya sanamu. Hivyo vyote vikawa sehemu ya imani na ibada ya ukristo. Kwa hiyo ukristo halisi ukachafuliwa sana, na kanisa likapoteza hadhi yake na uwezo wake. Walakini wengine hawakupotoshwa. Walishikilia kanuni yao ya imani ya kweli.

Makundi Mawili Kanisani

Kumekuwepo makundi mawili baina ya watu wajidaio kuwa wafuasi wa Kristo. Wakati kundi moja linajifunza maisha ya Kristo na linapojitahidi kufuata kielelezo chake kundi jingine linaepa kabisa kujifunza mambo ambayo yangedhihirisha makosa yao, maana hawataki kufuata ukweli. Walakini, hata kanisa lilipokuwa katika hali bora, halikuwa kamilifu kabisa. Yuda alihesabika kuwa mmojawapo wa wanafunzi ili kwa njia ya mafundisho ya Kristo na kielelezo chake angeweza kuona kasoro zake na kutubu. Lakini kwa ajili ya kushikamana na dhambi aliyakaribisha majaribu ya Shetani. Alichukizwa wakati kasoro zake zilipotajwa, na hivyo aliendelea mpaka akamsaliti Bwana wake. Marko. 14:10-11. TU 11.1

Anania na Safira mkewe walijipendekeza kuwa wametoa mali yao yote kwa Mungu wakati walipoficha sehemu yake kwa choyo chao. Roho wa Mungu alimfunulia mtume Petro tabia yao hasa ya wajipendekezao hawa, na hukumu za usafi wa kanisa. Soma Matendo 5:1-11. Mateso yalipowajia wafuasi wa Kristo yaliwadhihirisha wale waliokuwa wafuasi halisi. Lakini mateso yalipokoma, wakaingia watu kanisani ambao hawakuwa wafuasi halisi, na kwa njia hiyo shetani alipata nafasi ya kuliharibu kanisa. TU 11.2

Wakati wakristo waliporidhika kuungana na watu ambao hawakuongoka sawasawa, shetani alishangilia. Halafu aliwaamsha watu kama hao wawaudhi wale walioshikilia kanuni ya Mungu barabara. Wakristo wapotovu hawa ambao ni nusu wamizimu, walielekeza upinzani wao katika mafundisho yale ambayo ni muhimu kwa ukristo, ndiyo maagizo ya Kristo. Kutakikana msimamo imara kabisa kukabiliana na mafundisho mapotevu yaliyoingizwa kanisani. Biblia ilikataliwa wazi kuwa sicho kipimo cha ukristo. Uhuru wa dini ulihesabiwa kuwa kama uzushi na wale waliousikilia waliharamishwa TU 11.3

Baada ya mapambano ya muda mrefu, wale waongofu wa kweli waliona kuwa ni lazima kuwepo utengano. Hawakuweza kuvumilia makosa hayo mabaya yenye kuleta hatari kwao na kwa watoto wao na wajukuu wao. Wakaona kuwa amani ya kweli lazima igharimu. Kwamba ikiwa kuwa na amani na kutupilia mbali kanuni za Mungu ndiko kutaleta umoja, basi amani ya namna hiyo na ipotelee mbali, ikilazimu lazima kuwe na utengano na hata kwa vita. TU 11.4

Wakristo wa kwanza walikuwa waongofu wa kweli. Walikuwa wachache, bila kuwa na mali, heshima au vyeo nao walichukiwa na wale wamizimu, sawa kama vile Kaini alivyomchukia Habili. Soma Mwanzo 4:1-10. Tangu wakati wa Kristo mpaka leo, wafuasi wa kweli wa Mungu wamekuwa katika chuki na wale wapendao dhambi. TU 11.5

Sasa basi, Injili itawezaje kuitwa kuwa ujumbe wa amani? Malaika waliimba katika uwanda wa Bethlehemu “Atukuzwe Mungu juu mbinguni na dunia iwe amani kwa watu aliowaridhia.” Luka 2:14. Inaonekana kuwa iko tofauti kati ya maneno haya ya Unabii na maneno ya Kristo: “Sikuja kuleta amani, bali upanga” Mathayo 10:34. Lakini yakifahamika kwa kweli, hayana tofauti yoyote. Injili na ujumbe wa amani. Dini ya Kristo ikipokelewa na kutiiwa hueneza furaha na amani duniani. Kazi ya Yesu ilikuwa kuwapatanisha watu na Mungu, mtu na mtu mwenzake. Lakini dunia kwa ujumla inatawaliwa na shetani, ambaye ni adui mkubwa wa Kristo. Injili inaonyesha kanuni za uzima na maisha kwa ujumla, na hizo hupingana na utawala wa shetani. Kanuni hizo za shetani hazitaki maisha matakatifu yanayokuwa kinyume na dhambi. Hilo huamsha vita kwa watu wanaong'ang'ania maisha matakatifu. Ni kwa njia hii ndiyo sababu Injili ikaitwa kuwa ni upanga. Soma Mat. 10:34. TU 12.1

Watu wengi walio dhaifu katika imani wako tayari kuutupa ujasiri wao katika Mungu, kwa sababu huwafanikisha watu wabaya na watu wema husumbuka tu bila mafanikio. Mtu mwema, mwenye haki anawezaje kuchukuliana na hali ya jinsi hiyo isiyo na haki? Mungu ametuonyesha upendo wake kwa namna inayotosha. Hatuwezi kuona mashaka kwa wema wake, eti kwa sababu hatuelewi tu mipango yake TU 12.2

Mwokozi alisema: “Likumbukeni lile neno nililowaambia, mtumwa si mkuu kuliko Bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi” Yohana 15:20. Watu watakapopitia mateso, au hata mauti, huwa wamepitia njia ya Mwana mpendwa wa Mungu. TU 12.3

Wenye haki hupitia katika mateso machungu ili watakase wao wenyewe, na njia hiyo iwe kielelezo cha imani yao kwa wengine na uongofu wa halisi ulivyo. Hali yao izibe vinywa vya wapotovu wanaosema kuwa haiwezekani kuwa hiyo. Mungu huwafanikisha waovu na kuudhihirisha uadui wao jinsi inavyowastahili adhabu ya uharibifu wao. Kila kitendo cha ufedhuli kitendewacho mtu wa Mungu, kitahesabika kana kwamba kilitendwa kwa Kristo mwenyewe, nacho kitaadhibiwa. TU 12.4

Paulo asema, “Wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa” 2 Tim. 3:12. Kwa nini basi mateso yametulia? Sabatu yake ni kwamba kanisa limeungana na ulimwengu kimaisha, kwa hiyo hakuna upinzani wa kuchochea mashindano. Dini ya siku zetu hizi haifanani na ile ya siku za mitume katika utakatifu. Kwa kuwa ukweli wa Neno la Mungu unajaliwa kidogo tu, na kwa kuwa kuna uongofu kidogo tu kanisani, ukristo unakuwa kitu cha kawaida tu ulimwenguni. Hebu mwamko wa dini ya siku za mitume uwemo kanisani, hapo mto wa mateso utawashwa.

SURA YA 3: Giza la Kiroho Katika Kanisa la Kwanza

Mtume Paulo aeleza kwamba siku ya Kristo haitakuja “Usipokuja kwanza ule ukengeufu, akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu. Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi”. 2Wathesalonike 2:3,4-7. Hivyo hata siku hizo za mwanzoni mtume aliona uovu ukilitambalia kanisa ambao utaingiza upapa ndani. TU 14.1

Kidogo kidogo, “siri ya kuasi” iliendesha kazi yake ya udanganyifu. Kawaida za kimizimu ziliingizwa kanisani na kukubaliwa kuwa nia sawa, ingawa zilipingwa kwanza na kuleta mateso kwa njia ya wamizimu. Lakini mateso yalipokoma hali ya kanisa ilibadilika na kuacha kanuni halisi ya kikristo. Hali hiyo iliongozwa na mapapa na mapadri. Uongofu bandia wa mfalme Constatine ulileta burudiko kubwa kanisani. Kwa hiyo sasa uharibifu ulizidi mno kanisani. Ukafiri ulishinda kabisa na kutawala kanisani. Kawaida za kikafiri na mafundisho ya ushirikina viliingizwa kanisani na kuhesabiwa kuwa ni mojawapo ya kanuni za Kikristo. TU 14.2

Mapatano haya baina ya ukafiri na ukristo yalitokeza “mtu wa dhambi”, aliyetabiriwa katika Biblia. Dini ya uongo ni hila za Shetani, na juhudi yake ni kuketi katika kiti cha enzi apate kuutawala ulimwengu kama apendavyo. TU 14.3

Mojawapo ya mafundisho ya kanisa la Kiroma ni kwamba papa amepewa uwezo mkuu awe juu ya makasisi wote na wachungaji wote wa ulimwengu. Zaidi ya hayo, papa amepewa heshima ya kuitwa “Bwana Mungu Papa” na kwamba yeye hakosei hata kidogo. Dai lile lililodaiwa na shetani huko jangwani wakati wa majaribu ya Yesu lingali linaendelea katika kanisa la Kirumi; na watu wengi humtukuza jinsi hiyo. TU 14.4

Lakini wanaomcha Mungu huyapinga majivuno hayo kama Kristo alivyoyapinga ya mwovu shetani jangwani. “Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake” Luka 4:8. Kamwe Mungu hakumweka mtu ye yote kuwa kichwa cha kanisa. Ukuu wa upapa unapingwa na Maandiko Matakatifu. Papa hawezi kuwa kichwa cha kanisa la Kristo isipokuwa ajitwalie mamlaka hayo kwa nguvu. Warumi hawalaumu waprotestanti, na kusema kwamba wamejitenga na kanisa la kweli. Lakini wao ndio waliojitenga na Imani “ambayo kwanza ilikabidhiwa kwa watakatifu” Yuda 3. TU 14.5

Shetani alifahamu fika kuwa Mwokozi aliyapinga majaribu yake kwa njia ya Maandiko Matakatifu. Kila jaribu la shetani Mwokozi alilipinga kwa ngao ya kweli, akisema “Imeandikwa”. Ili kusudi shetani awashinde watu, na wasifahamu Maandiko Mataktifu. Ukweli Mtakatifu lazima ufichwe usifahamike. Kwa muda wa miaka mamia Biblia ilikatazwa kusomwa kabisa na kanisa la Kirumi. Watu waliruhusiwa kusoma na kueleza maana yake, ili kufaulisha mpango wao. Kwa njia hiyo Papa alitukuzwa kabisa ulimwenguni kama kaimu wa Mungu duniani. 

Jinsi Sabato “Ilivyobadilishwa”

Unabii unaeleza kuwa, Upapa utafikiri kubadili “Wakati na Sheria” Daniel 7:25. Ili kusudi kuimarisha ibada ya sanamu, heshima ya kuwakumbuka wafu na sura zao iliingizwa katika kanisa la Kikristo. Tamko la baraza lao kuu kwamba, mifano au picha za watu mashuhuri ziwekwe ili kuwakumbuka, lilithibitisha ibada ya sananu. Kwa njia hiyo Rumi ikathubutu kufuta amri ya pili katika amri za Mungu, ambayo inakataza kuabudu sanamu, halafu wakagawa amri ya kumi kuwa amri mbili ili hesabu ya amri iwe kamili TU 15.2

Viongozi wa kanisa ambao ni wapotofu, wakageuza amri ya nne, wakaondoa Sabato ya siku ya saba, siku ambayo Mungu aliibariki na kuitakasa (Mwanzo2:2-3), badala yake “wakatukuza siku ya jua” ambayo ilikuwa ikitukuzwa na wakafiri. Katika karne ya kwanza siku ya Sabato ilikuwa ikitukuzwa na wakristo wote. Lakini shetani alijitahidi kutimiza makusudi yake mapotofu, ndipo kutukuza Jumapili kulianza (siku ya jua) eti kuadhimisha siku ya ufufuo wa Kristo. Ibada za kidini ziliadhimishwa sasa hiyo kama kumbukumbu ya ufufuo wa Kristo. Walakini Sabato iliendelea kutumzwa kama siku Takatifu. TU 15.3

Shetani aliwaongoza Wayahudi kuitilia Sabato vikwazo vingi mpaka ikawa mzigo. Na sasa kwa mpango huu mpya aliougundua wa kutukuza siku ya ufufuo, alitupa laumu kwa Wayahudi kwamba Sabato ni ya Kiyahudi, wakati wakristo walikuwa wanafurahia siku ya ufufuo. Aliwaelekeza watu waone kuwa Sabato ya siku ya Saba ni ya huzuni na masikitiko tu, kwa hiyo haifai. Hii ilikuwa chuki kwa Wayahudi. TU 15.4

Mfalme Constantine aliamua kuwa Jumapili iwe siku ya kupunzika katika Dola yake yote. Siku ya jua ilitukuzwa na watu wake ambao ni wapagani, na wakristo pia wakaitukuza. Makasisi wa makanisa wakatilia mkazo amri hiyo maana ndio waliomshauri mfalme atoe amri hiyo. Makasisi kwa kutaka vyeo walidhani kuwa kama watu wote, wakafiri na wakristo pia wakiitukuza siku hiyo ya jua, ukuu wa kanisa utaenea na kuwa na mvuto zaidi. Lakini watu wa Mungu waliendelea kutukuza Sabato ya kweli, ingawa walianza polepole kuitukuza Jumapili kama ilivyoamriwa na mfalme. TU 16.1

Mchanganyaji mkuu alikuwa hajamaliza kazi yake bado. Alijihusisha kabisa katika kutumia uwezo wake kwa njia ya naibu wake mwenye kiburi anayejidai kuwa wakili wa Kristo (Papa). Halmashauri kubwa zilifanyika ambazo ziliidhinisha cheo hicho na kukitangaza ulimwenguni pote. Karibu kila baraza lililofanyika, Sabato ilishambuliwa kidogo, na jumapili ilitukuzwa. Hivyo sikukuu ya kipagani mwishowe ikapewa heshima kama siku ya Mungu, na Sabato ya Mungu ikatajwa kuwa ni siku ya Wayahudi kwa hiyo ikatajwa kuwa ni siku ya Wayahudi, kwa hiyo ikapigwa marufuku. TU 16.2

Uasi ukafaulu kujitukuza kama “Mungu na kuabudiwa” 2 Thes. 2:4. Amethubutu kubadili amri ya Mungu inayomtaja Mungu kuwa Mungu wa kweli aliye hai. Katika amri ya nne Mungu anadhihirishwa kwamba ni Muumba. Siku ya saba ya juma ilitakaswa na kutengwa kuwa siku ya kupumzika kwa wanadamu, ikimkumbusha kwamba Mungu ndiye muumbaji na siku hiyo ndiyo ya kuabudu. Shetani alijitahidi kumgeuza mwanadamu asiitii sheria ya Mungu na kwa hiyo shambulio lake, lilielekezwa kwa amri ya nne ambayo inamtaja Mungu kuwa Muumbaji. TU 16.3

Sasa Waprotestanti husema kwamba ufufuo wa Kristo siku ya Jumapili, huifanya siku hiyo iwe Sabato ya Kikristo. Lakini hakuna heshima ya namna hiyo iliyotolewa na Yesu au mitume. Utunzaji wa Jumapili ulianzia kwenye “Siri ya kuasi”. (2Thes. 2:7) ambayo ilianza kuonekana hata siku za Paulo. Itatolea sababu gani ya badiliko kama hilo, ambalo halikuidhinishwa na Biblia? TU 16.4

Katika karne ya sita askofu wa rumi alitajwa kuwa kichwa cha kanisa lote. Ukafiri umeingiza upapa. Joka amempa mnyama “uwezo wake na kiti chake, na mamlaka kuu” Ufu. 13:2. TU 16.5

Sasa imeanza miaka 1260 ya mateso ya mapapa ambayo ilitabiriwa na Unabii wa Danieli 7:25 na Ufunuo 13:5-7. Wakristo walilazimika kuchagua moja kati ya mambo mawili. Kukana Imani yao na kukubaliana na mipango ya ibada ya Rumi; au kuteseka vifungoni na kupoteza maisha yao. Sasa maneno ya Yesu yalitimia, yasemayo: “Mtasalitiwa na wazazi, na ndugu na jamaa na marafiki; na baadhi yenu mtauawa. Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu” Luka 21:16-17. TU 17.1

Dunia ikawa uwanja wa vita. Kwa miaka mamia kanisa la Mungu lilikuwa katika msukosuko mkuu. Watu wakawa wakiishi mafichoni tu. “Mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengezwa na Mungu, ili wamlishe huko Muda wa siku elfu na mia mbili na sitini” Ufunuo 12:6 TU 17.2

Kule kutawala kwa kanisa la Kirumi kuliko wa mwanzo wa wakati wa Giza. Imani kwa Kristo ilihamishiwa kuwa kwa papa wa Rumi. Badala ya kumtegemea Kristo mwana wa Mungu kuwa ndiye mwondoa dhambi, na mwenye uzima wa milele, watu watalazimishwa kwa papa wa Rumi na kwa maaskofu ambao papa amewapa mamlaka. Papa alikuwa ndiye mwombezi wao. Kwao alikuwa kama Mungu. Mtu aliyepinga maongozi yake alistahili hukumu. Kwa njia hiyo mawazo ya watu waligeuzwa upande, kutoka kwa Mungu kuelekea kwa binadamu mwenye dhambi, aliye katili, na kwa mkuu wa giza mwenyewe ambaye hutumia uwezo wake kuwapotosha. Wakati maneno matakatifu ya Biblia yanapoachwa, mtu hujivuna na kujitukuza na kutumbukia katika upotofu.

Siku Za Hatari Kwa Kanisa

Watu waaminifu walioshikilia ukweli walikuwa wachache. Wakati fulani ilionekana kana kwamba ubaya utatawala na kufunika ukweli kabisa. Kiasi cha kutoweka nchini. Injili ilitoweka na watu walishikilia tu mambo yaliyoshurutishwa kufanya. Walifundishwa kutegemea matendo yao mema ili kuwatakasa, na kuwaondolea dhambi. Waliambiwa mambo mengi sana yawezayo kuwapatanisha na Mungu na kuwapa haki ya kuwa watakatifu mbele za Mungu. Baadhi ya mambo hayo ni: kwenda safari ndefu za kuhiji, kulipa kitubio, kuabudu watakatifu kujenga makanisa, mahali patakatifu, madhabahu, kutoa mali nyingi kanisani. Mambo hayo yangewaletea upendeleo mbele za Mungu. TU 17.4

Panapo mwisho wa karne ya nane, wafuasi wa kanisa la Rumi (Roma Catholic) walidai kwamba kwenye karne za mwisho wa kanisa askofu wa Rumi alikuwa na uwezo katika mambo ya kiroho ambao unaonekana siku hizi. Maandiko ya kwanza yalikosewa na watawa. Maamuzi ya mabaraza ambayo yalikuwa hayajasikiwa yaligunduliwa, nayo yanamwezesha Papa kuwa na madaraka makuu ulimwenguni pote. Maamuzi haya ni ya mwanzoni kabisa. TU 17.5

Waaminifu wachache ambao wanasimama katika msingi wa kweli (Kor. 3:10-11) walitatanika. Wakiwa wamechoshwa na mapambano ya daima juu ya kweli na uongo, na mateso yasiyokoma na matatizo ya kila aina ambayo shetani amewaletea, baadhi yao walikata tamaa. Kwa ajili ya kuhofia maisha yao na mali zao, waliacha unyofu wao, wakaondoka katika msingi wa kweli. Wengine walikuwa majasiri katika kupingana na adui zao. TU 18.1

Ibada ya sanamu ilienea pote. Mishumaa iliwashwa mbele ya sanamu, na watu walizifanyia ibada na maombi. Matendo ya kipumbavu yalienea kuhusu dini. Watu wakajifanyia mambo tu bila kufikiri. Wakati huo huo, maaskofu na makasisi walikuwa wametopea katika anasa na ufedhuli, ambavyo watu waliwatazamia katika kuwaongoza. Hivyo watu wakafungwa katika ujinga na ubaradhuli. TU 18.2

Katika karne ya kumi na moja, Papa Greory VII alidai kuwa kanisa kamwe halijakosa hata kidogo wala halitakosa kamwe kama maandiko yasemavyo. Lakini maandiko hayadhibitishi madai hayo. Hata papa wa Rumi mwenye majivuno pia adai kuwa anao uwezo wa kuwaondoa wafalme katika utawala. Kithibitisho cha majivuno hayo kilikuwa kivitendo kilichotendwa kwa mfalme wa ujerumani, Henry IV. Kwa kuwa hakujali Papa, alizuiliwa na kutolewa katika utawala kwa njia ya amri ya papa kuwaamuru watoto wake mwenyewe wamwasi. TU 18.3

Henry aliona kuwa ni lazima akaungame kwa Papa. Aliondoka Ujerumani yeye na mkewe na mtumishi wake mwaminifu wakasafiri kuvuka milima ya Alps wakati wa baridi, ili akajinyenyekeze mbele ya papa na kuomba msamaha. Alipofika kwa makao ya papa Gregory aliwekwa nje kwenye ukumbi wa baridi, pale akiwa hana kitu cha kujifunika baridi na akiwa hana viatu alisubiri papa amruhusu kufika mbele yake, huko ndani. Alingoja pale siku tatu huku akiomba na kuungama, ndipo aliporuhusiwa kuingia ndani. Hata hivyo aliruhusiwa kutawala kwa masharti. Hivyo papa Gregory alijisifu kuwa anao uwezo wa kuweka na kuondoa kiburi cha wafalme. TU 18.4

Kuna tofauti kubwa kiasi gani baina ya mjivunaji huyu na Kristo. Yeye anayejieleza mwenyewe kuwa anasimama mlangoni akingojea kuingia. Kristo alifundisha kwamba: “Yeyote atakayekuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu”. Mathayo 20:27. TU 18.5

Jinsi Mafundisho ya Uongo Yalivyoingia.

Hata kabla ya kuingia upapa kanisani mafundisho ya kimizimu yalionekana kupokewa kanisani. Watu wengi walikuwa na hali ya mwenendo wa kimizimu, eti wapate kuwavuta wapagani kuingia kanisani. Kwa njia hiyo makosa mabaya sana yaliingizwa kanisani. TU 19.1

Jambo kuu kati ya mafundisho haya ya uongo ni imani kwamba mtu anayo hali ya kutokufa, na kwamba mtu akifa roho yake haifi. Fundisho hilo ndilo lilikuwa msingi wa kanisa la Rumi kuimarisha sala ya wafu, na kumtumaini bikira Maria apate kuwaombea, Kutokana na hapo uzushi ukaibuka kwamba kuna moto wa milele utakaowateketeza waovu bila kuzimika. TU 19.2

Njia ikafunguliwa ya kuingiza uzushi mwingine, kwamba huko ahera kuna mahali pa kutakasia dhambi (purgatory) ambao ni imani ya wamizimu, inayotumika kuwatishia watu na kuwashikilia katika hali ya ushirikina. Uzushi wa aina hiyo hudai kuwako huko ahera kuna mahali pa mateso makali ambayo watu wanaokufa hupitishwa humo kwanza mpaka watakaswe dhambi zao, ndipo huruhusiwa kuingia mbinguni. TU 19.3

Kuna jambo jingine ambalo Rumi hulitumia ili kuzidi kuwaogofya wafuasi wake, nalo ni fundisho juu ya kusamehe dhambi. Msamaha kamili wa dhambi uliahidiwa kwa wote ambao wangejiunga na papa katika vita vyake na adui zake, kwa njia ya kulipa fedha kanisa, ambazo fedha za msamaha wa dhambi zote za zamani, na za sasa na zijazo. Basi walimwaga pesa ili kusamehewa dhambi, na kuwaondoa rafiki na jamaa zao waliokufa ambao wamo katika shimo la mateso. Kwa hiyo Rumi kajaza masanduku na pesa, ambayo ziliwawezesha kuishi kifahari, na huku wakijidai kuwa wanamwakilisha yule ambaye hakuwa na mahali hata pa kulaza kichwa chake. TU 19.4

Huduma ya meza ya Bwana iliondolewa, badala yake akawekwa huduma ya kimizimu, yaani misa (mass). Makuhani wa papa wanajidai kuwa hugeuza ule mkate na ile divai kuwa “mwili na damu ya Kristo halisi”. Kwa kufuru nyingi hujidai kwa kiburi kuwa wanao uwezo wa kumwumba Mungu na kumgeuza mkate na damu kuwa Mungu, ambaye ni Mwumbaji wa vitu vyote. Wakristo walilazimishwa kuinama na kutenda mambo hayo, kwamba ndiyo ibada ya mbinguni. TU 19.5

Katika karne ya kumi na tatu lilianzishwa jambo jingine la kutisha la kipapa ndilo baraza kuu la kuwahukumu wapingaji. Katika mabaraza yao ya siri, shetani na malaika zake ndio waliowaongoza waovu hawa. Malaika wa Mungu alisimama katikati bila kuonekana akiandika mambo yote, historia yao yote, na maamuzi yao ambayo ni ya kutisha. “Babeli mkuu amelewa kwa damu ya watakatifu” Ufunuo 17:5-6. Wafia dini mamilioni wanamlilia Mungu alipize kisasi kwa utawala huu mwasi. TU 20.1

Utawala dhalimu wa kipapa umetawala dunia. Wafalme wa wafalme humwinamia Papa kwa muda wa miaka mamia mafundisho ya Roma yamepokewa sana. Waongozi wake wameheshimiwa na kukubaliwa. Kanisa la Rumi halijastawi na kufaulu kama sasa. TU 20.2

Lakini, “adhuhuri ya upapa ilikuwa usiku wa manane wa ulimwengu”. TU 20.3

Maandiko matakatifu hayakujulikana. Waongozi wa kiapa waliichukia nuru isije ikafichua dhambi zao. Sheria ya Mungu, ambayo ni kipimo cha haki, ilipokuwa imeondolewa, waliishi kifedhuli bila wasiwasi. Majumba ya akina papa na maaskofu yalijaa zinaa na ufedhuli, na ufasiki. Baadhi ya maaskofu walikuwa na hatia ya uasi na uvunjaji wa sheria kiasi cha kutovumiliwa na watawala wa Serikali. Kwa karne nyingi ulaya haikuwa na maendeleo katika elimu, na ustaarabu. Maendeleo ya elimu na ujuzi vimekufa ganzi katika mahali pa Ukristo. TU 20.4

Hayo yamekuwa hivyo kwa sababu neno la Mungu lilipigwa marufuku. 


Sura ya 4: Waldensia Waitetea Imani

Katika muda mrefu wa utawala wa upapa, kulikuwako na mashahidi wa Mungu waliothamini Imani katika Kristo kwamba ndiye Mwombezi na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu. Walishikilia mwongozo wa Biblia kuwa ndio kiongozi maishani, na kuitukuza Sabato ya kweli. Walidhihakiwa na kuitwa wazushi, maandiko waliyoandika yakapigwa marufuku na kuelezwa vibaya au kuharibiwa lakini walisimama imara tu. TU 21.1

Hawajulikani sana, isipokuwa mabarazani walikoshtakiwa. Walionekana kana kwamba ni wazushi, Rumi ilikusudia kuwaharibu wao au maandishi yao. Rumi pia ilijitahidi kuharibu kumbukumbu zote za mambo yao ya ukatili walivyowatendea wapinzani wao, yaani wale ambao hawakukubaliana na mafundisho yao. Kabla mashine za kuchapa vitabu hazijagunduliwa, vitabu vilikuwa vichache sana, kwa hiyo Warumi waliweza kuviharibu kwa urahisi na kuvimaliza. Muda si mrefu Papa alipata uwezo akafaulu kuwafuatilia mbali wale waliompinga. TU 21.2

Katika Uingereza ukristo uliingia na kustawi zamani sana, ambao haukupotoshwa na uasi wa Rumi. Mateso yaliletwa na watawala wakafiri, ndicho kitu kilichowapata huko England, walipata hifadhi huko Scotland. Na hivyo ukweli ukafika Ireland. Ukweli huo ulipokea kwa furaha na wenyeji wa nchi hizo. TU 21.3

Wakati watu wa Saxon walipovamia Uingereza, ukafiri ulipata nafasi ya kustawi huko, na hivyo wakristo walifukuziwa sehemu zilizo mbali. Kutoka Ireland alikuja Kolumba na wenzake ambao walifanya kazi yao na kuishi katika kisiwa cha Iona. Kati ya wahubiri hao alikuwamo mshika Sabato ya Biblia, na kwa hiyo Sabato ilijulishwa kwa watu. Shule ilianzishwa huko Iona, ambayo iliwatayarisha wahubiri waliokwenda Scotland, Uingereza, Ujerumani na Uswisi na hata Italia.

Roma Yakutana na Dini ya Biblia

Lakini Rumi iliazimu kuiweka Uingereza chini ya utawala wake. Katika karne ya sita wahubiri wake waliwageuza wapagani wa Saxon. Kazi ilivyozidi kuendelea waongozi wa papa walipambana na wakristo halisi wapole, wanyenyekevu, wenye kufuata Biblia, wenye tabia safi. Warumi walikuwa washirikina, watu wa fahari, wenye kiburi cha Kipapa. Rumi ilidai kuwa wakristo hawa hawana budi kumkiri papa na kujinyenyekeza kwake. Waingereza waliwajibu kuwa papa hasa hakuwa mkuu wa kansia, nao watamhesabu tu kama mtu wa kawaida. Hawajui bwana mwingine isipokuwa Kristo tu. TU 21.5

Sasa roho halisi ya upapa ilidhihirika. Kiongozi mmoja wa Rumi alisema: “Kama hamtaki kuwapokeeni ndugu wanaowaletea amani, mtawapokeeni maadui watakaowaleteeni vita! Vita na hila ndivyo vilitumiwa kwa wale walioitetea Biblia, mpaka waharibiwe kabisa, au wakubali kuacha imani yao na kufuata maongozi ya Rumi.” TU 22.1

Katika nchi ambazo zilikuwa mbali na utawala wa Rumi wakristo wa huko waliendelea na imani yao ya kweli bila kupotoshwa na mafundisho ya Rumi, kwa karne nyingi. Wao waliendelea kuiheshimu Biblia na kufuata mwongozo wake. Wakristo waliamini kuwa Sheria ya Mungu ni ya milele, walidumu kutukuza Sabato ya amri ya nne. Makanisa yaliyokuwa na kanuni hii yalionekana katika Afrika ya kati na katika Armenia katika bara la Asia. TU 22.2

Kati ya wale waliopingana na utawala wa papa, watu wa Waldenses walikuwa katika mstari wa mbele, mahali pale makanisa ya Piedomont yaliendelea na utaratibu wao sawia. Lakini wakati ulifika ambao Rumi iliwalazimisha waisalimu amri. Walakini hata hivyo baadhi yao walikataa kuanguka miguuni mwa papa, ila waliendelea kutunza unyofu wao. Ndipo mtengano ulitokea. Wale walioshikilia imani yao ya zamani walijitenga. Baadhi yao walihama makwao katika milima ya Alps wakaenda katika nchi nyingine na huko wakaendelea na imani ya wengine wakakimbilia milimani kwenye mapango na ngome za miamba, huko wakaendelea na imani yao na kumwabudu Mungu kwa uhuru. TU 22.3

Imani yao ilijengwa kwa Neno la Mungu. Wakulima wanyenyekevu hawa ambao wametengwa na ulimwengu hawakuupata ukweli huo kutokana na upinzani na upotovu wa Rumi. Imani yao ilirithiwa toka kwa babu na baba zao. Waliendeleza imani iliyokuwa kwa kanisa la mitume. Kanisa la “Waldenses” wala sio kanisa la majivuno la Rumi, lilikuwa kanisa la kweli la Kristo, ambalo lilikuwa mtunzaji wa hazina kuu ya Mungu iliyotolewa kwa ulimwengu. TU 22.4

Baadhi ya sababu zilizosababisha mtengano na Rumi ilikuwa chuki ya Rumi kwa ajili ya Sabato ya Biblia. Kama ilivyotabiriwa katika Biblia, uwezo wa upapa uliikanyaga sheria ya Mungu mavumbini. Makanisa yalilazimishwa na mapapa kuiheshimu Jumapili badala ya Sabato. Katika makosa yaliyoenea ni kwamba, ingawa watu wa Mungu waliitunza Sabato, pia walistarehe na Jumapili. Jambo hilo halikuwaridhisha viongozi wa Rumi. Walidai kuwa Sabato ipigwe marufuku na kutangazwa kuwa haitakiwi tena wakiwalaani watu walioendelea kuitukuza. TU 23.1

Miaka mamia kabla ya matengenezo ya kanisa kuanza Waldenses walikuwa na Biblia katika lugha yao. Jambo hili lilisababisha mateso yawakabili. Walilitaja kanisa la Rumi kuwa ni kanisa asi, Babeli wa mwisho. Walisimama kiume wakipinga upotofu wa kila hali, ingawa kufanya hivyo kulihatarisha maisha yao. Katika muda mwingi wa uasi Waldeses walipinga majivuno ya Rumi kwamba ndio wakuu wakapinga ibada ya sanamu na kuheshimu watakatifu wa zamani kuwa wanastahili kuabudiwa, waliendelea kuitunza Sabato ya kweli. TU 23.2

Waldenses hawa walipata makao nyuma ya majabali ya milima na chini ya mapango ya miamba, walijificha. Wakimbizi waaminifu hawa, waliwaonyeha watoto wao vilele vya milima vilivyoinuka juu, na kuwasimulia habari za Mungu Muumbaji, ambaye neno lake linadumu milele kuliko milima mirefu hiyo. Mungu ameiweka milima: Hakuna mkono wowote uwezao kuitikisa, isipokuwa uwezo wa Mwenyenzi tu ndio uwezao kuondoa. Kwa hali hiyo hiyo ameweka sheria yake ya milele isiyoweza kuondolewa. Ni rahisi watu kuing'oa milima, kuliko yodi moja ya sheria ya Mungu. Wasafiri hawa hawakunung'unika kwa ajili ya taabu yao, maana katika makao yao ya milima hawakujikuta upweke. Walifurahia uhuru wao wa kumwabudu Mungu. Walimsifu Mungu kwa furaha katika miamba mirefu iliyowazunguka, na majeshi ya warumi hayakuweza kuwanyamazisha wasimwimbie Mungu.

Kanuni za Kweli Zilithaminiwa

Walithamini kanuni za ukweli kuliko nyumba, na mashamba, jamaa, na marafiki, hata maisha yao wenyewe. Tangu kuzaliwa watoto walifundishwa kuheshimu madai ya sheria ya Mungu. Biblia zilikuwa chache; kwa hiyo walifundishwa kukariri na kuweka mioyoni maneno matakatifu ya Biblia. Wengi waliweza kukariri sehemu kubwa ya Agano la kale na Agano Jipya. TU 23.4

Walizoezwa kuvumilia taabu tokea utoto, na kujitegemea katika mambo mengi. Walizoezwa kushika madaraka, kuangalia usemi wao na kuelewa hekima ya kuwa kimya. Neno moja la kipumbavu linaaweza kuleta hatari kwa jamii nzima. Maana watu waliotetea uhuru wa dini waliwindwa sana, sawa na mbwa wa mwitu anavyowinda mawindo yake. TU 24.1

Waldenses walifanya kazi sana kwa uvumilivu ili kujipatia chakula chao. Kila kipande cha nchi milimani, ambacho kilifaa kulimika, kililimwa kwa uangalifu. Watoto walifundishwa kutotumia mali ovyo ovyo. Walifundishwa kuwa na tabia ya kujinyima. Walifundishwa kwamba uwezo wao wote ni wa Mungu. Kwa hiyo wautoe kwa kazi yake. TU 24.2

Makanisa ya Vaudois yalikuwa na imani sawa na makanisa ya siku za mitume. Walishikilia mafundisho ya Biblia tu kuwa ndiyo mwongozo usiokosea, na waliyapinga majivuno ya mapapa kuwa ndiyo mawakili wa Mungu. Wachungaji wao walilisha kundi la Mungu, wala hawakuwa kama mabwana wa Rumi walivyokuwa. Mafundisho yao yalikuwa katika neno la Mungu tu. Watu walikutanika, si katika majengo matukufu, au katika makanisa makubwa yaliyopambwa sana, ila walikutana katika mabonde ya milima chini ya miti, na wakati wa hatari, katika ngome imara milimani, ili wapate kusikia neno la Injili toka kwa watumishi wa Mungu. Walijitahidi kutembelea wagonjwa na kusistiza mfumo wa upendo wa ndugu. Walifanana na Paulo mtengenezaji wa mahema, nao kila mtu alijifunza aina fulani ya ufundi ili aweze kujisaidia kwa njia hiyo. TU 24.3

Vijana walipata mafundisho toka kwa wachungaji wao. Biblia ndiyo ilikuwa kitabu cha mafunzo. Injili ya Mathayo na Yohana pamoja na nyaraka nyingine vilikaririwa na kuwekwa vichwani. TU 24.4

Walijitahidi kuandika maneno matakatifu kwa shida sana, wakati mwingine ndani ya mashimo wakimulika na tochi (kurunzi), au vijinga vya moto. Waliandika fungu kwa fungu. Malaika wa mbinguni waliwazunguka watu hawa waaminifu. TU 24.5

Shetani aliwaongoza mapapa na maaskofu wao kulifukia, lakini kwa njia ya ajabu neno la kweli lilihifadhiwa, bila kupotoshwa kwa muda wote wa karne za giza. Neno la Mungu lilivuka salama katika mawimbi makali ya safina ya Nuhu iliyovuka salama, katika uharibifu. Sawa kama dhahabu na fedha hupatikana kwa kuchimba chini sana ndivyo neno la kweli la Mungu, ambalo ni hazina ya kweli hufunuliwa kwa watu wanyenyekevu, walitafutao kwa bidii kwa njia ya maombi. Mungu alikusudia kuwa neno lake yaani Biblia, kiwe ndicho kitabu cha mafunzo kwa wanadamu ili kimdhihirishe yeye mwenyewe. Kila ukweli unaojulikana ni ufunuo kamili wa tabia ya Mwenyewe. TU 24.6

Vijana wa Waldeses walipomaliza masomo katika shule zao, walitumwa katika shule za Ufaransa na Italia kuendelea na mafunzo ya juu zaidi. Vijana waliotumwa namna hiyo walihatarisha maisha yao, maana walikabiliana na majaribu mengi. Walikabiliana na madanganyo ya shetani, na mivuto mingi ya ufedhuli. Lakini mafundisho waliyopata katika utoto wao huko kwao, yaliwalinda wakasimama imara. TU 25.1

Katika shule hizo walikokwenda hawakuweza kuiga ukorofi wa aina yoyote. Mavazi yao yaliweza kuchukua hazina ya Maandiko matakatifu waliyokuwa nayo, yaani Biblia iliweza kuchukuliwa bila kuonekana; na kwa njia hiyo waliweza kuwafundisha na kuwapa watu wengine waliokuwa na haja ya kujua ukweli. Katika shule hizo waliweza kuongoa watu, na mara nyingi kanuni ya kweli ya msimamo wao iliweza kuenea katika shule nzima. Viongozi wa kipapa hawakuweza kugudua hali kama hiyo ilikotoka.

Vijana Walifundishwa Kuwa Wahubiri

Wakristo wa Vaudois walijisikia kuwa na wajibu wa kuangaza nuru yao kusiko na nuru. Kwa uwezo wa neno lake Mungu walitafuta kuvunjilia mbali utumwa ulioletwa na Rumi. Wachungaji wa Vausois walifanya kazi nje ya nchi yao muda wa miaka mitatu, kabla ya kurudi nyumbani kufanya kazi huko. Kufanya kazi nje kuliwasaidia kuwa wahudumu bora wafaao kukabili hali zote. Vijana hawakuona kuwa watu wa fahari, au matajiri, bali waliowaona kuwa watu wa kufanya kazi ngumu, wakikabili hatari kwa ujasiri, na mara nyingine kupoteza maisha yao. Wahubiri hawa walikwenda wawili wawili sawa kama wale waliotumwa na Yesu. TU 25.3

Kazi hiyo ya kutangaza ukweli wa neno la Mungu iliwahatarisha kabisa, kuwafanya wapingwe na Rumi. Kila mchungaji alijua kazi fulani ya ufundi, hivyo kila mchungaji alifanya kazi ya kuhubiri, huku akifanya kuwa ni fundi wa aina fulani au mfanya biashara. Walichukua nyuzi za hariri, lulu, na vitu vingine, kana kwamba ni wafanya biashara, na kumbe ni wahubiri. Walichukua Biblia au sehemu ya Biblia na kuzificha sana zisionekane, na kwa hekima wakaingiza mafundisho ya Biblia kwa watu kwa njia ya siri. Ilipobidi wakaacha maandiko matakatifu kwa watu waliotaka. TU 25.4

Wahubiri hawa walisafiri katika miji mingi, wakienda kwa miguu na bila viatu, wakiwa na mavazi hafifu. Katika njia zao walimopita makanisa yalijitokeza na damu ya wafia dini ilikuwa mashahidi wa ukweli. Neno la Mungu lilipokelewa kimya kimya katika mioyo ya watu na katika nyumba za watu. TU 26.1

Waldenses waliamini kuwa mwisho wa ulimwengu hauko mbali sana. Walivyokuwa wakisoma Biblia, waliona kuwa wana wajibu wa kuwaonya watu wengine. Walifarijika sana na kujiona kuwa na amani kuu kwa ajili ya kumwamini Yesu Kristo. Nuru ya Injili iliyowamulikia, waliona haja ya kuwamulikia waliokuwa gizani katika vifungo vya mapapa. TU 26.2

Watu wengi walifundishwa na mapapa kuwa matendo yao mema yanatosha kuwaokoa. Kwa hiyo daima walijitumaini. Walijitesa kwa kila hali katika mchafuko wa dhamira zao za dhambi, bila kuona furaha yoyote. Watu maelfu waliishi katika majumba ya watawa, walifunga mara kwa mara, na kujitesa, kukesha usiku kucha, kusujudu, na kujigaragaza katika unyevu, kukalia mawe yenye majimaji kwenda safari ndefu na kadhalika. Walirudia mambo hayo mara kwa mara, bila tumaini lolote mpaka dhamira zao zikafilisika, na mwisho wakaingia makaburini bila chembe ya faraja

Wenye Dhambi Kutazamishwa Kwa Kristo.

Waldenses walitamani kuwapa masikini hawa ujumbe wenye imani katika ahadi za Mungu na kuwatazamisha Kwa kristo ambaye ndiye tumaini lao la pekee la wokovu. Mafundisho wanayoshikilia kwamba matendo mema ya mtu yatamwokoa, ni mafundisho ya uongo. Neema ya mwokozi aliyekufa na kufufuka ndiyo msingi wa dini ya Kikristo. Matengenezo ya watu kwa Kristo, lazima yawe na mshikamano wa hakika kama vile mbavu zinavyoshikamana na mwili, au kama tawi linavyoshikamana na mti. TU 26.4

Mafundisho ya mapapa na maaskofu yamewapotosha watu kiasi cha kumwona Mungu na hata Kristo kuwa ni wakatili sana, wasio na huruma, kwa hiyo lazima maaskofu na mapadri wawepo ili kuombea wenye dhambi. Wale waliofunguliwa giza hilo wakaona nuru ya Injili, hutambua kuwa mtu lazima amwendee Mungu moja kwa moja bila kupitia kwa mwombezi wa kibinadamu, aungame dhambi zake, naye atapata msamaha na amani moyoni mwake. TU 26.5

Kushambulia Ufalme wa Shetani.

Wahubiri wa Vaudois waliendelea kutoa sehemu za Maandiko Matakatifu kwa uangalifu. Nuru ya Injili ilipenya kwa watu wengi, mpaka Jua la haki likang'aa mioyoni mwa watu kwa nguvu za kuponya. Kila mara aliyesikia neno alitamani apate sehemu ya Maandiko, ili ahakikishe yale aliyosikia. TU 27.1

Wengi waliona upuuzi wa maombezi ya watu yaliyofanywa na mapadri kwa wenye dhambi. Wengi walisema kwa furaha, “Kristo ndiye Kuhani wangu. Damu yake ndiyo kafara yangu, madhabahu yake ndilo ungamo langu” Kwa hiyo nuru kuu iliwaangazia watu wengi, ambao ilionekana kana kwamba inawapeleka mbinguni. Hofu yote ya kifo ilitoweka. Sasa walikuwa tayari kuingia gerezani, ikilazimu kwa ajili ya Mwokozi wao. TU 27.2

Neno la Mungu lilisomwa kwa siri, wakati fulani kwa mtu mmoja tu pengine kwa kikundi cha watu, kilichotamani kupata nuru. Wakati mwingine usiku kucha ulitumika kwa kujifunza Biblia kwa njia hiyo. Mara nyingi maneno haya yalitamkwa: “Je, Mungu ataikubali kafara yangu? Je, ataifurahia? Je, atanisamehe?” Majibu kwa maswali hayo yalisomwa: “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha” Mathayo 11:28. TU 27.3

Wahubiri hao walirudi nyumbani kwao kwa furaha ili kuendeleza nuru ya Injili, na kuwasimulia wenzao mambo waliyoona. Waligundua njia safi ya kuwafurahisha na kuwafariji. Maandiko matakatifu yalizungumza katika roho za watu walioyatamini. TU 27.4

Mjumbe wa kweli alikwenda zake. Na mara nyingi hakuulizwa kama atarudi au hatarudi. Watu walikuwa wamejazwa na furaha ya mshangao hata hawakuwa na nafasi ya kumwuliza maswali. Walijiuliza kwamba: Huenda akawa ni malaika aliyetoka mbinguni? TU 27.5

Wakati mwingine mjumbe wa Injili atakuwa amekwenda katika nchi nyingine, au anateseka gerezani, au amekwisha kufia dini na mifupa yake imetawanyika. Lakini maneno anayoyasema kabla ya kuondoka yanaendelea kutenda kazi. TU 27.6

Waongozi wa kipapa waliona hatari itokanayo na watumishi hawa wa Mungu. Waliona kuwa nuru ya Injili inayomulikwa na watu hao itaweza kuenea na kuondoa giza ilililowafunika watu. Nuru hiyo itawaelekeza watu kwa Mungu peke yake, na kuharibu majivuno ya Rumi. TU 27.7

Watu hawa walioshikilia imani ya kanisa la kwanza walikuwa ushindi wa kufunua uongo wa Rumi na uasi wake. Kwa hiyo chuki na mateso yalitokea. Kule kung'ang'ania ukweli wa biblia kukataa kukubaliana na Rumi, kulichemsha chuki na vita

Rumi Yaazimu Kuwaadhibu Waldenses

Sasa ulianzishwa mpango hatari wa kuwasaka watu wa Mungu katika maficho yao ya milimani. Wapelelezi waliwekwa ili kuwachunguza, Basi mara kwa mara, na tena na tena walishambuliwa na kuvurugwa. Makao yao na makanisa yao yaliharibiwa. Watu hawa hawakupatikana na uhalifu wa aina yoyote, isipokuwa walishitakiwa, eti kuwa ibada yao haifuati taratibu za papa. Na adhabu ya kosa hilo ilikuwa mateso makali mno ya ukatili usiosemeka. TU 28.2

Rumi ilipoazimu kuliondolea mbali dhehebu hilo la Wakristo wa Waldenses, tangazo lilitolewa na papa kuwa watu hawa wahesabiwe kuwa wazushi, na hukumu yao ni kuchinjwa. Hawakushitakiwa kwa kosa la uvivu, au uhaini au watangatangaji, bali walishitakiwa kwa kosa la uzushi, wenye kupotosha kondoo, kutoka katika zizi la kweli. Tangazo hilo lilitaka washiriki wote wa kanisa la Rumi kuhusika na kazi ya kuwaharibu wazushi hao. Kivutio kilichowekwa ni kwamba Wote wa watakaoshiriki kazi hiyo watakuwa huru kwa kila jambo wanalodaiwa, kama walikuwa na kesi yoyote iliyofanywa na watu wa Vaudois ilifutwa, na watu wote walikatazwa kutoa msaada wa aina yoyote kwao. Watu wakaruhusiwa kuwanyanga'anya mali zao bila kizuizi. Tangazo hili lilidhihirisha ghadhabu ya joka, wala siyo sauti ya Kristo. Roho ile ile ilimsulubisha Kristo na kuwaua mitume, roho ya kikatili ya Nero kwa watu wa Mungu, ndiyo hiyo iliyowaongoza kuwaangamiza watu wapendwa wa Mungu. TU 28.3

Ingawa mipango ya kuwaangamiza ilikuwa ikitekelezwa lakini watu hawa hawakuacha kutumia wahubiri ili kuendeza ukweli wa Biblia. Waliwindwa sana na kuuawa, lakini damu yao ilikuwa ndiyo maji ya kuotesha mbegu ya Injili. TU 28.4

Hivyo ndivyo Waldenses walivyomshuhudia Mungu Kabla Martin Luther hajatokea. Walipanda mbegu ya matengenezo ya kanisa yaliyoanza siku za Wycliffe yakakuwa mpaka wakati wa Luther, na yataendelea mpaka mwisho wa wakati. 


SURA YA 5: Nuru Yapambazuka Uingereza

Mungu hakuacha neno lake liharibiwe kabisa. Katika nchi kadhaa wa kadhaa za Ulaya watu waliamshwa na roho wa Mungu ili watafute ukweli kama watafutavyo hazina iliyosetirika. Hasa wakielekea kwenye Neno Takatifu la Biblia, walikuwa tayari kulifuata bila kujali vitisho. Ingawa hawakuuelewa ukweli wote. Waligundua mambo mengine yaliyofichwa kwa muda mrefu. TU 30.1

Wakati ulikuwa umefika ili neno la Mungu liweze kutolewa kwa lugha za watu, kila mtu lugha yao. Ulimwengu ulikuwa umekaa gizani, na sasa mapambazuko yalikaribia. TU 30.2

Katika karne ya kumi na nne, nyota ya asubuhi ya matengenezo ya kanisa ilitokea katika Uingereza. John Wycliffe alionekana katika chuo kikuu kuwa mcha Mungu sana na mwenye akili. Chuoni alijifunza utaalamu wa sheria na mambo ya dini. Mambo hayo yalimwandaa kwa kazi kubwa iliyokuwa mbele yake na uhuru wa dini. Alikuwa na elimu nzuri na kanuni imara. Hali hiyo ilimpatia heshima kwa rafiki zake na adui zake pia. Maadui zake walishindwa kudharau kazi ya matengenezo ya kanisa aliyokuwa akishughulikia, kwa ajili ya ujinga waliokuwa nao. Wycliffe alipokuwa angali mwanafunzi chuoni alikuwa akijifunza maandiko matakatifu. Wycliffe aliona upungufu mwingi sana ambavyo hakuweza kupata mahali pa kumridhisha. Katika neno la Mungu alipata jawabu la haja yake ambayo ameitafuta sana bila mafanikio. Hapa katika Biblia ndipo aliona kuwa Kristo ndiye Mwombezi wa pekee wa binadamu. Kwa hiyo alikusudia kuitangaza kweli hiyo aliyogundua. TU 30.3

Wycliffe hakuanza kazi hiyo na upinzani na Rumi mara moja. Lakini kwa kadiri alivyozidi kuona wazi makosa ya mapapa, ndivyo alivyoweza kufundisha ukweli hasa kama ulivyo katika Biblia. Aliona kuwa Rumi imekataa kufuata Biblia, ila inafuata hadithi za kibinadamu tu. Aliwalaumu mapadri kwamba hawafuati Biblia. Akasema kwamba Biblia lazima ifundishwe kwa watu na kufuatwa kama katika kanisa. Alikuwa mhubiri hodari, na maisha yake yalishuhudia mambo yale aliyohubiri. Ujuzi wake wa maandiko matakatifu, maisha yake ya utawa, na ujasiri wake, vilimpatia usikizi wa watu wote. Watu wengi waliona makosa ya kanisa la Rumi. Wakaikubali wazi kweli iliyohubiriwa na Wycliffe, lakini waongozi wa mapapa walijazwa na ghadhabu; wakasema, mtu huyu anapata heshima kuliko yetu. 

Mwepesi Kugundua Kosa.

Wycliffe alikuwa mwepesi wa kugundua kosa na kulitaja wazi bila hofu, ingawa Rumi ililitetea. Wakati alipokuwa kasisi wa mfalme, Wycliffe alipinga kwa ushujaa malipo ya ushuru ambayo papa alidai kwa mfalme wa Uingereza. Majivuno ya papa kwamba anayo mamlaka hata kwa watawala wa nchi, yalikuwa kinyume cha haki na maadili. TU 31.1

Madai ya papa yalichochea uchungu tu kwa watu, lakini mafundisho ya Wyclkiffe yalituliza watu. Kwa hiyo mfalme na mawaziri walikataa kulipa ushuru uliodaiwa na papa. TU 31.2

Maskini waombaji wa watawa walijazana Uingereza, wakatia kasoro ukuu na umaarufu wa taifa. Maisha ya watawa ya kivivu, na hali ya kuombaomba mabarabarani hayakupunguza mapato ya watu tu, bali yalileta hali ya kufanya kazi ionekane kuwa duni. Vijana walipotoshwa na kuharibiwa. Wengine walijiingiza katika hali ya kuwa watawa, bila kuruhusiwa na wazazi wao, bila wao kujua kile wanachotenda. Hali hii ya ufedhuli, ilitokeza hali ya kinyama kabisa, kama Luther alivyoisema baadaye. TU 31.3

Hata wanafunzi wa Chuo kikuu walishawishiwa na hawa watawa wakubali kufuata njia zao. Walipokwisha kunaswa ilikuwa vigumu kujinasua. Wazazi wengi walikataa kutuma watoto wao katika vyuo. Shule zilididimia, na ujinga ulistawi. TU 31.4

Papa alikuwa amewapa watawa hawa uwezo au idhini ya kusikia maungamo ya watu na kuwasamehe makosa yao. Jambo hilo ni asili ya uovu mkuu. Watawa hawa walijitahidi sana kuachilia makosa ya kila namna kwa watu ili kuongeza mapato yao maana mambo yote yalifuatana na malipo. Zawadi zilizowastahili wagonjwa na maskini, ziliingia mifukoni wa hao watawa. Utajiri wa hao watawa uliongezeka na ustawi wao na hali yao ya kianasa ilifilisi taifa. Walakini watawa hao waliendelea kuwashikilia watu katika hali ya ushirikina, na kuwafanya waamini kuwa shughuli zote za kidini ni kutambua utawala wa papa na kuitukuza heshima ya watakatifu pamoja na kutoa vipaji kwa watawa. Kutenda mambo hayo kulitosha kuwafikisha mbinguni. TU 31.5

Wycliffe akielewa vizuri, aligonga kwenye mzizi wa uovu, akieleza kuwa kawaida hiyo wanayoshikilia na kuiamini ni uongo mtupu, kwa hiyo lazima iachwe, na iondolewe. Mahubiri ya Wycliffe yaliamsha maswali na mawazo ya watu. Wengi walitaka kujua kama ni sawa kutafuta msamaha wa Mungu, au msamaha wa papa wa Rumi. “Watawa pamoja na maaskofu wa Rumi walisema, watu hawa (Wycliffe) wanatutafuna kama kanisa Mungu lazima atuokoe, au sivyo taifa litapotea” Watawa hao waombaji alisema kuwa wanafuata kielelezo cha Yesu na wanafunzi wake, ambao waliishi kwa kupata misaada ya upendo wa watu wasome Biblia ili waone ukweli ulivyo. TU 32.1

Wycliffe alianza kuandika vijizuu na kuvitoa kwa watu ili kuyapinga madai ya watawa na kuwaeleza watu katika mafundisho ya Biblia. Hakuna njia nyingine ambayo Wyclife alitumia kubomoa ngome ya uongo iliyojengwa na Rumi kuwashikilia watu katika ujinga. TU 32.2

Wycliffe aliyeitwa kutetea haki ya taji ya Uingereza kwa maingilio ya papa, alichaguliwa kuwa balozi wa Netherlands. Hapo Wycliffe alikutana na mapadri kutoka ufaransa, Italia na Spain. Alipata nafasi ya kuona ndani ya pazia yaliyokuwa yamefichika kwake alipokuwa Uingereza. Wajumbe hawa wa papa walionyesha tabia halisi. Baadaye alirudi Uingereza na bidii mpya ya kuendeleza mafundisho yake. Alitangaza kuwa huko Rumi ni majivuno na udanganyifu tupu ndivyo vilivyoko. Hivyo ndivyo mungu wao. TU 32.3

Aliporudi uingereza Wycliffe aliwekwa na mfalme kuwa kasisi wa Lutterworth. Jambo hili lilithibitisha kuwa mfalme hakuchukizwa na mahubiri yake ya wazi. Mvuto wa Wycliffe ulienea katika nchi yote. TU 32.4

Ngurumo za papa zilikuwa tayari kumlipukia Maazimio matatu ya papa yalitangazwa ili kumnyamazisha kimya huyo mzushi, mwalimu wa uongo. TU 32.5

Matangazo ya papa yalipofika Uingereza yaliamuru kumfunga gerezani huyo mzushi. TU 32.6

Ilionekana wazi kwamba Wycliffe karibu angeingia hatarini. Lakini yule aliyemwambia mtu wa zamani kuwa, “Usiogope…. Mimi ni ngao yako” Mwa. 15:1 Aliunyosha mkono wake kumlinda mtumishi wake. Kifo hakikumpata mtengenezaji wa mambo ya kanisa, bali kilimpata papa aliyeamuru kufungwa kwa Wycliffe. TU 33.1

Kifo cha Gregory XI kilifuatiwa na uchunguzi wa mapapa wawili ambao walioshindana sana. Kila mmoja alijitahidi kuwataka wafuasi wampinge mwenzake na kutoa laana kubwa kwa mwenzake, na kuahidi zawadi kubwa za mbinguni kwa wasaidizi wake. Walishindana wao kwa wao siku nyingi. Kwa hiyo kwa muda Wyclife alipata kustarehe kidogo wakati walipokuwa kipingana wao kwa wao. TU 33.2

Mafarakano hayo pamoja na uovu wote ulioletwa nayo yalitayarisha njia kwa matengenezo ya kanisa, maana watu waliona wazi maongozi ya upapa jinsi yalivyokuwa. Wyclife aliawaambia watu wafikiri na kuona kama mapapa mawili hao na mashindano yao si hakika kwamba wao ni wapinga Kristo! TU 33.3

Wycliffe akikusudia kueneza nuru ya Injili kote katika nchi, alianzisha makundi ya wahubiri, ambao ni watu waongofu wa kweli waliokuwa tayari kueneza ukweli, Watu hawa walihubiri sokoni, katika njia kuu za mjini, waliwafikia wazee na wago-njwa, na maskini wakawasomea habari njema za neema ya Mungu. TU 33.4

Katika chuo cha Oxford Wycliffe alihubiri neno la Mungu katika ukumbi wa chuo. Alitunukiwa heshima ya kuitwa Daktari wa Injili (Gospel Doctor). Lakini kazi kubwa aliyoifanya maishani mwake ni ile ya kutafsiri Biblia katika lugha ya Kiingereza ili kila mtu wa Uingereza aweza kusoma maajabu ya Mungu katika lugha yake. TU 33.5

Alishikwa na Ugonjwa wa Hatari.

Kazi ya Wyclife ilisimama kwa ghafla. Ingawa alikuwa hajafikia umri wa miaka sitini, kazi ngumu aliyoifanya, na shughuli za kujifunza, pamoja na mashambulio ya adui zake vilimdhoofisha sana na kuchakaza afya yake. Mara akashikwa na ugonjwa wa hatari sana. Watawa walidhani kuwa ataungama maovu aliyotenda kwa kupinga msimamo wa kanisa. Kwa hiyo walikwenda chumbani mwake wakitazamia kusikia maungamo yake. Wakamwambia, “Una mauti kinywani mwako. Jutia maovu yako, ukane mbele yetu maneno yote uliyotushutumia” TU 33.6

Wycliffe aliyasikiliza maneno yao hali amenyamaza kimya. Kisha akawaomba wamwinue juu ya kitanda. Halafu akiwakazia macho, alisema kwa ujasiri, kwa sauti kuu iliyokuwa ikiwatetemesha mara nyingi, “Sitakufa, bali nitaishi na nitaendelea kushutumu maovu ya watawa” kwa fadhaha na aibu, watawa hao walitoka kwa haraka chumbani humo. TU 33.7

Wycliffe aliishi na kuweka mikononi mwa watu wa nchi yake silaha kuu ya kuwapigia Warumi, yaani Biblia ambayo ilipangwa na mbingu ili iwaweke huru watu na kuwaangazia na kuwahubiria. Wycliffe alifahamu kuwa imebaki miaka michache ya kufanya kazi hiyo; aliona mapingano yaliyomkabili, lakini akifarijiwa na ahadi za neno la Mungu aliendelea mbele bila kusita. Akiwa na juhudi na moyo wa utendaji, na ujuzi mwingi, alikuwa ameandaliwa na Mungu kwa kazi hii kuu. Wycliffe akiwa kasisi wa Lutterworth, bila kujali dhoruba iliyokuwa ikivuma alijitia kazini mwake kamili. TU 34.1

Mwishowe kazi ilikamilika yaani Biblia ya Kiingereza iliyotafsiriwa ikatokea. Mtengenezaji wa kanisa amefaulu kuwapatia watu wa Uingereza nuru ya neno la Mungu katika lugha yao, ambayo haitazimika kamwe. Ametenda makuu kwa kuvunja ngome ya ujinga na kuwapatia watu uhuru kamili na kuiangazia nuru nchi yake, kuliko shujaa apiganaye vita. TU 34.2

Biblia ilipatikana tu kwa njia ya shida na kazi ngumu. Watu walipenda mno kupata Biblia, hata ikawa hazitoshelezi haja ya watu. Matajiri walinunua Biblia nzima na wengine walipata sehemu ya Biblia. Mara nyingi watu wa familia fulani fulani walishirikiana kununua Biblia moja nzima. Hivyo Biblia ya Wycliffe ilipata njia ya kuingia katika nyumba za watu. TU 34.3

Sasa Wycliffe akafundisha mafundisho ya Kiprotestanti, tofauti na yale ya Kirumi yaana wokovu hupatikana kwa njia ya imani na kwamba Biblia ni kamili hasa haina kasoro. Imani hii mpya ilikubaliwa na kupokelewa na karibu nusu ya watu wa Uingereza. TU 34.4

Kuonekana kwa maandiko kulifadhaisha utawala wa kanisa. Kwa wakati huo haikuwako sheria ya kupiga marufuku Biblia huko Uingereza, maana Biblia ilikuwa haijatafsiriwa katika lugha ya watu. Sheria hiyo iliwekwa baadaye na kusistizwa sana. TU 34.5

Tena waongozi wa papa walifanya njama ya kunyamazisha huyu mtengenezaji wa Kanisa. Kwanza mkutano wa viongozi wa Rumi waliamua kuyaharamisha maandiko ya Wycliffe, yaani kuwa itakuwa ni maandiko haramu. Walipomshawishi mfalme kijana Richard II akakubaliana nao hivyo amri ya kifalme ikatangazwa kuwa mtu ye yote ambaye angeendelea kutoa mambo hayo yaliyopigwa marufuku angetiwa gerezani. TU 34.6

Wycliffe akaomba rufaa kutoka kwa waongozi mpaka kwenye Bunge. Bila hofu aliwashitaki maaskofu mbele ya Bunge la taifa, na akadai matengenezo yafanywe ili kanisa lisitiwe madoa namna hii. Adui zake waliduwaa. Ilitazamiwa kuwa Wycliffe katika uzee wake, akiwa mwenyewe bila rafiki, atashindwa. Lakini badala yake, bunge likisisimka kwa habari za Wycliffe, likayafuta mashitaka yote yaliyotupwa juu ya mtengenezaji wa kanisa. Kwa hiyo Wycliffe aliwekwa huru tena. TU 34.7

Mara ya tatu Wycliffe aliletwa hukumuni tena. Safari hii katika baraza kuu katika ufalme. Hapo kazi ya Wycliffe ingekomeshwa; ndivyo mapapa walivyodhani. Kama wangekamilisha makusudi yao, Wycliffe angetoka barazani kwenda motoni.

Wycliffe Akataa Kukana Imani

Lakini Wycliffe hakukana imani yake na msimamo wake. Alishikilia msimamo wake na kuyakanusha mashitaka yao. Aliwaita wasikilizaji wake mbele ya baraza, na akapima hila na udanganyifu wa washitaki wake, na kuona kuwa maneno yao hayaafikiani na ukweli wowote. Uwezo wa Roho Mtakatifu uliwakalia wasikilizaji. Maneno ya Wycliffe yakachoma nyoyo zao kama mshale wa Bwana uchomavyo. Mashitaka waliyomshitaki kwamba ni mzushi yakawarudia wao wenyewe. TU 35.2

Akauliza, “Mnashindana na nani?” “Mnashindana na binadamu mzee aliyekaribia kuingia kaburini? La, mnashindana na ukweli, ukweli ulio na nguvu kuliko zenu, nao utawashinda” Alivyosema hivyo akaondoka, na wala hakuna mtu aliyethubutu kumzuia. TU 35.3

Kazi ya Wycliffe ilikuwa karibu imekamilika. Lakini mara moja tena alipaswa kutoa ushuhuda wa Injili. Alitakiwa afike mbele ya papa huko Rumi, ambako damu nyingi za watakatifu zilikuwa zimemwagwa. Lakini alipata ugonjwa wa baridi yabisi, kwa hiyo safari ya kwenda Rumi haikuwezekana. Walakini, ingawa sauti yake haikuweza kusikika Rumi aliweza kusikika kwa njia ya barua. Alimwandikia papa barua, ambayo iliandikwa kwa heshima na roho ya Kristo, lakini ilikuwa yenye masuto kwa majivuno ya upapa na hali yao ya ufedhuli. TU 35.4

Wycliffe aliweka mbele ya papa na maaskofu wake upole na unyenyekevu wa Kristo, akithibitisha kuwa hivyo ndivyo hali ambayo wao na wakristo wote wanapaswa kuiga. Wao wanajidai kuwa wajumbe wake, hali hawafanani naye. TU 35.5

Wyclife alitazamia kuwa maisha yake yangekuwa kafara ya uaminifu wake, yaani angeuawa. TU 36.1

Mfalme, papa na maaskofu wote waliungana ili kumwangamiza. Na ilionekana kuwa isingepita miezi mingi kabla hajauawa. Lakini hata hivyo ujasiri wake haukutishika. TU 36.2

Mtu ambaye alikuwa ameitetea kweli maisha yake yote, asingekufa kwa ajili ya chuki ya adui zake. Bwana alikuwa mlinzi wake, na sasa wakati maadui zake walipoona wazi kuwa angeangamia, Bwana alimhamisha na kumweka mahali pengine mbali nao. Katika kanisa la Lutterworth, alipokuwa akiandaa huduma ya Meza ya Bwna, alishikwa na ugonjwa wa kupooza na kwa muda mfupi akakata roho.

Ujumbe wa mwanzo Mpya.

Mungu alikuwa ameweka neno la kweli kinywani mwa Wycliffe. Maisha yake yalilindwa na kazi yake ilirefushwa mpaka misingi ya matengenezo ya kanisa iliwekwa. Hapakuwa na mtu aliyemtangulia Wycliffe, ambaye aliweka kielelezo cha kazi ya matengenezo. Alikuwa mjumbe mwanzo mpya. Walakini ukweli alioutangaza ulikuwa na mwungano na ukamilifu, ambao wale waliofuata baadaye hawakupata cha kuongeza, na hata wengine hawakufikia pale. Kazi yake ilikuwa kamili na imara, haikuhitaji marekebisho. TU 36.4

Kazi kuu ya kuondoa watu katika giza la Rumi, ambayo Wyclife aliianzisha inatokana na Biblia. Hapo ndipo mibaraka yote inapobubujika ambayo inawafikia watu waache ujinga na kuamini kuwa Rumi na mafundisho yake haikosei. Kwamba mambo yote ya Rumi lazima yakubaliwe bila swali. Mambo hayo yameshikwa kwa muda wa miaka maelfu. Wycliffe aliwafundisha watu kusikia sauti ya Mungu tu katika neno lake basi. Badala ya sauti ya kanisa kupitia kwa papa, lazima watu waitii sauti ya Biblia tu. Kwamba mtafsiri wa Biblia ni Roho mtakatifu, siye papa. TU 36.5

Wyclife alikuwa mtengenezaji wa kanisa mashuhuri kabisa. Alilingana na watu wachache tu waliomfuata baadaye. Alikuwa mtu mwongofu, hodari katika kujifunza, mwenye bidii kazini, na mwenye upendo wa kikristo, mwenye tabia safi, na mtangulizi katika watengenezaji wa kanisa. TU 36.6

Biblia ndiyo iliyomfanya awe jinsi alivyokuwa. Kujifunza biblia kutabadilisha kila wazo na fikra na kuhekimisha, ambavyo hakuna majifunzo ya namna nyingine yawezayo kufanya hivyo. Huuimarisha makusudi, na kuongeza ujasiri. Matakatifu kwa kicho, kutawapa watu wa ulimwengu ufahamu zaidi wa hali ya juu pamoja na kanuni bora kuliko vile vilivyopatikana katika vituo bora vya kufundishia ambavyo vinatumika ulimwenguni. TU 37.1

Wafuasi wa Wycliffe waliojulikana kama Wycliffites na Lolards, walitawanyika katika nchi nyingine wakiieneza injili. Sasa kwa kuwa kiongozi wao amefariki, wao walifanya kazi kwa bidii zaidi kuliko zamani. Makundi ya watu walifurika kuja kusikiliza. Watu mashuhuri hata mke wa mfalme walikuwa ni baadhi ya waongofu. Mahali pengi sanamu zilizofanywa na Warumi, ziliondolewa makanisani TU 37.2

Lakini muda mfupi tu baadaye, mateso ya kikatili yalilipuka kwa wale walioshikilia imani ya Biblia kama mwongozo wao. Kwa mara ya kwanza, katika hisoria ya Uingereza amri ilipitishwa kwamba wale wanaoiamini injili wachomwe moto, huku wakifungwa mitini. Mauaji ya kufia dini yakafuatana mfululizo: Waumini wa Injili wakawindwa kama maadui na wasaliti wa serikali. Walakini watu hawa waaminifu waliendelea kuhubiri kwa siri, mahali mahali wakijifichaficha nyumbani mwa watu maskini na hata mbali mapangoni mwa milima. TU 37.3

Upingaji wa dini ya uongo na uharibifu wa kawaida zote zilizoingizwa na Rumi uliendela kwa karne nyingi. Wakristo wa siku hizo walimpenda Mungu kabisa na kulitii neno lake na kwa hiyo walivumilia mateso kwa furaha. Wengi waliacha mali zao kwa ajili ya Kristo. Wale waliachwa kukaa salama, waliwasaidia ndugu zao walioteswa bila kinyongo. Na wao waliposhambuliwa na kufukuzwa hawakunung'unika. Wale walipata mateso kwa ajili ya ukweli wa neno la Mungu hawakuwa wachache. Na wote walifurahi kwa ajili ya kuteseka pamoja na Kristo. TU 37.4

Mapapa hawakuridhika kwamba mwili wa Wycliffe umezikwa kaburini, la. Baada ya kupita miaka zaidi ya arobaini tangu Wycliffe afe, walichimbua mifupa yake wakaichoma hadharani ili kuonesha chuki yao na majivu yake wakayatupa mtoni. Mwandishi mmoja alisema, “Mto huo uliyachukua majibu hayo mpaka mto wa Avon, Avon mpaka Sevem, Sevem mpaka bahari ndogo, toka hapa yatafikishwa katika bahari kuu. Hivyo majivu ya Wyclife ni mfano wa mafundisho yake, ambayo sasa yametawanyika na kuenea ulimwenguni.” TU 37.5

John Huss wa Bohemia aliongolewa na maandishi ya Wycliffe, akakataa makosa mengi ya Warumi. Kutoka Bohemia kazi iliendela na kufika katika nchi nyingine. Mkono wa Mungu ulikuwa unaandaa matengenezo makuu zaidi ya kanisa. TU 38.1

Picha mbili Zilimvutia Huss

Wakati ule ule wageni wawili walitoka Uingereza wenye elimu, walikuwa wamepokea nuru ya Injili, nao wamekuja kuendeleza Prague. Haukupita muda mrefu, wakanyamazishwa, lakini kwa kuwa hawakutaka kuacha kusudi lao, wakatumia njia nyingine. Kwa kuwa walikuwa wachoraji wa picha pamoja na kuhubiri, wakachora picha mbili. Moja ilionyesha maingilio ya Yesu katika Yerusalemu, akiwa mpole, amepanda mwanapunda, (Mathayo 21:5) akifuatwa na wanafunzi wake wakiwa na mavazi ya vivi hivi na bila viatu. Picha nyingine ilikuwa na msafara wa Papa, akiwa na mavazi yake rasmi na taji yenye kung'aa akipanda farasi aliyepambwa vizuri, akitangulia na wenye matarumbeta, na kufuatwa na maaskofu katika mavazi yao rasmi. TU 40.2

Watu wakakusanyika kuja kuangalia picha zao. Hakuna mtu ambaye alikosa kuzitambua. Kulikuwa na msukosuko mkubwa huko Prague, hata ikabidi wale wageni waondoke na kwenda zao. Lakini picha zile zilimwingia Huss moyoni sana, hata ikabidi asome sana maandiko ya Wycliffe na kuyatafakari. TU 40.3

Ingawa alikuwa bado hajakubali mafundisho yote ya Wycliffe aliona tabia halisi ya papa, naye akalaani majivuno, kutakabari, na upotovu wa upapa

Prague Iliwekwa Chini ya Karantini

Habari zilifika Rumi, na Huss akaitwa mbele ya papa. Kama akienda matokeo ni kifo tu. Mfalme na malkia wa Bohemia jamii ya Chuo Kikuu, watu mashuhuri wa wakuu wa serikali wote wakaungana kumsihi papa amwache Huss akae Prague asiende Rumi ili ajibu kwa kutuma mjumbe. Badala yake papa alitoa hukumu ya Huss na akautangazia mji wa Prague kuwa umewekwa chini ya karantini. TU 40.5

Hukumu ya papa katika TU 41.1

kipindi hicho iliwashtua watu. Watu walimhesabu papa kuwa mwakilishi wa Mungu, kwamba yeye anazo funguo za mbinguni na za kuzimuni pia na waliamini kuwa papa asipopendezwa, hawezi kumtoa mtu aliyekufa kutoka ahera na kuingia raha ya milele. Huduma zote za kidini zilikomeshwa. Makanisa yalifunga. Ndoa zilifungiwa katika uwanja wa kanisa. Wafu walizikwa bila kufanyiwa ibada, na wakazikwa popote mahandakini au mbugani. TU 41.2

Prague ilijaa ghasia nyingi. Watu walimlamu Huss, wakasema kuwa atolewe aende Rumi. Ili kutuliza ghasia, Huss aliondoka akaenda kwao kijijini. Lakini hakukoma kufanya kazi yake, ila alisafiri safari akiwahubiria watu waliopendezwa. Ghasia zilipopungua huko Prague Huss alirudi huko kulihubiri neno la Mungu. Maadui zake walikuwa hodari lakini Malkia pamoja na watu wengine mashuhuri walikuwa rafiki zake, na watu wengi pia walikuwa upande wake. TU 41.3

Huss alisimama mwenyewe katika kazi. Halafu Jerome aliungana naye. Watu hawa wawili waliungana kikamilifu hata mauti haikuwatenga. Sifa bora ndizo zilizofanya tabia zao zifae, Huss alikuwa nazo zaidi. Jerome ambaye alikuwa mnyenyekevu alikubaliana na Huss kamili. Wote kwa pamoja wakaieneza kazi ya matengenezo ya kanisa na kuisukuma mbele. TU 41.4

Mungu aliwajalia watu hawa kupata nuru, na kuwaonyesha makosa mengi ya kanisa la Rumi. Walakini hawakupata nuru yoyote iliyotakiwa kutolewa kwa ulimwengu. Mungu alikuwa akiwaongoza watu polepole kutoka katika giza la Rumi, hatua kwa hatua maana wasingeweza kupata yote mara moja na kuyachukua. Ni sawa na mwanga wa jua kwa wote walio gizani, huwazukia kidogo kidogo, ama kama nuru ingewazukia yote ingewapoteza. Kwa hiyo Mungu aliwafunulia taratibu. TU 41.5

Farakano kanisani liliendelea. Sasa mapapa watatu walikuwa wakishindania ukubwa. Mashindano yao yalileta fujo nyingi katika ukristo. Hawakutosheka na kulaumiana peke yake, lakini kila mmoja alitafuta silaha na askari. Bila shaka fedha zilikuwa lazima zipatikane. Kwa hiyo zawadi, vyeo na mibaraka ya kanisa vikatolewa kwa kuuzwa. TU 41.6

Kwa ujasiri Huss akaunguruma kuhusu machafuko hayo ambayo ni machukizo yanayoleta aibu kwa dini. Akashambulia kwa ushujaa kabisa. Watu wakailaumu Rumi wazi kuwa inaaibisha dini. TU 41.7

Mara tena Praggue ikaonekana kuwa kwenye ukingo wa kumwaga damu kwa mapambano. Kama ilivyokuwa zamani mtumishi wa Mungu alivyolaumiwa kuwa “Mtaabisha Israeli” 1 Fal. 18:17. Mji ukawekwa tena chini ya karantini na Huss akaondoka kwenda kwao kijijini. Ilimpasa aseme kwa nguvu zaidi kuhusu ukristo kabla hajauawa kama mashahidi wa kweli. TU 41.8

Baraza kuu liliitishwa kukutana huko Constance (Kusini Magharibi ya Ujerumani). Liliitishwa kwa matakwa ya mfalme Sigismud, kwa ajili ya mmoja wa wale mapapa watatu, aitwaye John XXIII. Papa John, mwenye tabia ya vivi hivi, ndiye alishika kazi ya uchunguzi. Naye hakuweza kupinga matakwa ya mfalme Sigismund. Kusudi la baraza hili lilikuwa ni kutafuta njia ya kumaliza farakano lililomo kanisani; na kung'olea mbali mizizi ya uzushi. Wale mapapa wawili aliokuwa wanashindana walitakiwa wafike barazani pamoja na John Huss. Wale mapapa waliwakilishwa na wajumbe. Papa John alikuwa na wasiwasi sana, akiogopa asije akatakiwa kueleza sababu za kuhafifisha umaarufu wa taji yao na heshima yao. Walakini aliingia katika mji wa Constance kwa fahari na kishindo akifuatana na makasisi, na wafuasi wa mfalme. Juu ya kichwa chake alikuwa na chombo cha dhahabu kikishikiliwa na mahakimu wanne. Mkate wa kufanyia ibada ya pasaka ulikuwa umechukuliwa mbele yake na mavazi ya maaskofu na wakuu wote, yalikamilisha onekano la fahari kuu. TU 42.1

Wakati huo huo msafiri mwingine pia alikuwa akija Constance. Huss aliagana na rafiki zake akienda Constance kana kwamba hawataonana kamwe. Alisafiri safari ambayo alijisikia kana kwamba anakwenda kuchomwa moto kwenye mti. Alipata mlinzi kutoka kwa mfalme wa Bohemia na mwingine toka kwa Mfalme Sixmund. Lakini alijitayarisha kwa kifo.

Mlinzi Toka kwa Mfalme

Katika barua aliyowaandikia rafiki zake alisema, “Ndugu, zangu ninaondoka nikiwa na mlinzi toka kwa mfalme ili nikakutane na maadui wengi wenye kufisha. Yesu aliteseka kwa ajili ya wapenzi wake; je, sisi tutaona ajabu kufuata kielelezo chake?….. Kwa hiyo wapendwa, ikiwa kifo changu kitamtukuza, ombeni basi ili kije upesi, na kwamba aniwezeshe kusimama kiume katika matatizo yote…. Hebu na tuombe kwa Mungu... kwamba nisivunje hata neno moja la heshim ya Injili, ili niwaachie ndugu zangu kielelezo safi cha kufuata”. TU 42.3

Katika barua nyingine, Huss alisema kwa unyenyekevu makosa aliyofanya ya kufurahia kuvaa mavazi ya fahari na muda liopoteza kwa kufanya mambo hafifu. Akaongeza, Hebu utukufu wa Mungu, na wokovu wa watu vijaze mawazo yenu, wala siyo mali na mashamba. Jihadharini na kupamba nyumba zenu kuliko kupamba mioyo yenu na zaidi ya yote kazaneni na mambo ya kiroho. Mwe wacha Mungu na wanyenyekevu, mkichukuliana na maskini. Msimalize mali zenu kwa ulafi. TU 43.1

Huko Constance Hus alipewa uhuru kamili. Pamoja na mlinzi wa mfalme, papa pia alimwongezea ulinzi zaidi. Lakini pamoja na hayo yote amri ilitoka kwa Papa kwamba Huss akamatwe na kutiwa kifungoni. Baadaye alihamishwa na kufungiwa ngomeni ng'ambo ya mto Rhine, na huko akawa mfungwa hasa. Halafu papa naye alitiwa kifungoni katika ngome ile ile alimokuwa Huss. Alipatikana na hatia ya ufedhuli, uuaji, biashara haramu ya uasherati. Dhambi ambazo hazifai kutajwa kwa mtu kama yeye. Baadaye alinyang'anywa kofia yake ya heshima. Hata wale mapapa waliokuwa wakishindania ukubwa waliondolewa pia, akachaguliwa papa mwingine. TU 43.2

Ingawa papa mwenyewe amepatikana na dhambi kubwa kuliko Huss kama alivyoshitakiwa na mapadri, hata hivyo baraza lile lile lililowashusha mapapa kwa ajili ya ukorofi wao, liliendelea kumwangamiza Huss, mtengenezaji wa kanisa. Kufungwa kwa Huss kuliamsha uchungu mwingi katika nchi ya Bohemia. Mfalme akakataa kwa ujeuri kwamba Huss asishitakiwe. Lakini maadui wa Huss wakaleta mashitaka kwamba, yeye hana imani bali ni mzushi. Wakaendela kushindilia mambo kwake, ingawa alikuwa na ulinzi toka kwa wafalme. TU 43.3

Huss akiteseka kifungoni, mahali penye unyevu, alipata ugonjwa uliomdhoofisha sana. Walakini hata hivyo aliletwa mahakamani kujibu mashitaka. Alisimama mbele ya mfalme akiwa na pingu mikononi na miguuni. Mfalme alikuwa na huruma kwake tangu hapo. Huss alitetea ukweli na kuyataja maovu ya maaskofu wa Rumi Dhahiri. Alipoulizwa kuchagua kati ya kukana imani yake na kuchomwa moto akifungwa mtini, alichagua kufa kuliko kukana ukweli wa imani yake. TU 43.4

Neema ya Mungu ilimsaidia. Wakati alipokuwa anangoja mwisho wake, alikuwa mtulivu na amani ya Mungu ilimjaza. Alisema, “Ninaandika barua hii nikiwa gerezani mkono wangu ukiwa na pingu, huku nikingojea utekelezaji wa hukumu juu yangu kesho…. Wakati tutakapokutana kwa neema ya Mungu huko paradiso, katika maisha ya baadaye, utaelewa jinsi Mungu mwenye rehema alivyojidhihirisha kwangu, jinsi alivyonisaidia, katika majaribu na katika dhiki.” 

Ushindi Unaonekana Kwa Njozi

Katika kifungo chake aliona ushindi wa imani ya kweli kimawazo. Katika ndoto alimwona papa na maaskofu wakiondoa picha ya Kristo ambayo aliyoichora kwenye ukuta huko Prague. Ndoto hiyo ilimwudhi, lakini kesho yake aliona ndoto nyingine yenye picha zaidi ya hiyo iliyofutwa. Aliona picha nyingi, tena zenye kung'aa zaidi zimechorwa kila mahali... Wachoraji... wakiwa wamezungukwa na kundi kubwa la watu wakisema, “Sasa Papa na maaskofu wake na waje waone, hawawezi kuzifuta tena” Mtengenezaji wa kanisa alisema, “Sura ya Kristo haiwezi kufutika kamwe. Wametaka kuiharibu, lakini itachorwa upya mioyoni mwa watu na wahubiri wa Injili vizuri zaidi kuliko mimi” TU 44.2

Mara ya mwisho, Huss aliletwa mahakamani, ambapo palikuwa pamejaa na penye fahari kuu. Palikuwako mfalme, wana wa kifalme, wajumbe, wakuu wa Roma, maaksofu, makasisi na kundi kubwa la watu. TU 44.3

Huss akitakiwa mara ya pili kutoa uamuzi wake: Kukana imani, au kufa, Huss alikanusha kwa nguvu kwamba msimamo wake ni ule ule na kushikilia imani yake. Akimkazia mfalme macho, alisema “Ninaazimu kusimama katika mahakama hii kwa nia yangu mwenyewe, nikiwa na haki ya kupata ulinzi wa taifa, na nikiwa na imani ya mfalme ambaye nasimama mbele yake.” Mfalme Sigismund akabadilika uso, kadri macho ya watu wote walipomtazama. TU 44.4

Baada ya kutamka maneno hayo, hali ya fedheha ilianza. Akisihiwa tena kukana imani, Huss alijibu huku akiwaelekea watu: “Niutazame uso gani? Sio wa mbinguni? Nawezaje kutazama watu ambao niliwahubiri Injili ya kweli? La, nauhesabu wokovu wao kuwa una thamani zaidi ya mwili wangu huu wa kimaskini, ambao umetajwa kwamba ufe” Mavazi ya kikuhani yalianza kuvuliwa moja moja wakati maaskofu wakijitayarisha kumwua huku wakimlaani. Mwisho wakamvalisha kofia ya karatasi ya kiaskofu ambayo ilikuwa imechorwa sanamu za mashetani, maneno yaliyoandikwa kwamba: “Mzushi mkuu” kwa upande. Huss akasema “Furaha kuu”. Yesu, ninavaa taji hii ya aibu kwa ajili yako, ambapo wewe ulivaa taji ya miiba kwa ajili yangu. 

Huss Achomwa Moto Mtini.

Sasa aliongozwa kwenda nje, Kundi kuu la watu lilimfuata. Matayarisho yote ya kuwasha moto yalikamilika, Huss alisihiwa tena ili aungame makosa ili ajiokoe. Akasema, “Nikane nini? Kuna kosa gani? Mimi sijui kosa lolote nililofanya”. “Namwita Mungu awe shahidi kwamba mambo yote niliyohubiri na kuyaandika, yalihusu wokovu wa watu, ili waepukane na dhambi na wasipotee milele. Kwa hiyo ninayo furaha kuu kwa kuuthibitisha ukwelli huo nilioandika na kuhubiri kwa damu yangu mwenyewe”. TU 45.1

Moto ulipowashwa katika mti alikofungiwa, alianza kuimba. “Yesu mwana wa Daudi unihurumie”. Aliendelea kuimba hivyo mpaka sauti yake ikaoma kwa milele, alipomalizikia katika ndimi za moto. Mfuasi wa Papa akizungumza baadaye, kuhusu kifo cha Huss na Jerome ambaye alichomwa moto baada ya Huss, akasema “Huss na Jerome walijitayarisha kwa kufa, kama wanavyojitayarisha kwa arusi. Hawakutoa neno la kulalamika kwa ajili ya maumivu. Moto ulipowashwa wao walianza kuimba. Wala ukali wa moto haukuweza kuzima sauti zao mpaka walipomalizikia humo. Mwili wa Huss ulipokwisha kutetekea majivu yake yalikusanywa na kutupwa katika mto wa Rhine, katika nchi zote mfano wa mbegu inavyotawanyika. Katika nchi ambazo hazikujua ujumbe wa Injili kutatokea matunda mengi, ushuhuda wa Injili. Sauti ya Huss iliyosikika katika mahakama ya Constance ilitoa mwangwi utakaosikika katika vizazi vijavyo. Kielelezo chake kilitia moyo wa imara kwa watu maelefu ili wakikabiliwa na kifo wasiogope. Kifo chake kimethibitisha ulimwenguni ukatili wa Rumi. Maadui wa haki waliendeleza mbele kusudi lao la uharibifu!” TU 45.2

Hata hivyo damu ya shahidi mwingine lazima ishuhudie ukweli. Jerome alikuwa amemtia Huss moyo wa uthabiti, akisema, kwamba ikiwa itamlazimu apate hatari yeye atamsaidia. Aliposikia kuwa Huss amefungwa, Jerome alijitayarisha kutimiza ahadi yake. Hivyo alianza safari ya kwenda Constance bila kuwa na ulinzi wowote. Alipofika alijua kwamba aliingia hatarini na hatamsaidia lolote Huss. Alitoroka, lakini alikamwatwa na kurudishwa kwa pingu. Alipofikishwa mahakamani mara ya kwanza, usemi wake ulikutana na makelele ya mkutano yakisema, “Motoni, Motoni” Kisha alitupwa kifungoni akilishwa chakula haba. Ukatili aliotendewa ulimletea ugonjwa, nusura ya kufa. Hapo adui zake walikuwa na wasiwasi kwamba kama angekufa kwa ugonjwa, wangekuwa wamepoteza tazamio lao la kumchoma motoni, hivyo walimtunza ili asife. Alikaa kifungoni kwa muda wa mwaka mzima. TU 45.3

Jerome Asalimu Amri Mahakamani

Ukatili aliotendewa Huss uliwachukiza watu. Kwa hiyo mahakama ilikusudia kutomchoma Jerome, badala yake wamlazimishe kukana imani yake. Alipewa uchaguzi: Kukana imani au kuchomwa moto akifungwa mtini. Jerome, hali akiwa amedhoofishwa na ugonjwa, na mateso na kifungo na hali ya upweke, pamoja na masikitiko ya kifo cha Huss alisalimu amri. Aliahidi kushikamana na mafundsiho ya Rumi na kuwa na imani yao. Alikubali shauri la mahakama la kuyalaani mafundisho ya Wycliffe na Huss akikubali kuwa ni ukweli wote waliofundisha. TU 46.1

Lakini katika hali yake ya upweke kifungoni alitafakari na kuona alichofanya. Alifikiri juu ya ujasiri wa Huss na jinsi alivyovumilia msalaba kwa ajilia yake. Kabla ya kukana imani yake, alifikiri juu ya faraja aliyopata kwa Mungu katika mateso yake. Sasa alijuta, akaona uchungu moyoni mwake. Alijua kuwa kabla hajaafikiana na Rumi kuna mambo mengine anayotakiwa kuyafanya. Njia ambayo ameshika itamwingiza tu katika uasi mkuu. TU 46.2

Jerome Atubu na Kuwa na Ujasiri

Baada ya muda mfupi Jerome alifikishwa tena mahakamani. Kule kukiri kwa kwanza alikokiri kwamba ameacha imani yake, na kuwa atashikamana na mafundisho ya Rumi hakukuwaridhisha mahakimu. Angejiokoa tu, kwa maungamo kamili kuwa hana uhusiano tena na mafundisho ya kweli. Lakini aliazimu kukanusa maneno yake kwamba ameacha imani yake. Alikusudia kudhihirisha imani yake wazi na kufuata nyayo za mwenzake aliyechomwa moto. Kwa hiyo akafanya hivyo. TU 46.3

Akataka apewe muda wa kujitetea vizuri kama mtu anayekuwa tayari kufa. Maaskofu walisisitiza kwamba Jerome alilaumu ukatili unaotendwa, bila haki, Akasema “Mmenifunga siku mia tatu na arobaini katika gereza chafu sana, mkasikiliza tu mambo ya adui zangu, na ya kwangu mkakataa kuyasikiliza…… Msinitendee dhambi, mkaiacha haki. Kwangu mimi, si kitu, mimi ni mtu dhaifu tu, na maisha yangu hayana maana yoyote, na ninapowasihi msinihukumu kikatili, hujisemea maneno yangu tu sio yenu” TU 47.1

Mwisho walikubali ombi lake. Jerome alipiga magoti mbele ya mahakimu, akaomba Roho wa Mungu ayaongoze mawazo yake, ili asiseme mapotofu. Kwake, siku hiyo ahadi ya Yesu ilitimia, kwamba: “Lakini hapo watakapowapeleka, msifikirifikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema. Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni roho wa Baba yenu aliye ndani yenu” Mathayo 10:19-20. TU 47.2

Kwa muda wa mwaka mzima Jerome alikaa kifungoni, akiwa hawezi kuona wala kusoma. Hata hivyo alipozungumza wakati wa kujitetea, usemi wake ulikuwa wazi na wenye nguvu kama ulivyoandaliwa vema na mtu aliyekuwa na nafasi ya kujitayarisha. Alitaja orodha ndefu ya watu wema ambao walitendewa ukatili na mahakimu waovu. Katika karne zote, watu wanyofu walitafuta kuinua hali za watu walitupwa nje. Kristo mwenyewe alihukumiwa sawa na watenda maovu. Alihukumiwa na mahakimu wasio haki. TU 47.3

Sasa Jerome aliungama makosa aliyofanya safari ya kwanza, aliposema kuwa anaikana imani yake. Sasa alitoa ushuhuda wake wazi na kwamba msimamo wake ni sawa na ule wa Huss, aliyeuawa, yaani mfia dini. Alisema, “Nilimfahamu Huss tangu utoto wake. Alikuwa mtu maarufu, mwenye haki, na mtakatifu. Alihukumiwa, walakini alikuwa mwenye haki …… Hata mimi niko tayari kufa. Sitayaepuka mateso yanayonikabili, ambayo yametayarishwa na adui zangu. Najua kuwa wao ni mashahidi wa uongo, ambao siku moja watatoa hesabu mbele za Mungu ya Matendo yao maovu, maana hakuna kitu asichojua” TU 47.4

Jerome aliendelea kusema, “Dhambi zote nilizotenda tangu utoto wangu, hakuna hata moja inayonishitaki katika dhamira yangu, na kunijutisha, sawa na ile niliyofanya hapa wakati nilipowashutumu Wycliffe na Huss kuwa ni wazushi, hasa Huss ambaye ni bwana wangu na rafiki yangu. Ndiyo na ungama dhambi hiyo kwa moyo wangu wote, kwamba nilikosa kabisa niliposhuhudia kuwa mafundisho yao ni ya uongo, nikiogopa tu kufa. Kwa hiyo usemi huo naukanusha hasa. Mwenyenzi Mungu anisamehe, hasa dhambi hii.” TU 47.5

Akiwasonda mahakimu, alisema kwa ushujaa: “Ninyi mliwahukumu Wycliffe na Huss …. Kwa mambo ambayo hakika yasiyokanika …. Hata mimi pia nafikiri kama wao” TU 48.1

Hotuba yake iliingiliwa kati. Maaskofu wakiwa wamejaa ghadhabu nyingi, walipaza sauti na kusema “Tunahitaji ushahidi gani zaidi? Tumeona kwa macho yetu ukaidi wa mzushi huyu”. TU 48.2

Jerome akisimama imara alisema: “Ninyi, mnadhani kuwa mimi niliogopa kufa? Mmenifunga gerezani mwaka mzima mahali pabaya kabisa, panazidi kifo. Siwezi kueleza hali ya namna hiyo inayotendwa kwa wakristo” TU 48.3

Apangiwa Kufungwa na Kuuawa

Lakini yeye alijibu: “Nionyesheni fungu la Maandiko kuthibitisha kosa langu, nami nitakubali. Mmoja wa washawishi wake alisema,” Maandiko matakatifu ndiyo yenye kuhukumu kitu? Nani atayafahamu yasipotafsiriwa na kanisa? TU 48.4

Jerome akasema, Je, mapokeo ya wanadamu yanathaminiwa kuliko Injili ya Mwokozi? Akajibiwa kwa kishindo, “Mzushi!” Mmoja akasema “Nasikitika kuwa nimepoteza muda wangu bure kukusihi, naona kuwa Ibilisi anakusukuma na amekujaza” TU 48.5

Kabla ya kupita muda mrefu aliongozwa kwenda mahali pale Huss alipochomewa. Alienda akiimba njia nzima. Uso wake uling'aa na alikuwa ametulia kabisa. Hofu ya mauti haikumtisha. Mwenye kuwasha moto alipokuwa tayari, Jerome alimwambia, “Anzia kuwasha upande wa uso wangu, usianzie nyuma, maana kama ningeogopa moto nisingekuwa hapa.” TU 48.6

Maneno yake ya mwisho yalikuwa ni sala “Bwana mwenye uwezo, nihurumie. Unisamehe dhambi zangu maana unajua kuwa mimi nimependa kweli yako siku zote.” Baada ya kuteketea, majivu yake yalikusanywa na kutupwa katika mto wa Rhine, sawasawa na ya Huss. Ndivyo wajumbe wachukuzi wa nuru wa Mungu walivyopotea. TU 49.1

Kifo cha Huss kilileta hasira na ghasia katika Bohemia. Taifa lote lilimtaja kuwa mwalimu mwaminifu, afundishaye kweli ya Injili. Mahakama ilishitakiwa kwa kosa la kuua. Mafundisho ya Huss yaliwavuta watu wengi kuliko hapo zamani. Na watu wengi waliamini. Basi papa na mfalme waliungana pamoja ili kuangamiza watu hawa wenye imani. Kwa hiyo majeshi ya mfalme Sigismund yalimwagwa Bohemia kwa kazi hiyo. TU 49.2

Lakini mkombozi alitokea Ziska, ambaye alikuwa amiri jeshi hodari sana, aliongoza majeshi ya bohemia. Watu hao wakiutumainia msaada wa Mugu waliweza kuyakabili majeshi makuu yaliyowavamia. Mfalme alivamia Bohemia mara nyingi na kila mara majeshi yake yalirudishwa nyuma kwa hasara kubwa. Wafuasi wa Huss walistushwa na kifo cha ukatili, wakawa wakali, wala hakuna kitu kilichoweza kusimama mbele yao. Shujaa Ziska alikufa, na mahali pake pakashikwa na shujaa zaidi jina lake Procopius. TU 49.3

Papa alitangaza vita na wafuasi wa Huss. Kwa hiyo jeshi kuu mno likapelekwa Bohemia kivamizi. Matokeo ni kuwa likashindwa vibaya kwa hasara kuu. Katika nchi zote za Ulaya mahali papa alipokuwa akitawala michango ilianzishwa ya fedha na mali, askari, zana za vita na kadhalika. TU 49.4

Basi jeshi kubwa mno likavamia Bohemia. Watu wakaungana kuwafukuza. Majeshi mawili yakakabiliana ila tu mto uliwatenga. Wavamizi walikuwa wengi mno. Badala ya kuvuka mto na kuwashambulia wafuasi wa Huss, walisimama wakiwatazama wapiganaji. TU 49.5

Kwa ghafla kishindo cha kimuujiza kikawaangukia wavamizi. Mara wakatawanyika kama wanafukuzwa na uwezo usiojulikana. Wafuasi wa Huss wakawakimbiza na kuwaangamiza wengi sana. Vita badala ya kuharibu Bohemia, ilistawisha. TU 49.6

Baada ya miaka michache chini ya papa mwingine, jeshi likatumwa kuvamia Bohemia kwa mguu. Wafuasi wa Huss wakajifanya kukimbia ili wawavute adui waingie katikati ya nchi. Mwisho jeshi la Procopius likawashambulia. Hofu kuu iliwashika hata kabla Wahuss hawajafika. Watu wote wakuu, majemadari, askari wakakimbia huku wakitupa silaha zao chini. Mara hiyo tena wakaangukia mikononi mwa Wahuss. TU 50.1

Mara nyingine tena jeshi lililofundishwa lilipotumwa likakimbizwa na uwezo wa kimuujiza. Aliyempigania Gideon na watu mia tatu, ndiye aliyewapigania wafuasi wa Huss. Zaburi. 7:19-25, Zaburi 53:5 TU 50.2

Walisalitiwa Kijanja

Viongozi wa papa mwishowe walitumia njia ya mazungumzo ya kijanja kama kwamba wana nia njema kumbe sivyo. Makubaliano yalifikiwa ambayo yaliwasaliti watu wa Bohemia, na kuwaweka chini ya mamlala ya Papa yaani utawala wa Rumi. Watu wa Bohemia walitaja masharti manne ya amani baina yao na Rumi (1) Uhuru wa kuhubiri na kufundisha Biblia bila kuingiliwa; (2) Haki ya kanisa zima kutumia mkate na divai wakati wa Meza ya Bwana, na uhuru wa kuabudu kwa kutumia lugha ya watu. (3) Waongozi wa kanisa (maaskofu, mapadri, makasisi na kadhalika) kutojihusisha na mambo ya serikali, wala kuchaguliwa kwenye madaraka serikalini. (4)Kuhusu uvunjaji wa sheria, mahakama za serikali ziwashughulikie wote, wanaohusika, kama ni askofu au mkristo wa kawaida. Utawala wa papa ulikubali mambo hayo manne, ila tu haki ya kuyaeleza na kuyafafanua iwe juu ya baraza ambalo huendeshwa na papa na mfalme. Rumi ikafanikiwa kwa njia ya udanganyifu na hila ambayo ilishindwa kwa njia ya kutumia nguvu. Katika kusafiri na kufafanua masharti ya watu wa Huss, papa alitumia ujanja wa kuyapotosha, na kuonekana kwamba yanatokana na Biblia. Hivyo alifaulu kwa hila kuendeleza upotofu wake. TU 50.3

Watu wengi wa Bohemia walipoona kuwa wamesalitiwa hawakukubali kushikana na mapatano hayo. Ugomvi ukazuka baina yao. Procopius alikufa. Na uhuru wa Bohemia ukaangamia. TU 50.4

Mara nyingine tena majeshi ya kigeni yalivamia Bohemia na wale waliokuwa waaminifu kwa Injili walikabiliwa na mateso ya umwagaji damu. Hata hivyo walisimama kishujaa. Ingawa iliwalazimu kukimbia mapangoni walidumu kusoma neno la Mungu na kuabudu. Kwa njia ya wajumbe watumwa kwa siri kwenda nchi yingine, walielewa kuwa katika milima ya Alps kulikuwepo na kanisa la watu waaminifu wacha Mungu wanaoshika kanuni ya Biblia na kuupinga upotofu wa rumi. Basi wakawa wakiwasiliana na Waldeses kwa furaha, maana ni wenzao katika ukristo. TU 51.1

Watu wa Bohemia wakishikilia kanuni za Biblia walisimama imara wakingoja na hata katika nyakati za giza la mateso makali walizidi kuwa imara kama walinzi wa usiku wangojavyo mapambazuko ya asubuhi. TU 51.2



SURA YA 7: Luther, Shujaa Kwa Wakati Wake

Katika watu waliotumiwa na Mungu kulitoa kanisa katika giza la upapa, na kuwaleta katika nuru ya kweli ya Biblia na imani halisi, Martin Luther ni mmoja wa hao katika mstari wa mbele. Hakujua kuogopa kitu kingine ila Mungu tu, wala hakujua msingi mwingine wa imani, ila ule uliomo katika Biblia. Alikuwa shujaa kwa wakati wake. TU 52.1

Alikulia katika jamaa ya mkulima katika nchi ya Ujerumani. Baba yake alikusudia kuwa afanye kazi ya uanasheria, lakini Mungu alimkusudia awe mjenzi wa hekalu lake ambalo lilikuwa likikua pole pole kwa karne nyingi. Shule ya Mungu iliyomfundisha Luther mpaka akahitimu ilikuwa shida, dhiki na maisha magumu sana. TU 52.2

Baba yake Luther alikuwa mtu hodari, mwenye nia thabiti. Mawazo yake yalimwamisha kuwa maisha ya utawa na kawaida zake, hayafai. Alichukizwa Luther alipoingia katika hali ya utawa bila kumwuliza. Ilipita miaka miwili kabla baba yake Luther hajapatanishwa na mwanawe, hata hivyo nia yake ilikuwa ile ile. TU 52.3

Wazazi wa Luther walijitahidi kuwaelimisha watoto katika neno la Mungu. Juhudi yao ilikuwa ya kuendelea kuwatayarisha watoto wao wafae kutumika maishani, wakati mwingine walikazana kwa uaminifu hata Luther mwenyewe alipendezwa pia na nia hiyo. TU 52.4

Katika shule, Luther alitendewa kikatili. Mara nyingi alishinda na njaa. Hali ya mawazo ya kidini ilimwogofya. Alipolala usiku alikuwa na moyo wa huzuni. Mara nyingi alimdhania Mungu kuwa ni jitu kali lisilo na huruma, kwa wakosaji, kuliko Baba wa mbinguni mwenye huruma. TU 52.5

Alipoingia katika chuo kikuu cha Erfurt, alikuwa na hali nzuri kuliko kwanza. Wazazi wake wakiwa wamejiwekea akiba kidogo, waliweza kumsaidia katika mahitaji yake, na marafiki zake wema waliweza kumfariji ajione nafuu. Kwa njia hiyo hapa mawazo yake alipanuka. Kwa bidii yake mwisho akajikuta juu kati ya wenzake. TU 52.6

Luter hakuacha kuomba kila siku. Roho yake ilikuwa na faraja na maongozi ya juu. Kila mara alisema “Kuomba vema ni bora, ni nusu ya mafundisho” TU 52.7

Siku moja aligundua Biblia ya Kilatini katika maktaba ya Chuo Kikuu. Alikuwa hajaona kitabu hicho. Alikuwa amesikia sehemu ya Injili na nyaraka, ambazo alidhani kuwa ndizo Biblia kamili. Sasa kwa mara ya kwanza katika maisha yake, alisoma neno kamili la Mungu. Sasa kwa mara ya kwanza katika maisha yake, alisoma neno kamili la Mungu. Alisoma kwa kicho na mshangao mkubwa, huku akitulia mara ya kwanza na kusema, “Lo Mungu anijalie nipate Biblia yangu mwenyewe!” Malaika walikuwa karibu naye. Miali ya nuru ya neno la Mungu ilifunua hazina kuu katika mawazo yake. Akajiona wazi kuwa yu mwenye dhambi.TU 53.1

Amani na Mungu

Akitamani kuwa na amani pamoja na Mungu, Luther alijitahidi kuishi katika hali ya utawa. Katika hali hiyo alitakiwa kufanya kazi ngumu sana, yaani kutumika kitumwa, na kuomba omba vitu nyumba kwa nyumba. Alivumilia mambo hayo yote akidhani kuwa hivyo ndiyo njia ya kusamehewa dhambi zake. TU 53.2

Akitumika kwa jinsi hiyo, na kujinyima usingizi saa za kulala, na hata saa za kula pia. Luther alipendelea kusoma biblia kila alipopata nafasi hata kama ni kidogo. Alipata Biblia imefungwa ukutani kwa mnyororo, katika nyumba ya watawa, kwa hiyo alienda kuko kila mara ili kuisoma. TU 53.3

Aliishi maisha ya kitawa kweli kweli. Alifunga kila mara, na kukesha usiku kucha. Alijiadhibu mwenyewe ili kufukuza dhambi zilizomo ndani yake. Baadaye alisema, “Kama watawa wataingia mbinguni kwa njia ya kuishi kitawa, mimi bila shaka nitaingia…. Ikiwa inatakiwa zaidi ya haya, mimi nitaendelea hata kufa!” Pamoja na juhudi hizo zote, lakini Luther hakupata pumziko, wala faraja yoyote. Mwisho alifika ukingoni mwa kukata tamaa. TU 53.4

Ilipoonekana kwamba mambo yote yamekuwa kazi bure. Mungu alimwinulia mwenzi jina Staupitz. Huyu Staupitz, alimfunulia Luther neno la Mungu, mawazo yake yakafunguka. TU 53.5

Staupitz, alimshauri kumtazama Yesu, wala asijitumainie mwenyewe. Akamwambia “Badala ya kujitesa ili usamehewe dhambi, jikabidhi katika mikono ya Mwokozi. Mtumainie yeye na haki yake tu, ukitumainia dhabihu yake kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako. Maana alikufa ili tuishi…. Mwana wa Mungu…. Alifanyika kuwa mwanadamu ili kukupatia uhakika wa rehema za Mungu. …Mpende yeye, maana yeye alikuwepo kwanza.” Maneno ya Staupitz yaliugusa moyo wa Luther, akapata faraja katika moyo wake wenye wasiwasi. TU 53.6

Luther alipofanywa kuwa kasisi, aliitwa kuwa mwalimu katika chuo kikuu cha Wittnemberg. Alianza kufundisha juu ya Zaburi na Injili na Nyaraka kwa makundi ya watu waliokuwa na hamu sana kusikia. Staupitz akamshauri apande mimbarani ili ahubiri. Lakini Luther alijiona kuwa hastahili kuhubiri badala ya Kristo. Baada ya mashindano makubwa ndipo alikubali mashauri ya rafiki yake, yaani ahubiri. Alikuwa mtu hodari katika maandiko na neema ya Mungu ilikuwa juu yake. Maelezo yake ya wazi na ujuzi wake wa maandiko, viliwavutia watu katika kuzibua mioyo yao. TU 54.1

Wakati huo Luther akiwa bado mwana wa kweli wa Rumi, hakudhani kuwa atakuwa mwingine. Alipotakiwa kwenda kuzuru Rumi, alisafiri kwa miguu, akilala katika nyumba za watawa njiani. Alishangazwa fahari aliyoona. Watawa walikuwa wakiishi katika nyumba za fahari kabisa wakivaa mavazi rasmi yenye bei ghali sana, na kula chakula cha kianasa kweli kweli. Mawazo ya Luther yakatatanika. TU 54.2

Baadaye, kwa mbali aliuona mji wa Rumi ukijengwa kwenye vilima saba. Akajitandaza chini akisema “Rumi mtakatifu Nakusalimu!” alizuru makanisa, akisikiliza hadithi za ajabu za mapadri na watawa na kushiriki katika kawaida zote zilizotakiwa. Kila mahali aliona mambo ya ajabu. Maovu yaliyoonekana kati ya viongozi, ufedhuli wa maaskofu vyote vilimstaajabisha. Alishangazwa na upotovu uliotendwa hata wakati wa huduma. Alikuta matendo ya uasherati ulevi na uchafu wa kila namna. Aliandika akisema hatuwezi kuwaza kwamba dhambi mbaya hizi hutendeka Rumi. Watu husema “Kama iko jehanam, Rumi imejengwa juu yake!” TU 54.3

Ukweli Juu ya Ngazi ya Pilato.

Msamaha umeahidiwa na papa kwa mtu yeyote atakayepanda ngazi ya Pilato kwa magoti. Yasemekana ngazi hiyo ililetwa kwa muujiza Rumi toka Yerusalemu. Siku moja Luther alikuwa akizipanda ngazi hizo, wakati aliposikia sauti kama ngurumo ikisema “Mwenye haki ataishi kwa Imani” Warumi 1:17. Mara akasimama kwa hofu na mshangao. Tokea siku hiyo aliona dhahiri jinsi ilivyo upuuzi wa kutegemea matendo mema, kwa wokovu. Akageuzia Rumi uso wake, yaani akaondoa matumaini yake kwa Rumi. Tokea wakati huo nia ya mtengano wa Rumi ikazidi kukua mpaka akavunja uhusiano wote na kanisa la mapapa. TU 54.4

Baada ya kurudi kutoka Rumi Luther alipokea shahada ya juu ya udaktari wa Biblia, yaani “Doctor of Divinity” Sasa alikuwa na uhuru wazi wa kushughulikia mambo ya Biblia kuliko zamani. Hayo ndiyo aliyopenda mno. Alikuwa amejiwekea nadhiri kulihubiri kwa uthabiti neno la Mungu, wala siyo mafundisho ya mapapa. Sasa hakuwa mtawa wa kawaida tu, bali alikuwa mhubiri halali wa Injili, aliyeitwa kuwalisha kondoo wa Mungu ambao wanateseka kwa njaa na kiu ya neno la Mungu. Alitangaza kwa nguvu kwamba, wakristo lazima wapokee mafundiho kutoka kwa Biblia tu, wala si mahali pengine. TU 55.1

Makutano yenye hamu ya neno walimkusanyikia. Habari njema za upendo wa Mwokozi, na msamaha wa dhambi unaopatikana kwa njia ya damu yake vilijaza furaha katika mioyo yao. Huko Wittenberg nuru ya Injili ilikuwa imewashwa tayari, ambayo itazidi kung'aa mpaka mwisho wa wakati. TU 55.2

Lakini kuna mapambano baina ya kweli na kosa. Mwokozi wetu mwenyewe alisema, “Sikuja kuleta amani, ila upanga” Mathayo 10:34. Luther naye alisema badala ya kuanza matengenezo, “Mungu… ananisikuma kwenda mbele…. Natamani kustarehe; lakini nimetupwa katikati ya machafuko na fujo” TU 55.3

Uuzaji wa Msamaha

Kanisa la Rumi lilifanya biashara ya neema ya Mungu. Chini ya ombi la kukusanya fedha za kujengea kanisa la Petro mtakatifu huko Rumi, vyeti vya msamaha wa dhambi vilitolewa kwa kuuzwa, kwa agizo la Papa. Kwa bei ya makosa kanisa lilijengwa ili kumwabudu Mungu. Jambo la namna hii ndilo lililochochea adui za papa wakaanzisha vita, vilivyotetemesha utawala wa Papa, na kuiondoa taji kichwani mwa papa. TU 55.4

Tetzel, ambaye aliwekwa huko Ujerumani ili auze vyeti hivyo vya msamaha wa dhambi, alipatikana na hatia ya kudhulumu watu na kuasi sheria ya Mungu. Lakini aliwekwa kuajiri mradi wa askari wa kukodiwa na papa katika Ujerumani. Alijulikana kwa ulaghai wake wa kudanganya watu wajinga kwa hadithi za ajabu ajabu na kuwahadaa. Kama wangelipokea neno la Mungu wasingalidangayika lakini Biblia iliondolewa kwao, kwa hiyo wakabaki tu katika hali ya ushirikina. TU 55.5

Tetzel alipokuwa akiingia mji fulani mjumbe humtangulia na kutangaza “Neema ya Mungu na ya Baba mtakatifu imewafikieni”. Basi watu humkaribisha mwenye kufuru huyu kama kwamba ndiye Mungu hasa. Tetzel akipanda mimbarani, katika kanisa husifu sana vyeti vya msamaha na kusema kuwa hivyo ndivyo karama ya Mungu ya thamani kwa wanadamu. Husema kuwa kwa njia ya vyeti hivyo dhambi zote ambazo mtu atatenda baadaye husamehewa wala hakuna haja ya kutubu. Cheti kimekamilisha mambo yote. Aliwahakikishia wasikilizaji wake kwamba cheti hicho kina uwezo wa kuokoa mtu aliyekufa; mara ile fedha inapotumbukizwa katika kisanduku. Roho ya marehemu hupita moja kwa moja bila kuingia matesoni kwanza mpaka mbinguni. TU 55.6

Hivyo fedha na dhahabu vikamiminika katika sanduku la Tetzel. Wokovu ulipatikana kwa njia ya kuununua ulikuwa rahisi kuliko wokovu unaopatikana kwa njia ya kutubu. Imani na juhudi ya kupinga majaribu ya dhambi, mpaka upate mtu ushindi. TU 56.1

Luther alijazwa na hofu mno. Wengi hata katika watu wake walikuwa wamenunua vyeti vya msamaha. Mara wakaanza kumjia mchungaji wakiungama dhambi huku wakitazamia kupata ondoleo la dhambi kwa njia hiyo, wala si kwa njia ya kujuta na kuziacha, wakitumaini vyeti kwamba vitawakamilisha. Luther alikataa mambo hayo na kuwaonya kuwa wasipotubu kamili na kugeuka moyo, wataagamia katika dhambi zao. Wakamwendea Tetzel wakilalamika kwamba yeye waliyekwenda kumwungamia, amekataa vyeti vyao, hata wengine wakadai warudishiwe fedha yao. Yule mtawa Tetzel akatoa matusi mazito kwa hasira nyingi, akaagiza moto uwashwe uwanjani, na akasema kuwa ameagizwa na papa kumchoma mtu yoyote atakayeupinga mpango huo mtakatifu. TU 56.2

Kazi ya Luther Yaanza

Sasa sauti ya Luther ikawa ikisikika mimbarani, akitoa maonyo. Aliwaonya watu waziwazi ubaya wa tabia ya kutenda dhambi na ya kwamba mtu hawezi kwa bidii yake kujiondolea hatia ya dhambi, na kuondokana na adhabu yake. Hakuna njia nyingine ya kuondokana na hayo na kutuokoa ila tu ni toba ya kweli na imani kamili kwa Mwokozi aliyetufia. Neema ya Kristo haiwezi kununuliwa, ni kipawachabure. Akawashauri watu wasinunue vyeti vya msamaha ila wamtazame mwokozi aliyesulubishwa kwa imani. Aliwasimulia jinsi alivyojitaabisha ili apate amani, lakini ikawa kazi bure, mpaka alipomwamini Kristo, ndipo akawa na amani na furaha. TU 56.3

Kadri Tetzel alivyoendelea na majivuno yake, Luther alikusudia kumpinga dhahiri. Kanisa la Wittenberg lilikuwa na vitu vya ukumbusho, ambavyo katika siku za sikukuuu huonyesha. Msamaha kamili wa dhambi ulitolewa kwa wote waliofika kanisani, na kuungama. Mojawapo ya sikukuu za namna hiyo ilikuwa karibu kutokea. Luther pia akiungana na msafara huo wa kwenda kanisani, alikwenda akatundika katika mlango wa kanisa maneno tisini na matano yanayopinga uzaji wa vyeti vya msamaha. TU 57.1

Maneno hayo aliyoyatundika liwavutia watu wote. Waliosomwa na kukaririwa kila upande. Mji mzima ukataharuki. Ikaonekana wazi kuwa uwezo wa kusamehe makosa na kuondolea adhabu ya dhambi, haukutolewa kwa papa kamwe, au kwa mtu mwingine yeyote. Ikafahamika kuwa neema ya Mungu na msamaha wa dhambi ni bure kwa wote wanaotubu na kuamini. TU 57.2

Maneno ya Luther yalienea katika nchi yote ya Ujerumani na kwa muda wa majuma machache yalienea Ulaya yote. Watu wengi waliokuwa wafuasi kamili wa Rumi waliyasoma maneno hayo ya Luther kwa furaha kubwa. Wakatambua kuwa hiyo ni sauti ya Mungu. Wakaona kuwa Bwana amenyosha mkono wake ili awatoe watu katika upotovu unaoendeshwa na kanisa la Rumi. Wakuu wa nchi na mahakimu walifurahia kisirisiri kwamba kumetokea kigingi cha kusimamisha majivuno ya upotovu wa Rumi. TU 57.3

Makasisi wenye hila walipoona kuwa pato lao linahatarishwa, walichukizwa mno. Hivyo Luther akakabiliwa na washitaki wenye uchungu sana. Aliposhitakiwa alisema “nani hajui kuwa ni mara chache mno, mtu kuweka kitu kipya bila... kushitakiwa kuwa mchafuzi? Kwa sababu walifanya mambo mapya bila kwanza kujinyenyekeza na kupata idhini ya wakubwa”. TU 57.4

Maalum ya adui za Luther, na kumwelewa kwao vibaya na chuki yao juu yake, vilimfurikia kama gharika. Yeye alitumaini kuwa viongozi watamwunga mkono, kwa hiyo alitulia tu. Katika jaribio lake, aliona matumaini mema na kuamsha kanisa. TU 57.5

Lakini sasa matumaini mema yamegeuka kuwa maalum. Wakuu na viongozi wengi wa kanisa waliona kuwa maneno hayo ya kweli waliyapokea yatadhoofisha mamlaka ya Rumi maana yatakomesha mafuriko ya fedha zinazokuja kwa hazina yake, na hivyo utukufu wa Rumi utafifia. TU 57.6

Kufundisha watu wamtazame Kristo pekee yake kutaangusha utawala wa papa na mwishowe kuangamiza mamlaka yake. Kwa hiyo wakakataa ukweli huu wa kumtazama Kristo kwa kumpinga mtu aliyetumwa na kuwaleta nuru. TU 58.1

Luther alitetemeka alipojifikiria. Mtu mmoja kupingana na uwezo mkuu katika nchi. Aliandika na kusema: “Mimi ni nani nishindane uwezo mkuu wa papa… ambaye wafalme wa nchi na ulimwengu wote humtetemekea?”... Hakuna ajuaye jinsi moyo wangu ulivyofadhaika katika muda wa miaka miwili hii, na jinsi nilivyokata tamaa na kuzama. Lakini msaada wa kibinadamu uliposhindwa alitazama kwa Mungu peke yake. Aliweza kutulia kwa amani katika mkono wa Mungu mwenye nguvu zote. Akimwandikia rafiki yake Luther alisema, “Wajibu wako wa mwanzo ni kuanza na maombi... usitumaini kitu chochote kutoka kwako, kwa uwezo wako, au kwa akili zako. Mtumaini Mungu kamili, katika mvuto wa Roho wake”. Hilo ndilo fundisho kwa watu wote wanaojisikia kuwa wameitwa na Mungu kutoa ujumbe wa kweli kwa wakati huu. Katika mashindano na maovu kunahitajika uwezo zaidi ya ule wa kibinadamu na hekima zaidi ya kibinadamu. TU 58.2

Luther Asimama Na Biblia Tu

Wakati adui za Luther walipokuwa wakitetea mapokeo ya kibinadamu, Luther yeye aliwapinga kwa njia ya kutumia Biblia tu. Nao hawakuweza kumshinda. Kutokana na mahubiri na maandishi ya Luther, machache ya nuru ya Injili yalianza kutokea. Nuru hiyo iliwamulikia watu maelfu. Neno la Mungu lilikuwa kama upanga mkali ukatao kuwili, uliokata mioyo ya watu. Macho ya watu yalifumbwa na mapokeo ya kibinadamu kwa muda mrefu, yalifumbuliwa, wakaacha matumaini ya bure ya kuwatumaini watu ili wapate wokovu. Wakamtumaini kwa imani Kristo, Mwokozi aliyewafia. TU 58.3

Mwamko mkuu huo uliwaogofya watawala wa kipapa. Ndipo Luther akapokea, “kuitwa shaurini” huko Rumi. Rafiki zake walifahamu hatari ya kwenda Rumi ambako kumejaa mauaji ya watakatifu. Wakamshauri asiende Rumi, ila shauri lake lisikilizwe Ujerumani. TU 58.4

Jambo hilo lilikubalika na papa akatuma mjume ili alisikilize huko Ujerumani. Mjumbe alifahamishwa kwamba Luther amekuwa mzushi tayari. Kwa hiyo lazima ashitakiwe bila kuchelewa. Mjumbe alikabidhiwa madaraka ya kumhamisha katika Ujerumani nzima, kumtia kizuizini na kumlaani, kumpiga marufuku na kumtoa katika umoja wa kanisa. Kuwaharamisha watu wote wanaoungana naye. Kuwazuia wote katika vyeo vyote walivyonavyo kanisani na serikalini isipokuwa mfalme atakayepuuza kumkamata Luther na wafuasi wake na kuwatoa wakabidhiwe Rumi. TU 58.5

Hakuna alama ya ukristo wa kweli iliyoonekana katika hati hiyo, wala aina yoyote ya haki. Luther hakuwa na nafasi ya kujitetea, na kuonyesha sababu ya msimamo wake. Walakini alitajwa tu kuwa ni mzushi, na kuhukumiwa pale pale. TU 59.1

Wakati Luther alipokuwa mpweke, na kuhitaji mwenzi, Mungu alimtuma Melanchthon huko Wittenberg, ili amsaidie na kumshauri. Hali ya Melanchthon na tabia yake imara pamoja na hekima yake, vilimpatia sifa njema iliyokubaliwa na watu wote. Mara moja mtu huyo akawa mwenzi mpenzi wa Luther. Uangalifu wake, uaminifu wake na upole wake vilikuwa sifa za kumtia moyo na nguvu Luther. TU 59.2

Huko Augsburg palikuwa pamechaguliwa kuwa mahali pa kusikiliza mambo ya Luther. Na Luther akasafiri kwa miguu kwenda huko. Vitisho vilikuwa vitolewa kwamba ataviziwa njiani na kuuawa, kwa hiyo rafiki zake walimsihi asijihatarishe kusafiri. Lakini jibu lake lilikuwa “Mimi ni mtu anayetaka kuwa mhubiri wa neno la Kristo ulimwenguni hana budi atazamie kifo wakati wowote” TU 59.3

Habari za kwenda kwa Luther huko Augsburg ziliwafurahisha sana wajumbe wa Papa. Mtu mkorofi, anayechafua ulimwengu aonekana sasa kuwa katika uwezo wa Rumi. Hivyo hawataaweza kuepuka. Wajumbe wa papa waliazimu kumlazimisha Luther ili akane imani yake, au kama hilo halitawezekana, wamtie mikononi mwa walinzi, wampeleke Rumi ili akashiriki mambo yaliyowapata akina Huss na Jerome. Hivyo basi, mjumbe wa papa akashauri, kwa njia ya balozi, kwamba wamshawishi Luther asafiri bila mlinzi akitumaini tu bahati yake. Jambo hili lilikataliwa na Luther. Hakukubali kusafiri, mpaka apate kuhakikishwa na mfalme kuwa atamlinda kamili, ndipo atakubali kwenda kuonana na wajumbe wa papa. TU 59.4

Basi, wajumbe wa papa walikusudia kumshawishi Luther kwa ujanja. Wakaonekana kuwa watu wa upendo mwingi kwa Luther. Wakamshauri akubali tu kushikamana na kanisa na kanuni zake bila ubishi, wala kuhojiana. Lakini jawabu la Luther lilionyesha jinsi anavyolipenda kanisa na ukweli wa Biblia. Pia kwamba yuko tayari kujibu maswali yote kuhusu mafundisho yake, na kukubali wakuu wa chuo alikofundisha watoe uamuzi wao juu ya mafundisho yake. Lakini alikanusha mambo ya maaskofu kwamba akane imani yake bila kumthibitishia kosa lake. TU 59.5

Wao walikazana tu kusema, “Kana imani yako! Kana Imani yako”. Luther aliwaonyesha kuwa msimamo wake unatokana na maandiko matakatifu na hakuweza kukana ukweli. Mjumbe wa Papa aliposhindwa kumthibitishia Luther kosa kutokana na Biblia, basi wafuasi wa Rumi wote wakamzomea na kumtukana, wakimwita kuwa mhalifu wa mapokeo ya wazee na mzushi na kadhalika. Wala Luther hakupata nafasi yoyote ya kusema. Baadaye alipata ruhusa ya kutoka kuonyesha majibu yake kwa maandishi. TU 60.1

Alipoandika rafiki yake, alisema, “mambo yaliyoandikwa yanaweza kutumiwa kumhukumu mtu mwingine. Pili, mtu anaweza kutatanika kwa hofu, wala si kwa dhamiri, wakati watu wanapopayuka payuka kwa majivuno na maneno mengi ya ovyo ovyo”. TU 60.2

Wakati mwingine Luther alipofikishwa barazani, alieleza wazi msimamo wake, ukiungwa mkono na maandiko matakatifu. Alisoma maneno yake aliyoyaandika katika karatasi, baada ya kuyasoma kwa sauti wazi, akampa askofu mkuu hiyo karatasi. Askofu mkuu aliitupa kando huku akimlaani Luther na kusema ni mwingi wa maneno maovu ya kivivu yasiyohusu. Sasa Luther akakutana na askofu mwenye kiburi, akamgusa kwenye siri yake. Akagusa mafundsiho wanayofundisha kanisa, ambayo ni mapokeo matupu. TU 60.3

Askofu akijaa na ghadhabu alipaza sauti, “Kana imani hiyo au sivyo nitakupeleka Rumi. Akarudia kusema tena Kana imani, au sivyo hutaonekana tena”. TU 60.4

Basi Luther na rafiki zake wakaondoka huku akisema kuwa wasitazamie kuwa atakana imani. Askofu hakukusudia kuwa mambo yatakuwa hivyo. Basi wakabaki wakitazamana kwa mambo yalivyotokea, na kwamba mpango wao umeshindwa. TU 60.5

Mkutano mkuu uliokutanika uliweza kupima kati ya watu hao wawili, roho ya aina gani waliyo nayo, na misimamo yao. Ukweli ulijidhihirisha uliko. Luther akiwa mtulivu, mwenye ukweli na imara mjumbe wa papa mwenye majivuno bila kuwa na neno lolote la Biblia lenye kumwunga mkono, huku akipiga tu kelele, “Kana imani, au sivyo nitakupeleka Rumi”.TU 60.6

Kuponyoka Kutoka Augsburg

Rafiki za Luther walisema kuwa ni kazi bure kuendelea kukaa Augsburg, kwa hiyo ingefaa aende tu Wittenberg bila kuchelewa, na hadhari kubwa lazima iangaliwe. Basi kesho yake asubuhi mapema akaondoka akiwa amepanda farasi, akifuatana na kiongozi aliyechaguliwa na hakimu. Aliondoka kungali giza akapita katika barabara za mji kisirisiri. Adui zake walikula njama ili wamwangamize. Wakati huo ulikuwa wa wasiwasi na maombi mengi. Alifika mlango mdogo wa ukuta wa mji. Alifunguliwa, akapita pamoja na kiongozi wake. Kabla mjumbe wa papa hajafahamu kuondoka kwa Luther, alikuwa ameenda mbali, na ilikuwa vigumu kumpata. TU 61.1

Mjumbe wa papa alipopata habari kwamba Luther ameponyoka, alighadhabika mno na kujaa uchungu. Alitumaini kujipatia sifa bora kwa kumkomesha mkorofi huyu anayevuruga kanisa. Katika barua aliyomwandikia mfalme Frederick wa Saxony alimlaani Luther kwa uchungu mwingi, akimtaka ampeleke Luther, Rumi au ampige marufuku huko Saxony. TU 61.2

Mfalme Frederick hakuelewa vizuri mafundisho ya Luther lakini alivutiwa sana na ujasiri, na usemi wake. Frederick alimleta Luther mpaka athibitishwe makosa yake. Katika majibu ya barua ya mjumbe wa papa, Frederick alisema “Kwa kuwa Doctor Martim Luther alifika mbele yako huko Augsburg, ungeridhika. Hatukutumaini kuwa ungemlazimisha kukana imani yake, bila kumdhihirishia makosa yake. Hakuna mtu mtaalamu ambaye ameniambia kuwa mafundisho ya Luther ni mapotovu, yampingayo Kristo na ya uasi.” Mfalme aliona kuwa kazi ya matengenezo ya kanisa, ambayo inafanywa na Luther inahitajika sana. Alifurahi sana kwa kuwa hali ya kanisa inaleta mvuto mzuri. TU 61.3

Mwaka mmoja tu ulipita tangu Luther alipotundika yale maneno tisini na matano kwenye mlango wa kanisa. Na maneno hayo yalienea kila mahali, na kusababisha watu wengi wasome maandiko matakatifu. Wanafunzi waliokuja kusoma hapo Witternberg mara ya kwanza waliinua mikono yao mbinguni wakimtukuza Mungu kwa kuwezesha nuru ya Injili kung'aa katika mji huo. TU 61.4

Luther hakuachana na mambo yote ya Rumi, aliyokuwa akifuata. Aliandika na kusema, “Lakini ninaposoma maagizo ya papa …. Nashindwa kuelewa. Sijui papa mwenyewe ndiye mpinga Kristo au mtume wake. Kwa hiyo Kristo huwakilishwa kwao kwa makosa sana na kusulubishwa kwake”. TU 61.5

Rumi ilizidi kukasirishwa na mashambulio ya Luther. Hapa wapinzani washupavu wa Luther madaktari katika vyuo vikuu vya katholiki walitangaza kwamba mtu atakayemwua Luther ataachiliwa dhambi zake kabisa. Lakini Mungu alikuwa mlinzi wake. Mafundisho yake yalisikika kila mahali, mashambani, katika nyumba ndogo, katika nyumba za watawa katika nyumba ya fahari ya wakuu katika vyuo vikuu, na katika majumba ya wafalme. TU 62.1

Wakati ule ule Luther akagundua kuwa ukweli wa kuhesabiwa haki kwa imani ulikuwa unaaminiwa na mtengenezaji mkuu wa kanisa Huss mtu wa Bohemia. Luther alisema “Sisi sote, yaani Paulo, Augustine na mimi, tumekuwa Wahuss tukifuata ukweli huu bila kujua ukweli huu umehubiriwa tangu karne iliyopita; na ukachomwa moto”. TU 62.2

Luther akiandika kuhusu vyuo vikuu alisema: “Naogopa, kwamba vyuo vikuu vitageuka kuwa malango ya jehanam, kama haiwezi kutia nia ya kuchunguza Biblia na kuifuata, na kuifundisha kwa vijana. Kila kituo cha mafunzo ambapo neno la Mungu halijaliwi, lazima kitapotoka” TU 62.3

Jambo hili lilienezwa kote katika Ujerumani. Taifa zima lilitaharuki. Wafuasi wa papa wakamtaka papa amchukulie Luther hatua kali. Basi mara moja amri ikatolewa kuwa mafundisho ya Luther yalaaniwe na kupigwa marufuku. Na tena Luther na wafuasi wake wote, kama hawataikana imani yao waharamishwe. TU 62.4

Hatari Kuu

Jambo hili lililoamriwa lifanyike lilikuwa la hatari kuu kwa matengenezo ya Luther. Hakuwa gizani kuhusu tufani iliyokuwa tayari kuvuma juu yake. Lakini alimtumaini Kristo kwa matokeo yote ambayo yangetokea. Alitamka na kusema: “Yale yatakayotokea, mimi sijui, wala sijishughulishi kuyajua … maana sivyo kama vile jani la mti liangukavyo bila amri kutoka kwa Baba. Basi kama ni hivyo sisi je hutunzwa kiasi gani! Ni jambo rahisi kufa kwa ajili ya Neno, ambaye neno alifanyika kuwa mwili, naye mwenyewe alikufa”. TU 62.5

Wakati amri ya papa ilipomfikia Luther, alisema “Mimi naidharau amri hiyo na kuilaani, maana ni ya kidhalimu tupu. Kristo mwenyewe ndiye anayeshutumiwa. Mimi najisikia kuwa huru rohoni mwangu, maana najua kuwa papa ni mpinga Kristo, na kiti chake cha enzi ni cha Shetani mwenyewe.” TU 62.6

Walakini utawala wa papa haukuwa bila misukosuko. TU 62.7

Watu dhaifu wasio imara walitetemeka kusikia amri hiyo. Wengi walipenda maisha haya. Je, kazi ya Luther mtengenezaji wa kanisa itakwisha? TU 63.1

Luther hakuwa na wasiwawi. Kwa ujasiri mkuu aliilaani Rumi, na kuichomelea mbali amri ya papa mbele ya watu wengi wa hali zote. Akasema, “Mashindano ya ajabu yameanza. Mpaka sasa tumekuwa tukicheza na papa. Mimi nimeanza kazi hizo kwa jina la Mungu, na kazi hii itamalizika bila mimi, ila kwa uwezo wake. Nani ajuaye kama Mungu hakuniteua na kuniita na iwapo hawaogopi kunidharau mimi hawajui kuwa wanamdharau Mungu?” TU 63.2

“Mungu hachagui mtu mkuu wa dunia ili awe nabii au kuhani, bali huteua watu wa hali ya chini, watu wa kawaida tu ambao hudharauliwa na watu, hata wachungaji kama Amosi. Katika kila kizazi watakatifu wa Mungu iliwapasa kukemea hata wafalme, watu wakuu watawala, na wenye hekima; ili wasiangamie dhambini. Sisemi kuwa mimi ni nabii; bali nasema kuwa lazima waogope, kwa sababu niko mmoja na wao ni wengi. Nina hakika ya jambo kwamba neno la Mungu liko ndani yangu na kwamba hawana Neno hilo”. TU 63.3

Walakini Luther alipita katika mashindano makuu alipoamua kutengana na kanisa la Rumi. Alisema, “Lo, ni maumivu kiasi gani yamenipata, ingawa Biblia inaniunga mkono, kwamba ni sawa kabisa kusimama imara katika kupingana na papa, na kumtaja kuwa ni mpinga Kristo! Ni mara ngapi sikujiuliza swali lile la uchungu, ambalo lilikuwa likitamkwa na papa kila mara, kwamba: Je, wewe peke yako ndiwe mwenye hekima? Je, watu wote ni wakosefu, ila wewe tu? Itakuwaje basi ikiwa wewe ndiwe mkosaji na kuwakosesha wengine wapate kuangamia? Hivyo ndivyo nilivyoshindana na nafsi yangu na shetani pia, mpaka Kristo kwa rehema zake aliukaza moyo wangu kwa neno lake lisilo na makosa, nikaondolewa mashaka.” TU 63.4

Amri mpya ya papa ikatokea ya kusema kuwa Luther ameharamishwa kutoka katika kanisa la Rumi, akilaaniwa na kutukanwa vibaya, kama mtu aliyelaaniwa na mbingu. Pamoja na hayo, wote watakaoyafuata mafudnsiho yake, wamelaaniwa pia. TU 63.5

Watu wote walioitwa na Mungu kuupeleka ujumbe kwa wanadamu “watapata mapingamizi” Katika siku za Luther kuliko wako na ukweli uliohusu wakati. Siku hizi kanisa linao ukweli wa wakati huu. Ukweli huu hauthaminiwi na watu kama vile haukuthaminiwa na papa na wenzake siku za Luther. Wanaotangaza ukweli wa wakati huu asitazamie kuwa utapokewa na watu wengi zaidi ya ulivyopokewa hapo mwanzao, siku za akina Luther. Mapambano makuu kati ya kweli na uongo, na kati ya Kristo na Shetani yataendelea na kuzidi mpaka mwisho wa historia ya ulimwengu. Soma Yohana 15:19-20; Luka 6:26. TU 63.6

SURA YA 8

Jasiri wa Kweli

 

Mfalme mpya alikalia kiti cha ufalme wa Ujerumani, ambaye ni Charles V. mtawala Saxony ambaye Charles alikuwa akimtegemea, alimshauri asijihusishe na habari za Luther, mpaka hapo akatapopewa nafasi ya kujitetea mbele zake. Kwa mashauri hayo mfalme alitiwa katika hali ya wasiwasi. Wafuasi wa papa wasingalitosheka na kitu chochote, ila kifo cha Luther. Mfalme wa Saxony alimwambia mfalme Charles V kuwa Luther apatiwe mlinzi ili “aje afike mbele ya wataalamu na watawa na mahakimu wasiopendelea” TU 65.1

Basi mkutano ukakutanika katika mji wa Worms. Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa wakuu wa Ujerumani kukutanika pamoja na mfalme wao kijana. Viongozi wa kanisa wakuu wa serikali na mabalozi kutoka nchi mbalimbali walikutanika huko Worms. Lakini tamasha halisi iliyoutayaharukisha mkutano ilikuwa “Mtengenezaji wa kanisa” yaani Martin Luther. Mfalme Charles aliambiwa mkuu kuja pamoja na Luther, huku akimhakikishia ulinzi kamili na uhuru wa kusema bila kizuizi. Luther alimwandikia mkuu huyu hivi, “kama mfalme ndiye ameniita, siwezi kuwa na wasiwasi, maana ni kama kuitwa na Mungu mwenyewe Kama wanakusudia kunidhuru…. Najikabidi mikononi mwa Bwana… Bwana asiponiokoa maisha yangu hayana faida…. Unaweza kutazamia kila kitu kutoka kwangu... Ila huwezi kunitazamia kukimbia au kukana imani yangu. Kukimbia siwezi, na kukana imani siwezi pia.” TU 65.2

Habari zilipoenea kwamba Luther atasimama mbele ya baraza la wakuu, wasiwasi mwingi ulienea. Alexander, ambaye ndiye mjumbe wa papa, alikasirika mno. Kuhusika katika kesi ambayo papa mwenyewe amekwisha kutoa hukumu na kumpiga mtu huyo marufuku ni jambo baya sana, linalofedhehesha mamlaka ya papa. Alimshauri Charles kutoruhusu kusimama na Luther huko Worms, na kutoruhusu akamshawishi mfalme akubali. Alexander hakutosheka na ushindi huo aliopata wa kumshawishi mfalme bali alijitahidi kusema kuwa Luther ni mwenye hatia anayestahili hukumu akimshitaki kuwa ni “Mchochezi, mwasi, mkaidi na mwenye kufuru”. Lakini harara yake ilidhihirisha aina ya roho iliyomwongoza kumshitaki. Alisukumwa tu na chuki kutaka kulipa kisasi. Hivyo ndivyo ilivyoonekana. TU 65.3

Alexander akamsisitiza mfalme kwa bidii sana ili atekeleze amri ya papa. Aliposhindwa na mashawishi ya Alexander mfalme akamwambia kuwa alete kesi hiyo mbele za wakuu. Wale waliomwunga Luther mkono wakasikiliza usemi wa Alexander kwa wasiwasi mwingi. Mtawala wa Saxony hakuwako siku hiyo, lakini baadhi ya washauri wake waliyaandika maneno ya hotuba ya ujumbe wa papa. TU 65.4

Luther Ashitakiwa Kuwa Mzushi

Alexander alimshambulia Luther kwa usemi wa nguvu na ufasaha, kwamba ni adui wa kanisa na wa serikali pia. Akasema kuwa makosa ya Luther yametosha, na yanasababisha kuwachomelea mbali wazushi laki nzima. TU 66.1

Kundi la wakufunzi wapotofu na wafedhulu, ambao ni makasisi walioharibika, na watawa wapumbavu, pamoja na jamii ya wa tu waovu, walisema. “Waluther hawa wana nini? Je hesabu yao inawiwa na hesabu ya Wakatoliki na uwezo wao ni kitu gani kwa uwezo wa Wakatoliki? Amri ikitolewa na watu hawa ingetekelezwa mara bila kupingwa na kitu”. TU 66.2

Mabishano yale yale bado yanaendelea kwa wote wanaoeneza ukweli wa neno la Mungu. Kila mara maswali hutokea, “ni nani hawa wanaojidai kutangaza mafundisho mapya? Kwanza hawana elimu, ni wachache kabisa, nao ni watu duni tu. Hata hivyo wanasema kuwa wanao ukweli na kwamba wamechaguliwa na Mungu. Ni wajinga kabisa na wamedanganyika. Je, kanisa letu linalinganishwaje nao kwa umaarufu na kwa wingi?” Mashindano ya jinsi hiyo hayatofautiani na yale ya wakati wa Luther. TU 66.3

Luther, akiwa na uwezo wa neno la Mungu ili kuwapinga na kuwaponda watetezi wa papa. Ilionekana kuwa sio mafundisho yake tu yangelaaniwa ila hata yeye angeangamizwa. Mambo yote Roma iliyokusudia kusema juu yake, yalisemwa kwa hiyo tofauti ilionekana baina ya ukweli na uwongo wakati wa mapambano ya wazi. TU 66.4

Sasa Bwana aliwaamsha wana baraza waone wazi juu ya udhalimu wa mapapa. Duke George wa Saxon akasimama katika baraza hiyo ya wakuu akafafanua kwa ukamilifu kabisa udanganyifu wa maovu ya kanuni za papa. TU 66.5

Dhuluma….. hupiga kelele kuhusu Roma. Aibu yote imewekwa kando, kile wanachokazania ni fedha…. Kwa hiyo wahubiri ambao wangehubiri ukweli, hawasemi lolote, ila madanganyo. Hivyo sasa wanavuna walichopanda. Kadiri mpango huo ndimo maji ya udhalimu hububujika. Upotovu unaonyesha udhalimu na tamaa ya mali mkononi….. Lo! Ni aibu inayoletwa na viongozi wa kanisa, inayowatumbukiza watu maskini katika uangamivu wa milele. Kazi ya matengenezo ya kanisa lazima ipingwe. Kwa kuwa msemaji wa papa alikuwa adui wa Luther aliwashawishi wasikilizaji ili wamwunge mkono. TU 66.6

Malaika wa Mungu walitoa nuru katika giza nene la makosa, akafungua mioyo ya watu wauone ukweli. Uwezo wa Mungu uliwakirisha hata wapinzani wakuu ili waandae njia kwa matengenezo makuu zaidi. Sauti ya mkuu zaidi ya Luther imesikika katika baraza hilo. TU 67.1

Kamati ikachaguliwa ili ipange mambo maovu ambayo wametendea na papa kwa watu wa Ujerumani. Orodha hio imepelekwa kwa mfalme, akiombwa ili achukue hatua kuhusu mambo haya ya udhalimu. Mtu mmoja kati ya waombaji alisema, “Ni kazi yetu kuzuia maovu na kuwaheshimu watu wetu. Kwa hiyo tunakuomba kwa unyenyekevu uamuru matengenezo ya kanisa yafanyike na kukamilishwa”. TU 67.2

Luther Atakiwa Ahudhurie

Sasa baraza ilidai kuwa Luther ahudhurie kikaoni. Mwishowe mfalme alikubali, na Luther akahudhuria. Pamoja na hayo, alipewa ulinzi. Hayo yalitokea Wittenberg kwa njia ya kuweka walinzi pote njiani mpaka Warmos. TU 67.3

Rafiki zake wakijua kuwa chuki na uadui juu ya Luther ni mkubwa, waliogopa kuwa huenda walinzi wake wasijaliwe. Yeye alijibu kusema “Kristo atanipa roho yake ili kuwashinda wajumbe hawa waovu. Nawadharau hawa katika maisha yangu. Nitazidi kuwashinda wakati wa kifo changu. Huko Worms, wanashughulika sana ili wanifanye nikane imani yangu. Na hii haitawezekana. Kwanza nilisema kuwa papa ni mjumbe wa Kristo sasa nasema kuwa papa ni adui wa Kristo na mtume mwovu”. TU 67.4

Rafiki watatu waliazimu kufuatana na Luther mbali ya mjumbe wa serikali aliyefuatana naye. Malanchthon ambaye ni mwenzi wa Luther, moyo wake ulifungwa na wa Luther naye alitaka sana kufuatana naye. Lakini matakwa yake ya kufuatana na Luther yalikataliwa. Luther ambaye ni mtengenezaji wa kanisa, alimwambia Malanchthon: “Kama sirudi na kama adui zangu wakiniua wewe uendelee kufundisha na kudumu katika ukweli. TU 67.5

Ufanye kazi badala yangu ….. Wewe ukibaki mzima, kifo changu kitakuwa na faida kidogo”. TU 68.1

Mioyo ya watu ilisumbuliwa na wasiwasi. Walifahamu kuwa maandishi ya Luther yamelaaniwa huko Worms. Mjumbe wa Luther akihofia usalama wake katika baraza, alimwuliza kama anataka kuendelea mbele. Luther alijibu: “Ingawa ninapigwa marufuku kila mji, lakini nitaendelea mbele” TU 68.2

Katika mji wa Erfurt Luther alipita katika barabara kwa maringo, akiangalia magereza alimofungiwa zamani akitafakari juu ya mashindano aliyopitia wakati alipokuwa akimulikia Ujerumani nuru ya Injili ambayo sasa imeenea katika nchi yote. Kwanza alizuiliwa asihubiri, lakini akapata ruhusa ya kuhubiri. Mtawa ambaye alikuwa akijitesa kwa ajili ya dini sasa ni muhubiri, huyo ndiye Luther. TU 68.3

Watu walimsikiliza kwa makini kabisa. Mkate wa uzima ulitolewa kwa watu wenye njaa. Kristo aliinuliwa juu yao akizidi mapapa na wafalme na watawala wote. Luther hakujifikiria na hatari yake. Katika Kristo alipoteza ubinafsi kwa mambo yote. Alijificha katika Mtu wa kalwari akitaka tu kumwinua Kristo juu ya kila kitu kama Mwokozi wa dhambi. TU 68.4

 Ujasiri wa Mfia Dini

Kwa kadiri mtengenezaji wa mambo ya kanisa, yaani Luther alivyoendelea na mafundiso yake walimkusanyikia huku wakiwa na hamu kuu ya kusikia ujumbe wa mbinguni, wakati huo sauti za amani zilimzungumzia kwamba adui zake Waroma wanamkabili. Walisema, “Watakuchoma, na kukuteketeza kabisa uwe majivu, kama walivyomfanya John Huss” Luther akajibu akasema: “Hata kama wakiwasha moto toka Worms mpaka Wittenberg ….. nitapita kati yake kwa jina la Yesu Bwana, nitaonekana mbele yao…. nikimkiri Yesu Kristo”. TU 68.5

Kufika kwake huko Worms kulileta wasiwasi mkubwa. Marafiki zake walihofia usalama wake, na maadui zake walikuwa na wasiwasi juu ya kusudi lao. Kwa ajili ya chuki na mchocheo wa Kiroma, ilisisitizwa kuwa Luther aende katika makao ya Wakuu ambao ni wa amani, ambavyo kulitangazwa kwamba tofauti zote zimesawazishwa na kuachwa. Lakini marafiki wa Luther walisema kuwa hatari ni kubwa, na hilo ni kubwa. Lakini Luther akitulia bila kutetemeka, alisema “Ingawa waovu wataongezeka katika Worms kama vigae juu ya paa la nyumba, hata hivyo nitaingia humo”. TU 68.6

Alipoingia Worms watu walijazana ili kumkaribisha. Taharuki ilikuwa kubwa. Luther alisema, Mungu ndiye atakuwa mlinzi wangu. TU 68.7

Kufika kwake kuliwatia wafuasi wa papa wasiwasi. Mfalme aliwaita washauri wake akawauliza: “Ni hatua gani itakayochukuliwa. Wakadai wafuasi wa papa walisema ‘Tumeshughulikia jambo hili kwa muda mrefu sasa. Hebu, mfalme mtukufu amalize jambo hili kwa kumwondoa mtu huyu asiishi. Je, Sigismund hakutoa amri John Huss akachomwa moto? Hatupaswi kuendelea kumtunza mzushi huyu’ Mfalme akasema” “La, lazima tutunze ahadi yetu”. Ikaamuliwa kuwa mtengenezaji wa kanisa budi asikilizwe. TU 69.1

Mji mzima ulitamani sana kumwona mtu huyu mashuhuri. Luther alikuwa amechoka na safari ndefu, alihitaji pumziko. Lakini alikuwa amepumzika kwa muda wa saa chache tu, wakati wakuu, mapadri, watu mashuhuri na raia wa mjini walipomkusanyikia. Kati ya watu hao waliokuwamo watu waliomtaka mfalme amlaani na kumtukana Luther. Walio wengi, maadui na marafiki pia walikuja kumwona mtawa huyu jasiri. Alionekana kuwa mtu jasiri. Uso wake ulionekana mtulivu uliojaa furaha. Maneno yake yalikuwa ya kishujaa hasa, hata adui zake walitekewa. Baadhi ya watu walikiri kuwa alikuwa na uwezo wa kimbingu, wengine walitamka kuwa alikuwa na pepo sawa kama walivyotamka kwa Kristo. Yohana 10:20. TU 69.2

Siku ya pili, mkuu wa serikali alimleta Luther katika jumba la baraza, katika mkutano. Kila mahali palijaa watu waliotaka kumwona mtu aliyethubutu kumpinga papa. Jemadari mzee ambaye alipigana vita vingi na kushinda alimwambia taratibu: “Wewe maskini, sasa uanenda kuamua uamuzi wa ajabu ambao, mimi au jemadari mwingine yeyote hakuufanya katika vita vyetu vya kumwanga damu. Lakini iwepo njia yako ni ya haki …. Endelea mbele katika jina la Mungu, usihofu kitu. Mungu hatakuacha” TU 69.3

Luther Asimama Barazani

Mfalme alikalia kiti, huku akizungukwa na watu mashuhuri katika utawala wake. Sasa Martin Luther atatakiwa atetee imani yake mbele ya baraza. “Onekano hilo lenyewe lilikuwa alama ya ushindi mkuu juu ya papa. Papa alikuwa amemlaani mtu huyu, na kumwita kuwa ni mzushi, na sasa anasimama mbele ya baraza ambalo lina uwezo kupita wa Papa. Papa alikuwa amempiga marufuku na kumtenga mbali na jamii ya wanadamu, na sasa alikuwa ameitwa mbele ya kusanyiko maarufu katika ulimwengu. Uwezo wa Roma sasa ulikuwa unafifia, na mtu mtawa huyu ndiye anayesababisha hali hiyo”. TU 69.4

Mtengenezaji huyu wa kanisa, ambaye alizaliwa katika hali duni, alionekana kuwa tishio na mwenye udhia. Wakuu walikutana naye safari kadhaa wa kadhaa, na mmoja wao alimnong'oneza akisema “Usiogope wale wanaoua mwili ambao hawawezi kuua roho” Mwingine akasema: “Wakati watakapowachukua mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, mtapewa saa ile mtakayosema” Mathayo 10:28, 18-19. Mkutano wote ukanyamaza kimya kabisa. Halafu mkuu mmoja wa Serikali akasimama, huku akielekeza kidogo kwa maandiko ya Luther, akadai kwamba Luther anajibu maswali mawili kwamba anayakiri kuwa ni yake, au kwamba anakusudia kuyakanusha. Majina ya vitabu, yaliyosomeka kwa Luther: Swali la kwanza alilijibu kuwa vitabu hivyo ni vyake. Kuhusu swali la pili alijibu, “Ningetenda bila busara kama nigejibu swali la pili bila kusababisha fujo. Budi lithibitishe zaidi bila kujali hali ilivyo. Kwa ajili hiyo nakusihi wewe mtukufu kwa unyenyekevu unipatie muda wa kujibu bila kwenda kinyume na neno la Mungu” TU 70.1

Luther aliwaamisha watu wote kuwa maneno yake hayatokani na mawazo tu bali ni ya kweli isiyobishiwa. Hali ilimwezesha baadaye kujibu maswali kwa njia ya hekima na heshima kamili. Majibu yake yaliwafedhehesha wapinzani wake kabisa. TU 70.2

Siku iliyofuata alitakiwa kutoa jawabu lake la mwisho. Kwa muda alifadhaika. Wapinzani wake walionekana kwamba watashinda. Mashaka yalimjaa, akaonekana kana kwamba ametengwa mbali na Mungu. Katika wasiwasi huo wa uchungu alimlilia Mungu, ambaye ndiye pekee yake aliyefahamu fadhaa yake. Alilia akisema “Oh, Mungu Mwenyenzi, kama nategemea uwezo wa dunia tu, hakuna tena yamekwisha. Saa yangu ya mwisho imefika, hukumu yangu imetajwa... Oh, Mungu, hebu nisaidie na hila zote za dunia... kazi hii ni yako, nayo ni kweli na ya milele. Oh, Mungu Unisaidie! Mungu mwenye haki, ambaye habadiliki, Situmaini kupata msaada kwa mtu yeyote. Wewe ndiwe uliyenichagua kwa kazi hii. Hebu uniwie karibu kwa ajili ya Mwanao Mpendwa Yesu Kristo, ambaye ndiye ngao yangu na ngome yangu, na mwamba wangu”. TU 70.3

Hata hivyo Luther hakufadhaishwa na hofu ya mateso au kifo. Alijiona kuwa hatoshi chochote. Kwa ajili ya udhaifu wake kazi itakwama. Hakujitahidi hivyo kwa ajili yake, bali kwa ajili ya kazi ya Mungu, ipate kufaulu. Katika wasiwasi wake, imani yake ilikazika kabisa kwa Kristo ambaye ni mwokozi mwenye uwezo. Kule barazani hangeonekana akiwa peke yake. Mara utulivu ukajaa moyoni mwake, naye alifurahi kwa kuwa amepata nafasi ya kumwinua Kristo mbele ya watu na “mataifa” TU 71.1

Luther alifikiri juu ya jawabu lake. Akafungua kurasa na maandishi yake, na akapanga mafungu ya Biblia yatakayomsaidia wakati wa kujibu. Ndipo hapo, akaweka mkono wake wa kushoto juu ya maandiko Matakatifu akainua mkono wake wa kulia kuelekea mbinguni akaahidi kudumu katika maongozi ya Biblia na kuwa mwaminifu kwa injili hata kama matokeo yake ni kumwaga damu yake. TU 71.2

Luther Mbele ya Baraza Tena

Wakati Luther alipofikishwa kwa wakuu tena alikuwa mtulivu bila kuwa na wasiwasi, akiwa na hali ya ujasiri kama mjumbe wa Mungu kati ya wakuu wa nchi. Sasa mkuu wa serikali alitaka atoe uamuzi wake. Je, aliazimia kukana imani yake? Luther alijibu kwa utulivu bila kutumia maneno ya karaha. Hakujitukuza, lakini hali yake ilikuwa imara sana hata iliwashangaza watu wote waliokuwepo. TU 71.3

Mfalme mtukufu na wakuu mashuhuri Luther alisema “Nasimama mbele yenu leo kama nilivyoagizwa jana. Kama nikikosea kwa ujinga naomba samahani, maana sikukulia katika jamii ya kifalme, ila nilikuwa katika mazingira ya kishambashamba” TU 71.4

Kisha akaeleza katika baadhi ya maandishi yake yaliyopigwa chapa, ambayo hata adui zake wanayasifu kwamba yafaa, basi kuyakanusa hayo ni kuikanusha kweli ambayo inaaminiwa na watu wote. Sehemu ya pili ya maandishi yake yalikuwa juu ya uovu na udhalimu juu ya Roma ikiongozwa na mapapa. Kuyatangua maandishi haya kutaimarisha na kustawisha udhalimu na uonevu wa Roma na kufungua mlango wa ukaidi wa kutojali mambo matakatifu ya Mungu. Sehemu ya tatu ya maandishi yalikuwa shambulio juu ya watu mmoja mmoja waliokuwa wakiutetea uovu. Kuhusu sehemu hii alikubali kuwa alikosea kushambulia watu kupita kiasi. Lakini hata kuhusu sehemu hii hakubali kuifuta. Maana akiifuta maadui wa ukweli watapata nafasi ya kuwadhulumu watu wa Mungu kwa ukatili mkuu. TU 71.5

Aliendelea kusema “Nitajitetea kama Kristo alivyofanya. Kama nimesema maovu, hayo yatanishuhudia ….. Kwa rehema za Mungu nakusihi mtukufu mfalme, na ninyi waheshimiwa wote, pamoja na watu wote mnithibitishie kutoka katika maandiko ya manabii, na maandiko ya mitume kwamba nimepotoka. Nikithibitishiwa hivyo kutoka katika Maandiko Matakatifu, nitakuwa tayari kukana na kuungama kila kosa nililolifanya. Nami nitakuwa mtu wa kwanza kuchukua vitabu vyangu na kuvitupa motoni. TU 72.1

Zaidi ya kuaibishwa, nafurahi kuona kuwa Injili sasa inaleta vita na mafarakano kama ilivyokuwa zamani. Hii ndiyo tabia ya hali ya Neno la Mungu. Yesu Kristo alisema, Sikuja kuleta amani duniani bali upanga….” Jihadharini msije mkasababisha mafarakano kwa kiburi. Mnaweza kulidhihaki neno Takatifu la Mungu, na kutumia nguvu za kutisha kulazimisha mambo kwa uwezo mkuu na kuleta uangamivu wa milele. TU 72.2

Luther, alikuwa amezungumza katika lugha ya Kijerumani, na sasa alitakiwa aseme maneno yale yale kwa lugha ya Kilatini. Basi aliyarudia maneno yale kwa Kilatini katika ufasaha kamili. Mungu alimwongoza usemi wake. Mara ya kwanza baadhi ya wakuu walipofushwa wasielewe ujumbe wa Luther, lakini aliporudia kusema kwa Kilatini waliona maana yake. TU 72.3

Wale waliofumba macho yao kwa ukaidi walikasirishwa na maneno ya Luther. Msemaji mmoja alinena kwa hasira. “Hakujibu swali aliloulizwa….. unatakiwa utoe jawabu wazi na dhahiri. Je, utakanusha mafundisho yako au hutayakanusha?” TU 72.4

Luther alijibu, “Kwa kuwa mfalme mtukufu na waheshimiwa wote mnataka nijibu wazi na dhahiri, nitawajibu hivi: Mimi sitakana imani yangu mbele ya papa wala mbele ya baraza, kwa sababu ni ya hakika kama siku, hata wapinzani wangu wanatofautiana katika maoni. Mimi nisipothibitishiwa kosa la Maandiko Matakatifu,….. sitaikana imani yangu kamwe, maana siyo salama kwa mkristo kusema kinyume cha dhamiri yake. Huo ndio msimamo wangu, siwezi kufanya vinginevyo, Mungu anisaidie. Amen” TU 72.5

Hivyo ndivyo alivyosimama mtu huyu mwenye haki. Ukuu wake, na ubora wa tabia yake, utulivu wake na furaha ya moyo wake vilidhihirika kwa wote walioshuhudia ukuu wa imani hiyo ishindayo ulimwengu. TU 72.6

Katika jawabu lake la kwanza Luther alizungumza katika hali ya heshima sana. Waroma walidhania kwamba kukawia kawia kwake kulikuwa kunatayarisha ili akane imani. Charles mwenyewe aliyemwona Luther katika hali hafifu, mdhaifu, mwenye mavazi ya kawaida tu, mwenye usemi wa taratibu sana, “Mtu huyu hatanidhihaki” Lakini ujasiri wake, uwezo wa maneno yake, uliwashangaza wote. Mfalme katika mshangao wake alisema “Mtawa huyu ananena kishujaa bila kutishika na lolote”. TU 72.7

Luther Mbele ya Baraza Tena

Wafuasi wa Roma wameshindwa kabisa na sasa wanataka kutumia vitisho ili kurudisha heshima yao iliyopotea. Wameshindwa kimaandiko. Msemaji mmoja alisema. “Kama hutaikana imani yako, mfalme na dola yake watatafuta njia nyingine ya kumfanyia mtu huyu asiyewezekana”. Luther alisema kwa utulivu, “Mungu awe msaada wangu, maana hakuna kitu cha kukana katika imani yangu”. TU 73.1

Aliambiwa aondoke wakati wakuu walipokuwa wakishauriana. Kuendelea kwa Luther kukataa kukiri kwamba alikosa huenda kukaleta badiliko fulani katika taratibu za kanisa. Basi iliamuliwa kwamba angepewa nafasi moja zaidi ya kukana mafundisho yake. Lakini swali liliulizwa tena kwamba, “Je, angekubali kukana imani yake na mafundisho yake?” Luther akasema, “Mimi sina jawabu lingine kuliko hilo nililojibu”. TU 73.2

Viongozi wa papa walijawa na chuki na uchungu, kwamba madaraka yao na mamlaka yao yanadharauliwa na mtu tu wa kawaida kama Luther. Luther amezungumza mbele yao kwa ujasiri na utulivu wa Kristo, akasema bila kutapatapa wala kubahatisha. Alijisahau, akasema akiwa mbele ya Mkuu anayewazidi wote hata mapapa, wafalme na watawala Roho wa Mungu amekuwa karibu naye na kuwatia uvuli wakuu wote waliokuwa barazani. TU 73.3

Baadhi ya wakuu walikubali kuwa maandishi ya Luther ni ya kweli kabisa. Watu wengine hawakusema neno wakati huo, lakini baadaye walimwunga Luther mkono. Mheshimiwa Frederick alisikiliza kwa makini sana usemi wa Luther akikiri kuwa huo ni usemi murua kabisa na akaazimu kumlinda na kumtetea kwa kila njia. Aliona kuwa hekima ya papa na ya wakuu na wafuasi wote wa Roma imeonekana bure kabisa mbele ya ukweli wa Luther. TU 73.4

Mjumbe wa papa alivyoona matokeo ya usemi wa Luther alikusudia kutumia kila njia ili amwangushe. Alimshawishi kwa njia zote mfalme kijana ili asimwache Luther kuendelea. Siku ya pili yake baada ya jawabu la Luther, Charles alitangaza mbele ya wakuu kuwa anaazimu kuilinda dini ya Katoliki, Akasema kuwa njia zozote zitatumiwa kumpinga Luther na wafuasi wake. Akasema, “Nitaacha utawala wangu, mali yangu, rafiki zangu, mwili wangu damu yangu, roho yangu na uhai wangu ….. Nitaendelea kupingana naye pamoja na Wafuasi wake kama wazushi. Nitatumia kila njia ili kuwaangamiza”. Walakini mfalme alitaka kuwa Luther lazima alindwe kabisa, na lazima arudi kwao kwa usalama. TU 73.5

Luther Alindwa Hatarini

Mara nyingine tena wajumbe wa papa walidai kwamba Luther asipewe ulinzi. Wakasema “Mto wa Rhine budi upokee majivu yake kama ulivyopokea majivu ya Joh Huss”. Lakini wakuu wa Ujerumani, ingawa walikuwa adui wa Luther, hawakukubali dhana hiyo. Walikumbusha kuhusu fujo na maafa yaliyotokana na kifo cha Huss. Hawakutaka Ujerumani irudie kupata maafa ya namna hiyo mara ya pili. TU 74.1

Charles katika jawabu lake kuhusu madai ya wajumbe wa papa, alisema “Ingawa wenye imani tofauti wanapaswa kuondolewa mbali ulimwenguni, lakini pia wanapaswa kulindwa na wakuu” Baadaye wajumbe wa papa walimhimiza Charles kama vile Sigsmund alivyomtendea Huss. Lakini Charles alikumbuka mabaya yaliyompata Huss kwa ajili ya imani yake, na msukosuko uliotokana na mambo hayo akasema, “Mimi sitaki kuingia katika hali ya aibu kubwa namna hii kama Sigsimund” Walakini Charles hakuamini ukweli ulipofundishwa na Luther. Hakupenda kuacha njia za mazoea yake na kufuata njia mpya. Kwa kuwa wazee wake waliishi humo, hivyo hata yeye hakutaka kuacha ukatoliki. TU 74.2

Siku hizi watu wengi huishi katika njia za baba zao. Hatutakubaliwa na Mungu eti kwa kuwa tunaishi kwa mapokeo toka kwa wazee wetu badala ya kuchunguza Maandiko Matakatifu sisi wenyewe. Nuru mpya inayotumulikia lazima tuifuate, ingawa baba zetu hawakuwa nayo. TU 74.3

Uwezo wa mbinguni ulipita kwa Luther ukawafikia wafalme na wakuu wa Ujerumani. Roho wa Mungu aliwasihi watu katika baraza hilo. Charles V akawa kama Pilato wa amani, akajitoa kufuata anasa za ulimwengu, na kwa kiburi akaukataa ukweli aliopewa. TU 74.4

Njama za kumwangamiza Luther zilienea mahali pengi, na zikasababisha msukosuko mji mzima. Marafiki wengi wa Luther hali wakitambua ukatili wa kikatoliki waliazimia kwamba Luther asitolewe mikononi mwa Wakatoliki. Watu maelfu walijitolea kumlinda. Milangoni mwa nyumba na katika mahali pa hadhara matangazo yalipigiliwa pote, mengine yakimlaani na mengine yakimuunga Luther mkono. Tangazo moja liliandikwa maneno haya: “Ole wako nchi, akiwa mfalme wako ni kijana” Mhubiri 10:16. Watu wajulikanao kwa ajili ya vyeo au utajiri walimthbitishia mfalme na wakuu kwamba, ikiwa Luther atapatwa na baa lolote, amani ya ufalme itatahayarika, na hata ufalme wenyewe utakuwa hatarini. TU 75.1

Juhudi ya Kumpatanisha na Roma

Fredrick wa Saxony alijificha sana asitambulike na watu jinsi anavyomfikiria Luther. Hakuonyesha chuki wala wema. Alinyamaza kimya huku akimchunguza Luther kisirisiri. Lakini watu wengi hawakuweza kuficha hali zao hivyo. Wengi walionyesha chuki yao au wema wao kwake Spalatin, aliandika akasema Chumba kidogo cha Luther hakikuweza kuweka watu wote waliofika hapo kumtembelea. Hata wale ambao hawakukubaliana na mafundisho yake walisifu ujasiri wake uliomfanya akabili hatari ya kifo bila hofu, ili mradi asipingane na dhambira yake. TU 75.2

Bidii nyingi ilifanywa ili kumshawishi Luther ili akubaliane na Roma. Watu mashuhuri na wakuu walimfikia mara nyingi wakimwambia kuwa akiendelea kupingana na Roma, ataharamishwa kabisa kutoka katika nchi yote, na hatapata mtu wa kumtetea. Tena na tena alishauriwa akubali kuungana na Roma kama mfalme alivyoshauri. Hapo akikubali atakaa salama. Yeye akajibu, “Nakubali kwa moyo wote kwamba mfalme na wakuu na wakristo wote, wachunguze mafundisho yangu wakiyalinganisha na neno la Mungu, kama wakiona tofauti basi nitasahihisha. Maana mwanadamu hana jingine ila kutii na kufuata neno la Mungu basi.” TU 75.3

Katika kishawishi cha siku nyingine, alisema, “Nakubali kuachana na walinzi wangu. Nitaweka maisha yangu mikononi mwa mfalme. Lakini kuacha neno la Mungu, kamwe sitaacha!” Alieleza kuwa, yeye yu tayari kukubaliana na uamuzi wa baraza, ikiwa uamuzi huo unasimama ndani na Maandiko mtakatifu kuhusu neno la Mungu na imani, kila mkristo anajua la kufanya vizuri sawa sawa na papa. Papa hana ujuzi wa peke kuliko mkristo mwingine yeyote. Basi watu waliokuwa wakimshawishi waliona kuwa ni kazi bure kuendelea kumshawishi. TU 75.4

Kama Luther angalikubaliana nao hata kwa neno moja tu, shetani na majeshi yake wangalipatia ushindi. Lakini msimamo wake wa imani ulikuwa njia ya kulipatia kanisa uhuru wa kuachana na udhalimu wa Roma. Mvuto wa mtu huyu shujaa aliyethubutu kusimama imara mwenyewe, ulisaidia kanisa, sio kwa wakati wake tu, ila hata kwa vizazi vijavyo. TU 76.1

Mara Luther aliamuriwa na mfalme arudi nyumbani. Tangazo hilo lingefuatiwa na hukumu yake. Vitisho vya kumwangamiza vilizagaa katika njia yake, lakini alipoondoka Woms, roho yake ilijaa furaha na sifa kwa Mungu. TU 76.2

Baada ya kuondoka alitaka ieleweke kwamba ujasiri wake sio wa uasi. Luther alimwandikia mfalme barua akisema “Mfalme mtukufu, nini niko tayari kutii wakati wowote, kwa heshima au kwa aibu, kwa uzima au kwa mauti, katika mambo yote, ila yanayotaka kunitenga na neno la Mungu, hayo siwezi kuyatii. Pale mambo ya milele yanapohusika, mambo ya binadamu budi yawekwe kando. Utii wa jinsi hiyo wa moyoni ndiyo ibada ya kweli, inayotakiwa kumpa Mwumbaji wetu” TU 76.3

Katika safari kutoka Worms, alikaribishwa na waongozi, ingawa ameharamishwa katika ushirika. Hata watawala walimheshimu ingawa mfalme mwenyewe alimlaumu. Ingawa alimharamisha alitakiwa ahubiri. Alisema, “Siahidi kufungia neno la Mungu nisilihubiri” TU 76.4

Hakukaa muda mrefu baada ya kutoka Worms kabla wafuasi wa papa kumlazimisha mfalme ampige marufuku Luther alitukanwa kwamba yeye ni shetani mwenye mfano wa mwanadamu, mwenye kuvaa vazi la mtu mtawa. Mara ulinzi wake ulikoma, watu wote walikatazwa kumsaidia kwa lolote. Walikatazwa wasimpe chakula au msaada wowowte. Aliwekewa ulinzi na wafuasi wake kukamatwa na mali zao kuchukuliwa. Vitabu vyake vikachomwa halafu watu wote waliokwenda kinyume na amri hii waliwekwa katika hukumu ile ile. Frederick wa Saxony rafiki wa Luther aliondoka Worm baada ya Luther. Amri ya mfalme ya kumpiga Luther marufuku ilipokewa na wakuu wote. Wafuasi wa Roma walishangilia kabisa. TU 76.5

Walidhani kuwa maangamizo ya mtengenezaji wa kanisa yamekamilika. TU 77.1

Mungu amtumia Frederick Saxony

Jicho la Mungu lisilosinzia lilikuwa likiangalia mienendo ya Luther. Mungu alimwandaa Frederick wa Saxony mtu mwenye moyo safi moyo wa kweli ili amtunze Luther. Katika safari ya kutoka Worms kurudi nyumbani, Luther alitengana na wenzake. Alichukuliwa kwa njia ya msituni kwenda katika gereza la Wartburg, ambako alifungiwa ili kumficha. Maficho yake yalikuwa ya siri hata Frederick mwenyewe hakufahamu. Kwa kuwa ilikuwa siri ya ulinzi Frederick alikaa bila wasiwasi bora tu yu salama. Majira ya kiangazi na masika yakapita, na Luther aliendela kukaa gerezani. Alexander, mfuasi wa Luther alifurahi sana. Nuru ya injili ilionekana kwamba imezimika. Lakini nuru ya Luther iling'aa kwa mng'ao mkubwa. TU 77.2

Usalama Huko Wartburg

Katika utulivu wa usalama wa Wartburg, Luther alifurahia hali hiyo ya utulivu kutoka katika joto la vita na matatizo. Lakini kwa kuwa amezoea maisha ya mapambano ukiwa sana kukaa kimya bila shughuli. Katika siku hizo za upweke hali ya kanisa ilififia. Alihofia kulaumiwa kuwa amekuwa mwoga na ya kuwa amejitoa kutoka katika mapambano. Basi akajilaumu sana kuwa na hali ya uvivu. TU 77.3

Hata hivyo kila siku alitimiza sehemu kubwa ya kazi kwa jinsi isiyodhaniwa kuwa mtu anaweza kufanya vile. Kalamu yake haikusinzia kuandika mambo. Adui zake walishangaa kwa uthibitisho wa ukweli aliokuwa akitoa; hivyo walichanganyikiwa. Vigazeti vingi sana viliandikwa na yeye na kusambazwa kote katika Ujerumani. Pia alitafsiri agano jipya katika lugha ya Kijerumani. Katika kifungo chake sawa na kile cha Patmo aliendelea kutangaza injili na kukemea maovu ya Roma kwa muda karibu mwaka mzima. TU 77.4

Mungu alikuwa amemwondoa mtumishi wake kutoka katika mapambano ya hadhara. Katika maficho yake milimani, Luther alitengwa mbali na mivuto ya misaada ya kibindamu. Aliwekwa mbali na hali inayoweza kuinuka kwa kiburi na kufaulu. TU 77.5

Kadri watu walivyofurahia uhuru ulioletwa na Injili, shetani alitaka kugeuza mawazo yao ili ajitegemee kuabudu kazi zao badala ya kuutegemea mkono wa Mungu unaofanya makuu. Mara nyingi viongozi wa dini wanaosifiwa namna hiyo hujitegemea wenyewe. Watu hushawishika kuwategemea na kutumainia uongozi wao badala ya kumtazamia Mungu. Kutoka katika hatari hiyo Mungu hutunza matengenezo ya kanisa. Macho ya watu yamgeukie Baba wa milele mwenye ukweli wote. TU 77.6

 

SURA YA 9
Nuru YawashwaUswisi

Majuma machache baada ya kuzaliwa Luther katika kibanda kidogo cha wachimba madini katika Saxony, Zuric Zwingli naye akazaliwa katika nyumba ya mfuga mifugo katika milima ya Alps. Kwa kuwa alikulia katika mazingira safi ya kawaida, mawazo yake yalianza kutafakari mambo ya Mungu na ukuu wake. Akiwa chini ya bibi yake, alisimuliwa hadithi nyingi za Biblia alizojifunza katika kanisa. TU 79.1

Alipopata umri wa miaka kumi na mitatu alikwenda katika mji wa Bern, ambako kulikuwa na shule maarufu katika Switzerland. Walakini hapo Bern hatari ilitokea. Watawa waliazimia kabisa kumshawisi ili aingie katika kundi la watawa. Kwa bahati nzuri baba yake alipata habari ya maazimio ya watawa hao. Akaona kuwa maisha ya mwanawe ya usoni hayatafaa lolote, tena yumo mashakani. Kwa hiyo alimwita arudi nyumbani. TU 79.2

Kijana alirudi lakini hakuridhika na maisha ya kwao kwenye mabonde ya milima. Baada ya muda akaenda Basel na kuanza tena masomo yake. Hapa ndipo Zwingli aliposikia Injili ya neema ya Mungu mara ya kwanza. Wittembach alipokuwa akijifunza Kigiriki na Kiebrania, aliongozwa na Roho kuchunguza Maandiko Matakatifu. Kwa njia hii nuru ya Mungu ikapenya mawazoni mwake. Akatangaza kwamba kifo cha Kristo ndicho fidia pekee ya mwenye dhambi. Maneno hayo yalipenya mawazoni mwa Zwingli, yakawa ndiyo mwanzo wa pambazuko la asubuhi. TU 79.3

Baadaye Zwingli aliitwa kutoka Basel kufanya kazi ya maisha. Mahali pake pa kazi poliko katika majimbi ya milima ya Alps. Alipowekewa mikono kuwa padri alishughulika na mambo ya kiroho, na kuchunguza maandiko ya kweli ya Mungu. TU 79.4

Kwa kadiri alivyozidi kuchunguza Maandiko Matakatifu ndivyo alivyozidi kupambanua wazi baina ya ukweli na uzushi wa Roma. Alijitolea kuamini Biblia kama Neno la kweli la Mungu, ambalo linatosha kuongoza watu. Aliona kuwa halina haja ya maelezo zaidi, maana lenyewe linajieleza. Alitafuta kila njia ya kumsaidia ili aelewe bila kupotoshwa. Aliomba Roho Mtakatifu amsaidie. Aliandika akasema “Nilianza kumwomba Mungu anipe nuru yake, halafu Biblia iliniwia rahisi kuelewa”. TU 79.5

Mafundisho ya Biblia Zwingli aliyofundisha hakuyapata kwa Luther. Aliyapata kwa Kristo. Mswisi huyu aliandika na kusema “Kama Luther anamhubiri Kristo, anafanya kama vile nifanyavyo…. TU 79.6

Kamwe hakuna neno lolote nililoandika kwa Luther, wala Luther kwangu ambalo linahusu wokovu. Kwa nini? Kwa kuwa mahubiri ya Luther na ya kwangu yote huongozwa na Roho Mtakatifu na wala hayatofautiani kwakuwa yanatokea mahali pamoja” TU 80.1

Katika mwaka wa 1516 Zwingli alialikwa ahubiri katika nyumba ya watawa huko Einsiedeln. Mahali hapa aliacha mvuto bora kabisa kama mtengenezaji wa kanisa halisi. Mvuto huo ulienea katika nchi yote ya kwao, milimani Alps. TU 80.2

Baina ya mambo makuu ya Einsiedeln ilikuwa sanamu ya bikira, ambayo ilisemekana kuwa ilikuwa na uwezo wa kufanya miujiza. Juu ya lango la nyumba ya watawa palikuwa na andiko lisemalo, “Hapa msamaha kamili wa dhambi hupatikana” Hapo palipohesabiwa kuwa mahali patakatifu watu makundi makundi walitoka pote katika nchi ya Switzerland, ufaransa hata Ujerumani pia, ili kupata msamaha wa dhambi. Zwingli alitumia nafasi hiyo ya kuwatangazia uhuru upatikanao katika Injili ya neema ili kuwatoa katika kifungo cha ushirikina. TU 80.3

Zwingli aliwaambia “Msidhani kuwa Mungu yumo katika hekalu hili kuliko mahali pengine, je, mambo hafifu haya mtendayo, kama vile safari ndefu kwa ajili ya dini, kutoa sadaka, kuheshimu sanamu za watakatifu, na kadhalika yatawapatia msamaha wa neema ya Mungu? Kuna manufaa gani ya kuvaa kofia yenye kung'aa, majoho maridadi, na mapambao ya aina aina? Kristo aliyetolewa kafara juu ya msalaba ndiye fidia ya dhambi kwa wote wamwaminio milele”. TU 80.4

Kwa wengi, walitiwa uchungu kuambiwa kuwa matendo yao kama safari ndefu wasafirizo ni za bure. Hawakuweza kuelewa maana ya msamaha wa dhambi kwa njia ya imani katika Kristo. Walitosheka tu na njia zile za Roma ilizowapangia. Kwao waliwatumaini mapadri na papa ili wawapatie ukombozi wala hawakujishughulisha na usafi wa moyo. TU 80.5

Lakini watu wengine walipokea habari ya wokovu kwa njia ya kumwamini Kristo kwa furaha kuu. Kwa imani wakapokea damu ya Kristo kuwa ndiyo njia ya kuwapatia wokovu. Watu hawa walirudi makwao wakawatangazia wenzao habari njema hii aliyoipokea. Kwa njia hii ukweli ulienea toka mji mpaka mji mwingine. Hesabu ya wasafiri waliokuwa wanamwendea bikira ikapungua. Hivyo matoleo yalipungua, hata mshahara wa Zwingli pia ukakatwa, maana ulitokana na matoleo hayo. Lakini jambo hili lilimfurahisha kwa kuona uwezo wa ushirikina unavunjika. Ukweli ulizidi kushikwa na watu wengi. TU 80.6

Zwingli Aitwa Kwenda Zurich

Baada ya kupita miaka mitatu, Zwingli aliitwa ili akahubiri katika kanisa kuu la Zurich, ambao ni mji maarufu sana katika Uswiss. Mvuto ambao ungeonyeshwa hapo ungeenea sana. Makasisi hawakukawia kumwongoza kuhusu kazi zinazompasa. Wakamwambia: “Utafanya bidii sana kukusanya mapato ya wakuu wa kanisa, bila kuachia hata kidogo kidogo…… uangalie sana kuongeza mapato katoka kwa wagonjwa, na kwa waabudu na kutoka katika huduma ya makasisi” “Kuhusu usimamizi wa huduma ya pasaka, na mahubiri, na utunzaji wa kundi …. Unaweza kubadili mambo hasa mafundisho unayohubiri”. TU 81.1

Zwingli alisikiliza maagizo hayo kwa utulivu, kisha alijibu “Maisha ya Kristo yamefichika kwa watu siku nyingi sana. Mimi nitahubiri Injili ya Mathayo yote kama ilivyo ….. Huduma yangu itakuwa lengo la kumtukuza Mungu, na kumtukuza Mwana wake Yesu Kristo, na kudhihirisha njia wazi ya wokovu, na imani ya kweli inayotakiwa”. TU 81.2

Watu walimiminika ili kusikia mahubiri yake. Alianza huduma yake kwa kufundisha mambo ya Injili zote, na kueleza habari za maisha na kazi ya kifo cha Kristo. Akasema. “Mimi nia yangu ni kuwaogozeni kwa Kristo ambaye ndiye asili ya wokovu.” Watu wataalamu wakuu, wenye elimu, na wakulima walimsikiliza Zwingli kwa makini. Aliyalaani maovu yanayotendwa na kanisa la Roma wazi wazi bila hofu. Wengi walikuwa na furarha na kumtukuza Mungu kwa mahubiri hayo. Walisema “Mtu huyu ni mhubiri wa ukweli. Atakuwa mkombozi wetu kama Musa, atakayetuongoza kutoka katika giza la Misri” Baada ya muda upinzani ulitokea. Watawala walimshambulia kwa maneno ya dharau wakimcheka na kumdhihaki. Wengine walikuwa wakimwendea na kumfanyia ufedhuli na kumtisha. Lakini Zwingli aliyavumilia yote hayo. TU 81.3

Mungu anapoandaa kuvunja pingu za ujinga na ushirikina, shetani naye hujitahidi sana kuwafunga watu wakae gizani. Roma ilijitahidi mno kueneza masoko yake ya kuuzia vyeti vya msamaha wa dhambi. Waliweka viwango mbalimbali vya dhambi na bei yake. Kama hazina ya kanisa ilikuwa imejaa vyeti vya msamaha wa dhambi vilitolewa bure. Kwa hiyo misimamo miwili ilikuwa inaendelea kusambaa: Roma inauza vyeti vya kusamehewa dhambi na kujaza hazina yake na Watengenezaji wa Kanisa wakilaani dhambi na kuwaelekeza wenye dhambi kwa Kristo ambaye ndiye mwokozi wao. TU 81.4

Uuzaji wa Vyeti Vya Msamaha Huko Uswiss

Katika nchi ya Ujerumani uuzaji wa vyeti vya msamaha uliendeshwa na mdhalimu Tetzel. Katika Uswisi biashara hiyo iliwekwa mikononi mwa mtawa mmoja wa Kiitalia aitwaye Samson. Samson alikuwa amepata fedha nyingi kwa kazi hiyo kutoka Ujerumani na Switerland akaziweka katika hazina ya mapapa. Sasa alipitia Switzerland akiwanyang'anya wakulima maskini mapato yao, ili kuongezea utajiri juu ya utajiri. Mtengezezaji wa kanisa ambaye ni Zwingli, mara moja alijitolea kumpinga. Huo ulikuwa ushindi wa Zwingli wa kumbainisha mtawa huyo katika maazimio yake, na mwisho aliondoka kwenda mahali pengine. Huko Zurich Zwingli alihubiri kwa nguvu sana akipinga uovu na mfanya biashara huyu wa kuuza msamaha. Samson alipofika mahali alipokwenda alipata ruhusa ya kuingia hapo kwa njia ya udanganyifu. Lakini alipogunduliwa alifukuzwa bila kuuza cochote na mwisho akaondoka Switzerland. TU 82.1

Tauni kubwa ilipiga nchi ya Uswisi katika mwaka wa 1519. Watu wengi waliona kuwa ilikuwa kazi bure kununua vyeti vya msamaha. Kwa hiyo walitamani kupata msingi wa hakika wa kusimamia imani yao. Huko Zurich Zwingli alipatwa na ugonjwa, na habari zilienea kuwa amekufa. Katika saa ya giza kama hiyo aliutazamia msalaba wa kalwari na kujikabidhi kamili kwake Mweza, akiwa na uthibitisho wa kusamehewa dhambi. Alipopona na kuondoka katika lango la mauti alihubiri Injili kwa nguvu zaidi kuliko kwanza. Watu wenyewe walikuwa wametoka katika hatari ya kifo cha tauni, kwa hiyo waliona thamani ya Injili kwa upya zaidi. TU 82.2

Zwingli mwenyewe alikuwa amefikia ujuzi dhahiri wa ukweli, na alikuwa ameona uwezo wa Injili katika maisha yake. Alisema “Kristo… ametununulia wokovu usio na mwisho. Hamu yake, dhabihu yake ya milele, na uwezo wake wa kuponya milele, hufanya haki yake itosheleze kila mtu anayemtumaini kwa imani isiyotikisika. Popote palipo na imani kwa Mungu juhudi huonekana ambayo huwabidisha watu ili watende matendo mema” TU 82.3

Matengenezo ya Kanisa yaliendelea hatua kwa hatua katika Zurich. Adui wa mtengenezaji walijitokeza wazi wazi na hatari hiyo ilionekana. Mara kwa mara Zwingli alipata mashambulio ya maneno. Kila mara sauti ilisikika ikisema, “Mwalimu huyu mzushi lazima anyamazishwe”. Askofu wa Constance alituma wajumbe watatu katika baraza au mahakama ya Zurichk, akimshitaki Zwingli kuwa anahatarisha amani na kuleta machafuko katika jamii. Akasema “Kama uongozi wa kanisa ukikaa kimya kitakachotokea ni machafuko nchini” TU 82.4

Baraza lilisita kuchukua hatua yoyote juu ya Zwingli. Roma ikaandaa mashambulio mapya. Zwingli akasema “Haya na waje; hofu yangu kwao ni sawa na hofu ya genge litokezalo juu ya maji ya bahari linavyoogopa mawimbi yanayovuma chini yake” Bidii ya wakuu wa Roma ya kuzima kazi ya Zwingli iliisukuma mbele zaidi. Ukweli wa Injili uliendelea mbele. Katika Ujerumani wale wafuasi waliorudi nyuma kwa kutokuwepo Luther, waliamka tena na kusimama upya kwa kadiri walivyoona maendeleo makubwa katika Uswisi. Kwa jinsi matengenezo yalivyostawi katika Zurich, matunda yake yalionekana zaidi katika kushinda uovu na kuimarisha utaratibu wa kweli. TU 82.5