METHALI ZA KISWAHILI MIA SITA NA KUMI (610)
- Aanguaye huanguliwa.
- Asiye sikia la mkuu, huvunjika guu.
- Abebwaye hujikaza.
- Adhabu ya kaburi aijuae maiti.
- Adui aangukapo, mnyanyue.
- Adui mpende.
- Adui wa mtu ni mtu.
- Afadhali ya Musa kuliko ya Firauna.
- Ahadi ni deni.
- Ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke.
- Akiba haiozi.
- Akili ni mali.
- Akili ni nywele kila mtu ana zake.
- Akili nyingi huondowa maarifa.
- Akutukanae hakuchagulii tusi.
- Akipenda chongo huita kengeza.
- Akufaae kwa dhiki, ndiye rafiki.
- Akufanyiaye ubaya, mlipe wema.
- Akupaye kisogo si mwenzio.
- Akutendaye mtende, mche asiyekutenda.
- Alisifuye jua, limeuangaza.
- Aliye juu msubiri chini.
- Aliye kando, haangukiwi na mti.
- Aliye kupa wewe kiti (kibao) ndiye aliye nipa mimi kumbi.
- Aliye kutwika, ndiye atakaye kutua.
- Akufukuzae hakwambii toka.
- Aliyekupa mkeka ndiye aliyenipa kumbesa.
- Amani haipatikani mpaka kwa ncha ya upanga.
- Ana hasira za mkizi.
- Anayekuja pasi na hodi, huondoka bila ya kuaga.
- Angurumapo simba, mcheza ni nani?
- Aninyimaye mbazi kanipunguzia mashuzi.
- Apewaye ndiye aongezwaye.
- Anaejipiga mwenyewe, halii.
- Asifuye mvuwa imemnyea.
- Asiye kubali kushindwa si mshindani.
- Asiye kujua, hakuthamini.
- Asiye kuwapo na lake halipo.
- Asiye lelewa na mamae hulelewa na ulimwengu.
- Asiye na mengi, ana machache.
- Asiye uliza, hanalo ajifunzalo.
- Asiyejua maana, haambiwi maana.
- Atangaye na jua hujuwa.
- Atangazaye mirimo, si mwana wa ruwari (Liwali).
- Atekaye maji mtoni hatukani mamba.
- Avumaye baharini papa kumbe wengi wapo.
- Baada ya dhiki faraja.
- Bahari hailindwi.
- Bamba na waume ni bamba, hakuna bamba la mume.
- Bandu bandu huisha gogo.
- Baniani mbaya, kiatu chake dawa.
- Bendera hufuata upepo.
- Biashara asubuhi.
- Bilisi wa mtu ni mtu.
- Bora kinga kuliko tiba.
- Bora lawama kuliko fedheha.
- Bora mchawi kuliko fitina.
- Biashara asubuhi.
- Bora nusu shari kuliko shari kamili.
- Bwawa limeingia ruba.
- Cha mtu mavi.
- Chaka la samba, halilali nguruwe.
- Chamlevi huliwa na mgema.
- Chanda chema huvikwa pete.
- Chelewa chelewa, utakuta mtoto si wako.
- Choko mchokoe pweza, binaadamu hutomuweza.
- Chombo cha kuzama hakina usukani.
- Chovya - chovya yamaliza buyu la asali.
- Chui hakumbatiwi.
- Chururu si ndo ndo ndo.
- Dalili ya mvua mawingu.
- Damu nzito kuliko maji.
- Daraja livuke ulifikapo.
- Dawa ya moto ni moto.
- Daraja ukilibomoa, ujue kuogelea.
- Dau la mnyonge haliendi joshi, likienda joshi ni matakwa ya Mungu.
- Dawa ya moto ni moto.
- Donda ndugu halina dawa.
- Dua ya kuku haimpati mwewe.
- Fadhila huna, hata hisani hukumbuki?
- Fadhila ya nyuki ni moto.
- Fadhila ya punda ni mateke (mashuz)
- Fahari ya macho haifilisi duka.
- Farasi hamuwawezi, tembo mtawalishani?
- Fata nyuki ule asali.
- Fimbo ya mbali haiui nyoka.
- Fumbo mfumbe mjinga, mwerevu huligangua.
- Funika kombe mwanakharamu apite.
- Ganda la mua la jana, chungu kaona kivuno.
- Gome la udi, si la mnuka uvundo.
- Haba na haba, hujaza kibaba.
- Haki ya mtu hailiki.
- Hakuna masika yaso mbu.
- Hakuna msiba usio na mwenziwe.
- Hakuna siri ya watu wawili.
- Hakuna ziada mbovu.
- Hala hala mti na macho.
- Hamadi ni ilio kibindoni, na silaha ni iliyo mkononi.
- Hapana marefu yasio na mwisho.
- Haraka haraka haina baraka.
- haraka haraka haina baraka.
- Haramu yako halali kwa mwenzio.
- Hasidi hasada.
- Hasidi mbaya.
- Hasira, hasara.
- Hatua ndefu hufupisha mwendo.
- Hauchi hauchi, unakucha.
- Hayawi hayawi, mara huwa.
- Heri kufa macho kuliko kufa moyo.
- Heri kujikwa kidole kuliko ulimi.
- Heri nitakula na nini?, kuliko nitakula nini?
- Heri ya marama kuliko kuzama.
- Hiari ya shinda utumwa.
- Hogo halihogoki mpaka kwa hogo jenziwe.
- Hucheka kovu asiye kuwa na jeraha.
- Ila ya kikwapa, kunuka pasipo kidonda.
- Yaliyoopita si ndwele, ganga yajayo.
- Iliyo jaa ndiyo ipunguzwayo.
- Imara ya jembe kaingojee shambani.
- Jambo usilolijua, usiku wa giza.
- Jina jema hungara gizani.
- Jini likujualo halikuli likakwisha.
- Jino la pembe si dawa ya pengo.
- Jitihada haiondoi kudura.
- Jitihadi haiondoi kudura.
- Jogoo la shamba haliwiki mjini.
- Jungu kuu, halikosi ukoko.
- Jununu fununu.
- Kafiri akufaaye, si muislamu asiye kufaa
- Kafiri akufaye si Isilamu asiyekufa.
- Kama hujui kufa,tazama kaburi.
- Kama wewe wasema cha nini, mwezio asema nitakipata lini.
- Kamba hukatika pabovu.
- Kanga hazai ugenini.
- Kawaida ni kama sheria.
- Kawia ufike.
- Kazi mbaya siyo mchezo mwema.
- Kelele za chura hazimzuwii ng'ombe kunywa maji.
- Kelele za mlango haziniwasi usingizi (Kelele za mlango hazimuudhi mwenye nyumba)
- Kenda karibu na kumi.
- Kesho kesho, kesho kiama.
- Kiburi si maungwana.
- Kibuzi na kibuzi hununua jahazi.
- Kichango kuchangizana.
- Kidole kimoja hakivunji chawa.
- Kikulacho ki nguoni mwako.
- Kikushindacho kukila usikitie ila.
- Kila chombo kwa wimblile.
- Kila mbwa hubwekea mlangoni kwao.
- Kila mlango na ufunguwo wake.
- Kila mtoto na koja lake.
- Kila mtu huzikwa na kaburi lake.
- Kila mtu na bahati yake.
- Kila mwamba ngoma ,ngozi huivuta kwake.
- Kila mtu hulilia mamae.
- Kila ndege huruka kwa ubawa wake.
- Kila shetani na mbuyu wake.
- Kilimia kikizama kwa jua, huzuka kwa mvua, na kikizama kwa mvua, huzuka kwa jua.
- Kilio huanza mfiwa ndipo wa mbali wakaingia.
- Kimya kingi kina mshindo mkubwa.
- Kinga na kinga ndipo moto uwakapo.
- Kingiacho mjini si haramu.
- Kinyozi hajinyoi.
- Kinywa ni jumba la maneno.
- Kipendacho moyo dawa.
- Kipofu hasahau mkongojo wake.
- Kipya kinyemi ingawa kidonda.
- Kisebusebu na kiroho papo.
- Kisokula mlimwengu, sera nale.
- Kisokula mlimwengu,sera nale.
- Kisu kimenifika mfupani.
- Kitanda usicho kilalia hukijui kunguni wake.
- Kitumbua kimeingia mchanga.
- Kivuli cha fimbo hakimfichi mtu jua.
- Kiwi cha yule ni chema cha; hata ulimwengu uwishe.
- Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.
- Konzi ya maji, haifumbatiki.
- Konzo ya maji haifumbatiki.
- Kosa moja haliachi mke.
- Kozi mwandada, kulala na njaa kupenda.
- Kuagiza kufyekeza.
- Kuambizana kuko kusikilizana hapana.
- Kucha M'ngu si kilemba cheupe.
- Kuchamba kwingi, kuondoka na mavi.
- Kufa kufaana.
- Kufa kwa jamaa, harusi.
- Kufa kwa mdomo,mate hutawanyika.
- Kufanaya kosa sio kosa, kosa ni kurudia kosa.
- Kuishi kwingi, kuona mengi.
- Kujikwa si kuanguka,bali ni kwenda mbele.
- Kujikwaa si kuanguka, bali ni kwenda mbele.
- Kukopa harusi kulipa matanga.
- Kukopa harusi, kulipa matanga.
- Kuku havunji yai lake.
- Kuku mgeni hakosi kamba mguuni.
- Kula kutamu ,kulima mavune.
- Kulea mimba si kazi kazi kulea mwana.
- Kukopa harusi, kulipa matanga.
- Kumuashia taa kipofu ni kuharibu mafuta.
- Kunako matanga kume kufa mtu.
- Kunguru mwoga hukimbiza mbawa zake.
- Kupanda mchongoma, kushuka ndio ngoma.
- Kupata si werevu, na kukosa si ujinga.
- Kupoteya njia ndiyo kujua njia.
- Kurambaramba ndio kula, kunenepa kwake Mola.
- Kusikia si kuona.
- Kutangulia si kufika.
- Kutoa ni moyo usambe ni utajiri.
- Kutu kuu ni la mgeni.
- Kuugua sio kufa.
- Kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi.
- Kuzima koleo si mwisho wa uhunzi.
- Kwa mwoga huenda kicheko na kwa shujaa huenda kilio.
- Kweli ilio chungu, si uongo ulio mtamu.
- Kwenda mbio siyo kufika.
- Kwenye miti hakuna wajenzi.
- La kuvunda halina rubani.
- La kuvunda halina ubani.
- Lake mtu halimtapishi bali humchefua.
- Leo kwako, kesho kwa mwenzio.
- Leo ni leo asemayo kesho ni mwongo.
- Liandikwalo ndiyo liwalo.
- Lila na fila hazitangamani.
- Lipitalo, hupishwa .
- Lisemwalo lipo,ikiwa halipo laja.
- Lisilo na mkoma, hujikoma lilo.
- Lisilokuwapo moyoni, halipo machoni.
- Maafuu hapatilizwi.
- Macho hayana pazia.
- Mafahali wawili hawakai zizi moja.
- Maiti haulizwi sanda.
- Maji hayapandi mlima.
- Maji hufuata mkondo.
- Maji ukiyavuliya nguo huna budi kuyaoga.
- Maji usiyoyafika hujui wingi wake.
- Maji ya kifuu, bahari ya chungu.
- Maji yakijaa hupwa.
- Maji yakimwagika hayazoleki.
- Maji yamenifika shingoni.
- Majuto ni mjukuu.
- Mali ya bahili huliwa na wadudu.
- Mama ni mama, hata kama ni rikwama.
- Mama nipe radhi kuishi na watu kazi.
- Mambo kunga.
- Manahodha wengi chombo huenda mrama.
- Maneno makali hayavunji mfupa.
- Maneno mazuri humtowa nyoka pangoni.
- Maneno si mkuki.
- Mapenzi ni kikohozi, hayawezi kufichika.
- Masikini akipata matako hulia mbwata.
- Masikini haokoti,akiokota huambiwa kaiba.
- Masikini na mwanawe tajiri na mali yake.
- Maskini hana kinyongo.
- Mavi usioyala, wayawingiani kuku?
- Mavi ya kale hayanuki.
- Mbinu hufuata mwendo.
- Mbio za sakafuni huishia ukingoni.
- Mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo.
- Mchagua jembe si mkulima.
- Mchagua nazi hupata koroma.
- Mchagua nazi si mfuaji.
- Mchakacho ujao,halulengwi na jiwe.
- Mchama ago hanyeli,huenda akauya papo.
- Mchamba kwingi mara ujitia dole.
- Mcheka kilema hafi bila kumpata.
- Mchele mmoja mapishi mengi.
- Mchelea mwana kulia hulia yeye..
- Mcheza hawi kiwete, ngoma yataka matao.
- Mcheza kwao hutuzwa.
- Mcheza na tope humrukia.
- Mchezea mavi, hayaachi kumnuka.
- Mchezea zuri, baya humfika.
- Mchimba kisima hungia mwenyewe.
- Mchonga mwiko hukimbiza mkono wake.
- Mchuma janga hula na wakwao.
- Mchumia juani,hulia kivulini.
- Mdharau biu, hubiuka yeye.
- Mdharau mwiba humchoma.
- Meno ya mbwa hayaumani.
- Mfa maji haachi kutapatapa.
- Mfa maji hukamata maji.
- Mficha uchi hazai.
- Mfinyazi hulia gaeni.
- Mfuata nyuki hakosi asali.
- Mfukuzwa kwao hana pakwenda.
- Mgaagaa na upwa hali ugari kande.
- Mganga hajigangi.
- Mgema akisifiwa tembo hulitia maji.
- Mgeni ni kuku mweupe.
- Mgeni njoo mwenyeji apone.
- Mgomba haushindwi na mkunguwe.
- Mgonjwa haulizwi uji.
- Miye nyumba ya udongo, sihimili vishindo.
- Mjinga akierevuka mwerevu yupo mashakani.
- Mjinga mpe kilemba utamuona mwendowe.
- Mjumbe hauawi.
- Mkaidi hafaidi mpaka siku ya idi.
- Mkamatwa na ngozi ndiye mwizi.
- Mkamia maji hayanywi.
- Mkamia maji hayanywi.
- Mkataa la mkuu huvunjika guu.
- Mkataa wengi ni mchawi.
- Mkataa ya Musa hupata ya Firauna.
- Mke ni nguo, mgomba kupalilia.
- Mkono moja hauchinji ng'ombe.
- Mkono moja haulei mwana.
- Mkono mtupu haulambwi.
- Mkono usioweza kuukata,ubusu.
- Mkosa kitoweo humangiria.
- Mkuki kwa nguruwe, kwa mwanadamu uchungu.
- Mkulima ni mmoja walaji ni wengi.
- Mla cha mwenziwe na chake huliwa.
- Mla cha uchungu na tamu hakosi.
- Mla kuku wa mwenziwe miguu humwelekea.
- Mla mbuzi hulipa ngombe.
- Mla mla leo mla jana kala nini?
- Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.
- Mlala na maiti haachi kulia lia.
- Mlenga jiwe kundini hajui limpataye.
- Mlimbua nchi ni mwananchi.
- Mnyamaa kadumbu.
- Mnywa maji kwa mkono mmoja,Kiu yake i pale pale.
- Moja shika, si kumi nenda urudi.
- Moto hauzai moto.
- Mpanda farasi wawili hupasuka msamba.
- Mpanda ngazi hushuka.
- Mpanda ovyo hula ovyo.
- Mpemba akipata gogo hanyii chini.
- Mpemba hakimbii mvua ndogo.
- Mpende akupendae asiyekupenda achana naye.
- Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonowe.
- Mpofuka ukongweni,hapotewi na njia.
- Msafiri kafiri.
- Msafiri masikini ajapokuwa sultani.
- Msasi haogopi mwiba.
- Msema kweli hukimbiwa na rafiki zake.
- Msema pweke hakosi.
- Mshika kisu, hashiki makalini.
- Mshale kwenda msituni haukupotea.
- Mshoni hachagui nguo.
- Msi bahati, habahatishi.
- Msi mbele, hana nyuma.
- Msishukuru mja, hamshukuru Molawe.
- Msitukane wagema na ulevi ungalipo.
- Msitukane wakunga na uzazi ungalipo.
- Mstahimilivu hula mbivu.
- Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
- Mtaka lake hasindwi.
- Mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba.
- Mtaka unda haneni.
- Mtaka uzuri hudhurika.
- Mtaka yote hukosa yote.
- Mtegemea nundu haachi kunona.
- mtegemea nundu, haachi konona.
- Mtego bila ya chambo, haunasi.
- Mtembezi hula miguu yake.
- Mteuzi heshi tamaa.
- Mti hauwendi ila kwa nyenzo.
- Mtondoo haufi maji.
- Mtoto akililia wembe mpe.
- Mtoto umleyavyo ndivyo akuavyo.
- Mtoto wa nyoka ni nyoka.
- Mtu hakatai mwito,hukata aitwalo.
- Mtu hujikuna ajipatapo.
- Mtu huulizwa amevaani ,haulizwi amekulani.
- Mtumai cha ndugu hufa masikini.
- Mtumi wa kunga haambiwi maana.
- Mtumikie kafiri upate mradi wako.
- Mtupa jongoo hutupa na mti wake.
- Muhitaji khanithi walau kana rijaali.
- Muiba yai leo kesho hua mwizi wa ng'ombe.
- Mume wa mama ni baba.
- Mungu hamfichi mnafiki.
- Mungu si asumani.
- Muonja asali haonji mara moja.
- Muuza sanda, mauti kwake harusi.
- Mvua nguo, huchutama.
- Mvumbika changa hula mbovu.
- Mvumbika pevu hula mbivu na mvumbika changa hula mbovu.
- Mvungu mkeka.
- Mvunja nchi ni mwananchi.
- Mvuvi ajuwa pweza alipo.
- Mwacha asili ni mtumwa.
- Mwamba na wako hukutuma umwambiye.
- Mwamini Mungu si mtovu.
- Mwana maji wa kwale kufa maji mazowea.
- Mwana mkuwa nawe ni mwenzio kama wewe.
- Mwana simba ni simba.The child of lion is a lion.
- Mwana wa kuku hafunzwi kuchakura.
- Mwana wa mtu ni kizushi, akizuka, zuka naye.
- Mwanga mpe mtoto kulea.
- Mwangaza mbili moja humponyoka.
- Mwanzo kokochi mwisho nazi.
- Mwanzo wa chanzo ni chane mbili.
- Mwanzo wa ngoma ni lele.
- Mwapiza la nje hupata la ndani.
- Mwekaji kisasi haambiwi mwerevu.
- Mwenda bure si mkaa bure,huenda akaokota.
- Mwenda mbio hujikwa kidole.
- Mwenda omo na tezi marejeo ni ngamani.
- Mwenda pole hajikwai.
- Mwenda wazimu hapewi panga.
- Mwenda wazimu hapoi, bali hupata nafuu.
- Mwenye haja hwenda chooni.
- Mwenye kelele hana neno.
- Mwenye kovu usidhani kapowa.
- Mwenye kubebwa hujikaza.
- Mwenye kuchinja hachelei kuchuna.
- Mwenye kuumwa na nyoka akiona jani hushtuka.
- Mwenye macho haambiwi tazama.
- Mwenye mdomo hapotei.
- Mwenye nguvu mpishe.
- Mwenye njaa hana miko.
- Mwenye pupa hadiriki kula tamu.
- Mwenye shibe hamjui mwenye njaa.
- Mwenye shoka hakosi kuni.
- Mwenye tumbo ni tumbole, angafunga mkaja.
- Mwenzako akinyolewa wewe tia maji.
- Mwibaji na watwana, mlifi ni mwungwana.
- Mwili wa mwenzio ni kando ya mwilio.
- Mwizi hushikwa na mwizi mwenziwe.
- Mwomba chumvi huombea chunguche.
- Mwosha hadhuru maiti.
- Mwosha huoshwa.
- Mwosha husitiri maiti.
- Mzaha,mzaha, mara hutumbuka usaha.
- Mzazi haachi ujusi.
- Mzigo usiouweza unaubebea nini?
- Mzigo Wa mwenzio ni kanda Ia usufi.
- Mzika pembe ndiye mzua pembe.
- Mzowea kutwaa, kutoa ni vita.
- Mzowea vya kunyonga, vya kuchinja haviwezi.
- Mzungu Wa kula hafundishwi mwana.
- Nahodha wengi, chombo huenda mrama.
- Nani kama mama?
- Natuone ndipo twambe, kusikia Si kuona.
- Nazi haishindani na jiwe.
- Nazi mbovu harabu ya nzima.
- Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu.
- Ndege mwigo hana mazowea.
- Ndevu sio shani, hata beberu anazo.
- Ndugu chungu, jirani mkungu.
- Ndugu mwui afadhali kuwa naye.
- Ndugu wakigombana, chukua jembe ukalime, wakipatana chukua kikapu ukavune.
- Ngoja! ngoja? huumiza matumbo.
- Ngoma ivumayo haidumu.
- Ngoma ivumayo haikawii kupasuka.
- Ngoma ya kitoto, haikeshi.
- Ng'ombe avunjikapo guu hurejea zizini.
- Ng'ombe haelemewi na nunduye.
- Ngombe wa Maskini hazai.
- Ngozi ivute ili maji. ( Udongo upate uli maji )
- Nguo ya kuazima, Haistiri matako.
- Nia njema ni tabibu, nia mbaya huharibu.
- Nifae na mvua nikufae na jua.
- Nimekula asali udogoni, utamu ungali gegoni.
- Nimekupaka wanja, wewe wanipaka pilipili.
- Nimerejesha kikombe na kisahani chake.
- Njia ya muongo fupi.
- Njia ya mwongo ni fupi.
- Njia ya siku zote haina alama.
- Nta Si asali; nalikuwa nazo Si uchunga.
- Nyani haoni kundule, huliona la mwenziwe.
- Nyani haoni kundule.
- Nyimbo mbaya haibembelezewi mtoto.
- Nyimbo ya kufunzwa haikeshi ngoma.
- Nyongeza huenda kwenye chungu.
- Nyota njema huonekana asubuhi.
- Nyumba usiyolala ndani huijui ila yake.
- Nyumba ya udongo haihimili vishindo.
- Nzi kufa juu ya kidonda Si haramu. (Jihadi ya nzi, kufa kidondani)
- Ondoa dari uwezeke paa.
- Pabaya pako Si pema pa mwenzako.
- Padogo pako Si pakubwa pa mwenzako.
- Painamapo ndipo painukapo.
- Paka akiondoka, panya hutawala.
- Paka hakubali kulala chali.
- Paka hashibi kwa wali, matilabaye ni panya.
- Paka wa nyumba haingwa.
- Panapo wengi hapaharibiki neno.
- Papo kwa papo kamba hukata jiwe.
- Pele hupewa msi kucha.
- Pema usijapo pema; ukipema Si pema tena.
- Penye kuku wengi usimwage mtama.
- Penye mafundi, hapakosi wanafunzi.
- Penye mbaya wako, hapakosi mwema wako/na mwema wako hakosi.
- Penye miti hakuna wajenzi.
- Penye nia pana njia.
- Penye urembo ndipo penye urimbo.
- Penye wazee haliharibiki neno.
- Penye wengi pana mengi.
- Penye wengi pana Mungu.
- Pilipili usoila, wewe inakuwashia nini?
- Pole pole ndio mwendo.
- Pwagu hupata pwaguzi.
- Radhi ni bora kuliko mali .
- Radhi za wazee, ni fimbo.
- Sahani iliyofunikwa, kilichomo kimesitirika.
- Sahau ni dawa ya Waja.
- Samaki mmoja akioza, huoza wote.
- Samaki mpinde angali mbichi.
- Shida haina hodi.
- Shida huzaa maarifa.
- Shika! Shika! na mwenyewe uwe nyuma.
- Shimo Ia ulimi mkono haufutiki.
- Shoka lisilo mpini halichanji kuni.
- Si kila king'aacho ni dhahabu.
- Si kila mwenye makucha huwa simba.
- Si Mungu mtupu na mkono wa mtu.
- Sikio halilali na njaa.
- Sikio halipwani kichwa. (Sikio halipiti kichwa).
- Sikio Ia kufa halisikii dawa.
- Siri ya mtungi aijuaye ni kata.
- Sitaacha kula mkate kwa kuogopa kiungulia.
- Siku njema huonekana asubuhi.
- Siku utakayokwenda uchi, ndiyo siku utakayokutana na mkweo.
- Siku ya kufa nyani, miti yote huteleza.
- Siku za mwizi, arubaini.
- Simba mwenda kimya (pole) ndiye mla nyama.
- Simbiko haisimbuki ila kwa msukosuko.
- Sio shehe bali ni shehena.
- Siri ya maiti aijuaye muosha.
- Sitafuga ndwele na waganga tele.
- Sitapiki nyongo harudi haramba.
- Subira ni ufunguo Wa faraja.
- Sumu mpe paka, mbuzi utamdhulumu.
- Sumu ya neno ni neno.
- Tabia ni ngozi ya mwili.
- Tamaa mbele, mauti nyuma.
- Taratibu ndio mwendo.
- Tawi kavu kuanguka si ajabu.
- Teke Ia kuku halimuumizi mwanawe
- Tonga si tuwi
- Tunda jema halikawii mtini.
- Ucheshi wa mtoto ni anga Ia nyumba.
- Ujuzi hauzeeki.
- Uchungu wa mwana, aujue mzazi.
- Udongo uwahi ungali maji (Udongo upate uli maji)
- Udugu wa nazi hukutania chunguni (Udugu wa nazi hukutana pakachani)
- Uji hajauonja, tayari ushamuunguza
- Ukenda kwa wenye chongo, fumba lako jicho.
- Ukimpa shubiri huchukua pima.
- Ukimuiga tembo kunya, utapasuka Makalio.
- Ukimwamsha alolala utalala weye.
- Ukinyofoa mnofu, ukumbuke kuguguna mfupa.
- Ukiona kwako kunaungua kwa mwenzako kunateketea.
- Ukiona moshi, chini kuna moto.
- Ukiona neno, usiposema neno, hutapatikana na neno.
- Ukiona vinaelea, vimeundwa.
- Ukiona zinduna, na ambari iko nyuma.
- Ukistahi mke ndugu, huzai nae.
- Ukitaja nyoka, shika fimbo mkononi.
- Ukitaka kula nguruwe, chagua aliye nona.
- Ukitaka salama ya dunia, zuia ulimi wako.
- Ukiujua wa mbele, nina ujua wa nyuma.
- Ukupigao ndio ukufunzao.
- Ukuukuu wa kamba Si upya wa ukambaa.
- Ulimi hauna mfupa.
- Ulimi unauma kuliko meno.
- Ulipendalo hupati, hupata ujaaliwalo.
- Ulivyoligema, utalinywa.
- Umeadimika kama la jogoo.
- Umegeuka mung'unye waharibika ukubwani.
- Umejigeuza pweza, unajipalia makaa?
- Umekuwa bata akili kwa watoto?
- Umekuwa nguva, huhimili kishindo?
- Umeruka mkojo unakanyaga mavi.
- Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
- Unajenga kwa mwenzio na kwako kunaporomoka!!
- Unakuja juu kama moto wa kifuu.
- Unamlaumu mwewe, kipanga yuwesha kuku.
- Ungalijua alacho nyuki, usingalionja asali.
- Ushikwapo shikamana (Ukibebwa usijiachie).
- Usiache kunanua kwa kutega.
- Usiache mbachao kwa msala upitao.
- Usiache tawi kabla ya kushika tawi.
- Usiandikie mate na wino ungalipo
- Usicheze na simba, ukamtia mkono kinywani.
- Usijifanye kuku mweupe.
- Usikaange mbuyu ukawaachia wenye meno
- Usile na kipofu ukamgusa rnkono.
- Usimgombe mkwezi, nazi imeliwa na mwezi.
- Usiniache njia panda.
- Usinikumbushe kilio matangani.
- Usinipake mafuta kwa nyuma ya chupa.
- Usinivishe kilemba cha ukoka.
- Usione simba kapigwa na mvua.
- Usipoziba ufa utajenga ukuta.
- Usisafirie nyota ya mwenzio.
- Usisahau ubaharia kwa sababu ya unahodha.
- Usishindane na Kari; Kari ni mja wa Mungu.
- Usitukane wagema na ulevi ungalipo.
- Usitukane wakunga na uzazi 'ungalipo.
- Utakosa mtoto na maji ya moto.
- Usiyavuke maji usiyoweza kuyaoga.
- Utaula na chua kwa uvivu wa kuchagua.
- Vita havina macho.
- Vita si lele mama.
- Vita vya panzi, neema ya kunguru
- Waarabu wa pemba, hujuana kwa vilemba
- Wache waseme.
- Wafadhilaka wapundaka.
- Wagombanao ndio wapatanao.
- Watu wanahisabu nazi, wewe unahisabu makoroma.
- Wapiganapo tembo wawili ziumiazo ni nyasi.
- Watetea ndizi, mgomba si wao.
- Wazuri haweshi.
- Wema hauozi..
- wengi wape.
- Zinguo la mtukufu, ni ufito.