Seventh-day Adventist® Church

PASTOR LETTA'S OFFICIAL WEBSITE

Menu

WAEFESO

MASWALI YA KUJADILI: WAEFESO 1:1-23

  1. Je watakatifu walioko Efeso wanaoandikiwa waraka huu walikuwa wakamilifu kiasi cha kustahili kuitwa watakatifu? (Waefeso 3:16-17). Je kuna mwanadamu aliye mkamilifu ambaye afanya mema tu asifanye uovu? (Mwanzo 6:9; Ayubu 1:1; Zaburi 53:3). Baraka zote za rohoni ambazo Mungu Baba ametubariki nazo ndani ya Kristo katika ulimwengu wa roho ni zipi?
  2. Mungu alituchaguaje katika Kristo kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu? Kwa nini atuchague na alituchagua miongoni mwa nani? Kama alituchagua tuwe watakatifu na watu wasio na hatia ilikuwaje akatuachia tutende dhambi? Kama alituchagua tuwe watakatifu na wasio na hatia je hiyo inamaanisha jukumu la kutufanya watakatifu na wasio na hatia ni letu au ni lake?
  3. Mungu alitangulia kutuchagua kabla ya nini? Kabla hatujafanywa kuwa wanawe tulikuwa na hadhi gani? Hali hiyo ya kufanywa wana imetuongezea nini cha muhimu ambacho hatukuwa nacho hapo mwanzo? Utukufu wa neema yake iliyotuneemesha katika huyo Mpendwa ukoje hata ustahili kusifiwa?Huyo Mpendwa anayetajwa hapo ni nani na kwa nini anaitwa Mpendwa?
  4. Ukombozi wetu umepatikanaje kupitia damu ya Yesu? Damu ya Yesu imewezaje kufuta dhambi za wanadamu? Damu hiyo ilizifuta dhambi baada ya kuungamwa na wanadamu au hata kabla? Ukombozi wetu ulimtegemea Yesu au ulitegemea utayari wetu wa kuokolewa? Mungu atavijumlishaje vitu vyote katika Kristo Yesu? Tulifanywaje urithi ndani ya Kristo?
  5. Tumaini la mwito wake Kristo likoje? Utajiri wa utukufu wa urithi wake Kristo ukoje? Ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio ukoje? Huyo ambaye Mungu alivitia vitu vyote chini ya miguu yake ni nani? Je ujumbe huu unamhusu Yesu peke yake au unawahusu hata watakaokombolew? (Waebrania 2:6-8)

MASWALI YA KUJADILI: WAEFESO 2:1-22

  1. Nini tofauti kati ya dhambi na makosa? Ni kwa namna gani dhambi na makosa vinasababisha hali ya kuwa mfu? (1 Timotheo 2:14). Mfalme wa uweza wa anga anayetajwa hapa ni nani? Kwa nini anaitwa mfalme wa uweza wa anga? Kwa nini kuyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia kunamfanya mtu awe mwana wa kuasi? Kwa nini wana wa kuasi wanaitwa pia watoto wa hasira?
  2. Kwa nini inatajwa kuwa Mungu alitupenda kwa mapenzi yake makuu? Hayo mapenzi yake makuu yakoje hata yakaitwa makuu? (Yhona 15:13). Mungu alituhuishaje pamoja na Kristo wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu? Ni kipi sahihi kusema tumeokolewa kwa neema au tutaokolewa kwa neema? (Wakolosai 1:13; 2 Timotheo 1:9; Tito 3:4; 2 Wakorintho 1:10).
  3. Ni lini Mungu alipotufufua pamoja na Kristo na kutuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho? Je, hiyo ni kumaanisha Mungu anatuchukulia kama tulioshinda tayari? Mungu anaudhihirishaje wingi wa neema yake upitao kiasi kwetu sisi katika Kristo Yesu? Kwa nini Maandiko yanasema wokovu wetu haukutokana na nafsi zetu? Tito 3:3-5).
  4. Je wanadamu wangeokolewa kwa kutegemea matendo yao wangekuwa watu wa kujisifu sana? Je wale wanaopenda kujisifu huku wakidai wameokolewa kwa neema kwa njia ya imani wanakwama wapi? Ni lini tulipoumbwa katika Kristo Yesu ili tutende matendo mema? Hayo matendo mema yalitengenezwaje ndani yetu ili tuenende nayo?
  5. Nikijihisi sina matendo mema natakiwa nifanye juhudi kuyatafuta na kuyafanya au natakiwa nimuombe Mungu ayaumbe tena ndani yangu? Zamani imetajwa sana katika sura hii. Unadhani zamani hiyo ni ipi na kwa nini inaitwa zamani? Ni kwa namna gani kufarakana kwetu na jamii ya Israeli kulitufanya wageni wasio na maagano ya ahadi na tusio na tumaini na tusio na Mungu duniani? Damu ya Yesu Kristo ilifanya nini kilichotuvuta sisi tuliokuwa mbali kuwa karibu?
  6. Damu ya Yesu Kristo ilifanya nini kilichotuvuta sisi tuliokuwa mbali kuwa karibu? Kristo aliuondoaje uadui uliokuwa baina ya jamii ya Israeli na mataifa mengine yasiyo na agano kwa njia ya mwili wake? Kwa nini Yesu anaitwa jiwe kuu la pembeni? Kwa nini Wayahudi waliodhaniwa wapo karibu na Mungu nao walihitaji kuhubiriwa amani?

 MASWALI YA KUJADILI: WAEFESO 3:1-21

  1. Paulo anakuwaje mtume wa Kristo Yesu kwa ajili ya Wamataifa na si kwa ajili ya Wayahudi? Kwa nini Paulo anaiita hali ya kuwatumikia Wamataifa kuwa ni ufungwa kwa ajili ya Kristo Yesu? Siri yake Kristo aliyofunuliwa Paulo ambayo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine ni ipi? Kwa nini Wamataifa kushirikishwa urithi pamoja na Wayahudi iitwe siri? Kwa nini jambo hilo halikufunuliwa mapema? Kwa nini bila injili Wamataifa hawawezi kushiriki urirhi na Wayahudi?
  2. Je ni lazima ufanywe mhudumu wa injili na Mungu ili kuihubiri injili? Kigezo gani kinakufanya udhani umefanywa mhudumu wa injili? Je kuhubiri injili ni kuhubiri utajiri wake Kristo usiopimika? Utajiri huo unahusu nini? Je katika kuzungumzia injili inawezekana kujiepushana na dhana ya utajiri? Je utajiri unapingana na injili? Kwa nini utajiri wake Kristo ni usiopimika? Je, Mungu ana kusudi la kutushirikisha utajiri huo?
  3. Kwa nini Wamataifa ndiyo wanufaikaji wakuu wa utajiri wake Kristo usiopimika? Kwa namna gani Paulo aliweza kuwaangazia watu wote madaraka ya siri hiyo? Hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ambayo kupitia kanisa Mungu amekusudia kuifikisha kwa falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho ni ipi? Kwenye kusudi la milele Mungu alikusudia nini katika Yesu Bwana wetu? Kwa nini linaitwa kusudi la milele?
  4. Je utu wetu wa ndani unafanywa imara kwa nguvu zetu wenyewe au kwa msaada wa Roho Mtakatifu? Kwa nini ili Kristo akae mioyoni mwetu tuatakiwa kuufanya upendo kuwa shina na msingi? Kwa nini kuufahamu upendo wa Kristo ni kwa mihimu kwa Mkristo? Upendo wa Kristo unapimikaje kwa upana, urefu, kimo, na kina? Kwa nini upendo wa Kristo unaitwa upitao fahamu au uelewa wetu? Kama unapita fahamu tutawezaje kuufahamu?
  5. Kwa nini kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu kunategemea jinsi tunavyouelewa upendo huu wa Kristo? Kuna ushahidi gani kwamba Mungu aweza kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo? Na ni kwa nini anafanya hivyo? Ile inayotajwa kama nguvu itendayo kazi ndani yetu ni nini na inatendaje hiyo kazi? Kwa nini Mungu atukuzwe kwa utendaji huo katika kanisa na katika vizazi vyote vya milele na milele?

MASWALI YA KUJADILI: WAEFESO 4:1-32

  1. Umoja wa Roho katika kifungo cha amani unahifadhiwaje? Ubatizo mmoja unaopendekezwa hapa ni upi? Ni ule wa kuzamishwa majini au ni ule wa kunyunyizwa maji kichwani? Huyo aliyepaa juu na kuteka mateka ni nani? Hao mateka walikuwa nani na kwa nini wanaitwa mateka? Ni nani anayewapa wanadamu vipawa na kwa kusudi gani?
  2. Kwa nini akili za watu wa mataifa zinetiwa giza? Matokeo ya akili zao kutiwa giza ni nini? Kwa nini utu wa kale unavuliwa na utu mpya unavaliwa kama vazi? Ili uvue na kuvaa utu wa kale na mpya kunahitajika kitu gani? Kwa nini ni lazima roho ya nia ifanywe upya ili mtu avue utu wa kale na kuvaa utu mpya? Je kuna hasira isiyotenda dhambi? Je hasira inatakiwa idumu kwa muda gani na kwa nini?
  3. Kwa nini kutunza uchungu kwa muda mrefu ni kumpa Ibilisi nafasi? Je kufanya kazi za mikono kwaweza kumzuia mtu asiwe mwizi? Kwa nini ni muhimu kuwa na pato la ziada kwa ajili ya kusaidia wahitaji? Unadhani uchungu unaotunzwa moyoni ndicho chanzo cha maneno maovu yanayotoka mdomoni? Utajuaje kama neno unalotoa ni jema la kumfaa anayesikia? Magomvi yanamhuzunishaje Roho Mtakatifu?

 MASWALI YA KUJADILI WAEFESO 5:1-33

  1. Kuna umuhimu gani wa kumfuata Mungu kama watoto wapendwao? Je ukiwa na hisia kuwa hupendwi unaweza kumfuata Mungu kwa mafanikio kama yule ajuaye kuwa anapendwa? Je, upendo unahusiana na kujitoa kwa ajili ya wengine? Kristo alijitoaje kwa ajili yetu kama sadaka na dhabihu kwa Mungu kuwa harufu ya manukato? (1 Yohana 3:16). Uchafu wowote wa kutamani ambao haupaswi kutajwa kwetu kama watakatifu ni upi? Kuna utofauti gani kati ya uasherati na uzinzi?
  2. Kwa nini Maandiko yanasema uasherati usitajwe kwetu? Je inamaanisha kutajwa au kufanywa? Kwa nini waasherati wala wachafu wala wenye tamaa hawatakuwa na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu? (Mwanzo 19:1-13). Matendo ya giza yasiyozaa ni yepi? Kwa nini katika zamani hizi za uovu inapendekezwa kwenda kwa hekima na kuukomboa wakati? Kuna uhusiano gani kati ya kulewa kwa mvinyo na kujazwa na Roho Mtakatifu? (Matendo 2:12-18).
  3. Kusemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni hufanyika kwa namna gani? Kwa nini kunaitwa kusemezana? Nyimbo za rohoni zikoje? Kwa nini kumshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo kunasisitizwa sana? Kwa nini shukrani hizo zisielekezwe kwa Yesu moja kwa moja? Kwa nini wake wanahimizwa kuwatii waume zao kama kumtii Bwana wetu? Je hii haiwezi kuwa ibada ya sanamu?
  4. Kwa nini tena wake wanatakiwa kuwatii waume zao kwa kila jambo? Je hii haimfanyi mke kunyanyasika na kuwa mtumwa wa mume? (1 Wakorintho 6:20; 1 Wakorintho 7:23). Je waume wanaweza kuwapenda wake zao kama Kristo alivyolipenda kanisa hadi kulifia? Je mume ni kichwa cha kanisa au ni kichwa cha mkewe? Je wake waweza kuwatii waume zao kama kanisa limtiivyo Krito?
  5. Je ni wajibu wa mume kusaidia kumuondolea mke wake tabia zisizofaa zinazofananishwa na makunyanzi kama afanyavyo Kristo kwa kanisa lake? Je ni wajibu wa mume kumtunza mke wake kwa kumhudumia kwa chakula na mavazi? Kuacha wazazi wakati wa kuoana kunawahusu wote wawili au mume tu? (Mwanzo 2:24; Waefeso 4:31). Kwa nini waume wanapenda sana kustahiwa?

MASWALI YA KUJADILI: WAEFESO 6:1-24

  1. Watoto wanawatiije wazazi wao katika Bwana? Je ni haki kumtii mzazi asiyejiheshimu na anayetia aibu kwa jamii kwa mienendo yake? Kutii wazazi kunaleta baraka gani katika maisha? Je ni halali kumtunza mzazi aliyeķutelekeza ulipokuwa mdogo au kwenye changamoto? Je, ni halali kuingilia ugomvi wa wazazi kwa kumzuia kwa kutumia nguvu baba anayemnyanyasa na kumuonea mama kwa vipigo vikali vya mara kwa mara?
  2. Wakina baba huwachokoza watoto wao kwa namna gani? Kwa nini lawama hii ni kwa wakina baba zaidi kuliko kwa wakina mama? Je, wakina baba huonekana wabaya kwa watoto kwa sababu ndiyo wamekuwa wakitoa adhabu na maonyo zaidi kwa watoto kuliko mama? Je, ni halali watumwa kuwataka wawatii mabwana zao wakati utumwa ni biashara haramu? Je mafungu kama haya yalitumika kuhalalisha biashara ya utumwa na hayafai kutumika leo?
  3. Kwa nini tunatakiwa kuwa hodari katika Bwana? Ni mambo gani tunatakiwa kufanya katika kuhakikisha tunakuwa hodari katika Bwana? Wakuu wa giza hili wanaotajwa hapa ni nani? Kuomba katika Roho kunafanyikaje? Kwa nini kuomba katika Roho kunahitajika kila wakati? Je kusali kwa kukesha kunahitajika leo? Je, kukesha ili kuitwe kukesha kunatakiwa kufanyike kwa muda. gani? (Mathayo 26:40).
  4. Kwa nini kuwaombea watumishi wa Mungu kunahitajika sana? Je watakatifu wanahitaji ƙombewa? Waombewe nini wakati wao ni watakatifu? Je kuhubiri kwa ujasiri siri ya Injili kunahitaji kuombewa? Siri hiyo ya Injili ni nini? Kwa nini inaitwa siri? Kwa nini Paulo anajiita mjumbe katika minyonyoro?