Seventh-day Adventist® Church

PASTOR LETTA'S OFFICIAL WEBSITE

Menu

WAEBRANIA

MASWALI YA KUJADILI: WAEBRANIA 1:1-14

  1. Njia nyingi ambazo Mungu alisema na baba zetu katika manabii ni zipi? Huyo Mwana ambaye Mungu amemfanya kuwa mrithi wa yote ni nani? Yesu alivichukuaje vitu vyote kwa amri ya uweza wake? Uweza na uwezo vinatofautianaje? Mkono wa kuume wa ukuu huko juu ina maana gani?
  2. Jina tukufu lipitalo jina la Malaika Yesu amelirithi kutoka kwa nani? Je Yesu kama Mwana ana kiti chake che enzi? Mwanadamu alitawazwa lini juu ya kazi za mikono ya Mungu? Ni lini vitu vyote vitakapowekwa chini ya nyayo zake?
  3. Maandiko yanaposema hakuna kilichosazwa kisichowekwa chini ya nyayo za binadamu yanamaanisha nini? Je Yesu alifanywa mdogo punde kuliko Malaika? Kama Yesu ni mdogo kwa Malaika kwa nini wanamsujudia? (Waebrania 1:6). Mateso yalitumikaje kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu?

MASWALI YA KUJADILI: WAEBRANIA 2:1-18

  1. Ipi ni fursa muhimu kati ya kusikia na kuzingatia yale yaliyosikiwa? (1 Wakorintho 9:27). Ni kwa nini inatokea kwa waliosikia kutonufaika na kusikia huko? (Waebrania 4:2). Yesu aliposema mwenye masikio ya kusikia alimaanisha masikio au uwezo wa kuzingatia ulihozingatia?
  2. Ni nini tofauti ya kosa na uasi? Ujira wa haki wa kos ana uasi ni upi? Kwa nini kutojali wokovu kunawaondolea wanadamu uwezekano wa kuokolewa? Je kutochagua kuokolewa ni kutojali wokovu? Kwa nini wokovu wa wanadamu unatambulika ama wokovu mkuu? (Waefeso 2:4-7; Waefeso 3:18-19).
  3. Biblia inaposema magawanyo ya Roho Mtakatifu inakusudia kusema nini? Unadhani Mungu alikuwa amekusudia injili ipelekwe kwa kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi? Nini kimezuia kwa sasa hali hiyo kujidhihirisha? Mungu hajauweka chini ya malaika ulimwengu ule ujao bali hini ya mwanadamu. Ukweli huo unakutambulisha ya mwanadamu kukombolewa itakuwaje?
  4. Unadhani hivyo vitu ambavyo havijawekwa chini ya mwanadamu kwa sasa na ambavyo vitawekwa wakati ujao ni vipi? Nini kinachozuia vitu hivyo visiwekwe chini ya mwanadamu kwa sasa? Taji ya utukufu na heshima aliyovikwa mwanadamu ni ipi nak wa nini amevikwa taji hiyo? Je, kile kinachomstahili kwa ushindi wake juu ya dhambi kinamstahili mwanadamu atakayekombolewa pia? (Waebrania 2:6-11; 1 Petro 4:13).
  5. Huyo ambaye vitu vyote vimekuwako kwa ajili yake na kwa njia yake ni nani? Huyo aliyekuwa anamkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso ni nani? Kulikuwa na ulazima gani kiongozi huyo wa wokovu akamilishwe kwa njia ya mateso? Anayetakasa na anayetakaswa wote wanatoka kwa mmoja. Huyo mmoja ni yupi?
  6. Kristo alimharibuje Ibilisi aliyekuwa na nguvu za mauti kwa njia ya mauti? Je, Ibilisi alikuwa na nguvu za mauti kwa njia gani? Wameachwaje huru wale ambao maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa? Kwa nini ilikuwa lazima Yesu asitwae asili ya malaika, ila atwae asili ya mzao wa Ibrahimu?

MASWALI YA KUJADILI: WAEBRANIA 3:1-19

  1. Kwa nini wote wenye kushiriki wito wa mbinguni wanaitwa watakatifu? Wito huo mkuu na mtakatifu ni upi? (2 Timotheo 1:9;1 Wakorintho 1:26; Waefeso 1:18; Waefeso 4:1, 4; Wafilipi 3:14). Nini kinathibitisha kuwa Yesu alikuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka?kwa ni ni Yesu anaitwa Mtume na Kuhani Mkuu? Je kuna wakati kama wanadamu tunatoa heshima kubwa kwa nyumba kuliko kwa yule aliyeifanya?
  2. Kushikamana na ujasiri na Fahari hadi mwisho limekuwa changamoto katika safari yetu ya kiroho. Unadhani nini kinahitajika ili kufaulu katika jambo hilo? (Waebrania 12:1-3). Kwa nini maisha ya kusafiri kwa Waisraeli jangwani yanaitwa “Siku ya kujaribiwa katika jangwa”? (Kumbukumbu 8:3, 16). Kuna faida gani ya kiroho mtu anapojaribiwa? Kwa nini Mungu anakataa kuwa huwa hamjaribu mtu? (Yakobo 1:13-15).
  3. Kutomjua Mungu na Kutozijua njia za Mungu kwaweza kuwa sababu ya watu kushindwa katika majaribu? (Ayubu 22:21; Ayubu 1:22). Je kutokuamini kunafanya moyo kuwa mgumu? Je kutokuamini kile Mungu alichosema kwaweza kufananishwa na dhambi ya kuasi?

MASWALI YA KUJADILI: WAEBRANIA 4:1-16

  1. Ahadi ya kuingia kwenye raha imetolewa kwa nani na kwa makusudi gani? Je, kujipatia wokovu kwa njia ya matendo mema yatokanayo na juhudi za binadamu kunashabihiana na utaratibu huu unaopendekezwa na Mungu wa kuwapa watu raha? (Mathayo 11: 28-29). Utunzaji wa Sabato ulioagizwa kwenye Amri ya nne ya Mungu ulilenga kumpatia mwanadamu rah ana starehe aipatayo mtu anapojisalimisha kwa Yesu? (Isaya 58:13; Waebrania 4:9).
  2. Kwa nini imesalia raha ya Sabato kwa watu wa Mungu? Sabato inahusianaje na watu wa Mungu? Kwa nini kuingia kwenye raha hiyo kunahitaji bidii? Je, Waisraeli waliikosaje kuingia kwenye raha hiyo? Neno la Mungu linatajwa kuwa ni hai kwa sababu gani? Mungu alistarehe kwa kupumzika siku ya saba. Mtu aweza kujipatia raha ile ile kwa kupumzika siku nyingine atakayojichagulia mwenyewe?
  3. Neno la Mungu lawezaje kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo? Kwa nini kunahitajika tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri? Ujasiri unaoshauriwa hapa ni wa namna gani? Kama Yesu alijaribiwa kama sisi tunavyojaribiwa kwa nini Yeye hakutenda dhambi? Je kujaribiwa ni dhambi?

MASWALI YA KUJADILI: WAEBRANIA 5:1-14

 


MASWALI YA KUJADILI: WAEBRANIA 6:1-20

  1. Kwa nini tunapoweka mipango yetu muhimu kusema "na hayo tutayafanya Mungu akitujalia"? Je Mungu asipotujalia mipango yetu inaweza isifanikiwe? Watu gani ambao wakianguka huwa vigumu kuwafanya upya hata wakatubu? Wafuasi wazirithio ahadi kwa imani utawatambuaje? Je, wokovu hupatikana kama ujira au kama zawadi? Je Mungu aliwachagua Waisraeli wawe warithi wake au urithi huu ulikuwa wa wanadamu wote? Mungu anakusudia kuturithisha nini na kwa nini
  2. Kwa nini Mungu ilimpasa kutoa kiapo kuhusiana na ahadi ya kutupa urithi? Je kiapo kilisemaje? Kwa kawaida kiapo hutolewa mbele ya mwenye mamlaka zaidi yako. Je, kama Mungu aliapa kwa nafsi yake nani alikuwa shahidi? Je kuna uwezekano kwa kiapo cha Mungu kubatilika? Hii inatupa uhakika gani juu ya wokovu wetu? Kama Mungu alimwahidi Ibrahimu kumpa urithi kupitia ahadi kwa nini torati iliingizwa baadaye? Je Mungu alibadilisha kile alichoahidi kwa kiapo? (Wagalatia 3:15-19)

MASWALI YA KUJADILI: WAEBRANIA 7:1-28

  1. Ni nani aliye mkuu kati ya Ibrahimu na kuhani wa kabila la Yuda aliyetoka viunoni mwake. Ni nani aliye mkuu kati ya Ibrahimu na Yesu aliye kuhani mkuu kutoka kabila la Yuda? Iliwezekanaje Yesu wa kabila la Yuda awe kuhani wakati makuhani walikuwa wanatoka kabila la Walawi? Kwa nini ukuhani ulienda kwa ukoo wa Yuda na si kwa ukoo wa Reuben aliyekuwa mzaliwa wa kwanza?
  2. Ukuhani wa Agano la Kale unatofautianaje na ukuhani wa Agano Jipya? Je kuhani katika Agano Jipya anaweza kuwa mwanamke? (1 Petro 2:9). Waliokombolewa watakuwa wanafanyaje kazi ya ukuhani mbinguni? (Ufunuo 20:6). Amri iliyotangulia na iliyobatilishwa ni ipi? Kwa nini Mungu huweka sheria ambazo baadaye analazimima kuzibatilisha? Kati ya Agano la Kale na Agano Jipya ni lipi lililo bora zaidi kuliko lingine na kwa nini?
  3. Kwa nini Yesu amefanywa mdhamini wa Agano Jipya? Alikuwa anamdhamini nani na kwa nini? Kwa nini torati iliwaweka wanadamu walio na unyonge wawe makuhani wakuu? Tofauti ya kuhani mkuu na kuhani wa kawaida ni ipi? Je waliokombolewa watakuwa wakifanya kazi ya kuhani wa kawaida au kuhani mkuu wakiwa mbinguni? Kulikuwa na ofisi kuu tatu za utawala wakati wa Agano la Kale; 1. ofisi ya Kuhani, 2. ofisi ya Nabii, 3. ofisi ya mfalme au Mwamuzi. Ni ipi ilikuwa ofisi kuu kati ya hizo? Je wachungaji wanawakilisha ofisi gani kati ya hizo?

MASWALI YA KUJADILI: WAEBRANIA 8:1-13

  1. Moja ya majukumu ya Kuhani Mkuu ni kuwachukulia kwa upole wale wasiojua na wenye kupotea. Je unajihisi kuwa na karama hiyo? Kwa nini wasiojua na wenye kupotea wanahitaji kuchukuliwa kwa upole?Licha ya kutoa dhabihu kwa ajili ya watu makuhani walitakiw a kutoa dhabihu kwa ajili yao wao wenyewe pia. Je viongozi wa kiroho wanaojitambua kuwa ni wenye dhambi wanaohitaji neema ya Mungu wana uwezekano wa kuwa na ufanisi katika kazi zao?
  2. Je kujitambua kuwa una mapungufu kwaweza kuwa muarobaini wa kutojitukuza? Mungu Baba alimwambia Kristo kuwa "Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa." Je hiyo ni kumaanisha maisha ya Kristo yalianzia siku ile. Katika hali ya kawaida siku ya kuzaliwa Baba aweza kuongea na mwanaye? Je, mateso yanamsaidia mtu kuwa mtii? Je ilikuwa ni lazima Yesu ateswe? Yesu anakuwaje sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii?
  3. Unadhani muda unaotumika kuelezea ukuhani wa kifalme wa Yesu unatosha? Kuna siri gani katika Yesu kuwa Kuhani Mkuu kwa mfano wa Melkizedeki? Je ni kweli kuwa watu wamekuwa wavivu wa kusikia Neno la Mungu hasa mambo yahusuyo wokovu wao?
  4. Kwa nini watu wa Mungu hupenda maziwa (mafundisho laini yasiyo na tija kwa wokovu) badala ya kupenda chakula kigumu kinachohusu unabii na namna tunavyohesabiwa haki? Je utajitambuaje kuwa ni mtoto mchanga unayehitaji maziwa na wala si vyakula vigumu vinavyokusaidia kupambanua mema na mabaya.
  5. Kwa nini ile hema ya mbinguni inaitwa hema ya kweli? Kama kila Kuhani Mkuu huwekwa ili atoe vipawa, Yesu alitoa vipawa gani? Kwa nini Yesu asingekuwa Kuhani kwa mujibu wa sheria kama angekuwa juu ya nchi (duniani)? Yesu ni mjumbe wa agano bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora. Hilo linaloitwa agano bora ni lipi? Linakuwa bora likilinganishwa na agano lipi?
  6. Ni ahadi gani bora zilizo kwenye agano bora ambazo hazikuwemo kwenye agano lililotangulia? Mapungufu ya Agano la kwanza yaliyosababisha kuwa naAgano la pili ni nini? Je mapungufu ya Agano la kwanza yanatokana na kuwapo kwa sheria na amri? Je sheria katika agano Jipya zinaondolewa au kurekebishwa? Kwa nini haziondolewi? Kwa nini badala ya kuandikwa kwenye mbao mbili za mawe kwenye Agano Jipya zinaandikwa mioyoni?
  7. Agano la kwanza lililo kuukuu na lililo karibu na kutoweka ni lipi? Hii inamaanisha vitabu vya agano la kale ni vikuukuu? Kama hema ya duniani haikuwa ya kweli (Waebrania 8:2) kwa nini ilianzishwa? Kwa nini Yesu alikuwa hastahili kuwa kuhani mkuu wa duniani? (fng 4). Yesu amepata huduma iliyo bora zaidi. Jadili ukieleza huduma hiyo inaizidi ipi na kwa vipi. Yesu ni mjumbe wa agano lililo bora zaidi. Tetea hoja hiyo ukieleza agano hilo ni bora zaidi katika maeneo gani na limelizi ubora agano lipi?
  8. Upungufu wa agano la kwanza ulitokana na nini? Je Mungu alitambua upungufu huo kabla au baada ya kulisimamisha. Nafasi ya agano Jipya ilitafutwa baada ya kugundua Agano la kwanza lina mapungufu au mapema kabla ya hapo? Je kulikuwa na sababu ya Mungu kuwalaumu waliohujumu agano la kwanza? Mungu anawatimiziaje nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda Agano Jipya?
  9. Kwa nini Agano Jipya litakuwa tofauti na Agano la Kwanza? Je, kama kwenye Agano la Kwanza walishindwa kushika sheria kwenye agano jipya sheria zitakuwepo au zitaondolewa? Kwa nini Waisraeli hawakudumu katika agano lao na Mungu? Agano linalotajwa hapa kama ni kuukuu ni vile vitabu vya agano la kale au ni makubaliano ambayo Mungu aliingia pale Sinai na Waisraeli?
  10. Kama hema ya duniani haikuwa ya kweli (Waebrania 8:2) kwa nini ilianzishwa? Kwa nini Yesu alikuwa hastahili kuwa kuhani mkuu wa duniani? (fng 4). Yesu amepata huduma iliyo bora zaidi. Jadili ukieleza huduma hiyo inaizidi ipi na kwa vipi. Yesu ni mjumbe wa agano lililo bora zaidi. Tetea hoja hiyo ukieleza agano hilo ni bora zaidi katika maeneo gani na limelizi ubora agano lipi?
  11. Upungufu wa agano la kwanza ulitokana na nini? Je Mungu alitambua upungufu huo kabla au baada ya kulisimamisha. Nafasi ya agano Jipya ilitafutwa baada ya kugundua Agano la kwanza lina mapungufu au mapema kabla ya hapo? Je kulikuwa na sababu ya Mungu kuwalaumu waliohujumu agano la kwanza? Mungu anawatimiziaje nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda Agano Jipya?
  12. Kwa nini Agano Jipya litakuwa tofauti na Agano la Kwanza? Je, kama kwenye Agano la Kwanza walishindwa kushika sheria kwenye agano jipya sheria zitakuwepo au zitaondolewa? Kwa nini Waisraeli hawakudumu katika agano lao na Mungu? Agano linalotajwa hapa kama ni kuukuu ni vile vitabu vya agano la kale au ni makubaliano ambayo Mungu aliingia pale Sinai na Waisraeli?

MASWALI YA KUJADILI: WAEBRANIA 9:1-28

  1. Kawaida za ibada za Agano la Kale zilikuwaje? Hema ya kwanza iliitwaje na hema ya pili iliitwaje? Samani gani zilikuwa zinapatikana kwenye hema ya kwanza na ya pili? Huduma ya kila siku ilikuwa inafanyika kwenye hema ipi na huduma ya mara moja kwa mwaka ilikuwa inafanyika kwenye hema ipi? Ni makuhani gani walikuwa wanahusika kutoa huduma katika hema hizo mbili? Je, kuna haja ya kuendelea kutumia vifaa vilivyotumika wakati huo (kama chetezo) katika ibada zetu za leo?
  2. Je vibao vya agano vinavyotajwa hapa ni Amri 10 za Mungu? Kwa nini ziliwekwa ndani ya sanduku la Agano kwenye chumba cha pili? Kwa nini kwenye utaratibu wa ibada ya Agano la Kale dhabihu zilizotolewa hazikuweza kumkamilisha aabuduye? Je, kama mtu angeacha kutoa dhabihu hizo angekuwa na hatia? Je, kama Yesu alipata ukombozi wa milele hiyo humaaisha kuwa wanadamu wana sababu ya kushangilia au ni mapema sana kuweza kushangilia? Je damu ya Yesu inatakasaje dhamiri zetu? Je, hiyo ni kusema kuwa hatutajisikia hatia mioyoni mwetu?
  3. Je agano la urithi lilihitaji mwenye kulitoa apatikane na mauti? Aliyekufa na kutufanya kuwa na uhalali wa kupokea urithi wa milele ni nani? Je, inawezekana kurithi mwenye kutoa urithi akiwa hai? Je, leo kuna haja ya kuwanyunyizia waabuduo chochote kama ishara ya kuwatakasa? Kwa nini pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo la dhambi? Chumba alichoingia Yesu mara baada ya kupaa mbinguni ili aonekane usoni pa Mungu ni kile cha kwanza au kile cha Mungu?

MASWALI YA KUJADILI: WAEBRANIA 10:1-39

  1. Torati ilikuwa inatengeneza kivuli cha mema yatakayokuja. Hayo mema yanayowakilishwa na Torati ni yapi? Ni katika maeneo gani torati haikuwa sura yenyewe ya mambo? Kwa nini Mungu hakupndezwa na sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi? Kwa kuwa Mungu hakupendezwa na taratibu nyingi za makafara zilizoelekezwa kwenye torati wapo wanaodhani haikuletwa na Mungu ila na Musa kinyume cha Mungu. Una maoni gani juu ya madai hayo?
  2. Je kwa toleo moja Yesu amewakamilisha hata milele wanaotakaswa? Je hao aliowakamilisha hata milele hawana uwezekano wa kupotea? Kuwakamilisha kunakosemwa hapa ni nini hasa? Mungu anaahidi kuwa dhambi zao na uasi wao hataukumbuka. Kutokumbuka dhambi na uasi kunamaanisha nini kuhusu uhakika wa wokovu? Kama bado unakumbuka dhambi ulizosamehe je ni kweli kuwa dhambi hiyo ulisamehe?
  3. Je, patakatifu tunapokuwa na ujasiri napo kupaingia ni pale pa duniani au pale pa mbinguni? Ujasiri huo unatokana na nini hasa? Je, pazia linalotenganisha chumba cha kwanza na cha pili kwenye hema ya duniani ulikuwa mwili wa Kristo? Je, unaiona sura ya msalaba kwenye huduma iliyokuwa inafanyika kwenye hema ya duniani? Mwenye haki ataishi kwa imani. Je kuishi kwa imani maana yake ni kutoshika Amri za Mungu? Kwa nini saburi inahitajika kwa wale wanaomngoja Yesu?

MASWALI YA KUJADILI: WAEBRANIA 11:1-40

  1. Unapokuwa na hakika na mambo unayotarajia hiyo ndiyo imani. Je ni lazima uhakika huo uwe umetokana na Neno la Kristo? (Warumi 10:17). Vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri. Jambo hilo lina ukweli wa kiasi gani? Je vilifanywa kwa kutumia nini? Je imani ilihusika katika kuumba dunia yetu?
  2. Kama huna imani kuwa Mungu huwapa thawabu wale wamtafutao, je kuna upungufu wowote katika imani yako hiyo? Kung'ang'ania kuwa Mungu aweza kufanya kile ulichomwomba kwa muda mrefu bila kuona matokeo uliyotarajia ni kulazimisha mambo au ndiyo imani yenyewe? Je kule kusema mapenzi yake yatimizwe kunatoa nafasi ya kuendelea kuliombea lile ambalo halijatimizwa kama ulivyotarajia?
  3. Je kupokea uwezo wa kuwa na mimba kunahitaji imani? Inakuwaje wengine wana imani na wengine hawana? Je imani ni karama au ni kitu ambacho kila mmoja anapaswa kuwa nacho? Je kizazi cha mwisho kitakuwa na tatizo la kupungukiwa imani? (Luka 18:8)

MASWALI YA KUJADILI: WAEBRANIA 12:1-29

  1. Mashahidi wanaotuzunguka wanaotajwa hapa ni wale waliotajwa kwenye Waebrania sura iliyopita au ni pamoja na wale tunaoishi nao? Unadhani mashujaa wa imani wa Waebrania sura ya 11 walishinda kwa sababu ya kumtegemea Yesu au kutokana na juhudi zao wenyewe? Yesu anaamzishaje na kutimiza imani yetu?
  2. Ikiwa wokovu wetu unategemea tunavyoamini kilichoamuliwa na kutimizwa na Mungu kwa ajili yetu na hata imani tunayotumia kuamini mambo hayo inatoka kwa huyo huyo Mungu, mchango wetu ni nini katika wokovu? Kumtafakari sana Yesu ni kutumia muda wa kutosha kumjadili na kumsema vizuri? Unadani ni kipi rahisi kati ya kutumia muda mwingi kumjadili Yesu au kutumia muda mwingi kumjadili Shetani?
  3. Kipi kinalipa zaidi? Tusipomjadili vya kutosha Shetani na mbinu anazotumia tunaweza kushinda dhambi? Kwa kusema hatujafanya vita hata kumwagika damu anamaanisha tufanye hivyo au tumtegemee Yesu aliyefanya hivyo kwa ajili yetu? Kwa nini kuadhibiwa ni kwa muhimu? Je mtoto unayempenda unaweza kumsababishia maumivu kwa kumwadhibu? Je adhabu ina uwezo wa kumfanya anayeadhibiwa kuwa sugu au kupoteza uwezo wa kujiamini?
  4. Nini kifanyike ili adhabu isilete matokeo hayo? Natafutaje amani kwa bidii na mtu ambaye hata nikimkwepa ananizulia mambo ya uwongo na kunichafua? Je, inawezekana kuwa na amani na watu wote hata walio adui zako? Kwa nini mtu asipokuwa na utakatifu hawezi kumuona Mungu? Je, kipimo cha kujua kama wewe ni mtakatifu ni kushika Amri 10 za Mungu? (Ufunuo 22:14; Mhubiri 12:13; Ufunuo 14:12).
  5. Kwa nini kupungukiwa neema ya Mungu kunazaa shina la uchungu linalosumbua na kuwatia watu unajisi? Kama Esau je, sisi ni warithi wa mzaliwa wa kwanza? (Warumi 8:17 Wagalatia 3;29; Warumi 8:29; Waebrania 12:22-23). Mungu ameahidi kuitetemesha siyo mbingu tu bali hata mbingu yenyewe. Unadhani mbingu anayozubgumzia ni ipi na ataitetemeshaje? Kwa nini Mungu anaitwa moto ulao?
  6. Kwa nini Yesu anatambulika kama mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu? Je hiyo ina maana pasipo Yesu sisi hatuwezi kuamini? Nini kilimwezesha Yesu kustahimili msalaba na kuidharau aibu? Ili tusichoke na kuzimia mioyoni mwetu tunashauriwa kufanya nini? Kwa nini kutafuta amani na watu wote kunapaswa kuwa kipaumbele chetu?
  7. Kwa nini kupungukiwa na neema ya Mungu huchipua shina la uchungu lenye kuwasumbua na kuwatia watu unajisi? Kwa nini mkutano mkuu wa kanisa litakalokusanyika mbinguni litakuwa la wazaliwa wa kwanza? Sifa ya uzaliwa wa kwanza inapatikanaje? Kazi ya wazaliwa wa kwanza itakuwa nini? (Zab 89:27; Danieli 7:27).

MASWALI YA KUJADILI: WAEBRANIA 13:1-25

  1. Ni nini hufanya upendano wa ndugu usidumu? Je upendano unaohimizwa hapa ni upendano wa ndugu wa damu au upendano wa ndugu wa imani? Upi ni mwepesi kufa kuliko mwingine na kwa nini? Unawezaje kumkaribisha malaika pasipo kujua kama ni malaika? Je Ibrahimu na Lutu waliwakaribisha malaika kwa sababu walijua ni malaika? (Mwanzo 18:1-22; Mwanzo 19:1-23).
  2. Je tunatenda wema kwa kusudi la kurudishiwa wema? Kama hiyo ndiyo nia ya kutenda wema kuna uwezekano wa kumtendea wema usiyemjua? Kwa nini kuwapambania wanaodhulumiwa leo hakuonekani kama mojawapo ya wajibu wa mcha Mungu wa kweli na hasa kama anayedhulumu ana madaraka au ana uwezo wa kipesa?
  3. Kwa nini Yesu anataka tuwaonee huruma waliofungwa huku akijua wapo pale kwa sababu ya maovu waliyotenda uraiani? Je walio kifungoni wakipewa huduma wanazozihitaji na walio nje haiwezi kuwafanya wapendelee kukaa gerezani na kufanya uhali watakapowekwa huru? Kwa nini ndoa inatakiwa iheshimiwe na watu wote?
  4. Wenye mazoea ya kutoheshimu ndoa ni watu gani? Kwa nini malazi yanatajwa katika kuiheshimu ndoa? Je waasherati na wazinzi wanachangia katika kutoiheshimu ndoa? Tabia ya kupenda fedha huzalisha waasherati na wazinzi? Kuwa radhi na vitu ulivyo navyo ni kuridhika. Je, kuridhika ni sawa na kubweteka? Je, mtu aliyeridhika anaweza kuwa na maendeleo?
  5. Je tungeamini ya kwamba Mungu hatarupungukia wala kutuacha tabia za kujipendeeza kwa kuwasifia hata wasiostahili (uchawa) zingekuwepo? Je tunashindwa kusimamia ukweli kwa kuhofu kile wanadamu watakachotutenda? Kwa nini viongozi wa zamani wanaonekana kuwa na tabia zinazofaa kuigwa kuliko wa sasa? (Waebrania 13:7). Ni kwa namna gani moyo hufanywa imara kwa neema?
  6. Kuna uhakika gani kama Yesu wa zamani ni sawa na Yesu wa sasa? Je wanaosema Yesu alibadilisha sabato wanamzungumzia Yesu yule yule au mwingine? (Marko 2:28; Zaburi 89:34; Malaki 3:6). Kama Yesu aliteswa hapa duniani na sasa anahudumu katika hekalu la mbinguni nje ya lango la kuingilia hekalu la mbinguni ni wapi? Je kutenda mema na kushirikiana ni sadaka? Mungu anachukuliaje tunapoacha kuwatii na kuwanyenyekea wanaotuongoza?
  7. Namna bora ya kuwahurumia walio kwenye dhiki ni kuhisi dhiki wanazopitia. Unadhani hili ni jukumu la kila mtu au la viongozi na watu wenye karama hiyo. Je huduma ya kuwaona wafungwa inafanyika kama inavyohimizwa na Maandiko? Je heshima ya ndoa inapatikana kwa wanandoa kuwa waaminifu kwa ndoa yao? Tofauti ya wazinzi na waasherati ni nini? Hukumu ya wasioheshimu ndoa hutolewa lini?
  8. Kwa nini mzinzi anachukuliwa kuwa ni mtu asiye na akili kabisa? (Mithali 6:32-33). Je kupenda fedha ni kosa sawa na kutafuta fedha? Je, hofu kwamba siku moja Mungu ataniacha yaweza kuwa chachu ya kufanya waitafute sana fedha leo? Mhubiri alimaanisha nini aliposema "fedha huleta jawabu la mambo yote"? (Mhubiri 10:19)
  9. Kuwatii na kuwanyenyekea wanaotuongoza hata makanisani imekuwa changamoto kubwa katika kizazi hiki. Unadhani nini kinachangia hali hii? Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu hutufanya wakamilifu katika kila tendo jema akitufanya tuyatende mapenzi yake. Je ukweli huo unakusaidiaje kuwa na uhakika na wokovu wako?