MASWALI YA KUJADILI: JOSHUA 11:1-23
- Vipi kama unagundua kuna njama za kukufanya vibaya zinazotekelezwa na kundi kubwa la watu utaendelea kuamini kuwa Mungu bado atakupigania na utashinda? Nini kinakupa uhakika kuwa Mungu yupo upande wako? (Warumi 8:32). Je, uwingi una msaada wowote katika kuleta ushindi? Kwa nini njama zinazoandaliwa juu ya wale wanaoshika amri za Mungu na imani ya Yesu hazitafanikiwa? (Ufunuo 13:13-16).
- Mungu akikuahidi kukutetea kuna haja ya kutafuta na kujipanga namna atakavyokutetea au unatakiwa ujiachilie mikononi mwake kwa imani? Je, katika mazingira ya kuzingirwa na adui maombi ni ya muhimu? (2 Nyakati 20:1-12). Ahadi ya kuwapa Israeli nchi yao ilitimia baada ya miaka 40 ya kungoja. Je, ipo haja ya kuvuta subira ili Mungu akutimizie ahadi yake kwa wakati?
- Njia ya kuifanya nchi itulie isiwe na vita tena ni ipi? Urithi wa Israeli unaopatikana kwa kumwaga damu unakufundisha nini? Je umwagikaji wa damu ungeweza kuepukwa kama wafalme wa nchi za Kanani wangekuwa wasikivu kama wenzao wa Gibeoni? Je kiburi cha wafalme wale kinafanana na kiburi cha Farao aliyekataa kusikiliza kilio wa Waisraeli na ombi la Mungu wao?
- Je ni jeshi gani kubwa unalolikabili – jambo linaloonekana kubwa zaidi ya uwezo wako? Unawezaje kumtumaini Mungu katika vita hiyo? Kwa nini Yoshua alivunja magari na kupiga farasi miguu? Ni vidokezo gani kuhusu kutokutegemea vitu vya hapa duniani zaidi ya kumtegemea Mungu?
MASWALI YA KUJADILI: JOSHUA 10:1-43
- Njia mojawapo ya kuwakabili maadui ni kuwatenganisha wasielewane ili kupunguza nguvu zao. Unaiona mbinu hiyo katika uongozi wa Yoshua? Kuna wakati ili kushinda mapambano dhidi ya adui yako unatakiwa kufanya kazi usiku kucha? Je, umewahi kupitia uzoefu wa aina hiyo? Je kufanya kazi usiku kucha hakuwezi kuuchosha mwili? Kama wanafunzi wa Yesu walishindwa kukesha angalao kwa saa moja unadhani Yesu alikesha kwa masaa mangapi? (Mathayo 26:40; Luka 6:12).
- Unayatambua na kuyakumbuka 'mawe ya barafu' yaliyowaangukia adui zako pale Mungu alipoamua kuingilia kati vita yako na kukupatia ushindi? Hao wafalme watano wangeweza kuokoa vifo vyao na vya watu wao kama wangejisalimisha mikononi mwa Mungu wa Israeli kama wenzao Wagibeoni? Kwa nini hawa wafalme hawakufuata njia ya wenzao? Je kujisalimisha kwa Yesu ni jambo rahisi analoweza kufanya kila mtu au linahitaji msaada kutoka kwa Mungu?
- Maji ya Bahari ya Shamu, maji ya Mto Yordani, Jua, na Nyota vyote vilitumika na Mungu kuwezesha watu wake kutimiza kusudi lake. Unadhani Mungu atafanya yote katika uwezo wake kutimiza kusudi lake kwako? Je unajua kusudi la Mungu kwako? Unadhani vitu hivi vya asili vinatambua kusudi la Mungu kwa maisha yako? (Mathayo 27:45-46).
- Unaamini Shetani na mawakala wake waliolisumbua kanisa na watu wa Mungu kwa muda mrefu watakutana na adhabu kali inayowastahili katika siku za usoni? Unadhani katika wakati huo kuna kiumbe atakayehisi kuwa wameonewa? (Ufunuo 16:4-7; Danieli 7:25-26). Je, kuwekewa nyayo za miguu shingoni ni kitendo kinachowakilisha dharau kubwa kwa anayetendewa? Je kutawadha miguu ni kitendo kinachowakilisha unyenyekevu?
- Ushindi wa Yoshua dhidi ya mataifa aliyokutana nayo baada ya aibu ya kushindwa na taifa dogo la Ai inakufundisha nini juu ya kusudi la Mungu la kutaka ushinde katika mambo yale yote yanayokupa changamoto kwa sasa? Unadhani ushindi wetu dhidi ya dhambi ungekuwa endelevu kama ule wa Yoshua, Yesu asingekuwa amekuja kutuchukua?
- Je, kuna namna ungependa Mungu asimamishe jua kwa ajili yako ili kukamilisha jambo ulilokuwa unafanya? Unaonaje ushirikiano kati ya maombi ya imani na hatua za haraka za Yoshua (kusafiri usiku kucha)?
MASWALI YA KUJADILI: JOSHUA 12:1-33
- Kama ushindi unatokana na Mungu kuna ugumu wowote ikiwa kiongozi ataishiwa nguvu kutokana na uzee? Uzee huja na majuto mengi hasa juu ya ulivyoutumia ujana wako? Unadhani uzee wako utakuwa na majuto ya namna hiyo? Unafanya nini sasa kuepuka hali hiyo? Je ipo haja ya kuangalia lini ukome kuzaa watoto usije ukakutwa na majukumu ya kuwatunza umri ukiwa umeenda?
- Je kushindwa kukamilisha mipango uliyojiwekea kwa kiwango ulichohitaji ni kushindwa kunakokuzuia kufurahia ushindi ulionao mkononi? Unadhani kuna mapungufu uliyonayo ambayo umeshindwa kuyaondoa maishani mwako? Je kuna wakati katika maisha unapaswa kujifunza kuishi na mapungufu yaliyoshindikana uliyonayo? Je mtu aweza kuyaondoa maumbile yake asiyoyapenda? Kuyakubali maumbile yetu tusiyoyapenda ni ushindi?
- Je, kuna ahadi ambazo bado hujazifanyia kazi? Je unachukua hatua gani ili kuzimiliki? Je Walawi wa Leo ni waaminifu katika kutoa huduma katika nyumba ya Bwana? Je makabila kumi na moja ya Israeli ya leo yana uaminifu katika kumtolea Mungu Ili kiwemo chakula katika maskani ya Bwana kwa ajili ya watumishi wake?
- Je kuacha kiporo ambacho hujakifanyia kazi baada ya kukamilisha sehemu kwaweza kuleta madhara kwa ushindi ulioupata? Kwa nini mwanadamu ana kawaida ya kuridhika na mafanikio madogo? Je hofu inachangia katika kuacha viporo vilivyoshindikana?
MASWALI YA KUJADILI: JOSHUA 12:1-33
- Kama ushindi unatokana na Mungu kuna ugumu wowote ikiwa kiongozi ataishiwa nguvu kutokana na uzee? Uzee huja na majuto mengi hasa juu ya ulivyoutumia ujana wako. Je unadhani uzee wako utakuwa na majuto ya namna hiyo? Unafanya nini sasa kuepuka hali hiyo? Je ipo haja ya kuangalia lini ukome kuzaa watoto usije ukakutwa na majukumu ya kuwatunza umri ukiwa umeenda?
- Je kushindwa kukamilisha mipango uliyojiwekea kwa kiwango ulichohitaji ni kushindwa kunakokuzuia kufurahia ushindi ulionao mkononi? Unadhani kuna mapungufu uliyonayo ambayo umeshindwa kuyaondoa maishani mwako? Je kuna wakati katika maisha unapaswa kujifunza kuishi na mapungufu yaliyoshindikana uliyonayo? Je mtu aweza kuyaondoa maumbile yake asiyoyapenda? Je kuyakubali maumbile yetu tusiyoyapenda ni ushindi?
- Je, kuna ahadi ambazo bado hujazifanyia kazi? Je unachukua hatua gani ili kuzimiliki? Je Walawi wa Leo ni waaminifu katika kutoa huduma katika nyumba ya Bwana? Je makabila kumi na moja ya Israeli ya leo yana uaminifu katika kumtolea Mungu ili kiwemo chakula katika maskani ya Bwana kwa ajili ya watumishi wake?
- Je kuacha kiporo ambacho hujakifanyia kazi baada ya kukamilisha sehemu kwaweza kuleta madhara kwa ushindi ulioupata? Kwa nini baadhi ya watu wana kawaida ya kuridhika na mafanikio madogo? Je hofu inachangia katika kuacha viporo vilivyoshindikana?
MASWALI YA KUJADILI: JOSHUA 14:1-15
- Wana wa Israeli walirithishwa nchi kadhaa kila kabila likitwaa nchi mojawapo. Unadhani urithi walioahidiwa watakaokombolewa utahusu kurithi mataifa yaliyopo leo ulimwenguni au sayari zilizotapakaa huko angani? Je unapomfuata Mungu kwa ukamilifu huwezi kutoa habari inayotia watu hofu? Kwa nini Joshua aliendelea kuwa mwenye nguvu hata baada ya kupigana vita ngumu na baada ya kufikisha miaka 85? Je ni kweli kuwa umri unaotumika kikamilifu katika kazi ya Mungu hauchoki wala kuzeeka?
- (Kalebu na Joshua) kati ya wapelelezi 12 walikuwa waaminifu na kufanikiwa kuimaliza safari yao kwa ushindi. Nini siri ya mafanikio yao? Je unafanya nini kujihakikishia unakuwa kwenye kundi la washindi? Kuwapa watu hofu kuwa Mungu ameliacha kanisa lake na kuwashawishi waliache au wasisikilize viongozi wao kunaashiria upo kwenye kundi la washindi watakaoimaliza safari yao kwa ushindi?
- Je kipi bora kujitwalia urithi mapema hata kwa njia ya hila na uchawa au kusubiri hata mwisho wakati wa uzee au wakati wa kustaafu Mungu awatumie watu kukupatia urithi na mali za kukusaidia maisha ya uzeeni? Je umehusika katika kufanya maisha yawaliomtumikia Mungu kwa uaminifu kuwa yenye baraka wakati wa uzee wao?
- Nini faida ya nchi kutulia na vita kukoma? Nini kinachopelekea nchi kutulia na vita kukoma? Ni jitihada gani zinapaswa kuchukuliwa kwa nchi zilizokuwa vitani ili kukomesha vita na kurejesha utulivu katika nchi? Je, una watu ulioshiriki nao kuanzisha safari ya kundi la kiroho ambao unafarijiana nao sasa mnapoangalia mlikotoka na pale Mungu amewafikisha kama kundi la kiroho lenye mafanikio?
- Je, kuna ahadi za Mungu ulizosahau kwa sababu zimechukua muda mrefu? Je, Kalebu anakutia moyo vipi? Ni maeneo gani ya maisha yako yanayoonekana kama “milima” yenye majitu yanayokusubiri, na unapokeaje changamoto hizo?
MASWALI YA KUJADILI: JOSHUA 15:1-63
- Aksa binti wa Kalebu alikuwa msaada kwa baba yake alipokuwa hana tena nguvu za ujanani za kupigana. Unadhani mabinti waweza kuwa msaada kwa wazazi wanapokuwa hawana nguvu kama ilivyo kwa watoto wa kiume? Je kigezo kimojawapo cha kuamua mvulana afaaye kumuoa binti yako ni yule atakayekusaidia uzeeni? Je kijana aliyeoa binti yako aweza kuwa msaada wako kuliko kijana wako uliyemzaa?
- Je binti ana haki ya kudai urithi kwa babaye kama ilivyo kawaida kwa watoto wa kiume? Kuna kitu gani unajifunza kwa mvulana huyu aliyeoa kwa Kalebu juu ya ujasiri na uhodari wake na hekima katika kufanya maamuzi? Je unaiona hali hiyo kwa vijana wetu wa sasa? Je uhuru wa kuchagua juu ya mchumba amtakaye unauona kwa Aksa? Wazazi bado wanayo nafasi ya kuwachagulia mabinti zao wachumba?
- Katika kugawiwa urithi unaona umuhimu wa kuainisha mipaka? Je ikitokea muumini amewapa uwanja bure ili mjenge kanisa kuna haja ya kuandikishiana na kuweka alama za mipaka?Je mtafanyaje akikataa kuandikishana na kuweka mipaka kwa madai kuwa hali hiyo inaashiria kuwa hamumuamini? Mali za urithi zisipowekwa bayana kwamba zinamhusu nani yaweza kuwa chanzo cha migogoro isiyoisha?
- Katika Yoshua 15:18-19 Kalebu anamuuliza binti yake, "Unataka nikupe nini?" Ni urithi gani wa kiroho na kimwili unatamani kuuacha kwa watoto au wale wanaokufuata? Yoshua 15:18-19 inaeleza mambo yaliyotendeka katika siku ya harusi ya Othinieli na Aksa. Je unafikiria mambo gani yatafanyika katika harusi yako (ikiwa bado hujaoa au kuolewa)? Je, unaona umuhimu wa kudai baraka zaidi (kama Aksa alivyofanya) bila kuonekana na tamaa? (Yoshua 15:18-19).
- Othinieli aliyemuoa Aksa binti wa Kalebu alibarikiwa kuridhi eneo lenye chemichem ifaayo kwa mifugo na kilimo na baadaye akawa mmojawapo wa Waamuzi wa Israeli. Je, kuoa binti wa mtu aliyemtumikia Mungu kwa uaminifu mfano Mchungaji kunalipa? Kwa nini kumiliki eneo lenye maji ni urithi ufaao? Je unafanya jitihada gani kumilikisha wanao urithi ufaao?
MASWALI YA KUJADILI: JOSHUA 24:1-33
- Joshua alifariki akiwa na umri wa miaka 110 baada ya kuwaongoza na kuwaingiza kwa mafanikio wana wa Israeli lakini wakaja kukengeuka baada ya kutokea kizazi kingine kisichofahamu wala kuthamini kazi yake. Hii ina ukweli gani leo ambapo viongozi wapya hupuuza mipango na njozi za waliowatangulia na kuanza njozi mpya ambazo huishia njiani bila kuwa na mafanikio?
- Unajifunza nini katika uongozi wa Joshua?
- Unadhani nini kilisababisha kizazi kipya kisithamini kazi za waliowatangulia?
- Ni kwa namna gani kuwa na mahusiano ya karibu na watu wasiomjua Mungu huwa miiba na tanzi maishani? Je, maisha ya utawa ndilo suluhisho la changamoto hii?
- Kwa nini Waisraeli walitumikia miungu ya Baali ambayo haikuwaokoa na kumsahau Mungu aliyewatendea mambo makuu maishani? Kwa nini mwanadamu anaweza kutendewa mema na mwenzi wake wa maisha na bado amsaliti na kuandamana na mwingine asiye na uzuri wala uwezo wa kumhudumia kama yule aliyemsaliti?
- Unadhani Mungu alitakiwa afanye nini cha ziada ili Waisraeli wasimuasi na kugeukia miungu mingine?
- Mungu anaposema, “Mimi milele sitalivunja hilo agano langu nililoagana nanyi,” anamaanisha nini? Ni kweli kuwa Mungu hawezi kuwaacha wanadamu bila kuwasaidia hata kama watamwasi?