NILICHOGUNDUA NA KUJIFUNZA: ESTA 1:1-22
- Hapo zamani kulikuwa na mtawala wa Umedi na Uajemi mwenye dola inayomiliki kuanzia Bara Hindi hadi Kushi (Ethiopia) iliyo barani Afrika. Ikiwa majimbo yote aliyotawala yapatayo 137 yalilipa kodi ni dhahiri alikuwa na utajiri wa kufuru. Utajiri huleta majivuno. Na waswahili wamesema pata fedha tujue tabia yako. Ahasuero alifanya karamu ya kufuru akiwaalika wasaidizi wake wote. Karamu iliyodumu kwa siku 180 yaani miezi 6. Haya ni matumizi mabaya ya kodi na michango ya watu. Tulio kwenye dhamana ya uongozi tujifunze jambo hapa.
- Ni jambo linalostahili kuigwa kuwafanyia karamu au kuwatuza wasaidizi wako au ndugu zako. Hata hivyo kitendo hicho kinapaswa kifanyike kwa namna ya kumpa Mungu utukufu na si kujiinua kama Ahasuero alivyofanya. Kitendo hicho cha kuonyesha fahari yake kwa wageni waalikwa hakitofautiani na kile kilichofanywa na mfalme Hezekia (2 Wafalme 20:6-17). Kila aliyefanikiwa anapaswa kukumbuka Mungu anapaswa kupewa sifa na utukufu kwa kuwa ndiye anayestahili.
- Sherehe inayohusisha vileo vya pombe kali ambazo mtu hujinywea bila kipimo ni aghalabu kuisha katika hali ya salama na amani. Aliyesema mvinyo hudhihaki na na kileo huleta ugomvi hakukosea (Mithali 19:28). Sherehe ya Ahasuero iliingia doa. Yeye mwenyewe akilemewa na pombe aliagiza malkia aje aonyeshe uzuri wake kwa wageni waalikwa. Tafsiri ya jambo hili ni kuwa alitaka malkia mkewe aje akiwa na mavazi yanayoonyesha maungo yake ya ndani. Malkia alikataa udhalilishaji huo na kupinga kutii amri ya mfalme. Si kila amri inayotolewa na kiongozi inafaa kutiiwa. Hasa zile amri zinazotolewa mtu akiwa hajielewi.
- Mke si wa kumdhalilisha mbele ya halaiki wala mbele ya watoto wako. Mungu anasisitiza waume wawape wake zao heshima (1 Petro 3:7). Mungu hapendezwi mwanamke anapotumika kama chombo cha kujistarehesha bila kuchunga utu wake.
- Heshima haiji kwa kulazimisha. Mfumo dume unaokandamiza haki za wanawake haukuanza leo. Pamoja na kuwa mume ni kichwa cha nyumba nafasi hiyo isitumike kulinda maslahi ya mume na kupuuza haki za mke. Hakikisha unapoandaa sherehe yako unamualika Mungu ili sherehe yako iishe vizuri. Usiweke kileo.
NILICHOGUNDUA NA KUJIFUNZA: ESTA 1:1-22
- Mara moja moja inapendeza kutoka na mkeo kwenye sherehe na kujumuika na watu. Maisha yanapokuwa na mitoko ya pamoja pale inapowezekana huyafanya maisha kuwa rahisi na huepusha misongo. Kiongozi asiyeandamana na mkewe au mumewe katika safari zake zote huzua maswali juu ya mahusiano yake ya ndoa. Ndege wanaofanana huruka pamoja.
- Wanaopendana huketi pamoja na kuendelea kuzungumza kwa kubadilishana mawazo. Hawakai kama mabubu. Tena inapendeza wakiibua mijadala mizito inayohusu mustakabali wa maisha yao. Na kama Biblia inavyoshauri waume wanapaswa kugundua hisia walizonazo wake zao ili wazirekebishe na kuyafanya maisha yao kujawa na furaha daima. Mke hujisikia vizuri pale anapotambua kuwa mumewe anamjali.
- Mke ana bahati ya kutambua afanye nini kwa mumewe ili atimiziwe haja yake. Anapoitumia vema karama hiyo ana uhakika wa kuwa salama siku zote. Mume anayeheshimiwa na kustahiwa na mkewe huona fahari kumtendea mema mkewe siku zote za maisha yake (Mithali 31:10-11).
- Watu wanafiki hawafai kuwa rafiki. Hujifanya kuwa wema machoni lakini moyoni wana chuki ya kutisha. Wanawake ni wepesi kutambua marafiki wabaya wa waume zao hasa wale ndumila kuwili. Usipuuze mkeo anapokuambia yule rafiki yako si mtu mzuri. Kwa asili wao wana siri nyingi wanazozijua ambazo hubaki nazo mioyoni. Kaa nao vizuri watakusaidia kubaini marafiki wa kweli na wa uongo.
- Wanawake ni majasiri inapokuja swala la kutetea haki na hasa kumtetea Mungu. Hawakuwahi kuwa sehemu ya mitume 12 wa Yesu lakini hiyo haikumaanisha wangekosa uadilifu. Wakiaminiwa na kutiwa nguvu wana uwezo wa kusimamia haki na kupambana na Ibilisi kwa mafanikio makubwa.
NILICHOGUNDUA NA KUJIFUNZA: ESTA 2:1-23
- Kufiwa na wazazi siyo mwisho wa maisha. Kwa kila aliyekuja duniani Mungu kuna jambo amepanga kwa ajili yake. Esta asiye na wazazi na anayeishi kwa huruma za mjomba yake aliyemlea kama binti yake, na aliye katika nchi ya ugeni na ya utumwa anakwaa nafasi ya kuwa malkia wa nchi. Uzuri wake usiotumia mikorogo ya kibinadamu lakini wenye upako wa Mungu ulimpa kibali mbele ya mfalme. Esta akawa kama Yusufu katika nchi ya Misri. Akifanywa waziri mkuu katika nchi yake ya utumwa. Mwamini Mungu usikate tamaa. Aliyemuinua Esta na Yusufu atakuinua na wewe.
- Watoto yatima wana nafasi yao katika maisha. Tuwachukue na kuishi nao kama alivyofanya Mordekai. Watoto hawa wakipewa malezi mema na mwongozo bora wa maisha wana uwezo wa kufanya makubwa. Watoto hawa wanaolelewa na vituo maalumu tuwatembelee na kuwapatia huduma za kiroho na hata kuwaalika kwenye matukio ya kidini. Tutapunguza panya road na kuwaibua kina Esta wa leo.
- Kupendwa au uzuri hautegemei urembo unaonunuliwa madukani au kutembea nusu uchi. Uzuri wa asili ni bora zaidi kuliko ule wa bandia. Mabinti wengi wanaolazimisha uzuri wa dukani huonekana vituko siku za harusi zao. Jipende, jikubali, ishi kulingana na maadili uliyofundwa na utapendeka na kila muoaji.
- Jaribu bahati yako. Wengi hushindwa kufikia makusudi ya Mungu kwa maisha yao sababu ya kushindwa kujaribu. Lazima uwe na focus ya maisha na uyaishi matumaini yako. Esta hakukata tamaa na uwingi wa watu waliokuwa wanawania nafasi ya umalkia. Wala hakuogopa kuwa si mwenyeji wa nchi ile bali ni mtumwa na hivyo kupoteza uwezekano wa kuteuliwa. Alisikiliza ushauri mjomba yake mcha Mungu na alimtumainia Mungu. Pambania chochote kilicho kizuri ukiamini Mungu atakupa ushindi.
MASWALI YA KUJADILI: ESTA 2:1-23
- Je unaafikiana na utaratibu wa kuchagua mke afaaye uliopendekezwa na watumishi wa mfalme? Je kutafuta mchumba mwingine ukiwa na hisia za hasira juu ya mchumba uliyenaye aliyekutenda vibaya ni salama katika kufanya uchaguzi sahihi?
- Mafanikio ya watoto yanachangiwa na malezi yao tangu utotoni. Unadhani mafanikio ya Esta yanaakisi ukweli huo? Je mabinti wanaotafuta kuolewa wana jambo la kujifunza kutoka kwa Esta?
NILICHOGUNDUA NA KUJIFUNZA: ESTA 2:1-23
- Kufiwa na wazazi siyo mwisho wa maisha. Kwa kila aliyekuja duniani Mungu kuna jambo amepanga kwa ajili yake. Esta asiye na wazazi na anayeishi kwa huruma za mjomba yake aliyemlea kama binti yake, na aliye katika nchi ya ugeni na ya utumwa anakwaa nafasi ya kuwa malkia wa nchi. Uzuri wake usiotumia mikorogo ya kibinadamu lakini wenye upako wa Mungu ulimpa kibali mbele ya mfalme. Esta akawa kama Yusufu katika nchi ya Misri. Akifanywa waziri mkuu katika nchi yake ya utumwa. Mwamini Mungu usikate tamaa. Aliyemuinua Esta na Yusufu atakuinua na wewe.
- Watoto yatima wana nafasi yao katika maisha. Tuwachukue na kuishi nao kama alivyofanya Mordekai. Watoto hawa wakipewa malezi mema na mwongozo bora wa maisha wana uwezo wa kufanya makubwa. Watoto hawa wanaolelewa na vituo maalumu tuwatembelee na kuwapatia huduma za kiroho na hata kuwaalika kwenye matukio ya kidini. Tutapunguza panya road na kuwaibua kina Esta wa leo.
- Kupendwa au uzuri hautegemei urembo unaonunuliwa madukani au kutembea nusu uchi. Uzuri wa asili ni bora zaidi kuliko ule wa bandia. Mabinti wengi wanaolazimisha uzuri wa dukani huonekana vituko siku za harusi zao. Jipende, jikubali, ishi kulingana na maadili uliyofundwa na utapendeka na kila muoaji.
- Jaribu bahati yako. Wengi hushindwa kufikia makusudi ya Mungu kwa maisha yao sababu ya kushindwa kujaribu. Lazima uwe na focus ya maisha na uyaishi matumaini yako. Esta hakukata tamaa na uwingi wa watu waliokuwa wanawania nafasi ya umalkia. Wala hakuogopa kuwa si mwenyeji wa nchi ile bali ni mtumwa na hivyo kupoteza uwezekano wa kuteuliwa. Alisikiliza ushauri mjomba yake mcha Mungu na alimtumainia Mungu. Pambania chochote kilicho kizuri ukiamini Mungu atakupa ushindi.
MASWALI YA KUJADILI: ESTA 3:1-15
- Je ni halali kumsujudia mwanadamu kutokana na cheo chake? Je Biblia iliposema "kila mtu aitii mamlaka . . ." (Warumi 13:1) utii huo ni pamoja na kusujudia? Ni amri ipi inayokataza kusujudia watu?
- Kwa nini kosa la Mordekai la kutosujudia wakuu wa wanadamu liliwajumuisha Wayahudi wote? Kwa nini wanaotii Amri za Mungu huchukuliwa kama waasi ambao haipasi kuchukuliana nao? Unadhani siku Shetani atakapopewa mamlaka ya kuwaangamiza wanadamu ataanza na watu gani na kwa nini?
- Je taarifa za kutunga na za kichonganishi zina madhara gani katika jamii? Ikitokea umechukiwa kwa taarifa za uongo zilizosambazwa na maadui zako utachukua hatua gani? Je, unatumia fursa ya kufahamiana na wakubwa kujenga taswira njema ya watu unaoishi nao au unawasilisha tabia zao vibaya (character assasination)?
MASWALI YA KUJADILI: ESTA 4:1-17
- Unapogundua kuna njama za kukuangamiza zinazofanyika kwa hila na wale uliotarajia wakusaidie wanaonekana kutoguswa na kutochukua hatua yoyote ya kukusaidia unafanyaje? Unadhani Mordekai alikuwa sahihi kukataa kuvua magunia?
- Unadhani nafasi ya Esta ilikuwa na nafuu yoyote kulingana na tangazo la mfalme la kuwaangamiza Wayahudi wote? Kama Esta asingeamua kuwasaidia ndugu zake Wayahudi nani mwingine angewasaidia? Je uchaguzi wa kusaidia ndugu na kupoteza kiti cha umalkia na kuhatarisha maisha ulikuwa mrahisi kwa binti mdogo kama Esta?
- Kwa nini wakati uonevu ukiendelea katika jamii baadhi ya watu huchagua kuendelea kukaa kimya kana kwamba hawahusiki? Je ushauri wa Esta kwamba Wayahudi wafunge kwa ajili yake ulikuwa unalenga kuwaonesha kuwa vita ni ya kiroho hivyo wamtegemee Mungu zaidi kuliko kumtegemea yeye? Kauli yake kwamba 'nikiangamia na niangamie' ilikuwa inaashiria woga au ujasiri?
MASWALI YA KUJADILI: ESTA 5:1-14
- Unaizungumziaje hekima ya malkia Esta katika kumuandaa mfalme Ahasuero kisaikolojia ili akubali ombi lake? Inawezekana kuwa mara nyingi tunakosa kutekelezewa haja zetu kwa sababu ya kutojua namna ya kuziwasilisha?
- Wivu na chuki vimewafanya baadhi ya watu kukosa amani na furaha licha ya kuwa Mungu amewajalia kuwa na kila kitu. Je unadhani ni rahisi kwa mtu mwenye wivu kuwa na furaha au maendeleo?
- Kuwasema watu vibaya na kuonesha chuki kwao kwenye mazungumzo ya kifamilia kunasaidia kitu katika kujenga mahusiano mema? Je watoto wanaathirikaje na hali hiyo? Njia sahihi ya kumsaidia nduguyo anayelalamikia watu wengine wasiomheshimu huko kazini na kwenye shughuli zake za kila siku ni ipi?
MASWALI YA KUJADILI: ESTA 6:1-14
- Kuwepo kwa kitabu cha maandiko ya taarifa kulileta nafuu gani kwa kiongozi wa taifa ili kuhakikisha haki inatendeka kwa raia wake? Je ni muhimu kuwa na kumbukumbu ya matendo mema na ya kizalendo yaliyotendwa na raia au waumini kwa ajili ya nchi yao au taasisi yao? Kama mambo yasipoandikwa kuna uwezekano wowote wa historia kupotoshwa?
- Ukipewa nafasi ya kupendekeza mtu anayestahili kupandishwa cheo utampendekeza yule anayestahili japo ni adui yako? Je kuchongea watu kunaweza kuleta madhara gani kwako wewe unayechongea? Je umeona jinsi Mungu anavyotawala matukio kwenye kuinuka na kushushwa kwa Mordekai na Hamani? Lipi bora kujipendekeza kwa Mungu au kujipendekeza kwa wanadamu?
- Kwa nini wenye hekima na Zereshi walimwambia Hamani kuwa hataweza kupambana na Mungu wa Wayahudi ambaye Mordekai anamtumainia? Kwa nini ushauri huu ulikuja kwa kuchelewa? Je ni sahihi kupambana na mtu usiyejua asili ya nguvu zake?
MASWALI YA KUJADILI: ESTA 7:1-10
- Je, unapoheshimiwa kuliko watu wa kwenu waliokulea na kukufikisha kwenye hatua ya mafanikio uliyonayo sasa unajisikia vizuri au unajisikia vibaya? Kwa nini Esta na Musa, licha ya kupata upendeleo wa kufika ikulu kubwa za kidunia hawakuwasahau watu wa kwao ambao katika nyakati hizo walikuwa wateule wa Mungu? (Waebrania 11:24-25) Je, tabia hiyo ina mlingano wowote na tabia ya Kristo? (Wafilipi 2:5-6)
- Je, kudai haki yako na ya watu unaodhani wanaonewa ni kujiingiza kwenye siasa au uharakati? Je, Esta alipokuwa anapigania haki za watu wake alikuwa anafanya siasa au uanaharakati? Je, siasa na utungaji wa sera na sheria za nchi unagusa Maisha ya kila raia wan chi husika? Nini hatari ya kuogopa kutetea haki za watu wengine wanaoonewa?
- Kwa nini Hamani baada ya kumkasirisha mfalme Ahasuero alienda kujitakia Maisha kwa kumlilia Vashti badala ya Kwenda kumlilia mfalme mwenyewe? Je, Kwenda kupunga upepo nje kwaweza kusaidia kupunguza hasira? Ilikuwaje mfalme asielewe njama za kuwaangamiza Wayahudi zilizofanywa na wasaidizi wake? Nini hatari ya watu wanaopenda kujipendekeza kwa watawala?
NILICHOGUNDUA NA KUJIFUNZA: ESTA 7:1-10
- Mara moja moja inapendeza kutoka na mkeo kwenye sherehe na kujumuika na watu. Maisha yanapokuwa na mitoko ya pamoja pale inapowezekana huyafanya maisha kuwa rahisi na huepusha misongo. Kiongozi asiyeandamana na mkewe au mumewe katika safari zake zote huzua maswali juu ya mahusiano yake ya ndoa. Ndege wanaofanana huruka pamoja.
- Wanaopendana huketi pamoja na kuendelea kuzungumza kwa kubadilishana mawazo. Hawakai kama mabubu. Tena inapendeza wakiibua mijadala mizito inayohusu mustakabali wa maisha yao. Na kama Biblia inavyoshauri waume wanapaswa kugundua hisia walizonazo wake zao ili wazirekebishe na kuyafanya maisha yao kujawa na furaha daima. Mke hujisikia vizuri pale anapotambua kuwa mumewe anamjali.
- Mke ana bahati ya kutambua afanye nini kwa mumewe ili atimiziwe haja yake. Anapoitumia vema karama hiyo ana uhakika wa kuwa salama siku zote. Mume anayeheshimiwa na kustahiwa na mkewe huona fahari kumtendea mema mkewe siku zote za maisha yake (Mithali 31:10-11).
- Watu wanafiki hawafai kuwa rafiki. Hujifanya kuwa wema machoni lakini moyoni wana chuki ya kutisha. Wanawake ni wepesi kutambua marafiki wabaya wa waume zao hasa wale ndumila kuwili. Usipuuze mkeo anapokuambia yule rafiki yako si mtu mzuri. Kwa asili wao wana siri nyingi wanazozijua ambazo hubaki nazo mioyoni. Kaa nao vizuri watakusaidia kubaini marafiki wa kweli na wa uongo.
- Wanawake ni majasiri inapokuja swala la kutetea haki na hasa kumtetea Mungu. Hawakuwahi kuwa sehemu ya mitume 12 wa Yesu lakini hiyo haikumaanisha wangekosa uadilifu. Wakiaminiwa na kutiwa nguvu wana uwezo wa kusimamia haki na kupambana na Ibilisi kwa mafanikio makubwa.
NILICHOGUNDUA NA KUJIFUNZA: ESTA 8:1-17
- Kuna wakati wa kurejeshewa haki yako iliyopokonywa kwa hila. Mgawa riziki hajakusahau ila Yeye hufanya kila jambo kwa mujibu wa ratiba yake. Kuna wakati wa aliye juu kushuka chini na aliye chini kupanda juu. Haki ya mtu haiwezi kupotea. Isubiri.
- Pete ni ishara ya mamlaka na ukuu. Mwana mpotevu aliporejea kwa baba yake alivalishwa pete kuashiria kukabidhiwa mamlaka yanayofanana na yale ya baba yake. Sisi tutakaokombolewa tutapewa ufalme na kuketi kwenye kiti cha enzi cha Mungu Baba yetu (Luka 12:32; Danieli 7:27). Mungu atatuinua kupita pale tulipokuwa kabla ya dhambi. Ajikwezaye atadhiliwa naye ajidhiliye atakwezwa (Luka 14:11). Subiri wakati wa Mungu.
- Nafasi ya upendeleo uliyopewa na mamlaka ya nchi isikupofushe macho ukaacha kuangalia masaibu yanayowakuta ndugu zako wasio na upendeleo ulionao. Musa alipoyaangalia mateso ya ndugu zake Waebrania waliokuwa utumwani aliwahurumia na kujaribu kuwasaidia (Kutoka 2:11-12). Na Yesu alipoona tulivyoanguka chini katika tope la dhambi alituhurumia akaja kutukomboa. Kila mtu ana nafasi ya kufanya kwa ajili ya wokovu wa wengine. Kinachotakiwa ni kuwa na busara kama nyoka na kuwa watu wapole kama hua (Mathayo 10:16).
- Kuna wakati wa watumwa kuitumia ikulu ya nchi ya ugeni kama wapendavyo. Watumwa kama Yusufu na Musa na Esta waliingia ikulu katika nchi ya ugeni kuashiria sisi tulio watumwa wa dhambi tutakavyoingia ikulu ya mbinguni tukiwa watawala (Wafilipi 3:20; Waefeso 2:19). Yesu aliyechukua asili yetu ni kaka yetu ambaye hajisikii vibaya kutuita ndugu zake (Waebrania 2:11).
- Hamani alikuwa mzalendo wa kweli mwenye kuipenda nchi wakati watu wengine wenyeji hasa wa Umedi na Uajemi walipokuwa wanafiki kwa mtawala wa nchi. Uzalendo wake uliokaribia kuhatarisha maisha yake kwa mfalme ulikuja kumlipa baadaye alipovalishwa vazi la kifalme juu ya farasi wa kifalme. Ndivyo itakavyokuwa kwa wale wote wanaotetea mamlaka ya Mungu wa mbinguni kwa kuzishika na kufundisha amri zake kumi bila kupindisha. Hawa watakuwa na nafasi za mbele kwenye ufalme wa Mungu (Mathayo 5:19).
MASWALI YA KUJADILI: ESTA 9:1-32
- Je, kitendo cha Wayahudi kujilipiza kisasi kwa kuwaua adui zao kwa kibali cha mfalme kilikuwa halali? Kwa nini ilikuwa muhimu watoto wa Hamani waadhibiwe kwa kutundikwa kwenye mti?
- Kwa nini mfalme Ahasuero alikuwa mwepesi kukubali chochote kutoka kwa malkia Esta? Wanawake wa leo wanafeli wapi katika kuwashawishi waume zao kuridhia mashauri mema wanayowapa?
NILICHOGUNDUA NA KUJIFUNZA: ESTA 9:1-32
- Watumishi wanafiki hawana kanuni za kudumu katika utendaji wao. Utendaji wao hutegemea aonavyo kiongozi mkuu katika siku husika. Maakida wa majimbo, majumbe, maliwali na wale waliofanya shughuli ya mfalme waliwasaidia Wayahudi si kwa sababu waliwapenda ila walitaka kujipendekeza kwa mfalme. Watu wa aina hii si wa kuwatumainia. Hawana upendo wa dhati bali wanatumikia matumbo yao (Warumi 16:18).
- Siku iliyopangwa kuwatawala walioonyesha utii kwa Mungu mkuu ndiyo siku iliyogeuka kuwa ya kuwatawala waliokusudia kuwaangamiza waaminifu wa Mungu. Unabii unatudokeza kuwa nguvu za uovu zitaungana kuwaangamiza watu wa Mungu katika siku za usoni pale amri ya Jumapili itakapowekwa. Mungu ajuaye kutawala matukio atageuza siku hiyo ya maangamizo kuwa ya kumpokea Mwokozi wao waliyemngoja (Isaya 25:9). Mungu kwetu ni kimbilio msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso (Zaburi 46:1-3).
- Vita ya kimbari ya kuwakomesha Wayahudi ilishindwa kama ambavyo vita ya kimbari ya kuwakonesha watunzao amri za Mungu na ushuhuda wa Yesu vitakavyoshindwa (Ufunuo 12:17; Ufunuo 15:2-4). Dhambi na waovu vitaangamizwa wala mahali pao hapakuonekana tena (Ufunuo 12:8). Wanafiki na waovu wanatafutiwa dawa yao. Baada ya dhambi na waovu kuchomwa moto uovu hautainuka tena (Nahumu 1:9).
- Si rahisi kumhujumu yule ambaye Mungu amekusudia kumbariki. Mungu akishabariki hakuna awezaye kubatilisha. Hata Balaki alipomkodisha nabii muasi aitwaye Balaamu ili amlaanie taifa la Israeli alijikuta akibariki badala ya kulaani (Hesabu 23:11). Kwa kuwa kila awagusaye watakatifu wake anagusa mboni ya jicho lake (Zekaria 2:8).
MASWALI YA KUJADILI: ESTA 10:1-3
- Kwa namna gani Mordekai anamwakilisha Yesu kwa mambo aliyoyatenda ugenini kwa ajili ya Wayahudi waliokuwa katika hali ya kuonewa? Ingawa kitabu hiki cha Esta hakitaji popote jina la Mungu unaona uwepo wa Mungu katika matukio yaliyotajwa?
NILICHOGUNDUA NA KUJIFUNZA: ESTA 10:1-3
- Nchi yenye idadi ya kutosha ya raia na yenye umakini katika kusimamia na kukusanya kodi nchi hiyo itakuwa na ufanisi katika kuwahudumia watu wake. Na taasisi za kidini zikifanikiwa kusimamia ukusanyaji na matumizi ya mapato yake zitafaulu katika kuhudumia kusudi la injili. Lipo wazo la kuwa na serikali moja yenye sarafu moja kwa matarajio ya kuifanya dunia itawalike vyema na kuchochea maendeleo. Mpango huo hautafaulu umechangamana na ubinafsi na kumwinua mwanadamu. Dunia inamhitaji mtawala aliyeushinda ubinafsi na mwenye kujikana nafsi kama Yesu. Yeye atasimamisha utawala utakaodumu milele ambamo haki yakaa ndani yake (Danieli 2:24; 2 Petro 3:13).
- Watawala wenye dhamira ya kuunda serikali ya pamoja watatumia kisingizio cha kuleta waumini wote pamoja huku msingi ukiwa kuimarisha mafundisho yaliyo mapokeo ya wanadamu. Watasaidia kuandika nyaraka na kutoa matamshi ya vitisho dhidi ya waaminifu wa Mungu. Hautakuwa wakati salama wa kutegemea msaada wa serikali ili kuifanya dini ya Mwenyezi Mungu kusimamia inachokiamini. Katika nyakati hizo watu wakiwa na nguvu za Roho Mtakatifu watasimama wenyewe wakiutetea ukweli. Yesu atasimama upande wa watu wake ili kuwatetea (Daniel 12:1).
- Haishangazi kuwa taarifa za matendo mema ya Mordekai pamoja na kufichua njama za kumpindua kiongozi wa nchi hazikuandikwa katika kitabu cha taarifa cha wafalme wa Umedi na Uajemi. Hii inaonesha watu kadhaa walio kwenye madaraka hawakuridhishwa na nafasi aliyopewa Mordekai na mfalme. Na hawakutaka ionekane mgeni alikuwa na mapenzi ya dhati na nchi kuliko wenye nchi wenyewe. Wapo wasiofurahi unapotenda mema. Na hawapo tayari kuona mema hayo yakitangazwa. Wana kawaida ya kudhoofisha wanaojituma. Kaa nao kimahesabu.
- Kitabu cha Esta kinatamatika kwa maelezo mafupi shujaa akiwa Esta na Mordekai – watu waliolitetea taifa la Mungu utumwani. Lakini kinatamatika bila neno Mungu kutajwa katika kurasa zake. Hata hivyo matendo ya Mungu yanaonekana dhahiri katika kila hatua ambazo watu wake walikuwa wanazipitia. Mungu anaweza asiwe anaonekana maishani mwako lakini matendo yake yanakudhihirishia kuwa yupo. Yupo licha ya changamoto unazozipitia (Zaburi 124:1-9).