Seventh-Day Adventist Church

PASTOR LETTA'S OFFICIAL WEBSITE

Menu

MAHUBIRI

WAZO KUU: USIKATE TAMAA

Fungu Kuu: Zaburi 31:24 Iweni hodari, mpige moyo konde, Ninyi nyote mnaomngoja Bwana

Mungu anakupenda rafiki yangu. Anajua shida yako na kilio chako na anajua wakati muafaka wa kuitatua shida yako. Endelea kuomba, endelea kutumaini, yeye hajakuacha. Ikiwa una dhambi unayojua kuwa inakutenga naye itubu. Isaya 59:1 “Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia. lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.”

Yeye yupo tayari kusamehe dhambi hata ikiwa kubwa kiasi gani. Isaya 1:18 “Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.” Yesu alikufa kwa ajili yako ili usiishi katika hali ya kuteseka. 1 Petro 2:24 “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.” Mungu akubariki unapochukua hatua muhimu za kuyasalimisha maisha yako kwake, katika Jina la Yesu Kristo wa Nazareti. Amina.