Seventh-day Adventist® Church

PASTOR LETTA'S OFFICIAL WEBSITE

Menu

UONGOZI USIO NA KANUNI

KANISA LISILOONGOZWA NA KANUNI

Kuna ubaya gani kanisa lisipoongozwa na Kanuni?
"Kanisa la Kristo liko hatarini wakati wote. Shetani anajaribu kuwaangamiza watu wa Mungu, kwa hiyo, mawazo ya mtu mmoja, maoni ya mtu mmoja, hayawezi kuaminika vya kutosha. Kristo anataka wafuasi wake wakusanyike kama kanisa, wakifuata taratibu, wakiwa na kanuni na nidhamu, na wote wakiwajibika kwa mwingine, huku wakiwachukulia wengine kuwa bora kuliko wao wenyewe.”—3T 445.

"Msiruhusu mawazo ya mtu ye yote yayumbishe imani yenu kuhusu utaratibu na mwafaka unaopasa kuwemo kanisani. ... Mungu wa mbinguni ni Mungu wa utaratibu, na anataka wafuasi wake wote wawe na sheria na kanuni, na kuhifadhi utaratibu.”—5T 274.
"Baadhi ya watu wamekuwa wakitoa wazo kuwa kadiri tunavyokaribia mwisho wa wakati, kila mtoto wa Mungu atafanya kazi bila kuwa katika muundo wo wote wa kidini. Lakini nimeelekezwa na Bwana kuwa katika kazi hii, hakuna suala la kila mtu kufanya kazi peke yake.”—TM 489.

“Idadi yetu ilipokuwa inaongezeka, ilionekana wazi kuwa bila muundo wa namna fulani kungekuwa na machafuko makubwa, na kazi isingesonga mbele kwa mafanikio. Muundo ulikuwa wa lazima kwa ajili ya kusaidia kazi ya Mungu, kuanzisha kazi katika maeneo mapya, kulinda makanisa na kazi ya Mungu dhidi ya washiriki wasiofaa, kutunza mali ya kanisa, kuchapisha ukweli katika viwanda vya uchapaji, na kwa ajili ya makusudi mengine mengi.”—TM 26.

“Mara kwa mara nimeelekezwa na Bwana kuwa hakuna uamuzi wa mtu ye yote unaopasa kusalimishwa kwa uamuzi wa mtu mwingine ye yote. Mawazo ya mtu mmoja au ya watu wachache yasichukuliwe kuwa yanatosha katika hekima na uwezo wa kuendesha kazi, na kuamua mipango ya kufuatwa. Lakini, uamuzi wa ndugu waliokusanyika toka sehemu zote za kanisa unapofanyika katika ‘Konferensi Kuu,’ uhuru binafsi na uamuzi binafsi haupaswi kuendelezwa kikaidi, bali uachwe. Mtenda kazi ye yote asichukulie kuwa jambo jema kung’ang’ania maoni yake ya binafsi, dhidi ya uamuzi wa chombo hicho kikuu.” – Testimonies for the Church, Kitabu cha 9 uk 260.

“Kauli hii ina nguvu katika vizazi vyote. Uwezo wa kuchukua hatua kwa niaba ya Kristo umewekwa kwa kanisa. Ni chombo cha Mungu kwa ajili ya kuhifadhi utaratibu na nidhamu miongoni mwa watu wake. Bwana amelipatia uwezo wa kuamua mambo yanayohusu ustawi, usa , na utaratibu wa kanisa. Kanisa lina wajibu wa kuondoa watu wasiofaa katika ushirika wake, wanaoudhalilisha ukweli kwa tabia yao isiyofanana na ya Kristo. Jambo lo lote ambalo kanisa litafanya kwa kufuata maelekezo yaliyotolewa katika Neno la Mungu litaidhinishwa mbinguni.”—7T 260-263.

“Mkombozi wa ulimwengu alilipatia uwezo mkubwa kanisa lake. Anaelezea kanuni za kufuatwa katika mashauri ya washiriki wake. Baada ya kutoa maelekezo dhahiri kuhusu njia ipasayo kufuatwa, Anasema: ‘Amin, nawaambia, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua [katika marudi ya kanisa] duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni. Kwa njia hiyo, hata mamlaka ya mbinguni huidhinisha marudi ya kanisa kwa washiriki wake kama kanuni ya Biblia imefuatwa. 

“Neno la Mungu haliruhusu mtu mmoja kung’ang’ania maoni yake yanayopingana na uamuzi wa kanisa, wala haruhusiwi kusisitiza maoni yake dhidi ya yale ya kanisa.”—3T 428.

“Kusingekuwa na marudi na utawala wa kanisa, kanisa lingepasuka vipande vipande; lisingeweza kushikamana kama jumuiya.”—3T 428.

“Ugomvi, mivutano na daawa kati ya ndugu hudhalilisha harakati za kueneza ukweli. Wanaochukua hatua hiyo hulisababishia kanisa dhihaka kutoka kwa maadui wake na kuzifanya nguvu za giza zishinde. Wanayachoma majeraha ya Kristo upya na kumfedhehi kwa dhahiri. Kwa kupuuza mamlaka ya kanisa wanaonesha dharau yao kwa Mungu, ambaye amelipa kanisa mamlaka yake.”—5T 242, 243.

“Wale wenye vyeo vyenye majukumu katika kanisa wanaweza kuwa na kasoro kama walivyo watu wengine na wanaweza kukosea katika uamuzi wao; lakini pamoja na hayo, kanisa la Kristo duniani limewapa mamlaka yasiyoweza kupuuzwa.”—4T 17.

“Waumini wa Thesalonike walikuwa wanakerwa sana na watu waliokuwa wanatokea kati yao wakiwa na mawazo na mafundisho yenye itikadi kali. Wengine walikuwa ‘waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine.’ Kanisa lilikuwa limeundwa kihalali, na mao sa walikuwa wamechaguliwa kuwa wachungaji na mashemasi. Lakini walikuwapo wengine waliokuwa wakaidi, wasio kiri, waliokuwa hawataki kuwa chini ya wale waliokuwa na mamlaka kanisani. Pamoja na kudai kuwa na haki ya kuwa na uamuzi wao wenyewe, walikuwa pia wanadai hadharani kuwa na haki ya kushinikiza mawazo yao kwa kanisa. Kutokana na hali hiyo, Paulo aliwakumbusha Wathesalonike juu ya heshima na staha iwapasayo wale waliochaguliwa kushika nafasi zenye mamlaka kanisani.”—AA 261, 262.

“Mungu ameweka kanisani wasaidizi wake aliowachagua, watu wenye talanta mbalimbali, ili kwa kuunganisha hekima ya wengi, nia ya Roho iweze kutimia. Watu wanaoenenda kwa kufuata tabia zao shupavu, wakikataa kushikamana na wengine walio na uzoefu mkubwa katika kazi ya Mungu, watapofushwa kwa kujiamini, wasiweze kutofautisha yale ya uongo na ya kweli. Si salama kwa watu kama hao kuchaguliwa kuwa viongozi kanisani; kwani watafuata uamuzi na mipango yao wenyewe, bila kujali uamuzi wa ndugu zao. Ni rahisi kwa yule adui kufanya kazi kwa njia ya wale ambao, licha ya wao wenyewe kuhitaji ushauri katika kila hatua, huamua kuongoza watu kwa nguvu zao wenyewe, bila kujifunza kwanza unyenyekevu wa Kristo.”—AA 279. (tazama uk. 34, 35, 114-116.)

"Ingawa Mungu hakai katika nyumba zilizojengwa kwa mikono, lakini huiheshimu mikutano ya watu wake kwa kuwepo kwake. Ameahidi kwamba wanapokusanyika kumtafuta, kukiri dhambi zao na kuombeana, atakutana nao kwa njia ya Roho wake. Lakini wale wanaokutana kwa ajili ya kumwabudu hawana budi kujitenga na kila jambo baya. Wasipomwabudu katika roho na kweli na katika uzuri wa utakatifu, kukusanyika kwao kutakuwa bure.”—PK 50.

“Kuna maelfu ya majaribu yaliyo chika ambayo yameandaliwa kwa ajili ya wale walio na nuru ya ukweli; na usalama pekee kwa ye yote kati yetu ni kutopokea fundisho lo lote jipya, fasiri yo yote mpya ya Maandiko, bila kuiwasilisha kwanza kwa ndugu wenye uzoefu. Iweke mbele yao kwa moyo mnyenyekevu unaofundishika, kwa maombi ya dhati; na wasipoona nuru ndani yake, ukubaliane na busara yao; kwani ‘kwa wingi wa washauri huja wokovu.’”—5T 293. (Tazama pia Mdo. 15:1-32.)

"Tusije tukapokea maneno ya wale wanaokuja na ujumbe unaopingana na hoja mahususi za imani yetu. Huwa wanakusanya Maandiko mengi, na kuyaleta kama ushahidi wa nadharia zao wanazozing’ang’ania. Mambo haya yamekuwa yakifanyika tena na tena katika miaka hamsini iliyopita. Pamoja na kwamba Maandiko ni Neno la Mungu na inapasa yaheshimiwe, matumizi yake yakiondoa nguzo moja kutoka katika msingi ambao Mungu ameusimamisha kwa miaka hii hamsini, litakuwa kosa kubwa. Mtu atumiaye Maandiko kwa jinsi hiyo haujui udhihirisho wa ajabu wa Roho Mtakatifu ulioupa nguvu na kani ujumbe uliotangulia ambao uliwajia watu wa Mungu.”—CW 32.

"Ingawa tuna kazi ya kila mmoja na wajibu wa kila mmoja mbele za Mungu, hatutakiwi kufuata maoni yetu wenyewe bila kujali maoni ya ndugu zetu; kwani hatua hiyo itasababisha vurugu katika kanisa. Ni kazi ya wachungaji kuheshimu uamuzi wa ndugu zao; lakini uhusiano kati yao na mafundisho wanayofundisha lazima vipimwe kwa sheria na ushuhuda; kisha kama mioyo inafundishika, hakutakuwa na migawanyiko kati yetu. Wengine wana mwelekeo wa kuwa na vurugu, na wanatanga mbali na mambo muhimu yanayoitambulisha imani; lakini Mungu anawavuvia wachungaji wake kuwa wamoja katika mafundisho na katika roho.”—TM 29, 30.