Seventh-day Adventist® Church

PASTOR LETTA'S OFFICIAL WEBSITE

Menu

MASWALI YA BIBLIA

MASWALI YA KUCHAGUA:LUKA 8:1-56
1. Yesu alikuwa akihubiri na kutangaza injili kwa kuzunguka-zunguka

(a) mijini na vijijini.

(b) mijini tu.

(c) vijijini tu.

  1. Na . . . kadhaa wenye pepo wabaya na magonjwa wakaponywa.

(a) wanaume

(b) wanawake

(c) wanaume na wanawake

  1. Hawa ni miongoni mwa wanawake waliokuwa kimhudumia Yesu kwa mali zao.

(a) Mariamu mama yake Yesu

(b) Mariamu aitwaye Magdalene

(c) Kuza

  1. Mbegu zilizoanza kumea zikakauka kwa kukosa rutuba ni zile zilizoangukia

(a) karibu na njia.

(b) kati ya miiba

(c) penye mwamba

  1. Walioangukia kwenye ________ ni wale walisikiao neno na kulishika na kuzaa matunda kwa _________

(a) uvumilivu

(b) wakati

(c) wingi

  1. Yesu alipomuuliza mwenye pepo jina lako nani alijibu jina langu ni

(a) Shetani

(b) Jeshi

(c) Maimuna

  1. Umri wa binti Yairo ndiyo umri ambao mwanamke aliyegusa pindo la vazi la Yesu alitumia

(a) kumtafuta Yesu amponye

(b) kutokwa na damu

(c) kugusa pindo la vazi la Yesu

  1. Yesu akiwa njiani kuelekea kwa binti Yairo walikuja watu kutoka nyumbani wakisema

(a) mhimizeni mwalimu afanye haraka mtoto amezidiwa

(b) mwambieni mwalimu amuombee mtoto hapa hapa njiani

(c) msimsumbue mwalimu binti yako amekwisha kufa

  1. Yesu alipomwona Yairo amefadhaika kwa taarifa za msiba alimwambia

(a) usiwe na hofu, amini tu naye ataponywa.

(b) usiwasikilize mtoto hajafa

(c) sina sababu ya kuendelea na safari maana mtoto amekufa

  1. Baada ya mtoto kufufuliwa Yesu aliamuru mtoto

(a) aombe

(b) apewe chakula

(c) apewe maji ya kunywa

 

MASWALI YA KUJADILI: LUKA 4:1-44

  1. Kama Yesu ni nafsi ya Mungu ilikuwaje akaongozwa na Roho Mtakatifu kwenye majaribu yake? Je Shetani alikuwa anamjaribu Yesu kama mwanadamu au kama Mungu? Kutokula kitu kuna msaada gani kwa anayejaribiwa? Je ni salama kwa wanadamu wa kawaida kufunga siku 40 bila kula? Je Shetani alitilia shaka Uungu wa Yesu? Je kwa Yesu kutogeuza jiwe kuwa mkate kulidhihirisha kuwa si Mwana wa Mungu?
  2. Kama lengo la Yesu kuja duniani ni kuja kurejesha umiliki wa dunia uliokuwa mikononi mwa Shetani kwa nini hakukubali pendekezo la Shetani la kusujudiwa ili apewe ulimwengu wote? Je Shetani huwa anasoma Maandiko? Kwa nini yameshibdwa kumbadilisha? Je mtu anaweza kusoma Maandiko kwa malengo mabaya? Kama Shetani anaweza kwenda juu ya kinara cha hekalu anaweza kushindwa kuingia kanisani? Kama hawezi kuogopa nyumba za ibada ni wapi palipo salama asipoweza kufika?
  3. Kwa nini Yesu alisoma kifungu cha Biblia kilichowakera waliokuja kuabudu? Kwa nini watu kwa kawaida hawampendi mhubiri anayewaambia ukweli? Je kunahitajika bìsara katika kuhubiri Neno la Mungu? Kwa nini watu wa Nazareti waliibua hoja ya unasaba wa Yesu? Je Yesu hakuwa anakubalika kijijini kwao? Je Yesu alikuwa na mahusiano mazuri na watu?
  4. Kwa nini watu wa vijiji vingine waliyapenda maneno ya Yesu wakiyasifia kuwa yalikuwa na nguvu? Yesu aliposema fumba kinywa alikuwa anamwambia mwenye pepo au pepo lenyewe? Je akiwepo mwenye homa unatakiwa umuombee au uikemee ile homa? Katika kuwaponya wenye maradhi ipo haja ya kuweka mikono juu yao?
  5.  

MASWALI YA KUCHAGUA; LUKA 3:1-38

  1. Ondoleo la dhambi husababishwa na

(a) ubatizo wa maji mengi

(b) ubatizo wa toba

(c) mahubiri

  1. Kwa mujibu wa Yohana Mbatizaji waliostahili kuuona wokovu wa Mungu walikuwa ni

(a) wote wenye mwili

(b) wote waliobatizwa

(c) wote waliotubu

  1. Askari waliokuja kwa Yohana Mbatizaji wakitaka kubatizwa aliwaambia

(a) toshekeni na mishara yenu

(b) msimdhulumu mtu

(b) msimshitaki mtu kwa kumsingizia

(c) msimdhulumu mtu

(d) majibu yote hapo juu ni sahihi

  1. Herode alimfunga Yohana Mbatizaji gerezani kwa sababu

(a) alikuwa anawabatiza watu Yordani bila kibali

(b) alikaripiwa kwa kumchukua mke wab nduguye

(c) aliwatuhumu askari wake kuwa hawatosheki na mishahara yao.

  1. Yesu alianza kufundisha akidhaniwa kuwa na miaka

(a) 30

(b) 27

(c) 31

 

MASWALI YA KUCHAGUA: LUKA 1:1-80

  1. Luka anatuthibitishia kuwa taarifa anazoandika zimetokana na utafiti aliofanya kwa

(a) wanafunzi wa Yesu

(b) mashahidi wenye kuyaona yaliyoandikwa na watumishi wa lile neno

(c) kutumia elimu yake ya kidaktari

  1. Zakaria na mkewe Elizabethi walikuwa

(a) makuhani nyakati za mfalme Herode

(b) wenye haki mbele za Mungu

(c) hawana mtoto maana wote wawili walikuwa tasa

  1. Zakaria alipotokewa na malaika hekaluni

(a) alijawa na furaha akijua maombi yake yamejibiwa

(b) alianguka kifudifudi akamsujudia

(c) alifadhaika, hofu ikamwingia

  1. Mtoto aliyetabiriwa na malaika kuzaliwa kwa familia ya Zakaria na mkewe angekuwa wa ________ na jina lake angeitwa ----------.

(a) kiume, Yohana

(b) kiume, Yohana Mbatizaji

(c) kike, Mariamu.

  1. Yohana alijazwa na Roho Mtakatifu

(a) siku aliyozaliwa

(b) siku aliyobatizwa

(c) tangu tumboni mwa mamaye

  1. Kitoto kichanga kiliruka tumboni mwa Elizabeti wakati

(a) sauti ya kuamkia ya Mariamu ilipoingia masikioni mwake

(b) Roho Mtakatifu alipoingia tumboni kwa Elizabeti

(c)

  1. Kitoto kichanga kiliruka tumboni mwa Elizabeti wakati

(a) sauti ya kuamkia ya Mariamu ilipoingia masikioni mwake

(b) Roho Mtakatifu alipoingia tumboni kwa Elizabeti

(c) Elizabeth alipokutana na Mariamu.

  1. Kuhani Zekaria alikuwa bubu kwa agizo la malaika kwa sababu

(a) alikosa adabu ķwa malaika

(b) hakusadiki maneno ya malaika

(c) ili asije akatoa siri ya yale waliyoongea na malaika.

  1. Mtoto aliyezaliwa kwa Zekaria na Elizabeth aliitwa Yohana kwa sababu

(a) kuna mtu katika jamaa yao aliitwa jina hilo.

(b) ndilo jina lililopendekezwa na malaika

(c) ndilo jina ambalo Zekaria na mke wake walipatana wampe mtoto wao.

  1. Mtoyo Yohana alikua na kiongezeka kiroho naye alikaa

(a) majangwani

(b) nyumbani kwa wazazi wake.

(c) hekaluni

 

MASWALI YA KUCHAGUA: MARKO 16:1-20

  1. Siku Yesu aliyofufuka inaitwa:

(a) siku ya kwanza ya juma

(b) siku inayofuata baada ya Sabato kuisha.

(c) Jumapili

(c) A, B na C, hapo juu ni sahihi.

  1. Sabato ni siku

(a) iliyo kabla ya siku ya kwanza ya juma

(b) iliyo kabla ya Jumapili

(c) ya Jumamosi

(d) A, B, na C hapo juu ni sahihi.

  1. Yesu alifufuka

(a) siku ya kwanza ya juma

(b) siku ya saba ya juma

(c) siku ya Ijumaa Kuu

  1. Mariamu Magdalene aliwafikishia wenzake habari za kufufuka kwa Yesu na kuwakuta wakiwa

(a) wamelala usingizi

(b) wanaomboleza na kulia

(c) wanaomba na kusali

  1. Waombolezaji waliposikia habari kuwa Yesu yu hai na ameonekana

(a) walifurahi na kumtukuza Mungu

(b) walijawa na hofu kubwa

(c) hawakusadiki

  1. Ipi kauli sahihi ya Yesu

(a) Aaminiye na kubatizwa ataokoka

(b) Asiyeamini akabatizwa ataokoka

(c) Aaminiye bila kubatizwa ataokoka

  1. Kijana aliyevaa mavazi meupe waliyemkuta kaburini aliwaambia "enendeni mkawaambie wanafunzi na _________ ya kwamba awatangulia kwenda ________.

(a) Yohana, Galilaya

(b) Mariam, Yerusalemu

(b) Petro, Galilaya

  1. Walioambiwa watashika nyoka na hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa ni kina nani?

(a) Wanafunzi wa Yesu

(b) Waaminio

(c) Waliokwenda kaburini siku Yesu alipofufuka

  1. Baada ya kufufuka Yesu aliwaagiza wanafunzi wake waende ulimwenguni wakaihubiri Injili

(a) kwa kila kiumbe

(b) kwa wanadamu wote

(c) kwa nyumba ya Israeli

  1. Yesu alipopaa mbinguni alienda

(a) kuketi mkono wa kuume wa Mungu.

(b) kuandaa makao ya watakatifu

(c) kufanya sherehe ya kukamilisha kazi ya ukombozi

 

MASWALI YA KUCHAGUA: MARKO 15:1-47

  1. Wakuu wa Wayahudi waliwataharakisha mkutano waombe wafunguliwe Baraba badala ya Yesu. Baraba alifungwa kwa kosa gani?

(a) Alikuwa amemsaliti Yesu

(b) Alikuwa amefanya fitina na kufanya uuaji.

(c) Alikuwa amehoji kwa nini Warumi wawatawale Wayahudi.

  1. Pilato alimfungulia Baraba kutoka gerezani kwa kuwa

(a) ni kawaida ya serikali ya Kirumi kumfungulia mfungwa mmoja aliyeombwa na raia wakati wa sikukuu

(b) alikuwa raia mwenye sifa njema kuliko Yesu

(c) alikuwa amejutia kosa lake na kujirekebisha

  1. Pilato alipowauliza makutano ni ubaya gani Yesu ametenda wao walijibu_______

(a) Anawadhulumu watu mali zao

(b) Anakufuru kwa kujifanya kuwa yeye ni Mungu.

(c) Msulibishe

  1. Wakamleta mpaka mahali paitwapo __________ yaani Fuvu la kichwa.

(a) Golgotha

(b) Getsemane

(c) Kalvari

  1. Waliomsujudia Yesu baada ya kupigwa mijeledi na kutemewa mate walifanya hivyo

(a) ili kumpunguzia maumivu

(b) ili kumtambua kuwa ni mfalme wa Wayahudi

(c) ili kumdhihaki

  1. Baada ya Yesu kuelemewa na uzito wa msalaba na kuanguka nao mara kadhaa askari wa Kirumi

(a) wakamshurutisha mtu aliyekuwa akipita aitwaye Simoni Mkirene aubebe.

(b) wakauchukua msalaba na kuuweka kwenye gari linalokokotwa na farasi.

(c) wakaufunga msalaba kwa kamba ili Yesu aukokote.

  1. Baada ya Yesu kusulubiwa msalabani wapita njia walitikisa vichwa vyao wakisema,

(a) jiponye nafsi yako ushuke msalabani

(b) mtu huyu hakuwa na hatia yoyote

(c) Yesu Mwana wa Daudi tuokoe

  1. Eloi, Eloi, lama sabakthani maana yake

(a) Mungu wangu, Mungu wangu, niokoe.

(b) Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?

(c) Mungu wangu, Mungu wangu, naiweka roho yangu mikononi mwako.

  1. Aliyetamka "hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu wakati wa kufa kwa Yesu alikuwa nani?

(a) mmojawapo wa wafungwa walisulibishwa na Yesu

(b) Pilato

(c) Akida

  1. Mtu aliyeingia kwa Pilato na kuuomba mwili wa Yesu ili akauzike alikuwa nani?

(a) Wanawake waliofuatana naye huko Galilaya ili kumtumikia

(b) Akida wa jeshi la Kirumi

(c) Yusufu wa Arimathaya

 

MASWALI YA KUCHAGUA: MARKO 14:1-72

  1. Waliotafuta njia ya hila ya kumkamata na kumwuua Yesu walikuwa

(a) Viongozi wa Serekali ya Kirumi

(b) Wakuu wa Makuhani na Waandishi

(c) Viongozi wa dini.

  1. Watu walilaumu kitendo cha mwanamke aliyempaka Yesu mafuta kwa sababu

(a) Mwanamke yule alikuwa malaya

(b) Mafuta yale yalikuwa na thamani kubwa.

(c) Mafuta yale yangeweza kuuzwa kwa dinari 300 na zaidi na kupewa maskini.

  1. Wakuu wa makuhani walipopata habari kuwa Yuda amekubali kumsaliti Yesu

(a) Walimkanya sana asifanye hivyo

(b) Wakafirahi sana wakaaodi kumpa fedha

(c) Walimwendea Yesu wakimwonya juu ya mpango wa Yuda.

  1. Yesu akawatuma wawili wa wanafunzi wake akawaambia nendeni mjini nanyi mtakutana na

(a) Mwanaume amechukua mtungi wa maji.

(b) Mwanamke amechukua mtungi wa maji

(c) Kundi kubwa la watu wanakuja kunilaki.

  1. Ingawa Yesu alijua atasalitiwa na kuuawa bado alimpa ole anayemsaliti kwa sababu

(a) ameyatekeleza hayo kwa tamaa zake na hajatumwa na Mungu.

(b) muda wake ulikuwa haujafika

(c) hakumshirikisha

  1. Nao walipokwisha _________ walitoka kwenda mlima wa Mizeituni.

(a) kusali

(b) kula

(c) kuimba

  1. Yesu alipowaambia wakeshe wasije wakaingia majaribuni alitaka

(a) waombe angalau kwa saa moja pamoja naye

(b) wajiandae kumtetea mara atakapokamatwa

(c) wajiandae kukimbia

  1. Yuda Iskariote aliwapa ishara gani wale wakamataji ili kumtambulisha Yesu?

(a) Jogoo kuwika mara tatu.

(b) Kumbusu

(c) Kuanguka kifudifu.

  1. Kuhani mkuu alirarua nguo zake kwa kuwa Yesu alikuwa amejitambulisha

(b) kama Mwana wa Mungu.

(a) kama Kuhani mkuu

(c) kama mfalme wa ulimwengu.

  1. Yule aliyemtambua Petro kama ni mwanafunzi wa Yesu alikuwa

(a) kijakazi wa Kuhani Mkuu.

(b) askari wa Kirumi

(c) mfalme Herode

 

MASWALI YA KUCHAGUA: MARKO 11:1-33

  1. Wanafunzi wa Yesu walipokuwa wanamfungua mwana-punda ‐------- wakawaambia, Mnafanya nini kumfungua mwana-punda?

(a) Baadhi ya watu waliosimama huko

(b) Wapita njia

(c) Wenye mwana-punda.

  1. Yesu aliuendea mtini asubuhi ili achume tini maana

(a) aliona njaa

(b) alikuwa na hamu na tini

(c) haukuwa wakati wa tini

  1. Yesu alisema yoyote myaombayo mkisali aminini ya kwamba

(a) mtayapokea nayo yatakuwa yenu.

(b) Baba yenu aliye mbinguni atawasamehe ninyi makosa yenu.

(c) yatajibiwa sawasawa na mapenzi ya Mungu.

  1. Ubatizo wa Yohana ulitoka wapi?

(a) mbinguni

(b) kwa wanadamu

(c) haijulikani

  1. Mambo aliyokuwa akiyatenda Yesu alikuwa akiyatenda kwa mamlaka gani?

(a) kwa mamlaka ya Mungu

(b) kwa mamlaka ya wanadamu

(c) kwa mamlaka ya Shetani.

 

MASWALI YA KUCHAGUA: MARKO 10:1-52

  1. Je ni halali mtu kumwacha mkewe?

(a) Ni halali. Ndiyo maana Musa aliruhusu waachane.

(b) Si halali. Maana alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe.

(c) Si halali. Ila kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya wanadamu Musa aliruhusu waachane na Mungu akaridhia.

  1. Yesu alichukizwa

(a) Kuletewa watoto wadogo ili awaguse

(b) Watoto kukemewa na wanafunzi wake.

(c) Kuletewa watoto wadogo ili awabatize.

  1. Yesu alimjibuje aliyemuuliza cha kufanya ili arithi uzima wa milele?

(a) Auze alivyo navyo awe maskini.

(b) Ashike Amri zote 10 za Mungu.

(c) Amepungukiwa upendo kwa binadamu wenzake.

  1. Yesu alipoulizwa "ni nani awezaye kuokoka" alijibu.

(a) Ni yule ategemeaye uwezo wa Mungu.

(b) Ni yule aliyeacha vyote akamfuata.

(c) Ni yule aliye wa mwisho hapa duniani.

  1. Yule mwombaji kipofu aliposikia kuwa Yesu anamuita

(a) Alianza kupaza sauti yake na kusema Mwana wa Daudi, Yesu, unirehemu.

(b) Alitupa vazi lake, akaruka, akamwendea Yesu.

(c) Alisema nataka nipate kuona.

 

MASWALI YA KUCHAGUA: MARKO 8:1-38

  1. Yesu aliwaita wanafunzi akawaambia

(a) Wawatawanye mkutano waende zao nyumbani.

(b) Kwa kuwa wanafunga watazimia njiani.

(c) Nawahurumia mkutano kwa kuwa hawajala siku tatu.

  1. Yesu alipovunja mikate 5 na kuwapa watu 5,000 wanafunzi walichukua vikapu vingapi vimejaa vipande? (a) 12 (b) 7 (c) 5
  2. Yesu alipovunja mikate 7 na kuwapa watu 4,000 wanafunzi walichukua makanda mangapi yamejaa vipande?

(a) 12 (b) 7 (c) 5

  1. Yesu alipomuuliza kipofu aliyemwekea mikono unaona nini alijibu,

(a) Naona watu wanatembea

(b) Naona miti inatembea

(c) Naona watu kama miti, inakwenda.

  1. Yesu alipowauliza wanafunzi wake vile watu wanavyomwita walisema yeye ni

(a) Yohana Mbatizaji

(b) Eliya

(c) Mmojawapo wa manabii

(d) Majibu yote hapo juu ni sahihi.

 

MASWALI YA KUJADILI: MARKO 7:1-37

  1. Kwa nini wanafunzi wa Yesu walidaiwa kula kwa mikono najisi? Kwa nini wanaofundisha maagizo ya wanadamu huku wakipinga Amri za Mungu wanatajwa kama waaomwabudu Mungu bure? Kwa nini kimtiacho mtu unajisi ni kile kimtokacho na si kile kimwingiacho?
  2. Kwa nini Yesu alimwambia mwanamke Myunani aache watoto washibe kwanza? Kwa nini Yesu katika kumponya kiziwi ilibidi atie vidole masikioni mwake? Efatha maana yake nini?

 

MASWALI YA KUCHAGUA: MARKO 7:1-37

CHAGUA JIBU LILILO SAHIHI: (kila swali marks 20).

  1. Unadhani hoja inayoshindaniwa kwenye Marko 7:1 – 23 ni

(a). uhalali wa kula vyakula najisi

(b) uhalali wa kula chakula kisicho najisi kwa mikono isiyonawiwa hadi kwenye kiwiko

(c) Kosa lililofanywa na wanafunzi wa Yesu la kula vyakula najisi vilivyokatazwa kwenye torati.

  1. Wayahudi:

(a) Waliacha amri za Mungu na kushika mapokeo ya wanadamu.

(b) Waliacha mapokeo ya wanadamu na kushika amri za Mungu.

(c) Walishika mapokeo ya wanadamu na amri za Mungu.

  1. Yesu kabla ya kumponya kiziwi

(a) Alimtemea mate usoni mbele za watu

(b) Alitema mate akamgusa ulimi

(c) Alimwambia Efatha maana yake Achia.

  1. Kilichomfanya Yesu kumponya binti wa mwanamke Mfoinike aliyekuwa na mapepo ni pale huyo mwanamke aliposema:

(a) Lakini hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto.

(b) Mtoe pepo katika binti yangu

(c) Si vizuri kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa

  1. Wanafiki kwa mujibu wa sura ya saba ya Marko ni wale:

(a) Wanaomheshimu Mungu kwa midomo ila mioyo yao ipo mbali.

(b) Wanaokataa kula nguruwe wakati alihalalishwa na Yesu.

(c) Wasionawa mikono mpaka kiwiko.