Ndoa ya kufana kati ya Mchungaji Samweli Mbilanga wa mtaa wa Ng'ambo -Biharamulo na Esther Komba wa Makongo Juu imefungwa Jumapili 29/09/2025 na Mchungaji Filbert Mwanga kwenye Kanisa la Waadventista wa Sabato Makongo Juu jijini Dar es Salaam. Tunawaombea wanandoa Mungu awaongoze na kuwabariki.