Seventh-day Adventist® Church

PASTOR LETTA'S OFFICIAL WEBSITE

Menu

KUTAYARISHA NJIA

Kujiweka Tayari Kumlaki Kristo

WAADVENTISTA Wasabato wote hutazamia sana wakati Yesu atakapokuja kuwaehukua kwenda kwenye makao mazuri ambayo amekwenda kuwaandalia. Katika yale makao ya mbinguni hapatakuwapo dhambi tena, wala huzuni, wala njaa, wala umaskini, wala ugonjwa, wala mauti. Mtume Yohana alipofikiri juu ya majaliwa haya yanayowangojea waaminifu hakuweza kujizuia kusema: “Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu Sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye.” - (1 Yohana 3:1, 2.) KN 8.1

Kufanana na Yesu katika tabia ndilo kusudi la Mungu kwa watu wake. Tangu mwanzo ulikuwa mpango wa Mungu kwamba wanadamu, walioumbwa kwa sura yake, wakuze tabia zinazofanana na tabia yake Mungu. Ili kulitimiza hili, wazazi wetu wa kwanza katika Edeni walipaswa kupokea mafundisho kutoka kwa Kristo na malaika kwa kuongea nao uso kwa uso. Lakini baada ya mwanadamu kutenda dhambi hakuweza tena kuzungumza kama apendavyo na malaika kwa jinsi hii. KN 8.2

Kusudi mwanadamu asiachwe pasipo mwongozo, Mungu alichagua njia zingine za kufunua mapenzi yake kwa watu wake, ambazo mojawapo na iliyo kuu ni njia ya manabii - wanaume na wanawake ambao wamepokea na kupeleka mbele ya watu wa Mungu ujumbe aliopenda wauchukue. Mungu aliwaeleza Waisraeli, “Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, Bwana, mtajifunua kwake katika maono, nitasema naye katika ndoto.” - (Hesabu 12:6.) KN 8.3

Ni kusudi la Mungu kuwa watu wake wawe wajuzi na waongofu, wakijua na kufahamu licha ya nvakati wanamoishi, bali hata zile zijazo. “Hakika Bwana Mungu natafanya neno lo lote, Bila kuwafunulia utumishi wake manabii siri yake.” (Amosi 3:7) Hili huwatofautisha watu wa Mungu “wana wa nuru”, (1 The. 5:5). Na watu wa ulimwengu huu. KN 8.4

Kazi ya nabii siyo kutabiri tu. Musa, nabii wa Mungu aliyeandika vitabu sita vya Biblia, aliandika maneno machache ya wakati ujao. Kazi yake imeelezwa na Hosea dhahiri zaidi, “Na kwa nabii Bwana alimtoa Israeli katika Misri, na kwa mkono wa nabii alihifadhiwa.” (Hosea 12:13). KN 8.5

Nabii si mtu anayewekwa na wanadamu wenzake, wala si mtu anayejiweka mwenyewe. Uchaguzi wa mtu ambaye hana budi kuwa nabii uko mikononi mwa Mungu tu,ambaye peke yake aweza kuona na kujua moyo wa mwanadamu. Ni jambo la maana kwamba katika historia ya watu wa Mungu, wanaume kwa wanawake pia mara nyingi wamechaguliwa na Mungu kusema badala yake. KN 8.6

Manabii hawa, wanaume na wanawake waliochaguliwa na Mungu wawe njia ya kutuletea habari za Mungu, wamenena na kuandika mambo ambayo Mungu amewafunulia katika njozi takatifu. Neno la Mungu lenye thamani lina ujumbe wao. Kwa njia ya manabii hawa wanadamu wameongozwa kufahamu vita ambayo inaendelea kwa ajili ya roho za watu, vita baina ya Kristo na malaika zake na Shetani na malaika zake. Tunaongozwa kuifahamu vita hii katika siku za mwisho za dunia, na njia zilizotolewa na Mungu kuihifadhi kazi yake na kuzikamilisha tabia za washiriki ambao watakuwa lile kundi la wanaume na wanawake wanaongojea kumlaki Bwana wao. KN 9.1

Mitume, waandishi wa mwisho wa Biblia wametupa maelezo dhahiri ya matukio ya siku za mwisho. Paulo aliandika juu ya “nyakati za hatari”, na Petro ameonya juu ya “watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe, wakiuliza, “Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake?” Kanisa wakati huu halina budi kuwa vitani maana Yohana alimwona Shetani “akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia.” KN 9.2

Hawa waandishi wa Biblia waliona kuwa lilikuwa kusudi la Mungu kutoa nuru ya pekee na msaada kwa watu wake kabla ya Yesu kuja. KN 9.3

Paulo asema kuwa kanisa lenye kutarajia na kungojea kuja kwa Kristo - Kanisa la Waadventista wa Sabato - halitapungukiwa na karama iwayo yote (1 Wakor. 1:7, 8). Litakuwa lenye umoja, hai, na lenye uongozi kama mitume, manabii, wainjilisti, wacnugaji na waalimu. (Waefeso 4:11). KN 9.4

Mtume Yohana huwatambulisha washiriki wa kanisa la siku za mwisho, “kanisa la masalio”, kama wale “wazishikao amri za Mungu” (Ufunuo 12:17). Pia kanisa hili litakuwa lenye “ushuhuda wa Yesu”, ambao ni “Roho ya Unabii”. (Ufunuo 19:10). KN 9.5

Basi ni dhahiri kuwa kwa mpango wa Mungu kanisa la Waadventista Wasabato - kanisa la unabii, lilipoanza kuwako, lilikuwa na Roho ya Unabii miongoni mwake. Lilikuwa jambo la kufaa kama nini kwa Mungu kusema na watu wake duniani siku za mwisho za dunia kama alivyokuwa amesema na watu wake nyakati za haja maalum kame nyingi zamani. KN 9.6

Na kanisa hili la unabii - kanisa la Waadventista Wasabato - lilipoanza wakati huo huo hasa liliainishwa na unabii, wa miaka mia moja na zaidi kidogo sauti ikasikika miongoni mwetu, ikisema, “Mungu amenionyesha katika njozi takatifu.” KN 9.7

Haya si maneno ya kujisifu, bali usemi wa kijana mwanamke mwenye umri wa miaka kumi-na-saba ambaye alikuwa ameitwa kusema kwa ajili ya Mungu. Katika muda wote wa miaka sabini ya kazi yake ya uaminifu sauti ile ilisikika miongoni mwetu, ikiongoza, ikisahihisha, ikifundisha. Na sauti ile ingali ikisikika hata leo kwa njia ya kurasa maelfu zilizotufikia za maandishi ya mjumbe aliyechaguliwa na Mungu, Ellen G White.

Njozi ya Vita Kuu Baina ya Kristo na Shetani

Nyumba ndogo ya shule katika kijiji kimoja upande wa mashariki ya Amerika ilikuwa imejaa wanaume na wanawake siku ile ya Jumapili alasiri katikati ya mwezi wa Machi, 1858, walipokuwa wamekusanyika kwa ibada. Mchungaji James White aliongoza mazishi ya kijana wa kiume, akihubiri mahubiri ya mazishi. Alipomaliza kusema, Ellen G. White aliguswa moyoni kusema maneno machache kwa wale waliokuwa wakiomboleza. Akasimama na kusema kwa dakika moja au mbili na kisha akanyamaza. Watu wakatazama juu ili kuyasikia maneno mengine kutoka midomoni mwake. Wakashangazwa kidogo na msemo wa ghafula wa maneno haya “Atukuzwe Mungu!” “Atukuzwe Mungu!” uliorudiwa mara tatu kwa mkazo zaidi. Ellen G White alikuwa katika njozi. KN 10.1

Mchungaji White akawaambia watu juu ya njozi alizopewa Ellen G White. Akaeleza kuwa alianza kupewa njozi akiwa kijana mwenye umri wa miaka kumi na saba. Akawaambia kuwa ingawa macho yake yalikuwa yamefumbuka, na ilielekea kana kwamba alikuwa akitazama kitu fulani mbali, alikuwa hana habari za lo lote la mahali alipo na hakujua cho chote kilichokuwa kikitendeka karibu naye. Akataja Hesbu 24:4 na 16 tusomapo habari za mtu “asikiaye maneno ya Mungu, yeye aonaye maono ya Mwenyezi, akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho.” KN 10.2

Akawaeleza watu kuwa hapumui awapo katika njozi na akageukia Daniel 10:17 na kusoma nali ya Daniel alipokuwa katika njozi. Akasema, “Kwangu mimi, mara hazikusalia nguvu ndani yangu, wala pumzi haikusalia ndani yangu.” Ndipo Mchungaji White akawaomba, waliopenda, waende wampime Ellen G White akiwa katika njozi. Daima alitoa uhuru wa kumpima namna hii, na alipendezwa kama aliweza kupatikana daktari kumpima akiwa katika njozi. KN 10.3

Kadiri watu walivyosongamana, waliweza kuona kuwa Ellen White hakuwa akipumua, lakini moyo wake uliendelea kupiga kama kawaida na rangi ya mashavu ya uso wake ilikuwa ya kawaida, Kioo kiliposogezwa karibu na pua na mdomo wake, hakuna ukungu uliokusanyika juu ya kioo. Kisha wakaleta mshumaa na kuuwasha na kuushikilia karibu na pua na mdomo wake. Lakini, mwali wa moto ulisimama wima, bila kuyumbayumba. Watu wakajua kuwa alikuwa hapumui. Alikwenda huko na huko chumbani, na kujongeza mikono yake taratibu akisema kwa kasi mambo yaiiyokuwa yakifunuliwa kwake. Kama Daniel, kwanza alipotewa na nguvu zake za asili, kisha akatiwa nguvu zisiso za kawaida. (Tazama Danieli 10:7, 18, 19). KN 10.4

Kwa muda wa saa mbili Ellen White alikuwa katika njozi. Muda wa saa mbili hakupumua hata kidogo. Kisha kadiri njozi ilivyokuwa inakwisha, akavuta pumzi sana, akanyamaza kwa muda wa dakika moja hivi ndipo akapumua tena, mara akaanza akapumua kwa kawaida. Mara hiyo aliweza kuyajua mazingira yake, na kufahamu mambo yaliyokuwa yakitendeka karibu naye. KN 11.1

Mtu mmoja ambaye alimwona mara nyingi Ellen White akiwa katika njozi, Bibi Marths Amadon, alitoa maelezo yafuatayo: “Akiwa katika njozi macho yake yalifumbuka. Hakupumua, lakini mabega, mikono, na viganja vya mikono vilisogea taratibu, vikionyesha mambo aliyokuwa akiyaona. Hakuna mtu aliyeweza kuisogeza mikono yake. Mara nyingi alitamka maneno ambayo yaliwaonyesha wale waliokuwa karibu naye hali ya maono aliyokuwa nayo, ama ya mbinguni ama ya dumani. KN 11.2

“Neno lake la kwanza katika njozi lilikuwa ‘utukufu’ lililosikika kwanza kwa nguvu, na kisha kufifia na kuelekea kana kwamba yuko mbali sana. Hili mara zingine lilirudiwa KN 11.3

“Wale waliokuwako wakati wa njozi hawakuwa na wasiwasi, wala hapakuwako na jambo lo lote la kuogofya. Lilikuwa jambo la taratibu, na tulivu KN 11.4

“Njozi ilipokwisha, na kupotewa na nuru ya mbinguni, akirudia dunia hii tena, alisema, alipoanza kupumua kama kawaida “GIZA’. Kisha alilegea na kukosa nguvu.” KN 11.5

Lakini yatupasa kurejea kwenye ile hadithi yetu ya njozi ya saa mbili shule. Kwa habari ya njozi hii Ellen White baadaye aliandika: KN 11.6

“Mambo mengi ambayo niliyaona zamani zaidi ya miaka kumi iliyopita juu ya vita ya zama zote baina ya Kristo na Shetani, yalirudiwa, nami naliagizwa kuyaandika.” KN 11.7

Katika njozi anjiona kuwa alikuwa akiyaona kwa macho mambo hayo kadiri yalivyokuwa yakidhihirika mbele yake. Kwanza ilielekea kana kwamba alikuwa mbinguni naye akashuhudia kwa macho dhambi na kuanguka kwa Nyota ya alfajiri (Lucifer). Kisha alishuhudia uumbaji wa ulimwengu huu na kuwaona wazazi wetu wa kwanza katika makao yao ya Edeni. Akawaona wakishindwa na majaribu ya joka nao wakafukuzwa kutoka makaoni mwao Bustanini. Kwa naraka mfululizo wa historia ya Biblia ukapitishwa mbele yake. Akayaona mambo yaliyowapata watakatifu wa zamani na manabii wa Israeli. Kisha akaona kwa macho maisha, na kufa kwa Kristo Mwokozi wetu, na kupaa kwake mbinguni mahali ambapo tokea hapo amehudumu kama Kuhani wetu Mkuu. Baada ya haya akawaona wanafunzi wa Yesu wakitoka kwenda kueneza ujumbe wa Injili hata miisho ya dunia. Upesi sana jambo hili lilifu- atiwa na uasi na miaka ya giza! Kisha akaona katika njozi Matengenezo (Reformation) ya kanisa, wanaume na wanawake wakiwa katika hatari ya kupoteza maisha yao kwa kusimama na kuitetea kweli. Alionyeshwa mambo ya hukumu ambayo ilianza mbinguni mwaka 1844, na kuendelea mpaka siku zetu, kisha alipelekwa katika mambo ya wakati ujao akaona kuja kwa Kristo katika mawingu ya mbinguni. Aliona mambo ya muda wa miaka elfu na nchi mpya. KN 11.8

Akiwa na maono haya dhahiri mbele yake, Ellen White alipokwisha kurejea nyumbani kwake alianza kuandika mambo aliyoyaona na kuyasikia katika njozi. Baada ya miezi sita kitabu kidogo cha kurasa 219 kikatoka katika mitambo ya kuchapisha vitabu chenye jina la The Great controversy Between Christ and His Angels and Satan and His Angels, yaani vita Kuu baina ya Kristo na Malaika zake na Shetani na Malaika Zake. KN 12.1

Kitabu hiki kidogo kilipokelewa kwa moyo mkuu, maana kilieleza dhahiri mambo yaliyokuwa mbele ya Kanisa na kufunua mipango ya Shetani na namna atakavyofanya akijaribu kulipotosha Kanisa na ulimwengu katika vita vya mwisho vya dunia Waadventista walishukuru mno kwamba Mungu alikuwa akisema nao siku hizi za mwisho kwa njia ya Roho ya Unabii, kama alivyoahidi kufanya. KN 12.2

Habari za Vita Kuu, ambazo zimesimuliwa kwa kifupi sana katika kitabu kidogo cha Spiritual Gifts, yaani, Karama za Kiroho, baadaye zilichapishwa tena katika nusu ya mwisho ya Early Writings.. KN 12.3

Lakini kadiri kanisa lilivyozidi kukua na siku zikapita, Bwana kwa njozi nyingi za baadaye alifunua kisa cha Vita Kuu kwa maneno mengi zaidi, na Ellen White akayaandika tena, kati ya mwaka 1870 na 1884, katika vitabu vinne vilivyoitwa The Spirit of Prophecy yaani Roho ya unabii. Kitabu cha TheStory of Redemption hutoa sehemu za maana zaidi za kisa cha Vita Kuu ambazo zimetwaliwa kutoka katika vitabu hivi. Kitabu hiki ambacho kimechapishwa katika lugha nyingi huwaletea watu mambo vale yaliyoonyeshwa katika njozi hizi za Vita Kuu. Pia Ellen White katika vitabu vitano vya baadaye vya jamii ile ya “Conflict of the Ages Series” -Partriarchs naa Prophets, Prophets and Kings, The Desire of Ages, Acts of the Apostles, na The Great Controversy, - alisimulia habari zote kabisa za Vita Kuu. KN 12.4

Vitabu hivi ambavyo hulingana sawa sawa na maneno ya Biblia toka uumbaji hadi wakati unaofuata mwanzo wa dini ya Kikristo (Christian Era) na kuendelea na hadithi hii hata mwisho, huutia moyo nuru. Hivi ni vitabu ambavyo husaidia kuwafanya Waadventista Wasabasto “wana wa nuru” na “wana wa mchana.” Twaona katika jambo hili utimilifu wa ahadi hii: KN 12.5

“Hakika Bwana Mungu hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.” KN 13.1

Akiandika jinsi nuru ambayo ameielezea katika vitabu hivi vya kisa cha Vita Kuu ilivyomfikia, Ellen White asema : “Kwa njia ya nuru ya Roho Mtakatifu, mambo ya vita ya muda mrefu baina ya mema na mabaya yamefunuliwa kwa mwandishi wa kurasa hizi. Mara kwa mara naliruhusiwa kutazama katika vizazi mbalimbali, kazi ya vita kuu ya Kristo, Mkuu wa uzima, Aliye asili ya wokovu wetu, Shetani, mkuu wa uovu, aliye asili ya dhambi, mwasi wa kwanza wa sheria takatifu ya Mungu ” KN 13.2

Kadiri Roho wa Mungu alivyonifunulia akilini mwangu maneno makuu ya kweli ya Neno lake, na mambo ya wakati uliopita na ya wakati ujao, nimeamuriwa kuwajulisha wengine mambo yaliyofunuliwa hivi-kufuatisha historia ya vita hivi zamani za kale na, hasa kuvionyesha kwa njia itakayoleta nuru kwenye shindano linalokaribia upesi la wakati ujao.” 

Jinsi Nuru Ilivyomjia Nabii

Wakati mmoja katika maisha ya wana wa Israeli, kama tulivyokwisha kuona, Bwana aliwaambia watu jinsi apendavyo kuwaletea habari kwa njia ya manabii. Akasema: KN 13.4

“Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, Bwana, nitajifunua kwake katika maono, nitasema naye katika ndoto.” (Hesabu l2:6). KN 13.5

Katika sura iliyopita umesoma juu ya njozi za Vita Kuu ambazo zilifuatana na mambo fulani ya ajabu yaliyoonekana kwa macho. Pengine mtu aweza kuuliza kwamba kwa nini njozi hizi zilitolewa kwa njia hii? Bila shaka ilikuwa kusudi kuimarisha imani ya watu na kuwahakikishia wote kuwa Mungu alikuwa akisema kwa kweli na nabii huyu. Mara nyingi Ellen White hakusema kwa maneno mengi juu ya hali yake akiwa katika njozi lakini siku moja, alisema, “Ujumbe huu ulitolewa kuthibitisha imani ya wote ili siku hizi za mwisho tuweze kuwa na matumaini katika Roho ya unabii.” Kadiri kazi ya Ellen White ilivyozidi kukua, iliweza kupimwa kwa majaribio ya Biblia kama vile, “Mtawatambua kwa matunda yao.” Lakini inachukua muda matunda kukua na Bwana mwanzo alitoa ushuhuda kwa habari za utoaji wa njozi hii ambayo iliwasaidia watu kuamini. KN 13.6

Lakini njozi zote hazikutolewa hadharani na kufuatwa na mambo ya kustajabisha ya kuonekana kwa macho. Katika fungu la Biblia mwanzoni mwa sura hii tumeambiwa kuwa siyo kwamba Mungu hujifunua tu kwa nabii “katika maono” bali huweza pia kusema naye “katika ndoto.” Hii ni ndoto ya unabii, kama ile Danieli asemayo habari zake: KN 13.7

“Katika mwka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli aliona ndoto, na maono ya kichwa chake, kitandani mwake; basi akaiandika ndoto, akatoa habari ya jumla ya mambo haya.” (Danieli 7:1). KN 14.1

Kama Danieli asimuliavyo mambo yaliyofunuliwa kwake, mahali kadha wa kadha anasema, “naliona katika maono yangu wakati wa usiku.” Mara nyingi katika maisha ya Ellen White alipewa njozi akili zake zilipokuwa zimeburudika wakati wa saa za usiku. Twasoma mafungu ya maneno ya mwanzoni kama haya. “Katika njozi za usiku nalionyeshwa dhahiri mambo fulani.” au Mungu mara kwa mara amesema na nabii huyu katika ndoto za unabii. Maswali yaweza kuulizwa juu ya uhusiano baina ya ndoto ya unabii au njozi ya usiku, na ndoto ya kawaida. Juu ya nili Ellen White aliandika mnamo mwaka 1868! KN 14.2

“Ziko ndoto nyingi zinazotokana na mambo ya maisha, ambazo hazihusiani lo lote na Roho ya Mungu. Pia kuna ndoto za uwongo, na maono ya uwongo, ambayo huongozwa na roho ya shetani. Lakini ndoto zitokazo kwa Mungu zimeainishwa katika Neno la Mungu pamoja na njozi. Ndoto za namna hii, tukikumbuka watu walio nazo, na hali ya mambo ambayo kwayo hutolewa, zina uthibitisho wake zenyewe juu ya ukweli wake.” KN 14.3

Wakati mmoja, baadaye sana katika maisha yake Ellen White, mwanawe, Mchungaji W.C. White, akitaka habari ili kuwasaidia wale wasio na haban, alimwuliza swali hili: “Mama, mara nyingi unasema mambo yaliyofunuliwa kwako saa za usiku. Unasema juu ya ndoto ambazo kwazo nuru hukuzukia. Sisi sote tunazo ndoto. Unajuaje kuwa Mungu anasema nawe katika ndoto ambazo mara nyingi unasema habari zake?” KN 14.4

Akajibu, “Kwa sababu malaika, mjumbe yule yule husimama karibu nami kuniamuru katika njozi za usiku kama asimamavyo karibu nami akiniamuru katika njozi za mchana.” Malaika anayesemwa habari zake hapa wakati mwingine ametajwa kama malaika,” “kiongozi wangu,” “mkufunzi wangu”, na kadhalika. KN 14.5

Hapakuwako na matatizo moyoni mwa nabii huyu, wala mashaka yo yote juu ya mafunuo ambayo yalikuja wakati wa saa za usiku; maana hali ya mambo yahusikanayo na mafunuo hayo ilidhihirisha kuwa yalikuwa mafundisho yaliyoamriwa na Mungu. KN 14.6

Nyakati zingine Ellen White alipokuwa akisali, akisema au akiandika, alipewa njozi. Wale waliomzunguka hawakuweza kufahamu juu ya njozi isipokuwa kama alikoma kidogo ikiwa alikuwa akisema au akisali mbele ya watu. Hivyo siku moja akaandika: KN 14.7

“Nilipokuwa nikiomba kwa bidii, nilipotewa na kila kitu pande zote kunizunguka; chumba kikajawa na nuru, nami nilikuwa nikisikiliza ujumbe katika mkutano ambao ulionekana kuwa Halmashauri kuu ya Kanisa Ulimwenguni(General Conference).” Miongoni mwa njozi nyingi alizopewa Ellen White katika maisha yake marefu na ya kazi ya miaka 70, njozi iliyokuwa ndefu kuliko zingine ilimchukua saa nne na iliyokuwa fupi ilichukua dakika tu. Mara nyingi zilikuwa kwa nusu saa, au zaidi kidogo. Lakini hakuna kanuni moja iwezayo kutajwa ambayo huzihusu njozi zote, maana ilikuwa kama Paulo alivyoandika: KN 14.8

“Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi.” (Waebrania 1:1). KN 15.1

Nabii huyu alipewa nuru kwa njia ya njozi, lakini nabii hakuandika akiwa katika njozi. Isipokuwa mara chache, Mungu hakumpa maneno hasa ya kusema. Wala yule malaika hakuuongoza mkono wa nabii katika maneno halisi ya kuandika. Kutoka katika akili zilizotiwa nuru kwa njozi, nabii alisema ama kuandika maneno ambayo yangeweza kupeleka nuru na mafimdisho kwa makutano wake wakiwa wanausoma ujumbe huo au kuusikia ukisemwa. KN 15.2

Pengine tutauliza, jinsi gani akili za nabii zilitiwa nuru-alipataje habari na maagizo ambayo alipaswa kuyatoa kwa watu? Kama ipasavyo na kanuni moja iwezayo kuwekwa kwa ajili ya kutolewa kwa njozi hizi, Kadhalika ndivyo ipasavyo na kanuni iwezayo kuwekwa kuitawala njia ambayo kwayo nabii alipokea ujumbe kwa kuongozwa na Roho wa Mungu. Lakini, kwa vyo vyote lilikuwa jambo lililo dhahiri ambalo haliondoki akilini mwa nabii. Kadhalika kama mambo tuyaonayo na yanayotupata maishani yanavyokazwa sana akilini mwetu kuliko yale tunayoyasikia tu, ndivyo maono haya kwa manabii, mahali ambapo walielekea kushuhudia kwa macho mambo yaliyobainika, yalivyotia mkazo wa daima akilini mwao. KN 15.3

Katika sura iliyopita, masimulizi ya njozi ya Vita Kuu aliyatumia maneno yake akielezea jinsi habari za mambo ya historia yalivyomjia. Wakati mwingine akieleza jinsi nuru ilivyomzukia akiwa katika njozi, alisema, “Usikivu wangu mara nyingi ulielekezwa kwenye mambo yaliyobainika duniani. Wakati mwingine napelekwa mbele zaidi katika wakati ujao na kuonyeshwa mambo ambayo hayana budi kuwa. Kisha tena naonyeshwa mambo kama yalivyotukia zamani.” KN 15.4

Kwa maneno haya inadhihirika kuwa Ellen G. White aliyaona mambo haya yakifanyika, akionekana kama shahidi aliyeyaona kwa macho. Yalitendwa mara ya pili mbele yake katika njozi, hivyo yalikazwa sana akilini mwake. KN 15.5

Wakati mwingine alijiona kana kwamba alikuwa akiyashiriki mambo aliyoonyeshwa, na ya kwamba aligusa, aliona, akasikia na kutii, hali alikuwa hatendi hivyo kwa kweli, lakini mambo haya yalikazwa akilini mwake kwa namna asivyoweza kuyasahau. Ndivyo ilivyokuwa katika njozi ya kwanza iliyotolewa katika kurasa 34. KN 15.6

Wakati mwingine akiwa katika njozi, Ellen White alionekana kana kwamba alikuwapo penye mkutano au nyumbani au shuleni mbali. Kujiona kama kweli alikuwa penye mkutano wa namna hii kulizidi hata aliweza kusimulia kwa maneno mengi matendo na maneno yaliyosemwa na watu wengi mbalimbali. Siku moja akiwa katika njozi, Ellen White alijiona kwamba alikuwa amechukuliwa safarini kwenda kwenye hospitali zetu, akizuru vyumba kama ilivyokuwa kawaida, akiona kila kitu kilichokuwa kinatendeka. Juu ya jambo hili akaandika: KN 16.1

“Mazungumzo yasiyo na maana, maneno ya mzaha, kucheka ovyo, kulisikika kwa uchungu sikioni... Nilishangazwa kuona moyo wa husuda, na kusikia maneno ya wivu, mazungumzo ya kijinga, yaliyopotoka, ambayo yaliwafanya malaika za Mungu kutahayari.” KN 16.2

Kisha hali zingine za kupendeza za hospitali hiyo hiyo zikafunuliwa. Alipelekwa penye nyumba “mlimotoka sauti ya sala. Sauti hii ilikuwa ya kufurahisha kama nini!” Ujumbe wa mafundisho uliandikwa kutokana na matembezi haya kwenye chuo hiki na juu ya maneno ya yule malaika aliyeonekana kana kwamba alimwongoza katika idara na vyumba mbalimbali. KN 16.3

Mara nyingi Ellen White alipewa nuru kwa njia ya maono kwa mfano halisi. Maono ya jinsi hii yameelezwa dhahiri katika mafungu manne ya maneno yafuatayo, kutoka kwenye ujumbe uliotumwa kwa mtenda kazi mkubwa aliyeonekana yuko hatarini. KN 16.4

“Wakati mwingine nilionyeshwa nikikuona katika hali kama ya jemadari, aliyepanda farasi, na kuchukua bendera. Mtu mmoja akaja na kukunyang’anya mkononi mwako bendera hiyo yenye maneno haya “Amri za Mungu na imani ya Yesu,’ nayo ilikanyagwa mavumbini. Nikakuona umezungukwa na watu waliokuungamanisha na walimwengu.” KN 16.5

Pia palikuwako na nyakati ambapo maono mawili mbalimbali yalionyeshwa kwa Ellen White-moja likieleza jambo ambalo lingetukia kama mipango fulani au sheria fulani zikifuatwa, na katikalingine matokeo ya baadaye ya mipango au sheria zingine. Mfano mzuri wa jambo hili waweza kupatikana kwa habari za kuwekwa kiwanda cha Vyakula vya Afya cha Loma Linda upande wa magharibi ya Marekani. Meneja na wanachama wake walikuwa wakipanga kujenga jumba kubwa karibu sana na jengo kubwa la hospitali. Wakati mipango ilipokuwa ikiendelea, Ellen White nyumbani mwake maili mamia mbali, siku moja usiku akapewa njozi mbili. Juu ya njozi ya kwanza asema: KN 16.6

“Nilionyeshwa jengo kubwa mahali ambapo vyakula vingi vilitengenezwa. Palikuwa na majengo mengine madogo karibu na mahali pa kuokea mikate. Nikisimama karibu, nilisikia sauti za mashindano juu ya kazi hiyo iliyokuwa ikitendeka. Hapakuwa na masikilizano miongoni mwa watenda kazi, na mashaka yalikuwa yameingia.” KN 16.7

Kisha akaona meneja aliyesumbuka akijaribu kujadiliana na watenda kazi kuleta maelewano. Akaona wagonjwa waliosikia mashindano haya, na ambao “walisema maneno ya kusikitisha kwamba kiwanda cha chakula kingejengwa juu ya udongo huu mzuri,” karibu sana na hospitali. “Kisha akatokea Mmoja na kusema: Haya yote yamefanywa yatukie mbele yako ili yawe fundisho, kusudi upate kuona matokeo ya kutimiza mipango fulani.” KN 17.1

Kisha mambo yakabadilika naye akaona Kiwanda cha Vyakula “mbali na majengo ya hospitali, kando ya barabara inayoelekea reli.” Hapo kazi hii iliendeshwa kwa njia ya kujidhili na kupatana na mpango wa Mungu. Katika muda wa saa chache za njozi hii, Ellen White akawa anawaandikia watenda kazi wa Loma Linda, na hili likakata shauri juu ya mahali pa kujengwa Kiwanda cha Vyakula. Kama mpango wao kwanza ungalitimizwa tungeona fadhaa baadaye kuwa na jumba kubwa la biashara karibu na hospitali hii. KN 17.2

Hivyo yaweza kuonekana kuwa kwa njia nyingi mbalimbali mjumbe wa Mungu alipokea habari na mafundisho kwa njia ya njozi mchana au usiku. Imekuwa kutoka akili zilizotiwa nuru kwamba nabii huyu alisema au kuandika, akipeleka ujumbe wa mafundisho na habari kwa watu. Katika kufanya neno hili Ellen White alisaidiwa na Roho wa Bwana, lakini aliachwa kuchagua maneno ambayo kwayo aweza kuupeleka ujumbe huu. Katika miaka ya mwanzoni mwa kazi yake aliandika katika gazeti la Kanisa letu: KN 17.3

“Ijapokuwa nategemea msaada wa Roho wa Mungu katika kuandika maono yangu kama nilivyo katika kuyapokea, lakini, maneno ninayotumia katika kuelezea mambo mliyoyaona ni maneno yangu mwenyewe, isipokuwa yakiwa yale niliyoambiwa na malaika ambayo siku zote nayatia katika alama za kunukuu.” 

Maisha na Kazi ya Ellen E.G. White

Ellen G. Harmon na dada yake pacha walizaliwa Novemba 26, 1827, Gorham, Maine, mashariki ya kaskazini mwa Marekani (United States). Alipokuwa na umri wa miaka tisa, Ellen alipatwa na ajali ambayo jiwe lililotupwa na mwanafunzi mwenzake mzembe lilimpiga. Jeraha hili la usoni lilikuwa karibu kumwua. nalo lilimtia uahaifu mwilini hata hakuweza kuendelea na masomo. KN 17.5

Alipokuwa na umri wa miaka kumi na mmoja alimpa Mungu moyo wake na si muda mrefu baada ya hapo akabatizwa kwa kuzamishwa majini baharini na akapokewa kama mshiriki wa Kanisa la Methodist. Pamoja na watu wengine wa jamaa yake, Ellen alihudhuria mikutano ya Kiadventista Portland, Maine, naye akayaamini mafundisho juu ya kukaribia kuja kwa Kristo mara ya pili, kulikoonyeshwa na William Miller na wenzake, na kwa matumaini mengi akatazamia marejeo ya Mwokozi. KN 17.6

Siku moja asubuhi Desemba, 1844, alipokuwa akisali pamoja na wanawake wengine wanne, uwezo wa Mungu ulimsnukia. Kwanza alihamishwa kimawazo kutoka duniani; kisha katika ufunuo wa mfano aliona safari za Waadventista kwenda kwenye mii wa Mungu, na ijara ya wale waliokuwa waaminifu. Kwa hofu na kutetemeka msichana huyu mwenye umri wa miaka kumi na saba alisimulia neno hili na njozi za baadaye kwa waumini wenzake wa Portland. Kisha kadiri alivyopata nafasi, akahubiri njozi hii kwa makundi ya Waadventista wa Maine na katika nchi jirani. KN 18.1

Agosti, 1846, Ellen Harmon akaoana na James White, mhubiri kijana Mwadventista. Katika miaka yote thelathini na mitano iliyofuata maisha ya Ellen White yaliungana kabisa na yale ya mumewe katika kazi ya Injili kwa junudi, mpaka kifo cha mumewe, Agosti 6, 1881. Walisafiri mahah pengi katika Marekani, wakihubiri na kuandika, wakipanda mbegu na kujenga, wakipanga mambo na kuamuru. KN 18.2

Muda na jaribio vimethibitisha jinsi misingi ambayo Mchungaji na Ellen White na wenzao waliiweka ilivyo mipana na imara, na jinsi walivyojenga vizuri kwa busara. Waliongoza miongoni mwa Waadventista wenye kuishika Sabato na kuanzisha kazi ya kuchapisha vitabu na magazeti mnamo mwaka 1849 na 1850, na kukuza utaratibu wa Kanisa kwa mipango mizuri ya habari za fedha katika miaka mingine baada ya 1850. Jambo hili lilikamilishwa na kupangwa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Waadventista wa Sabato’ mnamo mwaka 1863. Miaka iliyofuata mwaka huo ukawa ni mwanzo wa kazi yetu ya uganga, na, kazi yetu kuu ya elimu ya madhehebu kuanzishwa mara baada ya mwaka wa 1870. Mpango wa kufanya mikutano ya makambi ya kila mwaka ulikuzwa mnamo mwaka 1868, na mwaka 1874 Waadventista Wasabato walituma wamishenari wao wa kwanza. KN 18.3

Maendeleo haya yote yaliongozwa na maonyo mengi yaliyosemwa na kuandikwa ambayo Mungu aliwapa hawa kwa njia ya Ellen G. White. KN 18.4

Habari nyingi za mwanzoni ziliandikwa kwa njia ya barua za mtu mwenyewe, au kwa njia ya habari katika Present Truth (Ukweli wa Leo), gazeti letu la kwanza kuchapishwa. Mpaka mwaka 1851 ndipo Ellen White alipotoa kitabu chake cha kwanza cha kurasa 64, kilichoitwa A Sketch of the Christian Experience and View of Ellen G. White. … KN 18.5

Kuanzia mwaka 1855 aina kadha wa kadha za magazeti zilichapishwa, kila moja likiwa na jina la Testimony of the Church (Ushuhuda wa Kanisa). Haya yalitoa ujumbe wa kufaa wa mafundisho na maonyo ambayo mara kwa mara Mungu alichagua kuyapeleka kuwabariki, kuwakaripia, na kuwaongoza watu wake. Ili kuitimiza haja ya daima ya mafundisho maonyo haya, yalichapishwa mara ya pili mnamo mwaka 1885 katika vitabu vinne, na pamoja na ongezeko la vijitabu vingine, ambavyo vilichapishwa kati ya mwaka 1889-1909, na kufanya jumla ya vitabu tisa vya Testimonies for the Church (Shuhuda kwa Kanisa). KN 18.6

Bwana na Bibi White walizaa watoto wanne. Mtoto mkubwa wa kiume, Henry, aliishi akawa na umri wa miaka kumi na sita; mvulana mdogo kuliko wote, Herbert, alifariki akiwa na umri wa miezi mitatu. Watoto wa kiume wawili wa katikati, Edson na William, wakaishi hata wakawa watu wazima na kila mmoja akafanya kwa bidii kazi ya Kanisa la Waadventista Wasabato. KN 19.1

Kwa kuitikia mwito wa Halmashauri Kuu ya Kanisa, Ellen White alikwenda Ulaya wakati wa kiangazi mwaka 1885. Huko alitumia miaka miwili akiwatia nguvu na kuanzisha kazi mpya kwenye Bara hilo. Akiishi Basle, Switzerland, alisafiri mahali pengine kusini, katikati na kaskazini ya Ulaya, akihudhuria mikutano mikubwa ya Kanisa hili na kukutana na waumini katika mikutano yao. KN 19.2

Baada ya miaka minne alipokwisha kurejea Marekani Ellen White akiwa mwenye umri wa miaka 63, kwa kuitikia mwito wa Halmashauri kuu alisafiri baharini kwenda Australia. Kule alikaa kwa muda wa miaka tisa, akisaidia kuanzisha na kukuza kazi, hasa upande wa kazi ya elimu na utabibu. Ellen White alirejea mwaka 1900 kufanya makao yake upande wa magharibi mwa Marekani, katika St. Helena, California, Mahali alipokaa mpaka kufa kwake mwaka 1915. KN 19.3

Katika kazi ya Ellen White ya muda mrefu wa miaka 60 Marekani na miaka 10 katika nchi za kigeni, alipewa njozi karibu 2,0 ambazo kwa bidii zake nyingi katika kuwashauri watu mmoja mmoja, makanisa, mikutano ya watu kwa jumla, na hata wakati wa kikao kikuu cha Halmashauri kuu aliongoza maendeleo ya kanisa hili. Kazi ngumu ya kuwapa wote wahusikanao ujumbe aliopewa na Mungu hakuchoka kuifanya. KN 19.4

Maandishi yake yalikuwa zaidi ya kurasa mia moja elfu, Ujumbe aliouandika uliwafikia watu kwa kuwapelekea habari mwenyewe, na kwa makala za juma kwa juma katika magazeti ya madhehebu yetu na katika vitabu vyake vingi. Mafundisho hayo yalihusiana sana na historia ya Biblia, maisha ya Kikristo ya kila siku, afya, elimu, uinjilisti na mambo mengine makubwa ya kufaa. Vitabu kadha wa kadha miongoni mwa vitabu vyake arobaini na sita vimechapishwa katika lugha kuu ulimwenguni na nakala milioni nyingi zimeuzwa. KN 19.5

Alipokuwa mwenye umri wa miaka 81 Ellen White alivuka bara la (Marekani) kwa mara yake ya mwisho kuhudhuria kikao cha Halmashauri Kuu cha mwaka 1909. Miaka 6 ya maisha yake iliyokuwa imesalia aliitumia kumaliza kazi yake ya vitabu. Karibu na mwisho wa maisha yake Ellen White aliandika maneno haya: “Kama maisha yangu yakiachwa yazidi kuendelea, vema, ama sivyo, maandishi yangu yatasema daima, na kazi yake itasonga mbele mpaka siku ya mwisho.” KN 19.6

Kwa moyo usio na hofu kwa matumaini kamili kwa Mkombozi wake, akafa nyumbani kwake Julai 16, 1915, na akazikwa kando ya mumewe na watoto katika Oak Hill Cemetery, Battle Creek, Michigan. KN 20.1

Ellen White alithaminiwa na kuheshimiwa na watenda kazi wenzake, Kanisa, na watu wa nyumbani mwake, kama mama mcha Mungu na mtu mwaminifu, mkarimu, mtenda kazi hodari wa kidini. Kamwe hakushika kazi ya afisa wa Kanisa. Ilijulikana na Kanisa na yeye mwenyewe kwamba alikuwa “mjumbe” mwenye ujumbe kutoka kwa Mungu kwa watu wa Mungu. Kamwe hakuwataka watu kumtazama, wala hakutumia kipawa chake kujinufaisha kwa habari za fedha au ili kupendwa na wengi. Maisha yake na vyote alivyokuwa navyo vilitolewa wakfu kwa kazi ya Mungu. KN 20.2

Wakati wa kufa kwake mchapishaji wa gazeti lililopendwa sana na watu wengi, la kila juma, The Independent, katika toleo la Agosti 23, 1915, aliandika maneno yake yanayoelezea juu ya maisha ya Ellen White kwa kusema haya: “Alikuwa mwaminifu kabisa katika imani yake katika mafunuo yake. Maisha yake yalistahili. Hakuonyesha kiburi cho chote cha mambo ya kiroho, naye hakutafuta faida inayopatikana kwa njia mbaya. Aliishi na kutenda kazi ya kustahili nabii mwanamke.” KN 20.3

Miaka kadha wa kadha kabla ya kufa kwake, Ellen White alibuni Bodi ya Wadhamini, watu mashuhuri wa Kanisa alimoacha maandishi yake na agizo kuwa ni iuu yao kuyatunza na kuendelea kuyachapisha . Ikiwa na ofisi yake kwenye makao makuu ya Kanisa la Waadventista Wasabato Marekani, Bodi hii hukuza na kuendelea kutoa vitabu vya Ellen G. White katika lugha ya Kiingereza na kusaidia kutolewa ama vitabu vizima ama kwa sehemu katika lugha zingine. Pia wametoa vitabu kadha wa kadha kwa kutumia nakala za magazeti na maandishi yake. Kitabu hiki kimetolewa kwa idhini ya Bodi hiyo.

 

Ellen G. White Kama Alivyojulikana Kwa Wengine

Wakiwa wamepata habari za maisha ya ajabu ya Ellen White kuwa ni mjumbe wa Mungu, wengine wameuliza, alikuwa mtu wa namna gani? Je, alikuwa na shida tulizo nazo? Alikuwa tajiri, au alikuwa maskini? Alipata kucheka? KN 20.5

Ellen White alikuwa mama mwenye kufikiri, Alikuwa Bibi mwangalifu, mara nyingi aliwakaribisha watu wetu nyumbani mwake. Alikuwa jirani mwema. Alikuwa mwanamke mwenye nia thabiti, mwenye mwenendo mzuri, na mpole wa tabia na sauti. Hakuwa na natasi maishani mwake kuonyesha uso wa huzuni, kuwa na uso wa hasira, ama dini isiyo ya furaha. Mtu aliweza kujiona kuwa na raha kamili mbele zake. Pengine njia bora ya kumfanamu Ellen White ilikuwa kufika nyumbani kwake mwaka 1859, mwaka wa kwanza alipoanza kuandika kitabu cha kumbukumbu za kila siku. KN 21.1

Twaona kuwa watu wa nyumba ya Bwana na Ellen White waliishi viungani mwa mji wa Battle Creek, katika nyumba ndogo, kwa sehemu kubwa akitoa nafasi kwa bustani, miti mingi ya matunda, ng’ombe, na kuku, na mahali pa watoto wa kiume kufanyia kazi na michezo. Ellen White wakati huu alikuwa na umri wa miaka thelathini na mmoja. Mchungaji White alikuwa mwenye miaka thelathini na sita. Wakati huo palikuwa na watoto wa kiume watatu nyumbani, umri wao, miaka minne, tisa, na kumi na miwili. KN 21.2

Tungetazamia pia kuona msichana Mkristo mzuri katika nyumba hiyo aliyeajinwa kazi za nyumbani, kwa mama White, maana mara nyingi alikuwa safarini na mara kwa mara alikuwa akishughulika na mazungumzo yake na maandishi. Lakini, tunamuona Ellen White akifanya kazi za nyumbani, kupika, kusafisha, kufua na kushona. Siku zingine alienda kwenye nyumba ya uchapaji ambapo alipata mahali patulivu kwa ajili ya kuandika. Siku zingine tunamwona bustanim, akipanda maua na mboga za majani na wakati mwingine akibadilishana miche ya maua na majirani. Alikusudia kufanya nyumbani kuwa mahali pa kupendeza kwa watu wa nyumba yake kama alivyoweza, ili watoto wapahesabu nyumbani kuwa mahali pa kutamanika kukaa. KN 21.3

Ellen White alikuwa mnunuzi mwangalifu, na majirani Waadventista walifurahi walipoweza kwenda pamoja naye kununua vitu madukani, kwa sababu alijua ubora wa vitu. Mama yao alikuwa mwanamke mwenye busara na aliwafundisha binti zake mafundisho mengi ya thamani. Aliona kuwa vitu visivyotengenezwa vizuri mwisho vilikuwa vya gharama kubwa zaidi ya bidhaa bora. KN 21.4

Sabato ilifanywa siku ya kupendeza kuliko siku zingine za juma kwa watoto. Naam, watu wa nyumbani humu walihudhuria ibada kanisani na ikiwa Mchangaji na Mama White hawahudumu basi familia yote walipenda kuketi pamoja wakati wa ibada. Chakulani walipenda kuchagua vyombo visivyotumika siku zingine, na tena kama hali ya hewa ikiwa nzuri, Ellen White alipenda kutembea na watoto wake mwituni, au kando ya mto, nao waliweza kutazama uzuri wa viumbe na kujifunza kazi za Mungu na uumbaji. Kama siku hiyo ikiwa na mvua au baridi, aliwakusanya watoto jikoni ambapo alipenda kuwasomea, mara nyingi alisoma habari alizokusanya huko na huko akifanya safari zake. Baadhi ya hadithi hizi zilichapishwa baadaye ili wazazi wengine wazipate na kuwasomea watoto wao. KN 21.5

Ellen White hakuwa mzima wa afya sana wakati huu, na mara nyingi aliona kizunguzungu wakati wa mchana, lakini hili halikumzuia asiendelee na kazi yake nyumbani na kazi ya Mungu pia. Miaka michache baadaye, mwake 1863, akapewa njozi juu ya afya na utunzaji wa wagonjwa. Alionyeshwa katika njozi mavazi yafaayo kuvaa, chakula kifaacho kula, mazoezi ya mwili yalivyo muhimu na kupumzika, pamoja na ukubwa wa kumwamini Mungu kunavyotakiwa ili kuwa na mwili wenye nguvu na afya. KN 22.1

Nuru iliyotoka kwa Mungu juu ya mlo na madhara ya nyama ilimshtua sana Ellen White mwenyewe kwa maana alidham ya kuwa nyama ilikuwa murua kwa afya na nguvu. Kwa kutumia nuru ya njozi hii kuangaza akili zake alimwamuru yule msichana aliyemsaidia kutayarisha chakula kwa watu wa nyumba yake kuweka mezani vyakula safi tu, vyakula vyepesi, ambavyo vilifanywa kwa nafaka, mboga za majani, mbegu jamii ya njugu, maziwa, mafuta ya juu ya maziwa (ya mtindi), na mayai. Palikuwa na matunda tele. KN 22.2

Watu wa nyumbani walipofika mezani palikuwa na vyakula vingi vizuri, lakini hapakuwako na nyama. Ellen White alikuwa na uchu wa nyama, wala si wa vyakula vingine, hivyo akakata shauri kuondoka mezani mpaka atakapoweza kurudi na kupendezwa na chakula chepesi tu. Katika mlo mwingine mambo yakawa hali ile ile, lakini chakula chepesi hakikumvutia. Kisha tena wakafika mezani. Palikuwa na vyakula vyepesi, kama alivyoonyeshwa katika njozi kuwa ni jambo lililo bora kwa afya na nguvu na kukua. Lakini alitaka kula nyama, ambayo ameizoea. Walakini, sasa alikwisha kujua kuwa nyama haikuwa chakula bora. Anasema alishika mikono yake juu ya tumbo lake, na kuliambia maneno haya, “Waweza kungoja mpaka hapo uwezapo kula mkate.” KN 22.3

Haukuwa muda mrefu Ellen G. White akaweza kupendezwa na vyakula vyepesi, na kwa kubadili ulaji wake, afya yake ikawa bora mara, na siku zote za baadaye maisnani mwake akafaidi afya bora. Hivyo yaonekana kuwa alikuwa na shida zile zile tulizo nazo sisi sote. Ilimbidi kujipatia ushindi juu ya tamaa ya chakula katika maisha yake mwenyewe sawa na sisi sote tupasavyo kupata ushindi. Kutokutumia vitu vinavyodhuru afya (health reform) Kumekuwa mbaraka mkubwa kwa watu wa nyumba ya Bwa na Bibi White, kama kulivyo kwa maelfu ya Waadventista ulimwenguni mwote. KN 22.4

Baada ya njozi hii juu ya kutokutumia vitu vyenye kudhuru afya, na mageuzi katika nyumba ya Bwana na Bibi White ya njia nyepesi za kuwatibu wagonjwa, Mchungaji na Mama White waliitwa mara kwa mara na majirani wakati wa ugonjwa kusaidia kutoa matibabu, na Mungu alizibariki sana jitihadi zao. Nyakati zingine wagonjwa waliletwa nyumbani kwao na kutunzwa kwa uangalifu mwingi mpaka wakapona kabisa. KN 22.5

Ellen White alifurahia sana vipindi vya kupumzika na kuburudika, ama milimani, ama ziwani, ama kando kando ya bahari. Katika umri wa kati, wakati alipokuwa akikaa karibu na Pacific Press, nyumba yetu ya uchapaji wa vitabu magharibi mwa Marekani, katika nyumba hii ya uchapaji ilikusudiwa kwamba siku moja itumiwe katika kupumzika na kujiburudisha. Ellen White na watu wa nyumbani mwake na watenda kazi wa oflsini wakaulizwa kujiunga na watu wa kazi ya uchapaji wa vitabu, naye akaukubali mwaliko huu upesi. Mumewe alikuwa pande za mashariki katika kazi ya Kanisa. Tumepata habari hizi katika barua aliyomwandikia juu ya jambo hili. KN 23.1

Baada ya kufaidi chakula kizuri cha adhuhuri cha kufaa kwa afya ufukoni, kundi zima lilikwenda kupanda mashua katika ghuba ndogo ya San Francisco. Kapteni wa mashua hii alikuwa mshiriki wa Kanisa na ilikuwa alasin ya kupendeza. Kisha ikakusudiwa kwamba waende kwenye bahan pana. Katika kulisimulia jambo hili Ellen G. White ameandika: KN 23.2

“Mawimbi yalikuwa makubwa, nasi tulikuwa tukirushwa lakini sikuwa na maneno ya kumwambia mtu awaye yote. Lilikuwa jambo zuri! Manyunyu yalitudondokea. Upepo ulikuwa wa nguvu nje ya Golden Gate, nami kamwe nilikuwa sijawahi kufaidi jambo zuri hivi maishani mwangu!” KN 23.3

Kisha aliyatazama macho mapevu ya Kapteni huyu, na wepesi wa mabaharia kuzitii amri zake, naye akafikiri: KN 23.4

“Mungu anazishikilia pepo mikono mwake. Anatawala maji. Nasi tu vitu vidogo tu juu ya maji mengi, yenye kina ya Pasifiki: Lakini malaika wa mbinguni hutumwa kuilinda mashua hii ndogo ikishindana na haya mawimbi. Ah, kazi za ajabu za Mungu! Kupita kabisa ufahamu wetu! Akitazama mara moja huona mbinguni juu sana na katikati ya bahari pia!” KN 23.5

Ellen White alikuwa anao moyo mchangamfu. Siku moja aliuliza, “Je, unaniona kuwa mwenye huzum, mwenye kukata tamaa, mwenye kunung’unika? Ninayo imani yenye kulikataza jambo hili. Kutokufahamu vema tabia kamili ya Kristo na huduma ya Kikristo, ndiko kunakoleta miisho hii Kazi ya hiari ya moyo kwa Yesu huleta dini ya kupendeza. Wale wanaomwandama Kristo kwa karibu sana hawajahuzunika.” KN 23.6

Tena wakati mwingine aliandika: “Wakati mwingine watu wamependa kufikiri kuwa uchangamfu haupatani na adabu ya tabia ya Knsto; lakini hili ni kosa. Mbinguni ni furaha tupu.” Naye akafahamu kuwa kama ukionyesha uso wa furaha, utaonyeshwa pia uso wa furaha; kama ukisema maneno ya upole utarudishiwa pia maneno ya upole. KN 23.7

Ingawa mambo yalikuwa hivyo, kuna wakati alipoumia sana. Wakati mmoja wa jinsi hii ulikuwa mara baada ya kwenda Australia kusaidia kazi pande zile. Alikuwa mgonjwa sana karibu mwaka mmoja, akaumia sana. Alikuwa hawezi kutoka kitandani mwake wakati huo na hakuweza kulala usinginzi ila saa chache tu usiku. Juu ya jambo hili akamwandikia barua rafiki yake akisema: KN 24.1

“Nilipojiona katika hali ya kutojimudu, nilisikitika sana kuwa nilivuka bahari kubwa. Mbona nisiwe Marekani? Mara kwa mara nalificha uso wangu katika matandiko ya kitanda na kulia sana. Lakini sikupendelea kutoa machozi hivi. Nikasema kimoyo moyo, Ellen G. White, unafikiri nini? “Nikasema, ‘Ndiyo’. “Basi, kwa nini waona kuwa umetupwa na kukatishwa tamaa? Je, hii si kazi ya adui? Naamini ni kazi yake!’ “Nikayafuta machozi upesi nilivyoweza na kusema, ‘Yatosha. Sitaangalia upande wa giza. Niishi au nife, naikabidhi roho yangu kwake Yeye aliyenifilia. KN 24.2

“Kisha nikaamini kuwa Mungu atafanya yote kuwa sawa, na katika hii miezi minane ya kutokujimudu sikuwa na majonzi, wala mashaka. Sasa nalihesabu jambo hili kama sehemu ya kusudi kuu la Mungu kwa ajili ya faida ya watu wake hapa katika nchi hii, na kwa ajili ya wale walio Marekani na kwa raida yangu. Siwezi kueleza sababu wala jinsi mambo yalivyokuwa, lakini naliamini. Nami nafurahi katika mateso yangu. Naweza kumtumainia Baba yangu alive mbinguni. Sitalitilia shaka pendo lake.” KN 24.3

Ellen White akikaa nyumbani kwake California katika miaka kumi na mitano ya mwisho wa maisha yake, alikuwa akizeeka; lakini alipenda kazi ya shamba dogo, na kazi ya kuwaweka katika hali njema watu wa jamaa waliomsaidia kazini mwake. Tunamwona akishughulika na maandishi yake, mara nyingi akianza mara baada ya usiku wa manane, kwa kuwa alienda kulala mapema. Kama hali ya hewa ikiwa nzuri, alipenda, akipata nafasi kazini mwake, kwenda kutembea kwa gari mashambani, akisimama kuzungumza na mama aliyeweza kumwona shambani au katika ukumbi wa nyumba aliyopita. Wakati mwingine aliona wenye haja ya chakula na mavazi, naye alipenda kwenda nyumbani na kuwapatia vitu kadha wa kadha kutoka katika vifaa vyake nyumbani. Miaka mingi baada ya kufa kwake alikumbukwa na majirani wa bondeni alipokaa, kama bibi kizee aliyesimulia vizuri sana habari zake Yesu. KN 24.4

Alipokufa alikuwa anavyo vitu vingi kidogo vilivyotosha kumweka vizuri maishani. Hakuwauliza wengine kumhesabu kama kielelezo chema bali alikuwa mwenzetu miongoni mwetu, Waadventista Wasabato, mwenye kuyatumainia matendo mema ya Bwana wake aliyefufuka katika wafu na akajaribu kwa uaminifu kuitenda kazi aliyokabidhiwa na Bwana. Hivyo akiwa na matumaini moyoni mwake alifikia mwisho wa maisha yake, mnyofu katika maisha yake ya Kikristo. KN 24.5

Ujumbe Ambao Uliyaongoa Maisha

Mwinjilisti mmoja alifanya mikutano Bushnell, Michigan; lakini, mara baada ya ubatizo, akaondoka akawaacha watu bila kuwaweka imara waumini katika ujumbe huu. Pole pole watu wakakata tamaa na baadhi yao wakaanza tena mazoea yao mabaya. Mwishowe kanisa likawa dogo sana hata washiriki 10 au 12 waliosalia wakaamua kwamba haikuwa na maana kuendelea. Mara walipokwisha kutawanyika kutoka kwa mkutano walioudhania kuwa wa mwisho, wakapata barua kutoka posta na miongoni mwa barua ilikuwapo Review and Herald. Katika sehemu ya utaratibu wa mambo ya safari palikuwa na tangazo kuwa Mchungaji na Bibi White hawana budi kufika Bushnell kwa mikutano tarehe 20, Julai 1867. Tarehe hiyo ilikuwa baada ya juma moja tu. Watoto wakatumwa kuwaita watu warudi ambao walikuwa njiani kwenda zao nyumbani. Ikaamuriwa kwamba mtu mmoja anapaswa kutayarisha mahali penye miti na ya kuwa wote wamepaswa kuwaalika majirani zao, hasa washiriki waliorudi nyuma na kuiacha imani. KN 25.1

Siku ya Sabato asubuhi, Julai 20, Mchungaji na Bibi White wakafika mahali hapa penye miti walimokusanyika watu sitini. Mchungaji White akahutubu asubuhi. Alasiri Ellen White akasimama kusema, lakini alipokwisha kusoma fungu lake, akaonekana anafadhaishwa na tatizo. Bila maneno ya kueleza zaidi akaifunga Biblia yake na kuanza kuzungumza nao kwa njia ya pekee sana. KN 25.2

“Nikisimama mbele yenu alasiri hii, nazitazama nyuso za wale nilioonyeshwa katika njozi miaka miwili iliyopita. Nikiziangalia nyuso zenu mambo yenu nayakumbuka vizun, nami nina ujumbe kwenu kutoka kwa Mungu. KN 25.3

“Kuna ndugu huyu karibu na huu msunobari. Siwezi kulitaja jina lako maana sikujulishwa, lakini uso wako naujua, na mambo ya maisha yako ya dhaniri mbele yangu.” Kisha akasema na ndugu huyu juu ya kuacha dini kwake na kuyarudia mazoea mabaya. Akamtia nguvu kurudi na kutembea pamoja na watu wa Mungu. Kisha akamgeukia mwanamke mmoja katika sehemu nyingine ya makutano, akasema, “Dada huyu mwenye kuketi karibu na Bibi Myanard wa kanisa la Greenville-Siwezi kulitaja jina lako kwa sababu sikuambiwa ni jina gani-lakini, miaka miwili iliyopita nalionyeshwa mashauri juu yako katika njozi, na mambo ya maisha yako nayajua.” Ndipo Mama White akamtia moyo mwanamke nuyu. KN 25.4

“Tena kuna ndugu kule nyuma karibu na mti Ulaya (Muoki). Siwezi kukutaja jina lako pia, kwa kuwa sijakutana nawe bado, lakini mashauri yako ni dhahiri kwangu.” Kisha akasema habari za ndugu huyu, akimfunulia kila mmoja aliye kuwako pale mawazo yake ya moyoni na kumwambia mambo ya maisha yake. KN 25.5

Na kutoka kwa mtu mmoja hata kwa mwingine aliwageukia makutano, akiwaambia mambo aliyoonyeshwa miaka miwili iliyokuwa umepita katika njozi. Ellen White alipokuwa amemaliza mahubiri yake, ambayo yalihusisha maneno ya kukaripia na hata maneno ya kutia moyo, akaketi. Mmoja miongoni mwa makutano akasimama, akasema, “Nataka kujua kama mambo ambayo Ellen V/hite ametuambia alasiri hii ni kweli. Mchungaji na Mama White hawayajui hata majina ya wengi wetu, lakini amefika hapa alasiri hii na kutwambia kuwa miaka miwili iliyopita alipewa njozi ambayo kwayo alionyeshwa mashauri yetu, tena akasema nasi kila mmoja mambo hayo moja moja, akimfunulia kila mmoja aliyeko hapa mwenendo wetu na mawazo yetu ya moyoni. Mambo haya ndivyo yalivyo kwa kweli kwa kila mmoja? Au Ellen White amekosea? Nataka kujua.” KN 26.1

Watu mmoja mmoja wakasimama. Yule mtu aliyekuwa karibu na msunobari akasimama, na kusema Ellen White alikuwa ameeleza mashauri yake vizuri zaidi kuliko yeye mwenyewe angalivyoweza kuyaeleza. Akaungama upotovu wake. Akaonyesha nia yake karibu na kuenenda na watu wa Mungu. Mwanamke aliyeketi karibu na Bibi Maynard kutoka kanisa la Greenville pia alitoa ushuhuda. Akasema kuwa Ellen White amesimulia mambo ya maisha yake vizuri kuliko yeye mwenyewe angalivyoweza kuyasimulia. Yule mwanamume karibu na mti Ulaya, ambaye Ellen White alimkaripia na kumwambia maneno ya kumtia moyo akasema kwamba Ellen White alikuwa ameyaeleza mashauri yake vizuri kuliko yeye mwenyewe angalivyoweza kuyaeleza. Maungamo yakafanywa Dhambi zikaachwa. Roho wa Mungu akaingia, na pakawa na uamsho Bushnell. KN 26.2

Mchungaji na Mama White wakarudi tena Sabato nyingine iliyofuata, na pakafanywa ubatizo, na kanisa la Bushnell likaimarishwa vizuri na likawa na nguvu. KN 26.3

Mungu aliwapenda watu wake wa Bushnell kama awapendavyo wale wote wanaomtazamia. Lile Neno lisemalo “Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu” (Ufu. 3:19), halina budi kuwa neno lililowaingia moyoni baadhi ya wale waliokuwako. Watu walipojiona mioyoni mwao wenyewe kama Bwana alivyowaona, wakafahamu hali yao halisi na kutamani uongofu maishani mwao. Hili ni kusudi halisi la njozi nyingi alizopewa huyu Ellen White. KN 26.4

Mara baada ya kufa kwa Mchungaji White, Mama White akakaa karibu na Healdsburg College. Wasichana kadha wa kadha wakawa wanakaa nyumbani mwake walipokuwa wakihudhuria Chuo. Ilikuwa desturi wakati ule kuvaa wavu mwepesi juu ya nywele ili kuziweka vizuri kwa taratibu mchana kutwa. Siku moja mmoja wa wasichana hawa alipokuwa akipita chumbani mwa Mama White akauona wavu wa nywele uliokuwa umetengenezwa vizuri ambao aliutaka. Akidhani kuwa hautahitajika, akautwaa na kuuweka ndani ya sanduku lake. Baadaye kidogo Mama White alipokuwa akivaa ili atoke, akaukosa wavu wake na ikambidi kwenda bila kuwa nao. Jioni watu wa nyumbani mwake walipokuwa pamoja, Mama White akauliza juu ya wavu wake uliopotea, lakini nakuna hata mmoja aliyeonyesha kuwa anajua ulipo. KN 26.5

Siku moja baadaye Bibi White alipokuwa akipita chumbani mwa wasichana hawa, sauti fulani ikamwambia, “Fungua sanduku lile.” Kwa sababu sanduku hili halikuwa lake, hakupenda kufanya hivyo. Alipoamriwa mara ya pili akaitambua ile sauti kuwa ni ya yule malaika. Alipoinua kifuniko akaona sababu iliyomfanya yule malaika aseme, maana pale palikuwa na ule wavu wake. Watu wa nyumbani mwake walipokutanika tena Mama White akauliza tena juu ya wavu huu, akisema kuwa usingeweza kutoweka wenyewe. Hakuna aliyesema neno hivyo Mama White akaacha shauri hili. KN 27.1

Siku chache baadaye Mama White alipokuwa anapumzika kutoka katika kuandika akapewa njozi fupi sana. Akauona mkono wa msichana ukishusha wavu wa nywele kwenye taa inayotumia mafuta. Wavu huo ulipogusa mwali wa moto ukatoweka ghafula motoni. Huu ukawa ndio mwisho wa njozi hii. KN 27.2

Watu wa nyumbani mwake walipokutanika tena Mama White akakaza shauri lile la kupotea kwa ule wavu wa nywele tena, lakini hata hivyo hapakuwako na ungamo lo lote wala hakuna mtu ye yote aliyeelekea kujua ulipo. Ndipo baadaye kidogo Mama White akamwita kando msichana huyu akamwambia habari za ile sauti, na kile alichoona ndani ya sanduku na akamwambia habari za ile njozi fupi ambayo kwayo aliona wavu wa nywele ukiteketea juu ya taa. Akiwa na habari zote hizi mbele yake, yule msichana akaungama kuwa aliuchukua wavu huu, na kuuchoma moto asije akagundulika. Akakiri kosa lake na kulisawazisha shauri lake na Mama White na Mungu pia. KN 27.3

Pengine tutafikiri kuwa hili ni jambo dogo sana kwa Mungu kulihangaikia-wavu tu wa nywele. Lakini lilikuwa jambo la maana sana kuliko thamani ya kitu chenyewe kilichoibiwa. Hapa alikuwako msichana, mshiriki wa Kanisa la Waadventista Wasabato. Aliyejiona moyoni mwake kuwa yu salama, lakini hakuziona hitilafu katika tabia yake mwenyewe, hakuona moyo wa kujichunguza nafsi, wala si wengine, ambao ulimwongoza kuiba na kudanganya. Sasa alipofahamu jinsi mambo yalivyo na maana-kwamba Mungu angempa njozi mjumbe wake mwenye kazi nyingi hapa duniani kwa ajili ya wavu wa nywele tu-huyu msichana akaanza kufahamu jinsi mambo yalivyo hasa. Jambo hili likawa la kumbadilisha maishani mwake, naye akaishi maisha ya raha, ya Mkristo mnyofu. KN 27.4

Hiyo ndiyo sababu ya Mama White kupewa njozi. Ijapokuwa maneno mengi ya shuhuda yaliyoandikwa na Mama Wnite yalikuwa kwa ajili ya kueleza au kudhihirisha mambo maalumu sana Lakini, yanaonyesha kanuni zinazotimiza haja za Kanisa hili katika kila nchi ulimwenguni. Mama White amedhihirisha kusudi na mahali pa shuhuda hizi kwa maneno haya: KN 28.1

“Shuhuda hizi zilizoandikwa si za kutoa nuru mpya, bali za kuyakaza mioyoni maneno ya kweli yaliyotolewa kwa uongozi wa Roho wa Mungu ambayo yamekwisna kufunuliwa tayari. Wajibu mkubwa kwa Mungu na kwa wanadamu wenzake umpasao mtu umedhihirishwa katika Neno la Mungu; walakini ni wachache wenu tu wenye kuitii nuru iliyotolewa. Hapakutolewa neno la kweli lingine zaidi, bali Mungu kwa njia ya shuhuda hizi ameyarahisisha maneno ya kweli yaliyokwisha kutolewa tayari Shuhuda hizi hazipaswi kupunguza ukuu wa Neno la Mungu, bali kulikuza, na kuivuta mioyo ya watu kwalo, ili wepesi mzuri wa ukweli upate kuwaingia wote moyoni.” KN 28.2

Katika maisha yake yote Mama White alilishika Neno la Mungu mbele ya watu. Kitabu chake cha kwanza kabisa alikifunga kwa wazo hili. Alisema: KN 28.3

“Nakupa shauri, msomaji mpendwa, Neno la Mungu ni kanuni ya imani yako na ibada. Kwa Neno hilo hatuna budi kuhukumiwa. Mungu, katika Neno hilo, ameahidi kutoa njozi “Siku za mwisho”; si kwa ajili ya kanuni mpya ya imani, bali kwa ajili ya faraja ya watu wake, na kutoa makosa ya wale wanaopotoka katika ukweli wa Biblia.” KN 28.4

Njozi Isiyoweza Kusimuliwa

Katika mikutano ya Salamanca, New York, Novemba, 1890, ambapo Ellen White alikuwa akiihutubia mikutano mikubwa ya watu, alidhoofika kabisa, kwa kuwa alishikwa na ugonjwa wa mafua makali alipokuwa safarini kwenda katika mji huo. Baada ya mmojawapo wa mikutano hii akaondoka kwenda chumbani mwake akiwa amekata tamaa na huku yu mgonjwa. Akawa anafikiri kusali mbele za Mungu na kumtolea moyo wake kuomba rehema na afya na nguvu. Akapiga magoti kando ya kiti chake, na kwa maneno yake mwenyewe, akisimulia kilichotukia, anasema: KN 28.5

“Nalikuwa sijatamka neno wakati chumba chote kilipoonekana kana kwamba kimejawa na nuru nyeupe na uchungu wangu na kukata tamaa kuondolewa. Nikajazwa faraja na tumainiamani ya Kristo.” KN 28.6

Kisha akapewa njozi. Baada ya njozi hii hakutaka kulala tena usingizi. Hakutaka kupumzika. Alikuwa ameponywa-alikuwa amepumzishwa. KN 28.7

Asubuhi ilibidi kuamua. Ama aendelee na kwenda mahali pa mikutano ifuatayo, ama hana budi kurejea nyumbani kwake Battle Creek., Mchungaji. A.T. Robinson, aliyekuwa mkuu wa kazi na Mchungaji William White, mwana wa Bibi White wakaitwa chumbani mwake kupata jibu lake. Wakamkuta amevaa nguo, yu mzima. Alikuwa tayari kwenda. Akasimulia jinsi alivyopona. Akahadithia njozi hiyo. Akasema, “nataka kuwaambia jambo lililofunuliwa kwangu usiku huu uliopita. Katika njozi nalielekea kana kwamba niko Battle Creek, na malaika mjumbe akaniambia, “Nifuate” Kisha akasita. Hakuweza kuikumbuka. Akajaribu mara mbili kuisimulia, lakini hakuweza kukumbuka kile alichoonyeshwa. Katika siku za baadaye akaandika kile alichokuwa ameonyeshwa. Kilikuwa mipango iliyofanywa kwa ajili ya gazeti letu la Uhuru wa Dini lililoitwa siku zile The American Sentinel. KN 29.1

“Usiku nilikuwa kwenye mabaraza kadha wa kadha, na hapo nilisikia maneno yaliyorudiwa na watu wenye nguvu kuongoza kwenye matokeo mema kwamba kama The American Sentinel lingeacha kutumia maneno haya ‘Waadventista Wasabato katika safu zake, na lisiseme lo lote juu ya Sabato, watu mashuhuri ulimwenguni wangependelea kulinunua; nalo lingependwa na wengi, na kufanya kazi kubwa zaidi. Hili likahesabiwa kuwa jambo la kupendeza.” KN 29.2

“Nikaona nyuso zao ziking’aa nao wakaanza kuifuata njia hiyo kulifanya gazeti la The Sentinel kuwa la kupendwa na watu wengi. Shauri hili lote lilianzishwa na watu waliotaka sana ukweli uwepo akilini na moyoni.” KN 29.3

Ni dhahiri kwamba aliona kundi la watu likijadiliana juu ya mashauri ya utengenezaji wa gazeti hili. Kikao cha Halmashauri Kuu kilipofunguliwa Machi, 1891, Mama White akaombwa kuzungumza na watenda kazi kila siku asubuhi saa kumi na moja na nusu na kuhutubia kikao cha watu elfu nne siku ya Sabato alasiri. Fungu lake la Biblia siku ya Sabato alasiri lilikuwa. “Nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.” Mazungumzo yote yalikuwa ombi kwa Waadventista Wasabato kushikilia mambo yanayoonyesha imani yao. Mara tatu wakati wa mkutano huu alianza kusimulia ile njozi ya Salamanca, lakini kila mara alizuiwa. Mambo ya njozi hii yalimpotea akilini kwa urahisi. Kisha akasema, “Juu ya hii, nitakuwa na mengi ya kusema baadaye.” Akayasawazisha mahubiri yake kwa muda wa saa moja hivi, akamaliza vizuri, na watu wakaruhusiwa kuondoka na kwenda zao kutoka katika mkutano. Wote walikuwa wameona kuwa hakuweza kuikumbuka njozi hiyo. KN 29.4

Kiongozi wa Halmashauri Kuu akamwendea na kumwuliza kama angechukuwa mkutano wa asubuhi. KN 29.5

Akajibu, “La, nimechoka; nimetoa ushuhuda wangu. Huna budi kufanya mipango mingine kwa ajili ya mkutano wa asubuhi.” Mipango mingine ikafanywa. KN 30.1

Bibi White aliporudi kwake akawasimulia watu wa nyumbani mwake kuwa hakukubali mkutano wa siku ile kwa kuwa hakukubali kuhudhuria mkutano wa siku ile asubuni. Alichoka, naye alitumaini kupumzika. Alikusudia kupumzika ndani Jumapili asubuhi ndivyo alivyopanga katika makusuai yake. KN 30.2

Usiku ule, baaaa ya kikao cha Halmashauri Kuu kumalizika, kundi dogo la watu likakutanika katika mojawapo ya ofisi kwenve jengo la Review and Herald. Katika mkutano huo palikuwako wajumbe wa Nyumba ya uchapaji ambayo ilitoa gazeti la The American Sentinel; na pia walikuwako wajumbe wa Religious Liberty Association, (Chama cha Kutetea Uhuru wa Dini). Walikuwa wamekutana kujadili na kukata shauri juu ya neno la kutatiza sana-mpango wa utengenezaji wa The American Sentinel. Mlango ulikuwa umefungwa, na wote wakakubaliana kuwa mlango hautafunguliwa mpaka shauri hili liamuliwe. KN 30.3

Punde kabla ya saa tisa za usiku kabla ya kupambazuka Jumapili mkutano huu ukaisha kwa kupingana kwa madai ya upanae wa watu wa Religious Liberty (Kutetea Uhuru wa Dini kwamba Pacific Press isipokubali madai yao na kuacha kutaja jina la “Waadventista” na “Sabato” katika safu za gazeti hilo, hawatalitumia tena kama gazeti la Chama cha Kutetea Uhuru wa Dini. Hivyo maana yake ni kuliua hili gazeti. Wakafungua mlango, na watu wakaenda nyumbani mwao, wakaenda vitandani, na kulala usingizi. KN 30.4

Lakini Mungu, ambaye kamwe hasinzii wala kulala usingizi, akamtuma malaika wake mjumbe kwa chumba cha Ellen G. White saa tisa ya usiku ule. Akaamshwa usingizini mwake na kuamriwa kuwa hana budi kwenda katika mkutano wa watenda kazi saa kumi na moja na nusu, na hapo hana budi kutoa mambo aliyoonyeshwa Salamanca. Akavaa nguo, akaenda dawatini mwake, akatwaa daftari alimoandika mambo aliyokuwa ameyaonyeswa Salamnca. Maono yalipozidi kudhihirika wazi akilini mwake, akaandika zaidi mambo ya kwenda nayo. KN 30.5

Wahubiri walikuwa wakiinuka kutoka katika kusali Kanisani wakati Mama White alipoonekana akiingia mlangoni, akiwa na bunda la maandishi kwapani. Kiongozi wa Halmashauri Kuu ndiye aliyekuwa mhubiri, na akamsemesha: KN 30.6

Akamwambia, “Mama White, tumefurahi kukuona. Je, unao ujumbe kwetu?” Akamwambia, “Ndiyo ninao,” na akaenda mbele. Kisha akaanzia mahali alipoachia mazungumzo yake siku iliyopita. Akawaambia kuwa saa tisa usiku ule alikuwa ameamshwa usingizini mwake na kuamriwa aende kwenye mkutano wa watenda kazi saa kumi na moja na nusu na hapo atoe mambo aliyokuwa ameonyeshwa Salamanca. KN 30.7

Akasema, “Katika njozi, nalionekana kana kwamba niko Battle Creek. Nalichukuliwa mpaka katika ofisi ya Review and Herald, na yule malaika mjumbe akaniamuru, ‘Nifuate.’ Nikachukuliwa chumbani mahali kundi fulani la watu walipokuwa wakijadiliana sana shauri moja. Palionyeshwa moyo wa biaii, lakini sio wa hekima.” Akasema jinsi walivyokuwa wakijadili mpango wa utengenezaji wa The American Sentinel, akasema “Naliona mmoja wa watu hawa akitwaa nakala ya The Sentinel akaishikilia juu ya kichwa chake, na kusema, ‘Isipokuwa habari hizi juu ya Sabato na Kuja kwa Kristo Mara ya Pili zimeondoka gazetini humu, hatuwezi kulitumia tena kama gazeti la Chama cha Kutetea Uhuru wa Dini (Religious Liberty Association) ” Ellen G. White akazungumza muda wa saa moja, akieleza mkutano ule mambo aliyoonyesnwa katika njozi miezi kadha wa kadha zamani, na akitoa onyo lenye msingi juu ya mafunuo yale. Kisha akaketi. KN 31.1

Kiongozi wa Halmashuri Kuu akawa na wasi wasi asijue la kufanya juu ya neno hili. Kamwe alikuwa hajakuwa na mkutano wa namna hii. Lakini hawakungojea muda mrefu kupata maelezo; maana mtu mmoja alisimama upande wa nyuma wa chumba, naye akaanza kusema: KN 31.2

“Nilikuwa katika mkutano huo usiku huu uliopita.” Ellen White akasema, “Usiku huu uliopita, usiku wa leo? Nilidhani mkutano huo ulifanyika miezi kadha wa kadha zamani, nilipoonyeshwa habari zake katika njozi.” KN 31.3

Akasema, “Nilikuwa katika mkutano huo usiku huu uliopita, nami ndiye mtu ambaye alisema maneno yale juu ya habari katika gazeti hilo, nikiliinua juu kichwani mwangu. Nasikitika kusema kwamba nilikuwa upande mbaya; lakini nachukua nafasi hii kujiweka upande mzuri.” Akaketi chini. KN 31.4

Mtu mwingine akasimama kusema. Alikuwa ndiye mkuu wa Chama cha Uhuru wa Kutetea Dini. Tazama maneno yake; “Nilikuwa katika huo mkutano. Usiku huu uliopita baada ya kufunga kikao baadhi yetu tulikutanika chumbani mwangu katika ofisi ya Review mahali tulimojifungia na hapo tukajadili maswali na shauri ambalo tumepewa asubuhi hii. Tuhkaa katika chumba kile mpaka saa tisa usiku wa leo. Kama ningeanza kutoa maelezo ya mambo yaliyofanyika na moyo wa kila mtu aliyekuwako chumbani humo, singeweza kuyatoa kwa uhalisi na kwa usahihi kama yaliivyotolewa na Mama White. Sasa naona kuwa nilikosea na ya kwamba madaraka niliyojitwalia yalikuwa si halali. Kwa nuru ambayo imetolewa asubuhi hii, nakiri kwamba nilikosa.” KN 31.5

Wengine walisema siku ile. Kila mtu aliyekuwa katika mkutano ule usiku uliopita alisimama na kutoa ushuhuda wake, akisema kuwa Ellen White alikuwa ameeleza kwa usahihi mkutano ule na moyo wa wale waliokuwako chumbani. Kabla ya kufungwa kwa mkutano siku ile ya Jumapili asubuhi, kundi la Chama cha Kutetea Uhuru wa Dini waliitwa wakusanyike pamoja, nao wakavunja mapatano waliyofanya mbele ya saa tano tu zilizopita. KN 32.1

Kama Mama White asingezuiliwa naye angaliieleza njozi ile siku ya Sabato alasiri, ujumbe wake usingetimiza kusudi ambalo Mungu aliikusudia, maana mkutano ule ulikuwa bado kufanyika. KN 32.2

Lakini watu wale hawakutumia onyo kubwa lililotolewa siku ya Sabato alasiri. Walidhani wanajua mambo viziri zaidi. Pengine Mama White hakufahamu,” au “Tunaishi wakati mwingine sasa,” au “Onyo hilo lilihusu miaka ya zamani, lakini je halitufai sasa?” Mawazo ambayo Shetani huyanong’ona kwetu siku hizi ni yale yale aliyotumia kuwashawishi wale watu mwaka 1891. Mungu, wakati aliochagua mwenyewe na kwa njia yake mwenyewe, alidhihirisha wazi kwamba ilikuwa kazi yake; alikuwa akiongoza; alikuwa akiendesha. Ellen G. White atwambia kwamba Mungu “mara nyingi ameyaruhusu mambo yaelekee kuleta hatari, ili kuingilia kwake katika mambo hayo kufahamike. Ndipo atakuwa amedhihirisha kuwa kuna Mungu katika Israeli.”

Shuhuda na Msomaji

Kwa muda wa miaka sabini Ellen G. White alisema na kuandika habari za mambo ambayo Mungu alikuwa amemfunulia. Mara nyingi maonyo yalikuwa yametolewa kuwasahihisha wale ambao walipotoka kutoka katika ukweli wa Biblia. Mara nyingi walionyesha njia ambayo Mungu angependa watu wake waifuate. Wakati mwingine Shunuda hizi zilikuwa juu ya mwenendo wa maisha, nyumbani, na kanisani. Washiriki wa kanisa waliupokeaje ujumbe huu? KN 32.4

Tangu mwanzo wa kazi yake, viongozi wakubwa waliipima kazi yake wapate kuhakikisha kuwa mafunuo ya kipawa cha unabii yalikuwa ya kweli. Mtume Paulo aonya, “Msimzimishe Roho; msitweze unabii; jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema,” (lThe. 5:20, 21). Kipimo cha Biblia cha kumpima nabii kilitumika kuithibitisha kazi ya Ellen White. Na hivi ndivyo alivyopenda iwe, maana ameandika: KN 32.5

“Kazi hii ni ya Mungu, au sivyo. Mungu hafanyi shirika lo lote na Shetani. Kazi yangu kwa miaka thelathini iliyopita inao ama muhuri wa Mungu ama muhuri wa yule adui. Haiwezi kuwa nusunusu kwa jambo hili.” Biblia inatoa majaribio manne ambayo kwayo nabii hana budi kupimwa. Kazi ya Ellen White imeshinda katika kila kipimo. KN 32.6

1. Ujumbe wa nabii wa kweli hauna budi kupatana na sheria ya Mungu na maneno ya ujumbe wa manabii, (Isa. 8:20). KN 33.1

Maandishi ya Ellen G. White huiheshimu sheria ya Mungu na kuwaongoza daima wanaume na wanawake kwenye Biblia nzima. Anaelekeza kwenye Biblia kama kanuni ya imani na ibada na kama nuru kuu ambapo maandishi yake “nuru ndogo,” huwaelekeza wote wasomao. KN 33.2

2. Unabii wa kweli hauna budi kutimia. (Yer. 28:20). Huku kazi ya Ellen White ikiwa imefanana na ile ya Musa katika kuwaongoza watu, lakini yeye aliandika kwa njia ya kutabiri matukio mengi. Mwanzoni mwa kazi yetu ya kuchapisha vitabu na magazeti mnamo mwaka 1848, alisema jinsi ambavyo ingalikua na kueneza nuru ulimwenguni. Leo Waadventista Wasabato huchapisha vitabu na magazeti katika lugha 200 ambavyo vina thamani zaidi ya Shs. 140,000,000 kwa mwaka. KN 33.3

Mwaka 1890, walimwengu walipotangaza kuwa hapatakuwako na vita tena na ya kwamba muda wa miaka elfu ulikuwa karibu kuanza, Ellen G. White aliandika: “Dhoruba inakuja, nasi KN 33.4

yatupasa kujiweka tayari kuzikabili nguvu zake Tutaona matata KN 33.5

pande zote. Maelfu ya meli zitatupwa kwa nguvu vilindini mwa bahari. Manowari zitazama, na watu mamilioni watapoteza maisha yao.” Hili lilitimia katika Vita Kuu ya I na ya II. KN 33.6

3. Nabii wa kweli atakiri kuwa Yesu Kristo amekuja katika mwili, na ya kuwa Mungu alifanyika mtu halisi. (1 Yohana 4:2). Kusoma Tumaini la Vizazi Vyote hudhihirisha kuwa kazi ya Ellen G. White hulenga katika kipimo hiki. Tazama maneno haya: KN 33.7

“Yesu angaliweza kuendelea kukaa karibu na Baba. Angaliweza kushikilia ule utukufu wa mbinguni, na kupewa heshima na malaika. Lakini alichagua kuiweka enzi na utukufu wake mikononi mwa Baba yake, na kushuka kutoka katika kiti cha enzi cha mbinguni na kuja duniani ili kuwaletea nuru wale walio gizani, na uzima kwa wale wanaopotea. KN 33.8

“Yapata miaka elfu mbili iliyopita, sauti ya maana ajabu ilisikika mbinguni kutoka katika kile kiti cha enzi cha Mungu ikisema, ‘Tazama, nimekuja’. Dhabihu na toleo hukutaka, lakini Mwili uliniwekea tayari Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) niyafanye mapenzi yako, Mungu.’ (Waebrania 10:57). Kwa maneno haya umetangazwa utimizo wa kusudi lililokuwa limefichwa tangu zamani. Kristo alikuwa karibu kuuzuru ulimwengu wetu, na kufanyika mtu halisi Machoni pa walimwengu nakuwa na uzuri hata wamtamani; lakini, alikuwa Mungu aliyefanyika mtu halisi, nuru ya mbinguni na duniani. Utukufu wake ulifichwa. Ukuu na utukufu wake ulisetiriwa ili apate kuwakaribia wanadamu wenye huzuni na waliojaribiwa.” KN 33.9

4. Pengine kipimo muhimu sana cha nabii wa kweli hupatikana katika maisha yake, kazi yake, na mvuto wa mafundisho yake. Kristo alinena wazi jambo hili katika Mathayo 7:15, 16: “Mtawatambua kwa matunda yao.” Tukiyapima maisha ya Ellen G. White hatuna budi kusema kuwa aliishi maisha mema ya Kikristo yanayopatana na mafundisho yake, na kushika kile tunachoweza kumtazamia nabii. Tukiyaangalia matunda kama yalivyodhihirishwa maishani mwa wale ambao wameyafuata maonyo ya Roho ya Unabii, twaona kuwa ni mema. Shuhuda hizi zimezaa matunda mema. Tukilitazama Kanisa, tukijua kuwa tumeongozwa katika kazi za namna nyingi mbalimbali kwa mashauri haya, hatuna budi kukiri kuwa kazi ya Ellen White inashinda kipimo hiki. Hali ya umoja wa mafundisho yaliyo katika maandishi yaliyoandikwa kwa kalamu ya wino kwa muda mrefu zaidi ya miaka 70 pia hushuhudia hakika ukamilifu wa kipawa hiki.

Vipimo Vya Kufaa Kwa Nabii wa Kweli

Pamoja na vipimo hivyo vya Biblia, Mungu ametoa shuhuda zinazodhinirisha kuwa kazi hii ni ya maongozi yake. Miongoni mwa hayo ni: KN 34.2

1. Wakati unaofaa wa ujumbe huu. Watu wa Mungu wamo katika mahitaji maalumu, na ujumbe huu huwajia wakati hasa wanapouhitaji kuyatimiza mahitaji hayo, kama vile ilivyokuwa njozi ya kwanza aliyopewa Ellen White. KN 34.3

2. Hali ya kufaa ya ujumbe huu. Habari zilizofunuliwa kwa Ellen White katika njozi zilikuwa za thamani kuu, zenye kukidhi hitaji kubwa. Angalia jinsi ambavyo maonyo ya ushuhuda huu yaingiavyo kwa njia ya kufaa katika maisha yetu ya kila siku. KN 34.4

3. Uzuri wa kiroho wa maneno ya ujumbe huu. Hayasemi mambo ya kitoto au ya kawaida, bali mambo makubwa yenye maana. Lugha yenyewe ni bora sana. KN 34.5

4. Namna njozi hizi zilivyotolewa. Nyingi miongoni mwa njozi hizi ziliambatana na maajabu yaliyoonekana kwa macho kama ilivyoelezwa katika utangulizi huu. Mambo yaliyompata Ellen White katika njozi yalikuwa sawa na yale ya manabii wa Biblia. Hiki, ingawa si kipimo, lakini ni mojawapo ya mambo mengine yamshuhudiayo. KN 34.6

5. Njozi zilikuwa mambo halisi, siyo maono tu. Katika njozi, Ellen White aliona, akasikia, na kupokea maagizo kutoka kwa malaika. Njozi hizi zisingeweza kuhesabiwa kuwa zatokana na mambo ya kuhamakisha au ya kudhaniwa tu. KN 34.7

6. Ellen White hakushawishiwa na wale waliomzunguka. Alimwandikia mtu mmoja: “Unadhani watu wameongoza mafikara yangu, lakini nikiwa katika hali hii sifai kuaminiwa katika kazi ya Mungu.” KN 34.8

7. Kazi yake ilishukuriwa na watu wa hirimu au rika yake. Wale waliokuwa kanisani waliokaa na kufanya kazi pamoja na Ellen White, na wengi nje ya kanisa walimfahamu Ellen White kama “mjumbe wa Mungu” kweli kweli. Wale waliokuwa karibu sana naye walikuwa na imani kubwa sana katika mwito na kazi yake. KN 35.1

Vipimo hivi vinne vya Biblia na mambo haya dhahiri ambayo Mungu amewapa watu wake ili wapate kuwa na imani katika ujumbe huu na mjumbe huyu hutuhakikishia kuwa kazi hii ni ya Mungu nayo haistahili kutiliwa mashaka. KN 35.2

Vitabu vingi vya Ellen G. White vimejaa maonyo na mafundisho yenye thamani daima kwa kanisa. Ingawa shuhuda hizi zilikuwa za namna iliyopasa watu wote kwa jumla ama shuhuda za pekee kwa jamaa au kwa mtu mmoja mmoja lakini zinatufaa hata siku hizi. Juu ya jambo hili, Ellen White anasema: KN 35.3

“Kwa sababu maonyo na mafundisho yaliyotolewa katika shuhuda hizi kwa ajili ya watu mmoja mmoja huwahusu na kuwa na nguvu ile ile kwa wengine wengi ambao hawakuonyeshwa hasa kwa njia hii, ilionekana kuwa wajibu wangu kuchapisha shuhuda hizi za mtu mmoia mmoja kwa ajili ya faida ya kanisa Sijui njia nyingine iliyo bora zaidi kutoa maoni yangu juu ya hatari na makosa ya watu wote na wajibu wa wote wampendao Mungu na kuzishika amri zake, kuliko kwa kuzitoa shuhuda hizi.” KN 35.4

Ni kosa kutumia vibaya shuhuda hizi kwa kuzisoma ili kuona mahali pa kumhukumu ndugu mwenzako. Kamwe shuhuda hizi zisitumiwe kama rungu kuwalazimisha ndugu wa kiume au wa kike kuona mambo ambayo hayana budi kuachwa kwa mtu kuyamaliza mwenyewe na Mungu. KN 35.5

Maonyo haya yangesomwa ili kupata kanuni kubwa ambazo huyahusu maisha yetu siku hizi. Baadhi ya maneno ya ujumbe huu yalitolewa kama maonyo au makaripio kwa wakati fulani maalum au mahali fulani maalum, lakini kanuni zilizoelezwa ni zenye kuhusu po DOte kwa maana yake na wakati zinapotumiwa. Moyo wa mwanaaamu ni hali moja ulimwenguni mwote; shida za mmoja mara nyingi ni shida za mwingine. Ellen White ameandika, “Katika kuyakaripia makosa ya mtu, Mungu amekusudia kuwatoa makosa wengi.” “Huyadhihirisha makosa ya wengine ili wengine wapate kuonywa kwa njia hiyo.” Karibu na mwisho wa maisha yake Ellen White alitoa ushauri huu ufuatao: KN 35.6

“Kwa njia ya Roho wake Mtakatifu sauti ya Mungu imetujia daima kuonya na kufundisha Muda na mashindano havikuy-atambua mafundisho yaliyotolewa Mafundisho ambayo yali-tolewa siku ya mwanzo wa ujumbe huu hayana budi kushikwa kama mafundisho salama kufuatwa katika siku hizi za mwisho wake.” KN 35.7

Maonyo ambayo yanafuata yametwaliwa kutoka katika vitabu kadha wa kadha vya Ellen G. White-lakini zaidi sana kutoka katika vile vitabu vitatu vya The Testimony treasures, ambavyo ni muhtasari wa nakala za The Tesmonies for the Church-nayo nutoa mafimdisho yaliyofikiriwa kuwa yenye manufaa makubwa sana kwa kanisa mahali ambapo uchache wa hesabu ya washiriki wa kanisa huzuia isiwezekane kuchapisha kitabu kimoja cha ukubwa wa wastani. Kazi ya kuyachagua na kuyapanga mashauri haya ilifanywa na kamati kubwa, ikifanya kazi kwa ldhini ya Wadhamini wa Vitabu vya Ellen G. White ambayo ilihesabiwa kuwa kazi yao kutunza na kueneza matumizi ya mashauri ya Roho ya Unabii. Uchaguzi mara nyingi huwa mfupi na huwa na kikomo katika mafiindisho makubwa ya kufaa, na hivyo mafundisho mengi ya namna mbalimbali huwamo. KN 36.1

“Mwaminini Bwana, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.” (2 Mambo ya Nyakati 20:20). KN 36.2

Wadhamini wa KN 36.3

MAANDISHI YA ELLEN G. WHITE

Washington, D.C.

Julai 22, 1957.

 

 

 

Sura ya 1 - Njozi ya Ijara ya Waaminifu

(Njozi Yangu ya Kwanza)

WAKATI nilipokuwa nikiomba katika chumba cha ibada nyumbani, Roho Mtakatifu alinishukia, nami nikaona kama nainuliwa juu, juu mbali na ulimwengu wa giza. Nikageuka kuwatafuta Waadventista ulimwenguni, lakmi sikuweza kuwaona, sauti iliponiambia, “Tazama tena, na tazama kidogo.” Kwa maneno haya nikainua macho yangu, nikaona njia nyembamba iliyonyoka, juu iliyoinuliwa juu ya ulimwengu. Juu ya njia hii Waadventista walikuwa wakisaflri kwenda katika mji ambao ulikuwa mbali mwisho wa njia. Walikuwa nayo nuru kubwa iliyosimikwa nyuma yao mwanzoni mwa hiyo njia, ambayo malaika aliniambia kuwa ilikuwa Kilio cha Usiku wa Manane. Nuru hii iling’aa njiani pote na kuangaza miguuni mwao kusudi wasije wakajikwaa. Waliendelea kuwa salama ili mradi tu wanadumu kuyakaza macho yao kwa Yesu ambaye alikuwa mbele yao akiwaongoza kwenda mjini. Lakini mara wengine wakachoka, na kusema mji ulikuwa mbali sana, nao walitazamia kuwa wakati huo wangalikuwa wamekwisha kuuingia. Ndipo Yesu akawatia moyo kwa kuuinua mkono wake wa kuume wa fahari, na kutoka mikononi mwake nuru ikaja ambayo iliangaza juu ya kikosi cha Waadventista, nao wakapaza sauti, “Haleluya!” Wengine wakakanusha ile nuru nyuma yao na kusema kuwa si Mungu aliyekuwa amewaongoza mpaka napo. Nuru ile nyuma yao ikazimika, ikiiacha miguu yao gizani kabisa nao wakajikwaa na kukosa kuiona alama na Yesu, nao wakapotea njia na kushuka duniani penye giza na maovu. Mara tukaisikia sauti ya Mungu kama maii mengi, iliyotujulisha siku na saa ya kuja kwa Yesu. Watakatifu walio hai, hesabu yao 144,000 walijua na kuifahamu sauti hii, huku waovu wakifikiri llikuwa radi na tetemeko la nchi. Wakati Mungu alipotangaza wakati huo, akatumwagia Roho Mtakatifu, na nyuso zetu zikaanza kuang’azwa na kung’aa kwa utukufu wa Mungu, kama uso wa Musa ulivyong’aa aliposhuka kutoka Mlima Sinai. KN 37.1

Wale 144,000 wote walitiwa muhuri na walikuwa na umoja kabisa. Juu ya vipaji vya nyuso zao paliandikwa, Mungu, Yerusalemu Mpya, na nyota ya fahari yenye jina jipya la Yesu. Waovu waliikasirikia hali yetu takatifu na ya furaha, nao wakaturukia kwa nguvu kutushika ili kututupa gerezani, wakati huo tulinyosha mkono katika jina la Bwana, nao wakaanguka chini wasiweze kujimudu. Kisha ikawa sinagogi la Shetani (wale waliochagua kumfuata Shetani) wakajua kuwa Mungu alikuwa ametupenda sisi ambao tuliweza kutawadhana miguu na kuwasalimu ndugu kwa busu takatifu, nao wakasujudu miguuni mwetu. KN 37.2

Punde macho yetu yakavutwa mashariki, maana wingu dogo jeusi lilikuwa limezuka, ukubwa wake kama nusu ya kiganja cna mkono wa mtu, ambalo sote tunalijua kwamba lilikuwa ishara ya Mwana wa Adamu. Sisi sote kimya kabisa tukalikazia macho wingu lile likikaribia zaidi na kuzidi kuwa jepesi, tukufu, na la fahari zaiai, mpaka likawa wingu kubwa jeupe. Chini lilionekana kama moto; upinde wa mvua ulikuwa juu ya wingu hili huku pande zote kulizunguka palikuwa na taji nyingi Nyayo za miguu yake zilikuwa zinaonekana kama mto; katika mkono wake wa kuume alikuwa na mundu mkali; katika mkono wa kushoto, tarumbeta ya fedha. Macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, nayo yaliwachunguza watoto wake kabisa. Kisha nyuso zote zikabadilika rangi, na wale ambao Mungu amewakataa nyuso zao zikawa nyeusi. Kisha sisi sote tukapaza sauti, “Ni nani awezaye kusimama? Vazi langu ni jeupe lisilo na mawaa?” Ndipo malaika wakakoma kuimba, na pakawa na kitambo cha kimya cha ajabu, wakati Yesu aliposema: “wale wenye mikono safi na mioyo safi wataweza kusimama; Neema yangu yakutosha.” Hili likang’aza nyuso zetu, na furaha ikamjaa kila mmoja moyoni. Na wale malaika wakapiga muziki wakapaza sauti juu zaidi na kuimba tena, huku lile wingi likizidi kukaribia zaidi dunia. KN 38.1

Ndipo tarumbeta ya Yesu ya fedha ikalia akishuka juu ya wingu, amezingirwa na ndimi za moto. Akayakodolea macho makaburi ya watakatifu waliolala, kisha akayainua macho yake na mikono mbinguni, na kupaza sauti, “Amkeni! Amkeni! Amkeni! Enyi mlalao mavumbini, ondokeni.” Ndipo pakawa na tetemeko kuu la nchi. Makaburi yakafunuka, na watu wakatoka wamevikwa kutokufa. Wale 144,000 wakapaza sauti, “Haleluya!” wakiwatambua marafiki zao waliotengwa nao na mauti, na dakika hiyo hiyo tukabadilishwa na kunyakuliwa pamoja nao kwenda kukutana na Bwana hewani. KN 38.2

Sote tukaingia winguni pamoja, tukapaa siku saba kwenda penye bahari ya kioo, wakati Yesu alipozileta taji, na kwa mkono wake mwenyewe wa kuume kutuvika hizo taji vichwani mwetu. Akatupa vinubi vya dhahabu na alama za ushindi. Hapa juu ya bahari ya kioo wale 144,000 walisimama mraba kamili. Wengine wao walikuwa na taji zing’aazo sana, wengine hawakuwa na zenye kung’aa namna ile. Taji zingine zilionekana kuwa nzito kwa kuwa na nyota nyingi, huku zingine zikiwa na nyota chache tu. Wote waliridhika kabisa na taji zao. Nao wote walivikwa vazi jeupe la utukufu kutoka mabegani mwao hadi chini miguuni pao. Malaika walituzunguka pande zote tukitembea juu ya bahari ya kioo kwenda langoni mwa mji. Yesu akauinua mkono wake hodari, wenye utukufu, akaushika mlango wa lulu, kurudisha nyuma juu ya bawaba zake zinazomeremeta, na kutuambia, “Mmeyafua mavazi yenu katika damu yangu, mkasimama imara kuitetea kweli yangu, ingieni.” Sote tukaingia kwa taratibu na kujiona moyoni kuwa tulikuwa na haki kamili mjini. KN 38.3

Hapo tukauona mti wa uzima na kiti cha enzi cha Mungu. Katika kiti hiki cha enzi kukatoka mto wa maji safi, kila upande wa mto huu palikuwa na mti wa uzima. Upande mmoja wa mto huu palikuwa na shina la mti, na shina lingine tena upande wa pili wa mto, yote mawili ya dhahabu safi, yenye kupenya nuru. Kwanza nalidhani naliona miti miwili. Nikatazama tena, nikaona kuwa iliunganika juu na kuwa mti mmoja. Matawi yake yaliinama mpaka mahali tuliposimama, na matunda yalikuwa mazuri mno; yakaonekana kama dhahabu iliyochanganywa na fedha. KN 39.1

Sote tukaenda chini ya mti huu na kuketi kuangalia utukufu wa mahali hapa, wakati ndugu Fitch na Stockman, waliokuwa wameihubiri habari njema ya ufalme, na ambao Mungu alikuwa amewalaza kaburini kuwaokoa, wakapanda, kwetu na kutuuliza kilichokuwa kimetukia walipokuwa wamelala. Tukajaribu kukumbuka taabu zetu kubwa kabisa, lakini zilionekana kuwa ndogo sana zikilinganishwa na utukufu mwingi wa milele uzidio sana ambao ulituzunguka hata hatukuweza kuzitaja, nasi wote tukapaza sauti, “Haleluya, mbinguni ni rahisi ya kutosha!” nasi tukavipiga vinubi vyetu vizuri mno na kuifanya mbingu kurudisha mwangwi. KN 39.2

Yesu akatuongoza sote tukashuka kutoka mji ule mpaka duniani humu, juu ya mlima wa ajabu, ambao haukuweza kumstahimili Yesu, nao ukapasuka vipande vipande, pakawa na uwanda wa ajabu. Kisha tukatazama juu na kuuona ule mji mkuu, wenye misingi kumi na miwili, na milango kumi na miwili, mitatu kila upande, na malaika mmoja katika kila mlango. Sote tukapaza sauti, “Mji, mji mkuu, unakuja, unashuka kutoka kwa Mungu mbinguni,” nao ukaja na kutuama juu mahali tuliposimama. Kisha tukaanza kuvitazama vitu vya fahari nje ya mji huo. Hapo nikaona nyumba nzuri mno, zilizoonekana kama fedha, zimetegemezwa kwa nguzo nne, zilizopambwa kwa lulu nzuri mno kutazama. Hivi zilipaswa kukaliwa na watakatifu. Kila moja ilikuwa na kibao cha kutundikia ukutani cha dhahabu. Nikawaona watakatifu wengi waliingia nvumba hizi wakavua taji zao zing’aazo na kuziweka kibaoni, kisha wakaenda shambani karibu na nyumba hizo kufanya kitu na udongo; siyo kama tupaswavyo kufanya na udongo hapa; la hasha. Nuru nzuri ajabu iling’aa pande zote vichwani mwao, nao walikuwa wanaendelea kupaza sauti na kumsifu Mungu. KN 39.3

Nikaona shamba lingine lililojaa maua ya kila namna, na nikiyachuma, nikapaza sauti, “Kamwe hayatanyauka.” Tena nikaona shamba la majani marefu, zuri sana kutazama: lilikuwa la rangi ya kijani kibichi na lilikuwa likirudisha nuru ya fedha na dhahabu likipepea kwa fahari kwenye utukufu wa Yesu Mfalme. Kisha tukaingia uwanda mmoja uliojaa wanyama wa kila aina-simba, mwana-kondoo, chui, na mbwa wa mwitu, wote pamoja katika umoja kamili. Tukapita katikati yao nao wakafuata taratibu kwa amani. Kisha tukaingia mwituni, siyo kama misitu minene tuliyo nayo hapa; la hasha; siyo yenye giza kama hapa, bali ni mizuri mno pande zake zote; matawi ya miti yaliyumba-yumba, nasi sote tukapaza sauti, “Tutakaa salama mahali hapa pakame na kulala penye misitu.” Tukapita mapori, maana tulikuwa safarini kwenda Mlima Sayuni. KN 39.4

Tulipokuwa tukisaflri, tukakutana na kundi la watu ambao walikuwa pia wakiyakaza macho yao kutazama utukufu wa mahali pale. Nikaona rangi nyekundu kama pindo la mavazi yao; taji zao zilikuwa zenye kung’aa; mavazi yao yalikuwa safi meupe. Akasema walikuwa wafia dini (watu waliouawa kwa sababu ya kukataa kuikana imani yao) ambao walikuwa wameuawa kwa ajili yake. Pamoja nao palikuwako kundi la watoto wengi mno. Wao pia walikuwa na pindo la rangi nyekundu juu ya mavazi yao. Mlima Sayuni ulikuwa mbele yetu, na juu ya mlima palikuwako na hekalu zuri mno, na pande zote kuuzunguka palikuwa na milima mingine saba, ambayo juu yake palisitawi wandi na maua mazuri jamii ya yungiyungi. Nami nikawaona watoto wakipanda, au kama walichagua kufanya hivyo, walitumia mabawa yao madogo na kuruka, mpaka juu ya kilele cha milima hii na kuchuma maua ambayo kamwe hayanyauki. Palikuwa na miti ya kila aina pande zote kulizunguka lile hekalu kupapamba mahali hapo: namna ya mti mweupe mgumu (box), msunobari (pine), mwerezi, mfuta (the oil) namna ya mti mdogo (the myrtle), mkomamanga, na mtini uliinama chini kwa uzito wa tini zake za majira ya kufaa hii ilipafanya mahali hapa kuwa pazuri mno pande zote. Na tulipokuwa karibu kuingia hekalu takatifu, Yesu akipaza sauti yake tamu na kusema, “Wale tu KN 40.1

144,000 ndio wenye kuingia mahali hapa,” nasi tukapaza sauti, “Haleluya.” KN 40.2

Hekalu hili lilitegemezwa na nguzo saba, zote za dhahabu ipenyayo nuru, zimepambwa na lulu nzuri mno. Vitu vya ajabu nilivyoviona hapo siwezi kuvielezea. Ah, laiti ningeweza kusimulia kidogo juu ya utukufu wa ulimwengu ule mzuri zaidi. Nikaona pale vibao vya mawe ambamo majina ya wale 144,000 yaliandikwa kwa herufi za dhahabu. Tulipokuwa tumekwisha kuutazama utukufu wa lile hekalu, tukatoka, naye Yesu akatuacha na kwenda mjini. Mara tukaisikia sauti yake tamu tena, akisema, “Njoni, watu wangu, mmetoka katika dhiki ile iliyo kuu, na mmefanya mapenzi yangu; mkateseka kwa ajili yangu; njoni chakulani, maana nitajifunga, na kuwahudumia.” Tukapaza sauti, “Haleluya! Utukufu!” na kuingia mjini. Nami nikaona meza ya fedha safi; ilikuwa ndefu maili nyingi, walakini macho yetu yaliweza kuiona mpaka mwisho. Nikaona matunda ya mti wa uzima, mana, malozi, tini, makongamanga, zabibu, na matunda ya aina nyingi nyingine. Nikamwuliza Yesu kuniruhusu niyale matunda hayo. Akasema. “Siyo sasa. Wale wanaokula matunda ya nchi hii nawarudi tena duniani. Lakini muda kitambo, kama ukiwa mwaminifu, utakula matunda ya mti wa uzima na kunywa maji ya chemchemi.” Naye akaniambia, “Huna budi kurudi duniani tena na kuwasimulia wengine mambo ambayo nimekufunulia.” Kisha malaika akanichukua chini taratibu mpaka katika ulimwengu huu wa giza. Wakati mwingine nafikiri siwezi kukaa hapa tena; vitu vyote vya dunia huonekana kuwa vibaya vya kutia huzuni sana. Najiona hali ya upweke sana hapa, maana nimeona nchi nzuri zaidi. Ah, laiti ningekuwa na mabawa kama njiwa, ndipo ningeruka mbali na kuwa katika raha! (Early Writings, uk. 14-20). 

Sura ya 2 – Wakati wa Mwisho

TUNAISHI katika wakati wa mwisho. Dalili za nyakati hizi zinazotimia haraka hutangaza kuwa kuja kwa Kristo kumekaribia. Siku tunazoishi ni nyeti na za muhimu. Roho wa Mungu anaondolewa duniani, taratibu, lakini kwa hakika. Mapigo na hukumu tayari vinawaangukia wenye kuidharau neema ya Mungu. Misiba mikubwa katika nchi kavu na baharini, hali ya machafuko ya watu, habari za hatari za vita, ni za kuogofya. Haya yanaashiria matukio yanayokaribia ya mambo makubwa. Nguvu za uovu zinaungana na kujizatiti. Wanakusanya nguvu kwa ajili ya hatari kuu za mwisho. Mabadiliko makubwa hayana budi kutokea ulimwenguni mwetu siku si nyingi, na mabadiliko ya mwisho yatakuwa ya haraka haraka. Hali ya mambo ulimwenguni huonyesha kuwa nyakati za dhiki zinatukabili. Magazeti ya kila siku yamejaa mambo yanayoonyesha vita kali muda si mrefu ujao. Uporaji wa hadharani unatokea mara kwa mara. Migomo ni jambo la kawaida. Wizi na uuaji hufanywa kila upande. Watu makatili wanawaua watu, wanaume, wanawake, na watoto wadogo. Watu wamepumbazishwa na muovu, na kila aina ya uovu imeenea po pote. KN 42.1

Adui amefaulu katika kupotosha haki na katika kuijaza mioyo ya watu tamaa ya kujipatia mali isiyo ya halali. “Haki inasimama mbali sana; maana kweli imeanguka katika njia kuu, na unyofu hauwezi kuingia” (Isaya 59:14). Katika miji mikuu wako wengi wanaoishi katika nali ya umaskini na ufukara, karibia kabisa kukosa chakula, nyumba, na nguo; huku katika miji hiyo hiyo wakiwapo wale ambao wanacho kila kitu wanachotamani, wenve kuishi kitajiri, na kujipendeza kwa anasa, wakitumia pesa zao katika nyumba za kitajiri, mapambo ya mwili, au jambo lililo baya zaidi, kwa kujipendeza kwa tamaa mbaya za mwili, kwa pombe, tumbako, na vitu vingine vinavyodhuru nguvu za ubongo, na kuduwaza akili, na kuharibu moyo. Vilio vya watu wanaoumia kwa njaa vinapanda juu mbele za Mungu, huku kwa udhalimu wa kila aina na ukandamizaji watu wanajilundikia mali nyingi. KN 42.2

Katika tukio moja nikiwa kwenye jiji la New York, majira ya usiku nilionyeshwa majengo yakipanda ghorofa moja baada ya nyingine kuilekea mbingu. Majengo haya yalishuhudiwa kitaalam kuwa imara yasiyoweza kushika moto; na yalijengwa kuwatukuza wenye kuyamiliki na wajenzi. Majengo haya yakazidi kuinuka juu, nayo yalijengwa kwa kutumia vifaa vya gharama kubwa sana. Wale wamiliki wa majengo haya hawakujiuliza: “Twawezaje kumtukuza Mungu vizuri zaidi?” Hawakumwaza Mungu. Kadiri majengo haya marefu yalivyopanda juu, wamiliki wake walifurahi huku wakijazwa na tamaa ya kutaka makuu kwamba walikuwa na fedha ya kutumia katika kujitukuza nafsi zao na kuchochea wivu kwa maiirani zao. Fedha iliyo nyingi ambayo wameitumia kwa njia nii imepatikana kwa udnalimu, kwa kuwaonea maskini. Wamesahau kuwa mbinguni huandikwa habari za kila tendo; kila jambo lisilo la haki, kila udanganyifu, huandikwa pale. Maono mengine niliyoonyeshwa yalikuwa kelele ya dharura ya kujulisha watu hatari ya moto. Watu wakayatazama yale majengo marefu yaliyodhaniwa kuwa hayawezi kuungua moto na kusema: “Yako salama kabisa.” Lakini majengo haya yaliteketea kana kwamba yalikuwa yamejengwa kwa lami. Mashine za kuzimia moto hazikuweza kufanya cho chote kuzuia uharibifu huo. Zima moto walishindwa kabisa kutumia mashine hizo. KN 42.3

Nimeamriwa kuwa saa ya Bwana ifikapo, ikiwa hakuna mabadiliko yaliyofanyika katika mioyo yenye kiburi na majivuno, na ya wenye kutaka makuu, watu wataona kuwa mkono ule ambao ulikuwa na nguvu kuokoa utakuwa wenye nguvu kuangamiza. Hakuna nguvu duniani iwezayo kuuzuia mkono wa Mungu. Wala hakuna vifaa viwezavyo kutumiwa katika kujenga majengo ambavyo vitayalinda yasiharibiwe saa ya Mungu iliyowekwa ifikapo kuwapatiliza watu uasi wao juu ya Sheria yake na kujitakia makuu. Si wengi, hata miongoni mwa wataalamu na wakuu wa nchi wanaofahamu asili ya hali lliyoko sasa miongoni mwa jamii za watu. Wale wanaotawala serikalini hawawezi kutatua tatizo la kuharibika kwa tabia za watu, umaskini, ufukara, na kuongezeka kwa uhalifu wa sheria. Wanasumbuka bure kuweka sheria za kutenda kazi za biashara kwa njia ya salama zaidi. Kama wangeyatii mafundisho ya Neno la Mangu, wangepata jawabu la marumbo yanayowatatiza. KN 43.1

Maandiko Matakatifu huelezea hali ya ulimwengu karibia na Kuja kwa Kristo Mara ya Pili. Juu ya watu ambao kwa unyang’anyi na kutaka bei kubwa kwa vitu wanalundika mali nyingi, imeandikwa: “Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelel, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi. Mmefanya anasa katika dunia, nakujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo. Mmehukumu mwenye haki mkamwua; wala hashindani nanyi.” (Yakobo 5:3-6). KN 43.2

Lakini nani asomaye maonyo yaliyotolewa na dalili hizi zenye kutimia haraka za nyakati hizi? Walimwengu wanazionaje moyoni? Badiliko gani huonekana moyoni mwao? Hakuna zaidi ila moyo ule ule ulioonekana katika watu wa ulimwengu wa kale, siku za Nuhu. Kwa kushughulika sana na biashara na anasa, hata kutofikiri vingine, watu wale walioishi kabla ya gharika “wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote,’ (Mathayo 24:39). Walikuwa na maonyo yaliyotumwa kutoka mbinguni, lakini walikataa kusikiliza. Leo vile vile walimwengu hawajali hata kidogo sauti ya Mungu ya onyo. wanakwenda mbio penye uharibifu wa milele. Ulimwengu unastushwa na roho ya vita. Unabii wa sura ya kumi na moja wa Danieli karibu umefikia utimizo wake kabisa. Siku si nyingi maono ya dhiki iliyotajwa katika unabii huo yatatokea. KN 43.3

“Tazama, Bwana ameifanya dunia kuwa tupu, aifanya ukiwa, aipindua, na kuwatawanya wakaao ndani yake Kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele. Ndiyo sababu laana imeila dunia hii, na hao wanaoikaa wameonekana kuwa na hatia, ndiyo sababu watu wanaoikaa wame-teketea, watu waliosalia wakawa wachache tu Sauti ya furaha ya kinubi inakoma” (Isaya 24:1-8). “Ole wake siku hii! Kwa maana siku ya Bwana inakaribia, nayo itakuja kama uangamivu utokao kwake aliye Mwenyezi” (Yoeli 1:15). KN 44.1

“Naliiangalia nchi, na tazama, ilikuwa ukiwa, haina watu; naliziangalia mbingu, nazo zilikuwa hazina nuru. Naliiangalia milima, na tazama, ilitetemeka, na milima yote ilisogea huko na huko. Nikaangalia na tazama, hapakuwa na mtu hata mmoja, na ndege wote wa angani wamekwenda zao. Nikaangalia, na tazama, shamba lililozaa sana limekuwa ukiwa, na miji yake yote ilikuwa imebomoka” (Yeremia 4:23-26). “Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo; maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa nayo” (Yeremia 30:7). KN 44.2

Si wote ulimwenguni humu waliomwasi Mungu na kumfuata yule adui. Si wote waliochagua kutokumtii Mungu. Wako wachache walio waaminifu kwa Mungu; maana Yohana aandika: “Hapo ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu” (Ufunuo 14:12). Karibu kutakuwa vita kali baina ya wale wanaomtumikia Mungu na wale wasiomtumikia. Bado kitambo kidogo kila kitu kiwezacho kupepetwa kitapepetwa, ili vitu visivyoweza kupepetwa visalie. KN 44.3

Shetani ni mwanafunzi wa Biblia mwenye bidii. Anajua kuwa muda wake ni mfupi, naye anatafuta katika kila jambo kuzuia kazi ya Mungu duniani. Ni jambo lisilowezekana kutoa wazo lo lote kuhusu uzoefu wa watu wa Mungu ambao watakuwa hai duniani wakati utukufu wa mbinguni na kurudiwa kwa mateso ya zamani vitakapochangamana. Watatembea katika nuru itokayo kitini pa enzi pa Mungu. Kwa njia ya malaika daima kutakuwa na mawasiliano baina ya Mungu mbinguni na watu wake duniani. Naye Shetani, akizungukwa na malaika wabaya, na kujifanya kuwa yeye ni Mungu, atafanya miujiza ya kila namna, kuwadanganya yumkini, hata wateule. Usalama wa Watu wa Mungu hautapatikana katika kufanya miujiza, maana Shetani ataiga miujiza ltakayofanywa. Wakati wakishitakiwa na wakati wakijaribiwa, Watu wa Mungu watajipatia uwezo wa kusimama imara kutoka katika ishara iliyosemwa habari zake katika Kutoka 31:12-18. Yawapasa kuliamini Neno lenye uzima: “Imeandikwa.” Huu ndio msingi tu ambao juu yake wanaweza kusimama salama. Wale ambao wamevunja agano lao na Mungu siku ile watakuwa hawana Mungu wala matumaini. KN 44.4

Wenye kumwabudu Mungu watatambuliwa kwa kuiheshimu kwao amri ya nne, kwa kuwa hii ni ishara ya uwezo wa Mungu wa kuumba na ushuhuda wa madai yake juu ya kuheshimiwa na wanadamu. Waovu watabainika kwa jitihadi zao za kuvunja ukumbusho wa Muumbaji na kutukuza kile kilichoanzishwa na Rumi. Mwisho wa vita hii jamii ya Wakristo wote watagawanyika katika aina mbili kuu, wale wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu, na wale wanaomwabudu yule mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa yake. Ijapokuwa kanisa na serikali vitaunganisha nguvu zao kuwashurutisna wote, “wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa,” kupokea chapa ya mnyama, walakini watu wa Mungu hawataipokea (Ufunuo 13:16). Nabii wa Patmo anaona “wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na chapa yake, na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kando kando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu,” wakiimba wimbo wa Musa na wimbo wa Mwana-Kondoo (Ufunuo 15:2). KN 45.1

Majaribio na taabu za kutisha sana zinawangojea watu wa Mungu. Roho ya vita inayachochea mataifa kutoka upande mmoja wa nchi hata upande wa pili. Lakini katikati ya wakati huo wa dhiki ijayo,-wakati wa taabu ambayo mfano wake haujakuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati huo, – wateule wa Mungu watasimama imara. Shetani na jeshi lake hawawezi kuwangamiza maana malaika wanaowazidi nguvu watawalinda (9T 11 - 17).  KN 45.2

Sura Ya 3 - Jiweke Tayari Kukutana na Bwana

NALIONA kuwa haitupasi kuahirisha kuja kwa Bwana. Malaika amesema: “Jitayarisheni, kwa kile kinachoujia ulimwengu. Hebu matendo yenu yapatane na imani yenu.” Nikaona kuwa moyo hauna budi kukazwa kwa Mungu, na ya kuwa mvuto wetu wapaswa kuonyesha habari za Mungu, na za Neno lake la kweli. Hatuwezi kumheshimu Bwana tukiwa ovyo, tusiojali. Hatuwezi kumtukuza tukiwa tunakata tamaa. Hatuna budi kufanya bidii kwa ajili ya wokovu wa roho zetu, na kuwaongoa wengine. Jambo hili halina budi kupewa umuhimu wa kwanza ndipo mambo mengine yafuate. KN 46.1

Naliona uzuri wa mbinguni. Naliwasikia malaika wakiimba nyimbo zao za furaha, wakimpa Yesu sifa, heshima, na utukufu. Ndipo nikatambua kitu juu ya upendo wa ajabu wa Mwana wa Mungu. Aliacha utukufu na heshima yote aliyokuwa nayo mbinguni, naye alipenda sana kutuokoa hata kwa uvumilivu na upole akastahimili aibu na dharau ambayo wanadamu walimtwisha. Alijeruhiwa, akapigwa, na kuchubuliwa; aliwambwa msalabani Kalwari na kupatwa na kifo cha maumivu makuu ili kutuokoa na mauti, kusudi tupate kuoshwa katika damu yake na kuinuliwa kukaa pamoja naye katika makao anayotuandalia, kufurahishwa na nuru na utukufu wa mbinguni, kuwasikia malaika wakiimba, na kuimba pamoja nao. KN 46.2

Nikaona kuwa mbingu yote inapendezwa na habari za wokovu wetu; je sisi tunaohitaji wokovu tusijali? Je, tuidharau dhabihu ambayo imetolewa kwa ajili yetu? Wengine wamefanya jambo hili. Wamepuuza neema iliyotolewa, na ghadhabu ya Mungu inawakalia. Roho wa Mungu hatahuzunishwa daima. Ataondoka kama akizidi kusikitishwa. Baada ya kuyatenda yote ambayo Mungu angeweza kufanya kuwaokoa wanadamu, kama wakionyesha kwa mienendo yao kuwa wanaidharau rehema ya Yesu iliyotolewa, mauti itakuwa ndio fungu lao, nayo itanunuliwa kwa bei kubwa. Itakuwa mauti ya kutisha sana; kwa kuwa itawabidi kupata maumivu yale yaliyompata Kristo msalabani kuwanunulia ukombozi walioukataa. Ndipo watafahamu kile ambacho wamepoteza-uzima wa milele na urithi wa milele. Dhabihu kuu ambayo imetolewa kwa ajili ya roho zetu hutuonyesha thamani yake. Roho iliyo ya thamani kuu ikipotea, imepotea milele. KN 46.3

Nimemwona malaika akisimama na mizani mikononi mwake akiyapima mawazo na mioyo ya watu wa Mungu, hasa vijana. Upande mmoja wa mizani palikuwa na mawazo na moyo uelekeao mbinguni; Upande mwingine palikuwa na mawazo na moyo uelekeao duniani. Na katika mizani hii palitupwa vitabu vyote vya hadithi vya kusoma, mawazo ya mavazi na umalidadi, majivuno, kiburi, na kadhalika. Ni wasaa wa kutisha kama nini! Malaika wa Mungu wakisimama na mizani, wakipima mawazo ya watoto wanaojidai kuwa wake Mungu-wenye kujidai kuwa wamezifia anasa za duniani ili kuishi kwa Mungu. Mizani iliyojaa mawazo ya kidunia, kiburi na majivuno mara ikashuka chini, ijapokuwa uzito wa vitu kimoja kimoja ulikuwa ukimwagika kutoka mizani hiyo. Ile yenye mawazo na moyo wa kuelekea mbinguni ikapanda juu kadin upande mwingine wa mizani ulivyoshuka, ulikuwa mwepesi kama nini! Naweza kueleza neno hili kama nilivyoona; lakini kamwe siwezi kutoa maoni kamili yaliyoniingia moyoni mwangu, nikiona malaika akiwa na mizani akiyapima mawazo na mioyo ya watu wa Mungu. Malaika akasema: “Je hawa waweza kuingia mbinguni? La, hasha, kamwe hawawezi. Waambie matumaini waliyo nayo sasa ni bure, na kama hawatatubu haraka, na kupata wokovu, lazima watapotea.” KN 46.4

Mfano wa utauwa nauwezi kumwokoa ye yote. Wote hawana budi kuwa na uzoefu wa uhusiano wa karibu sana na Yesu. Hili tu ndilo litakalowaokoa wakati wa taabu. Ndipo kazi yao itajaribiwa na kuonekana ni ya aina gani; na kama ni dhahabu, fedha, na vito vya thamani, watasitiriwa mahali pa siri pa hema ya Bwana, Lakini kama kazi yao ni mti, majani makavu, na mabua, hakuna cho chote kiwezacho kuwakinga wasipatwe na ukali wa ghadhabu ya Yehova. KN 47.1

Naliona kuwa wengi walijipima wao kwa wao, na kuyalinganisha maisha yao na maisha ya wengine. Haipaswi kuwa hivyo. Hakuna mwingine ila Kristo tuliyepewa awe kielelezo. Ndiye Kielelezo chetu halisi, na kila mmoja apaswa kufanya bidii sana kumwiga Kristo. Tu watenda kazi pamoja na Kristo, kama sivyo, tu watenda kazi pamoja na yule adui. Tunakusanya pamoja na Kristo ama tunatawanya. Tu Wakristo wema, wanyofu, ama sisi si Wakristo hata kidogo. Kristo anasema: “Hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu” (Ufunuo 3:15, 16). KN 47.2

Naliona kuwa wengine walikuwa hawajajua maana ya kujikana nafsi au kujinyima, au maana ya kuteseka kwa ajili ya neno la kweli. Lakini hakuna atakayeingia mbinguni pasipo kujinyima. Moyo wa kujikana nafsi na kujinyima wapasa kuthaminiwa. Wengine hawajitoi dhabihu miili yao wenyewe, madhabahuni mwa Mungu. Wanajifurahisha kwa moyo wa kigeugeu, mara kushika mara kuacha, na kuziridhisha tamaa zao za chakula, na kutimiza mapenzi yao wenyewe, bila kuijali kazi ya Mungu. Wale wenye kukubali kujinyima kitu kiwacho chote kwa ajili ya uzima wa milele wataupata; nao utakuwa kitu kistahilicho kuumia ili kukipata, cha kustahili kuiisulibisha nafsi kwa ajili yake, na kuacha miungu yote kwa ajili yake. Utukufu mwingi mno wa milele humeza kila kitu na kushinda anasa zote za dunia (IT 123-126). 

Sura ya 4 - Umoja na Kristo na Upendo wa Kindugu

(Mmoja na Kristo kwa Mungu)

MUNGU amekusudia kuwa watoto wake wapatane katika umoja. Je, hawatazamii kuishi pamoja katika mbingu moja? Je, Kristo amegawanyika? Je atawapa watu wake ushindi kabla ya watenda kazi, kwa nia moja, kutoa wakfu mioyo, akili na nguvu kwa kazi takatifu sana machoni pa Mungu? Umoja ni nguvu; utangano ni udhaifu. Tukiwa na umoja sisi kwa sisi, tukishirikiana kazini kwa moyo mmoja kwa ajili ya wokovu wa watu, tutakuwa kweli “wafanya kazi pamoja na Mungu.” Wale wanaokataa kufanya kazi kwa uelewano wanamwaibisha sana Mungu. Yule adui wa roho za watu hupendezwa kuona wakifanya kazi kwa kupishana. Watu kama hao huhitaji kukuza upendo wa kindugu na unyenyekevu wa moyo. Kama wangeweza kufungua pazia lisetirilo mambo ya wakati ujao na kuona matokeo ya baadaye ya kufarakana kwao hakika wangeona haja ya kutubu. 1 

Umoja na Kristo na Umoja Baina Yetu Ndio Usalama Wetu

Walimwengu wanapendezwa kuona mafarakano miongoni mwa Wakristo. Wasioamini wanapendezwa sana. Mungu anahitaji watu wake wabadilike. Umoja na Kristo na umoja baina yetu ndio usalama wetu siku hizi za mwisho. Tusimpe nafasi shetani kuwasonda vidole washiriki wetu wa kanisa, akisema: “Tazama jinsi watu hawa, wasimamao chini ya bendera ya Kristo, wanavyochukiana. Hatuna sababu ya kuwaogopa wakiwa wanatumia nguvu nyingi zaidi kugombana wao kwa wao kuliko wanayoitumia vitani kupigana na majeshi yangu.” KN 49.2

Baada ya kushuka kwa Roho Mtakatifu wanafunzi walitawanyika kuhubiri habari za Mwokozi aliyefufuka, shauku yao ilikuwa moja tu, wokovu wa roho za watu. Walifurahia utamu wa ushirika wa watakatifu. Walikuwa wenye upendo, waangalifu, wenye kujikana nafsi, walio tayari kujinyima cho chote kwa ajili ya kweli. Katika kushirikiana wao kwa wao kila siku waliudhihirisha upendo ambao Kristo alikuwa amewaamuru kuuonyesha. Kwa maneno ya ukarimu, na matendo mema walijitahidi kuwasha upendo huu mioyoni mwa wengine. KN 49.3

Waumini walipaswa daima kuufurahia upendo uliojaza mioyo ya mitume baada ya kushukiwa na Roho Mtakatifu. Walipaswa kusonga mbele kwa utii wa hiari ya moyo kwa ile amri mpya: “Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo” (Yohana 13:34). Hivyo walipaswa kuungwa katika umoja na Kristo ili wapate kuwezeshwa kuyatimiza matakwa yake. Uwezo wa Mwokozi ambaye angeweza kuwahesabia haki kwa haki yake ulikuwa hauna budi kukuzwa. KN 50.1

Lakini wale Wakristo wa kwanza wakaanza kutafutana makosa. Kwa kutumia muda wao katika kukosoana, kutoa nafasi kwa lawama zisizo na huruma, wakashindwa kumwona Mwokozi na upendo mkuu aliokuwa amewafunulia wenye dhambi. Wakawa wakali zaidi kwa habari za kawaida za matendo ya dini ya nje, hasa juu ya kanuni za imani, wakazidi sana kuwa wakali katika ukosoaji wao. Katika jitihada zao kuwahukumu wengine wakasahau makosa yao wenyewe. Wakasahau fundisho la upendo wa kindugu ambalo Kristo alikuwa amewafundisha. Na jambo la kusikitisha kuliko yote, walikuwa hawafahamu upotevu wao. Hawakujua kwamba furaha na raha zilikuwa zikiondoka maishani mwao, na ya kuwa punde wangetembea gizani, wakiwa wameufungia upendo wa Mungu nje ya mioyoni mwao. KN 50.2

Mtume Yohana alifahamu kuwa upendo wa kindugu ulikuwa ukipungua kanisani, naye alikazia hasa juu ya jambo hili. Mpaka siku ya kufa kwake aliwasihi waumini kuonyesha daima kupendana wao kwa wao. Nyaraka zake kwa makanisa zinajaa wazo hili. Ameandika, “Wapenzi, na tupendane; kwa kuwa pendo ni la Mungu Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni ili tupate uzima kwa yeye Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana” (1 Yohana 4:7-11). KN 50.3

Katika kanisa la Mungu siku hizi upendo wa kindugu unakosekana sana. Wengi wa wale wanaodai kuwa wanampenda Mwokozi hawawapendi wale ambao wanaungana nao katika ushirika wa Kikristo. Tu watu wa dini moja, watu wa nyumba moja, wote watoto wa Baba, yule yule mmoja wa mbinguni, wenye tumaini lile lile la baraka la kutokufa. Basi kifungo kinachotufunga pamoja kingekuwa imara na cha upendo kama nini! Walimwengu wanatutazama kuona kama imani yetu inatoa mvuto unaotakasa juu ya mioyo yetu. Ni wepesi kuona kila kosa katika mienendo yetu, kutokupatana ko kote katika matendo yetu. Hebu tusiwape nafasi kuilaumu dini yetu. 2 

Mapatano na Umoja Ndiyo Ushuhuda Wetu Wenye Nguvu Sana

Siyo upinzani wa walimwengu unaotuhatarisha zaidi; bali maovu yanayofurahiwa na kutunzwa mioyoni mwa waumini ndiyo yanayoleta maangamizi makubwa na kuzuia sana maendeleo ya kazi ya Mungu. Hakuna njia nyingine ya hakika zaidi ya kuidhoofisha hali yetu ya kiroho kuliko kuwa na wivu, kutuhumiana, kujawa na roho ya kutafutana makosa na kudhaniana maovu. “Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani. Maana hapo palipo wivu na ugomvi, ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya. Lakini itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki. Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani” (Yakobo 3:15-18). KN 51.1

Mapatano na umoja ukiwapo miongoni mwa watu wenye tabia mbalimbali ni ushuhuda wenye nguvu sana uwezao kuonyesha kwamba Mungu amemtuma Mwanawe ulimwenguni kuwaokoa wenye dhambi. Tumepewa fursa ya kutoa ushuhuda huu. Lakini, ili kufanya hili hatuna budi kujitia chini ya amri ya Kristo. Tabia zetu hazina budi kuumbwa kupatana na tabia yake, nia zapaswa kutiwa chini ya nia yake. Ndipo tutafanya kazi pamoja pasipo kugongana hata kidogo. KN 51.2

Tofauti ndogo zinazopong’ang’aniwa sana huleta vitendo ambavyo huharibu ushirika wa Kikristo. Tusikubali kumnufaisha adui kwa udhaifu wetu huu. Tuzidi kumkaribia Mungu zaidi na kukaribiana sisi kwa sisi. Ndipo tutakuwa kama miti ya haki, iliyopandwa na Bwana, na kunyweshwa na mto wa maji ya uzima. Nasi tutakuwa wenye kuzaa matunda kwa wingi ajabu iliyoje! Je Kristo hakusema: “Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana” (Yohana 15:8). KN 51.3

Sala ya Kristo ikisadikiwa kabisa, mafundisho yake yakiingizwa katika maisha ya kila siku ya watu wa Mungu, umoja wa utendaji utaonekana katika watu wa ngazi zote. Ndugu atafungamanishwa na ndugu kwa vifungo vizuri vya thamani vya upendo wa Kristo. Roho wa Mungu peke yake ndiye awezaye kuleta umoja huu. Yeye aliyejitakasa aweza kuwatakasa wanafunzi wake. Wakiwa na umoja naye, watakuwa na umoja wao kwa wao katika imani takatifu sana. Tukijitahidi kwa ajili ya umoja huu kama Mungu anavyotaka sana kujitahidi kwa ajili yake, tutaupata. 3 KN 51.4

Siyo wingi wa sheria, majengo makubwa na kujionyesha kwa nje ambavyo Mungu anavihitaji bali utendaji kwa moyo wa maelewano wa watu wa pekee, watu wa thamani waliochaguliwa na Bwana waliungana wao kwa wao, ambao uzima wao umefichwa pamoja na Kristo kwa Mungu. Kila mtu anapaswa mwenyewe kusimama mahali pake, akitoa mvuto mzuri katika wazo, neno; na tendo. Watenda kazi wote wa Mungu wakifanya hili, na mpaka hapo tu, ndipo kazi yake itakamilika, na yote kuwa sawa. 4 KN 52.1

Mungu anahitaji watu wa imani kamili na akili bora wenye kutofautisha dhahiri kati ya kweli na uwongo. Kila mmoja anapaswa kujihadhari, akijifunza na kuyatumia mafundisho yaliyotolewa katika sura ya kumi na saba ya Yohana, na kulinda imani yenye nguvu katika ukweli wa wakati huu. Tunahitaji kujitawala ambako kutatuwezesha kuenenda sawasawa na ombi la Kristo. 5 KN 52.2

Moyo wa Mwokozi hufikiri juu ya wafuasi wake kutimiza kusudi la Mungu lote, kimo na kina chake pia. Yawapasa kuwa na umoja katika Yeye, ijapokuwa wametawanyika ulimwenguni. Lakini Mungu hawezi kuwafanya kuwa wamoja katika Kristo isipokuwa kama watakubali kuachana na njia yao wenyewe na kuifuata njia ya njia Kristo. 6 KN 52.3
 

Ushirika

Katika kuanzisha taasisi za kazi mahali papya mara nyingi hulazimu kuweka kazi za madaraka kwa watu ambao hawaielewi kazi hii kinagaubaga. Watu hawa hufanya kazi na kuleta hasara kubwa, na kama wao na watenda kazi wenzao hawatakuwa na moyo wa kufikiri wengine kuliko nafsi zao wenyewe katika kazi ya Mungu, patakuwako matokeo ya hali ya mambo ambayo yatazuia mafanikio yake. KN 52.4

Wengi huona kuwa aina ya kazi wanayoifanya ni yao wenyewe na ya kuwa hakuna mtu mwingine apaswaye kutoa shauri lolote kuhusu uboreshaji wa utendaji wao. Yawezekana watu hawa wakawa hawana uelewa kabisa juu ya kazi yao, lakini kama mtu akithubutu kuwapa shauri jema, hukasirika na kunuia kufuata waonavyo wao wenyewe. Tena, watenda kazi wengine hawakubali kusaidia au kuwafundisha watenda kazi wenzao. Wengine wasio na uzoefu hawataki kutokujua kwao kujulikane. Wanafanya makosa, wakipoteza wakati mwingi na vifaa, kwa sababu wanajivuna sana kiasi kwamba hawawezi kutaka shauri kwa mwingine. KN 52.5

Asili ya shida hii sio jambo gumu kuligundua. Watenda kazi wamekuwa nyuzi zinazojitegemea, wakati ambapo wanapaswa kujihesabu kama nyuzi ambazo hazina budi kusokotwa pamoja kusaidia kufanya kielelezo. KN 52.6

Mambo haya humhuzunisha Roho Mtakatifu. Mungu anataka kila mmoja awe radhi kujifunza toka kwa mwenzake. Kujitegemea kusiko safi hutuweka mahali ambapo Mungu hawezi kufanya kazi pamoja nasi. Hali ya mambo ikiwa hivi Shetani hupendezwa sana. KN 53.1

Kila mtenda kazi atapimwa ili kuona kama utendaji wake ni kwa manufaa ya kazi ya Mungu, au kwa kujinufaisha mwenyewe. KN 53.2

Dhambi ambayo karibia hakuna matumaini ya kuiondoa na inakaribia kabisa kutotibika ni kiburi cha mawazo na majivuno. Hii huzuia ukuaji wote. Mtu akiwa na kasoro kitabia, lakini akakosa kulifahamu jambo hili; akiwa amejawa na kujitosheleza kiasi kwamba hawezi kuona makosa yake atawezaje kusaflshwa? “Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi” (Mathayo 9:12). Mtu anawezaje mtu kuboresha hali yake ya kiroho wakati anadhani kuwa njia zake ni kamilifu? KN 53.3

Mkristo mwenye moyo mkamilifu ndiye tu anayeweza kuwa mwungwana halisi. 7 

Sura ya 5 - Kristo Haki Yetu

“TUKIZIUNGAMA dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote” (1 Yohana 1:9). KN 54.1

Mungu anataka tuziungame dhambi zetu, na kunyenyekea kumtumaini kama baba mwenye upendo ambaye hatawatupa wale ambao wanamtumainia. Wengi wetu tunaenenda kwa kuona kwa macho, wala siyo kwa imani. Tunayaamini mambo yale tuyaonayo, lakini hatuzithamini ahadi za thamani tulizopewa katika neno la Mungu; lakini hatuwezi kumwaibisha Mungu kwa makusudi zaidi ya kuonyesha kwamba hatuamini asemalo, na kuuliza kama Mungu ni mwaminifu kwetu sisi au anatudanganya. KN 54.2

Mungu hatuachi kwa sababu ya dhambi zetu. Pengine tunaweza kufanya makosa, na kumhuzunisha Roho wake; lakini tukitubu, na kumwendea kwa mioyo yenye toba, hatatufukuza. Viko vipingamizi vipaswavyo kuondolewa. Moyo mbaya umekuwapo, na pamekuwapo na kiburi, majivuno, kutosubiri, na manung’uniko. Haya yote hututenga na Mungu. Dhambi hazina budi kuungamwa, yapasa pawepo kazi kubwa yenye kina ya neema moyoni. Wale wanaojiona dhaifu na waliokata tamaa waweza kuwa watu wa Mungu wenye nguvu, na kufanya kazi bora kwa Bwana. Lakini hawana budi kufanya kazi kutoka kwa fikra za juu; hawana budi kuepukana na mvuto wa nia ya kujifikiri nafsi mwenyewe bila kujali wengine. KN 54.3

Yatupasa kujifunza katika shule ya Kristo. Hakuna kitu kingine ila haki yake tu ambayo ndiyo iwezayo kutupa haki ya mmojawapo wa mibaraka ya agano la neema. Tumetamani kwa muda mrefu na kujaribu kuipata mibaraka hii, lakini hatukuipokea, kwa sababu tumependelea wazo kwamba tungeweza kufanya kitu kutustahilisha mibaraka hiyo. Hatukuacha kujitazama wenyewe, na kuamini kuwa Yesu ni Mwokozi aliye hai. Haitupasi kufikiri kuwa neema yetu wenyewe na sifa zetu njema zitatuokoa; neema ya Kristo ndilo tu tumaini letu la wokovu. Kwa njia ya nabii wake Bwana anaahidi, “Mtu mbaya na aache njia yake na mtu asiye haki aache mawazo yake; na amrudie Bwana, naye atamrehemu; na arejee kwa Mungu wetu, naye atamsamehe kabisa” (Isaya 55:7). Yatupasa kuiamini ahadi kama ilivyo, wala siyo kukubali maoni ya moyoni kwa imani. Tukimwamini Mungu kabisa, tunapotegemea juu ya sifa njema za Yesu kama Mwokozi mwenye kusamehe dhambi, tutapokea msaada wote tutakaouhitaji. Tunajitazama nafsi, kana kwamba tunaweza kujiokoa nafsi zetu wenyewe; lakini Yesu alitufilia kwa sababu sisi wenyewe hatuwezi kujiokoa. Tumaini letu , pamoja na haki yetu viko kwake. Hatupaswi kukata tamaa, na kuogopa kwamba hatuna wa kutuokoa, au kwamba hakusudii kuturehemu. Wakati huu anapoendesha kazi yake kwa ajili yetu, anatualika kumwendea katika hali yetu dhaifu, bila msaada, tukaokolewe. Tunamtweza kwa kutokuamini kwetu. Ni jambo la kushangaza jinsi tunavyomtendea huyu Rafiki yetu mkubwa, jinsi tumaini letu lilivyo kidogo kwake yeye ambaye aweza kutuokoa kabisa, na ambaye ametupa kila jambo lionyeshalo upendo wake mkuu. KN 54.4

Ndugu zangu, mnatazamia kuwa tabia yenu nzuri itawashuhudia mpate kibali kwa Mungu, mkifikiri kuwa kwanza hamna budi kuachana na dhambi kabla ya kuuamini uwezo wake wa kuokoa? Kama haya ndiyo mashindano yanayoendelea mioyoni mwenu, hamtapata nguvu, na mwishowe mtakata tamaa. KN 55.1

Jangwani, wakati Bwana alipowaruhusu nyoka wenye sumu kuwauma Waisraeli walioasi, Musa aliagizwa kuinua nyoka wa shaba nyeupe, na kuwaamuru wote waliojeruhiwa kumwangalia ili wapate kupona. Lakini wengi hawakuona msaada katika dawa hii iliyoamriwa na Mungu. Maiti na watu waliokuwa katika hali ya kufa waliwazunguka pande zote, nao wakajua kuwa pasipo msaada wa Mungu hakika watakufa; lakini walilia na kuomboleza kwa sababu ya majeraha yao, maumivu yao, mauti yao mpaka wameishiwa na nguvu zao, na macho yao yamegeuka kama ya mtu kifoni, wakati ambapo wangeweza kuponywa mara moja kama wangemtazama yule nyoka. KN 55.2

“Kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika Yeye.” Kama unafahamu dhambi zako, usizitumie nguvu zako zote kuomboleza juu yake, bali tazama upate kuponywa. Yesu ndiye Mwokozi wetu peke yake; na ijapokuwa mamilioni wenye kuhitaji kuponywa watakataa rehema yake iliyotolewa, hakuna mtu ambaye ataamini sifa njema za Kristo atakayeachwa apotee. Kwa kuwa tunajua kwamba bila Kristo maishani tu wadhaifu sana, haitupasi kukata tamaa; inatupasa kumtegemea Mwokozi aliyesulibiwa na kufufuka. Jipe moyo maskini, mgonjwa wa dhambi, ulioyekata tamaa, tazama upate kuponywa. Yesu ameahidi katika neno lake ya kuwa atawaokoa wote wanaomwendea. KN 55.3

Njoo kwa Yesu, na upate pumziko na amani. Unaweza kupata mbaraka hata sasa. Shetani anakushauri kuwa u mdhaifu, bila msaada, na huwezi kujibariki mwenyewe. Ni kweli; u mdhaifu. Lakini mwinue Yesu mbele ya Shetani: “Ninaye Mwokozi aliyefufuka katika wafu. Namwamini, hataniacha nishindwe. Katika jina lake nitashinda. Ndiye haki yangu, na taji iletayo shangwe.” Pasiwepo mtu hata mmoja hapa anayeona moyoni kuwa hali yake haina matumaini; kwa kuwa sivyo ilivyo. Waweza kuona kwamba u mwenye dhambi na mpotevu; lakini hii ndiyo sababu unahitaji Mwokozi. Kama unazo dhambi za kuungama, usipoteze wakati. Dakika hizi ni za thamani kuu. “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote” (1 Yohana 1:9). Wale wenye njaa na kiu ya haki watajazwa; maana Yesu ameahidi hilo. Mwokozi wa ajabu! Mikono yake imekunjuliwa kutupokea, na moyo wake mkuu wa upendo unangojea kutubariki. KN 56.1

Wengine huelekea kuona moyoni kwamba hawana budi kuangaliwa waonekane kama wanafaa au hawafai, na ya kuwa hawana budi kuthibitisha kwa Bwana kuwa wameongoka, kabla hawajaweza kudai mbaraka wake. Lakini watu hawa wa thamani wanaweza kuudai mbaraka wake hata sasa. Yawapasa wapate neema yake, Roho wa Kristo, atakayewasaidia katika udhaifu wao, ama sivyo hawawezi kukuza tabia ya Kikristo. Yesu anapenda tumwendee, hivi tulivyo-wenye dhambi, wadhaifu, wasiojitegemea. KN 56.2

Toba, na msamaha pia, ni vipawa vya Mungu kwa njia ya Kristo. Ni kwa njia ya mvuto wa Roho Mtakatifu tunawezeshwa kuona hatia ya dhambi, na kuiona haja yetu ya msamaha. Wenye masikitiko kwa ajili ya makosa yao, na wala si wengine, ndio wanaosamehewa; lakini neema ya Mungu ndiyo inayoufanya moyo utubu. Anajua udhaifu wetu wote na upungufu, naye atatusaidia. KN 56.3

Wengine wanaomwendea Mungu kwa kutubu na kuungama na hata kuamini kuwa dhambi zao zimesamehewa, wangali wanakosa kudai, kama wapaswavyo, ahadi za Mungu. Hawaoni kuwa Yesu ni Mwokozi aliyehai daima; nao hawako tayari kukabidhi roho zao kwake azilinde na kumtegemea kuikamilisha kazi ya neema iliyoanzwa mioyoni mwao. Huku wakidhani wanajikabidhi kwa Mungu, wanajitegemea nafsi wenyewe zaidi. Ni wenye bidii wanaomwamini Mungu kwa sehemu na kwa sehemu kujiamini wenyewe. Hawamwangalii Mungu, kuwekewa uwezo wake, bali hutegemea kujihadhari na vishawishi, na kutenda wajibu fulani ili awakubaliwa. Hakuna ushindi katika imani ya namna hii. Watu wa jinsi hii husumbuka bure, bila kuwa na kusudi; roho zao daima ziko kifungoni, nao hawatapata pumziko hadi watakapoweka mizigo yao miguuni pa Yesu. KN 56.4

Kuna haja ya uangalifu wa daima, uaminifu, na uchaji wa upendo; lakini mambo haya yatakuja yenyewe wakati moyo wa mtu unapowekewa uwezo wa Mungu kwa njia ya imani. Hatuwezi kufanya lo lote, hata kidogo, kujistahilisha kupata kibali cha Mungu. Haitupasi kujitegemea hata kidogo wala kuyategemea matendo yetu mema; lakini kama wakosaji, wenye dhambi tukimwendea Kristo, twaweza kupata pumziko katika pendo lake. Mungu atampokea kila mmoja amwendeaye akiamini kabisa sifa njema za Mwokozi aliyesulibishwa. Upendo hutokea moyoni. Pengine hapawezi kuwapo kipindi cha kuona furaha moyoni, lakini kuna tumaini lidumulo la amani. Kila mzigo ni mwepesi. Kazi inakuwa furaha, na dhabihu jambo la kupendeza. Njia ambayo zamani ilionekana kama ilifunikwa gizani huwa safi ing’aayo kwa mionzi ya nuru itokayo kwa Jua la Haki. Huku ndiko kuenenda katika nuru kama Kristo alivyo katikanuru.


Sura ya 6 - Maisha Matakatifu

MWOKOZI wetu hudai vyote tulivyo navyo; anataka mawazo yetu ya kwanza yawe matakatifu sana, upendo wa ndani ulio safi kabisa. Kama tu washiriki kwa kweli wa tabia ya Mungu, tutamsifu daima mioyoni mwetu na kwa vinywa vyetu. Usalama wetu tu ni kumtolea vyote tulivyo navyo, na kudumu kukua katika neema na katika kuijua kweli. 1 KN 58.1

Utakaso ulioelezwa katika Maandiko Matakatifu unahusu mwili mzima-moyo, roho, na mwili. Hili ndilo wazo halisi la kujitoa wakfu kabisa. Paulo huomba dua kusudi kanisa la Thesalonike lipate kuufaidi mbaraka huu mkuu. “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo” (1 Wathesalonike 5:23). KN 58.2

Katika jamii ya watu wa dini, yako mafundisho ya utakaso ambayo ni ya uwongo na ya hatari kwa mvuto wake. Mara nyingi wenye kukiri utakaso huu hawana kitu halisi walichoshikilia. Utakaso wao ni mazungumzo na ibada potovu. KN 58.3

Huacha kutumia akili na busara, kutegemea hisia zao, wakijenga msingi wa madai yao ya utakaso katika msisimko ambao wamewahi kuupata. Ni wakaidi na wapotoshaji katika kusisitiza kauli za madai yao ya utakatifu, wakitoa maneno mengi, lakini yasiyo na matunda ya thamani kama uthibitisho. Watu hawa wenye kujidai kuwa ni watakatifu licha ya kujidanganya nafsi zao wenyewe kwa maneno yao ya hila, hata hutoa mvuto kuwapotosha wengi ambao hutaka sana kwa uaminifu kutii mapenzi ya Mungu. Wanaweza kusikika wakirudia tena na tena kusema, “Mungu aniongoza, Mungu ananifundisha! Naishi pasipo dhambi!” Wengi wakutanao na roho hii hupambana na giza, jambo wasiloweza kulifahamu. Lakini hilo nailo lililo kinyume hasa cha Kristo, ambaye ni Kielelezo cha kweli peke yake. 2 KN 58.4

Utakaso ni kazi ya kuendelea daima. Hatua moja moja zimewekwa mbele yetu katika maneno ya Petro: “Mkijitahidi sana wema wenu maarifa, na katika maarifa yenu kiasi na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa, na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.” (2 Petro 1:5-8). “Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe. Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuingia katika ufalme wa milele wa Bwana wetu, Mwokozi wetu Yesu kristo” (mafungu 10:11). KN 58.5

Hii ni njia ambayo kwayo twaweza kujihakikishia kuwa kamwe hatutaanguka. Wale ambao huufanyia kazi mpango huu wa ongezeko la kuzipata sifa njema za Kristo wameahidiwa kuwa Mungu atatekeleza mpango wa kuwazidishia katika kuwakarimia karama za roho wake. 3 KN 59.1

Utakazo si kazi ya punde tu, saa moja au siku moja. Ni kukua daima katika neema. Hatuwezi kujua leo jinsi mashindano yetu yatakavyokuwa magumu kesho. Shetani yu hai, naye ana bidii, na kila siku yatupasa kumlilia Mungu kwa bidii atupe msaada na nguvu ya kushindana naye. Ili mradi Shetani yu kazini tutakuwa na kazi ya kuitiisha nafsi, mashambulio ya kuyashinda, na hakuna kituo, hakuna mahali tuwezapo kuflka tukasema tumefikia mwisho kabisa. KN 59.2

Maisha ya Mkristo ni kusonga mbele daima. Yesu amekaa kama mtakasaji na msafishaji wa watu wake; na sura yake ikirudishwa ndani yao mithili ya nuru, ni wakamilifu na watakatifu, na walio tayari kuhamishwa kutoka ulimwengu huu. Mkristo anayo kazi kubwa. Tumeonywa kujitakasa na kuachana na uchafu wote wa mwili, na roho, utakatifu kamili katika kicho cha Mungu. Hapa twaona ilipo kazi kubwa. Kuna kazi ya daima kwa Mkristo. Kila tawi katika shina la mzabibu halina budi kutwaa uzima na nguvu kutoka katika mzabibu huo, ili kuzaa matunda. 4 KN 59.3

Pasiwepo watu wanaojidanganya wenyewe kwa kuamini kuwa Mungu atawasamehe na kuwabariki wakiwa wanakanyaga mojawapo la masharti yake. Utendaji wa dhambi inayofahamika wa makusuai huinyamazisha sauti ya ushuhuda ya Roho nao huitenga roho ya mtu na Mungu. Ijapokuwa hali ya kujaa furaha ya dini moyoni iwe ya namna gani, Yesu hawezi kukaa katika moyo usiojali sheria ya Mungu. Mungu atawaheshimu wale tu wanaomheshimu. 5 KN 59.4

Paulo alipoandika, “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa” (1 Wathesalonike 5:23), hakuwaonya ndugu zake kulenga kwenye kipimo ambacho hawawezi kukifikia; hakuomba kwamba wapate mibaraka ambayo haikuwa mapenzi ya Mungu kuitoa. Alijua kuwa wote ambao wangefanywa wafae kumlaki Kristo kwa amani hawana budi kuwa na tabia safi na takatifu. (Soma 1 Kor. 9:25-27; 1 Kor. 6:19, 20). KN 59.5

Kanuni ya Mkristo wa kweli haitaacha kupima uzito wa maana ya mambo. Haiulizi, watu watanifikiria nini kama nikifanya jambo hili? Au, Itakuwa na matokeo gani ya baadaye katika maelekeo yangu ya kidunia kama nikifanya hivyo? Kwa tamaa nyingi sana watoto wa Mungu wana hamu kujua angependa wafanye nini, kusudi matendo yao yapate kumtukuza. Mungu ametayarisha mengi ili mioyo na mienendo ya wafuasi wake wote iweze kutawaliwa na neema ya Mungu ili wapate kuwa kama nuru ziwakazo na kung’aa ulimwenguni. 6 

Mambo Halisi Yaonyeshayo Utakaso

Mwokozi wetu alikuwa nuru ya ulimwengu, lakini ulimwengu haukumtambua. Daima alitumika katika kazi za rehema, akitoa nuru katika njia ya wote; lakini hakuwaita wale walioingiliana naye kutazama maadili yake yasiyo na kifani, kujikana nafsi kwake, kujinyima, na wema wake. Wayahudi hawakuyasifu maisha ya namna hii. Waliihesabu dini yake kuwa isiyo na maana, kwa sababu haikupatana na kipimo chao cha uchaji wa Mungu. Wakaamua kuwa Kristo hakuwa mtu wa dini katika moyo au tabia; maana dini yao ilikuwa ya kutakabari, katika kusali hadharani mwa watu, na katika kufanya matendo ya kupenda wengine na kuwafadhili. KN 60.1

Tunda la thamani iliyo kuu la utakaso ni sifa njema ya upole. Uzuri huu ukitawala rohoni mwa mtu, tabia hufanyizwa kwa mvuto wake. Ndipo huwapo daima kumngojea Mungu na kuitiisha nia chini ya nia yake. KN 60.2

Kujikana nafsi, kujitoa dhabihu, wema fadhili, upendo uvumilivu, uhodari, na matumaini ya Mkristo ni matunda ya kila siku yazaliwayo na wale ambao wanahusiana kwa kweli na Mungu. Yawezekana matendo vao yasitangazwe kwa walimwengu, lakini wao wenyewe kila siku wanashindana na mwovu, na kujipatia ushindi wa thamani kuu juu ya majaribu na mabaya. Ahadi nzito hufanywa upya, na kutimizwa kwa nguvu zinazopatikana kwa kuomba kwa bidii na kukesha daima. Mwenye shauku haoni mashindano ya hawa watenda kazi walio kimya lakini jicho lake Yeye ambaye huona siri za moyoni, huona na kukubali kila jitihada itolewayo kwa unyenyekevu na upole. Sharti kupitia saa ya kujaribiwa ili kudhihirisha dhahabu safi ya upendo na imani katika tabia. Taabu na mashaka yanapolipata kanisa, ndipo bidii zisizolegea na upendo mkubwa wa wafuasi wa kweli wa Kristo hukuzwa. KN 60.3

Wote wanaoingia katika milki yake (mtu wa kweli wa dini) hutambua uzuri na harufu nzuri ya maisha yake ya Kikristo, hali yeye mwenyewe hafahamu, maana hupatana na mazoea yake na maelekeo yake. Huomba kwa ajili ya nuru ya mbinguni, na hupenda kuenenda katika nuru hiyo. Ni chakula na kinywaji chake kuyafanya mapenzi ya Baba yake aliye mbinguni. Uhai wake umefichwa na Kristo ndani ya Mungu; lakini hajisifu kwa hili, wala haonekani kulitambua. Mungu hufurahia wanyenyekevu na wenye kujidhili ambao hufuata kabisa nyayo za Bwana. Malaika huvutwa kwao, na hupenda kukaa muda mrefu njiani mwao. Wanaweza kupitwa kando kama wasiostahili kutambuliwa na wale ambao hujikweza na wenye kuyatukuza matendo yao mema, lakini malaika wa mbinguni huinama kwa upendo juu yao nao ni kama boma la moto kuwazunguka. 7

Danieli-Kielelezo cha Maisha Matakatifu

Maisha ya Danieli ni kielezo kilichovuviwa cha mambo yanayofanya tabia kuwa takatifu. Yanatoa fundisho kwa wote, na hasa kwa vijana. Msimamo mkali katika kupatana kabisa na matakwa ya Mungu ni wa manufaa kwa afya ya mwili na akili. Ili kuufikia upeo wa tabia ya moyoni na wa mafanikia ya kiakili, ni lazima kutafuta hekima na nguvu kutoka kwa Mungu na kuwa na kiasi katika mazoea yote ya maisha. 8 KN 61.1

Kadiri tabia ya Danieli ilivyozidi kuwa isiyo na lawama, ndivyo chuki ilivyozidi kuamshwa juu yake na adui zake. Walijawa na hasira hata kupotewa na akili, kwa sababu hawakuweza kupata neno katika tabia yake ya moyoni au katika namna yake ya kufanya kazi zake la kuwafanya wamnung’unikie. “Ndipo wale wakasema, hatutapata sababu ya kumshtaki Danieli huyo, tusipoipata katika mambo ya sheria ya Mungu wake.” (Danieli 6:5). KN 61.2

Fundisho kubwa kama nini limetolewa hapa kwa ajili ya Wakristo wote. Macho makali ya wivu yalikazwa kwa Danieli siku kwa siku; kutazama kwao kulitiwa makali na chuki; lakini hakuna neno wala tendo waliloweza kulihesabu kuwa kosa. Na hata hivyo hakujidai kutakaswa, bali alifanya kile kilicho bora sana-aliishi maisha ya uaminifu na ya kujitoa wakfu. KN 61.3

Amri inatolewa na mfalme. Danieli afahamu kusudi la maadui zake kumwangamiza. Lakini habadili njia yake hata kwa jambo moja. Kwa utulivu anafanya kazi zake alivyozoea, na saa ya kusali anaenda chumbani mwake, na madirisha yake yakiwa yamefunguka wazi kuelekea upande wa Yerusalemu, anaomba dua zake kwa Mungu wa mbinguni. Kwa njia yake hii ya kutenda mambo alionyesha kwa ujasiri kuwa hakuna mamlaka yo yote ya kidunia yenye haki kuingilia baina yake na Mungu wake na kumwambia nam wa kumwomba ama nani wa kutokumwomba. Mwangalieni huyu mtu mwenye cheo kikubwa anayeishi kulingana na kanuni za Mungu! Anasimama mbele ya walimwengu leo kama kielelezo cha ujasiri wa Kikristo na uaminifu. Anamgeukia Mungu kwa moyo wake wote, ijapokuwa anajua kuwa mauti ndiyo adhabu ya uchaji wake kwa Mungu. “Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danieli, wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danieli, Mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya.” (Fungu 16). KN 61.4

Asubuhi mapema mfalme akaenda haraka kwenye lile tundu la simba, akalia, “Danieli, Ee Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu wako, unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa?” (Fungu 20). Sauti ya nabii huyu ikasikika akijibu, “Ee mfalme, uishi milele. Mungu wangu amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako Ee mfalme, sikukosa neno. “Basi mfalme akafurahi sana, akaamuru wamtoe Danieli katika lile tundu. Ndipo Danieli akatolewa katika lile tundu, wala dhara lo lote halikuonekana mwilini mwake, kwa sababu alikuwa anamtumaini Mungu wake.” (Mafungu 22, 23). Hivyo ndivyo mtumishi wa Mungu alivyookolewa. Na mtego ambao adui zake walimwekea ili kumwangamiza ukawaangamiza wao wenyewe. Kwa amri ya mfalme walitupwa tunduni, na mara hiyo wakaliwa na wale wanyama wakali. KN 62.1

Wakati ulipokaribia mwisho wa ile miaka sabini ya utumwa akili za Danieli ziliwaza sana juu ya maneno ya unabii wa Yeremia. Danieli hautangazi uaminifu wake mwenyewe mbele za Mungu. Badala ya kujidai kuwa safi na mtakatifu, huyu nabii aliyetukuka kwa unyenyekevu alijifananisha na Israeli wenye dhambi hasa. Hekima ambayo Mungu alikuwa amempa ilikuwa kubwa sana kushinda hekima ya wakuu wa ulimwengu huu kama nuru ya jua ing’aayo mbingum adhuhuri ilivyo zaidi ya nyota hafifu sana. Hebu fikiria juu sala kutoka midomoni mwa mtu huyu mwenye kupendwa sana na Mbingu. Kwa unyenyekevu wa moyo, na kwa machozi na moyo ulioraruka, anajiombea na kuwaombea watu wa taifa lake. Anaufunua moyo wake wazi mbele za Mungu akiungama kutokustahili kwake mwenyewe na kukiri ukuu wa Mungu na adhama yake. KN 62.2

Huku sala ya Danieli ikiendelea, malaika Gabrieli anakuja haraka kutoka mbinguni kumwambia kuwa maombi yake yamesikiwa na kujibiwa. Huyu malaika mkuu ameamriwa kumpa akili na ufahamu kumfiinulia siri za zama zijazo. Hivyo akiwa katika kutafuta kwa bidii kujua na kuufahamu ukweli, Danieli aliingizwa katika kushirikiana na mjumbe wa Mungu. KN 62.3

atika jibu la ombi lake, Danieli hakupokea tu nuru na kweli ambayo yeye na watu wake walihitaji sana, bali maono ya mambo makuu ya wakati ujao, hata kuja kwa Mkombozi wa ulimwengu. Wale wanaojidai kuwa watakatifu, huku wakiwa hawana shauku ya kuyachunguza Maandiko Matakatifu au kushindana na Mungu katika maombi ili kupata ufahamu dhahiri zaidi wa ukweli wa Biblia, hawaujui utakaso wa kweli. KN 62.4

Danieli alizungumza na Mungu. Mbingu zilifunuliwa mbele yake. Lakini heshima kuu aliyopewa ilikuwa asili ya unyenyekevu na kumtafuta Mungu kwa bidii. Wote wanaoamini kwa moyo neon la Mungu wataona njaa na kiu ya kuyajua mapenzi yake. Mungu ndiye asili ya kweli. Hutia nuru akili zilizoingia giza na huutia moyo wa mwanadamu uwezo wa kushika na kufahamu maneno ya kweli ambayo ameyafunua. KN 62.5

Maneno makuu ya kweli yaliyofunuliwa na Mkombozi wa ulimwengu yanawahusu wale wenye kuitafuta kweli kama hazina iliyositirika. Danieli alikuwa mzee. Maisha vake yalikuwa yamepitia katikati ya mivuto ya jumbani mwa mfaime mkafiri, akili zake zilisumbuliwa na mambo ya dola kuu. Lakini anacha haya yote ili kuitesa roho yake mbele za Mungu, na kutafuta kujua makusudi ya Mwenyezi Mungu. Na kwa kuyajibu maombi yake, nuru itokayo mbinguni ilipelekwa kwa ajili ya wale ambao wangeishi siku za baadaye. Basi, kwa moyo wa bidii kama nini tungemtafuta Mungu, kusudi azifunue akili zetu kuyafahamu maneno ya kweli tuliyoletewa kutoka mbinguni. KN 63.1

Danieli alikuwa mtumishi wa Mungu aliyejitoa wakfu. Maisha yake ya siku nyingi yalijawa na matendo mema ya utumishi mzuri kwa Bwana wake. Usafi wake wa tabia na uthabiti wake vilikuwa sawa tu na unyenyekevu wake wa moyo na masikitiko yake mbele za Mungu kwa ajili ya makosa. Tunarudia, Maisha ya Daniel ni kielelezo kilichovuviwa cha utakaso wa kweli. 9 

Mungu Huwapima Wale Anaowathamini

Ukweli kwamba tumeitwa kustahimili taabu yaonyesha kuwa Bwana Yesu aona ndani yetu kitu cha thamani sana, ambacho anataka kukikuza. Kama hangeona cho chote ndani yetu ambacho kwacho aweza kutukuza jina lake asingetumia wakati wake kututakasa. Hatujisumbui kupunguzia miiba matawi. Kristo hatupi kwenye tanuru lake mawe yasiyo na thamani. Mawe ya madini ya thamani ndiyo anayoyapima. 10 KN 63.3

Kwa watu ambao hukusudia washike kazi za madaraka, kwa rehema hudhihirisha makosa yao yaliyositirika, ili waweze kuona na kuchunguza mahangaiko yanayowatatiza moyoni na mashindano ya mioyom mwao, na kuona neno lililo baya; hivyo waweza kugeuza tabia zao na kubadilisha njia zao. Mungu kwa majaliwa yake huwaleta wanadamu mahali awezapo kupima uwezo wa tabia zao za moyoni na kudhihirisha makusudi ya matendo yao, kusudi wapate kukuza hali ya mambo mazuri ndani yao na kuachana na mabaya. Mungu apenda watumishi wake wajue matengenezo ya tabia za mioyo yao wenyewe. Ili kulitimiza hili, mara nyingi huruhusu moto wa mateso kuwashambulia kusudi wapate kusafishwa. “Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au nani atakayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, nave atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki.” Malaki 3:2, 3. 11 KN 63.4

Mungu huongoza watu wake mbele, hatua kwa hatua. Huwapandisna katika mambo yaliyokusudiwa kudhihirisha kitu kilicho moyoni. Wengine hustahimili jambo moja, na kushindwa kwa lingine. Wengine hustahimili jambo moja, na kushindwa kwa lingine. Wengine hustahimili jambo moja, na kushindwa kwa iingine. Katika kila jambo linalozidi hali yake moyo hupimwa na kujaribiwa zaidi kidogo. Kama wale wanaojiita watu wa Mungu wanaona mioyo yao inahitilafiana na kazi hii nyofu, hilo lingewasadikisha kuwa wanayo kazi ya kufanya ili kushinda, kama hawataki kutapikwa kutoka mdomoni mwa Mungu. 12 KN 64.1

Mara tujuapo hali yetu ya kutoweza kuifanya kazi ya Mungu na kujitoa kuongozwa kwa hekima yake, Bwana aweza kufanya kazi pamoja nasi. Kama tutatoa moyoni kujipenda nafsi wenyewe bila kujali wengine, ataturuzuku mahitaji yetu yote. 13 

Onyo kwa Wale Watafutao Ahadi ya Kukubaliwa na Mungu

Wawezaje kujua kuwa umekubaliwa na Mungu? Jifunze neno lake kwa kuomba kwa bidii. Usiliweke kando kwa ajili ya kitabu kingine. Kitabu hiki huhakikisha hatia ya dhambi. Huidhihirisna wazi njia ya wokovu. Hufunua ijara yenye utukufu ung’aao. Hukufunulia Mwokozi kamili, na kukufundisha kuwa kwa njia ya rehema zake zisizo na kikomo pekee waweza kuutazamia wokovu. KN 64.3

Usipuuzie maombi ya faragha, kwa kuwa ni moyo wa dini. Kwa kusali kwa bidii, daima, omba usafi wa moyo. Omba kwa bidii, omba sana, kama ambavyo ungefanya iwapo ungekuwa hatarini kufa. Dumu mbele za Mungu mpaka shauku lfanywe ndani yako kutamani wokovu, na ushahidi uwepo ndani yako kuwa umesamehewa dhambi. 14 KN 64.4

Yesu hakukuacha kushangazwa na taabu na shida unazokutana nazo. Amekwisha kukuambia habari zake zote, na amekwambia pia usiangushwe chini na kulemewa taabu zikupatapo. Mtazame Yesu, Mkombozi wako, ufurahi na kushangilia. Taabu kubwa mno za kustahimili ni zile zitokazo kwa ndugu zetu, rafiki zetu wenyewe; lakini hata taabu hizi twaweza kuzistahimili kwa uvumilivu. Yesu halali ndani ya lile kaburi jipya la Yusufu. Amefufuka naye amepaa juu mbinguni, huko ili kutuombea. Tunaye Mwokozi aliyetupenda sana hata akatufilia, ili kwa njia yake tupate kuwa na matumaini na nguvu na moyo, na nafasi, ya kukaa pamoja naye juu ya kiti chake cha enzi. Aweza na anapenda kukusaidia umwitapo. KN 64.5

Je, unaona moyoni upungufu wako kwa cheo cha kazi ya madaraka uliyoaminiwa? Mshukuru Mungu kwa ajili hiyo. Kadiri uzidivyo kuuona udhaifu wako, ndivyo utakavyoelekea kutafuta msaidizi. “Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi.” Yesu anataka mwe wenye furaha, mwe wachangamfu. Anawataka mfanye mwezavyo kwa uwezo na Mungu, kisha mmwamini Bwana kuwasaidia na kuwainua wale ambao watakuwa wasaidizi wenu katika kuichukua mizigo. KN 64.6

Maneno makali ya watu yasikutie uchungu. Je, watu hawakusema maneno makali juu ya Yesu? Unakosea, na wakati mwingine unatoa nafasi kwa maneno yasiyofaa. Usitazamie fungu zuri zaidi maisha haya kuliko lile Mfalme wa fahari alilokuwa nalo. Maadui zako wakiona kuwa wanaweza kukutia uchungu, watafurahi, na Shetani atafurahi. Mtazame Yesu, na kufanya kazi kwa nia moja ukiuangalia utukufu wake. Ulinde moyo wako katika upendo wa Mungu. 15 

Maoni ya Moyoni Peke yake si Jambo Lionyeshalo Utakaso

Kuona furaha au kukosa raha si jambo lenye kuonyesha kuwa mtu ametakaswa au hakutakaswa. Hakuna utakaso wa ghafla. Utakaso wa kweli ni kazi ya kila siku, inayoendelea kadiri maisha yanavyoendelea mpaka mwisho. Wale wanaopigana na majaribu ya kila siku, wakishinda mivuto yao wenyewe ya dhambi, na kutafuta utakatifu wa moyo na maisha, hawajisifii utakatifu. Wanayo njaa na kiu ya haki, Dhambi huonekana kwao kuwa kitu kibayamno. 16 KN 65.2

Mungu hatuachi kwa sababu ya dhambi zetu. Pengine twafanya makosa na kuihuzunisha Roho yake; lakini tukitubu, na kumwendea kwa mioyo inayosikitaka kwa ajili ya makosa, hatatufukuza. Viko vipingamizi ambavyo havina budi kuondolewa. Maoni mabaya yametunzwa moyoni, kuna kiburi majivuno, kukosa saburi, na manung’uniko. Hayo yote hututenga na Mungu. Dhambi hazina budi kuungamwa, hapana budi pawepo kazi yenye kina ya neema moyoni. Wale wenye kujiona dhaifu na wenye kukata tamaa waweza kuwa watu hodari wa Mungu, na kufanya kazi bora kwa Bwana. Lakini hawana budi kufanya kazi kwa kiwango cha juu; wamepaswa kutovutwa na moyo wa kujifikiri waonekane. KN 65.3

Wengine huelekea kuona moyoni kwamba hawana budi kuwa muda wa kuangaliwa waonekane kama wanafaa au hawafai, na kwamba hawana budi kuthibitisha kwa Bwana kuwa wameongoka, kabla hawajaweza kudai mbaraka wake. Lakini watu hawa wenye thamani waweza kudai mbaraka wake hata sasa. Yawapasa wawe na neema yake. Roho wa Kristo, kuwasaidia udhaifii wao, ama sivyo hawawezi kukuza tabia ya Kikristo. Yesu anapenda tumwendee, hivi tulivyo-wenye dhambi, wadhaifu, wasiojitegemea. KN 65.4

Kutubu, na msamaha pia ni kipawa cha Mungu kwa njia ya Kristo. Ni kwa njia ya mvuto wa Roho Mtakatifu anayetusadikisha hatia ya dhambi, na kuiona haja yetu ya msamaha. Wenye masikitiko kwa ajili ya makosa, wala si wengine, hao ndio wanaosamehewa; lakini neema ya Mungu ndiyo inayoufanya moyo kuwa wenye kutubu. Anajua udhaifu wetu wote na upungufu, naye atatusaidia. 17 KN 66.1

Giza na mambo ya kukatisha tamaa wakati mwingine vitakuja moyoni na kutuogofya kutuangamiza, lakini haitupasi kutupilia mbali ujasiri wetu. Yatupasa kumkazia Yesu macho, tukiwa tunaona hivyo moyoni, ama tukiwa hatuoni hivyo. Yatupasa kutafuta kufanya kwa uaminifu kila wajibu tujuao na kisha kutegemea kwa utulivu ahadi za Mungu. KN 66.2

Wakati mwingine kujua sana hali yetu ya kutokustahili kutatia hofu moyoni, lakini hili si jambo la kuonyesha kuwa Mungu amebadilika kwetu, na kutuacha, au sisi tumemwacha Mungu. Hakuna jitihada zo zote ziwezazo kufanywa kuutawala moyo hata kuweza kuvutwa kwa urahisi kuona furaha. Pengine hatuoni leo amani na raha ambayo tuliiona jana; yatupasa kwa imani kushika mkono wa Kristo, na kumwamini kabisa gizani kama nuruni. KN 66.3

Kwa imani tazameni taji walizowekewa wale ambao watashinda; sikilizeni wimbo wa shangwe wa wale waliookoka. Astahili, astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa na ametukomboa kwa Mungu! Jaribuni kuyahesabu mambo haya kama ni ya hakika. KN 66.4

Kama tungeruhusu akili zetu kumfikin zaidi Kristo na jamii ya wale wa mbinguni, tungepata kitu cha kututia nguvu na kutusaidia katika kupigana vita vya Bwana. Kiburi na kuipenda dunia vingekosa nguvu kadiri tunavyotafakari utukufu wa ile nchi nzuri ambayo karibuni sana itakuwa makao yetu. Kwa uzuri wa Kristo mivuto yote ya kidunia itaonekana kuwa haina thamani hata kidogo. KN 66.5

Ijapokuwa Paulo mwishowe alifungwa gerezani Rumikuzuiwa asipate nuru na hewa ya mbinguni, kutengwa na kazi zake alizozitenda kwa bidii kuhubiri Injili, na kutazamia kwa muda kuhukumiwa kufa-lakini hakukubali kushindwa na mashaka au kukata tamaa. Kutoka katika lile gereza lenye giza lilitoa ushuhuda wake wa kufa, uliojaa imani na moyo mkuu ambao umeitia nguvu mioyo ya watakatifu na wafia dini katika vizazi vyote vya baaaaye. Maneno yake yanaeleza vizuri matokeo ya ule utakaso ambao tumejaribu kueleza katika kurasa hizi “Mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile, wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.” (2 Tim. 4:6-8).

Sura ya 7 - Mungu Anayo kazi Kwako Kufanya

KAZI ya Mungu duniani humu kamwe haiwezi kumalizika mpaka wanaume na wanawake walio washiriki wa kanisa letu wapate moyo tena kwa kazi na kushirikiana kwa umoja katika jitihadi zao na wachungaji na waongozi wa kanisa. 1 KN 67.1

Maneno haya “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.” (Marko 16:15) yamesemwa kwa kila mmoja wa wafuasi wa Kristo. Wote waliotoa maisha yao kwa Kristo wameamriwa kufanya kazi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu wenzao. Shauku ile ile aliyoona moyoni kwa ajili ya wokovu wa waliopotea yapasa kudhihirishwa ndani ya wafuasi wake. Wote hawawezi kusnika kazi ile ile, lakini kuna nafasi na kazi kwa wote. Wote waliojaliwa mibaraka ya Mungu wamepaswa kuitikia kwa kufanya kazi hasa; kila kipawa hakina budi kutumiwa kwa kueneza ufalme wa Mungu. 2 KN 67.2

Kuhubiri ni sehemu ndogo ya kazi ipasayo kutendwa kwa ajili ya wokovu wa roho za watu. Roho wa Mungu huwasadikisha wenye dhambi Neno la kweli, naye huwaweka katika mikono ya kanisa. Wachungaji huenda wakafanya sehemu yao, lakini, kamwe hawawezi kufanya kazi ambayo kanisa lingefanya. Mungu anataka kanisa lake kuwalea wale ambao ni wachanga katika imani na maisha, kuwaendea, si kusudi kupiga porojo nao, bali kusali, kuzungumza nao maneno ambayo yatawaimarisha katika imani. 3 KN 67.3

Mungu ameliita kanisa lake siku hizi, kama alivyowaita Waisraeli wa zamani za kale, kusimama kama nuru duniani. Kwa nguvu nyingi za neno la Mungu, ujumbe wa malaika wa kwanza , wa pili na wa tatu, amewatenga kutoka kwa madhehebu nyingi na kutoka kwa walimwengu kuwaleta karibu naye mwenyewe. Amewafanya watunzaji wa sheria yake na amewakabidhi maneno makuu ya unabii wa wakati huu. Kama maneno matakatifu aliyosema Mungu yalivyokabidhiwa kwa Waisraeli wa zamani zile za kale, haya ni amana takatifu ipasayo kutolewa kwa ulimwengu. KN 67.4

Malaika watatu wa Ufunuo 14 ni mfano wa watu ambao huipokea nuru ya ujumbe wa Mungu na kwenda kama mawakili waKe kutangaza onyo hili pande zote duniani. Kristo anawaambia wafuasi wake: “Ninyi ni nuru ya ulimwengu”( Mathayo 5:14). Kwa kila mmoja amkubaliye Yesu, msalaba wa Kalwari unasema: “Tazama thamani ya roho ya mtu. ‘Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe,” (Marko 16:15). Pasiruhusiwe kitu cho chote kuzuia kazi hii. Ni kazi ya maana kabisa kwa wakati huu, ni ya kudumu hata milele. Upendo ambao Yesu ameuonyesha kwa ajili ya roho za watu kwa dhabihu aliyoitoa kwa ajili ya wokovu wao, utawabidiisha wafuasi wake wote. 4 KN 67.5

Kristo hukubali hasha kwa furaha! Kila njia ya binadamu ambayo imetolewa kwake humwingiza mwanadamu kwenye umoja na Mungu, ili Mungu apate kuwapasha walimwengu habari za maajabu ya upendo wa Yesu Kristo Kufanyika mtu halisi. Ongea juu yake, Omoa juu yake, na zidi kusonga mbele mpaka ng’ambo ya pili.

Wafuasi wa Kweli wa Kristo Watamshuhudia

Kama kila mmoja wenu angekuwa mmishenari mwenye nguvu, ujumbe wa wakati huu ungehubiriwa kwa nguvu sana katika nchi zote, kwa kila taifa, na kabila na lugha. 6 KN 68.2

Wote wapendao kuingia mji wa Mungu hawana budi katika maisha yao hapa duniani kumtangaza Kristo katika shughuli zao. Hili ndilo linalowafanya wajumbe wa Kristo, mashahidi wake. Wamepaswa kutoa ushuhuda dhahiri, wa nguvu kuipinga mivuto yote mibaya, wakiwaelekeza wenye dhambi kwa Mwana-Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu. Huwapa wote wanaompokea, uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu. Uongofu ni njia tu ambayo kwayo twaweza kuuingia mji wa Mungu. Imesonga, na mlango tunaoingilia ni mwembamba, lakini njia hiyo ndiyo tupaswayo kuwaongoza wanaume na wanawake na watoto kupitia, tukiwafundisha kuwa, ili kuokoka, hawana budi kuwa na moyo mpya na roho mpya. Utu wa kale, tabia za kurithiwa hazina budi kushindwa. Tamaa za mwili za asili hazina budi kuongolewa. Udanganyifu wote, uongo wote, na mazungumzo yote mabaya hayana budi kuachwa. Maisha mapya, ambayo huwafanya wanaume na wanawake kufanana na Kristo, hayana budi kufuatwa. 7 KN 68.3

Ndugu na dada, mnataka kuvunja mvuto unaowashika? Mnapenda kuamka na kutoka katika mazoea haya ya uvivu ambayo ni kama usingizi wa mauti? Nendeni mkafanye kazi, haidhuru mnajisikia au hamjisikii hivyo moyoni . Jishughulisheni na mahubiri ya Injili ninyi wenyewe kuwaleta watu kwa Yesu na katika kulijua Neno la Mungu. Katika kila kazi mtaona kichocheo na dawa ya kutia afya na nguvu zenu za kiroho zitazidi kuongezeka, ili mweze kuushughulikia wokovu wenu wenyewe vizuri zaidi. Hali ya kuzimia imewapata wengi wanaomkiri Kristo. Onya, lalama, gombeza. Ijapokuwa wanaweza kukataa kusikia, kazi yako haitakuwa ya bure. Katika kufanya bidii kuwabariki wengine roho zenu wenyewe zitabarikiwa. 8 KN 68.4

Pasiwepo na mtu ye yote anayeona moyoni kuwa kwa sababu hawakuelimika, hawawezi kushiriki kazini mwa Mungu. Waweza kuyachunguza Maandiko Matakatifu wewe mwenyewe. “Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, na kumfahamisha mjinga” (Zaburi 119:130). Waweza kuiombea kazi hii. Sala ya moyo mnyofu, ikiombwa kwa imani, itasikiwa mbinguni. Nanyi yawapasa kufanya kazi kadiri ya uwezo wenu mlio nao. 9 KN 69.1

Malaika wa mbinguni wanangojea kushirikiana na vyombo vya kibinadamu, ili wapate kuwadhihirishia walimwengu kile wanadamu wawezacho kuwa na kile ambacho, kwa njia ya mvuto wao, waweza kukitimiza kwa ajili ya wokovu wa roho za watu ambao wako tayari kupotea. KN 69.2

Kristo anatuita kufanya kazi kwa uvumilivu na kwa kuendelea kwa bidii kwa ajili ya maelfu wanaopotea dhambini mwao, walioenea katika nchi zote, kama mabaki ya vitu vilivyoharibika ukingoni mwa jangwa. Wale wanaoushiriki utukufu wa Kristo hawana budi kushiriki pia kazini mwake, kuwasaidia wadhaifu, maskini, na waliokata tamaa. 10 KN 69.3

Kila muumini anapaswa kuwa na upendo kamili kwa kanisa. Mafanikio ya kanisa yapaswa kuwa jambo lake la kwanza linalompendeza. Kanisa lisipofaidika na ushirika wake ingekuwa heri asingekuwapo mshiriki maana hapo kanisa lingesaidiwa kwa kutokuwa na mzigo wa bure. Ni hiari ya wote kufanya kitu kwa ajili ya kazi ya Mungu. Wako wale ambao hutumia kiasi kikubwa cha fedha kwa anasa zisizo na maana; wanajiridhisha tamaa zao, lakini huona kuwa ni mzigo mkubwa sana kutoa mali kulisaidia kanisa. Wanapenda kupokea manufaa yote ya majaliwa ya kanisa, lakini hupendelea kuwaacha wengine kulipa fedha. 11 KN 69.4

Kanisa la Kristo laweza kufananishwa vyema na jeshi. Maisha ya kila askari yamejaa taabu, shida, na hatari. Kila upande, wako maadui walio macho, wenye kuongozwa na mkuu wa mamlaka za giza, ambaye kamwe hasinzii wala hatoroki na kuacha lindo lake. Mkristo aachapo kukesha zamu yake, huyu adui hodari hufanya shambulio la ghafula. Ikiwa washiriki wa kanisa hawatakuwa hodari na wenye bidii, watashindwa na hila zake. KN 69.5

Itakuwaje kama nusu ya askari jeshini wakiwa wavivu na walegevu au wakilala wanapoamriwa kuwa kazini? Matokeo yake yatakuwa kushindwa, kutekwa, au mauti. Wakiwapo askari wo wote katika hao wanaoponyoka mikononi mwa yule adui, wangehesabiwa kuwa wenye kustahili thawabu? La; wangepokea mara hiyo hukumu ya kufa. Kadhalika ndivyo ilivyo na kamsa la Kristo likikosa uangalifu au uaminifu; madhara ya baadaye yatakuwa makubwa zaidi sana. Jeshi la Kikristo lenye kulala usingizi-jambo gani la kutisha kuliko hili! Ni maendeleo gani yangaliweza kufanywa juu ya walimwengu, ambao wako chini ya mamlaka ya mkuu wa giza? Wale wanaosimama nyuma bila kujali siku ya mapigo, kana kwamba hawayatilii maanani mambo hayo, ni heri wabadili mwenendo wao au kuacha kabisa uaskari mara moja.

Mahali kwa Kila Mmoja wa Watu Majumbani

Wanawake na wanaume wanaweza kutwaa mahali pao katika kazi hii wakati wa hatari, na Mungu atafanya kazi kwa njia yao. Kama wamejazwa moyoni ujuzi wa wajibu wao, na kufanya kazi chini ya mvuto wa Roho wa Mungu watakuwa na utulivu ambao hasa hutakikana wakati huu. Mwokozi atatoa kwa wale wanawake wenve kujinyima nuru ya uso wake, na hii itawapa uwezo ambao utasninda ule wa wanaume. Wanaweza kufanya katika watu wa majumbani kazi ambayo wanaume hawawezi kufanya, kazi ambayo huyafikia maisha ya moyoni kwa ndani zaidi. Wanaweza kuikaribia mioyo ya wale ambao wanaume hawawezi kuifikia. Kazi yao inahitajika. Wanawake wenye busara na wanyenyekevu huweza kufanya kazi iliyo njema katika kueleza ukweli kwa watu majumbani mwao. Neno la Mungu lenye kuelezwa namna hii litatenda kazi yake ya kutia chachu, na kwa njia ya mvuto wake wote wa nyumbani wataongoka. 13 KN 70.1

Wote waweza kufanya kitu. Katika kujaribu kutoa udhuru, wengine husema: “Kazi za nyumbani mwangu, watoto wangu, hudai wakati wangu na mali zangu.” Wazazi, watoto wenu wangekuwa msaada kwenu, wakiongeza uwezo wenu kumtumikia Bwana. Watoto ni watu walio wadogo katika jamaa ya Mungu. Yawapasa kufundishwa kuwa uwezo wao wote wa mwili, akili, na moyo ni vyake Mungu. Wangefundishwa kusaidia katika kazi za namna mbalimbali za kufikiria wengine kuliko nafsi zao wenyewe. Usikubali watoto wako kuwa vikwazo. Yawapasa watoto kushiriki pamoja nawe mizigo ya kiroho na ya kimwili pia. Kwa kuwasaidia wengine wanaongeza furaha yao wenyewe na manufaa. 14 KN 70.2

Kazi yetu kwa ajili ya Kristo haina budi kuanzia kwa watu wa nyumbam. Mafundisho ya vijana yanapasa kuwa tofauti na yale yaliyotolewa wakati uliopita. Hali yao njema hudai kazi zaidi kuliko ilivyofanywa kwao. Hakuna kazi ya muhimu kupita hiyo kwa upande wa wanawake. Kwa mafundisho na kielelezo yawapasa wazazi kuwafundisha watoto wao kuwafanyia kazi watu wasioongoka. Yawapasa watoto kufundishwa hata wawahurumie wazee na wale wanaosumbuka nao watatafuta kupunguza maumivu ya maskini na wenye taabu. Yawapasa kufundishwa kuwa wenye bidii katika kazi ya utume; na tangu utotoni kujikana nafsi na kujinyima kwa ajili ya kuwanufaisha wengine na kuendeleza kazi ya Kristo kungefundishwa, kusudi wapate kuwa wafanya kazi pamoja na Mungu. 15 KN 70.3

Kuwa Mashahidi kwa Kuhamia Mahali Papya

Si kusudi la Mungu kuwa watu wake wakae mahali pamoja jamii kubwa. Wanafunzi wa Kristo ni mawakili wake duniani, na Mungu anakusudia kuwa watawanyike pande zote nchini, katika miji mikubwa na midogo, na vijijim, kama mianga katikati ya giza la ulimwengu. Wanapaswa kufanya kazi ya utume kwa ajili ya Mungu, kwa imani na matendo yao wakishuhudia kukaribia kuja kwa Mwokozi. KN 71.1

Washiriki wa makanisa yetu waweza kufanya kazi ambayo bado hawajaanza kuifanya ila kwa shida. Pasiwepo na watu wanaohamia mahali papya kwa ajili ya manufaa ya kiaunia tu; bali pakiwapo na mlango wa kupata maishilio, hebu jamaa walio imara katika Neno la Mungu waingie, watu wa nyumba moja au mbili mahali pamoja, kufanya kazi ya utume. Yawapasa kuona moyoni upendo kwa ajili ya roho za watu, mzigo wa kazi kwa ajili yao, na yawapasa kulifanya kuwa jambo la kujifunza jinsi ya kuwaleta kwenye ukweli. Wanaweza kugawanya vitabu na magazeti yetu, kufanya mikutano nyumbani mwao, kujua habari za majirani zao, na kuwaalika kuja katika mikutano hii. Hivyo ndivyo wawezavyo kuacha nuru yao kuangaza kwa matendo mema. KN 71.2

Hebu watenda kazi wasimame wenyewe kwa Mungu, wakilia, wakiomba, wakifanya kazi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu wenzao. Kumbukeni kuwa mnakimbia katika shindano, mkishindania taji ya milele. Huku wengi wakipenda sifa za watu zaidi ya kupata kibali kwa Mungu, fungu lenu na liwe kufanya kazi kwa moyo mnyenyekevu. Jifunzem kutumia imani katika kuwaweka majirani zenu mbele ya kiti cha neema na kumwomba Mungu kuigusa mioyo yao. Kwa njia hii kazi ya utume yenye matokeo mema yaweza kutendeka. Wengine waweza kufikiwa ambao wasingependa kusikiliza mhubiri au mwinjilisti wa vitabu. Na wale wanaofanya kazi kwa njia hii mahali papya watajifunza njia bora sana za kuwaendea watu na huweza kutayarisha njia kwa ajili ya watenda kazi wengine. 16 KN 71.3

Watembeleeni majirani zenu na kuwaonyesha kuwa mnajali wokovu wa roho zao. Amsheni nguvu zote za kiroho zifanye kazi. Waambieni mnaowaamkia ya kwamba mwisho wa vyote umekaribia. Bwana Yesu Kristo atafungua mlango wa mioyo yao na kuamsha mioyoni mwao shauku isiyokoma. KN 71.4

Hata wanaposhughulika na kazi zao za kila siku, watu wa Mungu waweza kuwaongoza wengine kwa Kristo. Na wakiwa katika kufanya hili watakuwa wanayo ahadi ya thamani kwamba Kristo atawapa maneno ya kusema ambayo yatawaburudisha na kuwatia nguvu maskini, wenye kusumbuka ambao wamo gizani. Imani yao wenyewe itatiwa nguvu wakifahamu kuwa ahadi ya Mkombozi matimizwa. Licha ya kuwa mbaraka kwa wengine, hata kazi waifanyayo kwa ajili ya Kristo huwaletea mbaraka wao wenyewe. KN 71.5

Kazi kubwa yaweza kutendwa kwa kuwafundisha watu Biblia kama inavyosomeka tu. Pelekeni Neno la Mungu kwa mlango wa kila mtu, sisitizeni maneno yake yaliyo dhahiri kwenye dhamiri ya kila mtu, waambieni tena wote agizo la Mwokozi: “Mwayachunguza Maandiko” (Yohana 5:39). Waonyeni kuichukua Biblia kama ilivyo, kuomba sana hekima ya Mungu, na kisha, nuru ikiangaza, kupokea kwa furaha kila mwonzi wa thamani na kwa ujasiri kustahimili matokeo yake ya baadaye. 18 KN 72.1

Miongoni mwa washiriki wa makanisa yetu yapasa pawepo na kazi zaidi ya kwenda nyumba kwa nyumba kutoa masomo ya Biblia na kugawanya vitabu na magazeti. Tabia ya Kikristo yaweza tu kufanyika sawa sawa na kwa ukamilifu mtu anapohesabu kuwa ni majaliwa kufanya kazi pasipo kutaka kujinufaisha mwenyewe katika kulihubiri Neno la Mungu na kuisaidia kazi ya Mungu kwa fedha. Hatuna budi kupanda mbegu kando ya maji yote, kuzikabidhi roho zetu katika upendo wa Mungu, kufanya kazi maadamu ni mchana, na kutumia njia zote tulizopewa na Mungu kufanya kazi yo yote ifuatayo. Lo lote mikono yetu ipatalo kulifanya, yatupasa tulifanye kwa uaminifu; dhabihu lwayo yote tutakiwayo kutoa, yatupasa kuitoa kwa moyo mkunjufu. Kadiri tunavyopanda mbegu kando ya maji yote tutaona kuwa “apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu” (2 Wakorintho 9:6).

Onyesho la Dini Lifaalo

Upungufu wo wote wa kazi itendwayo kwa bidii na ya uaminifu kwa Mungu husingizia uwongo dini yetu. Dini ya Kikristo ambayo tu hudhihirishwa kwa kazi ya uaminifu, ifaayo, ndiyo itakayowachoma mioyo wale ambao wamekufa katika uhalifu wa sheria na dhambi. Wakristo wenye kumwomba Mungu wanyenyekevu, na waaminio, wenye kuonyesha kwa matendo yao kuwa shauku yao kuu ni kuwajulisha wengine Neno la kweli liokoalo ambalo halina budi kuwajaribu watu wote, watavuna mavuno makubwa va roho kwa Bwana. KN 72.3

Hakuna udhuru uwezao kutolewa kwa ajili ya imani ya makanisa yetu kuwa hafifu hivi na dhaifu. “Irudieni ngome, enyi wafungwa wa tumaini” (Zekaria 9:12). Pana nguvu kwa ajili yetu ndani ya Kristo. Yu Mwombezi wetu mbele za Baba. Anatuma wajumbe wake kila upande wa ufalme wake kupeleka habari za mapenzi yake kwa watu wake. Anatembea miongoni kuwaadilisha wafuasi wake. Mvuto wa wale ambao humwamini kwa kweli utakuwa harufu ya uzima ulimwenguni. Anashikilia nyota katika mkono wake wa kuume, na ni kusudi lake kuiacha nuru yake iangaze kwa njia ya hawa kwa walimwengu. Hivyo anataka kanisa la juu. Ametupa sisi kazi kuu kufanya, tuonyeshe maishani mwetu kile Neno la Mungu lilichofanya. Hebu tuifanye kwa usahihi na nia. Imegharamu kujikana nafsi, kujinyima, nguvu zisizoshindika, na sala nyingi kukuza kazi ya kuihubin injili mahali inaposimama sasa. Kuna hatari kwamba baadhi ya wale ambao sasa wanashika kazi wataridhika na kuwa watu wasiofanya kazi vizuri, wakiona moyoni kuwa sasa hakuna haja ya kujikana nafsi mwenyewe na kutenda kwa bidii kazi ngumu isiyopendeza kama watangulizi wa ujumbe huu walivyofanya maishani; nyakati zile zimepita; na ya kwamba kwa kuwa kuna fedha nyingi zaidi kazini mwa Mungu, si lazima kwao kujiweka katika hali ngumu kama wengi walivyotakiwa kufanya mwanzo wa ujumbe huu. KN 72.4

Lakini kama bidii zile zile na moyo wa kujinyima ule ule ungeonyeshwa katika hatua hii ya kazi kama mwanzoni, tungeona ukifanya makuu mara mia kuliko ifanyavyo hivi sasa. 20 KN 73.1

Ungamo letu ni kuu. Sisi tulio Waadventista wenye kuishika Sabato twakiri amri zote za Mungu na kutazamia kuja kwa Mwokozi wetu. Ujumbe mzito sana wa onyo umewekwa amana kwa wachache waho waaminifu wa Mungu. Yatupasa kuonyesha kwa maneno na matendo yetu kuwa twafahamu maaaraka makubwa tuliyotwishwa. Nuru yetu ingeangaza hata wote wapate kuona jinsi tunavyomtukuza Baba katika maisha yetu ya kila siku na ya kwamba tumeungwa katika umoja na wale wa mbinguni na tu warithi warithio pamoja na Yesu Kristo, ili atakapoonekana katika uwezo na utukufu mwingi, tupate kufanana naye. 21 

Sura ya 8 - Mimi Hapa, Nitume Mimi

MWISHO u karibu, unatunyemelea, pasipo kuonekana, kama kunyatia kwa mwizi usiku. Mungu atujalie lli tusilale tena kama wengine wafanyavyo, bali tupate kukesha na kuwa na kiasi. Siku si nyingi Neno la Mungu litakuwa halina budi kushinda vizuri mno na wote ambao sasa wanachagua kuwa wafanya kazi pamoja na Mungu watashinda pamoja nalo. Muda ni mfupi; usiku waja ambapo mtu hawezi kufanya kazi. Hebu wale wanaofurahi katika nuru ya Neno la kweli la wakati huu, sasa waharakishe kuwapa wengine ukweli. Bwana anauliza, “Nimtume nani?” Wale wapendao kujinyima kwa ajili ya Neno la Mungu, wanapaswa, sasa kuitikia, “Mimi hapa, nitume.” KN 74.1

Tumefanya sehemu ndogo tu ya kazi ya kuhubiri Injili ambayo Mungu anataka sana tuifanye miongoni mwa majirani na maratiki zetu. Katika kila mji wa nchi hii yetu wako wale ambao hawajui ukweli. Na nje ya nchi yetu, ng’ambo ya bahari katika ulimwengu huu mkubwa kuna mahali pengi papya pa kazi ambapo yatupasa kuulima udongo na kupanda mbegu. 1 KN 74.2

Tuko karibu sana na wakati wa taabu na mashaka ambayo hayajafikiriwa na mtu ye yote bado. Uwezo utokao upande wa chini huwaongoza wanadamu vitani kinyume cha Mungu. Wanadamu wamefanya shauri moja na malaika wabaya kuitangua sheria ya Mungu. Walimwengu wanafanana na watu wa ulimwengu wa siku za Nuhu, ambao walikumbwa na Gharika, na kama watu wa Sodoma, ambao waliteketezwa kwa moto kutoka mbinguni. Nguvu za Shetani zinafanya kazi kupotosha akili za watu kutoka katika mambo ya hakika ya milele. Yule adui amepanga mambo yafae makusudi yake mwenyewe. Shughuli za kidunia, michezo, mitindo ya kisasamambo haya hushughulisha akili za watu wanaume kwa wanawake. Michezo ya furaha na masomo yasiyo na faida huharibu busara. Katika ile njia pana iendayo katika uharibifu wa milele pana maandamano makubwa. Ulimwengu, ukijawa na jeuri, karamu za furaha nyingi, na ulevi, unalibadilisha kanisa. Sheria ya Mungu, kipimo kitakatifu cha haki, inatangazwa kuwa isiyo na maana. 2 KN 74.3

Je yatupasa kungoja mpaka kutimizwa kwa maneno ya unabii wa mwisho kabla ya kusema lo lote juu yao? Basi maneno yetu yatakuwa na faida gani? Tungoje mpaka nukumu za Mungu zimwangukie mkosaji kabla hatujamwambia jinsi ya kuziepuka. Iko wapi imani yetu katika Neno la Mungu? Je lazima tuone mambo yahyotabiriwa yakitimia kabla hatujaamini kile alichosema? Kwa mionzi dhahiri, nuru imetujia, ikituonyesha kuwa siku kuu ya Bwana imekaribia, ” naam I milangoni.” Hebu tusome na kufahamu kabla hatujachelewa. 3

Talanta Zako zafaa Hitaji Fulani

Mungu ana nafasi kwa kila mmoja katika mpango wake mkuu. Talanta ambazo hazihitajiki hazitolewi. Talanta inayodhaniwa kuwa ni ndogo, Mungu ana mahali kwa ajili yake, nayo talanta hiyo moja, kama ikitumiwa kwa uaminifu, itafanya kazi ile ile ambayo Mungu ameikusudia iifanye. Talanta za kibarua zinahitajika katika kazi ya kuhubiri Injili nyumba kwa nyumba nazo zaweza kufanya makubwa zaidi katika kazi hii kuliko vipawa adimu. 4 KN 75.1

Watu wakitumia uwezo wao kama Mungu anavyoongoza, talanta zao zitaongezeka, uwezo wao utazidi, nao watakuwa na hekima itokayo mbinguni katika kutafuta kuwaokoa waliopotea. Lakini washiriki wa kanisa wakiwa walegevu na wasio waangalifu wa madaraka yao waliyopewa na Mungu kuwahudumia wengine, wawezaje kutazamia kupokea hazina ya mbinguni? Wenye kujidai kuwa Wakristo wasipoona mzigo moyoni kuwaangazia wale walio gizani, wakikoma kutoa neema na maarifa, wanapungukiwa ufanamu, wanapoteza hali ya kuyathamini majaliwa makubwa ya mbinguni; na kwa kukosa kuyathamini wao wenyewe, wanashindwa kutambua umuhimu wa kuyapeleka kwa wengine kwa wengine. KN 75.2

Tunaona makanisa makubwa katika mitaa mbalimbali. Washiriki wake wamepata ujuzi mkubwa wa Neno la Mungu, na wengi wanaridhika kulisikia Neno la uzima bila kujaribu kuwatolea wengine nuru. Hawaoni moyoni wajibu uwapasao kwa ajili ya maendeleo ya kazi hii, wanashauku ndogo sana juu ya wokovu wa roho za watu. Wamejawa na bidii katika mambo ya anasa za dunia, lakini dini yao haionekani katika shughuli zao. Wanasema: “Dini ni dini, na shughuli ni shughuli.” Wanaamini kwamba kila moja ina nafasi yake sawasawa, lakini husema: “acha yatengwe.” KN 75.3

Kwa sababu ya nafasi zisizojaliwa na kutumia vibaya majaliwa na bahati walizo nazo, washiriki wa makanisa haya hawakui “katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo” (2 Petro 3:18). Kwa hiyo ni wadhaifu katika imani, wapungufu wa ujuzi na watoto katika mambo ya maisha. Hawana mizizi wala msingi katika Neno la Mungu. Kama wakiendelea hivi, madanganyifu mengi ya siku za mwisho yamkini yatawadanganya, maana hawatakuwa na macho ya kiroho kupambanua kweli na kosa. 5 KN 75.4

Mungu ataka Sana Kutoa Kipawa cha Roho Mtakatifu

Jitihada maalumu zinapofanywa na watenda kazi wenye ujuzi mwingi katika mtaa wakaapo watu wetu waumini wenyewe wa mahali hapo wana wajibu mkubwa sana kufanya yote wawezayo kufungua njia kwa ajili ya Bwana kufanya kazi. Yawapasa kuchunguza mioyo yao kwa kuomba kwa bidii na kusafisha njia kuu ya Mfalme kwa kuondoa kila dhambi ambayo ingewazuia wasishirikiane na Mungu pamoja na ndugu zao. KN 76.1

Katika njozi za usiku, maelezo yalipitishwa mbele yangu, ya matengenezo miongoni mwa watu wa Mungu. Wengi walikuwa wanamsifu Mungu. Wagonjwa waliponywa, na miujiza mingine ikafanywa. Roho ya maombezi ikaonekana, kama ilivyodhihirishwa mbele ya siku kuu ya Pentekoste. Mamia na maelfu wakaonekana wakizuru watu wa nyumba mbalimbali na kuwafunulia Neno la Mungu. Mioyo ikasadikishwa hatia ya dhambi kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, na moyo wa uongofu wa kweli ukadhihirishwa. Kila upande milango ikafunguliwa kwa ajili ya kuhubiriwa Neno la Mungu. Ulimwengu ukaonekana kana kwamba uliangazwa kwa mvuto wa mbinguni na unyenyekevu wa moyo. Nikasikia sauti za shukrani na sifa, na ikaonekana kuwa kama yale matengenezo tuliyoona mwaka 1844. 6 KN 76.2

Mungu anataka sana kuwaburudisha watu wake kwa kipawa cha Roho Mtakatifu, akiwabatiza upya katika pendo lake. Hakuna sababu ya ukosefu wa Roho kanisam. Baada ya kupaa kwa Kristo, Roho Mtakatifu aliwashukia wale wanafunzi waliokuwa wakingojea, wakisali, na kuamini kwa uwingi na nguvu hata kuufikia kila moyo. Wakati ujao dunia haina budi kuangazwa kwa utukufu wa Mungu. Mvuto mtakatifu hauna budi kutoka kuwaendea walimwengu kutoka kwa wale ambao wametakaswa kwa kweli. Dunia haina budi kuzungukwa na mambo yavutayo mtu kuona neema. Roho Mtakatifu hana budi kufanya kazi moyoni mwa wanadamu, akitwaa mambo ya Mungu na kuyaonyesha kwa wanadamu. 7 KN 76.3

Mungu anapenda kufanya kazi kubwa kwa ajili ya wote wanaomwamini kwa kweli. Kama washiriki wa kanisa wasio watenda kazi walipwao mshahara wataondoka na kufanya kazi wawezayo kufanya, wakienda vitani kwa gharama zao wenyewe kila mmoja akiona kiasi awezacho kufanya katika kuongoza roho za watu kwa Yesu, tutaona wengi wakiacha kazi ya uaskari wa Shetani ili kusimama chini ya bendera ya Kristo. Kama watu wetu wataendesha nuru ambayo imetolewa kwa maneno haya machache ya mafundisho, (Yohana 15:8), yamkini tutaona wokovu wa Mungu. Uamsho wa ajabu utafuata. Wenye dhambi wataongoka na roho za wengi zitaongezwa kanisani. Tukiingiza mioyo yetu kwenye umoja na Kristo, na kuyapatanisha maisha yetu na kazi yake, roho iliyowashukia wale wanafunzi siku ya Pentekoste itatushukia. 8

Hatari Katika Kuchelewa

Katika njozi za usiku maono ya ajabu sana yalipita mbele yangu. Naliona mpira mkubwa sana wa moto ukianguka miongoni mwa majumba mazuri, na kuleta uharibifu wao ghamla. Nalisikia mmoja akisema: “Tulijua kuwa hukumu za Mungu zitakuja juu ya nchi, lakini hatukujua kwamba zingekuja upesi hivi.” Wengine, kwa sauti za maumivu makali, wakasema: “Mlijua! Mbona basi hamkutuambia? Sisi hatukujua.” Kila upande nikasikia maneno ya lawama yakisemwa. KN 77.1

Kwa wasiwasi mwingi nikaamka. Nikashikwa na usingizi tena, nami nikawa kana kwamba nimo katika mkutano mkubwa. Mkuu mmoja akawa anasema na kundi la watu, ambaye mbele yake palikunjuliwa ramani ya ulimwengu. Akasema kuwa ramani hiyo llionyesha shamba la Mungu la mizabibu, ambalo halina budi kupaliliwa. Kadiri nuru kutoka mbinguni inavyomzukia mtu awaye yote, mtu huyo hupaswa kuitupa kwa wengine. Taa zilikuwa hazina budi kuwashwa mahali pengi, na kutoka katika taa hizi zingine tena zilipaswa kuwashwa. KN 77.2

Maneno haya yakasemwa mara nyingi: “Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.” Mathayo (5:13 - 16). . KN 77.3

Kila siku ipitayo hutuleta karibu zaidi na mwisho. Je, hutuleta pia karibu na Mungu? Je tunakesha katika kuomba? Wale ambao tunashirikiana nao siku kwa siku huhitaji msaada wetu, na uongozi wetu. Huenda wakawa katika hali ya moyo ambao neno moja kwa wakati wake litaingizwa moyoni na Roho Mtakatifu kama msumari mahali palipo imara. Kesho baadhi ya watu hawa waweza kuwa mahali ambapo kamwe hatutaweza kuwafikia tena. Je mvuto wetu ni wa aina gani kwa hawa wasafiri wenzetu? Twafanya jitihadi gani kuwaongoza kwa Kristo? 9 KN 77.4

Maadam malaika wanazishikilia zile pepo nne, yatupasa kufanya kazi kwa uwezo wetu wote. Yatupasa kuchukua ujumbe wetu bila kuchelewa hata kidogo. Yatupasa kuonyesha wenyeji wa mbinguni, na wanadamu katika kizazi hiki kilichoharibika tabia, kuwa dini yetu ni imani na uwezo ambao Kristo ndiye Asili yake nalo neno lake ni maneno yaliyosemwa na Mungu. Roho za wanadamu zinaning’inia juu ya mizani. Watakuwa ama raia wa ufalme wa Mungu ama watumwa wa utawala wa Shetani. Wote wanapaswa kuwa na majaliwa ya kushikilia tumaini lililowekwa mbele yao katika Injili, nao wawezaje kusikia pasipo mhubiri? Wanadamu wanahitaji kufanywa upya tabia za moyoni, matayarisho ya tabia, ili wapate kusimama mbele za Mungu. Ziko roho za watu zilizotayari kupotea kwa sababu ya makosa ya kinadharia yanayoenea kila mahali, na ambayo hukusudiwa kuupinga ujumbe wa Injili. Nani ambao sasa watajitoa wakfu-kabisa kuwa wafanya kazi pamoja na Mungu? 10 KN 77.5

Leo sehemu kubwa ya wale ambao ni jumuia yetu ni wafu katika makosa na dhambi. Huja na kwenda kama mlango juu ya bawabu zake. Kwa miaka mingi wamesikiliza na kupendezwa na maneno ya kweli, mazito sana, yenye kuamsha moyo, lakini hawakuyatumia maishani. Kwa hiyo, wamezidi kupungua kuijua thamani ya Neno la Mungu. Maneno yanayogusa ya makaripio na maonyo hayawaamshi kutubu. Nyimbo tamu kabisa zitokazo kwa Mungu kwa njia ya midomo ya wanadamu-kuhesabiwa haki kwa imam, na haki ya Kristo-haviamshi kutoka kwao jibu la upendo na shukrani. Ijapokuwa tajiri wa mbinguni huweka mbele yao vitu vva thamani vya imani na upendo, ingawa huwaalika kununua kutoka kwake “dhahabu iliyosafishwa kwa moto,” na “mavazi meupe” wapate kuvaa, na “dawa ya macho” wapate kuona, huifanya migumu mioyo yao juu yake, na kukosa kubadili uvuguvugu wao kwa upendo na moyo wa bidii. Huku wakifanya ungamo, huzikana nguvu za utauwa. Kama wakiendelea katika hali hii, Mungu atawakataa. Wanajifanya wenyewe wasifae kuwa watu wa nyumba ya Mungu. 11 KN 78.1

Hebu washiriki wa kanisa wakumbuke kwamba ukweli kuwa majina yao yameandikwa katika vitabu vya kanisa si jambo litakalowaokoa. Hawana budi kujionyesha kuwa wamekubaliwa na Mungu, watenda kazi wasio na sababu ya kutahayari. Siku kwa siku wanapaswa kujenga tabia zao kupatana na maongozi ya Kristo. Wanapaswa kukaa ndani yake, daima wakitumia imani ndani yake. Hivyo watakua mpaka wawe wanaume na wanawake wenye kukifikia cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo-safi wachangamfu, Wakristo wazuri, wenye kuongozwa na Mungu katika nuru lzidiyo kuwa kubwa daima. Kama hayo si mambo yanayoonekana kwao, watakuwa miongoni mwa wale ambao sauti zao siku moja zitapaazwa kwa kuomboleza kwa uchungu: “Mavuno yamepita, kiangazi kimekwisha, na roho yangu haikuiokolewa! Mbona sikukimbilia kwenye Ngome kujisalimisha! Kwa nini nilichezacheza na wokovu wa roho yangu, na kuipinga roho ya neema?” 12 KN 78.2

Ndugu na dada mnaodai kuwa mmeliamini neno la Mungu muda mrefu, nawauliza kila mmoja wenu, ‘Je matendo yenu yanapatana na nuru, majaliwa, na nafasi mlizokarimiwa na Mungu?’ Hili ni swali zito lenye maana sana. Jua la Haki amelizukia kanisa na ni wajibu wa kanisa kuangaza. Kila mmoja amejaliwa kukua. Wale wenye uhusiano na Kristo watakua katika neema na katika kumjua Mwana wa Mungu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu cha wanaume na wanawake. Kama wote wanaodai kuliamini neno la Mungu wangetumia kwa faida uwezo wao na nafasi zao kujifunza na kutenda, wangeweza kuwa wenye nguvu katika Kristo. Si neno kazi yao ya maisha iwe ya namna gani,-wakiwa wakulima, mafundi wa mashine, walimu au wachungaji wa makanisa,kama wakiwa wamejitoa kabisa wakfu kwa Mungu watakuwa watenda kazi hodari kwa Bwana wa mbinguni. 13

Watenda Kazi wa Kufundisha Washiriki wa Kanisa

Ni dhahiri kuwa mahubiri yote ambayo yamehubiriwa hayakukuza jamii kubwa ya watenda kazi wenye kujikana nafsi. Somo hili lapasa kufikiriwa kuwa ni la muhimu sana na lenye matokeo makubwa sana. Mustakabali wetu wa uzima wa milele umo hatarini. Makanisa yanafifia kwa sababu wamekosa kutumia talanta zao kueneza nuru. Mashauri ya uangalifu yapaswa kutolewa ambayo yatakuwa mafundisho kutoka kwa Bwana, kusudi wote wapate kuitumia nuru yao kwa njia ya kufaa. Wale ambao wanayasimamia makanisa wangechagua washiriki wenye uwezo na kuwapa kazi za madaraka, na wakati huo huo wakiwapa mashauri mema juu ya jinsi wawezavyo kuwatumikia na kuwafaidia wengine. 14 KN 79.1

Mafundi wa mashine, wanasheria, wafanyabiashara, watu wa namna zote za kazi na uchumi, hujielimisha ili wapate kuwa wajuzi stadi wa kazi zao. Je, yawapasa wafuasi wa Kristo kupungua akili, huku wakiwa wanadai kuwa wanamtumikia kazini mwake wasijue njia za kutumia? Uhodari wa kujipatia uzima wa milele ni jambo kubwa kuliko inavyoweza kudhaniwa duniani. Ili kuwaongoza watu kwa Yesu inalazimu pawepo ujuzi wa hali ya binadamu ya asili na kujifunza moyo wa mwanadamu. Mawazo yanayofikiriwa kwa uangalifu mwingi na kuomba daima hutakikana lli kujua jinsi ya kuwaendea wanaume na wanawake juu ya somo kuu la Neno la Mungu. 15 KN 79.2

Mara kanisa liishapo kuanzishwa, mchungaji na aweke washiriki kazini. Watahitaji kufundishwa namna ya kufanya kazi vizuri. Mchungaji na atumie saa zake nyingi zaidi katika kufundisha kuliko katika kuhubiri. Na awafundisne watu jinsi ya kuwapa wengine ujuzi waliopokea. Huku waongofu wapya wakipaswa kufundishwa kutaka shauri jema kutoka kwa wale wenye maarifa mengi kazini, hawana budi pia kufundishwa kutomweka mchungaji mahali pa Mungu. KN 79.3

Msaada mkuu kabisa wawezao kupewa watu wetu ni kuwa-fundisha kumtumikia Mungu, na kumtegemea, wala si kuwategemea wachungaji. Hebu wajifunze kufanya kazi kama Kristo alivyofanya kazi. Nawajiunge na jeshi lake la watenda kazi na kumtumikia kwa uaminifu. 16 KN 80.1

Walimu wanaonyesha njia katika kufanya kazi miongoni mwa watu, na wengine, wakiungana nao, watajifunza kwa kielelezo chao. Kielelezo kimoja chafaa zaidi ya mafundisho mengi. 17 KN 80.2

Wale wenye kulisimamia kanisa kwa mambo ya kiroho yawapasa kuvumbua njia ambazo kwazo nafasi yaweza kutolewa kwa kila mshiriki wa kanisa kushiriki kazini mwa Mungu. Hili si jambo lililofanywa siku zote zamani? Mipango haikutimizwa kabisa ambayo kwayo talanta za wote zaweza kutumiwa jeshini. Wengi hawafahamu hasara ambayo imepatikana kwa sababu ya jambo hili. KN 80.3

Katika kila kanisa kuna talanta, ambayo kwa kazi nzuri, yaweza kukuzwa kuwa msaada mkubwa katika kazi hii. Yapasa pawepo mpango mzuri kwa kuwaajiri watenda kazi kuyatembelea makanisa yetu yote, makubwa na madogo, kuwafundisha washiriki wa kanisa kufanya kazi kwa ajili ya kulijenga kanisa, na pia kwa ajili ya wale wasioamini. Mafunzo, elimu, ndiyo inayotakiwa. Hebu wote wanuie moyoni mwao na akilini mwao kuwa wenye akili kwa habari za kazi ya wakati huu, wakijistahilisha kufanya kile ambacho ni chenye kufaa vizuri kukitenda. KN 80.4

Kinachohitajika sasa kwa ajili ya kuyajenga makanisa yetu ni kazi nzuri ya watenda kazi wenye busara kuona na kukuza talanta kanisani-talanta ambayo huweza kukuzwa na kuongozwa vizuri kwa ajili ya kazi ya Bwana. Wale ambao watafanya kazi ya kuyatembelea makanisa wangewapa ndugu na dada mashauri ya njia za kufaa za kuifanya kazi ya utume. Hebu pawepo na darasa la mafundisho kwa vijana pia. Vijana wa kiume na wa kike wanapaswa kufundishwa kuwa watenda kazi nyumbani, jirani na kwao, na kanisani. 18 KN 80.5

Malaika wa mbinguni wamekuwa wakingojea muda mrefu mawakili wanadamu-wasniriki wa kanisakushirikiana nao katika kazi hii kuu inayohitajika kufanywa. Wanakungojea. Mahali pa kazi ni pakubwa sana, na azimio lake lina mambo mengi pia, hata kila moyo uliotakaswa utavutwa kuingia kazini kama chombo cha uwezo wa Mungu. 19 KN 80.6

Kama Wakristo wangetenda mambo kwa umoja, wakisonga mbele kama mtu mmoja, chini ya maongozi ya Uwezo mmoja, kwa ajili ya kutimiza kusudi moja, wangetingisha ulimwengu. 20 KN 80.7

Mwito wa kutolewa katika “njia kuu” hauna budi kutangazwa kwa wote wenye sehemu ya kutenda katika kazi ulimwenguni humu, kwa walimu na kwa viongozi wa watu. Wale wenye kazi za madaraka makubwa katika maisha ya watu-madaktari na walimu, wanasheria na mahakimu maafisa wa mambo ya serikali na wafanyabiashara wanapaswa kupewa ujumbe dhahiri. “Itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote akipata hasara ya nafsi yake? Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake?” (Marko 8:36, 37). KN 80.8

Tunazungumza na kuandika mengi juu ya maskini waliotupwa; je, haipasi kuangalia pia matajiri waliotupwa? Wengi huwanesabu watu wa jamii hii kama wasio na matumaini, nao hufanya kiasi kidogo tu kuyafumbua macho ya wale ambao, kwa kupofushwa na kupumbazwa na nguvu za Shetani, wamepotewa na uzima wa milele katika hesabu yao. Maelfu ya matajiri wamekufa na kwenda makaburini mwao bila kuonywa kwa sababu wamepimwa kwa umbo la nje na kupitwa kando kama watu wasio na matumaini. Lakini, kinyume cha wanavyoonekana, nimeonyeshwa kuwa wengi wa watu wa jamii hii ni wenye kulemewa rohoni. Kuna maelfu ya matajiri wanaoumia kwa kukosa chakula cha kiroho. Wengi katika maisna yao ya kila siku huona haja yao ya kitu wasicho nacho. Wengi wao hawaendi kanisani, maana huona kwamba hawapati faida. Mafundisho wanayoyasikia hayagusi moyo. Je, tusijitanidi kwa ajili yao? KN 81.1

Wengine watauliza: Hatuwezi kuwafikia kwa vitabu na magazeti? Kuna wengi wasioweza kufikiwa kwa njia hii. Wanahitaji kuendewa. Je wafe bila kupewa onyo maalum? La, sivyo ilivyokuwa zamani za kale. Watumisni wa Mungu walitumwa kuwaambia wale walio na vyeo kwamba wangeweza kupata amani na raha kwa Bwana Yesu Kristo tu. KN 81.2

Mfalme wa mbinguni alikuja ulimwenguni mwetu kuokoa wanadamu waliopotea, na waliotenda dhambi. Kazi yake haikuwa kwa wale waliotupwa tu bali pia kwa wale wenye madaraka na heshima. Kwa akili alifanya kazi kupata njia ya kuzifikia roho za watu wa vyeo vikubwa wasiomjua Mungu na wasiozishika amri zake. KN 81.3

Kazi ile ile ilipaswa kuendelea baada ya kufa kwa Kristo. Moyo wangu umeumizwa sana nikisoma mambo yaliyofunuliwa na Bwana kwa Komelio. Komelio alikuwa mtu mwenye kazi ya madaraka, afisa katika jeshi la askari la Kirumi, lakini alikuwa akienenda kwa kuifuata sana num yote aliyokuwa ameipokea. Mungu akampelekea ujumbe maalum kutoka mbinguni, na kwa ujumbe mwingine uliomwongoza Petro kufika kwake na kumpa num. Lapaswa kuwa jambo kubwa la kututia moyo kazini mwetu kufikiri juu ya humma na upendo wa Mungu kwa wale ambao wanatafuta na kumwomba Mungu nuru. KN 81.4

Wako wengi ambao nimewaonyeshwa wenye kufanana na Komelio, watu ambao Mungu anataka sana wajiunge na kanisa lake. Humma zao ni juu ya watu wazishikao amri za Mungu. Lakini nyuzi zinazowarunga kwa ulimwengu huwashika imara. Hawana moyo wa adili kutwaa mahali pao pamoja na wanyenyekevu wa moyo. Yatupasa kufanya bidii maalum kwa ajili ya roho za watu hawa, ambao wanahitaji kazi maalum kwa sababu ya madaraka yao na majaribu. KN 81.5

Kwa nuru niliyopewa, nimeonyeshwa ya kuwa hata watu wenye madaraka, walio viongozi duniani, wanapaswa kuambiwa dhaniri lile neno la “Ndivyo asemavyo Bwana.” Ni mawakili ambao Mungu amewakabidhi amana kubwa. Kama watauitikia mwito wake, Mungu atawatumia kazini mwake KN 82.1

Kuna wengine ambao hufaa hasa kwa kazi kwa jamii za watu wakubwa. Hawa imewapasa kumtafuta Mungu kila siku, kulifanya jambo la kujifunza kujua jinsi ya kuwafikia watu hawa, siyo mazungumzo ya kubahatisha tu kujuana nao bali kuwashikilia kwa mahubiri na kwa imani yenye nguvu, yenye kuonyesha upendo mwingi kwa ajili ya roho zao, kutia nia hasa ili wapate ujuzi wa kweli kama ilivyo katika Neno la Mungu. 21

Sura ya 9 - Vitabu na Magazeti ya Kanisa Hili

KAZI yetu ya kuchapisha vitabu ilianzishwa kwa uongozi wa Mungu chini ya uangalizi wake maalum. Ilikusudiwa kutimiza kusudi halisi. Waadventista Wasabato wamechaguliwa na Mungu kuwa watu wa pekee, waliotengwa na walimwengu. Kwa ufa mkubwa wa Neno la kweli amewatenga na chimbo la mawe la walimwengu na kuwaunganisha naye Mwenyewe. Amewafanya wajumbe wake na amewaita mawakili wake katika kazi ya mwisho ya wokovu. Amana kubwa kabisa ya kweli waliyopata kuaminiwa wanadamu, maonyo mazito sana ya kutisha ambayo yapasa kupelekewa binadamu kutoka kwa Mungu, yamekabidhiwa kwao ili wawapelekee walimwengu; na katika kuitimiza kazi hii nyumba zetu za kuchapisha vitabu ni miongoni mwa njia za kufaa sana. KN 83.1

Vitabu na magazeti yatolewayo kutoka nyumba zetu za kuchapisha hayana budi kuwatayarisha watu kuonana na Mungu. 1 KN 83.2

Ikiwako kazi moja yenye maana zaidi ya nyingine, kazi hiyo ni ile ya kuvieneza vitabu na magazeti yetu kwa watu na kwa njia hii kuwaongoza kuyachunguza Maandiko. Kazi ya utume kuingiza vitabu na magazeti yetu nyumbani mwa watu, kuuza vitabu, na kusali nao na kuwaombea kwa Mungu ni kazi njema na mojawapo ambayo itawaadilisha wanaume na wanawake kufanya kazi ya uchungaji. 2 KN 83.3

Uuzaji wa vitabu vyetu ni aina ya kazi ya uinjilisti iliyo kubwa na yenye faida sana. Vitabu vyetu vyaweza kwenda mahali ambapo mikutano haiwezi kufanywa. Mahali kama hapa mwinjilisti wa vitabu huwa badala ya mhubiri. Kwa kazi ya kuuza vitabu ukweli hutolewa kwa maelfu ambao isingekuwa hivyo kamwe wasingeusikia. KN 83.4

Wainjilisti wa vitabu hawana budi kwenda kwenye sehemu mbalimbali za nchi. Ukubwa wa kazi hii hulingana kabisa na ule wa kazi ya uchungaji. Mhubiri na mjumbe aliye kimya, wote wawili hutakikana kwa kuifanya na kuitimiza kazi kuu iliyo mbele yetu. 3 KN 83.5

Mungu ameweka kazi ya uinjilisti wa vitabu kama njia ya kuwatolea watu nuru iliyomo vitabuni mwetu, na wainjilisti wa vitabu wangevutwa na ukubwa wa kuleta mbele ya walimwengu upesi iwezekanavyo vitabu vilivyo muhimu kwa ajili ya mafundisho yetu na kwa kuwapatia nuru ya kiroho. Hii ndiyo kazi hasa ambayo Mungu apenda watu wake waifanye wakati huu. Wote wanaojitoa wakfu kwa Mungu kufanya kazi kama wainjilisti wa vitabu wanasaidia kutoa ujumbe wa mwisho wa onyo kwa walimwengu. Si kwamba tunaithamini kazi hii kupita inavyostahili; maana isingekuwa kwa ajili ya jitihada za mwinjilisti wa vitabu, wengi kamwe wasingelisikia onyo hili. 4 KN 83.6

Yapasa vitabu na magazeti yetu kuenea kila mahali. Hebu yatolewe katika lugha nyingi. Ujumbe wa malaika wa tatu umepasa kutolewa kwa njia hii na kwa njia ya mhubiri. Ninyi wenye kuuamini ukweli kwa wakati huu, amkeni. Ni wajibu wenu sasa kuingiza njia zote iwezakanavyo kuwasaidia wale wanaolifahamu Neno la Mungu kulihubiri. Sehemu ya fedha ipatikanayo kwa kuuza vitabu na magazeti yetu yapasa kutumiwa kuongeza vifaa vyetu ili kuzidisha vitabu na magazeti zaidi ambavyo vitafumbua macho na kuutayarisha udongo wa moyo. 5 KN 84.1

Nimeamuriwa kwamba hata mahali watu wanapousikia ujumbe huu kutoka kwa mhubiri, mwinjilisti wa vitabu angeendelea na kazi yake akishirikiana na mhubiri; maana ingawa mhubiri aweza kuutoa ujumbe huu kwa uaminifu, watu hawawezi kuushika wote. Hivyo kitabu ni kitu cha maana, licha ya kuwaamsha waone ukubwa wa Neno la Mungu kwa wakati huu, hata kuwafanya watie mizizi na kuwa na msingi katika ukweli na kuimarishwa katika kushindana na makosa ya udanganyifu. Magazeti na vitabu ni njia za Bwana Mungu za kuweka daima ujumbe kwa ajili ya wakati huu mbele za watu. Katika kutia nuru na kuziimarisha roho za watu katika Neno la Mungu, vitabu na magazeti vitafanya kazi iliyo kubwa zaidi ya ile iwezayo kufanywa kwa kulihubiri Neno peke yake. Wajumbe wa kimya ambao huwekwa nyumbani mwa watu kwa njia ya kazi ya mwinjilisti wa vitabu watayatia nguvu mahubiri ya Injili kwa kila njia; maana Roho Mtakatifu ataichoma mioyo ya watu wakivisoma vitabu, sawa na anavyoichoma mioyo ya wale wanaoyasikiliza mahubiri ya Neno la Mungu. Huduma ile ile ya malaika hutumika kwa vitabu vyenye ukweli kama inavyotumika katika kazi ya mhubiri. 6 KN 84.2

Mipango ya busara na ifanywe kuwasaidia wanafunzi wanaostahili kujipatia gharama zao za Shule kwa kuviuza vitabu hivi, kama wakipenda. Wale ambao hujipatia fedha ya kutosha kwa njia hii hulipa gharama zao za shule katika vyuo vyetu wanamofundishwa watenda kazi watajipatia maarifa ya kufaa yenye maana sana ambayo yatawasaidia kwa kazi ya utume mahali papya katika nchi zingine. 7 KN 84.3

Washiriki wa kanisa wakifahamu ukubwa wa kuvieneza vitabu na magazeti yetu, watatumia wakati zaidi kwa kazi hii.” 8 KN 85.1

Kadiri muda wa kuangaliwa kama twafaa au hatufai unavyoendelea, patakuwako nafasi kwa mwinjilisti wa vitabu kufanya kazi. 9 KN 85.2

Ndugu na dada, Mungu atapendezwa kama mtashikilia kwa moyo kusaidia nyumba ya kuchapisha vitabu kwa sala zenu na kwa mali zenu. Ombeni kila siku asubuhi na jioni ili ipate kupokea mbaraka mkubwa wa Mungu. Msitie nguvu lawama na manung’uniko. Manung’uniko na malalamiko yasitoke midomoni mwenu; kumbukeni kuwa malaika huyasikia maneno hayo. Wote hawana budi kuongozwa kuona kuwa nyumba hizi za kazi zimewekwa na Mungu. Wale wanaozivunjia heshima ili kujipatia faida wao wenyewe itawabidi kutoa hesabu kwa Mungu. Mungu anakusudia kwamba kila kitu kihusucho kazi yake kitendewe kama kitakatifu. 10

 

Sura ya 10 - Imani kwa Mungu Aliye Hai

ITAONEKANA siku ya kukata maneno mara ya mwisho kuwa Mungu alijua jina la kila mmoja. Kuna shahidi asiyeonekana kwa kila tendo la maisha. “Nayajua matendo yako” ndivyo asemavyo “yeye aendaye katikati ya vinara saba vya dhahabu.” (Ufunuo 2:1). Imejulikana nafasi zilizodharauliwa, jinsi Mchungaji Mwema alivyofanya bidii bila kulegea kuwatafuta wale ambao wamepotea katika njia zilizopotoka, na kuwarudisha kwenye njia ya salama na amani. Mara kwa mara amemulika nuru ya Neno njiani mwao, ili wapate kuona hatari yao, na kuepuka. Lakini wamezidi kuendelea, wakifanya mzaha na kudhihaki wakisafiri katika njia pana, mpaka mwishowe muda wao wa kuangaliwa kama wanafaa au nawafai uishe. Njia za Mungu ni za haki na sawa; na hukumu itakapotolewa juu ya wale wanaoonekana wamepungua, kila kinywa kitafumbwa. 1 KN 86.1

Mungu ni roho; lakini ni nafsi, maana mtu aliumbwa kwa sura yake. Kazi ya mikono ya Mungu kwenye viumbe si Mungu mwenyewe. Viumbe vya asili ni ufunuo wa tabia ya Mungu; kwa njia ya viumbe hivyo twaweza kuufahamu upendo wake, uwezo wake, na utukufu wake; lakini haitupasi kuvihesabu viumbe kama ni Mungu. Akili ya kazi ya sanaa ya wanadamu hutoa ustadi mzuri ajabu, vitu vinavyopendeza macho, na vitu hivi hutupa sisi wazo fulani la fundi huyo wa sanaa; lakini kitu kilichofanywa si mtu. Siyo kazi, bali fundi ndiye mwenye kustahili sifa. Hivyo, huku viumbe vikiwa ufunuo wa mawazo ya Mungu, siyo viumbe bali Mungu aliyeviumba ambaye hupaswa kutukuzwa. KN 86.2

Katika kumwumba mtu nguvu za Mungu wa pekee zilidhihirishwa. Wakati Mungu alipokuwa amemwumba mtu kwa sura yake, umbo la binadamu lilikuwa kamili katika maumbile yake yote, lakini halikuwa na uhai. Kisha Mungu wa pekee, asiye na mwanzo wala mwisho ambaye hakuumbwa akalipuiizia lile umbo pumzi ya uhai, na mtu akawa nafsi hai, mwenye kupumua, mwenye akili. Viungo vyote vya mwili wa binadamu vikafanya kazi. Moyo, ateri, vena, ulimi, mikono, miguu, akili, ufahamu wa ubongo-vyote vikaanza kazi yao, na vyote viliwekwa chini ya sheria. Mtu akawa nafsi hai. Kwa njia ya Yesu Kristo Mungu wa pekee alimwumba mtu na kumjalia akili na uwezo. KN 86.3

Mwili wetu haukufichika kwake tulipoumbwa kwa siri. Macho yaliona mwili wetu, ijapokuwa si kamili; na kitabuni mwake viungo vyetu vya mwili viliandikwa, kabla havijakuwako hata kimoja. KN 86.4

Zaidi ya viumbe vyote duniani, Mungu alikusudia kuwa binadamu, aliye kazi bora zaidi ya uumbaji wa Mungu apaswa kuonyesha mawazo ya Mungu na kufunua utukufu wake. Lakini binadamu asijitukuze mwenyewe kama Mungu. 2

Mungu Baba Amefunuliwa kwa Njia ya Kristo

Mungu aliye nafsi ya pekee, amejifunua mwenyewe kwa njia ya Mwanawe. Yesu, mng’ao wa utukufu wa Baba, “chapa ya nafsi yake” (Waebrania 1:3), alionekana duniani katika umoo la mwanadamu. Yeye aliye Mwokozi wa pekee alikuwa ulimwenguni humu, na alipaa juu. Sasa Mwokozi huyu wa pekee huwaombea watu mbinguni. Mbele za kiti cha enzi cha Mungu huhudumu kwa ajili yetu “Mtu mfano wa Mwanadamu (Ufunuo 1:13). KN 87.2

Kristo, Nuru ya ulimwengu, alivua utukufu wenye kutia kiwi machoni kwa mng’ao wake ambao alikuwa nao katika hali yake ya Uungu akaja kukaa kama mtu miongoni mwa wanadamu, ili wapate, pasipo kuteketezwa, kujua habari za Mwumbaji wao. Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote isipokuwa kama alivyofunuliwa kwa njia ya Kristo. KN 87.3

Kristo alikuja kuwafundisha wanadamu jambo Mungu alilotaka sana walijue. Mbinguni juu, duniani, baharini, tawaiona kazi ya mikono ya Mungu. Viumbe vyote huushuhudia uwezo wake, hekima yake, na upendo wake. Lakini hatuwezi kujifunza kutoka kwa nyota au bahari au maporomoko ya maji habari za nafsi ya Mungu kama ilivyofunuliwa kwa njia ya Kristo. KN 87.4

Mungu aliona kuwa mafunuo dhahiri zaidi ya viumbe vya asili yalitakikana kueleza nafsi yake na tabia yake pia. Alimtuma Mwanawe ulimwenguni kufunua, kadiri ambavyo macho ya wanadamu yangaliweza kustahimili, tabia na sifa za Mungu asiyeonekana. KN 87.5

Kama Mungu angetaka kuelezwa kana kwamba Yeye Mwenyewe hukaa katika viumbe vya asili-ndani ya ua, mti, ncha za majani, -Kristo hangewaambia neno hili wanafunzi wake alipokuwa duniani? Lakini kamwe Mungu hakunenwa hivi katika mafundisho ya Kristo. Kristo na mitume walifundisha dhahiri ukweli wa kuwako kwa Mungu wa pekee. KN 87.6

Kristo alifunua habari zote za Mungu ambazo wanadamu wenye dhambi wangeweza kustahimili pasipo kuangamizwa. Yu Mwalimu wa mambo ya Mungu mwenye kutia nuru. Kama Mungu angetufikiria kuwa tunahitaji mafunuo mengine kuliko vale yaliyofunuliwa kwa njia ya Kristo na katika Neno lake lililoandikwa, angeweza kuyatoa

Kristo Huwapa Wanadamu Uwezo wa Kufanyika Watoto wa Mungu

Hebu tuyachunguze maneno yale Kristo aliyosema ghorofani usiku kabla ya kusulibiwa kwake. Alikuwa akiikaribia saa yake ya jaribio naye alijaribu kuwafariji wanafunzi wake, ambao iliwabidi kujaribiwa sana. KN 88.1

Wale wanafunzi walikuwa hawajayafahamu maneno ya Kristo juu ya uhusiano wake na Mungu. Mengi miongoni mwa mafundisho yake yalikuwa yangali giza kwao. Walikuwa wameuliza maswali mengi yaliyoonyesha kutojua kwao uhusiano wao na Mungu na juu ya rikra zao za mambo ya sasa na yale ya baadaye. Kristo alitaka sana wawe na ujuzi dhahiri zaidi juu ya Mungu. KN 88.2

Siku ya Pentekoste Roho Mtakatifu alipomiminwa juu ya wanafunzi, wakafahamu maneno ya kweli ambayo Kristo alikuwa ameyasema kwa mithali. Mafundisho ambayo yalikuwa mafumbo kwao yakadhihirishwa. Ufahamu walioupata kwa kumiminwa kwa Roho uliwafanya kuona aibu juu ya mafundisho yao ya upuzi. Mawazo na maelezo yao yalikuwa upumbavu yakilinganishwa na hekima ya mambo ya mbinguni ambayo sasa waliyapokea. Waliongozwa na Roho, na nuru iliangaza ufahamu wao ambao ulikuwa gizani. KN 88.3

Lakini wale wanafunzi walikuwa bado hawajapokea utimizaji kamili wa ahadi ya Kristo. Walipokea ujuzi wote wa Mungu ambao waliweza kustahimili, lakini utimizaji kamili wa ahadi ambayo Kristo angependa kuwaonyesha dhahiri juu ya Baba ulikuwa bado kuja. Ndivyo ilivyo leo. Ujuzi wetu juu ya Mungu ni sehemu tu na si kamili. Shindano litakapokwisha, na yule Mtu Kristo Yesu akiwakiri mbele za Baba watenda kazi wake waaminifu, ambao, katika ulimwengu wa dhambi, wamemshuhudia kwa kweli, watafahamu dhahiri mambo ambayo hivi sasa ni mafumbo kwao. KN 88.4

Kristo alichukua mbinguni ubinadamu wake uliotukuzwa. Huwapa wale wanaompokea, uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ili mwishowe Mungu apate kuwapokea kama walio wake, kukaa pamoja naye milele. Kama, katika maisha haya, ni waaminifu kwa Mungu, hatimaye “watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao” (Ufunuo 22:4). Ni furaha gani ya mbinguni zaidi ya kumwona Mungu? Furaha gani kuu atakayoipata mwenye dhambi aliyeokolewa kwa neema ya Kristo zaidi ya kuutazama uso wa Mungu na kumtambua kama Baba?

Fikira za Mungu kwa Kila Mmoja wa Watoto Wake

Maandiko Matakatifu huonyesha dhahiri uhusiano baina ya Mungu na Kristo, nao hudhihirisha wazi nafsi ya kila mmoja. Mungu ni Baba wa Kristo; Kristo ni Mwana wa Mungu. Kristo amepewa cheo cha juu. Amefanywa sawa na Baba Mashauri yote ya Mungu hufunuliwa kwa Mwanawe. Umoja huu huelezwa pia katika sura ya kumi na saba ya Yohana, katika sala ya Kristo kwa ajili ya wanafunzi wake: KN 89.1

“Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenltuma ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.” (Yohana 17:20-23). KN 89.2

Maneno ya ajabu! Umoja uliopo baina ya Kristo na wanafunzi wake hauharibu nafsi ya ye yote kati yao wawili. Wanalo kusudi moja, nia moja, tabia moja, lakini si nafsi moja. Hivyo ndivyo Mungu na Kristo walivyo mmoja. KN 89.3

Mbingu na nchi zimo chini ya amri ya Mungu wetu, naye ajua kile hasa tunachohitaji. Twaweza kuona kidogo tu njia iliyo mbele yetu; “lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake aliye na mambo yetu.” (Waebrania4:13). Juu ya uharibifu wa duniam aketi hali amevikwa taji; mambo yote ni wazi kwa uchunguzi wake wa kimungu; na kutoka katika ukuu na utulivu wake wa milele huamuru kile ambacho amri yake Mungu yaona ni bora. KN 89.4

Hata shomoro mmoja haanguki chini pasipo Baba kujua. Chuki ya Shetani juu ya Mungu humwongoza kufurahia kuviangamiza viumbe visivyoweza kusema. Ulinzi wa Mungu tu ndio unaowalinda ndege na kuwahifadhi ili wapate kutupendeza kwa nyimbo zao za furaha. Lakini hawasahau hata shomoro. “Msiogope basi; bora ninyi kuliko mashomoro wengi.” (Mathayo 10:32). 2 KN 89.5

Sura ya 11 - Wakristo Kuwa Mfano wa Tabia ya Mungu

MUNGU amekusudia kudhihirisha kwa njia ya watu wake kanuni za ufalme wake. Ili kwamba katika maisha na tabia wapate kuzidhihirisha kanuni hizi, anataka sana kuwatenga na kawaida, mazoea, na desturi za ulimwengu huu. Anataka kuwaleta karibu naye, kusudi apate kuwajulisha mapenzi yake. KN 90.1

Kusudi ambalo Mungu anataka kulitimiza kwa njia ya watu wake leo ni lile alilotaka kulitimiza kwa njia ya Waisraeli alipowatoa kutoka Misri. KN 90.2

Kwa kuutazama wema, rehema, haki, na upendo wa Mungu uliodhihirishwa kanisani, walimwengu hawana budi kuona mfano wa tabia yake Mungu. Na ndipo sheria ya Mungu ikionyeshwa kwa mfano namna hii maishani, hata walimwengu wataufahamu ukuu wa wale wampendao na kumwogopa na kumtumikia kuliko watu wo wote wengine duniani. KN 90.3

Bwana humwangalia kila mmoja wa watu wake; na mipango yake kumhusu kila mmoja wa watu wake; na mipango yake kumhusu kila mmoja. Ni kusudi lake kuwa, wenye kuyaruata mafundisho yake matakatifu wawe wateule. Maneno haya yaliyoandikwa na Musa akiongozwa na Roho yanawahusu watu wa Mungu leo sawa na yalivyowanusu Waisraeli zamani: “Wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako; Bwana Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi.” (Kumbukumbu la Torati 7:6). 1 KN 90.4

Kufanza Tabia Ifananayo na Ile ya Kristo

Dini ya Kristo kamwe haimwondolei heshima mwenye kuipokea; kamwe haimfanyi duni au asiye na adabu, mwenye dharau au mwenye kujivuna, mwepesi wa hasira au mkali, asiye na huruma. Kinyume cha hayo, huifanya tamaa iwe safi, huziadilisha akili za kuchagua vema, na kuyasafisha na kuyaongoza vema mafikara, ikiwateka nyara kwa Kristo. Wazo la Mungu kwa ajili ya watoto wake ni bora kupita wazo lililo bora sana la binadamu. Ametia katika sheria yake takatifu nakala ya tabia yake. KN 90.5

Kipeo cha tabia ya Mkristo ni tabia ya Kikristo. Pamefunguliwa mbele yetu njia ya maendeleo ya daima. Tunao mradi wa kujipatia, kipimo cha kukifikia, hicho ni pamoja na kila kitu kizuri na safi na adili na bora. Daima yapasa pawepo kujitahidi kufanya maendeleo mbele na juu kwenye ukamilifu wa tabia. 2 KN 90.6

Tutakua kila mmoja wetu, kwa muda na kwa milele, vile mazoea yetu yatufanyavyo. Maisha ya wale wenye kufanya mazoea mema, na walio waaminifu katika kufanya kila kazi, watafanana na mianga yenye kutupa mionzi ya nuru juu ya njia ya wengine; lakini mazoea ya kutokuwa na uaminifu yakipendelewa, kama mazoea mabaya ya ulegevu, uvivu, na uzembe yakiachwa kuwa na nguvu, wingu jeusi kuliko giza la usiku wa manane litakaa imara juu ya maelekeo ya maisha haya na yale ya milele kumzuia mtu asiupate uzima wa wakati ujao. 3 KN 91.1

Heri mtu yule ayasikiaye maneno ya uzima wa milele. Akiwa ameongozwa na “Roho wa kweli” kwenye kweli yote. Hatapendwa, hataheshimiwa, wala kusifiwa na walimwengu; lakini atakuwa mwenye thamani kuu machoni pa Mungu. “Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu hatutambui, kwa kuwa haukumtambua, yeye” (1 Yohana 3:4). 4 

Kuishi kwa Ujasiri Leo

Neno la kweli la Mungu likipokewa moyoni laweza kuwahekimisha hata kuupata wokovu. Kwa kuliamini na kulitii mtapokea neema ya kuwatosha kwa kazi na shida za leo. Neema kwa ajili ya kesho hamuihitaji sasa. Yawapasa mwone moyoni kuwa mnawajibika na mambo ya leo tu. Shinda kwa leo; jikane nafsi kwa leo; kesha na kuomba kwa leo; pata ushindi kwa Mungu kwa leo. Hali za mambo yetu na mazingira yetu, mabadiliko ambayo kila siku hubainika pande zote kutuzunguka, na neno la Mungu lililoandikwa lenye kuona na kuthibitisha mambo yote-hayo hutosha kutufundisha wajibu wetu na kile kitupasacho kutenda, siku kwa siku. Badala ya kuyazuia mawazo ya moyo wako kuingia katika mkondo wa mafikara ambayo hayatakufaidia, yakupasa kuyachunguza Maandiko Matakatifu kila siku na kuzifanya kazi zile ambazo katika maisha ya kila siku zaweza sasa kuwa za kukuchosha, lakini ambazo hazina budi kutendwa na mtu fulani. 5 KN 91.3

Wengi huukazia macho uovu wa kutisha ulio kwa wingi pande zote kuwazunguka, ukafiri na udhaifu kila upande, nao nuongea juu ya mambo haya mpaka mioyo yao imejawa na huzuni na mashaka. Hutukuza kazi ya yule mdanganyifu mkuu ya mawazo ya moyoni na kutafakari mambo ya kukatisha tamaa yanayowapata maishani mwao, huku wakielekea kukosa kuuona uwezo wa Baba aliye mbinguni na upendo wake usio na kifani ndivyo Shetani apendavyo. Ni kosa kumfikiria yule adui wa haki kama mwenye uwezo mkuu, huku tukifikiria kidogo tu juu ya upendo wa Mungu na uwezo wake. Yatupasa kuzungumza habari za uwezo wa Kristo. Sisi wenyewe hatuwezi hata kidogo kujifungua kutoka mikononi mwa Shetani tulimoshikwa; lakini Mungu ameweka njia ya kuokoka.. Mwana wa Mungu anazo nguvu kutupigania, na “tunashinda, na zaidi ya kushinda kwa yeye aliyetupenda.” KN 91.4

Hakuna nguvu za kiroho kwa ajili yetu katika kufikiria udhaifu na uasi wetu wa dini, na kulilia uwezo wa Shetani. Ukweli huu mkuu hauna budi kuimarishwa kama kanuni yenye nguvu mawazoni na mioyoni mwetu,manufaa ya dhabihu iliyotolewa kwa ajili yetu; kwamba Mungu aweza naye huokoa kabisa wote wanaomwendea wakiafikiana na masharti yaliyotajwa katika Neno lake. Kazi ni kuyaweka mapenzi yetu kando ya mapenzi ya Mungu. Ndipo kwa njia ya damu ya upatanisho, tunakuwa washiriki wa tabia ya Mungu; kwa njia ya Kristo tu watoto wa Mungu, nasi tunayo hakika kwamba Mungu atupenda, naam, kama alivyompenda Mwanawe. Tu hali moja na Yesu. Twatembea mahali Kristo atuongozapo; Anao uwezo kulifukuza giza ambalo Shetani hulitupa liifunge njia yetu, na penye giza na mambo ya kukatisha tamaa mwangaza wa utukufu wake hung’aa mioyoni mwetu. KN 92.1

Ndugu na dada, kwa kumwangalia ndipo tunabadilika. Kwa kuutafakari upendo wa Mungu na wa Mwokozi wetu, kwa kuufikiria ukamilifu wa tabia ya Mungu na kudai haki ya Kristo kama haki yetu kwa imani, hauna budi kubadilishwa kuwa wenye sura ile ile. Basi, tusikusanye picha zote zisizopendeza-udhalimu na uovu na mambo ya kukatisha tamaa, yenye kuonyesha uwezo wa Shetanikuyakumbuka daima kuyazungumza na kuyalilia mpaka roho zetu zikatishwe tamaa. Roho ya mtu aliyekatishwa tamaa ni mwili wa giza, licha ya kujikosesha kuipokea nuru ya Mungu, hata huizuia isiwafikie wengine. Shetani hupenda kuona matokeo ya picha za ushindi wake, yakiwafanya wanadamu kuwa watu wasio na imani na kuwavunja moyo. 6 

Kuonyesha Tabia ya Mungu kwa Maisha ya Kuwafikiria Wengine Kuliko Mwenyewe Binafsi

Dhambi ambayo inapendwa sana, na ambayo hututenga na Mungu na kuleta magonjwa mengi ya kiroho yenye kuambukiza, ni choyo (kujifikiria naisi mwenyewe bila kujali wengine). Hapawezi kuwapo kumrudia Bwana isipokuwa kwa kujikana nafsi. Sisi wenyewe hatuwezi kufanya lo lote; lakini, Mungu akitujalia nguvu, twaweza kuishi na kutenda mema kwa wengine, na kwa njia hii kuepukana na uovu wa choyo. Hatuhitaji kwenda nchi za washenzi kuudhihirisha moyo wetu wa kutoa vyote wakfu kwa Mungu katika maisha ya kuwafaidia wengine na ukarimu. Yatupasa kulitenda hili nyumbani, kanisani, miongoni mwa wale tunaoshirikiana nao na ambao tunahusiana kazini. Papo hapo katika maisha ya kawaida ndipo nafsi ipaswapo kukanwa na kutiishwa. Paulo aliweza kusema: “Ninakufa kila siku” Kufa kila siku kwa nafsi katika matendo madogo ya maisha ndiko kunakotufanya washindaji. Yatupasa kujisanau nafsi katika kutaka kuwatendea mema wengine. Wengi wanapungunkiwa sana na upendo kwa wengine. Badala kufanya kazi yao kwa uaminifu, hujaribu kujipendeza nafsi zao wenyewe. KN 92.3

Mbinguni hakuna ye yote atakayejifikiria nafsi mwenyewe, wala kutafuta kujipendeza nafsi mwenyewe; bali wote, kwa upendo wa kweli na safi, wataitafuta furaha ya wenyeji wa mbinguni pande zote kuwazunguka. Kama tukipenda kuifaiai hali ya mbingum katika nchi mpya, hatuna budi kutawaliwa hapa na kanuni za mbinguni. 7 KN 93.1

Nalionyenswa kwamba pamekuwako kujipima kupita kiasi sisi kwa sisi, tukiwatwaa wanadamu wenye kufa kuwa mfano, hali tukiwa na kielelezo amini, asiyekosea. Haitupasi kujilinganisha na walimwengu, wala na mawazo ya wanadamu, wala na vile tulivyokuwa zamani kabla ya kulipokea Neno la Mungu. Lakini imani na cheo chetu ulimwenguni, kama ilivyo sasa hakina budi kulinganishwa na kile tungalichokuwa kama mwenendo wetu ungekuwa umeendelea daima mbele na juu kwa kuwa tumejidai kuwa wafuasi wa Kristo. Huu tu ndio ulinganifu wa sala uwezao kufanywa. Kwa kila mmoja wa wengine wote itakuwa ni kujidanganywa. Kama tabia ya moyoni na hali ya kiroho ya watu wa Mungu hailingani na mibaraka, majaliwa, na nuru ambayo wamejaliwa kuwa nayo, wanapimwa kwa mizani, na malaika hutoa ripoti, WAMEPUNGUA. 8 KN 93.2

Dhambi Isiyosameheka

Ni nini kifanyacho dhambi juu ya Roho Mtakatifu? Ni kumdhania Shetani kazi ambayo kwa kweli inatendwa na Roho Mtakatifu. Kwa mfano, hebu fikiri kuwa mtu fulani ni shahidi wa kazi ya pekee ya Roho wa Mungu. Analo jambo linaloonyesha kwamba kazi hii ni kazi inayopatana na Maandiko matakatifu, Roho hushuhudia pamoja na roho yake pia kuwa ni kazi ya Mungu. Lakini, baadaye huanguka majaribuni; kiburi, ukinaifu, au tabia nyingine mbaya, humtawala; na akikataa mambo yote yaonyeshayo tabia takatifu ya kazi hiyo, husema kuwa kile ambacho zamani alikuwa akikiri kuwa ni uwezo wa Roho Mtakatifu kilikuwa uwezo wa Shetani. Mungu hufanyia kazi moyo wa binadamu kwa njia ya Roho wake; na watu wanapompinga Roho makusudi na kuitaja kuwa yatoka kwa Shetani, hukata njia ambayo kwayo Mungu huweza kuwasiliana nao. Kwa kulikana jambo ambalo huonyesna kwamba Mungu amependezwa kuwapa, wanaifungia nje nuru ambayo imekuwa iking’aa mioyoni mwao, na matokeo yake huwa kuachwa gizani. Hivyo maneno ya Kristo yanathibitishwa. “Basi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza; si giza hilo!” (Mathayo 6:23). Kwa muda, watu waliotenda dhambi hii huenda wakaonekana kuwa watoto wa Mungu; lakini pakitokea hali za mambo ili kuikuza tabia na kudhihirisha kuwa ni watu wenye moyo gani, itaonekana kuwa ni wa yule adui, wakisimama chini ya bendera yake nyeusi. 9 KN 93.3

Kumkiri au Kumkana Kristo

Katika kuchangamana kwetu na watu mtaani, jamaa, au katika uhusiano wo wote wa maisha tuwezapo kuwepo, ama kwa upungufu ama kwa wingi, kuna njia nyingi ambazo kwazo twaweza kumkiri Bwana wetu na njia nyingi ambazo kwazo kwa kusema mabaya juu ya wengine, kwa mazungumzo ya upuzi, ubishi na maneno ya mzaha, kwa maneno ya bure, yasiyo na maana, au maneno makali, ama kwa kusema uongo, kinyume cha kweli. Kwa maneno yetu twaweza kuonyesha kuwa Kristo hayumo ndani yetu. Kwa tabia yetu twaweza kumkana kwa kupenda raha, kwa kuepuka kazi na mizigo ya maisha ambayo mtu mwingine hana budi kuichukua kama sisi tusipoichukua, na kwa kupenda anasa za dhambi. Pia twaweza kumkana Kristo kwa kiburi cha anasa za dhambi. Pia twaweza kumkana Kristo kwa kupenda anasa za dhambi. Pia twaweza kumkana Kristo kwa kiburi cha nguo tuvaazo kwa kufuata mtindo wa walimwengu, au kwa mwenendo mbaya usio wa adabu. Twaweza kumkana kwa kuyapendelea maoni yetu wenyewe na kujaribu kuudumisha utu wa kale au kujihesabu wenyewe kuwa wenye haki. Pengine twaweza pia kumkana kwa kufikiri sana juu ya mambo mengi yadhaniwayo kuwa ni magumu na taabu kwetu. KN 94.1

Hakuna mtu awezaye kumkiri Kristo kwa kweli mbele ya walimwengu isipokuwa nia na roho wa Kristo hukaa ndani yake. Haiwezekani kutoa kile tusicho nacho. Yapasa maongezi na mwenendo uonyeshe halisi na dhahiri neema na Kweli ya moyoni. Ikiwa moyo ni safi, mtiifu na mnyenyekevu, matunda yake yataonekana nje nayo yatakuwa kumkiri Kristo kwa nguvu kunakoleta kile kitakiwacho. 10 KN 94.2

Sura ya 12 - Kuishi Ulimwenguni Bila Kuwa Mtu wa Ulimwengu Huu

NALIONYESHWA hatari yetu, kama watu, ya kufanana na walimwengu badala ya kufanana na Kristo. Tuko sasa mipakani mwa ulimwengu wa milele, lakini kusudi la yule adui wa roho za watu ni kuuahirishia mbali wakati wa mwisho. Shetani atawashambulia kwa kila njia aonayo yafaa wale wanaodai kuwa ni wenye kuzishika amri za Mungu na wenye kungojea Kuja kwa Mwokozi wetu Mara ya Pili katika mawingu ya mbinguni kwa nguvu na utukufu mwingi. Atawaongoza wengi iwezekanavyo kuahirisha siku ya mabaya na kufanana rohoni na walimwengu, wakizifuata desturi za ulimwengu. Nalitishika kuona kuwa roho ya walimwengu ilikuwa ikitawala mioyo na nia za wengi ambao huukiri sana ukweli. Choyo na kutimiza tamaa mbaya bila kujizuia kulipendelewa nao, lakini utauwa halisi na uaminifu safi havikuzwi. 1 

Uaminifu wa Mkristo

Katika kila shughuli uwe mwaminifu kabisa. Ijapokuwa ushawishiwe namna gani, kamwe usidanganye wala kusema uongo hata katika jambo lililo dogo kabisa. Wakati fulani tamaa ya mwili yaweza kukushawishi kuacha njia nyofu ya uaminifu, lakini usibadili hata kidogo. Kama katika neno lo lote ukisema vile utakavyofanya, na baadaye uone kuwa umejihatarisha kwa kuwapendelea wengine, usibadili hata kidogo kanuni inayoyaongoza maisha yako. Timiza mapatano yako. 2 KN 95.2

Biblia hukataza kwa uthabiti uongo wote, udanganyifu, na hila. Haki na kosa vimeelezwa dhahiri. Lakini nalionyeshwa kuwa watu wa Mungu wamejiweka upande wa adui; wameshikwa na ushawishi wake na huzifuata hila zake mpaka wepesi wao wa kuona umepunguzwa nguvu kabisa. Kosa dogo la kupotoka na kuuacha ukweli, kubadili kidogo na kuyaacha matakwa ya Mungu, hudhaniwa kuwa si dhambi kubwa ikiwa pana uhusiano na pato la faida au hasara ya fedha. Lakini dhambi ni dhambi, kama ikitendwa na mwenye fedha mamilioni au ikitendwa na maskini mwombaji barabarani. Wale wenye kujipatia mali kwa udanganyifu hujiletea hukumu rohoni mwao. Yote yapatikanayo kwa udanganyifu na hila yatakuwa tu laana kwa mpokeaji. 3 KN 95.3

Mtu mwenye kusema uongo au kutumia udanganyifu hujipotezea heshima. Huenda asijue kuwa Mungu humwona, na huifahamu kila shughuli, na ya kuwa malaika watakatifu huyapima makusudi yake na kuyasikiliza maneno yake, na ya kwamba ijara yake itakuwa kama kazi zake zilivyo; hata kama ingewezekana kulificha kosa lake lisichunguzwe na wanadamu wala Mungu, kwamba yeye mwenyewe alijua, humwaibisha moyoni mwake na kumwondolea cheo cha tabia yake. Tendo moja haliyakinishi tabia, ila huvunja boma, na jaribu lingine hupokewa upesi kwa urahisi zaidi, mpaka mwisho yafanywe mazoea ya kusema uongo na kudanganya kazini, mpaka mtu huyo asiweze tena kuaminika. 4 KN 96.1

Mungu anataka watu kazini mwake, chini ya bendera yake, kuwa waaminifu kabisa, wasio na upungufu wo wote au lawama katika tabia, ambao ndimi zao hazitasema masingizio yo yote. Ulimi hauna budi kuwa wa kweli, macho hayana budi kuwa ya kweli, matendo yote pia yawe ya namna ambayo Mungu aweza kuyasifu. Tunaishi machoni pa Mungu Mtakatifu, ambaye kwa kicho asema, “Nayajua matendo yako.” Jicho la Mungu daima hutuangalia. Hatuwezi kumficha Mungu tendo hata moja lisilo la halali. Ushuhuda wa Mungu kwa matendo yetu yote ni ukweli ambao wengi hawaufahamu. 5 

Mwenye Kuamini-Mtu Bora Katika Biashara

Mtu mwiminifu kama kilivyo kipimo cha Kristo, ni mtu ambaye ataonyesha uaminifu. Vipimo vya udanganyifu na mizani ya uongo, ambayo kwayo wengi hujaribu kujipatia faida ulimwenguni, ni chukizo machoni pa Mungu. Lakini wengi wanaojidai kuzishika amri za Mungu huvitumia vipimo vya uongo na mizani ya uongo. Mtu akiambatana na Mungu kweli, na akiishika sheria yake kwa kweli, maisha yake yatadhihirisha neno hili; maana matendo yote yatapatana na mafundisho ya Kristo. Hataiuza heshima yake kwa ajili ya pato la faida. Kanuni zinazoyaongoza maisha yake zimejengwa juu ya msingi imara, na mwenendo wake katika mambo ya ulimwengu ni nakili ya kanuni zake. Uaminifu thabiti hung’aa kama dhahabu miongoni mwa mavi ya madini na takataka za ulimwengu. KN 96.3

Udanganyifu, uongo, na kukosa uaminifu huweza kusetirika na kufichwa machoni pa mwanadamu, lakini si machoni pa Mungu. Malaika za Mungu, wenye kuangalia maendeleo ya tabia na kupima thamani ya tabia ya moyoni, huandika vitabuni mbinguni matendo haya madogo ambayo huidhihirisha tabia. Kama fundi katika kazi za maisha za kila siku si mwaminifu na huidharau kazi yake, walimwengu hawatahukumu isivyo sahihi kama wakikadiria cheo chake katika mambo ya dini kama kilivyo kazini. KN 96.4

Imani juu ya kukaribia kwa kuja kwa Mwana wa Adamu katika mawingu ya mbinguni haitamfanya Mkristo wa kweli kuwa mtu asiyejali kazi ya kawaida maishani. Wenye kungojea ambao hulitazamia tokeo la Kristo karibuni hawatakuwa wavivu, bali wenye bidii kazini. Kazi yao haitafanywa kwa uzembe na kwa udanganyifu, bali kwa uaminifu, upesi, na kwa ukamilifu. Wale wanaojidanganya kwa kusema kuwa kutojali mambo ya maisha haya ni jambo lionyeshalo hali yao ya kiroho na kujitenga kwao na walimwengu wanadanganyika sana. Kusema kweli kwao, uaminifu, na unyofu hupimwa na kuthibitishwa katika mambo yaliyo ya kitambo tu. Kama ni waaminifu katika lile lililo dogo kabisa watakuwa waminifu katika mengi. KN 97.1

Nimeonyeshwa kuwa hapa ndipo wengi watashindwa kulistahimili jaribio. Huzikuza tabia zao halisi kwa kuyamudu mambo ya kitambo tu yawapasayo. Hudhihirisha uongo, hila, udanganyifu, katika kushughulika na wanadamu wenzao. Hawafikiri kuwa kupata kwao uzima wa milele kwa wakati ujao hutegemea juu ya namna wanavyoenenda katika maisha haya, na ya kuwa uaminifu mkubwa ni jambo muhimu katika kufanyika tabia ya haki. Kukosa uaminifu ndiyo asili ya hali ya uvuguvugu ya wengi walio umoja na Kristo nao huzidanganya nafsi zao wenyewe. Naona uchungu kusema neno hili kuwa kuna ukosefu wa kutisha wa uaminifu hata miongoni mwa wale waishikao Sabato. 6 

Shirika za Biashara na Walimwengu

Wengine hawana werevu wo wote wa mambo ya ulimwengu. Hawana sifa zitakikanazo, na Shetani huwafaidi. Mambo yakiwa hivi, watu kama hawa hawataendelea kukosa kujua kazi yao. Yawapasa wawe wanyenyekevu kiasi cha kutosha kushauriana na ndugu zao, ambao huutumainia uamuzi wao, kabla ya kutimiza mipango. Naliongozwa kwa fungu hili la Biblia: “Mchukuliane mizigo na kutimiza hivyo sheria ya Kristo.” (Wagalatia 6:2). Wengine si wanyenyekevu kiasi cha kuwaacha wale wenye busara kuwafikiria mambo hata wamefuata mipango yao wenyewe, na wamejitia shidani wenyewe. Ndipo huona haja ya kupata shauri na uamuzi wa ndugu zao; lakini mzigo huu huwa mzito jinsi gani zaidi ya hapo kwanza. Ndugu wasiende kushtaki katika baraza la hukumu kama ikiwezekana waepuke kufanya hivyo; maana kwa kufanya hivi humpa adui nafasi kubwa kuwatega na kuwatatiza. Ingekuwa heri kufanya mapatano ijapokuwa pawepo hasara. KN 97.3

Naliona kuwa alichukizwa na watu wake kuwa wadhamini wa wale wasioamini. Naliongozwa kwa mafungu haya ya Biblia: Mithali 22:26: “Usiwe mmoja wao wapanao mikono, au walio wadhamini kwa deni za watu.” Mithali 11:15: “Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia; achukiaye mambo ya dhamana yu salama.” Mawakili wasio waaminifu! Huwekea dhamana kile ambacho ni mali ya mwingine-Baba yao aliye mbinguni-na Shetani husimama tayari kuwasaidia watoto wake kuwavuta ghafula kwa nguvu kutoka mikononi mwa watu wa Mungu. Yawapasa waishikao Sabato wasishirikiane na wale wasioamini. Watu wa Mungu wanayaamini sana maneno ya wale wasio waaminifu, na huuliza shauri la msaada mawakili wake, na huwatumia kuwatatiza na kuwanyang’anya watu wa Mungu. 7 

Sura ya 13 - Biblia

KATIKA Maandiko Matakatifu maelfu ya vito vya thamani vya ukweli vimesetirika visionekane kwa mtafutaji wa juu juu. Shimo mnamochimbwa ukweli kamwe halimaliziki. Kadiri mnavyozidi kuyachunguza Maandiko Matakatifu kwa moyo mnyenyekevu, ndivyo mtakavyozidi kupendezwa, na kuzidi kuona moyoni mseme pamoja na Paulo: “Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!” (Warumi 11:33). KN 99.1

Kristo na Neno lake hupatana kabisa. Wakilipokea na kulisikia, hufungua njia imara kwa miguu ya wote ambao hupenda kuenenda katika nuru kama Kristo alivyo katika nuru. Kama watu wa Mangu wangelithamini Neno lake, tungekuwa na mbingu kanisani hapa chini. Wakristo watake sana, na kuwa na njaa, ya kulichunguza Neno hili. Washughulike wakati mwingine kulinganisha andiko moja na andiko lingine na kutafakari juu ya neno hili. Watamani zaidi nuru ya Neno hili kuliko magazeti ya kila siku asubuhi, au vitabu vya hadithi zisizo za kweli. Kitu ambacho wangalikitamani sana kingekuwa kula mwili na kunywa damu ya Mwana wa Mungu. Na matokeo yake yangekuwa kubadilishwa maisha yao ili yapatane na kanuni na ahadi za Neno la uzima. Lingekuwa ndani yao kisima cha maji, yakibubujikia uzima wa milele. Manyunyu ya neema yenye kuburudisha yangeburudisha na kuirudishia nguvu roho, ikiwafanya wasahau taabu yote na uchovu. Wangetiwa nguvu na moyo kwa maneno haya ya uongozi wa roho. 1 KN 99.2

Katika namna na mafundisno yake mbalimbali, Biblia inacho kitu cha kumpendeza kila mtu akilini na kuvuta moyo wa kila mmoja. Katika kurasa zake hupatikana historia ya zamani sana; maandiko ya habari za kweli kabisa za maisha ya mtu; kanuni za serikali kwa ajili ya kuitawala nchi, na kawaida za watu wa nyumbani,-kawaida ambazo kamwe hazilingani na hekima ya binadamu. Biblia ina elimu ya maana sana, utenzi mtamu kabisa na bora sana, wa kuingia moyoni na wa kutia huruma sana. Thamani ya maandiko ya Biblia ambayo haiwezi kupimika inaipa thamani kuu yakifikiriwa juu ya uhusiano wao na wazo lenye maana na lililo kubwa. Yakifikiriwa kwa wazo hili, kila kiini cha habari zake huwa chenye maana mpya. Katika maneno yaliyoelezwa kwa urahisi sana ya kweli kuna mafundisho yenye kimo kilichokwenda juu kama vile mbingu zilivyo nayo huenea hata milele. 2 KN 99.3

Yawapasa kujifunza kitu fulani kipya kutoka kwa Maandiko Matakatifu. Yachunguzeni kama hazina lliyositirika, maana yana ndani yake maneno ya uzima wa milele. Mwombeni Mungu hekima na akili kuyafahamu haya Maandiko Matakatifu. Kama mtafanya hivi mtaona utukufu mpya katika neno la Mungu; mtaona moyoni mambo mbalimbali yahusianayo na ukweli; Maandiko Matakatifu yangethaminiwa upya kwenu. 3 KN 100.1

Maneno ya kweli ya Biblia, yakipokewa yatuinua moyo wa mtu kutoka katika hali yake ya kidunia na ubaya wake. Kama neno la Mungu lingethaminiwa kama ipasavyo, vijana na wazee pia wangekuwa na unyofu wa moyo, nguvu za mafundisho ambayo ingewezesha kuyapinga majaribu. 4 

Jifunzeni kwa Bidii na kwa Utaratibu

Wazazi kama mkitaka kuwafundisha watoto wenu kumtumikia Mungu ifanyeni Biblia kuwa kitabu chenu cha mafundisho. Inafunua hila za Shetani. Ni kitu kikubwa chenye kuliinua taifa, cha kugombeza na chenye kutoa makosa ya tabia ya moyoni, kitu cha kuvumbulia ambacho hutuwezesha kupambanua baina ya kweli na uongo. Lo lote lifundishwalo nyumbani au shuleni, Biblia, ikipewa nafasi hii Mungu hutukuzwa, naye atawafanyia kazi katika kuwaongoa watoto wenu. Kuna shimo la mali ya kweli na uzuri katika hiki Kitabu Kitakatifu, na wazazi yawapasa kujilaumu wenyewe kama wasipokifanya kuwa cha kuwapendeza kabisa watoto wao. 5 KN 100.3

“Imeandikwa” peke yake ilikuwa ndiyo silaha ambayo Kristo alitumia wakati mshawishi alipokuja na hila zake. Kufundisha ukweli wa Biblia ni kazi kuu na ya maana ambayo kila mzazi anapaswa kuifanya. Kwa moyo mzuri, wa furaha uyaweke maneno ya kweli kama yalivyosemwa na Mungu mbele ya watoto. Kama baba na mama, mwaweza kuwa mfano wa mafundisho kwa watoto katika maisha ya kila siku kwa kutumia uvumilivu, huruma, na upendo, kwa kuwavuta kwako. Msiwaache kufanya wapendavyo, lakini waonyesheni kuwa kazi yenu ni kulifuata Neno la Mungu na kuwalea katika malezi na maonyo ya Bwana. KN 100.4

Shikeni utaratibu katika kujifunza Biblia na watu wa nyumbani mwenu. Heri kutojali kitu cho chote kingine cha kidunia ambacho chadumu muda kitambo tu, .. Ila hakikisheni kuwa roho inalishwa mkate wa uzima. Haiwezekani kukadiria matokeo mema ya saa moja au hata ya nusu saa kila siku inayotolewa wakfu kwa moyo wa furaha, na kutumiwa na watu wote kwenye Neno la Mungu. Ifanye Biblia kuwa yenye kujieleza yenyewe, ukiwakusanya pamoja wote ambao husemekana kuwa wenye kuhusikana na somo lililotolewa nyakati mbalimbali na kwa mambo ya namna mbalimbali. Usivunje darasa lako la nyumbani kwa ajili ya watu wajao kuamkia au wageni. Kama wakifika wakati wa somo hili, wakaribishe walishiriki. Acha ionekane kuwa unauthamini zaidi ujuzi wa Neno la Mungu kuliko mapato ya faida au anasa za dunia. Kama tungejifunza Biblia kwa bidii na kwa kumwomba Mungu sana kila siku, tungeona kila siku ukweli mzuri katika nuru mpya, dhahiri, na yenye nguvu. 6 KN 100.5

Yakupasa kuifanya Biblia kuwa kiongozi wako kama ukipenda kuwalea watoto wako katika malezi na maonyo ya Bwana. Hebu maisha na tabia ya Kristo itolewe kama kielelezo kizuri kwao kukiiga. Kama wakifanya kosa, wasomee kile ambacho Mungu alisema juu ya dhambi za namna hiyo. Panatakikana uangalifu wa daima na bidii katika kazi hii. Tabia moja mbaya iliyovumilika na wazazi, isiyosahihishwa na walimu, yaweza kuifanya tabia yote ya mtu kuwa mbaya na isiyo imara. Awafundishe watoto kuwa yawapasa wawe na moyo mpya; ya kuwa akili mpya za kupambanua mazuri hasa, hazina budi kufanyika ndani yao, na nia mpya kutiwa moyoni. Hawana budi kupata msaada kutoka kwa Kristo; hawana budi kuifahamu tabia ya Mungu kama ilivyofunuliwa katika Neno lake. 7

Hekima Takatifu Imeahidiwa Kwa Msomaji

Neno la Mungu, kama tabia ya Mwandishi wake Mtakatifu, hutoa siri ambazo kamwe haziwezi kufahamika kabisa na wanadamu. Huziongoza akili zetu kwa Mwumbaji, ambaye hukaa “katika nuru isiyoweza kukaribiwa.” (l Timotheo 6:16). Hututolea makusudi yake, ambayo yataufikia utimilifu wao tu milele na milele. Hutufanya tuyangalie mafundisho yenye kina kisicho na mwisho na maana kuhusu utawala wa Mungu na hali ulimwenguni. KN 101.2

Kuingia kwa dhambi ulimwengum, kufanyika mtu halisi kwa Yesu Kristo, kuzaliwa mara ya pili, ufufuo, na mafundisho mengine mengi yaliyotolewa katika Biolia, ni siri kubwa sana kwa akili za mwanadamu kueleza au hata kufahamu kabisa. Lakini Mungu ametupa sisi katika Maandiko Matakatifu mambo ya kutosha kuonyesha utakatifu wao, nasi hatupaswi kuonea mashaka wamekifikia kikomo cha ujuzi na maarifa, wangekoma kuendelea. KN 101.3

Kama ingewezakana kwa viumbe kupata ufahamu kamili wa Mungu na kazi zake, basi, wakiwa wamekifikia kipeo hiki, pasingekuwako na ugunduzi mwingine tena wa ukweli, wala kukua lcatika kumjua, wala maendeleo mengine ya akili au moyo. Mungu asingekuwa tena Mwenyezi; na wanadamu, wakiwa wamekifikia kikomo cha ujuzi na maarifa, wangekoma kuendelea. Basi, tumshukuru Mungu kuwa hivyo sivyo mambo yalivyo. Mungu hana mwisho; ndani yake yeye kuna “hazina zote za hekima na maarifa.” Na siku zote milele watu watakuwa wakichunguza daima, kuiifunza daima walakini hawawezi kumaliza hazina za hekima yake, wema wake, na uwezo wake. KN 101.4

Pasipo uongozi wa Roho Mtakatifu tutaelekea daima kuyapotoa Maandiko Matakatifu au kuyafasiri vibaya. Kuna kusoma Biblia kwa namna nyingi ambazo hakuna faida, na mara nyingi ni madhara kwa kweli. Neno la Mungu linapofunuliwa ovyo bila kicho na pasipo kumwomba Mungu, mawazo na upendo wa moyoni visipokazwa kwa Mungu au kupatana na mapenzi yake, moyo utatiwa giza na mashaka; na ye yote anayefungua Biblia na kuisoma kwa njia kama hiyo, moyo wa kuonea mashaka utaimarika. Adui hutawala fikira, na kushauri tafsiri au maana zilizopotoka. 8 

Kupenda Kujifunza Biblia Si Jambo la Kawaida

Wazee na vijana pia hudharau Biblia. Hawaifanyi somo lao la kujifunza, kanuni ya maisha yao. Hasa vijana ndio wenye kosa hili la kuidharau. Wengi wao wanapata nafasi kusoma vitabu vingine, lakini kitabu hiki chenye kuelekeza njia iendayo uzimani hakisomwi kila siku. Hadithi zisizofaa husomwa kwa bidii, huku Biblia ikidharauliwa. Kitabu hiki ni kiongozi wetu kwa maisha bora zaidi, na matakatifu zaidi. Vijana wangekitaja kuwa kitabu cha kupendeza sana walichopata kusoma kama akili zao zisingalipotoshwa na kule kusoma hadithi za uongo. 9 KN 102.2

Kama watu waliopata nuru kuu, yatupasa kuwa wenye kuinua hali katika mazoea yetu, katika maneno yetu, katika maisha yetu ya nyumbani na katika jamaa. Lipe Neno la Mungu hadhi cnake kama kiongozi nyumbani. Hebu lihesabiwe kama mshauri katika kila shida, kanuni ya kila kazi. Je, ndugu na dada zangu watasadikishwa kuwa kamwe hapawezi kuwapo mafanikio halisi kwa mtu awaye yote nyumbani lsipokuwa kama neno la kweli la Mungu hekima ya haki litawaongoza? Jitihadi zote zingefanywa na akina baba na mama kujibiidisha na kuacha mazoea ya uvivu ya kuihesabu kazi ya Mungu kama mzigo. Uwezo wa Neno la kweli la Mungu hauna budi kuwa njia ya kutakasa nyumbani. 10 KN 102.3

Katika miaka yao ya kwanza watoto yawapasa kufundishwa madai ya sheria ya Mungu na imani kwa Yesu Mwokozi wetu inayosafisha mawaa ya dhambi. Imani hii haina budi kufundishwa siku kwa siku kwa mafundisho na kielelezo. 11 

Kusoma Biblia Huzitia Akili Nguvu

Kama Biblia ingesomwa kama ipasavyo, watu wangekuwa wenye nguvu akilini. Mafundisho yaliyoelezwa katika Neno la Mungu, urahisi wao mkuu, mambo bora ambayo Neno la Mungu huyatia akilini hukuza uelekevu ndani ya mtu ambao bila ya hayo usingekuzwa. Katika Biblia kuna nafasi kubwa isiyo na kikomo ya akili. Mwanafunzi wa Biblia atatoka katika kuyatafakari mambo makuu ya Biblia akiwa safi zaidi, hali ameadilishwa mawazoni na kuwa na furaha moyoni kuliko kama angeutumia wakati huo kusoma kitabu cho chote kingine kilichotungwa na mwanadamu, hasa neno lo lote la hizo zenye tabia hafifu. Akili za vijana hukosa kuyafikia maendeleo yao bora kabisa wanapokataa chimbuko bora sana la hekima-Neno la Mungu. Kisa kinachoacha tuwe na watu wachache tu wenye nia njema, imara na thabiti ni kwa kuwa Mungu haogopwi, Mungu hapendwi, kanuni za dini hazifuatwi maishani kama lpasavyo. Mungu angependa tufaidi kila njia ya kukuza na KN 102.5 kuimansha uwezo wa akili zetu Kama Biblia ingesomwa zaidi, kama maneno yake ya kweli yangefahamika vizuri, tungekuwa watu wenye hekima na zaidi. Nguvu hutiwa moyoni mwa mtu kwa kuzichunguza kurasa zake. 12 KN 103.1

Mafundisho ya Biblia yana maana kubwa juu ya mafanikio ya mtu kuhusu mambo yote ya miasha haya. Huzifunua kanuni ambazo ni jiwe kuu la pembeni la mafanikio ya taifa-kanuni ambazo kwazo hufungwa hali njema ya maisha ya watu kwa jumla, na ambazo ni kitu kinacholinda usalama wa watu nyumbani. Kanuni ambazo pasipo kuwa nazo mtu hawezi kupata manufaa, furaha, wala heshima katika maisha haya, wala hawezi kutumaini kuupata uzima wa milele wa siku zijazo. Hakuna mahali maishani, ama namna ya mambo yampatayo mwanadamu maishani mwake, ambapo mafundisho ya Biblia hayamtayarishi mtu na kumsaidia katika hali hizo. 13 

Kristo Katika Biblia Nzima

Uwezo wa Kristo, Mwokozi aliyesulibiwa ambao unaweza kutoa uzima wa milele, hauna budi kutolewa kwa watu. Yatupasa kuwaonyesha kuwa Agano la Kale ni Injili kweli katika mifano na vivuli vya mambo yajayo kama Agano Jipya lilivyo katika uwezo wake ambao umefunuliwa. Agano Jipya halitoi dini mpya; Agano la Kale halitoi dini ya kubatilishwa na Agano Jipya. Agano Jipya ni mwendelezo na mafunuo tu ya Agano la Kale. KN 103.3

Habili alikuwa mwenye kumwamini Kristo, naye kwa kweli alikuwa mwenye kuokolewa na uwezo wake Kristo kama Petro au Paulo. Henoko alikuwa mjumbe wa Kristo hakika kama alivyokuwa Yohana yule mwanafunzi mpendwa. Henoko alikwenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa. Huyu alikabidhiwa ujumbe wa kuja kwa Kristo mara ya pili. “Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia Bwana alikuja na watakatifu wake maelfu elfu, ili afanye hukumu juu ya wote.” (Yuda 14). Ujumbe aliohubiri Henoko na kule kutwaliwa kwake mbinguni ulikuwa hoja kubwa ya kuwasadikisha wote walioishi siku zake. Mambo haya yalikuwa hoja ambayo Methusela na Nuhu waliweza kuitumia kwa nguvu kuonyesha kuwa wenye haki huweza kuhamishwa. KN 103.4

Yule Mungu aliyetembea pamoja na Henoko alikuwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Yeye alikuwa nuru ya ulimwengu wakati ule kama alivyo sasa. Wale walioishi wakati ule hawakukosa walimu wa kuwaongoza katika njia ya uzima; maana Nuhu na Henoko walikuwa Wakristo. Injili unetolewa katika mafundisho ya Mambo ya Walawi. Utii kamili unatakiwa sasa, kama ulivyotakiwa wakati ule. Ni jambo muhimu kama nini kwamba tunaufahamu ukubwa wa neno hili! KN 104.1

Swali ni kwamba: Asili ya upungufu kanisani ni nini? Jibu ni hili: “Tunaacha akili zetu kupotoshwa kutoka kwa Neno hili. Kama Neno la Mungu lingeliwa kama chakula cha rohoni kama lingeelezwa kwa heshima na unyenyekevu, pasingelazimu kuwa na shuhuda nyingi ambazo hutolewa mara kwa mara. Mahubiri mepesi ya Biblia yangepokewa na kufuatwa. 14 

Sura ya 14 - Shuhuda kwa Kanisa

KADIRI mwisho unavyozidi kukaribia na kazi ya kutoa onyo la mwisho kwa walimwengu inavyozidi kuenea, ndivyo linavyozidi kuwa jambo kubwa kwa wale wanaokubali ukweli wa wakati huu kufahamu vizuri hali na mvuto wa Shuhuda hizi, ambazo Mungu kwa majaliwa yake amezifungamanisha na kazi ya ujumbe wa yule malaika wa tatu tokea mwanzo wake hasa. KN 105.1

Zamani Mungu alisema na wanadamu kwa kinywa cha manabii na mitume. Siku hizi asema nao kwa Shuhuda za Roho wake. Kamwe haujakuwako wakati ambapo Mungu aliwafundisha watu wake kwa moyo wa bidii kuliko anavyowafundisha sasa juu ya mapenzi yake na njia apendayo waifuate. KN 105.2

Maonyo na maneno ya kukaripia hayatolewi kwa wakosaji miongoni mwa Waadventista Wasabato kwa sababu maisha yao yanastahili kulaumiwa zaidi ya maisha ya watu wengine wanaodai kuwa ni Wakristo wa makanisa mengine bali kwa sababu wanayo nuru kuu, na kwa ungamo lao wametwaa mahali pao kama watu wa pekee, wateule wa Mungu, wenye sheria ya Mungu ikiwa imeandikwa mioyoni mwao. KN 105.3

Maneno ya ujumbe niliyopewa kwa ajili ya watu mbalimbali mara nyingi nimeyaandika kwa faida yao nikifanya hivi kwa wengi wao walionisihi sana kuwafanyia vile. Kadiri kazi yangu ilivyozidi, hili likawa jambo kubwa na sehemu ya kunichosna ya kazi yangu. KN 105.4

Katika maono niliyopewa zamani miaka kama ishirini hivi iliyopita (1871) naliamriwa kutoa, kanuni kuu kwa kusema na kuandika na wakati huo huo kueleza hatari, makosa, na dhambi za watu mbalimbali, ili wote wapate kuonywa, kuadilishwa, na kupewa shauri jema. Naliona kuwa wote wangechunguza sana mioyo na mienendo yao wenyewe ili kuona kama hawakufanya makosa yayo hayo kama wengine walioonywa kwa maandishi hayo au kama maonyo yaliyotolewa kwa ajih ya wengine hayakuwahusu wao pia. Kama m hivyo, wangepaswa kuona moyoni kuwa mashauri na maneno ya kukaripia yalitolewa kwa ajili ya wale, nayo yangewafaa na kuwahusu wao kana kwamba yalikuwa yakinenwa kwao hasa. KN 105.5

Mungu anakusudia kuipima imani ya wote wanaojidai kuwa wafuasi wa Kristo. Ataupima unyofu wa sala za wale wote wanaojidai kuwa wanataka sana kujua wajibu wao. Atadhihirisha wajibu huo. Atawapa wote nafasi kubwa kukuza kile kilichomo mioyoni mwao. KN 105.6

Bwana hukaripia na kutoa makosa watu wanaojidai kuishika sheria yake. Huonyesha dhambi zao na kudhihirisha uovu wao kwa sababu ataka kuwatenga na dhambi na uovu wote, ili waukamilishe utakatifu kwa kicho cha Bwanaa. Mungu hukaripia, hulaumu na huwatoa makosa kusudi wapate kuadilishwa kutakaswa, kukuzwa, na hatimaye kupandishwa juu kitini pake pa enzi. 1

Kuwaelekeza Wanadamu Kwenye Biblia

Shuhuda zilizoandikwa si za kutoa nuru mpya, bali kutia moyoni kwa nguvu maneno ya kweli yaliyotolewa kwa uongozi wa Roho ambayo yamekwisha kufunuliwa. Wajibu wa mwanadamu kwa Mungu na kwa mwanadamu mwenzake umeelezwa dhahiri katika Neno la Mungu, lakini ni wachache wenu wenye kuitii nuru hii iliyotolewa. Kweli nyingine haikutolewa; ila Mungu kwa njia ya Shuhuda hizi ameyadhihirisha maneno makuu ya kweli ambayo yamekwisha tayari kutolewa na kwa njia aliyochagua yeye mwenyewe akayaleta mbele ya watu kuamsha na kuwatia moyo kwayo, ili wote wasiwe na udhuru wo wote. Shuhuda hizi hazipaswi kulitweza Neno la Mungu, bali kuziinua juu na kuziadilisha akili za moyoni kulifikia, kusudi urahisi mzuri wa Neno la kweli upate kuwavuta wote. 2 KN 106.2

Roho hakutolewa wala hawezi kupewa watu kutangua Biblia; maana Maandiko Matakatifu husema dhahiri kuwa Neno la Mungu ni kipimo ambacho kwacho mafundisho na mambo yote ya maisha hayana budi kupimwa.... Isaya asema, “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili bila shaka kwa hao hapana asubuhi.” (Isaya 8:20). 3 KN 106.3

“Ndugu J. huzitatanisha akili kwa kujaribu ionekane kana kwamba nuru aliyoitoa Mungu kwa njia ya SHUHUDA hizi ni nyongeza ya Neno la Mungu, lakini kwa kufanya hivi hukosa. Mungu ameona kuwa njia hiyo yafaa kuyaongoza mawazo ya watu wake kwenye Neno lake, ili awafahamishe Neno lake wazi zaidi. Neno la Mungu latosha kuzitia nuru akili zilizoingia giza kabisa na laweza kufahamika na wale aambao wanataka kulifanamu. Lakini ingawa baadhi ya hao, wengine wanaodai kulifanya Neno Lll.a Mungu somo lao huonekana wakienenda kinyume cha mafundisho yake yaliyo dhahiri kabisa. Basi, ili kuwaacha wanaume na wanawake pasipo udhuru wawezao kutoa, Mungu hutoa shuhuda dhahiri na nalisi, zenye kuwarudisha kwenye Neno ambalo waliacha kulifuata. Neno la Mungu hufungamanisha kwa jumla kanuni za matengenezo ya mazoea mema ya maisha, na shuhuda hizi, kwa jumla na kwa kila mmoja zimekusudiwa kuwatazamisha zaidi kanuni hizi hasa. KN 106.4

Naliitwaa Biblia na kuizinga na hizi Shuhuda kwa Kanisa, ambazo zilitolewa kwa ajili ya watu wa Mungu. Hapa nikasema habari za watu karibu wote zaguswa. Dhambi ambazo wanapaswaw kuepukana nazo zimeonyeshwa. Mashauri mema ambayo huyatamani huweza kupatikana hapa, yametolewa kwa ajili ya mambo ya wengine yakiwa na hali ya kuwafaa wao wenyewe pia. Mungu amependezwa kuwapa amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni. KN 107.1

Lakini si wengi wenu wajuao kwa kweli kila kilichomo ndani ya Shuhuda hizi. Hamyajui Maandiko Matakatifu. Kama mngalilifanya Neno la Mungu somo lenu la kujifunza, mkiwa na moyo wa kutaka kukichunguza kipeo cha Biblia na kupata ukamilifu wa Mkristo, msingehitaji Shuhuda hizi. Kwa sababu mmedharau kukifahamu Kitabu hiki kilichotolewa kwa uongozi wa Roho ndiyo maana Mungu amejaribu kuwapata kwa shuhuda nyepesi na dhahiri, zenye kuwatazamisha maneno yaliyotolewa kwa uongozi wa Roho ambayo mmeacha kuyatii, na kuwasihi kuitengeneza mienendo yetu ipatane na mafundisho yake safi na yaliyo bora. 4

Zipimeni Shuhuda Hizi kwa Matunda Yake

Hebu Shuhuda hizi zipimwe kwa matunda yake. Roho ya mafundisho yake ni nini? Matokeo yake ya baadaye ya mvuto wao ni nini? Wote wanaotaka sana kufanya hivyo wanaweza kufahamu vizuri matunda ya niozi hizi. Mungu ameona yafaa kufahamu vizuri matunda ya njozi hizi. Mungu ameona yafaa kuwaacha wazidi kukaa na kuimarika katika kushindana na nguvu za Shetani na mvuto wa wanadamu ambao wamemsaidia Shetani kazini mwake. KN 107.3

Ama Mungu analifundisha kanisa lake, akigombeza makosa yao na kuimarisha imani yao, ama sivyo. Kazi hii ama ni ya Mungu, ama sivyo. Mungu hashirikiani na Shetani kwa lo lote. Kazi yangu .... ama ni yenye muhuri ya Mungu ama muhuri ya yule adui. Hakuna kazi nusu nusu katika neno hili. Shuhuda hizi ama ni za Roho wa Mungu, ama wa Ibilisi. KN 107.4

Kama Mungu alivyojidhihirisha kwa njia ya Roho ya unabii, wakati uliopita, wakati uliopo, na wakati ujao umepita mbele yangu. Nimeonyesnwa nyuso ambazo kamwe nalikuwa sijaziona, na miaka ya baadaye nalizitambua nilipoziona. Naliamshwa usingizini nikijua dhahiri mafundisho niliyoonyeshwa akilini mwangu; nami nimeandika usiku wa manane, barua ambazo zimekwenda hata kulivuka bara hili na, zikikutana na wakati wa hatari, zimeepusha hasara kubwa kwa kazi ya Mungu. Hii imekuwa ndiyo kazi yangu kwa miaka mingi. Nimetiwa nguvu kukaripia na kugombeza makosa ambayo nalikuwa sikuyafikiri. Je, kazi hii yatoka juu au yatoka chini? 5 

Kusudi la Shetani ni Kutia Mashaka

Mara nyingi Shuhuda hizi hupokewa kabisa, dhambi na uzoefu wa kujifurahisha kwa anasa ukavunjwa, na mara moja matengenezo mapya huanzwa yanayopatana na nuru ambayo ameitoa. Lakini mara zingine mazoea mabaya ya dhambi hupendelewa moyoni, Shuhuda hizi zikakataliwa, na uahuru mwingi kwa kweli ukatolewa kwa wengine kama sababu ya kukataa kuzipokea. Sababu ya kweli haitolewi. Kufanya hivi ni kukosa moyo wa uadilifu nia yenye nguvu na kutawaliwa na Roho wa Mungu, kuyakataa mazoea mabaya yenye madhara. KN 108.1

Shetani anao uwezo wa kutia mashaka na kufanya hila za vipingamizi vya ushuhuda huu halisi ambao Mungu hutuma, na wengi huudhania kuwa ni sifa, alama ya akili walizo nazo, kuwa watu wasioamini na wenye kutoa hoja na kulaghai. Wale wanaotaka kuzionea mashaka watakuwa na nafasi tele. Mungu hakusudii kuondoa uwezekano wote wa kutokuamini. Hutoa ushuhuda, ambao hauna budi kuchunguzwa kwa uangalifu kwa moyo mnyenyekevu na mwelekevu, na wote wanapaswa kuamua wakitegemea ushuhuda huu. Mungu hutoa ushuhuda wa kutosha kwa ajili ya moyo mnyofu kuamini; lakini yeye ambaye hajali uzito wa ushuhuda kwa sababu tu yako mambo machache yasiyomwelea vizuri ataachwa katika hali baridi ya kushushwa moyo ya kutokuamini na kuonea mashaka, naye atavunjikiwa na imani. KN 108.2

Ni kusudi la Shetani kuidhoofisha imani ya watu wa Mungu katika Shuhuda hizi. Shetani ajua jinsi ya kuranya mashambuiio yake. Atenda kazi mioyoni kuamsha husuda na kutokuridhika na wale walio wakuu wa kazi. Kisha ndipo huhoji juu ya karama walizo nazo; ndipo, huanza kutozithamini sana, na yale mafundisho yaliyotolewa kwa njia ya njozi huyadharau. Halafu hufuata moyo wa kuonea mashaka juu ya mambo makubwa ya imani yetu, nguzo za hali yetu, ndipo kwa kuyaonea shaka Maandiko Matakatifu, hushuka hata kupotea milele (bila tumaini la wokovu). Shuhuda ambazo zilipata kuaminiwa zamani, zinapoonewa mashaka na kuachwa, Shetani hujua kuwa waliodanganvwa hawatakoma kwa hilo tu; naye huzidisha jitihada zake mpaka kuanzisha uasi dhahiri, ambao hauponyeki na mwishowe huwa kwenye uharibifu. Kwa kutoa nafasi ya kuonea mashaka na kutokuamini juu ya kazi za Mungu, na kwa kupendelea moyoni kutokuamini na moyo wa husuda kali, wanajitayarisha kudanganyika kikamilifu. Nao huondoka wakiwa na uchungu juu ya wale wanaothubutu kusema makosa yao na kugombezwa kwa dhambi zao. KN 108.3

Siyo tu kwamba wale wanaokataa Shuhuda hizi, au wenye kupendelea moyo wa kuzionea mashaka, wamo hatarini. Bali kuidharau nuru ni kuikataa pia. KN 108.4

Kama ukipotewa na matumaini katika Shuhuda hizi utapotoka na kuiacha kweli ya Biblia. Naogopa kwamba wengi hupenda kuingia katika kuhoji na kuonea mashaka, na kwa wasiwasi wangu nilio nao kwa ajili ya roho zenu napenda kuwaonya Je, ni wangapi watakaolitii onyo hili? 6

Kutokuzijua Shuhuda Hizi Si Udhuru

Wengi wanakwenda kinyume kabisa cha nuru ambayo Mungu amewapa watu wake, kwa sababu hawasomi vitabu vyenye nuru na hekima katika maonyo na makaripio. Masumbufu ya ulimwengu huu, kupenda desturi za walimwengu, na kukosa dini kumewapotosha kutoka katika nuru Mungu aliyotoa kwa neema nyingi, huku vitabu na magazeti yenye makosa vikienda pande zote nchini. Moyo wa kuonea mashaka na ukafiri huzidi kila mahali. Nuru ya thamani kuu itokayo katika kiti cha enzi cha Mungu, imefichwa chini ya kibaba. Mungu atawahesabia watu wake hatia ya kukataa huku. Hesabu haina budi kutolewa kwake kwa kila mwonzi wa nuru kwa maendeleo yetu katika mambo matakatifu, au kukataliwa kwa sababu lilikuwa jambo la kupendeza kuifuata tamaa. KN 109.1

Shuhuda hizi zingeingizwa kwa kila watu wa nyumbani washikao Sabato, na yawapasa ndugu kujua thamani yao na kuombwa kuzisoma. Haukuwa mpango wa busara sana kuviwekea vitabu hivi hesabu ya chini na kuwa seti moja tu kanisani. Yapasa pawepo katika jamii ya vitabu (maktaba) ya kila watu nyumbani na kusomwa mara kwa mara. Hebu viwekwe mahali viwezapo kusomwa na wengi. 7 KN 109.2

Nimeonyeshwa kuwa kutokuziamini Shuhuda hizi zenye maonyo, faraja, na laumu hufungia nuru isiwafikie watu wa Mungu. Kutokuamani ni kuyafumba macho yao ili wasiione hali waliyo nayo hasa. Wanadhani ushuhuda wa Roho wa Mungu katika maneno haya ya kukaripia hautakikani au kwamba hauwahusu. Watu kama hao wanaihitaji sana neema ya Mungu na busara ya kiroho, ili wapate kutambua upungufu wao katika ujuzi wa mambo ya kiroho. KN 109.3

Wengi ambao wameliasi Neno la Mungu hutoa udhuru wa mwenendo wao kuwa hawaziamini Shuhuda hizi. Sasa swali ni hili: Je; wataacha miungu yao ya sanamu ambayo Mungu hukataza, au wataendelea katika upotovu wao wa uzoefu wa anasa na kuikataa nuru waliyopewa na Mungu kugombea mambo yayo hayo wanayojifurahisha nayo? Swali la kujibiwa nao ni hih: Je, nijikane nafsi mwenyewe na kuzipokea shuhuda hizi kama zimetoka kwa Mungu; Shuhuda ambazo hukemea dhambi zangu, au nizikatae Shuhuda hizi kwa sababu zinakemea dhambi zangu? 8 

Kutumia Vibaya Shuhuda Hizi

Idadi ya kwanza ya Shuhuda hizi iliyopata kuchapishwa ilikuwa na onyo juu ya kutumia isivyofaa nuru ambayo imetolewa hivi kwa watu wa Mungu. Nikasema kuwa wengine walikuwa wamefuata njia isiyo ya akili, waliposimulia imani yao kwa watu wasioamini, na uthibitisho ukawa umetakiwa, walikuwa wamesoma maandishi yangu badala ya kwenda kwenye Biblia kupata uthibitisho. Nalionyeshwa kuwa njia hii ilikuwa si sawa nayo ingeweza kuwachukiza vibaya wale wasioamini juu ya ukweli. Shuhuda hizi haziwezi kuwa na uzito ama maana kwa wale wasiojua lo lote rohoni mwao. Haifai kusoma habari zake kwa watu kama hao. KN 110.1

Maonyo mengine kwa habari ya matumizi ya Shuhuda hizi yametolewa mara kwa mara, kama ifuatavyo:“Wahubiri wengine wako nyuma sana. Wanadai kuusadiki ushuhuda uliotolewa na wengine wao hufanya madhara kwa kuzifanya utawala wa udhalimu kwa wale waliokuwa hawana ujuzi wo wote kwazo, hali hushindwa kuzifuata wao wenyewe. Wenyewe walipewa shuhuda mara kwa mara ambazo wamezidharau kabisa. Mwendo wa namna hii si sawa.” KN 110.2

“Naliona kuwa wengi wamefaidi kile Mungu alichoonyesha kwa habari ya dhambi na makosa ya wengine. Wameikaza mpaka imeelekea kuidhoofisha imani ya wengi katika mambo amoayo Mungu ameyaonyesha, na pia kulikatisha tamaa na kulivunja moyo kanisa.” 9

Hatari ya Kuzilaumu Shuhuda Hizi

Katika ndoto ya hivi karibuni naliletwa mbele ya mkutano wa watu wengi, ambao wengine wao walikuwa wakijitahidi kuondoa maneno yenye kuchoma moyo ya ushuhuda mzito sana wa onyo ambalo nimewapa. Wakasema: “Twaziamini shuhuda za Bibi White; lakini anapotwambia mambo ambayo hakuyaona wazi katika njozi katika jambo fulani lenye kufikiriwa, maneno yake hayawi na maana zaidi kwetu kuliko maneno ya mtu awaye yote mwingine.” Roho wa Bwana, alinijia, nami nikaondoka na kuwakaribia katika jina la Bwana. KN 110.4

Sasa kama wale ambao maonyo haya mazito yananenwa kwao, husema, “Ni mawazo yas Bibi White mwenyewe, itanibidi kufuata vile nionavyo mimi mwenyewe,” na kama wakiendelea kutenda mambo yale waliyoonywa kutoyatenda, huonyesha kuwa hulidharau shauri la Mungu, na matokeo yake ni yale tu ambayo Roho wa Mungu amenionyesha yangekuwa madhara kwa kazi ya Mungu na uharibifu kwao wao wenyewe. Wengine watakao kuimarisha hali yao wanayoyadhania kuwa yatasaidia maono yao, na watayatilia mkazo iwezekanavyo; lakini kile ambacho huhoji mwendo wao, au ambacho hakipatani na maoni yao, hukitaja kuwa ni mawazo ya Bibi White, wakikana kuwa hakikutoka mbinguni na kukisawazisha na maoni yao wenyewe. KN 110.5

Basi, ndugu nawasihi msijitie kati yangu na watu, na kuikinga nuru ambayo Mungu apenda iwafikie. Kwa lawama zenu msiziondolee nguvu zote, maana zina uwezo wote hizi Shuhuda. Msijione moyoni kuwa mwaweza kuzichungua ili zifae mawazo yenu wenyewe, mkidai kuwa Mungu amewapa uwezo kufahamu kile kilicho nuru kutoka mbinguni na kile kilicho maneno tu ya hekima ya mwanadamu. Kama Shuhuda hizi hazisemi sawasawa na Neno la Mungu, zikataeni. Krito na Beliari hawawezi kuunganishwa. Kwa ajili ya Kristo msizitatanishe akili za watu kwa werevu na moyo wa wanadamu, wa kuonea mashaka na kuifanya kazi hii isiwe na matokeo yo yote mema ambayo Mungu ataka kufanya. Kwa kukosa busara za kiroho, usifanye hii njia ya Mungu jiwe la kujikwaza ambapo wengi watafanywa wajikwae na kuanguka, “na kunaswa na kuchukuliwa.” 10 

Jinsi ya Kupokea Karipio

Wale ambao hukaripiwa na Roho wa Mungu haiwapasi kuondoka na kushindana na chombo hiki kiadilifu. Ni Mungu, wala si mwanadamu mkosaji, ambaye amesema ili kuwaokoa na uharibifu. Si jambo la kumpendeza mwanadamu kwa hali yake ya asili kupokea karipio, waia haiwezekani kwa moyo wa mwanadamu usioadilishwa na Roho wa Mungu, kufahamu lazima ya karipio au mbaraka uliokusudiwa kuletwa. Akili za movoni kupotoshwa. Maonyo ya dhamiri hudharauliwa, na sauti yake haisikiki wazi. Hupotewa kidogo kidogo na uwezo wa kupambanua baina ya mema na mabaya, mpaka awe na fahamu halisi za kusimama kwake mbele za Mungu. Huenda akawa anatimiza namna ya dini na kwa bidii kuyapata mafundisho yake, huku akiwa hana roho wake. Hali yake ndiyo ile iliyoelezwa na Shahidi aliye Mwaminifu: “Wasema, mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.” Wakati Roho wa Mungu, kwa ujumbe wa karipio, asemapo kuwa hii ndiyo hali yake, hawezi kuona kuwa ujumbe huu ni kweli. Kwa hiyo, apaswa kulikataa onyo? La. Mungu ametoa ushuhuda wa kutosha, ili wote wapendao kufanya hivyo waridhike na tabia ya hizi shuhuda; na wakiisna kuzikiri kuwa zatoka kwa Mungu, ni wajibu wao kukubali lawama, ijapokuwa hawaoni wao wenyewe ubaya wa njia yao. Kama wangefahamu kabisa hali yao, kungekuwa na haja gani ya karipio? Kwa sababu hawaijui, Mungu kwa huruma huiweka mbele yao, kusudi wapate kutubu na kuongoka kabla ya kuchelewa sana. Wale wenye kulidharau onyo hili wataachwa katika upofu na kuendelea kujidanganya wenyewe; lakini wale ambayo hulitii, na wafanyao bidii kujitenga na dhambi na kuziacha ili kuwa na sifa njema zitakikanazo, watakuwa wakiufimgua mlango wa mioyo yao ili Mwokozi apate kuingia na kukaa nao. Wale amoao wanahusiana sana na Mungu ni wale ambao huijua sauti yake asemapo nao. Walio wa kirono huyapambanua mambo ya kiroho. Watu kama hao watashukuru kuwa Mungu ameonyesha makosa yao. KN 111.2

Daudi alijifunza hekima kutoka kwa mambo Mungu aliyomtendea na akasujudu kwa unyenyekevu katika kurudiwa na Mwenyezi Mungu. Maelezo kamili ya hali yake hasa yaliyotolewa na nabii Nathani yalifanya Daudi kuzifahamu dhambi zake mwenyewe nayo yalimsaidia kuziacha. Akakubali mashauri mema kwa moyo mnyenyekevu na kujidhili mbele za Mungu. “Sheria ya Bwana,” asema, “ni kamilifu, huburudisha nafsi.” (Zaburi 19:7). KN 112.1

“Kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa si wana wa halali.” (Waebrania 12:8) Bwana wetu amesema: “Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi (Ufunuo 3:19). “Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.” (Waebrania 12:11). Ingawa marudi haya yawe makali, yameamuriwa kwa upendo wa Baba, “ili tuushiriki utakatifu wake.”  11 

 

Sura ya 15 - Roho Mtakatifu

NI bahati njema ya kila Mkristo, licha ya kutazamia, hata kuhimiza kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Kama wote wanaolikiri jina lake wangezaa matunda kwa utukufu wake, upesi kama nini ulimwengu wote ungepandwa mbegu za Injili. Kwa haraka mavuno ya mwisho yangekomaa, na Kristo angekuja kukusanya nafaka pevu. KN 113.1

Ndugu na dada zangu, ombeni mpate Roho Mtakatifu. Mungu yu tayari kutimiza kila ahadi aliyoitoa. Mkiwa na Biblia zenu mikononi, semeni: “Nimefanya kama ulivyosema. Naonyesha ahadi yako, “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, mtafunguliwa,” Kristo asema: “Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” “Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.” (Mathayo 7:7; Marko 11:24; Yohana 14:13). KN 113.2

Kristo huwatuma wajumbe wake katika kila sehemu ya milki yake kuwajulisha mapenzi yake watumishi wake. Hutembea katikati ya makanisa yake. Ataka sana kuwatakasa, kuwaadilisha, na kuwaongoza vema wafuasi wake. Mvuto wa wale wanaomwamini utakuwa ulimwenguni harufu ya uzima iletayo uzima. Kristo anashika nyota katika mkono wake wa kuume, na ni kusudi lake kuacha nuru yake iangaze ulimwenguni kwa kupitia kwao. Hivyo anataka sana kuwatayarisha watu wake kwa kazi bora zaidi katika kanisa lake. Ametupa sisi kazi kuu kuifanya. Tuifanyeni kwa uaminifu. Hebu tuonyeshe katika maisha yetu kile neema ya Mungu iwezacho kuwafanyia wanadamu. 1 KN 113.3

Umoja Hauna Budi Kutangulia Kumwagwa kwa Roho Mtakatifu

Fahamu kwamba ilikuwa baada ya wanafunzi kuwa na umoja kamili, wakati walipokuwa hawakishindanii cheo kikubwa kuliko vyote, hapo Roho alipomwagwa juu yao. Walikuwa na umoja. Hitilafu zote zilikuwa zimeondolewa. Na ushuhuda walioutoa baada ya kumwagiwa Roho ulikuwa mmoja. Angalia neno hili: “Jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja.” (Matendo 4:32) Roho wake Yeye aliyekufa ili wenye dhambi wapate kuishi alihuisha kusanyiko lote la waaminio.2 KN 113.4

Wale wanafunzi hawakujiombea mbaraka wao wenyewe. Walikuwa wakilemewa na mzigo wa roho za watu. Injili ilikuwa haina budi kuenezwa mpaka mwisho wa dunia, nao walidai karama ya uwezo ambao Kristo alikuwa ameahidi. Kisha ndipo Roho Mtakatifu alipomwagwa, na maelfu wakaongoka kwa siku moja. KN 114.1

Kadhalika ndivyo inavyoweza kuwa sasa. Hebu Wakristo waache mafarakano yote na kujitoa kwa Mungu kwa ajili ya kukiokoa kilichopotea. Hebu waombe kwa imani moaraka ulioahidiwa, nao utafika. Kumwagiwa Roho katika siku za mitume kulikuwa “mvua ya vuli,” na matokeo yake yalikuwa mazuri. Lakini mvua ya masika itakuwa nyingi zaidi. Je, ahadi gani iliyotolewa kwa wale wanaoishi katika siku hizi za mwisho? “Irudieni ngome, enyi wafungwa wa tumaini; hata hivi leo nasema ya kwamba nitakurudishia maradufu.” “Mwombeni Bwana mvua wakati wa masika, naam, Bwana afanyaye umeme, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi kondeni.” (Zekaria 9:12; 10:1). KN 114.2

Kufaa kwa Mtu Hutegemea Kujitoa Kwake kwa Roho Mtakatifu

Mungu hataki tufanye kwa nguvu zetu wenyewe kazi iliyo mbele yetu. Ametujalia msaada wa Mungu kwa hatari zote ambazo hushinda njia za wanadamu. Hutoa Roho Mtakatifu kusaidia katika kila shida, kutia nguvu matumaini yetu, kutia nuru akili zetu za moyoni na kuisafisha mioyo yetu. KN 114.3

Kristo amefanya matayarisho ili kanisa lake liwe jamii ya watu walioongoka, ambao wameangazwa na nuru ya mbinguni, wenye utukufu wa Imanueli. Ni kusudi lake (Kristo) kwamba kila Mkristo awe amezungukwa na hali ya kiroho ya nuru na amani. Hakuna kikomo cha hali ya kufaa ya mtu ambaye, huweka kando moyo wa choyo au kujifikiri nafsi mwenyewe, na kutoa nafasi kwa kazi ya Roho Mtakatifu moyoni mwake na kuishi maisha ya kujitoa wakfu kabisa kwa Mungu. KN 114.4

Matokeo ya baadaye ya kumwagiwa Roho ile siku ya Pentekoste yalikuwa nini? Habari njema za furaha ya Mwokozi aliyefufuka katika wafu zilienezwa hata miisho ya ulimwengu uliokaliwa na watu (zamani zile). Mioyo ya wale wanafunzi ililemewa na mzigo wa ukarimu mwingi, wenye kina, na wenye kuenea sana ambao uliwahimiza kwenda hata mwisho wa nchi wakishuhudia na kusema: “Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo.” (Wagatia 6:14). Kadiri walivyolihubiri neno la kweli jinsi lilivyo ndani ya Yesu, mioyo ilishindwa na uwezo wa ujumbe huu. Kanisa likaona waongofu wakilijia kwa wingi kutoka pande zote. Watu walioasi dini wakaongoka tena. Wenye dhambi wakaiiunga na Wakristo katika kuitafuta lulu ya thamani kuu. Wale ambao walikuwa adui wakali kabisa walioipinga Injili wakawa ndio wenye kuitetea kwa ujasiri. Unabii ukatimizwa: Yeye aliye dhaifu atakuwa “kama Daudi.” Nayo nyumba ya Daudi itakuwa “kama malaika wa Bwana.” Kila Mkristo aliona ndani ya ndugu yake mfano mtakatifu wa upendo na moyo wa ukarimu. Moyo mmoja ulienea kwa wote. Jambo moja la moyo wa bidii lilimeza mengine yote. Tamaa tu ya waaminio ikiwa kuonyesha tabia ya Kristo jinsi ilivyo na kufanya kazi kuueneza ufalme wake. KN 114.5

Kwetu leo, kama ilivyokuwa kwa wale wanafunzi wa kwanza, tunayo ile ahadi ya Roho. Mungu leo atawajalia wanaume Siku ya Pentekoste walisikie Neno la wokovu. Saa hii hii Roho wake na neema yake ni kwa wote wanaozihitaji na watakaoliamini Neno lake. 3 

Roho Mtakatifu Atakaa hata Mwisho

Kristo alisema kuwa mvuto mtakatifu wa Roho hauna budi kukaa na wafuasi wake hata mwisho. Lakini ahadi hii haithaminiwi kama ipasavyo; na kwa hiyo kutimizwa kwake hakuonekani kama ambavyo ingalikuwa. Ahadi ya Roho ni neno lisilofikiriwa sana na matokeo ya baadaye huwa yale tu yawezayo kutazamiwa-kukosa mvua ya kiroho, giza la kiroho, upungufu wa kiroho, na mauti. Mambo madogo yasiyo na maana hushika usikivu wa watu, na uwezo mtakatifu ambao unalazimu kwa maendeleo na mafanikio ya kanisa, na ambao ungeleta mibaraka yote mingine pamoja nao, unakosekana, ingawa umetolewa kwa wingi kabisa. KN 115.2

Utovu wa Roho ndio ufanyao kazi ya Injili isiwe na nguvu. Elimu, talanta, ufasaha wa maneno, kila kipawa cha asili au cha kujipatia, huweza kupatikana lakini, pasipo Roho wa Mungu, hakuna moyo utakaoguswa, wala mwenye dhambi atakayeongolewa kwa Kristo. Ambapo, kama wakiwa na umoja na Kristo kama wanazo karama za Rono, maskini kabisa na wajinga sana miongoni mwa wanafunzi wake watakuwa na uwezo ambao matokeo yake yataonekana mioyoni. Mungu huwafanya njia ya mafuriko ya mvuto bora kabisa ulimwenguni. KN 115.3

Moyo wa bidii kwa Mungu uliwasukuma wale wanafunzi kulishuhudia Neno la Mungu kwa nguvu. Je, haipasi moyo huu kuwaka mioyoni mwetu tukikusudia kusimulia habari za upendo uokoao, za Kristo aliyesulibiwa? Je, haipasi Roho wa Mungu kufika leo, kwa kujibiwa sala iliyoombwa kwa bidii, na kuwajaza watu uwezo wa kufanya kazi? Kwa nini, basi kanisa ni dhaifu sana na lisilo na Roho? 4 KN 115.4

Roho Mtakatifu akitawala mioyo ya washiriki wetu wa kanisa, itaonekana makanisani mwetu hali ya juu zaidi katika mazungumzo katika kazi, katika mambo ya kiroho, kuliko inavyoonekana sasa. Washiriki wa kanisa wataburudishwa na maji ya uzima, na watenda kazi wafanyao kazi chini ya Bwana mmoja, yaani Kristo, watamdhihirisha Bwana wao katika roho, katika neno, katika tendo, na wataiona nguvu kuonga mbele katika ongezeko la nguvu la umoja na upendo, ambao utatoa ushuhuda kwa walimwengu kwamba Mungu alimtuma Mwanawe kufa kwa ajili ya wokovu wa wenye dhambi. Neno takatifu la kweli litatukuzwa; na kariri ling’aavyo kama taa iwakayo tutalifahamu wazi zaidi. 5 

Sura ya 16 - Kuondoa Vuzuizi Vya Umoja kati ya Mungu na Mwanadamu

MISHIPA ya fahamu ya ubongo ambayo hupelekea habari mwili mzima ndiyo njia tu ambayo kwayo Mungu aweza kupelekea habari kwa mwanadamu na kuyabadili maisha yake ya moyoni kwa undani. Lo lote linalozuia mwendo wa upesi mno katika mishipa ya fahamu hupunguza nguvu na uwezo wa maana, na matokeo yake ya baadaye ni kuzidhooiisha akili za moyoni. 1 KN 117.1

Utovu wa kiasi wa namna iwayo yote hupoozesha viungo vya fahamu na kudhofisha uwezo wa ubongo hata mambo yadumuyo milele yakawa hayathaminiwi, bali hulinganishwa na mambo ya kawaida. Uwezo bora zaidi wa akili, uliokusudiwa kwa makusudi bora, hutekwa nyara kwa tamaa mbaya zaidi. Kama mazoea yetu ya mwili si mema, uwezo wa akili na tabia ya moyoni hauwezi kuwa wenye nguvu; maana kuna ushirika mkuu baina ya mwili na tabia ya moyoni. 2 KN 117.2

Shetani hufurahi kuona wanadamu wakijitumbukiza ndani zaidi kwenye taabu na mashaka. Ajua kuwa watu wenye mazoea mabaya na miili dhaifu, hawawezi kumtumikia Mungu kwa bidii, kwa moyo wa kuendelea, na safi kama wenye nguvu. Mwili wenye ugonjwa huwa na matokeo yanayoonekana katika ubongo. Kwa akili twamtumikia Bwana. Kichwa ni boma la mwili. Shetani hushinda katika kazi ya uharibifu aifanyao kwa kuwaongoza wanadamu kujifurahisha kwa mazoea yanayowaangamiza, na kujiangamiza wao kwa wao; maana kwa njia hii humnyang’anya Mungu ibada inayomstahili. KN 117.3

Shetani daima yu macho kuwaweka kabisa wanadamu chini ya utawala wake. Uwezo wake mkubwa sana juu ya mwanadamu ni kwa njia ya tamaa ya chakula, na hii hujaribu kuitamanisha kwa kila njia iwezekanavyo. 3 

Njia Kuu ya Shetana ya Kuleta Uharibifu

Shetani aliwakusanya malaika wabaya pamoja kutafuta njia ya kufanya uovu mkubwa iwezekanavyo kwa wanadamu. Mashauri yakatolewa moja moja, mpaka mwishowe Shetani mwenyewe akafikiri njia. Akapenda kuyatwaa matunda ya mzabibu, pia ngano, na vitu vingine vilivyotolewa na Mungu chakula, na kuvigeuza viwe sumu ambayo ingeuharibu uwezo wa mwanadamu wa mwili, akili, na tabia ya moyoni, na hivyo atazishinda akili za kupambanua mema na mabaya hata Shetani apate kutawala kabisa. Kwa mvuto wa pombe watu huweza kufanya makosa ya uhalifu wa sheria ya kila namna. Kwa njia ya tamaa ya chakula iliyopotoka, walimwengu huharibiwa. Kwa kuwaongoza kunywa kileo, Shetani huweza kuwafanya wazidi kupungua kwenye mizani. 4 KN 117.5

Shetani anauteka ulimwengu nyara kwa njia ya kutumia pombe na tumbaku, majani va chai na kahawa. Akili Mungu alizotoa, ambazo zapaswa kuwekwa safi bila kizuizi, hupotoshwa kwa kutumia vitu vinavyozimua nguvu mwilini. Ubongo hauwezi tena kupambanua vizuri mema na mabaya. Adui hutawaia. Mwanadamu ameuza akili zake kwa kile ambacho humfanya kuwa mwenye wazimu. Hajui kitu kilicho halali. 5 KN 118.1

Mwumbaji wetu amemjalia mwanadamu mengi kwa ukarimu. Kama majaliwa haya yote ya Mungu yangetumiwa kwa busara na kwa kiasi, umaskini, ugonjwa, na dhiki vingekuwa karibu sana kuondolewa mbali kutoka duniani. Lakini ole, twaona pande zote mibaraka ya Mungu ikabadilishwa kuwa laana kwa uovu wa wanadamu. KN 118.2

Hakuna watu wenye hatia ya upotovu na wenye kutumia vibaya vipaji vya Mungu vya thamani kuliko wale ambao huyatumia mazao ya udongo katika kutengeneza pombe. Nafaka za chakula, matunda matamu, hugeuzwa kuwa vinywaji ambavyo huzipotosha na kuzirusha akili. Kama matokeo ya kutumia sumu hizi maelfu ya watu nyumbani hukosa raha na hata riziki zenyewe za maisha, mauaji na uhalifu wa sheria huzidi, na magonjwa na mauti huwaharakisha maelfu ya wenye kuvitumia vitu hivi kwenye kaburi la mlevi. 6 

Mvinyo Unaolevya

Divai ambayo Kristo aliifanya kwa maji katika karamu ya arusi ya Kana ilikuwa majimaji matupu ya zabibu. Hii ni “divai mpya ipatikanavyo katika kichala,” ambacho Biblia yasema, “Usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake” (Isaya 65:8). KN 118.4

“Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi;
Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.”
“Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole?
Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.”
“Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole?
Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno?
Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu?
Ni nani aliye na macho mekundu?
Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo;
Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.
Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu;
Litiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;
Mwisho wake huuma kama nyoka;
Huchoma kama fira”. KN 118.5

(Mithali 20:1; 23:29-32).

Maneno haya yanaeleza mfano halisi wa uharibifu na utumwa unaompata mtu kwa sababu ya ulevi, kwa namna asivyoweza mwanadamu awaye yote kuuelezea. Ulevi unamtia mtu utumwani, unamwondolea heshima, na hata akijulishwa hali yake jinsi ilivyo mbaya sana, hawezi kujitoa katika tanzi; atazidi “kuitafuta tena” (Mithali 23:35). KN 119.1

Mvinyo, pombe, na kinywaji kinachotengenezwa kwa kusindika matofaa hulevya kama vile vileo vilivyo vikali zaidi. Kutumia vileo hivi kunaamsha kiu ya kutaka kuvipata vile vilivyo vikali zaidi, ndivyo mazoea mabaya ya ulevi wa pombe yanavyoanza. Kunywa vileo kwa kiasi ni shule ambapo watu hufundishwa kuwa na maisha ya mlevi. Ingawa kazi ya vileo hivi visivyo vikali ni ya pole pole, lakini ni njia kuu ya kuingilia ulevini kabla mtu hajadhania hatari yake. KN 119.2

Hakuna haja ya kutumia maneno mengi ili kuthibitisha ubaya wa matokeo ya ulevi. Wenye macho mekundu, wenye kupumbaa wanaoangamia kwa kunywa ulevi mwingi-watu ambao pia Yesu Kristo aliwafia, na ambao malaika huwalilia-wako kila mahali. Wanatia fedheha ustaarabu wa watu tunaojivunia. Wao ni aibu na balaa na hatari ya kila nchi. 7 

Pombe Humfanya Mtu kuwa Mtumwa

Kiu ya mvinyo inapoendekezwa mtu kwa hiari yake mwenyewe huwekea mdomoni mwake funda ambayo humshusha chini katika hali iliyo mbaya kuliko ile ya mnyama, mtu ambaye alifanywa kwa sura ya Mungu. Akili hupumbazwa, na kupoozeshwa, tamaa mbaya za kinyama huamshwa, ndipo hufuata uhalifu wa sheria wenye kuishusha sana tabia. 8 KN 119.4

Kwa mvuto wa kinywaji wanywacho, watu huongozwa kutenda mambo ambayo, kama wasingalikuwa wameonja kitu chenye kulevya na kurusha akili, wangeepuka kwa hofu kuyatenda. Wakiwa katika hali ya kulewa, wako kwenye mamlaka ya Shetani. Huwatawala, nao husaidiana naye. 9 KN 119.5

Hivyo ndivyo (Shetani) atendavyo kazi akiwavuta watu kwa werevu kuziuza rono kwa pombe. Huutawala mwili, akili na roho, wala si mtu huyo tena, bali Shetani, ndiye ambaye hutenda mambo. Na ukatili wa Shetani hudhihirishwa kadiri mlevi auinuavyo mkono wake kumpiga mke ambaye ameahidi kumpenda na kumtunza siku zote za maisha yake. Matendo ya mlevi yanaonyesha ukali wa Shetani. 10 KN 119.6

Watu wanaotumia pombe hujifanya wenyewe watumwa wa Shetani. Shetani huwashawishi wale ambao wana kazi za madaraka katika njia za magari ya moshi, meli, na wale walio wakuu wa mashua au motakaa zilizojaa watu kwenda kujifurahisha kwa anasa, kutimiza tamaa ya chakula iliyopotoka, na kwa kufanya hivi kumsahau Mungu na sheria zake. KN 120.1

Hawawezi kuona kitu wanachokikaribia. Ishara hutolewa kwa makosa, na gari hugongana. Ndipo hufuata kushikwa na hofu kuu, mvunjiko na kufa. Hali ya mambo ya jinsi hii itazidi kuonekana. Maelekeo ya uharibifu wa mlevi hupitishwa kwa watoto wake, na kwa njia ya hao nao hata kwa vizazi vijavyo. 11 

Tumbaku ni simu Itendayo Kazi Taratibu

Tumbako ina sumu mbaya sana inayodhuru, ingawa inatenda kazi yake kwa siri polepole. Ingawa itumiwe kwa njia iwayo yote, inadhihirika kwa kuzidhoofisha nguvu za mwili; tumbaku ina madhara zaidi kwa sababu matokeo yake ni ya polepole sana, nayo ni vigumu kujulikana mwanzoni. Kwanza inaishtua mishipa ya fahamu, halafu inaipoozesha. Inaudhoofisha ubongo na kuutia bumbuazi. Mara nyingi hudhuru mishipa ya fahamu kwa nguvu zaidi ya vileo. Ni vigumu kufahamu hivi, na matokeo yake ni vigumu kuyaondoa kabisa mwilini. Kuitumia tumbaku kunaamsha kiu ya kutaka vileo, na kwa watu wengi inakuwa sababu ya mazoea mabaya ya kunywa pombe. KN 120.3

Kuvuta tumbaku kunamletea mvutaji masumbufu na gharama nyingi, ni mazoea machafu yanayomnajisi mvutaji mwenyewe na kuwaudhi wengine. Madhara ya tumbaku kwa watoto na vijana hayaelezeki. Watoto wa kiume wanaanza kutumia tumbaku mapema wangali wadogo. Mazoea mabaya yanayofanywa namna nii, hasa wakati mwili na akili za mtoto zinapoweza kupatwa upesi na madhara yake, yanadhofisha nguvu za mwili, hudumaza mwili, hupoteza akili, na huharibu tabia ya mtu. 12 KN 120.4

Hakuna tamaa ya asili ya kutaka tumbaku isipokuwa imerithishwa. KN 120.5

Kwa kutumia majani ya chai na kahawa tamaa ya kutaka tumbaku hujengeka. KN 120.6

Chakula kinachokolezwa viungo vikali vya chakula huunguza matumbo, huharibu damu, na kuvitayarishia njia vileo vikali zaidi. 13 KN 120.7

Kitoweo cha nyama kilichokolezwa kwa viungo vya chakula, chai na kahawa, vitu ambavyo mama wengine huwatia moyo watoto wao kuvitumia, huwatayarishia njia kuonea uchi vitu vinavyozimua nguvu mwilini, kama tumbaku. Kuvuta tumbaku hutia nguvu kiu ya pombe. 14 KN 120.8

Moshi wa Tumbaku Una Madhara kwa Wanawake na Watoto

Wanawake na watoto huumia kwa kuwa imewabidi kuvuta hewa ambayo imechafuliwa kwa kiko, sigara, au pumzi chafu ya mvutaji tumbaku. Wale wanaokaa katika hewa hii daima wataugua. 15 KN 121.1

Kwa kuvuta hewa yenye harufu mbaya, ambayo hutolewa kutoka mapafuni na kwenye vinyweleo vya ngozi, mwili wa mtoto mchanga hujazwa sumu. Huku ikifanya kazi kwa watoto wachanga kama sumu polepole, na kuleta madhara katika ubongo, moyo, ini, na mapafu, nata viungo hivyo vikadhoofika na kupotewa na afya taratibu, kwa wengine ina madhara yaliyo dhahiri zaidi, kwa kuleta kifafa, ugonjwa wa kupooza, na kufa kwa ghafula. Kila pumzi itolewayo kutoka mapafuni mwa mtumwa wa tumbaku hutia sumu hewa inayomzunguka. 16 KN 121.2

Mazoea haya mabaya kwa afya ya vizazi vilivyopita huwadhuru watoto na vijana wa siku hizi. Utovu wa akili, udhaifu wa mwili mishipa ya fahamu zilizochafuliwa na uchu usio wa kawaida hupitishwa kama urithi kwa watoto kutoka kwa wazazi. Na desturi hizo hizo zikiendelea kwa watoto, huongeza na kudumishwa matokeo mabaya ya baadaye. 17 KN 121.3

Majani ya Chai na Kahawa Haviutii Mwili Afya

Chai (kinywaji kinachotengenezwa kwa majani ya chai hasa) hufanya kazi mwilini kama kileo, nayo ikitumiwa zaidi inaleta kulewa. Kahawa na vinywaji vingine vipendwavyo na watu wengi vinaleta matokeo ya jinsi hii. Kwanza matokeo yake ni kufurahisha. Mishipa ya fahamu inashtuliwa tumboni; nayo inafikisha mchocheo wake mpaka kwenye ubongo, nao huamshwa na kuongeza mapigo ya moyo, na mwili mzima huwa kama ukizidishiwa nguvu, lakini siyo nguvu halisi, nayo inadumu muda mfupi tu. Uchovu unasahauliwa, na inaonekana kana kwamba nguvu za mwili zimeongezeka. Akili zinaamshwa na mambo yale yasiyoelekea kuwa kweli, yanakuwa kana kwamba ni kweli. KN 121.4

Kwa sababu matokeo ya namna hii watu wengi wanadhani kwamba chai au kahawa inawafaa sana. Lakini hili ni kosa. Chai na kahawa hazisadii kuuulisha mwili hata kidogo. Matokeo yao huwa kabla ya kuyeyushwa na kutulia tumboni, na hali inayoonekana kuwa na nguvu ni mshtuo wa neva tu. Nguvu za kileo zinapomalizika ndipo nguvu za mwili zisizokuwa za kawaida zinapungua, na matokeo yake ni uchovu na udhaifu mwingi. KN 121.5

Kuendelea kuvitumia vileo hivi kunaleta maumivu ya kichwa, kukosa usingizi, kiherehere cha moyo, maumivu ya tumbo, kutetemeka, na mabaya mengi mengineyo; kwa kuwa vinadhoofisha nguvu mwilini. Mishipa ya fahamu (neva) ikichoka inahitaji kupumzishwa badala ya kuchochewa na kutumikishwa kupita kiasi. 18 KN 121.6

Wengi wameasi dini na kuzizimua nguvu za mwili kwa chai na kahawa. Wale wazivunjao kanuni za afya watapofushwa akilini mwao na kuivunja sheria ya Mungu. 19 KN 122.1

Kutumia Madawa Ya Sumu

Tendo moja ambalo ni sababu ya magonjwa mengi, na madhara mengi ni kutumia namna za dawa zenye sumu bila kiasi. Kuna watu wengine ambao wakishikwa na ugonjwa fulani, hawajisumbui kupeleleza asili ya ugonjwa. Wanashughulika tu wawezavyo kuyatuliza maumivu na masumbufu yao. KN 122.2

Kwa kutumia dawa zenye sumu, wengine hujiletea magonjwa ya maisha, na watu wengi hufa ambao wangeendelea kuishi kama wangetumia njia halisi za kuponya magonjwa yao. Sumu iliyomo ndani ya namna nyingi za dawa zisizoponya kwa kweli huanzisha tamaa na mazoea yanayoharibu roho na mwili. Namna nyingi za dawa za siri zinazopendwa na wengi, na hata namna nyingine mazoea fulani katika maisha, kama vile kutumia vileo, afyuni, na bangi, ambayo ni mazoea mabaya zaidi yanayokuwa fedheha kwa wanadamu. 20 KN 122.3

Kuyatibu magonjwa kwa kutumia dawa zile zenye sumu (drugs), kama inavyotumika kwa kawaida, ni laana. Jizoeze kuepukana na dawa hizi zenye sumu. Usizitumie ila kwa nadra sana, na tegemea zaidi juu ya njia kuu za kujipatia afya; ndipo mwili utafaidiwa na dawa za Mungu - hewa safi, maji safi, mazoezi mazuri ya viungo vya mwili, dhamiri safi. Wale wanaoendelea kutumia majani ya chai, kahawa na nyama wataona kuwa inawabidi kupata dawa hizi zenye sumu, lakini wengi waweza kupona pasipo kutumia hata kidonge kimoja cha dawa kama wakizitii kanuni za afya. Dawa zenye sumu zisitumiwe ila kwa nadra tu. 21 

Waadventisti Wasabato-Mfano kwa Walimwengu

Sisi tunaodai kuwa viongozi, kuwa wachukuzi wa nuru ulimwenguni, kuwa askari waaminifu wa zamu kwa ajili ya Mungu, tulinde kila njia ambayo kwayo Shetani angeweza kuingilia na majaribu yake kuipotosha tamaa ya chakula. Kielelezo chetu na mvuto wetu hauna budi kuwa nguvu ya matengenezo haya mema. Yatupasa kuepukana na mazoea yo yote ambayo yataeneza dhamiri au kutia nguvu majaribu. Tusifungue mlango wo wote ambao utamwezesha Shetani kuingia moyoni mwa mwanadamu awaye yote ambaye ameumbwa kwa sura ya Mungu. 22 KN 122.5

Kwa habari za chai, kahawa, pombe, tumbaku, bangi, na vileo, njia ya salama ni kutokuvigusa. Haja ya watu wa kizazi hiki kutaka msaada wa uwezo wa nia thabiti iliyotiwa nguvu kwa neema ya Mungu, ili kuyastahimili majaribu ya Shetani na kupingana na uzoefu wa kujifurahisha kwa tamaa lliyopotoka ni kubwa mara mbili ya ilivyokuwa zamani za vizazi kadha wa kadha vilivyopita. Lakini kizazi hiki ni chenye uwezo kidogo wa kujitawala kuliko ule waliokuwa nao wale walioishi zamani zile. Wale wanaojifurahisha kwa tamaa ya vileo hivi wamerithisha tamaa zao za chakula zilizopotoka na ashiki kwa watoto wao, na uwezo mkuu zaidi wa tabia ya moyoni hutakikana kuzuia utovu wa kiasi, kutojizuia, au ulevi. Njia ya salama kabisa kuifuata ni kusimama imara upande wa kiasi (kutokunywa kileo cha namna yo yote) na kutojihatarisha. KN 123.1

Kama akili za moyoni mwa Wakristo zingeamshwa kulifahamu jambo hili la kuwa na kiasi katika mambo yote, wangeweza, kwa kielelezo chao, kuanza mezani mwao, kuwasaidia wale ambao ni dhaifu katika kujitawala, ambao wako karibu kukosa kabisa uwezo wa kushindana na uchu. Kama tungeweza kufahamu kuwa mazoea tunayoyafanya katika maisha haya yatadhuru moyo wetu katika mambo yale yadumuyo milele, ya kwamba mwisho utakavyokuwa hutegemea juu ya mazoea ya kuwa na kiasi, tungefanya bidii tuwezavyo kuwa na kiasi katika kula na kunywa. Kwa kielelezo chetu na kujitahidi sisi wenyewe twaweza kuwa njia ya kuwaongoa watu wengi na kuwaepusha na hali mbaya ya utovu wa kiasi, kutojizuia, au ulevi, uhalifu wa sheria, na mauti. Akina dada waweza kufanya mengi katika kazi hii kubwa kwa ajili ya wokovu wa wengine kwa kutumia wakati wao ulio wa thamani katika kuzoeza uteuzi na tamaa ya chakula ya watoto wao, kufanya mazoea ya kuwa na kiasi katika mambo yote, na kuwavuta kujinyima na kuwa na ukarimu kwa faida ya wengine. 23 KN 123.2

Sura ya 17 - Usafi wa Moyo na Maisha

MUNGU amewapa makao kuyatunza na kuyahifadhi katika hali bora kwa ajili ya kazi na utukufu wake Mungu. Miili yenu si mali yenu wenyewe. “Au hamjuia ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu.” “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi,“ 1 KN 124.1

Katika zama hizi za uharibifu wakati adui yetu Shetani kama simba aungurumaye atembeapo huko na huko akitafuta mtu apate kumla, naona inavyolazimu kuipaza sauti ya onyo. “Kesneni muombe, msije mkaingia majaribuni” (Marko 14:38). Kuna wengi walio na talanta nzuri ambao kwa uovu huzitoa zitumike kwa kazi ya Shetani. Onyo gani ambalo naweza kuwapa watu hawa ambao nujidai kuwa wametoka kwa walimwengu na kuachana na kazi zao za giza na ambao Mungu amewafanya ghala za kuwekea sheria yake, lakini huku kama mtini wa fahari, huonyesha wazi wazi mbele za Mwenyezi Mungu, matawi yao yanayositawi, lakini hayazai matunda kwa utukufu wa Mungu? Wengi wao huyafurahia, mafikara yasiyo safi, mawazo mabaya, mapenzi yasiyo matakatifu, na tamaa mbaya. Mungu huyachukia matunda yanayozaliwa na mti wa namna hii. Malaika, wema na watakatifu huuchukia sana mwenendo wa namna hii, huku Shetani akiufurahia. Aha, laiti wanaume na wanawake wangefikiri kile ambacho hakina budi kupatikana kwa kuiasi sheria ya Mungu! Kwa hali iwayo yote, uasi ni fedheha kwa Mungu na laana kwa mwanadamu. Yatupasa kuuhesabu hivi, si neno uwe unaoonekana kuwa haki namna gani, na ijapokuwa utendwe na mtu gani awaye yote. 2 KN 124.2

Wenye moyo safi watamwona Mungu. Kila wazo lisilo safi huinajisi rono, huchafua akili za moyoni, na kuelekea kufutilia mbali mivuto ya Roho Mtakatifu. Hutia giza maono ya kiroho, ili mtu asiweze kumwona Mungu. Bwana aweza naye humsamehe mwenye dhambi atubuye; lakini ajapokuwa amesamehewa moyo utabaki na kovu. Uchafu wote wa maneno au wa mawazo hauna budi kuepukwa na mtu ambaye angependa kuwa na akili safi za kweli ya kiroho. 3 KN 124.3

Wengine wataukiri uovu wa anasa za dhambi, lakini watatoa udhuru kwa kusema kuwa hawawezi kuzishinda tamaa zao mbaya. Hili ni ungamo lililo baya kabisa kwa mtu awaye yote kulifanya ambaye hulitaja jina la Kristo. “Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu” (2 Timotheo 2:19). Kwa nini kuna udhaifu kama huu? Ni kwa sababu tamaa za kinyama zimetiwa nguvu kwa kuzitumia mpaka zimepata nguvu kuutawala uwezo ulio bora zaidi. Wanaume na wanawake hawana kanuni inayoyaongoza maisha. Wanakufa kiroho kwa sababu wamejilisha vyakula vitamu muda mrefu hata uwezo wao wa kujitawala unaelekea kama kwamba haupo. Tamaa duni za mwili wao zinatawala, na uwezo ule ambao ungepasa kutawala umekuwa mtumwa wa tamaa mbaya. Roho imeshikwa katika kifungo duni kabisa. Tamaa ya mwili imezima moyo wa kutafuta utakatifu na kupozesha mafanikio ya kiroho. 4 

Usilinajisi Hekalu la Mungu

Kuzitawala akili za moyoni mwa vijana, kuyaharibu mawazo na kuamsha tamaa mbaya ndiyo kazi kubwa ya Shetani siku hizi za mwisho; maana anajua kuwa kwa kufanya hivi aweza kuwaongoza kutenda mabaya, na hivyo uelekevu wote ulio bora hautakuwa na thamani iwayo yote, naye aweza kuwatawala apendavyo mwenyewe. 5 KN 125.1

Roho yangu yawasikitikia vijana wanaoziendeleza tabia zao katika kizazi hiki kilichopotoka. Naogopa na kutetemeka kwa ajili ya wazazi wao pia; maana nimeonyeshwa kwamba kwa kawaida nawafahamu wajibu wao kuwalea watoto wao katika njia iwapasayo. Mila na desturi zinashamirishwa, na mara watoto hujifunza kuvutwa nazo nao wakaharibika; huku wazazi wao wema wakiwa wao wenyewe wametiwa ganzi na kulala bila kujali hatari yao. Lakini ni vijana wachache sana wasio na mazoea mabaya. Wengi huruhusiwa sana kutofanya mazoezi ya viungo vya mwili kwa kuogopa kwamba watafanya kazi kupita kiasi. Wazazi hubeba mzigo wenyewe ambao watoto wao wangeuchukua. KN 125.2

Kufanya kazi kupita kiasi ni vibaya lakini matokeo yaletwayo na uvivu ni mabaya na yapasayo kuogopwa zaidi. Uvivu huleta mazoea mabaya ya kujifurahisha kwa anasa. Kufanya kazi kwa bidii hakuchoshi wala kumaliza hata sehemu tano kwa moja ya nguvu kama mazoea mabaya. Kama kazi nyepesi iliyopangwa vizuri huwachosha watoto wenu, jueni hakika, wazazi, kuwa kuna kitu fulani kingine, siyo kazi yao, ambacho hudhoofisha miili yao na kuleta uchovu wa daima. Wapeni watoto wenu kazi ya juhudi, ambayo itaitumikisha misuli. Uchovu unaotokana na kazi ya namna hii utapunguza tamaa yao kujifurahisha na anasa na mazoea mabaya. 6 KN 125.3

Epuka kusoma au kuona mambo ambayo yataleta fikira mbaya. Kuza tabia ya uadilifu na uelekevu. 7 KN 125.4

Licha Mungu kutaka kuyatawala mawazo yako, hata hutaka kutawala tamaa na mapenzi yako. Wokovu wako hutegemea juu kutawala tamaa na mapenzi yako. Wokovu kutegemea juu ya kujitawala kwako katika mambo haya. Tamaa na upendo ni njia zenye nguvu. Kama zikitumiwa vibaya, kama zikitiwa kazini kwa nia mbaya, kama zikitumiwa mahali pasipostahili, zinaweza kukuletea uharibifu na kukuacha katika hali mbaya, pasipo Mungu na bila tumaini. KN 125.5

Kama unazoea kujifurahisha kwa tamaa za bure, na kuuruhusu moyo wako kufikiri mambo yasiyo safi, unayo hatia kubwa mbele za Mungu kana kwamba mawazo yako yalikwisha kutimizwa kwa vitendo nasa. Kile kinachozuia kutimiza tendo ni kukosa nafasi. Mawazo ya mchana na usiku ni mabaya na mazoea mabaya ya hatari mno. Yakiisha kufanyiwa kazi, karibu haiwezekani tena kuyavunja mazoea ya namna hiyo, na kuyaongoa mafikira kwenye mambo safi, matakatifu, na yaliyo bora. Itakubidi kuwa askari mwaminifu wa kulinda macho yako, masikio, na milango yako yote ya maarifa kama ukitaka kuutawala moyo wako na kuyazuia mawazo mabaya yasiyo na maana yasiiharibu roho yako. Uwezo wa neema peke yake ndio uwezao kazi hii muhimu sana. 8 KN 126.1

Kujifunza kupita kiasi, kwa kuifanya damu nyingi iende ubongoni huleta hali mbaya ya fadhaa ambayo huelekea kupunguza uwezo wa kujitawala, na mara nyingi huchochea tamaa au tamaa. Hivyo mlango huwa wazi kwa ucham. Kutumia vibaya au kutokutumia kabisa nguvu za mwili ni asili ya upotovu mwmgi unaoenea mahali pengi ulimwenguni. “Kiburi, na kushiba, na kufanikiwa,” ni maadui wakubwa wa maendeleo ya wanadamu katika kizazi hiki kama yalivyokuwa asili ya uharibifu wa Sodoma. 9 KN 126.2

Uzoefu wa kujifurahisa na tamaa mbaya zaidi utawafanya wengi kuyafumba macho yao wasiione nuru, maana huogopa kuwa wataziona dhambi ambazo hawapendi kuziacha Wote waweza kuona kama wakipenda. Kama wakichagua giza badala ya nuru, uhalifu wa sheria utakuwa ni ule ule, wala hakuna tofauti. 10 KN 126.3

Kufa ni bora kuliko kuivunja au kuiasi sheria ya Mungu, hili ndilo lingekuwa neno la hekima (kaulimbiu ya) kila Mkristo, Kama watu wanaojidai kuwa waongozi, wanaoyathamini maneno matakatifu sana, ya kweli, yanayotakasa ya Neno la Mungu, hatuna budi kukiinua kipimo juu zaidi ya mahali kilipo hivi sasa. Dhambi na wenye dhambi kanisani yawapasa kufanyiwa mashauri yao mara bila kukawia, ili wengine wasije wakaambukizwa. Ukweli na usafi huhitaji tufanye kazi kamili kuisafisha kambi na kuwaondoa akina Akani. Basi wale wenye madaraka wasikubali dhambi kuwapo kwa ndugu. Mwonyesheni kuwa hana budi kuacha dhambi zake ama sivyo. Atengwe kanisani. 11 KN 126.4

Vijana waweza kuwa na kanuni thabiti sana hata majaribu makubwa ya Shetani yasiweze kuwapotosha, na kuwafanya waasi. Samweli alikuwa mtoto aliyezungukwa na mivuto mibaya sana. Aliona na kusikia mambo ambayo yaliisikitisha roho yake. Wana wa Eli, waliohudumu katika kazi takatifu walitawaliwa na Shetani. Watu hawa walichafua tabia yote iliyowazunguka. Wanaume na wanawake kila siku walishindwa na dhambi na mabaya, lakini, Samweli alienenda bila mawaa. Mavazi yake ya tabia yalikuwa safi yasiyo na doa. Hakushiriki, wala kupendezwa na dhambi zilizowajaza Waisraeli wote ripoti mbaya ya kutisha sana. Samweli alimpenda Mungu; aliuweka moyo wake karibu na Mungu hata malaika akatumwa kuzungumza naye kwa habari ya dhambi za wana wa Eli ambazo zilikuwa zikiharibu Israeli. 12

Matokeo Yanayoletwa na Uchafu wa Tabia

Wengine wafanyao maungamo makuu hawaifahamu dhambi ya mazoea mabaya na matokeo yake ya hakika. Mazoea yaliyokwisha kuimarika muda mrefu yameupofusha ufahamu wao. Hawatambui uovu mkubwa mno wa dhambi hii inayomwondolea mtu heshima, ambayo hudhoofisha mwili na kuharibu uwezo wa mishipa ya fahamu ubongoni. Kanuni inayoongoza tabia ya moyoni ni dhaifu mno haiwezi kushindana na mazoea yaliyokwisha kupata nguvu. Maneno mazito ya ujumbe utokao mbinguni hayawezi kuingia kwa nguvu katika moyo ambao haukujengewa boma la kuulinda na uzoefu wa kosa hili linalomwondolea mtu heshima. Mishipa hii ya fahamu ya ubongo imepotewa na afya yake kwa mambo mabaya ya kuiridhisha tamaa mbaya sana kwa anasa za mwili. 13 KN 127.1

Uasherati umefanya mengi zaidi ya uovu wo wote mwingine kuziharibu tabia za wanadamu. Unatendeka kwa kadiri kubwa ya kutisha nao huleta magonjwa karibu ya kila namna. KN 127.2

Kwa kawaida wazazi hawadhani kuwa watoto wao hufahamu lo lote juu ya uovu huu. Mara nyingi wazazi ndio wenye dhambi hasa. Wametumia vibaya haki za ndoa yao, na kwa uzoefu wa kujifurahisha kwa anasa wameziimarisha tamaa zao mbaya za mwili yaani za ashiki. Na kadiri hizi zilivyoimarika, ndivyo tabia ya moyoni na uwelekevu vilivyodhoofika. Hali ya kiroho imeshindwa na tabia ya kinyama, wakiwa wanayo chapa ya tabia ya wazazi wenyewe. Watoto wanaozaliwa kwa wazazi hawa karibu siku zote watarithi mazoea haya ya kuchukiza ya uovu wa siri. Dhambi za wazazi hawa zitapatilizwa kwa watoto wao kwa sababu wazazi hawa wamewapa chapa ya tamaa mbaya walizo nazo wao wenyewe. KN 127.3

Wale wanaoimarika kabisa katika dhambi hii inayoharibu mwili na roho hawawezi kupata raha ila kwa shida mpaka mzigo wao wa dhambi hii ya siri umefunuliwa kwa wale wanaoshirikiana nao. Udadisi huamshwa mara hiyo, na uvumi wa uovu huenezwa kutoka kijana mmoja hata kwa mwingine, na kutoka kwa mtoto mmoja hadi kwa mtoto mwingine, mpaka watu karibu wote wapate habari za tendo la dhambi hii yenye kumwondolea mtu heshima. 14 KN 127.4

Tendo la mazoea haya mabaya ya siri huharibu nguvu za uhai wa mwili. Matendo yote yasiyo lazima yenye kuzitumikisha nguvu za mwili mwishowe huleta ulegevu wa mwili. Miongoni mwa vijana kiungo kikuu cha uhai, ubongo, hutumikishwa vikali siku zao za ujana hata huwa na upungufu na uchovu mkubwa, na kuuacha mwili uweze kupatwa na magonjwa mengi ya namna nyingi malimbali kwa urahisi. KN 128.1

Kama mtu akiwa na mazoea haya kutoka umri wa miaka kumi na mitano na kuendelea, mwili utakataa matumizi mabaya uliyoyapata, na unaoendelea kuyapata, nao utawafanya wapate adhabu ya uhalifu wa sheria zake, hasa kutoka umri wa miaka thelathini hadi thelathini na mitano, kwa maumivu mengi mwilini na magonjwa mbalimbali, kama vile ugonjwa wa ini na mapafu, maumivu ya neva, baridi yabisi, ugonjwa wa uti wa mgongo, ugonjwa wa figo, na kuwa na saratani. Baadhi ya mashine nzuri za mwili hushindwa, zikaacha kutenda kazi nzito zaidi itakiwayo kutendwa, ambayo huchafua utaratibu mzuri wa mwili na mara nyingi huwapo na ugonjwa mkali wa mwili, ghafula, na mwisho ni kufa. KN 128.2

Kuyaangamiza maisha pole pole lakini kwa hakika namna hii ni dhambi kubwa machoni pa Mungu sawasawa na kumwua mtu ghafula. Watu wanaojiharibu wenyewe, kwa makosa, watapata adhabu hapa, na wasipotubu kwa kweli, hawataruhusiwa kuingia mbinguni baadaye kama vile mtu anayeua ghafula hataruhusiwa mbinguni. Mapenzi ya Mungu huthibitisha uhusiano uliopo baina ya asili ya ugonjwa na matokeo yake ya baadaye. KN 128.3

Hatusemi kuwa vijana wote walio dhaifu ni wenye hatia ya haya mazoea mabaya. Kuna wale ambao wana moyo safi na bidii ya kufanya vyema yote yapasayo, ambao huumia kwa mambo mballmbali yanayowashinda. KN 128.4

Uovu wa kisirisiri ni kitu kinachoharibu kusudi lililo bora, bidii, na nguvu za nia kufanya tabia njema ya dini. Wote ambao wana ujuzi wa kweli wa kile kinachotokana na kuwa Mkristo wanajua kwamba wafuasi wa Kristo wanao wajibu mkubwa kama wanafunzi wake kuzitiisha tamaa zao zote, uwezo wao wote wa mwili na uelekevu wa akili zao chini ya mapenzi yake. Wale wanaotawaliwa na tamaa zao mbaya hawawezi kuwa wafuasi wa Kristo. Wamejitoa sana kumtumikia bwana wao, yaani, mwanzishaji wa kila ovu, hata hawawezi kuyaacha mazoea yao mabaya na kuchaguShauri la Wazazi Wamchao Mungu

Pakiwako na matokeo mabaya ya ndoa namna hii, kwa nini vijana wasierevuke? Kwa nini waendelee kuona kuwa hawahitaji shauri la wazee na la watu wenye akili zaidi? Kazini, wanaume na wanawake vile vile hujihadhari sana. Kabla ya kushika kazi yo yote ya maana, wanajitayarisha kwa kazi yao. Wakati, fedha, na kujifunza sana kwa uangalifu hutumiwa kwa jambo hili, wasije wakashindwa kufaulu katika jambo wanalojaribu kufanya. KN 134.5

Basi, ni uangalifu mkubwa namna gani ungepasa kutumiwa katika kuingia ndoa-wajibu ambao unayo matokeo katika vizazi vya baadaye na kwenye maisha ya wakati ujao? Badala ya kufanya hivi, inaingiliwa kwa ubishi, bila kicho, kwa tamaa mbaya, upofu, bila kufikiri kwanza. Maelezo tu ya jambo hili ni ya kwamba Shetani hupenda kuona hali mbaya na uharibifu ulimwenguni, naye husokota wavu huu kuzitega roho za watu. Hufurahia kuwapata watu hawa walio wapumbavu kupotewa na furaha yao ya ulimwenguni humu na makao yao katika ulimwengu ujao. KN 134.6

Je, watoto wafuate mapenzi na tamaa yao wenyewe bila kujali shauri na maamuzi ya wazazi wao? Wengine kamwe hawaelekei kufikiri hata kidogo vile wazazi wao watakavyo, wala kujali maamuzi yao yaliyo ya utu mzima. Kushika lao bila kujali wengine kumeufungia mlango upendo wa baba na mama usiingie mioyoni mwao. Mioyo ya vijana yahitaji kuamshwa katika jambo hili. Amri ya tano ndiyo amri tu ambavo imeungana na ahadi, lakini inadharauliwa hata hajaliwi kabisa na dai la mchumba. Kuudharau upendo wa mama, kutoheshimu malezi ya baba ni dhambi zinazokaa hali ya kuandikwa kitabuni juu ya vijana wengi. KN 135.1

Mojawapo ya makosa makubwa kwa jambo hili ni ya kuwa vijana na wale wasio na maarifa hawataki mapenzi yao kupingwa, ya kuwa pasiwepo na cho chote kinachoyaingilia mambo ya upendo wao. Kama kuna jambo moja lenye kuhitaji kutazamwa pande zote, hili ndilo jambo hilo. Msaada wa maarifa waliyo nayo watu wengine, na kulifikiri kwa makini jambo hili pande zake zote ni muhimu kabisa. Ni jambo linalodharauliwa mno na watu wengi. Kubalini shauri la Mungu na la wazazi wenu wenye kumcna Mungu, vijana rafiki zangu. Mwombeni Mungu juu ya neno hili. KN 135.2

Pengine utauliza, “Wazazi wangechagua mchumba bila kujali moyo au maoni ya mwana au binti yao?” Nakuuliza swali kama ipasavyo: je, mwana au binti angepaswa kujichagulia mchumba bila kushauriana na wazazi, hali hatua ya namna hii haina budi kuwa na matokeo ya baadaye kuihusu furaha ya wazazi wakiwa wanapenda watoto wao? Tena ingempasa yule mtoto, bila kuiali shauri na maonyo ya wazazi wake, kuendelea bila kubadilika? Najibu kwa dhati ya moyo: La; sivyo kama haoi, Amri ya tano yakataza mwenendo wa namna hiyo. “Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.” Hii ni amri yenye ahadi ambayo Mungu hakika ataitimiza kwa wale wanaotii. Wazazi wenye busara kamwe hawatawachagulia watoto wao wachumba bila kuyajali mapenzi yao. KN 135.3

Baba na mama wangeona kuwa ni wajibu kuongoza upendo wa vijana, kusudi wapate kuwekwa kwa wale watakaokuwa wenzi wanaofaa. Wangeona kuwa ni wajibu unaowapasa, kwa mafundisho na kielelezo cha maisha yao wenyewe, kwa msaada wa neema ya Mungu, kukuza tabia ya watoto tokea utotoni mwao ipate kuwa safi na bora na wavutwe kwa wema na uadilifu. Wanaofanana huvutana; wanaofanana huthaminiana. Hebu upendo kwa neno la kweli na usafi na wema utiwe moyoni, na vijana watatafuta urafiki wa wale wenye tabia hizi

a kumtumikia Kristo. 15 KN 128.5

Vijana wanapochagua mazoea mabaya sana wakati moyo ungali mwepesi kuumia, kamwe hawatapata nguvu za kukua kwa ukamilifu na kwa usawa wa mwili, akili, na tabia ya moyoni. 16 KN 128.6

Tumaini tu la wale wenye mazoea mabaya sana ni kuyaacha milele ikiwa wanaithamini afya hapa na wokovu wa milele baada ya maisha haya. Mazoea haya yanapoendekezwa kwa muda mrefu, inatakikana jitihada kubwa kuyapinga na kukataa kujifurahisha kwa anasa mbaya. 17 KN 128.7

Usalama tu kamili kwa watoto wetu juu ya kila tendo la upotovu ni kutafuta kukubaliwa kuingia zizini mwa Kristo na kuwekwa chini ya ulinzi wa Mchungaji mwaminifu na wa kweli. Yeye atawaokoa na kila ovu, na kuwakinga wasipatwe na hatari yo yote, kama wataitii sauti yake. Asema, “Kondoo wangu waisikia sauti KN 129.1

yangu na wanifuata.” Ndani ya Kristo watapata malisho, nguvu, na tumaini; hawatasumbuliwa na tamaa zisizotulia za kutaka kitu kuzipotosha akili na kuuridhisha moyo. Wameiona lulu ya thamani kuu, na moyo umetulia na kupata raha. Furaha yao ni ya namna safi, ya amani, bora, ya mbinguni. Hawayaruhusu masingizio, wala majuto. Furaha za namna hii hazidhuru afya wala kulegeza nguvu za akili, bali ni zenye kutia afya. 18 

Sura ya 18 - Kuchagua Mume au Mke

NDOA ni jambo ambalo litakuwa na mvuto na matokeo katika maisha yako ulimwengungi humu na katika ulimwengu ujao pia. Mkristo mwaminifu hataendelea na mipango yake katika jambo hili pasipo kufahamu kuwa Mungu anaikubali njia yake. Hatataka Kujichagulia. Haitupasi kujipendeza wenyewe, kwa maana Kristo hakujipendeza mwenyewe. Maana yangu siyo kwamba mtu awaye yote angeoana na mtu asiyempenda. Hiyo ingekuwa dhambi. Lakini mahaba na hali ya kuvutwa kwa urahisi visiruhusiwe kuleta uharibifu. Mungu ataka moyo wote, upendo halisi. KN 130.1

Wale wanaonuia kuoana ingewapasa kufikiri namna ya tabia na mvuto wa nyumba wanayotaka kuianzisha . Wanapokuwa wazazi, ndipo wanakabidhiwa kazi takatifu. Hali njema ya watoto wao katika maisha haya na raha ya maisha yajayo huwategemea wazazi zaidi. Kwa kadiri kubwa, wazazi ndio wanaokaza tabia za kiroho na za kimwili pia ambazo watoto huzifuatisha. Hali ya mtaani inategemea hali ya nyumba moja moja za watu wanaoishi pale. Mvuto wa kila nyumba utasaidia kuinua hali ya jamii ya watu mtaani ama kuishusha hadhi yake. KN 130.2

Yawapasa vijana Wakristo kutumia uangalifu mwingi katika kufanya urafiki na katika kuchagua wachumba. Angalia isiwe kile unachokidhania sasa kuwa dhahabu safi kikatokea kuwa madini nyingine isiyo dhahabu. Marafiki wa kidunia huelekea kuweka vikwazo katika njia ya kazi yako kwa Mungu, na roho za wengi huharibiwa na urafiki usio mzuri wala furaha, ama kazini ama ndoani, na wale ambao kamwe hawawezi kuinua hali au kuadilisha. KN 130.3

Pima kila jambo na kuangalia maendeleo yote ya tabia ya yule ambaye wafikiri kuungana naye katika maisha yako yote. Hatua unayokaribia kufanya ni moja iliyo ya maana sana maishani mwako, na isingefanyawa kwa haraka. Huku ukiwa na upendo. Angalia usikupofushe macho. KN 130.4

Chunguza kwa uangalifu ili kuona kama maisha yako va ndoa yatakuwa ya furaha au ya kutokupatana na mabaya. Hebu jiulize, Umoja huu utanisaidia kuelekea mbinguni? Utaniongezea upendo wangu kwa Mungu? Tena utazidisha ukubwa wa manufaa yangu katika maisha haya? Kama mawazo haya hayana kizuizi, basi, kwa kicho cha Mungu songa mbele. KN 130.5

Kuchagua mchumba kungekuwa sawa kabisa na kutafuta kujipatia hali bora ya mwili akili, na moyo kwa ajili ya wazazi kwa ajili ya watoto wao; hali ambayo itawawezesha wazazi na watoto kuwanufaisha wanadamu wenzao na kumtukuza Mwumbaji wao. 

Mambo ya Kuangalia kwa Mke Anayetazamiwa

Mvulana na achague msichana atakayesimama imara kando yake ambaye ataweza kuchukua sehemu yake ya mzigo wa maisha, mke ambaye mvuto wake utamwadilisha mumewe na kumfanya safi, na ambaye kwa upendo wake atamfanya awe na raha. KN 131.1

“Mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana.” “Moyo wa mumewe humwamini ....Humtendea mema wala si mabaya, siku zote za maisha yake.” “Hufumbua kinywa chake kwa hekima, na sheria ya wema 1 katika ulimi wake. Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; wala hali chakula cha uvivu. Wanawe huondoka na kumwita heri; mumewe nave humsifu, na kusema, Binti za watu wengi wamefanya mema, lakini wewe umewapita wote.” Yeye apataye mke wa namna hiyo “apata kitu chema; naye ajipatia kibali kwa Bwana.” KN 131.2

Hapa ni mambo yapasayo kufikiriwa: Je, yule unayekusudia kumwoa ataleta furaha nyumbani mwenu? Yu (mwanamke) mwangalifu, awezaye kutunza mali, ama akisha kuolewa, licha ya upeteza mapato yake, hata mali yako ataitawanya bure, huku akionyesha upendo wa juu iuu tu? Mwenendo wake ukoje wakati huu? Anacho kitu cho chote anachokitegemea wakati huu? Nafahamu kwamba mvulana ambaye amerukwa na akili kwa sababu va upendo na mawazo ya kuoa atayadharau maswali haya kana kwamba hayana maana wala manufaa yo yote. Lakini mambo haya yangefikiriwa sawasawa, maana yana matokeo katika maisha yenu ya wakati ujao. KN 131.3

Katika kuchagua mke, peleleza tabia yake uijue. Je, atakuwa mstahimililivu na mwenye bidii ya kazi? Au atachoka kumtunza mama yako na baba yako wakati hasa wanapohitaji mwana aliye na nguvu wa kumtegemea? Je, atakutenga nao ili kuitimiza mipango na makusudi yake na kumfaa kwa anasa zake mwenyewe, na kuwatupa baba na mama ambao, badala ya kupata binti mpendwa watakuwa wamepotewa na mwana? KN 131.4

Mambo ya Kuangalia kwa Mume Anayetazamiwa

Kabla hajatoa mkono wake kutia ndoa, kila mwanamke apaswa kuuliza kama mwanamume anayekaribia kuungana naye maisha yake yote anafaa. Habari zake za siku zilizopita zikoje? Maisha yake ni safi? Mapenzi anayoonyesha ni bora, ya tabia njema, au ni mahaba ya ovyo tu? Anayo tabia itakayomfanya kuwa mwenye furaha? (Mkewe) aweza kupata amani na raha halisi akiwa nae? Ataruhusiwa kuendelea na tabia zake, au itambidi kuyatupilia mbali yake na dhamiri ya moyo wake kwa sababu ya mamlaka ya mumewe? Je, aweza kuyaheshimu madai ya Mwokozi kama wajibu ulio mkubwa kuliko mambo yo vote mengine? Mwili na roho, mawazo na makusudi, yataweza kuhifadhiwa katika hali safi na takatifu? Maswali haya yana maana sana iuu ya hali bora ya kila mwanamke anayetarajia maisha ya unyumba. KN 131.5

Kila mwanamke anayetamani kuwa na unyumba wenye raha na amani apendaye kuepukana na taabu na huzuni za baadaye, hujiuliza maswali haya kabla ya kutoa ukubali wake wa mapenzi. Je, mpenzi wangu anaye mama? Tabia ya mama yake ikoje? Anaufahamu wajibu wake kwa mamaye? Anajali haja na furaha ya mamaye? Ikiwa hamjali wala kumheshimu mama yake, kweli ataweza kuonyesha heshima na upendo, wema na usikivu kwa mkewe? Shani ya arusi itakapokuwa imekwisha, atadumu kunipenda? Atanivumilia kwa makosa yangu, ama atakuwa akinitoa makosa mara kwa mara, mgomvi na mkali? Mapenzi ya kweli yatasamehe makosa mengi; upendo hautayaona. KN 132.1

Msichana amkubali kama mwenzake wa maisha mtu yule tu aliye na tabia safi ya utu, mwenye bidii, mwangalifu mwenye heshima, mwaminifu na mnyofu, mwenye kumpenda na kumcha Mungu. KN 132.2

Epukana na wafidhuli au wale wasio na adabu. Epukana na mvivu; epukana na mtu mwenye kuyadhihaki mambo matakatifu. Usishirikiane na mtu mwenye kutumia maneno mabaya yasiyo ya dini, au mzoefu wa kunywa japo bilauri moja ya pombe. Usisikilize posa za mtu asiyefahamu wajibu wake kwa Mungu. Neno la kweli, safi, ambalo hutakasa roho ya mtu litakupa moyo mkuu kujitenga na kuachana na rafiki mwenye kupendeza sana ambaye wajua hampendi wala kumcha Mungu, ama haiui lo lote juu ya kanuni za haki halisi. Twaweza siku zote kuvumilia udhaifu wa rafiki na ujinga wake lakini kamwe hatuwezi kustahimili maovu yake. 

Upendo ni Kipaji cha Thamani Kitokacho kwa Yesu

Upendo ni kipaji cha thamani, tupatacho kutoka kwa Yesu. Upendo safi na mtakatifu siyo kuona moyoni, bali ni kanuni. Wale ambao wamevutwa na upendo wa kweli si wapumbavu wala vipofu. KN 132.4

Upendo halisi, wa kweli, wa moyoni, ni safi na adimu sana. Kitu hiki cha thamani chapatikana kwa shida. Wengine huita tamaa mbaya upendo. KN 132.5

Upendo wa kweli ni kanuni bora takatifu, tofauti kabisa na namna ya upendo unaoamshwa na tamaa, ambao hufa mara ukijaribiwa vikali. KN 132.6

Upendo ni mmea unaokua vizuri mno, nao hauna budi kukuzwa na kulishwa. Moyo wa upendo, maneno ya kweli na upendo, yatafanya watu wa nyumba kuwa wenye furaha na kutoa mvuto wenye kuinua hadhi kwa wote walio mahali wanapoweza kufikiwa na mvuto wao. KN 133.1

Huku upendo safi ukimwingiza Mungu katika mipango yake vote, na kupatana kabisa na Roho wa Mungu, tamaa mbaya itakuwa kaidi isiyosikia shauri la mtu, ya kipumbavu, yenye kudharau amri zote, nayo itafanya kitu ilichokichagua kuwa mungu wa sanamu. Katika tabia vote ya mtu mwenye upendo wa kweli, neema ya Mungu itadhihirishwa. Adabu, utovu wa anasa, unyofu, adili, na dini itafanywa kila hatua inayofanywa kuielekea ndoa. Wale ambao wametawaliwa hivi hawatamezwa na mazungumzo waliyo nayo, na kupoteza moyo wa kupenda mkutano na sala na ibada ya dini. Moyo wao wa bidii kwa Neno la Mungu hautakuwa kwa sababu ya kutojali nafasi na majaliwa waliyopewa na Mungu. KN 133.2

Upendo ambao hauna msingi bora ila kundhisha tu tamaa za mwili utaKuwa mgumu usiosikia shauri la mtu, kipofu, na usiozuilika. Heshima, kweli, na kila uwezo bora wenye kuinua hali ya moyo huwekwa chini ya utumwa wa tamaa mbaya. Mtu ambaye amefungwa katika minyororo ya namna hii huku akipotewa na akili mara nyingi ni kiziwi asiyesikisa sauti ya akili na dhamiri ya moyoni; majadiliano wala maombi hayawezi kumwongoza kuona ujinga wake. KN 133.3

Upendo wa kweli siyo tamaa mbaya yenye nguvu, kali, ya harahara. Kinyume chake, ni mtulivu na utokao moyoni kwa ndani. Unatazama siyo mambo ya juu juu tu, nao huvutwa tu na tabia. Ni wa akili na busara, na ni upendo wa kweli, wenye kudumu. KN 133.4

Ukiinuliwa au kukuzwa vema na kuachana na mambo ya ashiki na tamaa za mwili, upendo huwa mtakatifu, nao hudhihirishwa katika maneno na matendo. Mkristo hana budi kuwa na wema na upendo mtakatifu tu usio na pupa au masumbufu; ufidhuli, na tabia za kijinga zimepasa kulainishwa na neema ya Kristo. 

Sala na Kusoma Biblia ni Muhimu Ili Kufanya Uamuzi Ulio Bora

Kwamba imeanzishwa na Mungu, ndoa ni jambo takatifu; kamwe isingeingiwa kwa moyo wa kujipendeza nafsi mwenyewe, bila kujali wengine. Wale wanaotazamia hatua hii yawapasa kufikiri ukubwa wake kwa kicho na kuomba kwa bidii na kutafuta shauri kwa Mungu ili wapate kujua kama wamefuata njia yenye kupatana na mapenzi yake Mungu. Mafundisho yaliyotolewa katika neno la Mungu juu ya jambo hili yangefikiriwa kwa uangalifu. Mbinguni huangalia kwa furaha ndoa inayofanywa kwa haja ya kweli kupatana na maagizo ambayo yametolewa katika Biblia. KN 133.6

Kama kuna jambo ambalo lapasa kufikiriwa kwa makini na akili kamili zisizoharibika kwa tamaa, hilo ni jambo la ndoa. Ikiwa Biblia yatakikana kama mshauri, ni kabla ya kufanya hatua inayowafungamanisha watu pamoja maishani. Lakim, watu wengi wanavyoona ni kwamba katika jambo hili maoni ya moyoni hayana budi kuwa kiongozi, na kwa wengi mno wepesi wa kuvutwa na tamaa hushika usukani na kuwapeleka penye unaribifu fulani. Hapa ndipo mahali vijana wanapoonyesha upungufu wa akili kuliko katika jambo lo lote lingine; hapa ndipo wanapokataa kuhojiwa. Jambo la ndoa huelekea kuwa na nguvu za kupoteza akili juu yao. Hawajiweki chini ya Mungu. Akili zao zimerungwa minyororo, nao husonga mbele kwa siri, kana kwamba mipango yao yaweza kuingiliwa na mtu mwingine. KN 134.1

Wengi wanasafiri kwenda kwenye bandari ya hatari. Wanahitaji nahodha; lakini wanadharau kupokea msaada unaotakikana sana, wakiona moyoni kuwa ni wenye akili ya kutosha kuongoza jahazi lao wenyewe, wasifahamu kuwa limekaribia kugonga mwamba usioonekana ambao waweza kuwafanya wavun- KN 134.2

jikiwe na chombo chao cha imani na furaha Wasipokuwa wanafunzi hodari wa lile Neno (Biblia), watafanya makosa makubwa ambayo yataharibu furaha yao na ile ya wengine, kwa maisha haya na kwa yale ya wakati ujao pia. KN 134.3

Kama wanaume na wanawake wana mazoea ya kumwomba Mungu mara mbili kila siku kabla ya kulifikiri jambo la ndoa, yawapasa Kumwomba Mungu mara nne kila siku wakati wanapoitazamia hatua hii. Ndoa ni jambo ambalo litakuwa na mvuto na matokeo kwenye maisha yenu, ulimwenguni humu na katika ulimwengu ujao Ndoa zilizo nyingi za siku zetu na namna zinavyofanywa inazifanya ziwe mojawapo ya dalili za siku za mwisho. Wanaume kwa wanawake ni wakaidi, wasiosikia shauri la mtu, hata Mungu hawamjali katika neno hili. Dini imewekwa kando kana kwamba haihusiani hata kidogo na neno hili la dini tena lenye maana. KN 134.4

Shauri la Wazazi Wamchao Mungu

Pakiwako na matokeo mabaya ya ndoa namna hii, kwa nini vijana wasierevuke? Kwa nini waendelee kuona kuwa hawahitaji shauri la wazee na la watu wenye akili zaidi? Kazini, wanaume na wanawake vile vile hujihadhari sana. Kabla ya kushika kazi yo yote ya maana, wanajitayarisha kwa kazi yao. Wakati, fedha, na kujifunza sana kwa uangalifu hutumiwa kwa jambo hili, wasije wakashindwa kufaulu katika jambo wanalojaribu kufanya. KN 134.5

Basi, ni uangalifu mkubwa namna gani ungepasa kutumiwa katika kuingia ndoa-wajibu ambao unayo matokeo katika vizazi vya baadaye na kwenye maisha ya wakati ujao? Badala ya kufanya hivi, inaingiliwa kwa ubishi, bila kicho, kwa tamaa mbaya, upofu, bila kufikiri kwanza. Maelezo tu ya jambo hili ni ya kwamba Shetani hupenda kuona hali mbaya na uharibifu ulimwenguni, naye husokota wavu huu kuzitega roho za watu. Hufurahia kuwapata watu hawa walio wapumbavu kupotewa na furaha yao ya ulimwenguni humu na makao yao katika ulimwengu ujao. KN 134.6

Je, watoto wafuate mapenzi na tamaa yao wenyewe bila kujali shauri na maamuzi ya wazazi wao? Wengine kamwe hawaelekei kufikiri hata kidogo vile wazazi wao watakavyo, wala kujali maamuzi yao yaliyo ya utu mzima. Kushika lao bila kujali wengine kumeufungia mlango upendo wa baba na mama usiingie mioyoni mwao. Mioyo ya vijana yahitaji kuamshwa katika jambo hili. Amri ya tano ndiyo amri tu ambavo imeungana na ahadi, lakini inadharauliwa hata hajaliwi kabisa na dai la mchumba. Kuudharau upendo wa mama, kutoheshimu malezi ya baba ni dhambi zinazokaa hali ya kuandikwa kitabuni juu ya vijana wengi. KN 135.1

Mojawapo ya makosa makubwa kwa jambo hili ni ya kuwa vijana na wale wasio na maarifa hawataki mapenzi yao kupingwa, ya kuwa pasiwepo na cho chote kinachoyaingilia mambo ya upendo wao. Kama kuna jambo moja lenye kuhitaji kutazamwa pande zote, hili ndilo jambo hilo. Msaada wa maarifa waliyo nayo watu wengine, na kulifikiri kwa makini jambo hili pande zake zote ni muhimu kabisa. Ni jambo linalodharauliwa mno na watu wengi. Kubalini shauri la Mungu na la wazazi wenu wenye kumcna Mungu, vijana rafiki zangu. Mwombeni Mungu juu ya neno hili. KN 135.2

Pengine utauliza, “Wazazi wangechagua mchumba bila kujali moyo au maoni ya mwana au binti yao?” Nakuuliza swali kama ipasavyo: je, mwana au binti angepaswa kujichagulia mchumba bila kushauriana na wazazi, hali hatua ya namna hii haina budi kuwa na matokeo ya baadaye kuihusu furaha ya wazazi wakiwa wanapenda watoto wao? Tena ingempasa yule mtoto, bila kuiali shauri na maonyo ya wazazi wake, kuendelea bila kubadilika? Najibu kwa dhati ya moyo: La; sivyo kama haoi, Amri ya tano yakataza mwenendo wa namna hiyo. “Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.” Hii ni amri yenye ahadi ambayo Mungu hakika ataitimiza kwa wale wanaotii. Wazazi wenye busara kamwe hawatawachagulia watoto wao wachumba bila kuyajali mapenzi yao. KN 135.3

Baba na mama wangeona kuwa ni wajibu kuongoza upendo wa vijana, kusudi wapate kuwekwa kwa wale watakaokuwa wenzi wanaofaa. Wangeona kuwa ni wajibu unaowapasa, kwa mafundisho na kielelezo cha maisha yao wenyewe, kwa msaada wa neema ya Mungu, kukuza tabia ya watoto tokea utotoni mwao ipate kuwa safi na bora na wavutwe kwa wema na uadilifu. Wanaofanana huvutana; wanaofanana huthaminiana. Hebu upendo kwa neno la kweli na usafi na wema utiwe moyoni, na vijana watatafuta urafiki wa wale wenye tabia hizi.

Maonyo kwa Wale Wenye Kutazamia Ndoa

Vijana wanatumaini sana tamaa ya ghafula. Haiwapasi kujitoa kwa urahisi, wala kutekwa upesi mno na sura ya mchumba. Kadiri uchumba unavyoendeshwa katika zama hizi ni mpango wa udanganyifu na unafiki, ambao kwao adui wa roho za watu anahusiana sana nao kuliko Mungu. Busara njema yatakikana hapa, ikiwa ni hivyo; lakini ukweli ni kwamba, haitumiwi katika jambo hili ila kidogo. Wazo la upuzi, wepesi wa kuvutwa na tamaa, havina budi kuepukwa kwa hadhari kama ukoma. Vijana wengi sana wa kiume na wakike siku hizi ulimwenguni hawana adili; kwa hiyo onyo kubwa linatakikana. Wale ambao pamehifadhi tabia njema, ijapokuwa huenda wasiwe na tabia zingine nzuri zenye kutakikana, waweza kuwa wenye kustahili sifa. KN 136.1

Kuna hali hii duni ya kuvutwa kwa wepesi na tamaa iliyochangamana na mambo ya dini ya vijana wa zama hizi ulimwenguni. Dada yangu, Mungu anakutaka uongoke. Adilisha upendo wako, nakusini. Toa wakfu nguvu zako za akili na za mwili pia kwa kazi ya Mkombozi wako, aliyekununua. Yatakase mawazo na maom yako ya moyoni kusudi matendo yako yote yapate kutendwa kwa Mungu. Malaika wa Shetani wanakesha pamoja na wale wenye kutumia sehemu kubwa ya saa zao usiku katika kuposa. Kama wangefumbuliwa macho yao, wangemwona malaika akiyaandika maneno na matendo yao. Kanum za afya na adabu nzuri zinavunjwa. Ingefaa zaidi kuziacha saa zingine za uchumba kabla ya ndoa kuingia katika maisha ya ndoa. Lakini limekuwa kama jambo la kawaida ndoa kuwa mwisho wa upendo wote ulioonyeshwa katika siku za uchumba. KN 136.2

Shetani anajua mambo hasa apaswayo kushughulika nayo, naye hutumia werevu wake wa kishetani katika hila za namna mbalimbali kuzinasa roho za watu wapate kuangamia. Huangalia kila hatua inayofanywa, na kutoa mashauri mengi na mara nyingi mashauri nayo yanafuatwa badala ya shauri jema la Neno la Mungu. Wavu huu uliosokotwa vizuri, ambao ni hatari umetayarishwa kwa akili kuwatega vijana na wale wasiojihadhari. Mara nyingi huenda ukafichwa gizani; lakini wale wanaonaswa nao hujichoma wenyewe kwa huzum nyingi Kama matokeo yake, twaona mavunjiko ya utu kila mahali. KN 136.3

Mwenendo Usiofaa

Kuchezacheza na mioyo ni uhalifu mkubwa machoni pa Mungu Mtakatifu. Lakini, wengine watawapendelea wasichana kutaka wapendane, kisha waende zao na kusahau kabisa maneno yote ambayo wamesema na matokeo yake ya baadaye. Uso mpya huwavuta, nao huyarudia maneno yale yale, wakimtolea mwingine mivuto ile ile. Tabia hii itadhihirika katika maisha ya unyumba. Ndoa siku zote haiuimarishi moyo wa kigeugeu, usiosimama imara, na kuwa na kanuni hasa. Huchoka na uamimfu, na mawazo mabaya yatadhihirika kwa matendo mabaya. Ni jambo muhimu kama nini, basi, kwamba vijana wayaweke tayari kabisa mawazo yao na kuulinda mwenendo wao hata Shetani asiweze kuwavuta kwa werevu kuiacha njia nyofu. KN 136.4

Mvulana apendaye maongezi na kujipatia urafiki wa msichana bila ya kujulikana na wazazi wa msichana hafanyi wajibu wa Mkristo bora kwa msichana huyo wala kwa wazazi wa huyu msichana. Kwa njia ya kupelekeana habari na kukutana kisirisiri aweza kujipatia mvuto wenye kuizidi akili ya huyo msichana, lakini kwa kufanya hivyo hadhihirishi ubora wala uadilifu wa roho ambayo kila mtoto wa Mungu atakuwa nao. Kusudi kupata mradi wao, wanafanya mambo yasiyo ya kweli wala yasiyo dhahiri, na ambayo hayapatani na Biblia, na kujidhihirisha kuwa waongo kwa wale wawapendao na kujaribu kuwa walezi waaminifu juu yao. Ndoa zinazoandikwa chini ya mivuto ya namna hii hazipatani na neno la Mungu. Mtu atakayempotosha binti fulani auacne wajibu umpasao, ambaye atamtia mashaka mawazoni mwake juu ya amri za Mungu zilizo dhahiri na halisi kuwatii na kuwaheshimu wazazi wake, si mtu atakayekuwa mwaminifu kwa mapatano ya ndoa. KN 137.1

“Usiibe” imeandikwa kwa chanda cha Mungu juu ya mbao za mawe, lakini, mara ngapi wizi wa hila wa upendo nufanywa na kutolewa udhuru! Uchumba wa kudanganyana hushikiliwa kupelekeana habari kisirisiri huendelezwa, mpaka upendo wa mtu asiye na maarifa, na kipimo kisichoko kwa wazazi wake na kilichoondolewa kutoka kwao na kuwekwa juu yake mwenyewe ambaye huonyesha kwa mwenendo huo huo anaofuata kuwa hastahili upendo wa huyo msichana. Biblia yakataza udanganyifu wa kila namna. Wenye kudai kuwa ni Wakristo, ambao maisha yao yameainishwa kwa uadilifu, na ambao huelekea kuwa wenye akili juu ya mambo yote mengine, hufanya makosa ya kutisha hapa. Huonyesha hali, na nia thabiti kuwa mawazo hayawezi kubadilika. Huvutwa sana na maoni na tamaa mbaya hata hawatamani kuichunguza Biblia na kushirikiana na Mungu. KN 137.2

Mojawapo ya Amri za Mungu inapovunjwa, hatua za kushuka katika hali ya chini hazina budi kuwepo. Mara visetiri vya stara ya kike vinapoondolewa uzinifu hauonekani kuwa jambo ovu mno. Ole, matokeo mabaya kama nini ya mvuto wa mwanamke kwa maovu huonekana ulimwenguni siku hizi! Kwa njia ya vishawishi (utongozi) wa “malaya” maelfu wanatiwa vifungoni gerezani, wengi hujiua, na wengi huyakatiza maisha ya watu wengine. Maneno haya ya Biblia, “Miguu yake inatelemkia mauti; hatua zake zinashikamana na kuzimu,” ni ya kweli kama nini. KN 137.3

Mioto mikubwa ya kuonya hatari imewekwa pande zote za njia ya maisha ili kuwazuia watu wasipakaribie manali pa hatari ambapo panakatazwa lakini hata, hivyo, wengi huchagua njia ya mauti, kinyume cha maonyo ya fikira, kwa kuidharau sheria ya Mungu, na kutojali kisasi cha Mungu. Wale ambao huihifadhi afya ya mwili, akili timamu, na tabia njema huzikimbia “tamaa za ujanani.” Wale ambao watajibidiisha kweli kweli kupinga uovu unaokiinua kichwa kigumu cha uovu, na cha kibun miongoni mwetu huchukiwa na kusengenywa na watenda mabaya wote, Iakini watatukuzwa na kutunzwa na Mungu. 1

Sura ya 19 - Kutooana na Mtu Asiyeamini

MIONGONI mwa Wakristo kuna dharau na kutojali mafundisho ya Neno la Mungu; Hali ambayo ni ya kustaajabisha na kutia hofu juu ya ndoa ya Wakristo kuoana na makafiri. Wengi wanaojidai kumpenda na kumcha Mungu huchagua kufuata maelekeo ya mioyo yao wenyewe badala ya kukubali shauri la Mungu. Katika jambo ambalo linahusu kabisa raha na hali njema ya sehemu zote mbili kwa ulimwengu huu na kwa ule ujao, akili, busara, na kicho cha Mungu huwekwa kando; na tamaa mbaya ya kuharikisha, ukaidi huachwa kutawala. KN 139.1

Wanaume kwa wanawake ambao wangekuwa wenye akili na bidii ya kufanya vizuri mambo yote yawapasayo, huziba masikio yao wasisikie shauri jema; ni viziwi wasiosikia maombi na maonyo ya rafiki na jamaa wala ya watumishi wa Mungu. Maneno ya shauri ama onyo huhesabiwa kama ufidhuli, na rafiki anayekuwa mwaminifu hata kuthubutu kusema onyo hutendwa kama adui. Haya yote ndivyo Shetani apendavyo. Hufuma mtego wake kuizunguka roho ya mtu, naye hupotewa na akili, na kupumbazika. Akili hushindwa kujitawala na tamaa mbaya hutamalaki; ashiki hutawala, mpaka mtu akaamka akiwa amekwisha kuchelewa sana na kuwa katika maisha ya hali mbaya ya taabu na utumwa. Haya si mambo ya kuwaziwa tu, bali ni maneno ya kweli. Kibali cha Mungu hakitolewi kwa umoja ambao ameukataza wazi. KN 139.2

Bwana aliwaamuru Waisraeli zamani wasioane na watu wa mataifa yenye kuabudu miungu ya kishenzi waliokuwa wamewazunguka: “Wala usioane nao, binti yako usimpe mwanawe mume, wala usimtwalie mwanao mume binti yake.” Sababu yake imetolewa. Mungu, akiwa mwenye kuona mbele matokeo ya baadaye ya umoja wa namna hii, asema: “Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya Bwana juu yenu, naye atakuangamiza upesi.” “Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako; Bwana Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi.” KN 139.3

Katika Agano Jipya kuna maneno yanayokataza Wakristo kuoana na makafiri. Mtume Paulo, katika waraka wake wa kwanza kwa Wakorintho, asema: “Mwanamke hufungwa maadamu mumewe yu hai, lakini ikiwa mumewe amefariki, yu huru kuolewa na mtu ye yote amtakaye; katika Bwana tu. ” Tena, katika waraka wake wa pili, ameandika: “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi lsivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliali? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana si tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema Bwana, msiguse kitu kilicho kichafu, nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike asema Bwana Mwenyezi.” KN 139.4

Kamwe watu wa Mungu wasingethubutu kuingia mahali Palipokatazwa na Mungu. Ndoa baina ya waaminio na wasioamini imekatazwa na Mungu. Lakini mara nyingi moyo usioongoka hufuata tamaa zake wenyewe, na ndoa zisizokubaliwa na Mungu hufanywa. Kwa sababu hii wanaume na wanawake wengi hawana tumaini wala hawanaye Mungu ulimwenguni. Mivuto yao bora imekufa; kwa mnyororo wa hali ya mambo haya wameshikwa wavuni mwa Shetani. Wale wanaotawaliwa na ashiki na taama mbaya ya mwili watakuwa na mavuno machungu kuvuna katika maisna haya, na mwenendo wao waweza kuleta hasara ya roho zao mwishowe. KN 140.1

Wale wanaoungama kweli huyakanyaga mapenzi ya Mungu kwa kuoana na wasiaoamini; wanapoteza kibali cha Mungu na kufanya kazi ngumu kwa kutubu. Huenda mtu asiyeamini akawa mwenye tabia njema ya moyoni, lakini kwamba hajaungama majibu ya madai ya Mungu naye amekataa wokovu mkuu namna hii ni sababu ya kutosha inayoacha umoja usikamilishwe. Pengine tabia ya yule asiyeamini huenda ikafanana na ile ya yule kijana ambaye Yesu alimwambia maneno haya, “Umepungukiwa na neno moja;” hilo lilikuwa neno moja lenye kutakikana sana.

Je! Watu Wawili Waweza Kutembea Pamoja Wasipokuwa Wamepatana?

Mara zingine udhuru unatolewa kuwa huyo asiyeamini ni mtu mzuri kwa dini na kwa mambo yote yanayotakiwa kwa mchumba ila tu jambo moja si Mkristo. Ijapokuwa busara za kuchagua na mwenye kuamini zaweza kuonyesha jambo lisilofaa la umoja wa maisha na yule asiyeamini, lakini, tisa katika kila watu kumi, hushindwa na tamaa. Kupungua kwa hali ya mambo ya kiroho huanzia dakika ile ya kuahidi kwa kiapo kwenye mimbara; moyo wa bidii kwa mambo ya dini unapunguzwa, na ngome moja moja huvunjwa, mpaka wote wawili wamekuwa hali moja chini ya bendera nyeusi ya Shetani. Hata katika furaha za arusi roho ya kidunia hushinda dhamiri, imani, na kweli. Katika nyumba hiyo mpya na saa ya maombi haiheshimiwi. Bibi arusi na bwana arusi wamejichagua wenyewe na (kumfukuza kumwachilia mbali) Yesu. Kwanza yule asiyeamini pengine hataonyesha ushindani katika uhusiano huu mpya; lakini somo la Biblia linapotolewa ili kusikilizwa na kufikiriwa, uchungu utatokea mara moja: “Ulioana na mimi, ukijua kwamba nalikuwa hali hii nilivyo sasa; sitaki kusumbuliwa. Tangu sasa naijulikane kuwa mazungumzo juu ya mawazo yako mwenyewe hayana budi kupigwa marufuku.” Kama mwenye kuamini angeonyesha moyo wo wote wa bidii kwa habari za dini yake, inaweza kuwa kana kwamba hafanyi halali kwa yule asiyependezwa na maisha ya Kikristo. KN 140.3

Mwenye kuamini hufikiri kuwa katika uhusiano wake mpya hana budi kuacha mengine kwa mwenziwe aliyemchagua. Furaha, anasa za kidunia hupendelewa. Kwanza huwapo moyo usiotaka kufanya hivi, lakini upendo wa Neno la Mungu huzidi kupungua, na mashaka huwapo badala ya imani. Hakuna mtu ambaye angeshuku kuwa yule ambaye zamani alikuwa mwenye kuamini, imara na mwaminifu, na mfuasi mwaminifu wa Kristo angeweza kuwa mtu mwenye mashaka, na kusitasita alivyo sasa. Ah, mabadiliko yameletwa na ile ndoa isiyo ya busara! KN 141.1

Ni jambo la hatari kufanya ndoa ya kidunia. Shetani ajua sana kuwa saa ya ndoa ya vijana wa kiume na wa kike hufunga historia ya maisha yao ya dini na ya manufaa. Hawamo kwa Kristo. Pengine kwa muda mfupi watafanya jitihadi kuishi maisha ya Kikristo; lakini jitihadi zao zote zinakutana na mvuto wa nguvu unaozipinga. Zamani walijaliwa na kupendezwa kuzungumza juu ya imani na tumaini lao; lakini hawapendi kutaja somo hilo, wakijua kuwa mtu waliyeungana naye siku zote za maisha yao hapendezwi nalo. Kama matokeo yake, imani katika Neno la kweli la thamani kuu hufifia moyoni, na Shetani hufuma kwa werevu ili kuwazinga pande zote, utando wa mashaka. KN 141.2

“Je, watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wanapatana?” “Wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.” Lakini jambo hili huonekana kuwa la ajabu kama nini! Huku mmoja wa wale walioungana kabisa (katika ndoa) akishughulika na ibada, mwingine hajali; wakati mmoja wao anapoitafuta njia iendayo uzimam, mwingine yumo katika njia pana iendayo mautini. KN 141.3

Mamia wamemwacha Kristo na raha ya mbinguni kama matokeo ya kuoana na watu wasioamini. Yawezekana kwamba upendo na umoja na Kristo si mambo yenye thamani kwao tena ila kidogo tu hata wanapendelea zaidi urafiki wa maskini wenye kufa? Je, Mbinguni hapatnaminiwi ila kidogo tu hata wanapenda kuzihatarisha raha zake kwa ajili ya mtu asiyempenda Mwokozi wa ajabu?

Jibu la Mkristo kwa Mtu Asiyeamini

Kila Mkristo apaswa kufanya nini akiingizwa mahali pa kujaribiwa nguvu ya imani yake? Kwa uthabiti wenye kustahili kuigizwa yampasa aseme dhahiri: “Mimi ni Mkristo mwaminifu. Naamini kuwa siku ya saba ya juma ni Sabato ya Biblia. Imani na kanuni zetu zimeachana, ni tofauti hata hazipatani. Hatuwezi kufurahi pamoja, maana kama nikiendelea kujipatia ujuzi kamili zaidi wa mapenzi ya Mungu, nitazidi kuhitilafiana na walimwengu na kufanywa nifanane zaidi na Kristo. Kama ukiendelea kutoona uzuri ndani ya Kristo, wala mivuto katika Neno la kweli, utapenda ulimwengu, ambao mimi siwezi kuupenda, nikiwa nayapenda mambo ya Mungu, usiyoweza kuyapenda. Mambo ya kirono hufahamika kiroho. Pasipo ufahamu wa Kiroho hutaweza kuyaona madai ya Mungu kwangu, ama kujua wajibu unaonipasa kwa Bwana ninayemtumikia; kwa hiyo, utaona kwamba sikujali kwa ajili ya wajiou wa dini. Hutafurahi; utakuwa na wivu kwa sababu ya upendo ambao ninamtolea Mungu, nami nitakuwa hali ya upweke katika imani yangu ya dini. Maoni yako yatakapogeuka, moyo wako utakapoitikia madai ya Mungu, nawe utakapojifunza kumpenda Mwokozi wangu, ndipo uchumba wetu utakapoweza kufanywa upya.” KN 142.1

Hivi ndivyo mwenye kuamini anavyojinyima kwa ajili ya Kristo na kujitoa dhabihu ambayo huipendeza dhamiri ya moyoni mwake, na yenye kuonyesha kwamba nuuthamini uzima wa milele hata kukaa bila kuolewa kuliko kuungamanisha moyo wake wa kuupenda uzima na mtu mwenye kupendeleza anasa za dunia badala ya kumpenda Yesu, na ambaye angependa kumpotosha auache msalaba wa Kristo. 

Heri Kuvunja Uchumba Usio wa Busara

Kwa Kristo peke yake ndipo ushirika wa ndoa unamoweza kufungwa kwa usalama. Upendo wa mwanadamu ungefungamanishwa na upendo utokao mbinguni. Mahali Kristo anapotawala ndipo tu panapoweza kuonekana upendo wa kweli, usio wa hila wala kujipenda nafsi. KN 142.3

Hata kama uchumba umefanywa na mtu ambaye huelewi vyema tabia yake, usidhani kuwa kushika uchumba kutakulazimisha kutwaa kiapo cha ndoa, na kukuunganisha na mtu ambaye humpendi tena ambaye hutamheshimu maishani mwako, jihadhari sana unapofanya uchumba wenye masharti; lakini hata ikiwa ni uchumba wenye masharti, ni bora zaidi kuvunjilia mbali uchumba kama huo kabla ya kufunga ndoa kuliko kuja kuvunja ndoa baadaye, kama wengi wafanywavyo. Pengine utasema, “Lakini nimetoa ahadi yangu, je, niitangue? Mimi najibu, kama umekwisha kutoa ahadi kinyume cha Maandiko Matakatifu, kwa hali iwayo yote, itangue, bila kuchelewa, na kwa unyenyekevu mbele za Mungu tubu juu ya kupumbazika kwako ambako kulikufanya uharakishe kutoa ahadi kwa kiapo. Afadhali zaidi kuitangua ahadi ya namna hiyo, kwa kicho cha Mungu, kuliko kuitimiza, na kumdharau Mwumbaji wako. Kila hatua ihusuyo ndoa na iwe yenye adabu, unyofu, uaminifu, na kusudi jema la kumpendeza na kumheshimu Mungu. Ndoa huwa na matokeo ya baadaye katika ulimwengu huu na kwenye ulimwengu ujao pia. Mkristo mwaminifu hatafanya mipango ambayo haitampendeza Mungu. KN 142.4

Moyo unaoonea shauku upendo wa kibinadamu, lakini upendo huu sio wenye nguvu ya kutosha, au usafi wa kutosha, au tnamani ya kutosha kuwa badala ya upendo wa Yesu. Katika Mwokozi wake tu ndipo mahali mke awezapo kupata hekima, nguvu, na neema kuyakabili masumbufu, kazi, na taabu za maisha. Apaswa amfanye (Mwokozi) kuwa nguvu zake na kiongozi wake. Hebu mwanamke ajitoe kwa Kristo kabla ya kujitoa kwa rafiki awaye yote wa duniani, wala asiingie kwenye hali itakayokuwa kinyume cha hayo. Wale watakaoweza kupata furaha ya kweli hawana budi kuwa na mbaraka wa Mungu juu ya vyote walivyo navyo na juu ya mambo yote watendayo. Kutomtii Mungu ndiyo asili ya hali mbaya iliyo kwa wingi mioyoni na nyumbani mwa watu wengi. Dada yangu, kama usipoweza kupata nyumba isiyokuwa na hitilafu hata kidogo, usiungane na mtu aliye adui wa Mungu. KN 143.1

hauri Jema kwa Mtu Ambaye Huongoka Baada ya Ndoa

Mtu ambaye amefunga ndoa akiwa bado hajaongoka, kwa kuongoka kwake anajiweka chini ya wajibu mzito zaidi kuwa mwaminifu kwa mwenziwe, si neno nata kama dini zao zinahitilafiana namna gani lakini, madai ya Mungu yapasa kuwekwa juu zaidi ya uhusiano wao wo wote wa kidunia, ijapokuwa matokeo ya baadaye yawe taabu ama mateso. Kwa moyo wa upendo na upole, uaminifu huu waweza kuwa na mvuto wa kumwongoa yule asiyeamini. 1 KN 143.2

Sura ya 20 - Ndoa

MUNGU alimfanya mke kutoka kwa mume, awe mwenziwe na msaidizi wake akae pamoja naye, kumfurahisha, kumtia, moyo, na kumpendeza, naye mume amepaswa kuwa mzaidizi wake imara. Wote wanaoingia katika umoja wa ndoa wakiwa na kusudi takatifumume kuyapata mapenzi safi ya moyo wa mke, na mke kulainisha na kuikuza vizuri tabia ya mumewe na kuikamilisha hulitimiza kusudi la Mungu kwao. KN 144.1

Kristo hakuja kutangua kawaida hii, bali kuirudishia hali ya utakatifu na ubora lliyokuwa nayo mwanzoni. Alikuja kumrudishia mwanadamu tabia ya uadilifu ya kufanana na ile ya Mungu, naye alianza kazi yake kwa kuihalalisha ndoa. KN 144.2

Yeye ambaye alimpa Adamu mke, yaani, Hawa awe msaidizi wake alifanya mwujiza wake wa kwanza katika karamu ya arusi. Katika jumba la karamu mahali ambapo jamaa walifurahi pamoja, hapo naipo Kristo alipoanza kazi yake kwa watu. Hivyo alitoa idhini yake kwa ndoa, akionyesha kuwa ni desturi ambayo yeye mwenyewe alianzisha. Aliamuru ili wanaume na wanawake waungane katika ndoa takatifu, na kuwalea watoto ambao, wakiheshimiwa, wangejulikana kama watu wa jamaa ya nyumba ya Mbinguni. KN 144.3

Arusi Isiwe na Mambo Mengi, Bali iwe Wakati wa Furaha

Upendo mtakatifu utokao kwa Kristo kamwe hauharibu upendo wa kibinadamu, bali unakuwa nao ndani yake. Kwa njia ya upendo huo mtakatifu, upendo wa kibinadamu hutakaswa na kusafishwa, kukuzwa vizuri na kuadilishwa. Kamwe upendo wa kibinadamu hauwezi kuzaa matunda yake mazuri mpaka kwanza uwe umeunganishwa na tabia takatifu na kufundishwa kukua kuelekea juu mbinguni. Yesu ataka kuona ndoa za furaha, na nyumba zenye furaha. KN 144.4

Maandiko Matakatifu yasema kuwa Yesu na wanafunzi wake walialikwa katika karamu hii ya arusi (Kana). Kristo hakuwaruhusu Wakristo kusema wakati wanapoalikwa arusini, . Haitupasi kuwepo mahali penye sherehe ya namna hiyo. Kwa kuihudhuria yeye mwenyewe karamu hii Kristo aliifundisha kuwa angependa tufurahi pamoja na wale wanaofurahi tukiyashika maagizo yake. Kamwe hapingi sherehe za wanadamu ambazo hazifanywi kinyume cha shena ya Mungu. Mkutano ule ambao Kristo aliutukuza kwa kuwako yeye mwenyewe, ni halali kwamba wafuasi wake wamepaswa kuuhudhuria. Baada ya kufika kwenye karamu hii, Kristo alihudhuria zingine nyingine nyingi, akizihalalisha kwa kuwako yeye mwenyewe na kwa mafundisho pia. KN 144.5

Hatuna sababu ya kufanya maandamano makubwa ama sherehe kubwa sana, hata kama jamii ya watu karamuni wakiwa hali moja kabisa. KN 145.1

Kila mara huwa jambo lisilonipendeza kuona pakiwako na vicheko na shangwe za vigelegele ama mambo ya jinsi hiyo. La, hili ni agizo la Mungu, lipasalo kuheshimiwa kabisa kwa moyo wa kicho. Kadiri unyumba unavyofanywa hapa chini, hauna budi kuonyesha namna watu wa nyumba hiyo watakavyokuwa watu wa nyumba ya mbinguni juu. Daima utukufu wa Mungu hauna budi kufanywa kuwa jambo la Kwanza. 1 

Shauri Jema kwa Bwana Arusi na Bibi Arusi

Wapenzi Ndugu na Dada: Mmeungana katika agano la daima maisha yenu yote. Mafundisho yenu katika maisha ya unyumba yameanza. Mwaka wa kwanza wa maisha ya unyumba ni mwaka wenye mambo ya kupatwa nayo maishani, mwaka ambao mume na mke hujifunza tabia mbalimbali walizo nazo, kwa wao, kama vile mtoto anavyojifunza masomo shuleni. Katika mwaka huu wa kwanza wa maisha ya unyumba pasiwepo mambo yatakayoharibu furaha yenu ya wakati ujao. KN 145.3

Kupata ufahamu bora wa unyumba ni kazi ya daima maishani. Wale wanaooana huingia shule ambayo kamwe katika maisha haya hawaihitimu ama kuimaliza. Ndugu, wakati wa mkeo na nguvu na raha sasa vimeungamanishwa pamoja na yako. Mvuto wako kwake waweza kuwa harufu ya uzima iletayo uzima au harufu ya mauti. Angalia sana usije ukayaharibu maisha yake. KN 145.4

Dada yakupasa sana kujifunza mafundisho yako mazuri ya kwanza kwa habari za kazi na wajibu wa maisha ya unyumba. Hakikisha kuwa unajifunza mafundisho hayo kwa uaminifu siku kwa siku. Usikubali kushindwa na moyo wa kutokuridhika au kukata tamaa upesi. Usitamani maisha ya anasa na kujikalia kivivu. Daima jihadhari usishindwe na choyo ama moyo wa kujipendeza nafsi mwenyewe bila kujali wengine. KN 145.5

Katika umoja wenu wa maisha upendano wenu hauna budi kuwa sifa yenu kila mmoja, mkifurahisnana ninyi. Kila mmoja wenu hana budi kutumikia furaha ya mwenziwe. Haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwenu. Lakini huku mkipaswa kupatana na kuwa kitu kimoja, hali halisi ye yote kati yenu kupotewa na hadhi yake kwa ajili ya mwenziwe. Nafsi yako ni mali ya Mungu. Kila mmoja na amwulize Mungu hivi, Ni jambo gani linalofaa? Ni jambo gani lisilofaa? Nawezaje kulitimiza vizuri kusudi la maisha? “Ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinuliliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.” (Kwa kuwa ni hivyo, mtukuzeni Mungu kwa mwili wenu, na kwa roho yenu, ambayo ni mali ya Mungu.”-(Kiunguja) Upendo wenu kwa kile ambacho ni cha kibinadamu hauna budi kuwa pungufu kuliko upendo wenu kwa Mungu. Wingi wa upendo wenu hauna budi kufurika kwake yeye aliyeutoa uhai wake kwa ajili yenu. Kuishi kwa ajili ya Mungu, mtu hana budi kumpenda kabisa. Je, upendo wenu kwake aliyewafilia unafurika? Kama unafurika, upenao wenu ninyi kwa ninyi utatimiza agizo la Mungu. KN 145.6

Upendo waweza kuwa safi na mzuri, lakini unaweza kuwa wa juu juu tu kwa sababu haukujaribiwa. Mfanyeni Kristo kuwa wa kwanza na wa mwisho na bora zaidi ya mambo mengine yote. Daima mtazameni, ndipo upendo wenu kwake utakavyozidi na kuwa wenye nguvu kila siku kadiri unavyotolewa upate kujaribiwa. Na kadiri upendo wenu mlio nao kwake unavyozidi kuwa mwingi, upendano wenu utaongezeka na kuwa na nguvu. “Sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tufanane na mfano uo huo toka utukufu hata utukufu.”(2 Wakorintho 3:18). Sasa mnazo kazi za kufanya ambazo kabla ya kuoana hamkuwa nazo. “Basi....jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu.” “Mkienenda katika upendo, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi.” Soma kwa uangalifu maneno yafuatayo: “Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa Vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo. Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanis, akajitoa kwa ajili yake.” (Wakolosai 3:12; Waefeso 5:2, 22-25). KN 146.1

Ndoa, yaani umoja wa maisha, ni mfano wa ushirika ulio baina ya Kristo na kanisa lake. Moyo ambao Kristo alionyesha kwa kanisa ndio moyo ambao mume na mke wanapaswa kuwa nao wao kwa wao. Mume wala mke asijaribu kumtawala mwenzake kwa nguvu bila haki. Bwana ameweka kanuni ambayo imepasa kuwa kiongozi cha jambo hili. Mume apaswa kumpenda mkewe kama Kristo alipendavyo kanisa. Mke naye apaswa kumheshimu mumewe. Wote wawili wanapaswa kukuza vizuri moyo wa rehema, wakikusudia kutohuzunishana au mmoja kumdhuru mwingine. KN 146.2

Ndugu na dada, ninyi nyote walili mnao uwezo wa nia thabiti. Mwaweza kuufanya uwezo huu kuwa mbaraka mkubwa au laana kubwa kwenu wenyewe ama kwa wale wanaokutana nanyi. Usijaribu kumlazimisha mwenzako kuyakubali mapenzi yako. Hamwezi kufanya hivi na huku mkadumu kupendana. Kuonyesha ukaidi huharibu amani na furaha ya nyumbani. Msikubali unyumba wenu kuwa wenye ugomvi. Kama mkifanya hivyo mtakosa furaha wote. Semeni kwa upole na kutenda kwa upole, mkitangulizana. Jihadharini sana na maneno yenu, maana yana mvuto wenye nguvu kwa mema ama kwa mabaya. Msikubali ukali kuwapo katika sauti zenu. Ingizeni maishani mwenu umoja wenye harufu nzuri ya tabia ya Kristo. Kabla mwanamume hajaingia umoja mkubwa kama llivyo ndoa, yampasa ajifunze jinsi ya kujitawala na jinsi ya kuwatendea wengine. KN 146.3

Ndugu, uwe mfadhili; mwenye saburi na mvumilivu. Kumbuka kuwa mkeo alikukubali uwe mumewe, si kusudi upate kumtawala, la, bali ili uwe msaidizi wake. Usiwe mkali, mdhaiimu au mwenye kutoa amri na kushurutisha watu wa nyumbani kuzitii. Usitumie nguvu kumshurutisha mkeo kufanya upendavyo. Kumbuka kuwa anayo nia ya moyoni na ya kwamba yeye pia huweza kutaka kufanya mapenzi yake kama wewe. Pia kumbuka kuwa unayo bahati ya ujuzi mkubwa ulio nao. Kuwa mwenye huruma na mwenye staha. “Hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina unaflki.” (Yakobo 3:17). KN 147.1

Kumbukeni, ndugu na dada zangu, ya kuwa Mungu ni Upendo na kwamba kwa neema yake mwaweza kufaulu kupendezana ninyi kwa ninyi, kama mlivyoahidi kufanya katika mapatano na ahadi ya ndoa yenu. Kwa nguvu za Mkombozi mwaongeza kutumia busara na uwezo mlio nao kuyasaidia maisha ya watu yaliyopotoka yapate kunyoka na kumwelekea Mungu. Kuna jambo gani Kristo asiloweza kufanya? Yu mkamilifu katika hekima yake, katika haki, na katika upendo. Msijitenge, ridhikeni kuonyesha upendo wenu kila mmoja kwa mwenzake. Shikeni kila nafasi kuwafurahisha majirani, mkishiriki pamoja nao upendano wenu. Maneno ya upole, nyuso za huruma, shukrani za moyoni, vingeweza kuwag awia wengi wasumbukao, walio katika nali ya upweke, kama ikombe cha maji baridi kwa mtu mwenye kiu. Neno la kutia moyo, tendo la fadhili, lingeweza hata kupunguza uzito wa mizigo inay-owalemea watu waliokwisha kucholca. Huduma ya ukarimu ndiyo yenye kuleta furaha ya kweli. Na kila neno na kila tendo la huduma ya namna hii huandikwa vitabuni mbinguni kama limetendewa Kristo. Anasema, “Kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.” (Mathayo 25:40). KN 147.2

Kaeni kwenye pendo zuri la Mwokozi. Ndipo mvuto wenu utawanufaisha walimwengu. Roho ya Kristo na iwatawale. Sheria ya wema na iwe midomoni mwenu daima. Uvumilivu na ukarimu nauyaainishe maneno na matendo ya wale waliozaliwa mara ya pili, wapate kuishi maisha mapya ndani ya Kristo. 2

Sura ya 21 - Masikilizano na Maisha ya Heri

MUNGU ameamuru kwamba yapasa pawepo upendo kamili na masikilizano kati ya wale wanaofunga ndoa na kuoana. Bibi arusi na bwana arusi, mbele za wote mbinguni na duniani, wamepaswa kuahidi kupendana kama Mungu alivyowaamuru. Ni wajibu wa mke kumstahi na kumheshimu mumewe, na ni juu ya mume kumpenda na kumfurahia mkewe. KN 148.1

Wanaume na wanawake, mwanzoni mwa maisha yao ya unyumba, wangejitoa wakfu kwa Mungu. KN 148.2

Ingawa ndoa imepangwa kwa uangalifu na busara namna gani, ni watu wachache sana ambao huwa wameungana kabisa moyoni wakati ibada ya ndoa inapofanywa. Umoja wa kweli wa wale wawili wenye kuoana ni kazi ya miaka ifuatayo. KN 148.3

Mashaka na masumbufu ya maisha yanapoanza kuwapata wale waliooana karibuni, ile hali ya mahali iliyodhaniwa juu ya ndoa huanza kupungua. Mume na mke huanza kujifunza tabia zao wao kwa wao jinsi ambavyo hawakuweza kujuana zamani. Huu ndio wakati wa hatari sana katika maisha yao. Raha na utumizi wa maisha yao yote yafuatayo hutegemea kama wanavyoendeleza mwenendo wao mwema wakati huu. Mara nyingi watagundua katika tabia zao wao kwa wao manyonge na makosa fulani ambayo hawakuyashuku zamani; lakini pia mioyo ambayo imeungwa na upendo itagundua sifa zilizo bora zisizojulikana zamani. Basi, wote na watafute mema kuliko kutafuta mawaa. Mara nyingi ni mafikira yetu wenyewe, hali ya roho zetu sisi wenyewe, ambazo zinayakinisha mambo tutakayoyagundua kwa mwingine. KN 148.4

Kuna wengi ambao kufikiri ya kwamba kudhihirisha upendo ni kama kujipotezea hadhi, nao hukaa katika hali ya unyamavu unaowazuia wengine. Moyo wa namna hii huzuia mtu asidhihirishe huruma yake. Nguvu za wema na upaji zikizuiwa, hufifia, na moyo hubaki hali ya upweke na kupooza. Inatupasa kujihadhari na kosa hili. Upendo hauwezi kuaumu sana kama usipodhihirishwa. Usiache nata mmojawapo wa nyumba yako afadhaike moyoni kwa kutamani upendo na huruma yako, asipate. KN 148.5

Kila mmoja na aonyeshe upendo kuliko kuulazimisha. Kuzeni mambo yaliyo bora katika maisha yenu, na kuwa wepesi kwa kutambua sifa njema ninyi kwa ninyi. Kujua kwamba umethaminiwa na mwenzako ni jambo litialo nguvu na kuridhisha moyo Huruma na staha humtia kila mmoja nguvu apata kuwa bora zaidi, na upendo wao kwa wao huzidishwa kwa vile unavyowatamanisha wazidi kuwa watu wenye makusudi mema.

Kuyaunganisha Maisha ya Wawili Yawe Kitu Kimoja

Ingawa shida, matatizo na vipingamizi vije, mume wala mke asiweke fikara moyoni ya kwamba ushirika wao wa ndoa ni kosa au ya kwamba inashusha moyo kwa kuwa hali yake si kama ilivyotazamiwa. Nuieni kwamba mtashirikiana na kusaidiana katika mambo yote kadiri mwezavyo. Daima mkifanyiana mambo yapendezayo kama mwanzoni. Kwa kila njia mtiane nguvu kwa kupambana na mambo magumu ya maisha. Jitahidini kukuza furaha yenu, ninyi kwa ninyi, Upendano halisi na uwepo mkichukuliana katika upendo. Ndipo ndoa, badala ya kuwa mwisho wa upendo, itakuwa kama mwanzo wa upendo. Urafiki wa kweli, na kupendana, ni kama kuonja mbele raha za mbinguni. KN 149.1

Wote yawapasa kuongeza uvumilivu kwa kutumia uvumilivu. Kwa kule kuwa wapole na wavumilivu, upendo wa kweli waweza kudumishwa kuwa moto, usipoe moyoni, na tabia zitakazokuzwa zitakuwa za kumpendeza Mungu. KN 149.2

Shetani siku zote yu tayari kujinufaisha wakati ugomvi au neno lo lote baya linapotokea, na kwa kuchochea tabia mbaya kwa mume au mke, atajaribu kuleta mafarakano baina ya wale ambao walikwisha kuunganisha mioyo yao kwa agano takatifu la ndoa mbele za Mungu. Katika ahadi za ndoa wameahidi kuwa kitu kimoja, mke akaahidi kwa kicho kumpenda na kumtii mumewe, mume akaahidi kumpenda na kumfurahisha mkewe. Kama sheria ya Mungu ikishikwa roho mbaya ya ugomvi haitakuwako kwa watu wa nyumbani, na hapatakuwako na utengano, wala mafarakano hayataruhusiwa. KN 149.3

Huu ni wakati wa maana sana katika maisha ya wale ambao wamesimama mbele yenu kuunganisha mioyo na mapenzi yao, utu wao wema, upendo wao, na kazi yao, katika kazi ya kuziongoa roho za watu. Katika agano la ndoa pana hatua iliyo ya maana sana ambayo hutwaliwa-kuyachanganya ama kuyaunganisha maisha ya wawili yawe kitu kimoja. Mungu apenda kwamba mume na mke waungamanishwe pamoja kazini mwake, kuiendesha kwa utimilifu na utakatifu. Hao waweza kulifanya hili. KN 149.4

Mbaraka wa Mungu nyumbani mtakamokuwa na umoja huu ni kama mwangaza wa jua la mbinguni, kwa sababu Bwana anenda kuwa mume na mke waungane pamoja katika vifungo vitakatiru vya umoja, kwa Yesu Kristo, wakiwa naye kuwatawala, na roho yake kuwongoza. KN 149.5

Mungu ataka nyumbani pawe mahali pa furaha kabisa duniani, mfano wa makao ya mbinguni. Kuchukua madaraka haya ya ndoa nyumbani, kuiunganisha mioyo yao na Yesu Kristo, wakiutegemea mkono wake na ahadi yake, mume na mke wanaweza kushiriki umoja huo, furaha ambayo malaika wa Mungu huisifu. 1

Pakitokea Hitilafu

Ni jambo gumu kusawazisha matata ya watu wa nyumbani, hata kama mume na mke wanatafuta kufanya mapatano ya haki juu ya wajibu mbalimbali uwapasao, ikiwa hawakumpa Mungu moyo. Mume na mke wanawezaje kuwa na nyoyo moalimbau juu ya maisha yao nyumbani kisha wapendane, na kuwa na umoja imara? Yawapasa kuwa na moyo mmoja kwa mambo yote yahusuyo unyumba wao, na mke, kama ni Mkristo, atakuwa na moyo wa kumpenda mumewe na kumhesabu kama mwenzake kabisa: maana mume apaswa kuwa kichwa cha nyumba. KN 150.1

Roho yako ni mbaya. Unapoyatwaa madaraka, hupimi mambo vizuri na kufikiri kwanza matokeo ya baadaye yatakayoletwa na kule kuyashikilia maoni yako mwenyewe, huku ukijitegemea unazua tu maneno katika sala zako na maongezi, hali ukijua kuwa mkeo hana maoni hayo uliyo nayo wewe. Badala ya kuyaheshimu maoni ya mkeo na kuepuka kwa moyo mwema, kama mwungwana, mambo hayo ambayo wayajua kwamba mnahitilafiana, umetangulia kuyatafakari mabaya, na kuonyesha ukaidi ikisema maoni yako bila kumjali ye yote aliye nawe. Umeona kwamba wengine hawana haki kuyaona mambo haya tofauti, kinyume cha uonavyo wewe mwenyewe. Matunda haya hayazaliwi na mti wa Kikristo. KN 150.2

Ndugu yangu, dada yangu, fungua mlango wa moyoni kumpokea Yesu. Mkaribishe ndani ya hekalu la rohoni. Saidianeni kuvishinda vipingamizi katika maisha ya nyumba ya wote. Mtakuwa na vita vilivyo vikali kumshinda adui wenu Shetani, na kama mkimtazamia Mungu kuwasaidia katika vita hivi, hamna budi kuwa na umoja mkikata shauri kushinda, kufunga vinywa vyenu msiseme maneno yo yote mabaya, hata kama lkiwabidi kupiga magoti chini na kupaza sauti, “Bwana, mkemee adui wa roho yangu.” KN 150.3

Ikiwa mapenzi ya Mungu yatatimizwa mume na mke wataheshimiana na kuwa na upendano na matumaini. Lo lote ambalo lingeharibu imani na umoja wa watu wa nyumbani Iinapasa kukomeshwa kabisa, na fadhili na upendo vingependelewa. Mwenye kuonyesha moyo wa huruma, uvumilivu, na upendo ataona kuwa moyo huo huo unaonyeshwa kwake. Mahali Roho wa Mungu anapotawala, hapatakuwako na mazungumzo yasiyofaa unyumbani. Kama Kristo kwa kweli anawekwa moyoni, tumaini la utukufu, kutakuwako na umoja na upendo nyumbani. Kristo akaaye moyoni mwa mke atapatana na Kristo akaaye moyoni mwa mume. Watafanya bidii pamoja ili wayapate makao ambayo Kristo alikwenda kuwaandalia wale wampendao. KN 150.4

Wale wanaoihesabu ndoa kama mojawapo ya maagizo matakatifu ya Mungu, yenye kulindwa na mafundisho yake matakatifu, watatawaiiwa na maonyo ya akili ya moyoni. KN 151.1

Katika maisha ya ndoa wanaume na wanawake wakati mwingine hufanya kama watoto wasiopata malezi mazuri, wakaidi. Mume ashika lake, na mke anashika lake, wala hakuna atakayekushindwa. Hali ya mambo ya jinsi hii huleta tu huzuni kubwa. Wote mume na mke, yawapasa kukubali kwa hiari kushindwa kwa njia yake. Hawawezi kuwa na raha wakiwa wanakazania kila mmoja kile apendacho mwenyewe. 2 KN 151.2

Pasipo kuchukuliana na upendano hakuna uwezo duniani uwezao kukushikilia katika umoia na mumeo ndani ya umoja wa Kristo. Urafiki wenu katika ndoa wapasa uwe imara na wenye upendo, mtakatifu na bora, wenye kuwatia uwezo wa kiroho maishani mwenu, ili mpate kuridhisnana ninyi kwa ninyi kama neno la Mungu litakavyo. Mtakapoifikia hali ambayo Mungu ataka mwe nayo, mtapaonja mbinguni mkiwa mngali napa chini na Mungu mtamwona maishani mwenu. KN 151.3

Kumbukeni, ndugu na dada, kwamba Mungu ni upendo na ya kuwa kwa neema yake mwaweza kufaulu kupendezana, kama mlivyokwisha kuahidi katika ndoa yenu. 3 KN 151.4

Kwa neema ya Kristo mwaweza kupata ushindi juu ya nafsi na moyo wa choyo. Mkienenda kama alivyoenenda, na kuonyesha moyo wa kujinvima kwa kila hatua, daima mkiwahurumia zaidi wale walio shidani, wenye kuhitaji msaada, mtapata ushindi kila mara. Siku kwa siku mtafahamu zaidi kuushinda moyo wa kujifikiri nafsi mwenyewe bila kujali wengine na namna ya kuyaimarisha mambo manyonge ya tabia zenu. Bwana Yesu atakuwa nuru yenu, nguvu, yenu kipeo cha kufurahi kwenu, kwa sababu mkekubali nia yake iwe yenye kushinda na kuwa badala ya nia yenu. 4 

Sura ya 22 - Maisha ya Ndoa

WALE wanaoihesabu ndoa kama mojawapo ya maagizo matakatifu ya Mungu, yaliyohifadhiwa kwa mafundisho yake matakatifu, watatwahwa na maonyo ya akili ya moyoni. Yesu hakushurutisha watu wa jamii yo yote kukaa bila kuoa ama kuolewa. Hakuja ili kutangua ndoa takatifu, bali kuitukuza na kuirudishia usafi wake iliokuwa nayo mwanzoni. Anapendezwa kuona uhusiano wa watu nyumbani penye upendo mtakatifu na moyo wa ukarimu kuwa na nguvu. 

Ndoa ni Halali na Takatifu

Hakuna dhambi katika kula wala kunywa, ama katika kuoa na kuolewa. Ilikuwa halali kuoana siku za Nunu, na ni halali kuoana siku hizi, ikiwa kile kilicho halali kinatendwa vizuri wala hakizidi hata kuwa dhambi. Lakini katika siku za Nuhu watu walioana pasipo kutaka shauri kwa Mungu au kutafuta maongozi yake. KN 152.2

Kwamba uhusiano wote wa maisha ni wa kitambo tu yapasa uwe na mvuto uliogeuzwa kidogo juu ya mambo yo yote tutenaayo na yale tusemayo. Katika siku za Nuhu upendo usiokuwa na kiasi wa kile ambacho chenyewe kilikuwa halili ikiwa kingetumiwa vizuri, ndio uliofanya kuoa au kuolewa kuwa dhambi mbele za Mungu. Wako wengi wanaopoteza nafsi zao siku hizi kwa kufikiri sana juu ya ndoa na kushughulika na mambo yake hata kuwasahaulisha mambo mengine. KN 152.3

Ndoa ni takatifu, lakini katika kizazi hiki kibaya inachukua ubaya wa udanganyifu wote ndani yake. Imetumiwa vibaya nayo imekuwa uhalifu ambao huifanya iwe mojawapo ya dalili za siku za mwisho, naam, kama kuoa na kuolewa, kulivyokuwa siku zile kabla ya Gharika. Hali takatifu na madai ya ndoa yakifahamika vizuri, nata sasa itaweza kuwa jambo la kumpendeza Mungu; na matokeo yake yatakuwa furaha kwa pande zote mbili, na Mungu atatukuzwa. KN 152.4

Manufaa ya Ndoa

Wanaojidai kuwa Wakristo wangefikiri sawasawa matokeo ya kila jambo zuri la ndoa, na kanuni takatifu ingekuwa msingi wa kila iambo litendwalo nao. Wazazi wengi wametumia vibaya majaliwa yao mema ya ndoa, na kwa kuzoea kujifurahisha kwa anasa wametia nguvu tamaa zao za mwili. (Wakati mwingine Ellen White husema habari za “siri na manufaa ya ngono”) Kuzidi mno katika neno hili lililo halali ndiko kunakolifanya liwe dhambi kubwa. KN 152.5

Wazazi wengi hawana maarifa wapaswayo kuwa nayo katika maisha ya ngono. Hawakukingwa Shetani asije akawashinda na kuzitawala nia zao na maisha yao ya ngono na kujizuia ataka wayatawale maisha yao ya ngono na kujizuia wasiwe na hali iwayo ya kutokuwa na kiasi. Lakini wengi hawaoni kuwa ni wajibu wa dini kuzitawala tamaa zao mbaya. Wamejiunga katika ndoa kwa kusudi lao wenyewe na, kwa hiyo, huflkiri kuwa ndoa huhalalisha uzoefu wa kujifurahisha kwa tamaa mbaya zaidi. Hata wanaume na wanawake wanaojidai kuwa watauwa hushindwa kujizuia, nao hujitoa kwa tamaa zao mbaya wala hawafikiri kuwa Mungu huwahesabia hatia kwa kutumia vibaya nguvu za uhai, na kuudhoofisha ama kuuondolea mwili mzima nguvu, au kuyakatisha maisha yao.

Mazoea ya Kujizuia na Kuwa na Kiasi

Aha, laiti ningeweza kuwafahamisha wote wajibu wao kwa Mungu kutunza viungo vya akili na vya mwili na kuviweka katika hali bora kabisa wapate kumtumikia Mumbaji wao! Hebu mke aliye Mkristo ajizuie, kwa neno na kwa tendo pia, asiamshe tamaa za mwili za mumewe. Wengi hawana nguvu za kutupa ovyo kwa jambo hili Tokea utotoni mwao wamedhoofisha ubongo na kuufyonza mwili, kwa kutimiza tamaa mbaya za mwili bila ya kujizuia. Kujizuia na kuwa na kiasi yapasa liwe neno kubwa katika maisha yao ya ngono. KN 153.2

Tuko chini ya wajibu mzito kwa Mungu kutunza roho iwe safl na mwili uwe wenye afya, kusudi tupate kuwanufaisha wanadamu wenzetu na kumtumikia Mungu kwa ukamilifu. Mtume amesema maneno haya ya onyo: “Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata makazitii tamaa zake.” Anatusukuma mbele kwa kutuambia kuwa “kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika vote.” Anawaonya wote wajiitao Wakristo kuitoa miili yao iwe “dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu.” Asema: “nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.” KN 153.3

Upendo safi sio wenye kumchochea mwanamume kumfanya mkewe chombo cha kutumia kuiridhisha tamaa yake. Tamaa za mwili ndizo zenye kutimizwa bila kujizuia. Ni wachache kama nini wanaoonyesha upendo wao kwa njia ambayo imeelezwa na mtume: “Kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha (siyo kulinajisi)... bali liwe takatifu lisilo na mawaa.” Huu ni namna ya upendo utakiwao katika ndoa ambayo Mungu huihesabu kuwa takatifu. Upendo ni kanuni safi na takatifu, lakini tamaa mbaya haitakubali kujizuia wala haitatii ama kutawaliwa na akili ya moyoni. Haiyaoni matokeo ya baadaye, wala kuifikiri njia inayoifuata, na matokeo yake. KN 153.4

Shetani Anatafuta Kudhoofisha Kujizuia

Shetani hujitahidi kushusha kipimo cha usafi na hudhoofisha hali ya kujizuia ya wale wanaooana, kwa sababu ajua kuwa tamaa mbaya za mwili zikishinda, uwezo wa tabia ya adili utazidi kudhoofika, hivyo hana sababu za kujali maendeleo yao ya kukua kiroho. Pia ajua kwamba hawezi kwa njia yo yote nyingine, ila kwa njia hii tu, kutia vizuri chapa ya sanamu yake kwa watoto wao, na ya kuwa kwa njia hii aweza kuifanya tabia yao kuwa nyepesi kuliko awezavyo kufanya na tabia ya wazazi wao. KN 154.1

Enyi wanaume na wanawake, siku moja mtafahamu tamaa ya mwili ilivyo na matokeo ya kuitimiza bila kujizuia. Ashiki mayostahili iliyo ya kawaida huweza kupatikana katika ndoa sawa na nje ya umoja huo. Matokeo ya kuzitimiza tamaa mbaya bila kujizuia ni nim? Chumba cha kulala, mahali ambapo malaika wa Mungu wangeongoza, hunajisiwa kwa mazoea haya mabaya. Na kwa sababu ya desturi mbaya za kinyama, zenye kuaibisha kabisa, miili imeharibiwa; mazoea ya kuchukiza mno huleta magonjwa mabaya. Kila ambacho Mungu alikitoa kiwe mbaraka kimefanywa kuwa laana. KN 154.2

Kuzidi mno katika kutwaana kutaharibu upendo wa mazoea mema ya dini, kutanyang’anya ubongo nguvu zake zilizo faradhi kwa afya ya mwili na kutachosha kabisa nguvu za uhai. Haimpasi mwanamke awaye yote kumsaidia mumewe kwa kazi hii ya kujiangamiza mwenyewe. Hatafanya hivyo kama ameelimika na akiwa mwenye upendo wa kweli kwa mumewe. KN 154.3

Kadiri tamaa mbaya za mwili zinavyotimizwa pasipo kujizuia, ndivyo zinavyozidi kuwa na nguvu, nazo zitazidi lcutaka zitimizwe. Hebu wanaume kwa wanawake wamchao Mungu wajue wajibu wao. Wengi wanaojidai kuwa Wakristo wana ugonjwa wa kupooza na ubongo kwa sababu ya kutokuwa na kiasi katika jambo hili. KN 154.4

Waume Wawe Wenye Huruma

Yawapasa waume kuwa waangalifu, wenye bidii, waaminifu, na wenye huruma. Wangeonyesha upendo na moyo wa huruma. Kama wakiyatimiza maneno ya Kristo, upendo wao hautakuwa hali mbaya ya kidunia, wa kuamsha tamaa za mwili, wenye kuleta uharibifu wa miili yao wenyewe na kuwaletea wake zao udhaifu na ugonjwa. Hawatatimiza tamaa mbaya za mwili huku wakiwaambia wake zao kwamba hawana budi kuwatii waume kwa kila jambo. Mume akiwa na tabia njema , usafi wa moyo, ubora wa akili apaswao kila Mkristo wa kweli kuwa nao, itadhihirika katika unyumba. Ikiwa anayo ile nia ya Kristo hatakuwa mharibifu wa mwili, bali atajawa na upendo wa kweli, akijitahidi kukifikia kipeo cha juu kabisa ndani ya Kristo. KN 154.5

Hakuna mtu ampendaye kwa kweli mkewe atakayemkubalia awe mtumwa na mhudumiaji wa tamaa zake mbovu za mwili. Katika ustahimilivu wake hupoteza thamani aliyopata kuwa nayo machoni _pa mumewe. Humwona akidhoofu na kuwa na hali duni kwa kila jambo, na mara huanza kushuku kuwa (Mkewe) atakubali, bila kukaidi, kutendwa na mtu mwingine kama atendwavyo na mumewe mwenyewe. Huutilia shaka uaminifu na usafi wake, ulegevu wake, na hutafuta wengine wapya kuamsha na kuzidisha tamaa zake za mwili mbaya mno. Sheria ya Mungu hudharauliwa. Watu hawa ni wabaya kuliko wanyama wa mwitu; ni mashetani walio katika umbo la mwanadamu. Hawayafahamu mafundisho ya kweli yenye kuikuza hali na kuadilisha, wala upendo mtakatifu. KN 155.1

Mke pia humwonea wivu memewe na kumshuku kuwa kama pakiwa na nafasi, kwa urahisi atamtongoza mwingine kama amfanyiavyo. Huona kuwa hatawaliwi na dnamiri ya moyoni au kicho cha Mungu; vizuuizi vyote hivi vitakatifu vimevunjwa na tamaa mbaya za mwili; mema yote kwa mume yamefanywa kuwa yenye kuzitimiza tamaa mbaya za kinyama. KN 155.2

Wakati Madai yasiyofaa Yafanywapo

Neno la kukatwa sasa ni hili: Je, mke ataona kuwa hana budi kukubali kwa urahisi madai ya mumewe akiona kuwa siyo kitu kingine ila tamaa mbaya tu za mwili zinazomtawala mumewe, na moyoni na akilini mwake akisadiki kuwa akifanya hivyo audhuru mwili wake, ambao Mungu amemwamuru kuutunza na kuuweka katika hali takatifu na ya neshima, kuuhifadhi kama dhabihu iliyo hai kwa Mungu? KN 155.3

Upendo safi, mtakatifu haumwongozi mwanamke kutimiza shauku za mumewe na kupata hasara ya afya na uzima. Kama akiwa na upendo wa kweli na hekima, atafanya bidii kuigeuza nia yake na kuacha kuzitimiza tamaa mbaya za mwili na kuyaelekea mambo bora ya kiroho kwa kuyafikiri sana mafundisho ya dini yanayopendeza. Pengine italazimu kusisitiza mara nyingi kwa unyenyekevu na upendo, hata ikiwa ni kumchukiza, kwamba hawezi kuuharibu mwili wake kwa kukubali kutwaana kupita kiasi. Apaswa, kwa upole na moyo mzuri, kumkumbusha kuwa Mungu analo dai la kwanza na kuu kuliko mengine yote juu ya mwili wake mzima, na ya kuwa hawezi kulidharau dai hili, kwa sababu atatakiwa kutoa hesabu yake katika siku kuu ya Mungu. KN 155.4

Kama atayazidisha mapenzi yake na kwa utakatifu na heshima kuhifadhi hali bora ya kumstahili mwanamke, aweza kufanya makuu kwa mvuto wake wa busara kumwadilisha mumewe pamoja naye mwenyewe, hivyo afanya kazi maradufu. Katika jamoo hili, ambalo ni gumu na la shida kulitimiza, hekima nyingi na uvumilivu hutakikana, pamoja na moyo wa adili na uhodari. Nguvu na neema vyaweza kupatikana kwa maombi. Upendo safi hauna budi kuwa kanuni itawalayo moyoni. Upendo kwa Mungu na upendo kwa mume peke yake waweza kuwa msingi bora wa matendo. KN 156.1

Mke akikubali kutoa mwili wake na nia yake kutawaliwa na mumewe, akimwacha atende apendavyo kwa mambo yote, akiitoa dhamiri ya moyoni mwake, hesnima yake, hata hadhi yake, apoteza nafasi nzuri ya kujitahidi ambayo pengine ingekuwa na mvuto mwema ambao apaswa kuwa nao kumwinua mumewe awe na hali bora. Angeweza kuupunguza uakili wake, na mvuto wake utakasao ungeweza kutumiwa kwa njia ya kutakasa na kusafisha, ukimwongoza kukazana kwa bidii kuzitawala tamaa za mwili na kuwa mwenye moyo wa kupenda mambo ya kiroho, kusudi wapate pamoja kuwa washiriki wa tabia ya Mungu wakiwa wameuepuka uharibifu uliomo ulimwenguni kwa njia ya tamaa za mwili. Uwezo wa mvuto huweza kuwa kitu kikubwa cha kuiongoza nia ya mtu kwenye mambo bora, na kuyaacha mambo duni, kujifurahisha kwa tamaa mbaya za mwili, ambazo moyo usioongoka kwa kawaida kuyafuata. Kama mke akiona moyoni kuwa kusudi ampendeze mumewe hana budi kujidhili na kuwa na hali ya mumewe, wakati tamaa za mwili zikiwa msingi wa upendo wake na kanuni inayoyatawala matendo yake, humcnukiza Mungu; maana hautumii mvuto utakasao juu ya mumewe. Ikiwa anaona kuwa hana budi kushindwa na tamaa mbaya ya mumewe pasipo kusema neno lo lote la onyo, haufahamu wajibu wake kwa mumewe au kwa Mungu wake.

Mlinunuliwa kwa Thamani

Tamaa mbaya mno za mwili zina maskani ndani ya mwili nazo huutumia kufanya kazi. Maneno haya, “mwili” au “tamaa za mwili” yana maana ya hali mbaya mno, ufisadi; mwili wenyewe hauwezi kufanya kinyume cha mapenzi ya Mungu. Tumeamuriwa kuusulibisha mwili, pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Tutawezaje kulitimiza jambo hili? Je tujitie maumivu mwilini? La; bali tuliue lile jaribu lenye kutushawishi kutenda dhambi. Wazo baya lapaswa kuondolewa mbali. Kila wazo halina budi kutekwa nyara kwa Yesu Kristo. Shauku zote mbaya za mwili hazina budi kutawaliwa na nguvu bora zaidi za mtu. Upendo wa Mungu hauna budi kutamalaki; Kristo peke yake apaswa kutawala. Miili yetu haina budi kuhesabiwa kama mali iliyokwisha kununuliwa. Viungo vya mwili vyapaswa kuwa vyombo vya haki.l (1 )AH 121 - 128. 

 

Sura ya 23 - Mama na Mtoto Wake

BADALA ya kuzama kwenye kazi ya kuchosha ya watu wa nyumbani, hebu mke yaani mama atwae wasaa kusoma, kujielimisha, kuwa rafiki wa mumewe, na kujua maendeleo ya akili za moyoni za watoto wake. Hebu atumie kwa busara nafasi aliyo nayo sasa kuwavuta wapenzi wake kwa ajili ya maisha bora zaidi. Na atwae nafasi kumfanya Mwokozi mpendwa kuwa Rafiki wa daima na Msiri mkuu. Na atwae wasaa kwa kusoma Neno la Mungu, na kwenda pamoja na watoto mashambani na kujifunza habari za Mungu kwa njia ya kuutazama uzuri wa kazi zake Mungu. KN 157.1

Hebu awe mchangamfu na mwenye furaha. Badala ya kutumia kila dakika katika kushona kusiko na mwisho, na ufanye wakati wa jioni kuwa saa nzuri ya kustarehe, ya watu wa nyumbani kukutana tena pamoja baada ya kazi za mchana kutwa. Kwa njia hii watu wengi wangeweza kuongozwa kuipendelea jamaa hii kabla hawajachagua klabu ya pombe, Wavulana wangezuiwa wasiende mabarabarani. Wasichana wengi wangeepushwa na marafiki wasio na maana, wanaopoteza. Mvuto wa nyumbani ungekuwa kwa wazazi na watoto kile Mungu alichokusudia, kuwa mbaraka siku zote za maisha. KN 157.2

Swali liulizwalo mara kwa mara ni, “Mke asiwe na uhuru kuchagua apendavyo mwenyewe?” Biblia yaeleza wazi kuwa mume ni kichwa cha watu wa nyumbani. “Enyi wake, watiini waume zenu.” Kama agizo hili lingeishia hapa, tungeweza kusema kuwa cheo cha mke si cha kutamanika; lakini, tusome mwisho wa agizo hilo hilo, yaani, “kama kumtii Bwana wetu.” KN 157.3

Yatupasa kuwa na Roho wa Mungu, ama sivyo hatuwezi kuwa na masikilizano nyumbani. Mke, kama akiwa na Roho wa Kristo, atajihadhari na maneno yake; ataitawala roho yake, na kuwa mtiifu, wala hataona kuwa ni mtumwa, bali rafiki kwa mumewe. Kama mume ni mtumishi wa Mungu, hatajifanya bwana kwa mkewe; hatakuwa mdhalimu, asiyeshauriana na mtu juu ya neno lo lote, na mkali. Hatuwezi kufurahia upendano wa nyumbani kama tukiwa na wasiwasi mwingi; maana nyumbani, Roho wa Mungu akikaa humo, panafanana na mbinguni. Ikiwa mmoja anafanya kosa, mwingine atumie uvumilivu kama ule wa Kristo, wala asikate tamaa. 1 KN 157.4

Kila mwanamke aliye karibu kuwa mama, ijapokuwa mazingira yake yawe ya namna gani, daima angetia moyo mambo ya kufurahisha, uchangamfu, tabia thabiti, akijua kuwa kujitahidi kwake katika jambo hili kutalipwa mara kumi katika mwili, na katika tabia ya adili ya mtoto wake. Wala si hivyo tu. Aweza kuzoea kufikiri mambo mazuri ya kumpendeza, na kwa kufanya hivyo kuudumisha moyo wa furaha mawazoni na kueneza uchangamfu na furaha yake mwenyewe kwa watu wa nyumbani mwake, na kwa wale wanaoshirikiana naye. Kwa kiasi kikubwa afya yake itafanywa kuwa bora zaidi. Nguvu itatolewa kwa chemchemi za uzima, damu itatembea vizuri, siyo pole pole, kama ingalivyofanya ikiwa angekubali kufa moyo na kuhuzunika. Hali yake njema ya akili na ya tabia ya moyoni hutiwa nguvu na moyo wake wa ukunjufu. Uwezo wa nia huweza kupinga maneno ya moyoni nao utakuwa kitulizo kikubwa cha mishipa ya fahamu. Watoto wanaonyang’anywa nguvu hiyo ambayo wangepaswa kuirithi kutoka kwa wazazi wao wangeangaliwa sana. Kwa kuziangalia sana kanuni za mwili wao hali lliyo nzuri zaidi ya mambo huweza kuanzishwa. KN 157.5

Mwenye kutazamia kuwa mama angeitunza roho yake katika upendo wa Mungu. Moyo wake wapaswa uwe na amani; angepata raha katika upendo wa Yesu, akiyatimiza maneno ya Knsto. Angekumbuka kuwa mama ni mtenda kazi pamoja na Mungu. KN 158.1

Mume na mke wanapaswa kushirikiana. Tungekuwa na ulimwengu mzuri namna gani kama akina mama wote wangejitoa wakfu kwa Mungu na kumtoa wakfu mtoto wao, kabla ya na baada ya kuzaliwa kwaKe! KN 158.2

Matokeo ya baadaye ya mivuto kabla ya kuzaa kudharauliwa na wazazi wengi kama jambo lisilo na maana; lakini mbinguni sivyo inavyohesabiwa. Ujumbe uliotumwa kwa njia ya malaika wa Mungu, na kutolewa mara mbili kwa njia nzito sana, huonyesha kwamba jambo hili linapasa tulifikiri sana. KN 158.3

Maneno aliyoambiwa mama Mwebrania (mkewe Manoa), Mungu huwaambia mama wote wa kila kizazi. Malaika asema, “Asile kitu cho chote kilicho najisi; hayo yote niliyomwamuru na ayatunze.” Hali njema ya mtoto itadhuriwa na mazoea mabaya ya mama. Tamaa zake za chakula na tamaa mbaya za mwili hazina budi kutawaliwa na kanuni inayoyaongoza maisha. Yako mambo apaswayo kuepukana nayo, mambo apaswayo kuyapinga, kama akitaka kulitimiza kusudi la Mungu kwake katika kumpa mtoto aliye naye. KN 158.4

Ulimwengu umejaa mitego waliyowekewa vijana. Watu wengi huvutwa macho na maisha ya choyo, ama moyo wa kujipendeza nafsi mwenyewe na anasa. Hawawezi kuona hatari zilizo jificha au mwisho wa kutisha wa njia wanayoiona kuwa ya furaha. Kwa njia ya kuzitimiza tamaa mbaya za chakula na ashiki pasipo kujizuia, nguvu zao hutupwa bure, na mamilioni huangamia ulimwenguni humu na kuukosa ulimwengu ujao. Wazazi wangekumbuka kuwa watoto wo hawana budi kuyapinga majaribu haya. Hata kabla ya kuzaliwa mtoto, matayarisho yangeanza, ambayo yatamwezesha mtoto kufaulu katika kupigana vita na yule mwovu. KN 158.5

Ikiwa kabla ya kuzaliwa mtoto wake, mama mwenyewe ni mfisadi, kama ni mchoyo, mwenyewe harara, na mkali, tabia hizi zitaonekana kwa mtoto. Hivyo watoto wengi wamerithi mielekeo mibaya wasiyoweza kuishinda ila kwa shida sana. KN 159.1

Lakini ikiwa mama hushika, bila kusitasita, kanuni njema, kama akiwa mwenye kiasi na mwenyewe kujizuia, kama ni mwenye utu wema, mpole, na mkarimu, aweza kumrithisha mtoto wake tabia hizo za thamani kuu. KN 159.2

Watoto wachanga ni kioo kwa mama ambamo huweza kuona sura ya mazoea na mwenendo wake mwenyewe. Basi angejihadhari kama nini na maneno yake pamoja na mwenendo wake mbele ya hawa watoto wadogo! Tabia zo zote atakazo kuona wanazo hana budi kuwa nazo yeye mwenyewe. 

Wakati Kazi za Mama Zipaswapo Kupunguzwa

Ni kosa lifanywalo kwa kawaida kutotofautisha katika maisha ya mwanamke wakati akaribiapo kuzaa watoto. Wakati huo kazi ngumu za mama yapasa zipunguzwe. Mabadiliko makubwa yanafanyika mwilini mwake. Inatakiwa damu nyingi, na kwa hiyo nyongeza ya chakula kifaacho mwilini ili kuongeza damu hutakikana, Kama hapati chakula kifaacho kuulisha mwili, hawezi kuwa na nguvu za mwilini na mtoto wake hunyang’anywa nguvu. KN 159.4

Mavazi yake pia huhitaji kuangaliwa. Uangalifu mwingi ungetumiwa kuutunza mwili wake usipatwe na baridi. Asiulazimishe mwili kujihifadhi wenyewe bila lazima, kwa kukosa mavazi. Kama mama akikosa kupata chakula kizuri cha kutosha chenye kuulisha mwili atapungukiwa na damu nzuri, mwendo wa damu yake utakuwa dhaifu, na mtoto wake atakosa kuwa na vitu hivyo pia. Mtoto atashindwa kujitwalia mwilini mwake sehemu ya chakula inayobadilika kuwa damu nzuri kuulisha mwili. Siha ya mama na mtoto hutegemea sana mavazi mazuri ya joto na chakula cha kufaa mwilini. 

Moyo wa Mama Anyonyeshaye

Chakula bora kabisa kwa mtoto mchanga ni chakula kile ambacho hupatikana kutoka mwilini. Si vizuri kumnyima mtoto chakula hiki bila sababu ya kutosha. Ni ukatili mama, kwa ajili ya kujitakia nafasi au starehe, kujaribu kuepukana na kazi hii ya kumnyonyessha mtoto wake mdogo. KN 159.6

Wakati ambapo mtoto mchanga kunyonya ziwa la mama ni wa shida. Mama wengi, wakiwa wananyonyesha watoto wao wachanga, wameachwa kutumika kupita kiasi na kutia joto damu yao kwa kupika chakula; mtoto mchanga amepatwa na madhara vibaya, siyo tu kushindwa na homa inayotokana na kunyonya ziwa la mamaye, bali hata damu yake imetiwa sumu kwa chakula kisicho kizuri kwa afya cha mama, ambacho huutia homa mwili wake mzima, na kukidhuru chakula cha mtoto. Vile vile mtoto atapata madhara kwa hali ya moyoni mwa mama. Kama hana furaha, mwepesi kufadhaika, mwenye kukasirika upesi, mwenye kupandwa na hasira upesi, ziwa anyonyalo mtoto kutoka kwa mamaye litawaka, na mara nyingi, hali italeta msokoto wa tumbo, mpindano, na mara zingine kujipindapinda kwa ugonjwa, na ugonjwa wa ghafula wa muda. KN 160.1

Kadhalika tabia ya mtoto husaidiwa au kudhuriwa na chakula apatacho kutoka kwa mama. Basi, ni jambo kubwa kama nini kwamba mama, wakati anyonyeshapo, angekuwa na moyo wa furaha, akijitawala kabisa moyoni mwake mwenyewe. Kwa kufanya hivi, chakula cha mtoto hakitapata madhara yo yote, na mwenendo mtulivu wa kujiweza nafsi ambao mama huufuata katika kumtendea mtoto wake huhusiana sana na kule kuyafanyiza mawazo ya moyoni mwa mtoto mchanga. Kama akiwa mwepesi wa hasira, tabia ya uangalifu, na saburi ya mama itakuwa na mvuto wa kumtuliza mtoto na kumsahihisha, na afya ya mtoto yaweza kupata nafuu kubwa. 

Utaratibu Katika Utunzaji Mzuri wa Upendo

Watoto wamekabidhiwa kwa wazazi wao kama amana ya thamani, ambayo siku moja Mungu ataitaka mikononi mwao. Yatupasa kutumia saa nyingi zaidi kwa mafundisho yao, pamoja na uangalifu mwingi zaidi, na maombi zaidi. Wanahitaji zaidi malezi bora. KN 160.3

Mara nyingi ugonjwa wa watoto huweza kutokana na makosa ya maongozi. Kutokuwa na saa za kawaida za kula chakula, kutokuwa na mavazi ya kutosha jioni siku za baridi, ukosefu wa mazoezi ya viungo vya mwili kuuweka mwendo wa damu katika hali nzun ya afya, au ukosefu wa hewa safi ya kutosha kuisafisha damu, pengine nuwa ndiyo asili ya ugonjwa. Basi, yafaa waponye hali za makosa hayo upesi iwezekanavyo. KN 160.4

Watoto, kwa kawaida huzoezwa tokea utotoni kujifurahisha kwa kuiridhisha tamaa ya chakula na kufundishwa kwa kuishi ili kula. Mama ahusikana sana na kukuzwa kwa tabia za watoto wake utotoni mwao. Aweza kuwafundisha kuitawala tamaa ya chakula na kuwafanya walafi. Mama mara nyingi hupanga mipango yake kuitimiza sehemu fulani kwa siku; na naipo watoto wakimsumbua, badala ya kutumia wakati kutuliza huzuni zao ndogo na kuwafurahisha, huwapa kitu fulani kukila ili wanyamaze, ambacho hutimiza mradi wake huo kwa muda mfupi tu lakini mwishowe huyafanya mambo kuwa mabaya zaidi. Matumbo ya watoto hushindiliwa kwa chakula wakati wasipokihitaji hata kidogo. Kilichokuwa kikitakiwa tu ni wasaa kidogo wa mama na aungaiizi wake. Lakini amehesabu wakati wake kuwa wa thamani sana hata hawezi kuutoa kuwapendeza watoto wake. Pengine mpango wa nyumba yake kwa namna ya kuwapendeza wageni hata wausifu, na kukipika chakula chake vizuri ndiyo mambo anayoyathamini zaidi kuliko furaha na afya ya watoto wake. KN 160.5

Katika kutayarisha vazi la mtoto mchanga, hali ya kufaa, raha, na afya ingefikiriwa kwanza kabla ya kurikiria namna ama uzuri wa kusifika. Mama asingeumia wakati kwa mapambo na malidadi tu kuyafanya mavazi hayo madogo kuwa ya kupendeza macho, na kwa kufanya hivi kujichosha kwa kazi isiyo ya lazima pia. Asijishurutishe kushona kunakoyatumikisha macho na mishipa ya fahamu, wakati anapohitaji kupumzika na kufanya mazoezi mazuri ya viungo vya mwili. Apaswa kuufaha wajibu wake kutunza nguvu zake ili aweze kutimiza madai yatakayofanywa juu yake. 2

Haja ya Kujizuia Katika Kumtawala (Kumwadhibu) Mtoto

Katika malezi ya mtoto pana nyakati ambapo nia thabiti, ya utu uzima, ya mama inapokutana na nia kaidi, siyo ya haki, ya mtoto. Nyakati kama hizo inatakikana busara kubwa upande wa mama. Kwa kutotumia busara, kushurutisha kwa ukali, madhara makubwa huweza kufanywa kwa mtoto. KN 161.2

Kila iwezekanapo, matata haya yangeepukwa; maana huleta mashindano makali kwa mama na mtoto. Lakini mara matata ya namna hii yatukiapo, hubidi nia ya mtoto kushindwa na nia ya akili zaidi ya mzazi. KN 161.3

Yampasa mama kujizuia kabisa, asifanye jambo lo lote litakaloamsna ndani ya mtoto moyo wa kuasi amri (kutaka shari). Asitoe amri kwa sauti kubwa. Atafaidiwa zaidi akisema kwa sauti ndogo ya upole. Yampasa, kumtendea mtoto kwa njia itakayomvuta kwa Yesu. Anapaswa kufahamu kuwa Mungu ni Msaidizi wake; upendo ndio uwezo wake. KN 161.4

Kama yu Mkristo mwenye busara hatathubutu kumshurutisha mtoto kutii. Humwomba Mungu kwa bidii ili adui asipate kushinda, na, akisali hufahamu nafsim kufanywa upya maisha ya kiroho. Huona kwamba uwezo ule ule utendao kazi ndani yake hutenda kazi ndani ya mtoto pia. Huwa mpole zaidi. Ushindi umepatikana. Uvumilivu wake, wema wake, maneno yake ya hekima na kiasi, yamefanya kazi yao, Kuna amani baada ya matata, kama mwangaza wa jua bada ya mvua. Nao malaika, ambao wameyatazama mambo hayo, huimba mara hiyo nyimbo za furaha. KN 161.5

Matata ya namna hii huingia pia katika maisha ya mume na mke, ambao, isipokuwa wanatawaliwa na Roho wa Mungu, nyakati kama hizo wataonyesha moyo wa ghadhabu ya ghafula usio wa akila ambao unaonyeshwa mara nyingi na watoto. Jiwe gumu likipiga jiwe lingine gumu kutakuwako na ushindani wa nia moja kushindana na nia nyingine. 3 

 

Sura ya 24 - Baba na Mama Mkristo

KADIRI mfanyavyo kwa uaminifu wajibu wenu nyumbani baba kama kuhani wa nyumbani, mama kama mmishenari nyumbani mwazidisha njia za kufanya mema nje ya nyumba hiyo. Kadiri mnavyotumia vizuri uwezo wenu wenyewe, ndivyo mnavyofanywa kufaa zaidi kutumika kanisani na jirani. Kwa kufungamana na watoto wenu na kuwafungamanisha na Mungu, baba na mama na watoto pia huwa watenda Kazi pamoja na Mungu. 1

Uwakfu wa Kazi ya Mama

Yampasa mwanamke kushika madaraka ambayo Mungu alimwekea tangu zamani, sawa na yale ya mumewe. Ulimwengu una hitaji akina mama ambao ni mama siyo kwa jina tu, bali kwa kweli kama ilivyo maana ya neno lenyewe. Twaweza kusema kuwa kazi zimhusuzo mwanamke ni takatifu zaidi ya zile za mwanamume. Basi, mwanamke na afahamu uwakfu wa kazi yake na kwa nguvu na kicho cha Mungu ashike kazi yake ya maisha. Hebu awafundishe watoto wake kwa ajili ya manufaa katika ulimwengu huu na kwa ajili ya makao katika ule ulimwengu bora zaidi. KN 163.2

Mke na mama asingetoa nguvu zake na kukubali uwezo wake kutotumika, na kumtegemea kabisa mumewe. Nafsi yake haiwezi kuchanganyika ndani ya nafsi ya mumewe. Yampasa kuona kuwa ana haki sawa na mumewe-kusimama karibu naye, akiwa mwaminifu kwa kazi na wajibu umpasao. Kazi yake katika mafundisho ya watoto wake ni yenye kukuza hali kwa kila jambo na yenye kuadilisha sawa na kazi iwayo yote awezayo kufanya mumewe, hata kama kazi yenyewe iwe ya cheo cha iaji mkuu wa nchi nzima. KN 163.3

Mfalme penye kiti chake cha enzi hana kazi ya cheo kikubwa zaidi ya ile aliyo nayo mama. Mama ni malkia kwa watu wa nyumba yake. Anao uwezo wa kuzikuza tabia za watoto wake, kusudi wapate kufanywa wafae kwa maisha bora, ya milele. Malaika asingeweza kuomba kazi ya cheo kikubwa zaidi ya hiyo; maana kwa kufanya kazi hii (mama) humtumikia Mungu. Basi, na afahamu ubora wa kazi zake na kuvaa silaha zote za Mungu, ili apate kuyapinga mashawishi ya kukifuata kipimo cha walimwengu. Kazi yake ni ya wakati huu na ya umilele pia. KN 163.4

Kama waume huenda zao kazini, na kuwaacha wake zao kuwatunza watoto nyumbani, mke na mama hufanya kazi kubwa na ya maana sawa sawa kabisa na kazi ile afanyayo mume na baba. Ingawa mmoja yuko nje mahali pa kazi ya umishenari mwingine ni mmishenari nyumbani, ambaye shughuli zake na mashaka na mizigo yake mara nyingi hupita sana ile ya mume na baba. Kazi yake ni nzito na yenye maana. Mumewe nje kazini aliko aweza kupata heshima na sifa za watu, huku (mke) mwenye kutaabika nyumbani akiwa pengine asiyepata sifa yo yote ya kidunia kwa kazi yake. Lakini ikiwa hufanya kazi hii kwa faida ya jamaa yake, akitafuta kuziendeleza tabia zao zifanane na Kielelezo Kitakatifu, malaika mwenye kuandika kumbukumbu huliandika jina lake kama mmojawapo wa wamishenari wakubwa ulimwenguni. Mungu huona mambo vingine, tofauti na macho ya mwanadamu yenye kikomo yaonavyo. KN 163.5

Ulimwengu umejaa mivuto mibaya. Mitindo na mila hutoa mvuto wa nguvu juu ya vijana. Ikiwa mama anakosa kazini mwake kuwafundisna, kuwaongoza, na kuwashika watoto wake, kwa urahisi watayakubali mabaya na kuyaasi mema. Hebu kila mama amwendee Mwokozi wake kwa sala hii, “Tufundishe jinsi itupasavyo kumwamuru mtoto, na jinsi ya kumtendea.” Hebu na aangalie mafundisho ambayo Mungu ametoa katika neno lake, naye atapewa hekima kadiri anavyohitaji. KN 164.1

Kila mama na aone kuwa dakika zake zina thamani isiyohesabika; kazi yake itajaribiwa siku ile kuu ya kutoa hesabu. Ndipo itaonekana kuwa makosa na uhalifu wa wanaume kwa wanawake wengi hutokana na ujinga na dharau za wale ambao kazi ingekuwa kuwaongoza watoto katika njia nyofu. Tena itaonekana kuwa wengi walionufaisha ulimwengu kwa nuru halisi na kweli na utakatifu ni kwa sababu ya mafundisho ambayo yalikuwa chanzo cha mvuto wao na kufaulu kwa mama Mkristo mwenye kuomba kwa bidii.

Uwezo wa Mama kwa Mema

Pengine hali ya mama ni duni; lakini mvuto wake, ukiungamanishwa na ule wa baba, ni wenye kudumu milele. Uwezo mkubwa uliopata kuwako humu duniani, tusipohesabu uwezo wake Mungu, ni uwezo alio nao mama kwa ajili ya mema. KN 164.3

Mama Mkristo daima atakuwa macho kuzijua hatari zinazowazunguka watoto wake. Atauweka moyo wake mwenyewe katika hali safi, na takatifu; atatawala hasira yake na kanuni zinazoyaongoza maisha yake kwa Neno la Mungu naye atafanya kwa uaminifu wajibu wake, akiyashinda majanbu madogo madogo ambayo daima yatamshambulia. KN 164.4

Akili za watoto ni nyepesi, nao hutofautisha sauti za uvumilivu, na upendo na amri kali ya hasira, ambayo hukausha upendo na nia njema mioyoni mwa watoto. Mama Mkristo wa kweli hatawafukuza watoto wake machoni pake kwa ukali wake na kukosa huruma. KN 164.5

Akina mama, jueni kwamba mvuto na kielelezo chenu huwa na matokeo kwa tabia na hali ya baadaye ya watoto wenu; na kwa habari ya madaraka yenu, kuzeni nia njema na tabia safi, mkionyesha tu ukweli, wema, na uzuri. KN 165.1

Wanaume na watoto walio wengi wasiopata cho chote cha kuwavutia nyumbani, ambao daima husalimiwa kwa kushutumiwa na kunung’unikiwa, hutafuta raha na starehe mahali pengine mbali na nyumbani, ulevini au mahali penginepo penye mambo ya anasa yanayokatazwa. Mke ambaye ni mama, akiwa na shughuli nyingi za nyumbani, mara nyingi hajali adhabu ndogo ndogo zifanyazo nyumbani pawe mahali pa kupendeza kwa mumewe na kwa watoto, hata kama asipoyatafakari masumbuko na shida mbele yao. Akiwa katika shughuli ya kutayarisha chakula au nguo, mumewe na wanawe huingia na kutoka kama wageni. KN 165.2

Kama akina mama wakikubali kuvaa mavazi ovyo nyumbani, wanawafundisha watoto wao kuiga njia hiyo hiyo ya uzembe. Mama walio wengi hudhani kuwa kitu cho chote chatosha kuvaa nyumbani, hata kama ni nguo iliyoraruka vibaya na mbovumbovu. Lakini mara hupotewa na mvuto wao kwa watu wa nyumbani. Watoto huulinganisha mvao wa mama yao na ule wa wengine wenye kuvaa maridadi, na heshima yao kwake hupungua. KN 165.3

Mke halisi na mama wa watoto atafanya kazi zake kwa makini na moyo wa furaha, bila kufikiri kwamba ni jambo la kumwondolea heshima kufanya kwa mikono yake mwenyewe cho chote kilicho cha lazima kufanywa katika nyumba yenye utaratibu mzuri. 2 KN 165.4

Kichwa cha Nyumba Kumwiga Kristo

Mkuu wa watu wote nyumbani ni baba. Yeye ndiye mwenye kutunga sheria, na kuonyesha kwa kielelezo chake mwenyewe cha kiume kwamba anazo tabia thabiti; nguvu, uaminifu, unyofu, uvumilivu, moyo mkuu, bidii, na hali ya manufaa. Baba kwa neno moja ni kuhani wa watu wa nyumbani, awekaye madhabahuni mwa Mungu dhabihu ya asubuhi na jioni. Mke na watoto wangetiwa moyo kujiunga katika kuitoa sadaka hii na pia kushiriki wimbo wa kumsifu Mungu. Asubuhi na jioni, baba kama kuhani wa watu nyumbani, angeungama mbele za Mungu dhambi alizotenda yeye mwenyewe na zile walizotenda watoto wake katika siku hiyo. Dhambi zile azijuazo na zile za siri pia ambazo jicho lake Mungu peke yake limeziona; zote yapasa ziungamwe. Kanuni hii, ikitimizwa kwa moyo wa bidii na baba wakati akiwapo au na mama wakati baba asipokuwapo nyumbani itawaletea mibaraka watu wa nyumbani. KN 165.5

Kwa mwanaume ambaye ndiye mume na baba, napenda kusema, Hakikisha kwamba tabia safi, takatifu zaizunguka roho yako. Yakupasa kujifunza kila habari za Kristo. Kamwe haikupasi kuonyesha moyo wa udhalimu nyumbani. Mtu afanyaye hivi anatenda kazi pamoja na malaika wabaya. Yaweke mapenzi yako chini ya mapenzi ya Mungu. Fanya yote uwezayo kuyafanya maisha ya mkeo yawe mazuri na ya raha. Litwae Neno la Mungu liwe mshauri wako. Nyumbani yashike mafundisho ya Neno la Mungu. Ndipo utayashika maishani mwako kanisani nawe utaweza kulichukua manali unapofanyia kazi yako. Kanuni za mbinguni zitakuwezesha yote utendayo. Malaika wa Mungu watashirikiana nawe, wakikusaidia kumdhihirisha Kristo kwa walimwengu. Usikubali masumbuko ya kazi yako kuleta giza kwenye maisha yenu nyumbani. Kama, wakati mambo madogo madogo yanapotokea ambayo si sawa, unashindwa kuwa na saburi, uvumilivu, moyo wa fadhili, na upendo, hilo huonyesha kwamba hujamchagua kama rafiki yako Yeye ambaye alikupenda hata akautoa uhai wake kwa ajili yako, kusudi upate kuwa na umoja nave. KN 166.1

Ni jambo lionyeshalo tabia ya kiume aliyo nayo mume akifikiri daima cheo chake kama kichwa cha jamaa. Haimwongezei heshima kumsikia akiyatumia maneno ya Biblia kusaidia madai yake na madaraka yake. Haitamfanya azidi kuwa hodari kumtaka mkewe, mama na watoto wake, kutekeleza mipango ya mumewe kana kwamba haiwezi kukosewa. Bwana amemweka mume kichwa cha mke awe mlinzi wake; yeye ndiye kiungo cha jamaa, akiwafunga pamoja watu wa nyumbani, kama Kristo alivyo kichwa cha Ramsa na Mwokozi wa mwili. Hebu kila mume anayedai kumpenda Mungu ajifunze kwa uangalifu mapenzi ya Mungu katika cheo chake. Mamlaka ya Kristo yametumiwa kwa busara, kwa wema na upole wote; basi mume na autumie uwezo wake na kumwiga Kichwa kikuu cha kanisa. 3 KN 166.2

Wazazi, Fanyeni Kazi Pamoja kwa Ajili ya Wokovu wa Watoto Wenu

Pazia lingeweza kurudishwa nyuma na baba na mama waone kama Mungu aonavyo kazi ya siku hiyo, na kuona jinsi jicho la Mungu liilinganishavyo kazi ya mmoja na ile ya mwingine, wangeshangazwa na mafunuo ya mbinguni. Baba angeziona kazi zake dhahiri kidogo, ambapo mama angekuwa na moyo mpya na kupata nguvu kuendesha kazi yake kwa busara. Wakati baba alipokuwa akishughulika na mambo ambayo hayana budi kupotea na kupita, mama amekuwa akishughulika na kukuza akili za moyoni na tabia, akifanya kazi licha ya mambo ya muda mfupi tu, bali hata kwa ajili ya uzima wa milele. 4 KN 166.3

Kazi ya baba watoto wake haiwezi kuhamishwa na kupewa mama. Kama mama akifanya kazi yake mwenyewe, anao mzigo wa kutosha kuchukua. Kwa kushirikiana tu kazini ndivyo baba na mama wawezavyo kuitimiza kazi ambayo Mungu amewakabidhi. KN 167.1

Baba asitoe udhuru kwa kukosa kufanya sehemu yake ya kazi ya kuwafundisha watoto wake kwa ajili ya maisha haya na kwa ajili ya uzima wa milele. Hana budi kushiriki wajibu huu. Wote wawili, baba na mama wana wajibu uwapasao. Yafaa pawepo upendo na staha ambayo huonyeshwa na wazazi wao kwa wao, kama wakipenda kuona tabia hizi kwa watoto wao. KN 167.2

Baba wa wavulana apaswa afahamiane sana na wanawe, akiwanufaisha kwa maarifa yake mengi zaidi na kuzungumza nao kwa uelekevu na upole ili kuwafungamanisha moyoni mwake. Yampasa aache waone kuwa anawafikiria sana, na ya kuwa furaha yao huikumbuka daima. KN 167.3

Mwenye jamaa ya watoto wa kiume yampasa kufahamu kuwa, ajapokuwa ana kazi ya namna gani, kamwe asikose kuzijali roho alizopewa kuzitunza. Amewazaa watoto hawa ulimwenguni naye amejitwisha mzigo huu kwa Mungu kufanya kila kitu awezavyo kuwaepusha wasishirikiane na watenda mabaya wala kufanya urafiki nao. Haimpasi kuwaacha watoto wake wa kiume, watundu, kutunzwa tu na mama. Huo ni mzigo sana kwake. Hana budi kupanga mambo kwa faida ya mama na watoto hasa. Pengine itakuwa vigumu sana kwa mama kujitawala na kuyamudu vizuri mafundisho ya watoto wake. Kama ni hivyo, baba angechukua mzigo huo zaidi moyoni mwake. Yampasa akate shauri kujitahidi sana kuwaokoa watoto wake. 5 KN 167.4

Shauri Jema Juu ya Kutoa Hesabu ya Watoto

Watoto ni urithi wa Bwana, ni juu yetu kutoa habari za namna tufanyavyo na mali yake Mungu. Kwa upendo, imani, na sala, hebu wazazi wafanye kazi kwa ajili ya watu wa nyumbani mwao, mpaka kwa furaha waweze kufika mbele za Mungu wakisema, “Angalieni, mimi na watoto hawa niliopewa na Bwana.” KN 167.5

Mungu angependa wazazi kutenda lcama watu wenye akili na kuishi kwa njia ambayo kila mtoto aweza kufundishwa vizuri, ili mama apate kuwa na nguvu na nafasi ya kutumia uwezo wa akili zake katika kuwapa watoto wake wadogo malezi mema kwa kushirikiana na mafaika. Yampasa awe na moyo wa kutenda vizuri wajibu wake na kufanya kazi yake kwa kicho na upendo wa Mungu, kusudi watoto wake wapate kuwa mbaraka kwa jamaa na kwa watu mtaani. KN 167.6

Mume na baba angeyafikiria mambo haya yote ili mke na mama wa watoto wake asije akachoshwa na kulemewa kwa kukata tamaa. Apaswa kuona kuwa mama wa watoto wake hakutiwa katika shida mahali asipoweza kuwatendea haki watoto wake wengi, hata iwabidi kukua pasipo kupata malezi mazuri. KN 168.1

Wako wazazi ambao, bila kufikiri kama waweza kuwatendea ipasavyo jamaa kubwa ama sivyo, huzijaza nyumba zao watoto hawa wadogo wasioweza kujihudumia wenyewe, wenye kuwategemea tu wazazi wao kwa matunzo na kwa mafundisho. Hili ni kosa baya, si kwa mama tu, bali kwa watoto wake na kwa jamii ya watu mtaani. Mtoto mikononi mwa mama mwaka kwa mwaka ni udhalimu mkuuu kwake. Hupunguza, na mara nyingi huharibu starehe na kuongeza uchovu wa kazi nyumbani. Huwanyang’anya watoto matunzo, elimu na furaha ambayo wazazi wangeiona kuwa ni wajibu wao kuwapa. KN 168.2

(Wazazi) wangefikiri kwa makini riziki wawezazo kuwapatia watoto wao. Hawana haki kuzaa watoto ulimwenguni kuwa mzigo kwa wengine. KN 168.3

Mwisho wa mtoto utakavyokuwa ni jambo lisilofikiriwa ila kidogo tu kama nini! Kuiridhisha ashiki ndilo wazo kubwa tu, na mke na mama hutwishwa mizigo ambayo hudhoofisha nguvu zake za uhai na kupoozesha uwezo wake wa kiroho. Akiwa na afya dhaifu na moyo uliokatishwa tamaa hujiona amezungukwa na kundi la watoto asiloweza kulitunza kama impasavyo. Kwa kukosa malezi mazuri yawapasayo kupata, hukua na kumdharau Mungu na kuambukiza wengine maovu ya tabia zao wenyewe, na hivyo ndivyo lipatikanavyo jeshi ambalo Shetani huweza kulitumia kama apendavyo. 6 KN 168.4

Sura ya 25 - Nyumba ya Mkristo

KATIKA kuchagua nyumba, Mungu angependa tufikiri jambo la kwanza, mivuto ya tabia ya adili na ya dini itakayotuzunguka pamoja na jamaa zetu. Mahali pa kuiweka nyumba pakitafutwa kusudi hili halina budi kuwa jambo la kuongoza uchaguzi huo. Usitawaliwe na tamaa ya mali, mitindo, wala desturi za mtaa. Fikiri kile ambacho kitasaidia kuleta utovu wa anasa, usafi, afya na thamani halisi. KN 169.1

Badala ya kukaa mahali ambapo vitu vya kuonekana machoni na sauti zinazosikika hushawishi mawazo mabaya, mahali ambapo makelele na fujo huchosha na kutia wasiwasi, nenda mahali uwezapo kutazama kazi zake Mungu. Tafuta raha ya moyoni mahali penye uzuri na utulivu na amani ya viumbe vya asili. Hebu macho yatazame mashamba yenye neema, mahali penye miti mingi kidogo, na vilima. Angalia anga, isiyo na mavumbi wala moshi wa mjini, na kuvuta hewa safi itiayo afya na nguvu iliyojaa angani. KN 169.2

Wakati umewadia, ambao kadiri Mungu anavyofungua njia, jamaa za watu nyumbani wangehamia nje ya miji mikubwa. Watoto wangechukuliwa mashambam. Wazazi wangejipatia mahali pazuri pa kufaa kadiri wawezavyo kwa fedha zao. Ingawa makao yawe madogo, walakini pasikose kuwepo shamba linalopakana liwezalo kulimwa. KN 169.3

Baba na mama wenye kipande cha shamba na nyumba ya kupendeza ni wafalme na malkia. Ikiwezekana, nyumba lwe nje ya mji, mahali watoto wawezapo kupata udongo wa kulima shamba. Kila mmoja na awe na kipande cha shamba lake mwenyewe; na ukiwafundisha namna ya kutengeneza shamba, namna ya kuutayarisha udongo kwa ajili ya kupanda mbegu, na faida ya kupalilia shamba, wafundishe pia jinsi ilivyo muhimu kuondoa desturi mbaya na maovu maisham. Wafundishe kuzuia mazoea mabaya kama wanavyozuia magugu mashambani mwao. Itachukua muda mrefu kufundisha masomo haya, lakini italeta faida kubwa. KN 169.4

Dunia ina mibaraka iliyosetirika ndani yake kwa ajili ya wale wenye moyo na nia na ustahimilivu kuzikusanya hazina zake. Wakulima wengi wameshindwa kupata malipo ya kutosha toka mashambani mwao kwa sababu hushughulika na kazi hiyo kana kwamba ni ya aibu na yenye kuwaondolea heshima; hawaoni kuwa pana mbaraka ndani yake kwao na kwa watu wa nyumbani mwao. KN 169.5

Wazazi wana wajibu uwapasao kwa Mungu kufanya makao yao yawe na hali ipatanayo na ukweli wanaoukiri. Ndipo wanaweza kutoa mafundisho sahihi kwa watoto wao, na watoto wataweza kujifunza kufananisha makao haya hapa chini na yale makao ya juu mbinguni. Jamaa hii hapa haina budi, kama iwezekanavyo, kuwa mfano wa ile jamaa ya mbinguni. Ndipo vishawishi vinayowajia kuwavuta kujifurahisha kwa anasa za mambo hafifu na manyonge vitakosa nguvu. Yapasa watoto wafundishwe kuwa hapa duniani wao ni watu tu wanaojaribiwa kama watafaa ama sivyo, na kuelimishwa ili wawe wenyeji wa makao yale ambayo Kristo anawaandalia wale wampendao na kuzishika amri zake. Huu ndio wajibu wa kwanza kabisa uwapasao wazazi. KN 170.1

Kadiri iwezekanavyo, nyumba zote zinazokusudiwa kukaliwa na wanadamu zingejengwa mahali palipoinuka, palipokaushwa vizuri. Kufanya hivi kutahakikisha kuwa unacho kiwanja kikavu. Mara nyingi watu hawajali jambo hili. Basi, udhaifu wa daima, magonjwa mabaya, na vifo vingi ni matokeo ya unyevu na homa ya malaria inayopatikana katika nyanda za chini zisisoweza kukauka vizuri. KN 170.2

Katika kujenga nyumba, ni jambo la muhimu sana kuweka madirisha makubwa ili kuingiza hewa safi na mwanga wa jua. Hewa safi na mwangaza viwepo kwa wingi katika kila chumba nyumbani. Vyumba vya kulala na viwe mahali panapopata hewa safi mchana na usiku. Chumba cho chote kisichoweza kufunguliwa kila siku na kuingiliwa na hewa na mwangaza, hakifai kwa kulala. KN 170.3

Uwanja uliofanywa kuwa wa kupendeza kwa kupandwa miti huko na huko maua, kwa kuacha nafasi nzuri kutoka nyumba yenyewe, una mvuto mzuri kwa watu wa nyumbani, na ukitunzwa vizuri, hautaleta madhara yo vote kwa afya. Lakini miti ya kivuli na vichaka karibu na nyumba huifanya iwe ya kuleta ugonjwa, kwa kuwa huzuia hewa isiingie kwa wingi na kukinga mionzi ya nuru ya jua. Matokeo yake huwa unyevu ama uvundo unaojikusanya nyumbani, hasa siku za baridi. 

Vyombo vya Nyumbani Viwe Vyepesi Visivyo vya Bei Kubwa

Weka nyumbani mwako vyombo vyepesi, rahisi kutengenezwa, vitu ambavyo vitastahimili kutumiwa, viwezavyo kusafishwa kwa urahisi, na rahisi kupatikana, visivyo vya bei kubwa. Kwa kujaribujaribu, waweza kuifanya nyumba isiyo na vitu vya bei kubwa kuwa ya kupendeza na kuvutia macho, kama pakiwako upendo na moyo wa kuridhika. Raha haipatikani katika mambo ya kujionyesha tu. Utaratibu wa mambo ya watu wa nyumbani ukiwa mwepesi ndivyo nyumba hiyo itakavyozidi kuwa ya furaha. Si lazima kuwa na mastakimu na vyombo vya gharama kubwa kusudi kuwaridhisha watoto na kuwapendeza nyumbani kwao, lakini ni jambo la muhimu kuwaonyesha upendo na malezi mazuri. 1 KN 170.5

Mnapaswa siku zote kushirikikiana mali nyumbani mwenu. Kumbukeni kuwa mbinguni hakuna machafuko, na ya kuwa nyumba yenu ingekuwa kama mbinguni mkiwa bado mngali hapa chini. Kumbukeni kuwa kwa kufanya kwa uaminifu siku kwa siku mambo yale madogo madogo ya kufanywa nyumbani, mwatenda kazi pamoja na Mungu, mkithibitisha tabia ya Kikristo. Kumbukeni wazazi, kwamba mnauhudumia wokovu wa watoto wenu. Ikiwa mazoea yenu ni safi, yasiyo na makosa, kama mwaonyesha umaridadi na utaratibu, sifa nzuri na haki, utakaso wa roho, mwili na moyo, mwayatii maneno ya Mkombozi, “Ninyi ni nuru ya ulimwengu.” KN 171.1

Anza mapema kuwafundisha watoto kutunza mavazi yao.

Wapatie mahali pa kuweka vitu vyao na wafundishwe kukunja vizuri kila kitu na kukiweka mahali pake. Kama huwezi kuwanunulia dawati, tumia sanduku, uligawe vyumba vidogo vidogo, na kulifunika kwa kitambaa kizuri king’aacho. Kazi hii ya kufundisha usafi na utaratibu itachukua wasaa mdogo kila siku, lakini itakuwa na faida baadaye kwa watoto wenu, na mwishowe itakuokolea wakati na masumbufu mengi. KN 171.2

Wazazi wengine huwaacha watoto wao kuwa waharibifu kutumia kwa michezo vitu ambavyo hawana haki kuvigusa. Watoto wangefundishwa kuwa hawana ruhusa kutumia mali ya watu wengine. Yawapasa kujifunza kushika kanuni za adabu kwa ajili ya raha ya jamaa nzima. Haiwaongezei watoto furaha wanaporuhusiwa kutumia kila kitu wanachoona. Kama wasipofundishwa kuwa watunzaji, watakua huku wakiwa na tabia za uharibifu wa vitu. KN 171.3

Msiwape watoto vitu vya kuchezea vyenye kuvunjika kwa urahisi. Kufanya hivi ni kuwafundisha uharibifu. Hebu wapatie vitu vichache vya kuchezea, lakini viwe imara na vyenye kudumu siku nyingi. Mashauri ya namna hii, ingawa yaonekane kuwa madogo namna gani, yana maana sana katika malezi ya mtoto. 2 

Sura ya 26 - Mivuto ya Kiroho Nyumbani

Twaweza kupata wokovu wa Mungu nyumbani mwetu; lakini hatuna budi kuuamini, kuushika maishani mwetu, na kuwa na imani idumuyo daima, na kumtumainia Mungu. Amri ambazo Neno la Mungu hututolea ni kwa faida yetu wenyewe. Hutuongezea furaha ya watu wa nyumbani mwetu, na ya wote wanaotuzunguka. Huadilisha tamaa yetu, kuzitakasa akili zetu za kuchagua mazuri, na kuleta amani ya moyoni, na mwisho, uzima wa milele. Malaika wahudumuo watakaa zaidi kwetu, na kupeleka mbinguni habari za maendeleo yetu mema katika maisha ya dini; naye malaika mwandishi ataandika habari nzuri za kupendeza. KN 172.1

Roho ya Kristo itakuwa mvuto wa daima katika maisha ya nyumbani. Kama wanaume na wanawake watafunua mioyo yao kupokea mvuto wa mbinguni wa kweli na upendo, mafundisho haya yatamiminika tena kama vijito vya maji jangwani, yakiwaburudisha wote na kupaneemesha manali ambapo sasa ni jangwa tupu lisilo na kitu. 1 KN 172.2

Kudharau dini ya nyumbani, kutojali kuwafundisha watoto wenu, ni jambo lisilompendeza Mungu hata kidogo. Kama mmojawapo wa watoto wenu angetumbukia mtoni, na awe anashindana na mawimbi na kuwa katika hatari ya kuzama, ungekuwa na msukosuko wa jambo la kufanywa haraka namna gani! Jitihada kubwa kama nini zingefanywa-sala za namna gani zingeombwa, na bidii kubwa kama nini ingeonyeshwa, kuyaokoa maisha ya mtu huyo! Lakini hapa kuna watoto wenu nje ya Kristo, roho zao hazijaokoka. Pengine ni wakorofi na wasio na adabu, aibu kwa jina la Waadventista. Hupotea pasipo kuwa na tumaini wala Mungu ulimwenguni, nanyi hamjali. KN 172.3

Snetani hujitahidi sana kuwapotosha watu ili wakae mbali na Mungu; naye hulitimiza kusudi lake wakati maisha ya dini yanapotoswa kwenye shughuli za kazi, wakati anapozishika sana fikara zao katika kazi za uchumi hata wasiwe na nafasi tena ya kusoma Biblia zao, kusali faraghani na kutoa shukrani na kumsifu Mungu kama sadaka ya kuteketeza juu ya madhabahu asubuhi na jioni. Wachache kama mni hufahamu hila za adui mkuu! Wengi kama nini hawazijui hila zake! 2

Maombi ya Asubuhi na Jioni

Baba na mama, kila siku asubuhi na jioni wakusanyeni watoto wenu karibu nanyi, na kwa maombi ya unyenyekevu, inueni mioyo yenu kwa Mungu mpate msaada. Wapenzi wenu wako kwenye hatari ya majaribu. Udhia wa kila siku unasonga mapito ya vijana na wazee. Wale ambao wataishi maisha ya uvumilivu, upendano, na furaha hawana budi kumwomba Mungu. Twaweza kupata ushindi juu ya nafsi kwa njia tu ya kupokea msaada wa daima kutoka kwa Mungu. KN 173.1

Kama pamekuwako wakati ambapo kila nyumba ingekuwa nyumba ya maombi, sasa ndio wakati huo. Ukafiri na mashaka vimeenea. Uovu umejaa tele. Makosa mabaya yanafurika katika njia kuu za rohoni, na uasi dhidi ya Mungu hutokea katika maisha. Zikiwa zimetawaliwa na dhambi, akili za kuchagua mema na mabaya ziko chini ya utawala wa mabavu wa Shetani. Roho imefanywa kuwa uwanja wa majaribu yake; na ikiwa mkono fulani wenye nguvu hauwezi kunyoshwa ili kumwokoa, mwanadamu atakwenda huko anakoongozwa na mkuu wa uasi. KN 173.2

Lakini, wakati huu wa hatari za kutisha, wengine wanaodai kuwa ni Wakristo hawana maombi kwa watu wa nyumbani. Hawamheshimu Mungu nyumbani, hawawafundishi watoto kumpenda na kumcha Mungu. Wengi wamejitenga mbali naye hata hujiona kuwa wamestahili hukumu wakimkaribia. Hawawezi kukikaribia “kiti cha neema kwa ujasiri,” “huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano.” (Waebrania 4:16; lTimotheo 2:8). Hawana umoja na Mungu. Wana namna ya utauwa bila uwezo. KN 173.3

Wazo kwamba sala si faradhi ni mojawapo ya hila kubwa za Shetani anazotumia kuharibu roho za watu. Kuomba ni kushirikiana na Mungu, chemchemi ya hekima, Chimbuko la nguvu, na amani, na raha. Yesu alimwomba Baba dua “pamoja na kulia sana na machozi.” Paulo huwaonya waumini kuomba “bila kukoma” katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru haja zao zijulikane na Mungu. Yakobo asema, “Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana.” (Waebrania 5:7; 1 Wathesaloneke 5:17; Yakobo 5:16). Kwa kuomba kwa bidii wazazi wangewazungushia watoto wao kitalu. Yawapasa kuomba kwa imani kamili kuwa Mungu akae nao na ya kwamba malaika watakatifu wawalinde pamoja na watoto wao na kuwaepusha na nguvu za udhalimu za Snetani. KN 173.4

Yawapasa katika kila nyumba pawekwe saa ya maombi ya asubuhi na jioni. Ni jambo zuri kama mni kwa wazazi kuwakusanya watoto wao kuwazunguka kabla ya kufungua kinywa, kumshukuru Baba aliye mbinguni kwa ulinzi wake usiku kucha, na kumwomba msaada na uongozi na ulinzi wake mchana kutwa! Pia yafaa kama nini, inapokuwa jioni, kwa wazazi na watoto kukusanyika tena mbele za Mungu na kumshukuru kwa ajili ya mibaraka ya siku hiyo ambayo imepita. KN 173.5

Kila siku asubuhi jitoeni wakfu na watoto wenu kwa Mungu kwa siku hiyo. Msifikiri kwamba yafaa kufanya hivi baadaye miezi au miaka kadha wa kadha ikisha kupita; hiyo si yenu. Mmepewa siku moja fupi. Mtumikieni Bwana saa za siku hiyo, kana kwamba ndiyo siku yenu ya mwisho duniani. Wekeni mipango yenu yote mbele za Mungu, kutimizwa au kuachwa, kama Mungu anavyoamua mwenyewe. Kubalini mipango yake badala ya yenu wenyewe, ijapokuwa kuikubali hubidi kuyaacha mashauri yanayopendwa. Hivyo ndivyo yatakavyofanywa kufanana zaidi na kielelezo kitakatifu; na “amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zetu katika Kristo Yesu,” (Wafilipi 4:7). KN 174.1

Baba, au, wakati asipokuwako nyumbani, mama, angefanya maombi, kwa kuchagua fungu la Biblia zuri na jepesi kufanamika. Ibada hii iwe fupi. Sura ndefu ikisomwa na sala ndefu ikiombwa, ibada hii hufanywa kuwa ya kuchosha, na kumfanya mtu aone ni heri kuufikia mwisho wa haya maombi. Mungu hatukuzwi saa ya maombi inapofanywa kuwa lsiyopendeza na ya kuchosha, ikiwa ya taabu na isiyo na mambo ya kupendeza, hata kuwafanya watoto waichukie. KN 174.2

Enyi baba na mama, fanyeni saa ya maombi kuwa ya kupendeza sana. Hakuna sababu ya kuifanya saa hii isiwe nzuri na yenye kupendeza ya siku nzima. Matayarisho kidogo ya saa hii yatawawezesha kuifanya iwe ya kupendeza kabisa na yenye faida. Kila wakati ibada hii iwe na mambo mbalimbali. Maswali huweza kuulizwa juu ya fungu la Biblia lililosomwa, na maelezo mazuri machache yaweza kutolewa. Wimbo wa kumsifu Mungu waweza kuimbwa. Sala iombwayo iwe fupi na yenye kusudi maalumu. Kwa maneno mepesi ya uaminifu mwenye kuongoza maombi msifii Mungu kwa wema wake na kumwomba msaada. Ikiwezekana, waachieni watoto nafasi kushiriki katika kusoma na kusali. KN 174.3

Milele peke yake ndiyo itakayodhihirisha faida iletwayo na saa hizi za maombi. 3 

Sura Ya 27 - Mambo ya Fedha Nyumbani

BWANA anapenda watu wake wawe wenye akili na uangalifu. Angependa wajifunze kuzuia upotevu wa fedha katika kila jambo, wasipoteze cho chote. Yawapasa kujua wakati wa kujiwekea akiba na wakati wa kutumia. Isipokuwa tunajikana nafsi na kuchukua msalaba, hatuwezi kuwa wafuasi wa Kristo. Tungepaswa kuona mambo yanayolazimu na kuyalipia malipo kamili kadin tuendeleavyo; iweni waangalifu wa mambo maaogo madogo; lipeni fedha mnayowiwa bila kukawia, na kujua kile kilicho halali yenu wenyewe. Yawapasa kuhesabu fedha ndogo ndogo zinazotumiwa tu kwa tamaa na kuongeza tamaa mbaya, na uteuzi wa chakula bure. Fedha inayotumiwa kwa vyakula vitamu visivyo na faida ingeweza kutumiwa kuongezea starehe na manufaa ya maana nyumbani mwenu. Si lazima kuwa bahili; yakupasa kuwa mwaminifu nafsini mwako na kwa ndugu zako. Ubahili ni jambo lisilo la haki kwa vipaji vya Mungu. Upotevu wa mali (Kuitapanya) ni vibaya pia. Fedha ndogo ndogo inayotoka ambayo wadhani haina maana kutaja huwa kitu kikubwa mwishowe. KN 175.1

Unaposhawishiwa kutumia fedha kwa vitu vidogo vidogo vya mapambo, ungekumbuka kujikana nafsi na kujinyima jinsi ambavyo Kristo alistahimili ili awaokoe wanadamu walioanguka dhambini. Yawapasa watoto wetu kufundishwa kujinyima na kuitawala tamaa. Sababu ya watu wengi kuona kuwa wana shida katika mambo ni kwamba nawaziwekei masharti tamaa zao, tamaa za chakula na maelekeoyao. Kinachowafanya watu wengi kufilisika na kuiba mali ni kutamta kuzitimiza tamaa zipitazo kiasi za wake zao na watoto wao. Yawapasa akina baba na akina mama kuwa waangalifu kama nini kuwafundisha watoto wao uwekevu kwa maneno na kwa kielelezo pia! KN 175.2

Si jambo zuri kujidai kuwa tajiri, au kuwa na hali yo yote ambayo kwa kweli hatuna-wafuasi wanyenyekevu wa Mwokozi mpole na mnyenyekevu wa moyo. Tusiudhike moyoni kama majirani zetu wakijenga na kutegemeza nyumba zao vizuri kwa njia tusiyoweza kufuata. Yambidi Yesu kutazama namna gani riziki za wale wenye kujipendeza nafsi wenyewe bila kujali wengine kwa tamaa ya chakula, kuwapendeza wageni wetu, ama kuridhisha tamaa zetu wenyewe bila kujizuia! Ni mtego kwetu kukusudia kufanya fahari au kuwaacha watoto wetu, waho chini ya mamlaka yetu, kufanya hivyo. 1 KN 175.3

Cho chote kiwezacho kutumiwa kisitupwe. Kufanya hivi kunadai busara, na kufikiri kwanza, na uangalifu wa daima. Nimeonyeshwa kuwa kutoweza kujiwekea akiba, katika vitu vidogo vidogo, ni sababu ya jamaa wengi kuumia kwa kukosa riziki za maisha. 2

“Msiwiwe na Mtu Cho Chote”

Watu wengi walio maskini ni maskini kwa sababu hutumia fedha zao mara tu wazipatapo. Kuchukua na kutumia fedha kwa kusudi lo lote, kabla ya Kustahili kuipata kwa kazi, ni mtego. 3 KN 176.1

Ulimwengu una haki kutazamia uaminifu kabisa kwa wale wanaodai kuwa ni Wakristo wa Biblia. Kwa kutojali kwa mtu mmoja kulipa haki yake apaswavyo watu wetu wote wamo katika hatari ya kunesabiwa kuwa si waaminifu. Wale wanaojidai kwa hali yo yote kuwa wenye utauwa, yawapasa kujivika mafundisho wanayoyakiri, wala wasitoe nafasi kwa Neno la Mungu kutukanwa kwa sababu ya mwenendo wao wa kutojali. Mtume asema, “Msiwiwe na mtu cho chote.” 4 KN 176.2

Wengi, naam, wengi sana, hawajajifunza kwamba wanaweza kupunguza gharama ya matumizi yao isizidi mapato yao. Hawajifunzi kuchukuliana na hali ya mambo yalivyo, nao hukopakopa na kulemewa na madeni, hatimaye hukata tamaa na kuvunjika moyo. 5 KN 176.3

Yawapasa kuona kuwa mtu hayafanyi mambo yake kwa njia itakayomwingiza katika deni. Mtu akiwa na deni, yuko katika mmojawapo wa mitego ya Shetani, anayotumia kuzitega roho za watu. Kusudia kutokuwa na deni hata kidogo. Jinyime vitu elfu kuliko kuingia deni. Epukana na deni kama ungaliepukana na ugonjwa wa ndui. 6

Kutojali Vitu vya Lazima Si Uwekaji Akiba

Mungu hatukuzwi mwili unapoachwa kwa uzembe, au kutotunzwa, hata usifae kwa kazi ya Mungu. Kuutunza mwili kwa kuupatia chakula cha kuulisha na kuutia nguvu ni mojawapo ya kazi za kwanza za mwenye nyumba. Afadhali kuwa na nguo na vyombo visivyo vya bei kubwa kuliko kujinyima chakula. Watu wengine hupunguza vyakula vya watu wa nyumbani ili kuweza kuwakaribisha wageni kwa njia ya kitajiri. Hii si busara. Katika kuwakaribisha wageni pasiwepo anasa. Mahitaji ya watu wa nyumbani yaangaliwe kwanza. Uwekevu usio na maana na desturi za kubunibuni tu mara nyingi huzuia ukarimu unapotakiwa na ambapo ungekuwa mbaraka. Kiasi cha chakula mezani mwetu kingekuwa cha kutosha ili hata akifika mgeni asiyetazamiwa aweze kukaribishwa pasipo kumtwisha mama mwenye nyumba mzigo wa kupika kingine. 7 KN 176.5

Uwekaji akiba siyo uchoyo, bali kutumia mali kwa akili kwa sababu kuna kazi kubwa ya kufanywa. Mungu hataki watu wake wajinyime kile ambacho ni lazima kwa afya na raha yao, lakini hapendezwi na upotevu wa mali, gharama kubwa kupita kiasi, ama kufanya ufahari. 8 KN 177.1

Wajibu wa Wazazi Katika Kuwafundisha Watoto

Wafundishe watoto wako kuwa Mungu anadai kwa haki vyote walivyo navyo, na ya kwamba hakuna cho chote kiwezacho kulifuta dai hili; vyote walivyo navyo ni mali waliyodhaminiwa tu, ili kuhakikisha kama watakuwa watiifu. Fedha ni mali itakikanayo; basi, isitapanywe ovyo kwa wale wasioihitaji. Kuna mwenye haja ya vipaji vyako vya ukarimu. Kama u mharibif’u wa mali, punguza gharama za kupita kiasi maishani mara moja. Usipofanya hivi, utafilisika milele. 9 KN 177.2

Vijana wa siku hizi hudharau kujiwekea akiba nao huchanganya neno hili na ubahili na choyo. Lakini kujiwekea akiba hupatana na maoni ya akili nyingi na ya ukarimu; hapawezi kuwako ukarimu wa kweli bila ya uwekaji akiba. Mtu awaye yote asidhani kuwa hahitaji kujifunza kuweka akiba kwa njia zilizo bora za kutunza sehemu ndogo ndogo za mali. 10 KN 177.3

Basi kila kijana na kila mtoto afundishwe siyo kushinda shida za kuwaziwa tu, bali kuandika hesabu sahihi za mapato na matumizi yake mwenyewe. Ajifunze matumizi halali ya feaha kwa kuitumia. Wakipewa fedha na wazazi wao au wakiipata kwa kufanya kazi wao wenyewe, wavulana na wasichana na wajifunze kuchagua na kununua nguo zao wenyewe, vitabu vyao na mahitaji yao mengine; na kwa kuandika hesabu ya gharama zao, watajifunza kwa njia bora zaidi ya yo yote nyingine, thamani na matumizi ya pesa. 11 KN 177.4

Kuna jambo kama lile la kuwapa msaada watoto wetu bila kutumia akili. Wale wanaojilipia gnarama katika vyuo vikuu huthamini majaliwa waliyo nayo zaidi ya wale wanaolipiwa gharama na mtu mwingine, maana hujua inavyowagharamu. Tusibebe mzigo wa watoto wetu kupita kiasi hata kuwafanya wasiweze kujisaidia wenyewe. Wazazi nufanya kosa wanapotoa tu fedha kumpa kijana ye vote mwenye nguvu za kusudi aingie masomoni apate kuwa mhubiri au mganga kabla hajajua kazi ya juhudi iliyo na manufaa. 12 KN 177.5

Mazoea ya anasa au mke na mama kukosa kuumia akili huenda ikawa sababu ya upotevu wa mali; lakini mama huyo pengine hudhani kwamba afanya vizuri awezavyo kwa sababu nakufundishwa kutopoteza fedha kwa mahitaji yake au mahitaji ya watoto wake, naye hana ujuzi wala maarifa ya mambo ya nyumbani. Hivyo nyumba moja yaweza kuhitaji msaada maradufu ya ule ambao ungetosha jamaa nyingine kubwa sawa na hiyo. Mungu amependezwa kunionyesha maovu yaletwayo na mazoea mabaya ya kuponda mali, kusudi nipate kuwaonya wazazi kuwafundisha watoto wao kujiwekea akiba. Wafundisheni kuwa fedha inayotumiwa kwa kile wasichohitaji hasa imetumiwa kwa upotevu. 13 

Mashauri Mema kwa Waume na Wake Juu ya Mambo ya Fedha

Yawapasa wote kujifunza kuandika hesabu za fedha. Wengine huidharau kazi hii na kuhesabu kama haina maana, lakini kufanya hivi ni kosa. Gharama zote zingeelezwa kwa usahihi. 14 KN 178.1

Pengine leo ungeweza kuwa na akiba ya mali ya kutumia kwa hatari au matukio ya ghafula, na kusaidia kazi ya Mungu, ikiwa ungetumia fedha kiasi ikupasavyo. Kila juma sehemu ya mshahara wako ingewekwa akiba na kwa hali iwayo yote isiguswe isipokuwa kama ikibidi kwa sababu ya kuumia, au kumrudishia Mtoaji k’wa njia ya sadaka kwa Mungu. Fedha uliyojipatia kwa kazi haijatumiwa kwa busara na kwa kiasi ili kuacha akiba ya kukusaidia iwapo utapatwa na ugonjwa jamaa yako isije ikakosa pesa za matumizi unazoleta kuwasaidia. Yawapasa jamaa yako kuwa na kitu cha kutegemea kama ukiingia katika shida. 15 KN 178.2

Yawapasa kusaidiana. Usidhani kwamba kubania mfuko, na kukataa kumpa mkeo pesa ni sifa njema. Ni vizuri kumpatia mkeo kiasi fulani cha fedha kila juma na kumwacha afanye apendavyo na fedha hiyo. Hujampa nafasi kutumia busara yake au akili yake kwa sababu hujafahamu vizuri cheo apaswacho mkeo kuwa nacho. Mkeo ana akili bora na timamu. Mpe mkeo sehemu ya pesa upatazo. Mwache achukue hizo ziwe mali yake mwenyewe, na kuzitumia kama apendavyo. Yapasa aruhusiwe Kutumia mali anazojipatia kwa kazi yake kama aonavyo mwenyewe kwamba yafaa. Kama angekuwa na kiasi fulani cha fedna ya kutumia jinsi apendavyo mwenyewe, bila kulaumiwa. angepunguziwa mzigo mzito unaomlemea mawazoni mwake. 16 KN 178.3

Sura ya 28 - Kazi za Familia Wakati wa Likizo na Sikukuu

NALIONA kuwa likizo zetu zisingetumiwa kama zile za walimwengu, walakini zisingekosa kujaliwa, maana hili halitawapendeza watoto wetu. Katika siku hizi zenye uwezekano wa kuwahatarisha watoto wetu kwa mivuto mibaya na kuharibiwa na anasa na starehe za dunia, hebu wazazi watafute kwa bidii kupata kitu kingine badala ya hiyo michezo na starehe zenye hatari zaidi. Wafahamisheni watoto wenu kwamba mnawatakia mema na furaha. KN 179.1

Kwa kuadhimisha likizo walimwengu na watu wa kanisa wamefundishwa kusadiki kuwa siku hizi za kujikalia kivivu, bila kufanya kazi ni za lazima kwa afya na raha, lakini matokeo yake huonyesha kuwa zimejaa uovu. Tumejaribu sana kuzifanya siku za likizo ziwe zenye kupendeza iwezekanavyo kwa vijana na watoto, huku tukibadili kidogo utaratibu wa mambo. Kusudi letu liwe kuwaepusha na anasa zinazoonekana miongoni mwa wale wasioamini. KN 179.2

Baada ya siku ya kujipendeza kwa anasa, wapi kuridhika kwa mwenye kupenda anasa? Kama watenda kazi Wakristo, ni nani waliyemsaidia kupata maisha bora zaidi, na sifa zaidi? Wangeweza kuona nini ikiwa wangetazama habari ambazo malaika ameziandika? Siku hiyo haina faida kazini mwa Kristo, kwa sababu hakuna jema lo lote walilotenda. Wanaweza kuwa na siku zingine lakini si hiyo tena ambayo imepishwa kwa mazungumzo yasiyo na maana, ya kijinga, ya wasichana na wavulana, na wavulana na wasichana. KN 179.3

Kamwe nafasi hizo hazitapatikana tena. Afadhali kama wangefanya kazi ngumu ya juhudi katika likizo hiyo. Maana hawakuitumia vizuri likizo yao nayo imepita milele kuwakabili hukumuni kama siku isiyotumiwa kwa faida. KN 179.4

Kuifanya Kazi ya Mungu Kuwa Jambo la Kwanza

Je, si vizuri tukitumia likizo kwa mambo ya Mungu, tuwezapo kuamsha mafikara yetu na kukumbuka jinsi anavyotutendea? Je, halitakuwa jambo zuri kuifikiri mibaraka yake ya wakati uliopita, na kuyakumbuka maonyo ya ajabu yaliyotuingia nafsini mwetu hata tusiweze tena kumsahau Mungu? KN 179.5

Walimwengu wana sikukuu na likizo nyingi, na watu hushughulika na michezo, mashindano ya farasi, kucheza kamari, kuvuta tumbako, na ulevi. KN 180.1

Je, watu wa Mungu wasiwe na mikutano mitakatifu mara nyingi ambapo wanaweza kumshukuru Mungu kwa mibaraka yake mikubwa? KN 180.2

Twahitaji kanisani watu wenye uwezo kuleta katika mipango ya mambo na wenye kutoa kazi za kufaa kwa vijana wa kiume na wa kike za kupunguza mahitaji ya wanadamu na kutumikia wokovu wa roho za wanaume, wanawake, vijana, na watoto. Haitawezekana kwa wote kutoa wakati wao wote kwa kazi hii kwa sababu ya kazi ngumu wapaswayo kufanya kujipatia riziki zao za kila siku. Walakini hao nao wanazo likizo na sikukuu zao ambazo huweza kuzitumia kwa kazi ya Kikristo na kusaidia kwa njia hii, kama wasipoweza kutoa sehemu kubwa ya mali zao. KN 180.3

Ukipata likizo au sikukuu ifanye iwe siku nzuri ya furaha kwa watoto wako, pia ifanye siku ya kuwapendeza maskini na wenye taabu. Usiache siku hiyo ikapita bila kumletea Yesu shukrani na sadaka. KN 180.4

Siku Kuu za Kuzaliwa-wakati wa Kumsifu Mungu

Katika mfumo wa Kiyahudi kuhusu kuzaliwa kwa watoto sadaka ilitolewa kwa Mungu, kwa agizo lake Mwenyewe. Sasa twaona wazazi wakijisumbua hasa kuwapa zawadi watoto wao katika siku kuu za kuzaliwa kwao. Wanaufanya huu kuwa wakati wa kumtukuza mtoto, kana kwamba mtu ndiye mwenye kustahili sifa. Shetani amepata nafasi katika mambo haya; amezipotosha akili za moyoni na vipaji kwa wanadamu; hivyo mawazo ya watoto yamepotoshwa kujifikiri wenyewe, kana kwamba wao ndio watu wa kusherehekewa hasa. KN 180.5

Katika sikukuu za kuzaliwa watoto wangefundishwa kwamba wana sababu ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya wema wake katika kuyalinda maisha yao mwaka mwingine. Mafundisho ya thamani yaweza kutolewa kwa njia hii. Kwa ajili ya maisha, afya, chakula, na mavazi na kwa ajili ya matumaini ya uzima wa milele pia, tunawiwa na Mtoaji wa vipaji vyote vya rehema; na Mungu ana haki kupewa shukrani na sadaka zetu za shukrani kwa alivyotukirimia. Sadaka hizi za siku kuu ya kuzaliwa humpendeza Mungu. KN 180.6

Wafundishe kuyakumbuka mambo ya mwaka uliopita wa maisha yao, wafikiri kama wangependezwa kukutana na habari zake kama zilivyo vitabuni mbinguni. Wasaidie mawazoni wafikiri kama tabia yao, maneno yao, matendo yao, ni yenye kumpendeza Mungu. Je, wameyafanya maisha yao yapate kufanana zaidi na yale ya Yesu, mazuri na yenye kupendeza machoni pa Mungu? Wafundishe kumjua Mungu, njia zake na maagizo yake. KN 181.1

Nimekwisha kuwaambia watu wa nyumbani mwangu na marafiki zangu, ningependa asiwepo mtu awaye yote anayenipa zawadi ya siku ya kuzaliwa kwangu au zawadi ya sikukuu ya kuzaliwa kwake Kristo (Chrismas), isipokuwa ananiruhusu kuipitisha ipate kuingia katika hazina ya Bwana, ikatumike kuendesha kazi ya utume. 1

Sura Ya 29 - Maburudisho

IKO tofauti kubwa baina ya maburudisho na mazungumzo, maongezi ama michezo ya kujifurahisha tu. Maburudisho maana yake hasa ni kutia nguvu na kujenga. Hutusahaulisha kidogo kazi na shughuli zetu za kawaida, na kuburudisha akili na mwili, na kwa hivyo kutuwezesha kuzirudia kazi zetu tukiwa na nguvu mpya za kufanya kazi ya maisha kwa uaminifu. Ambapo mazungumuzo, maongezi ama michezo ya kujifurahisha tu ni kutafuta anasa, na mara nyingi inafulilizwa kupita kiasi; inatumia nguvu kupita kiasi; nguvu ambazo zinahitajika kwa kazi ya manufaa, na hivyo mwisho wake ni kuyapinga mafanikio halisi ya maisha” - Ed. 207. KN 182.1

Wakristo wana njia nyingi za kupatia furaha, nao huweza kusema kwa usahihi furaha zilizo halali na nzuri. Wanaweza kufaidi maburudisho ikiwa hayatapoteza akili wala kuharibu roho ya mtu, kama vile kukatisha tamaa na kuhuzunisha baadaye na kuharibu kujistahi nafsi au kuzuia njia ya manufaa. Kama wakimchukua Yesu pamoja nao na kuwa na moyo wa kumwomba Mungu kwa bidii, na salama kabisa. KN 182.2

Maburudisho yo yote ambayo waweza kuyashiriki na kuomba mbaraka wa Mungu juu yake kwa imani hayawezi kuwa yenye hatari. Lakini maburudisho (starehe) yo yote ambayo hukukosesna sala ya faragha, kwa ajili ya ibada ya wakfu wa mahali pa kuombea, au kushiriki kwenye mkutano wa maombi si salama, bali ni yenye hatari. KN 182.3

Sisi tu jamii ya wale wanaosadiki kwamba ni bahati yetu kila siku ya maisha yetu kumtukuza Mungu duniani, na ya kwamba haitupasi kuishi ulimwenguni humu kwa kujipendeza tu kwa anasa. Tuko hapa kuwanufaisha wanadamu na kuwa mbaraka kwa watu mtaani; tukiyaacha mawazo yetu kufuata njia ile mbaya ambayo wengi wanaotafuta ubatili na upuzi huyaacha mawazo yao kuifuata, twawezaje kuwanufaisha watu wa taifa letu na wa kizazi chetu? Twawezaje kuwa mbaraka kwa watu wanaotuzunguka? Tu wenve hatia kama tukijifurahisha kwa anasa yo yote itakayotufanya tusifae kwa kazi zingine zaidi za dini. Yako mambo mengi ambayo venyewe ni halali, lakini yaishapo hugeuzwa vibaya na Shetani, kuwa mtego kwa wale wasiojihadhari. KN 182.4

Kuna haia kubwa ya kuwa na kiasi katika starehe, na katika mambo yote mengine. Na hali ya mambo haya ingefikiriwa vizuri kwa uangalifu. Kila kijana apaswa kujiuliza, je, starehe hizi zitakuwa na mvuto gani katika afya ya mwili, akili, na kwenye tabia ya moyoni? Je, akili zangu zitapumbazwa hata kumsahau Mungu? Je, nitapotewa na utukufu wake? 1 KN 182.5

Ni bahati njema na wajibu wa Wakristo kujaribu kuziburudisha roho zao na kuitia nguvu yao kwa maburudisho halali, wakiwa na kusudi la kutumia uwezo wao wa mwili na akili kwa utukufu wake Mungu. Maburudisho yetu hayapaswi kuwa kujifurahisha na vicheko vya ovyo, visivyo na maana, vya upuzi. Hatuwezi kuyafanya kwa njia itakayowanufaisha na kuwainua wale tunaoshirikiana nao, na kutuwezesha kufaulu zaidi kwenye kazi zitupasazo kama Wakristo? 2 KN 183.1

Wakati unaotumiwa katika mazoezi ya kufaa ya viungo vyote vya mwili ni faradhi kwa kazi bora za kila kimoja. Ubongo ukichoshwa daima huku viungo vingine vya mashine hii yenye uhai visipofanya kazi, huwapo upotevu wa nguvu, mwilini na akilini. Mwili hunyang’anywa siha yake, akili hupotewa na nguvu zake, na mwishowe huleta fadhaa. KN 183.2

Wale wanaoshughulika sana na masomo wangekuwa na pumziko (ama michezo). Akili hazitaki kufikirishwa daima, kwa lcuwa mashine hii ndogo ya kichwani huchoka. Mwili na akili pia havina budi kupata mazoezi. 3

Maburudisho Yawezayo Kuwapendeza Matajiri na Maskini Pia

Vijana hawawezi kufanywa kuwa watulivu na wazito kama wazee, au mtoto afanywe mwenye busara wala mtaratibu kama bwana. Huku anasa za dhambi zikilaumiwa, kama ipasavyo, hebu wazazi, walimu na walezi wa vijana wawapatie badala yake furaha za halali ambazo hazitaharibu tabia za uadilifu. Msiwalazimishe vijana kutii amri kali ambazo zitawafanya wajione kuwa wanadhulumiwa hata iwafanye kuasi na kuzifuata njia za upotovu. Kwa mkono imara, mpole, na wa huruma shikeni madaraka mkiongoza na kuzitawala akili na makusudi:yao, walakini kwa upole, kwa busara, kwa upendo, ili wajue kuwa mnawafikiria na mnawatakia mema. 4 KN 183.4

Ziko namna za maburudisho ambazo zina faida kubwa akilini na mwilini pia. Akili yenye busara itapata njia ya kufurahi na mwilini pia. Akili yenye busara itapata njia ya kufurahishwa na kupumzishwa, siyo katika mambo yaliyo halali tu, bali yanayovutia pia. Michezo ya nje, kuzitafakari kazi za Mungu katika viumbe vya asili, yatakuwa mambo ya faida kabisa. 5 KN 183.5

Hakuna maburudisho yatakayowanufaisha sana watoto na vijana kama yale yanayowafanya wawasaidie wengine, kuliko nafsi zao wenyewe. Kwa kawaida vijana ni wepesi kushauriwa. 6 KN 183.6

Mungu ameruzuku kwa ajili ya furaha ya kila mmoja kile awezacho kufaidi tajiri na maskini pia-furaha ipatikanayo kwa kukuza usafi wa mawazo na matendo ya fadhila; furaha iletwayo na kusema maneno ya huruma na kutenda matendo mema. Nuru ya Kristo hung’aa kwa wale watendao huduma ya namna hii ili kuyatia nuru maisha yaliyotiwa giza na huzuni nyingi. 7 KN 184.1

Kuna mambo mengi ya muhimu, na manufaa yapasayo kutendwa ulimwenguni humu ambayo yangeifanya michezo ya kujifurahisha isilazimu sana. Ubongo, mifupa na misuli vitaimarika na kupata nguvu kwa kutumika kwa kusudi la kufanya mema, kufikiri sana, na kufanya mashauri kwa akili ambako kutavizoezesha viungo hivyo kuwa na uwezo wa akili na nguvu za mwilini zitakazotumika kwa manufaa ya talanta walizopewa na Mungu ambazo kwazo vyaweza kumtukuza Mungu. 8 KN 184.2

Sikatazi mazoezi mepesi ya kucheza mpira; lakini haya, ijapokuwa yawe mepesi pengine huwa ya kuchosna. KN 184.3

Naogopa siku zote matokeo ambayo hufuata mara baada ya hiyo michezo. Huleta matumizi ya fedha ambayo ingetumiwa kuwaletea nuru ya ukweli watu wanaopotea nje ya Kristo. Anasa na matumizi ya mali kwa kujipendeza nafsi mwenyewe, ambayo hupeleka kidogo kidogo kwenye kujitukuza, na kujizoeza katika michezo hii kwa ajili ya raha ama anasa tu huleta upendo na tamaa ya mambo yasiyofaa katika tabia kamilifu ya Mkristo. 9 

Urafiki na Mazoea Mema

Vijana wanaotupwa au kuachwa kwenye jamii wao kwa wao huweza kufanya urafiki wao kuwa mbaraka au laana. Huweza kuadilisha, kuneemesha, na kutiana nguvu, kuendelea vizuri katika mwenendo, katika tabia, katika maarifa; au, kwa kukubali kuwa wazembe na kutokuwa waaminifu, waweza kutoa tu mvuto wa upotevu. KN 184.5

Yesu atakuwa msaada wa wote wanaomtumainia. Wale wenye uhusiano na Kristo wanaweza kufurahi wapendavyo. Huifuata njia ambayo mwokozi huwaongoza, kwa ajili yake kuisulibisha nafsi pamoja na anasa na tamaa mbaya za mwili. Watu hao wanayo matumaini juu ya Kristo, na dhoruba za dunia hazina nguvu kuwaondoa kwenye msingi imara. KN 184.6

Ni juu yenu, vijana wa kiume na wa kike kama mkipenda kuwa watu wa kuamimwa, wema na wa kufaa hasa. Yafaa mwe tayari na kukusudia kusimama imara kuitetea kweli kwa hali iwayo yote. Mazoea yetu mabaya hayawezi kutwaliwa mbinguni pamoja nasi, na tusipoyashinda hapa, yatatufungia nje ya makao ya wenye haki. Mazoea mabaya yakipingwa, yatakuwa na ugumu; lakini kama vita ikifululizwa kwa nguvu na bidii, yanaweza kushindwa. KN 184.7

Ili kuwa na mazoea mema, yatupasa kutafuta marafiki wenye tabia ya uadilifu na mvuto wa dini. 10 KN 184.8

Ikiwa vijana wangeweza kuvutwa kufanya urafiki na kuwa waangalifu na wenye tabia nzuri, matokeo yangekuwa mazuri sana. Kama ukifanywa uchaguzi wa marafiki wamchao Bwana, mvuto huo utaongoza katika ukweli, wajibu, na utakatifu. Maisha ya Kikristo ni uwezo kwa mema. Lakini, kwa upande mwingine, wale wafanyao urafiki na wanaume na wanawake wenye tabia za mashaka watakuwa wenye mashaka pia; mwenye kuchagua marafiki waovu bila shaka atakuwa mwovu. Kwenda katika shauri la wasio haki ni hatua ya kwanza kabla ya kusimama katika njia ya wakosaji na kuketi barazani pa wenye mizaha. KN 185.1

Hebu wote wapendao kufanya tabia njema wachague marafiki wenye akili na busara na ambao hupenda mambo ya dini. Wale ambao wamehesabu gharama wanaotaka kujenga kwa ajili ya uzima wa milele wanapaswa kutia vifaa bora kwenye jengo lao. Kama wakikubali mbao zilizooza, kama wakiridhika na upungufu wa tabia, jengo litaangamia. Watu waangalie jinsi wajengavyo. Dhoruba ya majaribu italipitia jengo hilo, na kama halikujengwa imara na kwa uaminifu halitasahimili jaribio. KN 185.2

Sifa njema ni yenye thamani kushinda dhahabu. Vijana wanayo maelekeo ya kushirikiana na wale wenye nia na tabia mbaya. Ni furaha gani hasa kijana awezayo kuitazamia kwa kujiunga kwa hiari yake na watu wenye mawazo, maoni, na mwenendo mbovu, usio na maana? Wengine wamepotoka kwa tamaa na ni wenye mazoea mabaya, na wote wachaguao marafiki wa namna hii watakifuatta kielelezo chao. 11 KN 185.3

Pengine huwezi kuona hatari hasa katika kuchukua hatua ya kwanza ya upuzi na kujitafutia anasa nawe wafikiri kuwa utakapotaka kubadili mwenendo wako, utaweza kufanya mema kwa urahisi tu kama ilivyokuwa zamani kabla hujashindwa na mabaya. Lakini hili ni kosa. Kwa kuchagua rafiki wabaya wengi wamepotoshwa hatua kwa hatua kuiacha njia ya sifa njema na kuingizwa katika kutokutii na upotevuni, ambapo wakati mwingine waweza kuzama ndani yake. 12 KN 185.4

Msidhani kwamba Mungu anataka tuache kila kitu ambacho ni cha maana kwa raha yetu hapa. Atakacho tukiache ni kile ambacho hakitatunufaisha wala kuidumisha furaha yetu. 13 Pumziko Kamili na Kujifurahisha KN 185.5

Vijana wangekumbuka kuwa wanapaswa kutoa habari za majaliwa yote ambayo wamefaidi, na kwa kutumia kwa faida wakati wao, na kwa kutumia vizuri uwezo wao. Pengine watauliza, Je, tusiwe na michezo wala maburudisho? Tufanye kazi tu kila mara bila kuwa na badiliko? 14 KN 185.6

Kubadili kazi ya juhudi ambayo imezitumikisha nguvu za mwili kupita kiasi pengine italazimu sana kwa muda, ili wapate kushughulika tena na kazi kwa bidii na kufaulu vizuri zaidi. KN 185.7

Lakini kupumzika kabisa huenda hakutalazimu au hata hakutakuwa na matokeo mazuri baadaye kwa habari za nguvu zao za mwilini. Hawana sababu, hata wakichoka na kazi ya aina moja, kupoteza bure dakika zao zenye thamani. Pengine watataka kufanya kitu kingine ambacho hakiwachoshi hivyo, lakini kitakachowaletea mama na dada zao furaha. Katika kuyapunguza masumbuko yao kwa kujitwika wenyewe mizigo migumu kabisa wapaswayo kuibeba, wataweza kupata maburudisho ambayo hutokana na tabia na ambayo yatawapa furaha kamili, na wakati wao hautakuwa wa kupotezwa bure kwa mambo yasiyo na maana wala kwa kujipendeza nafsi wenyewe, kwa anasa. Wakati wao daima waweza kutumiwa kwa faida, wakiburudishwa kwa mambo mbalimbali, huku wakiukomboa wakati kusudi kila dakika iwe na faida kwa mtu fulani. 15 KN 186.1

Wengi hudai kwamba inalazimu kwa ajili ya kuhifadhi afya ya mwili kujifurahisha kwa machezo. Ni kweli kwamba kubadili kunatakikana kwa faida ya maendeleo ya mwili, maana akili na mwili huburudishwa na kutiwa nguvu na badiliko; lakini kusudi hili halitimizwi kwa kujifurahisha kwa anasa zisizo na maana, kwa kuacha kazi za kila siku ambazo vijana wangetakiwa kuzitenda. 16 KN 186.2

Jumba la maonyesho (theater) ni mojawapo ya mahali penye hatari sana pa anasa. Badala ya kuwa shule ya tabia ya uadilifu na sifa njema kama inavyosemekana kila mara, ni mahali pa maovu hasa. Maozoea mabaya na mwelekeo wa dhambi hutiwa nguvu na kuimarishwa kwa michezo hiyo. Nyimbo za ovyo, ufisadi wa matendo, maneno, na moyo huharibu akili na kushusha tabia. Kila kijana mwenye mazoea ya kwenda mahali pa maonyesho ya jinsi hii ataharibika tabia. Hakuna mvuto nchini mwetu wenye nguvu kutia akili sumu, kuharibu maoni ya ndani, na kupunguza nguvu za kupendezwa na starehe na utulivu halisi wa maisha zaidi ya michezo ya sinema. Kuyapenda mambo haya huzidisha kila anasa sawa na tamaa ya kileo inavyotiwa nguvu kwa kukitumia. Njia tu ya salama ni kuepukana na jumba la maonyesho(theater), kiwanja cha tamsha, na kila pahali pa machezo hiyo isiyofaa. 17 KN 186.3

Kucheza kwa Daudi kwa moyo wa kicho mbele za Mungu kumetajwa na wale wapendao anasa, lakini hoja ya namna hii haina maana. Siku hizi kucheza dansi kumeungana na upuzi na kujifurahisha usiku wa manane. Afya na tabia ya uadilifu hutupwa makusudi kujifurahisha na anasa. Kwa wazoefu wa chumba cha dansi Mungu siye awazwaye wala kuheshimiwa; maombi au nyimbo za kumsifu Mungu zingeonekana kuwa hazifai kwenye ngoma zao. Yapasa jaribio hili liwe la kukata maneno. Michezo ambayo huelekea kudhoofisha upendo wa mambo matakatifu na kupunguza furaha yetu kazini mwa Mungu haifai kutafutwa na Wakristo. Muziki na kucheza kwa furaha na kumsifu Mungu wakati wa kuhamisha sanduku la agano haukuwa na namna yo yote ya ufisadi wa dansi ya siku hizi. Ile ilikusudiwa kwa ukumbusho wa Mungu na kulitukuza jina lake takatifu. Lakini hii ya siku hizi ni hila ya Shetani kuwafanya watu wamsahau Mungu na kumdharau. 18 KN 186.4

Vijana kwa kawaida huenenda kama kwamba saa za thamani kuu za muda wa majaribio kama wanafaa au hawafai, pindi wakati rehema ikiendelea, ni sikukuu kubwa walizoruhusiwa kupumzika, nao wamewekwa ulimwenguni humu kwa michezo yao wenyewe na kujifurahisha kwa anasa daima. Shetani amekuwa akijitahidi kuwaongoza kutafuta furaha katika michezo ya kidunia na kujihalalisha kwa kujaribu kuonyesha kuwa michezo hiyo haina madnara, ni safi, halali, tena yenye maana kwa afya. 19 KN 187.1

Wengi wanashiriki sana micnezo ya kidunia, inayoharibu tabia ambayo Neno la Mungu laikataza. Hivyo hufarakana na Mungu na kujiweka pamoja na wale wapendao anasa za dunia. Dhambi zile zilizowaangamiza watu walioshi zamani kabla ya gharika na ile miji ya uwandani zaonekana siku hizi-siyo katika nchi za washenzi tu, wala siyo miongoni mwa wafuasi wa madhehebu ya dini ya Kikristo ipendwayo na wengi, bali miongoni mwa wale wanaokiri kuwa wanatazamia kuja kwa Mwana wa Adamu. Ikiwa Mungu angeziweka dhambi hizi mbele yako kama zionekanavyo machoni mwake, ungejawa na aibu na hofu. 20 KN 187.2

Tamaa ya tamasha na michezo ya kupendeza ni jaribu na mtego kwa watu wa Mungu na hasa kwa vijana. Shetani hutayarisha daima vishawishi kuivuta mioyo ipotoke na kuacha kazi takatifu ya matayarisho ya mambo ambayo hayako mbali, wakati ujao. Kwa njia ya watu wapendao anasa za dunia huyadumisha mambo ya kusisimua ili kuwashawishi wale wasiojihadhari kushiriki anasa za dunia. Pana maonyesho, hotuba, na michezo mbalimbali isiyo na mwisho ambayo imekusudiwa kuwaongoza watu kuipenda dunia; na kwa njia ya ushirika huu na walimwengu imani hudhoofishwa. KN 187.3

Mungu hamhesabu mwenye kutafuta anasa kama yu mfuasi wake. Wale tu wanaojikana nafsi wenyewe, wenye kiasi, unyenyekevu, na utakatifu maishani mwao hao ndio wafuasi wa kweli wa Yesu. Hao hawawezi kufurahia mazungumzo ya ovyo, yasiyo na maana, ya wapendao anasa za dunia. 21 KN 187.4

Kama kwa kweli u mtu wa Kristo, utakuwa na nafasi kumshuhudia. Utaalikwa kuhudhuria mahali penye starehe nawe utakuwa na nafasi kumshuhudia Bwana wako. Kama u mwaminifu kwa Kristo, basi, hutajaribu kutoa udhuru kwa kukosa kufika, bali utasema wazi tena kwa makini kwamba u mtoto wa Mungu, na kanuni zinazoyaongoza maisha yako hazikuruhusu uwepo ingawa kwa safari moja mahali ambapo huwezi kumwalika Bwana wako kuwapo. 22 KN 187.5

Kutakuwako na tofauti kubwa baina ya jumuia ya wafuasi wa Kristo kwa ajili ya maburudisho na mkusanyiko wa ngoma ya kidunia kwa ajili ya anasa na michezo. Badala ya sala na kumtaja Kristo na mambo matakatifu itasikika kutoka midomoni mwa hao wapendao anasa za dunia vicheko vya ovyo na mazungumzo yasiyo na maana. Wazo lao ni kuwa na sikukuu tu. Michezo yao huanza kwa mambo ya upuzi na kumalizika kwa mambo ya ovyo, yasiyo na maana. 23

Sura Ya 30 - Njia Ziendazo Moyoni Zinazopaswa Kulindwa

YAFAA wote kuzilinda akili za kuona, ili Shetani asije akawashinda; maana hizi ndizo njia za rohoni. Itakubidi kuwa askari mlinzi aliye mwaminifu wa macho yako, masikio, na akili zako zote kama ukitaka kuutawala moyo wako na kuzuia mawazo mabaya yasiyofaa yasiuharibu moyo wako. Uwezo wa neema peke yake ndio uwezao kuitimiza kazi hii itakikanayo sana. KN 189.1

Shetani na malaika zake wana kazi nyingi za kufanya ya kupumbaza akili ili mashauri, maonyo, na makaripio yasisikiwe; au kama yakisikiwa, lakini yasilete matokeo mema moyoni na kuyaongoa maisha. 

Shetani Hawezi Kuingia Moyoni Tusipokubali

Mungu ametayarisha ili tusije tukajaribiwa kupita tuwezavyo kustahimili, lakini pamoja na kila jaribu atafanya mlango wa kutokea. Kama tukimtii Mungu kabisa, hatutakubali moyo kuyafurahia mawazo ya kujifikiri nafsi wenyewe. KN 189.3

Pakiwako na njia yo yote ambayo kwayo Shetani aweza kuingia moyoni, atapanda magugu yake na kuyafanya yaote mpaka yatakapotoa mavuno mengi. Kwa vyo vyote Shetani hawezi kuyatawala mawazo, maneno, wala matendo, kama tusipokubali wenyewe kufungua mlango na kumkaribisha. Tukimkaribisha ataingia, na kwa kuifanyia nila mbegu njema iliyokwisha kupandwa moyoni, huyafanya maneno ya kweli yasiwe na matokeo mema. KN 189.4

Si salama kwetu kuendelea kufikiri habari za manufaa yawezayo kupatikana kwa kuyakubali mashauri ya Shetani. Dhambi ni uasi na balaa kubwa ni kwa kila mtu anayejifurahisha kwayo; lakini hupofusha na kudanganya kwa hali yake, nayo itatuvuta kwa werevu. Kama tukijihatarisna mahali pa Shetam, hatuna ahadi ya kulindwa na uwezo wake. Kwa hiyo ni juu yetu kufunga kila njia ambayo kwayo mshawishi aweza kutufikia. KN 189.5

Kila Mkristo nana budi kulinda zamu daima, kuangalia kila njia ya rohoni ambamo Shetani aweza kupata upenyo. Yampasa (Mkristo) Kuomba msaada wa Mungu huku akiyapinga kwa uthabiti maelekeo vote ya dhambi. Kwa moyo, kwa imani, kwa jitihada, aweza kushinda. Lakini akumbuke kuwa ili kuupata ushindi Kristo hana budi kukaa ndani yake naye kukaa ndani ya Kristo. KN 189.6

Kila kitu kiwezacho kufanywa ili kutuweka pamoja na watoto wetu mahali ambapo hatuwezi kuyaona maovu yatendwavo ulimwenguni kingefanywa. Yatupasa kujihadhari sana na macho yetu pamoja na masikio yetu kusudi mambo hayo mabaya yasiingie mioyoni mwetu. Usijaribu kuona jinsi gani uwezavyo kutembea ukingoni mwa jabali bila kuanguka. Epukana na hatari ya kwanza kabisa unayokaribiana nayo. Mambo ya kiroho hayafai kuchezacheza nayo. Mali yako kubwa ni tabia yako. Itunze kama ambavyo ungalitunza hazina ya dhahabu. Uadilifu, kujiheshimu (kuchunga cheo), uwezo mkuu wa kupinga, havina budi kuhifadhiwa kwa nguvu siku zote. Lazima kujihadhari kila wakati; tendo moja la utani, tendo moja lisilo la akili, laweza kuihatarisha roho ya mtu, kuyafungulia majaribu, na kudhoofisha uwezo wa kuyapinga.

Sura ya 31 - Uchaguzi wa Masomo

ELIMU siyo kitu kingine ila matayarisho ya uwezo wa mwili, akili, na roho kwa ajili ya kutenda kazi zote za maisha. Uwezo wa kustahimili pamoja na nguvu na utendaji wa kazi, hupunguzwa ama kuzidishwa kwa njia ambayo hutumiwa. Yafaa akili ziongozwe kusudi uwezo wake wote ukuzwe barabara. KN 191.1

Vijana wengi wanayo tamaa ya vitabu. Wanatamani kusoma kila kitu wawezacho kupata. Yawapasa wajihadhari na kile wasomacho na kile wasikiacho pia. Maana, nimeonyeshwa kwamba wamo katika hatari kubwa kabisa kuharibiwa na masomo yasiyofaa. Shetani anazo njia elfu za kutaharakisha akili za vijana. Wamo hatarini kama wasipoangalia kila wakati. Yawapasa kuangalia sana mioyo yao, wasije wakadanganywa na majaribu ya yule adui. 1 KN 191.2

Mvuto wa Masomo Mabaya Yasiyofaa

Shetani anajua kuwa akili hupatwa sana na kile inachojilisha kwacho. Atafuta kuwaongoza vijana na wazee pia kusoma vitabu vya hadithi za uongo, na masomo mengine. Wasomaji wa vitabu vya jinsi hii huwa watu wasiofaa kwa kazi zilizowekwa mbele yao. Huishi maisha ya mashaka, na hawatamani kuyachunguza Maandiko Matakatifu, kujilisha Mana ya mbinguni. Akili inayohitaji kutiwa nguvu hudhoofishwa, na kupoteza uwezo wake wa kujifunza maneno makuu ya kweli yahusuyo utume na kazi ya Kristomaneno ya kweli ambayo yangeimarisha moyo, kuamsha akili, na kuchochea tamaa ya kushinda kama Kristo alivyoshinda. KN 191.3

Kama ingaliwezekana sehemu kubwa ya vitabu vilivyokwisha kuchapishwa kutumiwa, baa linaloogofya sana watu akilini na moyoni lingezuiwa. Hadithi za mahaba, hadithi zisizo na maana zenye kusisimua, pia hadi vitabu vya jamii ile iitwayo hadithi za riwaya za kidini vitabu ambavyo ndani yake mwandishi hutia kwenye hadithi yake fundisho la wema na ubaya-ni laana kwa wasomaji. Maneno ya dini yaweza kuchanganywa katika kitabu cha riwaya, lakini-, mara nyingi Shetani hujivika mavazi ya malaika wema, apate kudanganya zaidi. Hakuna walioimarika katika mafundisno mazuri, wala hakuna wanaosalamika majaribuni, hata wasiweze kuwa hatarini kwa kujitoa kwa uovu unaoharibu hali ya kiroho, wenye kuliita giza uzuri wa Biblia. Huanzisha fadhaa, hutia wasiwasi akilini, hudnoofisha akili za moyoni zisiweze kuwa na manufaa, huiachisha roho ya mtu maombi, na kuiharamisha kwa ibada yoyote ya kiroho. KN 191.4

Mungu amewajalia vijana wetu wengi kuwa wenye akili bora; lakini mara nyingi sana wamedhoofishwa uwezo wao, wakatatiza na kuziondolea akili zao nguvu kwa kiasi ya kwamba kwa muda wa miaka mingi hawajafanya maendeleo ya kukua katika neema au katika ufahamu wazi wa madhumuni ya imani yetu kwa ajili ya uchaguzi wao usio wa busara wa mambo wanayoyasoma. Wale wanaomtazamia Bwana kuja upesi, wenye kutazamia lile badiliko la ajabu, wakati ambapo “sharti huu uharibikao uvae kutokuharibiksa,” hawana budi wakati huu wa kuangaliwa kama twafaa au hatufai kusimama mahali pa juu zaidi katika kutenda mambo bora. KN 192.1

Rafiki wapendwa, jiulizeni nafsi zenu wenyewe juu ya mvuto wa hadithi za kutahayarisha. Je, mnaweza, baada ya masomo ya jinsi hiyo, kuifungua Biblia na kuyasoma kwa moyo maneno ya uzima? Hamwoni kuwa Kitabu cha Mungu hakiwapendezi? Mvuto wa hadithi ya mahaba uko moyoni, ukiharibu hali njema ya moyoni, na kukufanya usiweze kukaza fikra zako juu ya maneno makubwa na mazito ya kweli yenye kuihusu hali yako ya milele. KN 192.2

Kwa moyo thabiti kataa masomo yote ya ovyo. Hayatakutia nguvu rohoni mwako, bali yataingiza akilini mambo ambayo yatapotosha mawazo, na kukufanya umdharau Yesu na kutokuyafikiri sana mafundisho yake yenye thamani. Jiepushe moyoni na mambo yote ambayo yaweza kuipotosha akili. Usiichoshe kwa hadithi hafifu zisizotia nguvu akilini. Mafikara huwa ya namna ile ile ya chakula ambacho ubongo hulishwa kwacho. 2

Masomo Yanayoharibu Roho ya Mtu

Kwa ajili ya wingi wa vitabu na magazeti vinavyomiminika daima kutoka katika mitambo ya kuchapisha wazee kwa vijana hufanya mazoea ya kusoma haraka-haraka na kwa juu juu tu, na hivyo ubongo hupoteza uwezo wake wa kupokea mawazo yaliyounganika na yenye nguvu. Juu ya hayo, sehemu kubwa ya magazeti na vitabu ambavyo, kama vyura wa Misri, vinatapakaa ncnini, sio kwamba ni vya hali ya chini tu, visivyofaa, na vyenye kudhoofisha, bali ni vichafu na vyenye kuaibisha. Matokeo yake siyo kulevya na kuharibu akili tu, bali kuchafua na kuangamiza roho. 3 KN 192.4

Katika mafundisho ya watoto na vijana, hekaya, hadithi za kizimwi, na hadithi za uongo sasa zinapewa nafasi kubwa. Vitabu vya namna hiyo hutumika shuleni, navyo hupatikana nyumbani mwa watu wengi. Wazazi ambao ni Wakristo huwezaje kuwaruhusu watoto wao kutumia vitabu vilivyojaa uongo jinsi hii? Watoto wakiuliza maana ya hadithi hizo ambazo ni kinyume cha mafundisho ya wazazi wao, hujibiwa kuwa hadithi hizo si za kweli; lakini hili halisaidii kuwaepusha na matokeo mabaya ya kuzitumia. Mawazo yatolewayo katika vitabu hivyo huwapotosha watoto. Huingiza maoni ya uongo ya maisha na kuzaa pamoja na kuchochea tamaa ya mambo yasiyo ya hakika, ya kuwaziwa tu. KN 192.5

Kamwe vitabu vyenye kuipotosha kweli visiwekwe mikononi mwa watoto au vijana. Watoto wetu wanapojielimisha kwa njia hii, wasiruhusiwe kuwa na mawazo ambayo yatakuwa mbegu za dhambi. 4 KN 193.1

Chimbuko lingine la hatari ambalo twapaswa kujihadhari nalo siku zote ni kusoma vitabu vilivyotungwa na makafiri. Vitabu vya namna hiyo huandikwa kwa uongozi wa yule adui wa ukweli, na hakuna mtu awaye yote awazaye kuvisoma bila kuihatarisha roho. Kwa kweli wengine wanaoathirika na vitabu hivyo hatimaye huweza kupona; wote wanaojituliza kwa mvuto mbaya wa vitabu hivyo hujiweka katika milki ya Shetani, nave huwafaidi sana. Wakiyakaribisha majaribu yake jinsi hiyo, hawana hekima ya kupambanua wala nguvu za kuyapinga. Kwa uwezo wa mivuto ya uzuri unaopoteza akili, kutoamini na ukafiri huimarika akilini. 5 

Hatari ya Kusoma Hadithi za Kushtusha

Watoto wetu watasoma nini? Hili ni swali kubwa ajabu tena lenye kudai jibu kubwa pia. Naudhika nikiona nyumbani mwa watu washikao Sabato vijitabu na magazeti yenye mfululizo wa hadithi zisizotoa nafasi ya mawazo mema akilini mwa watoto na vijana. Nimewaangalia wale ambao tamaa ya hadithi za uongo imekuzwa jinsi hii. Wamekuwa na nafasi ya kusikiliza ukweli; kujua habari za imani yetu; lakini wamekua hata kukomaa zaidi bila kumcha Mungu kwa kweli wala kuwa na utawa wa kufaa. KN 193.3

Wasomaji wa hadithi za upuzi zenye kutarakisha huwa watu wasiofaa kwa kazi za maisha mema. Wanaishi kwenye ulimwengu wa mashaka. Nimewaangalia watoto ambao wameachwa kuwa na mazoea ya kusoma hadithi hizo. Nyumbani au ugenini, hawakutulia, walikuwa wenye kuota ndoto au kuwaza mambo isivyo, wasioweza kuongea mambo mengine ila juu ya mambo ya hivi hivi tu. Mawazo na maongezi ya dim yalikuwa mambo mageni kabisa akilini mwao. Kwa kukuza upendo wa hadithi za kutisha akili hupotoshwa, na moyo hauridhiki hata kidogo mpaka ulishwe chakula hiki kibaya. Siwezi kufikiri jina la kuwafaa zaidi wale wanaojifurahisha kwa masomo ya jinsi hii kuliko kuwaita walevi wa akili. Mazoea ya kutokuwa na kiasi katika kusoma huleta madhara kwenye ubongo sawa na mazoea ya kutokuwa na kiasi katika kula na kunywa yanavyoudhuru mwili. 6 KN 193.4

Kabla ya kulipokea Neno la Mungu, wengine walikwisha kuwa na mazoea ya kusoma hadithi ndefu za uongo za kutungwa tu. Katika kujiunga na kanisa, wakajitahidi kuyashinda mazoea haya mabaya. Kuweka mbele ya watu wa jamii hiyo masomo yanayofanana na yale waliyokwisha kuyakataa ni sawa na kumpa mlevi pombe. Wakashindwa na majaribu yanayowakabili daima, hupotewa upesi na utamu wa masomo ya kweli. Hawapendi kusoma Biblia. Uwezo wa tabia yao ya moyoni hudhoofika. KN 193.5

Dhambi huzidi kuonekana kuwa jambo lisilo baya sana. Huonyesha zaidi kutokuwa na uaminifu, na kuzidi kuchukia kazi za maisha za manufaa. Kadiri akili inavyopotoshwa, ndivyo inavyozidi kuwa tayari kushika somo lolote lenye kutamanisha. Hivyo ndivyo Shetani anavyofunguliwa njia kuweka roho ya mtu chini ya utawala wake kabisa. 7 

Kitabu cha Vitabu

Hali ya mtu ya maisha ya dini hudhihirishwa kwa aina ya vitabu anavyochagua kusoma wakati awapo na nafasi. Ili kuwa na hali njema akilini na kanuni thabiti za dini, vijana hawana budi kushirikiana na Mungu maishani kwa njia ya Neno lake. Likielekeza njia ya wokovu ipatikanayo kwa Kristo, Biblia hutuongoza kwenye maisha bora zaidi. Inayo historia ya kupendeza sana, tena yenye mafundisho mengi pamoja na maandiko ya habari za maisha ya watu wengi zaidi ya maandiko yoyote mengine. Wale ambao mawazo vao havajapotoka kwa kusoma hadithi za uongo wataona kuwa Biblia ni kitabu cha kupendeza kuliko vitabu vingine. KN 194.2

Biblia ni kitabu cha vitabu. Kama unalipenda Neno la Mungu, na kulichunguza upatapo nafasi, ili upate hazina zake za thamani, na kutengenezwa kwa kila kazi njema, basi, uwe na hakika kuwa Yesu anakuvuta kwake. Lakini kuyasoma Maandiko Matakatifu kwa bahati, bila kutafuta kulifahamu fundisho la Kristo ili upate kuafikiana na masharti yake, hakutoshi. Kuna hazina ndani ya Neno la Mungu ambazo huweza tu kugunduliwa kwa kuchimba chini kabisa ya shimo la madini hayo ya kweli. KN 194.3

Moyo wa tamaa za mwili hukataa ukweli; roho ya mtu aliyeondoka hupatwa na badiliko la ajabu. Kitabu kile ambacho kwanza kilikuwa hakipendezi kwa sababu kiliyafunua maneno ya kweli ambayo yalimkanusha mwenye dhambi, sasa huwa chakula cha kiroho, furaha na kitulizo cha maisha. Jua la haki huzitia nuru kurasa hizi takatifu, na Roho Mtakatifu huzitumia kusema na roho ya mtu huyo. KN 194.4

Basi, wote wenye kuyapenda masomo hafifu, yasiyo na maana, sasa hawazielekezi akili zao kwenye neno hili lililo imara la unabii. Zitwaeni Biblia zenu, na kuanza kujifunza kwa moyo mpya Maandiko Matakatifu ya Agano la Kale na, Agano Jipya, kadiri mnavyosoma Biblia mara kwa mara, kwa moyo wa bidii, ndivyo itakavyozidi kuonekana kuwa nzuri, nanyi mtazidi kutopendezwa na masomo hafifu. Kazeni kitabu hiki cha thamini moyoni mwenu. Kitakuwa kwenu rafiki na kiongozi. 8

Sura Ya 32 - Muziki

UFUNDI wa sauti tamu za nyimbo takatifu ulikuzwa daima (katika shule za manabii). Hakuna ngoma ya upuzi iliyosikika, wala wimbo hafifu ambao ungemsifu mwanadamu na kupotosha akili kumwacha Mungu: bali zaburi takatifu za sifa kwa Mwumbaji zenye kulitukuza jina lake na kuyasimulia matendo yake ya ajabu. Hivyo muziki uhfanywa kulitimiza kusudi takatifu na kuyainua mawazo kwa kile ambacho kilikuwa safi, bora na kikuu pamoja na kuamsha rohoni uchaji na moyo wa shukrani kwa Mungu. 1 KN 195.1

Uimbaii ni sehemu ya ibada ya Mungu mbinguni, nasi tungejaribu, kwa nyimbo zetu za kumsifu, kukaribia, kadiri iwezekanavyo, ulinganifu wa sauti za waimbaji wa mbinguni. Mazoezi mazuri ya sauti ni jambo lenye maana katika mafundisho, lisingedharauliwa. Kuimba, kama sehemu ya ibada ya dini, ni tendo la ibada sawa na sala. Mtu hana budi kusikia wimbo moyoni kabla ya kuweza kuupatia maneno mazuri ya kuufaa. 2 KN 195.2

Nimeonyeshwa utaratibu kamili wa mbinguni, nami nimependezwa mno nilipokuwa nikisikiliza uimbaji ulio kamili pale. Baada ya kutoka katika njozi, nyimbo za hapa hazikunipendeza na sauti hazilingani. Nimeona jamii za malaika, waliosimama mraba, kila mmoja akiwa na kinubi cha dhahabu. Mwisho wa kinubi kuna chombo cha kubadilisha sauti. Vidole vyao havikuenda kwa uzembe juu ya nyuzi, bali waligusa nyuzi mbalimbali kutoa sauti mbalimbali. Palikuwa na malaika ambaye siku zote aliongoza ambaye kwanza hupiga kinubi na kutoa sauti, ndipo wote huungana naye kwa sauti kubwa ya uimbaji kamili wa mbinguni. Hauwezi kusifiwa mno kupita vile unavyostahili. Ni sauti tamu, takatifu, ya mbinguni, huku mionzi ya nuru ya sura ya Yesu iking’aa kutoka uso wa kila mmoja, kwa utukufu usioelezeka. 3 KN 195.3

Nalionyeshwa kuwa yawapasa vijana kujitia zaidi kwa jambo hili na kulifanya neno la Mungu kuwa mshauri wao na kiongozi wao. Vijana wana wajibu mzito ambao si wakuudharau. Ingizo la uimbaji nyumbani mwao, badala ya kuamsha utakatifu na hali ya mambo matakatifu limekuwa njia ya kupotosha mioyo yao kuiacha kweli. Nyimbo za upuzi na mtindo wa uimbaji upendwao na wengi huelekea kuwapendeza. Vyombo vya uimbaji vimechukua wakati ambao ungetumiwa kwa sala. Muziki, usipotumiwa vibaya, ni mbaraka mkubwa; lakini ukitumiwa vibaya, ni laana ya ajabu. Husisimua, lakini hautoi ile nguvu na moyo ambao Mkristo huweza tu kuupata kwenye kiti cha neema akionyesha kwa unyenyekevu wa moyo haja zake na, akilia kwa machozi, na kuomba kuongezewa nguvu za Mungu kumwezesha kushindana na majaribu makali ya yule mwovu. Shetani anawateka nyara vijana. Aha, nisema nini kuwaongoza kuukomesha uwezo wake wa kupumbazisha! Yu mpendezi mwerevu anayewashawishi kwenda hata jehanam. 4

Sura Ya 33 - Mateto na Matokeo Yake ya Baadaye

YAWAPASA Wakristo kujihadhari na maneno yao. Kamwe Wasieneze habari mbaya toka kwa rafiki mwingine huyu mpaka wanafahamu kwamba kuna mafarakano baina yao. Ni udhalimu kukonyeza na kusema kwa fumbo, kwamba unajua mengi juu ya rafiki huyo au kwamba unafahamu mambo mengine wasiyoyajua. Madokezo ya namna hiyo huenea mbali, na kuleta moyo mbaya kuliko kusema mambo wazi bila kutia chumvi. Kanisa la Kristo limepata madhara kama nini kwa mambo hayo! Mwenendo usiosawa wa kijinga wa washiriki wake umelidhoofisha kanisa kabisa. Matumaini yametupwa na washiriki wa kanisa hilo, walakini wakosaji hawakukusudia kutia fitina. Kutotumia busara katika kuchagua mambo ya kuzungumza kumeleta madhara mengi. KN 197.1

Ingefaa mazungumzo yawe juu ya mambo ya kirono, lakini yamekuwa kinyume chake. Kama kushirikiana na marafiki Wakristo hutumiwa zaidi kuzidisha ubora wa akili na moyo, hapatakuwa na majuto baadaye, nao wanaweza kutazama mambo ya nyuma na kuridhika. Lakini kama saa zinatumiwa kwa mazungumzo ya ovyo, bila kicho, na wakati wa thamani unatumiwa kwa kusengenya myenendo na tabia za wengine, maongezi ya kirafiki yatakuwa chanzo cha mabaya, na mvuto wako utakuwa harufu ya mauti iletayo mauti. 1 KN 197.2

Wapende Watu Wote

Tunaposikiliza lawama juu ya ndugu yetu, twajitwika lawama hiyo. Kwa swali hili, “Bwana, ni nam atakayekaa katika hema yako? Ni nani atakayefanya maskani yake katika kilima chako kitakatifu?” Mwandisni wa Zaburi amejibu, “Ni mtu aendaye kwa ukamilifu, na kutenda haki. Asemaye kweli kwa moyo wake, Wala hakumtenda mwenziwe mabaya, wala hakumsengenya jirani yake,” (Zaburi 15:1-3). KN 197.3

Mazungumzo hafifu yangezuilika kama nini ikiwa kila mtu angekumbuka kuwa wale wanaomwambia makosa ya wengine watatangaza makosa yake mara wakipata nafasi nzuri. Yafaa tujitahidi kuona mema kwa watu wote, hasa ndugu zetu, mpaka itakapotubidi kufikiri vinginevyo. Haitupasi kusifu upesi habari mbaya. Hizi mara nyingi hutokana na wivu na kutosikia vema, au pengine zimetiwa chumvi ama kutoa sehemu tu ya mambo ya kweli. Mara wivu na shuku vinapopewa nafasi, vitajieneza kama baruti. Kama ndugu akipotoka, huo ndio wakati wa kumwonyesha moyo wako hasa kwake. Mwendee kwa upendo, mwombee kwa Mungu ukiwa pamoja naye, kumbuka thamani isiyopimika ambayo Kristo amelipia ukombozi wake. Kwa njia hii waweza kuiokoa roho ya mtu na mauti, na kusetiri wingi wa dhambi. KN 197.4

Kutupia jicho, kutaja neno, hata kusema kwa sauti ya kuimba, huweza kujaa uongo wenye kupenya kama mshale wenye neno moyoni, utiao jeraha lisiloponyeka. Hivyo ndivyo mashaka, na lawama ziwezavyo kutupiwa mtu ambaye kwake Mungu angeweza kufanya kazi njema, na mvuto wake huharibiwa, na manufaa yake huangamizwa. Miongoni mwa wanyama wa aina nyingi, kama mmoja wao akijeruhiwa na kuanguka, mara hiyo hushambuliwa na kuraruliwa na wenzake. Moyo huo huo wa kinyama huonyeshwa na wanaume kwa wanawake wenye jina la Wakristo. Hao huonyesha moyo wa unafiki kuwapiga wengine mawe ambao ni wenye hatia pungufu kuliko waliyo nayo wao wenyewe. Kuna wengine ambao nuelekeza kwa kidole kwenye makosa ya wengine ili kuepusha hali yao wenyewe kutazamwa na watu, au ili kupata sifa kwa ajili ya moyo mkuu kwa Mungu na kwa kanisa. 2 KN 198.1

Wakati unaotumiwa kwa kuyalaumu makusudi na matendo ya watumishi wa Kristo ingekuwa bora ukitumiwa kwa maombi. Mara nyingi ikiwa wale wanaolaumu wengine wangejua ukweli juu ya watu wanaowalaumu, wangekuwa na maoni kinyume cha hayo juu yao. Basi, lingekuwa jambo bora kama nini ikiwa badala ya kuwalaumu na kuwashutumu wengine, kila mmoja angesema; “Sina budi kutimiza wokovu wangu mwenyewe. Ikiwa nashirikiana na Mwenye kutaka sana kuiokoa roho yangu, yanipasa kujilinda kwa uangalifu. Sina budi kuachilia mbali uovu wote maishana mwangu. Sina budi niwe kiumbe kipya ndani ya Kristo. Sina budi kushinda kila kosa. Ndipo, badala ya kuwadhoofisha wale wanaoshindana na maovu, naweza kuwatia nguvu kwa maneno yanayosaidia.” 3 KN 198.2

Mwenye Kijicho haoni Jema Lo Lote kwa Wengine

Tusikubali mashaka yetu na mambo nyenye kutukatisha tamaa kula rohoni mwetu na kutufanya wenye ucnungu na moyo wa harara. Yasiwepo mashindano yo yote, ama kuonea mabaya wala masengenyano, tusije tukamchukiza Mungu. Ndugu, ukifungulia wivu nakudhania maovu moyoni mwako, Roho Mtakatifu hawezi kukaa nawe. Tafuta ukamilifu uliomo ndani ya Kristo. Tumika kazini mwake. Kila wazo na neno na tendo navimdhihirishe. Wahitaji ubatizo wa kila siku wa upendo ambao siku za mitume uliwafanya wote kuwa na moyo mmoja. Upendo huo utaleta afya mwilini, akilini, na rohoni. Zungushia roho yako hali ya kupendeza ambayo itatia nguvu maisha ya kiroho. Kuza imani, matumaini, moyo mkuu, na upendo. Acha amani ya Mungu itawale moyoni mwako. 4 KN 198.3

Wivu siyo huharibu tu tabia ya mtu bali ni chuki, ambayo huchafua uelekevu wote. Umeanzishwa na Shetani. Yeye alitamani kuwa wa kwanza mbinguni, na kwa sababu hakuweza kupata mamlaka yote na utukufu aliotaka, akauasi utawala wa Mungu. Akawaonea wivu wazazi wetu wa kwanza akawashawishi kutenda dhambi, hivyo akawaharibu pamoja na wanadamu wote pia. KN 199.1

Mwenye kijicho huyafumba macho yake ili asione matendo mema na bora ya watu wengine. Yu tayari siku zote kudharau na kueleza vibaya kile kilicho bora. Watu mara nyingi huungama na kuyaacha makosa mengine, lakini hakuna matumaini ila kidogo tu kwa mwenye kijicho kufanya hivyo. Kwa kuwa mtu hawezi kuonea wivu mpaka kwanza akiri kwamoa ni mkuu; kiburi hakitamkubalia kuomba radhi. Kama jitihadi ikifanywa kusadikisha mwenye kijicho aina ya dhambi yake, huzidi kuona uchungu juu ya kitu kinachomchukiza, na mara nyingi hukaa hali hiyo bila kupona. KN 199.2

Mtu mwenye kijicho hueneza sumu po pote aendako, akifitini marafiki na kuamsha chuki na uasi juu ya Mungu na mwanadamu. Atafuta kudhaniwa kuwa yu bora na mkuu kuliko wote wengine, siyo kwa kuonyesha ushujaa, ili kuufikia upeo wa wema, bali kwa kusimama mahali alipo bila kusogea na kupunguza sifa inayozistahili bidii za wengine. KN 199.3

Ulimi unaofurahia fitina, ulimi wenye kubwata ambao husema, “Nipe habari, nami nitasimulia habari hizo.” umeelezwa na mtume Yakobo kuwa ni ulimi unaowasha moto wa jehanam. Hutawanya vinga vya moto kila upande. Kwani mwenezaji wa vijineno anajali kumsingizia mtu asiye na hatia? Hatazuia kazi yake ya uovu ingawa huharibu matumaini na kuwaflsha moyo wale ambao tayari wamekwisha kuanza kuzama ndani ya udhia wao. Anachojali tu ni kufungua njia ya mwelekeo wake wa kupenda machongezi. Hata wale wanaojidai kuwa ni Wakristo huyafumba macho yao wasione kitu chochote kilicho safi, amini, bora, na cha kupendeza, wakathamini chochote kile kilicho kibaya na cha kuchukiza, na kukitangaza kwa walimwengu

Wivu na Masuto

Naona uchungu kusema kuwa kuna walio na ndimi zisizotawaliwa miongom mwa washiriki wa kanisa. Kuna ndimi za uongo zenye kujilisha fitina. Kuna ndimi za hila zenye kunong’ona. Kuna wenye vijeneno, wafidhuli, ayari. Wengine miongoni mwa wale wapendao mazungumzo ya upuzi huchochewa na moyo wa utafiti, wengine huchochewa na wivu, na wengi huchochewa na chuki juu ya wale ambao kwa njia yao Mungu amesema nao kuwaonya. Mambo hayo yote yasiyopatana hufanya kazi. Wengine huficha nia zao hasa, huku wengine wakitaka sana kutangaza yote wajuayo, au hata vale wanayoshuku tu, juu ya ubaya wa mwingine. KN 199.5

Naliona kuwa roho ya ushuhuda wa uongo, ambao ungegeuza ukweli kuwa uongo, jema kuwa baya, na hali ya kutokuwa na hatia kuwa hali ya hatia, sasa inatenda kazi. Shetani hufurahia hali ya namna hii kwa watu wanaodai kuwa ni wa Mungu. Huku wengi wakiacha kuangalia roho zao wenyewe, wanatafuta sana nafasi ya kuwalaumu wengine. Wote wana hitilafu za tabia, na si vigumu kuona kitu ambacho wivu huweza kukielezea isivyo ili kuwadhuru. “Sasa,” ndivyo wasemavyo hao wanaojifanya wana sheria, “tunayo mamboya hakika . Tutawashitaki jambo wasiloweza kujiepusha na hatia.” Hungoja nafasi ya kufaa ndipo kutoa bunda la maneno matupu na kuleta vipande vidogo vizuri vya habari. KN 200.1

Katika kujitahidi kutimiza neno linalotakiwa, watu hao kwa asili wana uwezo mkali wa kuwazia mambo yasiyoonekana ila yanayosikika yakitajwa wamo katika hatari ya kujidanganya na kuwadanganya wengine. Hukusanya maneno ya kijinga kutoka kwa mwingine, husema kwa haraka na kukosea kuonyesha nia hasa za wasemaji. Lakini maneno hayo yasiyofikiriwa kabla ya kusema, ambayo mara nyingi ni vijineno tu visivyo na maana, huangaliwa kwenye kioo cha Shetani cha kukuza mambo hata yaonekane kuwa makubwa, yakifikiriwa, na kurudiwa mara nyingi mpaka vichuguu vya mchwa vinakuwa milima (mpaka yale maneno madogo yanakuwa makubwa). KN 200.2

Je, ni tabia ya Kikristo kukusanya habari zo zote, kufukua kila kitu kitakacholeta shuku juu ya tabia ya mwingine, ndipo kufiirahia kukitumia kumdhuru? Shetani hufurahi akiweza kumvunjia sifa au kumjeruhi mfuasi wa Kristo. Ni “mshitaki wa ndugu zetu.” Je, Wakristo wamsaidie katika kazi yake? KN 200.3

Jicho la Mungu lionalo yote huyaona makosa ya wote na hasira inayomtawala kila mmoja, lakini huyavumilia makosa yetu na kutuhurumia udhaifu wetu. Awaamuru watu wake kuihifadhi roho hiyo hiyo ya wema na uvumilivu. Wakristo wa kweli hawatafurahia kucnongea makosa na kasoro za wengine. Wataachilia mbali uovu na kombo, ili kukaza mawazo kwa kile ambacho ni kizuri na cha kupendeza machoni. Kwa Mkristo kila tendo la masuto, kila neno la lawama, huuma. 6 KN 200.4

Matokeo Yaletwayo na Lawama za Kanisa na Viongozi wa Jamii ya Watu

Moyo wa kutoa maneno ya upuzi na kuchongea ni mojawapo ya njia kubwa za Shetani za kueneza fitina na ugomvi ili kuwatenga marafiki, na kuharibu imani ya wengi katika ukweli wa hali zetu. Ndugu na dada wako tayari mno kuongea makosa ambayo hudhani yamo kwa wengine, na hasa kwa wale ambao wameutoa kwa uthabiti ujumbe wa maonyo walioupewa na Mungu. KN 201.1

Watoto wa hao wanung’unikaji husikiliza sana na kupokea sumu ya chuki. Hivyo ndivyo wazazi wanavyofunga, bila kujua, njia ambazo kwazo mioyo ya watoto hao ingeweza kufikiwa. Kwa hili Mungu hudharauliwa. Yesu amesema: “Kadiri mlivyomtendea mmoiawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi” (Matnayo 25:40). Hivyo Kristo hudharauliwa na kutukanwa na wale wanowasingizia watumishi wake. KN 201.2

Majina ya watumishi wateule wa Mungu yametumiwa kwa dharau, na wakati mwingine kwa aibu kabisa, na watu fulani ambalo wajibu wao ni kuwasaidia. Watoto hawakukosa kusikia maneno ya dharau ya wazazi wao kwa habasri za makaripio na maonyo ya nao watumishi wa Mungu. Wamefahamu maneno ya mzaha na ya kukashifu ambayo mara kwa mara yamesikika masikioni mwao, na mwelekeo umekuwa kuyalinganisha akilini mwao mambo mazuri ya kupendeza moyo na mambo matakatifu na ya milele, sawa na mambo ya kawaida ya ulimwengu huu. Kazi gani hii watendayo wazazi hao kuwafanya watoto wao kuwa makafiri hata utotoni mwao! Hivi ndivyo watoto wanavyofundishwa kuwa watu wasio na heshima na kuyaasi maonyo ya Mungu juu ya dhambi. KN 201.3

Upungufu wa hali ya kiroho huweza kuwa na nguvu mahali penye maovu. Hao baba na mama, wakiwa wamepofusnwa na yule adui, hustaajabu kwa nini watoto wao huelekea sana kutoamini na kulitilia shaka neno la kweli la Biblia. Hushangaa kuona kuwa ni shida sana kuwapata kwa mivuto ya adili na dini. Kama wangekuwa na macho ya kiroho, mara moja wangegundua kuwa hali hiyo mbaya ya kusikitisha ni matokeo ya mvuto wa nyumbani mwao wenyewe, imezaa wivu na mashaka yao. Hivyo ndivyo makafiri wengi wanavyofundishwa na kutayarishwa nyumbani mwa wale wanaojita Wakristo. KN 201.4

Kuna wengi wanaopendezwa hasa na kufikiri sana makosa, yakiwa ya hakika au ya kuwaziwa tu, ya wale wenye madaraka kazini mwa Mungu. Hawatazami mema ambayo yametendwa, na faida zilizotokana na kazi ngumu na moyo thabiti wa kicho kazini, bali hukazia macho kosa fulani lililo dhahiri, neno ambalo, likisha kutendwa na kupata mradi wake, huona kuwa lingeweza kutendwa kwa njia bora yenye matokeo mema zaidi; ambapo kama wangeachwa kuitenda kazi hiyo, wasingethubutu hata kidogo kufanya To lote kwa sababu ya mambo ya kukatisha tamaa ya hali hiyo, ama wangeweza kufanya hivyo kijinga zaidi ya wale walioifanya kazi hiyo, wakifuata majaliwa ya Mungu. KN 201.5

Lakini wasengenyaji hawa watashikilia mambo mabaya zaidi ya kazi, kama vile ukoga unavyoshikilia juu ya maparuzo ya mwamba. Watu hawa wamedumaa kiroho kwa kuendelea kukaa juu va kushindwa na makosa ya wengine. Hawana uwezo wa kiroho wa kuweza kupambanua matendo yaliyo mema na bora, jitihada zisizo za kujipenda nafsi, ujasiri wa kweli na kujinyima. Huharibu tabia kila siku na kuzidi kupungua maoni yao Uhafifu katika sehemu yao, na hali inayowazunguka ni sumu kwa amani na raha. 7 KN 202.1

Kila idara ya kazi itapaswa kushindana na shida. Dhiki hurusiwa ili kuipima mioyo ya watu wa Mungu na kwa kazi yake. Wakati kama huo mtu awaye yote asiyaangahe mambo vibaya na kuonyesha moyo wa mashaka na kutokuamini. Msiwalaumu wale wanaochukua mizigo ya madaraka. Mazungumzo nyumbani mwenu yasitiwe sumu na moyo wa kuwalaumu watenda kazi wa Mungu. Wazazi wenye moyo huo wa kulaumu hawawaletei watoto wao kile ambacho kitawahekimisha hata kupata wokovu. Maneno yao huelekea kuiharibu imani na matumaini siyo ya watoto tu, bali nata ya wazee pia. 8 KN 202.2

Wakubwa wa kazi zetu wanayo kazi ngumu kudumisha utaratibu na kuwatawala kwa busara vijana walio chini ya uangalizi wao. Washiriki wa kanisa wanaweza kufanya mengi kuimarisha mikono yao. Vijana wakikataa kukaa chini ya utawala wa wakuu wa idara ya kazi, au kwa jambo lo lote kuwa kinyume cha wakuu wao hukusudia kufanya kama wapendavyo wenyewe; basi wazazi wasiwasaidie wala kuwahurumia watoto wao bila kufikiri kwanza. KN 202.3

Ni heri watoto wenu kuumia, naam, heri walale makaburini mwao, kuliko kufundishwa kuzidharau kanuni zilizo msingi hasa wa kuutii ukweli kwa wanadamu wenzao, na kwa Mungu. 9 

Kujilaumu Mwenyewe Kwafaa Sana

Kama wote wanaojidai kuwa ni Wakristo wangetumia uwezo wao wa kujihoji ili kuona mabaya yapasayo kusahihishwa ndani yao wenyewe, badala ya kuongea juu ya makosa ya wengine, pangekuwa na hali njema kanisani leo. Bwana atengenezapo vito vyake vya thamani, waaminifu, wenye adili, watatazamwa kwa furaha. Malaika hutumiwa kuzitengeneza taji za watu wa jinsi hiyo, na juu ya hao taji zenye nyota zitang’aa na kutoa nuru ambayo hutoka katika kiti cha enzi cha Mungu. KN 202.5

Mungu huwapima na kuwathibitisha watu wake. Waweza kuwa mkali na mwepesi kuvumbua na kutoa makosa madogo madogo uliyo nayo mwenyewe kama upendavyo; lakini, uwe mpole, mwenye huruma, na mwenye adabu kwa wengine. Uliza kila siku; Nina maana, au ninajidanganya nafsini? Mwombe Mungu kukuokoa na udanganyifu wote juu ya jambo hili. Mambo ya milele hutatanisha. Je, naugu mpendwa, wengi wanapotamani heshima na faida isiyo ya halali, unatafuta kwa bidii ahadi ya upendo wa Mungu na kulia: Ni nani atakayenionyesha jinsi ya kufanya imara kuitwa kwangu na uteule wangu? KN 202.6

Shetani huchunguza kwa uangalifu dhambi za watu za asili, kisha huanza kazi yake ya kuwadanganya na kuwawekea mitego. Tumo kwenye majaribu makali, lakini tunaweza kushinda kama tukipigana kiume vita vya Bwana. Wote wako hatarini. Lakini kama mkienenda kwa unyenyekevu na kuomba kwa bidii mtatoka katika jaribio mkiwa wenye thamani zaidi ya dhahabu safi, naam, kuliko dhahabu ya Ofiri. Mkiwa wazembe na wasiomwomba Mungu, mtakuwa kama shaba iliayo na upatu uvumao.

Sura ya 34 - Onyo Juu ya Mavazi

KATIKA mavazi, kama ilivyo kwa mambo mengine pia, tumejaliwa kumtukuza Muumbaji wetu. Ataka sana mavazi yetu yawe safi na yenye kukidhi afya, tena mazuri na ya kufaa pia. KN 204.1

Yatupasa kujitahidi kuwa maridadi. Katika huduma ya patakatifu Mungu alieleza kila jambo lenye kuhusu mavazi ya wale waliohudumu mbele zake. Hivyo twafundishwa kwamba kuna uvaaji upendelewao zaidi kwa wale wanaomtumikia. Maagizo maalumu sana yalitolewa juu ya mavazi ya Haruni, maana uvaaji wake ulikuwa mfano wenye maana. Katika mambo yote yatupasa kuwa wajumbe wake. Kuonekana kwetu katika kila jambo kungeainishwa na umaridadi, adabu, na usafi. KN 204.2

Kwa viumbe vya asili (maua mazuri) Kristo aliuelezea uzuri ambao Mungu huuthamini, neema ya kutojivika kwa mapambo mengi, usafi, hali ya kufaa ambayo ingefanya uvaaji wetu kumpendeza. 1 KN 204.3

Kanuni za Mavazi

Vazi na mshono wake mwilini mwa mtu kwa kawaida huonekana kuwa kielelezo cha hali ya mwanamume au mwanamke. KN 204.4

Twafahamu tabia ya mtu kwa namna ya mavazi anayovaa. Mwanamke mwenye adabu, mcha Mungu atavaa kwa adabu. Akili nzuri, moyo wa uadilifu, utadhihirishwa katika kuchagua mavazi yanayofaa, yasio na mapambo mengi. Mtu ambaye si mwenye kiburi katika mavazi yake na hali yake huonyesha kuwa anafahamu kwamba mwanamke wa kweli huainishwa na uadilifu. Kutojipamba kwa mavazi ni jambo la kupendeza sana, ambalo kwa uzun laweza kulinganishwa na maua ya kondeni. KN 204.5

Nawasihi watu wetu kuenenda kwa uangalifu na kwa tahadhari mbele za Mungu. Igeni namna ya mavazi kadiri inavyopatana na kanuni za afya. Hebu dada zetu wavae pasipo urembo, kama wengi wafanyavyo, wakiwa na mavazi mazuri, ya vitambaa vidumuvyo, vya kufaa siku hizi; tena mavazi yasiwe jambo kubwa mawazoni. Yawapasa wajivike nguo za adabu, kusetiri aibu ya uchi na kuwa na kiasi. Wapeni walimwengu kielelezo cha nguvu cha kujipamba kwa neema ya Mungu. KN 204.6

Kama walimwengu wakianzisha namna ya mavazi ya adabu ya kufaa, na yenye kukidhi afya, yanayopatana na Biblia, haitadhuru uhusiano wetu na Mungu ama na walimwengu kuiga mtindo wa namna hiyo. Wakristo wangemwiga Kristo na kufanya uvaaji wao kupatana na Neno la Mungu. Wawe na kiasi. Kwa unyenyevu wangefuata unyofu, wasijaii sifa, wala lawama; yafaa washikilie kutenda mema kwa sababu ya uzuri wa wema huo. KN 204.7

Usijisumbue wakati wote kwa kujaribu kuiga namna zote za mavazi zisizo na maana. Vaa nguo safi na nzuri, lakini usijionyeshe ama kwa kuvaa maridadi kiasi ama kwa kuvaa vibaya, kwa uzembe. Tenda kana kwamba unajua kuwa jicho la mbinguni linakutazama, na ya kuwa unaishi chini ya kibali cha Mungu ama kinyume na mapenzi yake. 2 KN 205.1

Mafundisho ya Biblia

Kristo aliona upendo wa mavazi, naye alionya, naam, akaamuru wafuasi wake wasiyafikiri sana hayo. “Na mavazi ya nini kuyasumbukia? Fikiri maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti; nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.” Kiburi na upotevu wa mali katika mavazi ni dhambi ambayo mwanamke hupenda hasa; hivyo maagizo haya humhusu yeye hasa. Dhahabu au lulu au nguo za thamani kubwa ni vyenye thamani ndogo sana vikilinganishwa na upole na uzuri wa Kristo! KN 205.2

Nalielekezwa kwenye Maandiko naya yafuatayo. Malaika akasema, “Yapasa kuwafundisha watu wa Mungu. “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitin, pamoja na adabu nzuri, la moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu” (1 Timotheo 2:9, 10). KN 205.3

“Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upde na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. Maana nivyo ndivyo walivyo jipamba wanawake watakatifu wa zamani” (1 Petro 3:3-5). KN 205.4

Wengi huyadharau maagizo hayo na kuyahesabu kuwa ya zaman sana hata haina maana kuyajali; lakini Mwenye kuyatoa kwa wanafunzi wake alijua hatari zitokanazo na kupenda mavazi siku zetu, akatupelekea onyo kubwa. Je, tutalitii onyo hilo na kuwa wenye hekima? KN 205.5

Wale wanaotafuta kwa kweli kumfuata Kristo watajihadhari sana ra mavazi wavaayo; watajitahidi kutimiza masharti ya agizo hilo lililotolewa wazi na Bwana (1 Petro 3:3-5). 3 KN 205.6

Kiasi katika kuvaa ni sehemu ya wajibu wetu wa Kikristo. Kuvaa bila kujipamba, kuepukana na kujipamba kwa johari na mapambo ya kila namna, ni jambo linalopatana na imani yetu. KN 205.7

Wengi huhitaji mafundisho jinsi iwapasavyo kuonekana katika mikutano ya ibada siku ya Sabato. Haiwapasi kuingia mahali Mungu alipo wakivaa mavazi ya kawaida yaliyovaliwa siku za kazi katika juma hilo. Yafaa wote kuwa na mavazi maalumu ya Sabato yavaliwayo wakienda kuhudhuria ibada nyumbani mwa Mungu. Huku tukiwa hatupaswi kuiga mitindo ya kilimwengu, tusikose kujali hali yetu ya nje. Yatupasa tuwe maridadi, ingawa hatujipambi. Yafaa watoto wa Mungu wawe safi ndani na nje. 5 KN 206.1

Akili za moyoni huelekeza huko. Hiyo ndiyo sababu Wakristo huyaona maisha ya dini kuwa magumu sana na maisha ya kidunia kuwa rahisi sana. Akili zimezoezwa kutoa nguvu yake upande huo. Katika maisha ya kidini pamekuwako ukubali wa maneno ya kweli ya Biblia, lakini siyo kutendeka halisi kwa maneno hayo maishani. KN 206.2

Kukuza mafikara ya dini na moyo wa kumwabudu Mungu haifanywi kuwa sehemu ya mafundisho. Hayo yangeongoza na kuutawala mwili nzima. Mazoea ya kutenda mema hayapo. Kuna utendaji wa ghafla kwa mivuto mizuri, lakini kufikiri siku zote kwa urahisi juu ya mambo matakatifu si kanuni inayotawala akilini. KN 206.3

Akili za moyoni hazina budi kufundishwa na kuongozwa kupenda usafi. Upendo wa mambo ya kiroho ungetiwa nguvu; naam, hauna budi kutiwa nguvu, kama wakipenda kukua katika neema na kuujua ukweli. Tamaa ya wema na utakatifu wa kweli ni nzuri kadiri llivyo; lakini ukikoma hapo, haitakufaa cho chote. Makusudi mema hufaa, lakini hayatakuwa na maana kama vasipotimizwa kwa uthabiti. Wengi watapotea wakiwa wanatumaini na kutamani kuwa Wakristo; lakini hawajitahidi kwa moyo, hivyo watapimwa kwa mizani na kuonekana kuwa wamepungua. Nia haina budi kutumiwa kwa upande mzuri. Nitakuwa Mkristo kwa moyo wangu wote. Nitajua urefu na mapana, kimo na kina cha upendo kamili. Hebu yasikilize maneno ya Yesu: “Heri wenye njaana kiu ya haki; maana hao watashibisnwa.” Mathayo 5:6. Majaliwa makubwa hutolewa na Kristo kuiridhisha roho ya mtu mwenye njaa na kiu ya haki. 3 

Kuchuchumia Mambo ya Kiroho Yaliyo Bora Zaid

Kiini safi cha upendo kitaipanua roho ya mtu ili kutoanafasi kwa mambo bora zaidi, kwa ongezeko la maarifa ya mambo yi kiroho, kusudi isiridhike na hali pungufu. Wengi wanaodai ni Wakristo hawajui nguvu za kiroho ambazo wangaliweza kuzipata kama wangekuwa wenye nia, wenye bidii, na kujitahidi kupata ujuzi wa mambo matakatifu kama wafanyavyo kupata mambo hafifu valiyo ya kitambo tu katika maisha haya. Jamii ya watu wanaojidai kuwa ni Wakristo wameridhika kudumaa kiroho. Hawana nia kulifanya kusudi lao kuwa kuutafuta kwanza ufalme wa Mungu na haki yake; kwa kuwa utauwa ni siri iliyofichwa kwao, hawawezi kuifahamu. Hawamjui Kristo wa Hakika. KN 206.5

Wanaume na wanawake waridhikao na hali yao ya kudumaa na kuwa vilema katika mambo ya kiroho hebu wapelekwe mbinguni kwa ghafla waone kwa macho hali timilifu, bora na takatifu iliyoko kule daima kila nafsi imejawa na upendo; kila uso uking’aa kwa furaha; muziki wakupendeza sana kwa sauti tamu zinazolingana vizuri za kumtukuza Mungu na Mwana Kondoo; na nuru lsiyokoma ikiwazukia watakatifu kutoka usoni mwake Aketiye juu ya kiti cha enzi, na kutoka kwa Mwana Kondoo; basi, nawatambue kuwa kuna furaha kubwa zaidi bado ya kufaidi, maana kadiri wazidivyo kupokea furaha ya Mungu, ndivyo nafasi yao inavyoongezeka kupanda juu kwenye ile furaha ya milele, na kwa njia hiyo kuendelea kupokea manufaa mapya na makubwa zaidi kutoka katika machimbuko yasiyokoma ya utukufu na mbaraka usioelezeka -Nauliza, watu kama hao waweza kuwa miongoni mwa mkusanyiko wa mbinguni, kushiriki nyimbo zao, na kufaidi utakatifu, na utukufu bora utokao kwa Mungu na kwa Mwana Kondoo? Ah, la! Muda wao wa majaribio kama wanafaa au hawafai ulizidishwa miaka mingi ili wapate kujifunza lugha ya mbinguni, kusudi wapate kuwa “washiriki wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharioifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa” ( 2 Petro 1:4). Lakini walikuwa na shughuli za miili yao. Hawakuweza kumtumikia Mungu kwa moyo wote na kuhfanya hilo kuwa shughuli yao. Shugruli za dunia hapana budi zilifika kwanza na kutwaa uwezo wao ulio bora na wazo la muda mfupi tu hutolewa kwa Mungu. Watu kama hao watabadilishwa baada ya kukatwa shauri la mwisho: “Mtakatifu na azidi kutakaswa,” “mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu?” Wakati kama huo unakuja. KN 207.1

Wale ambao wamezizoeza akili zao kuyafurahia mambo ya kiroho ndio watakaoweza kuhamishwa wala wasiangamizwe na usafi la utukufu bora sana wa mbinguni. Pengine unaweza kuwa na maarifa bora ya kazi ya ufundi, ama unaweza kuwa na ujuzi wa elimuya ‘sayansi’, labda unaweza kushinda kwa ubora katika uimbaji na katika mwandiko, ama tabia yako ikawapendeza marafiki zako, lakini mambo hayo yanahusiana na matayarisho ya kwenda mbinguni? Yanahusiana na kukutayarisha kusimama mbele ya baraza la hukumu ya Mungu? 4 

Tabia ya Mbinguni Haina Budi Kupatikana Duniani

Msidanganyike. Mungu hadhihakiwi. Utakatifu tu, wala si kitu kingine, ndio utakaowafanya kuwa tayari kwenda mbinguni. Unyofu na uchaji wa hakika katika mambo ya maisha peke yake ndio uwezo wa kuwapa tabia safi, bora, na kuwawezesha kumgia mbele za Mungu akaaye penye nuru isiyoweza kukaribiwa. Tabia ya mbinguni haina budi kupatikana hapa duniani, ama sivyo kamwe naipatikani tena. Basi, anza mara moja. Usijidanganyike kuwa utafika wakati uwezapo kujitahidi kwa urahisi kuliko sasa, Kila siku huzidisha umbali wako kutoka kwa Mungu. Jitayarishe kwa ajili ya uzima wa milele. Zoeza mawazo ya moyo wako kuipenda Biblia, kuupenda mkutano wa maombi, kupenda saa ya kumtafakari Mungu, na, zaidi ya yote, saa ambayo roho hushirikiana na Mungu. Uwe mwenye kufikiri mambo ya mbinguni ukipenda kuungana, na lile kundi la waimbaji wa mbinguni katika makao ya juu. 

Pata Upendo wa Mungu Maadam Unaweza

Mawazo yangu hurudi nyuma kwa mwaminifu Ibrahimu, ambaye, kwa kuitii amri ya Mungu, alipewa katika njozi kule Beersheba, ashike nafasi yake akiwa pamoja na Isaka. Aliuona kwa mbele yake mlima ambao Mungu alikuwa amemwambia atamwonyesha kama mlima apaswao kutoa dhabihu juu yake. KN 208.1

Isaka alifungwa kwa mikono itetemekayo, ya upendo wa baba yake mwenye huruma kwa sababu Mungu amemwamuru. Mwana huyo akakubali kutolewa dhabihu kwa sababu aliamini uaminifu wa baba yake. Lakini kila kitu kilipokwisha kuwa tayari, imani ya baba na utii wa mwana vilipokwisha kupimwa kabisa, malaika wa Mungu aliuzuia mkono wa Ibrahimu ulioinuliwa juu ambao ulikuwa karibu kumchinja mwanawe na kumwambia, yatosha. “Sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee” (Mwanzo 22:12). KN 208.2

Tendo hili la imani kwa Ibrahimu limeandikwa kwa ajili ya faida yetu. Latufundisha fundisho kubwa la kuyatumaini masharti ya Mungu, ijapokuwa yawe mazito na makali namna gani; lawafundisha watoto utii kamili kwa wazazi wao na kwa Munga pia. Kwa utii wa Ibrahimu twafundishwa kwamba hakuna cho chote kilicho na thamani mno hata tusiweze kukitoa na kumpa Mungu. KN 208.3

Mungu alimtoa Mwanawe kwa maisha duni, kujinyima, umaskini, taabu, shutuma, na kifo cha maumivu makubwa ya kusulibishwa. Lakini hapakuwako na malaika kutoa habari ya furaha: “Yatosha; huna haja ya kufa, Mwana mpendwa wangu.” Vikosi vya malaika vilikuwa vikingojea kwa huzuni, vikitumaini kuwa, kama ilivyokuwa kwa Isaka, Mungu katika dakika ya mvisho angezuia kifo chake cha aibu. Lakini malaika hawakuruhnsiwa kutoa ujumbe wo wote wa namna hiyo kwa Mwana mpendwa wa Mungu. Aibu katika jumba la baraza la hukumu na njiani kv.enda Fuvu la Kichwa ikaendelea, akaendelea, akadhihakiwa, akachekwa, na kutemewa mate. Akastahimili dhihaka, shutuma na matusi ya wale waliomchukia, mpaka juu ya msalaba akakiinamisha ki:hwa chake akafa. KN 208.4

Mungu angeweza kutudhihirishia upendo wake kwa njia nyingine kuu kuliko hiyo ya kumtoa Mwanawe kupatwa na mateso hayo? Na kama karama ya Mungu kwa mwanadamu ilivyokuwa kipaji cha bure, na upendo wake usivyo na mwisho, kadhalika ndivyo madai yake juu ya matumaini yetu, utii wetu, moyo wetu wote, na wingi wa upendo wetu yasiyo na mwisho. Ahitaji yote awezayo mwanadamu kutoa. Utii wetu hauna budi kuwa wenye ulingamfu na kipawa cha Mungu; hauna budi kuwa kamili usiopungua cho chote. Wote tu wadeni wa Mungu. Anayo madai kwetu ambayo hatuwezi kuyatimiza pasipo kujitoa dhabibu kamili ya hiari. Adai utii wa upesi na wa hiari, wala hatakubali upungufu wo wote wa huo. Tunayo nafasi sasa kuupata upendo na kibali cha Mungu. Mwaka huu huenda ukawa mwaka wa mwisho wa maisha ya wengine walisomao neno hili. Kuna ye yote miongoni mwa vijana walisomao ombi hili ambaye angependa kuchagua anasa za ulimwengu huu badala ya ile amana ambayo Kristo humpa mwenye kuitafuta kwa moyo wa bidii na mwenye kufurahia kuyatenda mapenzi yake? 6

Kupimwa katika Mizani

Mungu huzipima tabia zetu, mwenendo wetu, na makusudi yetu kwa mizani ya patakatifu. Litakuwa jambo la kutisha kutajwa kwamba tumepungua katika upendo na utii kwa Mwokozi wetu, aliyekufa msalabani kuivuta mioyo yetu kwake. KN 209.2

Hasa wake wa wachungaji wetu wangekuwa waangalifu wasije wakayaasi mafundisho dhahiri ya Biblia juu ya jambo hili la zamani sana hata haina maana kuyajali; lakini Mwenye kuyatoa kwa wanafunzi wake alijua hatari zitokanazo na upendo wa mavazi katika siku zetu, akatupelekea onyo kubwa. Je, tutalitii onyo hili na kuwa wenye hekima? Upotevu wa mali katika mavazi huongezeka daima. Mwisho bado. Mtindo hubadilika kila mara, na akina dada huufuatilia, bila kujali wakati wala gharama. Fedha nyingi hutumiwa kwa mavazi, ambapo zingerudishwa kwa Mungu aliye Mtoaji. 6 

Mvuto wa Namna ya Mavazi

Kupenda mavazi huhatarisha tabia za uadilifu na kumfanya mwanamke kuwa kinyume cha mke Mkristo, mwenye tabia ya adabu na ya kiasi. Mavazi ya kujionyesha, ya bei kubwa, mara nyingi huzidisha tamaa ya mwili moyoni mwa mvaaji na kuamsha tamaa mbaya moyoni mwa mtazamaji. Mungu anaona kuwa uharibifu wa tabia mara nyingi hutanguliwa na kuendekeza kiburi na umaridadi usio na maana. Huona kuwa mavazi ya bei kubwa huzimisha tamaa ya kutenda mema. 7 KN 209.4

Mavazi rahisi, yasiyo na mapambo mengi yatakuwa sifa njema kwa dada zangu vijana. Hamwezi kwa njia iwayo yote nyingine kuacha nuru yenu langaze kwa wengine kuliko kwa njia hii ya mavazi yasiyo na mapambo mengi na mwenendo mzuri. Mwaweza kuWaonyesha wote kuwa, mwayathamini mambo ya maisha haya, hali kadhalika na yale ya uzima wa milele. 8 KN 210.1

Wengi huvaa kama walimwengu ili kuwa na mvuto kwa wale wasioamini, lakini kufanya hivyo ni kosa baya. Wakipenda kuwa na mvuto wa kweli uokoao, na wayashike maungamo yao maishani, waonyeshe imani yao kwa matendo yao ya haki, na kudhihirisha tofauti iliyopo baina ya Wakristo na ulimwengu. Maneno, mavazi, matendo, yangemshuhudia Mungu. Ndipo mvuto mtakatifu utaenezwa kwa wote wanaowazunguka, na hata wasioamini watawatambua kuwa wamekaa na Yesu. Kama wako wanaotaka mvuto wao ushuhudie ukweli, basi, wayashike maungamo yao maishani mwao na kwa njia hiyo wamwige Kielelezo Mnyenyekevu. 9 KN 210.2

Dada zangu, epukeni hata umbo baya la nje. Katika zama hizi za upotevu, za kuoza hata kunuka, hamko salama msipojilinda. Sifa njema na adabu havipatikani ila kwa shida. Nawasihi, nawaomba kama wafuasi wa Kristo, mfanyapo maungamo makuu, kukithamini kitu hicho cha thamani kuu cha adabu nzuri. Hicho kitahifadhi sifa njema. KN 210.3

Mavazi yasiyo ya kujipamba, pamoja na adabu nzuri, vitafanya makuu kumzungushia msichana usetiri mtakatifu ambao utakuwa kwake ngao ya kukingia hatari maelfu. 10 KN 210.4

Mavazi yasiyo na mapambo mengi yatamfanya mwanamke mwenye akili kuonekana bora sana. Vaeni kama iwapasavyo Wakristo kuvaa pasipo mapambo mengine, jitengenezeni kama wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu, kwa matendo mema. Wengi, ili wapate kuiga matendo ya kijinga, kupotewa na namna nzuri ya hali ya asili pasipo mapambo mengi nao nuvutWa na namna ya kuiga, isiyo ya asili. Hutoa wakati na fedha, nguvu za akili, na uadiliui na kuutumia mwili wao mzuri kwa desturi za akili, na uadilifu na kuutumia mwili wao mzuri kwa desturi za marsha ya kisasa. KN 210.5

Vijana wapendwa, nia mliyo nayo ya kuvaa kama ulivyo mtindo wa siku hizi,,na kuvaa vazi jembamba, na mapambo ya dhahabu, na vitu vya kuiga kwa urembo, haitaishuhudia kwa wengine dini yenu wala neno la kweli mnalolikiri. Watu wenye akili watahesabu jitihadi zenu za kujipamba kwa nje kama thibitisho la nia dhaifu mliyo nayo na mioyo ya kiburi. 11 KN 210.6

Kuna vazi ambalo kila mtoto na kila kijana aweza kulitafuta na kulipata tu pasipo kuwa na hatia. Hilo ni haki ya watakatifu. Ikiwa wangekubali tu kufanya bidii kulipata vazi hilo kama wanavyojitahidi katika mitindo ya mavazi yao katika kuwaiga walimwengu, haingepita muda mrefu wangevikwa haki ya Kristo, na majina yao hayangefutwa katika kitabu cha uzima. Mama, vijana, na watoto pia, Jiujitahidi kuomba, “Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu.” (Zaburi 51:10.) Huu usafi wa moyoni na uzuri wa roho ni vyenye thamani kuliko dhahabu kwa wakati huu na kwa uzima wa milele pia. Wenye moyo safi tu ndio watakaomwona Mungu. 12

Sura Ya 35 - Ombi kwa Vijana

VIJANA rafiki wependwa, kila mnachopanda mtakivuna pia. Sasa ni wakati wenu wa kupanda. Mavuno yatakuwaje? Mwapanda nini? Kila neno msemalo, kila tendo mtendalo, ni mbegu ambayo itazaa matunda mema au mabaya, nayo italeta furaha au huzuni kwa mpandaji. Kama ilivyo mbegu iliyopandwa, ndivyo yatakavyokuwa mavuno. Mungu amewapa nuru kubwa na mibaraka mingi. Baada ya nuru hiyo kutolewa, baada ya hatari kuonyeshwa dhahiri mbele yenu, mambo yanabaki juu yenu. Namna mnavyofanya na nuru ambayo mnapewa na Mungu italetsa furaha ama huzuni. Ninyi wenyewe mnajitayarishia mwisho wenu wenyewe. KN 212.1

Nyote mna mvuto wa mema ama wa mabaya katika akili zetu za moyoni na kwenye tabia za wengine. Na mvuto mnaoutoa huandikwa katika kitabu cha kumbukumbu mbinguni. Malaika anafuatana nanyi kila mwendako na kuandika habari za maneno na matendo yenu. Mnapoamka asubuhi, mwauona udhaifu wenu na hitaji lenu la nguvu kutoka kwa Mungu? Je, kwa moyo mnyenyekevu mwayafanya mahitaji yenu kujulikana kwa Baba yenu aliye mbinguni? Kama mwaranva hivyo, malaika hutazama sala zenu, na ikiwa sala hizo hazijatoka katika midomo ya kusingizia, wakati mkiwa katika hatari ya kufanya mabaya bila kujua na kutoa mvuto utakaowaongoza wengine kufanya mabaya, malaika akulindaye atakuwa karibu nawe kukusaidia kutenda mema, akikuchagulia maneno, na kuongoza matendo yako. KN 212.2

Kama hujioni hatarini, na ikiwa huombi kwa Mungu msaada na nguvu kuyapinga majaribu, bila shaka utapotea; kutojali wajibu wako kutaonyeshwa katika kitabu cha Mungu mbinguni, nawe utaonekana umepungua siku ile ya kupimwa. KN 212.3

Wako wengine pande zote kukuzunguka ambao wameongozwa kwa jinsi lpasavyo watu wenye dini na wengine ambao wameendekezwa, wakapendelewa, wakasifiwa isivyostahili, na kutukuzwa mpaka wameharibika hata hawafai hata kidogo maishani. Nasema juu ya watu niwajuao hasa tabia zao zimepotoshwa sana na anasa, sifa za bure, na uvivu hata hawana faida katika maisha haya. Na ikiwa hawafai kitu kwa maisha haya, twaweza kutumaini nini kwa yale maisha ambayo wote ni safi na watakatifu, na ambayo wote watakuwa wenye tabia zinazopatana? Nimewaombea watu hao; nimezungumza nao mimi mwenyewe. Naliweza kuona mvuto ambao wangeweza kuwatolea watu wengine katika kuwapotosha, upendo wa mavazi, kutojali mambo yao ya milele. Tumaini la pekee kwa watu wa aina hiyo ni wao wenyewe kujihadhari na njia zao, kunyenyekea mioyoni mwao na kuachana na kiburi cha bure mbele za Mungu, kuziungama dhambi zao, na kuongoka. 1 KN 212.4

Kuzeni Upendo wa Mambo ya Kiroho

Usalama tu kwa vijana ni kukesha kila wakati na kuomba kwa moyo mnyenyekevu. Wasijidanganye kwamba wanaweza kuwa Wakristo bila mambo hayo. Shetani huficha majaribu na hali zake na kuwafunika kwa nuru kama alivyofanya alipomshawishi Kristo jangwani. Alionekana kama mmojawapo wa malaika wa mbinguni. Yule adui wa roho zetu atujia kama mgeni wa mbinguni, na mtume atoa shauri kuwa kiasi na kukesha ndiyo tu salama yetu. Vijana ambao hujitayarisha kwa anasa bila kujali, na wasiofanya wajibu uwapasao Wakristo, daima huanguka katika majaribu ya adui, badala ya kushinda kama Kristo alivyoshinda. 2 KN 213.1

Wengi hudai kuwa upande wa Bwana, lakini sivyo; uzito wa matendo yao yote umo upande wa Shetani. Kwa njia gani tutaweza kuyakinisha tuko upande gani? Ni nani mwenye moyo? Mawazo yetu ni juu ya nani, na nguvu zetu? Ikiwa tuko upande wa Bwana, mawazo yetu ni kwake, na mafikara yetu bora ni juu yake. Hatuna urafiki na ulimwengu, tumetoa wakfu vyote tulivyo navyo, ni vyake. Twatamani kuwa na sura yake, na kumpendeza katika mambo yote. 3 KN 213.2

Elimu ya kweli ni uwezo wa kutumia akili zetu makusudi kupata matokeo yenye faida. Mbona basi dini tunaifikiria kidogo hivi huku mambo ya ulimwengu yakiwa na nguvu ubongoni, mifupani, na kwenye misuli? Sababu ni kwamba nguvu zote za mwili wetu zimeelekezwa upande huo. Tumejizoeza kushughulika kwa bidii na nguvu katika mambo ya kidunia mpaka imekuwa vyepesi kuwa Mungu ametujalia vipawa vikuu vyenye thamani. Ametupa nuru na ujuzi wa mapenzi yake, hata hatuna sababu ya kufanya kosa wala kutembea gizani. Kupimwa katika mizani na kuonekana kuwa umepungua siku ile ya kukatwa shauri la mwisho na kutolewa ijara litakuwa jambo la kutisha, kosa baya sana lisiloweza kusahihishwa tena. Vijana rafiki zangu, je majina yenu hayatapatikana katika kitabu cha Mungu? 4 KN 213.3

Mungu amewapa kazi ya kumfanyia ambayo itawafanva ninyi kuwa watenda kazi pamoja naye. Pande zote kuwazunguka kuna roho za watu zinazotaka kuokolewa. Wako wale mwenzao huwatia nguvu na kuwafanya kuwa wenye hali ya heri kwa jitihada zetu. Mwaweza kuziongoa roho za watu kwenye haki kutoka dhambini. Mkijua wajibu wenu kwa Mungu mtaona moyoni mwenu haja ya uamimfu katika kuomba na uaminifu katika kukesha msiingie kwenye majaribu ya Shetani. Ikiwa ninyi ni Wakristo kwa kweli, mtapenda zaidi moyoni kuhuzunikia giza la mambo matakatifu5 badala ya kujifurahisha kwa anasa na kiburi cha bure cha mavazi. Mtakuwa miongoni mwa wale wenye kupiga kite na kulia juu ya machukizo yatendwayo nchini. Mtayapinga majaribu ya Shetani msiingie kwenye majivuno na kujipamba kwa mapambo mengi ya fahari. Ubongo hudhoofishwa na akili hudunishwa ikiridhishwa na mambo hafifu na kutojali wajibu ulio bora. 6 KN 213.4

Vijana siku hizi huweza kuwa watenda kazi pamoja na Kristo wakipenda, na wakitenda kazi, imani yao itatiwa nguvu na ujuzi wao wa mambo matakatifu utaongezeka.. Kila kusudi la kweli na kila tendo la haki litaandikwa katika kitabu cha uzima. Laiti ningeweza kuwaamsha vijana kuona na kusikia moyoni hali ya dhambi ya kuishi kwa kujifurahisha wenyewe kwa anasa na kudumaza akili zao katika mambo hafifu, yasiyo na maana ya maisha haya. Kama wangeinua mawazo na maneno yao juu zaidi ya mivuto hafifu ya ulimwengu huu na kuwa na kusudi la kumtukuza Mungu, amani yake, ipitayo ufahamu wote, wangeipata. 7 KN 214.1

Mungu ataka vijana kuwa watu wenye mioyo hodari, kutayarishwa kuitenda kazi yake bora, na kufanywa wafae kuchukua madaraka. Mungu awaita vijana wenye mioyo safi, wenye nguvu na hodari, na wenye kukusudia kupigana kiume katika vita vilivyo mbele yao, ili wapate kumtukuza Mungu, na kuwanufaisha wanadamu. Ikiwa vijana wangeifanya Biblia kuwa somo lao, wangeweza kutuliza tamaa zao mbaya, na kuisikiliza sauti ya Muumbaji wao, licha ya kuwa na amam na Mungu, hata wangejiona kuwa wameadilishwa na kuzidishwa hadhi. KN 214.2

Chukua nuru po pote uendako; onyesha kuwa unalo kusudi lenye nguvu, kwamba hu mtu wa mashaka, mwenye kupelekwa huko na huko na vishawishi vya marafiki wabaya. Usikubali kwa urahisi mashauri ya wale wenye kumdharau Mungu, lakini jaribu kuongoa, ongoza vema, na kuokoa roho za watu toka maovuni. KN 214.3

Rudia kuomba, ongoza kwa upole na unyenyekevu wa moyo wale wanajipinga wenyewe. Roho ya mtu mmoja anayeokoka kutoka katika kutenda mabaya, na kuletwa chini ya bendera ya Kristo italeta furaha mbinguni, na kutia nyota ya furaha tajini mwako. Mtu aliyeokolewa, kwa njia ya mvuto wake mwema, ataleta watu wengine kuujua wokovu, na kwa hiyo kazi hii itazidi, na mafunuo tu ya siku ile ya hukumu ndiyo yatakayodhihirishwa jinsi kazi hiyo ilivyoenea. KN 214.4

Usisite kumtumikia Bwana kwa uaminifu; maana Mungu atafanya kazi na jitihadi zako. Ataliandika jina lako katika kitabu cha uzima kama mwenye kustahili kuingia katika furaha ya Bwana. 8

Sura ya 36 - Malezi Bora na Mafundisho kwa Watoto Wetu

MTAZAMO wa sasa ulimwenguni ni kuwaacha vijana kufuata nia zao wenyewe kwa kawaida. Na kama wakiwa wakaidi sana katika ujana wao, wazazi husema wataendelea vizuri baadaye kidogo wanapofikisha umri wa miaka kumi na sita au kumi na minane, watayapima mambo wenyewe, na kuacha mazoea yao mabaya, na hatimaye kuwa wanaume na wanawake wenye manufaa. Kosa gani! Kwa miaka mingi humwacha adui kupanda mbegu moyoni; huacha mafundisho mabaya kukua, na mara nyingi jitihada yote ya baadaye itakayofanywa juu ya mtu huyo haitakuwa na mafanikio yo yote. KN 215.1

Shetani ni mwenye hila, fundi hodari, na adui mkubwa. Wakati wo wote neno lisilo la akili likisemwa lenye kuwadhuru vijana, liwe kuwasifu mno wasivyostahili au kuwafanya wasichukie sana dhambi fulani, Shetani hulifaidi na kustawisha mbegu mbaya ipate kutelemsha mzizi na kuzaa mavuno mengi. Wazazi wengine wamewaacha watoto wao kuwa na mazoea mabaya, alama ambazo huweza kuonekana siku zote za maisha. Dhambi hiyo ni juu ya wazazi. Watoto hao waweza kujidai ni Wakristo, walakini, bila kazi maalumu ya neema moyoni na pasipo uongofu kamili maishani mazoea yao ya zamani yataonekana katika mambo yote ya maisha yao, na wataonyesha tabia ile ile ambayo wazazi wao waliwaacha kuwa nayo. 1 KN 215.2

Yawapasa wazazi kuwatawala watoto wao, kuzisahihisha tamaa zao, na kuwatiisha, ama sivyo Mungu atawaangamiza hao watoto siku ya hasira yake kali, na wazazi wasiowatawala watoto wao hawatakosa kuwa na hatia. Hasa ingewapasa watumishi wa Mungu kuwatawala watu wa nyumba zao wenyewe na kuwaweka chini ya utawala mzuri. Naliona kuwa hawako tayari kuhukumu wala kuamua mashauri ya kanisa, kama wasipoweza kutawala vizuri nyumba yao wenyewe. Kwanza hawana budi kuwa na utaratibu nyumbani, ndipo maamuzi yao na mvuto wao vitakuwa na matokeo kanisani. 2 KN 215.3

Kila mwana na binti angeitwa kutoa habari kama akikosekana nyumbani usiku. Yawapasa wazazi kujua marafiki za watoto wao na nyumba ya mtu wanamozitumia saa zao za jioni. 3 KN 215.4

Akili ya mwanadamu haijagundua zaidi ya kile Mungu ajuacho wala kubuni shauri bora zaiai juu ya namna ya kuwatendea watoto kuliko lile lililotolewa na Bwana wetu. Ni nani awezaye kuelewa vizuri zaidi mahitaji ya watoto kuliko Muumbaji wao? KN 215.5

Ni nani awezaye kuyatilia moyo zaidi mambo yao kuliko Yeye aliyewanunua kwa damu yake mwenyewe? Kama neno la Mungu lingesomwa kwa uangalifu na kushikwa kwa uaminifu maumivu makuu ya roho juu ya tabia zilizopotoka za watoto waovu yangepungua. KN 216.1

Watoto wanayo madai ambayo wazazi wao wapaswa kuyajua na kuyajali. Wana haki ya elimu na mafundisho yatakayowafanya kuwa wenye maana, wanaoheshimiwa na wenye kupendwa na watu hapa kuwapa hali ya tabia ya kufaa kwa jamii ya watu safi na watakatifu baada ya hapo. Vijana wangefundishwa kuwa hali yao ya wakati huu na lle ya wakati ujao pia hutegemea sana juu ya mazoea wanayofanya utotoni na katika siku za ujana. 4 KN 216.2

Wanaume na wanawake wanaodai kuheshimu Biblia na kuyashika mafundisho yake hushindwa mara nyingi kutimiza masharti yake. Katika kuwafundisha watoto hufuata tabia zao wenyewe zilizopotoka badala ya mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa wazi. Kukosa kufanya wajibu huo huleta hasara kwa roho za watu maelfu. Biblia imeweka kawaida za malezi bora ya watoto. Kama masharti hayo ya Mungu yangefuatwa na wazazi, tungeona leo jamii ya vijana walio tofauti kabisa wenye kupiga hatua ya juu ya utendaji. Lakini wazazi wanaodai kuwa ni wasomaji wa Biblia na wafuasi wa Biblia wanafanya kinyume kabisa cha mafundisho yake. Tunasikia kilio cha huzuni na maumivu makuu kutoka kwa akina baba na mama wanaosikitikia tabia ya watoto wao, wasifahamu ila kidogo tu kwamba wanajiletea huzuni wao wenyewe na maumivu hayo, na kuwaharibu watoto wao waliopewa na Mungu kwa kutowazoeza watoto wao mazoea mema tokea utotoni. 5 KN 216.3

Watoto ambao ni Wakristo wataupendelea upendo na kibali cha wazazi wao wanaomcha Mungu zaidi ya mibaraka yote mingine ya duniani. Watawapenda na kuwaheshimu wazazi wao. Yafaa njia ya kuwafurahisha wazazi wao iwe mojawapo ya mambo makubwa wanayojifunza maishani mwao. Katika zama hizi za uasi, watoto hawajapata mafundisho na malezi bora, hawajui ila kidogo tu wajibu uwapasao kwa wazazi wao. Mara nyingi ndivyo ilivyo, yaani, kadiri wazazi wao wanavyowatendea mema, ndivyo wanavyozidi kutokuwa na shukrani na kutowaheshimu. KN 216.4

Furaha ya wakati ujao ya watoto wao iko zaidi mikononi mwa wazazi. Kazi kubwa ya kuzirekebisha tabia za watoto hawa ni juu yao, mafundisho yaliyotolewa utotoni yatafuatana nao siku zote za maisha yao. Wazazi hupanda mbegu ambazo zitaota na kuzaa matunda ama kwa wema ama kwa ubaya. Huweza kuwafanya wana na mabinti zao kufaa kwa raha ama kwa hali mbaya sana. 6

Yawapasa Wazazi Kupatana

Watoto wana tabia za kutambua kwa upesi sana, na za upendo. Hupendezwa kwa urahisi na kukasirishwa kwa urahisi. Malezi mazuri ya upole kwa maneno na vitendo akina mama huweza kuwafungamanisha watoto wao na mioyo yao. Kuonyesha ukali na kuwadhulumu watoto ni makosa makubwa. Utawala imara usio wa hasira ni jambo muhimu kwa utii wa watu wa kila nyumba. Sema kile unachonuia kwa utulivu, kata shauri kwa busara, na kutimiza usemalo bila kwenda upande. 7 KN 217.1

Yawapasa wazazi wasisahau miaka yao ya utotoni, jinsi walivyokuwa wakikasirika walipolaumiwa na kukemewa bure. Yafaa wawe watoto tena katika maoni yao na kufahamu mioyoni mwao haja za watoto wao. Lakini, wakiwa imara, na wenye upendo pia, wangetaka utii kutoka kwa watoto wao. Neno la wazazi lingefuatwa kabisa. 8 KN 217.2

Kutokuwa imara katika utawala wa watu wa nyumbani ni jambo lenye madhara makubwa, kwa kweli ni baya karibu sawa na kutokuwa na utawala kabisa. Swali linaloulizwa kila mara ni ya kuwa, Mbona mara kwa mara watoto wa wazazi walio na dini ni wakaidi, wenye dharau, na waasi? Sababu ya hali hiyo hupatikana katika malezi ya nyumbani. KN 217.3

Kama wazazi hawapatani, afadhali waondoke mbele ya watoto wao mpaka hapo watakapoweza kusikilizana. KN 217.4

Ikiwa wazazi wanashirikiana katika kazi hiyo ya malezi, mtoto atafahamu kile anachotakiwa kufanya. Lakini kama baba, kwa neno au kwa mtazamo, huonyesha kuwa hakubaliani na malezi yatolewayo na mama; kama huona kuwa mama ni mkali mno na kudhani kwamba hana budi kumtuliza mtoto kwa kumbembeleza na kumwendekeza, mtoto huyo ataharibika. Atajifunza upesi kuwa aweza kufanya kama apandavyo. Wazazi wafanyao kosa hili kwa watoto, kuharibika kwa roho za watoto wao ni juu yao. 9 KN 217.5

Wazazi wangejifunza kwanza kujitawala, ndipo wanaweza kuwatawala vizuri watoto wao. Kila wakati wanaposhindwa kujitawala, na kuanza kusema na kutenda mambo kwa pupa, hutenda dhambi kwa Mungu. Yafaa kwanza kujadiliana na watoto wao, wayadhihirishe makosa yao, wawaonyeshe dhambi yao, na kuwafanya waone huzuni kwamba licha ya kuwakosea wazazi wao, hata wametenda dhambi kwa Mungu. Mkiwa na moyo laini na uliojaa huruma na masikitiko kwa ajili ya watoto wenu wakosaji, ombeni pamoja nao kabla ya kuwarudi. Ndipo mkiwarudi hawatawachukia. Watawapenda. Wataona kuwa hamwapi adhabu kwa sababu wamewachukiza, wala kwa sababu mwataka kuonyesha chuki yenu juu yao; bali kwa kuwa ni wajibu, kwa ajili ya faida yao, kusudi wasiweze kuachwa kukua dhambini. 10 

Hatari ya Malezi Makali Mno

Kuna watoto wa nyumba nyingi ambao huonekana kuwa wamepata malezi bora nyumbani; wakiwa bado chini ya malezi hayo; lakini jambo linalowaweka chini ya amri likivunjika, huelekea kwamba hawawezi kufikiri, kutenda, na kuamua mambo vizuri wao wenyewe. KN 218.1

Malezi makali ya vijana bila ya kuwafundisha kufikiri na kutenda wao wenyewe kadiri ya uwezo wao na nia yao ilivyo, ili kwa njia hiyo waweze kukua mawazoni, na kuwa na maoni ya kujiheshimu nafsi, na kutumaini kutenda kwa uwezo wao wenyewe, yatazaa siku zote jamii ya watu walio dhaifu wa akili na wa tabia ya moyoni. Nao wakisimama ulimwenguni kutenda mambo kwa faida yao watadhihirisha ukweli kwamba walilelewa kama wanyama, wala hawakufundishwa. Nia zao, badala ya kuongozwa, zilishurutishwa kutii kwa utawala mkali wa wazazi na walimu. Hawa wazazi na walimu wanaojisifu kwamba wanao utawala kamili wa akili na nia za watoto walio chini yao wangeacha kujisifu kama wangeweza kuona maisha ya siku zijazo ya watoto hao ambao wametiishwa kwa nguvu ama kwa hofu. Hao karibu wote si tayari kushiriki kazi ngumu za madaraka za maisha. Walimu wa aina hiyo wanaoridhika kuwa wana karibu utawala kamili wa nia za wanafunzi wao si walimu wenye kufaulu sana, ijapokuwa mambo yanavyoonekana kwa muda mfupi yaweza kuwa yenye kusifiwa kuliko inavyostashili. KN 218.2

Mara nyingi hunyamaza kimya, na kutumia madaraka yao kwa ukali, bila huruma; njia ambayo haiwezi kuipata mioyo ya watoto na wanafunzi wao. Ikiwa wangewakusanya watoto karibu nao, na kuonyesha kuwa wanawapenda, na kudhihirisha kupendezwa kwao katika bidii zote za watoto hata katika michezo yao na hata wakati mwingine kujifanya mtoto miongoni mwa watoto wangewafurahisha sana watoto na wangepata upendo wao na kuwafanya wawatumainie. Mara watoto wangeyaheshimu na kuyapenda madaraka ya wazazi na walimu wao. KN 218.3

Pili haifai kuwaacha vijana kufikiri na kutenda kama wapendavyo wenyewe, bila kutegemea maoni ya wazazi na walimu wao. Yafaa watoto wafundishwe kuheshimu maamuzi ya wenye maarifa na kuongozwa na wazazi na walimu wao. Yawapasa wafundishwe ili nia zao zipate kuungana na nia za wazazi na walimu wao, na kuongozwa ili wapate kuona uzuri wa kulitii shauri lao. Ndipo wakitoka na kuachana na mkono wa kuwaongoza wa wazazi na walimu wao, tabia zao hazitakuwa kama unyasi utikiswao na upepo. 11

Kuwaacha Watoto Kukua Ujingani ni Dhambi

Wazazi wengine wameshindwa kuwapa watoto wao mafundisho ya dini, na hawakujali pia elimu yao ya shuleni. Si vizuri kukosa kujali hata mojawapo ya mambo hayo. Akili za watoto zitakuwa nyepesi, na kama hazijishughulishi kwa kazi za nje, au kushikwa na masomo, zitahatarishwa kwa mivuto mibaya. Ni dhambi kwa wazazi kuwaacha watoto wao kukua ujingani. Yawapasa kuwapatia vitabu vizuri vya manufaa, na wangewafundisha kufanya kazi, kuwa na saa za kazi ya juhudi, na saa za kutumia kwa kujifunza na kusoma. Wazazi wangefanya bidii kuadilisha mioyo ya watoto wao na kuzidisha ubora wa akili zao za kichwani. Akili isipotumiwa, bila kukuzwa kwa kawaida huwa pungufu, ya ufisadi, na mbovu. Shetani hutumia vizuri nafasi yake na kukuza na kuongoza akili za watu wavivu. 12 KN 219.1

Kazi ya mama huanza mtoto akiwa mchanga bado. Yampasa kutuliza nia na hasira ya mtoto wake, na kumtiisha, kumfundisha kutii. Mtoto akizidi kukua, usilegeze mkono. Yafaa kila mama kutwaa wasaa kushauriana na watoto wake, kuwatoa makosa yao, na kuwafundisha kwa uvumilivu njia iliyo bora. Wazazi walio Wakristo wangejua kuwa wanawafundisha na kufanya watoto wao kufaa kuwa watoto wa Mungu. Mambo yote ya maisha ya dini ya watoto hao huongozwa na mafundisho yanayotolewa, na tabia inayofanyizwa na nia ya wazazi, itakuwa shida kujifunza fundisho miaka ya baadaye. Mashindano makali kama nini, vita kali kama nini, kujaribu kuishinda ile nia ambayo kamwe haikulainishwa, ipate kuyatii mapenzi ya Mungu! Wazazi wasiojali kazi hiyo kubwa hufanya kosa kuu, na kutenda dhambi kwa watoto wao maskini na kwa Mungu pia. 13 KN 219.2

Wazazi, mkikosa kuwapa watoto wenu elimu ambayo Mungu ameifanya wajibu wenu kuwapa, itawabidi kumjibu kwa ajili ya matokeo ya baadaye. Matokeo hayo hayataonekana kwa watoto wenu tu. Kama vile mbaruti mmoja ukiachwa kuota shambani unavyozaa mavuno ya namna yake, kadhalika ndivyo dhambi zinazotokana na uzembe wenu zitakavyofanya kazi kuwaharibu wote wanaokutana na mvuto wao. 14 KN 219.3

Laana ya Mungu kwa hakika itawakalia wazazi wasio waaminifu. Licha ya kupanda miiba ambayo itawajeruhi hapa, hata itawabidi kukutana na matokeo ya kukosa kwao uaminifu wakati hukumu itakapokaa. Watoto wengi watainuka hukumuni na kuwashtaki wazazi wao kwa kutowazuia, na kuwashtaki juu ya maangamizo yao. Huruma za bure na upendo wa kijinga wa wazazi huwafanya kuyasamehe makosa ya watoto wao na kuyapita bila kuwarudi, na natimaye watoto wao hupotea, na damu ya roho zao itawakalia wazazi wasio waaminifu. 15 

Ubaya wa Uvivu

Nimeonyeshwa kuwa dhambi nyingi zimetokana na uvivu. Mikono na bongo hodari kwa kazi hazina nafasi kusikiliza kila jaribu ambalo adui huwaletea, lakini mikono na bongo zenye uvivu ziko tayari kabisa kutawaliwa na Shetani. Akili, isiposhughulishwa vizuri, hufikiri mambo mabaya yasiyofaa. Yawapasa wazazi wawafundishe watoto wao kuwa uvivu ni dhambi. 16 KN 220.1

Hakuna jambo linaloelekea sana kutia maovuni zaidi ya kuwaondolea watoto mizigo yote, kuwaacha kuishi kivivu, bila shabaha yo yote, kutofanya lolote, ama kufanya kama wanavyopenda. Akili za watoto zina kazi, na kama zisiposhughulishwa kwa lile lililo jema na lenye manufaa, bila shaka zitageukia baya. Huku likiwa jambo zuri na la muhimu kwao kuwa na michezo wangefundishwa kufanya kazi, kuwa na saa za kawaida kwa kazi ya juhudi na pia kwa kusoma na kujifunza. Ona kwamba wanayo kazi inayowafaa kwa maisha yao na ya kwamba wanapatiwa vitabu vya kufaa vyenye kuwapendeza. 17 KN 220.2

Mara kwa mara watoto huanza kipande cha kazi kwa bidii; lakini, wakitatizwa au kusumbuliwa nayo, hutamani kubadili na kuanza kufanya kitu kingine kipya. Hivyo huenda wakaanza kufanya mambo mengi, walcikutana na jambo la kuwakatisha tamaa, na kuyaacha; kwa hiyo, huacha hili na kuanza kufanya lingine, bila kukamilisha kitu cho chote. Wazazi wasikubali moyo wa kupenda kubadilibadili ukawatawala watoto wao. Haifai washughulikie mambo mengine hata kukosa nafasi kutawala kwa uvumilivu na kukuza akili za watoto. Maneno machache ya kutia moyo au msaada kidogo kwa wakati wa kufaa, huweza kuwaepusha na taabu na tabia ya kukata tamaa; na kuridhika kutakakotokana na kazi waliyoifanya na kuitimiza vizuri kutawatia nguvu kufanya bidii kwa kazi kubwa zaida. 18 KN 220.3

Watoto ambao wameendekezwa na kungojewa, siku zote huitazamia; na kama matumaini yao yasipotimizwa hukatishwa tamaa na kufa moyo. Tabia ya namna hiyo hiyo itaonekana katika maisha yao yote; watakuwa dhaifu, wakiwategemea wengine kwa msaada, wakiwatazamia wengine kuwapendelea na kujitoa kwao. Na kama wakipingwa, hata baada ya kwisha kuwa watu wazima wa kiume na wa kike, wanafikiri kwamba wanatendwa vibaya; na kuharakisha kuingia katika anasa za ulimwengu, na kushindwa kujitegemea; mara nyingi hunung’unika na kuhangaika kwa sababu mambo yote yanawaendea vibaya. 19 KN 220.4

Mwanamke hujifanyia vibaya yeye mwenyewe na pia huwafanyia kosa baya watu wa nyumba yake, akifanya kazi yake na pia akileta kuni na maji, na hata kuchukua shoka ili kuchanja kuni, uku mumewe na wanawe wakakaa mekoni wakistarehe. Kamwe Mungu hakukusudia kwamba wake na mama wawe watumwa wa jamaa zao. Mama wengi husumbuliwa kupita kiasi huku watoto wake wakiwa hawafundishwi kushiriki mizigo ya nyumba. Kama matokeo yake, huzeeka na kufa mapema kabla ya uzee, na kuwaacha watoto wake wakati wake wakati mama anapotakikana sana kuiongoza miguu yao isiyojua kitu. Ni nani astahiliye kulaumiwa? KN 220.5

Yafaa wanaume kufanya yote wawezayo kuwaepusha wake na taabu na kuwafanya wastarehe. Kamwe uvivu usipendelewe wala kuruhusiwa kwa watoto, maana upesi huwa mazoea. 20

Wazazi, Waongozeni Watoto Wenu kwa Kristo

Pengine watoto watataka kutenda mema, huenda wakakusudia mioyoni mwao kuwa watiifu na wema kwa wazazi au walezi wao; lakini huhitaji msaada na maneno ya kuwatia moyo. Wanaweza kuwa na makusudi mema; lakini kama kanuni zinayoyaongoza maisha yao zisipotiwa nguvu kwa dini na maisha yao kuongozwa na neema ya Mungu itiayo nguvu, watashindwa kufaulu. KN 221.2

Yawapasa wazazi kuzidisha maradufu jitihadi zao kwa ajili ya wokovu wa watoto wao. Wangewafundisha kwa uaminifu, wasiwaache kuokota mafundisho yao huko na huko kama wawezavyo. Haifai watoto wadogo kuachwa kujifunza mema na mabaya ovyo bila kutumia busara, kwa kudhani kwamba baadaye mema yatakuwa na nguvu na mabaya yatakosa nguvu. Maovu yatazidi kuongezeka upesi kuliko mema. KN 221.3

Wazazi, mngeanza kuzitawala akila za watoto wenu wakati wangali wadogo sana, hadi mwisho ili wapate kuwa Wakristo. Jitihada zenu zote ziwe kwa ajili ya wokovu wao. Fanyeni kama kwamba wamekabidhiwa kwenu kufanywa wafae kama vito vya thamani kung’aa katika ufalme wa Mungu. Jihadharini msiwatie usingizi wakalala wakiwa katika hatari ya kuangamia kwa kukosea mkidhani kuwa si wenye umri wa kutosha kuwa na hatia, wala wakubwa wa kutosha kutubia dhambi zao na kumkiri Kristo. KN 221.4

Yafaa wazazi kueleza na kuurahisisha mpango wa wokovu kwa watoto wao kusudi akili zao changa zipate kuufahamu. Watoto wa miaka nane, kumi, au kumi na miwili ni wakubwa wakutosha kuzungumuziwa somo la dini la pekee. Msiwafundishe watoto wenu na kuwaelekeza kwenye wakati fulani ujao ambapo watakuwa wakubwa na kutosha; wadogo sana huweza kuona vizuri hali yao kama wakosaji na njia ya wokovu upatikanao kwa Kristo. Wachungaji mara nyingi hawajali hata kiaogo wokovu wa watoto wao; hawafanyi wajibu wao. Nafasi nzuri kuyavuta mawazo ya watoto mara nyingi hupitwa bila kutumiwa vizuri kwa manufaa. 21 KN 221.5

Akina baba na mama, mwafahamu ukubwa wa wajibu wenu? Mwajua inavyowapasa kuwalinda watoto wenu na mazoea ya uzembe yanayoharibu tabia? Msiwaruhusu kutoka nje saa za jioni kama msipojua mahali walipo na kile wanachofanya. Wafundisheni kanuni za usafi wa tabia ya adili. Ikiwa hamkujali kuwafundisha amri juu ya amri, kanuni, nuku kidogo na huku kidogo, anzeni mara moja kufanya wajibu wenu. Twaeni madaraka yenu na kufanya kazi kwa ajili ya muda kitambo na kwa ajili ya milele pia. Msikubali siku nyingine ikapita kabla ya kuungama kosa la kutowajali watoto wenu. Waambieni kuwa mnananuia sasa kutenda kazi mliyopewa na Mungu. Waombeni kushikamana nanyi katika kuongoka nuko. Fanyeni bidii kukomboa mambo ya wakati uliopita. Msikae tena katika hali ya kanisa la Laokidia. Kwa jina la Bwana nawasihi watu wa kila nyumba kujidhihirisha kama ilivyo hasa. Tengeneza kanisa nyumbani mwako mwenyewe. 22 

Usidharau Mahitaji ya Akilini

fslimeonyeshwa kuwa huku wazazi wanaomcha Mungu daima wakiwazuia watoto wao, wangejifunza tabia na moyo wao, na kujaribu kutimiza mahitaji yao. Wazazi wengine hushughulikia mahitaji ya muda ya watoto wao kwa uangalifu sana; huwauguza kwa huruma na uaminifu wanapoumwa, kisha hufikiri kwamba wametimiza wajibu wao. Hapa hufanya kosa. Kazi yao ndipo imeanza tu. Mahitaji ya moyoni yangeangaliwa. Inatakikana akili kutumia dawa ya kufaa kuponya akili za moyoni ambazo zimejeruhiwa. KN 222.2

Watoto wanazo shida ngumu kuchukua uzito katika tabia sawa na zile za watu wazima kwa umri. Wazazi wenyewe hawaoni hivyo saa zote. Akili zao mara nyingi hutatizwa. Hufanya kazi wakiwa na maoni yaliopotoka. Shetani hushindana nao, nao hushindwa na majaribu yake, husema kwa ghadhabu, na kwa njia ya kuichochea hasira kwa watoto wao, na wakati mwingine ni wakali na wenye kunung’unika. Watoto hao, maskini, huambukizwa moyo huo huo, na wazazi hawako tayari kuwasaidia, maana wao ndio asili ya taabu hiyo. Wakati mwingine kila jambo huelekea kwenda vibaya. Kuna uchungu pande zote, na wote wana hali mbaya sana, na taabu. Wazazi huwalaumu watoto wao na kuwadhania kuwa ni wahalifu na wakaidi sana, watoto wabaya kabisa ulimwenguni, hali asili ya fujo hiyo ni wao wenyewe. KN 222.3

Wazazi wengine huleta machafuko mengi kwa kukosa kuizuia hasira. Badala ya kuwauliza watoto kwa upole, kufanya hili au lile, huwaamuru kwa ukali, na mara hiyo kutoa midomoni mwao lawama na makaripio ambayo watoto hawakuyastahili. Wazazi, njia ya namna hiyo ikiruatwa kwa watoto wenu huharibu uchangamfu na nia yao ya kuendelea. Wanatimiza agizo lenu siyo kutokana na upendo, bali kwa sababu hawana la kufanya ila tu kulitimiza. Moyo wao haumo katika shauri hilo. Ni kazi ngumu isiyowapendeza, badala ya kuwa kitu cha kuwapendeza,. na hilo mara nyingi huwafanya kusahau kuyafuata maongozi yenu yote; hilo ni jambo lenye kuwaongezea uchungu, na kulifanya kuwa baya zaidi kwa. watoto. Lawama hurudiwa, na mwenendo wao mbaya kuwekwa mbele yao. KN 222.4

Msiache watoto wenu kuwatazama kwa ghadhabu. Kama wakishindwa na majaribu, na baadaye kuona na kutubu kosa lao, wasameheni kwa urahisi kama mnavyotumaini kusamehewa na Baba yenu aliye mbinguni. Wafundisheni kwa wema, na kuwafungamanisha kwenye mioyo yenu. Ni wakati wa hatari kwa watoto. Mivuto itaenezwa kuwazunguka ili kuwafanya waachane nanyi, jambo ambalo hamna budi Kushindana nalo. Wafundisheni kuwafanya ninyi kuwa tuamini lao. Hebu wanong’one sikioni mwenu shida na furaha zao. Kwa kulitia nguvu jambo hilo mtawaepusha na mitego mingi ambayo Shetani ameiwekea tayari miguu yao isiyojua kitu. Msiwatendee watoto wenu kwa ukali tu, na kusanau utoto wenu ninyi wenyewe, na kukosa kukumbuka kwamba wao ni.watoto tu. Msiwatazamie kuwa wakamilifu wala kujaribu kuwafanya wanaume wazima au wanawake wazima kwa matendo yao mara moja. Kwa kufanya hivyo mtafunga mlango wa kuingilia ambao pengine mngeweza kuwa nao kwao, na kuwalazimisha kufungulia mlango mivuto yenye madhara, na kuacha wengine kutia sumu akili zao changa kabla ya ninyi kuamka na kuiona hatari yao

Kamwe Usiwarudi Watoto Ukiwa Umekasirika

Kama watoto wako ni wahalifu, wangeadhibiwa. Kabla ya kuwaadhibu, jitenge, na kumwomba Mungu kuilainisha na kuituliza mioyo ya watoto wako na kukupa hekima katika kushughulika nao. Kamwe sijaona njia hii kushindwa kufaulu. Huwezi kumfahamisha mtoto mambo ya kiroho wakati moyo (moyo wa mzazi) umejawa na hasira. KN 223.2

Ungewatia adabu watoto wako kwa upendo. Usiwaache kufanya wapendavyo mpaka ukasirike, ndipo kuwarudi. Kuwarudi kwa njia hiyo husaidia tu mabaya, badala ya kuyaponya. KN 223.3

Kuonyesha ukali kwa mtoto mkosaji ni kuzidisha ubaya. Huamsha hasira mbaya ya mtoto na kumwongoza kuona kuwa humjali. Hufikiri kimoyomoyo kuwa usingemtenda hivyo kama ungemjali. KN 223.4

Je, unadhani kwamba Mungu haangalii njia ambayo kwayo watoto hao hutiwa adabu? Ajua, tena ajua kile ambacho kingekuwa matokeo bora ikiwa kazi ya kuwarudi ingefanywa kwa njia ya kuwapata badala ya kuwafukuza. 24 KN 223.5

Ukubwa wa Kuwatendea Watoto Haki Kabisa

Yafaa wazazi wawe vielelezo vya uaminifu, maana hili ndilo fundisho la kila siku la kukuzwa moyoni mwa mtoto. Kanuni imara ingetawala wazazi katika mambo yote ya maisha, hasa katika mafundisho na malezi ya watoto wao. “Hata mtoto hujijulisha kwa matendo yake; kwamba kazi yake ni safi, kwamba ni adili.” KN 224.1

Mama asiye na busara, asiyefuata maongozi ya Mungu, aweza kuwafimdisha watoto wake kuwa wadanganyifu na wanaiiki Dalili za tabia ya namna hiyo zikihifadhiwa zaweza kuendelea bila kubadilika hata kusema uongo kuwe jambo la kawaida kama vile kupumua. Kujisingizia kutakuwa badala ya unyofu na hakika. KN 224.2

Wazazi, kamwe msitoe maneno ya ujanja; kamwe msiseme uongo kwa mafundisho wala kwa kielelezo. Kama wataka mtoto wako awe mwaminifu, uwe mwaminifu wewe mwenyewe. Uwe mnyofu asiyekwenda upande. Hata ujanja kidogo usikubaliwe. Kwa sababu mama anazoea kutoa maneno ya ujanja na kuwa muongo, mtoto hukifuata kielelezo cha mama. KN 224.3

Basi, ni muhimu kwamba uaminifu utumiwe katika mambo yote ya maisha ya mama, na ni jambo la maana katika malezi ya watoto kuwafundisha vijana wa kike na wa kiume pia wasitoe maneno ya ujanja kudanganya hata kwa neno lililo dogo kabisa. 25 

Ukubwa wa Maendeleo ya Tabia

Mungu amewapa wazazi kazi yao, kufanyiza tabia za watoto wao zifanane na Kielelezo Kitakatifu. Kwa neema yake wanaweza kuitimiza kazi hiyo; lakini itatakikana uvumilivu, na bidii ya kazi, nia thabiti, bila kulegea, kuiongoza nia na kuzizuia tamaa mbaya. Shamba likiachwa bila kulimwa huzaa tu miiba na mbigili. Apendaye kupata mavuno ya manufaa au mazuri hana budi kwanza kuutayarisha udongo na kupanda mbegu, kisha apalilie miche, na kuondoa kwekwe na kuulainisha udongo, ndipo mimea ya thamani itasitawi na kumlipa maridhawa kwa masumbuko na kazi yake aliyoifanya. KN 224.5

Kuijenga tabia ndiyo kazi yenye maana sana waliyopata kukabidhiwa wanadamu na kamwe uchunguzi mkali wa kazi niyo haujapata kuwa jambo kubwa kama ilivyo sasa. Kamwe vizazi vilivyopita havikutakiwa kuyakabili mashindano makubwa namna hii; kamwe viiana wa kiume na wa kike hawakupambana na hatari zilizo kubwa kama wanavyokutana nazo siku hizi. 26 KN 224.6

Nguvu ya tabia ina mambo mawili-uwezo wa nia, na uwezo wa kujitawala nafsini. Vijana wengi hukosea na kuita tamaa isiyozuilika nguvu ya tabia; lakini ukweli ni kwamba mwenye kutawaliwa na tamaa yake ni mtu dhaifu. Ukuu halisi na ubora wa mtu hupimwa kwa uwezo wa maoni ya moyoni anayoyashinda, siyo kwa uwezo na wa maoni ya moyoni yanayomshinda. Mtu hodari ni yule, ambaye, huku akiwa mwepesi kutukanwa, lakini, ataizuia hasira na kuwasamehe adui zake. Watu kama hao ni mashujaa kweli kweli. KN 224.7

Wengi wanayo mawazo kidogo sana ya vile wawezavyo kuwa hata wataendelea kudumaa na kukonda, ambapo, kama wangetumia vizuri uwezo waliopewa na Mungu, huenda wangeweza tabia bora na kutoa mvuto ambao ungeongoa watu kwa Kristo. Elimu ni uwezo; lakini uwezo wa akili bila wema wa moyoni, ni uwezo kwa mabaya. KN 225.1

Mungu ametupa sisi uwezo wetu wa akilini na wa tabia ya moyoni, lakini zaidi sana kila mtu yu fundi mjenzi wa tabia yake mwenyewe. Kila siku jengo huzidi kupanda juu. Neno la Mungu hutuonya tujihadhari jinsi tujengavyo, tuone kuwa jengo letu limewekwa msingi wake juu ya Mwamba wa milele. Utakuja wakati ambapo kazi itadhihirika kama ilivyo hasa. Sasa ndio wakati kwa wote kukuza uwezo ambao Mungu amewapa, ili wapate kufanyiza tabia za kufaa hapa, na kwa maisha bora zaidi ya baadaye. KN 225.2

Kila tendo la maisha, ingawa liwe dogo kama nini, lina mvuto wake katika kuifanyiza tabia. Tabia njema ni yenye thamani zaidi kuliko mali za dunia, na kazi ya kuifanyiza ndiyo kazi bora kabisa ambayo wanadamu huweza kuifanya. Tabia zinazofanyizwa kwa hali ya mambo yalivyo hubadilika na ni mbaya kabisa. Wenye tabia hizo hawana shabaha bora wala kusudi maishani. Hawana mvuto unaoadilisha tabia za wengine. Hawana kusudi wala uwezo. KN 225.3

Muda mfupi wa maisha tuliowekwa hapa ungetumiwa vizuri kwa busara. Mungu apenda kanisa lake liwe hai, lililojitoa wakfu, lenye kufanya kazi. Lakini watu wa kanisa letu wako kinyume kabisa cha hayo wakati huu. Mungu ahitaji watu wenye nguvu, hodari, Wakristo wenye nguvu na bidii, wenye kumfuata Kielelezo wa kweli, na ambao watatoa mvuto wa nguvu kwa ajili ya Mungu na nuru. Bwana ametukabidhi amana takatifu, yenye maana sana na maneno mazito ya kweli, nasi tungeonyesha mvuto wake kwa maisha na tabia zetu. 27 

Mambo Yaliyompata Mtu Mwenyewe Katika Kuwaonya Watoto

Mama wengine hawana kanuni katika kuwatendea watoto wao. Wakati mwingine huwaendekeza kwenye madhara, na pengine huwakataza furaha nzuri ambayo ingewapendeza sana watoto moyoni. Kwa kufanya hivi hawamwigi Kristo; Yeye aliwapenda watoto; aliyafahamu mawazo yao ya moyoni na kuwahurumia katika furaha zao na katika taabu zao. 28 KN 225.5

Watoto wakiomba ili waende kwa marafiki hawa au kujiunga na kundi lile la wachezaji, huwaambia: “Siwezi kuwaruhusu mwende, watoto; ketini hapa; nami nitawaambia sababu. Nafanyia kazi uzima wa milele na namfanyia Mungu kazi. Mungu amempa ninyi kama watoto wangu; kwa hiyo sina budi kuwaangalia kama mtu atakayetakiwa kutoa habari siku ya hukumu ya Mungu. Je, mwataka jina la mama yenu kuandikwa katika vitabu vya mbinguni kama mtu aliyeshindwa kufanya wajibu wake kwa watoto wake, kama mtu mwenye kumwacha adui kuingia na kutangulia kutwaa mahali ambapo yanipasa kupatwaa? Watoto, nitawaambia njia iliyo bora, ndipo mkichagua kumwasi mama yenu na kufuata njia za maovu, mama yenu hatakuwa na hatia, bali mtaangamia kwa ajili ya dhambi zenu wenyewe.” KN 225.6

Hii ndiyo njia niliyotumia kwa watoto wangu, na kabla ya kumaliza kusema, walilia, na kupenda kusema, “Je, hutatuombea?” Naam, kamwe sikukataa kuwaombea. Nalipiga magoti karibu nao na kuomba pamoja nao. Kisha nalijitenga na kumwomba Mungu mpaka jua likapanda juu angani, usiku kucha, ili nguvu ya mvuto wa yule adui zipate kuvunjwa, nami nimepata ushindi. Ijapokuwa ilinlgharamisha kazi ya usiku mzima, lakini naliona nimelipwa kabisa wakati watoto wangu walipoweza kuning’inia shingoni mwangu na kuniambia, “Ah, Mama, twafurahi sana kwamba hukuturuhusu kwenda wakati tulipotaka kufanya hivyo. Sasa twaona kuwa ingekuwa vibaya.” KN 226.1

Wazazi, hii ndiyo njia iwapasayo kuitumia, kana kwamba mwainuia. Hamna budi kuifanya hiyo kuwa kazi yenu ikiwa mwatazamia kuwaokoa watoto wenu katika ufalme wa Mungu. 29 KN 226.2

Kamwe mafundisho mazuri hayawezi kutolewa kwa vijana katika nchi hii, wala katika nchi yo yote nyingine isipokuwa wametengwa mbali na miji mikubwa. Desturi na mazoea mijini huzifanya akili za vijana zisifae kuingiliwa na ukweli. 30

Haja Kubwa ya Wazazi ya Maongozi Ya Mungu

Hamwezi kutoyajali malezi bora ya watoto wenu, bila ya hofu ya kupata adhabu ama matokeo mabaya baadaye. Tabia zao zilizoharibika zitatangaza kukosa uaminifu kwenu. Mabaya msiyoyasahihisha, tabia mbaya, zisizo za adabu, kukosa heshima na kutotii, mazoea ya uvivu na kutojali, yataletea majina yenu fedheha na uchungu maishani mwenu. Mwisho wa watoto wenu utakavyokuwa ni katika mikono yenu zaidi. Mkikosa kufanya wajibu wenu mwaweza kuwaweka upande wa yule adui na kuwafanya mawakili wake katika kuwaharibu wengine; ambapo, kama mkiwafundisha kwa uaminifu, ikiwa katika maisha yenu wenyewe mwawaonyesha kielelezo chema, mwaweza kuwaongoza kwa Kristo, hao nao kwa zamu yao watawavuta wengine na hivyo wengi huweza kuokoka kwa njia yenu. 31 KN 226.4

Mungu ataka sana tuwatendee watoto wetu kwa moyo mnyofu. Twaelekea kusahau kuwa watoto hawajapata kuwa na miaka mingi ya malezi ambayo watu wazima kwa umri wamekuwa nayo. Kama watoto wasipofanya sawasawa na mawazo yetu kwa kila jambo, pengine twafikiri kuwa wanastahili kukaripiwa. Lakini hilo halitasawazisha mambo. Wapelekeni kwa Mwolcozi, mwambieni habara zote; kisha amini kwamba mbaraka wake utawakalia. 32 KN 227.1

Yafaa watoto kufundishwa kuiheshimu saa ya maombi kwa kicho. Kabla ya kuondoka nyumbani kwenda kazini, wote wa nyumbani wangeitwa mahali pamoja, na baba, au mama wakati baba asipokuwapo, angemwomba Mungu kwa bidii kuwalinda siku hiyo. Njoo kwa unyenyekevu moyo ukijawa na utu wema na kujua majaribu na hatari zilizo mbele yenu wenyewe na mbele ya watoto wenu, kwa imani wafungeni juu ya madhabahu mkiwaombea ulinzi wa Mungu. Malaika wahudumuo watawalinda watoto ambao wametolewa wakfu kwa Mungu kwa njia hiyo. Ni wajibu wa wazazi Wakristo, asubuhi na jioni kwa kuomba kwa bidii na imani daima, kufanya kitalu kuwazunguka watoto wao. Yafaa wawaamuru kwa uvumilivu, kwa upole na kuwafundisha bila kuchoka namna ya kuenenda ili kumpendeza Mungu. 33 KN 227.2

Wafundishe watoto wako kuwa wamejaliwa kupata kila siku ubatizo wa Roho Mtakatifii. Hebu Kristo akupatie kuwa u mkono wake wenye kumsaidia kuyatimiza makusudi yake. Kwa sala waweza kupata jambo ambalo litaifanya huduma yako kwa watoto wako kufaulu kabisa. 34 KN 227.3

Uwezo wa sala mama hauwezi kuthaminiwa mno kupita vile unavyostahili. (Mwanamke) mwenye kupiga magoti kando ya mwana na binti yake siku zote za mabadiliko ya utotoni, katika hatari za ujana, kamwe hatajua mpaka siku ya hukumu, mvuto wa sala zake juu ya maisha ya watoto wake. Kama akiungana kwa imani na Mwana wa Mungu, mkono wa upendo wa mama, waweza kumzuia binti yake asijifurahishe kwa anasa dhambini. Tamaa mbaya ikitaka kushinda, uwezo wa upendo, mvuto wa wenye kuzuia, wa kweli, thabiti huweza kuitegemeza roho upande wa mema. 35 KN 227.4

Baada ya kufanya wajibu wako kwa uaminifu kwa watoto wako, ndipo wapeleke kwa Mungu na kumwomba kukusaidia; Mwambie kuwa umefanya sehemu yako, na kisha kwa imani mwombe Mungu kufanya sehemu yake, ambayo huiwezi. Mwombe kugeuza tabia zao, kuwapunguza ukali na kuwafanya wapole kwa Rono Mtakatifu. Atakusikia ukiomba. Atapenda kuyajibu maombi yako. Kwa njia ya Neno lake amekuamuru kuwarudi watoto wako, “wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia” kwao nalo Neno lake lapaswa kufuatwa katika mambo haya. 36

Fundisha Heshima na Adabu

Mungu ameamuru hasa heshima nzuri kwa wazee. Asema, “Kichwa chenye mvi ni taji ya utukufu, kama kikionekana katika njia ya haki” mithali 16:31. Huonyesha vita vilivyokwisha kupiganwa na ushindi uliopatikana; mizigo iliyobebwa, na majaribu yaliyopingwa. Huonyesha miguu iliyochoka ikikaribia pumziko lao, na juu ya mahali ambapo si muda mrefu pataachwa tupu. Wasaidie watoto kufikiri hivyo, nao watayalainisha mapito ya wazee kwa adabu na heshima zao, na watajiletea neema na uzun katika maisha yao ya ujana kadiri wanavyoitii amri huu, “Mwondokeeni mtu mwenye mvi; heshimuni uso wa mtu mzee.” Mambo ya Walawi 19::32. 37 KN 228.1

Pia adabu, ni mojawapo ya karama za Roho, nayo ingekuzwa na wote. Ina nguvu ya kulainisha tabia ambazo pasipo hiyo zingeendelea kuwa nguvu na zisizo za heshima. Wale wanaodai kuwa ni wafuasi wa Kristo, na huku wakiwa watu wasio na adabu, wakali, na wasio na heshima, hawajajifunza bado juu ya Yesu. Pengine unyofu wao hauwezi kuonewa mashaka, wala uaminifu wao kutosadikiwa sana; lakini unyofu na uaminifu hautaridhisha kwa sababu hauna utu wema na adabu. 38 

Wajibu wa Kanisa

Wakati wa usiku nalionyeshwa kundi kubwa la watu ambapo jambo la elimu lilikuwa likijadiliwa na kutia wasiwasi akilini mwa watu wote waliokuwako. Mmoja ambaye amekuwa mwalimu wetu muda mrefu akawa akiwahutubia watu hao. Akasema: “Jambo hili la elimu lingekuwa lenye kulipendeza kanisa zima la Waadventista Wasabato.” 7 KN 230.2

Kanisa lina kazi maalum ya kufanya katika kuwaelimisha na kuwalea watoto wake ili kwa kuhudhuria shule au kuwa katika iamii yoyote nyingine wasiambukizwe na wale wenye mazoea mabaya. Ulimwengu umejaa maovu na kutojali masharti yake Mungu. Miji imekuwa Sodoma, na watoto wetu kila siku huhatarishwa kwenye maovu mengi. Wale wenye kuhudhuria shule za serikali mara nyingi hushirikiana na wengine waliotupwa zaidi, wale ambao, kando ya wakati unaotumiwa darasani, huachwa kupata elimu hafifu. Mioyo ya vijana huvutwa kwa urahisi, na kama mazingira yao yasipokuwa ya tabia nzuri, Shetani atawatumia hawa watoto waliotupwa ovyo kuwaambukiza wenzao ambao wamelelewa kwa uangalifu zaidi. Hivyo, kabla ya wazazi waishikao Sabato kujua kile kinachotendeka, mafundisho ya upotevu hujifunzwa, na roho za watoto wao wadogo huharibiwa. KN 230.3

Jamaa wengi, ambao, kwa kusudi la kuwaelimisha watoto wao, huhamia mahali ambapo kuna shule zetu kubwa, wangemfanyia Bwana kazi njema kama wangebaki mahali walipo. Yawapasa kulitia moyo kanisa ambalo ndipo ulipo ushirika wao kuanzisha shule ya kanisa mahali watoto wao wawezapo kupokea elimu bora ya Kikristo, yenye ulinganifu. Ingekuwa bora kabisa kwa ajili ya watoto wao, kwa ajili yao wenyewe, na kwa ajili ya kazi ya Mungu, kama wangedumu kukaa kwenye hayo makanisa madogo zaidi, mahali msaada wao unapohitajiwa, badala ya kwenda katika makanisa makubwa, ambapo, kwa sababu ya kutotakikana huko, kuna hatari siku zote ya kutumbukia kwenye jaribu la ulegevu wa kiroho. KN 230.4

Po pote penye wachache waishikao Sabato, wazazi wangejiunga kutayarisha mahali pa shule ya kutwa ambapo wanafunzi huhudhuria mchana na kulala makwao, mahali watoto na vijana wawezapo kufundishwa. Yafaa wamwajiri mwalimu Mkristo, ambaye, kama mmishenari aliyejitoa wakfu kwa Mungu, atawae-limisha watoto kwa njia ambayo itawaongoza kuwa wamishenari. 8 KN 230.5

Tumo chini ya agano zito na lililo takatifu kwa Mungu kuwalea watoto wetu kwa ajili yake wala si kwa ajili ya walimwengu; kuwafundisha wasishikamane na walimwengu bali wampende na kumcha Mungu na kuzishika amri zake. Yapasa watiwe mioyoni mwao wazo hili, waone kuwa wameumbwa kwa sura ya Mungu aliye Muumbaji wao na ya kwamba Kristo ndiye kielelezo chema ambacho wamepaswa kukifuata, ili kufanana naye. Uangalifu mwingi watakikana sana juu ya elimu ambayo ltawafunuha na kuwajulisha habari za wokovu, na kufanya maisha na tabia ya mtu ifanane na ile ya Mungu mwenyewe. 9 KN 231.1

Ili kutimiza haja ya watenda kazi, Mungu anataka sana kuwa vyuo vikuu vianzishwe katika nchi mbalimbali mahali wanafunzi wa ahadi wawezapo kuelimishwa juu ya sehemu za elimu ifaayo na katika kweli ya Biblia. Kadiri watu hawa wanavyoshughulika kazini, ndivyo watakavyoifanya kazi hii ya neno la kweli kwa wakati huu iwe kama ipaswavyo na kutofautikiana na kazi zingine mahali papya. KN 231.2

Isipokuwa tu kwa habari ya elimu ya wale ambao hawana budi kutumwa nje kama wamishenari, ingefaa watu wa sehemu za nchi mbalimbali ulimwenguni wafundishwe kufanya kazi kwa watu wa kwao, miongoni mwa majirani zao wenyewe; kadiri iwezekanavyo ni bora na salama zaidi kwao kupata elimu mahali pale pale watakapofanyia kazi. Isipokuwa mara chache tu, si vizuri, licha kwa mtenda kazi mwenyewe, hata kwa ajili ya maendeleo ya kazi, kwenda kusomea nchi za mbali. 10 KN 231.3

Kama kanisa, kama mtu mmoja mmoja peke yake, tukipenda kusimama bila hatia hukumuni, hatuna budi kujitahidi zaidi kwa moyo kuwaelimisha vijana wetu, ili wafae zaidi kwa sehemu mbalimbali za kazi hii kubwa iliyowekwa mikononi mwetu. Yatupasa tufanye mipango kwa busara, ili wale wenye talanta ya akili wapate kuimarishwa akili zao na kuadilishwa na kupewa malezi mema hata wawe na ubora sawa na ule wa mbinguni, ili kazi ya Kristo isipingwe kwa ajili ya utovu wa watenda kazi waelekevu, ambao wataifanya kazi yao kwa bidii na uaminifu. 11

Msaada wa Tabia ya Uadilifu katika Vyuo Vyetu

Yafaa baba na mama kushirikiana na mwalimu kazini kwa bidii kwa ajili ya uongofu wa watoto wao. Hebu wajitahidi kudumisha moyo wa kupendezwa na mambo ya kiroho na matakatifii nyumbani na kuwalea watoto wao katika malezi na maonyo ya Bwana. Hivyo ndivyo wawezavyo kuifanya saa ya mafimdisho kuwa ya kupendeza na yenye faida, na matumaini yao yataongezeka kwa njia hii ya kuutafuta wokovu wa watoto wao. 12 KN 231.5

Baadhi ya wanafunzi hurejea nyumbani wakiwa na manung’uniko, na wazazi na washiriki wa kanisa huyasikiliza maneno yao yaliyotiwa chumvi, yasiyo ya haki. Ingekuwa bora kama wangefikin kuwa hadithi ina pande mbili; lakini badala ya kufanya hivyo, hukubali rioti hizo zilizopotoka kujenga kizuizi baina yao na chuo hicho kikuu. Ndipo huanza kuonyesha hofu, mashaka, na shuku juu ya njia inayotumiwa kukiendesha chuo hicho. Mvuto wa namna hiyo huleta madhara makubwa. Maneno ya kutoridhika huenea kama ugonjwa unaoambukiza, na ushawishi ufanywao mawazoni ni shida kuuondoa kabisa. Uvumi huzidi kila mara mpaka kuwa mkubwa mno, ambapo uchunguzi ungeonyesha ukweli kwamba walimu hawakuwa na kosa wala walimu wakuu wa chuo hicho. Walikuwa wakifanya tu wajibu wao katika kuzitilia nguvu amri za shule, ambazo hazina budi kutimizwa, ama sivyo shule itachafuliwa. KN 232.1

Ikiwa wazazi wangejiweka mahali pa walimu na kuona jinsi inavyolazimu kuwa vigumu kuongoza na Kutawala shule ya wanafunzi mamia wa kila darasa na wa aina mbalimbali, huenda wakayaona mambo namna nyingine. Wangefikiri kuwa watoto wengine kamwe hawakupata malezi mema nyumbani. Kama watoto hao ambao wametupwa ovyo na wazazi wasio waaminifu wasipofanyiwa kitendo, kamwe hawatakubaliwa na Yesu; isipokuwa uwezo fulani wa kuwatawala unaletwa kuwasaidia, hawatakuwa na maana katika maisha haya wala hawatashiriki maisha ya wakati ujao. 13 KN 232.2

Baba na mama wengi hukosa kwa kulegeza bidii ya mwalimu mwaminifu. Vijana na watoto, kwa uwezo wa kufahamu usio kamili na maamuzi yao machanga hawawezi siku zote kufahamu mipango na njia zote za mwalimu. Lakini, wanapoleta nyumbani ripoti za mambo yasemwayo na kufanywa katika shule, hayo huzungumzwa na wazazi katika jamii ya watu wa nyumbani, na matendo ya mwalimu hulaumiwa bila kizuizi. Hapo watoto hujifunza mafundisho ambayo si vyepesi kujifunzwa. Wakati wo wote wanapopaswa kujizuia wasivyozoea, au kutakiwa kujifunza mambo magumu, huwalalamikia wazazi wao wasio na busara ili wawahurumie na kuwaendekeza. Hivi ndivyo moyo wa wasiwasi na kutokuridhika unavyotiwa nguvu, na shule nzima huumia kwa sababu ya mvuto huo ambao huichafua na mzigo wa mwalimu huzidi kuwa mzito. Lakini, hasara iliyo kubwa zaidi ni kwa watoto wenyewe wenye kufundishwa hivi na wazazi wao. Makosa ya tabia ambayo malezi mazuri yangeweza kuyasahihisha, huachwa kupata nguvu kadiri miaka iendavyo, kuharibu na pengine kuangamiza kabisa manufaa ya yule aliyo nayo. 14

Walimu Chini ya Mungu

Bwana hutenda kazi pamoja na mwalimu aliyejitoa wakfu; na ni kwa faida ya mwalimu mwenyewe kulifahamu neno hili. Walimu ambao wako chini ya utawala wa Mungu hupokea neema na kweli na nuru kwa njia ya roho Mtakatifu kuipitisha kwa watoto. Wako chini ya Mwalimu mkuu kabisa aliyepata kuwako ulimwenguni, na ingekuwa vibaya kama nini wakiwa na roho isiyo njema, sauti kali, na kujawa na chuki! Kwa jambo hili wangedumisha makosa yao wenyewe kwa watoto wao. KN 233.1

Mungu atazungumza na roho ya mtu kwa njia ya Roho Mtakatifu. Omba unapokuwa ukijifunza, “Unifumbue macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako” (Zab. 119:18). Mwalimu atakapomtegemea Mungu kwa maombi, Roho ya Kristo itamshukia, na Mungu atafanya kazi kwa njia yake kwa Roho Mtakatifu kwenye akili za mwanafunzi. Roho Mtakatifu huzijaza akili tumaini na moyo mkuu na maneno ya Biblia, ambayo yatapitishwa kwa mwanafunzi. Maneno ya kweli yataendelea kuwa na maana, nayo yatapanuka na kupata ukamilifu wa maana ambayo kamwe hajaota habari zake. Uzuri na sifa ya neno la Mungu vina mvuto unaoongoa akili na tabia; macheche ya upendo wa mbinguni yataanguka juu ya mioyo ya watoto kama maongozi ya Mungu Twaweza kuleta mamia na maelfu ya watoto kwa Kristo kama tukitende kazi ya kuwavuta kuja kwake. 15 KN 233.2

Kabla watu hawajaweza kuwa na akili hasa, yawapasa kufahamu tegemeo lao kwa Mungu, na kujazwa na hekima yake. Mungu ndiye chimbuko la akili na nguvu za kiroho pia. Watu mashuhuri amoao wamefikia vyeo vya juu sana vya elimu, kama waonavyo, hawawezi kulinganishwa na Yohana, mwanafunzi mpendwa wa Yesu wala mtume Paulo. Akili na nguvu za kiroho zikiunganishwa ndipo cheo cha juu sana maishani kinapoweza kufikiwa. Wale wafanyao hivi, Mungu atawakubali kama watenda kazi pamoja naye katika kuwaelimisha wengine. 16 KN 233.3

“Kazi kubwa sana ya jamii ya shule zetu wakati huu ni kuwaonyesha walimwengu kielelezo chema ambacho humtukuza Mungu. Malaika watakatifu huiongoza na kuisimamia kazi hiyo kwa njia ya wanadamu, na kila idara ya kazi hiyo haina budi kuwa na alama ya ubora mtakatifu. 17 

Sifa za Mwalimu wa Shule

Pateni mtu aliye hodari awe mkuu wa shule yenu, mtu ambaye nguvu za mwili wake zitamsaidia kufanya kazi kikamilifu kama mtawala ama mlezi mwema; mtu ambaye anastahili kuwalea watoto na kuwafanya wawe na mazoea mema ya utaratibu, unadhifu na utendaji wa kazi. Tenda kazi kikamilifu kwa lo lote ufanyalo. Karna ukiwa mwaminifu katika kuwafundisha mafundisho ya kawaida wanafunzi wako wengi wataweza kutoka shuleni na kusnika kazi kama wainjilisti. Hatuna sababu ya kufikiri kuwa ni lazima watenda kazi wote wawe na elimu ya juu. 18 KN 233.5

Katika kuwachagua walimu, yatupasa tuangalie sana kabla hatujawachagua, tukijua kuwa hili ni jambo kubwa, la dini, kama ilivyo katika kuwachagua watu kwa kazi ya uchungaji wa kanisa. Watu wenye busara ambao wanaweza kupambanua tabia za watu wangefanya uchaguzi huo; kwa kuwa mwenye kipawa bora sana ndiye anayetakiwa kuwaelimisha na kuwaadilisha watoto, na kuendesha kazi mbalimbali zitakazobidi kutendwa na walimu katika shule zetu za kanisa Msiweke walimu vijana, wasio na utawala; kwa kuwa jitihada zao zitaleta machafuko. 19 KN 234.1

Pasiwepo mwalimu anayeajiriwa, isipokuwa mmemshuhudia na kumpima kwa majaribio, mkaona kuwa anampenda na kumcha Mungu. Kama walimu wamefundishwa na Mungu, na kama mafundisno yao kila siku hutokana na Kikristo, watafanya kazi ya Kristo. Watawaongoa watu pamoja na Kristo; kwa kuwa kila mtoto na kila kijana ni mwenye thamam kuu. 20 KN 234.2

Yafaa mazoea na kanuni za mwalimu zikumbukwe kuwa ni mambo makubwa kuliko elimu yake. Kusudi awe na mvuto yampasa ajitawale kabisa yeye mwenyewe, na moyoni mwake mwenyewe ajawe na upendo kwa wanafunzi wake, ambao utaonekana katika uso, maneno, na matendo yake. 21 KN 234.3

Yampasa mwalimu siku zote afanye kiungwana kama Mkristo mwema. Yampasa awe na moyo wa kirafiki na mshauri mwema kwa wanafunzi wake. Kama watu wote wa kanisa letu walimu, wachungaji, na washiriki wa kanisa wangekuza moyo wa uadilifu na adabu ya Kikristo, wangepata kwa urahisi zaidi njia ya kuifikia mioyo ya watu; wengi zaidi wangeongozwa kulichunguza na kulipokea neno la kweli. Kila mwalimu atakapowafikiria wengine kuliko nafsi yake mwenyewe, na kupendelea sana maendeleo na mafanikio ya wanafunzi wake, akijua kuwa wao ni mali ya Mungu, na ya kwamba hana budi kutoa habari za mvuto wake juu ya nia na tabia zao, ndipo tutakuwa na shule ambayo malaika watapenda kukaa humo bila kuondoka upesi. 22 KN 234.4

Shule zetu zahitaji walimu wenye sifa bora za uadilifu; wale ambao huweza kuaminiwa; wale ambao wana nguvu katika imani, na wenye akili na uvumilivu; wale wenye kutembea pamoja na Mungu, na kujiepusha na hatua ya kwanza kabisa ya maovu. KN 234.5

Kuwaweka watoto wetu wadogo kwa walimu wenye kiburi na wasio wazuri ni dhambi. Mwalimu wa aina hiyo atasababisha madhara makubwa kwa hao ambao hukuza tabia kwa upesi. Kama walimu hawamtii Mungu, ikiwa hawana upendo kwa watoto wanaowaongoza, au kama huonyesha upendeleo kwa wale wenye sura zinazowapendeza, kutowajali wale wasio wazuri wa sura, wala wale walio watukutu na dhaifu, haifai kuajiriwa; maana kazi yao itamletea Kristo hasara ya roho za watu. Huhitajiwa, hasa kwa watoto, walimu ambao ni watulivu na wema, wanaoonyesha uvumilivu na upendo kwa wale hasa wanaouhitaji sana. 23 KN 234.6

Mwalimu atapoteza kiini hasa cha elimu, kama asipofahamu haja yake ya maombi, na kunyenyekea moyoni mwake mbele za Mungu. 24 KN 235.1

Ukubwa wa sifa za afya ya mwalimu ni vigumu kuudhania kuwa jambo kubwa kuliko ulivyo; kwa kuwa kadiri afya yake inavyozidi, ndivyo na kazi yake itakavyozidi kukamilika. Akili haziwezi kuflkin barabara na kuwa na nguvu kutenda kazi ikiwa nguvu za mwili zimedhurika kwa sababu ya udhaifu au ugonjwa. Moyo hushindwa na mawazo; lakini ikiwa, kwa sababu ya udhaifu wa mwili, ubongo kupotewa na nguvu zake, hapo ndipo njia ya maoni bora ya moyoni na makusudi safi itakuwa imezuiwa, na mwalimu hawezi tena kupambanua baina ya jema na baya. Ukiumwa na ugonjwa, si jambo rahisi kufurahi, wala kufanya kazi kwa uaminifu na haki. 25

Biblia Katika Elimu ya Kikristo

Kama njia ya kuelimisha, Biblia ni yenye matokeo zaidi ya kitabu kinginecho, au vitabu vyote vingine vikiunganishwa pamoja. Ubora wa maneno yake makubwa, na mepesi kueleweka, uzuri wa maneno yake yanayoleta mifano akilini, hutia nguvu na kukuza akili kuliko cnochote kingine. Hakuna mafundisho mengine yawezayo kutoa elimu kama bidii ya kuyafahamu maneno ya kweli ya mafunuo hayo. Akili ambazo zimeunganishwa na nia ya Mungu jinsi hiyo zitazidi tu kupata nguvu. KN 235.3

Pia uwezo wa Biblia una nguvu zaidi katika maendeleo ya hali ya kiroho. Binadamu, ambaye ameumbwa kusudi ashirikiane na Mungu, aweza tu kupata uzima na maendeleo yake halisi, kwa ushirika wa namna hiyo. Akiwa ameumbwa kwa namna inayomwezesha kupata fursaha yake ilio bora sana kwa Mungu, kile ambacho chaweza kutuliza kiu cha moyo hawezi kukipata kwa njia nyingine iwayo yote. Yeye ambaye kwa unyofu na uelekevu wa moyo hujifunza Neno la Mungu, akitaka kufahamu ukweli wake, atamfahamu Muumbaji wake; na isipokuwa kwa hiari ya mtu mwenyewe, hakuna kikomo cha uwezekano wa maendeleo yake. 26 KN 235.4

Hebu mafungu ya Maandiko Matakatifu yenye maana inayohusiana zaidi na mafundisho yanayotolewa yakaririwe hata yaweze kukumbukwa, si kama kazi ngumu, bali kama kitu cha faida. Ingawa mara ya kwanza huenda uwezo wa kukimbuka ukawa na upungufu, lakini, utapata nguvu kwa kuzoezwa, ili baada ya muda upendezwe kuyaweka moyoni maneno ya kweli. Nayo mazoea haya yatasaidia sana kukua kiroho. 27

Hatari Katika Kuwapeleka Watoto Shuleni Wakiwa Wangali Wadogo Sana

Kama wale waliokaa Edeni walivyojifunza kutoka kwa viumbe vya asili, kama Musa alivyouona mwandiko wa Mungu juu ya tambarare na milima ya Arabia, na kama Mtoto Yesu alivyoona juu ya mitelemko ya vilima vya Nazareti, ndivyo siku hizi wawezavyo kuona na kujifunza habari za Mungu. Mambo yale yasiyoonekana hufafanuliwa na yale yanayoonekana. KN 236.1

Basi, kadiri iwezekanavyo, mtoto awekwe tokea utotoni kabisa mahali ambapo kitabu hiki cha ajabu cha mafundisho kinweza kufunuliwa mbele yake. 28 KN 236.2

Msiwapeleke watoto wenu shuleni mapema mno. Yafaa mama aangalie sana jinsi anavyomwamini mtu mwingine kumfundisha mtoto wake mchanga, na kukuza tabia yake. Yawapasa wawe walimu bora kabisa wa watoto wao mpaka watoto wafikishapo umri wa miaka minane au kumi. Chumba chao cha kusomea kingekuwa nje, katika maua na ndege, na kitabu cha mafundisho yao kingekuwa viumbe wa asili. Mara wawezapo kufahamu kwa akili zao wenyewe, wazazi wawafunulie kitabu hiki kikubwa cha Mungu cha viumbe. Mafundisho haya yatolewayo mahali pa namna hii hayatasahaulika upesi. 29 KN 236.3

Licha ya afya ya mwili na ya akili ya watoto kuhatarishwa kwa kupelekwa shuleni mapema sana, hata wamekuwa wenye kupatwa na hasara katika mambo ya tabia ya uadilifu. Wanakuwa na nafasi kufahamiana na watoto waliokuwa washenzi kwa tabia zao wanatupwa katika jamii ya washenzi wasio na adabu, wasemao uongo, watukanaji, wevi, na wadanganyifu, na wenye kufurahia kuyashirikisha mafundisho yao maovu kwa wale walio wadogo kuliko wao wenyewe. Watoto wadogo, kama wakiachwa peke yao, hujifunza mabaya upesi zaidi ya mema. Mazoea mabaya hupatana sana na moyo wa asili, na mambo wanayoyaona na kuyasikia utotoni wakiwa wangali wachanga hukazwa akilini mwao; na mbegu mbaya iliyopandwa katika mioyo yao michanga itatia mzizi nayo itakuwa miiba mikali yenye kuijeruhi mioyo ya wazazi wao.

Ukubwa wa Mafundisho ya Kazi za Maisha Yenye Manufaa

Siku hizi, kama ilivyokuwa katika siku za Waisraeli, kila kijana angefundishwa kazi za maisha yenye manufaa. Kila mmoja angejipatia ujuzi wa kazi fulani ya mikono ambayo kwayo, kama ikilazimu, aweza kujipatia maisha yake. Hili ni jambo la muhimu, licha ya kuwa kinga ya mabadiliko ya hali ya mambo ya maisha, bali hata katika uhusiano wake na maendeleo ya mwili, akili na tabia ya moyoni. KN 237.1

Yafaa ufundi wa kazi mbalimbali ufundishwe shuleni mwetu. Kazi ya kuandika hesabu za fedha, useremala, na mambo yote yapasayo ukulima yafaa yawe miongoni mwa mafundisho ya ufundi wa kazi za mikono. Matayarisho yangefanywa kwa ajili ya kufundisha uhunzi, kupaka rangi, ushonaji wa viatu na upishi, uokaji, udobi; ufundi wa kukarabati vitu vikuukuu, kuandika kwa ‘komputa’, na kuchapisha vitabu. Kila uwezo tulio nao hauna budi kutumiwa katika mafunzo haya ya kazi za maisha yenye manufaa. KN 237.2

Ziko kazi nyingi kwa ajili ya wanafunzi wasichana ambazo yafaa zifundishwe ili waweze kupata elimu ya maana sana na yenye manufaa mengi. Yawapasa wafundishwe kushona nguo na kulima bustani. Yafaa wapande maua na matunda. Hivyo, huku wakifundishwa kazi za manufaa, watakuwa na mazoezi ya mwili nje ambayo hutia afya. 31 KN 237.3

Mvuto wa akili mwilini, na ule wa mwili akilini, ungekazwa. Nguvu za upesi ajabu za ubongoni, zikikuzwa kwa utendaji wa akili, hutia nguvu mwili mzima, na kwa njia hii msaada wa thamani sana katika kushindana na ugonjwa hupatikana. Pana ukweli juu ya habari za mwili wa mtu-ukweli ambao twahitaji kuufikiri katika Andiko hili, “Moyo uliochangangamka ni dawa nzuri. 32 KN 237.4

Ili watoto na vijana wawe na afya, furaha, wepesi, na misuli pamoja na akili zilizoadilishwa, yawapasa wawe nje saa nyingi, na kufanya kazi zinazosimamiwa vizuri pamoja na michezo. Watoto ambao hushindishwa shuleni na kujifunza vitabuni saa zote, hawawezi kuwa na miili yenye afya njema. Mazoezi ya akili katika kujifunza, bila kufanya mazoezi ya viungo vya mwili yanayolingana nayo, huleta damu ubongoni, na mwendo wa damu mwilini hauwezi kuwa sawa. Ubongo huwa na damu nyingi mno, na viungo vingine vya mwili kuwa na damu kidogo sana. Yapasa pawepo amri zinazotawala mafundisho ya watoto na vijana, wajifunze kwa saa fulani tu, kisha sehemu ya wakati wao unaobaki itumiwe katika kazi za juhudi. Tena, kama mazoea yao ya kula, kuvaa, na kulala yanaafikiana na kawaida za afya, wanaweza kupata mafundisho bila kukosa afya ya mwili, na akili

Heshima ya Kazi

Yafaa vijana waongozwe kuiona heshima halisi ya kazi za juhudi. Waonyeshwe kwamba Mungu ni mtendaji wa kazi daima. Viumbe wote kwa asili hufanya kazi waliyowekewa. Utendaji umeenea kwa viumbe wote, nasi ili kuitimiza kazi yetu, yatupasa pia kuwa watendaji hodari wa kazi. 34 KN 238.1

Kazi za juhudi ambazo huunganishwa pamoja na kuzitumikisha akili kwa ajili ya manufaa, ni utawala katika maisha ya manufaa, zikitiwa utamu siku zote na fikara ambazo huustahilisha na kuelimisha akili na mwili vizuri ili kuifanya kazi Mungu aliyowawekea wanadamu kuitenda katika idara mbalimbali za kazi. 35 KN 238.2

Mtu yeyote kati yetu asiionee kazi haya, hata iwe ni ndogo au ya kitumwa kiasi gam. Kazi ni heshima. Wote wanaofanya kazi, iwe ni kazi ya kichwa au ya mikono, nao waifanyao wakiwa waume au wanawake, ni watenda kazi. Na wote, iwe ni katika kufua nguo au kuosha vyombo vya jikoni, wanafanya wajibu wao na kuitukuza dini yao kwa kiasi kinacholingana barabara na wanapohudhuria katika mikutano. Wakati mikono inapojishughulisha katika kazi zilizo za kawaida sana, akili yaweza kuadilishwa na kukuzwa kwa kuwa na mawazo yaliyo safi na matakatifu. 36 KN 238.3

Sababu mojawapo iliyo kubwa inayofanya kazi ngumu za juhudi za mwili kudharauliwa ni kutokutengeneza, na kufanywa vibaya mara nyingi. Hufanywa kwa kuwa imebidi tu, wala si kwa hiari. Mtenda kazi hatii moyo kuifanya kazi hiyo, hachungi cheo, wala hapati heshima ya wengine. Mazoea ya kazi za juhudi yangeweza kulisahihisna kosa hili. Hayo yangekuza mazoea ya usahihi na bidii nyingi. 37 KN 238.4

Ni dhambi kuwaacha watoto kukua kivivu. Hebu wavizoeze viungo vyao na misuli, hata kama inawachosha. Ikiwa hawatumikishwi kupita kiasi, uchovu wawezaje kuwadhuru kuliko unavyokudhuru wewe? Kuna tofauti kabisa baina ya uchovu na ulegevu. Watoto wanahitaji mageuzi ya kazi mara kwa mara na vipindi vya pumziko zaidi kuliko watu wazima wanavyohitaji; lakini iwapo bado ni wachanga, waweza kuanza kujifunza kufanya kazi, na watakuwa na furaha mawazoni mwao kwamba nao waweza kujifanya kuwa wenye manufaa. Usingizi wao utakuwa mtamu baada ya kufanya kazi ya kutia afya, na watakuwa wameburudishwa kwa kazi ya siku itakayofuatia.

Haifai Lugha Yetu ya Asili Kudharauliwa

Katika kila sehemu ya mafundisho yako mambo ambayo yapasa kuonekana kuwa ni yenye faida zaidi ya yale yapatikanayo kwa elimu ya ufundi mtupu. Mathalan, mtu kuweza kuandika na kusema lugha ya kwao kwa urahisi na ufasaha ni jambo la maana zaidi ya elimu ya lugha za kigeni, zinazotumika au zile zilizokwisha kufa; lakini, hakuna elimu inayopatikana kwa njia ya sarufi iwezayo kulinganishwa thamani yake na mafundisho ya lugha kama ubora wake uonekanavyo. Hali njema ama hali nyonge kabisa hufungamana sana na mafundisho hayo. 39 

Vitabu Vyenye kutia Mashaka Vilivyokatazwa na Mungu

Je, ni kusudi la Mungu kwamba mafundisho ya uongo, mawazo ya uongo, na madanganyo ya Shetani yawekwe mbele ya vijana na watoto wetu? Je, mashauri ama maono ya kishenzi na kikafiri yatolewe mbele ya wanafunzi wetu kama ongezeko la thamani la mafundisho yao? Vitabu vya akili za watu walio na mashaka sana ni vitabu vya hila mbaya zinazotumiwa kwa huduma va yule adui, yaani Shetani. Je, yawapasa wale ambao hufanya bidii kuwaongoa vizuri watoto na vijana katika njia sawa, katika njia waliyowekewa wateule wa Bwana kuifuata, wafikiri kuwa Mungu angependa wawafundishe vijana mambo yale ambayo yangeeleza vibaya tabia ya Mungu na kumsingizia? Hasha! 40 KN 239.1

Matokeo ya Elimu ya Kikristo

Kadiri watoto walivyoimba hekaluni, “Hosana; ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana” (Markol 1:90), ndivyo siku hizi za mwisho sauti za watoto zitakavyopaswa kuutoa ujumbe wa mwisho wa onyo kwa ulimwengu unaopotea. Wale wenye akili mbinguni watakapoona kuwa watu hawaruhusiwi tena kulitoa Neno la Mungu, Roho wa Mungu atawajilia watoto, nao watafanya kazi ya kulihubiri Neno la Mungu, kazi ambayo watenda kazi wazee hawawezi kuifanya, kwa sababu njia yao itafungwa. KN 239.2

Shule zetu za Kanisa zimeamuriwa na Mungu ziwepo kuwatayarisha watoto kwa kazi hiyo kubwa. Hapa watoto wanapaswa wafundishwe maneno ya utume. Yawapasa kujiandikisha katika jeshi la watenda kazi kuwasaidia wagonjwa na wenye shida. Watoto huweza kushiriki katika utume kwa kazi ya utabibu, na kwa mambo yao madogo madogo huweza kuiendesha. Matoleo yao huenda yakawa madogo lakini kila kidogo husaidia, na kwa jitihada zao roho za watu wengi zitaletwa kwenye ukweli. Kwa njia yao ujumbe wa Mungu na nguvu zake za kuokoa utatangazwa kwa mataifa yote. Basi Kanisa na lichukue mzigo kwa ajili ya wanakondoo wa kundi hili. Watoto wafundishwe na kuzoezwa kumtumikia Mungu, maana wao ndio urithi wa Bwana. KN 239.3

Zikiendeshwa vizuri, shule za Kanisa zitakuwa njia ya kuinua hali ya ukweli mahali ambapo zinajengwa; kwa kuwa watoto wanaopokea elimu ya Kikristo watakuwa mashahidi wa Kristo. Kama Yesu hekalum alivyoeleza siri ambazo makuhani na wakuu walikuwa hawajazifahamu, ndivyo katika kazi ya mwisho wa dunia hii watoto ambao wamefundishwa vizuri watakavyofanya kwa maneno yao mepesi ambayo yatawashangaza watu ambao sasa husema juu ya “elimu ya juu zaidi.” 41 KN 239.4

Nalionyeshwa kuwa “Chuo Kikuu chetu” kilikusudiwa na Mungu kuitekeleza kazi hii kubwa ya kuokoa roho za watu. Ni hapo tu talanta za mtu zitakapowekwa chini ya mamlaka ya Roho wa Mungu na kutawaliwa naye ambapo zitatolewa zitumike kwa faida kamili. Mafundisho na kanuni za dini ni hatua za kwanza katika kupata elimu bora, na kuwa na msingi hasa wa elimu ya kweli. Maarifa na elimu havina budi kutiwa nguvu na Roho wa Mungu kusudi kufaa kwa makusudi bora sana. Mkristo peke yake ndiye awezaye kuitumia vema elimu. Ili elimu ithaminiwe kabisa, haina budi iangaliwe na kupimwa kwa upande wa dini. Moyo ambao umeadilishwa na neema ya Mungu nufahamu vizuri thamani halisi ya elimu. Sifa za Mungu, kama zionekanavyo katika kazi zake za kuumba, huweza tu kuthaminiwa kama tukimfahamu Muumbaji. Kusudi kuwaelekeza vijana kwenye chemchemi ya kweli, MwanaKondoo wa Mungu azichukuaye dhambi za ulimwengu, walimu hawana budi kuwa na elimu ya hakika juu ya njia takatifu. Elimu ina nguvu kama ikiunganishwa na kumcha Mungu kwa kweli

Wajibu wa Mwanafunzi Kusaidia Shule Yake

Wale wanafunzi wanaodai kumpenda Mungu na kulitii neno la kweli yafaa wajitawale na kuwa na nguvu za kanuni ya dini ambayo itawawezesha kudumu imara katikati ya majaribu na kusimama kumtetea Yesu katika chuo, katika bweni zao, ama po pote walipo. Dini si kitu cha kuvaliwa tu kama joho nyumbani mwa Mungu, bali kanuni za dini hazina budi kuifanyiza tabia ya maisha yote. KN 240.2

Wale wanaokunywa katika chemchemi ya uzima hawataonyesha tamaa ya mageuzi na anasa, kama walimwengu. Katika mwenendo na tabia yao pataonekana na amani na furaha ambayo wameipata kwa Yesu kwa kuyaweka kila siku mashaka na mizigo yao miguuni pake. Wataonyesna kwamba pana kuridhika na furaha pia katika njia ya utii na kazi. Watu kama hao watatoa mvuto kwa wanafunzi wenzao ambao utadhihirika katika shule nzima. KN 240.3

Wale walio miongoni mwa jeshi hilo aminifii watawaburudisha na kuwatia nguvu walimu na walimu wakuu katika jitihadi zao kwa kuzuia udanganyifu wa kila aina, fitina, ama kukataa kuzitii amri na kawaida za shule. Mvuto wao utaokoa, na matendo yao hayatapotea katika siku ile kuu ya Mungu, bali yatawafuata kwenye ulimwengu wa wakati ujao; na mvuto wa maisha yao hapa utadnihirika siku zote, milele. KN 240.4

Kijana mmoja aliye mwaminifu, mwenye bidii kutenda mema shuleni ni hazina kubwa mno. Malaika wa mbinguni humtazama kwa upendo. Mwokozi wake wa ajabu humpenda, na katika Daftari ya Mbinguni pataandikwa kila tendo la haki, kila jaribu lililopingwa, kila dhambi iliyoshindwa. Hivyo ndivyo atakavyoweka msingi mwema kwa ajili ya wakati ujao, kusudi apate kuushikilia uzima wa milele. KN 241.1

Hifadhi na ufulizo wa shule ambazo Mungu ameziazimia ziwe njia ya kuendeshea kazi yake hutegemea sana juu ya vijana. Madaraka hayo makubwa sana ni juu ya vijana wa siku hizi ambao huifikia hatua ya utendaji. Kamwe hapajakuwako muda ambao matokeo makubwa jinsi hii yalitegemea juu ya kizazi cha wanadamu; basi, ni jambo kubwa kama nini kwamba yafaa vijana na wahitimu kwa ajili ya kazi kuu, ambayo Mungu aweza kuwatumia kama vyombo vyake. Muumbaji wao anayo madai juu yao ambayo ni makubwa kuliko mengine yote. KN 241.2

Mungu ndiye aliyetoa uzima na karama zote za mwili na akili walizo nazo. Amewajalia akili nyingi, kusudi wapate kuaminiwa kazi ambayo itastahimili milele. Kwa hizo karama zake kuu hudai zikuzwe ipasavyo na kuzitumia vizuri akili na uelekevu wao wa moyo. Hakuwapa akili hizi ili waiipendeze tu kwa anasa, wala kutumiwa vibaya kwa mambo yaliyo kinyume cha mapenzi yake na majaliwa yake, bali wapate kuzitumia kuzidisha ujuzi wa kweli na mtakatifu ulimwenguni. Adai shukrani zao, kicho na upendo wao, kwa ajili ya wema wake wa daima na fadhili zake zisizo na mwisho. Adai kwa haki utii wa sheria zake na kwa kanuni zote za hekima ambazo zitawazuia na kuwalinda vijana na hila zake Shetani na kuwaongoza katika njia za amani. KN 241.3

Ikiwa vijana wangeona kuwa kwa kuzitii sheria na amri za shule zetu wanafanya tu kile ambacho kitazidisha ubora wa cheo chao miongoni mwa watu, kukuza tabia, kuadilisha moyo, na kuzidisha mraha yao, wasingeziasi amri za haki na masharti ya halali, wala kuingia katika kuanzisha shuku na lawama juu ya shule hizo. Yafaa vijana wetu wawe na roho ya nguvu na uthabiti kuyatimiza madai juu yao, na hilo litakuwa thibitisho la kufaulu kwao. Tabia ya kishenzi na ya upotevu wa vijana wengi katika kizazi hiki cha ulimwengu hutia uchungu moyoni. Lawama nyingi ni juu ya wazazi wao nyumbani. Pasipo kicho cha Mungu hakuna awezaye kufurahi kwa kweli

 

Sura Ya 37 - Elimu ya Kikristo

TUNAKARIBIA kwa haraka wakati wa hatari za mwisho wa historia ya ulimwengu huu, na ni bora tukifahamu kuwa faida ya elimu itolewayo na shule zetu haina budi kuhitilafiana na ile ya shule za kidunia. 1 KN 229.1

Mawazo yetu juu ya elimu ni kidogo sana na shabaha yetu iko chini sana. Kuna haja ya cheo cha juu, na shabaha bora zaidi. Maana ya elimu ya kweli siyo mfululizo wa mafundisho fulani tu, la, bali ma maana zaidi ya kujitayarisha kwa ajili ya maisha haya ya sasa. Huhusu mwili mzima wa mtu, muda wote wa maisha yake awezayo kuishi. Ni kukua kunakopata na mwili, akili na nguvu za kiroho. Humtayarisha mwanafunzi kwa ajili ya furaha ya kazi ulimwenguni humu na kwa ajili ya furaha bora zaidi ya kazi kubwa zaidi katika ulimwengu ujao. 2 KN 229.2

Maana halisi ya kazi ya elimu na ile ya kazi ya ukombozi ni moja; kwa kuwa elimu, kama ilivyo na ukombozi “msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani Yesu Kristo.” 3 KN 229.3

Kumrudisha binadamu apatane na Mungu, hata kumkuza na kumwadilisha moyoni mwake ili aweze tena kurudisha sura ya Muumbaji, ndilo kusudi kubwa la elimu na malezi yote ya maisha. Hii ilikuwa kazi ya maana sana hata ikamfanya Mwokozi ayaache makao ya mbinguni na kuja ulimwenguni humu katika hali ya mwili wa kibinadamu, Kusudi apate kuwafundisha watu jinsi ya kupata hali ya kufaa kwa maisha yale bora zaidi ya juu. 4 KN 229.4

Ni vyepesi zaidi kuingia polepole katika mipango na desturi za kidunia, bila kujua, na kusahau habari za wakati nasa tunamoishi, au kutofikiri kazi kubwa ipasayo kumalizwa, kuliko walivyokuwa watu wa siku zile za Nuhu. Kuna hatari daima kwa walimu wetu kwenda njia ile ile ya Wayahudi, na kufuata desturi, mazoea, na mapokeo ya wazee wao ambayo hayakutolewa na Mungu. Wengine hushikilia sana desturi za zamani na mafundisho mbalimbali ambayo si ya muhimu, kana kwamba wokovu huu unategemea juu ya mambo hayo. Kwa kufanya hivyo wanakiacha kitabu maalumu cha Mungu na kuwapa wanafunzi elimu pungufu na iliyo mbaya. 5 Imepasa pawepo wanaume na wanawake ambao wamestahili kufanya kazi makanisani kuwafundisha vijana wetu kazi maalumu, kusudi watu wawezeshwe kumwona Yesu. Shule zilizowekwa nasi zapaswa ziwe na kusudi hili daima. Wala zisiige taratibu za shule za madhehebu zingine, au kufuata taratibu za vyuo vikuu (seminaries au colleges) vya kidunia. Wamepaswa wawe na KN 229.5

utaratibu ulio bora zaidi ya shule zingine zote ambao hali ya ukafiri haiwezi kuonekana au kutokana nao ama kupendelewa nao. Wanafunzi hawana budi kufundishwa Ukristo wa kufaa, na Biblia imepasa ihesabiwe kuwa jambo kubwa kuliko mengine yote, na ya kwamba ni kitabu cha mafundisho kilicho cha maana sana. 6

Msaada wa Tabia ya Uadilifu katika Vyuo Vyetu

Yafaa baba na mama kushirikiana na mwalimu kazini kwa bidii kwa ajili ya uongofu wa watoto wao. Hebu wajitahidi kudumisha moyo wa kupendezwa na mambo ya kiroho na matakatifii nyumbani na kuwalea watoto wao katika malezi na maonyo ya Bwana. Hivyo ndivyo wawezavyo kuifanya saa ya mafimdisho kuwa ya kupendeza na yenye faida, na matumaini yao yataongezeka kwa njia hii ya kuutafuta wokovu wa watoto wao. 12 KN 231.5

Baadhi ya wanafunzi hurejea nyumbani wakiwa na manung’uniko, na wazazi na washiriki wa kanisa huyasikiliza maneno yao yaliyotiwa chumvi, yasiyo ya haki. Ingekuwa bora kama wangefikin kuwa hadithi ina pande mbili; lakini badala ya kufanya hivyo, hukubali rioti hizo zilizopotoka kujenga kizuizi baina yao na chuo hicho kikuu. Ndipo huanza kuonyesha hofu, mashaka, na shuku juu ya njia inayotumiwa kukiendesha chuo hicho. Mvuto wa namna hiyo huleta madhara makubwa. Maneno ya kutoridhika huenea kama ugonjwa unaoambukiza, na ushawishi ufanywao mawazoni ni shida kuuondoa kabisa. Uvumi huzidi kila mara mpaka kuwa mkubwa mno, ambapo uchunguzi ungeonyesha ukweli kwamba walimu hawakuwa na kosa wala walimu wakuu wa chuo hicho. Walikuwa wakifanya tu wajibu wao katika kuzitilia nguvu amri za shule, ambazo hazina budi kutimizwa, ama sivyo shule itachafuliwa. KN 232.1

Ikiwa wazazi wangejiweka mahali pa walimu na kuona jinsi inavyolazimu kuwa vigumu kuongoza na Kutawala shule ya wanafunzi mamia wa kila darasa na wa aina mbalimbali, huenda wakayaona mambo namna nyingine. Wangefikiri kuwa watoto wengine kamwe hawakupata malezi mema nyumbani. Kama watoto hao ambao wametupwa ovyo na wazazi wasio waaminifu wasipofanyiwa kitendo, kamwe hawatakubaliwa na Yesu; isipokuwa uwezo fulani wa kuwatawala unaletwa kuwasaidia, hawatakuwa na maana katika maisha haya wala hawatashiriki maisha ya wakati ujao. 13 KN 232.2

Baba na mama wengi hukosa kwa kulegeza bidii ya mwalimu mwaminifu. Vijana na watoto, kwa uwezo wa kufahamu usio kamili na maamuzi yao machanga hawawezi siku zote kufahamu mipango na njia zote za mwalimu. Lakini, wanapoleta nyumbani ripoti za mambo yasemwayo na kufanywa katika shule, hayo huzungumzwa na wazazi katika jamii ya watu wa nyumbani, na matendo ya mwalimu hulaumiwa bila kizuizi. Hapo watoto hujifunza mafundisho ambayo si vyepesi kujifunzwa. Wakati wo wote wanapopaswa kujizuia wasivyozoea, au kutakiwa kujifunza mambo magumu, huwalalamikia wazazi wao wasio na busara ili wawahurumie na kuwaendekeza. Hivi ndivyo moyo wa wasiwasi na kutokuridhika unavyotiwa nguvu, na shule nzima huumia kwa sababu ya mvuto huo ambao huichafua na mzigo wa mwalimu huzidi kuwa mzito. Lakini, hasara iliyo kubwa zaidi ni kwa watoto wenyewe wenye kufundishwa hivi na wazazi wao. Makosa ya tabia ambayo malezi mazuri yangeweza kuyasahihisha, huachwa kupata nguvu kadiri miaka iendavyo, kuharibu na pengine kuangamiza kabisa manufaa ya yule aliyo nayo. 14 

Walimu Chini ya Mungu

Bwana hutenda kazi pamoja na mwalimu aliyejitoa wakfu; na ni kwa faida ya mwalimu mwenyewe kulifahamu neno hili. Walimu ambao wako chini ya utawala wa Mungu hupokea neema na kweli na nuru kwa njia ya roho Mtakatifu kuipitisha kwa watoto. Wako chini ya Mwalimu mkuu kabisa aliyepata kuwako ulimwenguni, na ingekuwa vibaya kama nini wakiwa na roho isiyo njema, sauti kali, na kujawa na chuki! Kwa jambo hili wangedumisha makosa yao wenyewe kwa watoto wao. KN 233.1

Mungu atazungumza na roho ya mtu kwa njia ya Roho Mtakatifu. Omba unapokuwa ukijifunza, “Unifumbue macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako” (Zab. 119:18). Mwalimu atakapomtegemea Mungu kwa maombi, Roho ya Kristo itamshukia, na Mungu atafanya kazi kwa njia yake kwa Roho Mtakatifu kwenye akili za mwanafunzi. Roho Mtakatifu huzijaza akili tumaini na moyo mkuu na maneno ya Biblia, ambayo yatapitishwa kwa mwanafunzi. Maneno ya kweli yataendelea kuwa na maana, nayo yatapanuka na kupata ukamilifu wa maana ambayo kamwe hajaota habari zake. Uzuri na sifa ya neno la Mungu vina mvuto unaoongoa akili na tabia; macheche ya upendo wa mbinguni yataanguka juu ya mioyo ya watoto kama maongozi ya Mungu Twaweza kuleta mamia na maelfu ya watoto kwa Kristo kama tukitende kazi ya kuwavuta kuja kwake. 15 KN 233.2

Kabla watu hawajaweza kuwa na akili hasa, yawapasa kufahamu tegemeo lao kwa Mungu, na kujazwa na hekima yake. Mungu ndiye chimbuko la akili na nguvu za kiroho pia. Watu mashuhuri amoao wamefikia vyeo vya juu sana vya elimu, kama waonavyo, hawawezi kulinganishwa na Yohana, mwanafunzi mpendwa wa Yesu wala mtume Paulo. Akili na nguvu za kiroho zikiunganishwa ndipo cheo cha juu sana maishani kinapoweza kufikiwa. Wale wafanyao hivi, Mungu atawakubali kama watenda kazi pamoja naye katika kuwaelimisha wengine. 16 KN 233.3

“Kazi kubwa sana ya jamii ya shule zetu wakati huu ni kuwaonyesha walimwengu kielelezo chema ambacho humtukuza Mungu. Malaika watakatifu huiongoza na kuisimamia kazi hiyo kwa njia ya wanadamu, na kila idara ya kazi hiyo haina budi kuwa na alama ya ubora mtakatifu. 17 

Sifa za Mwalimu wa Shule

Pateni mtu aliye hodari awe mkuu wa shule yenu, mtu ambaye nguvu za mwili wake zitamsaidia kufanya kazi kikamilifu kama mtawala ama mlezi mwema; mtu ambaye anastahili kuwalea watoto na kuwafanya wawe na mazoea mema ya utaratibu, unadhifu na utendaji wa kazi. Tenda kazi kikamilifu kwa lo lote ufanyalo. Karna ukiwa mwaminifu katika kuwafundisha mafundisho ya kawaida wanafunzi wako wengi wataweza kutoka shuleni na kusnika kazi kama wainjilisti. Hatuna sababu ya kufikiri kuwa ni lazima watenda kazi wote wawe na elimu ya juu. 18 KN 233.5

Katika kuwachagua walimu, yatupasa tuangalie sana kabla hatujawachagua, tukijua kuwa hili ni jambo kubwa, la dini, kama ilivyo katika kuwachagua watu kwa kazi ya uchungaji wa kanisa. Watu wenye busara ambao wanaweza kupambanua tabia za watu wangefanya uchaguzi huo; kwa kuwa mwenye kipawa bora sana ndiye anayetakiwa kuwaelimisha na kuwaadilisha watoto, na kuendesha kazi mbalimbali zitakazobidi kutendwa na walimu katika shule zetu za kanisa Msiweke walimu vijana, wasio na utawala; kwa kuwa jitihada zao zitaleta machafuko. 19 KN 234.1

Pasiwepo mwalimu anayeajiriwa, isipokuwa mmemshuhudia na kumpima kwa majaribio, mkaona kuwa anampenda na kumcha Mungu. Kama walimu wamefundishwa na Mungu, na kama mafundisno yao kila siku hutokana na Kikristo, watafanya kazi ya Kristo. Watawaongoa watu pamoja na Kristo; kwa kuwa kila mtoto na kila kijana ni mwenye thamam kuu. 20 KN 234.2

Yafaa mazoea na kanuni za mwalimu zikumbukwe kuwa ni mambo makubwa kuliko elimu yake. Kusudi awe na mvuto yampasa ajitawale kabisa yeye mwenyewe, na moyoni mwake mwenyewe ajawe na upendo kwa wanafunzi wake, ambao utaonekana katika uso, maneno, na matendo yake. 21 KN 234.3

Yampasa mwalimu siku zote afanye kiungwana kama Mkristo mwema. Yampasa awe na moyo wa kirafiki na mshauri mwema kwa wanafunzi wake. Kama watu wote wa kanisa letu walimu, wachungaji, na washiriki wa kanisa wangekuza moyo wa uadilifu na adabu ya Kikristo, wangepata kwa urahisi zaidi njia ya kuifikia mioyo ya watu; wengi zaidi wangeongozwa kulichunguza na kulipokea neno la kweli. Kila mwalimu atakapowafikiria wengine kuliko nafsi yake mwenyewe, na kupendelea sana maendeleo na mafanikio ya wanafunzi wake, akijua kuwa wao ni mali ya Mungu, na ya kwamba hana budi kutoa habari za mvuto wake juu ya nia na tabia zao, ndipo tutakuwa na shule ambayo malaika watapenda kukaa humo bila kuondoka upesi. 22 KN 234.4

Shule zetu zahitaji walimu wenye sifa bora za uadilifu; wale ambao huweza kuaminiwa; wale ambao wana nguvu katika imani, na wenye akili na uvumilivu; wale wenye kutembea pamoja na Mungu, na kujiepusha na hatua ya kwanza kabisa ya maovu. KN 234.5

Kuwaweka watoto wetu wadogo kwa walimu wenye kiburi na wasio wazuri ni dhambi. Mwalimu wa aina hiyo atasababisha madhara makubwa kwa hao ambao hukuza tabia kwa upesi. Kama walimu hawamtii Mungu, ikiwa hawana upendo kwa watoto wanaowaongoza, au kama huonyesha upendeleo kwa wale wenye sura zinazowapendeza, kutowajali wale wasio wazuri wa sura, wala wale walio watukutu na dhaifu, haifai kuajiriwa; maana kazi yao itamletea Kristo hasara ya roho za watu. Huhitajiwa, hasa kwa watoto, walimu ambao ni watulivu na wema, wanaoonyesha uvumilivu na upendo kwa wale hasa wanaouhitaji sana. 23 KN 234.6

Mwalimu atapoteza kiini hasa cha elimu, kama asipofahamu haja yake ya maombi, na kunyenyekea moyoni mwake mbele za Mungu. 24 KN 235.1

Ukubwa wa sifa za afya ya mwalimu ni vigumu kuudhania kuwa jambo kubwa kuliko ulivyo; kwa kuwa kadiri afya yake inavyozidi, ndivyo na kazi yake itakavyozidi kukamilika. Akili haziwezi kuflkin barabara na kuwa na nguvu kutenda kazi ikiwa nguvu za mwili zimedhurika kwa sababu ya udhaifu au ugonjwa. Moyo hushindwa na mawazo; lakini ikiwa, kwa sababu ya udhaifu wa mwili, ubongo kupotewa na nguvu zake, hapo ndipo njia ya maoni bora ya moyoni na makusudi safi itakuwa imezuiwa, na mwalimu hawezi tena kupambanua baina ya jema na baya. Ukiumwa na ugonjwa, si jambo rahisi kufurahi, wala kufanya kazi kwa uaminifu na haki. 25 

Biblia Katika Elimu ya Kikristo

Kama njia ya kuelimisha, Biblia ni yenye matokeo zaidi ya kitabu kinginecho, au vitabu vyote vingine vikiunganishwa pamoja. Ubora wa maneno yake makubwa, na mepesi kueleweka, uzuri wa maneno yake yanayoleta mifano akilini, hutia nguvu na kukuza akili kuliko cnochote kingine. Hakuna mafundisho mengine yawezayo kutoa elimu kama bidii ya kuyafahamu maneno ya kweli ya mafunuo hayo. Akili ambazo zimeunganishwa na nia ya Mungu jinsi hiyo zitazidi tu kupata nguvu. KN 235.3

Pia uwezo wa Biblia una nguvu zaidi katika maendeleo ya hali ya kiroho. Binadamu, ambaye ameumbwa kusudi ashirikiane na Mungu, aweza tu kupata uzima na maendeleo yake halisi, kwa ushirika wa namna hiyo. Akiwa ameumbwa kwa namna inayomwezesha kupata fursaha yake ilio bora sana kwa Mungu, kile ambacho chaweza kutuliza kiu cha moyo hawezi kukipata kwa njia nyingine iwayo yote. Yeye ambaye kwa unyofu na uelekevu wa moyo hujifunza Neno la Mungu, akitaka kufahamu ukweli wake, atamfahamu Muumbaji wake; na isipokuwa kwa hiari ya mtu mwenyewe, hakuna kikomo cha uwezekano wa maendeleo yake. 26 KN 235.4

Hebu mafungu ya Maandiko Matakatifu yenye maana inayohusiana zaidi na mafundisho yanayotolewa yakaririwe hata yaweze kukumbukwa, si kama kazi ngumu, bali kama kitu cha faida. Ingawa mara ya kwanza huenda uwezo wa kukimbuka ukawa na upungufu, lakini, utapata nguvu kwa kuzoezwa, ili baada ya muda upendezwe kuyaweka moyoni maneno ya kweli. Nayo mazoea haya yatasaidia sana kukua kiroho. 27 

Hatari Katika Kuwapeleka Watoto Shuleni Wakiwa Wangali Wadogo Sana

Kama wale waliokaa Edeni walivyojifunza kutoka kwa viumbe vya asili, kama Musa alivyouona mwandiko wa Mungu juu ya tambarare na milima ya Arabia, na kama Mtoto Yesu alivyoona juu ya mitelemko ya vilima vya Nazareti, ndivyo siku hizi wawezavyo kuona na kujifunza habari za Mungu. Mambo yale yasiyoonekana hufafanuliwa na yale yanayoonekana. KN 236.1

Basi, kadiri iwezekanavyo, mtoto awekwe tokea utotoni kabisa mahali ambapo kitabu hiki cha ajabu cha mafundisho kinweza kufunuliwa mbele yake. 28 KN 236.2

Msiwapeleke watoto wenu shuleni mapema mno. Yafaa mama aangalie sana jinsi anavyomwamini mtu mwingine kumfundisha mtoto wake mchanga, na kukuza tabia yake. Yawapasa wawe walimu bora kabisa wa watoto wao mpaka watoto wafikishapo umri wa miaka minane au kumi. Chumba chao cha kusomea kingekuwa nje, katika maua na ndege, na kitabu cha mafundisho yao kingekuwa viumbe wa asili. Mara wawezapo kufahamu kwa akili zao wenyewe, wazazi wawafunulie kitabu hiki kikubwa cha Mungu cha viumbe. Mafundisho haya yatolewayo mahali pa namna hii hayatasahaulika upesi. 29 KN 236.3

Licha ya afya ya mwili na ya akili ya watoto kuhatarishwa kwa kupelekwa shuleni mapema sana, hata wamekuwa wenye kupatwa na hasara katika mambo ya tabia ya uadilifu. Wanakuwa na nafasi kufahamiana na watoto waliokuwa washenzi kwa tabia zao wanatupwa katika jamii ya washenzi wasio na adabu, wasemao uongo, watukanaji, wevi, na wadanganyifu, na wenye kufurahia kuyashirikisha mafundisho yao maovu kwa wale walio wadogo kuliko wao wenyewe. Watoto wadogo, kama wakiachwa peke yao, hujifunza mabaya upesi zaidi ya mema. Mazoea mabaya hupatana sana na moyo wa asili, na mambo wanayoyaona na kuyasikia utotoni wakiwa wangali wachanga hukazwa akilini mwao; na mbegu mbaya iliyopandwa katika mioyo yao michanga itatia mzizi nayo itakuwa miiba mikali yenye kuijeruhi mioyo ya wazazi wao. 

Ukubwa wa Mafundisho ya Kazi za Maisha Yenye Manufaa

Siku hizi, kama ilivyokuwa katika siku za Waisraeli, kila kijana angefundishwa kazi za maisha yenye manufaa. Kila mmoja angejipatia ujuzi wa kazi fulani ya mikono ambayo kwayo, kama ikilazimu, aweza kujipatia maisha yake. Hili ni jambo la muhimu, licha ya kuwa kinga ya mabadiliko ya hali ya mambo ya maisha, bali hata katika uhusiano wake na maendeleo ya mwili, akili na tabia ya moyoni. KN 237.1

Yafaa ufundi wa kazi mbalimbali ufundishwe shuleni mwetu. Kazi ya kuandika hesabu za fedha, useremala, na mambo yote yapasayo ukulima yafaa yawe miongoni mwa mafundisho ya ufundi wa kazi za mikono. Matayarisho yangefanywa kwa ajili ya kufundisha uhunzi, kupaka rangi, ushonaji wa viatu na upishi, uokaji, udobi; ufundi wa kukarabati vitu vikuukuu, kuandika kwa ‘komputa’, na kuchapisha vitabu. Kila uwezo tulio nao hauna budi kutumiwa katika mafunzo haya ya kazi za maisha yenye manufaa. KN 237.2

Ziko kazi nyingi kwa ajili ya wanafunzi wasichana ambazo yafaa zifundishwe ili waweze kupata elimu ya maana sana na yenye manufaa mengi. Yawapasa wafundishwe kushona nguo na kulima bustani. Yafaa wapande maua na matunda. Hivyo, huku wakifundishwa kazi za manufaa, watakuwa na mazoezi ya mwili nje ambayo hutia afya. 31 KN 237.3

Mvuto wa akili mwilini, na ule wa mwili akilini, ungekazwa. Nguvu za upesi ajabu za ubongoni, zikikuzwa kwa utendaji wa akili, hutia nguvu mwili mzima, na kwa njia hii msaada wa thamani sana katika kushindana na ugonjwa hupatikana. Pana ukweli juu ya habari za mwili wa mtu-ukweli ambao twahitaji kuufikiri katika Andiko hili, “Moyo uliochangangamka ni dawa nzuri. 32 KN 237.4

Ili watoto na vijana wawe na afya, furaha, wepesi, na misuli pamoja na akili zilizoadilishwa, yawapasa wawe nje saa nyingi, na kufanya kazi zinazosimamiwa vizuri pamoja na michezo. Watoto ambao hushindishwa shuleni na kujifunza vitabuni saa zote, hawawezi kuwa na miili yenye afya njema. Mazoezi ya akili katika kujifunza, bila kufanya mazoezi ya viungo vya mwili yanayolingana nayo, huleta damu ubongoni, na mwendo wa damu mwilini hauwezi kuwa sawa. Ubongo huwa na damu nyingi mno, na viungo vingine vya mwili kuwa na damu kidogo sana. Yapasa pawepo amri zinazotawala mafundisho ya watoto na vijana, wajifunze kwa saa fulani tu, kisha sehemu ya wakati wao unaobaki itumiwe katika kazi za juhudi. Tena, kama mazoea yao ya kula, kuvaa, na kulala yanaafikiana na kawaida za afya, wanaweza kupata mafundisho bila kukosa afya ya mwili, na akili. 33

Heshima ya Kazi

Yafaa vijana waongozwe kuiona heshima halisi ya kazi za juhudi. Waonyeshwe kwamba Mungu ni mtendaji wa kazi daima. Viumbe wote kwa asili hufanya kazi waliyowekewa. Utendaji umeenea kwa viumbe wote, nasi ili kuitimiza kazi yetu, yatupasa pia kuwa watendaji hodari wa kazi. 34 KN 238.1

Kazi za juhudi ambazo huunganishwa pamoja na kuzitumikisha akili kwa ajili ya manufaa, ni utawala katika maisha ya manufaa, zikitiwa utamu siku zote na fikara ambazo huustahilisha na kuelimisha akili na mwili vizuri ili kuifanya kazi Mungu aliyowawekea wanadamu kuitenda katika idara mbalimbali za kazi. 35 KN 238.2

Mtu yeyote kati yetu asiionee kazi haya, hata iwe ni ndogo au ya kitumwa kiasi gam. Kazi ni heshima. Wote wanaofanya kazi, iwe ni kazi ya kichwa au ya mikono, nao waifanyao wakiwa waume au wanawake, ni watenda kazi. Na wote, iwe ni katika kufua nguo au kuosha vyombo vya jikoni, wanafanya wajibu wao na kuitukuza dini yao kwa kiasi kinacholingana barabara na wanapohudhuria katika mikutano. Wakati mikono inapojishughulisha katika kazi zilizo za kawaida sana, akili yaweza kuadilishwa na kukuzwa kwa kuwa na mawazo yaliyo safi na matakatifu. 36 KN 238.3

Sababu mojawapo iliyo kubwa inayofanya kazi ngumu za juhudi za mwili kudharauliwa ni kutokutengeneza, na kufanywa vibaya mara nyingi. Hufanywa kwa kuwa imebidi tu, wala si kwa hiari. Mtenda kazi hatii moyo kuifanya kazi hiyo, hachungi cheo, wala hapati heshima ya wengine. Mazoea ya kazi za juhudi yangeweza kulisahihisna kosa hili. Hayo yangekuza mazoea ya usahihi na bidii nyingi. 37 KN 238.4

Ni dhambi kuwaacha watoto kukua kivivu. Hebu wavizoeze viungo vyao na misuli, hata kama inawachosha. Ikiwa hawatumikishwi kupita kiasi, uchovu wawezaje kuwadhuru kuliko unavyokudhuru wewe? Kuna tofauti kabisa baina ya uchovu na ulegevu. Watoto wanahitaji mageuzi ya kazi mara kwa mara na vipindi vya pumziko zaidi kuliko watu wazima wanavyohitaji; lakini iwapo bado ni wachanga, waweza kuanza kujifunza kufanya kazi, na watakuwa na furaha mawazoni mwao kwamba nao waweza kujifanya kuwa wenye manufaa. Usingizi wao utakuwa mtamu baada ya kufanya kazi ya kutia afya, na watakuwa wameburudishwa kwa kazi ya siku itakayofuatia.

 

Sura ya 38 - Mwito wa Kuwa na Kiasi Maishani

AFYA ni mbaraka mkubwa mno, na ni yenye uhusiano sana na dhamiri ya moyoni na dini kuliko wengi wanavyojua. Inahusiana sana na uwezo wa mtu kazini, nayo yafaa kulindwa kwa kicho kama tabia; maana kadiri afya izidivyo kuwa kamili, ndivyo juhudi zetu zitakavyozidi kukamilika kwa ajili ya maendeleo ya kazi ya Mungu na kwa ajili ya mbaraka kwa wanadamu. 1 KN 242.1

Mnamo Desemba 10, 1871, nalionyeshwa tena kwamba kuwa na kiasi ni mojawapo ya kazi kuu ambayo itawafanya watu wafae kwa kuja kwa Bwana. Inahusiana sana na ujumbe wa malaika watatu kama vile mkono unavyohusiana na mwili. Amri Kumi za Mungu zimedharauliwa na mwanadamu, lakini Bwana hapendi kuja kuwaadhibu waasi wa hiyo sheria bila kuwapelekea kwanza ujumbe wa onyo. Malaika wa tatu anahubiri ujumbe huo. Watu wangalitii hiyo sheria ya amri Kumi, na kutimiza maishani mwao kanuni za maagizo hayo, laana ya magonjwa yanayojaa sasa ulimwenguni isingalikuwako. KN 242.2

Wanaume kwa wanawake hawawezi kuiasi sheria ya asili kwa kuiridhisha tamaa ya chakula iliyopotoka pamoja na tamaa mbaya za mwili, bila kuasi sheria ya Mungu. Kwa hiyo, Mungu ameruhusu nuru ya matengenezo ya kuwa na kiasi kutuzukia, kusudi tuweze kuona dhambi yetu katika kuziasi sheria ambazo ameziweka mwilini mwetu. Furaha au huzuni yetu yote yaweza kuonekana kwamba hutokana na utii ama uasi wa sheria ya asili. Baba yetu aliye mbinguni huona hali mbaya ya kusikitisha ya watu ambao wengine kwa makusudi lakini, wengi bila kujua, huishi kwa kuziasi sheria zilizowekwa na Mungu. Na kwa kuwapenda na kuwahurumia wanadamu, ameifanya nuru iangaze kwenye kanuni bora za matengenezo ya afya. Aitangaza sheria yake na adhabu ambayo itafuata kwa kuiasi, ili wote wapate kujifunza na kuwa waangalifu kuitii sheria ya asili. Ametangaza sheria yake wazi kabisa na kuitukuza hata imekuwa kama mji ulio juu ya mlima. Watu wote wanaohusika waweze kuifahamu kama wakitaka. Wajinga hawatakuwa na hatia kuidhihirisha sheria hii ya asili, na kusisitiza kuitii, ndiyo kazi inayofuatana na ujumbe wa malaika wa tatu kuwatayarisha watu kwa ajili ya kuja kwa Bwana. 2 KN 242.3

“Ninyi si Mali Yenu Wenyewe”

Twaamini bila mashaka kuwa Kristo yu karibu kuja. Hii si hadithi tu kwetu; ni jambo la hakika. Ajapo natapaswa kutusafisha dhambi zetu, kutuondolea makosa katika tabia zetu, wala kutuponya udhaifu wa hali ya moyo na tabia zetu. Ikiwa haina budi kutendwa kwa ajili yetu, kazi hiyo yote yapasa kutekelezwa kabla ya wakati huo. KN 243.1

Bwana ajapo wale walio watakatifu watazidi kutakaswa. Wale ambao wamehifadhi miili na roho zao katika utakatifu, katika usafi na kicho, ndipo watapokea mguso wa mwisho wa kutokufa. Lakini wale wasio na haki, wasiotakaswa, na wachafu watadumu hali hiyo milele. Basi, hakuna kazi watakayotendewa kuondoa makosa yao na kuwapa tabia takatifu. Hiyo yote haina budi kutendwa saa hizi za kuangaliwa kama twafaa au hatufai. Sasa ndio wakati upasao kazi hiyo kutekelezwa kwetu. KN 243.2

Tumo katika ulimwengu ambao umezuiwa usipate haki na usafi wa tabia, pamoja na kukua katika neema. Po pote tunapotazama twaona uchafu na unajisi, ubaya na dhambi. Basi, ni kazi gani tupaswayo kujaribu kuifanya hapa kabla hatujaupokea uzima wa milele? Ni kuiweka miili yetu katika hali takatifu, roho zetu katika hali safi, ili tupate kusimama pasipo mawaa katikati ya makosa yanayojaa pande zote kutuzunguka siku hizi za mwisho. KN 243.3

Hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu” (1 Wakorintho 6:19, 20). KN 243.4

Sisi si mali yetu wenyewe. Tumenunuliwa kwa gharama ya thamani kubwa, naam, mateso na mauti ya Mwana wa Mungu. Ikiwa tungelifahamu neno hili, na kulitambua kabisa, tungeona moyoni kuwa wajibu mkuu unatukalia kujitunza katika hali bora kabisa ya afya, ili tupate kumtumikia Mungu kwa ukamilifu. Lakini, tukifuata njia ambayo hutumia nguvu zetu za uhai, na kupunguza nguvu zetu, au kutia giza akilini, twatenda dhambi dhidi ya Mungu. Kwa kufuata njia hiyo hatumtukuzi katika miili wala katika roho zetu ambazo ni mali yake, bali tunafanya kosa kubwa machoni pake. 3

Utii ni Wajibu wa Kila Mtu

Muumbaji wa mwanadamu amepanga mashine hii yenye uhai ya miili yetu. Kila sehemu imefanywa vizuri ajabu na kwa hekima. Mungu ameahidi kuitunza mashine hii ya mwili wa mwanadamu katika hali njema ya afya ikiwa mwanadamu atazitii sheria za Mungu na kushirikiana naye. Kila sheria inayoitawala mashine ya mwili wa mwanadamu ingefikiriwa kuwa takatifu kwa kweli kwa asili, kwa hali, na kwa ukubwa kama lilivyo Neno la Mungu. Kila tendo la kutojali na la uzembe, kuitenda vibaya mashine hii ya ajabu iliyo mali ya Mungu, kwa kutojali sheria zake zilizoelezwa wazi katika mwili wa mwanadamu, ni uasi wa sheria yake Mungu. Twaweza kuona na kuisifu kazi ya Mungu katika viumbe wa asili, lakini mwili wa mwanadamu ndio kitu cha ajabu kabisa. 4 KN 243.6

Kwa kuwa kawaida ya vitu vyote ni sheria za Mungu, ni dhahiri kuwa ni wajibu wetu kujifunza sheria hizo kwa uangalifu. Yatupasa kujifunza masharti yake kwa habari za miili yetu wenyewe na kuzitii. Kutojali mambo nayo ni dhambi. KN 244.1

Wanaume kwa wanawake wakiwa wameongoka kweli kweli, wataziheshimu kwa uaminifu kanuni za maisha ambazo Mungu ameziweka mwilini mwao, hivyo watatafuta kuepukana na udhaifu wa mwili, akili, na tabia ya moyoni. Utii wa sheria hizo hauna budi kufanywa kuwa wajibu umpasao kila mtu. Sisi wenyewe hatuna budi kupatwa na madhara ya kuiasi hiyo sheria. Hatuna budi kutoa habari kwa Mungu kwa ajili ya mazoea na matendo yetu. Kwa hiyo, swali kwetu si, “Walimwengu watasema nini?” Bali, “Nikiwa nadai kuwa ni Mkristo, nitautendeaje mwili niliopewa na Mungu? Je, nitafanya kazi kwa ajili ya ubora wa mambo ya dunia hii na ya kiroho kwa kuutunza mwili wangu kama hekalu akaapo Roho Mtakatifu, ama nitajitia mwenyewe katika mawazo na desturi za walimwengu?” 5 KN 244.2

Uzima wa Mungu Rohoni Ndilo Tumaini la Pekee la Mwanadamu

Dini ya Biblia si kitu cha kudhuru afya ya mwili wala akili. Mvuto wa Roho wa Mungu ni dawa nzuri sana kwa maradhi. Mbingunbi pote kuna afya; na kadiri mivuto ya mbinguni inavyozidi kujulikana, ndivyo hakika wagonjwa wanaoamini watakavyozidi kupona. Mafundisho ya kweli ya dini ya Kikristo huwafunulia wote chimbuko la furaha kubwa mno. Dini ni chemchemi inayobubujika daima, ambayo Wakristo huweza kunywa humo wapendavyo, wala wasiwezi kuikausha, chemchemi hiyo. KN 244.3

Hali ya mawazoni huwa na matokeo katika afya ya mwili. Ikiwa mawazo yana furaha, bila wasiwasi, kutokana na dhamiri safi za matendo mema na kuridhika kwa kuwafurahisha wengine, huanzisha uchangamfu ambao utarudisha hali kwenye mwili mzima, ukiufanya mwendo wa damu mwilini kuwa mzun zaidi, na kuutia nguvu mwili mzima. Mbaraka wa Mungu ni uwezo uponyao, na wale ambao huwafaidia wengine kwa wingi wataufahamu mbaraka huo wa ajabu moyoni na maishani pia. KN 244.4

Watu ambao wamejifurahisha kwa mazoea mabaya na matendo ya dhambi, bila kujizuia wakijitoa kwa uwezo wa Neno la Mungu, kutumiwa kwa hivo kweli moyoni huamsha nguvu za tabia njema, ambazo zilielekea kuwa zilipooza. Mwenye kuupokea huwa na ufahamu wenye nguvu zaidi, na bora kuliko alivyokuwa kwanza kabla hajaikaza roho yake kwenye Mwamba wa milele. Hata afya yake ya mwili huzidi kuwa bora kwa kufahamu usalama wake akiwa ndani ya Kristo. 6 KN 244.5

Watu wanastahili kujifunza kwamba mibaraka ya utii kamili wanaweza kuipata kama wakiipokea neema ya Kristo. Neema yake ndiyo inayomwezesha mtu kuzitii sheria za Mungu. Hii ndiyo inayomwezesha atoke katika kifungo cha mazoea mabaya. Ni uwezo huu peke yake uwezao kumfanya mtu adumu katika njia sawa. KN 245.1

Injili ni dawa ya kuponya magonjwa ambayo asili yake ni dhambi, kama ikipokewa na usafi na uwezo wote. Jua fa Haki litawazukia, “lenye kuponya katika mbawa zake.” Vitu vyote vitokavyo ulimwengum humu sivyo viwezavyo kuuponya moyo uliovunjika, wala kuleta amani mawazoni, wala kuondoa taabu wala kufukuza magonjwa. Fahari, akili halisi, ama majaliwa-vyote haviwezi kuuchangamsha moyo wenye huzuni wala kumrudishia mtu siku za maisha zilizotumiwa ovyo. Tumaini la pekee la mtu ni uhai wa Mungu moyoni mwake. KN 245.2

Upendo ambao Kristo anaueneza katika mwili mzima una uwezo utiao uhai. Kila kiungo-ubongo, moyo, mishipa ya fahamuhuguswa na kuponywa na uwezo huo. Kwa njia yake nguvu za mtu zinaamshwa ili zitende kazi yake. Unauondolea moyo hatia na huzuni, mashaka na taabu, ambazo huvunja nguvu za uzima. Hivyo huleta weupe wa moyo na utulivu. Unatia moyoni furaha ambayo hakuna kitu cho chote duniani kiwezacho kuiharibu,-yaani, raha ya roho, itiayo afya na uzima.

Maneno ya Mwokozi wetu, “Njoni kwangu, nami nitawa-

pumzisha,” ni dawa iliyoamriwa kwa ajili ya kuponya magonjwa ya mwilini, akilini na rohoni Ingawa wanadamu wamejiletea wenyewe taabu kwa matendo yao maovu, Mwokozi huwaangalia kwa nuruma. Kwake wanaweza kupata msaada. Atawafanyia makuu wale wanaomwamini. 7

Onyesha Utengemano wa Afya

Katika kazi yetu imepasa uangalifu mkubwa kutumiwa kwa utengemano wa kuwa na kiasi. Kila kazi inayohitaji utengemano huo huleta kuongoka, imani na utii. Yaani, huinua mtu kwenye maisha mapya na yaliyo bora zaidi. Hivyo kila utengemano wa kweli una mahali pake katika kazi ya ujumbe wa malaika wa tatu. Hasa kuwa na kiasi hudai uangalifu na msaada wetu. Katika mikutano yetu ya makambi ya kila mwaka tungeangalia kazi hii na kuifanya jambo lenye nguvu. Yafaa kuwaonyesha watu kanuni za kuwa na kiasi kwa kweli na kuwaita watu kutia sahihi ahadi ya kuwa na kiasi. Uangalifu mkubwa ungetumiwa kwa wale ambao wametawaliwa kabisa na mazoea mabaya. Yatupasa kuwaongoza kwenye msalaba wa Kristo. KN 245.5

Kadiri tunavyoukaribia mwisho hatuna budi kuzidi kuinuka juu kwa jambo hili la utengemano wa afya na kuwa na kiasi cha Kikristo, tukionyesha jambo hilo kwa njia dhahiri na thabiti. Yatupasa kujitahidi daima kuwafundisha watu, siyo kwa maneno yetu tu, bali kwa vitendo vyetu pia. Maneno na matendo yakiungana yana mvuto wenye nguvu. 8 KN 246.1

Sura Ya 39 - Faida ya Usafi

ILI kuwa na afya njema, hatuna budi kuwa na damu nzuri; maana damu ni mkonao wa uhai. Hujenga mahali palipoharibika, na kuulisha mwili. Ikipatiwa vyakula bora kwa afya na kusafishwa pamoja na kutiwa nguvu kwa kukutana na hewa safl, hupeleka uhai na nguvu kwa kila sehemu ya mwili. Kadiri mwendo wa damu mwilini unavyokuwa kamili, ndivyo na kazi hii itakavyotimizwa vizuri. 1 KN 247.1

Kutumia maji kwa kuusafisha mwili ni njia nyepesi ya kufaa sana kuurahisisha mwendo wa damu mwilini. Kuoga maji baridi au maji ya uvuguvugu kwafaa sana kwa ajili ya kuutia mwili nguvu. Maji ya kuogea yenye joto la kadiri huvifunua vinyweleo, na hivyo husaidia kuondoa uchafu mwilini. Kuoga kwa maji ya uvuguvugu au yenye joto la kutosha hutuliza na kuburudisha neva na kuusawazisha mwendo wa damu mwilini. KN 247.2

Mazoezi ya viungo vya mwili yanatia damu nguvu na kuusawazisha mwendo wake mwilini, lakini kukaa kivivu huifanya damu, isisaflri salama, na kwa hiyo mabadiliko ndani yake, ambayo ni ya muhimu sana kwa uhai na afya ya mwili, hayafanyiki. Ngozi pia haitendi kazi yake. Uchafu hautolewi kama vile ambavyo ingalikuwa ikiwa mwendo wa damu ungeharakishwa kwa kufanya mazoezi ya juhudi, na kuitunza ngozi ya mwili iwe na hali njema ya afya, pamoja na kuvuta hewa safi kwa wingi mapafuni. 2 KN 247.3

Yafaa mapafu kuachiwa nafasi ya kutosha iwezekanavyo. Ukubwa wake hunyoshwa na kunyumbuka kwa kupumua vizuri bila mbano wo wote; hupungua yakizuiwa na kubanwa. Kwa hiyo matokeo mabaya ya kuyabana yanaonekana, hasa kwa wale wafanyao kazi za kuketi kitako, wakizoea kujikunyata wasiketi wima. Kuketi hivi ni vigumu kupumua vizuri. Hatimaye kupumua kwa juu juu huwa mazoea, na mapafu hupoteza uwezo wake wa kunyumbuka. KN 247.4

Hivi, mwili haupati ‘oxygen’ ya kutosha. Damu huzunguka mwilini pole pole. Uchafu wenye sumu ambao unafaa kutoka mapafum wakati wa kuvuta pumzi, hukawilishwa, na damu huchafuka. Kwa njia hii, licha ya mapafu, hata na tumbo, ini na ubongo pia hudhuriwa. Ngozi inakunjuka na kupoteza rangi yake; kazi ya matumbo ya kukiyeyusha chakula hukawilishwa; moyo hupunguzwa nguvu; ubongo husumbuliwa; na mafikara huchafuliwa, moyo huwa mzito, na mwili wote hudhoofika na kulegea; na hivi huwa katika hali ya kupatwa na ugonjwa kwa urahisi. KN 247.5

Mapafu huwa aaima yanajiondolea uchafu, na hiyo yanahitaji kupewa hewa safi kwa uthabiti. Hewa chafu haiwezi kutoa okisijeni inayotakiwa, na hivyo damu hupita mpaka kwenye ubongo na hata kwenye viungo vingine vya mwili bila kutiwa nguvu. Kwa sababu hiyo kupisha hewa safi kwa kweli ni kitu cha lazima. Kuishi katika vyumba vilivyofungwa, vyenye uhaba wa kuingiza hewa safi, ambapo hewa imehanbika na mbovu, kunadhoofisha mfumo wote. Mwili unakuwa mwepesi wa kuona baridi kwa njia ya peke yake, na ukikaa nje penye baridi kidogo tu unavuta magonjwa. Kujifungia ndani ya nyumba ndiko kunakofanya wanawake wengi wawe dnaifu na kugeuka rangi. Wanavuta hewa iyo hiyo wakati wote mpaka inajaa vitu vyenye sumu zilizotupwa nje kwa njia ya mapafuni na kwenye vinyeleo, na hivyo uchafu hurudishwa tena kwenye damu. 3 KN 248.1

Wengi huumia kwa ugonjwa kwa sababu hawakubali kupata hewa safi ya usiku vyumbani mwao wakati wa usiku. Hewa safi ya anga, itolewayo bure, ni mojawapo ya mibaraka mikubwa tuwezayo kuifaidi. 4 KN 248.2

Usafi kamili katika kila jambo ni lazima kwa afya ya mwili na ya rohoni. Uchafu wa kila namna huondolewa mwilini daima kwa njia ya ngozi. Vinyweleo milioni vya ngozi huzibwa upesi visiposafishwa kwa maji mara kwa mara, na hivi uchafu ambao ungepitia ngozini huwa unavizidishia kazi viungo vingine vinavyoondosha uchafu toka mwilini. KN 248.3

Watu wengi wangefaidiwa kama wangeoga kila siku kwa maji baridi au yaliyo vuguvugu, asubuhi au jioni. Badala ya kuwa na nali ya kupatwa na mafua, akifanya bidii kuoga kila siku, atazuia mafua, kwa sababu kuoga kuna rahisisha mwendo wa damu mwilini; damu hukaribiwa na ngozi, na kutiririka kwa urahisi katika mishipa yake. Ubongo na mwili pia hutiwa nguvu. Musuli zinaweza kujimudu kwa urahisi zaidi, na akili zinaamshwa. Kuoga kunaburudisha neva. Kuoga kunasaidia matumbo na ini, na kuziletea afya na nguvu sehemu hizo, na hufanya tumbo kukiweza chakula. KN 248.4

Pia ni jambo la muhimu kuwa mavazi yawe safi, Mavazi yaliyovaliwa hushika uchafu unaotoka mwilini kwa njia ya vinyweleo; na yasipobadilishwa mara kwa mara na kusafisnwa, uchafu utaingizwa mwilini tena. KN 248.5

Uchafu wa kila namna huleta ugonjwa. Vijidudu vinavyoleta kifo hujificha mahali pa giza, katika pembe za nyumba zisizofagiliwa, katika takataka zilizooza, na penye chepechepe, kutu na koga. Mboga inayotupwa, au mafungu ya majani ya miti yaliyopukutika, yasingeachwa karibu na nyumba yaoze na kuitia hewa sumu. Kitu cho cnote kilicho kichafu ama kinachooza hakina budi kuondolewa mbali na nyumba. KN 248.6

Usafi kamili mwanga wa jua, uangalifu mkuu juu ya kila kitu cha maisha ya nyumbai, haya yote ni mambo ya muhimu sana ili watu waepukane na magonjwa, na kuwa na furaha na nguvu nyumbani. KN 249.1

Wafundishe watoto kuwa Mungu hapendezwi kuwaona na miili iliyo michafu wala mavazi ya ovyo yaliyoraruka. Kuwa na mavazi safi itakuwa ndiyo njia mojawapo ya kuyaweka mafikara katika hali nzuri ya usafi. Hasa kiia kitu kinachogusana na ngozi kingewekwa safi. KN 249.2

Kamwe Kweli hakukanyaga kwa miguu yake miangalifu katika njia yenye uchafu wala unajisi. Yeye ambaye alikuwa mwangalifu sana ili kwamba wana wa Israeli wahifadhi mazoea ya usafi hataruhusu uchafu wo wote nyumbani mwa watu wake leo. Mungu huuchukia uchafu wo wote. KN 249.3

Pembe chafu, ambazo zimeachwa ovyo nyumbani bila kutunzwa, zitaelekea kufanya pembe chafu zisizoangaliwa moyoni mwa mtu. KN 249.4

Mbinguni ni mahali pasafi na patakatifu, na wale ambao hupita katika malango ya mji wa Mungu huvikwa usafi wa ndani na nje pia. 6

Sura Ya 40 - Chakula Tulacho

MIILI yetu hujengwa na chakula tulacho. Kila mara mwili wa mwanadamu hupoteza sehemu yake; kila kiungo kinapojimudu hutokwa na sehemu ndogo, na sehemu zile zinazotoka hurudishwa na chakula tulacho. Kila kiungo mwilini mwetu huhitaji mifupa, musuli, na neva pia zinahitaji sehemu zao. Ni kazi ya sehemu ya chakula; mifupa. Ubongo hauna budi kupata sehemu yake; ajabu sana inayobadilisha chakula kuwa damu, na kutumia damu hii kwa kuvijenga viungo mbalimbali vya mwili; lakini kazi hii inaeendelea daima, lkileta uzima na afya kwa kila neva, misuli na minofu. KN 250.1

Vyakula ambavyo yafaa kuchaguliwa kwa matumizi ni vile tu ambavyo vinahitajiwa kwa kuujenga mwili. Maana yake, si kwamba inatupasa kuchagua chakula kwa ajili ya utamu wake tu. Tamaa ya chakula ya watu wengi imepotoka kwa ajili ya desturi mbaya za kula. Mara nyingi hutamam chakula kinachodhoofisha mwili na kuleta udhaifu badala ya nguvu. Si lazima tuongozwe na desturi za kikabila. Maradhi mengi na maumivu yanayoenea pote duniani hutokana na makosa ya wanadamu katika kuchagua vyakula. KN 250.2

Lakini si kwamba vyakula vyote vilivyo na manufaa vinafaa mahitaji yetu katika hali zote. Ingetupasa kujihadhari sana katika hali zote. Ingetupasa kujihadhari sana katika kuvichagua vyakula. Chakula chetu kingefuatana na hali ya majira, hali ya nchi tunapokaa, pamoja na kazi tunayoifanva. Vyakula vingine ambavyo vinaweza kutumiwa katika majira fulani ya mwaka na katika hali fulani ya nchi havifai kutumiwa kwa hali ya nchi nyingine, na katika majira mengine. Hivyo kuna vyakula maalumu vinavyofaa kwa watu wanaofanya kazi za namna mbalimbali. Mara nyingi chakula kinachofaa kutumiwa na watu wanaofanya kazi ngumu za juhudi hakifai kutumiwa na watu wanaofanya kazi za ofisini za kuketi na kufikiri. Mungu ametupa namna mbalimbali za vyakula vyenye kuleta afya, na inampasa kila mtu achague namna ya vyakula ambavyo kwa ujuzi wake ameviona kuwa vinafaa kwa mahitaji yake. 1 KN 250.3

Mpango wa Kwanza wa Mungu kwa Chakula cha Mwanadamu

Ili kujua namna ya vyakula vilivyo bora kabisa, inatupasa kujifunza mpango wa kwanza wa Mungu juu ya chakula cha mwanadamu. Yeye aliyemwumba mwanadamu na kufahamu mahitaji yake ndiye aliyemchagulia Adamu chakula chake. Akasema, “Tazama, nimewapa kila mehe utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu.” (Mwa. 1:29). Adamu alipoondoka Edeni apate kuishi kwa kulima mashamba, baada ya kulaaniwa kwa ajili ya dhambi, aliruhusiwa kutumia pia “mboga za kondeni.” (Mwa. 3:18). KN 250.4

Nafaka, matunda, kokwa, na mboga ndivyo vyakula tulivyochaguliwa na Muumba wetu. Vyakula hivi, vikiandaliwa bila kukolezwa viungo vikali, huleta afya mwilini na kututia nguvu. Humtia mtu nguvu, uwezo wa kuishi miaka mingi, na akili timamu ambazo hazipatikani katika vyakula vilivyoungwa sana. 2 KN 251.1

Mtu akitaka kudumu kuwa na afya njema, inampasa apate chakula kizuri cha kutosha, na kinachoujenga mwili. KN 251.2

Tukipanga mambo kwa busara, vyakula vinavyoleta afya vinaweza kupatikana karibu katika kila nchi. Namna mbalimbali za mchele, ngano, mahindi na shayiri zinapelekwa pande zote, na maharagwe, mbaazi na dengu vilevile. Vyakula hivi, pamoja na matunda ya asili pamoja na yale yanayoletwa kutoka nchi nyingine, na namna nyingi za mboga zinazositawi katika kila nchi, hutuwezesha kuchagua ulaji ya namna nyingi tupendavyo bila kutumia nyama. KN 251.3

Popote yapatikanapo matunda yaliyokaushwa, kama zabibu kavu, zambarau, na matunda madogo madogo kama vile maepo, mapea, mapichi, na aprocots kwa bei ya chini, yangetumiwa kama chakula cha kawaida, kwa sababu yanafaa sana kwa afya, na yanaweza kutumiwa na watu wanaofanya kazi ya aina yo yote. 3 

Elimu ya Upishi

Upishi si elimu ya kudharauliwa, na ni kazi ya muhimu zaidi katika maisha ya kila siku. Ni elimu inayompasa kila msichana kujifunza, na ingefundishwa kwa namna inayoweza kuwanufaisha watu wa aina zote. Kupika chakula kisichokolezwa kwa viungo, chenye manufaa, tena kukitengeneza kiwe kitamu, inatakikana ujuzi mwingi; lakini inawezekana. Inawapasa wapishi kujua namna ya kukitengeneza chakula chepesi kwa njia rahisi na ya afya, ili kiwe kitamu, na chenye kuitia afya, kwa jinsi kilivyotengenezwa bila kuchanganywa na viungo vingi. 4 KN 251.5

Tumnyeni maendeleo ya akili katika kukifanya chakula chetu kuwa chepesi (kisichokolezwa kwa viungo vikali) kwa majaliwa ya Mungu kila nchi hutoa vitu mbalimbali vyenye kutia afya ambavyo ni muhimu kwa kuujenga mwili. Hivi vyaweza kufanywa viwe vyakula vya kupendeza vitiavyo afya. 5 KN 251.6

Wengi hawaoni kuwa hili ni jambo liwapasalo, kwa hiyo, hawajaribu kutayarisha chakula vizuri. Hilo laweza kufanywa kwa njia nyepesi ya kutia afya, na kwa urahisi, bila kutumia shahamu, siagi, wala nyama. Akili haina budi kuchanganywa na utovu wa viungo vya chakula. Ili kufanya hivi, wanawake hawana budi kusoma, kisha kwa saburi, kuyapatanisha mambo wasomayo na kuyatumia maishani. 6 KN 251.7

Matunda, nafaka, na mboga za majani, vikitayarishwa kwa njia nyepesi bila kutiwa viungo wala shahamu yo yote, na kuchanganywa na maziwa au mafuta yanayopatikana katika maziwa yaliyochemshwa (cream) huwa chakula bora sana kwa afya. 7 KN 252.1

Nafaka na matunda bila shahamu, yakiwa na hali yake ya asili kadiri iwezekanavyo, hufaa kuwa chakula mezani mwa wote wanaodai kujitarisha kutwaliwa mbinguni. 8 KN 252.2

Sukari nyingi zaidi inatumiwa katika chakula. Keki, maandazi, sambusa, ute mzito ulio mtumu (jelly) na mraba vinakifanya chakula kisiyeyushwe kwa urahisi tumboni. Vyakula vyenye madhara zaidi ni vile vinavyotengenezwa kwa kuchanganya maziwa, sukari na mayai pamoja. Kutumia kwa wingi maziwa na sukari pamoja hakufai. 9 KN 252.3

Kadiri sukari pangufu inavyotumiwa katika kutayarisha chakula, ndivyo matata yanayotokana na joto la hali ya nchi yatakavyozidi kupungua. 10 KN 252.4

Maziwa yakitumiwa, yafaa kuchemshwa kabisa ili kuviua vijidudu vya ugonjwa; onyo hili likishikwa, hakuna hatari sana ya kupatwa na ugonjwa katika kutumia maziwa. 11 KN 252.5

Pengine utafika wakati ambapo haitakuwa salama kutumia maziwa. Lakini, ikiwa ng’ombe ni wenye afya na maziwa yakichemshwa vizuri, hailazimu kuufanya wakati huo wa shida ufike mapema zaidi kabla ya wakati wake. 12 KN 252.6

Vyakula Vilivyokolezwa Sana kwa Viungo KN 252.7

Viungo vikali vya kukoleza chakula, ambavyo mara nyingi hutumiwa na walimwengu, hudhuru kazi ya kukiyeyusha chakula tumboni. 13 KN 252.8

Katika zama hizi za ufasiki, chakula kisichochochea mwili chafaa zaidi, Kwa kawaida viungo vya kukoleza huleta madhara. Haradali, pilipili, viungo vingine vya chakula kama vile basibasi, dalasini, achali na vitu vingine vya jinsi hii, vinaunguza matumbo na kuuharakisha mwendo wa damu na kuunajisi. Hali ya kuungua inayoonekana katika matumbo ya mlevi ni kielelezo cha matokeo ya pombe. Hali ifananayo na hii inapatikana kwa kuvitumia viungo vya chakula vinavyounguza matumboni. Halafu mtu hawezi kuridhika na utamu wa chakula cha kawaida. .14 Mwili utakuwa ukihitaji na kutamani sana kitu ambacho huonekana kwamba kinautia mwili nguvu kumbe sivyo14 KN 252.9

Wengine wameiendekeza tamaa vao ya chakula, kama wasipopata chakula kile hasa wanachokitamani, hawana raha chakulani. Ikiwa viungo vikali vya chakula na vyakula vilivyokolezwa huwekwa mbele yao, hulifanya tumbo kutenda kazi kwa kutumia mchapo huo mkali; maana limetumiwa vibaya hata haliwezi tena kukubali chakula kisichochochea. 15 KN 253.1

Viungo vya chakula kwanza vinaunguza matumbo, lakini hatimaye hunaribu wepesi wa asili wa utando mweroro wa tumboni. Damu huchafuka, tamaa za kinyama huamshwa, huku nguvu za tabia ya uadilifu na za akili hudhoofishwa, na kutumikia tamaa mbaya zaidi za mwili. Yafaa mama ajifunze kuandaa chakula chepesi, kisichokolezwa kwa viungo, lakini chenye kuulisha mwili, mbele ya jamaa yake. 16

Wakati wa Kawaida wa Kula Chakula

Baada ya kula mlo wa kawaida, yafaa tumbo lipewe nafasi va kupumzika muda wa saa tano. Kipande cho chote cha chakula kisitiwe tumboni mpaka mlo mwingine. Katika nafasi hiyo tumbo litafanya kazi yake, kisha litakuwa tayari kupokea chakula kingine zaidi. 17 KN 253.3

Kula kwa wakati usiobadilika ni jambo lipasalo kuangaliwa sana. Haifai kula cho chote kati ya milo, pipi, njugu, matunda, wala chakula cha namna yo yote. Kutokuwa na saa za kawaida za kula chakula huharibu hali njema ya afya ya viungo vinavyoyeyusha chakula tumboni, hata kuidhuru afya na raha. Pia watoto wakifika mezani, hawapendezwi na vyakula bora; tamaa zao hukitamani kile ambacho ni chenye kuwadhuru. 18 KN 253.4

Tulalapo, yafaa tumbo liwe limefanya kazi yake yote, ili lipate kupumzika pamoja na viungo vinginevyo vya mwili. Hasa kwa watu wanaofanya kazi za kuketi, ni vibaya kula chakula usiku sana. KN 253.5

Mara nyingi uchovu unaoleta tamaa ya chakula huonekana kwa sababu viungo vinavyoyeyusha chakula vililemewa na kazi ngumu zaidi wakati wa mchana. Baada ya kula mlo mmoja, viungo vile vinavyokiyeyusha chakula vinahitaji kupumzika. Saa tano au sita zingepita katikati ya mlo mmoja na mwingine; na watu wanaofuata utaratibu huu wataona ya kwamba milo miwili yafaa kwa siku moja kuliko mitatu. KN 253.6

Desturi ya kula milo miwili kwa siku inaonekana hasa kuwa jambo la kufaa kwa afya; lakini, wakati mwingine, huenda watu wakahitaji mlo wa tatu. Walakini, kama ukitwaliwa, yafaa uwe kidogo sana, na wa chakula ambacho huyeyushwa kwa urahisi sana tumboni. 20 KN 253.7

Wanafunzi wakiwa wanachanganya kazi za juhudi za mwili na zile za akili hakuna kizuizi cha mlo wa tatu hata kidogo, wanafunzi hao waweza kuwa na mlo wa tatu, unaotayarishwa bila kuwa na mboga za majali, bali mwepesi wenye chakula bora, kama vile matunda na mkate. 21 KN 254.1

Haifai kula chakula kilicho na moto sana wala baridi sana. Chakula kikiwa baridi sana, nguvu ya tumboni hulazimishwa kukitia chakula hicho joto kabla ya kuanza kukiyeyusha. Vinywaji vya baridi havifai kwa sababu hiyo hiyo; pia kutumia sana vinywaji ndivyo inavyozidi kuwa vigumu kukiyeyusha chakula tumbom; kwa sababu ni lazima vinywaji vichujwe kwanza, ndipo kazi ya kukiyeyusha chakula ianzishwe. Usitumie chumvi nyingi sana, jiepushe na achali na vyakula vilivyokolezwa kwa kutiwa viungo vingi, tumia matunda mengi, na hamu ya maji mengi wakati ule ule wa chakula itatoweka. Yafaa chakula kiliwe pole pole, na kutafunwa kabisa. Jambo hili ni la muhimu ili mate yachanganywe vizuri na chakula, kiwe tayari kutumiwa na kuyeyusnwa na dawa za tumboni. 22 

Matumizi ya Kanuni za Matengeneo ya Afya

Kuna busara kweli katika matengenezo ya vyakula. Yafaa somo hili kuchunguzwa sana kwa ndani, na asiwepo mtu mwenye kuwalaumu wengine kwa sababu desturi yao katika mambo yote haipatani na ile yake mwenyewe. Haiwezekani kufanya kawaida moja kusawazisha mazoea ya kila mmoja; na haifai mtu ye yote kujifikiri kuwa yu kipimo cha tabia kwa wote. Watu wote hawawezi kula vitu vya namna moja. Vyakula ambavyo ni vitamu na vizuri kwa mtu mmoja huenda vikawa vya kumchukiza, ama hata kumdhuru mwingine. Wengine hawawezi kutumia maziwa, huku wengine wakinenepeshwa nayo. Watu wengine njegere na kunde haziwezi kuwatulia tumboni; wengine huziona ni chakula bora. Kwa wengine nafaka isiyosafishwa maganda ni chakula kizuri kwao, ambapo wengine hawawezi kabisa kuzitumia. 23 KN 254.3

Wale ambao wameyaendekeza mazoea mabaya ya ulaji, inawapasa kuongoka upesi na kuyaacha mazoea yale, pasipo kukawia. Ugonjwa wa kutokiweza chakula vizuri tumboni (dyspepsia) ukisha kuingia kutokana na kulitumikisha tumbo vibaya, ni heri jitihadi ifanywe kwa uangalifu ili kuihifadhi nguvu iliyobaki katika viungo vyenye maana sana kwa uzima, kwa kuacha kila tendo linalolemea tumbo. Pengine haliwezi kupona kabisa na kuirudia hali yake ya kawaida baada ya kutumiwa vibaya kwa muda mrefu; lakini kutumia chakula kinachofaa kunaweza kuzuia udhaifu usizidi; na wengine wanaweza kupata nafuu au kupona kabisa. KN 254.4

Watu wenye nguvu ambao kila siku hufanya kazi za juhudi, haiwalazimu kujihadhari sana juu ya utamu au wingi wa chakula walacho, kama wale wafanyao kazi za kuketi; lakini hata wale wafanyao kazi za juhudi wangekuwa na afya bora kama wangezoea kujizuia katika kula na kunywa. KN 255.1

Wengine wangependa pawe na kanuni halisi juu ya chakula kinachowafaa. Hakuna mtu awaye yote awezaye kuweka kanuni halisi za chakula kwa mwingine. Ingempasa kila mtu kutumia akili zake mwenyewe na kujitawala na kufanya mambo kwa kuzishika kanuni. 24 KN 255.2

Yafaa kuzidisha ubora wa chakula kuwe jambo la kuendelea daima. Kadiri magonjwa kwenye wanyama yanavyozidi, ndivyo kutumia maziwa na mayai kutakavyozidi kuwa jambo la hatari. Yafaa jitihadi zifanywe kupata vitu vingine badala yake ambavyo ni bora kwa afya na vya bei isiyo kubwa. Yafaa watu kila mahali wafundishwe jinsi ya kupika bila kutumia maziwa wala mayai, kadiri iwezekanavyo, lakini, wawe na chakula kizuri tena kitamu. KN 255.3

Mungu hatukuzwi miili yetu isipotunzwa ama ikitumiwa vibaya, na kwa njia hiyo hufanywa isifae kwa kazi yake. Kutunza mwili kwa kuupatia chakula kilicho na ladha na chenye kutia nguvu ni mojawapo ya wajibu wa kwanza wa mwenye nyumba. Ni heri kuwa na nguo na vyombo vya bei ndogo kuliko kujihinisha chakula. KN 255.4

Wenye nyumba wengine hutoa chakula kidogo mezani mwa watu wa nyumbani mwao ili wawakaribishe wageni kwa vyakula vya bei kubwa. Hiyo si busara. Yafaa makaribisho ya wageni yawe mapesi zaidi. Mahitaji ya watu wa nyumbani hayana budi kuangaliwa kwanza. KN 255.5

Kutotumia fedha kwa uangalifu pamoja na desturi zingine za kuiga ovyo mara nyingi huzuia ukarimu unapotakikana ambapo ungekuwa mbaraka. Kiasi cha chakula kwa kawaida mezani mwetu kingekuwa cha kutosha kusudi mgeni asiyetazamiwa akifika aweze kukaribishwa bila kumtwisha mzigo mama mwenye nyumba kufanya matayarisho mengine ya chakula. KN 255.6

Fikiria juu ya chakula chako kwa uangalifu. Jifunze njia itakayoleta matokeo mema. Kuza tabia ya kujizuia. Itawale tamaa ya chakula kwa busara. Kamwe usilitumie vibaya tumbo kwa kula kupita kiasi, lakini usijinyime chakula bora na kitamu kitakiwacho kwa afya. KN 255.7

Wale ambao huzifahamu kanuni za afya na wenve kutawaliwa na kanuni, wataepukana na vyakula vya anasa na kutojihusuru pia. Chakula chao huchaguliwa, siyo kwa ajili ya kuridhishwa tamaa ya chakula, bali kwa ajili ya kuujenga mwili. Wanatafuta kuuhifadhi kila uwezo katika hali njema kabisa kwa ajili ya kazi bora sana kwa Mungu na kwa wanadamu pia. Tamaa ya chakula hutawaliwa na akili na dhamiri ya moyoni, nao hupata ijara ya afya njema ya mwili na akili. Huku wakiwa hawasisitizi vibaya maoni yao kwa wengine, kielelezo chao ni ushuhuda wa mafundisho mazuri. Watu nawa wanao mvuto mkubwa kwa mema. 25 KN 255.8

Haitupasi kutumia chakula kingi zaidi siku ya Sabato. Badala ya kufanya hivyo, chakula kingekuwa chepesi, na kingeliwa kiasi cha kutosha tu, kusudi tuwe na akili timamu yenye nguvu ya kuyafahamu mambo ya kiroho. KN 256.1

Kupika chakula siku ya Sabato kungeepukwa; lakini maana yake si kwamba hatuna budi kula chakula baridi. Katika siku za baridi chakula kilichopikwa Ijumaa kingepashwa moto. Na ulaji wote ya siku ya Sabato, ingawa niwepesi namna gani, uwe ‘mtamu na wa kupendeza. Hasa katika nyumba ambapo kuna watoto, ni jambo jema, siku ya Sabato, kutumia chakula fulani kipendwacho, ambacho watu wa nyumbani humo hawakitumii kila siku. 26 

Kuitawala Tamaa ya Chakula na Uchu

Mojawapo ya majaribu makali kabisa ambayo mtu hana budi kuyakabili ni juu ya jambo la tamaa ya chakula. Kuna uhusiano wa ajabu baina ya akili na mwili. Hugeuzana. Kuutunza mwili katika hali ya afya, kukuza nguvu zake, ili kila sehemu ya mashine hii yenye uhai ipate kutenda kazi vizuri, yafaa liwe jambo la kwanza kuangaliwa maishani mwetu. Kutoujali mwili ni kutozijali akili za moyoni. Mungu hawezi kutukuzwa watoto wake wakiwa wenye miili dhaifu, ama akili zilizodumaa. Kuiridhisha tamaa kwa kuihatarisha afya ni kuzitumia vibaya akili kwa jambo lisilo la haki, Wale wenye kushiriki namna yo yote ya kutokuwa na kiasi, katika kula ama katika kunywa, hutupa ovyo nguvu zao za mwili na kuudhoofisha uwezo wa tabia ya uadilifu. Wataona malipo ambayo hufuatana na uasi wa sheria za mwili. 27 KN 256.3

Wengi hunyang’anywa nguvu za kazi akilini na mwilini pia kwa kula kupita kiasi na kujianisi. Tamaa za mwili hutiwa nguvu, huku hali takatifu na ya kiroho ikidhoofishwa. Tutakaposimama kukizunguka kile kiti kikuu cheupe cha enzi, habari za maisha ya wengi zitaonekana kuwa za ajabu kama nini. Ndipo wataona kile ambacho wangaliweza kufanya kama wasingaliuharibu uwezo wao waliopewa na Mungu. Kisha watatambua kipeo cha akili ambacho wangaliweza kupata kama wangalimpa Mungu nguvu zao zote za mwili na akili alizowakabidhi. Kwa majuto na maumivu mengi moyoni watatamani laiti wangeweza kuishi tena. 28 KN 256.4

Kila Mkristo wa kweli atatawala tamaa yake ya chakula pamoja na tamaa mbaya za mwili. Asipokuwa huru, na kutotawaliwa na tamaa ya chakula hawezi kuwa mtumishi mwaminifu na mtiifu wa Kristo. Kuiendekeza tamaa ya chakula na uchu ndilo jambo linalofanya ukweli usiwe na matokeo mema moyoni. Haiwezekani Roho na uwezo wa Neno la kweli kumtakasa mtu, roho, mwili na moyo, akiwa anatawaliwa na tamaa ya chakula pamoja na uchu. 29 KN 256.5

Sababu kubwa iliyoacha Kristo astahimili kule kufunga muda mrefu jangwani ilikuwa kutufundisha jinsi ilivyo muhimu kujikana nafsi mwenyewe na kuwa na kiasi. Yafaa kazi hiyo ianze mezani mwetu nayo haina budi kufululizwa katika mambo yote yahusuyo maisha. Mkombozi wa ulimwengu alikuja kutoka mbinguni kusaidia mwanadamu katika udhaifu wake, ili, kwa uwezo ambao Yesu alikuja kumletea, apate kuwa mwenye nguvu kushinda tamaa ya chakula na uchu, na kuwa mshindaji wa kila jambo. 30 

Sura Ya 41 - Vyakula vya Nyama

MUNGU aliwapa wazazi wetu wa kwanza chakula alichokusudia wanadamu wakile. Ilikuwa kinyume cha mpango wake kuua kiumbe cho chote. Hakupasa pawepo mauti katika Edeni. Matunda ya miti bustanini, yalikuwa chakula alichohitaji mwanadamu. Mungu hakumruhusu mwanadamu kula nyama mpaka baada ya gharika. Kila kitu ambacho mwanadamu angeweza kuponea kilikuwa kimekwisha kuharibiwa, na kwa hiiyo Mungu akampa Nuhu ruhusa kwa ajili ya riziki yao kula wanyama safi aliokuwa amewachukua ndani ya safma. Lakini nyama haikuwa chakuia chenye kutia afya kwa mwanadamu. KN 258.1

Baada ya gharika watu walikula zaidi chakula cha nyama. Mungu aliona kuwa njia za mwanadamu zilikuwa mbovu, na ya kuwa huelekea kujiinua kwa kiburi na kufanya kinyume cha mwumbaji wake na kufuata tamaa za moyo wake mwenyewe. Naye akawaruhusu watu wale waliokuwa wenye maisha marefu kula chakula cha nyama apate kuyafupisha maisna yao ya dhambi. Mara baada ya gharika watu wakaanza kupungua upesi kimo na miaka. 1 KN 258.2

Katika kukiteua chakula cha mwanadamu Edeni, Mungu alionyesha kile ambacho kilikuwa bora kuliko vingine vyote; katika kuteua Israeli alifundisha fundisho lile. Kwa njia yao alitaka sana kuwabariki na kuwafundisha walimwengu. “Mkate wa mbinguni.” Kwa sababu tu ya kutoridhika kwao na kunung’unika kwao kwa ajili ya vyungu vya nyama ya Misri ndiyo sababu tu iliyoacha wanewe chakula cha nyama, nacho kilitolewa kwa muda mfupi tu. Kukitumia kulileta magonjwa na kufa kwa maelfu. Ingawa ya hayo kutumia chakula kisicho cha nyama halikuwa jambo lililopendwa kwa moyo. Kikaendelea kuwa asili ya kutoridhika na kuleta manung’uniko wazi au siri, nacho hakikufanywa kiwe cha daima. KN 258.3

Katika kukaa kwao Kanaani, Waisraeli waliruhusiwa kutumia chakula cha nyama, lakini kwa masharti maalumu, ambayo yalielekea kupunguza matokeo mabaya ya baadaye. Kutumia nyama ya nguruwe kulikatazwa, na pia nyama ya wanyama wengine na ndege na samaki wengine hawakuwa halali. Juu ya nyama lliyoruhusiwa, kula shahamu na damu kulikatazwa vikali. KN 258.4

Wanyama hao waliweza tu kutumiwa kwa chakula wakiwa katika hali njema. Hakuna kiumbe kilichoraruliwa, kilichokufa chenyewe, wala kisichotolewa damu kwa uangalifu, kilichoweza kutumiwa kwa chakula. KN 258.5

Kwa kuasi mpango wa Mungu ulioamriwa kwa habari za chakula. Waisraeli walipata hasara kubwa. Walikitamani chakula cha nyama, wakavuna matokeo yake ya baadaye. Hawakukifikia kipeo cha Mungu cha tabia wala kulitimiza kusudi lake. Bwana “akawapa walichomtaka, akawakondesha roho zao” (Zab. 106:15). Walithamini anasa za dunia zaidi ya mambo ya kiroho, na hawakupata sifa takatifu ambayo aliwakusudia. KN 259.1

Wale wanaokula nyama hula nafaka na mboga za majani zilizokwisha kutumika; maana mnyama hupata kutoka kwa vitu hivyo chakula ambacho husaidia kukua. Uzima uliokuwa ndani ya nafaka hizo hupita na kuingia ndani ya mwenye kuzila. Twaupokea kwa kula nyama ya mnyama hatimaye. Basi, ingekuwa bora kama nini kuupata moja kwa moja, kwa kula chakula ambacho Mungu ametupa sisi kukitumia! 2 

Asili ya Magonjwa Mengi

Kamwe nyama haikuwa chakula bora; lakini kuitumia sana kumekuwa jambo baya maradufu, kwa kuwa magonjwa ya wanyama huongezeka upesi sana. Mara nyingi kama wangewaona wanyama hao wakiwa hai na kujua hali ya nyama wanayoila, wangeiacha na kuichukia kabisa. Watu daima huila nyama inayojawa na vijidudu vya ugonjwa wa kifua kikuu na vya donda baya la ‘saratani’. Kifua kikuu, ‘saratani’ na magonjwa mengine makubwa huenezwa kwa njia hiyo. 3 

Kuelekea kushikwa na ugonjwa huzidishwa mara kumi kwa kula nyama. 4

Wanyama wana ugonjwa, na kwa kuishiriki nyama yao, twapanda mbegu za ugonjwa katika minofu na damu yetu wenyewe. Ndipo tukibadilisha makao na kuwekwa mahali penye malaria, twajiona kuwa tuko hatarini zaidi; pia tukiwa mahali penye magonjwa ya kulipuka na yenye kushika watu wengi pamoja na wenye kuambukiza, mwili hauna hali ya kujikinga. KN 259.4

Kwa nuru niliyopewa na Mungu, kuenea kwa ‘saratani’ na magonjwa mengine yanayoleta uvimbe hutokana zaidi na kula nyama kwa wingi. 5 KN 259.5

Mahali pengi samaki huharimishwa kwa uchafu wanaokula ambao huleta ugonjwa. Hali hiyo huonekana hasa mahali ambapo samaki hukutana na taka za kila namna za miji mikubwa. Samaki ambao wanajilisha takataka za maji hayo machafu huweza kupita mpaka kwenye maji yaliyo mbali, nao huweza kunaswa manali ambapo maji ni safi. Hivyo wakitumiwa kwa chakula huleta ugonjwa na mauti kwa wale wasiodhani kuna hatari kama hiyo. KN 259.6

Madhara ya chakula cha nyama wakati mwingine hayawezi kubainika upesi, lakini hilo si jambo lenye kukithibitisha kuwa hakina madhara. Ni wachache wawezao kusadikishwa kwamba nyama waliyokula ndiyo ambayo imetia sumu damu yao na kuwaletea maumivu. Wengi huuawa na magonjwa ambayo hutokana hasa na kula nyama, asili yake hasa haidhaniwi nao wenyewe wala na watu wengine. 6 

“Nguruwe Ni Najisi Kwenu”

Nyama ya nguruwe ina wingi wa vijidudu vya magonjwa; juu ya nguruwe Mungu amesema: “Huyu ni najisi kwenu; msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse” Kumbukumbu 14:8. Amri hiyo ilitolewa kwa sababu nyama ya nguruwe haifai kwa chakula. Nguruwe ni wanyama. Kamwe kwa hali iwayo yote, nyama yao haikustahili kuliwa na wanadamu. Haiwezekam kwa nyama ya kiumbe cho chote chenye uhai kuwa kitu kizuri kwa chakula ikiwa chakula cha kiumbe hicho ni uchafu, na kiumbe huyo akiwa mwenye kula kitu kibaya, chenye kuchukiza. 7 KN 260.1

Nyama ya nguruwe, ijapokuwa ni mojawapo ya vyakula vikuu, ni mojawapo ya vitu vyenye madhara makubwa. Mungu hakuwakataza Waebrania kula nyama ya nguruwe kwa kuonyesha tu madaraka yake, bali kwa sababu haikuwa kitu kizuri kwa chakula cha mwanadamu. Ingeweza kuujaza mwili vijidudu vya ugonjwa wa kuvimba, na hasa kwa kuwa katika hali ya nchi za joto huleta ukoma, na magonjwa ya namna nyingine mbalimbali Matokeo yake mwilini katika hali hiyo ya nchi yalikuwa mabaya zaidi kuliko katika nchi za baridi Nyama ya nguruwe zaidi ya nyama ya wanyama wengine wote, huleta hali mbaya katika damu. Wale wenye kula sana nyama ya nguruwe huweza kuambukizwa ugonjwa. 8 KN 260.2

Hasa misnipa mizuri ya fahamu ya ubongoni hudhoofishwa na kufanywa isiweze kufahamu mambo matakatifu, ila kuwekwa chini kwenye mambo hafifu. 9 KN 260.3

Wale wenye kufanya mazoezi mengi nje hawapatwi na madhara ya kula nyama ya nguruwe, kama wale ambao maisha yao ni ndani ya nyumba saa nyingi, na ambao wanayo mazoea ya kukaa kitako, na wenye kazi za kutumia akili. 10 KN 260.4

Madhara Yake Akilini na Rohoni

Ubaya wa nyama kwa tabia ya moyoni haupungui neno lo lote kwa yale madhara yake mwilini. Chakula cha nyama ni chenye kudhuru afya, na ijapokuwa matokeo yake mwilini yawe ya namna gani huwa yenye kudhuru akili na roho pia. 11 KN 260.5

Chakula cha nyama huibadili tabia na kutia nguvu hali ya kuvutwa kwa tamaa za mwili tu. Miili yetu hufanywa na chakula tulacho, na kula nyama kwa wingi kutapunguza uhodari wa akili. Wanafunzi wangeweza kufaulu mambo mengi zaidi katika masomo yao kama wasingeonja nyama. Kadiri minofu ya mwili wa mtu inavyotiwa nguvu kwa kula nyama, ndivyo uwezo wa akili unavyopungua. 12 KN 260.6

Kama kuna wakati ambapo yafaa chakula kiwe chepesi sana, sasa ndio wakati huo. Haifai kuweka nyama mbele ya watoto wetu. Madhara yake ni yenye kusisimua na kutia nguvu tamaa mbaya, na huelekea kuua uwezo wa tabia ya adili. 13 KN 261.1

Yafaa matengenezo makubwa zaidi yaonekane miongoni mwa watu wanaodai kutazamia kutokea kwa Kristo upesi. Matengenezo ya afya (health reform) hayana budi kufana miongoni mwa watu wa kanisa letu, kazi ambayo bado haijapata kutendeka. Kuna wale ambao yapasa kuamshwa waione hatari ya kula nyama, ambao wangali wakiila nyama ya wanyama na kwa njia hiyo kuihatarisha hali ya afya ya mwili, akili, na ya kiroho. Wengi ambao hivi sasa wameongoka nusu tu juu ya jambo hili la kula nyama watawaacha watu wa Mungu, wasifuatane nao tena. 14 KN 261.2

Wale ambao hudai kuliamjtii neno la kweli yawapasa kuzilinda kwa uangalifu nguvu za mwili na za akili, kusudi Mungu na kazi yake asidharauliwe kwa njia yoyote kwa maneno yao wala kwa matendo yao. Mazoea na desturi havina budi kuwekwa chini ya mapenzi yake Mungu. Yatupasa kuangalia sana chakula chetu. Nalionyeshwa dhahiri kuwa watu wa Mungu yawapasa kusimama imara kupingana na ulaji wa nyama. Je, Mungu kwa miaka arobaini angewapa watu wake ujumbe kwamba ikiwa wanataka kuwa na damu safi na akili timamu hawana budi kuacha kutumia nyama, hali ya kinyama hutiwa nguvu na hali ya kiroho hudhoofishwa. 15

Mafundisho Juu ya Kubadili Chakula

Ni kosa kudhani kwamba nguvu za musuli hutegemea juu ya kutumia chakula cha nyama. Mwili waweza kupatiwa mahitaji yake vizuri zaidi, na kuwa na afya bora bila kutumia nyama. Nafaka, pamoja na matunda, njugu, na mboga za majani, vina lishe yote ya chakula inayolazimu kuifanya damu iwe nzuri. Vitu hivyo havipatikani vizuri wala kamili kwa chakula cha nyama. Kama kutumia nyama kungekuwa jambo bora kwa afya na nguvu, nyama ingalikuwa miongoni mwa chakula alichoamriwa mwanadamu mwanzoni. KN 261.4

Nyama ikiachwa kutumiwa, mara nyingi mtu hujiona kuwa ana udhaifu, na asiye na nguvu. Wengi husisitiza neno hili kama jambo linalothibitisha kuwa nyama ni kitu bora; lakini ni kwa sababu vyakula vya watu hao ni vyenye kusisimua nguvu mwilini, kwa kuwa huitia damu homa na kusisimua neva, ndiyo maana wanatamani sana kuvipata. Wengine wataona shida kuacha kula nyama sawa na ilivyo kwa mlevi kuacha kiasi kidogo cha ulevi wake, lakini itawafaidia kubadili. KN 261.5

Chakula cha nyama kikikataliwa, yafaa badala yake pawepo nafaka, njugu, mboga za majani, na matunda; vitu ambavyo vitatia mwili afya na vyenye utamu. Hilo hulazimu hasa kwa wale ambao ni wadhaifu, au wenye kutumikishwa kazini daima. 16 KN 262.1

Hasa mahali ambapo nyama haifanywi chakula kikuu ni bora kupika vitu muhimu. Kitu fulani hakina budi kutayarishwa kuwa badala ya nyama, na vitu hivyo vilivyo badala ya nyama havina budi kutayarishwa vizuri, kusuai nyama isitamamke tena. 17 KN 262.2

Naiua jamaa ambao wamekiacha chakula cha nyama na kutumia chakula cha kimaskini. Chakula chao hupikwa ovyo sana hata tumbo hukichukia kabisa; watu kama hao wameniambia kuwa kutokula nyama si jambo wanalopatana nalo, kwamba wamekuwa wakipungukiwa na nguvu za mwili. Yafaa chakula kitayarishwe bila kukolezwa kwa viungo, lakini kiwe na ladha. 18 KN 262.3

Ni kwa faida yao wenyewe kwamba Mungu hulionya kanisa la masalio kuacha kutumia nyama, majani ya chai, na kahawa, na vyakula vingine vyenye madhara. Kuna vitu vingine vingi tuwezavyo kuponea ambavyo ni vya kufaa. KN 262.4

Miongoni mwa wale wenye kungojea kuja kwa Bwana, wataachilia mbali kula nyama hatimaye; nyama itakoma kuwa sehemu ya chakula chao. Yatupasa kukumbuka mwisho huo daima, na kujitahidi kufanya kazi kwa uaminifu kuukaribia. 19 KN 262.5

Nguvu za akilini, moyoni, na mwilini hupunguzwa na mazoea ya kutumia nyama. Kula nyama huharibu mwili, nuduwaza akili, na kupunguza nguvu za fahamu za moyoni. Twawaambieni, ndugu na dada wapendwa, njia ya salama kabisa kwenu ni kutotumia nyama. 20 

Sura ya 42 - Uaminifu Katika Kutunza Afya

ANGALIA: Ujumbe huu wenye kutaja mara nyingine mambo makuu katika matengenezo ya afya ulitolewa na Mama White kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu mnamo mwaka 1909. Mkutano wa mwisho wa aina hiyo aliopata kuhudhuria. KN 263.1

Nimeamuriwa kutoa ujumbe kwa watu wetu wote juu ya somo hili la matengenezo ya afya maana wengi wameasi na kuacna utii wao wa kwanza wa kanuni za matengenezo ya afya bora. KN 263.2

Kusudi la Mungu kwa watoto wake ni ya kuwa waweze kukua hata kuufikia utu uzima wa wanaume na wanawake kwa Kristo. Kusudi kulitimiza hilo, hawana budi kutumia vizuri kila uwezo wa akili, na mwili. Hasara wawezayo kuipata kwa kutupa ovyo nguvu za akili ama za mwili ni kubwa mno. KN 263.3

Swali juu ya jinsi ya kuitunza afya ni kubwa na la maana sana. Tunapolichunguza swali hili kwa kicho cha Mungu tutajifunza kuwa ni bora, kwa ajili ya maendeleo yetu ya mwili na ya roho pia, kushika kanuni za utovu wa chakula cha anasa. Basi, tulichunguze jambo hili kwa makini. Twahitaji maarifa na busara ili kuendelea kwa akili katika jambo hili. Sheria za asili si za kupingwa bali za kutiiwa. KN 263.4

Wale ambao wamepokea mafundisho juu ya ubaya wa kutumia nyama, majani ya chai, na kahawa, pamoja na vyakula visivyofaa kwa afya, wenye kukusudia kufanya agano na Mungu kwa kujinyima, hawataendelea kuiendekeza tamaa yao ya chakula wanachojua kwamba si bora kwa afya. Mungu anadai kuwa tamaa ya chakula iwe safi, na ya kuwa kutumiwa kwa kiasi kitumiwe kwa habari ya vitu hivyo ambavyo si vizuri kwa afya. Hiyo ndiyo kazi ambayo itakuwa haina budi kutendwa kabla watu wake kuweza kusimama wakiwa wakamilifu mbele zake. KN 263.5

Watu walio masalio wa Mungu hawana budi kuwa waongofu. Kuhubiri kwa ujumbe kumepasa kuleta uongofu na utakaso wa roho za watu. Yatupasa kuona moyoni uwezo wa roho ya Mungu katika kanisa hili. Huu ni ujumbe wa ajabu na wenye maana dhahiri; haupungui lo lote kwa mwenye kuupokea, nao hauna budi kuhubiriwa kwa sauti kuu. Yatupasa kuwa na imani ya kweli, idumuyo, ya kwamba ujumbe huu utatoka na kuzidi kuwa wenye maana mpaka mwisho. KN 263.6

Wako wengine wanaodai kuwa ni waumini, wenye kukubali sehemu fulani tu za Shuhuda (Testimonies) hizi kama ujumbe wa Mungu, huku wakikataa sehemu zile zenye kukataza anasa zao wazipendazo. Watu kama hao wanafanya kinyume cha usitawi wao wenyewe na usitawi wa kanisa pia. Yafaa tuenende katika nuru maadam tunayo nuru. Wale wanaodai kuwa wanayaamini matengenezo ya afya, lakini wanafanya kinyume cha kanuni zake katika matendo ya maisha ya kila siku, kwa roho zao wenyewe na huacha mivuto mibaya mawazoni mwa waumini na mawazoni mwa wale wasioamini pia.

Nguvu kwa Njia ya Utii

Wajibu mzito huwakalia wale wanaoijua kweli, hata matendo yao yote yatapatana na imani yao, na ya kuwa maisha yao yatasafishwa na kutakaswa nao huwa tayari kwa kazi ambayo haina budi kutendwa upesi katika siku hizi za mwisho za ujumbe huu. Hawana nafasi wala nguvu za kutumia kwa kujifurahisha kwa tamaa ya chakula. Yafaa maneno haya yatujie sasa na msukumo wa moyoni: “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana” (Matendo 3:19). Kuna wengi miongoni mwetu wenye upungufu katika mambo ya kiroho na ambao, kama wasipoongoka kabisa, yamkini watapotea. Je, mwaweza kufanya ujasiri! KN 264.1

Mungu ataka watu wake wawe na maendeleo ya daima. Tunahitaji kufahamu kuwa tamaa mbaya ya chakula ni kipingamizi kikubwa cha maendeleo bora ya akili na ya utakaso wa roho ya mtu. Kwa maungamo yetu yote ya matengenezo ya afya wengi wetu hula vibaya, isivyofaa. Kuiendekeza tamaa ya chakula ni sababu kubwa kabisa ya udhaifu wa mwilini na pia ni chanzo hasa cha udhaifu na kufa kabla ya uzee. Basi, mtu mwenye kujitahidi kuwa na usafi wa moyoni na akumbuke kuwa ndani ya Kristo kuna uwezo wa kuitawala tamaa ya chakula. KN 264.2

Kama tungaliweza kufaidiwa na kule kuendekeza uchu wa nyama, nisingaliwatolea ombi hili; lakini najua hatuwezi kunufaika. Vyakula vya nyama hudhuru hali njema ya mwilini, nasi twapaswa kutovishiriki. Wale walio mahali wawezapo kujipatia chakula kisicho cha nyama, lakini wanaochagua kuyafuata mapenzi yao wenyewe katika jambo hili, kula na kunywa kama wapendavyo, kidogo kidogo watazidi kuwa watu wasioyajali mafundisho ambayo Bwana aliyatoa juu ya mambo mengine ya kweli ya wakati huu nao watapotewa na akili zao za kuona ukweli; yumkini watavuna walivyopanda. KN 264.3

Nimeamriwa kwamba wanafunzi katika shule zetu wasipewe vyakula vya nyama wala vyakula visitayarishwe kwa njia zinazojulikana kuwa hazifai kwa alya. Si vizuri kitu cho chote ambacho kitaamsha kiu na vileo kuwekwa mezani. Nawasihi wazee na vijana na watu wazima. Jihinisheni vitu hivyo ambavyo huwadhuru. Mtumikieni Bwana kwa kujinyima. KN 264.4

Kuna wengi ambao huona kuwa hawawezi kuendelea vizuri bila vyakula vya nyama; lakini ikiwa hao wangejiweka upande wa Bwana, wakiwa wamekwisha kuazimia kabisa kuenenda kadka njia anayowaongoza, wangepokea nguvu na hekima kama Danieli na wenzake. Wangeona kuwa Bwana angewapa busara nzuri. KN 265.1

Wengi wangeshangazwa kuona kiasi ambacho kingaliweza kuwekwa akiba kwa ajili ya kazi ya Mungu kwa matendo ya kiasi. Idadi ndogo ya fedha mayopatikana kwa kujinyima itafanya makuu kwa kuijenga kazi ya Mungu kuliko ile vipaji vikubwa zaidi vinayofanya, ambavyo havikuhitaji kuwa na kiasi.

Mwito Kusimama Imara

Waadventista Wasabato hushughulika na maneno ya kweli yenye maana sana. Zamani zaidi ya miaka arobaini iliyopita (mwaka 1863), Bwana alitupa nuru ya pekee juu ya matengenezo ya afya, lakini tunaenenda jinsi gani katika nuru hiyo? Wangapi wamekataa kuyashika maonyo ya Mungu maishani mwao! Kama watu, yafaa tufanye maendeleo yanayolingana na nuru tuliyopokea. Ni wajibu wetu kufahamu na kuheshimu kanuni za matengenezo ya afya. Juu ya jambo hili la kuwa na kiasi yatupasa tuwashinde watu wote wengine; lakini hata hivyo wako miongoni mwetu washiriki wa kanisa waliofundishwa vizuri, hata wahubiri wa Injili, wasiojali ile kidogo tu, nuru ambayo Mungu ameitoa juu ya jambo hilo. Hula kama wapendavyo na kufanya kazi kama wapendavyo. KN 265.3

Hebu wale walio walimu na viongozi kazini mwetu wasimame imara kuitetea Biblia juu ya matengenezo ya afya na kutoa ushuhuda wa dhati kwa wale wenye kusadiki kwamba tunaishi katika siku za mwisho wa historia ya dunia hii. Mstari wa kutofautisha baina ya wale wanaomtumikia Mungu na wale wanaojitumikia wenyewe hauna budi kuchorwa. KN 265.4

Nimeonyeshwa kuwa mafundisho tuliyopewa mwanzoni mwa ujumbe huu yangali na maana nayo yanapasa kuheshimiwa sana siku hizi kama yalivyokuwa yakiheshimiwa zamani. Kuna wengine umbao kamwe hawajaifuata nuru iliyokwisha kutolewa juu ya jambo hili la chakula. Sasa ndio wakati wa kuitwaa taa kutoka chini ya pishi na kuiacha iangaze vizuri, na kutoa nuru. KN 265.5

Kanuni za afya zina maana sana kwa kila mmoja wetu na kwa sisi sote kwa jumla. Ujumbe wa matengeneo ya afya ulipoanza kunijia, nalikuwa dhaifu, mwenye kuzimia mara kwa mara. Nikamwomba Mungu msaada, naye akinifunulia jambo hili kuu la matengenezo ya afya. Akaniamuru kuwa wale wanaozishika amri zake hawana budi kutiwa kwenye umoja mtakatifu wake mwenyewe, na ya kwamba kwa kiasi katika kula na kunywa yawapasa kuitunza akili na mwili katika hali njema sana kwa kazi. Nuru hiyo imekuwa mbaraka mkubwa kwangu. Ninayo afya njema leo, ijapokuwa ninao umri mkubwa, kuliko niliokuwa nao siku za ujana wangu. KN 265.6

Imesemekana kwamba sikuzifuata kanuni za matengenezo ya afya kama nilivyoziandika kwa kalamu yangu; lakini naweza kusema kuwa nimekuwa kiongozi mwaminifu wa matengenezo ya afya . Wale ambao wamekuwa watu wa nyumbani mwangu wanajua kuwa hilo ni kweli. 

“Fanyeni Yote kwa Utukufu wa Mungu”

Hatuchori mstari halisi wa kufuatwa katika chakula; lakini twasema kuwa katika nchi zenye matunda, nafaka, na mbegu jamii ya njugu kwa wingi, nyama si chakula bora kwa watu wa Mungu. Nimeamriwa kuwa nyama yaelekea kufanya mwili uwe na tamaa mbaya za kinyama, kuwanyang’anya wanaume na wanawake ule upendo na huruma ambazo yawapasa kuwa nazo kwa kila mmoja wao, na kuacha tamaa mbaya za mwili kutawala uwezo bora wa mtu. Ikiwa kula nyama kulipata kuwa jambo la manufaa kwa afya, sasa si salama. Magonjwa ya donda baya ‘saratani,’ uvimbe, na magonjwa ya kifua hutokana zaidi na kula nyama. KN 266.2

Haitupasi kufanya ulaji wa nyama kipimo cha ushirika, lakini yafaa kufikiri mvuto wa wale wanaodai kuwa ni waumini ambao hutumia nyama, juu ya wengine. Je, kama wajumbe wa Mungu, hatutawaambia watu: “Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu?” (1 Wakorintho 10:31). Je, tusitoe ushuhuda thabiti kupinga tamaa ya chakula iliyopotoka? Je, mhubiri awaye yote wa Injili, mwenyewe kulihubiri neno la kweli zito lililopata kupewa wanadamu, ataonyesha kielelezo kwa kuvirudia vyungu vya nyama ya Misri? Je, wale ambao hulipwa kutoka katika nyumba ya Mungu watakubali kwa kujifurahisha kwa anasa kutia sumu mkondo wenye kutia uzima unaotiririka mishipani mwao? Afya ya mwili haina budi kuhesabiwa kuwa kitu cha maana kwa kukua katika neema na upataji wa moyo mtulivu. Kama tumbo lisipotunzwa vizuri, kufanywa kwa tabia nyofu na ya uadilifu kutazuiwa. Ubongo na neva hulihurumia tumbo. Kula na kunywa ambako kuna makosa huleta kufikiri na kutenda kwenye makosa. KN 266.3

Wote sasa wanapimwa kuthibitishwa. Tumebatizwa katika Kristo, na ikiwa tutafanya wajibu wetu kwa kujitenga na kila kitu kiwezacho kutuburura chini na kutufanya tuwe vile isivyotupasa kuwa, tutapewa nguvu kukua ndani ya Kristo, ambaye yu kichwa chetu chenye uhai, nasi tutaona wokovu wa Mungu. KN 266.4

Tukiwa tu wenye akili juu ya kanuni za maisha ya afya ndipo tuwezapo kuamshwa kabisa kuona mabaya yanayotokana na chakula kisichofaa. Wale ambao baada ya kuyaona makosa yao, wana moyo kuyabadili mazoea yao, wataona kuwa njia ya matengenezo huhitaji jitihada na uvumilivu mwingi; lakini tamaa nzuri za chakula zikiisna kufanywa, watatambua kuwa kutumia chakula ambacho kwanza kilihesabiwa kuwa kisicho na madhara kuliweka pole pole msingi wa ugonjwa wa kutokiweza chakula vizuri tumbom na magonjwa mengine. KN 267.1

Baba na mama, kesheni na kuomba. Jihadharini juu ya kutokuwa na kiasi kwa namna iwayo yote. Wafundisheni watoto wenu kanuni za matengenezo halisi ya afya. Ghadhabu ya Mungu imeanza tayari kuwapatiliza wana wa uasi. Uhalifu wa sheria kama nini, dhambi kama nini, maovu kama nini, hudhihirishwa kila upande? Kama watu yatupasa kutumia uangalifu mkubwa katika kuwalinda watoto wetu na marafiki wabaya. 

Fundisheni Watu

Yafaa jitihada kubwa zaidi kutolewa kuwafundisha watu kanuni za matengenezo ya afya bora. Shule za upishi zingeanzishwa, na mafundisho yangetolewa nyumba kwa nyumba juu ya upishi wa chakula kizuri kwa afya. Yawapasa wazee na vijana kujimnza jinsi ya kupika chakula chepesi zaidi. Po pote neno la kweli lifundishwapo, yapasa watu wafundishwe jinsi ya kutayarisha chakula kwa njia nyepesi, tena ya kukifanya kiwe na ladha. Yafaa waonyeshwe kuwa cnakula kitiacho afya chaweza kupatikana bila ya kutumia nyama. KN 267.3

Wafundisheni watu kuwa ni heri kujua jinsi ya kujitunza katika hali njema ya afya kuliko kujua jinsi ya kutibu ugonjwa. Yafaa madaktari wetu wawe walimu wenye busara, wanaowaonya wote juu ya kujifurahisha kwa anasa na kuonyesha kuwa kutokula vitu ambavyo Mungu amevikataza ndiyo njia tu ya kuulinda mwili na akili visipatwe na uharibifu. KN 267.4

Yafaa akili na busara nyingi zitumiwe katika kukitayarisha chakula kitiacho afya badala ya kile ambacho zamani kilifmywa kuwa chakula cha nao wenye kujifunza kuwa viongozi wa haya matengenezo ya afya. Imani kwa Mungu, kusudi la kweli, na hiari ya kusaidiana vinahitajika. Chakula kisicho na sehemu nzuri zenye kuulisha mwili huyaletea matengenezo ya afya fedheha. Sisi tu wenye kufa, nasi hatuna budi kujipatia chakula bora ambacho kitautia mwili afya. KN 267.5

Ushupavu Hudhuru Matengenezo ya Afya

Wengine miongoni mwa watu wetu, huku wakiwa wanaacha kabisa kula vyakula vibaya, hawajali kujipatia vitu vinavyolazimu kuihifadhi afya ya mwili. Wale wanaoshupaa katika kuyafikiri haya matengenezo ya afya wako katika hatari ya kutayarisha vyakula visivyo na ladha, na visivyo na utamu hata kuwafanya wasiridhike navyo. Chakula kingetayarishwa kwa njia ambayo itakuwa venye ladha na kutia afya pia. Yafaa kisinyang’anywe kitu kile ambacho mwili wakihitaji. Natumia chumvi, na siku zote nimefanya hivyo, kwa sababu chumvi si kitu chenye madhara, bali kwa tamu kwa maziwa kidogo au mafuta yanayoganda juu ya maziwa yaliyochemswa (cream), au kwa kutumia kitu kingine cha aina hiyo. KN 268.1

Huku maonyo yakiwa yametolewa juu ya hatari ya watoto wadogo kupatwa na ugonjwa kwa kutumia siagi, na mdhara ya kutumia mayai, lakini, haitupasi kuhesabu kuwa m uhalifu wa kanum za afya kuyatumia mayai yatokayo kwa kuku wanaotunzwa vizuri na kulishwa vizuri. Mayai yana nguvu ambazo ni zenye kuzuia sumu fulani. KN 268.2

Wengine wakiacha kutumia maziwa, mayai na siagi, hukosa kuupatia mwili chakula cha kufaa, na hatimaye hudhoofika na kushindwa kufanya kazi. Kwa njia hiyo matengenezo ya afya hupata sifa mbaya. Kazi tuliyojaribu kuijenga kwa uthabiti inatiwa mashakani na mambo mageni ambayo Mungu hakuyataka yawepo, na nguvu za kanisa zinapoozeshwa. Lakini, Mungu ataingilia kuyazuia matokeo ya baadaye ya mawazo hayo yenye nguvu mno. Injili yapasa kuwapatanisha wanadamu wenye dhambi. Yapasa kuwakusanya pamoja matajiri na maskini miguuni mwa Yesu. KN 268.3

Utakuja wakati ambapo yaweza kutubidi kuacha kutumia vyakula vingine tunavyotumia sasa, kama vile maziwa na mafuta yanayopatikana katika maziwa na mayai; lakini si lazima kujitwisha mashaka kwa kufanya hivyo mapema na kuzidi mno katika kutokutumia vitu vya aina hiyo sasa. Ngojeni mpaka hali ya mambo itakapolazimu kufanya hivyo na Bwana aitayarishie njia. KN 268.4

Wale ambao watafanikiwa katika kutangaza kanuni za matengenezo ya afya hawana budi kulifanya Neno la Mungu kiongozi na mshauri wao. Kadiri tu walimu wa hizi kanuni za matengenezo ya afya wanavyofanya hivi ndivyo wawezavyo kusimama mahali pafaapo kuyakinga mashambulio. Kamwe tusitoe ushuhuda ulio kinyume cha matengenezo ya afya kwa kutotumia chakula bora, kitamu, badala ya vyakula vyenye madhara ambavyo tumevikataa. Usitie nguvu kiu ya vileo kwa njia iwayo yote. Kula tu chakula kifaacho, chepesi, kisichokolezwa kwa viungo vikali vya chakula; tena mshukuru Mungu daima kwa ajili ya kanuni za matengenezo ya afya. Kwa mambo yote uwe mwaminifu na mnyofu, nawe utapata ushindi wa thamani.

Hali za Nchini Zipasazo Kufikiriwa

Huku tukipingana na ulafi na ulevi, hatuna budi kutambua hali inayowatawala wanadamu. Mungu amewajalia riziki wale wanaoshi katika nchi mbalimbali ulimwenguni. Wale wanaotamani kuwa watenda kazi pamoja na Mungu hawana budi kufikiri kwa uangalifu kabla ya kuainisna vyakula ambavyo wamepaswa kula na vile wasivyopaswa kula. Yatupasa kuhusiana na jamii. Matengenezo ya afya katika hali yake izidiyo kiasi yangefundishwa kwa wale ambao hali zao huwazuia kuyaiga, badala ya faida yangeleta madhara makubwa zaidi. Nikihubiri Injili kwa maskini, nimeamriwa kuwaambia kula chakula chenye kutia afya. Siwezi kuwaambia: “Msile mayai, wala mziwa, wala mafuta ya maziwa. Msitumie siagi kwa kupikia chakula.” Injili haina budi kuhubiriwa kwa maskini, lakini wakati haujafika bado kuamuru chakula halisi kabisa. KN 269.1

Ndipo Mungu Ataweza Kubariki

Wale wachungaji wanaojiona wako huru kuindekeza tamaa ya chakula wana upungufu mkubwa. Mungu anataka wawe viongozi wa matengenezo ya afya. Ataka waifuate maishani mwao, nuru lliyotolewa juu ya jambo hili. Nasikitika nikiona wale ambao yawapasa wawe wenye bidii kuzishika kanuni zetu za afya, hawajaongoka bado na kuifuata njia bora ya kuishi. Naomba ili Bwana apate kuwavuta mioyoni mwao kusudi waone hasara kubwa inayowakabili. Ikiwa mambo yangekuwa kama ipasavyo nyumbani mwa watu wa makanisa yetu, tungeweza kumfanyia Bwana kazi iliyo kubwa maradufu. KN 269.2

Kusudi kutakaswa na kudumu kuwa safi, Waadventista Wasabato hawana budi kuwa na Roho Mtakatifu mioyoni mwao na nyumbani mwao, Bwana amenionyesha kwamba Israeli wa leo wakijinyenyekeza mbele yake, na kulisafisha hekalu la rohoni, na kuondoa uchafu wote, atazisikia sala zao kwa ajili ya wagonjwa, na atayabariki matumizi ya dawa zake kwa magonjwa. Kwa imani mwanadamu akifanya yote awezayo kupigana na ugonjwa, akizitumia njia nyepesi za kutibu magonjwa ambazo Mungu ametoa, jitihada zake zitabarikiwa na Mungu. KN 269.3

Ikiwa baada ya nuru kubwa hivi kutolewa, watu wa Mungu watakuwa wakiyafurahia mazoea mabaya, wakijipendeza nafsi na kukataa kuongoka, watapatwa na madhara yanayotokana na uasi. Kama walikusudia kuiriahisha tamaa ya chakula lliyotoka kwa hali iwayo yote, Mungu hatawaokoa na madhara ya anasa zao kwa mwujiza. Watalala “kwa huzuni,” Isaya 50:11. KN 269.4

Wengi kama nini hupotewa na mibaraka mikubwa ambayo Mungu amewawekea akiba katika afya na mibaraka ya mambo ya kiroho! Wako watu wengi wenye kujitahidi kupata ushindi wa pekee na mibaraka maalum ili wafanye makuu. Mpaka sasa huona daima kuwa yawapasa kushindana, vikali katika maombi kwa machozi. Hao nao wakiyachunguza Maandiko kwa kuomba ili kujua wazi mapenzi ya Mungu, ndipo wayatimize mapenzi yake kwa moyo wote bila kujipendeza nafsi wenyewe, watapata raha. Maumivu yote, machozi na jitihada zote, havitawaletea mbaraka ambao wanatamani kuupata. Nafsini mtu hana budi kujitoa. Yawapasa kuifanya kazi mayojitokeza yenyewe na kujitwalia kwa wingi neema ya Mungu waliyoahidiwa wote waombao kwa imani. KN 269.5

Yesu alisema, “Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate” (Luka 9:23). Tumfuateni Mwokozi katika utovu wake wa anasa na kuwa na kiasi. Tumwinueni yule Mtu wa Kalwari kwa neno na kwa mwenendo mtakatifu. Mwokozi huwakaribia sana wale wanaojitoa wakfu kwa Mungu. Ikiwa palikuwapo wakati ambapo tulihitaji kazi ya Roho wa Mungu mioyoni na maishani mwetu, ni sasa. Basi na tushike sana uwezo huu mtakatifu ili tuwe na nguvu kuishi maisha matakatifu na ya kujitoa. 1