Seventh-day Adventist® Church

PASTOR LETTA'S OFFICIAL WEBSITE

Menu

MWONGOZO WA WANAWAKE

MWONGOZO WA WACHUNGJI NA WAZEE IDARA YA HUDUMA ZA WANAWAKE

MWONGOZO YAKINIFU KWA VIONGOZI WA KANISA MAHALIA.

UTANGULIZI:

SEHEMU YA KWANZA:
FALSAFA NA UTUME WA HUDUMA ZA WANAWAKE

 • Falsafa.
 • Njozi ya Idara.
 • Kaulimbiu iliyokusudiwa.
 • Dondoo za dada Ellen White kuhusu wanawake.
 • Historia fupi ya huduma za Wanawake.
 • Tamko la Kanuni za Kanisa.
 • Huduma za Wanawake leo.
 • Changamoto sita zinazo wakabili wanawake.
 • Logo ya Huduma za Wanawake.
 • Rangi za Huduma za Wanawake.

SEHEMU YA PILI:  MUUNDO WA IDARA

 • Kiongozi wa idara ya Huduma za Wanawake katika kanisa mahalia.
 • Sifa za kiongozi wa idara ya Huduma za Wanawake.
 • Malengo na makusudi.
 • Majukumu ya kazi.
 • Kufanya kazi na Idara zingine.

SEHEMU YA TATU:  NAMANA YA KUANZISHA HUDUMA ZA WANAWAKE KATIKA

KANISA  MAHALIA.

 • Mwombe Mungu akuongoze.
 • Fanya kazi na wenzako.
 • Lenga huduma zako.
 • Tanguliza vipaumbele.
 • Tanguliza vitendea kazi.
 • Chunguza kwanza.
 • Chunguza huduma za wanawake katika mtandao.
 • Chunguza ujuzi wa Huduma za Wanawake.
 • Fanya kazi na Mchungaji wako.
 • Tambua karama za roho.
 • Weka magoli yanayofikika.
 • Weka katika program zako.
 • Weka bajeti kwa ajili y huduma za wanawake.
 • Fomu ya bajet
 • Tangaza program zako.
 • Kupanga mikutano ya huduma za wanawake.

SEHEMU YA NNE:  UONGOZI.

 • Namna ya kuwapata na kuwalea wanojitolea kujiunga na huduma za wana wa kike.
 • Hatua za kuchukua.
 • Fanya kazi kama timu moja.
 • Mafunzo ya kufanya kazi kama timu.
 • Mambo sita ya kufanya katika kufanya kazi kwa pamoja.
 • Kuweka program za kujenga akili.
 • Mwalimu/mwezeshaji ni nani?
 • Kutengeneza program ya kikanisa kwa ajili ya kukuza akili.

SEHEMU YA TANO:  PROGRAM.

 • Program za huduma za wanawake.
 • Program za kufadhili  za  huduma za wanawake.
 • Program za huduma za wanawake katika kanisa mahalia.
 • Program za huduma kwa jamii za hudumu za wanawake.
 • Huduma za kusaidia.
 • Huduma za vikundi vidogo vidogo.
 • Program za kuunda urafiki.
 • Mawazo ya huduma.

SEHEMU YA SITA:  SIKU MAALUM KWA AJILI YA HUDUMA ZA WANAWAKE.

 • Kalenda ya siku maalumu.
 • Siku ya kimataifa ya wanawake ya maombi.
 • Siku ya kuwekea mkazo Idara.
 • Siku yakuzuia unyanyasaji.

SEHEMU YA SABA:
UINJILISTI/UTUME.

 • Mapendekezo ya uinjilisti.
 • Mradi wa  B = U:  Biblia sawa sawa na ubatizo.

UTANGULIZI:

Agano jipya hufundisha kwa ufasaha wa huduma za kichungaji kwa waumini wote na kila mtu katika familia kuthaminiwa na kuitwa kushiriki katika kuhubiri habari njema. Kilichowaunganisha Wakristo wa awali ilikuwa ni kujitoa kwao kwa ufalme wa Kristo na uwezo wa Roho Mtakatifu kukamilisha utume wa Mungu. Miongoni mwa wafuasi wa Kristo walikuwa wanawake kama Yule Mwanamke Msamaria katika kisima cha Yakobo ambaye alitumika kama mwinjilisti wa vitabu wa kwanza kabisa; Wanawake waliotawazwa walionyesha ukarimu kwa Yesu.  Mariam alikuwa wa kwanza kuhubiri kufufuka kwa Yesu.  Hata kwa wale wanafunzi wa Yesu kumi na moja wasio na imani waliobaki.

Vivyo hivyo, kanisa la awali liliimarika kadri wanawake wa imani walivyo unganisha juhudi binafsi za kufundisha, uongozi, unabii, maombi na kujenga na kuimarisha kusudi la Mungu. Utagundua yakuwa Muongozo huu ulio rahisi kuusoma na kuutekeleza hutoa mwongozo kwa wachungaji, wazee, na viongozi wengine wa kanisa ili kuweka mtazamo wa kiroho katika mikutano kutia moyo huduma za wanawake kama sehemu ya mipango ya kanisa kuwaandaa watu kwa ajili ya ujio waYESU mara ya pili. Huduma ya kichungaji ya Konferensi kuu inafurahi kuunganisha nguvu na uwezo na Idara ya Huduma za Wanawake Konferensi kuu katika kuwatia moyo viongozi wote kila mahali kutumia fursa zote na muumini yeyote aliyetayari kutumika kuhamasisha kuja kwa Yesu mara ya pili. 

James A. Cress     Tleather – Dawn Small

KIONGOZI WA HUDUMA ZA KICHUNGAJI                                            KIONGOZI                                                                                                                                                                                                  SEHEMU YA KWANZA:  FALSAFA NA UTUME WA HUDUMA ZA WANAWAKE.

FALSAFA YA IDARA

Idara ya Huduma  wanawake iko kwa ajili ya kuwatia moyo, kuwapa changamoto, kuwawezesha na kuwakuza wanawake wakiadventista wanapofanya sehemu yao katika kupeleka ujumbe wa wokovu ulimwenguni. Bwana ana kazi kwa ajili ya wanawake kama ilivyo kwa wanaume.  Waweza kuchukua nafasi zao katika kazi katika wakati huu na atafanya kazi kupitia kwao.   Katika familia wanaweza wakafanya kazi ambayo wanaume hawawezi kuifanya kazi inayofikia maisha ya ndani ya mtu. Wanaweza kuifikia mioyo ambayo wanaume wanaweza kushindwa kuifiki.Juhudi zao zinahitajika”. – Welfare Minisry P. 145.

UTUME WA IDARA.

Utume wa Huduma za Wanawake ni kumfahamu Yesu kwa karibu na kumtumikia Mungu, pia kuwafanya wanawake wengine kuwa wanafunzi.

NJOZI YA IDARA.

Kusudi la msingi la Idara ya huduma za wanawake ni kulea, kuhimiza na kuwasaidia wanawake katika maisha yao ya ukristo kama wanafunzi wa Yesu Kristo na washirikiri wa kanisa la ulimwengu kwa kushauriana na uongozi wa idara zingine za kanisa idara ili hushiriki katika mikakati ya uinjilisti wa kiulimwengu na kutoa mafunzo kuwawezesha wanawake katika kanisa kumuinua Kristo kanisani na ulimwenguni pia. Tunaweza kumfanyia Mungu kazi nzuri endapo tutakuwa tayari.  Mwanamke hajui uwezo wake …. Kuna kusudio la juu sana kwa wanawake lenye kifiko, kizuri.  Anaweza kukuza na kujenga nguvu zake, kwa kuwa Mungu anaweza kuwatumia katika kazi kubwa y kuokoa roho kutoka katika uangamivu wa milele”  - Tesmonies for the church, vol. 4, p. 642.

CHANGAMOTO ZINASHUGHULIKIWA NA IDARA YA HUDUMA ZA WANAWAKE

Idara ya Huduma za wanawake imelenga katika kushughulika na changamoto sita – zilizobainishwa na kiongozi wa huduma za wanawake wa Divisheni na kupitishwa na kikao rasmi cha Huduma za Wanawake kama vikwazo vinanvyowazuia wanawake kutofikia viwango vyao vya juu kabisa vya utendaji kazi.

 1. Ujinga
 2. Umaskini
 3. Hatari za kiafya
 4. Mzigo wa kazi.
 5. Unyanyasaji.
 6. Kujiamini katika uongozi.

TAMKO LA UTUME

Idara ta Huduma za Wanawake ipo kuwatia moyo na kuwapa changamoto ya utendaji kazi wao kama wanawake wa kiadventista walio katika safari yao kama wanafunzi wa Yesu na washiriki wa kanisa la ulimwengu. Utume wetu upo katika mtazamo mpana unaofanya  wakristo wote  kumuinua Kristo ndani ya kanisa na duniani.  Lakini zaidi sana tumeitwa ili:

(a)   Kuwatia moyo wanawake kutambua thamani yao kwamba wameumbwa pia wamekombolewa kwa damu ya Yesu.

(b)  Kuwawezesha wanawake kuwa na imani thabiti na kushiriki ukuaji wa kiroho na kufanywa upya.

(c)  Kujenga ushirikiano kati ya wanawake ndani ya kanisa la ulimwengu waungane na kuwa marafiki ili kusaidiana na kuwa wabunifu katika kubadilishana mawazo.

(d)  Kuwatia akili wanawake vijana wa kiadventista, katika kushiriki  katika  shughuli za idara na kuandaa njia wanapotamani kufikia viwango vya juu katika Kristo.

(e)  Kushughulikia mahitaji ya kiulimwengu ya wanawake.

(f)   Kutumia mtazamo wenye upekee wa wanawake katika matatizo yanayokabili kanisa la ulimwengu.

(g)  Kutafuta kupanua huduma za kikristo za wanawake.

(h)  Kumpa changamoto kila mwanamke muandventist kutumia uwezo wake akuunganisha na talanta ya wanawake wengine pamoja na wanaume wanapofanya kazi bega kwa geba katika utume wa kiulimwengu wa kanisa la waadventista Wa-Sabato.  Ili uzoefu tuliopata katika Kristo tuweze kupewa uwezo wa kuutumia katika familia zetu miongoni mwa waumini wenzetu na katika ulimwengu unaohitaji wokovu.

DONDO ZA DADA ELLEN WHITE KUHUSU WANAWAKE.

"Wakati kazi kubwa inayohitaji maamuzi inatarajia kufanywa Mungu huchagua wanaume na wanawake kuifanya hiyo kazi na itakuwa na hasara endapo talanta za wote hazita changanywa." (Evangelism, uk.  469.) 
“Tunaweza kufanya kazi njema ya Mungu kama tumeamua.  Mwanamke hajui nguvu yake kwa ajili ya Mungu …. Kuna kusudi kubwa kwa ajili ya mwanamke kufikiri.  Anapaswa kukuza nakujenga nguvu zake kwa kuwa Mungu anaweza kuzitumia katika kazi kubwa ya kuongoa roho kutoka katika uangamivu wa milele." (T
estimonies to the church vol4 uk. 642, Evangelism uk. 465.)

"Hapajawa na muda ambapo watendakazi walihitajika kama sasa kuna ndugu ambao wangeweza kujinyenyekeza kueneza ukweli.  Ni jukumu la wote kujifunza mambo mbalimbali ya imani yetu."  (Review and Herald, April, 1880.)

“Wote wanaomfanyia Mungu kazi wanapaswa kuwa na roho ya Martha na Miariamu zikifanya kazi pamoja na utume wa hiari na upendo wa kweli.  Ubinafsi unapaswa kuwekwa kando.  Mungu anawaita watendakazi wa kike waaminifu, watendakazi walio na moyo wenye furaha, upole na kanuni za ukweli zikitawala ndani yao.  Anawaitwa wanwake wavumilivu ambao watatumia akili zao na sio ubinafsi … naye atawaweka wajikite kwa Kristo.  Atawasaidia kuongea kweli yote na kuwafanya wafanye kazi ya kuongoa roho." (Testimony  Treasures, vol. 2 uk. 405.)

"Wanawake wanaweza kuwa vitendea kazi vya utakatifu wakitoa huduma takatifu.  Ni Mariam aliyekuwa wakwanza kuhubiri kufufuka kwa Yesu kama kungekuwa na wanawake ishirini sehemu ambapo kuna mwanamke mmoja ni nani ambaye angelifanya huduma hii ya mtu mmoja mmoja na kufurahia kazi yake, tunapaswa kuona wengi wakiongolewa kujiunga na kweli.  Ushawishi laini wa mwanamke mkristo unahitajika katika kazi kubwa ya kuhubiri injili." (Evangelism uk. 471.)

"Bwana ana kazi kwa ajili ya wanawake kama ilivyo kwa wanaume.  Watakamilisha kazi nzuri kwa ajili ya Mungu kama kwanza watajifunza katika shule ya Kristo iliyo njema. Masomo muhimu ya upole na unyenyekevu. Hawapaswi tu kuwa na jina la Yesu bali pia kumpokea Roho Mtakatifu. Ni lazima watembee kama Yesu mwenyewe wakitakasa nia zao zisichafuliwe na chochote. Watawawezesha wengine kwa kumwakilisha Yesu kwao."

HISTORIA FUPI YA HUDUMA ZA WANAWAKE

Kazi katika miaka ya 1,800. 

Wakati ni kweli kuwa huduma za wanawake hazi kuwa idara inayojitegemea mpaka mwaka 1995, kanisa la Waadventista Wasabato limeenelea kutambua umuhimu wa kutoa huduma kwa wanawake kuanzia miaka ya 1800.  Huduma za wanawake zilianza mwaka 1898 wakati dada Sarepta Myrenda Irish Henry wakisaidiana na Ellen G. White waliainisha “Huduma za wanawake” Alipewa kibali cha huduma na Conferensi kuu na akawa mwanamke wa kwanza kuwa Kiongozi wa Idara ya Huduma za Wanawake  wa Konferensi kuu.

KAZI KATIKA MIAKA YA 1,900

Shughuli za huduma za wanawake hazikuwekwa katika maandishi kutoka mwaka 1900 – 197. Miaka hii iliitwa mika ya ukimya. “Angizo la kwanza kujifunza kazi za mwanamke kanisani uliandaliwa Septemba 1973 na kufikiwa muafaka katika kambi la Moharen huko Ohio. Katika mwaka wa 1990, wanawake 35 wakiwa wamewakilisha makundi mengine walikutana huko Pennsylvania kuliuliza kanisa kumchagua kiongozi wa kudumu wa Huduma za wanawake katika ngazi zote.  Viongozi hawa watapanga mikakati itakayofikia mahitaji ya wanawake; Pia wataainisha kazi za mwanamke ndani ya kanisa. Watafadhili mikutano itakayoleta uamsho kiroho ndani ya kanisa, na kuwaelimisha wanawake kuhusiana na kanuni za kanisa na miongozo ya kanisa katika ngazi ya Konferensi kuu huyu aweza kuwa katibu.  Katika ngazi zingine zote cheo hiki kinapaswa kitengewe fedha kwa ajili ya kusafiri na bajeti ya kutoa machapisho, kufafsiri, kuandaaa vitendea kazi na mikutano mbalimbali.

DHARURA YA IDARA.

Katika mwezi Julai mwaka 1995, mkutano mkuu wa kanisa ulipitisha kikamilifu uwepo wa Idara ya Huduma za Wanawake.  Rose Otis alichaguliwa kuwa kiongozi wa Huduma za Wanawake wa Konferensi kuu. Leo Huduma za Wanawake zimekua sehemu ya Huduma ulimwenguni na kila Divisheni ina kiongozi ambaye huona mbali maisha ya kiroho ya wanawake kuwafundisha na kuwakuza kiakili wanawake.

KAULI YA KANUNI ZA KANISA.

Huduma za wanawake huendeleza, huimiza, na kuwapa changamoto wanawake katika kutembea kwao kila siku kama wanafunzi wa Yesu Kristo na washiriki wa kanisa lake.

MALENGO YAKE NI:-

 1. Kuhamasisha ukuaji wa kiroho na uamsho.
 2. Kusisitiza kuwa wanawake wanathamani isiyopimika kwa sababu ya kuumbwa na kukombolewa kwao.
 3. Kuwaandaa kwa ajili ya kutuma na kueleza mitazamo ya wanawake katika masuala ya kanisa;
 4. Kuhudumia upeo wote wa mahitaji ya wanawake kwa kuzingatia mitazamo ya utamaduni wa makabila  mbalimbali.
 5. Kushirikiana na Idara zingine kurahisisha huduma za wanawake na kwa wanawake kujenga mapenzi mema miongoni mwa wanawake.
 6. Kuwashauri na kuwatia moyo wanawake na kutengeneza njia kwa ajili ya ushiriki wao katika kanisa;
 7. Kutafuta njia na namna ya kumpa changamoto kila mwanamke kutumia karama zake kuendeleza utume ulimwenguni.

KIONGOZI WA HUDUMA ZA WANAWAKE.

Kiongozi wa huduma za wanawake aliyechaguliwa kuanzisha hudumia maalum kulea wanawake na kuaandaaa kwa ajili ya huduma.  Yeye ni mwenyekiti wa kamati ya Huduma za Wanawake na kuhamisisha mawazo na mipango inayokuza mchango wa wanawake katika kazi ya kanisa. Kiongozi huyo hulisaidia baraza la kanisa kwa kujumuisha shughuli na program za wanawake katika program kuu ya kanisa.  |Hulipataia kanisa taarifa ya mchango wa huduma za wanawake katika uhai wa kanisa.  Mtu wa kuwasiliana na kiongozi huyo kuhusu mafunzo na vitendea kazi ni Mkurugenzi wa huduma za wanawake wa Konferensi.

 SIFA ZA KIONGOZI WA HUDUMA ZA WANAWAKE.

Kiongozi wa huduma za wanawake hana budi awe mwanamke makini anayefali ambaye anawiwa na huduma ya wanawake na matatizo yao, mwenye ulingano katika mitazamo yake, mwenye uwezo wa kuwatia moyo wanawake wengine kukuza karama zao za kiroho na mwenye uwezo wa kuhudumia vizuri wanawake, akishirikiana na mchungaji na baraza la kanisa.

KAMATI YA HUDUMA ZA WANAWAKE.

Kamati ya huduma za wanawake huhamasisha huduma kwa wanawake katika kanisa.  Kamati hii haina budi kuundwa na watu wanaopenda kuhudumia upeo wote wa mahitaji na huduma za wanawake na wenye talanta na uzoefu mbalimbali.

MAJUKUMU MBALIMBALI YA KAMATI YA HUDUMA ZA WANAWAKE.

 1. Kutambua mahitaji mbalimbali ya wanawake waliokoa kanisani na katika jamii kwa kushauriana na wachungaji na wazee wa kanisa.
 2. Kupanga mikakati na kushirikiana na idara zingine kuandaa program zitakazotoa huduma kwa wanaweke.
 3. Kupanga na kutekeleza mipango mbalimbali inayohusu huduma za wanawake na mahitaji mengine kwa kushirikiana na wachungaji na wataalamu mbalimbali na viongozi wa kanisa.
 4. Kuhamasisha kanisa mahalia kushiriki katika mipango mbalimbali ya mwaka na shughuli zilizo andaliwa na Konferensi, au divisheni au Konferensi kuu kwa mfano; siku ya maombo ya wanawake ulimwenguni, na huduma za vikundi vidogovidogo kusaidia na kuwatia moyo katika utumishi ili kufahamu zaidi wasiliana na kiongozi wako wa Konferens, Union, Divisheni au Konferensi kuu ya Huduma za wanawake.  Kiongozi wa Huduma za wanawake pia ni mjumbe wa Baraza la kanisa (Kanuni uk 111) Huduma binafsi (Kanuni uk. 10-) pia huchaguliwa na kibaraza cha uchaguzi.  (Kanuni uk 120)

HUDUMA ZA WANAWAKE LEO.
Huduma za wanawake leo ni ….

 • Ni fursa ya kufanya uanafunzi, kukuza na kulea wnawake.
 • Ni sehemu ya kushughulika na mahitaji ya wanawake kiroho, kihisia, kimwili na kijamii ndani ya kanisa.
 • Ni sehemu ambapo wanawake hutiwa moyo kukuza uwezo wao katika kushiriki katika utume wa kanisa
 • Ni tegemeo la wanawake walioachika, kunyanyaswa au wapweke.
 • Nisehemu ya kuelezea mambo mbalimbali yanayowaathiri wanawake.
 • Ni kimbilio kwa wanawake vijana kunapokuwa na program za kuwatia moyo wnawake vijana kujiendeleza.
 • Ni sehemu ambayowanawake hutiwa moyo kushiriki katika huduma katika makanisa yao, jamii pamoja na nyumbani kwao.
 • Ni sehemu ambapo wanawake vijana hukuzwa kiakili ili wapate furaha katika Bwana.
 • Ni sehemu ambapo wanawake huwezeshwa na kupewa mafunzo kuwa viongo wa kiroho.

Huduma za wwanawake huhitaji ushiriki katika program zote. Huduma za wzimegundua kuwa wanawake wana karama hivyo huwawezesha wanake kutumia karama za roho katika huduma kanisani.

Huduma za wanawake si ….

Huduma za wanawake sio kitu kigeni, idara ya kwanz ya huduma za wanawake katika kanisa la Waadventista Wasabato ilianza 1898 chini ya uongozi wa Sarepta M. I. Henry, kwa kutiwa moyo na Dada Ellen White.  Kwa bahati mbaya huyu Dada Sarepta alifariki na idara ikafa naye.  Baada ya miaka 100 mnamo mwaka 1990 kanisa la Waadventista wa sabato likafungua ofisi ya Huduma za Wanawake ambayo ikawa idara kamili mnamo mwaka 1995.

Huduma za wanawake…

 • Sehemu ya wanawake kuleta malalamiko yao dhihi ya waajiri wao, ziwe sahihi au sivyo.
 • Sio mahali pa kufafuta usawa wa wanawake dhidi ya wanume.
 • Sio jukwaa la wanawake kudai kuwekewa mikono japo tunaamini kila mtu anafursa ya kuifanya kazi ya Mungu kwa ajili ya utukufu wa Bwana
 • Sio sehemu ya kuwajadili wanaume  na kuwatenga.  Huduma za wanawake hupambana na kwa ajili ya kuwa sehemu ya Huduma na sio kuwatenga wengine.

CHANGAMOTO SITA ZINAZOWAKABILI WANAWAKE NA HUDUMA ZAO.

 1. Ujinga.
 2. Umaskini.
 3. Matatizo ya kiafya.
 4. Mgizo wa kazi.
 5. \unyanyaswaji.
 6. Kujiamini katika uongozi.

UJINGA:

Mojawapo ya changamoto kubwa pia ni hitaji la wanawake ulimwenguni ni hitaji la kujifunza kusoma na kundika. UNESCO, 2001 wanasema katika sunia ya leo kuna zaidi ya watu wazima bilioni moja wasiojua kusoma na kuandika. Hii ni asilimia 26 ya watu wote duniani.  Wnawake ni 2/3 ya wote wasiojua kusoma na kuandika.Kati ya wanawake watatu ulimwenguni mmoja hajui kusoma na kuandika katika ulimwengu mzima. Hawawezi kusoma maelekezo kujaza fomu za ajira au kusoma barua. Zaidi ya hayo mwanamke asiyejua kusoma na kuandika hawezi kusoma Biblia hili huzuia ukuaji wa kiroho na hata kuwafunsha watoto wao. Mwanamke akifjifunza kusoma, familia yake yote inanafasi kubwa ya kuwa wasomi.Akishajua kusoma anaweza kuanzishiwa masomo ya malezi yenye Afya ya kikkristo. “Ukimuelimisha mwanaume umemwelemisha mtu mmoja; lakini ukimwelimisha mwanamke umeielimisha jamii nzima."

UMASKINI:

Zaidi ya watu bilioni moja ulimwengni leo – zaidi sana wanawake huishi maisha ya kimaskini zaidi sana katika nchi inayoendelea.  Katika karne iliyopita, idadi ya wanaweake wanaoishi katika mazingira ya kimaskini imeongezeka.  Tatizo hili limehusishwa na kukosekana kwa fursa mbalimbali za kiuchumi pamoja na kukosa nafasi ya kupata elimu na mchango wao mdogo katika kushirikishwa kufanya maamuzi.

MATATIZO YA KIAFYA:

Afya iliyo dhoofu huondoa uwezo wa mwanamke kuwa sehemu ya ushiriki katika kazi ya Mungu.  Afya ya mwanamke huzorota ulimwenguni kote. Afya ya mwanamke huhusisha Afya ya kihisia, kijamii na kimwili.  Afya ya mwanamke huathiriwa moja kwa moja kijamii, kisiasa na kiuchumi.  Ubora wa afya ya mwanamke huhusishwa na maisha yake, familia yake na jamii kwa ujumla. Pia na hayo bado wanawake wengi ni wahanga wa afya dhaifu.

MZIGO WA KAZI:

Wanawake ulimwenguni ktote na katika tamaduni mbalimbali hupatachangamoto ya kuwa na mzigo wa kazi. Katika nchi nyingi, wanawake hufanya kazi masaa mengi kuliko wanaume.  Machapisho yanaonyesha kuwa katika nchi zinazoendelea wanawake katika mazingira ya kijijini hutumia zaid ya masaa mawili kwa siku wakibeba maji y a kupikia, kunywa, usafi pamoja na kuogea; katika mazingira mengine ya kijijini wanawatumia siku 200 kila mwaka, kuokota au kusenya kuni. Katika ulimengu unaoendelea wanawake hutegemewa kuwa na majumkumu mazito katika kuijenga famila ili iwe na maaadili mema.  Kuweka sawa mategemeo ya jamii kwa ajili ya familia yenye afya huishia katika kuwa na siku ndefu muda mfupi wa kupumzika na muda kidogo sana wa kujifunza biblia na hata kufanya maombi binafsi.

UNYANYASWAJI:

Unyanyaswaji ni tatizo la kiafya ulimwenguni.  Unyanyaswaji huwa zaidi ya watu million 1.6 kila mwaka.  Watalam wa Afya ya jamii husema kuwa hii taarifa ni kwa ochache sana.  Wanasema kuwa vitendo vingi vya unyanyaswaji huteneka nyuma ya milango iliyofungwa na hairipotiwi. Shirika la Afya duniani linatoa taarifa ya kuwa miongoni mwa wanawake 3, mmoja kati yao anapitia uzoefu mgumu wa unyanyasaji.  Bila kujali mwathiriwa ni nani, unyanyasaji katika familia ni tatizo kubwa na ni lazina lisemwe wazi na mashirika ya kidini Dundianikote.  Hakuna jamii iliyokingwa na unyanyaswaji pamoja na machafuko.   Kama kanisa ni imani yetu kuwa kuvumilia unyanyaswaji ndani ya kanisa ni kumpinga Kristo.

KUJIAMINI KATIKA UONGOZI:

Fursa ya wanawake kwa ajili ya oungozi na kujiendeleza zimewekwa chache sana karibia kila nchi Duniani. Wanawake wamefanya kazi majumbani kwa kuwasaidia waume zao, au kwa malipo. Wameshirikishwa kanisani japo kwa kiwango kikubwa kama msaidizi. Katika Historia wameshika nafasi chache sana za uongozi katika kanisa la Waadventista Wasabato.  Kwa sasa kuna uhitaji mkubwa wa wanawake kushirikishwa katika uongozi.  Hili linahitaji wanawake waaandaliwe kwa ajili ya majukumu hayo.  Kwa bahati mbaya wanawake wengi hawa hupata nafasi ya mafunzo ya uongozi na kuwa viongozi.  Katika huduma za wanawake tunathaminin kila mwanamke na kutambua mahitaji yake binafsi na karama zake.  Kama haitoshi kiongozi lazima shirikishwe katika elimu endelevun pamoja na mfunzo.

Lazima awe na taarifa za hivi karibuni za uongozi mpya na kuangalia namna nyingine ya kuwahudumia wengine.  Idara ya Huduma za wanawake umeandaa miongozo kwa ajili ya kuwaelimisha wanawake katika uongozi. Mpango wa uongozi upo katika ngazi nne na ina semina 63 zilizopo katika vipeperushi na kupitia komputa (power point prerentations). Ni muhimu kuwa wanawake washirkishwe katika kukuza kiakili na kujikuza yeye mwenyewe.  Hii huhakiki kuwa kila mmoja sio kwamba anatoa elimu tu bali pia anapokea.


NEMBO YA HUDUMA ZA WANAWAKE.

Idara ya Huduma za wanawake katika konferensi yetu kuu iliandaa Nembo mara tu baada ya idara kuzaliwa; ikionyesha wanawake 4.  Wanawake hawa wanne huwakilisha sio tu ushiriki wao katika Idara ya Huduma za wanawake bali pia malengo ya Huduma za wanawake.

 • Hushirikisha wanawake wa umri wote
 • Hushirikisha wanawake wenye tamaduni mbalimbali
 • Hushirikisha wanawake wanaofanya kazi pamoja
 • Hushirikisha wanawake walio na kitabu.  Kitabu hicho chaweza kuwa Biblia ambacho huwakilisha ukuaji wa kiroho. Chaweza pia kuwa kitabu cha taaluma, au chaweza pia kuwa kitabu cha sehemu nyingineyo yoyote waipendayo wanawake.  Inawezekana kabisa wanawake hawa wanajifunza wenyewe au wanawafundisha wengine. Huenda wanajifunza uongozi au kuwalea kiakili wanawake wengine. Haijalishi ni nini wanawake wanakuwa na wanajifunza pamoja.

Wanawake wanasaidiana na kuleana wao kwa wao kwa pamoja huwakikisha sehemu muhimu katika kanisa na kwa pamoja wanaweza kuleta tofauti. Wanaweza kutumia nembo hii au ukatafuta nyingine kulingana na mazingira yako au waweza tumia zote mbili kwa pamoja.  Katika ulimwengu wote hii ndiyo nembo inayotumika.

RANGI ZA HUDUMA ZA WANAWAKE

Rangi mbili zimechaguliwa kama rangi rasmi kwa ajili ya huduma za wanawake.  Hizi zinaweza kutumika kwa ajili ya nembo au kwa ajili ya kazi yoyote ya sanaa. Hudhibitiwa kutumia rangi hizi.  Rangi hizi ni:-

 1. Bluu bahari
 2. Zambarau mpauko.


SEHEMU YA PILI.

MUUNDO WA IDARA YA HUDUMA

KIONGOZI WA HUDUMA ZA WANAWAKE KATIKA KANISA MAHALIA:

- Huyu huchaguliwa na kibaraza cha uchaguzi ili kuwalea wanawake na kuwaimarisha kwa ajili ya utumishi, vilevile kujenga maisha yao ya kiroho kama Yesu alivyofanya kwa wanafunzi wake na washiriki wa kanisa la ulimwengu.

- Kiongozi wa Huduma za wanawake ni mjumbe wa baraza la kanisaakishirikisha shughuli za wanawake na program za kanisa.

- Yeye pia ni mwenyekiti wa vikao vyote vya Huduma za wanawake,akiwatia moyo wanawake kufikia malengo yao na kuweka mikakati ya kufanya kazi ya kansia.

SIFA ZA KIONGOZI WA HUDUMA ZA WANAWAKE

 • Awe mcha Mungu.
 • Awe tayari kutoa muda wake kufanya kazi ya Mungu.
 • Awe mtu apendaye maombi, neno la Mungu na kushuhudia.
 • Awe mvumilifu, mpole, msikivu wa kusikiliza na kusaidia wenye shida.
 • Mwenye kuheshimu na kuwajali watu.
 • Mwenye moyo wa kazi na aliyetayari kushirikiana na wengine.
 • Awe mtu mwepesi wa kuhisi, anayejali, mwenyemzigo wa huduma na matatozo ya wanawake. 
 • Awe ni mtu anayeweza kufanya kazi vizuri na wanawake kanisani, mchungaji na baraza la kanisa.

Kiongozi wa huduma za wanawake hufany kazi pamoja na mchungaji na baraza la kanisa na kamati ya huduma za wanawake kanisani. Kamati hii inapaswa kuwa na watu wanaopendelea kwa upeo mpana mahitaji na huduma za wanawake ili kuunda timu yenye uwiano, wajumbe wawe watu wenye talanta na uzoefu mbalimbali. (Kanuni za kanisa  toleo la 2005).

MALENGO NA MAKUSUDI.

 1. Kiongozi alisaidie kanisa kufikia mahitaji ya wanawake ya kiroho, kihisia na kitaaluma katika Nyanja mbalimbali za maisha pamoja na utofauti katika tamaduni zao.
 2. Kiongozi atengeneze mazingira yatkayokuza uwezo wa kufanya kazi na kutambua juhudi, pia kutoa fursa za kiroho ambazo wanawake wanaweza kukuza.
 3. Kiongozi kupitia tafiti mbalimbali atambue mahitaji ya wanawake kasha aaandae parogramu zitakazo wasaidia kufikia mahitaji  yaliyoainishwa baada ya utafiti.
 4. Kiongozi kama mmojawapo wa viongozi katika baraza la kanisa kutoa program zake na kuzioanisha na ratiba za kanisa.  Hufanya kazi kwa karibu sana na mchungaji na kiongozi wa huduma za wanawake katika Konferensi yake.
 5. Kiongozi anayechaguliwa  ni mtu mwepesiwa kuhisi, anayejali, mwenye mzigo na matatizo ya wanawake.

 

MAJUKUMU YA KIONGOZI WA IDARA.

 1. Atafanya kazi kwa karibu na kamati yake kuchunguza mahitaji ya wanawake katika kanisa na ndani ya jamii.
 2. Atafanya kazi na kamati yake na mchungaji kufanikisha program za wanawake na semina akishikamana na makundi mbalimbali ndani ya kanisa.
 3. Ni mwenyekiti wa kamati ya Huduma za wanawake.  Ataandaa ajenda, atasimamia mjadala na kuhyamasihs umoja katika maombi na ushirika.
 4. Ni mtetezi wa matatizo ya wanawake, mahitaji na michango yao kwa uhai wa kanisa.

KUFANYA KAZI NA IDARA ZINGINE

Huduma za wanawake ni idara ambayo haipaswi kufanya kazi yenyewe bali na idara zingine sio kwa kuwa wanawake wameshirikishwa katika kazi zingine kanisani bali ni kwa sababu idara hii inahitaji kutegemezwa na idara zingine. Na yenyewe pia yapaswa kuwategemeza. Kwa mfano, Idara ya Huduma za familia  hutoa huduma kwa familia kushirikiana na mahusiano ndani ya familia. Tunaweza kualika Huduma za familia kushirikiana nasi katika program mbali mbali zinazotuhusu wote hivyo tutashirikiana.

Huduma za wanawake hueza pia kushirikiana na Idara ya Elimu hususani kwa wanawake vijana au na Idara ya Afya kwa ajili yam abo yanayohusu Afya na matatizo mbalimbali ya kiafya yanayo wakabili wanawake. Hili hutoa mwanya kwa wanwake kufanya kazi katika huduma mbalimbali , pia maeneo mbalimbali na hata kufanya kazi na Idara mbalimbali kwa kuzingatia karama aliyopewa na Mungu.  Itakuwa vyema kiongozi huyu akijenga mahusiano mema na viongozi wa idara zingine akitafuta namna anavyoweza kuhamasisha huduma za kanisa kwa ujumla. Hivyo basi wote watafaidika na huduma hizo.

Katika utendaji kazi huu ni rahisi sana kuvuka mipaka ne ya huduma za wanawake.  Chama cha Dorkasi ikiwa imelenga kutoa huduma kwa jamii pamoja na shule ya biblia wakati wa likizo na Idara ya Huduma binafsi, wote kama shemu ya Idara ya Huduma binafsi huhitaji taarifa.  Kuna uwezekano mkubwa wa wanawake kushiriki katika program za vyama hivyo hivyo wanapaswa kutoa taarifa kwa shule ya sabato au Idara ya Huduma binafsi.
 

SEHEMU YA TATU 

NAMANA YA KUANZISHA HUDUMA ZA WANAWAKE KATIKA KANISA MAHALIA.

Wanawake wengi hupenda kuanzisha kikundi cha Huduma za wanawake lakini hawajui pa kuanzia.  Wengine huona hawana viwango bali Mungu Mungu ana nyakati za pekee kwa ajili yetu ikiwa tu tutamtegemea na kushiriki katika huduma ambayo hukamilishwa vyema chini ya uongozi wake.

MUOMBE MUNGU AKUONGOZE.

Hatua ya kwanza kabisa ni kuomba.  Soma neno la Mungu na Roho ya Unabii kwa muongozo.  Kisha ongea na viongozi wengine wa Huduma za wanawake.  Katika hatua za mwanzo huenda wanawake wachache waweza kujali program mbalimbali za huduma, lakini kwa kadiri utakavyo mruhusu Mungu kuongoza, wengine watapenda kushiriki.

FANYA KAZI NA TIMU YAKO.

Kusanya kundi la wanawake dogo kuweka  mipango ya awali. Uwe na uhakika wa uwakilishi wa hao wachache huwakilisha wanawake wote ndani ya kanisa kwa mfano umri tofauti tofauti, iti kadi mbalimbali, tofauti za kielimu na uchumi. Itakuwa vizuri pia kupata uwakilishi wa wanawake wanaoishi peke yao, walioachika, walemavu na kadhalika.Ukifanya hivyo utakuwa unaandaa Huduma jumuishi itakayokidhi mahitaji ya kila mtu. Ikiwa mke wa mchungaji atapenda itakuwa bora zaidi. Endapo ratiba yake haitaruhusu basi muombe awe mshauri wako.

LENGA HUDUMA YAKO.

Bila shaka utachunguza wanawakewa kanisa lako wanahitaji program zipi, madarasa au kuwafikia wengine, hivyo basi utatambua hitaji la kanisa lako.  Hakikisha mipangilio  yako itafikia mahitaji hayo.  Hili ndilo lilikua kusudi la Yesu.  Hakutoa Huduma hivihivi tu bali alitoa huduma ili kufikia mahitaji ya watu halisi. Njia mojawapo ya kuchunguza mahitaji ya wanawake ni kuyaandika na kuyafunga vizuri yapendeze kisha wape wanawake wayapitie na kuonyesha nia zao bila kuhitaji kujua majina yao, kisha shughulika na hitaji lililopewa uzito zaidi na ufanye jambo moja kwa wakati mmoja ili waweze kukubali huduma yako kwao.

UWE NA VITENDEA KAZI.

Unapopanga program yoyote kanisani, mkutano, semina au hata kikao ni vizuri uwe na vitendea kazi kwa mfano kalamu, daftari, zana za kielimu.  Wazungumzaji wa mikutano yako pia wapewe vitendea kazi vya kutosha na kusafirishwa. Wasiliana na kiongozi wa Konferensi yako, Union au Divisheni kama kuna miongozo mipya iliyofika, vipeperushi, video au vitendea kazi vinginevyo.  Kuna vitabu vizuri sana kama mwanamke katika Biblia, kujithamini, vikundi vidogo vya maombi na vitabu rejea vya kujifunza Biblia.

KUFANYA UCHUNGUZI.

Likujua mahitaji ya kundi unaloliongoza ni vyema ukawaomba kujazafomu maalum za uchunguzi. Fomu hizi zaweza kuwa na maswali yafuatayo:-

 1. Kama mwanamke mkristo ni nini hitaji lako kubwa au unahitaji ukuaji katika shemu gani ili ukue kiroho?
 2. Ni mahitaji gani unayapa kipaumbele uliyoyagundua kwa ragiki yako asiye mkristo?
 3. Ukitazama wanawake wa kanisa lako ni nini ungependa kifanywe kwa ajili yao?  Ni kundi gani la wanawake unadhani wahahitaji uangalizi wa karibu?  (Kwa mfano akina mama, wasioenda shule, walioachika, wafanyakazi, wajane, n.k)
 4. Andika mambo mazito matatu yanayokabili jamii yako.  Unadhani Hduma za wanawake za kanisa lako itasaidiaje kushughulikia matatizo hayo?

Baada ya kujadiri mahitaji ya wale unaowaongoza, unaweza ukaandaa mpango kazi.  Baraza la kanisa liidhinishe kamati ya kupanga ili kuhakiki kiongo wa huduma na timu yake kulingana na muda wa uchaguzi.  Kamati hii pia yaweza kuchaguliwa na Baraza la uchaguzi.  Hawa watapanga mikakati itakayo husisha bajeti, aina ya program, tarehe ya kunaza program hizo na mipango mingine.  Ni vyema kuanza taratibu na kuendelea kukua.

KUCHUNGUZA MAHITAJI YA HUDUMA ZA WANAWAKE.

Ni masomo gani ungependa Huduma za wanawake ishughulike nayo?   Tunahitaji msaada wako ili kujua ni namna gani tunaweza kuandaa mipango ya baadae.  Soma orodha ifuatayo kisha weka vipaumbelevyako vinne kwa kuandika namba 1 – 4.

 • Uzee
 • Mbinu za kujifunza biblia
 • Kujithamini
 • Vikundi vidogo vya kujifunza biblia
 • Wakristo waseja
 • Kukabiliana na misongo
 • Matumizi mazuri ya pesa
 • Kurejezwa kutokana na machungu ya maisha
 • Kutumia muda vizur.i
 • Historia ya familia kutokana na ulevi, unyanyasaji.
 • Namana ya kushinda, kuachana na mazoea mabaya.
 • Namana ya kuwa mkristo katika ajira.
 • Wajibu wa mwanamke kanisan.i
 • Namana ya kuishi baada ya kuachika.
 • Wanawake katika uinjilisti.
 • Namana ya kuwa msomi.
 • Kutunza uzito wako.
 • Namana ya kuendesha kamati au Baraza.
 • Mawasiliano.
 • Namana ya kuomba
 • Ujinga
 • Ulaji mbaya
 • Namana ya kukuza akili
 • Magonjwa hatarishi kwa maisha yetu
 • Semina za uongozi
 • Namana ya kutoa hotuba
 • Namana ya kuwafanya kuwa wanafunzi
 • Kumshuhudia mwezi asiyeamini
 • Maombi na upendo huokoa.
 • Mengineyo.

KUCHUNGUZA UWEZO KATIKA HUDUMA ZA WANAWAKE.

Tafadhali angali sehemu zote unazoweza kujifunza na wengine.

 • Ukimwi.
 • Ulevi na madawa ya kulevya.
 • Mambo mazito katika Biblia.
 • Unyanyasaji wa motto
 • Mawasiliano
 • Mahitaji ya jamii
 • Kushauri matatizo makubwa
 • Kifo au kufa
 • Kufanya maamuzi
 • Msongo au kujinyonga
 • Mazoezi au Lishe bora
 • Kuachika
 • Ulaji mbovu
 • Matumizi mabaya ya Hisia
 • Fedha
 • Upweke
 • Hotuba
 • Kujitambua
 • Uzinzi
 • Malezi ya mzazi mmoja
 • Kuongoa roho
 • Kuwa mtu wa kiroho
 • Uwakili
 • Msongo
 • Kujali nafsi yangu
 • Kufundisha kama ujuzi
 • Kujitolea
 • Majukumu ya mwanamke
 • Kufanya kazi na vijana kwenye umri kati ya 13 – 19
 • Afya.

 

FANYA KAZI NA MCHUNGAJI WAKO.

Ni busara kufanya kazi kwa karibu sana na mchungaji wako.  Kuania mwanzo unapopanga mipango yako, mshirikishe mchungaji wako.  Utahitaji msaada wake ili ufanikiwe, pia atakushauri. Huduma za wanawake zitamsaidia mchungaji na mwenzi wake katika malengo yake ya familia kubwa ya kanisa.  Usifanye jambo lolote bila kumfahamisah mchungaji.Ni vyema program zako zote ziwepo katika kalenda ya kanisa mapema.

TAMBUA KARAMA ZA ROHO.

Mojawaqpo ya makusidi ya idara ya huduma za wanawake ni kuwasaidia wanawake kutambua na kutumia karama zao vema. Wasaidie kuzitambua karama zao mapema kabisa.  Njia nzuri kabisa ni kufanya kazi katika vikundi vidogo vidogo. Saidia kila kikundi kichore picha ya mwanamke.Kisha shauri kila mwanamke aanike jina lake katika sehemu mojawapo ya viungo vya mwili ambacho kinahusisha karama aliyonayo.  Ikiwa anapenda kufanya vitu kwa mikono yake basi aandike jina lake kwenye mikono. Huenda ameitwa kuhubiri basi aandike jina lake kwenye mikono. Huenda ameitwa kuhubiri basi aaandike jina lake mdomoni.  Masikio kwa ajili ya usikivu, moyo kwa ajili ya kupenda na kuhurumia n.k.  Kisha muombe kila mwanamke aeleze ni kwa nini anahisi kuwa hiyo ni karama yake. Na kama muda unaruhusu atawezaje kuwabariki wengine kwa karama hii.

ANDIKA MALENGO YANAYOFIKIKA.

Wanawake wanaweza kufurahi kuanisha idara ya huduma za wanawake lakini wakati mwingine wanashindwa kuweka malengo yanayofikika.  Programu zako zitakuwa na mafanikio makuba ikiwa utaweka malengo yanayofikika.

 • Je kiini cha program yako ni Kristo?
 • Tunahitaji watu wangapi?
 • Tutafana nii ili kupata idadi hiyo?
 • Wasio wanachama wetu wangapi tunatarajia wawepo?

Andika malengo yako kwa kutumia maandishi.  Hili litakusaidia kugundua mwanya wowote utakaoangusha mipango yako.  Ili ufanikiwe malengo yako lazima yawe maasusi, yanayofikika na pia yanayo pimika. 

JIULIZE:-

 • Je malengo yetu ni mahususi?
 • Je yanafikika?
 • Je tunategemea kuwa  mibaraka ya Mungu kwa malengo yetu yanayofikika
 • Je yanaweza kufikiwa na wanawake wa kanisa letu?
 • Je mafanikio yake yanapimika?

Ikiwa utaweza kujibu vizuri maswali hayo hapo juu basi utakuwa na hakika ya kuwa Huduma katika kanisa lako zitakuwa na mafanikio. Ni vyema kutathimini program yako baada ya kukamilika katika kanisa lako. Je ulifikia malengo yako?  Unaweza kuboresha program zako kwa wakati mwingine? Angalia vipengele vyote katika mpango kazi wako kuona ni jambo gani unahitaji kuboresha.

 

KUWEZESHA PROGRAM ZAKO KIFEDHA.

Hili laweza kuonekana kama kikwazo kukubwa kukishinda.  Waweza kuwa katika kanisa ambapo baraza la kanisa hukupa bajeti ya kutosha au unaweza usipate chochote kabisa hivyo unapaswa kuwa mbunifu kwa vyovyote vile utahitaji bajeti.  Kama huna karama hiyo muombe mtunza hazini wa kanisa wakufundishe namana ya  kupanga bajeti.  Panga mapema kuepuka gharama za mlipuko.  Tunza kumbukumbu na stakabadhi zote za manunuzi yoyote uliyofanya.  Fuata bajeti yako vinginevyo utahitajika kulipa gharama zilizozidi.ukifanya hivyo huduma yako itakuwa njema.

Kadiri muda unavyo kwenda na Idara ya Huduma za wanawake inazoeleka ni vizuri kuweka bajeti ya huduma za wanaweke.  Ikiwa huduma yako ni mpya katika kanisa lako unaweza usipewe masaada wa kifedha. Utapaswa kuzitafuta hizo fedha mwenyewe. Wanawake wanaweza kupika, kuoka mikate, kuandaa program za uimbaji, kuanzisha sehemu ya kuuza vitu na njia nyinginezo nyingi ambazo wanawake wanaweza kutumia katika kufafuta fedha. Kadri unavyopanga program zako vizuri ndivyo zitakavyoonekana kuwa na msaada katika kanisa, na ndivyo utakavyokuwa na fursa ya kupata pesa kutoka katika bajeti ya kanisa kwa ajili ya mipango ya baadae.

KUANDAA BAJETI YA HUDUMA ZA WANAWAKE.

Bajeti ni makadilio ya kiwango cha fedha unacho fikiria kutumia katika kipindi Fulani cha muda. Wakati fulani bajeti zinapaswa kupitiwa kwa sababu ya matumizi yaliyozidi au mahitaji ambayo hayakufikiriwa kuonekana ya muhimu au kujitokeza. Kupitiwa kwa bajeti husababisha fedha toka akaunti moja kwenda nyingine ndani ya bajeti halisi kutumika. Furahia bajeti yako kwa kuwa kamati mbalimbali huzipunguza, kwa kiwango kidogo au kikubwa. Ni vizuri kuomba kisasi kikubwa na usipate, niafadhali kuacha kile uliochokipenda kwa kwa kukosa bajeti kuliko kama kukikosa kwa kutokiombea bajeti. Katika kuwasilisha bajeti yako kwa kwa kamati, fanya sehemu yako kisha uonyeshe msingi wa kiwango unachoomba. Elewa kuwa ngazi zote za Huduma ya Idara ya wanawake hutumia fedha kwa akili. Fanya kiazi karibu sana na uongozi. 

Hakikisha shughuli zote za Huduma za wanawake zimewekwa katika kumbukumbu nzuri kwa kuwa matokeo yake yatakuwa kama ifuatavyo:-

 1. Wanawake hujisikia vizuri kama kanisa hutoa fursa kama hizi.
 2. Wanawake huwaalika rafiki zao walio na vuguvugu la kiroho kuhudhuria mikutano yao na rafiki hao hufurahia na kupokea mwito katika mtazamo wa kiroho na kijamii kanisani.
 3. Mikutano ya kiroho ni sehemu nzuri ya kuwasaidia wanawake hawa kufanya maaumzi ya kubatizwa.
 4. Wanawake hukua kiroho na kuwa washuhudiaji wazuri katika jamii zao.

Tambua mchango wa Union au Konferensi katika maandishi au kwa maneno kwa ajili ya kukutegemeza, na kukutia moyo.

MFANO WA BAJETI (KANISA MAHALIA)

Imependekezwa ………….(mwaka) Bajeti ya Huduma za wanawake.

 

Gharama                                                                Kiasi cha fedha

 1. Mahitaji ya ofisi                                                 Sh……............
 2. Gharama za vitabu, makaratasi, kalamu n.k        Sh.…………………
 3. Mawasiliano                                                      Sh.……...........
 4. Mengineyo                                                        Sh……….........

Jumla ya gharama  za ofisi                                    Sh................  

MIKUTANO

 1. Mikutano ya wanawake                                     Sh…………….....
 2. Gharama za mnenaji                                        Sh.……………....
 3. Kumsafirisha mnenaji                                       Sh.……………....
 4. Malazi                                                             Sh………..........
 5. Mengineyo                                                       Sh…………….....
 6. Mikutano ya Conference au Union                      Sh………………...

Jumla ya gharama za mikutano                                 Sh………….......

 

PROGRAM MBALIMBALI

 1. Kuitangaza au kutitambusha idara                     Sh………….......……
 2. Zawadi na vipeperushi                                      Sh…………............
 3. Vitulizo vya akili (Refreshments)                        Sh…………….........
 4. Kukodi chumba                                                Sh…………….........
 5. Kukodi vitaa au kununua                                   Sh…………….........
 6. Mengineyo                                                       Sh……………..........

Jumla ya gharama za program mbalimbali           Sh……………......

 

SAFARI

 1.  Mikutano ya kiroho ya Konferensi yako              Sh.……………….......

Jumla ya gharama za safari                                      Sh……………..........

Jumla kuu ya bajeti yote                                       Sh………………....

 

VIPATO

 1. Bajeti ya kanisa                                              Sh………………..........
 2. Zawadi na michango ya hiari mbalimbali           Sh.………….............
 3. Kuomba changizo mbalimbali                           Sh.………….............

Jumla ya vipato vyote                                          Sh.…………..........

 

TAMBULISHA PROGRAMU ZAKO

Waweza kuwa ma program nzuri sana. Inaweza isifaminiwe kwa sababu watu hawaifahamu. Watu wamatangazo wanasema ni lazima urudie jambo zaidi ya mara moja ili watu walifahamu na kulikumbuka. Hivyo basi fikiri kwa kadiri uwezavyo namana ya kushirikisha wengine katika program zako. Unaweza kutumia ubao wa matangazo wa kanisa, barua na ha hata matangazo kkatika mbao za matangazo mbalimbali.  Unaweza kutangaza kwa kutuma vipeperushi. Ikiwa utahitaji wasio na uanachama wa hudhurie basi tumia redio au televisheni kutangaza na visa katika magazeti. Washirikishe wanawake kutoka katika madhehebu mengine.Kila program yako iwafikie wengine wasiomjua Yesu. Uwe tayari kuwashirikisha wakristo na wasio wakristo na kamwe usikate tamaaa wala kuwakatisha tama wengine na kutmia lugha chafu. Utakuwa katika nafasi nzuri endapo utaweza kutumia kanisa zima kushiriki kuzitambulisha program zako.Shirikisha vikundi vya maombi kuombea program zako.  Watie moyo washiriki wa kanisa kuwaleta rafiki zao.  Uwe mbunifu!

KUANDAA MKUTANO WA HUDUMA ZA WANAWAKE.

Maana ya mkutano;
Mikutano ya Huduma za Wanawake ni kwa ajili ya wanawake ikiongozwa na kiongizi wa Huduma za Wanawake.  Pamoja na kamati ya mkutano.  Kamati inapaswa kuwa na viongozi wafuatao pamoja na wengine watakao hitajika kwa ajili ya program fulani;

 • Kiongozi wa program mbalimbali
 • Mtunza muda
 • Kiongozi wa chakula
 • Mhudumu wa mnenaji mkuu
 • Msimamizi wa vifaa mbalimbali
 • Mratibu wa uimbaji
 • Msajiri
 • Mwenyekiti wa mapambo
 • Mratibu wa kikundi cha maombi
 • Mhazini
 • Na wengine kwa kadri ya uhitaji na mazingira uliyopo.

KUSUDI LA MKUTANO

Kusudi la mkutano ni kukuza watu kiroho, ushirika na fursa za kuwapa changamoto wanawake wajihusishe na utume wa kanisa.

AINA YA MKUTANO

 1. Mkikutano ya kanisa mahalia makundi ya makanisa mbalimbali, Konferensi au Union.
 2. Mikutano ya uongozi
 3. Mikutano ya mama au binti
 4. Mikutano ya wanawake vijana katika umri wa miaka 13 – 19.

MAHALI PA MKUTANO:

Makambi ya vijana, maeneo ya Konferensi, Hotelini, maeneo ya mapumziko, shule za boarding wakati wa likizo.

Nani anashiriki?

Wanawake wa umri tofauti tofauti kutoka katika Nyanja mbalimbali za maisha.  Wanenaji, waimbaji, waratibu wa vipindi, wote wawe wanawake.  Watie moyo wanawake kualika marafiki au majirani zao washiriki pia.

NENO KUU.

Kamati ichague neno kuu la mkutano au kumuomba mnenaji mkuu achague.Mapambo ya aina mbalimbali yatengenezwe kuonyesha neno kuu.  Ni lszima liwe la kuvutia na liwe na wito kwa wanawake.  Wimbo mkuu, muziki, nyimbo mbalimbali, utambulisho na vyote hivyo vilenge neno kuu.

MNENAJI AU WANENAJI WAKUU.

Mnenaji mkuu hualikwa kuzungumzia mada ambazo ni vulivu au zinazo wagusa wanawake.  Huwaanapewa neno kuu mapema ili aandae masomo yake kulingana na neno kuu.  Ni vyema ikiwa mnenaji mkuu atafika siku moja kabla ya kuanza mkutano wako, ili aonanae na uongozi.  Hili litasaidia kila mtu afuate ratiba na kutumia ratiba kuizoea na kuombea mafanikio ya mkutano.  Ujumbe wowote unao walenga wahudhuriaji wa mkutano umfikie na meneja mkuu pia kwa mfano nguo za kubeba, kama kuna kuogelea, matembezi na kadhalika.  Hili litamfanya nay eye pia ashiriki katika ratiba hizo.

MUDA.

Muda wa mwoshoni wa juma yaani Ijumaa jioni mpaka Jumapili mchana unafaa kwa wanawake watakao hudhuria.  Kila kipindi kianze kwa wakati na kuisha kwa wakati.  Mtunza wakati ateuliwe ili ahakikishe kuwa jambo hili linatendeka.

CHAKULA.

Chakula kiandaliwe na kutengwa na watu wengine tofauti na wale waliohudhuria kwenye mkutano.  Kikundi Fulani kiajiriwe kulisha mkutano au waume wa baadhi ya wanawake hao ikiwa watapenda waweza pia kufanya shughuli hiyo (Kulingana na mazingira).  Kanisa pia laweza kuchukua hilo kama mradi wa kanisa.

GHARAMA.

Mikutano huwa na gharama.  Bajeti ipangwe kwa uangalifu mkubwa kisha kila mwanamke achangie kwa kiwango Fulani.  Ikiwa utapewa fedha kutoka Konferensi au Union, hakikisha umerejesha matumizi pia zitumie kwa uangalifu mkubwa.  Makanisa yanaweza kutafuta wafadhili mbalimbali wa progamu zao, vinginevyo fedha za Konferensi au Union zaweza kuwa msaada mkubwa kwa wale ambao wangependa kwenda lakini hawawezi kuhudhuria kwa sababu ya kipato chao kidogo.  Kila kamati ichunguze njia za kupunguza gharama na pia njia za kuwasaidia wahitaji.  Bado gharama zinaweza kushushwa sana na kufanya mikutano hii iwe ya Baraka kwa wanawake na pia waifurahie.

MFANO WA PROGRAM

Kamati ya program itapanga vipengele vyote vya program na kuweka katika kijitabu kidogo cha ratiba. Ratiba hii iwe na vichwa vya masomo ya mnenaji mkuu, nyimbo na vikundi vya uimbaji, n.k. Unapopanga ratiba, uwe na muda wa mapumziko na muda wa wanawake kufahamiana na bila kutoroka katika vipindi.

ANGALIZO:

Haya ni mapendekezo tu.  Kamati inaalikwa kuwa wabunifu kuandaa ratiba itakayo wafaa kutokana na mazingira waliyomo na pia wahudhuriaji wa mkutano huo.

MFANO WA RATIBA.

IJUMAA

10 : 30      Usajiri

12 : 30      Chakula cha jioni

 01: 00      Uimbaji

 01 :30      Mnenaji mkuu

 02 :30      Vikundi vya maombi

 

JUMAMOSI

01 : 00        Matembezi ya asubuhi ( sio lazima)

02 : 00        Ibada

02 : 30        Kifungua kinywa

03 : 30        Uimbaji

04 : 00        Mnenaji mkuu

04 : 45        Mapumziko

05 : 00        Uimbaji

05 : 15        Mnenaji mkuu

06 : 00        Shuhuda na kusifu

06 : 30        Chakula cha mchana

09 : 00        Maombi

10 : 30        Washa mbalimbali

12 : 00        Chai au chakula cha jioni

1 : 00          Maburudisho

Maombi ya Asubuhi ni kipengele kizuri sana kwa jumapili asubuhi.  Mnenaji mkuu aweza kusimamia hili pia. Ifuatayo ni ratiba iliyopendekezwa.

 

JUMAPILI:

2 : 00  Ibada

2 : 30  Kufungasha na kufanya usafi

3 : 00  Mnenaji mkuu

4 : 45  Mgawanyiko

6 : 15  Kufunga

 

SEHEMU YA MAOMBI

Wahuskia waweza kupangwa kulingana na tarehe za kuzaliwa, Rangi niipendayo, n.k.  Makundi hayo yanaweza kukubaliana ni lini na ni wapi wanaweza kukutana kwa ajli ya maombi, pia wanaweza kujipangaia ratiba zao. Andaa picha ya moyo au kitu chochote, kigawe mara mbili wape wanawake vikiwa nusu nusu hivyo hivyo.Mwambie kila mwanamke atafute kipange cha pili.Akimpata huyo ndiye atakua mwenzake katika maombi.

SHUHUDA.

Programu hii huwapa au huwatia nguvu wanawake wanaposikia shuhuda toka kwa wanawake wenzao.  Shuhuda zaweza kuwa majibu kwa maombi, mguso kutoka katika kitabu au gazeti, nguvu au msaada wa kiungu katika kutatua tatizo kubwa alilokua nalo au sifa na shukrani kwa ajili ya mibaraka.  Wakumbushwe kuwa muda wa ushuhuda sio muda wa kumkosoa mtu au kutoa mawazo hasi dhidi ya mwingine.

WASHA MBALIMBALI

Washa zitoe nafasi kwa vitendo vinavyotatua mambo mazito ambayo ni changamoto kwa wanawake. Mada hizi zitolewe katika mtindo wa kuvutia badala ya kufunda. Wanawake wanao hudhuria katika kila kipengele cha mgawanyiko wasizidi 25. Mgawanyiko wa Jumapili waweza kuwa ni marudi ya mgawanyiko wa Jumamosi jioni ikiwapa  fursa wanawake kuingi katika washa ambayo hakuhudhuria Jumamosi jioni.  Kiwango cha juu cha washa kwa ajili ya kuchagua kiwe washa 4.

Programu mbadala ya Jumamosi usiku.

Hii yaweza kuwa sherehe ya upendo inayoambatana na uwashaji wa mishumaa.  Chakula chaweza kua (Matunda, Mikate, Karanga,na kadhalika).  Shuhuda zaweza kuffuata, zikitaja ushindi na sifa na shukrani kwa Mungu.  Unaweza pia ukaandaa vizawadi vidogo vidogo kwa ajili ya wale wote watakao hudhuria.  Vinaweza kuwekwa katika vitanda vyao au wakapewa wakati wa shuhuda na muda wa kuagana.

SEHEMU YA NNE.

NAMNA YA KUWAPATA WANAOJITOLEA.

Kufanya kazi na wale wanaojitolea sio mchakato rahisi.  Kiongozi mwenyewe mfanikio hutumia taratibu fulani kuwapata wanawake wanaojitolea.  Kufanya kazi na idara hii ni pamoja na kuwaelekeza mambo ya kufanya, kuwaelekeza mambo ya kufanya na kusimamia shughuli na utekelezaji wake kwa moyo wa furaha.

 

HATUA ZA KUCHUKUA.

Jua hitaji lako.

Kiongozi mwenye mafanikio lazima kwanza atambue hitaji la wale anaowaongoza wa jamii kwa ujumla.  Kisha huandaa kauli mbiu inayokidhi hitaji hilo na muitikio wake.

Anza kutafuta wanachama ukirejea kwa wasaidizi wako kwa sasa. 

Je wanajisikiaje?  Je wanajisikia kuwa wao ni sehemu ya program hiyo?  Je kuna wanaojisikia kutengwa?Je wanajisikia furaha kuwa sehemu ya huduma hii wakiwavutarafiki zao kushiriki?

Tambua uwepo wa wasomi wanaojitolea.

Ni wangapi kati yao wasiojishirikisha na huduma yako.  Je kuna wasomi miongoni mwao?Je wanaweza kusaidia kutoa huduma?  Ni nani mwingine unaweza kumpa changamoto ili atumike kutoa huduma?

Fahamu kile unachotaka unaowaongoza wafanye.

Uwe na mipango kazi unaoonyesha malengo, makusudi na mambo ya kufanya.

Panga ratiba za mafunzo mbalimbali.

 Neno mafunzo lisikutishe sana.  Wasaidizi wako wanahifaji maelekezo kutoka kwako kwa ajili ya majukumu uliyowapa kufanya.  Hili litazuia kukata tama baadae pamoja na msongo isiyo na sababu.  Kiongozi anapogawa madaraka ni lazima ampe uwezo Yule anaye mgawia madaraka ili afanye kazi zake vizuri.

FANYA KAZI KWA PAMOJA (KAMA TIMU)

Tafuta ni nini kinachowatia moyo wasaidizi wako. Wanachama wako wanapaswa kujisikia kuwa wanaleta tofauti. Orodha ifuatayo ni mbinu za kuwa motisha unaowaongoza.

 1. Wafanye wajisikie kuwa wanahitajika
 2. Majukumu yao yaendane na uwezo wao, vitu wanavyovipenda na mahitaji yao ya kisaikolojia.
 3. Wape majukumu yanayotekelezeka
 4. Wasaidie wawe na mafanikio makubwa
 5. Wafanye wajisikie kukubaliwa

Namna ya kujenga umoja.

Kama kiongozi toa fursa kwa wanaofanya vizuri zaidi ili uweze kufikia malengo. Wanachama wanataka kutambuliwa, kuwaminiwa na kuheshimiwa. Wanahitaji kujisikia wao ni sehemu ya Jumuia hiyo.  Wanahitaji kujua kuwa kazi wanayoifanya ni sehemu ya majukumu ya jumuiya hiyo. Haya yakiwa yamekwisha basi tutakua na timu nzuri.

Mambo sita yanayojenga umoja:

 1. Kuwaelezea wanatimu majukumu yako
 2. Kujenga imani
 3. Kuwakumbusha wanachama kuchangia mafanikio ya utendaji kazi wa idara
 4. Kutambua mafanikio ya magoli mbalimbali
 5. Kufahamu ujuzi wao wa kutatua matatizo
 6. Kutumia mbinu shirikishi.

TABIA ZA TIMU ZILIZOSHIKANA SANA

-       Wanatimu wanaelewa na kufuata njozi ya kiongozi

-       Wanachama huheshimiana na kupendana

-       Mawasiliano yako wazi

-       Wanakikundi hujivunia umoja wao

-       Kuna mitafaruku kidogo sana na kama ikitokea hutatuliwa kwa kutumia njia zinazojenga

-       Kutambuliwa na kupongezwa kwa kazi nzuri ni jadi ya timu hiyo.

-       Wanatimu wanaelewa kusudi, malengo na njozi ya idara

-       Kufanya kazi kwa pamoja hukuza mazingira ya kuaminiana.

KUWEZESHA UKUAJI WA VIONGOZI WENZAKO

Kama kiongozi watie moyo wenzako kwa kuwaambia  kwamba kila mtu ni lazima akue bila kujali cheo wala majukumu aliyopewa kazi za kila siku hebu na ziwe darasa kamili. Namna ya kukuza ukuaji binafsi.

-       Hudhuria semina na washa mbalimbali

-       Fanya kazi moja kwa moja na wanachama

-       Buni karakana za vikundi kwa ajili ya mafunzo mseto

-       Pata nafasi ya kutembelea vikundi mbalimbali vya huduma za wanawake.

-       Andaa semina za uongozi kanisani au hudhuria semina hizi ikiwa zimeandaliwa na Konferensi au Union

-       Ruhusu karakata za pekee zinazokuza ujuzi na uwezo

-       Soma vitabu na magazeti ili kujiendeleza zaidi

-       Panga mikutano ya wafanyakazi kwa ajili ya kamati zako

-       Wape kazi wanawake ili kuwawezesha

-       Pata mrejesho uwe tayari kwa mabadiliko

-       Ruhusu maswali

-       Wasifu, watie moyo na kuwalea wanachama wako

-       Waendeleze wanachama wako

Njia yoyote utakayoitumia, ujumbe wowote utakaotumia unapotea mkazo katika ukuaje na kuongeza ujuzi wa viongozi wenzako utaleta mafanikio makubwa.

KUWEZESHA PROGRAM YA MALEZI

Yesu alichagua wanafunzi wake 12 kutoka katika Nyanja mbalimbali za kimaisha. Kwa miaka 3 aliwafundisha kila alichoweza kuwafundisha. Alipoondoka aliwaachia agizo la kuwaeleza wengine mpango wa wokovu. Hata leo changamoto hiyo ni yetu na Yesu ndiye mfano wetu katika kuandaa viongozi wazuri kanisani.

MAANA HALISI YA MALEZI

Malezi ni kumuathiri mwingine kwa wema katika maisha yake ili kumbadilisha kuelekea wema kupitia hudima ya mtu mmoja kwa mmoja. Mlezi huyu huunda urafiki, hufundisha na pia  kumwezesha kukua. Kupitia  kumshirikisha mwanamke kijana basi mlezi huyu humfundisha  kutokana na hazina yake. Huwatia moyo wanawake vijana  washiriki katika program mbalimbali kuhusiana na malezi ya watoto, ndoa na mahusiano ya ndani ya mtu binafsi. Mlezi huyu humweleza mwanamke kijana atumie uwezo wake wa juu kabisa ndani ya yesu. Kama mlezi usiangalie au usitatue wanawake  wasio na mawaa bali wale waliokubali Biblia na wanalishika neno.

KUANDAA PROGRAM ZA MALEZI ZA KANISA

Panga mikutano ya makundi kama vile mada za malezi kwa mfano;

a)   Namna ya kulea watoto kanisani

b)   Namna ya kuvaa kwa ajili ya mafanikio

c)   Namna ya kugundua uwezo wako wa kiroho

d)   Namna ya kukabiliana na msongo


Waunganishe au kuwapanga wanawake wenye ujuzi na wale wanaohitaji malezi kwa mfano;

a)   Akina mama wa siku nyingi na akina mama wachanga

b)   Wanawake wachanga katika taaluma ya kazi na wale walio hitimu katika ngazi za juu

c)   Akina bibi na mabinti wadogo wanaosoma shule za bweni

Weka mipango kama vile rafiki wa siri, dada wa siri na rafiki wa maombi. Hakikisha kuna fursa sawwa na kujitoa. Ifanye kuwa fursa ya kusaididana kiroho, tafuta namna ya kuwasaidia wajitathmini bila garama yoyote. Pata muongozo zaidi kutoka katika uongozi wa Konferensi au Union yako.

SEHEMU YA TANO

Kama wakristo tunaotamani kufuata mfano wa yesu, tunaamini kuwa ni muhimu kufanya kile tunachoweza kufanya kugusa maisha ya watu , kufikia mahitaji yao na kujenga mahusiano, kuwa na Imani na kuwasaidia kufikia magoli yao.

PROGRAM ZA HUDUMA ZA WANAWAKE KATIKA KONFERENSI KUU

 1. Kitabu cha maombe cha huduma za wanawake konferensi kuu.

Idara ya huduma za wanawake ulimwenguni huwatia moyo wanawake ulimwenguni kote kutoa mchango wao katika kuandaa kitabu cha maombi kwa kutumia uzoefu wao binafsi wa kimaisha  na namna walivyoona mkono wa Mungu katika maisha yao. Faida zitakazopatikana kutokana na mauzo ya kitabu hicho hutumika kupelekwa katika mfuko wa ufadhili na kuwasaidia wanawake katika masomo yao.

MAELEKEZO YA JUMLA

-       Mchango kutoka katika uzoefu mpana wa kimaisha kiroho, kutia moyo na kuonyesha uwepo wa Mungu katika maisha ya wanawake, utazingatiwa mahubiri hayatakubalika.

-       Kitaby hiki kitauzwa nje ya kanisa na ndani ya kanisa maneno yote yatakayotumika yasiwe kikwazo kabisa kwa wale wasio washiriki

-       Oktoba 1 ya kila mwaka itakuwa ndio mwisho wa kutuma mchango wako wa kuweka katika kitabu cha maombi cha idara ya huduma za wanawake.

 1. Program ya ufadhili ya huduma za wanawake konferensi kuu

Huduma za wanawake konferensi kuu imeandaa program za ufadhili kwa wanawake wa kiadventista wasabato ambao hawawezi kumudu gharama za elimu ya kikristo.

 1. Program ya kutoa vyeti vya uongozi

Program hii imeanzishwa kanisani kuwawezesha wanawake wa kanisa letu kutumika katika nyanjja nyingi za uongozi kama tunavyojitahidi kukidhi hitaji la utumishi kanisani. Dada Ellen G White anatukumbusha kuwa  “Kuna kusudi kubwa kwa mwanamke anapaswa akuze na kujenga uwezo wake kwa ajili ya kuokoa roho." (Evangelism uk. 465). Kukuza uwezo wa wanawake ni kazi mojawapo ya idara hii, program hii inalenga kuwawezesha wanawake kuwa viongozi watakaofanikiwa sana.

PROGRAM ZA HUDUMA ZA WANAWAKE KATIKA MAKANISA MAHALIA

Jambo mojawapo gumu katika idara ni kuandaa program, tunaanzaje? Ni matukio gani yanapaswa kuwepo? Tunamlenga nani? Yafuatayo ni mawazo yatakayokufanya uanze. Ni nini kusudi la program hizi? Ni kuwasaidia wanawake wakue kiroho, hivyo basi unapopanga program ni muhimu kuona sio tu program itakayowafaidisha wanawake ndani ya kanisa ila itakavyowaleta wanawake wengine ndani ya kanisa. Katika program hizi wanawake wote wanaweza kukua kiroho. Lakini pia wageni watiwe moyo kujenga uhusiano utakaowafanya warudi kwa ajili ya program za kiinjilisti.

Makundi madogo ya huduma kwa ajili ya wanawake ambao:

 1. Wameachika
 2. Wameolewa hivi karibuni
 3. Wazazi wa watoto miaka 13-19
 4. Hulea
 5. Mzazi mmoja
 6. Wana majonzi
 7. Wamenyanyaswa
 8. Wagonjwa mara kwa mara
 9. Wanata waushinde ulevi,uvutaji wa sigara nk.

Kundi la afya ya mwanamke

 1. Madarasa ya kuacha uvutaji
 2. Kliniki ya kupoteza uzito
 3. Masomo ya lishe
 4. Madarasa ya kupika
 5. Madarasa ya kufanya mazoezi
 6. Wanaotembea pamoja

Kundi la maombi

 1. Maombi ya asubuhi
 2. Kapu la maombi
 3. Maombi katika mandhari ya nje (bustanini)
 4. Makundi ya maombe
 5. Wemza wa maombi
 6. Mnyororo wa maombi

HUDUMA ZA WANAWAKE KATIKA KUISHUHUDIA JAMII

Wakati program za nje za idara ya huduma za wanawake hufanywa kwa lengo la uinjilisti baada ya program zipangwe kuwavutia wanawake katika jamii. Hizi zinaweza kuwea pia ni maandalizi ya mikutano ya hadhara inayokuja hivi karibuni.

1)   Makundi ya kujifunza biblia ya ujirani mwema

2)   Maombi ya asubuhi pamoja na dini zingine

3)   Madarasa ya kupoka vyakula visivyo vya nyama

4)   Kurejeza walioachika

5)   Kuwafariji wenye majonzi

6)   Siku ya kusoma maandiko

7)   Chakula cha watoto cha pamoja

8)   Program ya kumkaribisha mtoto mchanga

9)   Program ya kuondoa ujinga

10) Elimu ya afya kwa wanawake waliotoka kuolewa hivi karibuni

11) Matumizi mazuri ya fedha

12) Kuondoa au kupunguza msongo

13) Huduma ya magereza

14) Kuwahudumia watoto walioathirika na Ukimwi

MAKUNDI YA HUDUMA YENYE KUTOA MSAADA:

UTAANZAJE?

 1. Omba ili upate viongozi war oho mtakatifu ikiwa wanawake hawa watapenda kuomba pamoja nawe itakua vyema. Watafute watu wengine wanaoweza kuvutiwa na program hii kasha mkae na kuandaa mipango. Mhusishe mchungaji yeye anaweza kushauri au kusaidia kusukuma program yako.
 2. Chagua viongozi na wengine watakaopenda kwa hiari yao wenyewe kushiriki. Ikiwa kuna ulazima pata ruhusa kutoka katika baraza la kanisa utahitaji kufanya hivyo ikiwa utahitaji fedha, vyumba vya mikutano vya kanisa, n.k waweza kutengeneza bajeti ikiwa utahitaji fedha.
 3. Andaa sehemu na muda kwa ajili ya kikao  cha kwanza yaelewe mahitaji ya kundi hilo kwa mfano wanahitaji msaada wa aina gani? Je ni ushirika? Uvuvio wa kiroho? Fahamu ni mahitaji gani kasha panga program ya kuanza kufikia mahitaji hayo.
 4. Panga kiini cha program yako

-       Andaa mnenaji au mfundishaji mkuu

-       Weka muda wa somo fupi pamoja na maombi

-       Andaa mtu wa kuandaa sehemu ya kikao mfano viti, mwanga, n.k

-       Andaa projekta, makaratasi, kalamu, maiki n.k

-       Wape vinywaji au vitu vidogo vya kutafuna kama ikiwezekana

-       Ikiwa kikao kitahusisha mzazi mwenye mtoto mdogo basi andaa namna ya kumtunza huyo mtoto

-       Kumbuka kufanya usafi baada ya kikao
Tangaza kikao chako cha kwanza kwa kutumia njia mbalimbali kwa mfano mbao za matangazo za kanisa simu n.k

Baada ya kikao chako cha kwanza kutana na viongozi kasha ufanye tathmini nini kibadilishwe na kufanyiwa kazi kabla ya kikao kingine.

 

ILI KUWA NA KIKUNDI CHA KUTOA MSAADA CHENYE MAFANIKIO FANYA AU KUTOFANYA YAFUATAYO;

 

FANYA                                                                             USIFANYE

-       Toa fursa za kufanya ushirika           -  Usiruhusu masengenyo na manun’guniko

-       Toa fusa za kufanya mawasiliano      -  Usiruhusu udanganyifu wa aina yoyote

-       Baki kwenye misingi ya Biblia           -  Usipoteze muda

-       Uwe na nia ya kuwakubali wote        -  Usitoke nje ya mada iliyopangwa

-       Tumia lugha ya kawaida                   -  Usiwape watu majina

-       Tunza siri za watu                            -  Usiwahukumu wengine

 

KUWAREJEZA WALIOACHIKA

Leo, jambo linaloikumba dunia kwa haraka ni kuachana (mume na mke kupeana talaka). Kuna hitaji la kuweka mazingira ya faraja, kuachana huwa kanisa litoe msaada. Wahusika wanamahitaji ya kiroho, kiuchumi,kijamii na kihisia. Idara iwe na program ya kuwasaidia walioachika kupona machungu ya kuachika kusudi kubwa la program ni kupata maelezo, msaada na marafiki watakaosikiliza bila kutoa lawama. Hakuna mwisho wa machungu yatokanato na kuachana, kuna matatizo ya mahusiano yatokanayo na kuachana maana mara kwa mara kuna hisia za machungu zisizokoma.

Program ifanyikeje?

-       Kuwepo na kikundi cha watu wanaohitaji msaada baada ya kuachika

-       Saa ya kwanza inatumika kwa ajili ya maswali na shuhuda

-       Saa ya pili itumiwe na mzungumzaji akitoa msaada wa ushauri

-       Kubali umeachika

-       Anza kuzoea madhara yote yatokanayo na kuachana

-       Wasaidie watoto kuzoea

-       Mwombe Mungu akujalie uwezo wa kusamehe toka moyoni

-       Mtafute Mungu aujazie upweke ulio nao kwa pendo lake la ajabu

HUDUMA KWA WAJANE

Kusudi ya huduma hii ni kutoa huduma kwa waliovunjika moyo;

    Malengo

 1. Kuwafikia kwa upengo wale waliowapoteza wapendwa wao
 2. Kuonyesha kuwa tunajali majonzi yao na kutoa faraja. Hili lifanyike katika mtazaamo wa Biblia na sio utamaduni
 3. Kufanya mwanya ambao utawawezesha wale wanaoumia kukutana pamoja kubadilishana uzoefu kusoma biblia na kuomba pamoja
 4. Kuwasaidia hawa wanawake wanaojaliwa kufanya shughuli ndani ya kanisa na kujisikia wao ni sehemu ya kanisa.

Mnaweza kukutana mara mbili kwa mwezi mchana au jioni kulingana na umri wa wahusika.

MAISHA BAADA YA AJIRA

Maisha baada ya ajira huwahusu wanawake walioko katika ajira wasioweza kufikiwa. Huduma hii imekuwa ya muhimu sana ktika huduma za wanawajjke. Program zifuatazo zaweza kuandaliwa kwa ajili yao.

 1. Kujifunza Biblia wakati wa mapumziko ya chakula kwa wanawake wanaofanya kazi ya kula  chakula kazini
 2. Kutoa semina mbalimbali zihusuzo maisha katika ulimwengu wa ajira
 3. Kujifunza biblia wakati wa jioni baada ya kazi kabla ya kwenda nyumbani
 4. Kujifunza biblia kwa undani sana wakati wa usiku kwa wanawake wanaohitaji kujua biblia kwa undani
 5. Program ya kila jumatatu usiku ya kukutana wanawake wote wafanyakazi kupewa semina mbalimbali zinazohusu maisha ya kazi nyimbo na mengineyo yahusuyo maisha ya ajira
 6. Kuwa na jumapili nne kwa mwaka ambapo wataalam mbalimbali watazungumzia mambo yatokanato kazini katika vyumba vya mkutano au hoteli mojawapo.

 

HUDUMA ZA VIKUNDI VIDOGO VIDOGO

KUSUDI;

Huduma za vikundi vidogo vidogo ni njia bora ya kufikia mahitaji ya wanawak. Vikundi hivi vinaweza;

-       Kutengengeza mtandao wa kusaidia wanawake wenye mahitaji yanayofanana

-       Kujenga mahusiano

-       Lenga katika ukuaji wa kiroho

-       Kufundisha kwa ajili ya kuwafikia wengine

-       Vinaweza vikafanya kazi bila bajeti


Kwa nini vikundi vidogo vidogo?

Kanisa ni sehemu pekee ya upatanishi duniani kimsingi hushughulika na kuwaleta  watu pamoja  kiafya, kukuza mahusiano na Mungu na wengine

Kipaumbele cha kikundi kidogo

Kikundi kidogo kinapaswa kuwasaidia watu na kuwakuza. Juhudi zote zilenge kutufanya tupende zaidi na kupatana. Ikiwa jambo hili litatendeka ndani ya kanisa litawavuta wengine kwetu

Ukubwa wa vikundi

3-12=vikundi vidogo

15-40= kikundi cha kati

 

AINA SITA YA VIKUNDI VIDOGO VIDOGO

Kikundi cha maombi:

Hawa  hushuhudia majibu kwa maombi yao na pia hufurahia kuomba pamoja na wenzao.

Kikundi cha kujifunza Biblia:

Huweka mkazo katika usomaji wa biblia ili kuweza kujadili na wenzao katika kipindi kinachoandaliwa baadae.

Kikundi cha malezi:

Kikundi hiki ni kwa ajili ya wanachama waliobatizwa hivi karibuni wanaohitaji kuwa na marafiki. Ni kikundi kwa ajili ya wanachama wapya wanaotaka kufurahia ushirika wa kikristo na ukuaji katika Bwana.

Kikundi chaa kutoa msaada:

Wanawake hawa huwa na wahitaji yanayofanana wanaweza kuwa walioachwa wajane, walionyanyaswa, walioolewa na wenzi wao wasio waadventista wasabato n.k

Kikundi cha kushuhudia:

Kikundi hiki kina uhitaji wa pekee katika uinjilist wanafurahia mafunzo ya biblia na aina zote za ushuhudiaji, hebu na wawe wabunifu kwa kila wanachokifanya lakini wapate mibaraka ya mchungaji kabla ya kuanza program yoyote.

Kikundi cha kanisa la nyumbani:

Hiki huhusisha watu ambao hawawezi kwenda kanisani kwa sababu ya sababu za msingi wanazozifahamu, kwa mfano hakuna kanisa lililo jirani au kanisa lili jirani nao liko mbali sana au pengine kwa sababu za kiafya. Watu katika hali hizi wanaweza kuanzisha kikundi kidogo ili kutia moyo wengine kushiriki.

MAPENDEKEZO YA KUTOA HUDUMA

Mungu ndani ya viatu:

Yaweza isiwe viatu huwakilisha vitu vingine vingi mfano keki, kitenge, chakula n.k. Katika hili wanawake huchukua viatu na kuwapelekea wale wasio na viatu hivyo kugusa maisha yao na kujitolea kwa Yesu.

Huduma ya wanawake vijana:

Hawa huuunda kikundi chao cha kuchagua kiongozi wao kasha hukaa na kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili na pia hutoka na kuwafikia vijana wa kike wenzao na kushauuriana nao kuhusu changomoto za vijana chini ya uangalizi wa kiongozi wa idara pamoja na mchungaji

Akina Dada kwa ajili ya Kristo:

Hii ni kwa ajili ya kuwapa wasichana mwanya mwa kukutana na kujadili changamoto mbalimbali zinazowakumba wasichana. Hili pia ni kutengeneza mazingira yenye hisia chanya za kuwasaidia wasichana hawa.

 

MAPENDEKEZO YA MIRADI MBALIMBALI:

Maombi ya asubuhi: 

Wanawake hukutana asubuhi, humsikiliza mhubiri na kuomba pamoja.

Mikutano ya hadhara ya wanawake:

Wanawake wameonyesha kuwa wainjilisti wazuri kwa kutumia mbinu mbalimbali. Wakati wengine wanafanya mikutano ya chinichini wengine hufundisha biblia majumbani na wengine kuhubiri.

Mikutano ya wanawake:

Wakati mikutano hii ikipangwa na viongozi wa idara wanawake wanashauriwa kuwaalika wanawake wengine ambao sio waadventista wasabato. Baada ya kupata mahali msemaji mkuu anatafutwa kunakua na washa mbalimbali ambazo zinahusu mada za vitendo na za kiroho pia, kwa mfano namna ya kufundisha biblia “Afya ya mwanamke” utunzaji wa muda, uimbaji upangwe na milo iandaliwe vizuri kuwepo na maombi na ushirika pia.

Siku ya wanawake:

Kuna makanisa yanayofurahia kuacha sabato hiyo iendeshwe na wanawake wakati wengine hawapendi kwa wale wasiopenda hivyo basi wanawake waongozwe program zote za shule ya sabato. Hatimaye mchana baada ya chakula kunaweza kukawa na washa mbalimbali matukio maalum kwa mfano maigizo, nyimbo na kadhalika.

Vyama vya kusoma:

Wawepo wanawake wanaopenda kusoma na kasha wasimulie walicho kisoma wakati wa kujisomea basi kunaweza kukawa na vinywaji, matunda au vitu bya kutafuna katika program hii. Huu ni wakati mzuri wa kujenga urafiki pamoja na ushirika na wanawake wengine maana unapata uzoefu wao.

Utume kwa nyumba za malezi:

Yaweza kuwa malezi ya watoto yatima, wazee au wasiojiweza na wagonjwa. Peleka kadi, maua, sabuni au mahitaji mengine yanayoweza kuwasaidia kulingania na mazingira. Program zingine ziambatane na hizi nyimbo nzuri, miradi ya sanaa mbalimbali pamoja na kujifunza biblia

Malezi ya wazee:

Hii huhusika kuwatembelea wazee kuomba pamoja nao na kufahamu mahitaji yao, ukiweza wasaidie kama haitoshi kuwaalika katika milo mbalimbali majumbani mwetu. Wao ni hazina inayokaribia kutoweka nii huduma itawaongezea mwanga wa maisha ili tuendelee kuwatumia katika ushauri wa mambo mbalimbali.

Wanawake waliojifungua hivi karibuni:

Huduma hii ni kwa ajili ya wanawake waliotoka kujifungua mtoto hivi karibuni, mtoto huyu hukaribisha kwa kupelekewa zawadi hospitalini au nyumbani. Nia ni kuonyesha msada kujali kwa mama huyo ambaye ameongeza majukumu katika malezi

 

SEHEMU YA SITA

SIKU MAALUM IDARA YA HUDUMA ZA WANAWAKE

 1. Juma la kwanza la machi-siku ya kimataifa ya maombi ya wanawake duniani
 2. Juma la pili, juni- siku ya msisitizo wa idara ya huduma za wanawake
 3. Juma la nne Agosti-siku ya msisitizo wa sasa basi ( siku ya kuzuia unyanyasaji)

 

SIKU YA KIMATAIFA YA MAOMBI YA WANAWAKE

Kuanzia mwaka 1990 konferemso kuu ya idara ya huduma za wanawake wameweka siku maalum ambapo wanawake hutiana ngjuvu kwa maombi kwa kujiombea na kuombeana. Wanawake wanaweza kuhubiri na kuwa na program maalumu siku hiyo. Siku hii huwapa wanawake fursa ya kuwafahamu wenzao na kuombeana.  Kumuombea mwanamke kila mahali hutengeneza mfungamano wa kiroho na huruma miongoni mwa wanawake wakiadventista.  Wanaumekwa wanawake wengi hukusanyika pamoja na kuomba.  Wengi waweza kuzidisha siku wakiwa wanaomba na kufunga.  Hili litawasaidia hata watoto wetu  kujenga maisha ya maombi.

SIKU YA MSISITIZO WA IDARA YA HUDUMA ZA WANAWAKE.

Siku hii inawapa fursa wanawake kuongoza program mbalimbli na kulielimisha kanisa juu ya makusudi ya idara ndani ya kanisa.  Baada ya ibada watu wanaweza kula pamoja kukuza ushirika pia program mbalimbali za ibada zaweza kundeshwa.  Siku hii pia kiongozi wa idara anaweza kutambua mchango wa wanawake katika kazi ya Mungu kwa kuwatunuku au kuwapa vyeti kwa sababu ya utendaji wao mbalimbali.  Ubunifu wa kanisa mahalia pia ni mzuri zaidi.

3. SIKU YA KUKATAA UNYANYASAJI.

Siku hii inawapa fursa makanisa kuzungumzia njia mbalimbali za unyanyasaji na kulielimisha kanisa, kiongozi na jamii kwa ujumla.   Hili litasaidia waathirika wa unyanyasaji kutambua kuwa kanisa linawajali.  Kiongozi wa idara wa kanisa afanye kazi kwa karibu sana na mchungaji ili aweze kufanya siku hiyo iwe na mafanikio makubwa.

 

SEHEMU YA SABA.

 

UINJILISTI.

Uinjilisti huchukua nafasi na mifumo mbalimbali.  Katika sehemu hii utakutana na uinjilisti wa mtu mmoja mmoja kupitia kujifunza Biblia, uinjilisti wa vikundi vidogo vidogo, uinjilisti kwa njia ya semina na hatimaye ni umuhimu wa kuwafanya wanafunzi.

MAPENDEKEZO YA NAMANA YA KUFANYA UINJILISTI.

Uinjilisti wa mtu mmoja mmoja:

Mbinu yenye tija ni ile ya kumshuhudia mtu mmoja mmoja kwa kumpa mafundisho ya Biblia.  Yaweza kukuchukulia muda lakini utagundua ni moja wapo ya uzoefu mzuri sana katika uinjilisti.  Nawezaje kumpata mtu wa kujifunza naye Biblia?  Ni katika sehemu za kazi, jamii inayo tuzunguka, rafiki ambaye amekuwa akichunguza maisha yako nakuona kuwa una amani. Uinjilisti wa watu wawili wawili huhusisha kama Yesu alivyowatuma wanafunz wake nah ii ndio njia nzuri ya pekee.  Jinsi ambavyomtu aweza kumshauri mtu mwingine na kujifunza biblia pamoja.

KUJIFUNZA BIBLIA KULIKO NA TIJA.

Kumpa mtu masomo ya Biblia ni njia rahisi kupita zote ya uinjilisti. Hii humfanya msomaji wa biblia kuwa na mfanikio makubwa sana. Siri kubwa katika kujifunza biblia ni maombi. Kabla ya kuanza kumfunidhs mtu ni vizuri ukawa na vitendea kazi mwenyewe kwanza ili uweze kujifunza vyema. Unapaswa kuwa na Biblia, itifaki ya bilbia pamoja na miongozo ya kujifunza biblia. Miongozo ya kujifunza Biblia humsaidia mwanafunzi kulenga katika kile anacho hitaji kujifunza.

-        Panga muda unaofahamika kwa wote.

-       Tunza  muda na kujifunza kwa kadri iwezekanavyo

-       Usiwe na masomo marefu.

-       Usimpe manafunzi nafasi ya kutoa udhuru wa kutotaka kujifunza.

-       Baada ya kujifunza toa wito kisha muombee.

-       Kuza tabia ya kujitoa baada ya kila somo toa wito.

-       Toa ushuhuda wa uzoefu wako kabla ya kukutana na Yesu, na baada ya kukutana na Yesu.

-       Mfanye mwanafunzi aelewe kuwa wote tunamuhitaji Kristo.

 

UTARATIBU WA MAFUNZO YA BIBLIA.

 1.  Fika kwa wakati, mwanafunzi wa biblia awe rafiki yako hivyo chukua muda kidogo ukuze urafiki wenu.
 2. Tambulisha somo na kuomba.  Utangulizi kidogo wa somo lako utamfanya mwanafunzi ajue lengo la somo.  Muwe na ombi la dhati kabisa mkimsihi Roho Mtakatifu awaongoze.
 3. Kujifunza somo kwa njia ya maswali na majibu ni nzuri sana, pia waweza mruhusu mwanafunzi wako asome biblia ili kupata jibu.  Ukifanya hivyo atakua na ujasiri katika kujifunza neno la Mungu pia itampa hamu ya kutaka kujifunza zaidi.  Msibishane juu ya misingi ya Imani mpaka muwe mmesha jifunza pamoja.
 4. KUMBUKA; ni kazi ya Roho Mtakatifu kumfanya mtu afanye aumuzi kwa kile alichojifunza.
 5. Kujitoa na maombi.    Anza na somo  la kwanza kabisa katika kumuandaa kujitoa.  Waweza kumpa ushuhuda binafsi juu ya somo husika lilivyo badilisha maisha yak.
 6. Panga kikao kingine na kuagana.  Ni vyema kutawanyika mara tu baada ya maombi alkini uhakiki kama atawepo kwa ajili ya somo linalofuata.  Hapa pia waweza mualika kanisani au katika mkutano wa injili kama upo.


UINJILISTI WA VIKUNDI VIDOGO VIDOGO

Aina nyinge ya uinjilisti wenye mafanikioa ni kujifunza biblia kupitia vikundi vidogo vidogo, kuna sababu za kutosha zinazofanya ufanikiwe.

 1.  Watu huwa huru kwenye vikundi vidogo vidogo na hujifunza kwa uhuru.
 2. Huweza kufanywa katika eneo lililo karibu na nyumbani
 3. Kikundi kinaweza kuonyesha hali ya kulea na kujali.
 4. Watu wanakuwa na fursa ya kujifunza kwa namna wanavyotaka wao wenyewe.
 5. Kundi dogo laweza kuwa kishawishi endelevu cha kuwafanya kuwa wanafunzi.

 

Lengo kubwa la uinjilisti wa vikundi vidogo vidogo ni kuandaa mazingira ya upendo, kukubalika ambako huchochea kugundua na uhuru wa kuongea juu ya Bibli bila uoga wala kashfa.  Hili litajenga ushirika wa kikristo uliochanya.

 1. C.   UINJILISTI KWA NJIA YA KUTOA SEMINA.

 Njia hii huhusisha majibizano kuliko kama ambavyo ungefanya katika mikutano ya

hadhara.  Kuna njia mbalimbali za kufuata katika aina hii ya uinjilisti.

(a)  Kuwa na mtu unayemuombea naye anakuombea.

(b) Ufafanuzi wa biblia ni wa muhimu.

(c) Waweke wazi wasilizaji wako kwamba lengo lako ni kumuinua Yesu.  Zungumza habari za Yes utu.

Waelekeze kuwa lengo letu ni kujifunza matukio ya siku za mwisho, lakini pia kuwasaidia wajiandae kwa siku hiyo.

 

UINJILISTI WA KUFANYA KAZI KWA PAMOJA.

Usifanye uinjilisti wa semina peke yako, sio busara kufanya hivyo, washirikishe wengine katika kuandaa mada, kuwaandikisha watu.   Kumbuka kujenga uhusiano mzuri na watu wanaokuja.


KUWAFANYA  WANACHAMA WAPYA KUWA WANAFUNZI. 

Katika Mathayo 28, Yesu anatuambia tufanye mambo 4 makubwa.

 1.  Enendeni
 2. Kuwafanya kuwa wanafunzi
 3. Wabatize
 4. Wafundishe kuyashika yale niliyowaamuru.

Kama kanisa tunafanya vizuri katika namba 1-3. Kipengele cha nne baada ya ubatizo hakitendewi kazi kabisa.  Hatuwafundishi vizuri na ndiyo maanda wengi wanarudi nyuma. Kwa kawaida mabadiliko ni magumu sana katika maisha nan di maana watu wanakataa mbadiliko.  Mnapo waita mtahitaji wabadilishe mfumo mzima wa maisha, wabadilishe dini, chakula, marafiki, mavazi n.k. Tunapaswa kuwa wavumilivu watakati haya yote yanafanyiwa kazi na mtu ili kujiunga na kanisa. Moja ya njia za kuwawezesha ni kuwafanya wawe wakristo waliokomaa kiroho. 

KUWAFUNDISHA NA KUWALEA WANAFUNZI WAPYA

Wanapaswa kufundishwa kabla na baada ya ubatizo.

 1.  Madarasa ya ziada juu ya misingi ya kanisa letu ipangwe.
 2. Madarasa maalumu wakati wa shule ya sabato yaandaliwe kwa ajili yao.
 3. Wafundishe namana ya kusoma biblia na kuomba.

Zaidi sana ni vizuri kujifunza nao biblia na kuomba pamoja nao.  Waweze kuchagua mafungu katika Biblia na kujifunza nao.

 

MRADI WA B=U (BIBLIA SAWASAWA NA UBATIZO)

Mradi huu ulianzia Brazilna ukaleta mafanikio makubwa. Ni njia mojawapo nzuri ya kuwapa wanawake fursa za kufanya kazi kwa ajili ya familia zao na rafiki zao kwa ajili ya uinjilisti wa mtu mmojammoja.

MRADI WENYEWE

Kwanza kabisa kuna maombi. Wanawake watauombea mradi huukatika hatua zake za awali kabisa. Pili ni kukaa na mchungaji na wazee wa kanisa na kukubaliana juu ya mradi huu na namna ya kuweza kununua hizo biblia.ikiwezekana tarehe zipangwe mwanzoni kabisa mwa mwaka ili kutoa fursa ya kuweza kuandaa mradi huu vizuri. Waweza kupanga katika siku mojawapo za idara.

Andaa fomu ya kujisajili na kasha utangaze huu mradi. Mradi huu waweza kuhusisha shuhuda mbalimbali, uimbaji,maongezi maalum kuhusu wanawake, habari maalum za huduma za wanawake.na kadhalika kulingana na ubunifu wa kanisa mahalia. Kiongozi wa huduma za wanawake atazungumzia juu ya furaha katika kukujifunza neon la Mungu pamoja na wengine.

Kisha atawaomba vijana kwa wazee wajitoe kuchukua biblia, masomo ya bible na cheti cha ubatizo kwa ajili ya wengine. Wataombwa watafute mtu mmoja wa kujifunza naye biblia,wamwandae kwa ajili ya ubatizo, hatimaye mwishoni mwa mwaka wamuombe ajitoe kwa ajili ya ubatizo. Jina la mtu atakayekubali kujifunza nao biblia liwe ni sehemu ya jina tajwa katika maombi ya jumatano. Kila atakayekubali kuifanya hiyo kazi atasimamiwa na idara ya huduma za wanawake. Biblia hiyo itamilikiwa na Yule anayejifunza mara tu atakapokua amebatizwa. Yoyote atakayeomba ubatizo aelekezwe kwa mchungaji.

NAMNA YA KUHITIMISHA PROGRAM HII

Wanawake washirikishwe katika kuhitimisha program hizi kama walivyofanya zilipokua zikianza. Biblia zipambwe vizuri kabisa ndipo zikabidhiwe kwa aliyebatizwa na kuomba waziinue juu kuonyesha ushindi mkuu. Ikiwezekana picha zipigwe kama kumbukumbu ya kanisa kwa kufanikisha mradi huo. Wale waliokubali kuchukua biblia kwenda kujifunza na watu hao basi wasimame pamoja nao na kupiga picha pamoja nao.

UANAFUNZI UNAANZISHWA.

Baada ya program hii uanafunzi unaanza. Madarasa yaanzishwe kwa ajili ya hawa waliobatizwa .mpango huu uandaliwe ili kuwaandaa hawa waliobatizwa kuwa na uwezo wa kuwafundisha wengine. Hili litafanyika kwa kuweka mkazo kwa kile walichojifunza ili kuwaimarisha. Baada ya program hii sasa mahafali kubwa iandaliwe na watu hawa wapewe vyeti vya kumaliza mafunzo hayo Ndiyo inawezekana kabisa kwa mwanamke kufanya uinjilisti. Ulimwengu unaweza kuonywa pia kupitia juhudi za wanawake katika uinjilisti. Katika maisha yetu yote hebu na tumruhusu roho mtakatifi afanye kazi ndani ya mioyo yetu akiwasha moto wa uhai na kututia nguvu  kuimaliza kazi yake ili kuharakisha kuja kwa Bwana.