Washiriki wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Mtaa wa Magunguli wanajenga nyumba ya mchungaji wao kwa kujitolea. Mtaa wa Magunguli unaotokana na mtaa wa Mgololo umetengwa hivi karibuni baada ya kazi ya Mungu kupanuka katika eneo hilo. Tuwaombee na kuwaunga mkono washiriki hao ili wakamilishe ujenzi huo kwa wakati. Kanisa la Magunguli lipo katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.