Seventh-day Adventist® Church

PASTOR LETTA'S OFFICIAL WEBSITE

Menu

MITHALI

MASWALI YA KUJADILI: MITHALI 2:1-22

  1. Kama wanadamu wangalitafuta hekima na busara kwa bidii kama wanavyotafuta pesa ni mabadiliko gani yangetokea katika maisha yao? Je hekima na busara vyaweza kupatikana kwa mtu ambaye hakwenda shule? Kwa nini Mungu ni mwenye hekima na busara kuliko viumbe wote? (Isaya 40:28; Mithali 3:19; Zaburi 147:5). Unadhani ni masharti gani anayotakiwa mtu kukidhi ili apewe hekima na busara na Mungu? (Yakobo 1:5).
  2. Unadhani dhambi ilipata nafasi kwa viumbe wa Mungu (wanadamu na malaika) kwa sababu ya kukosa hekima na busara? (Ezekieli 28:17). Ilikuwaje mfalme Sulemani aliyejaliwa hekima na Mungu kuhadaiwa na wanawake wa kipigani hadi akamtenda Mungu dhambi? (1 Wafalme 11:3-4). Je kujiona mwenye hekima machoni pako mwenyewe hutokeaje? (Mithali 3:7) Je, hiki ndicho kilichotokea kwa Sulemani?
  3. Kwa nini inadhaniwa wazee ndiyo wenye hekima kuliko vijana? (Ayubu 12:12). Kwa nini kumcha Bwana kunatajwa kuwa chanzo cha hekima? (Ayubu 28:28). Kwa nini sheria ya Bwana huaminika kuwa ina uwezo wa kumtia mtu hekima? (Zaburi 19:7). Je hekima inahitajika ili kumuokoa mtu na malaya mwenye kubembeleza kwa maneno yake?
  4. Je unadhani ni kwa nini Yesu alijaa hekima katika maisha yake (Luka 2:40) Je hekima ilikuwa ya muhimu kwa Yesu ili kufanikisha kazi aliyopewa ya kumkomboa mwanadamu? Kwa nini Kristo anaitwa hekima ya Mungu? (1 Wakorintho 1:17, 30; Unadhani mpango wa kumuokoa mwanadamu umejengwa juu ya hekima?

MASWALI YA KUJADILI: MITHALI 3:1-35

  1. Je, sheria za Mungu zinashikwaje moyoni? Je unatofautishaje sheria ya Mungu inayoshikwa rohoni na ile inayoshikwa kimwili? Kwa nini torati inaitwa ya rohoni? (Warumi 7:14). Je, mtu wa mwilini aweza kuishika sheria ya Mungu au torati iliyo ya asili ya rohoni? Kama sheria imeandikwa moyoni mtu awezaje kuisahau? (Waebrania 8:10).
  2. Je maagizo ya Torati yanatimizwaje kwao wao wafuatao mambo ya rohoni na si mambo ya mwilini? (Warumi 8:4). Je Mungu anaweza kuvunja sheria alizozitunga yeye mwenyewe? Mungu Alipomwagiza Ibrahimu amchinje mwanae Isaka alikuwa anatenda dhambi ya kukusudia kuua? Je ni halali kusema Mungu yupo juu ya sheria?
  3. Biblia inaposema hatupo chini ya sheria inamaanisha nini? Je ukiukwaji wa sheria za Mungu unachangia kuharibu afya ya kiroho na kimwili? Mungu anaheshimiwaje kwa mali zetu na kwa malimbuko ya mazao yetu yote? Je, kutotoa sadaka na kutomrudishia Mungu zaka ni kumvunjia heshima?
  4. Ghala zitakazojazwa kwa wingi kama matokeo ya kutoa zaka na sadaka ni ghala zipi? Je ni ghala za kanisa mahalia, za ngazi za juu za kanisa au za mtoaji mwenyewe? Kama muumini mwenzako ni mhitaji wa daima kwa sababu ya kutotoa zaka na sadaka unapaswa kumsaidia?

MASWALI YA KUJADILI: MITHALI 5:1-23

  1. Je kila uzee huja na busara na hekima? Kwa nini watoto wanapaswa kuwasikiliza wazee na si wazee kuwasikiliza watoto? Kwa nini mfalme Rehoboamu alipokea ushauri wa vijana badala ya ule wa wazee? (1 Wafalme 12:3-17).

MASWALI YA KUJADILI: MITHALI 6:1-35

MASWALI YA KUJADILI: MITHALI 7:1-27

  1. Kwa nini mtu anayenaswa kirahisi na malaya anatambulika kama mjinga au asiye na akili kabisa? (Mithali 6:32). Kwa nini hekima ya Sulemani haikumnusuru katika mtego wa wanawake wa kipagani? (1 Wafalme 11:3-4). Unadhani kosa la huyu kijana mpumbavu ni kupita njia zenye vishawishi au kupita njia hizo nyakati za giza au yote mawili?
  2. Mavazi ya kikahaba aliyovaa mwanamke aliyekutana na kijana mpumbavu yalikuwa na nini hata yakaitwa ya kikahaba? Watu wanaovaa mavazi hayo kwa kawaida wanapatikana wapi? Je mavazi hayo yameanza kuvaliwa kwenye mikusanyiko ya kiroho siku hizi? Je viongozi wa kiroho wametumia juhudi ya kutosha kukemea uvaaji huu wa mavazi ya kikahaba unaokithiri?
  3. Malaya ana sifa ya kutotulia nyumbani na kuwa na werevu wa moyo. Sifa hizi zinamsaidiaje kutimiza malengo yake? Kushika na kubusu kuna madhara gani kwa yule asiyetaka kutumbukia kwenye ngono isiyotarajiwa? Je kijana mpumbavu alikuwa na uwezo wa kukataa kushikwa na kupigwa busu na malaya? Kwa nini hakukataa au hata kukimbia kama alivyofanya Yusufu?
  4. Mwanamke malaya aliyemrubuni kijana mjinga alikuwa mke wa mtu. Kwa nini wake au waume za watu hawatosheki na wenzi wao? Huyu mke wa mtu alikuwa anatafuta nini kwa kijana huyu mdogo? Je vijana wa kiume kuoa watu wazima au watu wazima kuoa mabinti kunatokana na nini?

NILICHOJIFUNZA NA KUGUNDUA MITHALI 12:1-28: 

  1. Kufundishwa ni hatua ya kukubali kuambiwa juu ya ujinga wako. Ni kukubali kuwa ulikuwa mjinga. Ili uelimika ni lazima ukubali kuachana na ujinga uliokuwa nao. Mara nyingi maarifa mapya huchukua nafasi ya maarifa ya awali ambayo hayakuwa sahihi. Ujasiri katika kujifunza unakuja kwa kukubali kukosolewa. Yule asiyekubali kukosolewa hubaki na ujinga wake na hiyo ndiyo sababu ya kufananishwa na wanyama.
  2. Mwenye moyo wa ukaidi hudharauliwa. Ukaidi ni hali ya kujiona unajitosheleza na usiyehitaji msaada wowote. Watu wa aina hii wana tabia ya kujifanyia tathmini ya upendeleo wakijihesabu kuwa ni wakamilifu kuliko wengine. Mtu wa aina hiyo atakosa upendeleo kutoka kwa Mungu kwa kuwa Mungu huwahesabia haki wanaotambua udhaifu wao. Watu wajihesabiao hako uovu wao hautaondolewa kamwe.
  3. Mafanikio ya mtu huja kwa msaada wa mwenzi wake wa maisha na kushindwa kufikia mafanikio kunatoka na uchaguzi mbaya wa mwenzi wa maisha. Maana msaada mkuu wa mwenzi wa maisha ni kupitia ushauri wake. Uzuri wa mume au mke hutokana na akili aliyonayo. Ndoa nyingi zimeharibika kwa kufuata upuuzi na kuendekeza matumizi yasiyo na tija na kuweka jitihada ndogo katika uwekezaji na shughuli za kiuchumi.
  4. Kutafuta kupendwa na kusifiwa na kila mtu ni mtego uliowarudisha nyuma wengine hata wameshindwa kufanikiwa kimaisha. Jambo muhimu maishani ni uwezo wa kumiliki mali. Kama unachokifanya kinakuwezesha kumiliki mali endelea nacho hata kama kinadharauliwa na watu wa jamii yako. Jambo muhimu ni kuwa kisiwe kinyume cha maadili. Mafanikio huja kwa kazi ya mikono na ushauri utokao midomoni mwako. Huna sababu ya kuwaonea wivu waliofanikiwa.
  5. Mtu mwerevu husitiri aibu kwa kuwa makini katika majibu yake na katika kupokea ushauri. Hulipima jambo linaloumiza na kuahirisha hasira yake. Halipatia muda jambo linalotatanisha na hawi tayari kujazwa ubaya na watu wanaomzunguka. Hujizuia kusambaza mambo ya watu wengine ili kuwasitiri na aibu. Mtu atawalaye mdomo wake huku akifanya kwa bidii kazi zake za kujiingizia kipato ana uwezo wa kutawala mausha yake na maisha ya watu wengine. Huyo atabaki mchngamfu daima maana haja jambo la kuusumbua moyo wake. Atakuwa na nafasi ya kufaidi mali zake.

NILICHOGUNDUA NA KUJIFUNZA: MITHALI 13:1-25

  1. Maskini hasikii ogofyo maana hana cha kupoteza. Lakini umaskini siyo fungu alilopangiwa mtu na Mungu. Wanadamu wote wana fursa sawa za kufanikiwa kiuchumi. Kupuuzia ushauri wa wazazi au wazazi kushindwa kuwarithisha watoto ari ya kufanya kazi na kujitegemea ndicho chanzo kikuu cha umaskini wa kipato. Wavivu na wasiojifunza kwa wenzao watakula jeuri yao. Watu wanaoota kuwa na maisha mazuri huku wakikataa kujishughulisha watabaki wakiiga maisha ambayo hawawezi kuyaishi.
  2. Mtu ajifanyaye kuwa maskini na ana mali nyingi ni mtu asiyependa kuishi maisha ya maonyesho na sifa. Kuna watu wenye bidii ya kuelezea mipango mizuri waliyonayo lakini utekelezaji hauendani na maneno yao. Bali wenye hekima hujifunza na kutafuta ushauri kwa waliofanikiwa. Hawana papara ya kutajirika kwa haraka. Wanafanya uwekezaji wa muda mrefu na muda mfupi katika maeneo yenye tija. Waliofanikiwa wana kawaida ya kuifikiria kesho yao. Hofu ya wakati ujao ndiyo inayowasukuma kutenda kazi kwa maarifa.
  3. Waliofanikiwa wanaitumia kila fursa inayopatikana sasa ambayo huko mbele inaweza isiwepo. Wasio na busara hawaihangaikii kesho. Wanadhani watakufa kesho na badala yake wanajikuta wakiishi maisha marefu yenye taabu na yasiyo na heshima. Umaskini na fedheha huwapata wale wapuuzao ushauri unaotolewa na wenzao huku wakikataa kujifunza kwa waliofanikiwa. Wanaendekeza ukaribu na walioshindwa maisha kiuzembe huku wakifarijiana. Hawa hufa bila kuacha urithi wa maana kwa watoto na wajukuu zao.
  4. Lakini mtu mwema apokeaye mashauri na kujifunza kwa waliofanikiwa huwaachia wanawe urithi wa mazoea ya kupenda kazi na mtaji wa maisha. Watoto waliolelewa kimayai huishi maisha ya taabu wazazi wanapofariki. Lakini watoto waliozoezwa kupenda kazi na kujitegemea na kuadhibiwa wanapofanya uzembe hayumbi wazazi wanapofariki. Kuwa maskini au tajiri ni matokeo ya maamuzi tunayoyafanya tangu tukiwa wadogo. Wazazi wanahusika sana.

NILICHOGUNDUA NA KUJIFUNZA: MITHALI 14:1-35

  1. Nyumba huvunjika pale mume anapohisi kudharauliwa na mke asipoonyeshwa kupendwa. Na ugomvi huibuka pale aliyefanyiwa dharau anaposhindwa kutawala hasira zake. Mke ana nafasi kubwa ya kuzuia ugomvi usiibuke au usikue nyumbani mwake kwa kupima athari za maneno anayotumia kumjibu mwenzie (Mithali 15:1). Hadhihirishi hasira yake yote bali hulinda heshima ya mumewe. Mke mpumbavu huona fahari kutangaza aibu za nyumbani mwake. Mke ajuaye kumshika mumewe vizuri ana uhakika wa kudumisha ndoa yake.
  2. Geuza hasira kwa kujibu kwa upole na epuka maneno yaumizayo kwa kuwa yanachochea ghadhabu. Usiruhusu ulimi kutamka kila unachokijua kwa kuwa ukorofi wa ulimi huvunja moyo. Tumia ulimi wako kueneza maarifa na ili uwe na maarifa ni lazima uyatafute maarifa. Mtu hulifurahia jibu la kinywa chake; Na neno linenwalo wakati wa kufaa ni jema kama nini!
  3. Macho ya Mungu yanamchunguza mbaya na mwema ili kuona mahali msaada unapohitajika. Msaada wa Mungu hutolewa kupitia maonyo. Asiyesikia maonyo hata sadaka yake ni chukizo kwa Bwana na mapato hayakai na hayamletei furaha. Lakini Mungu husikia sala ya mwenye haki anayetambua asivyostahili na asivyo na uwezo wa kushinda bila Yesu.
  4. Moyo wenye furaha huuchangamsha uso bali kwa huzuni ya moyo roho hupondeka. Amani ya moyo ni muhimu kuliko kumiliki utajiri. Familia nyingi zilizosambaratika zilisambaratika kwa kukosa amani na si kwa kukosa mali. Chakula cha mboga penye mapendano ni bora kuliko ng'ombe aliyenona pamoja na kuchukiana. Ili kuepusha mafarakano na kudumisha utengamano nyumbani vikao vya mashauriano ni vya muhimu. Mashauri hayo yasiibue ugomvi mpya bali yaongozwe na roho ya upole na unyenyekevu (Wagalatia 6:1) kwa kuwa mashauri mabaya ni chukizo kwa Mungu.
  5. Mwonekano wa nje huakisi kinachoendelea moyoni mwa mtu. Na mtu mwenye amani moyoni huwa na mwonekano wenye kuvutia ufananishwao na habari njema inenepeshayo mifupa. Ishi ili kubariki wengine. Tamaa ya kutaka kujilimbikizia mali isivyo halali imewafanya baadhi ya wasichana kupokea zawadi ambazo baadaye ziligeuka kuwa tanzi kwao. Achukiaye zawadi ataishi bali mwenye kutafuta vya bure ataishia kubaya. Kumbuka kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.

NILICHOGUNDUA NA KUJIFUNZA: MITHALI 16:1-33

  1. Mwanadamu amepewa fursa ya kuandaa mipango ya maisha yake lakini Mungu ana nafasi ya kuipitia mipango hiyo na kuiboresha. Usikurupuke kutekeleza mipango uliyojiwekea bila kumshirikisha Mungu. Mungu amekuandalia jambo bora maishani mwako na anajua wakati na namna atakavyolitekeleza.Mungu ndiye aongozaye hatua za mwanadamu kuelekea kwenye mafanikio yake. Hata hivyo mwanadamu amepewa uhuru wa kuchagua kinachomfaa kati ya mawazo ya Mungu na yake
  2. Ukaidi au kiburi vimemfanya mwanadamu ajidhanie ana mawazo bora kuliko wengine. Wale waliojizoeza kumfanya Mungu kuwa mshauri wao wana hekima na ufahamu mwingi. Aliye na hekima moyoni ataitwa mwenye busara naye hukifundisha kinywa chake cha kusema. Maneno yapendezayo nyumbani ni kama sega la asali. Linatibu roho na mwili na kuepusha magomvi na mafarakano.
  3. Njia za mtu zikimpendeza Mungu, hata adui zake huwapatanisha naye. Aliye rafiki wa Yesu atakuwa rafiki wa watu wote. Ataridhika na kipato kidogo kuliko kudhulumu watu na kisha kusumbuliwa na hatia moyoni. Usifanye urafiki na wadhulumaji na wasiozingatia neno la Mungu maana ni afadhali kuwa pamoja na maskini kuliko kugawana nyara na wenye kiburi.
  4. Hasira ya mfalme ni kama wajumbe wa mauti (pepo wachafu) lakini mtu (mke) mwenye hekima ataituliza. Panahitajika hekima kubwa kuituliza hasira ya mtawala wa familia au taaisi nyingine yoyote. Hekima kama ya Abigaili inahitajika hasa kuwakabili waume kama Nabali na Wafalme wenye hasira kama Daudi (1 Samweli 25:1-44). Hakuna mkate mgumu mbele ya chai.

NILICHOGUNDUA NA KUJIFUNZA: MITHALI 17:1-28

  1. Ndoa ni makubaliano ya hiyari ya kuishi pamoja hata kama afya na uchumi vitayumba. Ndoa yenye upendo wa kweli haiwezi kutetereka kutokana na kuyumba kwa uchumi. Utajiri peke yake hausaidii kuituliza ndoa. Ingekuwa utajiri una msaada kwa wanandoa matajiri wasingeachana. Afadhali mego kavu pamoja na utulivu kuliko nyumba yenye karamu nyingi pamoja na magombano.
  2. Ugumu wa maisha una kawaida ya kukomaza wanandoa pamoja watoto wao. Watoto waliolelewa kwenye maisha magumu hufanya vizuri katika maisha kutokana na kuzoea shuluba. Hawa hupata urithi bora wa tabia ya kupenda kazi na moyo wa kujituma kuliko watoto wa wale waliokuwa wanakaa kwao. Yapokee maisha magumu unayoyapitia ili yakufundishe kuvumilia mambo yatakapokuwa si rafiki.
  3. Kama dhahabu inavyosafishwa kwa moto wa mtakasaji na ndivyo Mungu anavyojaribu mioyo kupitia kipindi cha maisha magumu. Mungu ana mpango wa kumuinua maskini kwa majira yake. Usiongeze uchungu wa maisha anayopitia kwa kumcheka au kumdhihaki Mungu wake hafurahii. Wazazi na hasa baba analo jukumu kubwa kuwanasua watoto wake wasitumbukie kwenye umaskini wa kupitiliza. Mzazi bora ni yule anayewafikiria watoto wa wanawe (wajukuu) watakavyokuwa pale yeye atakapokuwa hana nguvu za kusaidia.
  4. Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee. Kila mtoto ajaye duniani huja na uwezo wa kumsaidia kukabili changamoto za maisha na kumwingizia kipato halali. Wajibu wa mzazi ni kutambua na kuendeleza uwezo au vipawa hivyo badala ya kumlazimisha kufanya kazi asiyoipenda. Mtoto anayechagua masomo asiyoyamudu au kazi asizoziweza kutokana na shinikizo la wenzake asidiwe hata ikibidi kwa ukali ili afanye kitakachomsaidia maishani. Mtoto hana uzoefu wa kutosha kumwezesha kufanya maamuzi sahihi kama wazazi.
  5. Wazazi wasinaswe kwenye mtego wa kuwapendelea watoto wao maana hiyo huharibu tabia zao na tabia na za wale wengine wasiopendelewa. Kumbuka upendeleo wa Yakobo kwa Yusufu ulivyoleta vita nyumbani kwake. Majirani na waalimu wanapokosoa tabia ya wanao wasikilize na ushirikiane nao. Chanzo cha magomvi nyumbani ni roho ya kulipiza kisasi. Yeye arudishaye mabaya badala ya mema, mabaya hayataondoka nyumbani mwake. Hakuna faida ya kudumisha mashindano nyumbani.
  6. Kunyamaza wakati mgogoro wa maneno unapozuka husaidia kuepusha magomvi. Hata mpumbavu akinyamaza huhesabiwa hekima na mwenye roho ya utulivu ana busara. Kauli tata ndizo zinazozua vita ndogo na kubwa duniani. Kupenda ugomvi ni kupenda dhambi. Jizoeze kuwapenda hata wanaokuudhi. Kumbuka moyo uliochangamka ni dawa nzuri, bali roho (akili) iliyopondeka (yenye msongo) huikausha mifupa (hupunguza kinga ya mwili).

NILICHOGUNDUA NA KUJIFUNZA: MITHALI 18:1-24

MASWALI YA KUJADILI: MITHALI 21:31 

MASWALI YA KUJADILI: MITHALI 22:1-29

  1. Wajenzi wa mnara wa Babeli walitaka kujifanyia jina ikawa machukizo machoni pa Mungu (Mwanzo 11:4-8). Lakini tunashauriwa kuchagua jina jema lenye sifa njema kama lilivyo Jina la Yesu (Matendo 4:12). Jina jema huja kwa kutenda jambo linalobariki watu, linalogusa maisha ya watu, na litakaloacha alama ya kudumu hata baada ya kuondoka. Kujijengea jina zuri huja kwa kumcha Mungu na kuzingatia mashauri yake. Kwa kuzingatia ushauri wa Mungu mtu huweza kuwa mwadilifu na Mwenye uchumi nzuri. Mcha Mungu na Mwenye uchumi nzuri atafanya mengi na makubwa kuinua hali ya wanyonge na maskini.
  2. Mtu muadilifu hutengenezwa na jamii na malezi ya awali ya mtoto ndiyo yanayomuandaa kuishi maisha ya mafanikio hapo baadaye. Mtoto asilelewe kwa kudekezwa bali kwa kuelekezwa. Na kuelekezwa kuandamane na adhabu ndogo ndogo kumsaidia kukumbuka kilicho sahihi na kisicho sahihi maishani. Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto, lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.
  3. Uvivu ni janga na chanzo kikuu cha umaskini wa kipato. Wavivu wote duniani wanafanana. Wanajua kujenga hoja za kwa nini hawajitumi. Lakini sababu yao ya msingi ni kuwa hawataki kiitesa mwili. Wanaamini mahitaji yao watayapata kwa njia ya mkato isiyohitaji kuumia. Na matokeo yake hujikuta wakiwa wahitaji na wakopaji. Lakini mwenye bidii katika kazi yake husimama mbele ya wafalme. Na tajiri humtawala maskini na mkopaji ni mtumwa wa yule akopeshaye. Jiepushe na uvivu.
  4. Jiepushe kufanya urafiki na malaya, mwenye hasira, mvivu, au kuwa mdhamini wa madeni ya watu. Bali ujiweke karibu na wenye hekima wala usijaribiwe kudhulumu mali za watu. Tosheka na pato la jasho lako. Na katika mali ulizojaliwa usiwasahau wahitaji maana mwenye jicho la ukarimu atabarikiwa. Magomvi huleta umaskini. Kiini cha magomvi katika familia na katika jamii ni dharau. Mtupe au jiepushe na mwenye dharau na ugomvi utakoma.

MASWALI YA KUJADILI: MITHALI 23:1-35

  1. Mali hujifanyia mabawa kama tai arukaye hivyo usizitegemee akili zako mwenyewe kupata mali. Usitafute mali kwa kuingia katika mashamba ya yatima wala kwa kuondoa alama ya mipaka ya zamani. Kwa sababumtetezi wao atawatetea juu yako. Wala usiwaonee wivu waliofanikiwa au kujipendekeza kwao maana hujui wanachokuwazia. Msikilize baba yako aliyekuzaa wala usimdharau mama yako akiwa mzee.
  2. Mkabidhi Mungu moyo wako ili autawale na kuuongoza usije ukanaswa na wenye mazoea ya dhambi. Mungu atakuepusha na mitego ya malaya na kukutia umaskini. Mungu aweza kukuepusha pia na ulevi uwatiao watu hasara ya mali na kuwaachia ulemavu na makovu. Uwezo wa mlevi kutafsiri ayaonayo hupungua na hivyo kujikuta akifanya maamuzi yamleteayo majuto na kuonekana kituko katika jamii. Macho ya mlevi huona mambo mageni hata akiumizwa hasikii maumivu kwa kuwa hisia zake zimeuliwa na nguvu ya pombe. Pombe ni chanzo cha uovu wa kila aina.
  3. Inunue kweli wala usiiuze. Watu huiuza kweli kwa kipande cha mkate kwa kuwa mwenye njaa ana kawaida ya kutosimamia hekima, mafundisgo, na ufahamu. Tumeshuhudia wengi wakienda kinyume na misimamo yao ya awali katika ndoa, katika imani, na katika jamii kwa ajili ya kutafuta maslahi ya kitambo. Hao wameuza kweli. Hata kunyamaza wakati dhuluma ikitendeka ni kuuza kweli.
  4. Adhabu ya fimbo kwa watoto ina umuhimu wake. Mtoto asiyeadhibiwa amenyimwa haki yake maana asiyefunzwa na kiboko atafunzwa na maisha. Uchapaji wa fimbo kwa watoto ni lazima uwe na kanuni na usimamiwe ili mtoto asiadhibiwe kupita kiasi. Watoto wasioadhibiwa wanapokosa wamekuwa mzigo kwa familia, kwa jamii, na kwa taifa husika. Tusifike huko.

MASWALI YA KUJADILI: MITHALI 24:1-34

MASWALI YA KUJADILI: MITHALI 25:1-28

  1. Kwa nini ni utukufu kwa Mungu kuficha jambo? Unadhani mambo ambayo Mungu ametuficha yalikuwa na umuhimu kwetu? Je yule tuliyofichwa tuna wajibu wa kuyachunguza Ili tuyajue? Je kufichwa jambo kuna uhusiano na uwezo wetu mdogo wa kulipokea hilo jambo? Ni sahihi kumficha mtu taarifa za kifo cha mgonjwa ukisubiri wakati muafaka wa kumjulisha jambo hilo? Je hiyo haiwezi kuwa uongo na dhambi?
  2. Kwa nini watu huwa hawasubiri kuambiwa njoo huku mbele badala yake hulazimisha nafasi zisizo zao? Kwa nini kujitukuza mbele ya mfalme ni jambo lisilofaa? Je kuwanyenyekea wakuu ni kujipendekeza au ni wajibu? Kufunua siri ya mtu mwingine kuna ubaya gani? Je ikiwa hiyo siri yaweza kumletea madhara au kuwaletea madhara watu wengine haistahili kufunuliwa?
  3. Je neno linenwalo wakati wa kufaa huitwaje kwa jina moja? Kwa nini neno hilo limelinganishwa na machungwa katika vyano vya fedha? Mwonyaji mwenye hekima anatofautianaje na mwonyaji asiye na hekima? Kwa nini huonekana kama kipuli Cha dhahabu na pambo la dhahabu safi kwa sikio lisikialo? Je maneno ya hekima ni sawa na ulimi laini unaovunja mfupa?
  4. Kwa nini inashauriwa mguu wako kuingia kwa jirani yako kwa kiasi? Kuna ubaya gani kuzoea sana nyumbani kwa jirani yako? Au ndiyo maana amesema asali pamoja na uzuri wake inatakiwa kuliwa kwa kiasi? Kwa nini adui yako akiwa na njaa unashauriwa kumpa chakula ili aishi? Kwa nini kumsaidia adui kunalinganishwa na kumtilia makaa ya moto kichwani pake?
  5. Kwa nini habari njema imefananishwa na maji ya baridi kwa mtu mwenye kiu? Kwa nini wahubiri wa injili hupendelea kuongelea habari mbaya kuliko habari njema? Ujumbe wa malaika yule wa tatu unazungumzia habari njema au habari mbaya? (Ufunuo 14:6-7).

MASWALI YA KUJADILI: MITHALI 27:1-27

  1. Kwa nini kujisifu kunaonekana kuwa kosa? Kuna utofauti gani kati ya kujisifu na kusifiwa? Kwa nini kusifiwa kunaonekana kuwa nafuu kuliko kujisifu? Ni nani aliye katika hatari ya kujisifu kati ya mwenye sifa njema na mwenye sifa mbaya? Ikiwa watu hawakusifu kwa sababu ya chuki, wivu, au kwa sababu hawayajui mema yako naweza kuanza kujisifu mwenyewe? Je naweza kuweka mipango ya kesho hali ya kuwa sijui yatakaayotokea kesho?
  2. Mtu mwenye tabia ya kupenda kusifiwa angependa kuwa na marafiki wanaomkosoa? Ikiwa rafiki yako hapendi kukosolewa utafanyaje ili kudumisha urafiki wenu? Unatofautishaje ukosoaji wa kweli na ule unaotokana na wivu? Kwa nini jeraha utiwazo na rafiki zako ni bora kuliko busu za uongo? Kwa nini kwa kawaida binadamu hapendi kukosolewa? Kwa nini kuyaona mabaya na kujificha huchukuliwa kuwa ni busara? Je kulaumiwa ni njia nyingine ya kukutahadharisha kuwa huko uendako si salama?
  3. Kwa nini jirani aliye karibu ni bora kuliko ndugu aliye mbali? Je kuna rafiki apendaye kuliko ndugu? Kwa nini ndugu wakikaa pamoja wana kawaida ya kugombana? Je mwenzie wa maisha ni ndugu, ni rafiki, au ni vyote? Kama magomvi kati yako na mwenzie wako wa maisha hayakomi ni hatua gani stahiki inapaswa kuchukuliwa? Je kuna uwezekano wa watu wanaogombana kuweza kupatana? Je kuna wakati suluhisho la watu wanaogombana huwa ni kuachana? Mtu huunoaje uso wa rafiki yake? Je kuna wakati wanandoa waliokaa pamoja huanza kufanana mioyo kama uso ufananavyo na uso katika maji?
  4. Nani mwenye wajibu wa kujua hali ya makundi yake kwenye familia na kwenye jumuiya ya kidini? Je makundi yanayotajwa hapa yanahusu mifugo tu au hata watu? Je wajibu wa kuitunza familia na kuipatia mahitaji yake ni ya nani? Je ni sahihi kumlaumu baba kwa kushindwa kuitunza familia yake? Kuna matokeo gani kwa mke na watoto waliokosa matunzo kwenye familia? Nani wa kulaumiwa ikiwa ng'ombe au mbuzi hatoia maziwa ya kutosha kwa kukosa majani? Je mkubwa naye anahitaji kuhudumiwa ili atoe huduma inayotarajiwa kwa usahihi?

MASWALI YA KUJADILI: MITHALI 28:1-28

  1. Kwa nini waovu hukimbia hata wasipofuatiwa na mtu? Je kuwa na hatia moyoni humfanya mtu asijihisi salama? (Zaburi 38:1-4). Kwa nini wenye haki ni wajasiri kama Simba? (Warumi 8:14-15). Kuna uhusiano gani kati ya kumtumainia Yesu na ujasiri waupatao wenye haki? Je mtu ajihesabiaye haki ni mwenye haki? Kwa nini kuiacha sheria kunafananishwa na kuutukuza uovu? Sheria ina mchango gani katika kuwabaini waovu? Ni kwa namna gani waishikao sheria hushindana na waovu? Kwa nini Shetani anawapiga vita waishikao sheria ya Mungu? (Ufunuo 12:17). Je, hukumu ya Mungu itahusisha sheria yake? (Mhubiri 12:13-14)
  2. Kwa nini sala ya mtu asiyesikiliza sheria (asiyeitii kwa makusudi) huwa chukizo kwa Mungu? Je kutoitii sheria huchochea wengine kutoitii pia? Je unapowafundisha watu kutoshika sheria unashiriki dhambi zao? Kwa nini ushindi wa wenye haki huleta utukufu? Ni nani hupata utukufu wenye haki washindapo? Kwa nini mkuu asiye na akili huwaonea watu sana? Je moja ya sifa ya kiongozi ni kuwa na akili? Unapima nini ili kujua kama mtu ana akili? Je viongozi wanahusika katika kupendelea watu? Je wanaojipendekeza kwa viongozi wanafanya hivyo kwa ajili ya kujipatia kipande cha mkate?
  3. Je kulima shamba ni njia ya kutokomeza umaskini? Umaskini aupatao mtu asiyelima shamba lake kwa nini uitwe umaskini wa kumtosha? Mambo ya upuuzi yasababishayo watu kutojiingiza kwenye shughuli za kiuchumi ni yapi? Je utajiri huja kwa mtu kuwa mwaminifu? Ni adhabu gani aipatayo mtu afanyaye haraka kuwa tajiri? Je ni sahihi kutegemea mali ya baba na mama bila wewe mwenyewe kujishughulisha? Hatari ya mali ya kurithi ni nini?
  4. Kwa nini wasio haki waangamiapo, wenye haki huongezeka? Kwa nini kujitumainia moyo kunaonekana kuwa ni ujinga? Kwa nini Mtawala ajitumainiaye mwenyewe analinganishwa na simba angurumaye na dubu mwenye njaa? Kwa nini kuficha dhambi siyo jambo lenye mafanikio? Je kuungama na kuacha dhambi kunampaje mtu rehema? Kwa nini watawala waliomwaga damu za watu huwa na mwelekeo wa kukitafuta kifo?

MASWALI YA KUJADILI: MITHALI 29:1-27

  1. Kwa nini kukaidi kunaitwa kushupaza shingo? Kwa nini kuvunjika au madhara hutokea ghafla kwa anayeshupaza shingo? Maonyo yanatakiwa yafanyike mara ngapi ili isionekane kuwa umeshupaza shingo? Kwa nini kushikamana na makahaba kunapelekea kutapanya mali? Mtawala asiyepokea rushwa huithibitishaje nchi kwa hukumu? Mtawala asiyejihusisha na madai ya maskini anapungukiwa na nini?
  2. Kujipendekeza kwa jirani kunatandikaje wavu wa kuitega miguu yako? Je, dharau huwezaje kuwasha mji moto? Kiongozi anayedharau anaowaongoza hupata changamoto gani katika kuwaongoza hao watu? Kwa nini mwenye hekima hufanikiwa anapojadiliana na wapumbavu? Yupi ni mwenye hekima kati ya yule anayedhihirisha hasira yake yote na yule anayeizuia na kuituliza?
  3. Kwa nini mtawala hapaswi kusikiliza umbeya au uwongo? Ni wakati gani ambapo maskini na mdhalimu hukutana pamoja? Fimbo zikienda sambamba na maonyo huwezaje kumtia mtu hekima? Je fimbo kwa mtoto zinatakiwa kukoma akifikia umri gani? Au achapwe hadi atakapokuwa mzee? Unaionaje sera ya kutowachapa watoto viboko inasaidia kuwaimarisha au inawabomoa?
  4. Watoto waliozoezwa viboko na waliozoezwa kuonywa kwa lugha ya kiungwana ni wepi wenye mwelekeo wa kuzimudu changamoto za maisha? Kwa nini mtoto aliyeachiwa (aliyedekezwa) humwaibisha mamaye na si babaye? Kwa nini pasipo maono watu huacha kujizuia? Je maono hapo anamaanisha sheria? Kwa nini mtu mwenye hamaki katika maneno hafai kutumainiwa? Kuna mtego gani katika kuwaogopa (kuwaabudu) wanadamu.

MASWALI YA KUJADILI: MITHALI 3:1-35

  1. Je, sheria za Mungu zinashikwaje moyoni? Je unatofautishaje sheria ya Mungu inayoshikwa rohoni na ile inayoshikwa kimwili? Kwa nini torati inaitwa ya rohoni? (Warumi 7:14). Je, mtu wa mwilini aweza kuishika sheria ya Mungu au torati iliyo ya asili ya rohoni? Kama sheria imeandikwa moyoni mtu awezaje kuisahau? (Waebrania 8:10).
  2. Je maagizo ya Torati yanatimizwaje kwao wao wafuatao mambo ya rohoni na si mambo ya mwilini? (Warumi 8:4). Je Mungu anaweza kuvunja sheria alizozitunga yeye mwenyewe? Mungu Alipomwagiza Ibrahimu amchinje mwanae Isaka alikuwa anatenda dhambi ya kukusudia kuua? Je ni halali kusema Mungu yupo juu ya sheria?
  3. Biblia inaposema hatupo chini ya sheria inamaanisha nini? Je ukiukwaji wa sheria za Mungu unachangia kuharibu afya ya kiroho na kimwili? Mungu anaheshimiwaje kwa mali zetu na kwa malimbuko ya mazao yetu yote? Je, kutotoa sadaka na kutomrudishia Mungu zaka ni kumvunjia heshima?
  4. Ghala zitakazojazwa kwa wingi kama matokeo ya kutoa zaka na sadaka ni ghala zipi? Je ni ghala za kanisa mahalia, za ngazi za juu za kanisa au za mtoaji mwenyewe? Kama muumini mwenzako ni mhitaji wa daima kwa sababu ya kutotoa zaka na sadaka unapaswa kumsaidia?

MASWALI YA KUADILI: MITHALI 5:1-23

  1. Je kila uzee huja na busara na hekima? Kwa nini watoto wanapaswa kuwasikiliza wazee na si wazee kuwasikiliza watoto? Kwa nini mfalme Rehoboamu alipokea ushauri wa vijana badala ya ule wa wazee? (1 Wafalme 12:3-17).

MASWALI YA KUJADILI: MITHALI 7:1-27

  1. Kwa nini mtu anayenaswa kirahisi na malaya anatambulika kama mjinga au asiye na akili kabisa? (Mithali 6:32). Kwa nini hekima ya Sulemani haikumnusuru katika mtego wa wanawake wa kipagani? (1 Wafalme 11:3-4). Unadhani kosa la huyu kijana mpumbavu ni kupita njia zenye vishawishi au kupita njia hizo nyakati za giza au yote mawili?
  2. Mavazi ya kikahaba aliyovaa mwanamke aliyekutana na kijana mpumbavu yalikuwa na nini hata yakaitwa ya kikahaba? Watu wanaovaa mavazi hayo kwa kawaida wanapatikana wapi? Je mavazi hayo yameanza kuvaliwa kwenye mikusanyiko ya kiroho siku hizi? Je viongozi wa kiroho wametumia juhudi ya kutosha kukemea uvaaji huu wa mavazi ya kikahaba unaokithiri?
  3. Malaya ana sifa ya kutotulia nyumbani na kuwa na werevu wa moyo. Sifa hizi zinamsaidiaje kutimiza malengo yake? Kushika na kubusu kuna madhara gani kwa yule asiyetaka kutumbukia kwenye ngono isiyotarajiwa? Je kijana mpumbavu alikuwa na uwezo wa kukataa kushikwa na kupigwa busu na malaya? Kwa nini hakukataa au hata kukimbia kama alivyofanya Yusufu?
  4. Mwanamke malaya aliyemrubuni kijana mjinga alikuwa mke wa mtu. Kwa nini wake au waume za watu hawatosheki na wenzi wao? Huyu mke wa mtu alikuwa anatafuta nini kwa kijana huyu mdogo? Je vijana wa kiume kuoa watu wazima au watu wazima kuoa mabinti kunatokana na nini?

NILICHOJIFUNZA NA KUGUNDUA MITHALI 12:1-28:

  1. Kufundishwa ni hatua ya kukubali kuambiwa juu ya ujinga wako. Ni kukubali kuwa ulikuwa mjinga. Ili uelimika ni lazima ukubali kuachana na ujinga uliokuwa nao. Mara nyingi maarifa mapya huchukua nafasi ya maarifa ya awali ambayo hayakuwa sahihi. Ujasiri katika kujifunza unakuja kwa kukubali kukosolewa. Yule asiyekubali kukosolewa hubaki na ujinga wake na hiyo ndiyo sababu ya kufananishwa na wanyama.
  2. Mwenye moyo wa ukaidi hudharauliwa. Ukaidi ni hali ya kujiona unajitosheleza na usiyehitaji msaada wowote. Watu wa aina hii wana tabia ya kujifanyia tathmini ya upendeleo wakijihesabu kuwa ni wakamilifu kuliko wengine. Mtu wa aina hiyo atakosa upendeleo kutoka kwa Mungu kwa kuwa Mungu huwahesabia haki wanaotambua udhaifu wao. Watu wajihesabiao hako uovu wao hautaondolewa kamwe.
  3. Mafanikio ya mtu huja kwa msaada wa mwenzi wake wa maisha na kushindwa kufikia mafanikio kunatoka na uchaguzi mbaya wa mwenzi wa maisha. Maana msaada mkuu wa mwenzi wa maisha ni kupitia ushauri wake. Uzuri wa mume au mke hutokana na akili aliyonayo. Ndoa nyingi zimeharibika kwa kufuata upuuzi na kuendekeza matumizi yasiyo na tija na kuweka jitihada ndogo katika uwekezaji na shughuli za kiuchumi.
  4. Kutafuta kupendwa na kusifiwa na kila mtu ni mtego uliowarudisha nyuma wengine hata wameshindwa kufanikiwa kimaisha. Jambo muhimu maishani ni uwezo wa kumiliki mali. Kama unachokifanya kinakuwezesha kumiliki mali endelea nacho hata kama kinadharauliwa na watu wa jamii yako. Jambo muhimu ni kuwa kisiwe kinyume cha maadili. Mafanikio huja kwa kazi ya mikono na ushauri utokao midomoni mwako. Huna sababu ya kuwaonea wivu waliofanikiwa.
  5. Mtu mwerevu husitiri aibu kwa kuwa makini katika majibu yake na katika kupokea ushauri. Hulipima jambo linaloumiza na kuahirisha hasira yake. Halipatia muda jambo linalotatanisha na hawi tayari kujazwa ubaya na watu wanaomzunguka. Hujizuia kusambaza mambo ya watu wengine ili kuwasitiri na aibu. Mtu atawalaye mdomo wake huku akifanya kwa bidii kazi zake za kujiingizia kipato ana uwezo wa kutawala mausha yake na maisha ya watu wengine. Huyo atabaki mchngamfu daima maana haja jambo la kuusumbua moyo wake. Atakuwa na nafasi ya kufaidi mali zake.

NILICHOGUNDUA NA KUJIFUNZA: MITHALI 13:1-25

  1. Maskini hasikii ogofyo maana hana cha kupoteza. Lakini umaskini siyo fungu alilopangiwa mtu na Mungu. Wanadamu wote wana fursa sawa za kufanikiwa kiuchumi. Kupuuzia ushauri wa wazazi au wazazi kushindwa kuwarithisha watoto ari ya kufanya kazi na kujitegemea ndicho chanzo kikuu cha umaskini wa kipato. Wavivu na wasiojifunza kwa wenzao watakula jeuri yao. Watu wanaoota kuwa na maisha mazuri huku wakikataa kujishughulisha watabaki wakiiga maisha ambayo hawawezi kuyaishi.
  2. Mtu ajifanyaye kuwa maskini na ana mali nyingi ni mtu asiyependa kuishi maisha ya maonyesho na sifa. Kuna watu wenye bidii ya kuelezea mipango mizuri waliyonayo lakini utekelezaji hauendani na maneno yao. Bali wenye hekima hujifunza na kutafuta ushauri kwa waliofanikiwa. Hawana papara ya kutajirika kwa haraka. Wanafanya uwekezaji wa muda mrefu na muda mfupi katika maeneo yenye tija. Waliofanikiwa wana kawaida ya kuifikiria kesho yao. Hofu ya wakati ujao ndiyo inayowasukuma kutenda kazi kwa maarifa.
  3. Waliofanikiwq wanaitumia kila fursa inayopatikana sasa ambayo huko mbele inaweza isiwepo. Wasio na busara hawaihangaikii kesho. Wanadhani watakufa kesho na badala yake wanajikuta wakiishi maisha marefu yenye taabu na yasiyo na heshima. Umaskini na fedheha huwapata wale wapuuzao ushauri unaotolewa na wenzao huku wakikataa kujifunza kwa waliofanikiwa. Wanaendekeza ukaribu na walioshindwa maisha kiuzembe huku wakifarijiana. Hawa hufa bila kuacha urithi wa maana kwa watoto na wajukuu zao.
  4. Lakini mtu mwema apokeaye mashauri na kujifunza kwa waliofanikiwa huwaachia wanawe urithi wa mazoea ya kupenda kazi na mtaji wa maisha. Watoto waliolelewa kimayai huishi maisha ya taabu wazazi wanapofariki. Lakini watoto waliozoezwa kupenda kazi na kujitegemea na kuadhibiwa wanapofanya uzembe hawayumbi wazazi wanapofariki. Kuwa maskini au tajiri ni matokeo ya maamuzi tunayoyafanya tangu tukiwa wadogo. Wazazi wanahusika sana.

NILICHOGUNDUA NA KUJIFUNZA: MITHALI 14:1-35

  1. Nyumba huvunjika pale mume anapohisi kudharauliwa na mke asipoonyeshwa kupendwa. Na ugomvi huibuka pale aliyefanyiwa dharau anaposhindwa kutawala hasira zake. Mke ana nafasi kubwa ya kuzuia ugomvi usiibuke au usikue nyumbani mwake kwa kupima athari za maneno anayotumia kumjibu mwenzie (Mithali 15:1). Hadhihirishi hasira yake yote bali hulinda heshima ya mumewe. Mke mpumbavu huona fahari kutangaza aibu za nyumbani mwake. Mke ajuaye kumshika mumewe vizuri ana uhakika wa kudumisha ndoa yake.

MASWALI YA KUJADILI: MITHALI 14:1-35