Seventh-day Adventist® Church

PASTOR LETTA'S OFFICIAL WEBSITE

Menu

MGOGORO WAREJESHWA KWENYE MAZUNGUMZO

JAJI ASHAURI KURUDI KWENYE MAZUNGUMZO

Baada ya kesi ya waliovamia Shule ya Sekondari Ndembela kutajwa kwa mara ya kwanza kwenye Mahakama Kuu ya Kanda mjini Mbeya ilikofunguliwa, Jaji anayesikiliza kesi hiyo Mheshimiwa Chocha alipendekeza wamiliki wa shule ambao ni Kanisa la Waadventista Wasabato kwa upande mmoja na Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe na sehemu ya wanakijiji wa Ndembela kurudi kwenye meza ya mazungumzo ili kutafuta muafaka kwa kuwa jambo lenyewe linazungumzika. Jaji alitoa pendekezo hilo baada ya kuagiza kuwa shule iendelee kutoa elimu kama ilivyokuwa inafanya na kuwa wanafunzi waliokuwa likizo wapokelewe wanapokuja kwa muhula mwingine, na ya kuwa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe ione namna ya kuwapatia wamiliki wa shule, vifaa walivyochukua ili kuwezesha huduma shuleni hapo kuendelea kama kawaida.

Jaji alipendekeza Tume ya watu kumi iundwe yenye watu watano kutoka kila upande na wakutane mapema shuleni Ndembela ili kupendekeza msuluhishi atakayekubalika na kila upande, na kisha kuratibu mapaendekezo yatakayotolewa na kila upande yatakayokuwa hadidu za rejea za kamati. Jaji aliagiza kwamba, Kamati hiyo itapaswa kufikisha kwake mapendekezo watakayofikia kabla ya tarehe 18/09/2003, siku ambayo, kesi ya msingi itakapotajwa tena. Katika siku hiyo watuhumiwa wote 23 watatakiwa kuja mahakamani kujibu mashtaka yaliyofunguliwa, na aliwapa siku 21 kuanzia siku kesi ilipotajwa kuwa wameandika hoja zao zinazojibu mashtaka waliyofunguliwa nayo.

Hadi wakati huo Kamati hiyo imekutana mara mbili na kuratibu mapaendekezo ya kila upande lakini imeshindwa kufikia maafikiano jambo lililosababisha kumuomba msuluhishi aliyependekezwa na kila upande Mheshimiwa mkuu wa Mkoa Ndugu Abbasi Kandoro, (ambaye wakati akipelekewa ombi hili alikuwa likizo) kuwakutanisha wajumbe na kuanza mazungumzo kama Jaji alivyoagiza. Wakati hayo yakiendelea sehemu kubwa ya Waadventista Wasabato wanaamini kuwa tendo hilo la uvamizi ni la uonevu lisilostahili kutendwa na watu waliopewa dhamana ya uongozi kwa kuwa halikuzingatia utawala wa sheria na ya kuwa lina harufu ya udini ndani yake.

Privileges

Everyone