MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 2:1-23
- Hawa Mamajusi wa Mshariki waliokuja kumwabudu Yesu walikuwa nani? Kwa nini wao ndiyo waliojulishwa kuzaliwa kwa Yesu na si viongozi wa Wayahudi? Walijuaje kuwa Yesu ni mfalme wa Wayahudi? Kwa nini taarifa ya kuzaliwa kwa Yesu ilimfadhaisha Herode? Kwa nini wakuu wa makuhani na waandishi walijua kuwa Yesu angezaliwa lakini wakati wa kuzaliwa kwake uliwapiga chenga?
- Kwa nini Herode aliwaita Mamajusi faraghani na kwa nini aliwaagiza waje kumpasha habari za mtoto wakati wa kurudi kwao? Kwa nini walienda kumuona mtoto wakiwa na zawadi? Kama Yesu ni zawadi ya wanadamu je, wanadamu wana haja ya kumpelekea zawadi? Kwa nini Mungu waliwaonya Mamajusi wasimrudie Herode katika kurudi kwao? Kwa nini habari njema zaweza kuwa habari mbaya kwa wengine?
- Kwa nini Misri palionekana kuwa kimbilio salama la mtoto Yesu? Je Afrika ilistahili kupata upendeleo wa Mungu kutokana na kumhifadhi Yesu alipokuwa akitafutwa kuuawa?Kwa nini hasira ya Herode ilikuwa kwa watoto na si kwa Mamajusi waliomdhihaki? Kwa nini Mungu aliruhusu watoto wasio na hatia wauawe na Herode?Kwa nini Mungu anamwagiza Yusufu amchukue mtoto na mama yake ili waende Israeli hali akijua huyo mtoto si wake?
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 3:1-17
- Yohana Mbatizaji alijuaje kuwa ufalme wa mbinguni umekuja? Je ilikuwa lazima Yohana Mbatizaji avae vazi la singa za ngamia na kula nzige na asali? Je Yesu anapokuja mara ya pili watakuwepo watu wenye sifa za Yohana Mbatizaji watakaoandaa ujio wake? Yohana Mbatizaji alipewa na nani mamlaka ya kubatiza watu?Ubatizo wa Yohana ulikuwa wa kunyunyizwa maji kichwani au wa kuzamishwa majini?
- Kwa nini Mafarisayo na Masadukayo walioujia ubatizo Yohana aliwaita wazao wa nyoka? Mazao yapasayo toba waliyotakiwa kuzaa ni yapi? Mungu anawezaje kumwinulia Ibrahimu watoto kutoka kwenye mawe? Aliyetabiriwa kuja kubatiza watu kwa Roho Mtakatifu ni nani? Kwa nini ni lazima watu wabatizwe kwa Roho Mtakatifu? Kipi sahihi kati ya kubatizwa kwa Roho Mtakatifu, kubatizwa kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu, na kubaizwa kwa jina la Yesu Kristo? (Mathayo 28:19-20, Matendo 10:48)
- Kama Yesu alikuwa na nguvu kuliko Yohana Mbatizaji ilikuwaje Yohana aliweza kumbatiza? Makapi yatakayoteketezwa kwa moto usiozimika ni nini? Je Yesu alikidhi sifa za kubatizwa? Kwa nini alibatizwa? Je mtu anayetaka kubatizwa anaweza kuzuiwa? Yesu alikuwa anataka kutimiza haki gani alipomsihi Yohana ambatize? Je, kuna nyakati za kulikubali jambo hata kama hulielewi kwa matarajio kuwa utalielewa hapo baadaye?
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 4:1-25
- Je kujaribiwa na Shetani kulikuwa kwa lazima katika maisha ya Yesu? Kwa nini ilibidi Yesu apandishwe na Roho Mtakatifu katika kujaribiwa kwake? Kufunga kwa siku arobaini kulikuwa kwa lazima kwa Yesu kabla ya kujaribiwa kwake? Je, ni salama leo kwa wafuasi wa Yesu kufunga kwa siku 40?
- Kwa nini Yesu hakutumia uwezo wake kumzuia shetani asimjaribu? Je, kujaribiwa na shetani ni dhambi? Mtu anaishije kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu? Shetani aliwezaje kumchukua Yesu hadi kwenye kinara cha hekalu? Je, Shetani anajua Maandiko? Kwa nini ujuzi wake wa Maandiko haumsaidii kumtii Mungu na kuokolewa?
- Je Yesu angemsujudia Shetani ni kweli angempa milki zote za ulimwengu? Je Yesu asingemwambia Shetani ondoka angeondoka? Yesu alienda Kapernaumu kwa kuwa Maandiko yalitabiri hivyo. Je maeneo tunayoyapelekea injili yalitabiriwa? Kwa nini Yesu aliposikia Yohana aliyembatiza amefungwa hakwenda kumfungua mara moja?
- Petro na Andrea waliwezaje kuziacha nyavu zao na kumfuata Yesu? Je wasingeweza kumfanyia Yesu huku wakiendelea na kazi zao? Kazi ya Yesu ilikuwa kuhubiri, kuponya, kufundisha, au vyote? Habari njema ya ufalme aliyokuwa akiihubiri Yesu ni ipi? Kwa nini iliitwa Habari Njema? Kilichofanya watu wengi kumfuata Yesu kila aendako ni nini? Je huduma ya uponyaji leo bado ingalipo kwenye mikutano yetu?
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 5:1-48
- Kwa nini Yesu alikuwa anaketi wakati wa kutoa hotuba? Kwa nini maskini, wapole, na wenye huzuni wanapongezwa?Tabia hizi zilizopongezwa na Yesu zina nafasi gani katika kumfanya mtu kuwa raia wa mbinguni? Utajijuaje kama una kiu ya haki? Je kushutumiwa na kuudhiwa kwa ajili ya Neno la Mungu kunatokana na nini? Je ukristo wa kweli unapimwa kwa mambo hayo?
- Masharti gani ni magumu kibinadamu je ni yale yaliyokuwamo kwenye torati au yale aliyoyatoa Yesu? Kwa nini maagizo ya Yesu na ya torati yanaonekana kama yanapingana? Kama Yesu alikuja kutimiliza torati kwa nini alionekana kama anavunja torati? Je tatizo lilikuwa kwenye torati au katika kuitafsiri torati? Tofauti za mafundisho tunazoshuhudia kwa watumiaji wa Biblia leo zinatokana na Biblia au tafsiri za Biblia?
- Kuwapenda adui kuna faida gani? Kwa nini wafuasi wa Kristo wanafananishwa na chumvi? Matendo mema yanachangiaje watu kumtukuza Mungu?Kwa nini Mungu anawaangazia jua lake waovu na wema? Anavutiwa nini na waovu hadi awatendee wema huo? Je, njia ya kuepuka kushindana na mwovu ni kumruhusu akutendee ubaya mara mbili ya hitaji lake la awali?
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 6:1-34
- Wema unaofanywa bila kujitangaza una faida yoyote? Kwa nini Mungu anamwepusha mwanadamu na kupenda sifa wakati yeye Mungu mwenyewe anapenda sifa? Je, mwanadamu ana uwezo wa kutenda mema? (Mhubiri 7:20). Kuna wakati kusali kwaweza kufanyika kama maonyesho (show off) ili uonwe na kusifiwa na watu? Kuna haja ya mtu anayetolewa mapepo kuwekewa kipaza sauti ili watu wasikie anayosema? Je kuna umuhimu wa kudai risiti kwa sadaka uliyomtolea Mungu? Kuna haja ya kujua kama fedha uliyotoa imemfikia Mungu?
- Je kuna haja ya kuweka kamera za usalama kanisani ili kuthibiti wezi au Mungu mwenyewe anatosha? Kwa nini kupayuka katika kuomba kunakatazwa? Tofauti ya kuomba kwa sauti na kupayuka ni ipi? Je kuna watu wanaoomba kwa kupayuka leo? Je, unadhani wanafanya hivyo kwa sababu hawajasikia agizo linalowakataza wasipayuke? Kama Mungu anajua tunayohitaji kwa nini tuombe? Je ukiomba mapenzi ya Mungu yatimizwe kuna uwezekano wa baadhi ya mambo uliyoomba kukosa vigezo vya kujibiwa? Kwa nini Mungu aliweka hili sharti kwenye maombi yetu?
- Nitajuaje mapenzi ya Mungu ninayopaswa kuyaingiza kwenye maombi yangu? Je nikiomba Sala ya Bwana kila ninapoomba bila kuongeza maneno yangu itakuwa sawa? (Wafilipi 4:6; Isaya 41:21). Je ni Mungu mwenye kawaida ya kuwatia watu majaribuni au ni Shetani? Je zile alama azipatazo mtu mwilini kutokana na kusali (kwenye paji la uso au magotini) zinampa mwombaji nafasi ya kukubalika zaidi kwa Mungu? Je kuna ubaya kujiwekea hazina duniani kwa kufanya uwekezaji au kufungua akaunti benki kwa Mkristo? Je sadaka unazotoa zinawekwa kwenye akaunti yako ya mbinguni? Kusumbuka ili kujihakikishia una chakula au mavazi kwa ajili ya kesho ni dhambi? Kwa nini Yesu alisema tusisumbukie hayo?
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 7:1-29
- Je, kuhukumu ni kumwambia mtu makosa yake? Kwa nini inaonekana kuhukumu ni jambo baya? Kwa nini mwenye makosa huwa mwepesi kuyaona makosa yale yale yanapitendwa na wengine? Mbwa na nguruwe wanaotajwa hapa wasiostahili kupewa vitu vya thamani ni nani?
- Kwa nini kuomba kunatakiwa kuandamane na kutafuta na kubisha mlango? Je, Mungu ana mpango wa kuwatendea mema wanaomuomba? Je manabii wa uongo tutawatambuaje? Kwa nini manabii wa uongo wanafanikiwa kuwadanganya watu? Kwa nini Mungu atawakataa waliofanya miujiza siku ya mwisho mwisho?
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 8:1-34
- Kwa nini makutano wengi walimfuata Yesu aliposhuka mlimani? Kama Yesu asingekuwa Mungu mwenye ukoma angemsujudia? Kumgusa mwenye ukoma nyakati ilikuwa ni kujitia unajisi. Je, Yesu alipomgusa mwenye ukoma hakunajisika? Kwa nini muujiza aliomtendea mwenye ukoma hakutaka utangazwe kwa watu? Kuna tofauti gani na leo ambapo miujiza inatangazwa kwa nguvu na vipaza sauti?
- Kwa nini mwenye ukoma alimwambia Yesu ukitaka waweza kunitakasa? Je kuna wakati Yesu asipotaka hawezi kukutendea unachotaka? Huyu Akida anayepigania afya ya mtumishi wake anawafundisha nini wanaonyanyasa watumishi wao? Imani ya yule Akida ambayo Yesu aliisifia ilisababishwa na jambo gani? Je unaamini kuwa Yesu ana mamlaka juu ya mambo yale yaliyokushinda? Yesu alipoombwa amponye mwenye kupooza alijibu 'nitakuja nimponye' Je una imani kuwa Yesu ana mpango wa kuja kukuponya?
- Je kugusa kuna mchango gani katika iponyaji? Yesu aliyachukuaje magonjwa yetu? Kwa nini wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje? Maandiko yana maana gani yanaposema 'mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu na kuyachukua magonjwa yetu"? Yesu alimaanisha nini aliposema 'waache wafu wazike wafu wao'?
- Kwa nini Yesu alizikemea pepo na bahari kana kwamba anakemea mapepo? Au kulikuwa na mapepo kwenye hizo pepo na bahari? Je shetani anaujua muhula wa kuteswa kwake?Kwa nini Yesu aliruhusu mapepo waingie kwa nguruwe? Hakuona kuwa anawatia hasara wale wenye nguruwe? Kwa nini wenyeji wa nchi ile walimsihi Yesu aondoke mipakani mwao?
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 9:1-38
1. Je Yesu anapaswa kushauriana na nani ili akusamehe dhambi? Kwa nini tangu mwanzo Yesu hakuonekana kuwa na hadhi ya Mungu? (Isaya 53:3). "Jipe moyo mwanangu" na "Jipe moyo binti yangu" ni maneno aliyoyatumia Yesu kabla ya kuwaponya wagonjwa aliokutana nao. Jambo hili linakupa hisia gani kuhusu tabia ya Yesu kwa watu wanaopitia changamoto?
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 10:1-36
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 11:1-30
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 12:1-50
- Je kula ngano mashambani siku ya Sabato ni dhambi? Je, ni jambo gani lililo halali kufanya siku ya Sabato? Kwa nini uelewa juu ya namna ya kutunza Sabato ulitofautiana kati ya Yesu na Wayahudi? Upi ulikuwa mtazamo sahihi kati ya ule wa Yesu na Wayahudi? Kwa nini Yesu anatetea kitendo cha Daudi na wenzake kuila mikate ya wonyesho? Je mtu anaweza kuinajisi Sabato asipate hatia? Kwa nini Yesu anajitambulisha kuwa ni mkuu kuliko hekalu?
- Kuwalaumu wasio na hatia kunatokana na nini? Kwa nini Yesu anajitambulisha kama Bwana wa Sabato? Je yeye ndiye aliyeanzisha Sabato? Kama yeye ni mwasisi wa Sabato kwa nini Wayahudi walimshitaki kama anavunja sabato? (Yohana 5:18; Yohana 9:14). Utajuaje kuwa hili ni jambo jema linalostahili kutendwa siku ya Sabato?Kwa nini Wayahudi walijali Sabato kuliko kumjali binadamu? Kwa nini Sabato yao haikuwa na utu ndani yake? Je inawezekana leo kufanya kosa hilo pia?
- Utambi utokao moshi hatauzima maana yake nini? Je kuna upofu na ububu unaotokana na mapepo? Je Shetani aweza kumtoa Shetani mwenzake? Kwa nini kumsema vibaya Roho Mtakatifu ni kosa kubwa kuliko kumsema Yesu mwenyewe? Kwa nini ni jambo lisilowezekana kunena mema wakati wewe ni mbaya? Kwa nini kizazi hiki kinaonekana kibaya kuliko kizazi cha Yona?
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 13:1-58
- Yesu alipotaka kufanya mkutano hakualika watu kama tufanyavyo lakini mikutano yake ilijaa watu. Nini siri ya mafanikio hayo? Tunatakiwa kuboresha nini ili kuifikia hali hiyo? Kwa nini kwenye hotuba zake alitumia sana mifano? Kwa mujibu wa Yesu matokeo mazuri yanapokosekana kwa wasikilizaji tatizo hasa huwa ni la wasikilizaji au mnenaji? Kwa nini kuna tofauti katika upokeaji wa ujumbe?
- Je kuzijua siri za ufalme wa mbinguni kunatokana na kujaliwa na Mungu? Kwa nini Yesu alisisitiza wenye masikio ya kusikia wasikie? Kwani wengine wana masikio ya aina gani? Je mtu aweza kujitambua kama ana masikio gani?Je kutumia mifano kuna msaada gani kwa wale wasiojua siri za ufalme wa mbinguni? Je kuna namna ya kushughulika na watu walioamua kujizima data au kujitoa ufahamu? Shetani anaitumiaje fursa ya mtu aliyeshindwa kulielewa neno? Natakiwa nifanyeje ikiwa sijalielewa somo?
- Asiye na kitu Yesu anasema hata kile alicho nacho atanyang'aywa. Atanyang'anywa nini wakati hana kitu? Kwa nini mbegu zilizopandwa kwenye rutuba huzaa kwa viwango tofauti? Kwa nini ngano na magugu vinaruhusiwa kuendelea kukua pamoja? Hiyo ghala ambamo ngano hukusanywa ni wapi? Kwa nini ufalme wa mbinguni unafananishwa na vitu vingi? Wenye haki watang'aa kama jua? Maana yake ni nini?
- Ufalme wa mbinguni una kitu gani chenye uthamani kinachoufanya ufananishwe na lulu? Je, inawezekana wengi hawajaupa uthamani unaostahili ufalme huo na ndiyo maana hawajaamua kuuza vyote ili kuupata? Kuwa na elimu ya ufalme wa mbinguni kunamfanyaje mtu atoe vitu vipya na vya zamani? Kwa nini watu wa Nazareti walichukizwa na Yesu?
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 14:1-36
- Kwa nini mtu mwenye hatia kwa kawaida huwa mwoga na katili? Je Yohana alijisababishia mwenyewe matatizo kwa kumkemea kiongozi wa nchi kwa namna alivyofanya? Je unaridhika na namna Yesu alivyoshughulikia taarifa kuwa Yohana Mbatizaji (mchungaji wake aliyembatiza) amefungwa katika mazingira ya uonevu? Je nani alaumiwe kati ya mtoto aliyeomba kichwa cha Yohana, mama aliyemshawishi, na mfalme aliyetekeleza ombi?
- Je Herode angejitetea baada ya kutekeleza hukumu ile kuwa maamuzi yale hayakuwa yake lakini yalitokana na pombe utetezi wake ungekuwa na mashiko?Taarifa kuwa Yesu anao uwezo wa kulisha watu 5,000 wakashiba na kusaza linakupa ujasiri gani unapokabiliwa na changamoto za kukosa chakula? Je anaweza kufanya hayo aliyofanya miaka 2,000 iliyopita kwenye mazingira ya sasa. Kama unao uwezo wa kutoa chakula kwa nini aliamuru kilichobaki kikusanywe? Je unajua kuwa unapomwaga chakula kuna wengine wanakitafuta na wengine wanapoteza maisha kwa kukosa chakula?
- Yesu alipenda kufanya maombi ya faraghani. Je unadhani hiyo ilikuwa inamuandaa kukabili changamoto zilizokuwa mbele yake? Kwa nini Yesu alimruhusu Petro atembee juu ya maji? Je uwezo wa kutembea juu ya maji ulimuongezea Petro kiburi au unyenyekevu. Ni hatari gani inayowakabili wale waliopewa uwezo wa kutenda miujiza? Yesu alikuwa tumaini la watu katika njaa, katika misukosuko ya maisha na katika magonjwa. Unadhani Yesu angekuwa anaishi leo mahali ulipo umaarufu wake ungefanana na wa nani? Je idadi ya wanaomwamini ingeongezeka?
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 15:1-39
- Nani ana makosa zaidi kati ya yule anayehalifu mapokeo na yule anayehalifu Amri Kumi? Kwa nini kufundisha mafundisho ya wanadamu (yasiyothibitishwa na Maandiko) kunafanya ibada ya mtu huyo isitambulike? Hayo mapando ambayo Mungu hajayapanda (mafundisho ya uongo) yatang'olewa lini? (Yeremia 1:10). Chuki iliyooneshwa na Mafarisayo ilitokana na maumivu ya kung'olewa kwa mafundisho yao ya uongo?
- Je ufafanuzi wa Yesu juu ya wanafunzi wake waliokuwa wanakula bila kunawa hadi kwenye viwiko ulilenga kuruhusu ulaji wa nguruwe na wanyama najisi wa (Kumb.14:3-21 na Walawi 11:1-47)? Kama Yesu aliruhusu ulaji wa wanyama najisi ilikuwaje Petro alikataa kula alipoagizwa achinje na kula wanyama hao (Matendo 10:9-14)? Kitendo cha Yesu kumponya binti wa mama Mkananayo (asiye wa taifa la Israeli) lilikusudia kutoa fundisho gani kwa Wayahudi na wanafunzi wake?
- Ni kitu gani unajifunza kwa imani ya mama yule? Walemavu na wagonjwa walikuwa wanahudumiwaje kabla ya Yesu? Familia za walioponywa na walioponywa wenyewe walikuwa wanajisikiaje kubusu ujio wa Yesu? Wale unaowahudumia wanajisikiaje kuhusu wewe? Je unadhani ni wagonjwa na walemavu wote waliponywa wakati wa Yesu katika maeneo aliyokuwa akiyatembelea?
- Kuyahalifu mapokeo ya wazee kulikofanywa na wanafunzi wa Yesu kulikuwa halali? Je kulitokana na nini? Kumheshimu Mungu kwa midomo kuna ubaya gani? Je kisichokubalika ni kumheshimu Mungu kwa midomo au kumheshimu Mungu mioyo ikiwa mbali? Kwa nini kimwingiacho mtu huwa hakimtii unajisi ila kimtokacho? Kwa maana hiyo kula vyakula najisi hakumtii mtu unajisi?
- Je kipofu aweza kumuongoza kipofu mwenzake? Unatambuaje kama fundisho fulani ni pando lisilotoka kwa Mungu? Ni lini ambapo Mungu ataling'oa pando asilolipanda? Je kitendo cha Yesu kuwauliza wanafunzi wake "hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili" lilikuwa sahihi au lilionyesha dharau? Mawazo yatokayo moyoni humtiaje mtu unajisi? Kwa nini Yesu alipoombwa kumtoa binti mapepo alikaa kimya?
- Kauli aliyoitoa Yesu kwamba sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli haionyeshi ubaguzi na kufuta madai kwaba alikja kuwakomboa wanadamu wote? Je, hao wengine hawakuwa wamepotea? Je lugha hiyo ililenga nini? Nini kilichofanya Yesu atambue kuwa yule mama Mkananayo alikuwa na imani kubwa? Je inawezekana wakati mwingine tumezuia mibaraka yetu kwa kukosa imani kwenye maombi yetu?
- Kuyahalifu mapokeo ya wazee kulikofanywa na wanafunzi wa Yesu kulikuwa halali? Je kulitokana na nini? Kumheshimu Mungu kwa midomo kuna ubaya gani? Je kisichokubalika ni kumheshimu Mungu kwa midomo au kumheshimu Mungu mioyo ikiwa mbali? Kwa nini kimwingiacho mtu huwa hakimtii unajisi ila kimtokacho? Kwa maana hiyo kula vyakula najisi hakumtii mtu unajisi?
- Je kipofu aweza kumuongoza kipofu mwenzake? Unatambuaje kama fundisho fulani ni pando lisilotoka kwa Mungu? Ni lini ambapo Mungu ataling'oa pando asilolipanda? Je kitendo cha Yesu kuwauliza wanafunzi wake "hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili" lilikuwa sahihi au lilionyesha dharau? Mawazo yatokayo moyoni humtiaje mtu unajisi? Kwa nini Yesu alipoombwa kumtoa binti mapepo alikaa kimya?
- Kauli aliyoitoa Yesu kwamna sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli? Je, hao wengine hawakuwa wamepotea? Je lugha hiyo ina ubaguzi ndani yake? Nini kilichofanya Yesu atambue kuwa yule mama Mkananayo alikuwa na imani kubwa? Je inawezekana wakati mwingine tumezuia mibaraka yetu kwa kukosa imani kwenye maombi yetu?
- Je kutunza Sabato kwa mujibu wa Yesu ni mzigo au ni jambo lenye neema lililojaa baraka? Kwa nini ilionekana mara nyingi Yesu akitofautiana na Wayahudi juu ya namna sahihi ya kutunza Sabato? Je Yesu alikuja kuondoa Sabato? Kwa nini kumkufuru Roho Mtakatifu ni dhambi isiyosameheka? Yesu anauliza mwawezaje kuwa wema mkiwa wabaya? Nini kinapaswa kutangulia kati ya kutenda wema na kuwa mwema?
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 16:1-28
- Kwa nini Yesu aliyaita mafundisho yanayopotosha ya Mafarisayo na Masadukayo kuwa ni chachu? Kwa nini mafundisho hayo ya uwongo sehemu nyingine yameitwa mvinyo wa uasherati? (Ufunuo 17:2). Yesu aliposema juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa, je mwamba aliokuwa anaulenga ni Petro au ni yeye mwenyewe? (1 Wakorintho 10:4).
- Aliyepewa funguo za ufalme wa milele na Yesu alikuwa ni Petro au kanisa lake lililoaminifu? Ni wakati gani funguo hizo zinatumika kufunga na kufungua? Kitendo cha Petro kumkemea Yesu kilionyesha utovu wa nidhamu au alikuwa Shetani akiongea ndani yake? Hatua ya Yesu kumuita Petro Shetani nenda nyuma yangu u kikwazo kwangu kilikuwa halali?
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 17:1-27
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 18:1-35
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 19:1-30
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 20:1-34
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 21:1-46
- Kwa nini mwenye punda alipoambiwa Bwana anamhitaji hakumzuia? Je kulikuwa na mapatano ya awali baina yake na Yesu? Je inawezekana leo Mungu kukuelekeza kwa mtu atakayekuwa tayari kutoa mali zake ili kuitegemeza kazi ya Mungu? Je, Mungu anao watu aliowaandaa ili kunusuru kazi ya Mungu kwa mali na vipawa vyao? Katika maisha yake Yesu aliishi kama raia wa kawaida. Kwa nini mara hii alikubali kuingia Yerusalemu kwa fahari na huku akitukuzwa na watu?
- Kwa nini Yesu alifananisha yaliyokuwa yakiendelea kwenye hekalu la Yerusalemu kama pango la wanyang'anyi? Je, ni rahisi kukemea dhambi zinazotendwa kwenye makanisa makubwa ya mjini? Yesu alikuwa faraja kwa vipofu na viwete lakini akawa mwiba kwa Mafarisayo. Jadili. Unaona nyumba ya ibada leo ikitumika zaidi kama nyumba ya sala? Ni kipi kinachukua muda zaidi kati ya hotuba, majadiliano na sala? Kwa nini inakuwa hivyo?
- Kama Yesu angekuwepo leo angeuliza nini kuhusu ubatizo? Kama angeuliza ubatizo wa maji mengi ulitoka wapi viongozi wa dini wa leo wangejibuje? Ubatizo una umuhimu gani kwa wanadamu hata Yesu atake kujua uelewa wa watu kuhusu mada hiyo? Makahaba wanawezaje kuwatangulia wasio makahaba kwenye ufalme wa Mungu? Je, makahaba wana nafasi yao mbinguni
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 22:1-46
- Mfalme alimfanyia mwanae harusi. Je, wazazi wa kizazi hiki wanawafanyia watoto wao harusi au ni jukumu la kamati za harusi? Je kama watu wangekuwa hawachangii harusi wangekuja ukumbini? Mfalme aliandaaje harusi bila kuwa na uhakika wa wahudhuriaji? Je alikuwa na mahusiano mazuri na watu? Je harusi aliyoiandaa Mungu itajaa waovu kwa wema? Kwa nini walioalikwa hawakustahili?
- Je, kuvaa vazi la harusi ilikuwa sharti la lazima au la hiyari? Kama ilikuwa lazima kwa nini aliruhusiwa kuingia ukumbini? Kama ilikuwa hiyari kwa nini aliadhibiwa? Kwa nini waitwao ni wengi na wateule ni wachache? Kama ilijulikana kwamba hawatateuliwa kwa nini waliitwa? Je, huo siyo usumbufu? Mtu akikuambia hutazami sura za watu katika kufanya maamuzi anamaanisha nini? Katika kujibu maswali ni muhimu kujua nia ya muuliza swali? Utaijuaje nia yake kama amelenga kukutega?
- Je, kumpa Kaisari yaliyo ya Kaisari maana yake ni nini? Je, Wakristo wanapaswa kuitii mamlaka ya kidunia na kuisifia? Kulipa kodi na ushuru kwa serikali ni kwa lazima kwa Mkristo? (Warumi 13;1-3; 1 Timotheo 2:1-2; Warumi13:7). Je, Yesu kama Mungu anayetawala mbingu na ardhi alikuwa na ulazima wowote wa kulipa kodi?
- Je agizo la Musa kuwa mjane asiye na mtoto aolewe na ndugu wa marehemu ili ampatie uzao lilikuwa na kibali cha Mungu? Kwa nini haifanyiki hivyo leo? Je mbinguni watu wataruhusiwa kuishi na wake zao? Je Yesu ni Mwana wa Mungu? Kama Yesu ni Mwana ilikuwaje Mungu amtambulishe kama Mungu? (Waebrania 1:8).
- Kwa nini mwenye punda alipoambiwa Bwana anamhitaji hakumzuia? Je kulikuwa na mapatano ya awali baina yake na Yesu? Je inawezekana leo Mungu kukuelekeza kwa mtu atakayekuwa tayari kutoa mali zake ili kuitegemeza kazi ya Mungu? Je, Mungu anao watu aliowaandaa ili kunusuru kazi ya Mungu kwa mali na vipawa vyao? Katika maisha yake Yesu aliishi kama raia wa kawaida. Kwa nini mara hii alikubali kuingia Yerusalemu kwa fahari na huku akitukuzwa na watu?
- Kwa nini Yesu alifananisha yaliyokuwa yakiendelea kwenye hekalu la Yerusalemu kama pango la wanyang'anyi? Je, ni rahisi kukemea dhambi zinazotendwa kwenye makanisa makubwa ya mjini? Yesu alikuwa faraja kwa vipofu na viwete lakini akawa mwiba kwa Mafarisayo. Jadili. Unaona nyumba ya ibada leo ikitumika zaidi kama nyumba ya sala? Ni kipi kinachukua muda zaidi kati ya hotuba, majadiliano na sala? Kwa nini inakuwa hivyo?
- Kama Yesu angekuwepo leo angeuliza nini kuhusu ubatizo? Kama angeuliza ubatizo wa maji mengi ulitoka wapi viongozi wa dini wa leo wangejibuje? Makahaba wanawezaje kuwatangulia wasio makahaba kwenye ufalme wa Mungu?
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 23:1-39
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 24:1-51
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 25:1-46
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 26:1-75
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 27:1-66
MASWALI YA KUJADILI: MATHAYO 28:1-20