MASWALI YA KUCHAGUA: LUKA 1:1-80
✅1. Luka anatuthibitishia kuwa taarifa anazoandika zimetokana na utafiti aliofanya kwa
(a) wanafunzi wa Yesu
(b) mashahidi wenye kuyaona yaliyoandikwa na watumishi wa lile neno
(c) kutumia elimu yake ya kidaktari
✅2. Zakaria na mkewe Elizabethi walikuwa
(a) makuhani nyakati za mfalme Herode
(b) wenye haki mbele za Mungu
(c) hawana mtoto maana wote wawili walikuwa tasa
✅3. Zakaria alipotokewa na malaika hekaluni
(a) alijawa na furaha akijua maombi yake yamejibiwa
(b) alianguka kifudifudi akamsujudia
(c) alifadhaika, hofu ikamwingia
✅4. Mtoto aliyetabiriwa na malaika kuzaliwa kwa familia ya Zakaria na mkewe angekuwa wa ________ na jina lake angeitwa ----------.
(a) kiume, Yohana
(b) kiume, Yohana Mbatizaji
(c) kike, Mariamu.
✅5. Yohana alijazwa na Roho Mtakatifu
(a) siku aliyozaliwa
(b) siku aliyobatizwa
(c) tangu tumboni mwa mamaye
✅6. Kitoto kichanga kiliruka tumboni mwa Elizabeti wakati
(a) sauti ya kuamkia ya Mariamu ilipoingia masikioni mwake
(b) Roho Mtakatifu alipoingia tumboni kwa Elizabeti
(c)
✅7. Kitoto kichanga kiliruka tumboni mwa Elizabeti wakati
(a) sauti ya kuamkia ya Mariamu ilipoingia masikioni mwake
(b) Roho Mtakatifu alipoingia tumboni kwa Elizabeti
(c) Elizabeth alipokutana na Mariamu.
✅8. Kuhani Zekaria alikuwa bubu kwa agizo la malaika kwa sababu
(a) alikosa adabu ķwa malaika
(b) hakusadiki maneno ya malaika
(c) ili asije akatoa siri ya yale waliyoongea na malaika.
✅9. Mtoto aliyezaliwa kwa Zekaria na Elizabeth aliitwa Yohana kwa sababu
(a) kuna mtu katika jamaa yao aliitwa jina hilo.
(b) ndilo jina lililopendekezwa na malaika
(c) ndilo jina ambalo Zekaria na mke wake walipatana wampe mtoto wao.
✅10. Mtoyo Yohana alikua na kiongezeka kiroho naye alikaa
(a) majangwani
(b) nyumbani kwa wazazi wake.
(c) hekaluni
MASWALI YA KUCHAGUA: LUKA 3:1-38
✅1. Ondoleo la dhambi husababishwa na
(a) ubatizo wa maji mengi
(b) ubatizo wa toba
(c) mahubiri
✅2. Kwa mujibu wa Yohana Mbatizaji waliostahili kuuona wokovu wa Mungu walikuwa ni
(a) wote wenye mwili
(b) wote waliobatizwa
(c) wote waliotubu
✅3. Askari waliokuja kwa Yohana Mbatizaji wakitaka kubatizwa aliwaambia
(a) toshekeni na mishara yenu
(b) msimdhulumu mtu
(b) msimshitaki mtu kwa kumsingizia
(c) msimdhulumu mtu
(d) majibu yote hapo juu ni sahihi
✅4. Herode alimfunga Yohana Mbatizaji gerezani kwa sababu
(a) alikuwa anawabatiza watu Yordani bila kibali
(b) alikaripiwa kwa kumchukua mke wab nduguye
(c) aliwatuhumu askari wake kuwa hawatosheki na mishahara yao.
✅5. Yesu alianza kufundisha akidhaniwa kuwa na miaka
(a) 30
(b) 27
(c) 31
MASWALI YA KUJADILI: LUKA 4:1-44
- Kama Yesu ni nafsi ya Mungu ilikuwaje akaongozwa na Roho Mtakatifu kwenye majaribu yake? Je Shetani alikuwa anamjaribu Yesu kama mwanadamu au kama Mungu? Kutokula kitu kuna msaada gani kwa anayejaribiwa? Je ni salama kwa wanadamu wa kawaida kufunga siku 40 bila kula? Je Shetani alitilia shaka Uungu wa Yesu? Je kwa Yesu kutogeuza jiwe kuwa mkate kulidhihirisha kuwa si Mwana wa Mungu?
- Kama lengo la Yesu kuja duniani ni kuja kurejesha umiliki wa dunia uliokuwa mikononi mwa Shetani kwa nini hakukubali pendekezo la Shetani la kusujudiwa ili apewe ulimwengu wote? Je Shetani huwa anasoma Maandiko? Kwa nini yameshibdwa kumbadilisha? Je mtu anaweza kusoma Maandiko kwa malengo mabaya? Kama Shetani anaweza kwenda juu ya kinara cha hekalu anaweza kushindwa kuingia kanisani? Kama hawezi kuogopa nyumba za ibada ni wapi palipo salama asipoweza kufika?
- Kwa nini Yesu alisoma kifungu cha Biblia kilichowakera waliokuja kuabudu? Kwa nini watu kwa kawaida hawampendi mhubiri anayewaambia ukweli? Je kunahitajika bìsara katika kuhubiri Neno la Mungu? Kwa nini watu wa Nazareti waliibua hoja ya unasaba wa Yesu? Je Yesu hakuwa anakubalika kijijini kwao? Je Yesu alikuwa na mahusiano mazuri na watu?
- Kwa nini watu wa vijiji vingine waliyapenda maneno ya Yesu wakiyasifia kuwa yalikuwa na nguvu? Yesu aliposema fumba kinywa alikuwa anamwambia mwenye pepo au pepo lenyewe? Je akiwepo mwenye homa unatakiwa umuombee au uikemee ile homa? Katika kuwaponya wenye maradhi ipo haja ya kuweka mikono juu yao?
MASWALI YA KUCHAGUA:LUKA 8:1-56
✅1. Yesu alikuwa akihubiri na kutangaza injili kwa kuzunguka-zunguka
(a) mijini na vijijini.
(b) mijini tu.
(c) vijijini tu.
✅2. Na . . . kadhaa wenye pepo wabaya na magonjwa wakaponywa.
(a) wanaume
(b) wanawake
(c) wanaume na wanawake
✅3. Hawa ni miongoni mwa wanawake waliokuwa kimhudumia Yesu kwa mali zao.
(a) Mariamu mama yake Yesu
(b) Mariamu aitwaye Magdalene
(c) Kuza
✅4. Mbegu zilizoanza kumea zikakauka kwa kukosa rutuba ni zile zilizoangukia
(a) karibu na njia.
(b) kati ya miiba
(c) penye mwamba
✅5. Walioangukia kwenye ________ ni wale walisikiao neno na kulishika na kuzaa matunda kwa _________
(a) uvumilivu
(b) wakati
(c) wingi
✅6. Yesu alipomuuliza mwenye pepo jina lako nani alijibu jina langu ni
(a) Shetani
(b) Jeshi
(c) Maimuna
✅7. Umri wa binti Yairo ndiyo umri ambao mwanamke aliyegusa pindo la vazi la Yesu alitumia
(a) kumtafuta Yesu amponye
(b) kutokwa na damu
(c) kugusa pindo la vazi la Yesu
✅8. Yesu akiwa njiani kuelekea kwa binti Yairo walikuja watu kutoka nyumbani wakisema
(a) mhimizeni mwalimu afanye haraka mtoto amezidiwa
(b) mwambieni mwalimu amuombee mtoto hapa hapa njiani
(c) msimsumbue mwalimu binti yako amekwisha kufa
✅9. Yesu alipomwona Yairo amefadhaika kwa taarifa za msiba alimwambia
(a) usiwe na hofu, amini tu naye ataponywa.
(b) usiwasikilize mtoto hajafa
(c) sina sababu ya kuendelea na safari maana mtoto amekufa
✅10. Baada ya mtoto kufufuliwa Yesu aliamuru mtoto
(a) aombe
(b) apewe chakula
(c) apewe maji ya kunywa
MASWALI YA KUCHAGUA: LUKA 11:1-54
✅1. Mtu aliyegongewa mlango usiku na rafiki yake ili amsaidie mkate
(a) alikataa kumfungulia huyo rafiki yake
(b) alimfungulia na kumpatia mikate kwa kuwa alimhurumia
(c) alimfungulia na kumpatia mikate kwa kuwa alikerea na usumbufu wake
✅2. Maadui wa Yesu walimtuhumu kuwa anatoa pepo kwa nguvu za Beelzebuli lakini Yeye alisema anatoa
(a) kwa kidole cha Mungu
(b) kwa kutumia maombi
(c) kwa kutumia wana wenu
✅3. Watu wa wakati wa Yesu walikuwa wanatafuta ishara ila Yesu aliwaambia hawataona ishara ila
(a) ishara ya Yona
(b) ishara ya malkia wa Sheba
(c) ishara ya Sulemani
✅4. Mafarisayo walikuwa wanasafisha kikombe na sahani kwa nje lakini
(a) walikuwa hawasafishi kwa nje
(b) ndani yao walikuwa wamejaa unyang'anyi na uovu
(c) walikuwa hawatoi sadaka
✅5. Yesu aliwaambia Wanasheria kuwa wanafanya kosa la
(a) kuwatwika watu mizigo isiyochukulika
(b) kujengea maziara manabii wakati baba zao ndiyo waliowaua
(c) a na b hapo juu ni sahihi
MASWALI YA KUCHAGUA: LUKA 12:1-59
✅1. Yesu aliwaonya watu kutomuogopa awezaye kuua mwili bali wamwogope
(a) asiyeua mwili
(b) asiyeua roho
(c) awezaye kumtupa Jehenamu aliyemuua
✅2. Ushahidi kuwa Mungu anatujali ni ukweli kuwa
(a) nyele za vichwa vyetu zote zimehesabiwa.
(b) mashomora watano hawauzwi kwa senti mbili
(c) hatuogopi
✅3. Atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa lakini aliyemkufuru Roho Mtakatifu
(a) atapokea mapigo
(b) atakuwa amefanya dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu
(c) hatasamehewa
✅4. Mtu mmoja aliyemuomba Yesu amgawanyie mali za urithi na ndugu yake alimwambia
(a) jilinde na choyo
(b) sina muda wa kuwagawia mali za urithi
(c) ni heri mwenye mali chache kuliko mwenye mali nyingi.
✅5. Yesu aliwaambia makutano
(a) msijisumbue kutafuta mali
(b) utafuteni kwanza ufalme wa mbinguni
(c) uzeni mali mlizonazo muwe maskini
✅6. Mwana wa Adamu atakuja
(a) katika saa tusiyodhani
(b) katika zamu ya tatu
(c) wakati watu wote wamelala
✅7. Yesu alikuja duniani ili
(a) kuleta amani
(b) kuleta mafarakano
(c) kutupa moto duniani ili wanadamu waungue
✅8. Asiyejua naye amefanya yastahiliyo mapigo
(a) atapigwa kidogo
(b atapigwa sana
(c) atasamehewa
✅9. Wakili mwaminifu na mwenye busara ni yule
(a) anayewapiga wajoli wake walio wazembe
(b) anayekunywa, kula na kulewa
(c) anayewapa watu posho kwa wakati wake.
✅10. Msiogope enyi kundi dogo kwa kuwa Baba yenu ameona vema
(a) kuwapa ule ufalme
(b) kuwalindia mali yenu kule mbinguni ili nondo wasiiharibu
(c) kuiweka mioyo yenu pale hazina yenu ilipo.
MASWALI YA KUCHAGUA: LUKA 14:1-35
✅1. Yesu alienda nyumbani kwa mmojawapo wa Mafarisayo siku ya Sabato ili kwenda
(a) kumponya
(b) kula chakula
(c) kusali
✅2. Maafarisayo walikuwa wanamvizia Yesu waone kama
(a) ataponya siku ya Sabato
(b) atakula chakula siku ya Sabato
(c) ataweza kuponya
✅3. Yesu alipowauliza wanasheria na Mafarisayo ni halali kuponya siku ya sabato wao
(a) walimjibu ndiyo ni halali
(b) walimjibu hapana si halali
(c) walinyamaza kimya
✅4. Yesu anasema ukialikwa arusini usikae viti vya mbele kwa sababu
(a) viti vya mbele huwa ni vichache sana.
(b) viti vya mbele ni vya waalikwa waliochangia arusi
(c) kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.
✅5. Yesu anasema ukiandaa karamu waalike maskini
(a) kwa maana hawana cha kukulipa
(b) wasije wakakosa kukualika kwenye karamu zao
(c) kwa maana utalipwa kwenye ufufuo wa wenye haki
(d) a na c hapo juu ni sahihi
✅6. Katika wale walioalikwa hakuna hata mmoja atakayeionja karamu kwa sababu
(a) hawakuthamini mwaliko
(b) hawakuja kwa wakati
(c) hawakuvaa vazi la arusi
✅7. Ili kuwa mwanafunzi wa Yesu ni lazima (a) ujitwishe msalaba umfuate
(b) umchukie ndugu yako
(c) umfurahishe kila mtu
✅8. Mungu ameandaa karamu mbinguni ambayo waalikwa ni
(a) Wayahudi
(c) Wakristo
(c) Wanadamu wote
✅9. Kwa nini ni muhimu kuhesabu gharama kabla ya kufanya maamuzi magumu ya kuwa mfuasi wa Yesu?
(a) ili watu wasije wakakucheka
(b) ili usije ukashindwa kuendelea kumfuata Yesu
(c) ili usije kufilisika
✅10. Wafuasi wa Yesu walioshindwa kumwakilisha Yesu katika mwenendo wao wanafananishwa na
(a) na mtu aliyeandaa karamu
(b) na chumvi iliyoharibika
(c) na mtu asiye na masikio ya kusikilizia
MASWALI YA KUJADILI: LUKA 15:1-32
- Wenye dhambi walitambulika kwa kigezo gani wakati wa Yesu? Je kwenye jamii zetu kuna wanaoonekana wenye dhambi zaidi kuliko wengine? Kwa nini wenye dhambi walipenda kumsikiliza Yesu? Je tunao wahubiri katika jamii zetu ambao wenye dhambi hupenda kusikiliza mahubiri yao? Ukiwa mhubiri unayependwa na wenye dhambi jamii inakuonaje?
- Kwa nini mtu ahangaike na kondoo mmoja aliyepotea wakati ana kondoo 99 zizini? Je hawezi kuhatarisha maisha yake kwa kitendo hicho? Kwa kufanya hivyo anaonesha anathamini mali zake au anathamini uhai wa kiumbe wake? Je muda na gharama anazotumia kumtafuta kondoo huyo haziwezi kuwa kubwa kuliko thamani ya kondoo huyo? Kama kondoo aliyepotea ni jamii ya wanadamu hao majirani Mungu atakaowaalika kushuhudia kurudi kwetu nyumbani ni nani?
- Unadhani furaha ya Mungu wakati huu anapoendelea kututafuta imekamilika? Je furaha ya Mungu haikamiliki hadi anapokuwa na wanadamu? (Mithali 8:31) Tofauti ya wenye dhambi na wenye haki ni ipi? Kwa nini wenye dhambi wana uwezekano mkubwa wa kuingia mbinguni kuliko wenye haki wasiotubu? Wenye haki wanawezaje kutubu hali wao ni wenye haki?
- Kutafuta shilingi iliyopotea na kondoo aliyepotea ni kupi kuna changamoto zaidi na kwa nini? Aliyeomba kugawiwa urithi alikuwa ni mwana mdogo kwa nini katika kugawa baba aliwagawia wote wawili? Je mtoto alijuaje kama ana urithi kwa baba yake? Je alifanya vizuri kuomba urithi wake? Umewaandalia urithi gani watoto wako? Je Mungu ametuandalia urithi gani? (Mathayo 25:34; 1 Petro 1:4). Je unadhani hii ndiyo sababu ya Shetani kutuchukia sana? (Mathayo 21:38; Marko 12:7).
- Kwa nini mwana mdogo hakuondoka mara tu baaada ya kupewa urithi wake? Kwa nini baba yake alimruhusu kuondoka? Je unajifunza nini kwa malezi ya baba huyu? Je anadekeza watoto kwa kuwapa uhuru uliopitiliza? Kwa nini mali za kurithi hutumika vibaya? Urithi bora usiofilisika kwa watoto ni upi? Ni sahihi kumhakikishia mtoto kuwa mali zako ni zake au anatakiwa kukaririshwa tangu akiwa mdogo kuwa mali zako si zake?
- Njia bora ya kuwekeza mali uliyonayo ili ikusaidie siku zijazo ni ipi? Biblia si imehimiza tuwape watu vitu nasi tutajaziwa hadi kusukwa sukwa? Mwana Mpotevu alikosea wapi mbona mali zake aliwagawia watu? Utajuaje kama unaowaasaidia watakuja kukutelekeza siku utakapofilisika? Je anayekipenda kwa sababu ya mafanikio uliyonayo anafaa kuoana naye? Unamsaidiaje mtu anayependa kutumia pesa zake kwa anasa? Mtu bahili na mtumiaji wa pesa kwa anasa ni yupi ana nafuu?
- Je unaweza kumwita mwenyeji wa nchi ile aliyemhifadhi Mwana Mpotevu kwa chakula cha nguruwe kama Msamaria Mwema au mtesaji? Je wakati wa kujitafuta na wakati huna ajira waweza kufanya kazi yoyote ili mradi mkono uende kinywani? Je kutambua kuwa umefulia au umepotea ni karama? Je asiyejua aendako anaweza kupotea? Je Mwana Mpotevu alikuwa na njozi aliyokuwa anajaribu kuifukuzia?
- Mwana Mpotevu alikumbuka kurudi nyumbani. Vijana wasiokumbuka kurudi nyumbani baada ya kupote wanapungukiwa na nini? Je upendo wa yule uliyemkosea una mchango katika kukufanya utubu? Je Mungu anatamani kuwa na watu wanaomtii wakivutwa na upendo wake au na wale wanaomtii hata kama hawatambui upendo wake?
- Ni mtoto yupi alikuwa anastahili kuitwa mwanae kati ya yule mkubwa au mdogo? Kwa nini baba alimfanyia sherehe mtoto mtukutu na kushindwa kufanya hivyo kwa mtoto mtiifu?
MASWALI YA KUJADILI: LUKA 16:1-31
- Tajiri alimtuhumu wakili wake kuwa anatapanya mali zake kutoka kwa watu wanaomfahamu wakili. Je inafaa kuamini maneno unayopewa na watu juu ya mtu fulani? Ukiona mtu anasisitiza kutoamini maneno ya watu ni ishara kuwa ana mambo mabaya anayofanya? Je kama tajiri angepuuza maneno aliyoambiwa angepata hasara au faida? Je ni vizuri kuamini kila unachoambiwa kuhusu mtu fulani bila kumhoji mhusika?
- Je watu walio waaminifu kwa maswala ya pesa ni wepesi wa kutoa taarifa? Je mtu anayeogopa kulima na kuomba msaada mwishowe aweza kuishia kuwa mwizi? Kati ya kulima na kuomba msaada jambo gani huwa gumu zaidi na kwa nini? Yupi ana mwelekeo nafuu kati ya anayependa kuomba msaada akiwa na viungo timilifu na yule anayeona haya kuomba? Kizazi cha leo kinapendelea nini kati ya kulima na kuomba? Je tatizo la watu wanaotegemea wengine ni kukosa njozi ya maisha?
- Wizi wa kwenye karatasi na utakatishaji wa fedha ni janga kwa jamii yetu kwa kiasi gani? Mjuzi wa kupindisha mahesabu na asiyejua hesabu za kiuhasibu ni yupi sahihi zaidi kumpa dhamana ya kutunza pesa? Je ni rahisi kwa wajuzi wa mahesabu kutumia ujuzi wao kuiba? Wahasibu na wadaiwa wa taasisi wanazoziwakilisha waweza kushirikiana kumhujumu tajiri au taasisi? Je serikali (TRA) inaweza kuwa inapoteza mapato kupitia watumishi wasio waaminifu wanaoshirikiana na wafanyabiashara?
- Je ni kweli kuwa Yesu anatuhimiza kujifanyia rafiki kwa mali ya udhalimu au alikuwa anashauri nini? Je kukosa uaminifu kwa mali ya mtu mwingine au mali ya taasisi kwaweza kukukosesha uzima wa milele? Je unafanyaje unapokuwa kwenye ajira ambayo tajiri hakulipi kama mlivyokubaliana? Je kumdhulumu hapo kunahusu? Je kutumia mapato yako kuitegemeza kazi ya Mungu kwaweza kufananishwa na kile alichofanya wakili asiye mwaminifu?
- Je baada ya maisha haya kuna watu watakuwa na maisha mazuri kwa kutumia mali na alizopata duniani na nafasi yake katika jamii kuitegemeza kazi ya Mungu? Je watakaourithi uzima wa milele watakuwa na mali kuliko walizowahi kumiliki hapa duniani? Kwa nini ni jambo lisilowezekana kutumikia Mungu na mali kwa wakati mmoja? Je kupenda fedha ni dhambi? (1 Timotheo 3:3; 1 Timotheo 6:10; 2 Timotheo 3:2; Waebrania 13:5).
- Kwa nini lililotukuka kwa mwanadamu huwa chukizo kwa Mungu? Kwa nini wanaojidai kuwa na haki mbele ya wanadamu huwa na mioyo michafu? Kwa nini torati haiwezi kutanguka? Kwa nini tangu Yohana watu hujiingiza kwa nguvu? Je torati na habari njema ya ufalme wa Mungu vinahusianaje?
- Je kisa cha Lazaro ni kisa halisi kinachoweza kutumiwa kama fundisho la hali ya wafu? Je wanaokufa wakiwa wema huenda kifuani kwa Ibrahimu? Je wanaokufa wakiwa wabaya huenda mahali pa mateso? Yesu alikuwa na kusudi gani kusimulia kisa hiki? (Luka 16:30-31)
MASWALI YA KUJADILI: LUKA 17:1-37
- Kwa nini makwazo hayana budi kutokea? Je hakuna namna ya kuzuia makwazo yasitokee? Je makwazo yaweza kuwarudisha watu wengine nyuma? Faida za makwazo ni nini? Waletao makwazo watendewe nini? Je kitendo cha kumfungia jiwe na kumtosa baharini mwenye kuleta makwazo kina upendo ndani yake? Je adhabu hiyo siyo kubwa sana ikilinganishwa na kosa lililotendwa?
- Je waweza kujitambuaje kama umekuwa kwazo kwa watu wengine? (2 Wakorintho 6:3). Je mtu anayekukosea mara saba kwa siku anafanya hivyo kwa makusudi au kwa bahati mbaya? Je anastahili kusamehewa au anafanya mzaha? Je imani hupatikana kwa kuongezewa au kwa kuamini? (Waebrania 11:1; Marko 9:24). Je unaweza kujitambua kama una imani ndogo au huna kabisa?
- Inakuwaje wengine wanakuwa na imani kubwa kuliko wengine? Kama imani ya punje ya haradali (sawa na mbegu ya mchicha) yaweza kuhamisha milima je imani ya punje ya kunde ingeweza kufanya nini? Kwa nini imani zetu ni ndogo hivyo? Je. Mungu anapaswa kutushukuru kwa kutii maagizo yake? Je ni kweli kuwa sisi ni watumwa wasio na faida tunafanya tu yanayotupasa kufanya?
- Kama ukihisi unahitaji kutambuliwa kwa mambo uliyomfanyia Mungu hiyo ni ishara kuwa una tatizo gani? Kwa nini wenye ukoma walisimama mbali? Kwa nini wale kenda waliotakaswa ukoma wao hawakurudi kumshukuru Yesu? Kama aliyerudi kushukuru alikuwa Msamaria wale kenda unadhani walikuwa wa kabila gani?
- Je kuna umuhimu kumshukuru Mungu kwa makuu anayotutendea? Unadhani ni nini kinachozuia kutoa shukrani unapotendewa mema? Kwa nini Mafarisayo walitaka kujua ufalme wa Mungu utakuja lini? Je walikuwa wamejiandaa kuupokea? Unawachukuliaje wale ambao leo wanataka kujua ufalme wa Mungu unakuja lini? Wanafanana na Mafarisayo? Kwa nini ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza?
- Ufalme wa Mungu unakuwaje mioyoni mwetu? Je Mwana wa Adamu atakuja kwa kificho kiasi kuwa watu wengine hawatabahatika kushuhudia tukio hilo? Kwa nini kuja kwake kunafananishwa na umeme (radi) umulikao kutoka upande huu wa dunia hadi upande mwingine? Kwa nini tukio la kuja kwa Yesu mara ya pili linafananishwa na tukio la gharika na tukio la moto wa Sodoma? Kuna mlingano gani katika matukio hayo?
- Je Mungu angependa wanadamu wajue siku na saa ya kuja kwake? Kuna faida na ubaya gani wanadamu wakijua siku na saa ya kuja kwa Yesu? Je Mungu angetambulisha siku na saa ya kuja kwa Yesu watu wasingetoa mali zao kusaidia maskini na kutegemeza kazi ya Mungu? Je hiyo ingekuwa ni udhihirisho kuwa wanawapenda watu na Mungu au wanajipendekeza kwa Mungu? Msemo kuwa ulipo mzoga ndipo watakapokutanika tai unamaanisha nini?
MASWALI YA KUJADILI: LUKA 18:1-43
- Kwa nini kuomba kunahitajika siku zote? Je wanaoshindwa kuomba siku zote inatokana na uvivu au kukata tamaa au vyote? Kwa nini kuna wakati kumwomba Mungu kunakatisha tamaa? Je Mungu anakatisha tamaa kwa kutoa majibu mabaya au kwa kuchelewa kujibu? Je kuna wakati katika maombi yako hutamani kusema mapenzi yako yatimizwe? Je kuna wakati unadhani Mungu huwapendelea waombaji wengine kuliko wewe?
- Je umwendeapo Mungu ukiwa na dhana kwamba hajibu maombi au anapendelea ni rahisi maombi yako kujibiwa? (Waebrania 11:6; Yakobo 1:6-7). Je, ni haki gani ambazo kwa kawaida wajane hudhulumiwa? Je njia mojawapo ya kudai haki hizo ni maombi? Je haki zingine haziwezi kupatikana kwa kuwatumia wanasheria?
- Je wanasheria na mahakimu wasiomcha Mungu na wasiojali watu wamekuwa wakikalia haki za watu? Nini kifanyike kwa mawakili na mahakimu wa aina hiyo? Je kuna umuhimu kwa wanasheria kuwa wacha Mungu na wanaojali wat? Je ni kweli kuwa haki haiombwi bali hudaiwa au hunyakuliwa? Katika kudai haki ipo haja ya kuwasumbua wale tunaowadai?
- Je Mungu hujibu maombi ya wale wanaomchosha na wanaomwomba mchana na usiku zaidi kuliko wale wasiomchosha? Je maombi ya usiku yana umuhimu gani? Ni nani anayeonyesha kuwa ana hitaji zaidi kati ya yule aombaye sana na anayeonba kidogo? Je atakapokuja Mwana wa Adamu ataikuta imani duniani hasa hiyo ya kuomba usiku na mchana bila kukata tamaa?
- Unadhani kadri siku za kuja kwa Yesu zinavyokaribia ndivyo vitendo vya kukandamiza haki za watu vitazidi kuongezeka? Je kadri vitendo hivyo vinavyoongezeka kiwango cha kuomba nacho chapaswa kuongezeka? Je wenye haki wana kawaida ya kudharau wengine? Kwa nini wasio haki hupenda kudharau wengine? Kwa nini wasio haki hupenda kujionyesha kuwa ni wenye haki?
- Kati ya Farisayo na Mtoza ushuru ni nani alikuwa anaonekana kama mwenye dhambi na kwa nini? Ukijiona u mwenye haki kuliko wengine je ibada yako inakubalika? Kwenye maombi kuna haja ya kujilinganisha na wengine wasiofanya vizuri? Kama wewe u mwema kuliko wengine kuna haja ya kulisema hilo kwa watu au kwa Mungu? Mungu humkubali yupi kati ya yule mwenye matendo mema na yule anayejitambua kuwa ni mwenye dhambi?
- Je kuna wakati watu wenye hali njema ya kiroho umekukatisha tamaa kumsogelea Mungu? Ni nani anastahili kati ya yule anayejiona anastahili na yule anayejiona hastahili? Je Yesu si mwema? Kwa nini alikataa kuitwa mwema? Je ni kawaida ya watu wema kutopenda kusifiwa? Je kama una kawaida ya kupenda kusifiwa utashindaje tabia hiyo? Je wenye mali wanaweza kuokoka?
- Mbona Ayubu alokuwa na mali lakini alikuwa mwaminifu? Je ni lazima kuacha vitu vyote ili kumfuata Yesu? Kwenye ulimwengu ujao watu watapewa mali gani zinazozidi hizi wanazozitoa sasa kwa ufalme wa Mungu? Kwa nini Yesu aliwaambia wanafunzi wake mambo mabaya yatakayompata? Alitaka kuwatia hofu au kuwaimarisha? Kwa nini wanafunzi wake hawakumwelewa?
MASWALI YA KUJADILI: LUKA 19:1-48
- Kwa nini watuza ushuru huwa matajiri? Utajiri wao unatokana na kipato halali? Je kawaida kwa mtoza ushuru kiongozi na tajiri kutafuta kumwona Yesu enzi hizo? Je matajiri huwa na shauku ya kumtafuta Mungu? Kwa jinsi Yesu alivyokuwa akizungukwa na umati wa watu unadhani ilikuwa rahisi kumuona Yesu? Kwa nini Zakayo hakuona aibu kupanda kwenye mkuyu wakati alikuwa mkuu wa watoza ushuru na tajiri? Siri ya matajiri wanaonyenyekea ni nini?
- Pamoja na kuzongwa na watu wengi bado Yesu alitambua Zakayo yupo juu ya mti na anataka kumiona. Hii inakuambia nini juu ya umakini wa Yesu katika kushughulikia changamoto za watu? Kama Zakayo asingeambiwa shuka lengo lake la kumwona Yesu lingekuwa limetimia? Kwa nini Yesu alimwambia Zakayo wokovu umefika nyumbani mwako?
- Kwa nini watu hawakutaka Yesu aende nyumbani kwa Zakayo? Kwa nini Zakayo alitangazwa na Yesu kuwa ni mwana wa Ibrahinu? Je ni kutokana na kutoa mali zake kwa maskini au kutokana na kuwarudishia aliowadhulumu mara nne? Je kuna wakati unaweza kumdhania mtu ni mdhambi kwa anavyoobekana au kwa kazi anayofanya wakati kiroho ni mtu nzuri?
- Je, Yesu bado anatafuta kilichopotea au ameshakipata? Ipi ni jazi kubwa zaidi kati ya kutafuta na kuokoa kilichopotea? Je ufalme wa mbinguni utatolewa kwa watu kulingana na walivyotumia fursa walizopewa na Mungu? Kila atakayeshinda atapewa ufalme wa kuumiliki wenye ukubwa unaolingana na alivyotumika duniani? Kwa nini wasiotaka kutawaliwa wanachinjwa?
- Je ili uwe mtawala ni lazima ukubali kutawaliwa? Kwa nini wenye punda walipoambiwa Bwana anamhitaji hawakuhoji zaidi wala kumzuia? Je upo tayari kuona Yesu akitumia mali yako bila malipo? Kwa nini Mafarisayo hawakupenda jinsi watu walivyokuwa wanamsifia Yesu? Watu wanapokupa heshima ambayo viongozi wako hawapewi unajisikiaje? Je hiyo inakuweka kwenye mazingira ya hatari?
- Kwa nini Yesu hakuwakataza watu wasimsifie? Je ulimwengu leo unajua majira ya kujiliwa kwake? Nani mwenye wajibu wa kuwajulisha watu juu ya kile kinachoujia ulimwengu? Je, kuna namna leo nyumba za ibada zimeanza kuwa pango la wanyang'anyi? Je sala au maombi inachukua nafasi gani katika ibada zinazofanyika makanisani? Unadhani muda mwingi ungetumika kwa maombi ni mabadiliko gani chanya yangetokea?
MASWALI YA KUCHAGUA: LUKA 20:1-47
- Je kulikuwa na kosa lolote kwa Yesu kuwafundisha na kuwahubiri watu habari njema? Je kufundisha na kuhubiri habari njema kwa watu kunahitaji kibali kutoka kwa wenye mamlaka? Unadhani ni kwa nini wakuu wa makuhani, waandishi na wazee walimtokea Yesu kwa ghafla? Kwa nini Yesu hakujibu swali aliloulizwa na badala yake akawauliza swali waliomuuliza?Waliomdanganya Yesu kuwa hawajui ubatizo wa Yohana ulitoka wapi walijua kuwa Yesu asingetambua kuwa wanadanganya?
MASWALI YA KUCHAGUA: LUKA 21:1-38
✅1. Akainua macho akawaona ____________ wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina.
(a) maskini
(b) matajiri
(c) wajane
✅2. Katika siku za mwisho wale watakaokuwa waaminifu watasalitiwa na
(a) viongozi wao
(b) wazazi wao
((c) watoto wao
✅3. Hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na __________ ndipo jueni kwamba uharibifu wake umekaribia.
(a) majeshi
(b) maadui
(c) malaika
✅4. Hayo yatakapotokea ndipo wale walio Uyahudi watatakiwa wakimbilie
(a) Misri
(b) Yerusalemu
(c) milimani
✅5. Basi kila mchana Yesu alikuwa akifundisha hekaluni na usiku huenda kulala katika mlima uitwao
(a) Sinai
(b) Golgota
(c) Mizeituni
MASWALI YA KUJADILI: LUKA 23:1-56
- Chuki ya hawa watu kwa Yesu ilitokana na nini hasa maana aliwatumikia vyema akiwafundisha na kuwaponya? Walikuwa wamechoka na huduma zake au walikuwa wameingiliwa na pepo mchafu? Yesu alilipotoshaje taifa la Kiyahudi? Kuna wakati Yesu alielekeza watu wampe Kaisari yaliyo ya Kaisari na Mungu yaliyo ya Mungu, je hapo aliwazuìa watu wasitoe kodi kwa Kaisari? (Mathayo 22:16-21).
- Licha ya mashtaka waliyoyaibua Wayahudi kwa nini Pilato alisema haoni jambo ovu juu ya Yesu? Kwa nini hakubaki na msimamo huo huo hadi mwisho? Je ni rahisi kusimamia haki ya mtu anayechukiwa na watu wengi? Je Wayahudi walitaka kumchonganisha Pilato na mkuu wake wa kazi Kaisari? Pilato aliona nini hata akamuuliza Yesu wewe ni mfalme wa Wayahudi?
- Herode alifurahi kupelekewa kesi ya Yesu kwa sababu alitamani kumuokoa? Unawezaje kumtambua mtu anayekufurahia huku akiwa na nia ovu? Kwa nini Yesu hakumjibu lolote Herode? Kumshitaki mtu kwa nguvu sana kunakuwaje? Kunatumia zaidi hoja zenye nguvu au nguvu za hoja? Je hakimu anaruhusiwa kumdhalilisha mtuhumiwa ambaye hajahukumiwa? Je, maadui wanaweza kupatana kutokana na wote kuwa na adui wa aina moja?
- Kwa nini waliomshitaki Yesu walibadilika na badala ya kutoa hoja walipiga kelele asulibiwe asulibiwe? Je asiye na hoja mara nyingi hukimbilia kupiga kelele? Kwa nini Wayahudi walikuwa radhi waachiwe Baraba mtu aliyetupwa gerezani kwa ajili ya uuaji badala ya Yesu aliyekuwa akiwaponya? Inawezeka leo watu wakampenda muuaji kuliko mtu mwuungwana?
- Pilato anamhukumu Yesu kwa kuzingatia hoja ya washitaki badala ya hoja yake yeye hakimu aliyepewa dhamana ya kuamua kwa mujibu wa sheria. Hali hii inatokana na nini? Je hali hiyo inashuhudiwa leo kwenye mahakama zetu? Hukumu ikishatolewa mwenye kutekeleza hukumu hiyo ni wale walioshitaki au mtu maalumu aliyewewa na serikali?
- Kwa nini kwenye kesi ya Yesu haikuwa hivyo badala yake washitaki waliambiwa wamfanyie watakavyo? Kwa nini ni wanawake tu waliomuonea Yesu huruma? Je wanawake wana asili ya huruma? Kwa nini Simoni Mkirene ambaye ni mwafrika alimuonea Yesu huruma akamsaidia kubeba msalaba? Je kwa asili Waafrika ni watu wenye huruma? Je uonevu unaofanywa sasa katika jamii zetu una uwezekano wa kuleta majanga makubwa siku za usoni kwa watoto na wajukuu zetu?
- Kwa nini Yesu aliwaombea msamaha watesi wake? Wale waliomdhihaki Yesu ni kweli walikuwa na shaka juu ya uwezo wake wa kutenda miujiza au walikuwa wanashangaa kwa nini hatendi miujiza? Je kumwambia Yesu jiokoe na utuokoe na sisi ni kutukana? Kwa nini baada ya kifo cha Yesu watu wakijipigapiga vifua?
- Je kuna uwezekano wa kuwepo watu wasiokubaliana na uovu unaofanywa na kundi lao kwa maadui zao? Wajibu wa watu hao ni nini ili kuepusha madhara zaidi kwa jamii ya wanadamu? Je uoga huweza kuwafanya watu wasijitokeze uovu unapotendeka katika jamii? Marafiki wa Yesu walikuwa na msaada gani wakati Yesu akipitia vitendo hivi vya uonevu?
MASWALI YA KUJADILI: LUKA 24:1-53
- Kwa nini siku waliyokwenda kaburi wakiwa na manukato yaliyotayarishwa inaitwa siku ya kwanza ya juma? Kwa tafsiri hii Jumapili ni siku ya kwanza ya juma? Kama Jumapili ni siku ya kwanza ya juma hii ni kusema Jumamosi ni siku ya saba ya juma? Kwa nini leo watu wanatatanika kuijua siku ya saba ya juma ni lini? Je hoja kuwa Biblia haijasema Jumamosi ni siku ya saba ya juma bado ina mashiko?
- Ni nani aliyeliviringisha jiwe mbali na kaburi? Watu wawili waliowatokea walioenda kaburini ni nani? Je Yesu alijua siku atakayofufuka? Kwa nini taarifa za wanawake kuwa Yesu amefufuka zilionekana kama upuuzi kwa wanafunzi wa Yesu? Je kilikuwa na haja ya Petro kwenda kaburini kuhakikisha kama Yesu amefufuka kweli? Kwa nini Yesu aliandamana na wale wasafiri wawili waliokuwa wakielekea Emau?
- Je alivutiwa na safari yao au alivutiwa na mazungumzo yao? Yesu hakujua tukio walilokuwa anazungumzia au alijifanya halijui? Kukifanya hujui jambo ni kwa nia ya kutaka kupata taarifa zaidi na msimamo wa wazungumzaji ni kusema uwongo? Kwa maana hiyo Yesu alisema uwongo? Tukio la kuteswa, kusulubiwa na kufa kwa Yesu na kufufuka kwake ilikuwa ni lazima kila aliye Yerusalemu alifahamu?
- Kwa nini lilikuwa tukio kubwa namna hiyo? Kwa nini Yesu anatambulika kama nabii mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na mbele za watu wote? Kwa nini hawakumtambua kama Masihi au Mkombozi wa ulimwengu? Je sababu ya Yesu kujiunga na wasafiri hawa ilikuwa kuwafafanulia yeye ni nani? Je kama wangekuwa wasomaji makini wa Maandiko wangekuwa na sababu ya kupata mkanganyiko kwa mambo yaliyotokea?
- Je karibu mambo yote yanayowatatiza wanadamu yamefunuliwa ndani ya Maandiko Matakatifu? Baada ya kuona wanakaribia kijiji wanachoenda kwa nini Yesu alifanya kama anataka kuendelea mbele? Je wale wanaosema kumpiga mtu chenga unapocheza naye mpira ni kusema uwongo wanazungumziaje tukio hili la Yesu? Macho ya wale wasafiri wawili yalifumbuliwa kutokana na nini? Ni kutokana na walichosikia au walichoona?
- Kwa nini Yesu baada ya kugundulika kuwa ni nani alitoweka? Kama mioyo ya wale wasafiri wawili iliwaka pale msafiri mwenzao alipokuwa akiwafunulia Maandiko kwa nini hawakumuuliza wewe ni nani na mbona mioyo yetu inawaka? Je Yesu asingekubali mwaliko wao nyumbani wangepoteza nafasi muhimu maishani? Je ipo haja ya kupokea ukweli wakati ule ule unapotolewa? Kwa nini waliondoka usiku ule ule kuelekea Yerusalemu wasingoje kupambazuke?
- Kwenye mikono na miguu ya Yesu kulikuwa na nini kilichowathibitishia wanafunzi kuwa alikuwa Yesu kweli? Je Torati imeongea chochote kuhusu yale Yesu aliyotendewa? Kwa nini Torati huonekana kama inayopingana na Kristo na Ukristo? Je kuelewa Maandiko kunahitaji kufunuliwa?
- Je unadhani utabiri wa Yesu kwamba mataifa yote watahubiriwa habari ya toba na ondoleo la dhambi kwa jina lake limetimia? Kwa nini kabla ya kwenda kuhubiri injili ya Yesu wanafunzi walitakiwa wavikwe uwezo utokao juu? Je hata leo uwezo huo unahitajika? Kwa nini baada kuchukuliwa mbinguni walipata ujasiri wa kumwabudu?