Seventh-day Adventist® Church

PASTOR LETTA'S OFFICIAL WEBSITE

Menu

SOMO LA FAMILIA 2020

KANISA LA WAADVENTISTA

 

WA SABATO TANZANIA

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Juma la Umoja

 

wa

 

Familia

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Septemba 6-12, 2020


 

 

1


Ujumbe kwa Wasomaji

 

Wapendwa katika Bwana Pokeeni salaam nyingi kutoka katika Idara ya Huduma za Familia ya Union zetu mbili za Tanzania (Northern Tanzania Union Conference na Southern Tanzania Union Mission).

 

Kwa mara nyingine tena tunawaletea Masomo ya Juma la Umoja wa Familia. Masomo haya yameandaliwa na Idara ya Huduma za Familia ya Konferensi Kuu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato (GC) na kuletwa kwenu na Mch. Davis Fue (Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Familia, Northern Tanzania Union Conference), akishirikiana na Mch. Hebert Nziku (Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Familia, Southern Tanzania Union Mission). Yametafsiriwa na Moseti Chacha wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Lemara – Arusha.

 

Masomo haya 8 ambayo yataanza Jumapili Septemba 6 hadi Jumamosi, Septemba 12, 2020 yamechaguliwa ili kukidhi mahitaji ya sasa ya familia zetu zinazopitia changamoto nyingi. Ndani yake kuna mashauri kwa wanandoa, maendeleo ya watoto, malezi ya watoto walioachwa baada ya talaka, athari za matumizi ya mitandao ya kijamii na kadhalika.

 

Tunaamini kuwa masomo haya yatakuwa na mchango mkubwa katika kukuza umoja wa familia zetu. Hebu Mchungaji, Wazee wa Kanisa na Wakurugenzi wa Idara ya Huduma za Familia washirikiane pamoja ili kuhakikisha kuwa washiriki wote wanahudhuria Juma hili la Maombi.

 

Mungu awabariki!


 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

2


Yaliyomo

Jumapili: Kushauri Wanandoa ….......................... 4

Jumatatu: Kuunda Maendeleo ya Watoto.............. 13

Jumanne: Mitandao ya Kijamii ….........................31

Jumatano: Matunzo ya Watoto walioachwa baada

ya talaka …............................................................... 41

Alhamisi: Uthibitisho wa Wanandoa ….............. 44

Ijumaa: Kambi la familia........................................................... 46

Jumamosi: Unataka Nikutendee Nini?...................... 54


 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

3


Jumapili, Sept. 6, 2020

 

Kushauri Wanandoa

(CURTIS A. FOX)

 

Magari ni mifumo migumu kuelezeka. Yanahitaji uangalizi mkubwa, matengenezo, na aina ya mafuta ya daraja la juu ili yafanye kazi kwa ukamilifu. Inatakiwa kuchunguza vimiminika mara kwa mara ili kuhakikisha havishuki kupita kiwango kilichokusudiwa. Matairi yanahitaji kuzunguka na kutunzwa kwa hali timilifu. Mapendekezo ya watengenezaji ni lazima yafuatwe, bila hivyo kutakuwa na uhakika wa matatizo. Ikiwa magari yanahitaji uangalizi mkubwa namna hii, yakirekebishwa kila mara ili yadumu, kwa nini uhusiano wa wenzi wawili ambao ni mgumu kuelezeka kuliko magari usihitaji uangalizi na utunzaji mkubwa ili kufanya kazi kwa namna Muumbaji alivyokusudia?

 

Rafiki yangu wa kike kabla hajawa mke wangu, alinieleza uzoefu ambao aliwahi kuwa nao mchana wa Ijumaa moja. Akirudi kutoka matembezini akiwa amekaribia nyumba kwake kama mwendo wa dakika 40 hivi, aligundua kwamba mwenendo wa gari lake ulibadilika. Kisha akaona kipima-joto kinasogea kuelekea upande usio sahihi kwa kuashiria kwamba kulikuwa na shida katika injini joto lilikuwa likiongezeka. Mara moja alijua kwamba alitakiwa kuchukua hatua haraka, kwa hiyo akatafuta mahali salama pa kuchepuka kutoka katika barabara kuu ili kutafuta mtu anayeweza kumsaidia kutambua tatizo kwa namna rahisi. Alipata mahali na kuchepuka, lakini moshi wa mateso yake ulikuwa dhahiri, ukipanda kutoka katika injini. Kwa mshangao mkubwa injini ilikuwa kama imekaangwa. Hakuna kitu ambacho fundi wa magari angeweza kufanya


 

4


katika hali ile. Ni dhahiri kwamba alitafuta msaada akiwa amechelewa sana.

 

Makala hii fupi itashughulikia dhana muhimu, inayohusu kushauri wanandoa ifuatayo: Thamani ya kushauri, mienendo inayogusa namna watu wanavyopata uzoefu wa kushauri; namna kushauri kunavyofanyika; na vigezo ambavyo vinaathiri mafanikio ya uhusiano wa kitabibu kati ya wenzi wawili walio kwenye ndoa na mshauri.

 

Je, kushauri wanandoa ni kufanyaje?

 

Kushauri wanandoa ni kumsaidia mtu mmoja au wawili kuona kutoka katika mtazamo wa mtaalamu wa tiba wakati wameshindwa kumudu masuala ya uhusiano wao kwa namna itakayoleta ufumbuzi unaowezekana. Mara nyingi mshauri anaweza kukaa nao – kwa kawaida kwa muda wa saa moja – kwa vipindi kadhaa kwa wiki au miezi kadhaa. Atawasikiliza kwa uangalifu bila kuegemea upande wowote, na kuwasaidia kupitia namna ya mpangilio wa maingiliano yao, na kuweka malengo ya tiba, akionesha jinsi wanavyoweza kuchukua hatua kuelekea katika malengo yao. Ni dhahiri kwamba changamoto zitajitokeza hapo baadaye, lakini hawa wenzi watakuwa wamejifunza mikakati bora ya kukabiliana na matatizo yao katika ushauri na namna ya kuutumia, pia watakuwa wamepata somo kuhusu namna yenye ustawi ya kutatua migogoro na kuendelea kuleta mabadiliko na matokeo chanya kwao wenyewe kila mmoja.

 

Tunapokuwa katika uhusiano wa wenzi, kwa haraka sana tunajikuta katika mpangilio wa utendaji ulio thabiti na usioweza kubadilika mara tu unapokuwa umewekwa. Kwa kawaida mpangilio unatekelezeka, lakini unaweza usitekelezeke na ukawa tishio kwa uimara na ustawi wa uhusiano. Ukihusisha mihemko yote – tamaa ya kulaumu

 

5


au kutetea msimamo binafsi, kutokuweza kuhusiana vema na mwenzi wako, au kupitia uzoefu wa msamaha kwa baadhi ya makosa, kupoteza shauku kwa mwenzi mmojawapo, au masuala halisi ya usalama – mara nyingi ni vigumu kueleza pale tatizo lilipoanzia au kwa nini linaendelea. Kabla muda haujapita, inaweza kuonekana kuwa ni vigumu kubadilisha mpangilio wa maingiliano yaliyo hasi na hawa wenzi wakajikuta wamekwama. Wakati wanapokuwa wamekwama, matokeo ya jitihada zao zote yanakuwa mabaya, yakiwaacha bila kuridhika, wakiwa wamezidiwa bila matumaini.

 

Kwa sababu ya kuona haja ya kujadili suala hili, baadhi ya watu huwageukia marafiki, jamaa wa karibu, wapenzi wa zamani, wana familia, au wengine tu ili kupata msaada. Kwa kawaida yule mtu wanayemtafuta anakuwa ameunganika kimhemuko na mmoja au wenzi wawili walio katika uhusiano, na kwa sababu wanaweza kuwa hawana mafunzo kiasi cha kusaidia watu kutatua matatizo magumu kama hayo, basi majanga yanakuja karibu zaidi nyumbani kwa sababu ya ule ukaribu uliopo na mtu anayejaribu kusaidia. Kutafuta msaada kwa mtu kama huyo wakati uhusiano upo katika hali mbaya ni jambo baya sana. Ushauri mzuri unafanyika kwa ubora na mtu ambaye hayuko karibu sana na mmoja wa wenzi walio katika uhusiano wa ndoa, na atakuwa ni mshauri aliyepitia katika mafunzo na ameweka mipaka ya kimaadili na anatafutwa kwa wakati muafaka kabla uhusiano haujageuka kuwa shubiri. Matabibu wengi wanashauri kwamba ushauri kwa wanandoa unaweza kufuatiliwa kwa miaka sita baada ya kipindi kile ambacho msaada ulitafutwa.

 

Kwa nini watu huwa wanachelewa kutafuta ushauri hadi hapo wanapokuwa wamekaribia mwisho wa uhusiano wao? Watu wengi wanapenda kuamini kwamba wanaweza 6


kushughulikia masuala yao bila kutafuta msaada. Zaidi ya hapo, idadi kubwa ya watu wamelelewa na miiko kuhusi kutafuta ushauri, na hiyo miiko inawafanya wasitafute msaada kutoka kwa mtu yeyote, hata kwa mtaalamu wa tiba. Wanaweza kuamini kwamba kutafuta ushauri ni ishara ya udhaifu, ukosefu wa Imani, au kukubali kwamba kuna tatizo. Wengine kwa makosa wanadhani kwamba wenzi wana pokuwa wamemwamini Mungu, hawawezi kupatwa na matatizo ambayo wao wenyewe hawawezi kuyatatua kwa ushirikiano na Mungu, inawezekana wasiwe na matatizo ya kutatua na Mungu. Hiyo ni dhana potovu na ni dhana iliyowaelekeza wenzi wengi kwenye barabara ya kukata tamaa, majanga, uharibifu, na hatimaye talaka. Wakati mwingine kuna mantiki kukubali uwepo wa tatizo na kutafuta msaada kutoka kwa wataalam mapema kuliko kujifanya jeuri usiyedhurika na tatizo hilo, ukijiridhisha kuwa litatatuliwa kiroho kumbe linaongezeka.

 

Jinsi kushauri wanandoa kunavyofanya kazi

 

Je, kushauri wanandoa kunafanya kazi namna gani? Pale mwanandoa au wenzi wawili wanapokuja na kufanya miadi na mshauri wa ndoa, huyu tabibu anawasikiliza ili kujua kusudi la kutafuta msaada. Kwa kawaida anakuwa akijua fika kwamba kila mmoja atajaribu kueleza tatizo kutokana na mtazamo wake. Wakati huo atataka pia kufahamu kwamba, ni yupi atakayeanza kutaka msaada au ushauri, akiwachunguza kwa uangalifu akianzia wakati wanapoingia, jinsi wanavyokaa, jinsi wanavyoongea au wasivyoongea, jinsi wanavyoitikiana wao kwa wao, mihemuko yao, wanavyogonganisha macho, jitihada za wakati uliopita na zile zilizopo za kujaribu kutatua tatizo lao, mpangilio wa maingiliano yao, utayari wao wa kubadilika, na kadhalika. Mambo yote haya yanayoonesha mwenendo yanachunguzwa kadiri mshauri anavyozungumza

 

7


nao, anavyowauliza maswali, anavyojaribu kuwafanya wacheke na mwitiko wao, wanavyoonesha utayari wa kufanya yale wanayoambiwa wafanye, wanavyofanyia kazi majarida na maandiko wanayoshauriwa kusoma, shughuli za kuwaunganisha, wanavyohimizwa kupunguza nafasi kati yao au na watoto wao, na kuwafanya wadumu kujielekeza katika malengo yao ya tiba. Wakati mwingine inaweza kuwa vigumu sana wakati wa ushauri au hata baada ya kutoka hapo, lakini kujielekeza katika malengo na kutambua umuhimu wa zoezi zima.

 

Zoezi la kubadilisha mwenendo au mpangilio wa utendaji halijawahi kuwa zoezi rahisi. Mara nyingi tunakataa mabadiliko au matazamio ya mabadiliko. Watu wengi wanapenda kuhisi kama vile wanataka kuacha tiba kwa sababu tu mabadiliko hayafurahishi. Ni jambo la kufurahaisha kutambua kwamba hata kama wenzi hawapendi kuingia katika matatizo, bado huwa hawakubali mabadiliko, na mara nyingi wanakuwa na sababu za kutokurudi katika tiba ili kuchakata mabadiliko katika mahusiano yao. Sababu wanazotoa ni pamoja na ratiba zao, ukosefu wa fedha, au wanadai kwamba tatizo limetatuliwa au haliwezi kutatuliwa. Wengine wanaacha kwenda kwenye tiba kwa sababu hawampendi tabibu au wanaamini kwamba tabibu anaelemea upande wa mwenzi mmoja dhidi ya mwingine. Hizi ni baadhi tu ya sababu halisi ambazo watu wanazua ili kukataa mabadiliko.

 

Inawezekana kabisa kwamba washauri wa ndoa wakatenda kinyume na matarajio yako. Lengo la tabibu haliwezi kutambulika kwa wenzi walioenda kutaka ushauri au msaada. Wengine wanaweza kuuliza kwamba ni vigezo vipi vinavyowezesha ndoa kufanikiwa? Hapa chini kuna mambo ya muhimu katika kujibu swali hilo:


 

8


 1. Ni muhimu huyo tabibu kukubalika na wenzi wanaotafuta msaada. Sula la umri kwa watu wengine, au kabila, rangi, uzoefu wa maisha, hali ya uchumi, namna ya kukabili tiba, dini au hali ya kiroho, kukubaliana na mgawanyiko wa binadamu, pamoja navigezo vingine vyote hivyo vinaweza kuathiri urari kati ya wateja na tabibu. Tiba inafanya kazi vyema mteja anapokuwa na Amani na tabibu, akiamini kwamba atapatiwa huduma ya hali ya juu. Hali ya wanadamu kuelemea upande mmoja ni uhalisia wa maisha ya binadamu usiopendeza. Ni dhahiri kwamba hali hiyo ipo. Upande mwingine kunaweza kuwepo na masuala ambayo huyu tabibu anayo pia. Kwa tabibu, siyo vyema kuendelea na zoezi ikiwa kuna hali ya kuelemea upande mmoja hasa anapotoa tiba au ushauri unaotazamiwa kuwa bora. Katika hali kama hii, tabibu anashauriwa kushauriana na wataalamu wenzake, na kuona kama wanaweza kupata ufumbuzi au kumwelekeza kwa mtaalamu mwingine baada ya kumweleza hali iliyopo ya kujikuta anaelemea upande mmoja.

 

 1. Kigezo kingine kinachoweza kuathiri matokeo ya tiba ni kile kinachowafanya wahusika wasihudhurie, au wasiwe makini au waishawishike kuwa tabibu ana uwezo wa kutatua tatizo lao. Maana yake ni nini? Ikiwa mtu atakuja kwa tabibu lakini hataki kuwa pale au hashawishiki na utendaji wa huyu tabibu, ni dhahiri kwamba atajihami, kwa kuonesha kutomkubali, na kutokuwa tayari kujaribu chochote kitakachopendekezewa katika jitihada za kusaidia. Kuna namna nyingine ambayo mtu anaweza kuvurugwa katika mchakato wa tiba. Kwa mfano, ikiwa mtu atakuwa katika hali ya ulevi au ametumia vitu vingine ambavyo vitakuwa vimemwondoa katika utimamu akiwa kwenye matibabu, na kwa sababu hiyo

 

9


akapunguza uwezekano wa matokeo chanya. Katika hali kama hii, tabibu anapotoshwa. Na ikiwa huyo mtu yuko katika ushauri lakini ana mahusiano na mtu mwingine wa nje (kama vile mmoja wa wafanyakazi wenzake, au mtu wa kanisani kwake, na kadhalika), hatakuwa na uwezo wa kuongoza kuelekea katika mabadiliko au hali bora zaidi. Huyo anatakiwa kutiwa moyo ili kuacha mambo yanayomfanya asimakinike katika ushauri na kuutendea kazi kwa jitihada zote.

 

 1. Kutokuwa na uwezo wa kusamehe mwenzi au kupokea msamaha kutoka kwa mwenzi mmojawapo baada ya mapungufu au kushindwa. Mara nyingi hali hii inasababisha kugota na huwa inakuwa vigumu kupiga hatua au kupata mabadiliko katika mahusiano pasipokuwepo na msamaha. Wapo watu wanaoenda kutafuta tiba, hata wakabadilisha matabibu, lakini wanashindwa kupata uzoefu wa kukua kwa sababu pengine wamejikuta katika hali hiyo kama matokeo ya mgogoro wa zamani ambao haukupata ufumbuzi. Hadi hapo atakapomweka huru mtu kutoka katika kushindwa au hapo atakapokubali msamaha kwa kile kilichotendeka, ndipo watakapoweza kuishi chini ya wingu litakaloleta mguso katika hali ya hewa ya uhusiano wao. Ni kweli kwamba mara nyingi tunaomba kuwa, “Utusamehe deni zetu kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.” Lakini ombi hili linafanyika kabla hata ya tendo lenyewe kutokea katika uhusiano. Watu wengi wanashindwa kusamehe hasa wanapokuwa wameathirika wenyewe kwa vitendo vya wenzi wao. Ni namna gani tunavyopitia katika uzoefu na kufanyia kazi neema ya Mungu – au tunavyoshindwa kufanya hivyo – inaweza kuwa na mguso chanya au hasi kwa matokeo ya tiba. Tunamshukuru Mungu kwamba upendo wake na neema yake vinaangaza ndani na nje

 

10


ya mioyo yetu. Tunapopata uzoefu wa upendo wake kwetu, ndipo tunapoweza kugawa upendo huo kwa wengine. Kwa hiyo neema ya Mungu ikiwa juu ya maisha ya wenzi walio katika ndoa inaweza kuwa na mguso kwa matokeo ya ushauri wa ndoa. Ukweli ni kwamba, watu wengi wanashindwa kuhusisha neema katika maisha yao binafsi na katika uhusiano wao.

 

 1. Nimegundua kwamba ukosefu wa matumaini ni kigeza kikubwa ambacho kina uzito katika matokeo ya tiba. Wengi wanakata tamaa kwa mahusiano yao. Wanadhani kwamba hakuna sababu ya kuendelea nayo. Wanahisi kwamba wamejaribu kila namna na hakuna matokeo yoyote, na kwa hiyo wanafikia hitimisho kuwa hakuna kitakachoweza kusaidia. Wengine wanakuwa wamejiwekea ukomo wa muda. Wanataka mambo yafanyike mara moja huku wakisahau kwamba wana maisha yao yote pamoja kuweza kushughulikia masuala yao. Hali kama hiyo inawafanya wapoteze ustahimilivu na hatimaye kukata tamaa. Wengine wanataka uhusiano mkamilifu, wanaposhindwa kupata huo ukamilifu basi wanakata tamaa. Wengi wanaondoka katika uhusiano hasa wanaposhindwa kuona kesho yao ng’ambo ya haya mambo ya sasa yanayowapa machungu na kuwakatisha tamaa. Tabibu angeweza kufaya vyema kuhakikisha kwamba vipindi anavyokutana nao havitumiki tu kwenye kujilisha katika hali hasi ya maisha ya hawa wenzi isiyoonekana kurekebika. Badala yake anatakiwa kuwaongoza kuangalia ng’ambo ya upeo unaoonekana kwa macho yao. Ikiwa tumaini litafufuka, matokeo bora zaidi yanaweza kuonekana kwao wote.

 

 1. Ieleweke kwamba mtaalamu wa matibabu ni yule ambaye ana mafunzo, uzoefu, na stadi za kuelewa misukumo ya wenzi na familia na kuitumia katika tiba na katika maisha ya hao wenzi au familia.

 

11


Kushauri ni sayansi lakini pia ni Sanaa. Mshauri wa ndoa anapoweza kuunganisha watu wawili, nao wakabaki katika muunganiko, akiwasaidia kupitia katika masuala yanayowakabili, ndipo atakapopata uzoefu ulio mzuri usioelezeka. Nimekutana na watu wengi ambao wamezungumza kuhusu mibaraka waliyopata kupitia kwa mshauri wa ndoa. Walitambua uhitaji wao wa msaada na kutegemezwa, wakachukua hatua, wakapambana dhidi ya mila na desturi, wakajitoa mhanga, wakapitia katika uzoefu na kujifunza stadi nyingi za kumudu au kutatua matatizo mengi waliyokuwa wakikabiliana nayo katika maisha yao mara kwa mara. Sasa wanajua kwamba katika maisha, watu halisi wanaweza kukumbana na matatizo halisi na kwamba watu wengine walio halisi wanaweza kuwasaidia kukabili na kushinda hayo matatizo. Sasa wanajua kwamba Mungu anatumia baadhi ya wataalamu kama vyombo vyake vya uponyaji hasa katika nyakati ngumu za maisha yao, na kwamba katika baadhi ya mazingira ya matibabu, Mungu anatimiza mapenzi yake katika maisha yetu.

 

Ndoa ni mbaraka wa ajabu na malezi ya yule ambaye umebarikiwa naye ni uamuzi mkubwa sana. Wakati mwingine itaonekana kama vile ni rahisi, lakini siyo siku zote. Ikiwa magurudumu yatakuwa yanazunguka katika matope, jitihada za kuzungusha hilo gurudumu zinaweza kusababisha kukwama zaidi. Msaada kutoka nje ya uhusiano unaweza kuwa ndiyo ufumbuzi wenye maana unaohitajika. Unaweza ukapiga kelele ili usaidiwe au ukamhimiza mwenzi wako kufanya hivyo ikiwa utaona kuwa ndiyo haja. Kutambua haja hiyo mapema ndiyo hatua itakayokuwa ya maana na yenye kusaidia hawa wenzi kufikia ukamilifu na kupata uzoefu mkuu kwa kipindi chote cha ndoa yao.


 

12


Jumatatu, Sept. 7, 2020

 

Kuunda Maendeleo ya

Mtoto Wako,

 

(KATELYN CAMPBELL NA JOSEPH KIDDER)

 

“Wazazi wanapaswa kuelekeza kwa watoto wao maagizo na mafunzo wakiwa bado wachanga hadi hapo watakapokuwa Wakristo. Wanawekwa kwenye ulinzi na mafunzo kutoka kwetu siyo kama warithi katika kiti cha enzi cha himaya ya kidunia, lakini kama wafalme kwa Mungu, ili kutawala vizazi vyote.”1 Katika aya hii iliyonukuliwa kutoka katika kitabu cha Ellen G. White cha Wazee na Manabii, tunaweza kuona dhahiri kwamba jukumu la wazazi ni la muhimu sana. Kina baba na kina mama wamepewa wajibu wa malezi kwa watoto ambao Mungu anawathamini. Wanatakiwa kuwafundisha, kuwaelimisha, na kuwafinyanga kwa namna iliyo bora huku wakiwawezesha.

 

Jambo moja la muhimu ambalo wazazi wanaweza kufanya kwa ajili ya watoto wao ni kukuza mtazamo wa Kibiblia kuhusu dunia ndani ya moyo wa mtoto. Kufanya hivi kutamfanya mtoto wa kike au wa kiume kujengeka katika mapito yenye uhusiano ulio chanya na Yesu Kristo. Katika Makala hii yenye sehemu tatu zinazofuatana tutajadili mtazamo wa Kibiblia kuhusu dunia, ngazi za maendeleo ya watoto, na kile ambacho wazazi wanaweza kufanya ili kuleta mguso kwa watoto wao na kuwajenga katika Bwana. Huu ndio wajibu wa kimbingu ambao wazazi wamepewa.

 

Kutoka katika kuzaliwa kwa mtoto hadi kufikia umri wa ujana, mama, baba, na wasaidizi wengine wanaohudumia watoto wanajaribu kushikilia huku kuyumba na mguso katika maisha ya mtoto. Katika utafiti uliofanywa na Taasisi

 

1

Ellen White, Patriarchs and Prophets (Napa, ID: Pacific Press, 2002), 244.

 

13


ya Fuler Youth, iligundulika kwamba “wazazi wanaendelea kuwa na mguso mkubwa kwa Imani ya watoto wao.”2 Kwa kawaida baada ya utoto, mvuto wa wazazi unapungua, wakiwa na wenzao wa rika moja, shuleni, vyombo vya mawasiliano, na vitu vinavyofanana na hivyo, vinakuwa na mvuto mkubwa kwa mtoto. Hata hivyo ni katika miaka hii ya utoto ndipo mivuto ya wazazi inapokuwa mikubwa kiasi kwamba mtazamo wa kidunia kimsingi unajengeka. Kwa hiyo ikiwa wazazi watawasaidia watoto wao kujenga msingi imara wa Kibiblia kabla ya kufikia umri wa ujana, watakuwa wamewatayarisha kwa ajili ya kujitoa kikamilifu katika maisha ya Kikristo siku zote za maisha yao.

 

Ndiyo maana katika Makala hizi tunajielekeza katika malezi ya watoto kutoka katika umri wa uchanga hadi miaka 12 au 13 hivi. Hapa tutajadili kile ambacho ni mtazamo wa Kibiblia kuhusu dunia, kujua jinsi ya kuhusisha na mtazamo wa kidunia katika hatua mbalimbali za maendeleo ya mtoto, na kuangalia katika mifano nyeti ya Kibiblia ya mivuto ya wazazi kwa mtazamo wa mtoto. Wazazi wanaweza kutumia miaka hii ya uchanga ya maisha ya watoto wao kwa maombi na tafakuri inayofanyika kabla, kwa kukusudia ili kuwa na mvuto wa milele.

 

Mtazamo wa Kibiblia kuhusu Dunia

 

Kwa sababu ya Makala hii, tutafafanua mtazamo wa kidunia kama mkusanyiko wa dhana za msingi kuhusu maisha na ulimwengu, kujenga maono ambayo yanaweza kutumika na mtu kuangalia. Mtazamo wa mtoto wako kidunia ni kile ambacho kitamsaidia kumwelekeza yeye katika maisha yake.

 

 

2      Dustin McClure, “Helping Kids Keep the Faith,” Fuller Youth Institute, accessed

March 28, 2019, https://fulleryouthinstitute.org/articles/helpingkids-keep-the-faith.

14


Kama vile tu ramani inayoweza kubadilisha mandhari kuwa ishara za maeneo mbalimbali zinazotofautishwa, mtazamo wa kidunia unatoa namna ya kutafsiri uhalisia wa dunia. Mtazamo wa kidunia ambao mtoto wako atajenga, utajibu swali la msingi kutoka kwake kwamba, Mimi ni nani? Kwa nini nipo hapa? Nimetoka wapi? Ninaenda wapi? Ni nini ambacho ni halisi? Ni kipi ni sahihi na kipi siyo sahihi? Maswali yote haya na mengine mengi yanajibiwa na mtazamo ambao mtoto wako anajenga, akiunda mtazamo wake wa dhana za msingi. Kila mmoja ana mitazamo ya kidunia: uibukaji, uumbaji, dhana ya hatima ya mwanadamu iliyo nje ya uwezo wake kubadili, na ile hali ya ubinadamu, ni mifano michache tu. Dhumuni kubwa la Makala hii ni kukusaidia kujenga mtazamo wa Kibiblia ndani ya watoto wako kuhusu dunia, ambao utawaongoza kuishi maisha ya Kikristo kwa utimilifu wake wote.

 

Hebu tujiulize kwamba mtazamo wa Kibiblia kuhusu dunia ni nini? Kuna misingi kadhaa ya jambo hili. Mtazamo wa Kibiblia kuhusu dunia unaegemea katika Maandiko kama ufunuo wa kimbingu wenye mamlaka. Mungu kama muumbaji, tabia yake ya haki na upendo, mpango wake kwa maisha yetu, kafara ya Yesu iokoayo, neema ikomboayo, na amri kumi ndizo kitako cha mtazamo wa Kibiblia kuhusu dunia. Hatimaye, mtazamo wa Kibiblia kuhusu dunia umejengeka katika Imani kwa Mungu na kujitoa kikamilifu kumfuata yeye. Kama vile James Sire anavyodokeza kuwa, “Katika mtazamo wa Kibiblia kuhusu dunia kwa kifupi, kila kitu kwanza kabisa kinaamuriwa na asili na tabia ya Mungu.”3 Kupitia katika mboni hii, Yesu anaonekana kama Muumba, Mwokozi, Mkombozi, na Rafiki, na kwa kutumia mtazamo wa Kibiblia kuhusu

 

3                       James Sire, Naming the Elephant: Worldview as a Concept (Downers Grove, IL:

Inter-Varsity Press, 2004), 55.

15


dunia, tunapata uwezo wa kufikiri kama Yesu, na kutimiza maneno ya Paulo katika Wafilipi 2:5 kuwa, “Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu.”

 

Utafiti uliofanywa na George Barna umeonesha kwamba watoto wengi wanaanza kujenga mtazamo wao wenyewe wa kidunia wanapokuwa na umri wa miaka miwili. Ile dira ya mtoto ya maadili inakuwa katika utendaji katika umri wa miaka 9, na pale mtoto anapokuwa amefikisha umri wa miaka 13, mtazamo wa kidunia unakuwa umejengeka kwa ukamilifu na upo katika utendaji.4 Uzoefu mpya mwingine wowote utakuwa unachujwa kupitia katika mtazamo wake huu wa kidunia katika kutafsiri na kuelewa. Kama vile tu maendeleo ya mwili na akili yalivyo muhimu katika utoto, kujenga mtazamo wa kidunia kuanzia pale mtoto anapozaliwa hadi miaka 13 kunaandaa mapito kwa ajili ya siku za baadaye za mtoto.

 

Dhana isiyohakikishwa na matokeo ya kudhania ambavyo vinafanya mtazamo wa mtoto wa kidunia siyo tu kwamba vinajibu swali la msingi kuhusu dunia, lakini vinasaidia pia kujenga maadili ya mtoto na matakwa yake, ambayo hatimaye yanaongoza mwenendo wa mtoto na uwezo wake wa kufanya maamuzi. Hakuna uamuzi unaofanyika bila kuwa na mtazamo wa kidunia. Ili kufanya maamuzi ambayo ni chanya na yenye ustawi, mtoto anahitaji mtazamo wa kidunia ulio chanya na wenye ustawi. Mtazamo wa Kibiblia kuhusu dunia unaweza kuwasaidia watoto kufanya maamuzi yenye mantiki ambayo yatamheshimu Mungu na kuwa na faida kwa wengine pia kama vile wao wenyewe. Hili ndilo jambo ambalo Mungu anataka kuona

 

4                      Barna Group, Ltd., “Changes in Worldview Among Christians over the Past 13 Years,” March 9, 2009https://www.barna.com/research/barnasurvey-examines-

changes-in-worldview-among-christians-over-the-past-13-years/.

16


katika maisha ya watoto wake: “…mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.” (Yohana 10:10).5 Mtazamo wa Kibiblia kuhusu dunia una mambo ya kutoa: fursa ya kuishi maisha ambayo Muumba alikusudia tuishi.

 

Hatua za Kujifunza

 

Jean Piaget aliyekuwa mwana saikolojia maarufu aliweka msingi imara kwa uelewa wa maendeleo ya watoto kiakili. Alipendekeza kwamba maendeleo ya utambuzi wa mtu yanatokea katika hatua nne za msingi.6 Tangu kuzaliwa hadi umri wa miaka 2 ni hatua ya kujenga “sensorimotor” (ukuaji wa neva za fahamu). Wakati huu, mtoto anajifunza kutoka katika kutumia neva za fahamu binafsi akiingiliana na dunia inayomzunguka. Kujifunza kunatendeka kwa kugusa, kuonja, kutazama, kunusa na kusikia. Dunia inaanza kuwa katika mpangilio kwa mtoto kadiri anavyokutana na vitu vilivyomo na kuvichezea. Wazazi wanaweza kuwafundisha watoto wao katika mwelekeo wa neva za fahamu, kupitia katika kuwaruhusu waone, wasikie, waguse, na kutenda kwa namna ya kuielewa dunia. Hapa pana mifano kadhaa: Kwa mwonekano waoneshe watoto picha za wanyama au watu waliopo kwenye Biblia; imba na watoto wako nyimbo za kwenye Biblia; waongoze katika kukunja mikono wakati wa kuomba; wapatie matawi, mawe, au vitu vingine kutoka katika asili ili waguse na kushikilia. Kadiri unavyowaunganisha watoto wako kwa Yesu kupitia neva zake za kufahamu, ndivyo mtoto anavyoendelea kupata uelewa wake.

 

5                      Unless otherwise noted all Bible quotes are taken from the Swahili Union Version (SUV)

 

6                      Saul McLeod, “Piaget’s Theory of Cognitive Development,” Simply Psychology, accessed March 28, 2019. https://www.simplypsychology.org/piaget. html#stages.


 

17


Kuanzia umri wa miaka 2 hadi 7, mtoto yuko kwenye hatua ya kujitayarisha kuingia katika utendaji. Wakati huu, kumbukumbu na fikra zinaanza kujengeka, na dhana za mambo ya nyuma, ya wakati huu uliopo, na ya usoni yanathibitika. Dhana za ishara zinaanza kuwa na maana kwa mtoto, kwa maana kwamba sasa mtoto anaweza kutambua kuwa neno au umbo fulani linaweza kuwakilisha kitu fulani. Kuwafundisha watoto katika hatua hii ya umri maana yake ni kutumia uwezo wao wa kufikiria au kujenga dhana. Wahimize kuchora visa vya Biblia, au waunganishe watoto wako katika kuigiza visa vya Biblia. Unaweza kuwapeleka kwenye bustani za kufugia wanyama pori, madimbwi ya kufugia samaki, au kwenye hifadhi za wanyama na kuwataka wajenge taswira ya Yesu akiumba mimea, miti, na wanyama.

 

Ruthie Jacobsen katika kitabu chake cha “Putting Their Hands in His” ameandika kuwa, “Yule bingwa wa kuelezea visa – yaani Kristo – mara nyingi alitumia maumbo katika asili kusaidia katika kuzamisha ukweli mkubwa wa kiroho. Alitumia vitu vya asili vinavyoonekana ambavyo wasikilizaji wake walikuwa na uzoefu navyo – mashamba ya nafaka iliyokomaa, mpanzi akipanda mbegu zake, kondoo aliyepotea, na kadhalika. Kuna mafundisho makubwa ya kidunia tunayopata kutoka katika asili. Baadhi ya mafundisho hayo yanaweza kuwa yanatisha hata kuwaogopesha watoto, lakini hata katika uhalisia wa asili, kuna ukweli wenye nguvu. Kuna visa pia na mafundisho ya ukuu na uweza mkubwa wa Mungu.”7 Kwa kuwa katika hatua hii ndipo watoto wanapopata uelewa wa muda, unaweza kuelezea kisa cha Bustani ya Eden, uwepo wa Mungu katika maisha yetu wakati huu, na kuja kwake

 

7              Ruthie Jacobsen, Putting Their  Hands in His (Pittsburgh, PA: Autumn House,

 

2001), 63.

18


mara ya pili kulikokaribia ili wapate kuelewa ule mstari wa dunia hii wa wakati. Unaweza pia kuanza kuwafundisha watoto wako sehemu ya Maandiko inayohitaji kukaririwa, ukiwazawadia kwa jitihada zao: katika hatua hii, watoto wengi watakuwa tayari kutaka kukariri. Kadiri mtoto wako anavyojenga taswira, dhana ya wakati, na uwezo wa kumbukumbu vyote ni vya msingi kwa kumsaidia katika kujifunza.

 

Umri wa miaka 7 hadi 11 ndio umri ambao hatua ya kujizatiti kiutendaji inatokea. Mtoto katika hatua hii anaanza kujenga namna ya kuchakata mawazo kwa mantiki. Zoezi la kufikiria na kutatua matatizo linakuwa ni kitu ambacho mtoto anafanya ndani kwa ndani katika fikra zake bila kugusa au kusaidiwa na vitu vya nje. Wakati huu unaweza kumpitisha mtoto wako katika mchakato wa dhana, kweli na mpako. Kwanza wahadithie visa vya Biblia na kueleza elimu inayoptikana katika Maandiko – hizi ndizo dhana halisi. Mara tu dhana zinapokuwa zimejengeka, jadili masomo wanayoweza kujifunza kutoka katika visa hivyo, na aya za Biblia – hizi ndizo kweli. Hatimaye zungumza na mtoto wako namna kweli zinazopatikana katika Biblia zinavyoleta tofauti katika maisha yake na hata namna haya masomo na dhana yanavyoweza kushirikishwa wengine – haya ndiyo matumizi. Kufanya hivi kutawaongoza kwenye kukua kiroho katika misha ya mtoto wako na kuhakikisha ukomavu. Katika umri huu, watoto wataweza kufikiria dhana hizi kwa kina huku wakiwa na upevu wa mawazo na kwa mantiki, kwa hiyo uwe na uhakika wa kuwahusisha katika aina hii ya fikra.

 

Katika umri wa miaka 11 na kuendelea, hatua ya utendaji rasmi inajitokeza ikionesha uwezo uliothibitika wa mtoto kufanya kazi kwa matiki katika matatizo ya kikili. Watoto wanaweza kutambua dhana za kuwazika akiziruhusu 19


kujitokeza kuanzia katika hali rahisi hadi katika ukweli thabiti na wa kina, dhana zinazoendelea kubadilisha maisha. Kusoma Maandiko kunaweza kutoa zaidi ya taarifa zinazohitajika: kunaweza kuwa na badiliko. Wakati huu, wazazi wanaweza kufundisha watoto wao kwamba sehemu ya Maandiko ni kwa ajili ya kukua kiroho, ukomavu, kuendeleza hekima yao na kuwapa fursa za utakaso. Huu ndiyo umri ambao hali ya kiroho ya mtoto kwa uhakika inaanza kuwa yakwake mwenyewe. Ni muhimu kuhimiza watoto kuchukua visa muhimu vya Biblia na kuvifanya vya kwao wenyewe vinavyowasaidia katika maisha ya umilele. (Wafilipi 2:16)

 

Kwa kuweka hatua hizi za kujifunza mawazoni, wazazi wanaweza kuwafundisha watoto wao vyema kumhusu Mungu na Biblia, wakikutana nao pale penye maendeleo ya utambuzi wao. Hata hivyo bila kujali kiasi ambacho wazazi watawafundisha watoto wao, pengine ni muhimu kwamba wawafundishe kuhusu tabia ya Mungu – upendo wake, jinsi anavyotukubali, msamaha wake, wema wake, na kadhalika. Ellen G. White anaeleza jinsi wazazi wa Yesu walivyomfanyia hayo tuliyoyataja hapo: “Walimkumbusha Yesu utambulisho wake kama Mwana wa Mungu. Walimfundisha kupitia kwenye nyimbo na kupitia katika maumbile ya asili. Kadiri walivyoendelea kumfundisha, wao wenyewe walikua na kujifunza zaidi kumhusu Mungu na Maandiko yake.”8 Kwa jinsi hiyohiyo wazazi wa Yesu walikua katika kumjua Mungu kwa namna iliyo bora zaidi wakifundisha tabia yake, wazazi wa leo pia wanaweza kukua katika uelewa wao wa Mungu kadiri wanavyowafundisha watoto wao.

 

 

 

8

Ellen White, Youth’s Instructor (Sept. 8, 1898).

 

20


Athari ya Utamaduni

 

Uchunguzi wa hivi karibuni uliofanywa na Taasisi ya Wamarekani ya Utamaduni na Imani (American Culture and Faith Institute) ulidhihirisha kwamba nusu ya watu wazima katika nchi ya Marekani (51%) wanaamini kwamba ukengeufu wa sasa katika utamaduni una athari hasi kwa watoto na vijana.9 Uchunguzi huu ulionesha kwamba asilimia 93 ya watu wazima ambao wanadai mtazamo wa Kibiblia kuhusu dunia, wanaamini kwamba utamaduni unaathiri watoto kwa namna hasi na hata watu wazima (48%) ambao hawakubaliani na mtazamo wa Kibiblia kuhusu dunia bado wanasema kwamba hali ya kawaida ya utamaduni wa nchi inaathiri watoto kwa namna hafifu. Ikiwa sisi kama Wakristo tutakuwa na nia ya kutegemeza ukuaji wa kiroho wa watoto wetu, litakuwa ni jambo la hekima kwa kuona namna vipengele vya utamaduni vinavyowagusa na ni nini kinachoweza kufanyika ili kupunguza athari hasi hazi na kuongeza athari chanya. Hakuna mtu anayeishi katika ombwe: sisi sote tunaathiriwa na kile kinachoendelea katika mazingira tunayoishi na kila kitu kinachotuzunguka.

9                      George Barna, “Americans Worried About Children,” June 28, 2017. http:// www.georgebarna.com/research-flow/2017/6/28/

americans-worried-about-children.

 

21


Nguvu zinazoumba Mtazamo wa

Kidunia wa Mtoto wako.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Katika umbo hilo hapo juu, kuna baadhi ya vipengele vya msingi vinavyoweza kuwa na mvuto kwa mtoto. Mtoto anapokuwa mchanga, wazazi wake watakua na mvuto mkubwa katika maisha yake. Kadiri mtoto anavyoendelea kukua, vipengele vingine vinakuwa na mvuto kwake zaidi kuliko wazazi. Hata hivyo, ikiwa wazazi watakusudia kumfundisha mtoto wao na kumjengea mapito mazuri katika huo umri wa uchanga, atajua namna ya kupenya katika vipengele vya maisha vyenye mvuto kwa namna iliyo bora hapo baadaye. Ni muhimu katika utoto wazazi wakachukulia kwa uangalifu vipengele vya utamaduni wanavyotaka watoto wao wajihusishe navyo, na kwamba ni sehemu zipi za utamaduni wanazotaka kuwaepusha.


 

22


Kwa hakika ukiuliza swali hili, ni kama kuuliza aina ya kautamaduni kadogo unakotaka kujenga ambako ni “aina ya utamaduni tofauti unaoshirikisha kundi dogo ambalo mara nyingi lipo katika eneo fulani au ndani ya taasisi.”10 Pamoja na kwamba familia yako ipo katikati ya utamaduni mahalia – wenye lugha yake, mila na desturi zake, vyombo vya habari vya aina yake, na kadhalika – bado familia yako hiyo ni utamaduni wa pekee ulio tofauti. Inaweza kuathiriwa na vigezo vya desturi zinazoizunguka, lakini ina kanuni zake zilizowekwa, mila na namna ya kuendesha maisha. Wazazi wakiwa nyumbani, wanaweka vigezo vinavyohusu desturi za nyumbani. Kadiri watoto wanavyokua, wataanza kuwa na mchango katika hako kautamaduni kadogo, lakini familia inapoanza, ni mama na baba ambao wanachangia katika sehemu kubwa ya maendeleo ya hako kautamaduni kadogo. Ni ndani ya haka kautamaduni kadogo ndipo watoto wataanza kujifunza dhana za msingi zisizohakikiwa kuhusu ulimwengu unaowazunguka kadiri mtazamo wao wa kidunia unavyoanza kujengeka. Kulingana na mamlaka nyingi zilizoko kwenye maendeleo katika utoto,11 ni mama na baba (ambao kimsingi ndiyo walezi) ndio wenye mvuto mkubwa katika ukuaji wa mtoto. Kwa hiyo swali kwa wazazi linabakia kuwa: Ni aina gani ya haka kautamaduni kadogo unayotaka uwe nayo nyumbani kwako?

 

Ikiwa unatafuta kulea mtoto wako kwa mtazamo wa Kibiblia kuhusu ulimwengu, haka kautamaduni kadogo ka familia yako kwa makusudi kabisa katahitaji kuundwa kwa namna ya kukuza mtazamo huu wa kibiblia kuhusu

 

10                  Open Education Sociology Dictionary, accessed March 28, 2019. https:// sociologydictionary.org/microculture/

 

11                  See these examples: Damon Verial, “The Effects of Environment on a Child’s Behavior,” accessed March 28, 2019. https://www.livestrong.com/article/122830-effects-environment-childsbehavior/;and https://www.bartleby.com/essay/

The-Effects-of-the-Environment-on-Children FKJBTZUATJ

23


dunia. Ellen G. White anaandika kuwa, “Kwa maombi, wakiungana baba na mama wanatakiwa kubeba wajibu mkubwa wa kuongoza watoto wao katika njia iliyo sahihi.”12 Mahali pazuri pa kuanzia hizi fikra endelevu za kautamaduni kadogo ni kuchunguza kile ambacho Maandiko yanapendekeza: “Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.” (Wafilipi 4:8). Ikiwa unahusianisha lugha ambayo ni ya upendo, vyombo vya habari ambavyo ni safi, kanuni ambazo ni za haki, na mambo kama hayo, utakuwa unajenga mfumo wa nje utakaogusa watoto kwa namna iliyo chanya.

 

Chunguza namna hako kautamaduni kadogo kalivyopangiliwa nyumbani kwako – muziki unaochezwa nyumbani kwako, aina ya Sanaa zinazoning’inia kwenye kuta za nyumba yako, visa mnavyosoma pamoja nyakati za jioni. Je, ni vyenye uadilifu? Je, vyote hivyo vinafundisha kumhusu Mungu? Katika kizazi hiki cha kutanguliza teknolojia na kujielekeza katika vyombo vya habari, tunapendekeza kwamba uweke ukomo wa muda kwa familia kukodolea skrini, tathmini kile ambacho watoto wako wanatazama na kuweka mfano chanya kwa wao kufuata. Chagua kwa uangalifu na tafakuri maudhui ambayo yatajenga familia yako. Tumia muda kujadili kile ambacho mnatazama au michezo mnayocheza, ukielekeza mafundisho kuhusu maadili na kuchukulia kile ambacho Mungu angefurahia au kutokufurahia.13


 

12

Ellen White, Review and Herald (Silver Spring, MD: Pacific Press, 2002).

13                  Joseph Kaidder and David Penno, “A Christian Perspective on Watching Secular TV Programming,” Healthy Families for Eternity

(Silver Spring, MD: North American Division Corporation of the Seventh-day Adventist

 

24


Lakini usiachie desturi zako kuwa ndizo zinazokaa katika kochi siku nzima! Jaza muda wa familia yako na mambo ya kufurahisha na shughuli zinazothibitisha maudhui mazuri. Inaweza kuwa rahisi kufikiria mambo yote ambayo hautaki yawepo katika kautamaduni kadogo ka familia yako. Lakini fikiria kielelezo kutoka kwa Yesu:

 

“43 Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate. 44 Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa. 45 Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.” (Mathayo 12:43-45)

 

Usiondoe uovu katika nyumba yako na kuiacha ikiwa tupu. Ijaze na mambo mema, na uwepo wa Mungu. Shiriki mambo mazuri na watoto wako. Cheza nao michezo, wasomee vitabu, pika chakula, tembea nao katika mazingira na kuwapa nafasi ya kuvumbua mazingira yalivyo, na ukiwa katika kutembea wafundishe kuhusu Baba wa mbinguni. Mtunga Zaburi aliandika kuhusu furaha ya maisha yanayopitishwa mtu akiwa na Mungu akisema kuwa,

 

“Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele.” (zaburi 16:11)

 

 

Wazazi wakiwa na mvuto wenye ustawi wanaweza kujenga desturi kwa watoto wao na kupitia katika desturi hii wakapata uzoefu wa ukamilifu wa furaha ya Mungu na kukuza mtazamo wa Kibiblia kuhusu dunia.

Church), 61-62.

25


Mvuto wa Wazazi: Fundisho kutoka katika maisha ya Timotheo.

 

Katika Agano Jipya, Timotheo ni mfano wa msingi wa kile ambacho kijana mdogo anaweza kuwa kama atakuzwa na mtazamo wa Kibiblia kuhusu dunia. Timotheo alikuwa mchungaji na mwinjilisti sambamba na Paulo, lakini ilimchukua miaka kadhaa ya kunidhamishwa ili awe mhubiri mashuhuri wa Injili. Maandiko yanatuambia kwamba familia yake ilikuwa na sehemu kubwa katika ukuaji wake wa kiroho. Katika waraka wa kwanza kwa Timotheo, Paulo anaawaandikia vijana wadogo akisema, “Walakini mwisho wa agizo hilo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki.” (1 Timotheo 1:5).

 

Hawa wawili, mama yake Timotheo na bibi yake walimlea kwa Imani katika Bwana. Mivuto yao ilikuwa na mchango mkubwa kiasi kwamba waumini katika maeneo yaliyowazunguka walikuwa na mambo mengi chanya ya kusema kumhusu. “Basi akafika Derbe na Listra, na hapo palikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, mwana wa mwanamke Myahudi aliyeamini; lakini babaye alikuwa Myunani. Mtu huyo alishuhudiwa vema na ndugu waliokaa Listra na Ikonio.” (Matendo 16:1, 2). Kabla hata Timotheo hajakutana na Paulo, Imani yake katika Bwana ilikuwa dhahiri. Ellen G. White anaandika kuwa, “uchaji Mungu na mvuto wa maisha ya nyumbani kwao, havikuwa katika mpangilio hivi hivi, bali safi, wenye maana na usioghoshiwa na hisia potovu. Mivuto ya kimaadili ya nyumbani ilikuwa na uzito. Neno la Mungu lilikuwa kanuni iliyomwongoza Timotheo. Alipata maagizo kutoka kwa aya moja ya Maandiko hadi nyingine, kipengele kimoja hadi kingine, hapa kidogo na huku kidogo. Taswira za mpangilio wa hali ya juu zilibakia katika fikra zake. Wale

 

26


wote waliomwelekeza kule nyumbani walikuwa shirika na Mungu katika kumwelimisha huyu kijana namna ya kuchukuliana na mizigo aliyokuwa anatazamia katika maisha yake kwenye huo umri mdogo.14 Sehemu kubwa ya kupandikiza huo mtazamo wa Kibiblia kuhusu dunia kimsingi unaanza na wazazi wa mtoto pamoja na walezi wake wa awali.

 

Jukumu la Jumuiaya ya Imani

 

Ingawaje tumekuwa tukizungumza kuhusu mvuto wa wazazi, waumini wote wanatakiwa kuhusika katika ukuaji wa kiroho wa watoto, vijana wadogo, na vijana wakubwa. Ni dhahiri kwamba katika maisha ya Timotheo, baada ya Paulo kuamua kumweka chini ya mbawa zake, ule mchakato wa ushauri ulianza. Katika kitabu cha Wafilipi 2:22 Paulo anazungumza kumhusu Timotheo katika kanisa la Filipi akisema, “Ila mwajua sifa yake, ya kuwa ametumika pamoja nami kwa ajili ya Injili, kama mwana na baba yake.” Kiungo imara cha uhusiano kilikuwa kimejengeka kati ya wawili hawa. Paulo alikuwa amekusudia kuhusu uhusiano wake wa karibu na Timotheo, kumfundisha, na kumwezesha na fursa za kutumika na kupanua upeo wa ufalme wa Mungu.

 

Hata hivyo Paulo alikuwa na Imani na matumaini makubwa kwa huyu kijana. Anasema kuwa, “Kwa sababu hii nimemtuma Timotheo kwenu, aliye mwanangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakayewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama vile nifundishavyo kila mahali katika kila kanisa.” (1 Wakorintho 4:17). Paulo alimlea kijana wake aliyekuwa mwerevu na kumtuma kwenda kufanya mambo makubwa kwa ajili ya Mungu. Tunaweza

 

14                  Ellen White, SDA Bible Commentary, vol. 7 (Washington D.C.: Review and Herald Publishing Association, 1957), 918.27


kuona dhahiri hapa hitaji la kuwa na waalimu wa vijana wa ziada na washauri nje ya familia zao. Pamoja na hayo, kama methali ya kale ya Afrika inavyosema kuwa, “…inahitaji kijiji kizima kulea mtoto.” Paulo alitamani kujenga desturi ya malezi na ushauri ndani ya kanisa, jambo ambalo yeye mwenyewe alikuwa amelianzisha na kuwaagiza wengine nao wafanye vivyo hivyo.

 

Katika kitabu cha Tito, Paulo alimwandikia mmoja wa washauri wake, akiweka maneno haya, “2 …ya kwamba wazee wawe wenye kiasi, wastahivu, wenye busara, wazima katika imani na katika upendo na katika saburi.

 

3   Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema; 4 ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao; 5 na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe. 6 Vivyo hivyo na vijana waume uwaonye kuwa na kiasi; 7 katika mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahivu, 8 na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.” (Tito 2:2-8). Paulo alikuwa akitoa maagizo kwa watu wazima wa kanisa kuwa siyo tu wawajibike kwa mwenendo wao, bali wahakikishe wanafundisha kizazi kinachofuata cha waumini kwa namna iyo hiyo. Kanisa linatakiwa kuwa ni eneo la kufundisha watoto na vijana wadogo ili wakue katika Kristo. Kama mtunga Zaburi aivyondika kuwa, “Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako, Kitayatangaza matendo yako makuu.” (Zaburi 145:4).

 

Petro ameandika katika 1 Petro 5:1-2 kuwa, “Nawasihi 28


wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye; lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo.” Kama wana-jumuiya ya imani, kanisa zima limeitwa kushauri na kwa huruma kuelekeza vijana na wasichana, waliooa na kuolewa, kadiri wanavyokua kama Wakristo. Sisi sote tunayo sehemu ya kufanya katika kukuza mtazamo wa kidunia wa kizazi kifuatacho.

 

Tunaweza kuona malezi kama hayo kote katika Biblia: Eli alihudumia kijana mdogo Samweli ndani ya hekalu, akimfundisha jinsi ya kutambua sauti ya Mungu (1 Samweli 2:11; 1 Samweli 3); Naomi alimkuza mwali wake

 

– Ruth mke wa kijana wake – na kumfundisha kuhusu Mungu wa kweli wa mbinguni na duniani (Ruth 1:15-19); Mordekai alimfariji na kumwezesha Esta, akimtia moyo kutimiza mpango ambao Mungu alikuwa ameweka mbele yake (Esta 4); na wale wenzi wawili Prisila na Akwila walimchukua Mhubiri mchanga Apolo na kumfundisha kweli mpya kumhusu Kristo (Matendo 18:24-26). Ukianza kuwatafuta, utashangaa kile ambacho vijana wa Mungu wanaweza kuweka katika mapito yako.


 

 

 

 

 

 

29


Hitimisho

 

Kujenga mtazamo wa Kibiblia kuhusu dunia hakutokei usiku mmoja tu, au bila kupanga, tena kwa makusudi kabisa; inahitaji wazazi kujitoa kikamilifu kufundisha na kukuza watoto wao kwa namna Mungu anavyotaka mwenyewe. Kama tunavyosoma katika Mithali 22:6 kuwa, “Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.” Ikiwa kwa hakika unataka kumwona mtoto wako akikua na kukomaa, akawa mtu imara katika Imani, unatakiwa kuanza mchakato huo leo.

 

Wazazi siku zote wamekuwa, na wataendelea kuwa na mvuto mkubwa kwa Imani ya watoto wao. Utafiti uliotajwa hapo awali uliofanywa na Fuller Youth Institute umetengua dhana iliyoeleweka visivyo katika utamaduni wetu leo, kwamba wazazi hawana mguso wala mvuto kwa watoto wao.15 Kwa kweli dhana hii siyo kweli. Pamoja na udanganyifu wa tamaduni, wazazi bado wana namna imara ya kuweza kuelekeza mtazamo wa kidunia wa watoto wao.

 

Mvuto wa mzazi kamwe hauwezi kupuuzwa. Watoto wako siku zote wanaangalia na kusikiliza, wakiwa tayari kuvutwa na kuundwa na wewe kama mzazi. Kwa kutambua pale mtoto wako alipo katika hatua ya maendeleo ya ukuaji, unaweza kujihusisha naye kwa namna bora inayoweza kumfundisha kuhusu Kristo. Hapa tumeanza kuorodhesha njia ambazo unaweza ukalifanya hili – kusoma, kuweka katika utendaji, na kukariri Maandiko; kuimba nyimbo za sifa na zaburi pamoja; na kufurahia kwa kutafuta uwezo wa uumbaji wa Mungu katika maumbile ya asili. Katika Makala mbili zinazofuata tutajadili njia za utendaji na mbinu ambazo unaweza kutumia kutekeleza nyumbani kwako ili kukuza mtoto wako kwa Mungu.

15            Dustin McClure, “Helping Kids Keep the Faith.”

 

30


Jumanne, Sept. 8, 2020

 

Mitandao ya Kijamii:

Mbaraka au Laana!

(WILMA KIRK-LEE)

 

 

5 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. 6 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; 7 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. 8 Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako.” Kumbukumbu la Torati 6:5-8

Katika dunia ya leo, muda ni bidhaa adimu katika familia. Hata hivyo maneno ya Kumbukumbu la Torati bado yana maana! Uongozi unatolewa kwa wazazi. Ni kama Mungu anatamka kuwa “Yaweke ndani yako” kwanza, kisha uyaweke mioyoni mwa watoto wako! Maneno ya Bwana ni dhahiri kuhusu matazamio yake kwa uongozi wa nyumbani; wazazi ni lazima watii maagizo yake kwanza kisha “Kuyaweka ndani ya watoto wao.” Maandiko katika Mithali 22:6 yanaagiza kutoka katika mwongozo wa wazazi wa siku nyingi, yaani Biblia kwamba, “Mlee mtoto katika njia impasayo [kumfundisha kutafuta hekima ya Mungu na mapenzi yake kwa ajili ya uweza wake na talanta zake], Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.” Lakini pamoja na hayo, mara nyingi zoezi la kufundisha kanuni hizo kwa watoto linaachiwa shule na kanisa. Tambua maana ya uongozi: mtu anayeongoza au kuelekeza kundi.

 

Wakati uliopita, familia zilikusanyika kuzunguka meza ya chakula cha jioni na kushirikishana jinsi siku yao


 

31


ilivyokuwa. Leo hii familia chache zinashiriki chakula pamoja, na pale wote wanapokuwa mahali pamoja, wanakuwa wameunganishwa na dunia nyingine ng’ambo ya ile meza ya chakula kupitia katika simu zao janja na vyombo vingine vya habari.

 

Hebu tupitie baadhi ya takwimu kutoka katika Chombo cha Habari cha Mantiki ya Kawaida (Common Sense Media), ambacho ni chanzo kikuu cha maburudisho na mapendekezo ya teknolojia kwa familia:

 

 • Chombo cha habari cha simu (janja) kimekubalika kwa sehemu kubwa duniani kama mandhari ya vyombo vya habari kwa watoto katika ngazi zote za jamii.

 

 • Karibu watoto wote hadi kufikia umri wa miaka 8

(asilimia 98) wanaishi katika nyumba ambazo zina aina moja au nyingine ya chombo cha mawasiliano, na asilimia hiyohiyo wana runinga nyumbani kwao. Umiliki wa vyombo vya habari vya mawasiliano ulikuwa hadi 52% mwaka 2011 na ulikuwa hadi 75% mwaka 2013

 

 • Asilimia tisini na tano ya familia zenye watoto wenye umri wa miaka 8 kurudi chini wana simu janja, hadi 41% mwaka 2011 na hadi 63% mwaka 2013. Lakini pia 78% wana kompyuta bapa (kuanzia 8% mwaka 2011 na 40% mwaka 2013).

 

 • Asilimia 42 ya watoto wa kizazi hiki kila mmoja ana kompyuta bapa yake mwenyewe – ilikuwa hadi 7% miaka minne iliyopita na chini ya 1% mwaka 2011.

 

Kulingana na uchunguzi wa Pew uliofanyika miaka ya 2014 na 2015, asilimia 94 ya vijana ambao wanaingia


 

32


kwenye mitandao kwa kutumia vyombo vya habari vya mawasiliano wanafanya hivyo kila siku. Vijana wanatumia majukwaa kadhaa ya mitandao ya kijamii. Ambayo yamezoeleka sana ni Facebook, Istagram, na Snapchat, na asilimia 71 ya vijana wanasema kwamba wanatumia zaidi ya mtandao mmoja wa kijamii.

 

“Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala. [kubakia katika uwiano na mwelekeo thabiti kuhusu mambo ya Mungu ili kwamba mawasiliano yako yawe dhahiri, yenye maana, mahsusi na ya kumpendeza Yeye]” 1 Petro 4:7

 

 

Changamoto ya Teknolojia

 

Teknolojia ya kisasa imeleta katika maisha ya familia na majumbani mwetu changamoto ambazo hazikuwahi kuwa katika ndoto. Vizazi vilivyopita viliwasiliana na wale walio nje ya nyumba zao kutumia simu ambazo zilishikizwa ukutani katika nyumba ya familia. Ulipoenda mbali na nyumbani, ilibidi utafute kibanda cha simu ukitazamia kwamba una sarafu mfukoni ya kudumbukiza ili upige simu. Watu walitumia vibanda vya simu kuwasiliana na hata kuacha ujumbe pale waliposhindwa kuwapata waliokusudiwa. Wakati mwingine walibandika majina na namba za simu mahali fulani kwenye kibanda hicho. Ni wale walioingia katika kibanda hicho tu ndiyo wangejua jina na namba hiyo.

 

Katika zama hizo za vibanda vya simu, nilifundishwa kwamba: “Majina ya wajinga, na sura za wajinga ndizo zinapatikana kwenye maeneo ya hadhara!” Katika zama hizi za “kutokufahamika” kwenye mitandao ya kijamii, inaonekana kama misemo hii haina nafasi tena. Naam, ina nafasi – hata kama tunaongozwa kudhani kwamba


 

33


mambo yanayorushwa kwenye mitandao hayawezai kuonekana. Siku zote yatabakia kuwa pale! Vijana wa kileo wanapotuma maombi kwenye taasisi ili kuajiriwa, au chuoni ili kusajiliwa, mtu anaingia kwenye akaunti yake katika mtandao wake wa kijamii. Kile ambacho wamerusha kwenye mitandao ya kijamii kinaleta tofauti kati ya kukubaliwa au kukataliwa.

 

Jambo la kwanza la kuchukulia ni hili: Kanuni ya thamani siku zote inashikwa, siyo kufundishwa. Wazazi wanapaswa kuchunguza mwenendo wao kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii. Leo hii kila mmoja ana simu janja. Baadhi ya watoto wanaishi kwenye nyumba ambazo kabisa hazina simu ya kamba, bali ni simu janja pekee. Watu wazima wanalipia na kusambaza simu janja kwa watoto wao nyumbani. Pia wanafanya simu janja kuwa ni mwenzi wa kudumu katika maisha yao. Matumizi ya teknolojia yenye ustawi ni lazima kwanza yadhihirishwe kwa mifano. Wazazi ni lazima wahamishe mfano wa mwenendo wao kwa watoto wao, la sivyo hawa watoto hawatajifunza somo wanalotarajia kuwafundisha. Je, tunafahamu matumizi haya ya teknolojia yenye ustawi na ni yapi siyo matumizi ya teknolojia yenye ustawi?

 

Bila kujali mahali ulipo, na kwamba wewe ni nani, kuna jambo moja katika maisha ambalo linafanana kwa kila mtu: Wakati! Kila mmoja wetu anatawaliwa na siku 365 za mwaka, majuma 52 ya mwaka, siku 7 za juma, dakika 24,1140, na sekunde 86,000 zilizopo katika siku. Wakati wetu ni mali ya Mungu. Ellen G. White aliandika kwamba, “Kila wakati ni Wake na sisi tuna wajibu mkuu wa kuuboresha huo wakati kwa utukufu wake. Hakuna talanta aliyotoa asiyotaka hesabu yake kwa usahihi kuliko wakati wetu aliotupatia. (Christ’s Object Lessons, uk. 342)


 

34


Kujitawala/Kiasi katika Mambo Yote

 

Ili kufundisha watoto wetu kujifunza kujitawala (kiasi) wakati wanatumia vyombo vya mawasiliano, kujitawala ni lazima kuwe ni sehemu ya mtindo wa maisha ya familia kwa makusudi kabisa. Kuna mahali pa vyombo vya habari na vya mawasiliano, lakini hakuna kitu kama “huduma ya uwepo.” Wazazi lazima watoe fursa kwa watoto kushiriki hisia zao, mambo yanayowagusa, mashaka na wasiwasi wao, pamoja na changamoto zao bila kuingiliwa au hata kuharakishwa. Kufanya hivi kunawataka wazazi kupanga kwa kipaumbele jinsi muda wao utakavyotumika.

 

Bwana anatutaka tena kutenga muda wetu kwake kama kipaumbele. Msikilize akiongea katika Zaburi 46:10 “Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.” Hapo awali palikuwa na teknolojia ya kisasa, Mungu alifahamu kwamba tungeweza kukengeushwa kirahisi kwa namna tunavyoweka vipaumbele kwa wakati au muda wetu. Tunapomtanguliza Mungu katika vipaumbele vya wakati wetu, anatukumbusha kuhusu karama za thamani. Ametudhamini watoto mikononi mwetu. Anatukumbusha pia kuwa mfano kwa watoto wetu ambao hatimaye wataakisi upendo wake kwetu.

 

Mara nyingi kiasi au kujitawala kunatajwa sambamba na masuala ya uraibu. Ikiwa tutachukulia kujitawala (kiasi) kama mtindo wa maisha, basi tutakuwa na akili timamu namna tunavyotumia vitu vyote katika maisha vinavyogusa wakati wetu, hiyo ikiwa ni pamoja na vyombo hivi vya mawasiliano. Paulo anayaweka haya kwa namna hii: “Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika.” (1 Wakorintho 9:25).


 

35


Hitimisho

Ni wakati wa kuangalia jinsi tunavyotumia wakati wetu. Je, Sabato ndiyo muda pekee tunaompatia Bwana na kazi yake? Je, tumeshikika katika kutafuta maisha kiasi kwamba tumesahau jinsi ya kuishi? Pengine hatua ndogo ingesaidia.

 

Anza kwa kusisitiza kuhusu muda wa kujifunza masomo ya shule ya Sabato na ibada. Mjadala tunaokuwa nao katika meza ya chakula wakati wa chakula chetu unaweza kuelekezwa katika kile tulichojifunza kutoka katika muda wetu na Mungu katika kujifunza kwetu.

 

Tunatakiwa kuhimiza kiasi katika matumizi ya vyombo vya mawasiliano na katika umri ambao ni stahiki. Matokeo ya tafiti yanaonesha kwamba watoto chini ya umri wa miaka sita wasiruhusiwe kutumia vyombo hivi vya mawasiliano. Zaidi ya hapo, wazazi wanatakiwa kuweka ukomo wa matumizi ya vyombo vya mawasiliano kwa watoto wenye umri unaozidi miaka sita na kudhibiti matumizi ya vyombo vya mawasiliano.

 

Simu na vyombo vingine vya mawasiliano vinatakiwa kuwekwa mahali pamoja, eneo linalosimamiwa wakati wa chakula na wakati wa kulala. Wazazi watakapofuata kwa uaminifu miongozo hii na kuiweka katika utendaji kwa watoto wao, watakuwa wanawafundisha katika njia iwapasayo. Kumbuka kanuni ni kushika wala siyo kufundisha!

 

Kuwa kiongozi mfano siku zote ni kugumu. Lakini hata hivyo Mungu wetu ametukabidhi hawa watoto tuwafundishe katika njia iwapasayo, na yeye anafanya kazi kwetu wakati huohuo! Huu ni ufunuo wa ajabu wa upendo na neema. Tunawapatia watoto wetu urithi wenye ustawi kwa muda wetu, kumbukumbu zetu, na hisia zetu za kuunganika wanazoondoka nazo majumbani kwetu. Ili kukamilisha tamanio hili la kifalme, kunahitajika mambo mawili: Wakati na Uwepo! Haya mambo yote hayana gharama! Uchaguzi wa kuyatumia kwa hekima uko mikononi mwetu.

 

Rejea

The Common Sense Census: Media Use by Kids Age Zero to Eight. (2017). Retrieved from https://www.commonsensemedia.org/sites/default/ files/uploads/research/census_researchreport.pdf

 

Pew Research Survey. (2015, March 7-April 10). Retrieved from www. pewresearch.org

 

(Tumia kipimo kilichopo hapa chini kujua kwamba ni kiasi gani cha muda unaoutumia na vyombo vyako vya mawasiliano.)


 

36


NOMOPHOBIA

 

(Hofu isiyo ya kawaida kwa kutokuwa na simu ya mkononi au kushindwa kutuma simu kwa sababu fulani)

 

Je wewe ni jalala la simu janja? Hebu pima kila kipengele katika mzani wa 1 (kutokukubaliana kabisa) hadi 7 (kukubali kwa uthabiti) na jumlisha alama zote ili kujua. Uwe mkweli!

 

 1. Ningeweza kukosa Amani bila kuwa na taarifa muda wote kupitia katika simu janja niliyo nayo

 

1           2             3             4             5             6             7

 

 1. Ningeweza kukasirika kama ningeshindwa kusoma taarifa katika simu janja niliyonayo wakati nilipotaka kufanya hivyo.

 

1         2             3             4             5             6                 7

 

 1. Kutokuwa  na  uwezao  wa  kupata  taarifa  (kwa

mfano, matukio, hali ya hewa, na kadhalika) katika simu janja niliyonayo kungeweza kunifanya nichanganyikiwe.

 

1      2             3             4             5                6               7

 

 1. Ningeweza kukasirika ikiwa ningeshindwa kutumia simu janja niliyo nayo na/au uwezo wa kufanya

hivyo wakati nilipotaka kufanya hivyo

1      2             3             4             5             6                 7

 

 1. Moto  unapoisha  kwenye  betri  ya  simu  janja

niliyonayo ninatishika sana

 

 

 

1

2

3

4

5

6

7

6.  Ningeishiwa

 

salio

au

kufikia

 

kiwango

changu  cha  matumizi  ya  muda  wa  mtandao,

ningechanganyikiwa.

 

 

 

 

1

2

3

4

5

6

7


 

37


 1. Kama nisingekuwa na ishara ya muda wa mtandao au nisingeweza kujiunga na Wi-Fi, basi ningekuwa ninachunguza kila wakati kuona kama kuna ishara au kama naweza kupata mtandao wa Wi-Fi jirani.

 

1             2             3             4             5             6                 7

 

 1. Kama nisingeweza kutumia simu janja niliyo nayo, ningeogopa kuwa ninaweza kukwama mahali.

 

1            2             3             4             5             6                 7

 

 1. Kama nisingeweza kuangalia kwenye simu janja yangu kwa muda, ningehisi kutaka kuangalia.

 

1            2             3             4             5             6                 7

 

 1. Ikiwa sikuwa na simu janja yangu… ningehisi wasiwasi kwa sababu siwezi kuwasiliana moja kwa moja na familia au marafiki.

 

1        2             3             4             5             6                 7

 

 1. Ninaweza kuingiwa na wasiwasi kwa sababu familia yangu na/au marafiki zangu wasingeweza kunifikia kwa simu.

 

1        2             3             4             5             6                 7

 

 1. Ningehisi kuchanganyikiwa kwa sababu sikuweza kupokea jumbe na miito.

 

1     2             3             4             5             6                 7

 

 1. Ningekuwa na wasiwasi kwa sababu nisingeweza kuwasiliana na familia yangu na/au marafiki

 

1             2             3             4             5             6                 7

 

 1. Ningekuwa na wasiwasi kwa sababu nisingeweza

kufahamu ikiwa kuna mtu amejaribu kunitafuta.

 

1

2

3

4

5

6

7

 

 1. Ningekuwa na wasiwasi kwa sababu muunganiko wangu na familia yangu na/au marafiki

usingekuwapo

 

1           2             3             4             5             6                 7


 

38


 1. Ningechanganyikiwa kwa sababu ningekuwa nimekatwa kimawasiliano kutoka kwenye

utambulisho wa mtandao.

 

 

 

 

1

2

3

4

5

6

7

 

 1. Ningekosa Amani kwa sababu nisingeweza kwenda

na wakati kuhusiana na mitandao ya kijamii na

mitandao mingine kwa ujumla.

 

 

 

1

2

3

4

5

6

7

 

 1. Ningehisi hovyo kwa sababu nisingeweza kuangalia vidokezo vya kujiweka sawa na wakati kwa sababu ya kiungo changu na mitandao

1           2             3             4             5             6                 7

 1. Ningepata  wasiwasi  kwa  sababu  nisingeweza

kuangalia jumbe zangu kwenye baruapepe.

 

1

2

3

4

5

6

7

 

 1. Ningejisikia vibaya kwa sababu nisingeweza kujua jambo la kufanya.

 

1             2             3             4             5             6                 7

 

Alama ulizopata zinakwambia nini?

 

20:              Siyo zote ni nomophobia. Unao uhusiano wenye ustawi na vyombo vyako vya mawasiliano na wala hauna tatizo kutenganishwa navyo.

 

20-60: Nomophobia hafifu. Unapata hali ndogo ya kuchanganyikiwa unaposahau simu yako nyumbani kwa siku nzima au unapokwama mahali bila kuwa na Wi-Fi, lakini wasiwasi unakuwepo

 

61-100:Nomophobiayawastani.Umejishikizakatika chombo chako cha mawasiliano kiasi fulani. Mara nyingi unachungulia kwa jumbe za kuhuisha kila wakati kadiri unavyotembea njiani au unapokuwa


 

39


ukielekea kwa rafiki, na mara nyingi unakuwa na wasiwasi mawasiliano yanapokatika. Je, huu sasa ni wakati wa kuondoa sumu ya kidijitali?

 

101-120: Nomophonia kali. Hauwezi kupitisha sekunde 60 bila kuchungulia jumbe kwenye simu yako. Ni kitu cha kwanza kuchungulia mara tu unapoamka asubuhi na kitu cha mwisho kuchungulia kabla haujalala usiku, na kwa kweli simu inatawala muda mwingi ulio kati ya shughuli zako. Inaweza

 

kuwa ni wakati muafaka wa kuingilia kati.


 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

40


Jumatano, Sept. 9, 2020

 

Matunzo ya Watoto Walioachwa

Baada ya Ndoa Kuvunjika

(WLLIE NA ELAINE OLIVER)

 

SWALI: Nilipewa talaka mwaka jana baada ya ndoa yetu kudumu kwa miaka 6 ambayo kwa kuanzia, haikuwa sahihi! Binti yangu mwenye miaka 13 huwa ananiambia kwamba mimi na mtaliki wangu tunafanana na sumu kwa sababu tunaoneshana chuki kubwa kila mmoja kwa mwenzake. Anasema kuwa anajisikia mpweke, aliyetelekezwa, na asiyependwa, na anasema pengine ingekuwa vyema kama asingekuwepo. Nitamsaidiaje kubadili mtazamo wake ili apate kujihisi vyema zaidi?

 

JAWABU: Talaka inayosababisha kutengana kwa aina yoyote inaweza kusababisha maumivu makubwa kwa wote wanaohusika, lakini hasa kwa watoto. Pamoja na kwamba kuna Imani shirikishi kwamba watoto wana ahueni katika mazingira ambapo wazazi hawagombani, mara nyingi watoto wanachanganyikiwa kuona familia yao ikivunjika – ikiwa hawapo katika nyumba yenye unyanyasaji wa kimwili, kingono, au kimhemuko. Kigezo cha talaka ambacho huwa wazazi wengi hawachukulii kwa ajili yao wenyewe au kwa ajili ya watoto wao, ni mchakato wa huzuni unaoenda sambamba na kupoteza ndoa yao na kuvunjika kwa familia kwa ujumla. Kwa mtoto – hata kwa wazazi pia – talaka inaacha vidonda vikubwa vya kisaikolojia na makovu ambayo ikiwa yataachwa bila kushughuikiwa, yataathiri mahusiano yote ya baadaye.

 

Mtoto wako anaonesha kujeruhiwa akiwa na maumivu makali, ambayo wewe kama mzazi hupaswi kuyapuuza. Na kwa sababu inaonekana kwamba tayari ameshapitia


 

41


uzoefu wa maumivu ya kutengana mara mbili katika maisha yake mafupi haya, inawezekana anahisi kukosa matumaini kusikopimika. Inawezekana pia kwamba anajidhania kuwa ndiye chanzo cha mashaka yote haya yanayoonekana kwa watu wazima katika maisha yake. Aina hii ya maumivu kwa maisha ya mtoto inaweza kusababisha tabia hatarishi kama vile matatizo shuleni, kuchagua marafiki wasio sahihi, na hata kuleta matatizo ya kisheria hapo baadaye.

 

Katika hali kama hii, tunamtia moyo atafute ushauri wa kitaalamu mara moja kutoka kwa mtu ambaye ana utaalamu katika kufanya kazi na familia na vijana walipevuka. Wakati huohuo hapa chini kuna mambo kadhaa ambayo unaweza kufanya ili kusaidia kuepusha baadhi ya hofu ya binti yako:

 

 1. Ufanye ustawi wake kuwa kipaumbele chako cha kwanza. Hata hivyo, hakikisha kwamba unadumisha ustawi wako kisaikolojia, kimhemuko, kiroho na hata kimwili ili kwamba uwe na akiba ya kumhudumia binti yako. Wengi wa watu waliotalikiana wanatumia nguvu nyingi kujaribu kuwarudia wale walioachana nao, au kuingia katika mahusiano mapya ya kimapenzi ili kuwasaidia kurejea kutoka katika athari ya kuvunjika kwa mahusiano ya kwanza. Ufumbuzi huu wa haraka haraka kwa kweli hauwi wenye afya kwa sehemu zote mbili zinazohusika, na kwa hakika badala ya kuponya ni kama kuweka dawa sehemu moja tu ya kidonda kikubwa ukiacha sehemu kubwa na kusababisha uharibfu zaidi kwa watoto wanaohusika. Pia unaweza kuwa na kidonda ambacho kinahitaji kupona, na sasa ndiyo wakati mzuri wa kuanza kupona na kujenga hali ya kujitambua zaidi.

 

42


 1. Mhakikishie binti yako kwamba unampenda na kwamba atakuwa thabiti kimawazo katika maisha yake. Mkumbatie kwa wingi na kumwambia kwa maneno kuwa unampenda. Hata kama itakubidi utumie muda zaidi katika kazi ili kupata riziki ya kuwatosha, hakikisha umejenga mpangilio ambao unakupatia muda wa ibada ya familia, kifungua kinywa mkiwa pamoja, chakula cha jioni pamoja, na hata muda wa kufurahi pamoja.

 

 1. Jitoe kikamlifu kuwa na uhusiano ulio chanya na mtaliki wako aliyemzaa huyo mtoto ikiwa bado mtakuwa mnaendelea kukutana. Jizuie kadiri iwezekanavyo kutoa maneno mabaya kwa mtaliki wako mbele ya binti yenu. Watoto wa wazazi walio wahanga wa talaka mara nyingi wanahisi kwamba pengine walikosea mahali fulani au wanahisi hatia kwa hiyo talaka. Bila kujali sababu ya talaka, hata kama hali ni mbaya kiasi gani, jaribu kufanya maelezo yako yawe ya kweli bila kuyapamba kwa undani wa hali yoyote. Ikiwa atakuwa na uhusiano wa karibu na mzazi wake huyo mwingine – awe ni yule aliyemzaa au ni wa kambo – tafuta namna yoyote ya kuwafanya wabakie katika maisha yake ikiwa utaona kwamba inafaa.

 

Tunasoma katika 2 Wakorintho 12:9 kuwa, “Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.” Tunaomba kwamba katika vipindi hivi vigumu vya maisha yako na binti yako, upitie uzoefu wa tumaini na uponyaji kupitia kwa neema ya Mungu, upendo wake na uweza wake.


 

43


Alhamisi, Sept. 10, 2020

 

Uthibitisho wa Ndoa

 

Utangulizi

Masuala yanayohusu ndoa yanaweza kuonekana katika sura yake kamili pale tu yatakapotazamwa dhidi ya ukweli wa awali wa ndoa halisi ya kimbingu. Ndoa ilianzishwa kimbingu kule Edeni na kuthibitishwa na Yesu Kristo ili iwe ni ndoa ya mke mmoja inayohusu jinsia tofauti, muunganiko wa wenzi wanaopendana maisha yote. Katika kuhitimisha shughuli zake za uumbaji, Mungu alimuumba mume na mke kwa mfano wake mwenyewe, na akaanzisha ndoa ya kwanza yenye agano la muunganiko wa jinsia mbili kimwili, kimhemuko na kiroho, muunganiko ambao umenenwa katika Maandiko kama “mwili mmoja.”

 

Mwili Mmoja

Chimbuko lake ni mgawanyiko wa jinsia mbili za wanadamu, umoja wa sura ya ndoa katika namna moja yenye umoja ndani ya mgawanyiko wa Mungu Baba. Kote katika Maandiko, muunganiko wa jinsia mbili katika ndoa umeinuliwa kama ishara ya muunganiko kati ya Uungu na ubinadamu. Ni ushuhuda wa mwanadamu kwa upendo wa kujitoa kwa Mungu mwenyewe na agano na watu wake. Ile hali ya kupatana na kuletwa pamoja kwa mwanamume na mwanamke katika ndoa inatoa picha ndogo ya umoja wa jamii ambayo inaheshimu wakati kama kiambato cha jamii zilizo imara. Zaidi ya hapo, Muumbaji alikusudia kuwa masuala ya ngono katika ndoa yasibakie tu kama kigezo cha kuunganisha mume na mke, bali pia yawe na kusudi la kupandikiza na kuendeleza familia ya wanadamu.

 

Kwa kusudi la mbingu, kitendo cha kuzaa kinatokana na muunganiko, na mchakato fulani ambao unaleta furaha kwa mume na mke, pia starehe na ukamilifu. Ni kwa ajili ya mume na mke ambao upendo umewawezesha


 

44


kufahamiana kwa undani wa kuunganika katika tendo la ndoa ili kudhaminiwa kwa mtoto. Huyo mtoto wao ni udhihirisho wa kule kuwa “mwili mmoja.” Mtoto anayekuwa anashamiri katika mazingira ya upendo wa ndoa na umoja uliosababisha yeye kuzaliwa na kwa hiyo anafaidi ule uhusiano uliopo kwa hali ya asili ya wazazi.

 

Muunganiko huu wa mume na mke mmoja katika ndoa unathibitishwa kama msingi wa familia na maisha ya jamii uliowekwa wakfu na mbingu. Ni muunganiko pekee ulio sahihi kimaadili wa via vya uzazi au namna nyingine yoyote ya kudhihirisha ukaribu wa mahusiano ya kimwili. Hata hivyo, hii taasisi ya ndoa ndiyo mpango pekee wa Mungu wa kukutanisha uhitaji wa mahusiano ya wanadamu au kwa kufahamu uzoefu wa familia. Kuwa pekee, na hata urafiki wa wawili walio pekee pia upo katika ubunifu wa kimbingu. Kule kuwa karibu na kutegemezana kwa marafiki kunaoneshwa kwa ukubwa wake kote katika Maagano mawili ya Biblia yaani Agano la Kale na Agano Jipya. Ushirika wa kanisa ambayo ni kaya ya Mungu, upo kwa wote bila kujali hali yao ya ndoa. Hata hivyo Maandiko yanaweka mipaka thabiti kijamii na hata kingono kati ya uhusiano wa urafiki na uhusiano wa ndoa.

 

Msimamo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato

Kwa mtazamo huu wa ndoa basi, kanisa la Waadventista wa Sabato linashika bila maswali, na kuamini kwamba kushusha viwango vya mtazamo huu kwa hali yoyote ile ni sawa na kushusha viwango vikamilifu vya kimbingu. Na kwa sababu ndoa imeharibiwa na dhambi, ule usafi na uzuri wa ndoa kama ilivyokusudiwa na Mungu unahitaji kurejeshwa. Kupitia kwa kazi njema ya Yesu Kristo inayokubalika na kazi ya Roho Mtakatifu ndani ya moyo wa mwanadamu, lile kusudi la awali la ndoa linaweza kufufuliwa ili ile furaha ya uzoefu wa ukamilifu wa ndoa iweze kutambuliwa na mume na mke wanaounganisha maisha yao katika agano la ndoa.

 

45


Ijumaa, Sept. 11, 2020

 

Kambi la Familia:

Kuwafikia na Kuwahusisha

(ANNE-MAY MULLER)

 

Nilijikuta nikisema kuwa, “Samahani, siwezi kucheza na wewe sasa. Mama yangu ameshikika na kazi ya kupanga kambi la familia, kwa hiyo nakuomba uende tu ukacheze na kaka yako.”

 

Yule mtoto wa miaka saba kwa mshangao alijibu, “Kambi la Familia?” Mara maswali yakaanza kumiminika kutoka kwake mara moja kuwa, “Tutaenda kwenye kambi la familia hivi karibuni? Ni lini? Kesho? Ninaweza kukusaidia! Ninaweza kuanza kupanga nguo zangu kwenye mkoba wangu. Je, ninaweza kumwalika rafiki yangu?”

 

Kwetu sisi kambi la familia limekuwa ni jambo jema la kutazamia. Hebu nieleze kwa nini na pia nishiriki kwa nini mtoto wangu alitamani kiasi hiki kumwalika rafiki yake ambaye anatoka katika familia isiyo ya Kikristo.

 

Kwa kweli kipindi cha kambi la familia ni kipindi ambacho huwa mshike mshike kwangu, lakini watoto wangu wanafahamu kwamba ni wakati wa kukutana na watoto wenzao wanaolingana nao. Wanatazamia mwisho wa juma wenye furaha na michezo mingi ya ndani, ibada, usharika, hata michezo ya nje, na ni muda wa wazazi wao kukutana na watu wazima wenzao ambao wanafahamiana kwa uzuri zaidi. Ikiwa wazazi watapenda kwenda kwenye kambi la familia, watu wazima pia wanapenda.

 

Kwa hiyo ni kwa namna gani tunaweza kutumia kambi hizi kuwafikia watu na kuwarejesha? Mimi siwezi kujifanya kuwa nina jibu kwa swali hili, bali ninaweza kukuambia


 

46


jinsi sisi katika Union ya Denmark tulivyopitia katika uzoefu.

 

Ninapokuwa nikipanga kambi ya familia pamoja na timu yangu ya wanaojitolea, tunapanga katika maeneo matatu yafuatayo: Ustawishaji Kijamii, Kiroho, na Kielimu. Tunataka vipengele vyote hivi vitatu vya utendaji viwepo katika kambi letu. Hatujielekezi katika eneo moja tu, bali tunalenga kupata uzoefu mkamilifu kila wakati tunapokutana. Kwa kufanya hivi, tunapata kitu fulani kwa familia zinazojihusisha katika kanisa na kuwa na maisha ya kiroho yaliyo hai, familia ambazo hazina uzoefu wa kanisa wala Mungu, na familia zenye upeo mdogo wa elimu ya Mungu na ambazo zinahudhuria kwa sababu tu kuna marafiki wanaoenda hapo.

 

Maeneo hayo matatu ni ya muhimu kwetu wote ikiwa tunataka kuwa familia bora, na kwa hiyo ni muhimu kuwa na program zenye uwiano na zinazotoa nafasi kwa maeneo yote hayo.

 

Kujichanganya Kijamii

Baadhi ya watu wazima wanaweza kuhisi upweke katika “mapovu yanayotokana na malezi.” Watoto wanaweza kutumia muda wao wote, na nguvu zao hata rasilimali za kiakili. Wakati mwingine wazazi wanaweza kuhisi kuwa wana njaa kijamii, na ni mara chache wanapata fursa ya kuzungumza na watu wazima wenzao au kukaa pamoja tu. Ili kusaidia kukidhi hitaji hili la kuwafanya watu wazima waunganike tunapanga muda zaidi wakati wa chakula na saa za jioni kwa ajili ya watu wazima kuweza kujichanganya. Kufanya hivi kunawapatia watu wazima muda wa kufanya marafiki kadiri wanavyoendelea kufahamiana. Ni mazungumzo yenye thamani kubwa hasa wanapozungumza na wazazi wenzao kuhusu


 

47


changamoto na furaha ya kulea watoto. Kufanya hivi pia kunaweza kupunguza mizigo kwa kuona familia zingine zinavyopambana na magumu hayohayo. Huu urafiki mpya unaojengwa unaweza kuendelea hadi siku zenye mambo magumu. Kubadilishana mawazo na mashauri ya maana ya changamoto za kuwa familia katika kizazi hiki kilichosongwa na mahangaiko na namna ya kuwezesha familia hizi kwa kile wasichokuwa nacho na kuwapatia hali ya kujiamini pamoja na nyenzo za kushughulikia masuala kama hayo mara wafikapo nyumbani.

 

Huwa tunajumuisha pia shughuli za kufanya nje kwa watoto na watu wazima – bila kujali hali ya hewa itakuwaje. Tunapata hewa safi, tunafurahi pamoja, na kupata fursa ya kuzungumza pamoja. Huwa ni wakati wakutembea kuzunguka kambi kwa shangwe au tukijaribu kuvumbua mazingira na kufanya zoezi la utume. Pengine tutawasha moto na kuchoma mahindi, tukishauriana na kuulizana maswali na vitendawili, au chochote ambacho waliopanga na kukusudia kwamba kifanyike. Shughuli zote hizi ni fursa kubwa kwa watu wazima na watoto kufanya mambo ambayo wakiwa nyumbani yanasahauliwa - kama vile kucheza pamoja.

 

Unapokuwa umetoka na kushirikiana na timu yako kujaribu kujaza maji kwenye pipa kwa kutumia mikono yako, kwa haraka kuliko timu unayoshindana nayo, na ile furaha ya kufanya kazi na timu yako kuangusha vizuizi. Ni rahisi kuzungumza kuhusu maisha unapokuwa umetoka katika changamoto na kuikamilisha ili kufurahi pamoja.

 

Kwa kawaida kunakuwa na usiku uliopangwa kuwa na mchezo kwa familia, pale michezo ya kitamaduni inachezwa – ile michezo ambayo babu zetu walikuwa wakicheza kabla teknolojia haijawa sehemu ya maisha yetu.


 

48


Michezo hii inafurahisha na kufanya watu wacheke sana. Watoto wanaipenda kwa sababu wanaona watu wazima wakijiunga nao katika ulimwengu wa kucheza. Kufanya hivi kunawasaidia watoto kujenga mahusiano na wengine, na watu wazima nao kujenga mahusiano na watu wazima wenzao.

 

Mchezo wa mpira wa meza unaweza kuwa na umuhimu katika programu kama vile tu mhadhara, kwa sababu hapa ndipo tunapojenga viungo vya kijamii na kupata marafiki wapya ambao tutajenga ubia katika safari ya maisha na katika kujenga shughuli za familia.

 

Jambo jingine linalosaidia kujenga mandhari ya kufurahisha ni chakula kinachotolewa kwa kila mtu. Familia hazihitaji kusaidia kutayarisha chakula. Kwa familia ambazo zina kazi nyingi na watoto wachanga wanaohitaji kuhudumiwa, kushiriki hapo ni jambo linaloleta nafuu! Haya mambo yanayotuchukulia muda yanaposhughulikiwa, maana yake ni kuwa na nafasi kwa wazazi kupumzika na kuwapatia nguvu za ziada ili kushughulikia familia zao pamoja na mahusiano wanayojaribu kuendeleza wakiwa na watu wazima wenzao waliopo.

 

Uzoefu wa Kiroho

Huwa tunapanga maudhui ya kiroho mengi katika kambi za familia. Ibada za asubuhi na jioni siku zote zinafanyika kama “ibada za familia” ingawaje tunaweza kuwa washiriki wanaokaribia au kuzidi 100 katika chumba. Familia kwa ujumla ndiyo inayoshiriki katika ibada. Ni rahisi, na ya kuvutia, shirikishi na ya kufurahisha. Kunakuwa na sifa, kuimba, masomo na maombi, lakini yakiendeshwa kwa namna ambayo kila familia inachukua mfano wa ibada za nyumbani. Familia nyingi zinapata shida kujirekebisha kwa muda uliopangwa wa ibada, na wanapofanya


 

49


hivyo kunakuwa na changamoto ya kufahamu wafanye nini na wafanye kwa namna gani. Ndiyo maana huwa tunahakikisha kuwa tunaambia familia kwamba hii ibada ya familia ni rahisi kufanya na rahisi kutekeleza kiasi kwamba wataweza kujaribu wakiwa nyumbani hapo watakaporudi. Tunawaonesha wazazi na watoto kwamba muda wa ibada ya familia ni muda wa kuhisi kuwa karibu na kila mmoja, muda wa furaha wenye maana na wakati wa muhimu zaidi. Hii kambi inayofanyika mwisho wa juma inapofikia mwisho wake, unakuta kila familia imekuwa sehemu ya familia nne za ibada, ambazo zimepewa vitendea kazi na dhana za kuimarisha ibada nyumbani. Wale Wakristo ambao wamepoa au familia ambazo siyo za Kikristo wanaelewa na kujifunza umuhimu wa ibada za namna hiyo. Wazazi wote wanataka kuhamisha sifa nzuri kwa watoto wao, na wanaona matokeo yaliyopatikana kwa familia zao pale muda unapotengwa kwa ajili ya ibada ya familia.

 

Tunapokuwa tunaandaa huduma ya ibada ya Sabato, hiyo siku yote ndiyo ibada ya familia. Hii siyo huduma yenye mahubiri marefu kwa ajili ya watu wazima na mahubiri mafupi kwa ajili ya watoto. Huu ni uzoefu wa ibada mtambuka kwa makundi ya umri tofauti wenye vigezo vilivyoandaliwa kwa namna ambayo watoto wanaelewa, na kupata ustawi mkubwa wa kiroho. Tunaweza kuwaonesha watoto na wazazi kwamba kanisa ni mahali pa furaha na kwamba ibada nzuri inaweza kuwa ya kuvutia na yenye maana. Ikiwa itakuwa ya kuvutia na yenye maana kwa watoto wetu, basi itakuwa ya kuvutia na yenye maana kwa familia ambazo hazina uzoefu na Ukristo au maisha ya kanisani.


 

 

 

50


Ukuaji wa Kielimu

Wazazi wote wanapenda kuwa ni wazazi bora kadiri iwezekanavyo. Ndiyo maana tunalenga mafunzo ya hali ya juu katika kambi zetu za familia. Wanasaikolojia, wataalamu wa masuala ya familia, waalimu, waganga, mayaya wa watoto, wataalamu wa lishe, vyombo vya habari, na kadhalika wanakutanika pamoja ili kuwafundisha watu wazima. Ni muhimu kwamba tutenge muda wa kuboresha uwezo wetu katika kile tunachofanya, lakini wazazi wengi wanapotea katika wingi wa mawazo yanayohusu malezi. Tunatoa maagizo thabiti kwa wazazi wakati watoto wao wakiwa wanafurahia muda wa shughuli mbalimbali au mikutano ya kiroho inayoendeshwa na watu wazima wenye uwezo waliojitolea.

 

Vipindi mbalimbali vinapokelewa vizuri, na wazazi wote walio Wakristo. Na wale wasio Wakristo wanafaidi kutoka katika maeneo mbalimbali ambayo yanashugulikiwa. Tunalenga kuwa wazi kwa vigezo mbalimbali vingi vya malezi, makuzi ya watoto, afya, na ukuaji wa akili, lakini pia tunashughulikia masuala magumu kama vile yale yanayohusu ngono, mipaka binafsi, matumizi ya vyombo vya habari, na kadhalika. Mwisho wa kambi hili la familia tunawauliza washiriki wataje ni somo gani na eneo gani wangependa kujifunza zaidi katika makambi ya familia ya baadaye. Kwa kufanya hivyo, tutajua kile ambacho wanapenda kufahamu na hasa kile ambacho wanatafuta.

 

Ili kuwapatia wazazi nyenzo na stadi za kuwawezesha kufanya kwa ubora nyumbani, tutakuwa tunawanufaisha siyo wazazi tu, bali hata watoto. Wanakuwa na shukurani kwa kupata stadi mpya walizojifunza kama matokeo ya kutenga muda kwa ajili ya kuwekeza katika familia zao. Wazazi hawa wanapata uzoefu wa nguvu zilizohuishwa na matumaini katika uwezo wao wenyewe kama wazazi wanaporudi nyumbani.

 

51


Zamu Yako

Kwa hiyo, kwa nini tunakuwa na aina mbalimbali za familia zikihudhuria kambi letu? Pengine ni kwa sababu tunajielekeza katika mambo matatu. Pengine ni kwa sababu tunajaribu kufanya kambi liwe la kirafiki kwa familia ambazo hazina muunganiko imara kwa kanisa la Waadventista wa Sabato mahalia. Hata hivyo, kadiri iwezekanavyo ni kwa sababu familia ambazo zinahudhuria huwa zinapenda kuja katika kambi hili. Wanawakaribisha marafiki zao katika mpangilio wa kanisa kwa sababu ni uzoefu ambao wanaweza kuuelezea. Mara nyingi tumeona kwamba familia ambazo zinapendelea kuhudhuria, huwa wanawezesha familia nyingine kwa kuwalipia ili waje na kupata uzoefu huo pia.

 

Katika hali ya kuongezeka, makanisa ya Denmark yamekuwa katika ongezeko la familia pale mmoja tu wa wenzi katika ndoa anapodai na kuwa Mkristo aliye hai. Ni muhimu kuwa na nafasi kwa ajili ya familia kama hizi. Kambi la familia ni moja kati ya matukio ambapo familia nzima inaweza kufurahia kuwa pamoja katika mkao wa kanisa bila mmojawapo wa wenzi katika ndoa kujisikia kuzidiwa na uzoefu huo. Watoto katika familia hizo pia wanabarikiwa kwa sababu wanahudhuria pamoja na wazazi wao katika tukio la kiroho. Kambi la familia wakati mwingine ni kanisa la kwanza ambalo hizi familia zitakuwa zimehudhuria, na wakati huohuo kuwapatia wazazi nyezo bora kadiri iwezekanavyo ili kukuza watoto wao na kuwahamishia sifa njema. Hili ndilo tamanio kubwa la kila mzazi.

 

Tukirudi katika swali ambalo mtoto wangu aliniuliza wakati tulipokuwa tukiandaa kambi hilo. Jawabu langu lilikuwa ni “Ndiyo” yenye shauku. Siyo kwamba angekuja na rafiki yake tu, bali rafiki yake aliweza kuwashawishi wazazi wake kuhudhuria, na wakaja.

 

52


Ninaamini kwamba kambi la familia linaweza kuwa ni namna nzuri ya kunganisha familia ambazo hazijichukulii kuwa za Kikristo au za Kiadventista. Ninaamini kwamba kambi la familia linaweza kuwa ni namna nzuri ya kuunganisha familia ambazo haziwasiliani nasi kwa sababu yoyote ile, na ninaamini kambi la familia linaweza kuwa ni mahali ambapo familia zenye mmoja wa wenzi asiye Mwadventista kuweza kupata namna ya kuunganika na wengine kama familia moja katika upeo wa kiroho na katika kujenga tunu za kiroho.

 

Ninawahimiza kufikiria namna ya kupanga kambi la familia kunavyoweza kukusaidia katika kufikia familia na neema ya Yesu na upendo wa Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu.


 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

53


Jumamosi, Sept. 12, 2020

 

Unataka Nikutendee Nini? Nakala halisi ya Wema wa Yesu (DIANE THURBER)

 

Shirika la Afya Duniani linashiriki dhana muhimu zifuatazo kuhusu upofu na udhaifu katika kuona:

 

 • Inakadiriwa kwamba watu takribani bilioni 1.3 duniani kote wanaishi na aina moja au nyingine ya udhaifu wa kuona.

 

 • Kuhusu kuona kwa mbali, watu milioni 188.5 wana kiwango kidogo cha udhaifu wa kuona. Milioni 217 wana matatizo ya kuona ya wastani hadi makubwa, na milioni 36 ni vipofu

 

 • Asilimia takribani 80 ya matatizo ya kuona duniani kote yanaweza kuepukwa.

 

 • Watu wengi wenye matatizo ya kuona ni wale wenye umri wa miaka zaidi ya 50

 

Inaweza kuchosha sana pale unapofikiria kuhusu takwimu hizi. Lakini hatupaswi kwenda mbali sana ili kutambua kwamba kuna mmoja anayeweza kuongoza maisha pale penye changamoto za kuona. Kila jumuiya katika kila nchi za mabara yote kuna mtu ambaye ni kipofu au ana udhaifu wa kuona, na mara nyingi hawa watu wananyanyapaliwa na jamii. Sababu zinaweza kuwa za kukanganya, za kishirikina, ukosefu wa elimu, stadi, rasilimali au kwa wengine ni hali ya kutokujali.

 

Nilipokea simu kutoka kwa mwanamke ambaye alitaka tu kuzungumza na mtu. Kwa nini? Kwa sababu tangu


 

54


alipopofuka hakuna aliyemtendea kama hapo awali. Hapo awali alikuwa akijihusisha na kazi za kanisani na za jumuiya, lakini upofu wake umemletea uhalisia mpya. Lakini ndani yake alikuwa ni mtu yule yule, ila familia yake na marafiki zake walimgeuzia mgongo na kumkataa, walikuwa wakiona aibu kuwa naye, ndiyo sababu alijisikia mpweke na mwenye hofu kwa mara ya kwanza katika maisha yake. Alihisi kama vile amekataliwa.

 

Yesu na watu waliotengwa.

Ni jambo la kushangaza kutambua kwamba Yesu alishirikiana na watu waliotengwa na jamii kadiri alivyotembea safari yake hapa duniani, na bado anashirikiana na wenye uwezo tofauti huku wakitengwa na familia, jumuia, jamii, au hata kanisa. Yeye ni rafiki wa wote.

 

Kama vile tu kudharau umaskini na mapungufu mengine ya kijamii, kuhudumia wale wenye upungufu wa kuona kunaweza kuwekwa kwenye “kabati ya makabrasha” na wale ambao wanafikiri kwamba masuala ya watu wenye uhitaji ni matatizo yanayotakiwa kutatuliwa na mtu fulani au kushughulikiwa na kizazi kingine. Hata hivyo, ikiwa sisi ni wanafunzi wa Yesu Kristo, ni lazima tupokee utambuzi kuwa agizo la utume katika Mathayo 28:18-20 siyo kwa ajili ya wachache tu waliochaguliwa; Ni kwa dunia nzima na kwa kila mtoto wa Mungu duniani – wale wenye uwezo wa kuona vizuri na wale wasio na huo uwezo.

 

Sisi kama Wakristo, ni dhahiri kwamba tunaelewa wito wetu wa kufundisha mataifa yote na kuwabatiza kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, lakini tunapowasilisha ule utume wetu mkuu, Yesu pia anaagiza wanafunzi wake kuwafundisha “kuyashika yote niliyowaagiza.” (Mathayo 28:;20)


 

55


Yesu alikuwa Mwalimu Mkuu. Siku zote alikuwa na wafuasi, na wakati mwingine idadi ya wafuasi waliokuwa wakimfuata ilikuwa ni kwa maelfu wakisikiliza kila neno alilosema na kufuatilia kila tendo alilotenda. Alifundisha kwa njia mbali mbali. Alihadithia visa na kutoa mifano na vielelezo; aliuliza maswali; alitumia vielelzo vinavyoonekana. Namna nyingine ambayo Yesu alitumia kufundisha ilikuwa ni kwa kudhihirisha mafundisho ya thamani. Kwa mfano Yesu hakufundisha tu kwa kuzungumzia kuwafungua wafungwa, bali alimtafuta Mathayo mtoza ushuru na akaenda na kushiriki chakula nyumbani kwake. Mafarisayo waliwauliza wanafunzi wake kwamba ni kwa nini Mwalimu alikula na watoza ushuru na wenye dhambi. Yesu aliposikia akasema, “… Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi.” (Tazama Mathayo 9:10-12)

 

Wakati mwingine vitendo vya Yesu vya kufundisha vilipangiliwa na wakati mwingine tunaona kuwa alianza tu alipopata fursa ya kufundisha ili wafuasi wake waone.

 

Tunafikiri kuhusu vitendo vya Yesu kwa wale ambao walikuwa vipofu kwa namna ambayo havikupangiliwa; ilikuwa ni kulingana na hitaji. Hata hivyo Yesu hakupoteza muda wa kufundisha au fursa ya kuhuisha. Uponyaji uliofanyika nyakati kama hizo haukuwa tu wa kimwili na wa kiroho, bali ulikuwa pia uponyaji wa kimhemuko, kwa namna alivyowainua watu na kuwarejesha katika nafasi yao stahiki katika jumuiya yao. Yesu alirudisha heshima na thamani kadiri alivyodhihirisha kwa wale waliokuwa wakimwona (pamoja na kizazi kijacho) jinsi ya kushughulikia wengine. Alilisaidia kanisa lake na mwili wa Kristo kuona kwamba wajibu unavuka mduara wa kawaida wa jamii na kuwafikia wote. Aliweka mapito.


 

56


Yesu alijishughulisha na wale ambao wengine waliwadhani hawastahili kushughulikiwa na Mwokozi. Alizungumza kwa heshima. Angalia kile alichofanya alipokutana na Batimayo kipofu, alimuuliza kuwa, “Wataka nikufanyie nini? Akasema, Bwana, nipate kuona.” (Luka 18:41).

 

Ingawaje ilikuwa wazi kabisa kwa baadhi ya wale waliokuwa wakitazama kile ambacho mtu huyo alikuwa akitaka, bado Yesu alimpatia fursa ya kuweka Imani yake katika utendaji, Yesu pia alionesha heshima kwa kukubali kumsikiliza Batimayo na kuruhusu sauti yake isikike. Inawezekana sauti yake ilikuwa imenyamazishwa kwa miaka mingi. Inawezekana pia kwamba sauti yake ilikuwa imepuuzwa kwa muda mrefu, au kubezwa. Hata hivyo, Imani ya Batimayo ilimsukuma kusihi kwa kujiamini, “… Akasema, Bwana, nipate kuona.” (Luka 18:41)

 

Mbingu Inaona Kustahili

Kadiri Yesu alivyokabiliana na mahitaji ya wale aliokutana nao, alidhihirisha kwa uwezo mkubwa kwamba wakati wengine wanapobeza kustahili kwao, mbingu haikufanyii hivyo. Je, jambo hili lilisababisha mabadiliko katika fikra na matendo ya wale waliokuwa wakimwangalia huyu Mwalimu Mkuu? Je, inatusababisha kutulia na kufikiria mwenendo na matendo yetu? Ikiwa kuchukua hatua katika kuleta tofauti katika maisha ya mtu mmoja aliyekuwa kipofu ilikuwa ni muhimu kwa Yesu – basi ni budi ipewe kipaumbele cha juu katika orodha yetu pia. Ikiwa hautakuwa na uhakika, basi uliza maswali haya: Ikiwa siyo sisi, ni nani? Ikiwa siyo sasa, ni lini? Hatimaye mtu fulani atawajibika kupeleka Injili ulimwenguni mwote, na hapajawahi kuwapo na wakati nyeti kuliko katika nyakati hizi za mwisho wa historia ya dunia hii.


 

 

57


Yesu alipowaambia wanafunzi wake kwamba, “Kwa maana maskini mnao sikuzote pamoja nanyi; bali mimi hamnami sikuzote.” (Yohana 12:8) alikuwa akinukuu aya nyingine inayoeleweka vyema kutoka katika Torati ya Wayahudi (yaani vitabu vitano vya mwanzo vya Biblia ya Waebrania). Kwa kweli wanazuoni wanaamini kwamba wale waliomsikia akisema maneno hayo wangetambua mara moja kuwa alimaanisha nini. Hapa chini tuna nukuu kamili ya kile alichosema:

 

7 Kama akiwapo mtu maskini pamoja nawe, nduguzo mmojawapo, ndani ya malango yako mojawapo, katika nchi yako akupayo Bwana, Mungu wako, usifanye moyo wako kuwa mgumu, wala usimfumbie mkono wako nduguyo maskini; 8 lakini mfumbulie mkono wako kwa kweli, umkopeshe kwa kweli yatoshayo haja yake katika ahitajiayo. 9 Jitunze, msiwe na neno lisilofaa moyoni mwako, kusema, Umekaribia mwaka wa saba, mwaka wa maachilio; jicho lako likawa ovu juu ya nduguyo usimpe kitu; naye akamlilia Bwana juu yako, ikawa ni dhambi kwako. 10 Mpe kwa kweli, wala moyo wako usisikitike utakapompa; kwa kuwa atakubarikia Bwana, Mungu wako, kwa neno hili katika kazi yako yote, na katika kila utakalotia mkono wako. 11 Kwa maana maskini hawatakoma katika nchi milele; ndipo ninakuamuru na kukuambia, Mfumbulie kwa kweli mkono wako nduguyo, mhitaji wako, maskini wako, katika nchi yako.” Kumbukumbu la Torati 15:7-11

 

 

 

 

Tunaweza kuingiza neno “kipofu” katika aya hii badala ya neno “maskini”, na ninaamini tuna nakala halisi ya ukarimu katika huduma kwa watu walio vipofu na familia zao. Hili ni agizo moja kwa moja kutoka kwa Mungu likitutaka kuwa wakarimu.


 

58


Changamoto iliyopo katika kuhudumia wale walio vipofu ni kwamba hakuna vipofu wawili wanaofanana au wenye mahitaji yanayofanana. Hakuna mahitaji ya mtu mmoja yanayofanana katika kila hatua ya maisha. Kwa hiyo tunafanya nini kama watu na kama kanisa ili kufuatilia hii nakala halisi ya ukarimu iliyowasilishwa na kuonyeshwa na Yesu kwa namna iliyo nzuri?

 

Ukarimu Badala ya Kutokujali

Kwanza tunachagua ukarimu badala hali ya kutokujali. Tunafungua mikono yetu na mioyo yetu kwa ndugu na dada zetu. Tunachagua kuwa kama waumini wa awali ambao walichukua changamoto hii kwa uzito wake wote kiasi kwamba aya za kitabu cha Matendo 4:33, 34 zinafafanua ukarimu wao: “Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote. Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa,”

 

Hebu fikiria hilo! Hiki ndicho kinchotokea tunapofuata mafundisho ya Yesu na kutegemeza na kulea kupitia kwenye urafiki. Anatukaribisha tuwaoneshwa watoto wake (ambao ni vipofu na familia zao) maana ya kuwa sehemu ya mwili wa Kristo, mwili ambao siyo kwamba unakidhi tu mahitaji bali unawajaza na kufurika.

 

Kiongozi wa Huduma Maalum ya Wahitaji kwa kanisa la ulimwengu la Waadventista wa Sabato aitwaye Larry Evans, anaendelea kuwahusisha viongozi wa kanisa na washiriki katika kila ngazi duniani, akiwakumbusha kwamba “Wote wamejaliwa, wanahitajika, na wanathaminiwa.” Anawapa changamoto kanisa kushughulikia wale ambao hawajiwezi kwa namna moja au nyingine wakichukulia haya maeneo ya msisitizo: Ufahamu, Ukubali na Utendaji.


 

59


Ufahamu

Nilizungumza kuhusu ufahamu hapo nyuma nilipokuwa nikikazia takwimu za wale waliopo kati yetu ambao ni vipofu au wenye udhaifu wa kuona. Kuna mengi zaidi ambayo tunaweza kujifunza kwa kuenda katika maktaba au vituo vya elimu. Ni lazima tuwe na ufahamu pia kuhusu vikwazo na chuki bila sababu zinazowakabili wale ambao wana upungufu fulani kadiri wanavyojaribu kukabili maisha ambayo Mungu amewapangia. (Tazama Yeremia 29:11). Mungu ana mipango kwa kila mmoja wetu. Ni lazima tuongeze ufahamu wetu kila mmoja na kwa pamoja kama kanisa kwa kuelimisha kuhusu sababu za upofu, na kwa kushirikiana na viongozi wa huduma za afya, kuelimisha kuhusu namna ya kuepuka udhaifu wa kuona. Ni lazima pia tuwaelimishe kuhusu tamanio la Mungu la ujumla wa mwili wa Kristo. Kuhusisha kwa ujumla maana yake ni zaidi ya kumkaribisha rafiki. Maana yake ni kuwahusisha pia wale ambao wana udhaifu wa kuona na wengine ambao wana mahitaji maalum katika masuala yote ya ibada na utume. Maana yake zaidi ni kuondoa vikwazo na kuhakikisha kwamba mabadiliko haya yanatokea.

 

Ukubali

Yesu aliwakubali wale waliokuwa wamekataliwa na jamii, hata wanaokataliwa sasa. Ni lazima tukue katika upendo, neema na rehema kadiri tunavyowakubali watu wote kwa namna ambayo Yesu alifanya. Hata hivyo, Yesu anamkubali kila mmoja wetu kwa jinsi tulivyo, bila ukamilifu. Ni lazima tubadilishe fikra zetu kuhusu namna Mungu anavyowachukulia wale ambao ni vipofu. Tunatakiwa kuwakaribisha wote katika mwili wa Kristo watumie talanta zao na karama zao za roho kuleta tumaini na msaada kwa ulimwengu unaokufa, na kuwafanya wawe wanafunzi hasa wale waliopo katika miduara. Wanao


 

60


ushuhuda ambao utakuwa na nguvu kwa mtu fulani aliye katika mazingira sawa na ya kwake kuliko kile nilichoweza kutoa. Kukubali kunaweza kuwa ni namna ya kutangaza ndani ya familia makanisa, na jumuiya kwa niaba ya mtu fulani aliye kipofu.

 

Utendaji

Mwisho, ni lazima tukusudie kushughulikia mahitaji – mahitaji ya kimwili, mahitaji ya kiroho na ya kimhemuko.

 

Kwa hiyo, baadhi ya haya mahitaji ni yapi? Ninaweza kukutajia baadhi ya mahitaji niliyoona nilipokaribishwa katika uhusiano wa usharika na watu ambao ni vipofu. Pale nilipokuwa sina uhakika wa kile ninachoona na kujifunza, niliuliza ili kupata ufafanuzi kwa sababu ya kupata uelewa zaidi. Yeyote aliye na hiari ya kutumika atahitaji kufanya hivyohivyo ili kusaidia kukidhi mahitaji ya rafiki hadi kipimo cha kumwagika, na kuwakumbatia katika Mwili wa Kristo na katika maisha ya Kanisa.

 

Tunatakiwa kujitoa ili kujenga mahusiano na mtu fulani aliye kipofu. Tutahitaji kupanga muda wetu, nguvu zetu, vipaumbele, na masuala ya fedha ili kuleta tofauti, kama vile tu tunavyofanya kwa uhusiano wenye maana kwetu. Tunahitaji kuuliza kama Yesu alivyouliza kwamba, “Unataka nikutendeeje?” Na tunahitaji kuwauliza, siyo hao watu mmoja mmoja, bali familia zao pia. Baadhi ya mahitaji ni kama:

 

 • Urafiki
 • Chakula
 • Usafiri
 • Malezi ya watoto
 • Gharama za matibabu
 • Malazi

 

61


 • Vitu vya nyumbani
 • Ajira
 • Kutunza nyumba
 • Kufua
 • Vifaa mbali mbali
 • Rasilimali zinazoweza kufikiwa
 • Kuwatunza au mbwa anayeongoza kipofu
 • Huduma za rufaa.

 

Orodha ya mahitaji inaweza kutofautiana kutegemea mtu na mtu, upeo wake wa upofu, mahali alipo katika maisha na mapato yake, rasilimali alizo nazo na mahitaji ya familia yake.

 

Nilizungumza na mtu mmoja aliyekuwa kipofu kama mwaka mmoja baada ya kukutana naye. Tulikuwa tunazungumza mara kwa mara, lakini wakati huu nilihitimisha mazungumzo kwa kauli hii: “Rafiki, nimefurahi kuzungumza na wewe.”

 

Kulikuwa na kipindi kirefu cha ukimya, kisha akiwa anatokwa na machozi aliitikia kuwa, “Ninapenda kusikia ukisema ‘Rafiki.’ Sina watu wengi walio tayari kuwa marafiki zangu.”

 

Nilikuwa sijajua kuwa tamko la kawaida kama hilo lingeweza kuwa na maana kwa mtu fulani. Kwa kweli wema na urafiki unapunguza wingi wa maumivu na uzoefu wa huzuni ambao mtu ambaye ni kipofu anapitia. Hii ni huduma iliyo muhimu tunayohitaji wote hadi hapo Yesu atakaporudi. Kujenga urafiki kunaweza kuanza kwa neno la kawaida “Halo,” kisha unaendele katika uhusiano mzuri ikiwa tuna nia ya dhati na tuna ugumu fulani kuwanyooshea mkono wa uhusiano na ile huduma ya uponyaji ya Kristo.


 

62


Mara tu tunapokuwa marafiki na kuanzisha uhusiano uliojengeka katika uaminifu, tunaweza kuanza kuweka njozi na huyo rafiki wetu mpya. Tunaweza kuuliza maswali kama haya: Kama usingekuwa na vikwazo, ungependa kufanya nini? Ungependa kuwa nani? Je, unaamini kwamba Mungu anakujali? Ungependa kujifunza zaidi kumhusu Mungu anayewapenda watu wote? Je, unafikiri Mungu alikuumba ili uwe nani? Je, unaamini vipi kwamba umeitwa ili kumtumikia?

 

Mara nyingi tunaweka watu ndani ya “Boksi” kwa kuweka ukomo wa matazamio ya kile ambacho wanaweza kuwa, na kile wanachoweza kuchangia katika ulimwengu na hata kanisani. Hii siyo haki ya watu fulani tu. Nafasi yetu ni kutembea pembeni na kuwasaida kufungua milango ya fursa wanapokuwa wamekaribishwa na wanahitajika, kuwashtua au kuwakumbusha kadiri wanavyoongozwa na Roho Mtakatifu

 

Mazoezi

Kadiri tunavyojenga stadi, ikiwa ni za kucheza kinanda au kukimbia marathon, ni lazima tufanya mazoezi. Ikiwa tutataka uwezo mkubwa wa kuwapenda watu walio vipofu, tutaanza kwa kuwatumikia na kumwomba Mungu kuwa nasi. Kadiri tutakavyokuwa tunaachia upendo wa Mungu kupitia katika maneno na matendo yetu, Mungu ataongeza uwezo wetu wa kupenda na kutumika. Tunahitaji kumwomba Mungu atusaidie kupenda kwa jinsi alivyopenda. Upendo wa kweli kama vile Yesu alivyomaanisha kujitoa wenyewe kwa faida ya wengine: “” (Yohana 15:13)

 

Kuna fungu zuri katika kitabu cha Ufunuo ambalo lina maana maalum kwa wale walio vipofu: Ufunuo 1:7 linasema kuwa, “Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho


 

63


litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.” Hebu fikiria umuhimu wa maneno hayo kwa mtu ambaye ni kipofu na amemkubali Yesu kama Mwokozi wake.

 

Tunapowaangalia wale ambao ni vipofu katika dunia yetu hii, tunaweza kushtuka kwa takwimu hizo, au tunaweza kutulia kwanza kama Yesu alivyofanya alipokutana na mtu aliyekuwa kipofu katika huduma yake alipokuwa hapa duniani. Tunahitaji kumuuliza kuhusu mtu ambaye amemweka katika mapito yetu: “Je, unataka nifanye nini?” naye atatuonesha.

 

Mwaandishi maarufu aitwaye Helen Keller, ambaye pia ni mwanaharakati wa kisiasa, na mhadhiri aliyekuwa kipofu, aliwahi kusema kuwa: “Peke yetu tunaweza kufanya kidogo sana; tukiwa pamoja tunaweza kufanya kikubwa sana.” Hebu tufanye kazi kama mtu mmoja mmoja lakini pia tufanye kazi kwa kushirikiana hadi hapo Yesu atakapokuja. Hebu na tukamilishe zaidi kwa ajili ya Mwokozi wetu kwa niaba ya watoto wake walio vipofu. Mbingu itakuwa ni mahali pazuri sana kwa wote, na hasa kadiri macho yetu yatakavyokuwa yakiona uso wa mpendwa wetu Yesu ambaye alikuja ili wote tupate kufurahia uzima wa milele pamoja naye.

 

Huduma ya wahitaji maalum ya Waadventista wa Sabato ina vyanzo mbalimbali vinavyokusudiwa kusaidia kuhudumia watu ambao ni vipofu. Anza kwa kutembelea tovuti hii: https: //specialneeds.adventist.org/ blind kisha jiunge na kiongozi wa Huduma wa Divisheni, Union na Konferensi ya wenye uhitaji maalum ili kujifunza jinsi ya kushiriki katika kuleta mguso katika kila jimbo la dunia.


 

 

 

64