Seventh-day Adventist® Church

PASTOR LETTA'S OFFICIAL WEBSITE

Menu

MTAALA WA ELIMU SHULE YA MSINGI

UTANGULIZI

Mtaala huu ni mali ya Tanzania Union Mission - toleo la Mtaala wa Biblia. Ni kozi ya  Biblia kwa muda wa miaka 13 ambayo imeandaliwa kukidhi mahitaji ya mafundsidho ya dini kuanzia shule za awali hadi elimu za sekondari (kidato cha nne).

Kozi hii imeganywa katika ngazi tatu:
1. Miaka miwili ya Elimu ya Awali
2. Miaka saba ya Elimu ya Msingi
3. Miaka minne ya Elimu ya Sekondari

Kozi hii itakuwa inatolewa kwa kuendelea (spriral system) kwa sababu mada zinategemeana na zimerudiwa katika ngazi mbalimbali kwa kuingia ndani zaidi. Mtaala huu umekusudiwa pia kutumika kfundishia vijana wa kiadventista wanaosoma katika shule zisizo za kanisa. Kwa kuwa fildi na konferensi zinaweza zisifanikiwe kuwa na walimu wa kutosha kufundisha wanafunzi katika shule zisizo za kanisa, inashauriwa kuunganisha darasa la kwanza na la pili, la tatu na la nne, la tano, la sita na la saba, kidato cha kwanza na cha pili na kidato cha tatu na cha nne. Sehemu ya kidato cha tatu na cha nne ya mtaala huu ina mada ambazo zimelenga kuwaanda wanafunzi kwa ajili ya kufanya mtihani wa kidato cha nne wa Biblia uitwao Bible Knowledge (Maarifa ya Biblia).

 

TATHMINI YA MAHITAJI

1. Maandiko Matakatifu ni kipimo kikamilifu cha ukweli na kwa hiyo yanapaswa kupewa nafasi ya juu sana katika elimu. “Ili kupata elimu inayostahili jina (la Mungu), ni lazima tumjue Muumbaji na Kristo Mkombozi kama wanavyofunuliwa katika maneno matakatifu” (Education, uk.27).

2. Elimu haikamiliki bila dini kama kitu cha kuidhibiti. Ni lazima ijengwe juu ya Maandiko Matakatifu.

3. Mitaala katika shule zetu ni lazima imfanye Mungu kuwa kiini cha elimu hiyo na Biblia kikiwa kitabu kinachoongoza mambo yote ya elimu.

4. Mtaala huu umeingiza maadili ya kiafrika yanayofaa kwa kutumia mifano ya kufundishia kutoka katika jamii mbalimbali za kiafrika.

 

UMUHIMU WA MTAALA HUU

Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataishahu hata atakapokuwa mzee, (Mithali 22:6).Kwa hiyo, ni wajibu wa kila mhusika anayejali, awe mzazi, shule, makanisa na walimu kufanya kazi kwa pamoja ili kutoa mafundisho yanayofaa kwa vijana. Mafundsiho yatakayowawezeaha kuwa watenda kazi wenza pamoja na Kristo na yatakayowandaa kwa ujio wake (Yesu) wa mara ya pili. “Kwa jeshi hilo la watenda kazi kama vijana wetu, wakiwa wamefundishwa kwa usahihi, watatoa kwa haraka kiasi gani ujumbe wa Mwokozi aliyesulubishwa na kufufuka na anyekuja upesi, ujumbe unaweza kupelekwa katika dunia yote”. (Ellen White, 1943, uk. 555).

Mtaala huu utakuwa mwongozo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa mada zinazofundshwa zinafanana na zinakubaliana na mafundisho ya Kanisa la Waadventista Wasabato.

 

NAMNA YA KUTUMIA MTAALA HUU

Wakurugenzi wa Elimu wa Konferensi na Fildi watahitajika:

  • Kuwa waratibu wakuu wa mtaala
  • Kuwasimamia na kwasaidia walimu wa Biblia walei
  • Kuteua wakufunzi/walimu wa kusaidia kazi ya kufundisha
  • Kuendesha mafunzo kwa walimu walei
  • Kujadili na walimu juu ya mada ngumu
  • Kupata mrejesho kutoka kwa wote wanaotumia mtaala huu
  • Kusaidia katika kufanya marekebisho ya mtaala kwa kuzingatia mapendekezo, mafanikio na matatizo yatokanayo na matumizi ya mtaala

Mtaala huu utatumika kwa majaribio kwa muda fulani na kwa hiyo maoni ya kuuboresha yanakaribishwa ili kuufanya uwe rahisi zaidi kuutumia.

 

MALENGO YA MTAALA

Malengo yaliyoorodheshwa hapa chini ni ya jumla na yanahusu mtaala mzima. Walimu wanategemewa kuwa na malengo mahsusi kwa kila mada inayofundishwa. Lengo la kwanza kabisa kwa mwalimu linapaswa kuishi maisha ambayo yatakuwa  kielelezo cha misingi ya biblia anayayoifundisha kwa wanafunzi. Kila mada inapomalizika inapaswa kutoa  fundisho la kiroho kwa wanafunzi.

Inatarajiwa kuwa mwisho wa kozi hii ya kina, wanafunzi wataweza:

  1. Kumuelewa Mungu kama nafsi ambaye wanaweza kumjua
  2. Kuielewa Biblia kama njia ya kumjua Mungu
  3. Kufahamu ufunuo wa ukweli juu ya Mungu kupitia kila tukio lililoandikwa na kila fundisho
  4. Kuyaelewa maandishi ya Ellen G.White kama ushuhuda mwingine juu ya ukweli kuhusu Mungu
  5. Kufahamu kuwa kusudi la ibada ni ili tuwe zaidi na zaidi kama Kristo tunayempenda
  6. Kuwa na uelewa wa misingi 28 ya imani ya Kanisa la Waadventista Wasabato
  7. Kufahamu asili ya uasi ambao umetokea ulimwenguni, mabadiliko ambayo uasi huu umeleta ulimwenguni pamoja na suluhisho na uasi huo ambalo linapatikana kwa kumjua Mungu.
  8. Kujifunza kwamba kushiriki imani yao na watu wengine itakuwa ni namna ya asili ya kukuza uelewa wao juu ya Mungu
  9. Kutambua kuwa Mungu aliyeumba ulimwengu ulio huru amewapatia upendeleo na wajibu wa kufanya uchaguzi wao wenyewe. Kwa hiyo wanaonyesha kama wanaweza kuaminiwa kwa kuwa na uhuru na uzima wa milele
  10. Kuwa na uelewa wa ujumbe wa afya kama sehemu ya muhimu ya Mafundisho ya Kanisa la Waadventista Wasabato
  11. Kuelewa asili ya Mwanadamu: Mwanadamu aliyeanguka na anayehitaji kurejeshwa katika sura ya Mungu, Yohana 3:16

 

NJIA ZA KUFUNDISHIA NA SHUGHULI ZA KUFANYA

 

Njia za kufundisha zitakuwa tofauti wakati wote, kutegemeana na mwalimu, mada, aina ya wanafunzi na darasa walilofikia. Hata hivyo, hapa chini kuna mifano michache ya njia ambazo zinatumiwa mara nyingi na walimu na kwa kiasi Fulani zimebainika kuleta ufanisi.

1.a Ufundishaji wa moja kwa moja

Hii ni kanuni ya ufundishaji ambapo mwalimu ndiye mtoaji mkuu wa maarifa. Mwalimu huhamisha kweli fulani kutoka kwake kwenda kwa wanafunzi kwa nia ya moja kwa moja kwa kadri inavyowezekana. Tofauti na njia ya kutoa mhadhara, katika njia hii ya ufundishaji wa moja kwa moja mwalimu anapaswa kuhakikisha kuwa wakati wa kufundisha kutakuwa na mawasiliano kati ya mwalimu na mwanafunzi yanayohusisha maswali na majibu, marudio na mazoezi na masahihisho.

Faida kubwa za njia ya ufundishaji wa moja kwa moja ni kwamba:
(i) Ni njia iliyo na mwelekeo wa kitaaluma zaidi ambapo mwalimu huelekeza, kutawala na kupunguza muda wa mwanafunzi kujifunza.

(ii) Hutoa nafasi kwa mwalimu kufuatilialia uelewa wa mwanafunzi kwa sababu mwalimu huwasilisha mada yake kwakwa hatua zilizopangiliwa na kwa kawaida ataenda kwenye hatua inayofuata baada ya wanafunzi kuielewa hatua iliyopita

1.b Mchezo-kielelezo

Hii ni njia ya ufundishaji ambapo wanafunzi darasani wanachaguliwa ili kuigiza halifulani huku wanafunzi wenzao wakiwaangalia na kuchukua masuala fulani ya mchezo kwa kufuata maelekezo ya mwalimu. Njia hii ni nzuri lakini haitumiki sana na inahitaji muda wa kutosha na maandaalizi yaliyopangaliwa vizuri. Mchezo kielelezo, usipopangailiwa vizuri, unaweza kuishia kuwa maburudisho badala ya kuwa njia ya kufundishia. Kwa maneno mengine, wanafunzi wanaweza wasipate maarifa yaliyokusudiwa na mwalimu anaweza asifikie malengo yaliyokusudiwa.

Mchezo-kielelezo huwaweka wanafunzi katika mazingira halisi ya tukio au shughuli husika. Kwa mfano, wanaweza kuigiza kisa cha Yusufu na ndoto zake, wanawali kumi, mwana mpotevu n.k. Kwa hiyo, pale inapowezekana, mwalimu atumie njia hii. Ili kufanikiwa kufikia malengo ya somo yaliyokusudiwa, mchezo kielelezo ni lazima upangiliwe na kuandaliwa vizuri.

1.c Kusimulia visa

Ufundishaji kwa njia ya kusimulia visa ni njia yenye yenye mafanikio makubwa hasa ikitumika kwa wanafunzi wa elimu ya Awali na Msingi. Hata hivyo, mwalimu ni lazima ajipange na kuandaa vizuri mada yake ili kisa kiwe hai na kivutie. Matumizi ya lugha rahisi na vielelezo kutoka katika mazingira yao na shghuli za kila siku ni muhimu sana. Kwa visa rahisi vya biblia, mwalimu awape kazi ya kuvisoma wao wenyewe kutoka kwenye Biblia na kisha kuvisimulia kwa wanafunzi wenzao darsani.


1.d “Project”

“Project”zinaweza kufanywa na mwanafunzi mmoja au kikundi. Mwalimu anapaswa kutoa maelekezo yanayoeleweka vizuri juu ya nini wanafunzi wanatakiwa kufanya. Baadhi ya project zinaeza kuwa:

          i.    Vikundi vya maombi

          ii.    Mikutano maalum ya kidini (retreats)

          iii.   Kutembelea kanisa jingine au shule nyingine

          iv.   Ushuhudiaji

          v.    Kwaya

Shughuli hizi zote zinaweza kusaidia kukuza hali ya kiroho ya wanafunzi. Kwa ajili ya ufanisi, shughuli hizi ni lazima ziratibiwe vizuri na mwalimu.

1.e Mijadala

Itapendeza kama kutafanyika mjadala baada ya wanafunzi kusoma mada fulani iliyoandaliwa. Mjadala unaweza kufanyika katika vikundi vya watu wachache na baadaye kila kikundi kikawasilisha yale yaliyojadiliwa. Katika maandalizi ya mjadala, ni muhimu mwalimu aandae maswali mahususi kwa ajili ya majadala husika na ausimamie vizuri mjadala huo. Kwa:

            i.     Kupanga dakika zitakazotumika kwa ajili ya mjadala

            ii.    Baada ya mjadala, kila kikundi kipewe muda wa kuwasilisha waliyojadili

            iii.   Mwalimu ahitimishe mjadala kwa kutoa muhtasari wa yaliyojadiliwa na kutoa majibu ya maswali yaliyokuwa yanajadiliwa

 
1.f Kupaka rangi

Upakaji rangi ni njia nyingine ya kujifunza inayowavutia  wanafunzi hasa wa shule za awali na msingi. Pale inapowezekana, wanafunzi wapewe kazi ya kupaka rangi picha zinazowakilisha kisa fulani cha Biblia.

Sambamba ba njia hizi za ufundishaji, ushauri ufuatao unaweza kumsaidia mwalimu:

  1. Kila somo la Biblia lianze kwa ombi na kuhitimishwa kwa ombi
  2. Kila somo lazima lihitimishwe na kitu cha kujifunza kiroho
  3. Biblia itumike kwa kila somo la Biblia na wanafunzi wapewe fursa ya kufanya rejea na kusoma katika Biblia zao wenyewe
  4. Mwalimu ajitahidi kutumia vifaa vinavyosaidia kufundisha kama vile  overhead Over head projector, ramani, picha n.k
  5. Mwalimu aepuke kuhubiri bali afundishe

Kwa jaili yoyote ya ufundishaji itakayotumika, walimu waadventista ni lazima waige mfano wa Mwalimu mkuu (Yesu) kama kielelezo cha ufundishaji. Aliishi maisha yanayoendana na kile alichofundisha. Misingi mikuu katika ufundishaji wake ilizingatia: upendo, wema, uvumilivu, unyenyekevu na haki.

 

ELIMU YA AWALI

MWAKA WA KWANZA

MUHULA WA KWANZA

 

WIKI

MADA

REJEA

Sura na kurasa zilizoonyeshwa ni katika vitabu vya kiingereza

WIKI YA 1

Mungu:

  1. Mungu ni nani?
  2. Yuko wapi?
  3. Utatu Mtakatifu wa mbinguni
  4. Tufundishe kuomba – Sala ya Bwana

 

 

WIKI YA 2

Baraka za Mungu

  1. Hewa
  2. Maji
  3. Uzima
  4. Pumziko
  5. Mazozezi
  6. Tufundishe kuomba - Sala ya Bwana

 

WIKI YA 3-6

Hapo Mwanzo

  1. Juma la uumbaji

                                i.            Siku ya kwanza na pili

                                ii.           Siku ya tatu nay a nne

                                iii.          Siku ya tano nay a sita

                                iv.           Siku ya Saba

  1. Tufundishe kuomba

Mwanzo 1:5

Wazee na Manabii  sura ya 2, 47 na 48

Mathayo

WIKI YA 7

Bustani ya Edeni:

a. Bustani iliyo nzuri

b. Adamu na Hawa wakifanya kazi bustanini

c. Mahali pa kukutania na Mungu

d. Amri na maelekezo ya Mungu

Mwanzo 2

WIKI YA 8

a. Lusifa, malaika mkuu na mzuri

b. Nafasi ya Lusifa mbinguni

c. Anguko la Lusifa

 

Wazee na Manabii sura ya 36-43

Story of Redemption sura ya  13-18

Tumaini Kuu 496-498,500.

WIKI YA 9 - 10

Muongo mkuu:

a. Adamu na Hawa wadanganywa

b. Adamu na Hawa wavunja amri ya Mungu

c. Wafukuzwa bustanini

d. Mungu awafanyia nguo

Ufunuo 12:7- 9

Wazee na Manabii uk. 41-43

Story of Redemption uk. 17-19

Tumaini Kuu uk. 498-500

WIKI YA 11

a. Watoto wa kwanza kuzaliwa duniani: Kaini na Habili

b. Kazi za Kaini na Habili

c. Kaini amuua ndugu yake Habili – mtu wa kwanza kufa

d. Matokeo ya dhambi

 

 

WIKI YA 12

Henoko: Mtu aliyetembea na Mungu:

a. Henoko alikuwa nani?

b. Henoko alienda pamoja  na Mungu

c. Henoko alitwaliwa na Mungu

d. Tunaweza kuenda pamoja na Mungu

Mwanzo 5

Wazee na Wafalme sura ya 6

Story of Redemption sura ya 7

WIKI YA 13

Safina ya kwanza kujengwa duniani:

a. Nuhu aambiwa na Mungu kujenga safina

b. Nuhu ahubiri kwa miaka 120

c. Mungu aleta mvua kubwa na mafuriko

d. Nuhu na familia yake waokolewa pamoja na wanyama waliochaguliwa

c. Upinde wa mvua

Wazee na Manabii uk. 95 - 97

Story of Redemption uk. 64

Mwanzo  sura ya 6 hadi 9

WIKI YA 15

a. Jengo la kwanza la ghorofa duniani

b. Mungu awatawanya wajenzi wa ghorofa

Mwanzo sura ya 11

WIKI YA 16-18

a. Isaka: Mtoto wa pekee wa Abrahamu

b. Esau na Yakobo: Watoto wa Isaka

c. Esau auza  uzaliwa wake wa kwanza

d. Yakobo amdanganya baba yake ili kupata mibaraka

e. Ndoto ya Yakobo: Ngazi ndefu

f. Yakobo apigana na malaika

 

WIKI YA 19-20

Familia ya Yakobo:

a. Watoto 12 wa Yakobo

b. Yusufu:Mtoto anayependwa

c. Ndoto za Yusufu

d. Yusufu auzwa na nduguze

Mwanzo 37:1-36

Wazee na Manabii uk. 209 -231

 

 

ELIMU YA AWALI

MWAKA WA KWANZA

MUHULA WA PILI

WIKI

MADA

VITABU VYA REJEA

WIKI YA 1-2

Kisa cha Yesu:

a. Yusufu na Mariamu: wazazi waYesu

b. Yesu azaliwa katika hori la ng’ombe

c.  Malaika watoa taarifa

d. Mamajusi wa Mashariki

Mathayo sura ya 1

WIKI YA 3

a.Mtoto Yesu akimbizwa Misri kwa usalama

b.Safari ya kurudi Nazareti

Mathayo sura ya 2

WIKI YA 4

a.Yesu aenda hekaluni na wazazi wake

b.Yesu abaki hekaluni na kutoonekana kwa siku  3

Luka sura ya 2:41-52

WIKI YA 5

a.Yesu abatizwa

b. Yesu ajaribiwa na shetani

Mathayo sura ya 3 na 4

WIKI YA 6-7

a. Yesu: Rafiki wa watoto

b. Yesu:Tabibu mkuu

c.  Yesu ashtakiwa na kusulubishwa

Mathayo sura ya 4

WIKI YA 8-10

Kuzaliwa kwa Samweli:Kijana mdogo aliyeitwa kumfanyia Mungu kazi

a. Ombi la mama ili kupata motto

b. Kuzaliwa kwa Samweli

c. Hanna amtoa Samweli kwa Mungu

d. Samweli aitwa na kuongea na Mungu

Samweli sura ya 1-3

Wazee na Manabii uk. 569-573

WIKI YA 11-14

Daudi:Mvulana  mchungaji

a. Maisha ya Daudi kama mchungaji

b. Daudi na Goliathi

c. Daudi na Yonathani

Wazee na Manabii uk. 635-648

1 Samweli sura ya 16-20

WIKI YA 15-18

a. Mtu mkubwa mfupi

b. Mara 490 na zaidi

c. Nyumba juu ya mwamba

d. Nuru na chumvi

e. Taa ndogo kumi

Luka  sura ya 19

Mathayo sura ya 25

WIKI YA 19-20

Mfalme kijana mwenye hekima:Sulemani

Kuishi maisha yenye afya

1 Wafalme 3:17 – 22

Wazee na Manabii uk. 750-755

Wazee na Wafalme uk.25-50

1 Mambo ya Nyakati sura ya 28 na 29

2 Mambo ya Nyakati sura ya 1,6, 7:1-4

 

 

SHULE YA AWALI

           MWAKA WA PILI

     MUHULA WA KWANZA

 

WIKI

MADA

VITABU VYA REJEA

WIKI YA 1-2

a. Kuzaliwa kwa Musa

b. Musa afichwa pembeni mwa mto

c. Musa aokotwa na binti Farao

d. Musa katika nyumba ya Farao

e. Musa akimbia kwa Farao

Kutoka

Wazee na Manabii uk. 241-244

Matendo 7:22-29

Wazee na Manabii uk. 247 -265

WIKI YA 4-5

a. Musa mchunga kondoo

b. Kichaka kinachoungua

c. Musa arudi tena Misri

Kutoka 4:27-31; 5,6

Wazee na Manabii uk.257 - 265

WIKI YA 6-9

Waache watu wangu waende:

a. Vyura,chawa, mainzi, magongwa,

majipu, mvua yam awe, nzige na giza

c. Kutoka Misri

d. Kuvuka bahari ya Shamu

Kutoka 8, 9:1-7, 9:8-35

Wazee na Manabii uk.265 -287

Kutoka sura ya 11, 12, 13, 14

Wazee na Manabii uk.287 -296

Zaburi 104:33

WIKI YA 10

Mafuriko kutoka mbinguni:

a.Mungu awalisha watu wake kwa mana na kwale kutoka mbinguni

 

Kutoka 15:22-27

Kutoka 16:1-21

Wazee na Manabii uk. 291- 295

WIKI YA 11

Mali ya Mungu:

a. Zaka na sadaka

b. Miili yetu

c. Mazoezi

 

WIKI YA 12-13

Anguko la Yeriko

a. Wapelelezi watatu

b. Wapelelezi wawili

c.  Rahabu awaokoa wapelelezi

d.  Anguko la Yeriko

Joshua  sura ya 5:10-15

Joshua sura ya 6

Wazee na Manabii uk. 487 – 493

Waebrania 11:30

WIKI YA 14 -16

Samson: Mtu ambaye hakuwahi kunyoa

a. Kuzaliwa kwa Samsoni

b. Mpango wa Mungu kwa Samsoni kuwaokoa watu wake

c. Kifo cha Samsoni

 

WIKI YA 17 - 18

Amri kuu za Mungu:

a. Musa akutana na Munu katika mlima Sinai

b. Mungu atoa mbao mbili za mawe zenye amri za Mungu

c. Amri kumi za Mungu

Kutoka 20:12-17

Wazee na Manabii uk. 308-309

WIKI YA 19 -20

Gidioni

a. Mungu amwita kijana Gidioni

b. Gidioni apigana vita akiwa na watu 300

Wafalme sura ya 7

Wazee na Manabii uk. 546-556

 

MUHULA WA PILI

WIKI

MADA

VITABU VYA REJEA

WIKI YA 1-2

Kisa cha Ayubu

a. Ayubu na utajiri wake

b. Ayubu apoteza mali zake zote

c. Ayubu augua

d. Ayubu abarikiwa tena

e. Uwakili: Vyote viijazavyo ni mali ya Bwana

Ayubu sura ya 1-4

WIKI YA 3-4

Nabii aliyekimbia

a. Yona aitwa na Mungu

b. Yona aitwa ajaribu kumkimbia Mungu

c. Yona katika tumbo la samaki

d. Samaki amtapika Yona

e.Hatuwezi kumkimbia Mungu

 

WIKI YA 5-6

Kisa cha Eliya na mfalme Ahabu

a.Nabii Eliya atumwa na Mungu kwenda kwa Ahabu

b.Nabii Eliya na manabii wa Baali katika mlma Karmeli

1 Wafalme sura ya 16 hadi 21

WIKI YA  7- 11

Vijana wanne wa kiyahudi huko Babeli:

a. Jaribu la chakula kwa siku 10

b. Tanuru la moto

c. Ndoto  za Nebukadreza

d. Mfalme aliyekula nyasi kwa siku

e. Sherehe amayo haikukamilika

f. Maadnishi ukutani

g. Kutupwa katika tundu la simba

Danieli sura ya 1 hadi 6

WIKI YA 12-13

a. Mwana mpotevu

b. Kondoo mpotevu

c. Lulu ya thamani

Luka sura ya 15

WIKI YA 14

Kanuni ya muhimu:

a. Kisa cha msamaria

Luka sura ya 10:25-37

WIKI YA 15-16

Kisa cha Lazaro:

a. Kifo ni nini?

b. Yesu ana uwezo wa kufufua wafu

c. Lazaro afufuliwa

 

Yohana sura ya 11

WIKI YA 17-18

Kutoka mteasji hadi mhubiri mashuhuri:

a.Sauli katika barabara ya Dameski

b.Sauli akutana na Mungu njiani

c. Sauli awa Paulo mhubiri

Matendo sura ya 9

WIKI YA 19-20

Esta awaokoa watu wake

a. Esta awa malkia

b. Esta aokoa maisha ya Mordekai

c. Haman anyongwa

Esta sura ya 1 hadi ya 8

 

SHULE YA MSINGI

DARASA LA KWANZA

MUHULA WA KWANZA

WIKI YA 1-4

Hapo mwanzo:

a. Mungu na malaika

b. Mungu ni nani?

c. Utatu wa mbinguni

   i.  Mungu Baba

   ii. Mungu mwana

   iii.Mungu Roho Mtakatifu

  1. Tufundishe kuomba (Sala ya Bwana)

Mwanzo sura ya 1

 

Mathayo sura ya 6

WIKI YA 5-8

Kisa cha uumbaji

a. Uwezo wa Mungu wa kuumba

b. Juma la uumbaji

c. Mungu apumzika siku ya saba

d. Eden:Nyumbani kwa Adamu na Hawa

Mwanzo sura ya 1

WIKI YA 9-13

Vita mbinguni

a. Nafasi ya Lusifa

b. Mwanzo wa ubinafsi

c. Lusifa ashindwa na kutupwa duniani

Wazee na Manabii uk.34-38

Tumaini kuu uk.392-498

Story of Redemption uk.13-15

Isaya 14:13

Ufunuo 12:7-9

Kumbukumbu 32:4

WIKI YA 14-16

Mibaraka ya Mungu:

a. Maji

b. Uzima

c. Hewa

 

WIKI YA 17-19

Anguko la mwanadamu

a. Maelekezo ya Mungu kwa Adamu na Hawa

b. Muongo mkuu

c. Matokeo ya kuotii maelekezo ya Mungu

d. Adamu na Hawa wafukuzwa Edeni

e. Kifo na laana

Mwanzo sura ya 2

Wazee na Manabii uk.36-38

Ezekieli 18:4

Mwanzo sura ya 3

1 Timotheo 6:15

1 Wakorintho 15:20-22

 

MUHULA WA PILI

WIKI

MADA

VITABU VYA REJEA

WIKI YA 1-4

Kaini na Habili:

a. Tabia na kazi zao

b. Mtu wa kwanza kufa na muuaji wa kwanza

c. Mungu husikia na hujibu maombi yetu

Mwanzo sura ya 4

Mwanzo 2:17

WIKI YA 5-6

Uwakili wa miili yetu

a. Kuishi maisha yenye afya

b. Pumziko na mazoezi

 

WIKI YA 7-8

Kutembea na Mungu

a. Henoko:Mtu aliyekwenda pamoja na Mungu

b.Uaminifu wa Henoko

Mwanzo sura ya 5

Wazee na Manabii sura ya 5

Story of redemption sura ya 6

WIKI YA 9-12

Kisa cha gharika

a. Nuhu mtu pekee mwaminifu

b. Mungu  amwambia Nuu kutengeneza safina

c. Nuhu atengeneza safina na kuhubir I kwa  kwa miaka 120

d. Nuhu aingia kwenye safina pamoja na familia yake na wanyama safi

e. Mvua kubwa yanyeha kwa siku 40

f. Nuhu atoka kwenye safina

g. Upinde wa mvua

h. Matokeo ya gharika

i.   baada ya gharika

Mwanzo sura ya 6

Wazee na Manabii uk.90-95

Story of Redemption uk.62-64

WIKI A 15-19

Kisa cha jengo la ghorofa

a. Mnara wa Babeli

b. Mungu awatawanya wajenzi

Mwanzo sura ya 11

 

DARASA LA PILI

MUHULA WA KWANZA

WIKI

MADA

VITABU VYA REJEA

WIKI YA 1-4

Familia ya Abraham

Kuitwa kwa Abramu:

a. Mungu amuita Abramu na kumulekeza kwenda katika nchi isiyojulikana

b. Safari ya Abramu kwenda Kanaan kupitia Harani

c. Abramu aenda Misri na kisha kurudi tena Kanaani

 

Mwanzo sura ya 12-14

WIKI YA 5-9

Upendo kwa wengine

a. *Abrahamu amuokoa Luthu

b. Luthu ahamia Sodoma

c.  *Abrahamu apata wageni

d. Ombi maalumu la Abrahamu kwa ajili Luthu na Sodoma

d. Kungamizwa kwa Sodoma

e. Mke wa Luthu

*Ni Abrahamu au Abramu?

 

Mwanzo sura ya 13, 18 na 19

Wazee na Manabii uk 138 -140 na uk. 156 - 169

WIKI YA 10-14

Ahadi za Mungu ni za kweli wakati wote:

a. Mungu atoa ahadi ya motto kwa Abramu

b. Hajiri na Ishmaeli

c. Isaka, mtoto wa pekee

d.Isaka amuoa Rebeka

e.Jina la Abramu labadilika na kuwa Abrahamu

Mwanzo sura ya 21, 23 na 24

Wazee na Manabii uk. 145- 147 na uk. 171-176

 

WIKI YA 15-19

Isaka na familia yake

a.  Ndugu wawili pacha waliokuwa tofauti

b.  Esau auza uzaliwa wa kwanza

c.  Yakobo amdanganya baba yake

d. Yakobo akimbilia Harani: ngazi ndefu

e.  Maisha ya Yakobo huko Harani

f.  Yakobo aoa

g. Yakobo arudi nyumbani:Ashindana na malaika:Jina la Yakobo labadilika kuwa Israeli

 

Mwanzo sura ya 23, 24, 26 na 27

 

Isaya 65:25

 

DARASA LA PILI

MUHULA WA PILI

WIKI

MADA

VITABU VYA REJEA

WIKI YA 1-4

Yakobo na familia yake huko Kanaani

a. Watoto 12 wa Yakobo

b. Yusufu: Mtoto anayependwa, muotaji

c.Yusufu:Kutoka mtoto anayependwa hadi mtumwa

Mwanzo sura ya 29, 37, 39, 41 na 45

Wazee na Manabii uk. 209 - 231

WIKI YA 5-8

Yusufu akiwa Misri:

a. Yusufu katika nyumba ya Potifa

b. Yusufu atafsiri ndoto  ya Farao

c. Yusufu awa kiongozi

 

Tufundishe namna ya kusali: Sala ya Bwana

Mwanzo sura ya 37,

39, 41 na 45

Wazee na Manabii uk. 221-223

 

Mathayo sura ya 6

WIKI YA 9-12

Neno la Mungu

a. Biblia

b. Kuandikwa kwa Biblia

c. Msingi wa ibada ya kweli

d. Je, Mu ngu husikia na kujibu maombi?

SDA Believe sura ya 1

WIKI YA 13-15

Yakobo na familia yake waenda Misri:

a.Yakobo na familia yake wakaa Misri

b.Mateso baada ya kuifo cha Yusufu

Mwanzo sura ya 42

Kuotka sura ya 1

WIKI YA 16-20

Nguvu ya Mungu ya iokoayo na ilindayo:

a. Kuzaliwa kwa Musa

b.Maisha ya Musa katika nyumba ya Farao

c. Musa aenda Midiani

d. Maisha ya Musa utotoni akiwa na mama yake

e. Musa aitwa na Mungu:Kichaka kinachowaka moto

 

Kutoka sura ya 2 na 3

Wazee na Manabii uk. 251- 256

 

DARASA LA TATU

MUHULA WA KWANZA

WIKI

MADA

VITABU VYA REJEA

WIKI YA 1-5

Mungu aokoa watu wake:

a. Musa na Haruni wakutana na Farao

b. Mapigo kumi

c. Kutoka Misri

d. Kuishi maisha yenye afya:Mazoezi, Maji, Hewa safi, pumziko

Kutoka sura ya 4 - 6

Wazee na Manabii uk. 257-265

Wazee na Manabii uk.265 -282

WIKI YA 6-9

Wokovu wa mwanadamu:

a. Kuzaliwa kwa Yesu

b. Kifo na kufufuka kwa Yesu

Mathayo sura ya 1-2

WIKI YA 10-13

Safari ya waisraeli jangwani:

a. Kuvuka bahari ya Shamu

b.Wingu na moto

c. Chakula kutoka mbinguni na maji kutoka kwenye mwamba

Kutoka sura ya 14 – 16

Wazee na Manabii uk. 283-298

WIKI YA 14-17

Safari ya kutoka bahari ya Shamu hadi mlima Sinai:

a. Amri kumi za Mungu

b. Ndama wa dhahabu

Kutoka sura ya 20

WIKI YA 18-20

Kunaguka kwa mji wa Yeriko:

a. Wapepelelezi 12: Yoshua na Kalebu

b. Musa aupiga mwamba mara mbili

c. Kifo cha Musa

Kutoka sura ya 20!

 

DARASA LA TATU

MUHULA WA PILI

WIKI

MADA

VITABU VYA REJEA

WIKI YA 1-4

Sheria ya Mungu

a.Musa aongea na Mungu katika mlima Sinai

b.Amri kumi za Mungu

c.Ibada ya sanamu/wanyama katika jamii za kiafrika

e.Tufundishe namna ya kusali:sala ya Bwana

Kutoka sura ya 20, 24 na 52

Wazee na Manabii uk. 308-330

 

Mathayo sura ya 6

WIKI YA 5-6

Matokeo ya kutokumtii Mungu:

a. Taifa la Israeli walimuasi Mungu

b. Mungu atuma nyoka wenye sumu

c. Musa atengeneza nyoka wa shaba

Hesabu sura ya 10, 11, na 21, 12

Wazee na Manabii uk.376 - 405

WIKI YA 7-8

Maisha ya Kikristo:

a. Miili yetu kama hekalu la Roho Mtakatifu

b. Chakua cha awali

SDA Believe sura ya 21

1Wakorintho 6:15

WIKI YA 9-11

Yoshua ateuliwa:

a. Makosa ya Musa na adhabu yake

b. Joshua ateuliwa kuchukua nafasi ya Musa

c. Kifo cha Musa

Yoshua sura ya 1

Hesabu 20: 1-13

Wazee na Manabii uk.406-421 na

 462-480

WIKI YA 12-13

Taifa la Israeli chini ya uongozi wa Yoshua:

a. Kushambuliwa kwa mji wa Yeriko

b. Kuvuka mto Yordani

Wazee na Manabii uk. 481 – 486

Yoshua sura ya 1, 3-6

Wazee na Manabii uk. 487- 493

WIKI YA 14-16

Taifa la Israeli lapata mfalme:

a.Wana wa Israeli wakataa utawala wa Mungu

b.Wana wa Israeli wataka wawe na Mfalme:

c. Familia zetu leo

d.Mahusiano ya familia na jamii

e. Familia ya kikristo/Familia ya Mungu

1 Samweli sura ya 8 na 9

Wazee na Manabii uk. 592 -615

Elimu uk.45-50

WIKI YA 17-20

Familia na maisha ya familia:

a. Familia katika muktadha wa kiafrika

b. Familia ya awali

c. Familia zetu leo

d. Mahusiano kati  ya familia na jamii

e. Familia ya kikristo/Familia ya Mungu

SDA believe sura ya 2

Mwanzo 12:3

Waefeso 3:15

 

DARASA LA NNE

MUHULA WA KWANZA

WIKI

MADA

VITABU VYA REJEA

WIKI YA 1-4

Kisa cha Daudi:

a. Daudi atiwa mafuta kuwa mfalme wa pili wa Israeli

b. Daudi na Goliathi

c. Daudi na Yonathani:Marafiki wa kweli

1 Samweli 16 na 17

Wazee na Manabii uk.637-648, 660 – 664, 701-702

2 Samweli 5

 

 

WIKI YA 5-9

Maisha na kifo cha Yesu:

a. Maisha ya awali ya Yesu

b.Yesu aenda kanisani

c. Ubatizo:Yesu abatizwa na Yohana

d. Maana ya ubatizo na maandalizi kwa ajili ya ubatizo

e. Ubatizo wa kuzamishwa majini

f. Umuhimu wa ubatizo

Mathayo?

SDA believe sura ya 14

Mathayo sura ya 20

Matendo sura ya 13

Warumi 6:14

Waebrania 6:2

Waefeso 4:5

Wakolosai 2:12

SDA believe sura ya 4

WIKI YA 10-14

Kifo:

a. Maelezo ya kiafrika kuhusu hali ya wafu

b. Maelezo ya biblia kuhusu hali ya wafu

c. Uwezo wa  Yesu dhidi ya kifo

SDA believe

Zaburi 6:5

Yohana 11:11-14

1 Thesalonike 4:16-18

 

WIKI YA 15-19

a. Yesrusalemu: Mji mkuu wa Daudi

b. Vita dhidi ya wafilisti

c. Daudi apanga kujenga hekalu

d. Dhambi ya Daudi

e. Daudi na Nathan

f. Dhambi kubwa ya Daudi

2 Samweli 10 -12

Wazee na Manabii 714-726, 745-748

2 Samweli 19-24

 

 

DARASA LA NNE

MUHULA WA PILI

WIKI

MADA

VITABU VYA REJEA

WIKI YA 1-5

a. Abrahamu: Rafiki wa Mungu

b. Wageni wa Abrahamu

c. Wageni wa Luthu

d. Maisha ya Luthu akiwa Sodoma

e. Sodoma yaangamizwa

Mwanzo 15- 19

Wazee na Manabii uk. 136-140

WIKI YA 6-9

a. Isaka:mwana wa ahadi

b. Mungu amjaribu Abrahamu

c. Abrahamu ashinda jaribu

Mwanzo 21 na 22

Wazee na Manabii uk. 145-147

WIKI YA 10-12

a. Mapacha waliokuwa hawafanani

b. Kudanganya ili kupata mibaraka ya Mungu

c. Mungu amsamehe Yakobo

d.Yakobo asafiri kurudi nyumbani

Mwanzo 25, 28-29

Wazee na Manabii uk. 179-181

 

 

WIKI YA 13-16

a. Yusufu:Muotaji

b. Kutoka mtoto anayependelewa hadi mtumwa anayedharauliwa

c. Kijana mdogo ambaye hangeweza kutenda dhambi

c. Mwana mpotevu

Mwanzo sura ya 37-39

Wazee na Manabii uk. 211-212

WIKI YA 17-19

a. Kutoka mtumwa hadi mtawala

b. Ndugu wenye njaa

c. Dhifa ya kushtukiza

d. Yusufu ajitambulisha

 

Mwanzo sura ya 37 -39

Wazee na Manabii uk. 221 - 223

 

DARASA LA TANO

MUHULA WA KWANZA

WIKI YA 1-3

a. Siku za giza katika Israeli

b. Eliya:Yahwe ni Mungu wangu

c. Mungu amficha Eliya

1 Wafalme 16, 17 na 18

 

WIKI YA 4

Mtumishi mchoyo

2 Wafalme 5

WIKI YA 5-6

a.Yosia:Mfalme wa Yuda mtoto

b.Yosia aliongoza taifa kwa Mungu

2 Wafalme 22

2 Wafalme 23

WIKI YA 7-9

a. Ndoto iliyosahaulika

b. Tanuru la moto

Danieli sura ya 2 na ya 3

WIKI YA 10-13

a. Mvulana kutoka Nazarethi

b. Malaika waimba

c. Mamajusi wa Mashariki

d. Kukimbilia Misri

e. Yesu katika pasaka yake ya kwanza

Luka sura ya 1 na ya 2

WIKI YA 14-17

a. Yesu aenda kisimani

b. Yesu apumzika katika kisima cha     Yakobo

c.Yesu aponya akiwa mbali

d. Sabato yenye shuhuli nyingi

e. Kipofu mwombaji apata hitaji lake

f. Dhoruba katika ziwa Galilaya

g.Yesu atumia chakula cha mchana cha mvulana

h. Mmoja ashukuru badala ya kumi

Yohana sura ya 1, 4 na 6

Marko sura ya 1, 4 na 4

Luka sura ya 7

 

WIKI YA 18-19

a. Huduma ya Yesu katika hekalu la mbinguni

b. Kuja kwa Yesu mara ya pili

c. Kifo na ufufuo

Adventist believe

 

DARASA LA TANO

MUHULA WA PILI

WIKI

MADA

VITABU VYA REJEA

WIKI YA 1-5

Uaminifu na mkono wa Mungu wa ulinzi:Danieli, Meshaki, Shadraka, Abednego wakiwa Babeli

a. Jaribu juu ya chakula

b.Shadraka, Meshaka na Abednego katika tanuru la moto: Jaribu juu ya ibada ya kweli

c.Danieli katika tundu la sindano: Maombi na ushuhudiaji

d. Umuhimu wa maombi na matokeo yake

SDA believe sura ya 21

Mwanzo sura ya 1

Njia Salama uk….

WIKI YA 6-9

Maisha ya baadaye ya Abrahamu na Lutu

a. Njaa katika nchi ya Kaanani:Abrahamu ahamia Misri

b. Abrahamu atengana na Lutu

c. Lutu ashambuliwa na kuokolewa na Abrahamu

Mwanzo sura ya 14

WIKI YA 10-14

Lutu akiwa Sodoma:

a. Abrahamu atembelewa na wageni watatu

b. Ombi la Abrahamu kwa ajili ya Lutu

c. Kuangamizwa kwa Sodoma

d. Lutu na familia yake waokolewa

e.  Mke wa Lutu ageuka kuwa nguzo ya chumvi

 

Mwanzo sura ya 18 na 19

Wazee na Manabii uk.138-140 na 156-167

WIKI YA 15-20

Ubatizo

a. Yesu abatizwa na Yohana mbatizaji

b. Maana ya ubatizo

c. Maandalizi ya ubatizo wa kweli

d. Ubatizo wa maji mengi

  1. Umuhimu wa ubatizo

Mathayo sura ya 20

Warumi 6:4

Matendo sura ya 13

Waebrania 6:2

Waefeso 4:5

Wakolosai 2:12

SDA believe sura ya 14

 

 

 

 

DARASA LA SITA

MUHULA WA KWANZA

WIKI

MADA

VITABU VYA REJEA

WIKI YA 1-4

Kuzaliwa kwa Isaka na utii wa Abrahamu:

a. Kuzaliwa kwa Isaka

b. Mungu amjaribu Abrahamu kwa mtoto wake wa pekee

Mwanzo 21:35

Wazee na Manabii uk.145-147

WIKI YA 5-9

Ndoa na familia ya Isaka:

a. Isaka amuoa Rebeka

b. Maisha yaawali ya ndugu pacha:Esau na Yakobo

c. Yakobo amdanganya baba yake na aondoka nyumbani

c.  Njia ndefu kuelekea kwenye usalama

d.  Yakobo akiwa Harani

e.  Safari ya Yakobo kurudi nyumbani

Mwanzo sura ya23 na 24

Wazee na Manabii uk. 171-176

Isaya 65:24

WIKI YA 10-13

Sabato:

a. Asili ya Sabato

b. Sabato kama kumbukumbu ya uuumbaji

c. Siku ipi ya wiki ndiyo Sabato?

d. Namna ya kutunza Sabato

e. Asili ya utunzaji wa Sabato

f. The ten commandments

Mwanzo sura ya 2

Luka 4:16

Yohana 7:10-12

Isaya 56:1-8

Kutoka 16:22-30

Isaya sura ya 58

Mathayo 28:1

Matendo 20:6-16

SDA believe sura ya 19

WIKI YA 14-16

Taifa la Isareli lakataa uongozi wa Mungu

a. Taifa la Israeli baada ya kifo cha Yoshua

b. Ombi la kuwa na mfalme

c.  Sauli awa Mfalme wa kwanza

d. Taifa la Israeli chini ya mfalme Sauli

e.  Mwisho wa ufalme wa Sauli na kifo chake

1 Samweli sura ya 8-11

WIKI YA 17-20

Mchungaji wa kondoo mdogo aliyekuja kuwa mfalme

a. Maisha ya awali ya Daudi

b. Daudi atiwa mafuta na nabii Samweli

c. Daudi apigana na Goliathi

d. Daudi na Yoanthani:marafiki wa kweli

1 Samweli sura ya 16

2 Wafalme sura ya 2

 

DARASA LA SITA

MUHULA WA PILI

WIKI

MADA

VITABU VYA REJEA

WIKI YA 1-3

Ndoa na familia:

a. Ndoa ya awali iliyofanyika Edeni

b. Mpngo wa Mungu kuhusu ndoa

c. Ndoa katika mila za kiafrika

d. Sala ya familia

SDA Belive sura ya 22

 

Njia salama

WIKI YA 4-7

Mtu aliyeishi ndani ya samaki kwa muda wa siku  3:

a.Yona aitwa na Mungu

b. Yona ajaribu kumkimbia Mungu

c. Safari ya Yona

d. Yona atapikwa na samaki na aenda Ninawi

Yona sura ya 1-4

WIKI YA 8-11

Uaminifu na imani:Kisa cha Ayubu

a. Maisha ya awali ya Ayubu

b. Ayubu ashtakiwa na shetani

c. Jaribu la kwanza la Ayubu

d. Jaribu la pili la Ayubu

e. Ayubu abaki mwaminifu kwa Mungu wake

f. Ayubu afnikiwa tena

Ayubu sura ya 1-2

WIKI YA 12-14

MARUDIO

 

WIKI YA 15-20

Esta amuokoa mjomba wake pamoja na wayahudi

a. Esta awa malkia

b. Esta aokoa maisha ya watu wake

c. Mordekai apewa heshima

d. kifo cha Hamani

e. Mkono wa Mungu uokoao kwa wanaomtumaini na kumtegemea

Esta sura ya 1-7

 

DARASA LA SABA

MUHULA WA KWANZA

WIKI

MADA

VITABU VYA REJEA

WIKI YA 1-3

Sisi ni mawakili wa Mungu:

a. Uwezo ( Ability)

b. Muda

c. Mali

SDA Believe sura ya 20

WIKI YA 4-6

a. Mfano wa talanta

b. Kafara na sadaka katika ibada za asili za kiafrika

c. Suala la utunzaji wa muda katika muktadha wa kiafrika

 

WIKI YA 7-8

Maisha ya awali ya Yesu:

a. Kuzaliwa kwa Yesu

b. Masiha ya awali ya Yesu

c. Yesu abatizwa

d. Ubatizo wa kweli na maana yake

e. Yesu ajaribiwa

Mathayo sura ya 2

Tumaini la vizazi vyote

WIKI YA 9-12

Huduma ya Kristo:

a. Yesu aanza kuhubiri

b. Kuitwa kwa wanafunzi wa kwanza

c. Yesu afundisha kwa mifano

d. Hubiri la mlima i

e. Yesu aponya wagojwa na kufanya miujiza

f. Yesu azungumzia ufalme wa mbinguni

i. Vazi la harusi

ii. Wanawali kumi

iii. Sifa za heri

Mathayo sura ya 4 na 5

WIKI YA 13-14

Kifo cha Yesu:

a. Yesu asalitiwa

b. Ashtakiwa na kuhukumiwa

c. Yesu asulubiwa

d. Kufufuka kwa Yesu

e. Umuhimu wa kifo na ufufuko wa Yesu

f. Imani za kiafika kuhusiana na hali ya wafu

 

WIKI YA 15-17

Wokovu:

a.Kisa cha Zakayo

b.Kijana tajiri

c.Kisa cha Lazaro

d.Yohana mbatizaji

Luka sura ya 18 na 19

Yohana sura ya 3

 

WIKI YA 18-20

Vijana watumwa wasimamia imani yao

a. Kisa cha Yusufu akiwa Misri

b. Kutoka gerezani hadi katika ikulu ya mfalme

c. Danieli, Meshaki, Shadraka na Abedinego wakiwa Babeli

d. Unaweza kusimama leo

 

 

DARASA LA SABA

MUHULA WA PILI

WIKI

MADA

VITABU VYA REJEA

WIKI YA 1-2

Mlima Sinai na agano:

a.  Amri kumi za Mungu

b. Ndama wa dhahabu

c. Kutengenzwa kwa patakatifu

d. Kazi za patakatifu

e. Samani (fenicha) za patakatifu

Kutoka sura ya 20, 25-27

 

WIKI YA 3-5

a. Huduma ya Hekaluni

b. Kuhani alimwakilisha Kristo

c. Mungu aonyesha mpango wake wa ukombozi

Kutoka sura ya 25-31

Wazee na Manabii uk. 347-349

Ufunuo 24:5-9

WIKI YA 6-8

Musa amaliza huduma yake:

a. Musa afanya kosa

b. Mrithi wa Musa

c. Kifo cha Musa

Kumb. Sura ya 31-34

Wazee na Manabii uk. 462-480

WIKI YA 9-13

Kuingia na kuishi Kanaani:

a. Kutoka Kadeshi Barnea hadi Yordani

b. Nchi ya Kanaani au Palestina

c. Kuingia kwa wana wa Israeli katika nchi ya ahadi

d. Kuanguka kwa mji wa Yeriko

Wazee na Manabii uk. 482

Yoshua sura ya 5 na 6

WIKI YA 14-17

a.Yoshua katika kuingia Kanaani

b.Kugawanywa kwa nchi

c.Kifo cha Yoshua

Yoshua sura ya 9, 14-21

Wazee na Manabii uk. 505-517

Hesabu sura ya 30-34

WIKI YA 18-20

Waamuzi:

a.Waamuzi wa awali

b.Debora na Baraka

c. Gidioni

d.Yefta

e. Samsoni

f. Samweli

1 Waamuzi sura ya 5-6, 13-16

Wazee na Manabii uk.545-547, 560-582

Ruthu sura ya 1-4

1Samweli sura ya1-3