Seventh-day Adventist® Church

PASTOR LETTA'S OFFICIAL WEBSITE

Menu

SIKU 10 ZA MAOMBI 2022

WITO WA MAOMBI WA MALAIKA WATATU

MWONGOZO WA KIONGOZI

Karibu tena katika Siku Kumi za Maombi mwaka 2022! Tunaamini kuwa, katika maombi ndipo mahali uamsho unapozaliwa. Mungu ametenda miujiza mingi katika miaka iliyopita kadiri tulivyokuwa tukimtafuta katika maombi na kufunga. Roho Mtakatifu amewezesha uamsho, mabadiliko, hisia za uinjilisti zilizojengwa upya, makanisa yaliyoamshwa, na mahusiano yaliyoponywa. Je, sauti ya Mungu imekuwa ikikuita kufanya uamsho? Biblia imejaa ahadi kwa ajili yako: “Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao” (2 Nyakati 7:14). “Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote” (Yeremia 29:13). “Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa” (Yoeli 2:32). “Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi” (Yakobo 4:8). “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami” (Ufunuo 3:20). Po pote ulipo katika maisha wakati huu wa sasa, Mungu yupo karibu na wewe zaidi kuliko unavyofikiria. Anataka kumwaga mibaraka yake kwa familia yako, kwa kanisa lako, kwa jamii yako, na kwa ulimwengu wako. Ungana nasi sasa katika kutikia wito wa malaika watatu wa kuomba.

Mambo ya kawaida ya maombi katika siku kumi za maombi Miongozo ya Maombi ya Kila Siku

Tumetoa mwongozo wa maombi ya kila siku katika siku hizi kumi. Mwongozo wa kila siku husika unajumuisha aya ya Biblia itakayotumika katika kuomba, somo la kesha, aya za Biblia za kutumia katika kuomba, mapendekezo ya maombi, na mapendekezo ya nyimbo. Tunashauri kuwa ikiwezekana utoe nakala ya kurasa za miongozo ya kila siku ili kila mshiriki aweze kuwa na nakala yake apate kufuatisha katika ule muda wa maombi. Makanisa ulimwenguni yataungana katika kuomba yakijikita katika mada ya siku husika. Ungana nao katika kuomba kupitia katika aya na mahitaji yaliyoletwa, lakini usihisi kwamba unapaswa kupitia kwa haraka katika orodha yote ya mahitaji ya maombi. Mnaweza kugawanyika katika vikundi vidogo na kila kikundi kikaombea sehemu ya orodha ya mahitaji yenu ya kuombea Pia tumejumuisha ukurasa unaoitwa Maombi ya Kanisa la Kiulimwengu. Ni muhimu kuomba pamoja kwa ajili ya familia ya kanisa letu la kiulimwengu, lakini unaweza kutenga muda zaidi wa kuombea mahitaji ya sehemu mahalia ikiwa kundi lako linajumuisha wageni kutoka katika jamii husika. Omba kuhusu namna unavyoweza kuwakaribisha wageni kwa ubora zaidi na kuwafanya wajisikie kuwa ni sehemu ya kundi hilo.

Muda unaopendekezwa kwa ajili ya kila Kipengele cha Maombi

Fanya muda wenu wa maombi kuwa wa kawaida na rahisi kadiri iwezekanavyo ili kikundi chenu kiweze kuelekeza mawazo katika kuomba. Muda utakaotumika katika kila kipengele utatofautiana. Mwongozo ufuatao ni mapendekezo tu: • Kukaribisha/Utangulizi – dakika 2 hadi 5
• Usomaji wa “Kesha” (mwongozo wa maombi wa kila siku) – dakika 5
• Kuomba Kupitia mafungu katika “Kuomba Neno la Mungu” (mwongozo wa maombi wa kila siku) – dakika 10 hadi 15
• Kuombea mahitaji katika “Mapendekezo zaidi ya Maombi” (mwongozo wa maombi wa kila siku) – dakika 30
• Kushukuru kwa nyimbo na sifa – dakika 5 – 10

Kuombea Wengine

Hamasisha kila mtu kuombea watu watano hadi saba ambao Mungu ameweka katika maisha yao. Wanaweza kuwa ndugu, marafiki, wafanyakazi wenza, majirani, au watu wanaofahamiana nao. Wahamasishe kumwomba Roho Mtakatifu awaongoze katika kuchagua majina ya watu hao na kuhakikisha wanawafikia katika siku hizi kumi za maombi. Unaweza kutoa kadi au vikaratasi ambavyo watu watatumia kuandika majina watakayokuwa wakiombea.

Huduma za Sabato katika Kipindi cha Siku Kumi za Maombi

Maombi na yalenge katika kitu mahususi, na ni vyema kushiriki pamoja shuhuda mbali mbali za maombi yaliyojibiwa katika huduma siku ya Sabato kanisani Jumamosi zote mbili. Iweni wabunifu – kuna namna nyingi za kushiriki pamoja na familia ya kanisa mambo yanayotokea katika mikutano ya maombi ya kila siku.

Sherehe za Sabato ya Kuhitimisha

Sabato ya mwisho inapaswa kutayarishwa kwa namna itakayokuwa ni muda wa furaha kuu kwa yale yote Mungu aliyotenda katika siku hizi kumi. Tenga muda wa kutosha kwa ajili ya shuhuda za maombi yaliyojibiwa, kwa ajili ya mafundisho ya kibiblia/mahubiri juu ya maombi, na kwa ajili ya nyimbo. Ongoza kusanyiko katika muda wa maombi ili kwamba hata wale ambao hawakuhudhuria mikutano ya kila siku, wapate uzoefu wa furaha ya kuomba pamoja na wengine. Tafadhali tazama mwongozo wa Sherehe za Sabato kwa mawazo zaidi.

Kufuatilia kipindi hiki cha maombi ya siku kumi

Omba ili kupata ufahamu jinsi Mungu anavyotaka kanisa au kikundi chako kuendeleza kile Alichoanzisha katika kipindi hiki cha Siku Kumi za Maombi. Pengine mtaendelea kukutana kila juma kwa ajili ya maombi. Au pengine Mungu anataka muanze huduma mpya ndani ya kanisa lenu au katika kuifikia jamii. Muwe tayari na kumfuata Mungu kule anapowaelekeza. Hakika mtashangazwa kadiri mnavyotembea pamoja naye. Ukurasa wa Changamoto ya Kuwafikia Wengine umejaa mawazo ya huduma. Shuhuda Tafadhali shiriki visa vinavyoonesha jinsi Mungu alivyotenda kazi katika Siku Kumi za Maombi! Visa vyako vitakuwa msaada na hamasa kwa wengine wengi. Shuhuda zinaweza kutumwa kwa: stories@ministerialassociation.org  au kutumwa mtandaoni kwenye tovuti hii: www.tendaysofprayer.org.

Vielekezi vya kuunganika katika maombi

Kubalianeni

Mtu anapoombea hitaji fulani kwa Mungu, hakikisha kuwa wengine pia wanaombea hitaji hilo hilo na kukubaliana – kufanya hivi kuna nguvu! Usifikiri kwamba kwa sababu mtu mmoja ameomba kuhusu hitaji hilo, hakuna haja ya mwingine kuliombea. “Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni” (Mathayo 18:19). Inatia moyo kiasi gani kuinuliwa katika maombi!

Kudai Ahadi za Mungu

Hamasisha kikundi kudai ahadi za Mungu kadiri wanavyoomba. Ni rahisi sana kujielekeza katika matatizo yetu. Lakini tunapodai ahadi za Mungu, tunaongeza imani yetu na kujikumbusha kwamba hakuna kinachoshindikana kwa Mungu. Ahadi hizo hutusaidia kuondoa macho yetu kwenye madhaifu yetu, na magumu tunayokabiliana nayo, hivyo kuyaelekeza kwa Yesu. Tunaweza kupata ahadi za Biblia za kudai kwa kila udhaifu na kila pambano. Himiza watu kutafuta ahadi nyingi zaidi kadiri iwezekanavyo na kuziandika ili waweze kuzidai katika maombi wakati ujao.

Kufunga

Alika wale wanaoungana nawe katika Siku Kumi za Maombi kufikiria aina ya kufunga watakayoshiriki, kwa mfano kufunga na kuacha kutazama televisheni, kuacha kusikiliza muziki wa kidunia, kuacha kutazama filamu, kuacha kuingia mtandaoni, kuacha kula vitu vitamu vitamu kama vile pipi, au aina nyingine ya vyakula ambavyo ni vigumu kumeng’enywa. Tumia muda wa ziada katika kuomba na kujifunza Biblia, ukimwomba Mungu akusaidie wewe na kusanyiko lako kudumu kikamilifu zaidi katika Kristo. Kwa kuchagua mlo mwepesi, tunaruhusu akili zetu kuwa sikivu zaidi kwa sauti ya Roho Mtakatifu.

Roho Mtakatifu

Hakikisha unamwomba Roho Mtakatifu akuonyeshe jambo la kuombea katika maisha ya mtu fulani au katika hali fulani. Biblia inatuambia kwamba hatufahamu tuombe nini, na kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayetuombea. “Hatupaswi kuomba tu kwa jina la Kristo, bali kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu. Hii huelezea maana halisi tunaposema kuwa Roho “hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.” (Warumi 8:26). Mungu hufurahia kujibu ombi kama hilo. Tunapoomba kwa dhati na kwa nguvu tunaomba kwa jina la Kristo, katika nguvu hiyo kuna ahadi kutoka kwa Mungu kwamba anakaribia kujibu maombi yetu kama tunavyosoma kuwa, “Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu” (Waefeso 3:20)” (Christ Object Lessons, uk. 147, msisitizo umeongezewa).

Kutunza Taarifa ya Maombi

Kutunza daftari la kumbukumbu ya maombi kwenye kipindi chote cha Siku Kumi za Maombi kunaweza kuwa njia bora ya washiriki kuhifadhi moyoni wazo kuu la maombi ya kila siku, kufanya maagano thabiti na Mungu, na kutambua mibaraka yake kwao. Kuorodhesha maombi yetu na kutunza kumbukumbu ya majibu ya Mungu ni njia iliyothibitishwa ya kutia moyo. Ikiwa utapenda, unaweza kutenga muda pale mnapokutanika kwa ajili ya maombi, ili watu wapate kuandika mwitikio wao kwa Mungu kwenye shajara zao binafsi za maombi. Au unaweza kutunza shajara ya kikundi cha maombi na majibu yake – linaweza kuwa ni daftari, au bango kubwa, au unaweza kutunzia mtandaoni. Inafurahisha na pia inajenga imani unapotazama nyuma na kuona jinsi Mungu alivyojibu maombi!

Kicho

Himiza na kujenga mtazamo wa kicho na unyenyekevu. Tunakaribia chumba chenye kiti cha enzi cha Mfalme wa ulimwengu. Hebu tusitumie muda huu wa maombi vibaya kwa mkao na kwa mwenendo wetu usiofaa na hata katika mazungumzo yetu. Hata hivyo, siyo lazima kila mmoja apige magoti muda wote. Unahitaji watu wawe huru kwa saa moja, hivyo wahamasishe watu kupiga magoti au kukaa au kusimama kadiri Mungu atakavyokuongoza na kwa namna wanavyokuwa huru zaidi.

Maombi kwa Sentensi

Maombi yanapaswa kuwa mafupi, na yaelekezwe moja kwa moja kwenye hitaji. Kufanya hivi kutawapatia wengine pia fursa ya kuomba. Jaribu kufupisha maombi yako yawe ni ya sentensi chache. Kila mmoja anaweza kuomba mara kadhaa. Maombi mafupi yatafanya kipindi cha maombi kiwe cha kufurahisha na siyo cha kuchosha na hivyo kumruhusu Roho Mtakatifu aguse kundi zima akiwaonesha namna ya kuomba. Siyo lazima kuanza na kumaliza ombi fupi la sentensi kwa maneno kama “Mungu wetu mpendwa” na “Amina.” Ni mawasiliano endelevu na Mungu.

Ukimya

Wewe kama kiongozi usitawale kipindi cha maombi. Lengo kubwa ni kuwawezesha wengine kuomba. Kipindi cha ukimya kina thamani kubwa ajabu, kwani humpa Mungu muda wa kuzungumza na mioyo yetu. Mruhusu Roho Mtakatifu afanye kazi kwa kumpa kila mmoja muda wa kutosha wa kuomba.

Kuimba

Nyimbo za hapa na pale kutoka kwa vikundi zikiunganishwa kwenye maombi, huongeza uzuri katika mkutano wa maombi. Nyimbo zilizopendekezwa zimeorodheshwa mwisho wa kila ukurasa wa wazo la siku. Siyo lazima kutumia nyimbo zote – haya ni mapendekezo tu. Kuimba pia ni njia nzuri ya kuhama kutoka kwenye kipindi kimoja kwenda kwenye kipindi kingine.

Kukusanya Mahitaji ya Kuombea

Usiulizie wala kukusanya mahitaji ya kuombea kutoka kwenye kikundi. Badala yake, waambie watu wataje mahitaji yao wakati wanapoomba na kuwahimiza wengine kujiunga wakikubaliana nayo kwa kuungana katika maombi kimya kimya. Sababu kubwa ni Muda! Kuzungumza kuhusu mahitaji ya kila mmoja kunaweza kutumia muda mwingi wa maombi. Shetani anafurahi akiweza kutudumisha katika kuzungumzia tatizo badala ya kuomba kwa ajili ya tatizo hilo. Wanakikundi wanaweza kuanza kushauriana na kupendekeza ufumbuzi. Uwezo unatoka kwa Mungu! Kadiri tunavyoongeza maombi ndivyo anavyoachia uwezo wake.

Muda wako wa kila siku

Ni wa muhimu sana! Hakikisha wewe kama kiongozi unatumia muda wako mwingi miguuni pa Yesu, ukizungumza naye na kusoma Neno lake. Ikiwa utafanya kumfahamu Mungu kuwa kipaumbele katika Maisha yako, utafunguliwa uzoefu ulio mzuri wa ajabu. “Kutoka katika sehemu ya siri ya maombi ilitoka Nguvu ya ajabu iliyotikisha dunia na kuleta Matengenezo Makuu. Hapo, kwa utulivu mtakatifu, watumishi wa Bwana waliweka miguu yao katika mwamba wa ahadi zake” (The Great Controversy, uk. 210). Kiongozi anapoomba, Mungu hushughulika na mioyo!

Utangulizi

         Karibu katika Siku Kumi za Maombi 2022! Tunaamini kuwa, katika maombi ndipo mahali uamsho unapozaliwa. Mungu ametenda miujiza mingi katika miaka iliyopita kadiri tulivyokuwa tukimtafuta kwa kuomba na kufunga. Roho Mtakatifu amewezesha uamsho, mabadiliko, hisia za uinjilisti zilizojengwa upya, makanisa yaliyoamshwa, na mahusiano yaliyoponywa. Hapa kuna baadhi ya shuhuda katika miaka iliyopita:
        Siku kumi za maombi… kwa kweli zimebadilisha Maisha yangu. Kimekuwa ni kipindi cha badiliko kubwa katika Maisha yangu. (Ruth, K.)
        Tumeguswa sana kwa masomo. Watu walimlilia Mungu kwa dhati ya mioyo yao. Tulijifunza kwa mara ya kwanza maana ya kuomba kulingana na ahadi za Mung una kudai zawadi ya thamani ya Yesu – yaani Toho Mtakatifu. (Moureen K.)
Kabla ya siku kumi za maombi, watu wengi kaninsani kwangu walikuwa wanaumwa magonjwa mbali mbali. Lakini ndani ya siku hizi za maombi, wote walipona! Zaidi ya hapo, roho saba zilikabidhi Maisha yao kwa Yesu Kristo na kubatizwa. (Mugabe, G.)
        Je, sauti ya Mungu imekuwa ikikutia katika uamsho? Biblia imejaa ahadi kwa ajili yako:
“Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao” (2 Nyakati 7:14). “Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote” (Yeremia 29:13). “Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa” (Yoeli 2:32). “Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi” (Yakobo 4:8). “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami”(Ufunuo 3:20). Po pote ulipo katika maisha sasa, Mungu yupo karibu zaidi kuliko unavyofikiri. Anataka kumwaga mibaraka yake kwa familia yako, kanisa lako, jamii yako, na kwa ulimwengu wako. Ungana nasi sasa katika kuomba kwa ajili ya uamsho wa kiroho kupitia kwa Roho Mtakatifu!

Mada yetu ya Maombi: Wito wa Maombi wa Malaika Watatu

Mwaka huu tunakualika kutafuta uamsho na matengenezo kupitia kwenye nguvu ya Roho Mtakatifu katika Siku Kumi hizi za Maombi. Kadiri unavyoomba, kupitia katika ujumbe wa malaika watatu, hebu jumbe hizo na ziangaze kwa umuhimu mpya na kukuongoza wewe pamoja na kikundi chako cha maombi katika uzoefu wa kina na Yesu. Mungu anataka kufanya mambo ya ajabu katika maisha yetu na katika makanisa yetu leo. Mipango yake inazidi uwezo wetu, ni kwa muunganiko wa kudumu wa maombi pamoja naye, ndipo tunapoweza kukamilisha kazi yaliyotuandalia. Anatusihi, “Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua” (Yeremia 33:3). Ungana nasi katika kuomba kwa ajili ya uamsho, na kujitoa upya kwa dhati katika wito wetu wa wakati wa mwisho, na ahadi ya kumwagwa kwa Roho Mtakatifu!

Mwongozo unaopendekezwa wakati wa maombi

• Jitahidi kufanya maombi yawe mafupi – sentensi moja au mbili zilizojengeka katika mada husika. Kisha wape nafasi wengine. Unaweza kuomba mara nyingi kadiri unavyojisikia, kwa namna ile ile unayozungumza katika mazungumzo.
• Usiogope kuwa kimya, kwani kuwa kimya kunampatia kila mmoja muda wa kumsikiliza Roho Mtakatifu.
• Kuimba nyimbo pamoja kadiri Roho Mtakatifu atakavyowaongoza ni mbaraka mkubwa. Hamhitaji kinanda ili kuwaongoza; kuimba bila ala ya mziki ni sawa pia.
• Badala ya kutumia muda wa thamani wa maombi ukizungumza kuhusu mahitaji yako ya kuombea, bali yaombee tu. Kisha wengine pia wanaweza kuombea mahitaji yako na kudai ahadi kwa ajili ya mahitaji yako.

Kudai Ahadi

Ni faida kwetu kudai ahadi za Mungu katika maombi yetu. Maagizo yote ya Mungu na mashauri yake pia ni ahadi. Hawezi kudai kutoka kwetu jambo fulani ambalo hatuwezi kufanya kwa uweza wake.

Tunapoomba, ni rahisi kujielekeza katika mahitaji yetu, magumu yetu, changamoto zetu – na hasa kulalamika na kulaumu katika maombi kuhusu hali tuliyo nayo. Hili silo kusudi la maombi. Kusudi kubwa la maombi ni kuimarisha imani yetu. Ndiyo maana tunakuhimiza kudai ahadi za Mungu katika muda wako wa maombi. Hamisha macho yako kutoka katika mahitaji yako na changamoto zako na kuyaelekeza kwa Yesu Kristo. Ni kwa kumwangalia yeye pekee ndipo tunapobadilishwa na kuchukua sura yake. Ellen White anatutia nguvu kwamba: “Kila ahadi katika Neno la Mungu ni kwa ajili yetu. Katika maombi yako, wasilisha neno lililoahidiwa la Yehova uidai kwa imani ahadi zake. Neno lake linatupatia uhakika kwamba ukiomba kwa imani, utapokea mibaraka yote ya kiroho. Endelea kuomba nawe utapata zaidi ya yale uyaombayo au uyawazayo.” (In Heavenly Places, uk. 71). Ni kwa namna gani unaweza kudai hizo ahadi za Mungu? Kwa mfano, unapoomba kwa ajili ya amani, unaweza kudai Yohana 14:27 na kusema kuwa, “Bwana umetuambia katika Maandiko yako kwamba ‘Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.’ Ninakuomba unipatie amani uliyoahidi kutuachia.” Kisha mshukuru Bwana kwamba atakupatia hiyo amani hata kama haujisikii kuwa na amani wakati huo.

Kufunga

Tunakuhamasisha kufanya Mfungo kama ule wa Danieli katika Siku hizi Kumi. Kuanza mwaka kwa maombi ya kufunga ni njia bora ya kuweka wakfu maisha yetu kwa Mungu kwa mwaka unaoanza. Ellen White anatuambia kuwa, “Sasa na kuendelea hata mwisho wa wakati watu wa Mungu wanapaswa kuwa na bidii zaidi, kuwa macho zaidi, kutokuamini hekima yao wenyewe, lakini kuamini hekima ya kiongozi wao, ambaye ni Yesu. Wanapaswa kutenga siku kwa ajili ya kufunga na kuomba. Kujitenga kabisa na chakula kunaweza kusiwe lazima, lakini wanapaswa kula vyakula rahisi zaidi” (Counsels on Diet and Foods, uk. 188, 189). Tunafahamu kuhusu Danieli, aliyekula matunda na mboga mboga kwa siku kumi. Sisi pia tunakuhamasisha kuwa na mlo rahisi sana katika siku hizi kumi. Kama tunataka akili zilizo wazi zaidi ili kuisikia sauti ya Mungu, na kama tunataka kuwa karibu zaidi na Mungi, tunahitaji kuhakikisha kwamba chakula chetu hakiwi kikwazo. Kufunga si kujitenga tu na chakula. Tunakuhamasisha pia kufunga kutazama televisheni, filamu, michezo ya kompyuta, na hata Facebook na YouTube. Wakati mwingine vitu visivyo vibaya, kama Facebook na YouTube, huweza kutuchukulia muda mwingi sana. Weka kando kila kinachowezekana ili uwe na muda mwingi wa kukaa na Bwana. Kufunga siyo namna ya haraka ya kupata mibaraka kutoka kwa Mungu. Kufunga ni kujinyenyekeza wenyewe ili kwamba Mungu aweze kufanya kazi ndani yetu na kupitia kwetu. Hebu na tusogee karibu naye kupitia maombi ya kufunga, naye atasogea karibu zaidi nasi.

Roho Mtakatifu

Hakikisha unamuomba Roho Mtakatifu akuonyeshe unachopaswa kuombea katika maisha ya mtu fulani, au katika hali fulani. Biblia inatuambia kwamba hatujui tuombee nini na kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayetuombea. “Hatupaswi kuomba tu kwa jina la Kristo, lakini kwa msukumo wa Roho Mtakatifu. Hii huelezea maana ya maneno kwamba Roho “hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.” (Warumi 8:26). Ombi kama hilo Mungu hufurahia kulijibu. Tunapoomba kwa dhati na kwa nguvu tunaomba kwa jina la Kristo, katika nguvu hiyo kuna ahadi kutoka kwa Mungu kwamba anakaribia kujibu maombi yetu ‘zaidi ya tuyaombayo au tuyawazayo’ (Waefeso 3:20” (Christ Object Lessons, uk. 147).

Imani

Tunasoma katika Roho ya Unabii kwamba “maombi na imani vitafanya kile ambacho hakuna nguvu duniani inachoweza kufanya” (The Ministry of Healing, uk. 509). Pia tunaambiwa kwamba “ahadi yo yote aliyoahidi, tunaweza kuiomba; kasha tunapaswa kuamini kwamba tumeipokea, na kurudisha shukrani kwa Mungu kwamba tumepokea” (Education, uk. 258). Hivyo jenga tabia ya kumshukuru Mungu kwa imani kabla kwa kile anakachoenda kutenda na namna atakavyojibu maombi yako.

Ombea Wengine

Katika siku hizi kumi tunakuhimiza kuombea watu ambao Mungu amewaweka katika maisha yako kwa namna ya pekee. Chagua watu watano hadi saba – wanaweza kuwa ndugu, marafiki, wafanyakazi wenzako, majirani, au hata watu unaowafahamu tu. 
Tenga muda kumuuliza Mungu kuwa, angependa umuombee nani. Mwombe pia akupatie mzigo halisi wa watu hawa. Andika majina yao kwenye karatasi na uitunze sehemu salama, kama kwenye Biblia yako. Kuna jambo lenye nguvu katika kuyaandika majina hayo, na utashangazwa namna Mungu anavyofanya kazi katika kujibu maombi yako!

Mchangiaji mkubwa kwa mwongozo wa maombi ya kila siku ni Dr. Mark A. Finley
Masomo haya yameandaliwa na Idara ya Huduma, Konferensi Kuu ya kanisa la Waadventista wa Sabato.
Isipokuwa pale ambapo imeelezwa vinginevyo, nukuu zote zinatoka katika toleo la Biblia la “Swahili Union Bible” © 1997

USIKU WA MAOMBI:

Fikiria kuandaa huduma ya maombi ya usiku mzima kama sehemu ya Siku Kumi za Maombi. Kwa mfano, unaweza kuanza saa 12 jioni na kumaliza saa 12 asubuhi. Chagua ratiba itakayofaa kwa kundi lako.

Kwa nini kuwa na Usiku wa Maombi?

Hakuna chochote “kitakatifu” katika kukaa macho huku ukiomba usiku kucha. Hata hivyo, ni kweli kwamba usiku unaweza kuwa ni wakati wa pekee ambao watu hawana mambo mengi ya kufanya au kuwa katika hali ya haraka. Tunaamini kwamba lengo lako halipaswi kuwa kukaa macho usiku kucha, bali ni kuomba sana kadiri inavyohitajika hadi utakapokuwa umeombea vitu vyote unavyohisi kwamba Mungu anataka uviombee. Tunapendekeza kwamba baadhi ya watu waongoze usiku huo. Hakikisha kunakuwa na mapumziko. Kama kiongozi, unaweza kuona hali ilivyo na kufahamu wakati mapumziko yanapohitajika na wakati utakapoona inafaa kuhamia katika kipengele kinachofuata cha maombi. Unaweza pia kuingiza usomaji wa vifungu vya Biblia katika muda wako wa maombi. Unaweza kufanya mambo yote yaliyopendekezwa au baadhi yake, inategemea kile kilicho bora kwa kikundi chako. Kuwa huru kubadilisha mtiririko kadiri utakavyoona inafaa.

Mapendekezo ya Mpangilio wa Usiku wa Maombi
Anza kwa kipindi cha sifa. Msifu Mungu katika maombi yako na pia kupitia nyimbo.
Tumia muda kwa ajili ya kuungama, ukihakikisha kwamba hakuna kinachomzuia Mungu kusikia maombi yako. Wapatie watu muda wa maungamo binafsi na weka muda wa kuungama kwa pamoja. Hamasisha watu kuungama dhambi za binafsi wakiwa pekee yao na kuungama dhambi za wazi kwa uwazi. Katika Danieli 9:1-19 tunasoma kumhusu Danieli, aliyeomba na kuungama kwa wazi dhambi za watu wa Mungu.
Ombea mahitaji ya watu walio katika mkutano huo wa maombi. Watu wengi wanaumia au wana uhitaji wa maombi, au wanamfahamu mtu mwenye uhitaji wa maombi. Tengeneza duara, weka kiti katikati, na alika wale wenye maombi maalumu waje mmoja baada ya mwingine na kushiriki maombi yao. Kisha kusanyikeni kumzunguka mtu huyu na waruhusu watu wawili au watatu kuomba kwa ajili ya mahitaji mahususi ya mtu huyo na kudai ahadi za Mungu.
Gawa kikundi katika vikundi viwili vidogo. Waruhusu wanawake kuomba katika chumba kimoja (wakiwa na kiongozi wa kike) na wanaume katika chumba kingine (wakiwa na kiongozi wa kiume). Mahitaji mengi binafsi hayawezi na hayapaswi kushirikishwa na kila mtu. Ni rahisi zaidi kushiriki pamoja na wale wa jinsia moja.
Baada ya kurudi pamoja, ombea mahitaji ya jamii na kanisa lenu. Pia tumia muda kwa ajili ya maombi ya kanisa la kiulimwengu (yaliyoorodheshwa katika ukurasa wa maombi ya kanisa la kiulimwengu). Siyo lazima kumaliza orodha nzima ya maombi, kwa hiyo usiharakishe ukiwa na hisia za kutaka kumaliza orodha yote. Unaweza kugawa maombi katika vikundi vidogo vidogo na kuwapatia kila kikundi sehemu ya orodha hiyo.
Ombea orodha ya watu watano hadi saba uliokuwa ukiwaombea katika siku hizi kumi
Chagua kifungu cha Biblia na kuombea.
Funga muda wa maombi kwa kipindi kingine cha kusifu na kushukuru.

Changamoto za Kuwafikia watu walio nje katika Siku Kumi za Maombi

Yesu hatuiti kwa ajili ya kuomba tu bali anatuita pia ili kuhudumia mahitaji ya wale wanaotuzunguka. “Kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia” (Mathayo 25:35, 36).

Katika kitabu cha Huduma ya Uponyaji (The Ministry of Healing) tunasoma kuwa, “Tunapaswa kuishi maisha yenye sura mbili – maisha ya mawazo na matendo, na maisha ya maombi ya kimya na kazi inayofanywa kwa juhudi” (uk. 512). Tumepokea upendo mwingi sana kutoka kwa Mwokozi wetu; na tuna fursa ya kushiriki upendo huo na marafiki, majirani, hata watu tusiowafahamu wenye uhitaji.

Muulize Mungu katika maombi namna bora ya kuwafikia wengine katika Siku hizi Kumi za Maombi. Unapokuwa ukifanya kazi ya kupanga kila kitu, epuka kuruhusu shughuli hizo kukufanya ushindwe kuomba. “Jitihada binafsi kwa ajili ya wengine zinapaswa kwanza kutanguliwa na maombi mengi ya faragha; kwani hekima kubwa inahitajika ili kuelewa sayansi ya kuokoa roho. Kabla ya kuwasiliana na watu, wasiliana na Kristo. Pata maandalizi ya kuhudumia watu kutoka katika kiti cha enzi cha neema ya kimbingu.” (Maombi, uk. 313).

Hapa kuna baadhi ya njia unazoweza kutumia kusaidia wengine. Chagua njia yo yote utakayoona inakidhi mahitaji ya wale unaokwenda kuwahudumia, na jisikie huru kuongeza mawazo yako.
• Mpikie mgonjwa chakula.
• Mkaribishe jirani/mfanyakazi mwenzako kwenye kusanyiko la kijamii.
• Mpatie chakula mtu asiye na makazi.
• Tafuta mzee mmoja. Mtembelee kila siku na umsaidie kazi, kama vile kumnunulia mahitaji, kumpikia, au kumsaidia kazi za bustani, n.k.
• Oka mkate na ushiriki huo mkate na jirani.
• Saidia kwenye miradi katika maeneo yanayokuzunguka.
• Jitolee kukaa na mgonjwa au mtu asiyejiweza ili wale wanaomhudumia waweze kufanya shughuli zingine.
Jitambulishe kwa jirani mpya aliyehamia maeneo yenu na kumpelekea chakula. Mfanye ajisikie kukaribishwa katika maeneo hayo.
• Nunua mahitaji ya jikoni na upelekee familia yenye uhitaji.
• Toa msaada miwani yako ya zamani.
• Jitolee kutoa masomo ya Biblia
• Tembelea sehemu za kutunzia watu wenye uhitaji na kuwafariji.
• Mpatie mwanafunzi fedha ya “chakula.”
• Kusanya nguo kwa ajili ya wahitaji. Unaweza kuanzisha kabati la nguo kanisani kwako kwa ajili ya kushirki na wale walio na uhitaji.
• Toa msaada kompyuta yako au vifaa vingine vya kielektroniki usivyotumia.
• Toa msaada gari lako lililotumika.
• Andaa “Tamasha la Kupima Afya.”
• Tuma kadi kwa mtu aliyefungiwa ndani.
• Andaa mfululizo wa mambo ya uinjilisti.
• Mpatie mtu kitabu unachodhani angekipenda.
• Wapigie simu jirani zako na kuwajulia hali.
• Gawa vijarida na vijuzuu kwa watu. Vinapatiakana kwenye tovuti ifuatayo hapa: www.glowonline.org /glow
• Mwalike mtu kumpokea Yesu.
• Endesha darasa la mapishi.
• Fanya “Mradi wa machapisho 28.” Katika Juma la kwanza, gawa kitabu kimoja. Juma la pili, gawa vitabu viwili. Juma la tatu, gawa vitabu vitatu. Endelea hadi utakapogawa vitabu vyote 28.
• Mpelekee chakula mtu aliyepoteza (aliyefiwa na) mpendwa wake.
• Mtembelee mtu hospitali ili kumtia moyo au kumsaidia kwa namna moja au nyingine.
• Msomee mzee kitabu.
• Tembelea makazi ya watoto yatima pampja na wanaoishi katika mazingira magumu na toa msaada kwa wafanyakazi wa hapo.
• Anza kundi la kushona/kufuma ili kutengeneza nguo kwa ajili ya wahitaji.
• Msomee Biblia kwa sauti mtu asiyeona au asiyeweza kusoma.
• Endesha usiku wa vijana nyumbani kwako.
• Toa makazi kwa watu walionyanyaswa.
• Gawa baadhi ya vitabu kwenye makazi ya watoto.
• Panga na kusimamia siku ya kufurahi kwa ajili ya watoto na wenye mahitaji maalumu pamoja na familia zao.

Andaa siku ya kufanya usafi katika jamii.
• Anzisha chama cha afya katika kanisa lako. Alika marafiki na majirani.
• Muulize mtu kama angependa kuungana na wewe kutazama mkanda wenye ujumbe wa kiroho. Kadiri mnavyotazama pamoja, omba kwamba Roho Mtakatifu anene na moyo wa mtu huyo.
• Buni mradi wako mwenyewe. Kwa vitendea kazi zaidi juu ya ushuhudiaji, tembelea tovuti ifuatayao:
www.revivalandreformation.org/resources/witnessing.

 

Ahadi za Biblia za Kudai kwenye Maombi Ahadi za Roho Mtakatifu

“Mwombeni Bwana mvua wakati wa masika, naam, Bwana afanyaye umeme, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi kondeni.” Zakaria 10:1
“Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?” Luka 11:13
“Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia… Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.” Yohana 14:26; 16:8
“Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.” Yohana 14:12 – 14
“Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi.” Zakaria 4:6

Ahadi kwamba Mungu Hujibu Maombi

“Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.” Yohana 15:7
“Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.” Waebrania 4:16
“Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” Marko 11:24 “Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.” Zaburi 50:15
“Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.” Mathayo 18:19
“Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea.” Mathayo 21:22
“Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.” Yohana 14:13, 14
“Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.” Yohana 16:23, 24
“Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.” 1 Yohana 5:14, 15

Ahadi kuhusu Nguvu ya Mungu

“Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda Bwana? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume.” Mwanzo 18:14
“Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.” Kutoka 14:14
“Yesu akawakazia macho, akasema, Kwa wanadamu haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo; maana yote yawezekana kwa Mungu.” Marko 10:27 “Yeye ni mwaminifu ambaye awaita, naye atafanya.” 1 Wathesalonike 5:24
“Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika.” Ayubu 42:2
“Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu? Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?” Warumi 8:31, 32
“Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?” Hesabu 23:19
“Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki. Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya;
watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.” Isaya 40:28 – 31

Ahadi za Uongozi wa Mungu

Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.” Yoshua 1:9
“Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.” Mwanzo 28:15
“Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.” Kutoka 23:20
“Lakini huko, kama mkimtafuta Bwana, Mungu wako, utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote, na roho yako yote.” Torati 4:29 “Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.” Yeremia 33:3
“Kila bonde litainuliwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopotoka patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patasawazishwa; Na utukufu wa Bwana utafunuliwa, Na wote wenye mwili watauona pamoja; Kwa kuwa kinywa cha Bwana kimenena haya.” Isaya 40:4, 5
“Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.” Zaburi 32:8
“Naye Bwana, yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike.” Torati 31:8
“Ni nani amchaye Bwana? Atamfundisha katika njia anayoichagua.” Zaburi 25:12
“Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.” Mithali 3:5, 6
“Na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri. Naye Bwana atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.” Isaya 58:10, 11
“Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.” Isaya 65:24

Ahadi za Moyo Uliobadilishwa

“Nami nitawapa moyo, wanijue ya kuwa mimi ni Bwana; nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao; kwa maana watanirudia kwa moyo wao wote.” Yeremia 24:7
“Bwana, Mungu wako, atautahiri moyo wako, na moyo wa uzao wako, ili umpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, upate kuwa hai.” Torati 30:6
“Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.” Ezekieli 36:26
“Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;” Wafilipi 1:6 “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.” 1 Wakorintho 5:17
“Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.” Wagalatia 2:20
“Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo. Yeye ni mwaminifu ambaye awaita, naye atafanya.” 1 Wathesalonike 5:23, 24

Ahadi za Msamaha
“Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.” 1 Nyakati 7:14
“Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe, Na mwingi wa fadhili, Kwa watu wote wakuitao.” Zaburi 86:5 “Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.” Marko 11:25
“Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.” Waefeso 4:32
“Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.” 1 Yohana 1:9
“Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.” Isaya 1:18
“Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.” Isaya 43:25 “Maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.” Yeremia 31:34
“Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.” Waefeso 1:7

Ahadi za Ushidi Dhidi ya Dhambi

“Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.” 1 Yohana 5:4
“Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.” Warumi 8:37
“Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.” 1 Wakorintho 15:57
“Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.” Isaya 41:10
“Zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.” Waefeso 6:16
“Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.” Wagalatia 2:20
“Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.” Wafilipi 2:13
“Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.” Wagalatia 5:16
“Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. Amina.” Warumi 16:20
“Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.” Warumi 12:2
“Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.” 1 Yohana 2:15

Ahadi za Uponyaji

“Akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi Bwana nikuponyaye.” Kutoka 15:20
“Makomeo yako yatakuwa ya chuma na shaba; Na kadiri ya siku zako ndivyo zitakavyokuwa nguvu zako.” Torati 33:25
“Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote. Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema, Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai.” Zaburi 103:2 – 5
“Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche Bwana, ukajiepushe na uovu. Itakuwa afya mwilini pako, Na mafuta mifupani mwako.” Mithali 3:7, 8
“Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya
kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” Isaya 53:3-5
“Uniponye, Ee Bwana, nami nitaponyeka; uniokoe, nami nitaokoka; kwa maana wewe ndiwe uliye sifa zangu.” Yeremia 17:14 “Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye.” Yeremia 30:17
“Tazama, nitauletea afya na kupona, nami nitawaponya; nami nitawafunulia wingi wa amani na kweli.” Yeremia 33:6
“Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake; nanyi mtatoka nje, na kucheza-cheza kama ndama wa mazizini.” Malaki 4:2
“Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.” Yakobo 5:14, 15

Ahadi kwa ajili ya Nguvu za Kufanya Mapenzi ya Mungu

“Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana; tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.” 2 Wakorintho 4:16-18
“Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.” Wagalatia 6:9 “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” Wafilipi 4:13
“Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.” Wafilipi 2:13
“Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.” 2 Wakorintho 12:9

Ahadi Kuhusu Kuwa Mashahidi wa Mungu

“Msiogope wala msifanye hofu; je! Sikukuhubiri haya zamani na kuyaonyesha? Na ninyi ni mashahidi wangu. Je! Yuko Mungu zaidi yangu mimi? Hakika hapana Mwamba; mimi sijui mwingine.” Isaya 44:8
“Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana umekuzukia.” Isaya 60:1
“Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho.” 2 Wakorintho 5:18
“Lakini Bwana akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru.” Yeremia 1:7
“Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.” Matendo 1:8
“Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu.” 1 Petro 2:9
“Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.” 1 Petro 3:15

Sherehe ya Siku ya Sabato

Buni Sabato ya Mwisho ya Siku Kumi za Maombi kwa ajili ya kusherehekea wema wa Mungu na nguvu yake kuu. Shiriki namna ulivyopata uzoefu wa kumwagwa kwa Roho Mtakatifu katika siku hizi kumi zilizopita. Sherehekea kwa yale Mungu aliyotenda, anayotenda, na atakayotenda. Mahitaji ya kila kusanyiko yanatofautiana, hivyo tafadhali fanya kazi pamoja na viongozi wa kanisa mahalia ili kuandaa mpango mahususi kwa ajili ya kanisa lako. Hapa kuna baadhi ya mambo ya kujumuisha katika ibada ya kanisa lako katika Sabato ya Mwisho.

Wazo Kuu:

Wito wa Maombi wa Malaika Watatu

Fungu Elekezi: “Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa.” (Ufunuo 14:6).

Mapendekezo ya Nyimbo:

Saa Heri ya Maombi, No. 135
Ati, Kuna Mvua Njema, No. 39
Njoni Kwangu, No. 103
Mtazame Mwokozi, No. 212
Mungu Atukuzwe, No. 3



Mapendekezo ya Hubiri

Mruhusu mchungaji, mzee wa kanisa, au kiongozi wa maombi kuhubiri somo fupi kuhusu wito wa ujumbe wa malaika watatu kwetu wa kuomba na kufanya matengenezo siku hizi za mwisho. Aya za Maandiko ni katika Ufunuo 14:6-12

[AU]

Wapatie nafasi washiriki wa Siku Kumi za Maombi kupokezana katika kutoa muhtasari kwa dakika 1 au 2 wa kila mwongozo wa maombi wa siku 10. Shiriki kichwa cha somo, fungu elekezi, na wazo kuu. (Andaa mapema ili muhtasari uwe ndani ya dakika 1-2. Kwa watu wengi, dakika moja ni maneno 125-150 yanayozungumzwa).

[AU]

Andaa vijana watatu wa kuwasilisha hubiri fupi la dakika kama tano hivi kuhusu jinsi ujumbe wa kila mmoja wa wale malaika watatu anavyotuita kuomba na kufanya matengenezo kabla Yesu hajarudi. Vijana wanaweza pia kusaidia katika muziki au shuhudia.

Mawazo mengine ya Programu:

Shuhuda za washiriki juu ya maombi yaliyojibiwa Muda wa maombi ya vikundi vidogo Matangazo ya maombi na shughuli zijazo za huduma Kisa cha watoto kuhusu maombi Chaguzi za nyimbo maalumu

Mahitaji ya Kuombea ya Kanisa la Kiulimwengu
Angalizo kwa viongozi:

Ifuatayo ni orodha ya mahitaji ya kuombea ambayo ni endelevu kwa kanisa la kilimwengu la Waadventista wa Sabato. Kwa sababu masuala ya kilingwengu na ya kanisa yanabadilika kwa kasi kubwa, tutatoa orodha ya nyongeza ya mahitaji ya kuombea iliyoboreshwa katika tovuti yetu kadiri muda unavyoenda. Unaweza kutembelea tovuti ya: www.tendaysofprayer.org kwa nyongeza ya mahitaji.
1. Bwana, hebu ruhusu ule uamsho wa kale wa uungu ufunike kanisa lako katika siku hizi za mwisho. Tuwezeshe kusimamia ukweli hata kama mbingu zingeanguka.
2. Tunaomba kwa ajili ya uhuru wa dini, na haki ya dhamiri ulimwenguni kote. Bwana, tunaomba ufungue milango ili Neno lako lipate kutangazwa.
3. Bwana, tunaomba kanisa lako ulimwenguni liitikie wito wa kutangaza ujumbe wa malaika watatu kwa mapana yake kwa kila taifa, lugha, na jamaa. Onesha jinsi ya kujenga mafundisho yote haya katika upendo na haki ya Kristo.
4. Bwana, wezesha Waadventista wa Sabato wote ulimwenguni kutamka kuwa “Nitakwenda” na kuitikia wito wa kukutumikia na kutangaza habari njema ya wokovu.
5. Tunaomba utupatie hekima ya kuchunguza, kuelewa na kuifuata Biblia Takatifu ya Mungu. Tufundishe kutenga maneno ya ukweli na uaminifu ili kushiriki na wengine.
6. Bwana, tunaomba uamshe upya hali ya kuthamini maagizo kutoka mbinguni yanayopatikana katika maandiko yaliyovuviwa ya Ellen G. White.
7. Tunaomba utumwagie mvua ya masika ya Roho Mtakatifu ili kuleta nguvu katika ushuhuda wetu itakayotuwezesha kumaliza kazi tuliyopewa na Mungu kufanya kabla ya kuja mara ya pili kwa Yesu Kristo.
8. Bwana, tunaomba upanyaji wako na rehema katika maeneo yaliyoathirika sana kwa janga hili la UVIKO-19
9. Tunawaombea wataalam wa tiba, wanasayansi, viongozi wa serikali, na maafisa wa afya ya jamii wajaliwe hekima kwa maamuzi mengi magumu wanayalazimika kufanya.
10. Tunaomba kwamba Waadventista wa Sabato wote ulimwenguni wawe tayari kusaidia na kutia moyo wale wote wanaopitia katika adha ya maumivu. Tupatie ujasiri, ubunifu, na roho isiyo na ubinafsi pale majirani wetu wanapokuwa wakituhitaji sana.
11. Tunawaombea wale wote waliathirika kifedha kwa sababu ya kupoteza ajira kufuatia tamko la kuzuiwa majumbani.
12. Bwana, tunaomba uwaoneshe waumini makanisani namna ya kuwasaidia wale ambao wanapambana na matatizo ya afya ya akili huku wakitengwa.
13. Tunawaombea wachungaji pamoja na makanisa kupata namna ya kuwezesha waumini kubakia katika muunganiko wakati huu wa kuzuiliwa majumbani. Bwana, tafadhali leta pamoja kanisa lako katika huduma na ibada.
14. Tunaomba kwa ajili ya uamsho wa kiroho kati ya vijana wa kanisa la Waadventista wa Sabato wanaohudhuria katika vyuo vikuu na taasisi zingine za elimu ulimwenguni kote. Tunaomba Bwana uwafanye kuwa mabalozi wakereketwa wa Kristo.
15. Tunaombea asilimia 69 ya watu ulimwenguni ambao hawajapokea mawasilisho yasiyochafuliwa ya Yesu.
16. Tunaombea watu milioni 62 katika miji 28 ambayo haijafikiwa au imefikiwa kwa uchache katika nchi ya Urusi (Divisheni ya Euro-Asia.)
17. Tunaomba Mungu ainue wamisionari jasiri walio tayari kufanya kazi kati ya makundi 746 yaliyopo katika nchi 20 za Mashariki ya kati.
18. Tunaombea wimbi kubwa la Waadventista wa Sabato watakaokuwa tayari kumtumikia Mungu kwa kuwapenda wengine na kwa kushiriki na watu kutoka katika tamaduni na dini zingine.
19. Bwana, tafadhali inua wanafunzi Wa-Aldensia ambao wako tayari kukutumikia katika maeneo magumu.
20. Tunaombea washiriki wa kanisa la Waadventista wa Sabato wanaokabiliwa na mateso na kutupwa gerezani kwa ajili ya Imani yao.
21. Tunaomba kwa ajili ya watu milioni 202 waliopo katika miji 41 iliyofikiwa kwa uchache katika Divisheni ya Asia Pacific kusini wapate kumfahamu Yesu.
22. Tunaomba kwa ajili ya Idara ya Shule ya Sabato na Huduma Binafsi ya kila kanisa mahalia kadiri wanavyotafuta mpango wa Mungu na kuwafikia walio nje katika jamii kwa huduma za upendo, mafunzo ya Biblia, na ushuhuda binafsi.
23. Tunaomba kwa ajili ya shirika la misaada la Waadventista wa Sabato (ADRA) kadiri wanavyokabiliana na mahitaji ya watu ulimwenguni kote.
24. Tunawaombea watu milioni 16 katika miji 6 ambayo imefikiwa kwa uchache sana katika divisheni ya Pacific ya kusini.
25. Tunaomba kuwa Roho Mtakatifu atusaidie kufahamu jinsi ya kufikia watu milioni 406 katika miji 105 ya divisheni ya Asia Pacific ya kaskazini ambayo haijafikiwa au imefikiwa kwa uchache sana.
26. Bwana, tunaomba ubariki Huduma ya Uchaplensia ya kanisa la Waadventista wa Sabato iweze kuhamasisha wahudumu pamoja na waumini wenye shauku ya kuhudumia watu waliopo magerezani.
27. Ee Bwana, tunaombea waalimu wa Shule ya Sabato. Wasaidie kufahamu umuhimu wa kazi yao kwa watoto wetu.
28. Bwana, tunaomba uongozi kwa vituo vingi vya mvuto, programu za afya na familia, pamoja na klabu za Watafutanjia ulimwenguni kote.
29. Tunaomba kwamba utusaidie kupenda, kulea, na kufanya wanafunzi wale washiriki wapya na wageni wanaohudhuria kanisani. 30. Bwana, tunaomba utuoneshe jinsi ya kupeleka machapisho yaliyojawa na kweli kwa jamii zetu. Tunaomba kwamba uwajalie kuyasoma na kwamba Roho Mtakatifu alete ushawishi katika ukweli wa Biblia.
31. Bwana, tunaomba ulinzi wako kwa wamisionari wanaofanya kazi katika maeneo hatarishi
32. Tunakuomba uinue wainjilisti wa vitabu, wanafunzi wa kujitolea, waandishi, wataalam wa mitandao ya kijamii, pamoja na wafadhili watakaosaidia kueneza maneno ya matumaini na uzima.
33. Tunaomba kwa ajili ya shule za kanisa la Waadventista wa Sabato, wanafunzi, pamoja na waalimu ulimwenguni kote. Hebu shule hizi zifundishe kwa uaminifu kweli za Biblia na kuwaongoza vijana katika utume, huduma na kushiriki uhusiano na Kristo. 34. Bwana, tupatie hekima ya kufikia tamaduni zingine ambazo hazina shauku ya dini. Hebu Roho wako Mtakatifu aangushe kuta ambazo zinazunguka roho hizo.
35. Tunakuomba utubariki kadiri tunawavyofikia watu waliofungwa katika ibada ya mizimu, ibada ya sanamu, na imani za kinyama. Tusaidie kuelewa mtazamo wao wa kidunia na kuwatambulisha kwa Mwokozi wao binafsi.
36. Bwana, tunakuomba ulete uvuvio kwa kanisa la Waadventista wa Sabato ulimwenguni kote wapate kuomba kwa namna ambayo hawajawahi kuomba. Tufundishe kudai ahadi zako na kutazamia kwamba utahamisha milima zaidi tunapoomba.
37. Tunaomba kwa ajili ya makundi 514 ya watu katika nchi 18 za divisheni ya Afrika India Kusini. Tafadhali waongoze katika ukweli wa Biblia.
38. Tunakuomba utuoneshe jinsi ya kupata mahitaji ya kiroho ya wakimbizi. Hebu kanisa letu lifahamike kwa upendo wetu kwa watu wote, bila kujali kuwa ni akina nani au wanatoka wapi.
39. Tunakuomba uinue wamisionari wa mijini wapate kuanzisha makanisa kwa makundi 806 ya watu katika nchi 20 za divisheni ya Ulaya.
40. Tunakuomba uinue jeshi la watendakazi watakaoanzisha makanisa kati ya makundi 948 ya watu katika nchi 38 za divisheni ya Amerika (Inter-America Division)
41. Bwana, tunakuomba uandae vijana watakaojihusisha katika kuanzisha makanisa kati ya makundi 788 ya watu katika nchi 9 za divisheni ya Amerika kaskazini.
42. Tunakuomba uandae watu wa kujitolea ili kuhudumia makundi 70 ya watu katika Field ya Israeli.
43. Tunakuomba uinue wamisionari matabibu ili kuanzisha makanisa kati ya makundi 830 ya watu katika nchi 11 za divisheni ya Afrika ya Mashariki na Kati.
44. Tunakuomba uinue mashujaa wa maombi wapate kuombea makundi 2,568 ya watu katika nchi 4 za divisheni ya Asia kusini. 45. Tafadhali wezesha familia zetu kudhihirisha upendo wako majumbani mwetu na katika jamii zinazotuzunguka. Tunaomba uleta upatanifu majumbani, ponya mahusiano yaliyovunjika, linda wahanga wa unyanyasaji, na dhihirisha uwezo wako utakasao katika hali zinazoonekana kutokuwa na matumaini.
46. Tunakuomba uinue wauguzi na madaktari wa kuanzisha makanisa mapya kati ya makundi 1,978 ya watu katika nchi 22 za divisheni ya Afrika ya kati.
47. Tunaomba kwa ajili ya watu milioni 49 katika miji 19 ambayo hijafikiwa au imefikiwa kwa uchache sana katika divisheni ya Trans Europe
48. Tunaomba kwa ajili ya Watoto wetu, tafadhali wawezeshe kusimama kwa ujasiri kukutetea wanapokabiliana na vikwazo na misukumo. Wasaidie kufanya chaguzi sahihi na kusimamia ukweli.
49. Tunaomba utufundishe kufuata mfano wa Yesu usiokuwa na ubinafsi kwa kukabiliana na mahitaji ya kila siku ya watu wanaotuzunguka. Tuwezeshe kuhudumu kama wamisionari matabibu, watu wanaojitolea katika jamii, na marafiki wa watu wenye uhitaji.
50. Tunaombea viongozi wa vijana ulimwenguni kote ambao ni waaminifu katika kupatia vizazi vinavyofuata urithi wa utambulisho wa Kristo, utume wa kanisa la Waadventista wa Sabato, na uongozi katika makanisa mahalia.
51. Tunaomba kwa ajili ya vijana wetu wanaoishi katika hali hatarishi kwa ajili ya Bwana kupitia katika program ya OYIM na Mission Caleb.
52. Tunaombea washiriki wa kanisa la Waadventista wa Sabato, wachungaji, na viongozi ulimwenguni kote wapate kujilisha katika Neno la Mungu kila siku. Utuwezeshe kukutafuta katika maombi kila siku. Tukumbushe kwamba, bila wewe hatuwezi kufanya lolote.





Siku ya Kwanza

Umuhimu wa Maombi

Fungu Elekezi: Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?Luka 11:13

Kazi ya Kukatisha Tamaa

Idadi ya watu duniani inaongezeka kwa mlipuko. Takwimu za hivi karibuni za idadi ya watu duniani zinaonesha kwamba kuna watu takribani bilioni 7.8 waliosongamana katika tufe hili tunaloliita dunia kadiri linavyozunguka angani kwa kasi ya kilometa kama 107,300 kwa saa. Kila siku wanazaliwa Watoto 385,000, ambao ni kama milioni 140 kila mwaka, na tunashangaa jinsi tunavyoweza kuifikia dunia yote kwa Habari njema za Injilii na kurudi kwa Yesu mara ya pili kunakokaribia. Kila mwaka wanazaliwa watu wengi mara saba kuliko idadi ya Waadventista wa Sabato waliopo sasa hivi.

Au fikiria changamoto hii kwa namna nyingine. Miji iliyoko ulimwenguni inaogezeka kwa kasi kubwa. Kuna miji 548 kwa uchache yenye idadi ya watu kama milioni moja hivi au zaidi kila mmoja. Sehemu kubwa ya hii miji iko maeneo ambayo uwepo wa kanisa la Waadventista wa Sabato ni mdogo sana. Kazi ya kukatisha tamaa inayohitaji kuufikia upande huu wa ulimwengu kwa ujumbe wa malaika watatu iko mbele yetu kwa uzito wote. Mamilioni ya watu wanapoteza Maisha yao bila Kristo wala elimu ya habari njema ya wokovu na tumaini la kuja kwake mara ya pili. Wakati mwingine kazi iliyo mbele yetu inaonekana kama haiwezekani – hivyo, hisia hizi na zitupeleke magotini kwa maombi ya dhati.

Kupitia katika uwezo wa Roho Mtakatifu

Hakuna kiasi cha jitihada za kibinadamu zianazoweza kutufanya tuufikie ulimwengu wetu kwa ajili ya Kristo. Mipango ya binadamu haina uwezo hadi pale inapowezeshwa na Roho Mtakatifu. Ni kupitia katika uwezo wa Roho Mtakatifu pekee ndipo tunapoweza kuufikia ulimwengu huu tukiwa na ujumbe wa wakati wa mwisho. Ni kupitia katika uwezo wa Roho Mtakatifu pekee ndipo tutaweza kufikia mamilioni ya watu waliopo katika miji mikuu ya ulimwengu huu. Ni kwa kupitia katika uwezo wa Roho Mtakatifu pekee ndipo injili inaweza kupenya na kufikia nchi ambazo haziingiliki.

Ni kwa kupitia katika uwezo wa Roho Mtakatifu ndipo tunapoweza kuzifikia jamii zetu. Na Habari njema hasa ni kwamba Mungu tayari anafanya kazi katika maeneo haya ambayo ni “magumu kufikia.” Anatualika tumtafute ili tupate nguvu za kukamilisha kazi iliyoko mbele yetu.

Hatazidi sana

Yesu anasema kuwa, “Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?” (Luka 11:13). Tambua msemo huu, hatazidi sanakatika aya hii. Yesu anataka kuzidi sana kufanya kwa ajili yetu kila mmoja binafsi, na zaidi sana kwa kanisa lake kuliko tunavyodhani. Anatusihi tumwombe Roho Mtakatifu, kusihi hasa kwa ajili ya Roho Mtakatifu, kutafuta mibaraka ya Roho kwa moyo wetu wote – siyo kwa sababu hataki kutupatia, bali kwa sababu hatujawa tayari kuipokea. Tunapoanza siku hizi kumi za maombi mwaka huu, hebu na tudai kwa pamoja ahadi hii. “Ahadi ya Roho Mtakatifu haikuwa kwa ajili ya kizazi fulani tu, au kwa ajili ya watu wa aina fulani tu. Kristo anatamka kwamba nguvu ya kimbingu ya Roho Mtakatifu itaandamana na wafuasi wake hata mwisho wa dunia. Tangu siku ile ya Pentekosti hadi wakati wetu huu, yule msaidizi amepelekwa kwa wale wote waliojitoa kikamilifu kwa Bwana na kwa kazi yake.” The Acts of Apostles, uk. 49. Tuombe pamoja…

Wakati wa Maombi (Dakika 30-45)

Ushuhuda kutoka katika maombi ya siku kumi mwaka 2021

“Ninashukuru sana kwa siku kumi za maombi… Ninahisi kama kuna moto umewashwa ndani yangu. Ninajikuta ninapitisha muda mwingi nikisoma Biblia na katika maombi na Bwana… Ninashukuru na kumsifu Mungu kwa kufungua macho yangu, moyo wangu na mawazo yangu nipate kumkubali Yesu na Roho Mtakatifu kikamilifu katika Maisha yangu.” (Constance)

Ahadi Yenye Nguvu

“19 Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. 20 Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.” (Mathayo 18:19, 20). Niombe mimi, nami nitakujibu. Ahadi inatolewa kwa masharti kwamba maombi yanafanywa na kanisa kwa kuungana pamoja, na inawezekana majibu yatakayotolewa yakawa kwa upeo mkubwa kuliko kama maombi hayo yangefanywa katika ngazi binafsi. Nguvu inayotolewa itakuwa katika uwiano na ule umoja wa wale washiriki na upendo wao kwa Mungu na kwa kila mmoja.” EGW, Manuscript Release, vol. 9, uk. 303 Vikundi vyote vya maombi vina namna tofauti ya kuomba pamoja. Tunawahimiza kutumia dakika 30-45 zinazofuata katika maombi ya pamoja kwa namna yoyote ile ambayo Roho Mtakatifu ataongoza. Hapa chini pana mfano wa jinsi ya kuomba kupitia kwa Maandiko. Unaweza kuomba kupitia katika aya za Maandiko, pitia kule kwenye mwongozo wa kiongozi kwa ajili ya mawazo tofauti ya maombi.

Kuomba Kupitia katika Neno la Mungu Luka 11:13

“Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?”

“Hatazidi sana…”

Ee Mungu, wewe ni mwema, Unanitakia mema kwa namna ambayo hata baba mwenye upendo hawezi kutoa. Unanifahamu vyema katika undani wangu moyoni, ni wewe pekee unayeelewa jinsi ya kunirejesha, kuniponya, na kunibadilisha.

“Roho Mtakatifu”

Ee Yesu, nashukuru kwa ajili ya ahadi yako ya Roho Mtakatifu. Analeta mibaraka ya Mungu katika Maisha yetu. Anakutukuza katika mioyo yetu. Anatumia faida ya wokovu uliouwezesha pale Kalwari katika Maisha yetu. Ahsante sana kwa zawadi hii!

“Nani Anayemuuliza”

Baba, leo ninadai ahadi iliyoko katika kitabu cha Luka 11:13. Kila siku nitakuomba kwa furaha, ujaze Maisha yangu kwa uwepo na uwezo wa Roho Mtakatifu. Ninakuomba uondoe katika Maisha yangu chochote kile kinachoweza kusimama katika mapito yangu ya kujitoa kwangu kwako. Nibatize mimi na kanisa langu kwa Roho Mtakatifu ili tuweze kumtukuza Yesu katika ulimwengu unaokuhitaji.

Mapendekezo zaidi ya Maombi

Shukurani na Sifa:
Shukuru kwa mibaraka mahususi na msifu Mungu kwa wema wake.
Kuungama: Tumia dakika chache kwa ajili ya maungamo binafsi na msifu Mungu kwa msamaha wake.
Uongozi: Mwombe Mungu akupatie hekima kwa changamoto na maamuzi ya sasa.
Kanisa Letu: Muombe Mungu kwa ajili ya mahitaji ya kanisa katika ngazi ya majimbo na kanisa la ulimwengu (tazama karatasi nyingine yenye mahitaji).
Mahitaji ya eneo mahalia: Ombea mahitaji ya washiriki wa kanisa, familia, na majirani.
Sikiliza na Itika: Tumia muda kuisikiliza sauti ya Mungu na kuitikia kwa sifa au wimbo.

Mapendekezo ya Nyimbo:

Nijaze Sasa (#40)
Roho Mtakatifu (#41)
Zitakuwa Nyota Tajini (#58)
Saa Heri ya Maombi (#135)

 




Siku ya Pili

Injili ya Milele na Maombi

Fungu Elekezi: Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaaUfunuo 14:6

Ujumbe wenye Umuhimu Mkubwa

Mungu ameipatia sayari hii ujumbe wa muhimu sana uliokusudiwa mahususi kwa ajili ya wakati wetu huu katika jumbe za malaika watatu wa Ufunuo 14:6-12. Mtume Yohana akiwa kizuizini katika kisiwa cha Patmo anatutambulisha katika jumbe hizi. Tunatakiwa kuzingatia mambo matatu kabla hatujaingia katika ujumbe wenyewe. Jambo la kwanza ni kuwa ujumbe huu ni wa kimbingu. Unakuja moja kwa moja kutoka katika kiti cha enzi cha Mungu. Unaonekana kutolewa kwa wanadamu na malaika anayeruka kati kati ya mbingu. Jambo la pili la kutambua kuhusu huu ujumbe ni kuona malaika “akiruka.” Ni ujumbe wenye umuhimu wa haraka. Ni lazima utangazwe bila kuchelewa. Na jambo la tatu ni kuwa ujumbe huu ni wa milele, ikimaanisha kuwa ujumbe huu unahusu vizazi vyote. Haulengi utamaduni fulani au kikundi fulani cha lugha au jamaa. Ni lazima ujumbe huu utangazwe kwa kila taifa na kabila na lugha na jamaa.

Kiini cha ujumbe huu ni “Injili ya Milele” au, habari njema ya maisha ya kujitoa kafara ya Yesu, huduma yake ya upendo, kifo chake cha upatanisho, jinsi alivyofufuka, huduma yake ya maombezi kama kuhani wetu mkuu, na jinsi atakavyorudi mara ya pili kwa utukufu mwingi. Ile njozi ya injili ya milele katika Ufunuo 14 inathibitisha maneno ya Yesu katika kitabu cha Mathayo 24: “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.” (Mathayo 24:14). Haya maneno ya Kristo ni ahadi kwamba, “injili itahubiriwa katika ulimwengu wote” kabla ya kurudi kwake mara ya pili. Kutakuwa na uamsho wa pekee kati ya watu wa Mungu. Watajitokeza kwa changamoto hii, wakitambua umuhimu wa saa yenyewe, huku wakiwa wamejawa na Roho Mtakatifu, watadhihirisha upendo wa Yesu, neema yake na ukweli kwa ulimwengu uliochafuliwa na dhambi na unaoonekana kuelekea katika hatima yake.

Ellen G. White anaiweka kwa jinsi hii, “Kabla ya hukumu ya Mungu kutolewa kwa ulimwengu huu, kutakuwa na uamsho wa pekee wa kiungu kati ya watu wa Bwana kwa namna ambayo haijawahi kushuhudiwa tangu enzi za mitume. Roho Mtakatifu na uwezo wa Mungu utamwagwa juu ya Watoto wake. Wakati huo, wengi watajitenga kutoka katika kanisa, ambao kwao, upendo wa dunia hii umezidi upendo kwa Mungu na Neno lake. Wengi wao, wachungaji pamoja na watu wa kawaida, watapokea kwa furaha kweli hizi ambazo Mungu amesababisha kutangazwa wakati huu ili kutayarisha watu wake kwa ajili ya kurudi mara ya pili kwa Bwana.” (EGW, The Great Controversy, uk. 464)

Kabla ujumbe wa Ufunuo 14 haujatangazwa kwa ulimwengu wote, kutakuwa na uamsho kati ya watu wa Mungu utakaowawezesha kushirikiana na Mungu katika kumaliza kazi yake. Hebu tuombe pamoja ili uamsho huu wa kiroho ufanyike katika Maisha yetu wenyewe kwa ajili ya kututayarisha kwa matukio ya wakati wa mwisho wa historia ya dunia hii.

Wakati wa Maombi (Dakika 30-45)

Ushuhuda kutoka katika maombi ya siku kumi mwaka 2021

“Siku kumi za maombi zimesababisha muujiza wa uponyaji kwangu. Nilikuwa nimelazwa hospitalini kwa sababu ya ugonjwa ulionishika ghafla kabla ya kuanza kwa siku hizi kumi za maombi. Nikakaribishwa kujiunga na program ya siku kumi za maombi nikiwa kitandani kule hospitali. Ilikuwa ni mara ya kwanza kwangu kushiriki. katika mkutano wa usiku kupitia katika mtandao wa Zoom, wengi waliniombea nipate kupona. Ninamtukuza Mungu kwa roho za wale walioomba kwa dhati kwa kila hitaji lililotolewa kila siku usiku… Mungu amekuwa mwenye neema kwangu kwa sababu niliruhusiwa kutoka hospitalini hata kabla siku kumi za maombi hazijafikia mwisho. Ni uwezo wake wa uponyaji ulioniwezesha kurudia afya yangu. Nilikuwa mgonjwa, naye akanigusa. Ni dhahiri kuwa hilo lilikuwa ni jibu kwa maombi yetu!” (Harley)

Kuomba Kupitia katika Neno la Mungu Ufunuo 14:6

“Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa,”

“Injili ya Milele”

Mungu ananipatia namna ya kutambua na kufurahia ujumbe wa injili. Ananipatia furaha ya wokovu na kubadilisha Maisha yangu kiasi kwamba wengine wanaponiona, wanaona uwezo wa injili katika utendaji na hivyo, kuvutwa kwa Yesu.

“Awahubiri hao wakaao juu ya nchi”

Baba, natamani uzoefu wa injili nikiwa nawe, ili kwamba nipate kushiriki Habari hii njema na wengine kwa maneno na kwa matendo. Ninaomba unitumie kushuhudia familia yangu, mrafiki, watendakazi wenzangu, majirani zangu na watu waliopo katika upeo wa mvuto wangu.

“Kwa Kila Taifa”

Ulimwengu huu unafikia mwisho wake, na mabilioni ya watu bado wako gizani. Ee Yesu, tafadhali nipatie fursa juma hili ya kushiriki Habari njema kuhusu nafasi ya wokovu unayotoa kwa mtu fulani. Nipatie stadi na hekima ya kushuhudia watu wa mataifa mengine, tamaduni zingine, na lugha na jamaa zingine. Ahsante sana kwamba unawaita wanadamu wote wakuamini wewe.

Mapendekezo zaidi ya Maombi

Shukurani na Sifa:

Shukuru kwa mibaraka mahususi na msifu Mungu kwa wema wake.
Kuungama: Tumia dakika chache kwa ajili ya maungamo binafsi na msifu Mungu kwa msamaha wake.
Uongozi: Mwombe Mungu akupatie hekima kwa changamoto na maamuzi ya sasa.
Kanisa Letu: Muombe Mungu kwa ajili ya mahitaji ya kanisa katika ngazi ya majimbo na kanisa la ulimwengu (tazama karatasi nyingine yenye mahitaji).
Mahitaji ya eneo mahalia: Ombea mahitaji ya washiriki wa kanisa, familia, na majirani.
Sikiliza na Itika: Tumia muda kuisikiliza sauti ya Mungu na kuitikia kwa sifa au wimbo.

Mapendekezo ya Nyimbo:

Kuwatafuta Wasioweza (#100)
Nataka Nimjue Yesu (#54)
Msalabani Pa Mwokozi (#19)
Hadithi ya Kisa cha Yesu (#34)
Kuwa na Yesu Mwokozi (#51)
Mtakatifu, Mtakatifu (#1)

 




Siku ya Tatu

Utume wa Mungu na Maombi
Sehemu ya 1

Fungu Elekezi: Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.Matendo 1:8

Ahadi kwa Utume Usiowezekana

Jumbe za malaika hawa watatu ni jumbe zenye wito muhimu wa haraka wa utume. Kazi inayoonekana kutokuwezekana ya kuufikia ulimwengu kwa injili itawezekana tu kupitia kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Changamoto ya utume wakati wa mwisho ni sawa na changamoto ambazo kanisa la awali la Agano Jipya lilikabiliana nazo katika kitabu cha Matendo. Ahadi ya Roho Mtakatifu inatolewa kwetu kwa namna ile ile iliyotolewa kwao na Yesu katika Matendo 1:8 “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.” Kwa kupitia katika uwezo wa Roho Mtakatifu, kanisa la wakati wa Agano Jipya lilikuwa na mguso mkubwa kwa ulimwengu wa wakati huo. Maelfu ya watu walimkubali Kristo kama Masihi na kubatizwa.

Kitabu cha Matendo kinadhihirisha ule uhusiano wa karibu uliokuwepo kati ya kanisa linaloomba na kanisa lililojawa na Roho Mtakatifu linaloshuhudia. Tunasoma katika Matendo 1:14 kuwa, “Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake.” Na katika Matendo 2:42 tunasoma pia kuwa, “Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.” Tunapata nyongeza katika Matendo 4:31 kuwa, “Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.” Tunatambua mambo matatu katika aya hii ya mwisho. Waumini waliomba, walijazwa na Roho Mtakatifu, na matokeo yake, walinena Neno la Mungu kwa ujasiri – au kwa tafsiri nzuri zaidi – walinena Neno la Mungu kwa kujiamini. Maombi, Roho Mtakatifu, na utume vinaunganika kwa ukamilifu. Ukurasa wa 42

Ni lazima Tuwe Naye

Akitoa wazo kuhusu uzoefu wa mitume, Ellen G. White anatambulisha kuwa, “Tunapaswa kuomba kwa dhati kwa ajili ya kushuka kwa Roho Mtakatifu kama vile mitume walivyoomba wakati ule wa Pentekosti. Ikiwa walimhitaji Roho Mtakatifu wakati ule, ni dhahiri kwamba sisi leo hii tutakuwa tunamhitaji zaidi yao.” (EGW, Testimonies for the Church, vol. 5, uk. 158). Ni utambuzi gani wa kimbingu huo! Ikiwa mitume walihitaji kumwagwa kwa Roho Mtakatifu ili waweze kuifikia dunia ya wakati wao kwa injili, ni dhahiri kwamba sisi tutahitaji nguvu ya huyo Roho Mtakatifu kwa kiwango kikubwa zaidi. Ulimwengu ni mkubwa, uliojichanganya sana ukishuhudia kupungua kwa sehemu kubwa kwa ile hali ya uungu.

Huu ndio wakati wa kumtafuta Mungu kwa maombi ili kupokea nguvu zisizopimika za Roho Mtakatifu kwa sababu ya kukamilisha kile ambacho kinaonekana kutokuwezekana. Ellen G. White anaandika kuwa, “Kushuka kwa Roho Mtakatifu katika kanisa kunatazamiwa siku za usoni, lakini ni faida ya kanisa kuwa naye wakati huu wa sasa. Mtafute Roho Mtakatifu, mwombee, na uamini. Ni lazima tuwe na Roho Mtakatifu, na ni kweli kwamba mbingu zinasubiri kutupatia.” (EGW, Evangelism, uk. 701) Hebu sisi sote tutafute huo uwezo na nguvu za Roho Mtakatifu ili kukamilisha zoezi la kuhubiri ujumbe wa malaika watatu katika kizazi hiki. Hebu na tumtafute Mungu pamoja katika maombi tupate kumwagiwa Roho Mtakatifu kwa upeo mkubwa.

Wakati wa Maombi (Dakika 30-45)

Ushuhuda kutoka katika maombi ya siku kumi mwaka 2021

“Nilitumia muda mwingi wa maisha yangu ukubwani nikijaribu kutafuta furaha katika mambo ya dunia hii. Niliendelea kujiambia kwamba kama ningepata mtu aliye sahihi, nikapata kazi sahihi, nikapunguza uzito kidogo, pengine hatimaye ningepata furaha ninayotaka. Kwa kweli sikufahamu kwamba kadiri nilivyokuwa nikijiachia katika madhahabu ya dunia hii ndivyo nilivyozidi kujisikia mtupu. Nimekuwa nikipokea machapisho ya siku kumi za maombi kupitia kwenye baruapepe yangu, lakini kwa hakika sikuwahi kuyapitia kikamilifu na kuyamaliza. Nilidhani nimeshikika sana nikijichimbia mabirika yavujayo, yasiyoweza kuweka maji badala ya kuchota maji ya uzima yaliyokuwa karibu nami tu. Wakati huu niliamua kumjaribu Yesu na kumchukulia kwa Neno lake. Nakiri kwamba siku hizi kumi zimekuwa za ajabu sana kwangu! Kama vile Mariamu katika kaburi la Yusufu wa Arimathayo, nimemwona Yesu na, kwa kweli Yesu yu hai. Kristo amenipatia mtazamo mpya kwa maombi, utii, na Ukurasa wa 43 Imani. Nilimpatia moyo wangu upya baada ya kuungama dhambi zangu, na nimemwomba adumu ndani yangu. Sasa hivi nina sababu kubwa ya kuishi!” (Thuto)

Kuomba Kupitia katika Neno la Mungu Matendo 1:8

“Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”

“Mtapokea Nguvu…”

Ee Mungu, ninafahamu kwamba sina uwezo wala nguvu kuniwezesha kutekeleza utume wa ujumbe wa malaika watatu uliotupatia. Ni ujumbe mgumu, na kwa mtazamo wa kibinadamu hauwezekani. Ninakushukuru kwa ahadi ya nguvu za Roho Mtakatifu. Ninatambua hitaji langu kuu la ubatizo wa Roho Mtakatifu kila siku, na ninaamini katika ahadi zako za kuwapatia nguvu wale ambao wanakutumaini.

“Nanyi Mtakuwa Mashahidi Wangu…”

Ee Yesu, ninakushukuru kwa kunifanya shahidi wa upendo wako, ukweli, na nguvu ibadilishayo. Ninakuomba unipatie ujasiri wa kushiriki kile ambacho umetenda kwa ajili yangu pamoja na wale wanaonizunguka katika siku hizi za mwisho wa historia ya dunia hii. Nakuomba unipatie fursa zaidi ya kukushuhudia na kuwaambia wengine jinsi wewe ulivyo Mkuu.

“Hata Mwisho wa Dunia…”

Baba, ninatambua kwamba eneo langu la utume linaanzia nyumbani na kuenea kwa majirani wangu, jumuia yangu, kijiji changu na mji ninaokaa, na hata ulimwenguni kote. Nakuomba unioneshe jinsi nitakavyojiunga na utume wako pale nilipo leo, na jinsi ninavyoweza kutegemeza kazi ya injili ulimwenguni kote.

Mapendekezo zaidi ya Maombi

Shukurani na Sifa:
Shukuru kwa mibaraka mahususi na msifu Mungu kwa wema wake.
Kuungama: Tumia dakika chache kwa ajili ya maungamo binafsi na msifu Mungu kwa msamaha wake.
Uongozi: Mwombe Mungu akupatie hekima kwa changamoto na maamuzi ya sasa.
Kanisa Letu: Muombe Mungu kwa ajili ya mahitaji ya kanisa katika ngazi ya majimbo na kanisa la ulimwengu (tazama karatasi nyingine yenye mahitaji). Ukurasa wa 44
Mahitaji ya eneo mahalia: Ombea mahitaji ya washiriki wa kanisa, familia, na majirani.
Sikiliza na Itika: Tumia muda kuisikiliza sauti ya Mungu na kuitikia kwa sifa au wimbo.

Mapendekezo ya Nyimbo:

Nilipotoka Kabisa (#118)
Ati Kuna Mvua Njema (#39)
Niwe Kama Yesu (#136)
Huniongoza Mwokozi (#151)
Nionapo Msalaba (#63)
Fanyeni Kazi Zenu (#59)
Twae Wangu Uzima (#146)

 





Siku ya Nne

Utume wa Mungu na Maombi
Sehemu ya 2

Fungu Elekezi: 3 Twamshukuru Mungu, Baba yake Bwana wetu Yesu Kristo, siku zote tukiwaombea; 4 tangu tuliposikia habari za imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo mlio nao kwa watakatifu wote; 5 kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni; ambalo habari zake mlizisikia zamani kwa neno la kweli ya Injili; 6 iliyofika kwenu, kama ilivyo katika ulimwengu wote, na kuzaa matunda na kukua, kama inavyokua kwenu pia, tangu siku mlipoisikia mkaifahamu sana neema ya Mungu katika kweli.Wakolosai 1:3-6.

Ukuaji wa Kasi

Ukuaji wa kanisa la awali la Agano la Kale ulikuwa wa mlipuko. Katika kujibu maombi ya dhati kutoka katika mioyo ya mitume Roho Mtakatifu alimwagwa kwa nguvu kubwa. Watu elfu tatu walibatizwa mahali pamoja kwa siku moja. Katika Matendo 4 tunakumbushwa kwamba, “…wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini; na hesabu ya watu waume ikawa kama elfu tano.” (Matendo 4:4). Ikiwa tutajumuisha wanawake na watoto, idadi ya waumini kwa hakika ingeongezeka siku chache baada ya Pentekoste na kufikia 15,000 hadi 20,000. Ukipitia kitabu chote cha Matendo ya Mitume, utaona kuwa kanisa lilikua na kuongezeka kwa kasi kubwa. Katika Matendo 6 tunasoma kuwa makuhani na viongozi wa dini wakaitii ile Imani (fungu la 7). Maelezo yatupatia kisa cha Filipo akihubiri katika Samaria, safari za kitume za Paulo katika ulimwengu wa Mediterania, Petro akijifunza Maandiko na Kornelio, na waumini wakijazwa na Roho Mtakatifu huku wakishiriki ujumbe wa Kristo kila mahali. Mguso wa injili ulikuwa mkubwa kiasi kwamba Paulo aliweza kusema kwamba injili ilihubiriwa kwa viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu. (Wakolosai 1:3)

Uzoefu wa kanisa la awali la Agano Jipya unakuwa kama namna ya kuelekeza kanisa la leo kadiri tunavyosubiri kuja kwa Bwana wetu mara ya pili. Kiini cha mafanikio yao kilikuwa ni nini? Kwa nini hilo kanisa la awali la Agano Jipya liliongezeka kwa kasi hivyo? Hebu tupitie baadhi ya sababu. Kanisa la awali la Agano Jipya lilijaza maombi katika kila shughuli waliyofanya. Waliishi Maisha yaliyokuwa yamekabidhiwa Ukurasa wa 46 kikamilifu kwa Mungu na kumtegemea kwa yote. Walitambua kwamba hawakuwa na uwezo wa kukamilisha utume wa Yesu bila nguvu za Yesu. Ellen G. White anaeleza wazi wazi kuwa: “Tunahitaji kumtazama Yesu daima, tukitambua kwamba ni nguvu zake zinazofanya kazi. Pamoja na kufanya kazi kwa dhati kwa wokovu wa waliopotea, ni lazima pia tutenge muda wa kutafakari, wa maombi, na wa kujifunza Neno la Mungu. Ni kazi ile inayokamilishwa kwa maombi, ikitakaswa na kule kustahili kwa Kristo, ndiyo itakayothibitika na kuwa na ufanisi katika mema.” EGW, The Desire of Ages, uk. 362

Utume wa Mungu Kwa namna ya Mungu

Tambua maagizo haya kwa uangalifu. Ni uwezo wa Kristo unaokamilisha kazi yake kupitia kwetu. Siyo hekima yetu, akili zetu, mvuto wetu, wala elimu yetu. Ile hekima ya kuongoa roho inatoka kwa Yesu. Nguvu ya kubadilisha Maisha ni ya Kristo na Kristo pekee. Hatimaye, ni kazi ile inayokamilishwa kwa maombi, ikitakaswa na kule kustahili kwa Kristo, ndiyo itakayothibitika na kuwa na ufanisi katika mema. Utume wa Mungu ni lazima ukamilishwe kwa namna ya Mungu.

Je, kuna mpendwa wako unayetamani kumwona katika ufalme wa Mungu? Je, kuna Rafiki au mfanyakazi mwenzako anayemhitaji Yesu? Kuna mtu fulani unayemfahamu ambaye hapo awali alitembea na watu wa Mungu lakini leo hii yuko kivyake? Andika majina yao katika kipande cha karatasi na kukiweka ndani ya Biblia yako penye aya hizi: 1 Yohana 5:14-17. Kila siku, dai hiyo ahadi ya Mungu kwa niaba ya hao wapendwa wako. Hebu sasa hivi na tutumie muda kidogo kumwomba Mungu atukumbushe watu ambao angependa tuwashuhudie. Tupige magoti na kuwaombea kwa pamoja.

Wakati wa Maombi (Dakika 30-45)

Kuomba kupitia kwa Neno la Mungu
Wakolosai 1:3-6
“3 Twamshukuru Mungu, Baba yake Bwana wetu Yesu Kristo, siku zote tukiwaombea; 4 tangu tuliposikia habari za imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo mlio nao kwa watakatifu wote; 5 kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni; ambalo habari zake mlizisikia zamani kwa neno la kweli ya Injili; 6 iliyofika kwenu, kama ilivyo katika ulimwengu wote, na kuzaa matunda na kukua, kama inavyokua kwenu pia, tangu siku mlipoisikia mkaifahamu sana neema ya Mungu katika kweli.”

Kuomba Kila Siku

Ukurasa wa 47 Bwana, tunaungama kwamba hatukutumia muda wa kutosha katika maombi. Mara nyingi tunategemea hekima yetu wenyewe, na mipango yetu katika yote tunayofanya. Inapokuja suala la kukamilisha utume wako, hatutafuti uongozi wako kiasi cha kutosha. Tafadhali utusamehe. Tusaidie kuwa watu na kanisa la maombi linalokutegemea kwa mafanikio na siyo mawazo na mipango ya kibinadamu. Badilisha Maisha yetu ya maombi na kuleta kwetu uamsho wa pekee.

Imani yako kwa Yesu Kristo

Bwana, tunatambua kwamba ni kazi ile inayokamilishwa kwa maombi, ikitakaswa na kule kustahili kwa Kristo, ndiyo itakayothibitika na kuwa na ufanisi katika mema. Tunakuomba utusaidie kufanya maombi ya dhati na ya kudumu kuwa kipaumbele cha juu katika jitihada zote za utume na shughuli za kanisa letu, lakini pia katika Maisha yetu binafsi na familia kwa ujumla. Ongeza Imani yetu katika uwezo wako wa kutimiza ahadi ulizotupatia.

Upendo Wako kwa Watakatifu Wote.

Mungu wa upendo, wewe ulituumba tukiwa na uwezo wa ndani yetu wa kukua katika upendo wako. Ahsante sana kwa kumwaga upendo wako mioyoni mwetu ili kwamba tupate kuwezeshwa kuwapenda wale wanaotuzunguka.

Mapendekezo zaidi ya Maombi

Shukurani na Sifa:
Shukuru kwa mibaraka mahususi na msifu Mungu kwa wema wake.
Kuungama: Tumia dakika chache kwa ajili ya maungamo binafsi na msifu Mungu kwa msamaha wake.
Uongozi: Mwombe Mungu akupatie hekima kwa changamoto na maamuzi ya sasa.
Kanisa Letu: Muombe Mungu kwa ajili ya mahitaji ya kanisa katika ngazi ya majimbo na kanisa la ulimwengu (tazama karatasi nyingine yenye mahitaji).
Mahitaji ya eneo mahalia: Ombea mahitaji ya washiriki wa kanisa, familia, na majirani.
Sikiliza na Itika: Tumia muda kuisikiliza sauti ya Mungu na kuitikia kwa sifa au wimbo.

Mapendekezo ya Nyimbo:

Bwana Ninakuhitaji (#16)
Yanipasa Kuwa Naye (#154)
Twapanda Mapema (#55)
Waponyeni Watu (#56)
Popote na Yesu (#133)

 





Siku ya Tano

Mtindo wa Maisha ya Utii na Maombi

Fungu Elekezi: Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.1 Yohana 5:14, 15.

Hatuna Uwezo, Lakini Yeye ni Mwenye Uweza Wote

Ujumbe wa malaika watatu unatutaka tuishi Maisha ya utii. Malaika wa kwanza anasema kuwa, “Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.” (Ufunuo 14:7). Agano Jipya liliandikwa kwa lugha ya Kiyunani, na neno Mchenilililotumika katika aya hii, linaweza pia kutafsiriwa kama heshima, uchaji, au stahi sana. “Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.” (Muhubiri 12:13, 14)

Tunapofikiria kuhusu kushika amri za Mungu, ni rahisi sana kujielekeza katika udhaifu wetu, mapungufu yetu, na ukosefu wetu wa uwezo wa kufanya kile ambacho ndani yetu tunatamani kukifanya. Mara nyingi tunatamani kutenda mema, lakini tunashindwa kupata nguvu na uwezo wa kutimiza matamanio yetu. Hapo ndipo tunapoungana na Mtume Paulo kutambua kuwa, “… sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.” (Warumi 7:15). Ufumbuzi wa mtume kwa changamoto hii ulikuwa ni upi? Na mwisho wa sura hiyo anauliza swali kuwa, “Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.” (Warumi 7:24, 25). Kuna ufumbuzi kwa tatizo ambalo daima linatuangusha, tunatubu, na kuangauka tena. Paulo anasema kuwa, ufumbuzi ni Yesu Kristo Bwana wetu. Sisi ni wadhaifu, lakini yeye ni mwenye nguvu. Sisi ni dhaifu, lakini yeye ni mwenye uweza Ukurasa wa 49 mkuu. Hatuna nguvu, lakini yeye anazo nguvu zote. Ellen G. Whita anaweka kwa namna ya kuvutia katika Makala yake aliyoandika mwaka 1897 kuwa: “Mfano wa Yesu unatuonesha kwamba tumaini letu pekee la ushindi ni kuendelea kupinga mashambulizi ya Shetani. Yeye aliyemshinda adui wa roho katika pambano lenye majaribu, anafahamu uwezo wa Shetani dhidi ya ubinadamu, na ameshinda kwa niaba yetu. Yeye kama mshindi ametupatia faida ya ushindi wake, ili kwa jitihada zetu tupinge majaribu ya Shetani tukiunganisha udhaifu wetu na nguvu zake, kutokustahili kwetu na kustahili kwake. Na katika kufanya hivyo, tutegemezwe kwa uwezo wake unaostahimili chini ya majaribu makuu, tuweze kumpinga adui kwa uwezo wa jina lake lenye nguvu kama yeye mwenyewe alivyoshinda. Signs of the Times, May 27, 1887

Kudai Ushindi

Tulikuwa washindi katika Maisha ya Kikristo pale tulipojielekeza katika uwezo wa Kristo, tukisahau udhaifu wetu. Kadiri tunavyoingia katika maombi, hebu na tudai ahadi iliyoko katika 1 Yohana 5:14, 15 “Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba” Kadiri tunavyodai ahadi hii kwa uaminifu, Yesu atatenda mambo makubwa ya kushangaza, na kutuimarisha ili kuweza kuishi Maisha ya kimbingu wakati tukijitayarisha kwa kurudi kwake mara ya pili ambako kumekaribia.

Wakati wa Maombi (Dakika 30-45)

Kuomba kupitia kwa Neno la Mungu
Mhubiri 12:13, 14

“Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.”

Mcheni Mungu

Bwana, tunatambua kwamba wewe ndiye Mungu Muumba mwenye uwezo, mwenye maarifa yote. Wewe umezidi upeo wa mwanadamu wa utambuzi, lakini bado upo karibu nasi kuliko hata wapendwa wetu wanaoonekana kuwa karibu. Tupo chini ya utisho wa ukuu wako na tunakuabudu wewe tukikusudia kukuheshimu katika Maisha yetu.

Shika Amri Zake.

Ukurasa wa 50 Ee Mungu, sisi hatuna uwezo ndani yetu wa kushika amri zako, wa kuenenda sawa sawa na mapenzi yako. Ni Yesu pekee anayeweza kutusaidia. Tunatamani kutenda mapenzi yako, kuwa waaminifu, lakini mara nyingi tumeshindwa. Ahsante sana kwamba Yesu anao uwezo wa kuleta ushindi katika Maisha yetu. Tunamgeukia na kujitoa kikamilifu katika mikono yake ya uaminifu. Ee Yesu, tunaomba kwamba uishi Maisha yako ndani yetu.

Kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.

Baba, ninatambua kwamba hakuna jambo lililofichika mbele yako. Unaufahamu moyo wangu, unafahamu mapito yangu. Unatambua fika kila kitu kinachotokea katika ulimwengu unaonizunguka. Ahsante sana kwamba, pamoja na jinsi ninavyojisikia, unaniwazia kwa upendo na neema, na sina hofu na hukumu kadiri ninavyodumu ndani ya Yesu.

Mapendekezo zaidi ya Maombi

Shukurani na Sifa:
Shukuru kwa mibaraka mahususi na msifu Mungu kwa wema wake.
Kuungama: Tumia dakika chache kwa ajili ya maungamo binafsi na msifu Mungu kwa msamaha wake.
Uongozi: Mwombe Mungu akupatie hekima kwa changamoto na maamuzi ya sasa.
Kanisa Letu: Muombe Mungu kwa ajili ya mahitaji ya kanisa katika ngazi ya majimbo na kanisa la ulimwengu (tazama karatasi nyingine yenye mahitaji).
Mahitaji ya eneo mahalia: Ombea mahitaji ya washiriki wa kanisa, familia, na majirani.
Sikiliza na Itika: Tumia muda kuisikiliza sauti ya Mungu na kuitikia kwa sifa au wimbo.

Mapendekezo ya Nyimbo:

Yote Namtolea Yesu (#122)
Nitembee Nawe (#14)
Ni Wako Bwana (#144)
Njiani Huniongoza (#155)
Wimbi Litakasalao (#188)





Siku ya Sita

Kuwa na Imani katika Hukumu na Maombi

Fungu Elekezi: 3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; 4 kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. 5 Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake 6 Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.Waefeso 1:3-5.

Saa ya hukumu yake imekuja

Ujumbe wa malaika wa kwanza wa Ufunuo unatangaza kuwa, “Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja...” (Ufunuo 14:7). Katika mng’ao wa nuru ya umilele, uhalisia wa hukumu ya kimbingu kule mbinguni unatuongoza kutafuta uhusiano wa kina na Mungu kwa maombi ya dhati. Hukumu katika hekalu la mbinguni ilioneshwa kwa kivuli cha siku ya upatanisho katika Israeli ya kale. Katika siku hiyo kuu ya upatanisho, katika mfumo wa hekalu la Agano la Kale Waisraeli wote walikusanyika kuzunguka hekalu, wakiungama dhambi zao na kutafuta msamaha wa Mungu. Katika kitabu cha Mambo ya Walawi 23:29 tunasoma kuwa, “Kwa kuwa mtu awaye yote asiyejitesa mwenyewe siku iyo hiyo, atakatiliwa mbali na watu wake.”

Heshima na hadhi ya Mungu iko hatarini katika hukumu ya mbinguni ya mwisho. Maswali yamekuwa yakijitokeza kuhusu tabia yake mbele ya ulimwengu. Je, Mungu anatenda haki? Amri zake Je? Ni ngumu kutunza? Ana upendo na ni mwenye haki? Katika hukumu, Mungu atadhihirisha kwamba amefanya kila lililowezekana kuokoa ubinadamu. Hakuna Zaidi ambacho angefanya kuliko kile ambacho amefanya. Neema yake yatosha kwa wote. Ni neema ndiyo inayotuokoa kutoka katika adhabu ya dhambi na nguvu ya dhambi. Ni neema inayosamehe mambo yetu ya nyuma na kutuwezesha wakati huu uliopo.

Uharaka wa ujumbe wa saa ya hukumu unatuelekeza katika uhusiano wa kina na Kristo. Tunatamani kuheshimu jina lake na kuepuka kufanya kile kitakachochafua heshima yake. Hatuhitaji kuhofia hukumu kwa kuwa Yesu ndiye Wakili wetu, yeye ndiye msimamizi wa mashtaka, na pia ndiye hakimu wetu (Yohana 5:22). Katika Kristo, sisi tu wana na binti wa Mfalme wa mbingu na nchi na vyote vilivyomo, yaani sehemu ya familia ya kifalme ya mbinguni. Nabii Danieli anatoa taswira ya Yesu katika hekalu la mbinguni akionekana mbele ya Baba kwa niaba yetu kwenye hukumu ya mwisho ya mbinguni. Viumbe wa mbinguni elfu kumi mara elfu kumi mara elfu wamezunguka chumba cha mahakama ya mbinguni. Pambano kuu kati ya wema na uovu linafikia tamati. Jina la Mungu – yaani tabia yake – litainuliwa mbele ya malimwengu yote (Danieli 7:9-14). Itakuwa ni madhari ya haki na yenye rehema, ambayo imekabidhi mbingu zawadi ya thamani katika Yesu.

Kupitia katika vizazi visivyokoma vya umilele, tutashangilia tukisema kuwa, “3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; 4 kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. 5 Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake 6 Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.” (Waefeso 1:3-6)

Katika kipindi chetu cha maombi leo, na tuchunguze mioyo yetu na kumwomba Mungu adhihirishe kitu chochote kisichokuwa katika upatanifu na nia yake. Hebu tumwombe atusafishe kutoka katika dhambi zilizozama na kisha tumshukuru kwa neema yake, msamaha wake, na nguvu zake za kushinda. Zaidi ya yote, hebu na tumshukuru Yeye kwa ajili ya Yesu.

Wakati wa Maombi (Dakika 30-45)

Kuomba kupitia kwa Neno la Mungu
Ufunuo 14:7

“… akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.”

Mcheni Mungu

Ee Mungu, tunakuabudu wewe. Wewe unastahili heshima yote na utukufu. Wewe ni Mkuu wa mbinguni, Mungu uliye Muumbaji, wewe ni wa milele – tunakucha na kukuheshimu wewe. Hakuna kitu kinachoweza kukumiliki. Ukurasa wa 53

Na Kumtukuza

Ee Mungu, ni jambo la ajabu kufikiri kwamba ungependa kujidhihirisha, na kuonesha tabia yako ya upendo kupitia kwangu. Ninakuomba unijaze kwa Roho wako Mtakatifu ili kuleta kwako ule utukufu unaokusudia. Ninakuomba uishi ndani yangu na kupitia kwangu na kunipatia ushindi dhidi ya dhambi. Niwezeshe kuishi kwa upatanifu na mapenzi yako.

Saa ya Hukumu yako Imekuja

Ahsante sana Yesu kwa ajili ya hukumu. Ahsante sana kwamba hukumu ni kwa ajili yetu na kwamba utarejesha haki katika ulimwengu. Ahsante sana kwamba wewe ndiye Wakili wetu na Kuhani wetu Mkuu na kwamba haki yako itatupatia uhakika tunaouhitaji ili kusimama kidete kwa furaha tukikushukuru. Utukumbushe umuhimu wa nyakati tunazoishi na kutusaidia kuelekeza watu wengi kadiri tunavyoweza ili wapate ukombozi wa milele ndani yako.

Mapendekezo zaidi ya Maombi

Shukurani na Sifa:
Shukuru kwa mibaraka mahususi na msifu Mungu kwa wema wake.
Kuungama: Tumia dakika chache kwa ajili ya maungamo binafsi na msifu Mungu kwa msamaha wake.
Uongozi: Mwombe Mungu akupatie hekima kwa changamoto na maamuzi ya sasa.
Kanisa Letu: Muombe Mungu kwa ajili ya mahitaji ya kanisa katika ngazi ya majimbo na kanisa la ulimwengu (tazama karatasi nyingine yenye mahitaji).
Mahitaji ya eneo mahalia: Ombea mahitaji ya washiriki wa kanisa, familia, na majirani.
Sikiliza na Itika: Tumia muda kuisikiliza sauti ya Mungu na kuitikia kwa sifa au wimbo.

Mapendekezo ya Nyimbo:

Yesu Uje Kwetu (#13)
Nimekombolewa na Yesu (#135)
Wapenzi wa Bwana (#70)
Ni Salama Rohoni Mwangu (#127)
Jina Langu Limeandikwa Je? (#170
Yesu Kwa Imani (#123)  





Siku ya Saba

Ujumbe wa Malaika Watatu,
Sabato na Maombi

Fungu Elekezi: Nitawapa hawa nyumbani mwangu, na ndani ya kuta zangu, kumbukumbu na jina, lililo jema kuliko kuwa na wana na binti; nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali. Na wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la Bwana, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu. Nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yoteIsaya 56:5-7.

Kuumbwa kwa Kusudi

Ujumbe wa Malaika watatu ni wito ulio wazi wa kumwabudu Muumbaji wetu. Hatukuibuka tu, wala sisi siyo matokeo ya makosa ya kijenetiki. Mungu alituumba, na uhai ni zawadi ya pekee inayotoka kwa Yesu. Mtume Yohana anasema, “Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa” (Ufunuo 4:11). Ni wazo la kicho na lenye kuvutia kutambua kwamba tunaishi kwa neema ya Mungu. Sabato inatukumbusha kwamba tuliumbwa kwa kusudi fulani. Inaturudisha hadi nyumbani kwetu kwenye bustani ya Eden na kutukumbusha upendo wa Muumba wetu ambaye anatukusudia mema pekee kwenye Maisha yetu. Katika ulimwengu uliojaa maumivu na maradhi, Mungu wa Uumbaji anaahidi kwamba “Hatakupungukia kabisa, wala hatakuacha kabisa” (Waebrania 13:5). Ukweli huu pekee unapaswa kutufanya twende magotini katika kumsifu Mungu kwa zawadi ya uhai na kule kutambua mipango mahususi aliyo nayo kwa ajili ya Maisha yetu.

Sabato Wito wa Maombi, Sifa, na Kupiga Mbiu

Sabato inatukumbusha pia kuhusu zawadi ya wokovu. Kadiri tunavyopumzika katika Sabato, tunapumzika katika kazi ya Kristo iliyokamilika kwa niaba yetu (Waebrania 4:9, 10). Tunapumzika katika neema yake. Sabato si hitaji la kisheria lilitolewa kwa taifa la Israeli. Ni siku iliyojawa neema kwa wanadamu wote, ikituongoza kumtegemea Kristo Ukurasa wa 55 kikamilifu kwa ajili ya ukombozi wetu (Isaya 56:6, 7). Yesu alihitimisha lile juma la Uumbaji kwa maneno haya, “Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya” (Mwanzo 2:1, 2). Pia alihitimisha kazi yake msalabani kwa maneno, “Imekwisha.” Hatukushiriki kwa namna yoyote ile katika kazi ya uumbaji ya Kristo pale mwanzo. Aliianza kazi hiyo, na Aliimaliza. Vivyo hivyo, hatukuhusika kwa kwa namna yoyote ile katika kazi ya Kristo ya ukombozi pale msalabani. Aliianza kazi ya wokovu, na Aliimaliza. Sabato inatukumbusha kufurahi katika upendo wake, kupumzika katika uangalizi wake, na utukufu kwa Kristo aliyelipa gharama kubwa sana kwa ajili ya wokovu wetu. Sabato ni wito wa kuomba, wito wa kusifu, na wito wa kutangaza wema wake.

Sabato pia inatukumbusha kwamba hatupo peke yetu katika ulimwengu wenye huzuni. Uzuri wa uoto wa asili huzungumza kuhusu Mungu wetu Muumbaji katikati ya maumivu ya dunia hii. Sabato inaturejesha katika Uumbaji, lakini pia hutuelekeza mbele katika mbingu mpya na nchi mpya, ambapo Mungu ataumba upya dunia hii kwa uzuri ule wa Edeni.

Sabato ni siku ya kushukuru. Tunashukuru kwamba Mungu alituumba na ana mpango na Maisha yetu. Tunashukuru kwamba alitukomboa na amelipa gharama kubwa sana kwa ajili yetu. Tunashukuru kwamba anarudi tena kutuchukua na ataumba mbingu mpya na nchi mpya. Hebu tumtafute kwa mioyo yenye shukrani kadiri tunavyoomba.

Wakati wa Maombi (Dakika 30-45)

Kuomba Kupitia katika Neno la Mungu
Isaya 56:5-7

“Nitawapa hawa nyumbani mwangu, na ndani ya kuta zangu, kumbukumbu na jina, lililo jema kuliko kuwa na wana na binti; nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali. Na wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la Bwana, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu. Nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.”

“Hata Kwao”

Mungu, ulituumba sisi sote. Ulikusudia tuwepo na unatamani ushirika wa milele pamoja nasi. Ndiyo, unatamani ukombozi wa wanadamu wote. Kila taifa na kabila na kundi la Ukurasa wa 56 watu. Tunakusifu! Asante kwa Sabato ya kila juma inayotukumbusha kuhusu uhalisia huu.

Kila aishikaye sabato asiivunje”

Bwana, mara nyingi tumevunja sabato au kutokuitakasa. Tunakuomba utusamehe. Tafadhali tusaidie kutunza saa za Sabato tukikutambua na kukuinua wakati huo wa Sabato. Fungua macho na masikio yetu ili tufahamu na kutenda mapenzi yako kila siku, ili katika Sabato tuweze kusherehekea na kushuhudia uaminifu wako kwa juma zima.

“Na kulishika sana agano langu”

Ee Yesu, Asante kwamba Sabato si ishara na fursa pekee ya kukukumbuka wewe kama Muumba wetu lakini pia ni ishara ya wokovu. Asante kwamba tunaweza kupumzika tukiwa tumehakikishwa katika haki yako, inayotufunika na kutujaza kadiri tunavyoshika sana ahadi za agano lako. Hebu utunzaji wetu wa Sabato ukaakisi uzoefu wa kila sika wa uaminifu wako kwetu.

Mapendekezo zaidi ya Maombi

Shukurani na Sifa:
Shukuru kwa mibaraka mahususi na msifu Mungu kwa wema wake.
Kuungama: Tumia dakika chache kwa ajili ya maungamo binafsi na msifu Mungu kwa msamaha wake.
Uongozi: Mwombe Mungu akupatie hekima kwa changamoto na maamuzi ya sasa.
Kanisa Letu: Muombe Mungu kwa ajili ya mahitaji ya kanisa katika ngazi ya majimbo na kanisa la ulimwengu (tazama karatasi nyingine yenye mahitaji).
Mahitaji ya eneo mahalia: Ombea mahitaji ya washiriki wa kanisa, familia, na majirani.
Sikiliza na Itika: Tumia muda kuisikiliza sauti ya Mungu na kuitikia kwa sifa au wimbo.

Mapendekezo ya Nyimbo:

Ikumbuke Sabato (#84)
Ni Siku ya Furaha (#82)
Uliniimbie Tena (#139)
Yesu Unipendaye (#30)
Bwana Uniongoze Juu (#73)
Anakuja Upesi (#159)
Wapenzi wa Bwana (#70)





Siku ya Nane

Kuanguka kwa Babeli na Maombi

Fungu Elekezi: Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake. Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukizaUfunuo 18:1-2.

Ujumbe wa Malaika wa Pili

Ujumbe wa Malaika watatu wa Ufunuo 14 umeandaliwa mahususi ili kuandaa watu kwa ajili ya ujio wa Yesu. Unadhihirisha mipango ya Mungu na kufichua mipango ya ibilisi. Ujumbe wa Malaika wa pili hutoa onyo zito: “Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake” (Ufunuo 14:8). Kama Babeli ya zamani ilivyopigana vita na Mungu katika uasi dhidi ya sheria zake, Babeli ya kiroho husimama katika uasi dhidi ya Mungu. Anaeneza “kikombe cha mvinyo” wa mafundisho ya uongo ili kuwadanganya wengi. Ellen G. White anailezea Babeli kwa namna hii: “Dhambi kubwa Zaidi ya Babeli ni kwamba ‘aliwanywesha mataifa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake.’ Kikombe hiki cha kilevi anachowasilisha duniani kinawakilisha mafundisho ya uongo ambayo ameyakubali kama matokeo ya muunganiko wake usio wa kisheria na wakuu wa dunia. Urafiki na dunia unaathiri Imani yake, na kama matokeo yake, anakuwa na mvuto wenye uharibifu katika dunia kwa kufundisha mafundisho yanayopingana na nukuu za wazi za Maandiko Matakatifu” (The Great Controversy, uk. 388). Uzinzi ni muunganiko haramu. Babeli ya kiroho inaachana na mpenzi wake wa kweli, Yesu, na kuungana na serikali au nguvu ya kisiasa.

Muunganiko wa kanisa na serikali, kama inavyoelezewa katika Ufunuo 17, unasababisha kushinikizwa kwa alama ya mnyama. Babeli inawakilisha mfumo wa kidini ambao unapotosha Maandiko na kujikita katika mafundisho ya wanadamu. Ujumbe wa Malaika wa pili, pamoja na unabii wa Ufunuo 17 na Ufunuo 18, unadhihirisha kile kinachoujia ulimwengu kwa namna ya kushangaza sana. Nguvu za kidini zilizoasi zitaungana na nguvu za kisiasa na kiuchumi ili kuleta umoja katika kipindi cha maafa na hali ya hatari.

Ujumbe wa Malaika wa pili unatoa wito wa muhimu na wa haraka wa maombi kwa maeneo angalau matatu. Kwanza, unatuita kuwa waaminifu kwa Kristo na Neno lake. Mwafaka katika Maisha yetu binafsi utatuelekeza tu katika nyakati za mwisho za historia ya Dunia katika kuungana na Babeli na vita dhidi ya watu wa Mungu.

Jambo la pili, ujumbe huu unatuelekeza katika Imani inayoweza kustahimili kipimo cha majaribu. Nabii wa Mungu anatusihi kwa bidi kuwa, “Dhoruba inakuja, isiyo na huruma katika ghadhabu yake. Je, tumejiandaa kukabiliana nayo? Hatuhitaji kusema, hatari za siku za mwisho karibu zitatujia. Zimekwisha kuja. Tunahitaji sasa upanga wa Bwana ukate kila nafsi na kiini cha tamaa za kimwili, hamu, na hisia kali. Fikra zilizoachiliwa katika mawazo hafifu zinahitaji kubadilika… Mawazo yanapaswa kujikita kwa Mungu” (With God at Dawn, uk. 113)

Tatu, ujumbe huu hutuelekeza kualika marafiki zetu katika uhusiano wa kina na Yesu na uelewa wa kweli za Ufunuo kwa wakati huu wa mwisho. Tunaposujudu kwa ajili ya kuomba, hebu tuombee mahitaji haya mahususi:
1. Uelewa sahihi wa Neno la Mungu, upendo mkuu kwa Yesu, na roho isiyotafuta mwafaka.
2. Imani inayoweza kustahimili kipimo cha majaribu.
3. Ujasiri wa kuwashuhudia wale wanaotuzunguka.

Wakati wa Maombi (Dakika 30-45)

Kuomba Kupitia katika Neno la Mungu
Ufunuo 14:8

“Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake.”

“Umeanguka Babeli”

Baba wa Milele, kando ya Neno lako Takatifu, hakuna kitu kingine katika dunia hii kinachoweza kuaminiwa kutoa msingi imara na wenye kuaminika wa Maisha. Tusaidie kujenga Maisha yetu kwa neema yako, kupitia kwa Roho wako, katika Neno Lako pekee.

“Amewanywesha Mataifa Yote”

Mungu, tumebahatika kukufahamu na kuwa na uelewa wa ukweli kupitia katika Neno lako. Pia tunatambua wajibu wetu kwa sababu ya hilo. Leo tunaomba kwa ajili ya mabilioni ya watu walionaswa katika dini za uongo. Tusaidie kuwaonyesha ukweli Ukurasa wa 59 kuhusu wewe mwenyewe ulivyo, na unavyowapenda na kuwataka waje katika ukamilifu wa kweli.

“Mvinyo ya Ghadhabu ya Uasherati Wake”

Yesu, tunakubali kwamba nyakati fulani tumekengeushwa na madanganyo na vishawishi kadhaa vya shetani. Nyakati fulani tunakoma kukutazama na badala yake tunajielekeza katika nafsi zetu wenyewe na kwenye uzoefu wenye ubinafsi. Tunakuomba utusamehe. Tuokoe dhidi ya kujiachia katika asili yetu ya kimwili, na ujenge ndani yetu ushindi ambao wewe pekee ndiye unayeweza kuutoa.

Mapendekezo zaidi ya Maombi

Shukurani na Sifa:
Shukuru kwa mibaraka mahususi na msifu Mungu kwa wema wake.
Kuungama: Tumia dakika chache kwa ajili ya maungamo binafsi na msifu Mungu kwa msamaha wake.
Uongozi: Mwombe Mungu akupatie hekima kwa changamoto na maamuzi ya sasa.
Kanisa Letu: Muombe Mungu kwa ajili ya mahitaji ya kanisa katika ngazi ya majimbo na kanisa la ulimwengu (tazama karatasi nyingine yenye mahitaji).
Mahitaji ya eneo mahalia: Ombea mahitaji ya washiriki wa kanisa, familia, na majirani.
Sikiliza na Itika: Tumia muda kuisikiliza sauti ya Mungu na kuitikia kwa sifa au wimbo.

Mapendekezo ya Nyimbo

Hatujui Saa (#173)
Njoni Kwangu (#103)
Mtazame Mwokozi (#212)
Usinipite Mwokozi (#22)
Twendeni Askari (#65)  





Siku ya Tisa

Alama ya Mnyama na Maombi

Fungu Elekezi: Baada ya hayo nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, sauti kubwa mbinguni, ikisema, Haleluya; wokovu na utukufu na nguvu zina BWANA MUNGU wetu. kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki; maana amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake mkononi mwake. Wakasema mara ya pili, Haleluya. Na moshi wake hupaa juu hata milele na milele. Na wale wazee ishirini na wanne, na wale wenye uhai wanne, wakasujudu na kumwabudu Mungu, aketiye katika kile kiti cha enzi, wakisema, Amina, Haleluya. Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuuUfunuo 19:1-5

Onyo la Dhati

Ujumbe wa tatu na wa mwisho wa malaika watatu ni moja ya onyo zito zaidi katika Biblia. Ni onyo mojawapo ambalo watu wengine wangependa kulipuuza, ingawaje ni onyo linalodhiihirisha kweli za kiroho zinazobadilisha maisha ambazo zinazungumza na ule uhitaji wetu wa ndani zaidi na kutuvuta karibu na Yesu. Mtume Yohana ameandika kuwa, “Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, ‘Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo’” (Ufunuo 14:9, 10). Kanuni ya kwanza ibadilishayo maisha inayohusu onyo hili ni kuwa, ni onyo linalotoka katika moyo wa Mungu mwenye upendo anayetaka kutuokoa sisi katika ufalme wake kuliko kitu kingine cho chote. Huu ni ujumbe wa kimbingu wa onyo ili watu wa Mungu wasije wakanasa bila kujitambua katika madanganyo yanayokuja. Jambo la pili, linahusiana na ibada. Malaika anasema, “Mtu awaye yote akimsujudia huyo mnyama.” Jambo hili linatofautiana moja kwa moja na ujumbe wa Malaika wa kwanza katika fungu la 7 wa kumsujudia Muumbaji. Kumwabudu Muumbaji kunawaongoza wafuasi waaminifu wa Kristo kuitikia upendo wake, kuamini neema yake iokoayo, kutii Neno Lake, na kushika amri zake. Kumsujudia mnyama kunawelekeza wat kuishi Maisha ya ubinafsi wakijitegemea na kumweka Mungu Ukurasa wa 61 pembeni kwa kukosa kutii amri zake. Kumsujudia mnyama kunajielekeza zaidi katika mtu binafsi badala ya kujielekeza kwa Yesu.

Mnyama Ndani Yetu

Ujumbe huu wa Malaika wa tatu huzungumza kuhusu wakati unaokuja ambapo kanisa litaungana na serikali chini ya utawala wa upapa ili kushurutisha ibada katika siku ya kwanza ya juma. Ujumbe wa mwisho wa Malaika watatu ni wito wa maombi ya bidii na ya dhati. Kanuni ya mpinga kristo – ya kiburi badala ya unyenyekevu, kujiinua badala ya kujitoa kwa ajili ya wengine, na Imani katika hekima ya kibinadamu badala ya uvuvio wa kimbingu wa Maandiko – imejengeka kwa kina sana katika asili zetu za kuanguka. Je, ufumbuzi wa kanuni hizi za mnyama anayeishi ndani yetu ni upi? Kuna suluhisho moja tu, na hilo ni Yesu – neema yake, nguvu yake, upendo wake kujaza mioyo na Maisha yetu. Msimamo wetu kwake usipokuwa imara kuliko mvuto wa ulimwengu, tutatawaliwa na kanuni za mnyama huyo leo na siku moja tutaikubali chapa ya mnyama. Onyo hili dhidi ya chapa ya mnyama katika ujumbe wa Malaika wa tatu linapaswa kutunyenyekeza magotini katika kujisalimisha kwa unyenyekevu kwa kristo, tukiomba Roho Wake atutakase kikamilifu kutoka ndani na kufanya muujiza wa neema ya kimbingu ndani ya mioyo yetu. Pia onyo hilo linapaswa kutuelekeza katika kuomba kwa ajili ya familia, marafiki, na majirani, kwamba wao nao wafungue mioyo yao kwa ujumbe wa siku za mwisho wa Kristo uokoao. Ujumbe huu unapaswa kutuhamasisha kutazamia ile siku ambapo tutafurahi Pamoja na Kristo kuzunguka kiti chake milele (Ufunuo 19:1- 5).

Wakati wa Maombi (Dakika 30-45)

Kuomba Kupitia katika Neno la Mungu
Ufunuo 14:9, 10

“Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, ‘Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana- Kondoo.’”

“Mtu Awaye Yote Akimsujudu huyo Mnyama na Sanamu Yake”

Mungu, wewe ni Mungu unayejali, Mungu unayetamani wote tuokolewe wala tusipotee. Watu wengi hutazama dini za uongo, falsafa zilizogeuzwa, na miungu ya siku za sasa kama chanzo cha cha nguvu zao na utimilifu hali ya kuvunjika katika Maisha yao. Tunakushukuru kwamba unajali sana kiasi cha kuwaonya na kwamba tunaweza Ukurasa wa 62 kutenda jambo katika kuwaongoza kwa Yesu kama Mwokozi pekee anayestahili kuabudiwa.

“Ghadhabu ya Mungu”

Ee Mungu, inatupatia Faraja kubwa kutambua kwamba wewe una ghadhabu takatifu dhidi ya dhambi, ubaya, na uovu. Asante kwa kutamani kuharibu dhambi milele na kwamba siku moja utajenga upya upendo mkamilifu, na uwiano katika ulimwengu. Asante kwa kutuonyesha kwa uwazi kupitia kwa Yesu kwamba siyo nia yako kuwahukumu watu bali kuwaokoa. Asante kwa kumpatia kila mwanaamu uchaguzi na fursa ya kupata wokovu katika Kristo. Tafadhali tuokoe na kutulinda dhidi ya kufuata kanuni ya mpinga kristo ya kujiinua na kiburi. Badala yake, tuongoze katika kumfuata Mwanakondoo po pote aendapo.

“Mbele za Mwana Kondoo”

Ee Yesu, tunapata Faraja kubwa kufahamu kwamba katika hukumu ya mwisho itadhihirika kwamba ahadi yako ya neema na wokovu haikuwa imetenganishwa na haki. Asante kwa kuchukua adhabu ya wale wote waliojisalimisha kwako. Asante kwamba, ijapokuwa vigumu kushuhudia uangamivu wa wale waliochogaua kung’ang’ania katika dhambi, kila mmoja atakiri kwamba wewe umekuwa mwenye haki, na mwenye neema katika mambo yako yote.

Mapendekezo zaidi ya Maombi

Shukurani na Sifa:
Shukuru kwa mibaraka mahususi na msifu Mungu kwa wema wake.
Kuungama: Tumia dakika chache kwa ajili ya maungamo binafsi na msifu Mungu kwa msamaha wake.
Uongozi: Mwombe Mungu akupatie hekima kwa changamoto na maamuzi ya sasa.
Kanisa Letu: Muombe Mungu kwa ajili ya mahitaji ya kanisa katika ngazi ya majimbo na kanisa la ulimwengu (tazama karatasi nyingine yenye mahitaji).
Mahitaji ya eneo mahalia: Ombea mahitaji ya washiriki wa kanisa, familia, na majirani.
Sikiliza na Itika: Tumia muda kuisikiliza sauti ya Mungu na kuitikia kwa sifa au wimbo.

Mapendekezo ya Nyimbo

Nasifu Shani ya Mungu (#38)
Na Tumwabudu Mfalme Mtukufu (#5)
Jina la Yesu, Salamu (#4)
Ukingoni mwa Yordani (#178)
Watakatifu Kesheni (#160)





Siku ya Kumi

Watu wa Mungu, Masalia, na Maombi

Fungu Elekezi: Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.(Ufunuo 14:12)

Lengo la Mwisho

Ujumbe wa Malaika watatu una kusudi moja kuu, mwelekeo mmoja mkuu: kuwaandaa watu kwa ujio wa Yesu. Jumbe hizi zenye uvuvio wa kimbingu hufikia kilele chake katika Ufunuo 14:12, Yohana anapoelezea matokeo ya mwisho ya kuuelewa na kuukubali ujumbe wa Mbingu wa wakati wa mwisho. Mtume anaeleza kwamba jumbe hizi zitakuwa na matokeo ya kuwa na watu ambao inaweza kuandikwa kuwahusu kwamba, “Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu” (Ufunuo 14:12).

Neno Subira linaweza kutafsiriwa kwa ubora zaidi kama ustahimilivu. Kwa neema yake, watu wa Mungu watastahimili majaribu ya siku za mwisho na kutoka wakiwa washindi. Watakabiliana na ghadhabu ya mnyama wala wasiache ushawishi thabiti wa dhamiri zao. Licha ya kushindwa kununua au kuuza na kukabiliana na mateso, kufungwa, na kifo kwa ajili ya Kristo, bado watadumu kuwa watii kwa amri zake. Hawawezi kushurutishwa kutokusalimisha utii wao kwa Kristo. Wanaishi Maisha yaliyojawa na neema, yenye kumtukuza Kristo, na yenye utii katikati ya ulimwengu wenye dhambi na uasi, ulimwengu usio na utii wakati wa saa ya mwisho ya dunia hii.

Imani ya Yesu

Kuna kitu kingine cha kufurahisha kuhusu Ufunuo 14:12. Waumini hawa wa wakati wa mwisho siyo tu kwamba wana Imani katika Yesu, bali pia wana Imani ya Yesu. Imani ya Yesu ni nini? Imani ya Yesu ni kiwango kilekile cha Imani kwa Mungu ambayo Yesu alikuwa nayo pale msalabani. Yesu alipoangikwa msalabani akiwa amebeba hatia, aibu, na shutuma za dhambi za wanadamu, alihisi kutelekezwa na Mungu. Wingi wa dhambi Ukurasa wa 64 ulikuwa mkuu kiasi cha Yesu kuhisi kutelekezwa na Mungu. Hii ndiyo sababu Yesu alilia kwa uchungu akisema kuwa, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” (Mathayo 27:46). Je, Mungu alikuwa amemwacha? Kwa hakika hapana! Macho yake yalikuwa msalabani wakati wote. Moyo wake wa upendo ulikuwa umevunjika kwa uchungu ambao mwana wake alikuwa akipitia. Yesu aliamini wakati alikuwa hawezi kuona. Imani yake ilizidi kile kilichokuwa kikitendeka katika mazingira yake. Ndiyo maana maneno yake ya mwisho yalikuwa kwamba, “Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu” (Luka 23:46).

Kabla tu kurudi kwa Yesu, kulingana na unabii wa Ufunuo, watu wa Mungu watahitaji kwa mara nyingine kuamini katika mazingira ambayo kila kitu kinachowazunguka kikionekana kupingana nao. Ni kitu gani kitawavusha katika wakati huu wa majaribu? Ni “Imani ya Yesu.” Ni kwa namna gani tunajenga Imani hii ya Yesu? Kwanza, kama wokovu ulivyo zawadi, Imani pia ni zawadi ambayo Mungu huiweka ndani ya mioyo yetu ambayo inakua kadiri tunavyoifanyia mazoezi (Warumi 12:3-8). Tunapopitia katika uzoefu mgumu na katika hali ya kukata tamaa tukang’ang’ania ahadi za Mungu, Imani yetu hukua. Tunapojaza akili zetu kwa Neno la Mungu, Imani yetu hukua (Warumi 10:17). Tunapokiri kuwa Imani yetu imepungua, na kuomba kwa bidii kwamba Mungu aongeze Imani yetu, Imani hiyo hukua (Luka 17:5).

Katika muda wetu wa maombi leo, hebu tumuombe Mungu atupatie ustahimilivu kadiri tunavyokabiliana na majaribu ya Maisha. Hebu tuombe kwamba Mungu atupatie nguvu za kuwa watiifu kwa nia yake katika kila eneo la Maisha yetu, na tuombe Mbingu itupatie ongezeko la Imani ili “Imani ya Yesu” ijaze Maisha yetu na kutuandaa kwa ajili ya hatari ya mwisho ya Dunia. Kisha siku moja tutaishi na Yesu milele!

Wakati wa Maombi (Dakika 30-45)

Kuomba Kupitia katika Neno la Mungu
Ufunuo 14:12

“Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.”

“Hapa ndipo penye Subira ya Watakatifu”

Bwana, tumesubiri ujio wako mara ya pili kwa muda mrefu sana. Pia tunafahamu kwamba mipango yako haijawahi kukosewa na kwamba unafahamu kilicho bora kwa ajili yetu. Asante kwamba kadiri Roho Mtakatifu anavyokaa ndani yetu, atajenga Subira na ustahimilivu ndani yetu. Tuonyeshe namna tunavvyoweza kutumia muda tulio nao Ukurasa wa 65 kwa ubora zaidi ili kukupatia utukufu. Tunapokabiliana na majaribu na maudhi, tutafarijika katika kufahamu kwamba unatoa nguvu na Subira ya kimbingu.

“Hao Wazishikao Amri”

Ee Mungu, Nia yako ni upendo. Upendo kwako na upendo kwa wengine. Upendo kama ulivyodhihirishwa katika Neno la Mungu na katika Maisha ya Yesu. Ninashangilia katika ukweli kwamba wewe unaweza na upo tayari kubadilisha mioyo yetu yenye uasi ikawa mioyo ambayo ina uwiano na kanuni kubwa ya upendo.

“Imani ya Yesu”

Mungu, ninashangazwa kwa Imani na uaminifu ambao Yesu aliuonyesha hapa duniani, hasa wakati akifa pale msalabani. Kama Imani yake ilivyokuwa mfano kwetu, hakuiacha pale bali anaitoa kwa wote wanaoamini fursa za kujenga Imani ya kiwango hicho hicho. Yesu, tafadhali kuza Imani yetu, zaidi na zaidi kila siku. Tunajisalimisha kwako, Mwkozi wetu mpendwa na mwaminifu.

Mapendekezo zaidi ya Maombi

Shukurani na Sifa:
Shukuru kwa mibaraka mahususi na msifu Mungu kwa wema wake.
Kuungama: Tumia dakika chache kwa ajili ya maungamo binafsi na msifu Mungu kwa msamaha wake.
Uongozi: Mwombe Mungu akupatie hekima kwa changamoto na maamuzi ya sasa.
Kanisa Letu: Muombe Mungu kwa ajili ya mahitaji ya kanisa katika ngazi ya majimbo na kanisa la ulimwengu (tazama karatasi nyingine yenye mahitaji).
Mahitaji ya eneo mahalia: Ombea mahitaji ya washiriki wa kanisa, familia, na majirani.
Sikiliza na Itika: Tumia muda kuisikiliza sauti ya Mungu na kuitikia kwa sifa au wimbo.

Mapendekezo ya Nyimbo

Msingi wa Kanisa (#195)
Bwana Uniongoze Juu (#73)
Wamwendea Yesu? (#117)
Mishale ya Nuru (#164)
Uniongoze Yehova (#156)
Mungu Atukuzwe (#3)